Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1241 | 1242 | (Page 1243) | 1244 | 1245 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Phili Mangula akikmkaribisha Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, kwa ajili ya mazungumzo, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

  0 0

   Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo katika semina ya kuwajengea  uwezo wa kujiamini na kukabiliana na  changamoto mbalimbali chini ya mpango unaojulikana kama HerAfrica.
  Wanafunzi  wasichana wa shule ya sekondari  ya Premier iliyopo Bagamoyo katika picha ya pamoja wakati  wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na mpango wa HerAfrica.
  ---
  Kampuni ya TBL Group imeelezea dhamira yake ya kuunga mkono serikali na taasisi mbalimbali zinazotekeleza mpango wa kuwajengea uwezo watoto wa kike na kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kusababisha wabaki nyuma.
  Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala yanayohusiana na kampuni wa TBL Group, Georgia Mutagahywa,aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akieleza jinsi kampuni ilivyoshiriki katika semina ya mpango wa kuzungumza na wasichana kuhusiana kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ujulikanao kama HerAfrica.
  “Mtazamo wetu ndani ya kampuni suala la jinsia tunalipa umuhimu mkubwa kwa kuwa tunaamini kuwa wanawake wanao uwezo wa kufanya vizuri wakipata fursa na kuondokana na changamoto zinazosababisha wabaki nyuma na tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi mbalimbali zinazopambana na usawa wa kijinsia na kuondokana na mila potofu zinakwamisha wanawake na kusababisha wabaki nyuma” alisema Mutagahywa.
  Katika semina ya taasisi ya HerAfrica iliyofanyika katika sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo, Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga ,aliungana na wanawake wengine kutoa mada za kuwajengea uwezo wa kujiamini wasichana wanaosoma katika shule hiyo.
  Mbali na mada za kuwajengea uwezo wa kuamini pia wanafunzi hao wasichana walielezwa changamoto mbalimbali wanazoweza kukutana nazo katika ujana wao zinazoweza kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zao na walipewa mbinu na mikakati ya kuzikabili ili waweze kutumiza ndoto zao pia walielezwa umuhimu wa kujibidiisha na masomo yao kwa kuwa elimu ni silaha pekee itakayoweza kuwakomboa.
  Mratibu wa programu hiyo nchini,Lilian Matari,kutoka kampuni ya Ushauri wa kitaalamu ya LAS alisema kuwa hii ni semina ya pili ya kuongea na wasichana kufanyika na mkakati wa kampuni ni kuendesha semina nyingi nchini kote ili kuwafikia wasichana wengi hususani waliopo mashuleni.

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam wakielezea adha wanayokumbana nayo kutokana na uharibifu wa Daraja
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally wakikagua daraja lililovunjika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
  Muonekano wa Daraja la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam likiwa limeharibika

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam


  Na Nasri Bakari, Dar es salaam

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumamosi, Mei 20, 2017 ameagiza kujengwa kwa daraja jipya kutokana na kuharibika kwa daraja la awali katika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.

  Agizo hilo amelitoa mapema hii leo wakati akizungumza Na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara uliowajumuisha pia Mtendaji wa Kata, wajumbe wa mitaa na wataalamu mbalimbali kutoka Manispaa ya Ubungo.

  Mhe Makori amesema kuwa amejionea adha iliyopo katika daraja hilo ambapo sio ubovu wa miundombinu pekee bali pia ni swala la usalama hasa kwa watoto wanaopita katika daraja hilo waendapo shuleni na sehemu mbalimbali.

  "Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii sitojisikia vizuri kuona tunahatarisha maisha ya binadamu kwa namna yoyote ile, lazima nihakikishe mnakuwa salama wakati wote"

  "Hivyo nakuagiza Mkurugenzi kuanza haraka ujenzi wa daraja hili ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidi wananchi Wetu hawa kupita kwa usalama zaidi" Alisema Mhe Makori.

  Aidha amesisitiza kuwa kodi zinazokusanywa na serikali ni kwa ajili ya kugharamia na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kama vile kuboresha Sekta ya Elimu, Afya na huduma nyingine za kijamii, hivyo ni lazima serikali ishughulikie na kusimamia mahitaji ya Msingi kwa wananchi wake.

  Sambamba na hayo pia Mhe Makori amewaomba wananchi kufika kwa viongozi wao pindi wanapopata kadhia mbalimbali zinazowasumbua katika jamii inayowazunguka kwani wameajiriwa kwa ajili yao na serikali ya awamu ya tano inajali wananchi wote hususani wanyonge.

  Kwa upande wake Injinia wa Ujenzi Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga amesema kuwa daraja lililokuwa limejengwa awali lilikuwa Dogo ukilinganisha Na wingi wa Maji Jambo lililopelekea kuharibika haraka.

  Mbanga Alisema utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya nitaanza haraka iwezekanavyo ili kufikia mwanzoni mwa mwaka 2018 lianze kutumiwa Na wananchi hao ambao wamepata adha kubwa kwa muda mrefu.

  Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Msumi Ndg Hemed Abdallah Gulamu amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa Kazi kubwa anayoifanya tangu alipoteuliwa kuongoza Wilaya hiyo.

  Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ufanisi katika utendaji Na kusema kuwa uongozi wake utaacha alama kubwa na kukumbukwa na watanzania wote.

  0 0

   
   Anna Makinda ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya(NHIF)akiongea na wagonjwa waliofika leo hospital ya Mkoa wa kigoma kwaajili ya kupata matibabu toka kwa madaktari bingwa.
   Anna Makinda akikata utepe katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma kuzindua zoezi la utoaji wa huduma kwa madaktari bingwa kwa hospitali za pembezoni
   Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya(NHIF)Anna Makinda akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika katika hospita ya Mkoa wa Kigoma(maweni)kwaajili ya kupata huduma za madaktari bingwa.
   
   
  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.

  MAMIA ya wananchi wa mkoa Kigoma wamejitokeza katika kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika mpango unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF).matibabu hayo yanayotolewa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni yanahusisha magonjwa ya kina mama ,magonjwa ya moyo,magonjwa ya watoto ambayo madaktari bingwa wake watafanya kazi hiyo moja kwa moja huku magonjwa mengine ambayo hayana madaktari bingwa utatolewa ushauri wa hatua za kuchukua.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo,Anne Makinda alisema kuwa hakuna mtanzania atakayekufa kwa sababu ya kukosa pesa za matibabu kutokana na serikali kuweka mfumo mzuri unaohakikisha wananchi wote wanapata matibabu kwa gharama nafuu.

  Makinda alisema kuwa kwa sasa wananchi wote wataweza kujiunga na huduma za matibabu za mfuko huo kupitia makundi mbalimbali yalipo kwenye jamii na mitaa na wananchi watapata huduma za matibabu nchi nzima bila kubagua hospitali.

  Alisema kuwa pamoja na hilo mfuko huo unatambua kuwepo kwa changamoto za uhaba wa madawa,vitendea kazi,uchache wa majengo na vifaa vingine vya kutolea tiba na kwamba mfuko huo umzingatia changamoto hiyo na kwa sasa mfuko unatoa mikopo kwa vituo vya afya,zahanati na hospitali ili kuwezesha huduma bora kupatikana wakati wote.

  Akizungumzia utoaji huduma kwa wagonjwa alisema kuwa mfuko unapokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na lugha mbaya na za kuudhi zinazotolewa na watoa huduma na kwamba ikithibitika kwamba yupo mtoa huduma ametoa lugha mbaya kwa wagonjwa watachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.

  Awali wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bernad Konga alisema kuwa mfuko unatambua changamoto iliyopo ya uhaba wa madaktari bingwa uliopo nchini na ndiyo maana mfuko umeanzisha mpango wa huduma za madaktari bingwa wanaotembea ili kuweza kuwafikia wananchi.

  Pamoja na kutoa huduma kwa wananchi Konga alisema kuwa mpango huo pia unalenga kutoa mafunzo kwa watoa huduma waliopo kwenye vituo ambavyo mpango huo unatekelezwa ili waweze kuendeleza huduma husuka baada ya madaktari bingwa hao kuondoka.

  Alisema kuwa tangu kuanza kwa mpango huo jumla ya wananchi 13,000 wamfikiwa na kati yao zaidi ya 600 wamepatiwa huduma za upasuaji wa magonjwa mbalimbali na hivyo kufanikisha mpango wa kuwafikia wananchi kwa karibu.

  Akizungumza kabla ya kuzindua mpango huo Mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga alisema kuwa kumekuwa na uhitaji wa madaktari bingwa mkoani humo ikizingatiwa kuwa kwa sasa mkoa unao madaktari bingwa wawili tu jambo ambalo linafanya wananchi kutumia muda na gharama kubwa kutafuta huduma hizo nje ya mkoa.

  Alisema kuwa mpango huo ni wa maana sana kwani utawasaidia wananchi wa mkoa huo kupunguza makali ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakati huu na kwamba serikali ya mkoa itatoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unakuwa wa mafanikio.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiogea katika kikao hicho cha TRA na Waandishi wa habari Jijini Mwanza, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
  Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ( Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza)
   Viongozi wa Tanzania Chamber of Commerce Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Kamishna wa TRA nchini wakati wa kikao hicho na waandishi wa habari Mkoani Mwanza.

  Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
  Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.
  Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

  “Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

  Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.
  Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

  TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

  Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.

  TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza.
  Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani, kutozwa faini au vyote viwili.
  Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

  “Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

  Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.
  Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

  TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

  Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza.

  Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani, kutozwa faini au vyote viwili.
  Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

  “Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

  Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.
  Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

  TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

  Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella 

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa namna gani TRA inaweza kufanya ili kurahisisha mfumo wa malipo kwakutumia mitandao ya simu, amesema wao kama TRA kila siku hupokea maoni ya wadau ili kuboresha shughuli zao na kwa hali hiyo wanaona ni wazo jema.
  Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, pamoja na majukumu yake imeongezewa jukumu lakukusanya kodi za majengo ambapo mara baada yakukusanya kodi hizo, zitatolewa taarifa, lakini pia zitapelekwa kwenye Halmashauri husika  kwa ajili ya shughuli za Maendeleo.

  0 0

  Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.

  Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu. 

  Taarifa iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo mkuu.

  Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa  mbalimbali yakiwemo  dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.

  “Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.

  SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.
   Naibu Inspekta jenerali wa polisi, Abdulrahmani Kaniki, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO)  ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. 
  Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kamati hizo ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  Jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

  0 0

   Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko cha Mtule (Mtule AMCOS), Bw. Ali Fadhil Ali akiongea wakati Benki ya Kilimo ilipotembelea Kijiji cha Mtule kukagua miradi ya kilimo inayohitaji mikopo.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akizungumza na wanachama wa  Mtule AMCOS (hawapo pichani) kuhusu dhima ya Benki ya Kilimo kuwapatia mikopo nafuu wakulima nchini. Kushoto  ni Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo na Afisa Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Nassor Mohammed (katikati).
   Wanachama wanawake wa Mtule AMCOS wakifuatilia mawasilisho ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB (hayupo pichani) kuhusu uwepo wa mikopo nafuu kutoka Benki hiyo.
   Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kulia) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko cha Mtule.
   Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis (kulia) akiwaonesha eneo linaloendelezwa la Chama chao linalojengwa kwa michango wa wanachama. Alioongozana nao ni Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati).
   Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (kushoto) akitoa ushauri kwa Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis (kulia) kuhusu uendelezaji wa miundombinu ya Ofisi ya Chama.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) akihimiza jambo baada ya kuoneshwa miundombinu ya Ofisi ya Chama cha Mtule AMCOS. Pichani ni Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (kushoto) na Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis (kulia).
  Ugeni wa Benki ya Kilimo wakiwa katika ya pamoja na wanachama wa  Mtule AMCOS.

  Na mwandishi wetu, Zanzibar.

  Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko cha Mtule (Mtule AMCOS) kinachojishughulisha na kilimo cha mbogamboga na matunda  kimeweka bayana nia yake ya kuchangamkia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuwasaidia katika kuendeleza kilimo chao.

  Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea kijijini Mtule, Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis amesema kuwa Chama chake kimejidhatiti katika kufikia soko kubwa la matunda na mboga mboga ila wanarudishwa nyuma na uduni wa mtaji pamoja miundombinu ya masoko.

  “Tulisikia uwepo wa Benki ya Kilimo ila hatukuwa tunajua namna ya kuwapa, leo tunaamini kuja kwenu kijiji hapa kumefufua matumaini yetu ya kupatiwa mikopo ili kuongeza tija kilimo chetu na kipato chetu kwa ujumla,” alisema.

  Akiwasilisha malengo ya safari yao na umuhimu wa Benki hiyo kwa wakulima nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

  Bw. Assenga aliongeza kuwa kilimo cha mbogamboga na matunda  ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa mbogamboga na matunda  nchini.

  Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa kilimo cha mazao yote yatokanayo na mbogamboga na matunda  ili kuongeza tija kwa wakulima nchini kote.

   “Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya uongezaji tija wa kilimo cha mboga mboga na matunda, uongezaji wa thamani wa mazao ya mboga mboga na mtunda ili kuchagiza uongezaji wa kipato kwa mkulima,” alisema.

  Naye, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

  “Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” alisema.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori wakati wa semina kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, malikale na maendeleo ya utalii nchini iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii kwa Wabunge na kufanyika jana Bungeni mjini Dodoma. SOURCE: Daily News-Habarileo Blog.
   Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti (TAWIRI), Dk. Robert Fyumagwa akitoa mada katika semina hiyo juu ya athari za muingiliano wa mifugo na Wanyamapori.

   Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Prof Dos Santos Silayo akitoa mada juu ya umuhimu wa uhifadhi misitu nchini. 

  Profesa Dos Santos Silayo, wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu nchini alisema ni vyema misitu ikatunzwa kwa kuwa ndio utajiri mkubwa kwa watanzania.

  Alisema misitu ndio huzalisha vyanzo vya maji, husababisha mvua, hutumika kama utalii wa ikolojia, hutunza wanyama na ndege lakini kubwa zaidi husaidia katika kutunza mazingira.
   Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCC), Richard Rugimbana akitoa mada yake juu ya maendeleo ya Utalii na Umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania.
   Maofisa wa Wizara ya Mali Asili na Utalii wakiwa katika semina hiyo.
   Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori. 

  Profesa Songorwa endapo uoto wa asili usipohifadhiwa kuna hatari ya kupungua kwa maeneo yaliyohifadhi hewa ya oxygen.

  Changamoto nyingine za kutohifadhi uoto wa asili ni kufa kwa mfumo wa ikolojia, wanyamapori na vivutio vya kitalii kuharibika na kupungua na hata kutoweka. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

  Mbunge Aida Khenani akifuatilia mada.
   Mbunge wa Mpwapwa, George Malima Lubeleje akisoma moja a majarida ya utalii wakati wa semina hiyo.
   Wabunge wakifuatilia mada katika semina hiyo.
   Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akitoa mwongozo katika semina hiyo.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akifuatilia mada
   Wanahabari wakifuatailia kwa makini mijadala katika semina hiyo.
   Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika akliachangia.
   Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel akichangia.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanziakifuatilia mijada ya wabunge katika semina hiyo.
   Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akichangia.
   Mbunge wa Muheza, Adadi Mohamed Rajab alikuwa mmoja wa wachangiaji.
   Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia
  Mbunge wa Newala Vijijini Ajali Rashid Akibar akichangia

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima (katikati) akimuelezea mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Sifuni Mshana (kulia) kiasi cha fedha itakayotumika katika ujenzi wa awali wa miundombinu ya shule mbili kongwe za kilakala na Mzumbe mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua kiwango cha uchakavu wa miundo mbinu hiyo.
  Mshauri muelekezi wa Nousoto Associates, Bw. Thomas Kalugula akitoa taarifa ya upembuzi yakinifu wa mahitaji ya ukarabati wa shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro na kubainisha kuwa, ujenzi wa awali utahusisha mifumo ya maji taka ambayo haifanyi kazi ipasavyo huku akihaidi kuwa watasimamia ujenzi huo hadi hatua ya mwisho.
  Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Morogoro, Bi. Veneranda Seif akikabidhiwa mkataba wa ujenzi wa shule kongwe za Kilakala na Mzumbe ambazo zilielezwa kugharimu kiasi cha shillingi billioni mbili katika ujenzi wa awali huku mkataba huo ukimtaka mkandarasi huyo kuanza ujenzi mapema 2 Juni mwaka huu.
  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu (TEA), Bi. Graceana Shirima akiwa na timu ya wataalamu wakiwemo waandishi wa habari mkoani Morogoro katika kukagua miundo mbinu ya shule ya sekondari Kilakala ili kujionea hali halisi ya majengo na kubaini uwepo wa jengo ambalo halitumiki kutokana na kukosa ukarabati.
  Walimu wa shule ya Mzumbe mkoani Morogoro na wakandarasi wakiwa na kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima wakiangalia shimo la maji taka ambalo lilielezwa kuwa limetitia likazuiwa na magogo kwa tahadhari zaidi hata hivyo majani yanaoneka yameota katika eneo hilo huku likisikika kutoa harufu kali ya vinyesi.
  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima (katikati) akiwa darasani kukagua dali zilizotoboka katika moja ya jengo la kujifunzia shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro.
  Timu ya watalaamu wakiwa na mkandarasi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Morogoro, Bi. Veneranda Seif (wa pili kutoka nyuma) katika ziara ya Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima akikagua majengo yaliyochakaa.
  Bweni la wanafunzi kama linavyoonekana.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Mwalimu Wencelaus Kihongoti akimpa maelekezo machache Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe.
  Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
  ----
  Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetenga kiasi cha shilingi billioni mbili ili kukarabati miundombinu ya shule kongwe za Sekondari za kilakala na Mzumbe kwa wamu ya kwanza ikiwa ni kuboresha kiwango cha elimu na kurudisha umaarufu wa shule hizo ambazo zimetoa wasomi wakubwa na watalaamu mbalimbali hapa nchini.
  Akiongea katika makabidhiano ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya shule kongwe ya Mzumbe sekondari na kilakala sekondari mkoani morogoro Kaimu mkurugenzi mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima amesema ukarabati wa shule hizo umeingia mkataba na mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya shillingi Billioni 2 kwa awamu ya kwanza huku meneja waShirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi. Veneranda Seif amehaidi kuhakikisha ujenzi wa miundo mbinu hiyo unafanyika kwa kiwango kikubwa kuhakikisha thamani ya fedha iliyotolewa inatumika kikamilifu.
  Kwa upande wake mshauri wa mradi, Bw. Thomas Kalugula amesema katika upembuzi yakinifu kuna sehemu ya miundo mbinu inatakiwa kufanyiwa ukarabati ikiwemo mifumo ya maji taka katika shule hizo huku wanafunzi wakiipongeza mamlaka ya elimu Tanzania kwa kuwandalia mazingira bora ya kujisomea.

  0 0


  Mr. Saleh Said, Directors of Pennyroyal Gibraltar Limited and Mr Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International, along with other executives from both companies.  .Slated to open in 2021, the 90 room all-suite and villa resort will provide the quintessential Indian Ocean experience amidst an idyllic island setting

  DUBAI, United Arab Emirates, May 22, 2017/ -- Marriott International (NASDAQ: MAR) (www.Marriott.com) today announced the signing of an agreement with Pennyroyal Gibraltar Limited, to debut The Ritz-Carlton brand (www.RitzCarlton.com) in the exotic Zanzibar Archipelago. Slated to open in 2021, the 90 room all-suite and villa resort will bring the defining luxury experience of The Ritz-Carlton to one of the most magical destinations in the world. Located within a convenient 45-minute drive from Zanzibar International Airport, The Ritz-Carlton, Zanzibar will provide easy access to the fabled and magnificent UNESCO World Heritage Site, Stone Town, often referred to as the cultural heart of Zanzibar.

  The signing of The Ritz-Carlton, Zanzibar took place at an intimate ceremony attended by the owners, Mr. Saleh Said and Mr. Brian Thomson, Directors of Pennyroyal Gibraltar Limited and Mr Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International, along with other executives from both companies.

  “Celebrated as one of the world’s most exotic destinations, Zanzibar, is a perfect destination for The Ritz-Carlton,” said Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International. “The Archipelago has the potential to strengthen its position as a key leisure destination in the Indian Ocean and to effectively compete with the more established islands of Mauritius, Seychelles and Maldives. The Ritz-Carlton, Zanzibar will compliment Marriott International’s strong presence in the Indian Ocean and provide the necessary impetus to put the destination on the global itinerary of our guests.”

  Mr. Saleh Said and Mr. Brian Thomson, Directors of Pennyroyal Gibraltar added, “We are delighted to partner with Marriott International to debut The Ritz-Carlton in such a culturally significant destination and are confident that the brand’s allure, coupled with Marriott International’s strong base of loyal guests, will entice the affluent travelers to visit this enchanting destination, making it one of the most coveted resorts in the region.”

  The Ritz-Carlton, Zanzibar will be an all-suite and villa resort with 90 luxuriously appointed spaces including over water villas, each with its own private pool and a distinct contemporary design inspired by the island’s tropical tableau and unique culture. It will boast of a distinctive dining scene with four restaurants and bars allowing The Ritz-Carlton chefs to showcase their culinary versatility and engage with guests through curated and immersive dining experiences.
   
   Leisure facilities will include an outdoor pool, a Health Club, a Beach Club and a Kids Club. Guests will have access to a tranquil Spa with eight private Spa Suites offering individual and couple treatments as well as outdoor treatments. An intimate meeting facility will complement the resort facilities for personalized and bespoke events.

  The hotel will be part of the Amber Resort complex expected to be the largest mixed use development in Africa occupying approximately 1,750 hectares of pristine Indian Ocean coastline in the north east of the island. The complex proposes to provide an integrated high end lifestyle experience with a marina, a signature golf course designed by Ernie Els, residential villas and condominiums as well as leisure and entertainment facilities including a water park, and an equestrian center.

  The Ritz-Carlton brand currently operates 12 properties across Middle East and Africa and is gearing up to open hotels in Amman (Jordan), Tunis (Tunisia), Ras Al Khaimah (UAE), Sharm El Sheikh (Egypt) and three properties across Morocco – Tamuda Bay, Marrakech and Rabat. The Ritz-Carlton, Zanzibar will be a significant addition to this fast growing brand portfolio across the region.

  0 0

  Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi nyaraka halali za Benki ya NMB zinazoonyesha kuingizwa kwa fedha za mshindi wao Sospeter Muchunguzi pichani kushoto jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika Bahati Nasibu yao ya Ijue Nguvu ya Buku, droo iliyochezeshwa Jumapili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  MSHINDI wa droo ya saba ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Sospeter Muchunguzi, amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini.

  Muchunguzi aliyasema hayo jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakati anakabidhiwa fedha zake na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

  Akizungumza kwa msisitizo mkubwa, Muchunguzi mwenye ndoto za ujasiriamali alisema kwamba watu wote waliofanikiwa katika maisha yao walithubutu katika mambo waliyokusudia kuyafanya, hivyo ni budi kila mmoja kupita njia hiyo.
  Sospeter Muchunguzi katikati akisaini nyaraka za benki ya NMB kwa ajili ya fedha zake kuingizwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo jana baada ya kuibuka kidedea katika droo ya Biko ya Sh Milioni 10. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage na kushoto ni Afisa wa NMB.


  Alisema uhakika wa kushinda ni mkubwa ikiwa mtu ameamua kweli kuingia katika sekta ya michezo ya kubahatisha, hususan mchezo wa Biko ambao hata uchezaji wake upo wazi na hakuna dalili zozote za kudanganya washindi.

  “Nilipoona utaratibu wa Biko ni mzuri nikathubutu kucheza huku nikiamini kwamba endapo naweza kuibuka na ushindi naweza kusogea katika hatua moja kwenda nyingine hivyo Watanzania wenzangu hakuna haja ya kuogopa ili tusonge mbele.

  “Nimefurahi kupata fedha hizi kutoka Biko maana hata uchezaji wao kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuandika kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ya 2456 ni rahisi hali inayoweza kumfanya kila mtu amudu kucheza mahala popote na wakati wowote,” Alisema Muchunguzi.

  Naye Grace Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, aliwataka Watanzania kila pembe za nchi kucheza kwa wingi ili wajiwekee mazingira ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, huku pia donge nono la Sh Milioni 10 likitolewa katika droo ya Jumatano na Jumapili.

  “Lengo letu ni kutoa zawadi nono kwa kila mshindi wetu, hivyo umnachotakiwa kufanya ni kucheza Biko kwa wingi kwa kununua tiketi kuanzia Sh 1000 na kuendelea ili mshinde, maana kucheza mara nyingi zaidi ndio njia ya kufanikisha ushindi,” Alisema Grace na kuongeza kuwa tiketi moja inatoa nafasi mbili, ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10.

  Kwa mujibu wa Grace, washindi wao wanaoshinda zawadi za papo kwa hapo wanatumiwa fedha zao kwa kupitia simu walizocheza na wale wa droo kubwa wakikabidhiwa katika benki ili kuleta usalama wa fedha wanazotoa kwa washindi wao.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Longido, Danial Chongolo akiwa nchini China ambako pamoja na wakuu wa wilaya wenzie wako katika ziara ya mafunzo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

  0 0


  HUU NI UJUMBE WA MWALIMU HUYO.

  HABARI KAKA-Kuna mwanafunzi wangu anaitwa Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani kidato cha 4 mwenye umri wa miaka 16 tu ana matatizo makubwa ya tumbo. Alifanyiiwa opereshen ya kwanza  akiwa darasa la 3. Baadae  upasuaj uliendelea takriban mara 9.    
                     
  Hali yake kiafya imezorota tena baada ya kuimarika katika miezi 2 Iliyopita kufuayia operation aliyofanyiwa pale Muhimbili .Ilikuwa ni operation ya kumi kwa huyu binti mwenye umri chini ya miaka 18                       
  Dogo kwa sasa ni wa kutapika tu, tumbo limevimba tena na kitu kiumizacho zaidi ni kuwa FAMILIA YAKE IPO TAABANI KIUCHUMI KWA SASA...!                     Anaumwa kiukweli dogo hata kukaa hawez..!   

  Habari Ndugu Mtanzania Mzalendo,Kwa majina Naitwa Exaud Mtei,Mwandishi wa Habari nchini Tanzania,kwa Masikitiko makubwa Imebidi niwe Balozi wa Kusambaza Ujumbe huu ambao nimeupata kutoka kwa mwalimu wa shule ya Kawe Ukwamani akinieleza Kuhusu maisha ya mwanafunzi wake wa Kidato cha Nne ambaye anashindwa kundelea na masomo kutokana na Matatizo yanayomkumba-                   
  Pleeeeease wadau hebu kila mmoja wetu afikirie nini anachoweza kumfanyia malaika huyu kunusuru kiza  kinene cha mustakabali wake kimaisha. Kiukweli wazazi wake wamefikia hatua ya kutokujua hatma ya mtoto wao kipenzi. 
                        
  Wazazi hawana kitu imebaki ni kumtazama tu, mtoto Analia wazazi wanalia basi ni tafrani Inaumiza sana pale Mariam anapokuambia japo kama ingekuwa inawezekana basi yeye akupatie nafsi yake nawe umpatie yako japo kwa masaa 2 ( dakika 120) japo naye apumzike maumivu kwa muda huo.
    
  Msaada unaohitajika kwa sasa ni Matibabu ya haraka nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo ya madaktari. Na kwa msaada wa madaktari wa Tmj, Sanitas na Shree Hindumabdal hospital tulifanikiwa kupata mawasiliano, hospital na daktari ambaye alitupatia gharama za natibabu ya tatizo la mtoto wetu sambamba na gharama nyingine kuwa ni takriban dola elfu nane ( 8000) za marekani.             
      
  Please wadau hata kwa kuwashirikisha watu wengine na taasisi mnazozifahamu tumnusuru huyu MALAIKA...!  SANAHANI KWA MAKALA NDEFU. NI MIMI MWALIMU MLEZI WA MARIAMU IBRAHIMU MWEMA. Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii ya mama yake 0685379888 ASANTENI 
                        
  Picha nilizoambatanisha ni Picha za Mariamu Ibrahimu Mwema siku chache kabla ya upasuaji kwa mara ya kumi.!

  TUUNGANE KUSAMBAZA UJUMBE HUU NA KUMCHANGIA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA SWALA HILI

  Kwa mawasiliano Zaidi—

  Mama wa Mtoto -0685379888

  Mwalimu wa mtoto huyo Kawe Ukwamani- 0683916283

  Au ukihitaji Zaidi Kuwasiliana na Msambaza Ujumbe huu ni 0712098645


  ASANTEN TUSAIDIANE KUOKOA UHAI WA MTOTO MARIAM.
  Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani akiwa amelala Kitandani,anahitaji msaada wa Watanzania wote kwa sasa.

  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe akiwaaga wafanyakazi wa kurugenzi yake leo akielekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Lilian Karumuna.
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe akifurahia jambo na wafanyakazi wa kurugenzi yake wakati akiwaaga leo kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kurugenzi hiyo mara baada ya kuwaaga leo akielekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akihutubia maelfu ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Arusha zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid iliyofanyika mwishoni mwa wiki.   Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akiambatana na Meneja wa Mauzo wa Coca-Cola kwa Jiji la Arusha Boniface Mwasi, wakisalimia wachezaji wa moja ya timu za sekondari zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimia moja ya timu ya shule za sekondari kutoka mkoa wa Arusha, katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Umisseta mkoani hapa yaliyofanyika mwisho wa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola iligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa shule za serikali na binafsi kwa ajili ya ushiriki wa michuano yam waka huu.
  Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola hapa nchini, kwa ushirikiano na TAMISEMI, imefanya uzinduzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari (Umisseta) kwa kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha kwa kugawa vifaa vya michezo kwa shule mbalimbali za sekondari za serikali na binafsi. Katika uzinduzi wa mashindano hayo jijini Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo, ambapo aliishukuru kampuni ya Coca cola kwa udhamini kufanikisha michuano yam waka huu. Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Coca-Cola mkoa wa Arusha, Boniface Mwasi alisema kuwa kampuni hiyo imeona umuhimu wa kuibua vipaji vya michezo ndio maana wamejikita kufadhili michezo kama hiyo kwa vijana.
  “Tumeamua kushirikiana na serikali katika michezo hii ya Umisseta lengo letu kubwa likiwa ni kuibua vipaji vingi vya michezo kwa kuwa tunaamini mtandao wa shule za sekondari ni mkubwa na ni rahisi kuibua vipaji vingi kutoka sehemu zote za nchi”, Alisema Mwasi. Aidha, aliongeza ya kwamba kampuni ya Coca-Cola itaendelea kuunga mkono jitihaa za serikali za kukuza sekta ya michezo nchini hususani katika ngazi za chini ambako imekuwa ni vigumu kupata ufadhili kwa kuwa tunaamini kuwa vipaji vinapaswa kuibuliwa na kukuzwa. “Tunayo dhamira kuona vijana wa kitanzania walioibukia kwenye mashindano haya wanafika mbali kimichezo”, Alisisitiza Mwasi.

  0 0

    NI BAADA YA WAKULIMA 18 KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU.

  ·        ATAKAYEKAMATWA TUMBAKU YAKE KUTAIFISHWA
   
  Na Tiganya Vincent
   RS-Tabora

   
  Mkuu wa  Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa  tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza  tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao.
   
  Marufuku hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia  Chama gani cha Msingi.
   
  Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa  masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii (26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
   
  Alisema kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni  tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
   
  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.
   
  Alisisitiza kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa , hawezi kukubali watu wakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka kuwanyonya wakulima wengine.
   
  Kufuatia hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Wilaya kushirikiana na Watendaji ngazi za chini na kuwakamata wao na mizigo yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi wa tumbaku wenye vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.
  Atoa angalizo kwa vyombo vyote vinavyotumika kusafirisha tumbaku kutoka eneo moja kwenda jingine kuhakikisha mzigo waliopakia katika magari unavibali vyote baada ya ununuzi katika soko kupitia Chama cha Msingi ili kuepuka usumbufu na kuchukuliwa hatua.
   
  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Wakurugenzi Watendaji, Maafisa Ushirika,Wanasheria na Wawakilishi wa Benki za CRDB na NMB kukaa meza moja na kuangalia uwezekano wa kuweka makubaliano ambayo yatawahakikisha wakulima wote wa tumbaku ambao walilima kwa kutumia pembejeo zao wasiathirike na makato ya madeni ya wakulima wanaodaiwa.
   
  Alipendekeza kuwepo na Akaunti mbili, moja ni ile inayomlinda mkulima wa aliyejitegemea na nyingine ya wakulima ambao wanadaiwa ili kila mtu apate haki kulingana na alivyojiandaa katika kilimo hicho.
   
  Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa hakuna atakayenyimwa haki yake kwa sababu ya watu wengine.
   
  Hata hivyo wadau hao wa tumbaku walisema hakuna  haja ya kuwa na akaunti mbili badala yake Benki zinaweza kuweka utaratibu mzuri wa utambuzi wa mtu aliyelima kwa kujitegemea na kumpa fedha zake zote na wale wanaodaiwa wakaendelea na utaratibu wanaoutumia.
   
  Walisema kuwa hatua itawasaidia wakulima waliojitegemea na kuamua kuuzia tumbaku yao kupitia vyama vya msingi kupata haki yao bila kuchelewa kwa kusubiri deni la Chama cha Msingi limalizike kwanza ndio walipwe.
   
  Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amesema kuwa baadhi ya matatizo na migogoro katika zao la tumbaku yamesababishwa na maslahi binafsi ya baadhi ya watumishi wakiwemo Maafisa Ugani, Maafisa Ushirika , Wafanyakazi wa Mabenki na watumishi wengine wanaojihusisha ununuzi usio halali wa zao hilo na kilimo hicho.
   
  Alisema kuwa watumishi hao ndio wamekuwa wakichochea migogoro na wengine kuwarubuni wakulima kwa kununua tumbaku yao kinyume cha utaratibu na kuwafanya walaze madeni.
   
  Dkt. Ntara alisema kuwa ili zao hilo limsaidie mkulima  ni vema wataalum wakafanyakazi zao za utaalam kuliko kuwa  washindani wa wakulima na hivyo wakati kuanzisha migogoro kwa maslahi yao binafsi ili hatimaye wakulima wakate tamaa na kuanza kuuza tumbaku katika masoko yasiyo rasmi.

  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewahamasisha wananchi wenye majengo katika Jiji la Mwanza kuhakikisha wanalipa kodi ya majengo kwa wakati ili kuepuka kutozwa faini au kufikishwa mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa kodi jijini Mwanza jana Kichere alisema kodi ya majengo ipo kwa mujibu wa sheria na italipwa mara moja kwa mwaka, hivyo ni muhimu wananchi wakailipa mwaka huu wa fedha kabla ya Juni 30 .

  Alisema TRA haina sababu ya kufikishana mahakamani an wananchi lakini watakaoshindwa kulipa ndani ya muda wa kisheria watalazimika kulipa na tozo au kufikishwa mahakamani na kulingana na matakwa ya sheria za mamlaka hiyo watalipa sh. 70,000 badala ya viwango vya sh. 20,000 (Nyamagana) na sh. 15,000 (Ilemela) vya sasa.

  “ TRA na Serikali ya Mkoa wa Mwanza inalenga kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kulipa kodi hii bila adhabu ifikapo Juni 30, mwaka huu ambayo ni mwisho.Wenye majengo kwenye Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilemela ambao hawajapokea Ankara zao za kodi wakazichuke ofisi za TRA au kwa viongozi wa serikali za mitaa yao ama wajisajili na kulipia benki yoyote ya biashara,”alisema Kichere.

  Alisema TRA mkoa wa Mwanza inasimamia kodi ya majengo yaliyokamilika na kutumika kwa makazi na biashara yaliyothaminishwa au la,yaliyopimwa na yasiyopimwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela.

  Alieleza kuwa nyumba zilizothaminiwa wamiliki watalipa kodi kwa asilimia ya thamani ya jengo na nyumba za maeneo yasiyopimwa na ambazo hazijathaminiwa kodi italipwa kwa viwango maalumu vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

  Kamishna mkuu huyo wa TRA alifafanua kuwa baadhi ya majengo ya serikali pamoja na ya ibada yamesamehewa, pia wastaafu au wazee wenye umri wa miaka 60,walemavu kwa nyumba moja wanazoishi lakini zisiwe zinatumika kwa biashara nao wamesamehewa.

  Hata hivyo aliwaondoa hofu Wakuu wa Wilaya, Naibu Meya pamoja Wakurugenzi wa Jiji na Manispaa ya Ilemela kuwa kodi hiyo si mali ya TRA ni mali ya halmashauri za miji, majiji na serikali za mitaa na hivyo baada ya kukusanywa itarejesha kwenye halmashauri zikatekeleze shughuli za maendeleo.

  Kichere alieleza zaidi kuwa ushirikiano wa serikali ya mkoa, serikali za mitaa, umewezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati pamoja na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema jukumu la kulipa kodi ya serikali ambayo inawezesha kujengwa kwa barabara na huduma zingine za jamii ni la wananchi ambapo TRA wanafanya kazi ya kuikusanya kwa dhamana waliyopewa na serikali.

  “ Dar es Salaam wanatuzidi kwa historia tu.Kulipa na kukusanya kodi ya serikali za mitaa kwa uadilifu tukifanya hivyo nchi yetu itakwenda.Kwenye mkoa wangu nimeagiza hakuna mkurugenzi wa halmashauri kutoka nje hadi amekusanya kodi tuliyokubaliana kisha tupigiane hesabu na tuelewane,” alisema Mongella.

  TRA inasimamia na kukusanya kodi ya Majengo kuanzia Julai 2016 kutokana na Sheria ya Fedha ya Serikali Mitaa Sura 290, Sheria ya Miji Sura ya 298 na Sheria za Mamlaka ya Mapato Tanzania sura 339.


  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumzia umuhimu kodi ya majengo kwenye mkutano wa wadau wa kodi uliofanyika Ukumbi wa Ofisi yake.Kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi Cloudwing Mtweve na wa kwanza kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA.Picha zote na BALTAZAR MASHAKA
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akielezea umuhimu wa wananchi kulipa kodi ya majengo kwenye mkutano wa wadau wa kodi uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi yake.Kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi Cloudwing Mtweve na wa kwanza kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles E. Kichere akizungumza na wadau wa kodi pamoja na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhamasisha ulipaji kodi ya majengo kwa wakati bila shuruti.Watatu kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Katibu Tawala mkoa, CP Cloudwing Mtweve (wa pili kulia) naRichard Kayombo,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA wa kwanza kulia , kushoto wa kwanza ni Ernest Dundee,Meneja wa mamlaka hiyo mkoani humu .

  0 0


  0 0

  Vijana kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN), mjini Arusha wametakiwa kuchambua masuala yaliyopo mbele yao kwa makini ili kutoa jawabu kwa matatizo ya dunia yanayohitaji ushiriki wao.

   Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa serikali katika mkutano huo Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa anayeshughulikia dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  Aliwataka vijana wanaoshiriki TIMUN kuhakikisha wanaangalia kwa makini mambo yanayogusa nchi zao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa ndio njia pekee ya kutekeleza malengo endelevu ya dunia ambayo yanahitaji ushirikiano wa ndani na wa kimataifa. TIMUN ambayo kirefu chake ni Tanzania International Model United Nations hufanyika kila mwaka na ujumbe mbalimbali na mwaka huu ujumbe wa TIMUN ni: “kuwawezesha vijana katika diplomasia na uongozi” Picha juu na chini ni Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaofanyika kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

  TIMUN huandaliwa na Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) taasisi ya vijana isiyotengeneza faida inayotangaza shughuli za Umoja wa Mataifa na kushirikisha vijana katika utekelezaji wa shughuli hizo. 

  Aidha aliwashukuru waandazi wa mkutano huo kubwa unaofanana na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (General Assembly) wenye lengo la kukutanisha vijana kujadili mustakabali wa malengo ya dunia. 

  Alisema vijana wana nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo hayo ya maendeleo endelevu jukumu ambalo dunia imejipa kwa miaka 15 hadi mwaka 2030. Pamoja na kuwashukuru Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kambi hiyo, hali iliyoonesha kwamba wanajali vijana, mwakilishi huyo wa serikali alisema kwamba Tanzania ipo tayari kusukuma mbele ajenda ya ushirikishaji vijana katika maendeleo endelevu kwa kuwa inaamini juu ya hilo.  “Wakati serikali inafanyakazi kwa karibu na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo yanatekelezeka, baraza la vijana ambalo litakutana litakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza sauti ya pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo” Alisema kwamba malengo ya dunia ambayo yapo 17 yanagusa kila sehemu ya maisha na hivyo ni vyema kama vijana watatoka na majibu ya maswali yanaoumiza vichwa kuhusu malengo hayo hasa mazingira na dunia endelevu. 

  Aliwataka vijana kutumia nafasi yao vyema katika jukwaa hilo kwani maisha ya watu bilioni 7 duniani wanategemea namna ambavyo wanajengwa na vijana, wenye mchango muhimu wa kulinda mazingira na kuhakikisha maendeleo endelevu. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017), unaofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

  Awali Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba zaidi ya vijana elfu 20 nchini Tanzania wamefunzwa malengo endelevu ya dunia, toka ulipofanyika uzinduzi Juni, 2016. 

  Akizungumza katika hafla ya kambi ya mwaka huu ya Tanzania International Model United Nations (TIMUN), inayofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST), Bw. Rodriguez alielezea kufurahishwa na idadi hiyo ya vijana waliohamasishwa na kusema kwamba malengo ya maendeleo endelevu 2030 yanahitaji kila mmoja kushiriki. Aidha alielezea umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya maendeleo kutokana na uwingi wao hapa nchini. Asilimia 67 ya watu nchini ni vijana.  Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha. Bw. Rodriguez alishukuru machampioni kwa kuwezesha vijana wenzao kutambua malengo endelevu ya dunia na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kuwashawishi vijana wenzao kuelewa na kushiriki katika malengo hayo. 

  “Nataka kuwatafadhalisha kwamba huu ni mwanzo tu, kuna mengi ya kufanya. Kama Umoja wa Mataifa, tunawataka wote mshiriki, si tu katika kuelimisha kuhusu malengo haya ya dunia, lakini pia katika kuangalia mwenendo wa maendeleo hayo katika jamii na namna yanavyotekelezwa. Tukio kama hili la TIMUN linasaidia kuongeza uwezo wa kufikia malengo ya dunia,” alisema Bw. Rodriguez. Vijana 50 wa kwanza machampioni walifunzwa mwaka jana katika TIMUN 2016. Kwa sasa kuna vijana machampioni 500 nchini Tanzania ambao wamepeleka ujumbe kwa vijana wenzao 20,000.  Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), Tajiel Urioh akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea jijini Arusha.

   Ujumbe ambao umekuwa ukisambazwa na machampioni kwa wenzao umeelezwa kulenga kuchochea hamasa ya kuelewa malengo kwa ajili ya maendeleo.

  “Kama watu hawatajua malengo ya maendeleo endelevu, hawataweza kufanya malengo hayo kuwa ya kweli,” aliusema ujumbe huo Gloria Nassary, ambaye ni mmoja kati ya vijana 50 waliopewa mafunzo ya kwanza ya kuwa machampioni wa malengo ya dunia. Naye Tajiel Urioh ambaye ni Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), pamoja na kusisitiza amani kama sehemu muhimu ya kusukuma mbele utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu aliwahimiza vijana kutokata tamaa katika kuhimiza utekelezaji wa malengo hayo. Ofisa wa Mawasiliano NUNV anayeshughulikia tovuti na mitandao ya kijamii katika ofisi ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Edgar Kiliba akiendesha kipindi cha maswali na majibu wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017) unaoendelea jijini Arusha kwenye ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha.

   Alisema bila amani kuanzia katika ngazi ya familia, uwezekano wa kutekeleza malengo hayo unakuwa mgumu kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya amani na utekelezaji wake. Alisema amani ni kionjo muhimu cha maendeleo kinapokosekana hata jukumu la vijana kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu halitawezekana.

   Alisisitiza kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo na kufikiwa kwa malengo ya Umoja ya Mataifa ambayo ni malengo ya dunia katika kuimarisha ustawi wa jamii na kuinua uchumi . Urioh katika mazungumzo yake alisema suala la uchafuzi wa mazingira ni suala gumu na mtambuka na kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na kuvurugwa kwa tabaka la ozoni halihusu Ulaya pekee, ambao wanachafua bali kila mmoja duniani; akiongeza kuwa mwishoni mwa siku wanaoathirika ni zaidi nchi zinazondelea akitolea mfano nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.  Championi wa Malengo ya dunia (Global Goals) nchini, Rio Paul akitoa maoni katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea jijini Arusha.[/caption] Alisema suala la kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi si kutulia bali kuwajibika kutekeleza wajibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba hakuna uharibifu wa mazingira unaofanyika katika taifa la Tanzania. 

  Alisema vijana wanaweza kufanya zaidi ya yale ambayo kwa sasa wameyafanya katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kwamba wana elimu ya kutosha kuhusu malengo hayo na kushirikiana kuyatekeleza kwa kuangalia changamoto mbalimbali ambazo wanazipatia majibu. Alisema lengo la malengo hayo ni kusaidia jamii vivyo hivyo vijana nao wanatakiwa kujitoa mhanga kuhakikisha kwamba jamii inaendelea kustawi na kuendelea kwa manufaa ya kizazi kijacho. Mmoja wa washiriki kutoka nchini Uingereza akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

  Aliwataka vijana kutafuta majawabu ya mambo yanayoikabili dunia kwa namna ya busara na kitaalamu zaidi huku wakizingatia diplomasia. Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu. Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini, Jacqueline Kamwamu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini Arusha.

   Kushoto ni Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), Tajiel Urioh[/caption] Wakati akiwa Arusha, Mratibu pia alifuatilia matokeo ya mafunzo yaliyofanyika Novemba mwaka jana katika chuo kikuu cha Tumaini Makumira yaliyofanywa kwa pamoja kati ya Umoja wa mataifa na Jumuiya ya Ulaya. 

  Katika mafunzo hayo machampioni 80 walifunzwa wakiwemo wanachuo 30 kutoka Taasisi ya Uhasibu ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha -IAA). Mkutano huo umefadhiliwa Umoja wa Mataifa (UN), Serikali, Covenant Bank, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) pamoja PIU.  Katibu wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini Arusha.      Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala, Dr. Musa Chacha (kushoto) baada ya kuwasili ofisini kwa Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Karoli Njau (katikati) jijini Arusha. Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) Prof. Karoli Njau akiwa kwenye mazungumzo ofisini kwake na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) aliyeambatana na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa kwanza kulia), Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa pamoja na Ofisa wa Mawasiliano NUNV anayeshughulikia tovuti na mitandao ya kijamii katika ofisi ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Edgar Kiliba.  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) Prof. Karoli Njau kitabu chenye taarifa na ripoti mbalimbali za Umoja wa Mataifa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini humo Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) Prof. Karoli Njau wakieleka kwenye eneo maalum la kupiga picha kwenye taasisi hiyo. Meza kuu kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) katika picha ya pamoja. Meza kuu katika picha ya pamoja na waandaaji wa TIMUN 2017. Picha ya pamoja na washiriki wa TIMUN 2017 kutoka nje ya Tanzania. Picha ya pamoja na washiriki wa kambi ya TIMUN 2017 inaoendelea jijini Arusha [caption id="attachment_2142" align="aligncenter" width="1404"] Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa TIMUN 2017 akiwemo Mshiriki wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu (katikati).[/caption]

  0 0older | 1 | .... | 1241 | 1242 | (Page 1243) | 1244 | 1245 | .... | 1898 | newer