Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1247 | 1248 | (Page 1249) | 1250 | 1251 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam muda mchache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo. Leo Mei 26, 2017.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akiwaongoza wananchi kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
   Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara

  Wananchi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori mara baada ya kuzuru kujionea eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa ajili ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.

  Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na hatimaye kuzitatua.

  Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara, Mtendaji Kata ya Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya Wananchi wa eneo hilo.

  Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo linakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kutoa maagizo kama hayo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.

  Mhe Makori alisema kuwa madarasa anayoagiza yaanze kujengwa yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amewaahidi wananchi hao kujengwa madarasa kwa viwango vya kisasa.

  Naye Moses Mzakwe na Deogratius Stephano ambao ni wakazi wa Mtaa wa Mavurunza wameomuomba Mkuu wa Wilaya kutilia mkazo swala la upimaji wa viwanja ili wananchi waweze kumiliki ardhi huku wakimpongeza kwa kuzuru katika eneo hilo kwani ameonyesha uwezo wa kujali wananchi anaowaongoza.

  Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wananchi hao Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.

  Alisema kuwa Rais Magufuli anapaswa kutilia mkazo zaidi kwa kuwawekea kufuli watu waliokuwa wanalihujumu Taifa kwa wizi na ufisadi katika sekta mbalimbali nchini.

  Mhe Manota alisema kuwa tayari zimetolewa jumla ya shilingi milioni mia moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule hiyo ambapo mara baada ya kukamilika itawarahisishia wanafunzi kupata elimu bora pasina mateso wanayoyapata sasa kutokana na ukosefu wa shule ya serikali ya Sekondari katika Kata nzima ya Kimara.

  MWISHO

  0 0


  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia watu wanne wakiwemo wahudumu wawili wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala kwa kosa la kupasua maiti na kuiba dawa za kulevya kisha kwenda kuziuza.

  Kamanda wa kanda Maalum, Kamishna Simon Sirro amesema, mbali na wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti, mtuhumiwa mwingine ni Ally Mahamud Nyundo (41) ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kujihusisha na biashara hiyo.

  “Watuhumiwa walikamatwa kutokana na kuwepo taarifa ya kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana katika hospitali hiyo, aliyedaiwa kufariki katika nyumba ya kulala wageni kutokana na kumeza dawa za kulevya,” amesema Kamanda Sirro.

  Amesema mtu huyo ambaye bado hajafahamika jina lake alifariki dunia Machi 14 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Red Carpet iliyoko Sinza, wilaya ya kinondoni.

  Kamanda Sirro amewataja waliokamatwa kuwa ni Omari Rukola (47) na Athuman Mgonja (48) wote wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti na katika mahojiano walikiri kuuchana mwili wa marehemu na kuchukua kete 32 za dawa za kulevya ambapo alimkabidhi Omary Wagile (47) mfanyabiashara ambaye naye aliziuza kwa Nyundo.

  Kamanda Sirro amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla na kuwatakia kheri katika mwezi huo,pia amewataka kujitahidi kufanya ibada kwa wingi,ikiwemo kusima Quran,kuswali sana hasa swala za Suna na kutoa zaka.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Pikipiki na Vipuri  vyake pamoja na baadhi ya wabunge, ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu  Vijijini, Fratei Massay kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Wapili kulia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makiragi na Anna Lupembe kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makumira kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kushoto ni  Mbunge wa Newala Mjini, Capt. George Mkuchika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Tiganya Vincent

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amesema wachimbaji wadogo wadogo waliofichua maovu yanayofanywa na Watendaji wa Ofisi ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni zilizopewa leseni za kuchimba madini katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge wasiwe na wasiwasi kwani Serikali itawashika mkono ili wasidhurike.

  Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge kwenye Mkutano wa hadhara uliowahusisha wachimbaji wadogo wadogo , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya ya Sikonge na viongozi wa Kampuni zenye leseni ya uchimbaji wa madini kufuatia malalamiko kuwa wachimbaji hao wanaosema ukweli wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa wamiliki wa migodi na baadhi ya watendaji.

  Alisema kuwa wamesema ukweli na kufichua maovu yanayoendelea katika eneo la machimbo hayo, Serikali inawahakikishia ulinzi wa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yoyote atayenyanyaswa kwa kufichua uovu unafanywa na Kampuni za Uchimbaji Madini katika eneo hilo.

  Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Sikonge washirikiane na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge kuhakikisha kuwa vijana wote walieleza uovu wa watendaji wa Ofisi ya Madini ya Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni za madini wanakuwa salama na kuendelea na kazi zao.

  Alisema kuwa kiongozi yoyote awe wa Serikali au Kampuni ya Madini asijaribu kuwagusa vijana wote walioeleza matatizo mbalimbali yanayowakabili vingine atakayewagusa atakuwa anakosa sifa za kuendelea kuwa mtumishi wa umma au kuendelea na kazi zake za uchimbaji madini.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Serikali hii iko makini inataka kila mtu au Kampuni itekeleza wajibu wake kama ni kulipa kodi za Serikali ilipe na sio kuendesha shughuli zake kiujanjanja tu na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

  Mmoja wa Mchimbaji Wadogo wadogo wa Madini katika eneo hilo la Kitunda Bw. Linus Saidi alisema kuwa Kampuni ya Kapumpa Gold Mining imekuwa ikiwanyanyasa wachimbaji madini wanaonekana kutetea haki za wenzao na kufichua maovu yanayoendelea katika eneo hilo kwa kuwafukuza na kuyafukia mashimo yao.

  Alisema uovu mwingine unaendelea ni Kampuni ya Kapumpa kufukua mashimo(maduara) yaliyokataliwa na Serikali kwa hofu za usalama wa wachimbaji wadogo wadogo na kuendelea uzalishaji wakati viongozi hao katika eneo hilo na pindi wanaposikia wanakuja wafurika kwa kuweka majani na miti ili yaonekana kama hayafanyikazi.

  Saidi aliongeza kuwa viongozi wa Kampuni ya Kapumpa wamekuwa wakiwadhulumu wachimbaji wadogo wadogo ambao mashimo yao yameonekana kuwa na uzalishaji mzuri na kuwafukuza au kuwakataza kuingia katika eneo la mgodi.

  Kwa upande wa mchimbaji madini mwingine Simon Chacha alisema kuwa baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Tabora wamekuwa wakishirikiana na Kampuni ya Kapumpa katika kuwakandamiza wananchi na kutorosha mapato ya serikali kwa kutoa taarifa zisizo halisi za kiwango cha dhahabu iliyozalishwa.

  Aliongeza kuwa mmoja wa watendaji wa Ofisi ya Madini ameongezwa kuwa Mwanahisa wa Kampuni ya Kapumpa , hatua inayosababisha kuficha takwimu za uzalishaji.

  Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa huyo ameahidi kuzifuatilia tuhuma hizo na ikibainika ni kweli kila atachukuliwa hatua kulinga na alivyohusika kwenye tuhuma mbalimbali zilizotajwa.Aliwaomba vijana hao kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati itakapokuwa ikiendelea kufuatilia tuhuma mbalimbali zilizoelewa .

  0 0

  KAMPUNI inayojishughulisha na uuzaji wa Vilainishi Duniani ( SINOPEC) imefanya Semina ya kuwaelimisha na kuwafundisha wateja wake mbalimbali namna ya kutumia ,kwa lengo la kulinda na kutunza Mazingira.

  Akizungumza hayo mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Mkurugenzi mtendaji wa SINOPEC amesema kuwa,wameamua kuwekeza nchini Tanzania kutokana na Serikali ya awamu ya Tano,kupunguza vikwazo kwa wawekezaji kama ilivyokuwa awamu zilizopita.

  " Kwa Afrika tumeanza kutoa Semina nchini Tanzania, yote hiyo imetokana na mazingira ya uwekezaji kuwa rafiki,hali nzuri ya Usalama pamoja na urafiki wetu wa muda mrefu na Tanzania" alisema Wang

  Amesema kutokana kuweko kwa mazingira rafiki na wezeshi ya uwekazaji,wanaamini kampuni yake itajitanua zaidi kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania,ikiwa sambamba na kuhakikisha serikali inajipatia mapato stahiki kwa kulipa kodi .

  Mkurugenzi huyo amewaomba Watanzania kwa ujumla wao kuvitumia vilainishi hivyo vyenye ubora wa Kimataifa,katika mitambo yao,mashine mbalimbali,magari na vifaa vinginevyo vinavyohitaji kutumia vilainishi.

  Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SINOPEC, Jafali Mswahili amesema wateja wote pamoja na mainjinia watakuwa na utaratibu wa kupewa elimu ili kuwahikikishia wateja wao wanapata na kutumia vilainishi vilivyo bora zaidi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SINOPEC, Andy Wang akionesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia), akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. Bi. Ng'itu amekuwa Mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Dkt. Mlima aliwapongeza na kuwasihi wafanyakazi waliofanya vizuri kuwa zawadi walizokabidhiwa iwe chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi katika utumishi wao. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimpongeza Bi. Ng'itu kwa kuwa mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Bw. Mohammed Kheri kutoka Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akipokea zawadi yake kwa kuwa mfanyakazi bora wa Idara hiyo. 
  Bw.Joseph Mlingi akipokea zawadi kwa kuwa mfanyakazi bora kwa upande wa madereva wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Bw. Emannuel Luangisa akipokea zawadi yake ya kuwa mfanyakazi bora wa Idara ya Asia na Australasia. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Mratibu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago naye akipokea zawadi ya ufanyakazi bora wa Idara ya Diaspora 
  Bi Eva Kaluwa kutoka Idara ya Sera na Mipango akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima. 
  Bi. Kisa Mwaseba akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora wa Idara ya Mashariki ya Kati. 
  Bi. Upendo Mwasha akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. 
  Bi. Nelusigwe kutoka Kitengo cha Ununuzi na Ugavi akipokea zawadi baada ya kuibuka mfanyajkazi bora wa Kitengo hicho. 
  Bw. Erick Ngilangwa kutoka Idara ya Afrika akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara hiyo 
  Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rose Mbilinyi akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima. 
  Katibu Mkuu Dkt. Mlima akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar akichangia jambo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi. 
  Sehemu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu alipo kuwa akizungumza nao 
  Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu, Dkt. Mlima na wafanyakazi bora kutoka kwenye Idara na Vitengo vya Wizara. Mwanamke pekee aliyeketi ni Bi. Eva Ng'itu ambaye ameibuka mfanyakazi hodari wa Wizara nzima kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

  0 0


  Viongozi wa UVCCM mkoa wa Iringa wakiunga mkono utendaji kazi wa Rais Dkt John Magufuli leo baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa tamko la kumpongeza Rais kwa kazi nzuri ,kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ,katibu UVCCM Iringa mjini Alophonce Munyinga , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza , katibu UVCCM mkoa James Mgego , katibu UVCCM Iringa vijiji Ignas Kinyowa na viongozi wengine .

  Vijana walioshiriki zoezi hilo

  Vijana wa UVCCM wakiwa katika zoezi hilo la kumpongeza Rais Dkt Magufuli  Vijana wakiajiandaa kutoa tamko lao leo

  Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa James Mgego katikati akiwa na makatibu wake wa wilaya kushoto ni katibu wa Iringa mjini Alophonce Munyinga na kulia ni katibu wa UVCCM Iringa vijijini Ignas Kinyowa  Na MatukiodaimaBlog


  UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umepongeza hatua ya Rais Dkt John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu na kataka mawaziri zaidi watakaohusishwa na ufisadi kutumbuliwa .


  Huku mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akidai kuwa mkoa wake hauzui wananchi kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia ila hatapenda kuona wananchi wanaunga mkono maamuzi mbali mbali ya Rais kwa kufanya vurugu na kuandamana barabarani .


  Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake juu ya tamko hilo la kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa James Mgego alisema vijana mkoani hapa wamepokea kwa mikono miwili uamuzi huo wa Rais wa kumuondoa waziri Prof Muhongo na kutaka mawaziri na viongozi wengine wa umma kuwajibika kwa faida ya umma na si vinginevyo.


  “ Umoja wa vijana mkoa wa Iringa unaungana na kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt John Pombe Magufuli kwa hatua alizozichukua za kizalendo kwa maslahi ya watanzania kwa kutengua uteuzi wa waziri wa Nishati na madini ….Rais amefanya jambo zuri ambalo linapongezwa na kila mtanzania kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo “


  Alisema kuwa Rais Dkt Magufuli amechukua uamuzi sahihi wakati sahihi kwani nchi ilikuwa ikipoteza raslimali nyingi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache kwa maslahi yao wenyewe na sio jamii ya kitanzania .


  Hivyo alisema kuwa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa umeona ni vema kujitokeza mbele ya vyombo vya habari kupinga vikali vitendo vya rushwa na ufisadi ,dhuruma na wizi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wasio wazalendo na Taifa .


  Mgego alisema UVCCM mkoa wa Iringa haitasita kuwafichua wale wote ambao wanaikwamisha serikali kwa kufanya vitendo vya ufisadi ama dhuruma dhidi ya watanzania kwa kutumia nafasi zao za uongozi walizo pewa .


  Aidha alisema kwa kuwa ripoti ya pili ya kiuchunguzi dhidi ya mchanga huo wa madini inakuja ni vizuri wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine kujitafakari na kuchukua hatua ya kujiuzulu nafasi walizopewa kabla ya kutumbuliwa na Rais .


  Pia katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza mafisadi ambao wapo kuona CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya chama .


  Katibu wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Alphonce Muyinga alisema kuwa wanazo taarifa za wote wanaohujumu uchaguzi wa CCM mkoani Iringa na kuwa dawa yao inachemka kwani hawataona haya kuwashugulikia watu hao wanaotaka kukwamisha uchaguzi huo wa CCM .


  Mkuu wa mkoa wa Iringa Masenza ambae alialikwa katika zoezi hilo la utoaji wa tamko alipongeza hatua ya vijana hao kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli na hata kutoa tamko hilo la pongezi .


  Masenza alisema kuwa kumekuwepo na maombi kutoka kwa wananchi wa kawaida maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa kuomba kufanya maandamano makubwa ya kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na maamuzi mbali mbali yenye lengo la kuwakomboa watanzania na kuwa hakuna kiongozi anaye zuia wao kukutana kutoa pongezi zao kwa Rais ila si kwa kuandamana mitaani .


  “ Mimi kama mkuu wa mkoa wa Iringa nawapongeza pia wananchi wangu ambao wametambua kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu katika Taifa ….nawaomba sana wananchi wenye pongezi kwa rais ruksa kuzitoa ila utaratibu ambao wanapaswa kuutumia ni kukutana katika vikao vya ndani kama walivyofanya vijana wa CCM na sio kufanya maandamano mitaani”

  0 0

  Wasanii wa kizazi kipya Fid Q, Snura, Madee, Dogo Njaja, Stamina na Navy Konzo wanatarajia kutoa burundani katika matamasha ya Taifa Moja ambayo yatafanyika kesho (Jumamosi) kwenye mikoa mine tofauti hapa nchi.
  Burandani hio itaenda sambasamba na kutoa elimu kwa Wananchi wa mikoa husika juu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambayo ni ushirikiano wa makampuni matatu ya simu za mkononi kupitiia huduma zao Tigo Pesa, Airtel Money na Ezy Pesa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema wasanii wote washathibitisha kushiriki kwao kwenye matamasha hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika huku akiwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.

  Wasanii Stamina na Fid Q watambuiza kwenye tamasha litakalofanyika kwenye uwanja wa Mwembetongwa mjini Iringa wakati Dogo janja na Baba Levo wakifanya ya kwao kwenye uwanja wa Community Center grounds uliopo mjini Kigoma huku Snura na Madee wakiwashika vilivyo wakazi wa mji wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano. Navy Kenzo huku akitamba na wimbo wake wa kamati ya chini, atakuwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Sabasaba iliyopo mjini Morogoro.


   

  Tangu tuanze kampeni yetu ya Taifa Moja tumekuwa tukitumia wasanii wetu kutoa elimu kwe Wananchi kupitia burudani na tumetapata mafanikio makubwa sana ya kufikisha ujumbe wetu wa uhuru wa kutuma pesa bila mipaka kupitia burudani kwa Watanzani. Naomba nitoe wito wangu kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kesho kushuhudia wasanii wetu ambao wamehaidi kutoa burundani ya uhakika.

  Bali na kupata burundani, Watanzania wataweza kufahamu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwani kwa njia ya kutuma pesa kwenda mtandao wowote ule kwa gharama ile ile imetoa urahisi kwa kuongeza watumiaji wengi wa huduma ya kutuma pesa na hivyo kuwa rahisi Wananchi kupata huduma za kifedha.


  Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi vitanda moja kati ya 25 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi ambavyo ni miongoni mwa mgao wa vifaa tiba walivyopewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wilaya ya Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi Mgao wa mashuka 50 kutoka kwa Rais John Magufuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwenye wilaya ya Pangani katika halfa iliyofanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani juzi wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa 
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakitembelea hospitali ya wilaya ya Pangani kabla ya kukabidhi Msaada wa vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli
  Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga kulia akimueleza Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Changamoto zinazowakabili wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli kwa Mbunge huyo kwa ajili ya wilaya ya Pangani ambayo ni mashuka 50 na vitanda 25
  Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga kulia akielezea Changamoto zinazowakabili wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli kwa Mbunge huyo kwa ajili ya wilaya ya Pangani wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa ntiba wilaya ya Pangani
  Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza katika makabidhiano hayo
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabasi Chambasi akizungumza katika halfa hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso mara baada ya hafla hiyo kwa kumshukuru Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa tiba kwenye wilaya hiyo
  Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo 

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua miradi ya Tasaf.
  Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
  Balozi Seif akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga wakishuhudiwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula.


  Picha na – OMPR – ZNZ.

  Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.

  Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.

  Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yao waliyoianzisha. 

  Bwana Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.

  Alifahamisha kwamba Benki ya Dunia kupitia washirika wake imeamua kuunga mkono miradi ya Maendeleo kwa Wananchi Maskini katyika Nchi zinazoendelea ikilenga kuona ufanisi wa kudumu unapatikana katika kustawisha maisha yao ya kila siku.

  Wakitoa ufafanuzi zaidi wa ziara hiyo ya kukagua Miradi ya Tasaf Visiwani Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto { UNICEF} Bwana Paul Quarles walisema upo ushahidi wa fedha zainazotolewa na Tasaf kutumika katika utaratibu Maalum uliowekwa.

  Walisema ujenzi wa nyumba za kudumu, upatikanaji wa sare za skuli, uanzishwaji wa Vitalu vya miti ya kudumu, ujenzi wa majengo ya Skuli na Madrasa kwa kaya Maskini ni mfanbo wa matumizi hayo sahihi ya fedha hizo.

  Wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarpamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa usimamizi wake mzuri kwenye miradi ya Mfuko huo wa Tasaf.

  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Benki ya Dunia kupitia Wadhirika wake wa Maendeleo haikupoteza Fedha iliyotoa katika kuanzishwa kwa Mradi huo.

  Balozi Seif alisema Mfuko wa Tasaf tokea kuanzishwa kwake katika awamu zote mbili zilizopita imeibua miradi mingi ya Jamii katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba na kuweza kusaidia ajira na kupunguza Umaskini.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Ujumbe huo ameiomba Benki ya Dunia kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika harakati za kupambana na ukali wa maisha na kustawisha Jamii.

  Ujumbe huo wa Viongozi wa Benki ya Dunia ulioambatana na Washirika wake wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Umoja wa Mataifa Kuhudumia Watoto { UNICEF} na lile la Idadi ya Watu {UNFPA}na Viongozi wa Tasaf Bara na Zanzibar walikuwepo Zanzibar kwa ziara ya siku Nne kukagua Miradi ya Tasaf.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  26/5/2017.

  0 0

  DJ Buster kutoka Lake Fm akisababisha burudani kweny Gulio la katika Mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza.

  102.5 Lake FM Mwanza, #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo leo Mei 26,2017 imezindua rasmi burudani za Gulio la Mtaa kupitia kampeni yeke ya usafi ya Ng'arisha Nzengo Uchafu Nuksi.

  Burudani leo iko katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza kisha itahamia kwenye minada yote Jijini Mwanza ambapo kuna makumi ya wasanii watakaoshusha burudani kali balaa.

  Kupitia burudani, Lake Fm inahamasisha suala la usafi minadani na mkoani Mwanza kwa ujumla. Pia kila mnada atatafutwa Mama Lishe Bora, Balozi Imara na Mwananzengo Hodari ambapo watajipatia zawadi.

  Burudani za Gulio la Mtaa zimepewa nguvu na Pepsi, Tigo, Busy Bee, Barmedas Tv, Genic Studio, Mama Salakika Deco, Lake Zone Tents & Supply, Mamba Entertainment, CF Hospital, Gerusalem Sound na BMG.
  Wanyakazi wa Lake Fm
  Wanyakazi wa Lake Fm
  Mwananzengo katika ubora wake
  Raha ya Rock City
  Burudani
  Wanyakazi wa Lake Fm, kulia ni Tatu Jabu na kushoto Fatuma Sinda
  Vester JTZ kutoka Lake Fm Mwanza
  Morice kutoka Lake Fm akihost burudani ya Gulio la Mtaa, Mnada wa Nyakato
  Haroun Tambwe kutoka Lake Fm
  Amina Swedy kutoka Lake Fm
  Eve kutoka Lake Fm
  Amos kutoka Lake Fm
  Mtangazaji wa kipindi cha Kijiji Pub kutoka Lake Fm
  Washereheshaji kutoka Barmedas Tv Mwanza
  Stage ya Gulio la Mtaa
  Wananzengo kwenye ubora wao
  Katikati ni Mkurugenzi wa Lake Fm, Doreen Noni, akiteta jambo kwenye Gulio la Mtaa
  Zawadi za tisheti kwa Wananzengo
  Wananzengo kwenye Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa na Wananzengo wa Lake Fm
  Back Stage, Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wananzengo na Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wananzengo na Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wananzengo na Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Back Stage, Wananzengo na Wasanii watakaoshambulia jukwaa la Gulio la Mtaa
  Shukurani sana Tigo, Jaza Ujaziwe
  Wananzengo tayari kwenye Gulio la Mtaa
  Wananzengo wako tayari kwenye Gulio la Mtaa
  Wananzengo wako tayari kwenye Gulio la Mtaa
  Wananzengo wako tayari kwenye Gulio la Mtaa
  Burudani zimeanza kwa kasi
  Sogea Mnada wa Nyakato National upate burudani za Gulio la Mtaa kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga. Picha na Fatma Salum- MAELEZO   Na Fatma Salum (MAELEZO)

  Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi utakaosaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Lazaro Kitandu alisema uamuzi huo wa kuanzisha mfumo mpya umekuja baada ya Serikali kugundua kuwa kwa muda mrefu matumizi ya mbolea hapa nchini si ya kuridhisha kutokana na bei ya mbolea kuwa juu.

  “Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mbolea imeanzisha mfumo huu baada kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam waelekezi wa ndani na nje ya nchi na kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja” Alisema Kitandu.

  Kitandu alieleza kuwa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA), Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye matumizi ya chini ya mbolea kwa kutumia kilo 19 za virutubisho hivyo kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo ambapo kiasi hicho hakiendani na malengo ya azimio la Maputo la nchi za SADC linalotaka kufikia angalau kilo 50 kwa hekta moja.

  Alisema kuwa kwa msimu wa mwaka 2017/2018 mfumo huo utaanza na aina mbili tu za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na mbolea nyingine zitafuata baadaye kadri itakavyoonekana mfumo huo kuleta manufaa kwa wakulima.

  Akifafanua kuhusu faida za mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja, Kitandu alisema utasaidia kuimarisha utaratibu wa usambazaji wa mbolea ambapo wadau wote watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani.

  Kwa mujibu wa Kitandu pia mfumo huo utawezesha wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

  “Ununuzi wa mbolea kwa pamoja pia utasaidia kudhibiti bei ya mbolea iwapo kutajitokeza ongezeka lisilokuwa na sababu (soko holela) kwa kuwa bei itatangazwa kwa kuzingatia bei halisi ya mbolea, gharama halisi za usafirishaji wa mbolea, tozo mbalimbali na kiwango stahiki cha faida ya mfanya biashara” alibainisha Kitandu.

  Serikali kupitia mfumo huu inatarajia matokeo chanya katika kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima hivyo kuongezeka kwa matumizi ya mbolea na uzalishaji wenye tija ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungua mashindano ya COPA UMISSETA uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yussuph Singo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya CocaCola Eric Ongara na anayefuatia ni Rais wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Bw.Vitalus Shija.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kwa mashindano ya COPA UMISSETA katika uwanja wa mpira wa Taifa.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na washiriki wa michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi iliyofunguliwa leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipiga mpira kuashiria kufungua mashindano ya michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

  Na Lorietha Laurence-WHUSM
  Dhana ya kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya COPA UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

  “Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Kampuni ya CocaCola katika kuhakikisha tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa  kupata  wanamichezo mahiri wa baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.

  Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi.
  Vilevile aliwataka walimu kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo kwa shughuli nyingine.

  Hata hivyo Mhe. Mwakyembe aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawapatia watoto wao nafasi ya kucheza na kujifunza michezo mbalimbali inayowajenga kimwili na kiakili.“Michezo inafaida kubwa kwa afya ya binadamu  ikiwemo kuimarisha akili na mwili, kujenga ushirikiano na urafiki baina ya watu “ alisema Mhe. Mwakyembe.

  Naye Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya CocaCola Bw. Eric Ongara alisema kuwa Kampuni ya CocaCola inaamini katika kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini ndio maana wamekua wakidhamini mashindano hayo.

  Pia aliongeza kuwa Kampuni ya Coca-Cola itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa michezo inazaa matunda na kufikia lengo lililokusudiwa la kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza.

  Michezo ya COPA UMISSETA ilifunguliwa rasmi  Mjini Dodoma Aprili 28 mwaka huu ambapo kitaifa yanatarajiwa  kuanza Juni 6 hadi 15 mwaka huu katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza .

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Dk. Juliana Palangyo amewaagiza wahandisi wa Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara nchini Tanroads kufanya nguvu kwa pamoja ili kuweka alama za miundombinu ya mradi wa kuboresha umeme wa Dar es Salaam itapita katika barabara ya Mandela mpaka kurasini.

  Dk .Palangyo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akikagua sehemu ya miundombinu hiyo itakayopita kwa kushirikiana na Tanroads .

  “Tanesco wamekubaliana na Wakala wa Barabara nchini kupitisha sehemu ya miundombinu ya umeme kando kando mwa barabra ya Mandela hili kuweza kuongeza nguvu katika kituo cha kurasini na mkoa mzima wa Dar es Salaam.Makabuliano haya yamefikiwa leo mara baada ya mimi kutembelea katika ofsi za Tanroads na sehemu ambapo miundombinu hiyo itatakiwa kupita”.

  Dkt. Palangyo amesema kuwa wameamua kufanya mazungumzo na Tanroads hili kufikia muafaka kwakuwa wao nao walitaka kutumia eneo hilo katika moja ya miradi yao hivyo kufikia muafaka wa hili kumewezesha mradi wa tanesco kwenda kwa kasi zaidi ya awali.


  0 0

  Kampuni ya simu ya Mkononi ya itel imemtambulisha Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa Balozi wa kampuni hiyo hapa nchini.

  Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Irene amesema amejisikia faraja kuwa balozi na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.

  Amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na kuweza kufanya makubaliano ya kuwa balozi katika kuunganisha itel na watanzania  kwa ujumla.

  Kwa upande  Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan amesema kuwa wanatarajia  jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Irene Uwoya katika matukio ya kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi kwa utoaji wa misaada.

  Amesema kuwa wanamkaribisha balozi mpya itel Tanzania Irene Uwoya kuungana na familia ya kubwa ya itel.

  "Sote tunafahamu mchango wa Irene Uwoya kwenye jamii amekuwa akielimisha kupitia filamu zake na kutambua umuhimu wake sisi itel Mobile tutashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha jamii inapata kile inachotarajia kukipata kwetu na kwake pia" amesema Chan.
   Mkuruegenzi wa itel, Coopeer Chan akisaini makubaliano  na Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency  jijini Dar es Salaam.
   Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akizungumza na waandishi wa habari juu kuwa balozi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi leo jijini Dar es Salaam.
   Afisa Masoko  wa itel, Asha Mzimbili akizungumza na waandshi habari  juu makubaliano katika balozi mpya itel, Irene Uwoya leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuruegenzi wa itel , Coopeer Chan akibadilishana hati ya makubaliano  na Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency  jijini Dar es Salaam.
  Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akiwa katika picha ya pamoja wafanyakazi itel leo jijini Dar es  Salaam.

  0 0  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Tixon Tuyangine Nzunda  kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Benard Mtandi Makali kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Clifford Katondo Tandari kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Ikulu jijini Dar es Salaam.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Viongozi waliopishwa wakila Kiapo cha Uadilifu –Ikulu jijini Dar es Salaam. wakwanza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Tuyangine Nzunda, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Mtandi Makali,  Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clifford Katondo Tandari pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe, akitoa ufafanuzi mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari,kuhusiana na namna mfuko huo unavyoweza kuhudumia wateja wake,katika semina iliyofanyika leo mapema leo jijini Dar.Pichani kati ni
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga pamoja na Katibu wa Jukwaa hilo Neville Meena. 
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga akichokoza Mada zilizowasilishwa na wataalamu wa mfuko huo wa LAPF,mbele ya Wahariri wa Vyombo vya Habari,zikiwemo mada zilizohusu Afya,mambo ya Uzazi kwa akina mama,Mafao mbalimbali ikiwemo fao la Elimu,fao la Kujitoa.Pichani kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe,kushoto ni Ofisa Mwandamizi Mipango na Uwekezaji, Eliya Shola pamoja na Meneja Mafao wa LAPF, Ramadhan Mkeyenge kutoka LAPF
  Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo wa LAPF.
  Meneja Mafao wa LAPF, Ramadhan Mkeyenge, akitoa mada katika semina hiyo.Mkeyenge alisema kuwa mfuko huo mpaka sasa umeweza kutoa mafao na mikopo kama vile,mafao ya uzazi ambapo zimetolewa zaidi ya bilioni 12,mkopo wa elimu zaidi ya bilioni moja zimetolewa,mkopo wa kujikimu zaidi ya bilioni 5,mikopo ya nyumba zaidi ya bilioni 2,pamoja na hayo akaongeza kusema kuwa pia kuna waliolipwa kabla ya muda wa kustaafu Zaidi ya bilioni moja.
  Ofisa Mwandamizi Mipango na Uwekezaji, Eliya Shola, akitoa ufafanuzi kuhusiana na uwekezaji mbalimbali unaofanywa na mfuko huo,ikiwemo katika suala la viwanda na namna ambavyo imechukua tahadhari katika suala zima la usimamizi wa viwanda hivyo
  Ofisa Habari wa Mfuko wa LAPF, Rehema Mkamba (kushoto), akiwa na baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo.


  Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina hiyo ilioandaliwa na LAPF,na kufanyika mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi JR.


  0 0


  Lori lililopakia Boti ya MV MKONGO likipita chini ya daraja la Furahisha jijini Mwanza. Boti hiyo inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inasafirishwa kuelekea mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo
  Boti ya MV MKONGO inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikiwa imepakiwa kwenye lori, Boti hiyo inasafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea Utete Pwani kwa ajili ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo.
  Lori lililobeba Boti ya MV MKONGO inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) likiwa njiani kuelekea mkoa wa Pwani, boti hiyo inatarajiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo.PICHA ZOTE NA THERESIA MWAMI (TEMESA)

older | 1 | .... | 1247 | 1248 | (Page 1249) | 1250 | 1251 | .... | 1897 | newer