Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 26,2017


Mfuko wa LSF watoa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii. Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii. Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii. Wakili Harold Sungusia akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada anuai. Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Robart Zephania (mbele aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo.

ZANTEL KUTOA OFA KWA WATEJA WAKE KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI

$
0
0


·         Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo  mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia vifurushi cha kimataifa cha uarabuni.

Tunapokaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini  wanapoelekea kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.

Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bwn. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana  na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.

Bwn. Janin ameelezea kwamba kutakua na bidhaa mbalimbali zitakazotolewa katika kipindi hiki na anawasihi wateja wa Zantel wavipe kipaumbele bidhaa hizi. Ofa hizi zitaanza rasmi tarehe 26/5/2017.

Akielezea Zaidi kuhusu ofa hii, Meneja wa bidhaa na mawasiliano Bi. Rukia Mtingwa amesema “Ofa hii itashirikisha vifurushi vya Bonga na Mpakabasi ambapo wateja wa Zantel watapata punguzo la asilimia 50 kupiga simu kuanzia saa 5usiku hadi saa 11 asubuhi na Zaidi wataweza kupata huduma zetu mpya tulizozindua hivi karibuni kama ‘ZanteL Madrassa’ ambapo wateja wanaweza kupata mufunzo ya dini ya kiislamu kama Quran, Hadith, duah, habari za bakwata, na huduma nyingine nyingi zinazopatikana kupitia kupiga simu, ujumbe wa maneno na programu za simu”.

Bi.Mtingwa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi  kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu  Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 10 kupiga simu kwenda kwenye  nchi tajwa, na fedha hizi zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti za salio za wateja.

Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586

Zantel inaendelea na mradi wake wa kuboresha mtandao wake kuwa wa kisasa Zaidi visiwani Zanzibar ili kuhakikisha wateja wake wanafurahia huduma zinazoaminika Zaidi zikiwemo huduma ya mtandao wa intaneti wa kasi Zaidi wa 4G, na kwa mara ya kwanza huduma za kibenki za KIISLAM kupitia simu za mkononi.

TASAF YANG’ARISHA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KISIWANI UNGUJA.

$
0
0

NA ESTOM SANGA-ZANZIBAR.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – unaendelea kuboresha maisha ya walengwa wake Kisiwani Unguja ambao wameanza kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali kwa kutumia fedha za zitolewazo na Mpango huo.

Mmoja ya walengwa wa Mpango huo kutoka shehia ya kijini ,kisiwani Zanzibar Bi. Hafsa Seleman Abdallah mama wa watoto WANANE amewaambia wadau wa maendeleo na viongozi nwa TASAF waliotembelea kijijini hapo kuonana na walengwa wa Mpango huo kuwa kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF ameweza kuanzisha shamba la migomba ambalo limeanza kumwingizia kipato kutokana na mauzo ya ndizi kutoka shambani humo.

“Ninaishukuru sana serikali na watu wa TASAF kwa kunitoa kwenye dimbwi la umaskini hadi sasa namiliki shamba hili la migomba kupitia fedha walizonipatia” amesema mama huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hivi.

Amesema mikungu ya ndizi iliyoko shambani mwake imekwishanunuliwa hata kabla ya kuvunwa kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo hasa wakati huu wa kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo mkungu mmoja huuzwa kwa shilingi 20,000.

Katika hatua nyingine walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika eneo la Kijini huko Makunduchi kisiwani Unguja wameanzisha vitalu vya miche ya matunda na kupanda mboga mboga kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda .Kwa mujibu wa maelezo ya sheha , eneo hilo hapo awali halikuwa likizalisha mboga mboga kutokana na aina ya ardhi iliyochanganyika na mawe.

Hata hivyo chini ya utaratibu wa ajira za muda walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini wameweza kuboresha ardhi hiyo kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na wameweza kulima mboga za majani , pilipili hoho na hata vitunguu mazao ambayo huyauza na kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga aliyeshika kitabu akiwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Kijini kisiwani Unguja Bi. Hafsa Seleman Abdallah wakiwa katika shamba la migomba alilolianzisha mlengwa huyo kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo la Kijini ,Makunduchi –Unguja Bi. Hafsa Seleman Abdallah akiwa ndani ya shamba lake la migomba alilolianzisha kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa kijiji cha Kijini ,Makunduchi kisiwani Unguja wakisikiliza nasaha kutoka kwa wadau wa maendeleo (hawapo pichani ) waliotembelea eneo hilo kuona na mna walengwa hao wanavyonufaika na fedha za Mpango huo.
Wadau wa Maendeleo na viongozi wa TASAF wakiangalia Kamba za kungia mifugo zilizosukwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo la Kijini,Makunduchi –Unguja kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. Uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa walengwa ni sehemu muhimu ya Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.
Picha ya juu na chini ni baadhi ya wadau wa maendeleo na viongozi wa TASAF wakiwa katika bustani ya mboga iliyoanzishwa na walengwa wa Kijini ,Makunduchi kisiwani Zanzibar chini ya utaratibu wa Ajira ya Muda ambayo hutekelezwa kwa siku 15 kila mwezi kwa kipindi cha miezi minne wakati wa hari na kisha hulipwa ujira ili kuwaongezea kipato.
Moja ya nyumba iliyoezekwa kwa mabati yaliyonunuliwa na Mlengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini katika eneo la Kijini –Makunduchi kisiwani Zanzibar.
Kiongozi wa shughuli za TASAF katika benki ya Dunia,TTL, Bwana Muderis Mohamed akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (hawapo pichani ) baada ya kutembelea kaya za walengwa katika eneo la Kijini, Makunduchi kisiwani Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara ya wadau wa maendeleo kuona mafanikio na changamoto cha Mpango. 
Bi. Hafsa Seleman Abdallah (aliyeshika kikapo) mkazi wa kijiji cha kijini Makunduchi kisiwani Unguja akiwa katika picha na baadhi ya wadau wa maendeleo waliotembelea shamba la migomba alilolianzisha kwa kutumia fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini. Aliyevaa suti nyeusi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga na kulia kwake ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Muderis Mohamed.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHEREHEKEA KUWASILI KWA NDEGE YAKE YA 10 AINA YA A380

$
0
0
 Wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad wakifurahia kuwasili kwa ndege yao ya 10 na ya Mwisho aina ya A380
 Ndege ya Etihad A380s inatoa huduma kutokea nchi za uarabuni kwenda mji mkuu wa London, Sydney, New York na kuanzia tarehe 01/07/2017 watakua Paris.        

 Wafanyakazi wa shirika la Ndege la Etihad wakijumuika pamoja katika uwanja wa ndege wa Hamburg Finkenwerder nchini ujerumani barani Ulaya ambapo ndege hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa shirika la ndege la uarabuni kabla ya kuanza safari zake za uwasilishaji nchini  Abu Dhabi.
   
Ndege za aina ya A380s zilizojishindia tuzo kadhaa, ni ndege za kibiashara zenye utofauti wa kipekee kwenye huduma zao kama malazi –vyumba vitatu vyenye ukubwa wa kuweza kuishi watu mpaka wawili vikiwa na sebule, bafu binafsi na chumba cha kulalia. Ndege hizi pia zinajivunia kuwa na “appartments” 9, studio za biashara 70, mahala pa kupumzikia na siti nzuri 415 kwenye daraja la uchumi.

DC MTATURU AKABIDHI NYUMBA 12 ZA WALIMU WA SEKONDARI

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizindua rasmi nyumba zilizojengwa kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari za Minyughe na Wembere baadhi ya aliofuatana nao ni mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Minyughe Saddack. Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua nyumba 12 za walimu baada ya kuzizindua.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wilaya,kata na walimu waliokabidhiwa nyumba kwenye shule ya sekondari ya Minyughe.

…………………………………………………

MKUU wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amekabidhi nyumba 12 za walimu wa shule ya Sekondari ya Minyughe na Wembere huku akiwaasa walimu kumpa nguvu rais dokta John Pombe Magufuli kwa kuzitunza ili zidumu na kama sehemu ya kuunga mkono jitihada zake za kuwatumikia wananchi.

Nyumba hizo zimejengwa kupitia mpango wa serikali wa kuendeleza shule za sekondari(SEDEP II) uliogharimu shilingi milioni 300 hadi kukamilika kwake.

Akikabidhi nyumba hizo Mtaruru alimshukuru rais dokta Magufuli kwa dhamira yake njema ya kuwahudumia watanzania ili wawe na maisha mazuri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ya mwaka 2015 iliyoeleza uboreshaji wa elimu ikiwemo mazingira ya kufundishia.

“Tukio hili ni ushahidi tosha wa namna ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo,nyumba hizi zitasaidia kuwasogeza walimu karibu na mazingira ya shule na hivyo kuwapa utulivu wa kuandaa masomo yao hali itakayosaidia kuongezeka kwa ufaulu kama moja ya maazimio ya mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika mwezi disemba mwaka jana lakini pia itaondoa kero ya walimu kuhangaika mitaani,”alisema Mtaturu.

Aliwataka walimu kuendelea kuiamini serikali wakati inaendelea kushughulikia kero,stahili na madai yao na kuwapongeza kwa ushirikiano walioutoa kwa wakandarasi uliorahisisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri Ally Mwanga alisema uamuzi wa kupeleka mradi huo kwenye shule hizo aliufanya kwa kushirikiana na madiwani baada ya kata hizo kuwa na mazingira magumu ya kukosekana hata nyumba za kupanga na kuwapongeza wataalam kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati na kwa kiwango bora.

“Tunaishukuru serikali yetu kwa kuwajali walimu kwa kuhakikisha wanapata makazi bora lakini pamoja na upatikanaji wa nyumba hizi bado kuna uhaba wa makazi ya walimu ambapo mahitaji ni nyumba 524 na zilizopo ni 60 tu,”alisema Mwanga.

Mkuu wa shule ya Minyughe mwalimu Augustino Nkhotya akizungumza kwa niaba yaw engine alisema kukamilika kwa nyumba hizo ni ukombozi mkubwa kwa kuwa awali walikuwa na nyumba mbili hali iliyowalazimu walimu kupanga umbali wa zaidi ya kilomita mbili na hivyo kupunguza tija ya ufundishaji.

Nae mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati aliipongeza serikali kupitia mkuu wa wilaya kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM ambayo kipindi cha kampeni waliinadi na wananchi waliichagua na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na wananchi katika kuboresha maisha yao.

Mradi wa SEDEP II ulitengewa jumla ya shilingi milioni 777 kwa wilaya ya Ikungi ikiwa ni ujenzi wa madarasa,nyumba za walimu na matundu ya vyoo miradi ambayo yote imekamilika

CCM YAMPONGEZA JPM SAKATA LA MCHANGA WA MADINI, YALAANI VIKALI MAUAJI MKOANI PWANI

$
0
0
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Mathias Canal

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya ushindi ya CCM ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Kimetoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Polepole alisema kuwa uamuzi wa kuundwa kwa kamati hiyo ulitokana na kukamatwa kwa makontena 277 ya mchanga huo katika bandari ya Dar es salaam Machi 23 Mwaka huu baada ya Rais kufanya ziara ya kushitukiza katika bandari hiyo na kukuta makontena 20 yakiwa mbioni kusafirishwa kinyume cha maelekezo yake ya Machi 2 ya kuzuia kusafirisha mchanga huo nje ya nchi.

Alisema kuwa huu sio wakati wa kulumbana na kutofautiana kisa itikadi za vyama bali ni wakati wa kusimama pamoja na kuikabili vita ya kiuchumi kwani kwa kuzingatia taarifa iliyosomwa na Profesa Mruma mbele ya Rais Magufuli imebainisha jinsi Taifa lilivyopata hasara ya mabilioni ya fedha kwa kuwa makontena yaliyozuiliwa bandarini yana thamani ya madini yaliyomo kwa kiwango cha wastani wa shilingi Bilioni 829.4 na kiwango cha juu ni Shilingi Trioni 1.4

"Tumeibiwa na kudhulumiwa sana mali zetu ambazo tumezirithi kutoka kwa babu zetu lakini awamu ya Tano ikiongozwa na Rais Magufuli imeamua kwa dhati kabisa kutilia mkazo Vita dhidi ya Rushwa, Uhujumu uchumi, Udhalimu wa kila namna, sambamba na wizi na ufisadi kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania na Watanzania wote" Alisema Polepole

Akizungumzia Mauaji yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini hususani Mkoani Pwani katika Wilaya ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga alisema kuwa kipindi hiki kigumu kwa kuwapoteza ndugu zetu vyama vya siasa vilipaswa kushikamana kwa pamoja pasina kujali itikadi zao badala yake vimeanza kutumia misiba hiyo kwa maslahi ya kiuongozi kuliko maslahi ya Taifa.

Polepole alisema kuwa vyombo vyote vya serikali vinavyoshughulikia ulinzi vinapaswa kutumia Rasilimali zao, Weledi na Utendaji wao, na kuweka umaalumu katika kuyakabili matukio ya mauaji na kuyakomesha kabisa.

"Hakuna dini yoyote Duniani inayoamini katika kutoa uhai wa mtu ambapo pia kuua mtu ni kinyume na Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Tunataka amani ya wananchi wetu inarudi" 

"Tunatambua kuwa wananchi wetu wanapita katika wakati mgumu kutokana na kukatishwa kinyama maisha ya Wananchi wenzao, Viongozi, Askari, Watendaji wa serikali, Wanachama wa CCM si kwa sababu ya mapenzi ya Mungu Bali kwa sababu yamekatishwa katika namna inayokiuka ubinadamu kwa kuuawa kikatili na watu wasio na Utu, Hisia na Imani ya Dini" Alisema Polepole

Polepole ametilia msisitizo wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kuhusu watu wanaofanya mauaji hayo kwani ushirikiano huo utasaidia kufichua uovu wa wadhalimu wanaokatisha maisha ya watanzania.

Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu

$
0
0
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella alipowasili kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na wadhamni hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe akimsikiliza jambo kwa makini Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(katikati) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana, kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella.
Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi,akiongea wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi mbalimbali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe, akiongea na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe,akipewa hongera na Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi baada ya kuongea na wadau walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.

“Kama sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa nchi kwani wanamichezo wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua yote haya yanawezekana na dalili zimeanza kuonekana.

Alisema Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo mingine kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika kutangaza Taifa na pia michezo huchangia kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.

“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau timu zote zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa zawadi zao leo.

Ni matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza kuandaliwa vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,” alisema Hisham.

TAARIFA KWA UMMA:Ngos Zinazotarajiwa Kufutiwa Usajili

Mwakaboko: Milioni za Biko zinanikomboa kiuchumi

$
0
0
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia zoezi la kuingiza fedha hizo katika akaunti ya mshindi huyo wa Milioni 10 na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa droo ya nane ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Daniel Mwakaboko, jana amepokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa zawadi aliyoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko itamkomboa kiuchumi na kumuondoa kwenye hatari ya umasikini inayowakumba vijana wengi.

Akizungumza jana katika makabidhiano ya fedha zake, Mwakaboko alisema kwamba zawadi ya fedha taslimu Sh Milioni 10 ni nyingi kwa wakati huu anaposaka maisha bora kwa kutafuta mtaji mara kadhaa bila mafanikio.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.


Alisema kwa sasa anafanya kazi ya kuchapisha majarida na vitu tofauti tofauti vya kiofisi katika ofisi ya mtu mwingine, hivyo ni wakati wake wa kuangalia namna gani atazitumia vizuri fedha za ushindi alizokabidhiwa baada ya kuibuka na ushindi kartika droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumatano.

“Biko ni mchezo mzuri usiochosha na unaoweza kumpa kila mmoja wake ushindi kwa sababu hata uchezaji wake wa kuweka muamala kwa simu za Tigo Pesa, MPESA na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ni rahisi maana unachotakiwa ni kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 tayari kusubiri zawadi ya papo kwa hapo au droo kubwa ya Sh Milioni 10.

“Nina ndoto ya kufanikiwa kiuchumi lakini pia sitahasahau kiwanja maana vitu vyote hivi vilikuwa vikisisumbua kwa siku nyingi na nadhani Mungu amejibu maombi yangu maana hapo kabla hali yangu ilikuwa ngumu,” Alisema Mwakaboko mkazi wa Tabata na mwenye asili ya mkoani Mbeya.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba kampuni yao imejipanga ipasavyo kuhakikisha kwamba kila mtu anavuna mamilioni ya Biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni Moja ambayo hulipwa papo kwa hapo dakika chache baada ya mshindi kupatikana.

“Nawaomba Watanzania wote bila kuangalia unapatikana eneo gani la Tanzania kucheza Biko mara nyingi zaidi ili kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi na kupata suluhu ya changamoto za kimaisha kwa kupitia mchezo wa Biko maarufu kama Nguvu ya Buku,” Alisema Heaven.

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi ambapo pindi mtu anaposhinda hupewa zawadi yake kwa haraka, ambapo mpaka sasa zaidi ya wateja 32000 wamepatikana na jumla ya Sh Milioni 80 zimelipwa kwa washindi nane tu.

“Mpaka sasa tumefanya droo kubwa za kuwania Sh Milioni 10 nane na tayari wateja wameshapewa stahiki zao hivyo kuifanya Biko kutoa Sh Milioni 80 kwa washindi wake nane ukiacha wale wanaolipwa papo kwa hapo ambao ndio wengi na wanatoka kila mikoa ya Tanzania,” Alisema.

Droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10 inayochezeshwa na Biko inafanyika mara mbili kwa wiki ambapo ni Jumatano na Jumapili, huku mshindi wa zawadi za papo kwa hapo akipatikana kila baada ya dakika chache.

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Mfalme Letsie wa III wa Lesotho

$
0
0
Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho 
Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho, alipo kutana nae na kufanya mazungumzo. 


Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amemhakikishia Mfalme Letsie wa III wa Lesotho kuwa Asasi ya Ushirikiano ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama imethibitisha pasipo mashaka utayari wa wapiga kura wa nchi hiyo kupiga kura siku ya Jumamosi tarehe 3 Juni 2017. 

Hayo yamesemwa kwenye mazungumzo ya viongozi hao ambapo Mhe. Dkt. Mahiga alimuelezea Mtukufu Mfalme Letsie wa III, hatua mbalimbali za uangalizi wa uchaguzi zilizochukuliwa na Jumuiya ya SADC tangu alipofika nchini Lesotho. Jumuiya hiyo mbali na kupeleka waangalizi 41 wa uchaguzi kutoka kwenye nchi tisa wanachama, pia ina wajumbe wawili wa Baraza la Ushauri wa Masuala ya Uchaguzi ambapo mmoja wa wajumbe hao ni Jaji Mstaafu John Tendwa wa Tanzania. 

Mhe. Mahiga pia alisifu jitihada za Serikali na Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho ambao kwa pamoja wamehakikisha kuwa mazingira mazuri yameandaliwa yatakayoruhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufanyika kama ilivyopangwa.

Kwenye mazungumzo yao, Mhe. Mahiga alitumia pia nafasi hiyo kumpelekea Mfalme Letsie salaam za heshima kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ambayo inaundwa na nchi za Tanzania, Msumbiji na Angola kwa sasa. 

Kwa upande wake, Mtukufu Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho alimshukuru Mhe. Rais Magufuli kama kiongozi wa asasi hiyo muhimu ya Jumuiya ya SADC na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa chini ya uongozi wake makini na mahiri, nchi wanachama wa Jumuiya watatekeleza kwa ufanisi majukumu yao muhimu ya kuendeleza jumuiya. 

Mfalme huyo mrithi wa baba yake Mfalme Moshoeshoe wa II anayetawala Lesotho tangu mwaka 1996 kama Falme ya Kikatiba, alisema anaiheshimu sana Tanzania kwa mchango mkubwa kwa nchi hiyo hususan kwenye kuendeleza taaluma mbalimbali nchini humo. Alisema kwa miaka mingi sasa wataalamu wa masuala ya afya na elimu kutoka Tanzania wameendelea kufanya kazi Lesotho na kuongeza kuwa hata yeye binafsi alifundishwa Chuo Kikuu cha Lesotho na Mtanzania masomo ya Sheria na Sayansi ya Siasa. 

Mtukufu Mfalme Letsie alimaliza kwa kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Lesotho na Tanzania ambapo chimbuko lake ni kuwa nchi zote mbili ni wanachama waanzilishi wa Jumuiya ya SADC. Aidha alionesha nia kubwa ya kuzuru Tanzania siku za usoni, na kumuomba Mhe. Dkt. Mahiga, kufikisha salamu za heshima na ushirikiano kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Maseru, Lesotho 25 Mei, 2017

DC WA SIMANJIRO AWAASA WANANCHI WA KIJIJI CHA LOSOITO KUITUNZA NA KUTOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Ubwani
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Losoito juu ya utunzaji wa
miundombinu ya maji na maendeleo mengine.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula
amewataka wananchi wa Kijiji cha Losoito ,kuitunza na kutohujumu
miundombinu ya maji yaliyowezeshwa na kampuni ya TanzaniteOne.

Mhandisi Chaula aliyasema hayo juzi alipofanya ziara ya siku moja
kwenye kijiji hicho mara baada ya kupatiwa taarifa kuwa kuna baadhi ya
watu wameharibu miundombinu hiyo kwa kukata mabomba.

Alisema miundombinu hiyo imewezeshwa kwa pamoja na kampuni ya
TanzaniteOne na Serikali kwani wanamiliki mgodi huo kwa asilimia 50
kwa 50 hivyo jamii inapaswa kuyatunza kuyathamini na kuyalinda maji.

Alisema atamchukulia hatua mtu yeyote atakayekamatwa akiharibu
miundombinu ya maji kwani wananchi wa eneo hilo kwa muda mrefu
waliteseka kufuata huduma hiyo umbali mrefu hadi Mirerani.

“Nimeambiwa awali kuna mama alishajifungua njiani wakati akifuata maji
na baba wa kimasai akakata kitovu cha mtoto kwa kutumia sime kasha leo
mtu anaharibu miundombinu hii,” alisema mhandisi Chaula.

Mkazi wa Kijiji hicho, Magdalena Peter alisema anashukuru kampuni ya
TanzaniteOne kwa kuwezesha mradi huo wa maji ila bado kuna changamoto
ya upatikanaji kwani wanayapata mara mbili kwa wiki.

“Awali tulikuwa tunapata maji hayo kwa wakati fofauti na tulivyokuwa
tunatembea kilomita 40 hadi Mirerani ila hivi sasa tunawakati mgumu
baada ya tenki hilo kupasuka,” alisema Peter.

Ofisa mahusiano wa kampuni ya TanzaniteOne, Halfan Hayeshi alisema
anaomba apewe muda wa wiki mbili ili ahakikishe anafanyia matengenezo
sehemu za miundombinu iliyoharibika eneo hilo.

“Nitakuja na mafundi wiki ijayo ili waangalie na kuikarabati
miundombinu hiyo na pia tutanunua tenki lenye ujazo wa lita 10,000
tofauti na hili la lita 5,000 linalotumika hivi sasa,” alisema
Hayeshi.

MAONESHO YA VYUO VIKUU VYA NCHINI INDIA KUFANYIKA KESHO UBALOZINI JIJINI DAR

$
0
0
MAONESHO ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho huku yakitarajiwa kutoa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kuvifahamu vyuo vilivyopo nchini humo na ubora wa taaluma zake.

Maonesho hayo ambayo yameandaliwa na Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ubalozi wa India nchini yatafanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

Akizungumzia maonesho hayo, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema, wanafunzi wa kitanzania wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa ya kudsoma katika vyuo ambavyo havina ifa.

“Unakuta mwanafunzi anapewa taarifa ambazo si sahihi hata katika vyuo anachokwenda, na ndio sababu tumeamua kuandaa maonesho hayo ili kubaini vyuo sahihi,” alisema.

Amesema wanafunzo wengi wamejikuta wakisoma katika vyuo ambavyo havina hadhi sawa na ile waliyotegemea, hatua inayowawia vigumu katika kutambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).

Kwa upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema maonesho hayo yatafanyika Kesho na keshokutwa katika ubalozi wa India na kwamba lengo kubwa ni kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wanaolenga kusoma katika nchi hiyo na vyuo vyenye ubora.

Arya amesema maonesho hayo yatashirikisha taasisi 20 za vyuo vikuu ambazo zinazotoa fani tofauti katika ngazi zote za elimu ya juu.

01.Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumzia juu ya maonesho hayo ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).jijini Dar es Salaam.

JUMIA TRAVEL YAANZISHA KAMPENI YA 'DEMOCRATIZE TRAVEL' INAYOLENGA KUWAKOMBOA WAAFRIKA KUSAFIRI NDANI NA NJE YA NCHI KWA GHARAMA NAFUU

$
0
0

Kampuni ya Jumia Travel imeanzisha kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo . 

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee amesema bara la Afrika limekuwa katika mabadiliko ya matumizi ya Mtandao na kufanya kuongezeka kwa mapato ndani katika sekta ya Utalii. 

Amesema kampeni hiyo ina dhumuni la kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni linapokuja suala la mchakato mzima wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine pamoja kupunguzwa kwa gharama za malazi. 

Fatema amesema idadi ya watumiaji wa internet imezidi kuongezeka kwa bara la Afrika na kufikia watumiaji milioni 300 sawa na asilimia 27.7. Matumizi ya Internet yameweza kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii kwa njia ya mtandao ikiwemo na usafiri wa anga. 

Fatema amesema kutokana na takwimu hizo zinafanya kuamini Bara la Afrika lina fursa katika ukuaji wa sekta ya Utalii kwa njia ya mtandao. 

Amesema ripoti ya utalii Afrika 2017 iliyowasilishwa na Jumia Travel inajihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao , ambapo inaonyesha kuwa huduma za simu zimeiingizia Bara la Afrika mapato ya ndani kwa asilimia 6.7 kwa mwaka 2015 sawa na dola za Kimarekani bilioni 150 na itaongezeka kufikia dola za Kimarekani bilioni 210 sawa na asilimia 7.6 ya jumla ya pato la ndani la kitaifa kufikia 2020. 

"Jumia Travel nimeona ujio wa Internet na kupokelewa vizuri na waafrika ni ishara kwamba sekta ya utalii itakua ukizingatia ina mchango mkubwa kwenye kuchangia pato la Taifa",alisema Fatema.

Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari,wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma,Godfrey Kijanga .

Meneja Uhusiano wa Umma-Jumia Travel ,Godfrey Kijanga akitoa ufafanuzi kuhusiana na kampeni hiyo 'Democratize Travel' inavyoweza kurahisisha mambo mbalimbali kwa wateja wao,ikiwemo suala la kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine,kulia ni Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee 
Mwakilishi kutoka hoteli ya Hong Kong ya jijini Dar Es Salaam,Dusa Suleiman akielezea namna Jumia Travel inavyoweza kurahisisha ufanyikaji wa shughuli za kila siku za hoteli,amebainisha kuwa wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kuliko hapo awali kupitia mtandao huo wa Jumia Travel,amesema kupitia mtandao huo wateja wameweza kujua huduma zao mbalimbali,hivyo wateja wao wameongezeka .

Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na  Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee kuhusiana na uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni .Picha na Michuzi JR.

SERIKALI ZA TANZANIA NA UGANDA ZATILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM.

Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55, mjini Kampala Uganda, leo.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi na Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.

Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba  hilo hilo.
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda
 Ujumbe wa Tanzania na Uganda ukishuhudia tukio la utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
 Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi, akihutubia baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakionesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, baada ya kuusaini, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.

TAARIFA KWA UMMA.

WIZARA YA VIWANDA YAANZISHA DAWATI LA BIASHARA

$
0
0

Na Daudi Manongi, MAELEZO,DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha dawati la wepesi wa kufanya biashara ambao lina jukumu la kuondoa ugumu wa kuanzisha na kuendesha biashara  nchini.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni Mhe. Jamal Kassim Ali.

“Ujenzi wa Viwanda nchini unategemea zaidi mazingira ya uwekezaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi yenye miundombinu wezeshi,sera mbalimbali,mifumo ya kodi na mifumo ya upatikanaji wa vibali  vinavyotakiwa kisheria ambayo ni majukumu ya Serikali”Alisema Mhe.Mwijage.

Aidha Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji imeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wa kitanzania ili kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

Miongoni mwa Mikakati hiyo ni Mafunzo yanayotolewa kwa watanzania wenye nia ya kuwekeza katika viwanda juu ya kuibua mawazo ya kibiashara,kuanzisha ,kuendesha na kusimamia biashara kupitia SIDO,kutoa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuchagua teknolojia sahihi inayoendana na wazo la ujenzi wa kiwanda alilonalo Mtanzania kupitia TIRDO,TEMDO na CAMARTEC na namna ya kupata ama kukuza mtaji wa ujenzi wa viwanda kupitia NEDF,SIDO na TIB.

Pamoja na hayo Wizara imeandaa mwongozo kwa Mikoa,Wilaya,Kata na Vijiji kutenga maeneo ,kusimamia sheria,kanuni,taratibu na kutoa maelekezo kwa wawekezaji.

“Watanzania wnaaotaka ama walio na mitaji mikubwa wanaweza kuwekeza kupitia maeneo ya EPZA ambayo yametengwa mahsusi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi,Pia wanaweza kuwasiliana na TIC kupata vivutio mbalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji,Alisisitiza Mhe.Mwijage.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage.

BULEMBO AANZA LEO ZIARA YA KIKAZI KATIKA MIKOA MITANO

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo, leo ameanza ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Jumuia zake, katika mikoa ya Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita, Pichani, Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto, leo katika Ukumbi wa CCM Wilaya hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo, akilakiwa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manayara, Injinia Shekue Pashua alipowasili katika mkoa huo akitokea mkoani Dodoma, kuanza ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa huo, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Manyara Pazo Mwamlima.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa (kulia) akimlaki Bulembo na Msafara wake, alipowasili katika mkoa huo akitokea mkoani Dodoma, kuanza ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa huo, leo. Wapili Kulia ni Mlezi wa CCM Wilaya ya Kiteto, Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu
Msaafara wa Bulembo ukielekea Ofisi ya CCM, Wilaya ya Kiteto leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili Ofisi ya CCM wilaya ya Kitetokuanza kazi
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akisainikitabu cha Wageni katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Injinia Shekue Pashua
Bulembo akimskiliza Kaimu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kiteto Injinia Shekue Pashua, alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya kisiasa na mwenendo wa hali ya uchaguzi wa CCM ngazi za mashina
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Kiteto baada ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM, Wilayani humo leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Manyara Pazo Mwamlima na Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Injia Shekue Pashua
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Kiteto baada ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM, Wilayani humo leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto, leo
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto wakimshangilia Bulembo alipowasili ukumbini kuzungumza nao leo

Baadhi ya wajumbe ukumbini
Baadhi ya wajumbe ukumbini.
Wajumbe wakinyoosha mikono kuunga mkono jambo
Katbu wa CCM Wilaya ya Kiteto akimkaribisha Bulembo kuzungumza
Mmoja wa viongozi waliofuatana na Bulembo kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Ndugu Kalolo akisalimia
Kalolo akikoleza salam zake

Mlezi wa CCM Wilaya ya Kitedo Mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu akisalimia wananchi wajumbe alipotambulishwa
Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Makao Mkuu, Ndugu Mgaya akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa
Meza kuu wakisimama kucheza wimbo wa 'CCM Nambari wani' baada ya kuanzishwa na wajumbe kuchangamsha ukumbi
Mmoja wa viongozi wa CCM akionyesha ushangiliaji wa furaha wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto, leo katika Ukumbi wa CCM Wilaya hiyo.PICHA ZOTE NA BSHIR NKOROMO

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 35, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 26, 2017.

$
0
0
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charels Mwijage akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kuhudhulia kipindi cha Asubuhi cha kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba Bunge la 11 Mei 26, 2017.
 Mbunge wa Mtwara Vijini (CCM) Mhe. Hawa Ghasia wakijadiliana jambo na Mbunge wa Momba (CHADEMA) Mhe. David Silinde katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhulia kipindi cha Asubuhi cha kikao cha 35 Mkutano wa Saba Bunge la 11 Mei 26, 2017.
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.   
 Mbunge wa Mpwapwa (CCM) George Lubeleje akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.    
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakifurahia jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
  Mbunge wa Kaliua (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.    
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
 Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anstazia Wambura(kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe(katikati) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
 Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Mhe. Joseph Haule (Kulia) pamoja na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule (wa pili kulia) na Mbunge wa Tunduma (CHADEMA) Mhe. Frank Mwakajoka (aliyeipa kisogo kamera) wakimsikiliza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charels Mwijage wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
  Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Bulaya akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Ritha Kabati katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Compassion English Medium kutoka mkoani Njombe wakiwa Bungeni wakifuatilia shughuli za Bunge katika dhumuni la kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  

Picha Zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO, DODOMA

Whether at home or abroad Magufuli makes the difference

$
0
0
By Said Ameir

When President John Pombe Magufuli took over the chairmanship of EAC Heads of State Summit during the 17th EAC ordinary summit held early March, 2016 at Ngurdoto, Arusha, none expected that he would give shocking plea to EAC secretariat- stop your lavish spending and spare the community funds to serve the poor!.

His first summit after being elected in power, President Magufuli never showed any newness to the occasion and instead showed his true color by hammering what was unexpected to any of his fellow Heads of State and government.

In his acceptance speech, he never wasted time to pin point that he was of the opinion that the regional body was unwisely spending community funds something which does not reflect the actual state of the economies of the member states.

President Magufuli urged the Secretariat to take cost- cutting measures to rid the regional body from wasting its hard fought resources from their poor citizens and strongly warned members of the secretariat not to mess around with community money!

He pledged to take same measures implementing in his country to reduce government spending including curbing lavish spending on travels and meetings and went further to question as to why the secretariat favors convening meets in expensive resorts instead of using conference halls at the regional body’s headquarters.

The President challenged the Secretariat to become problem solver instead of being always ‘moaners’ and restrict them from being parasitic at the detriment of the poor citizens of member states.

He was of the opinion that the regional body is capable of effectively and efficiently running its business with the merger resources coming from members’ contributions if cost cutting measures were put in place and if Secretariat is to make rational financial decisions.

There were those who were not convinced if that would be possible and some even thought that the President was off target and ill informed. But today, one year down the road, President Magufuli has proved his doubters wrong.

During the 18th Ordinary Summit held in Dar es Salaam recently, where President Magufuli handed over the chairmanship to his Uganda counterpart, President Yoweri Museveni, it was reported that for the first time the regional bloc has managed to save about US $ 2.5 million from its budget due to cost cutting measures imposed during his chairmanship.

President Magufuli has identified himself with group of modern type of leaders who are earnest and shrewd with direct approach to issues. To many Tanzanians and to some of our neighbors, it was not a surprise! He was well known since he was a minister that he was a person who was fond of fine details of all matters under his jurisdiction.

He was never afraid of telling the truth or rather calling a spade a spade. The good thing of him is his strong willpower and firmness to achieve what he believed to be achievable. He is a result oriented leader who is always geared to get the best out everything he believes and cherishes. He likes challenges and that is what he distinguishes himself from others.

He clearly knew that the promise to employ cost cutting measures at EAC secretariat was not an easy task but he was convinced that he has firm support of his fellow Heads of State and government of the member states.

As a leader he made his homework and see how viable was his appeal to introduce cost cutting at the Secretariat and he realized that, it can be done if and only if everyone plays his part.

He warned to use his leadership moto ‘Hapa Kazi tu’ in exercising his duties as Chairperson of EAC and also warned to use his style of ‘kutumbua majipu’ to those who would not heed to his plea but fortunately things went well probably because Secretariat knew that Magufuli is a man of few words but means what he says.

Whilst, we congratulate President Magufuli for showing the way, appreciation should also go to members of the secretariat under chairmanship of the Secretary General Amb. Libérat Mfumukeko for not letting down President Magufuli and his fellow Heads of State.

And as the saying goes ‘When there is will there is a way’. He promised and he has delivered it. This is why they say ‘Magufuli always means business.’ Congratulations for your efforts to make new and prosperous Tanzania, Your Excellency, Dr. John Pombe Magufuli.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images