Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1240 | 1241 | (Page 1242) | 1243 | 1244 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego akifanya yake kwenye Shoo ya Wapo iliyofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Zakhem jijini Dar....Akiimba sambamba na mashabiki zakeMsanii Kala Jeremiah alivyowarusha mashabiki kwenye Shoo ya Wapo.Msanii Kala Jeremiah alivyowarusha mashabiki kwenye Shoo ya Wapo.Mashabiki wakiwa na furaha ya burudani.Msanii Barnaba na Shilole wakifanya yao kwenye jukwaa la Dar Live jana usiku. 

   Msanii Shilole akikata nyonga na shabiki wake.Mchekeshaji Mkali Wao na Ninyetwa Ebitoke wakionesha uwezo wao.DJ Zero akitoa saluti kwa mashabiki wake. ONESHO kabambe la Wapo Concert lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa burudani wa Taifa wa Dar Live hakika liliacha historia kwa mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia onesho hilo ambalo ni la aina yake kufanyika ndani ya ukumbi huo. 

   

  Onesho hilo lililowashirikisha wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Nay wa Mitego, Barnaba, Shilole ‘Shishi Bay’, Kala Jeremiah na mabingwa wa vichekesho hapa nchini, Mkali Wenu na wenzake, hakika lilikuwa la aina yake na liliacha simulizi kubwa kwa mashabiki waliojitokeza kulishuhudia. Onesho hilo lililoongozwa na DJ Ziro na DJ Max wa Dar Live ambao walizikonga nyoyo za mashabiki, lilianza kwa shamrashamra kwa wasanii waliopanda jukwaani kupiga shoo za utangulizi. 

   

  Nusura baadhi ya mashabiki hao wavunjike mbavu kwa vicheko kufuatia vichekesho vilivyoletwa na Mkali Wenu na wenzake kwani jamaa hao ni noma kwa kuvunja mbavu watu, hata walipomaliza kutoa burudani mashabiki waliwaita warudie tena nao wakafanya hivyo. Ilikuwa kama mvua inataka kutibua onesho hilo lakini mashabiki hawakujali mvua ambayo ilikuwa inanyesha kwani waliendelea kula shangwe bila kujali mvua iliyokuwa inamwagika kwa wingi. 

   

  Hata Barnaba alipopanda jukwaani na wimbo wake wa Milele, aliwakuta mashabiki hao wameshapagawa na yeye kuwaongezea mzuka kwa burudani ya nguvu. Mashabiki hao walizidi kupagawa zaidi baada ya Barnaba kumpandisha jukwaani Shishi Baby na kuimba nae pamoja wimbo mpya wa Shilole wa Hatutoi Kiki. Shishi Baby alimpisha Kala Jeremiah ambaye aliwakuta mashabiki hao wamewehuka kwa burudani, naye akaongeza ngoma juu ya ngoma. 

   

  Ukumbi ulirindima zaidi baada ya Nay wa Mitego kuvamia jukwaa kwa wimbo wake wa Muziki Gani, mashabiki wakavamia jukwaa huku baadhi wakitaka japo wamguse. Nay aliweka historia kubwa ndani ya ukumbi huo wa taifa wa burudani uliopo Mbagala jijini hapa alipowatendea haki mashabiki hao kwa kuwadondoshea ngoma zake zote mwanzo mwisho.

  (PICHA/HABARI: ISSA MNALY/GPL)

  Tazama Shoo Nzima ya Nay wa Mitego 'Wapo Concert' Dar Live - Mbagala


  0 0


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za kupata ajali kwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting FC iliyotokea leo barabara ya Manyoni mkoani Singida wakati kikosi hicho kikitokea Shinyanga kwenda Pwani.

  Taarifa kutoka Singida zinasema gari hilo lilipata ajali baada ya kupasuka tairi moja la mbele hivyo kuyumba na kuacha njia eneo la Itigi - kilometa 200 kutoka Singida mjini kuelekea Manyoni  hivyo kutoka barabarani kuu kabla ya kugonga mti.

  Taarifa hizo zilizothibitishwa na Masau Bwire, zinasema wachezaji watatu akiwamo Bwire mwenyewe ndio waliopata majeraha na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Singida kwenda kutibiwa. Wachezaji hao ni Yussuf Nguya, Abdul Mpambika na Saidi Dilunga.

  Timu hiyo ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao 2-1, hata hivyo imebaki kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao baada ya kushika nafasi ya saba. 

  Mara baada ya kupata taarifa hizo, Rais wa TFF Jamal Malinzi mara moja ametuma salamu za kuwapa pole uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania pamoja na timu nzima ya Ruvu Shooting.

  “Nawapa pole viongozi wote, makocha na wachezaji. Na kwa wachezaji ambao wamejeruhiwa na viongozi wote waliojeruhiwa akiwamo ndugu yetu Masau Bwire, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka,” amesema Malinzi.

  Rais Malinzi alimshukuru Mungu kwa kuepusha vifo kwa wanafamilia hao wa mpira wa miguu hasa wakati huu Watanzania wakiwa makini kufuatilia maendeleo ya timu za taifa.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ametuma salamu za pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida ulioingia madaraka jana Mei 20, 2017.

  Mbunge wa Singida Mjini, Mheshimiwa Mussa Sima amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa SIREFA baada ya kuwashinda wenzake Erasto Sima, Hussein Mwamba, Said Mnyampanda na Samwel Nakei.

  Katika salamu zake kwa SIREFA, Rais Malinzi amesema anashukuru kwa uamuzi wa kidemokrasia uliofanywa na wajumbe wa mkoa huo na kwamba ana imani na uongozi ulioingia madarakani.

  “Kwa namna ya wanafamilia wa mpira wa miguu wa Mkoa wa Singida walivyodhamiria kutaka kuleta maendeleo ya mpira wa miguu, nina imani na uongozi wa Mheshimiwa Sima katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya soka mkoani huo,” amesema Malinzi.

  Katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini Singida na kusimamiwa na Mwenyekiti Stella Maila, pia ulimchagua Katibu Mkuu Rashid Koba wakati Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ni Nurfus Ndee huku Hamza Ntoga akichaguliwa kuwa Mweka Hazina Msaidizi.

  Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Ally Ramadhani Nkhangaa aliyekuwa mgombea pekee wakati Koba alimshinda Edward Ihonde na Ndee alimshinda Manase Abel.

  Uchaguzi wa SIREFA ulifanyika baada ya viongozi wengine walioingia madarakani mwishoni mwa mwaka jana, kujiuzulu kutokana na kubanwa na majukumu mbalimbali.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0
 • 05/21/17--09:22: TUZO ZA LIGI KUU 2016/17
 • SHEREHE za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

  Kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo.

  Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).

  Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu huu.

  Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

  Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.

  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuonesha kuthamini kipaji cha mchezaji huyi wakati wa uhai wake.

  Kutokana na mabadiliko hayo tuzo zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.

  Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima, Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye Nidhamu.

  Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.

  Hata hivyo Mfungaji Bora safari hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo kamati itapitia vigezo vilivyopo katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora w Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupata mshindi ambaye atatangazwa siku hiyo ukumbini.

  Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:  Mchezaji Bora wa Ligi Kuu

  Aishi MANULA - Azam

  Simon MSUVA - Yanga

  Shiza KICHUYA - Simba

  Haruna NIYONZIMA - Yanga

  Mohammed HUSSEIN – Simba

  (Majina ya wanaowania tuzo hiyo yalitolewa Jumatano iliyopita na upigaji kura unaendelea ukiwahusisha Makocha wa timu za Ligi Kuu na Makocha Wasaidizi,Wahariri wa habari za michezo na Manahodha wa timu za Ligi Kuu, ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni Jumanne Mei 23 mwaka huu).
  KIPA BORA

  Aishi MANULA - Azam

  Owen CHAIMA - Mbeya City

  Juma KASEJA - Kagera Sugar
  KOCHA BORA

  Joseph OMOG - Simba

  Mecky MEXIME - Kagera Sugar

  Ettiene NDAYIRAGIJE - Mbao  MWAMUZI BORA

  Shomari LAWI – Kigoma

  Elly SASII – Dar es Salaam

  Hance MABENA - Tanga  MCHEZAJI BORA WA KIGENI

  Haruna NIYONZIMA - Yanga

  Method MWANJALE - Simba

  Yusuph NDIKUMANA - Mbao  MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA

  Mbaraka ABEID - Kagera Sugar

  Shaaban IDD - Azam

  Mohammed ISSA - Mtibwa
  TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)

  Shaaban IDD - Azam

  Abdalah MASOUD - Azam

  Mosses KITAMBI - Simba  TUZO YA HESHIMA

  (Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tuzo).


  GOLI BORA LA MSIMU

  (Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).


  TIMU YENYE NIDHAMU

  (Mshindi atatangazwa ukumbini siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).


  WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL XI 2016/17

  (Watatangazwa ukumbini siku hiyo ya sherehe).


  Kamati inayohusika na usimamizi wa tuzo inawaomba wadau wote ambao wameombwa kupiga kura katika Tuzo ya Mchezaji Bora wafanye hivyo kulingana na fomu walizotumiwa na mchango wao una thamani kubwa.
   
   
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe uliofanyika kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
  Bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha wananchi walijitokeza na kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa mjini Magharibi, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi,Wafadhili waliochangia kufanikisha kampeni ya Mimi na Wewe inaleta tija kwa wananchi wa mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar za kusaidia wananchi wanaokabiliwa na hali duni ya maisha kwa kuahidi kutoa mifuko ya saruji 1000 na mabati 600 kwa ajili ya kusaidia wananchi hao.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo mjini Unguja wakati anazindua kampeni maalum ya MIMI NA WEWE inayolenga kuhamasisha wananchi kuungana pamoja katika kutoa misaada ya hali na mali ili kuboresha huduma za kijamii katika sekta za afya, elimu,mazingira,maji safi na salama, matumizi bora ya ardhi na kusaidia watu wasiojiweza.

  Makamu wa Rais katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo amekemea vikali tabia ya ubinafsi kwa baadhi ya viongozi inayosababisha wananchi kutopatiwa taarifa muhimu za maendeleo yao hali inayopelekea uduni katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi katika maeneo mbalimbali kujenga tabia ya kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazopata na jinsi zilivyotumika ili kuwapa moyo wananchi katika kuchangia kwenye shughuli za maendeleo kwa sababu watakuwa na imani kuwa fedha zao walizochanga zinatumika vizuri.

  “Maendeleo endelevu ni lazima yazingatie Utu na heshima ya mtu, mshikamano wa dhati na mafungamano ya Kijamii,” Amesisitiza Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais pia amehimiza wadau mbalimbali wa maendeleo hasa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kujenga moyo wa kujitolea na kutoa misaada ili kuhakikisha taifa linasonga mbele kimaendeleo kuliko kutegemea wafadhili wa nje ya nchi tu.

  Ameeleza kuwa kampeni ya Mimi na Wewe ina umuhimu wa kipekee kwani inakusudia kuwaomba na kuwahamasisha wananchi hasa wa Zanzibar kuchangia kwa hali na mali katika kusaidia wananchi wenzao ambao hali zao za maisha bado ni duni ili kutimiza malengo ya mapinduzi kujenga maisha bora na usawa kwa kila mtu.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuweka kando itikadi zao za kisiasa hasa wa Zanzibar na wajenge Zanzibar imara yenye upendo, umoja na mshikamano ili kuharakisha juhudi za maendeleo.

  Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amesema wameamua kuanzisha kampeni hiyo maalum ili kurejesha moyo wa kusaidiana miongoni wa Wazanzibar hatua ambayo itasaidia maradufu uboreshaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

  Mkuu huyo wa mkoa wa Mjini Magharibi amesema mkoa huo ndio unaongoza kwa kuwa na wananchi wengi kwa Zanzibar ambao wanafikia zaidi ya laki Tano hivyo idadi hiyo kubwa ya watu inahitaji rasilimali nyingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi hao kitu ambacho bado ni changamoto kubwa inayohitaji ushirikiano ili kuipatia ufumbuzi.

  Amesema anaimani kubwa kuwa kampeni maalum ya Mimi na Wewe itawaibua wadau wa maendeleo na wananchi wenyewe katika kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kujitolea katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo jambo ambalo litasaidia kubadili maisha ya wananchi maskini kwa kuwasaidia kupata kipato kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.

  0 0

  Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba  wakiyarudi magoma wakati walipokuwa wakiingia ukumbini katika tafrija maalum ya kuwapongeza kwa kuungana kwao iliyofanyika katika ukumbi wa Tausi uliopo Kiluvya mkoani Pwani.

   Maharusi   wakiwa katika pozi

  Maharusi katika picha ya pamoja na wazazi na ndugu wa karibu

   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba wakishukuru wahudhuriaji
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba wakipewa mikono ya pongezi
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba wakipongezwa
   Sehemu ya waalikwa kwenye harusi ya Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na ndugu
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na ndugu
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na Mama mdogo Zamaradi Kawawa
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na mama wakubwa
   Waalikwa wakifurahia harusi ya Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba 
   Miondoko ya kila aina harusini
   Furaha harusini
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na mdau
  Paparazi wakirekodi harusi ya  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba

  0 0
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Rais wa Kampuni ya TBEA ya China, Zhang Xin kwa ajili ya kujadili masuala ya uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini.

  Mkutano huo wa Waziri Muhongo na Rais huyo ambaye ameongozana na Ujumbe wake umefanyika Mei 21, 2017 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Waziri Muhongo aliuelezea ujumbe huo baadhi ya fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini na kuwashauri wachague eneo ambalo wanahitaji kuwekeza ili taratibu zianze mapema.

  “Fursa ni nyingi sana, ni nyinyi kuamua wapi mmelenga ili taratibu ziendelee ikizingatiwa kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha tunakuwa na Tanzania ya Viwanda,” alisema Waziri Muhongo.

  Aliagiza wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini kukutana na Ujumbe huo hapo kesho ili kujadili kwa undani dhamira yao ya uwekezaji ikiwemo kuchagua eneo ambalo wangependa kuwekeza.

  Kwa upande wake Xin alisema kampuni yake inaridhishwa na kasi ya Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli na hivyo wanatarajia kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 10 kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Nishati, Barabara, Uendelezaji wa Miji, na Usafirishaji.

  Alisema uchumi wa Tanzania umezidi kuimarika na hivyo kuzidi kuvutia wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali hususan ikizingatiwa kuwa Tanzania ni Taifa lenye amani linalokuwa kwa kasi kubwa.

  Ujumbe huo upo nchini Tanzania na unatarajia kukutana na Wizara mbalimbali ili kubaini fursa zaidi za uwekezaji nchini

  0 0

  Meneja Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (Kulia) akishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo.

  Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo. 
  Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo.
   
  Meneja Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (mwenye kofia nyeusi kulia) na Meneja Mwajiri Zantel, Frank Jackson (mwenye kofia nyeusi kushoto) wakikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko la Samaki la Kunduchi mara baada ya wafanyakazi wa Zantel kumaliza zoezi la kufanya usafi katika soko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Zoezi hilo ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira safi na salama ambapo kampuni hiyo iliwataka wadau hao kuendeleza utamaduni huo.
   

  0 0


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi (AQRB) , Dkt Geraldine Kikwasi akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kuwahamasisha Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule hiyo kuwapa elimu kuhusiana na fani mbili za ubunifu majengo na Wakadriaji Majenzi kwa masomo ya sayansi.
  ARCH. Daniel Matondo kutoka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi akiwaelezea Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi katika sekta ya ujenzi.
  Mwalimu wa shule ya Sekondari Majani ya Chai akiwasisitizia wanafunzi kusoma zaidi masomo ya sayansi wakati wakati wa ziara ya kuwahamasisha Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule hiyo.

  Wanafunzi kutoka chuo cha ardhi. wanayesomea fani ya Wabunifu Majengo wakiwapa elimu wanafunzi kuhusiana wasomo ya fani ya wabunifu majenge.
  Afisa Uhusiano kutoka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi (AQRB) Bw.Hamis Sungura. akiwatambulisha viongozi wa Bodi.
  Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wakifuatilia elimu ya fani mbili ya ubunifu majengo na Wakadriaji Majenzi kwa masomo ya sayansi.
  Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi (AQRB) , wakiwasili katika Shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kuhawamasisha Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule hiyo kuwapa elimu kusomea fani mbili za ubunifu majengo na Wakadriaji Majenzi kwa masomo ya sayansi (mbele kulia) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Dkt Geraldine Kikwasi, katikati ARCH Daniel Matondo na Kushoto Afisa Uhusiano wa Bodi Bw.Hamis Sungura.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta  Ndetiye (kushoto) akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Semina hiyo ilihusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini.
  Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi kabla ya kuanza kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika semina hiyo. Mada zilizowasilishwa katika semina hiyo ni Kwanini Watanzania tuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori, Athari za Muingiliano wa Mifugo na Wanyamapori, Maendeleo ya Utalii na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na Umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu Nchini.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jeneral Gaudence Milanzi akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mkurugenzi wa Idara wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa askiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Watanzania kuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori katika semina hiyo. Kushoto waliokaa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya viongozi na wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Prof. Songorwa akiwasilisha mada hiyo. 
  Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Dkt. Robert Fyumagwa akiwasilisha mada juu ya Athari za Muingiliano wa Mifugo na Wanyamapori katika semina hiyo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akiwasilisha mada juu ya Umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu Nchini. Alieleza kuwa umuhimu wa misitu ni sawa na hewa safi ambayo inatoa uhai kwa mwanadamu na endapo misitu hiyo itatoweka kutokana na uharibifu unaoendelea basi maisha ya binadamu nayo yatakuwa hatarini kwa kuwa hewa hiyo chanzo chake ni misitu na mimea.
  Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana akiwasilisha mada kuhusu Maendeleo ya Utalii na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania kwa wabunge hao.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta  Ndetiye (kushoto) wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
  Aliyekuwa MC wakati wa semina hiyo, Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete akiteta jambo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwa muda mfupi baada ya kuhitimishwa semina hiyo.
   Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili walioshiriki semina hiyo bungeni mjini Dodoma.
  Bungeni wakati wa semina hiyo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu Wizara ya Maliasili, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa wakitoka katika ukumbi wa bunge mara baada ya semina hiyo.

  0 0


  Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Tigo, Aidan Komba, akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mkoani Singida, kushoto ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Singida Raymond Royer.

  Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma ya 4G LTE mkoani singida mapema leo.


  Singida, Mei 22, 2017-Wateja wa Tigo mkoani Singida hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika soko.

  Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo unafuatia mafanikio yaliyopatikana baada ya kuizindua katika mji mingine mikubwa nchini.

  Komba alisema kwa kuifanya huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo kwa mara nyingine tena imeonesha kujikita kwake katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu katika soko hili.”

  Alitangaza kuanza kwa enzi mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano ndani ya Singida akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha kunakuwepo uwezo mkubwa na muhimu katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.

  “Singida ni kituo muhimu kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia huduma Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa rahisi zaidi.”

  “Mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na hali kadhalika kukuza uchumi na biashara”, alisema Komba.

  “Kama mnavyojua, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri ukiwa ni uchimbaji wa visima 12 ambavyo tulivitoa kama msaada kwa vijiji vya Singida mwaka jana,” Komba alibainisha.

  Aliongeza kwamba gharama ya vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua kuwa wateja wanachotakiwa ni kuwa na kifaa kinachowezesha 4G LTE ama simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja wanaweza kubadilisha au kununua kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika duka la Tigo la huduma kwa wateja lililopo Singida Mjini.

  Akizungumzia uwekezaji katika mtandao, Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya kisasa, ikilenga kusaidia katika maendeleo endelevu ndani ya mkoa.

  Alihitimisha kwa kusema, “Mipango imo njiani katika kupanua huduma kwa ajili ya mikoa iliyobakia ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”

  Kwa upande wake, Meneja wa mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer alibainisha umuhimu wa huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha huduma za uwanda mpana wa simu za mkononi.

  Royer alisema, “Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia 90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”

  Aliongeza, “Kwa hiyo teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za data zilizo na kasi kubwa na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko ambayo itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”

  Mtandao wa 4G LTE unamaanisha kasi kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada kutoka katika intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango kikubwa inaboresha uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya mikutano. Hali kadhalika inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na kutiririsha video kutoka katika mitandao ya kijamii.

  0 0
 • 05/22/17--03:25: MV KAZI YAFANYIWA MAJARIBIO
 • Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
  Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
  Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
  Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari. 


  Na Alfred Mgweno, TEMESA 

   Kivuko cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. 
  Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.

  Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo. 

  Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.

  Miongoni mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. 

  Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.

  0 0

  Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
  Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
  Taswira ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
  Taswira ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.

  0 0


  Afisa mwandamzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kushoto), akitoa mada iliyoelezea faida mbalimbali amzipatazo mwanachama wa Mfuko huo kwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya maafisa polisi wanawake wa Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO) kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MAAFISA wa polisi waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tatu ya polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO), wamepata fursa ya kuelewa kwa undani huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mada mbalimbali zilizotolewa na Maafis wa Mfuko huo mwishoni mwa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Maafisa hao waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda walipata fursa ya kujua uendeshaji wa Mfuko huo ambao wanachama wake ni pamoja na Watumishi wote wa Umma, Sekta binafsi, na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi.
  Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa, aliwaambia maafisa hao wa polisi kuwa, pamoja na kutambua na kusajili wanachama, kukusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama na kuweka michango katika vitega uchumi mbalimbali.
  Alisema, majukumbu mengine ni pamoja na kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati.
  Aidha kwa upande wake, Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha M.Ngalo, yeye alizungumzia mwongozo wa ujumuishaji wa michango (totalization and period of contribution guidelines 2013) kama ulivyofanyiwa marekebisho kwa polisi waliochangia GEPF na PSPF.
  Aidha Maafisa hao wa PSPF, walioongozwa na Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila Maghimbi, waliweza kutoa huduma za kuwabadilishia vitambulisho na kuwapatia vitambulisho vipya baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, lakini pia maelezo uhusu Mafao yatolewayo na Mfuko katika mpango wa uchangiaji wa lazima, ambayo yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Mafao ya huduma za Muda Mfupi kama vile fao la Uzazi. “Katika kujali ustawi wa wanachama wetu, Mfuko unatoa fao la uzazi kwa mwanachama mwanamke anapojifungua na dhumuni kubwa ni kumuwezesha kujikimu kimaisha wakati wa likizo ya uzazi.” Alisema Bi.Leila Maghimbi.
  Fao la Mkopo wa Elimu, Fao la Kujitoa, lakini pia PSPF hutoa Mkopo kwa mwajiriwa mpya ili kujipanga kimaisha lakini faida nyingine ya anayopata mwanachama ni fursa ya kupata mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkkopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu.
  Aidha Bi.Maghimbi alsiema, aina ya pili ya Mafao ni Mafao ya Muda Mrefu, ambayo ni pamoja na Fao la uzeeni, (Old age benefit), Fao la ulemavu, Fao la Mirathi na Fao la kufukuzwa/Kuachishwa Kazi.
  Sambamba na utoaji wa mada hizo, lakini pia palikuwepo na utoaji elimu wa mtu na mtu (One to One), ambapo Bi Hawa Kikeke, ambaye ni Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, alikuwa akitoa elimu kwa kukutana na mtu mmoja mmoja, huku washiriki hao waliotoka mikoa yote nchini, ikiwemo Unguja na Pemba, walipata fursa ya kuuliza utaratibu wa kupata taarifa za michango yao kwa njia ya mtandao na wengine kuchapishiwa nakala na kuondoka nazo.
  Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila Maghimbi, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Maafisa wa polisi wanawake wa Shirika la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO), kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda, (kulia), akizungumza.
   Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa(kulia), akitoa mada.
  Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha M.Ngalo, akitoa mada
   Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kulia), akimuonyesha Mwanachama huyu michango yake
    Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), akimsikilzia Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke.
   Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke, (katikati), akiwaelekeza namna ya kutumia mtandao wa simu kujipatia taarifa mbalimbali za Mfuko.
   Mwendesha mashtaka wa polisi kutoka mkoani Mwanza, Doroth Thomas, (kulia), akiuliza maswali kuhusu michango yake kwa Afisa huyu wa PSPF
  Afusa wa PSPF, akiwahudumia wanachama hawa kupata taarifa za michango yao
   Afisa wa PSPF, akitoa ufafanuzi kwa wanachama hawa wa Mfuko huo ambao ni maafisa wa polisi
    Wasirki wakifuatilia kwa makini

   Wasirki wakifuatilia kwa makini

   Washiriki wakinakili masuala muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa na maafisa wa PSPF
  Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa(kulia), akisalimiana na Naibu Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Morogoro, D/RCO, Maria Dominic Kway, (kushoto), huku Bi. Kikeke akishuhudia
   Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), Mrakibu  wa Polisi, (SP), kutoka idara ya Uhusiano wa Kimataifa Polisi Makao Makuu, Emma Mkonyi, (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na  Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke
   Mshiriki akisoma kipeperushi chenye taarifa muhimu za PSPF
   Afisa wa polisi akizungumza kwenye mafunzo hayo

  Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda,(watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa PSPF.

  0 0

  Serikali imesema kuwa mabadiliko ya sekta ya fedha ya mwaka 1991 yalipelekea Serikali kujitoa katika uendeshaji wa  moja kwa moja wa shughuli za kibenki nchini ili kuruhusu mfumo wa Soko Huria, hususan nguvu ya soko kuamua viwango vya riba za mikopo, riba za amana na gharama zingine za huduma za kibenki.

  Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu  swali la  msingi la Mbunge wa  Viti Maalumu Mhe. Jesca David Kishoa (CHADEMA), aliyehoji licha ya kuwa na benki nyingi zaidi kuliko nchi zote Kusini na Mashariki mwa Afrika, kwa nini wingi huo bado haujaleta unafuu katika tozo ya riba.
  Akijibu swali hilo Mhe. Dkt. Kijaji alisema kuwa, viwango vya riba za mikopo hupangwa kwa kuzingatia gharama za upatikanaji wa fedha, uendashaji, bima, sifa za mkopaji na hatari ya mkopaji kutolipa mkopo, pamoja na kasi ya mfumuko wa bei.

  “Dhana ya uhitaji na utoaji wa mikopo siyo kigezo pekee kinachoweza kupunguza viwango vya riba hapa nchini, hatari ya kutolipa mkopo ni kigezo kikubwa kinachotumiwa na benki kupanga viwango vya riba za mikopo, hususan kwa wajasiriamali wadogo”. Alisema Dkt. Kijaji 
  Dkt. Kijaji aliongeza kuwa, uzoefu uliopo  unaonesha kuwa, benki zinapendelea kukopesha wajasiriamali waliojiunga katika vikundi kuliko mjasiriamali mmoja mmoja ili kupunguza kiwango cha mikopo isiyolipika.

  Aidha, Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Jesca David Kishoa, alihoji ni kwa nini Serikali isiweke  ukomo wa riba kisheria kwa benki hizo ili kumsaidia mjasiriamali wa sekta binafsi kama ilivyofanya nchi ya Kenya.

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa,  kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za Fedha ya Mwaka 1991, iliyotungwa kwa kuzingatia misingi ya mfumo wa soko huria,  Benki Kuu imepewa jukumu na mamlaka ya kusimamia na kuzichukulia hatua taasisi za fedha zinazoendesha shughuli zao kwa hasara.

  Aliongeza kuwa, kutoa maelekezo kwa benki kutumia viwango fulani vya riba, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuzichukulia benki hatua endapo zitapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza.

  Katika swali la nyongeza Mbunge huyo, alieleza kuwa mikopo isiyolipika imekua kwa kiwango kikubwa tangu mwaka 1991 huku akitaja sababu kubwa mbili ambazo ni mazingira magumu ya biashara pamoja na riba kubwa kwa wafanyabiashara hao.

  ‘’Je Serikali haioni umuhimu wa kuwasaidia kwa kuwapa riba nafuu ili iweze ‘Kustimulize’ (kuchochea) biashara zao’’. Alihoji Mhe. Kishoa.Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mwaka 1991 ya sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha, Benki Kuu au Serikali haiwezi kutoa mweleko au ukomo wa Taasisi za fedha.
  Mwisho

  0 0  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa, akizungumza na waandishi wa habarai Dar es Salaam jana wakati wa semina kwa vijana kuhusu namna ya kutumia Fursa kujikwamua kiuchumi. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Ubunifu Endelevu (HDIF),David McGinty.


  ,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habarai jijini pichani kati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa


  Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Umoja wa Mataifa (UN) na shirika la Human Development Innovation Fund (HDIF) leo wameungana na kuzindua mafunzo ya aina tano za ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mbinu bora za ujasiriamali mdogo na wa kati hapa nchini Tanzania.

  Misingi ya ujuzi na mbinu hizi inalenga kukuza na kuboresha uzoefu wa vijana katika ujasiriamali. Ujuzi huu utawasaidia kuwa imara na kuweza kuhimili ushindani wa kiuchumi.

  Mafunzo haya yenye mbinu tano yatalenga ukuzaji wa bidhaa, mauzo, kumbu kumbu za mauzo, ujuzi wa kawaida pamoja na taratibu na sheria za kufanya kazi.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Bw. Beng’i Issa alisema anaamini ya kwamba uzinduzi wa mafunzo haya yatasaidia Taifa kufanikisha malengo ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2015.

  Kuendeleza wajasiriamali ni muhimu sana kama kweli Tanzania ina lengo la kuwa nchi ya viwanda. Wajasiriamali watajenga fursa nyingi ambazo zitatoa ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi. "Uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukuza ujasiriamali ni njia mojawapo sahihi itakayoleta mafanikio katika Taifa letu", alisema Issa.

  "Kigezo kikubwa kinachohitajika kuwa mshiriki wa mafunzo hayo ni kuwa na ujuzi wa ujasiriamali na kuwa na malengo endelevu ya kukua kibiashara", alisema Issa.

  Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alisema ni muhimu kwa taifa lolote lenye nia ya kujiendeleza kufikia kuwa nchi ya viwanda halina budi kuwathamini na kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati. Bw. Rodriguea alisisitiza kuwa wajasiriliamali ndio wenye nafasi kubwa ya kutoa ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

  Naye mwanzilishi wa Taasisi ya Fursa Tanzania, Bw. Ruge Mutahaba alisema uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukua kijisiriamali kutafungua nafasi pana kwa taasisi na watu binafsi watakaotaka kuunga mkono na kuwa sehemu ya kuendeleza mradi huu. Hii itawapa nafasi pekee ya kushirikiana na vijana wajisiriliamali kutatua changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo yao.

  0 0


  NA ESTOM SANGA-TASAF.

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- na wadau wa maendeleo wameanza mkutano wa kutathimini utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kipindi cha miezi SITA iliyopita.

  Mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TASAF mjini Dar es salaam pia unawajumuisha maafisa wa serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar,pamoja na mambo mengine umefahamishwa juu ya mafanikio na changamoto zilizopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kwa kipindi cha kuishia mwezi Marchi mwaka huu.

  Katika mawasilisho ya shughuli zilizotekelezwa na TASAF katika kipindi kilichopita, imeonyeshwa kuwa zaidi ya kaya milioni MOJA za walengwa zimeendelea kunufaika na Mpango kupitia ruzuku na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoibuliwa na walengwa kupitia utaratibu wa ajira ya muda ambapo hulipwa ujira baada ya kutekeleza kazi hizo.

  Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa kumekuwa na mwitikio chanya wa walengwa katika kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kutumia fedha zinazotolewa na TASAF chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha, na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa ongezeko la kipato kwa kaya zilizoandikishwa kwenye Mpango.

  Mafanikio mengine yaliyoonyeshwa ni ongezeko la mahudhurio ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoka katika kaya za walengwa kupata huduma za kliniki kwa lengo la kuboresha afya na makuzi yao pamoja na kuongezeka kwa mahudhurio shuleni kwa watoto wanaotoka kwenye kaya za walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini.

  Katika kuboresha zaidi huduma kwa walengwa, TASAF kwa kushirikiana na idara nyingine za serikali imeandaa utaratibu wa kuanza kutoa ruzuku ya fedha kwa njia ya kielektroniki ambapo majaribio yataanza katika baadhi ya maeneo ya Utekelezaji wa Mpango huo.

  Wadau hao wa Maendeleo baada ya kuhudhuria mkutano huo wa siku moja watapata fursa ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango huko Zanzibar,Itirima,Magu,Lindi Longido ambako watawatembelea walengwa wa Mpango kuona namna wanaoendelea kunufaika na fedha zinazotolewa katika jitihada za serikali kupitia TASAF katika kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.

  Zifuatazo ni picha za washiriki wa mkutano huo wa wadau wa maendeleo ,baadhi ya maafisa wa serikali na watumishi wa TASAF unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo jijini Dar es salaam. 


  Msimamizi wa shughuli za TASAF (Benki ya Dunia) Bwana Muderis Mohamed (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na TASAF .
  Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Maafisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF – wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini.

  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa maendeleo na TASAF (picha ya juu na chini ) wakiwa kwenye mkutano ulioanza leo kujadili utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akitazama namna mbogamboga za wakulima kwenye Jimbo lake zilivyoharibika hivi karibuni kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji
   Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika  akizungumza na wakulima wa mbogamboga kwenye Jimbo lake  hivi karibuni ambao bidhaa zao ziliharibika kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji
    Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika  akizungumza na wakulima wa mbogamboga kwenye Jimbo lake  hivi karibuni ambao bidhaa zao ziliharibika kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji
    Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika  akizungumza na wakulima wa mbogamboga kwenye Jimbo lake  hivi karibuni ambao bidhaa zao ziliharibika kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji
   Kushoto ni mmoja wafanyabiashara wakimuelezea Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia hasara walizozipata kutokana na ubovu wa miundombinu
   Baadhi ya bidhaa za mbogamboga ambazo zimeharibika kama zinavyoonekana
   Mbunge wa Jimbo la Lushoto(CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akiwa na mfanyabiashara mara baada ya kuangalia namna alivyopata hasara kutokana na ubovu wa miundombinu ambapo pia alitumia nafasi hiyo kuwapa pole
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto(CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika akiwa na wananchji wa Jimbo hilo wakati alipowatembelea hivi karibuni kuona athari za mafuriko kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

older | 1 | .... | 1240 | 1241 | (Page 1242) | 1243 | 1244 | .... | 1896 | newer