Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA

$
0
0

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu Hedhi salama kwa wasichana  (Manustretion Hygiene) wakati wa kampeni iliyoendeshwa na chama hicho  katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG………………………………………………
Na Richard Mwaikenda, MtamaWALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.

Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.

Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.

 Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.
Pia aliwashauri akina baba na kaka kutokuwa mbali na wasichana kwani nao ni wajibu wao kuwasaidia na ikiwezekana kuwapatia msaada wa hali na mali ikiwemo kuwanunulia vifaa vinavyowafaa wakiwa hedhi.

Mwalimu Mariamu Hashima wa Shule ya Msingi Lihimba, aliiisifia kampeni hiyo kwa kuendeshwa kwa uwazi na ukweli, lakini alishauri kuwa mafunzo hayo yatenganishwe kwa watoto wa shule za msingi kuwafundisha zaidi jinsi ya kujiandaa kupata hedhi na vifaa anavyopaswa kuwa navyo.

Timu ya kampeni hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, Mkufunzi Msaidizi Rehema Kijazi, Kiongozi wa Girl Guides Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango.

 Wanafunzi wakishangilia baada ya kufurahishwa na elimu ya hedhi salama
 Mmoja wa viongozi wa Girl Guides Happiness akihamasisha wakati wa kampeni hiyo
 Walimu kutoka shule mbalimbali Jimbo la Mtama, wakisikiliza kwa makini wakati wa kampeni hiyo
 Rachel ambaye ni Girl Guides kutoka Uganda, akiwalekeza wasichana jinsi ya kutengeneza pad
 Girl Guides kutoka Madagascar akionesha namna ya kutengeneza pad
 Michelle Girl Guides kutoka Rwanda ambaye yupo nchi katika exchange program akionesha jinsi ya kutengeneza pad ya kawaida
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia na kuwahamasisha wanafunzi wasichana kujiunga na TGGA
 Mratibu Elimu  Kata ya Majengo, Marsenus Lukanga (kulia) akimkabidhi kasha la vihifadhi (Pad),  Mwanafunzi wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama (Manustretion Hygiene) kwa Wasichana iliyoendeshwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi.
 Viongozi wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya vihifadhi ya pad zitakazogawiwa kwa watakaopata hedhi shuleni kwao.
 Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.
Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.

WAFANYABIASHARA WAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA CHA WAATHIRIKA WA MAAFA YA UPEPO NA MVUA ZA MASIKA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akipokea fedha taslimu za Kitanzanuia Shilingi Millioni kumi kutoka kwa Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais na Mfanyabishara Mhe,Ahmada Yahya Abdulwakil   katika hafla ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,(wa pili kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
MD1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akizungumza na wafanyabishara katika hafla ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni, vilivyotolewa na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo,(wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
MD3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea msaada wa Chakula kutoka kwa Hassan Mohamed Raza kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni,chakula hivyo vikiwemo Unga wa Ngano,Mafuta,Mchele na Sukari, vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar (wa pili kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi na (kushoto) Mfanyabiashara Said Bophar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
MD4
Baadhi ya Waandishi wa habari na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni, vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
MD5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na wafanyabishara mbali mbakli katika hafla ya kukabidhi Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni,mazungumzo hayo yalifanyika leo  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

Wachimbaji wadogo wa madini, wachuuzi na madalali nchini kufanya mdahalo wa kitaifa kuhusu umuhimu wa sekta hiyo

$
0
0
Wachimbaji wadogo wa madini, wachuuzi na madalali wa madini nchini wanatarajia kufanya mdahalo wa kitaifa juu ya umuhimu wa sekta ya madini na namna ya kuwanufaisha zaidi.

Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini Amani Mhinda, akizungumza mji mdogo wa Mirerani na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema) alisema mdahalo huo utafanyika mkoani Geita.

Mhinda alisema lengo la mdahalo huo ni kuwaleta wadau mbalimbali kwa pamoja ili kuzungumzia changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa wachimbaji wadogo na kutafakari kitaifa maono ya wachimbaji. 

Alisema wanatarajia kufanya mdahalo huo mwishoni mwa mwezi Juni kwa kushirikiana na shirika kiongozi duniani la maendeleo la International Institute for Environment and Development (IIED). 

“Haki madini tunarajia mpango huu utatoa jukwa hitajika kwa wadau kushirikiana na kubadilishana ujuzi na kukuza utawala bora kuwa sauti kubwa, usalama na utengenezaji,” alisema Mhinda.

Alisema uchimbaji mdogo wa madini unaweza kutoa mchango chanya wenye umoja na usawa wa maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi, kwani husaidia mamilioni ya watu hasa wanawake na watoto. 

Katibu wa Marema Tawi la Mirerani, Abubakari Madiwa alisema kupitia mdahalo huo wanatarajia wachimbaji mdogo kunufaika kwa kujengewa uwezo hivyo wamejiandaa kushiriki mara utakapofanyika.

“Haki madini imekuwa msaada mkubwa kwa wachimbaji madini wadogo kwani tumekuwa pamoja bega kwa bega kwa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata haki zao,” alisema Madiwa.
 Viongozi wa chama cha wachimbaji madini Mkoani Manyara, Marema Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro, wakizungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita
Mtafiti wa shirika la IIED la Uingereza, Fitsum Weldegiorgis akizungumza juzi na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, Marema (kushoto) ni Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini, Amani Mhinda.
Viongozi wa chama cha wanunuzi na wachuuzi wa madini ya Tanzanite Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita.

Trust Care Tanzania Foundation yawanoa wanafunzi vyuo vikuu Dar

$
0
0
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Dk. Rodrick Ndomba akizungumza kufungia semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) na kushirikisha wanafunzi anuai kutoka vyuo vya IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM, MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI.
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.
Msanii Nick Wa Pili akiwasilisha mada leo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).
MKURUGENZI Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo. Alisema mada zilizotolewa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo.

Kwa upande wa wadhamini wakuu wa semina hiyo Kampuni ya TTCL, Injinia Enocent Msasi Mkurugenzi wa Biashara TTCL alisema kampuni hiyo imeunga mkono kampuni ya Trust Care Tanzania kwa dhumuni lake la kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta za kiafya, kielimu na kijamii. Aliongeza kuwa lengo hilo linashabihiana na lengo la TTCL kuhakikisha inakuwa na jamii bora zaidi kiteknolojia, kielimu, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla.

“TTCL imedhamini semina hii kwasababu inatoa mchango mkubwa katika kujenga taifa lenye vijana wachapakazi, vijana wenye mtizamo chanya, vijana wenye uwezo wa uthubutu, na kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha, ” alisema Msasi na kuongeza kuwa TTCL kupitia huduma zake bora za intaneti, sauti na SMS inawaunga mkono vijana mara zote na itakuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.
Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).
Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).
Mmoja wa wawasilishaji mada kwa wanafunzi (hawapo pichani) wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).
Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) nje ya ukumbi wa semina hiyo leo.
Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

RC GAMBO AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI KWA AJILI YA KUNYWESHEA MIFUGO NA BINADAMU WILAYANI NGORONGORO

$
0
0
Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amezindua mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo(cattle trough) na matumizi ya binadamu katika kata ya Ndepes wilayani Ngorongoro.

Mradi huo mkubwa wa maji umetumia takribani milioni 200 ikiwa ni gharama nzima za mradi huo, utekelezaji wa mradi huo umesimamiwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa mapema mwezi wa Desemba 2016, moja ya maagizo yake ilikua ni wananchi kujengewa mfumo wa maji kwa matumizi yao na mifugo yao ili kuzuia  uingizwaji wa mifugo katika crater ya Ngorongoro.

Aidha Mhe. Gambo ameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kuutekeleza mradi huo kwa wakati na kuendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuwa agizo la kutoingiza mifugo ndani ya crater linaendelea na amezitaka mamlaka kuanza mchakato wa kuligeuza agizo hilo kuwa sheria ili liweze kutekelezeka kwa vitendo zaidi.

Wananchi wa eneo la Ndepes wameishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wananchi hawafuati maji umbali zaidi ya mita mia nne kama ilivyo ahidiwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
 

  

Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao

$
0
0









Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Manyara, Mhandisi Munis Weransari akifungua warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati


Katibu Tawala Msaidizi Mkoani Manyara, (Huduma za Uchumi na Uzalishaji) Felix Mwasenga akifunga warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati .
……………………………………………………………………………………..

Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata), umelalamikia tozo, ushuru wa masoko na tozo za kusafirisha kwa gunia badala ya kutozwa kwa uzito, kwani hujenga mazingira shawishi kwa wanunuzi na madalali kuzidisha uzito wa vifungashi zaidi ya kiwango stahiki.

Mratibu wa Mviwata mkoani Manyara, Martin Pius alisema hayo mjini Babati kwenye warsha ya uboreshaji matumizi ya vipimo na kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya kilimo.

Pius alisema lengo lao ni kutafuta hatua za pamoja kwenye kuboresha biashara ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo ili kuongeza tija kwa wakulima, wanunuzi na halmashauri kwa ujumla.

Alisema inatakiwa kuandaa mpango wa pamoja unaotekelezeka kwa ajili ya kuwezesha matumizi ya vipimo katika wilaya ya Babati na kupashana habari ya maboresho katika sheria ya vipimo, kanuni zake na marekebisho yaliyofanywa.

“Matumizi sahihi ya vipimo ni muhimu sana katika kuhakikisha uwazi na uhakika wa vipimo vinavyotumika, ili wazalishaji, wanunuzi na watumiaji walindwe na serikali ikusanye mapato inayostahili na takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo zipatikane,” alisema.

Alisema tafiti zinaonyesha ukosefu wa uelewa kuhusu vipimo sahihi siyo kwa wakulima au wanunuzi tu bali hata kwa watumishi wa umma ambao wana dhamana kubwa katika kusimamia utekelezaji wake.

Alisema mazoea ya kufanya biashara ya mazao ya kilimo bila kutumia vipimo sahihi yapo kila mahali na kimsingi, biashara ya mazao ya kilimo inayofanyika mashambani hufanywa bila kuhusika kwa wakala wa vipimo.

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo Weransari Munisi alisema ni vyema kutambua pia kuwa sio uzito tu wenye shida katika biashara hii, bali hata vipimo vinavyotumika vinatofautiana kutoka eneo moja na eneo jingine.

Alisema warsha hiyo ni ya muhimu kutokana na mkazo unaowekwa na serikali kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo ikiwa ni pamoja na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya kilimo.

“Ni matazamio yangu kuwa wakala wa vipimo watajenga uelewa wa kutosha kuhusu sheria husika na vipimo stahili kwa mazao ya kilimo na utajenga mtandao wa washirika kudhibiti matumizi ya vipimo visivyo sahihi,” alisema Munisi.

Alisema uuzaji wa mazao mabichi shambani ni kosa na hasara kubwa kwa wakulima kwani huwa hakuna kipimo cha kupima mazao yaliyo shambani, na kunmkosesha mkulima mapato makubwa yatakayopatikana na uuzaji wa mazao hayo pindi atakapovuna na kuuza kwa kutumia vipimo sahihi vya ujazo.

TGNP MTANDAO YAWAPONGEZA WASICHANA WALIOFANYA VIZURI KATIKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi habari kuhusu kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika vyuo mbalimbali nchini katika ukumbi wa TGNP  leo jijini Dar es Salaam. 
 Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela akizungmza na waandishi habari juu umahiri wake ambao ulimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya mwisho katika chuo katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.
 Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha  Kairuki, Flora Njiku akizungmza na waandishi habari juu rushwa ya ngono kwa watoto wa kike vyuoni katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini wakifuatia kinachoendelea kwenye mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar
Mkutano uliendelea 


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TGNP Mtandao imesema kuwa changamoto inayowakabili wanafunzi wa vyuo  vikuu nchini ni rushwa ya ngono.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38  waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa  TGNP,  Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.
Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.

Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri  katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.

Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkomboa mwanamke katika changamoto mbalimbali.

Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri , Aisha Soudy  kutoka  Chuo cha  Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.

Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.

Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama  akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti  kuliko vile wanavyofikiria.

Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.

TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza Katibu na Mwanasheria wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Hilali Vuai (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Kassim Maalim Suleiman (kushoto) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akiwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu visiwani Zanzibar.
Meneja wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Usi (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati).
Wadau wa Zao la Karafuu wakifuatilia kwa makini wasilisho kutoka TADB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wazalishaji Karafuu Zanzibar (ZACPO), Bw. Abubakari Mohamed Ali akiuliza swali kwa TADB kuhusiana na fursa za mikopo kutoka Benki hiyo.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika wa Kikao cha Wadau wa Karafuu.

…………………………………………………………………………………….


Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imewahakikisha kuwapatia mikopo wakulima wa Zao la Karafuu visiwani Zanzibar katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika wakulima hao.

Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akitoa mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu visiwani Zanzibar katika Kikao cha Wadau wa Karafuu kilichokuwa kinafanyika mjini Unguja.

Bw. Assenga alisema kuwa Serikali inatambua changamoto wanazokutana nazo wakulima nchini na hivyo uanzishwaji wa TADB unalenga kutekeleza hatua mbalimbali zikilenga kuharakisha mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo ikiwemo uendelezaji wa zao la karafuu ambalo ni zao kuu la biashara visiwani Zanzibar.

“Tunatambua kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliweka Mkakati Maalum wa miaka 10 (2011 -2021) wa kuongeza uzalishaji, usafirishaji, ubora na tija wa zao la karafuu kwa kutambua hilo Benki inakuja kuongeza kasi juhudi hizi za Serikali,” alisema.

Alisema kwa kutambua juhudi za SMZ zao la karafuu lilipewa kipaumbele cha pekee miongoni mwa minyororo ya thamani ya kwanza kuanza kupatiwa mikopo na Benki hiyo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali nchini.

Aliongeza kuwa maeneo yanayowekewa mkazo katika undelezaji wa kilimo cha karafuu ni pamoja na uongezaji tija wa kilimo cha karafuu ambapo TADB inatoa mikopo na kusaidia shughuli mbali mbali za uongezaji tija wa mazao yatokanayo na kilimo cha karafuu.

“Katika kuhakikisha kuwa uongezaji tija wa kilimo cha karafuu unafanyika ipasavyo Benki inashirikisha wadau wa Kilimo, utafiti na huduma za ugani na ili kuwapatia wakulima mafunzo ya kilimo cha kisasa cha karafuu na kutumia mbinu bora za kilimo ili kuongeza mazao ya karafuu,” Bw. Assenga alisema.

Bw. Assenga aliongeza pia Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za kilimo (mbegu bora na miche ya karafuu yenye kuvumilia magonjwa, wadudu, na inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha karafuu, mbolea, madawa na mengineyo); na kugharamia teknolojia bora na nafuu ya umwagiliaji (panapohitajika).

Aliyataja maeneo mengine yanapatiwa mikopo ni pamoja na ununuzi wa vifaa, mashine na mitambo mbalimbali ya kilimo cha karafuu na mtaji kwa ajili ya uendeshaji wa shamba, uongezaji wa thamani na gharama za uhifadhi na masoko

Bw. Assenga alisema kuwa TADB pia inatoa mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa zao la karafuu katika kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa karafuu kwa ajili ya kuongeza thamani mazao ya karafuu. Ikiwemo ununuzi wa mashine bora za uvunaji, ukaushaji, usafirishaji na uhifadhi wa karafuu; ununuzi wa vifaa vya teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno. Mikopo mingine ni kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya usindikaji pamoja na vifungashio vya karafuu; uchambuzi wa madaraja na ubora wa karafuu na uwekaji wa utambuzi wa muuzaji; na kugharamia mahitaji mengineyo ili kuongezea karafuu thamani.

Kwa upande wa miundombinu ya masoko, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa Benki inatoa mikopo kwa zao la karafuu kwa lengo la kuendeleza miundombinu ya masoko kama vile ujenzi wa maghala/vifaa vya kuhifadhia karafu na mazao yake na miundombinu ya masoko; kugharamia usafirishaji wa karafuu na mazao yake yaliyo tayari kwenda sokoni. Mikopo mingine ni kwa ajili ya uanzishaji wa mifumo ya upatikanaji wa taarifa za masoko, kuwezesha uhusiano wa masoko ya ndani na masoko ya kikanda na kugharamia mahitaji mengineyo ya kuwezesha miundombinu ya masoko.

Naye, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Karafuu ni zao la kipaumbele katika uchumi wa Zanzibar ambapo Serikali ya Mapinduzi kupitia Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) imekuwa ikifanya Mageuzi makubwa katika Sekta nzima ya Karafuu ikiwa ni pamoja na kutengeneza Sheria, Sera na Miongozo madhubuti ya kusimamia Sekta hii ambapo faida, tija na ustawi wa maisha ya wanaotegemea kupata kipato katika zao hili unaonekana.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 21,2017

Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dar es salaam

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwenye Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambukilisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Rwanda Mhe. Francois Kanimba kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni  kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimwo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni  kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kikanda Dkt. Augustine Mahiga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
Viongozi wakijiandaa na mkutano wao wa ndani
Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto akiongea na Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania Profesa Paramagamba Kabudi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
Ujumbwe wa Rwanda mkutanoni hapo
Gavana wa Benki Kuu Mstaafu Mzee Edwin Mtei (kati) akiwasili ukumbini
Meza kuu ya viongozi ikiwa imesimama wakati wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mpiga picha wa Naibu Rais wa Kenya akiwa kazini
Sehemu ya wajumbe na mabalozi wa nchi mbalimbali
Wajumbe na mabalozi 
Mabalozi na wageni waalikwa
Mshereheshaji akitoa maelezo ya awali
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuhutubia
Wajumbe wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea na hotuba
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimalizaia hotuba na kuaga rasmi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribishwa kitini pake Mwenyekiti mpya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli na anayeingia Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakirekebisha mkao wa majina
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Dkt Libérat Mfumukeko akifungua pazia
Wajumbe na wageni waalikwa wakifuatilia
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya akiendesha mkutano
Wajumbe wa Tanzania
Mkutano ukiendelea
Viongozi wakiweka sahihi makubaliano yaliyofikiwa
Mwanahabari kutoka Burundi akiwa kazini
Wajumbe wakifurahia jambo
Jaji Charles Oyo Nyawezo kutoka Sudan ya Kusini akila kiapo  kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Jaji Charles Oyo Nyawezo kutoka Sudan Kusini  akipongezwa kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
Jaji Charles Oyo Nyawezo kutoka Sudan Kusini akipongezwa kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
Mhandisi Steven Mrote kutoka Tanzania akila kiapo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Eng.Steven Mrote kutoka Tanzania kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akimpongeza Eng.Steven Mrote kutoka Tanzania kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 

Mshindi wa tano wa insha akipongezwa
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Museveni wa Uganda akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa kitado cha nne aliyejishindia nafasi ya nne katika mashindano ya uandishi wa insha ya Jumuiya hiyo kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Tanzania Joseph Mbogo 
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa kitado cha nne aliyejishindia nafasi ya nne katika mashindano ya uandishi wa insha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Tanzania  Joseph Mbogo 
Mshimdi wa tatu wa insha akipokea zawadi yake
Mshindi wa pili wa insha kutoka Uganda akipokea zawadi yake
Mshindi wa jumla wa mashindano ya insha kutoka Burundi akipokea zawadi yake

Tamko la kulimganisha mitaala ya elimu ya juu kwa nchi zote wanachama

Wanahabari kazini
Wajumbe wakifuatilia kinachoendelea
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akihutubia mkutano
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akihutubia mkutano
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akihutubia mkutano
Wajumbe wakiwa wamefurahishwa na hotuba ya  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni baada ya kuhutubia kwenye Mkutano 
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akionesha waraka baada ya kuhutubia kwenye Mkutano 
Mabalozi wakifuatilia hotuba kwa makini
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Mstaafu Mzee Edwin Mtei
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja na Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya
Picha ya pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya
Picha ya pamoja na mabalozi
Picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wao
Viongozi wakiwapongeza wanafunzi walioshiriki mashindano ya insha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni baada ya Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana kwa Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimwo 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimwo 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Rwanda Mhe. Francois Kanimba
. akiagana na Bw. AggreyTisa Sabuni, Mshauri wa Uchumi wa Rais wa  Sudan yaKusini

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba  kwa kuhitimisha vyema mkutano huo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ali Idi Siwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri  wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Dkt. Augustine Mahiga kwa kuhitimisha vyema mkutano huo
Waziri  wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Dkt. Augustine Mahiga akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ali Idi Siwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana. Picha na IKULU

WANAWAKE 18 WAHITIMU MAFUNZO YA UONGEZAJI THAMANI MADINI

$
0
0

Na Veronica Simba - Arusha

Jumla ya wanawake 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini, jana (Mei 19, 2017) wamehitimu mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha. 

Wahitimu hao wa awamu ya nne, wamefanya idadi ya waliohitimu tangu kuanzishwa mafunzo husika katika Kituo hicho kufikia 65.

Akizungumza katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, alitoa wito kwa wadau wa madini ya vito nchini, kuwapa ajira na ushauri wa kitaalam wahitimu, ili waweze kujiajiri katika shughuli za uongezaji thamani madini. 

"Lengo ni kuhakikisha kuwa ukataji unafanyika kwa viwango vya kimataifa ili kuweza kuuza zetu kwenye masoko ya nje."

Aidha, Dkt. Pallangyo alitoa changamoto kwa wadau wote wa madini ya vito kuendelea kukuza shughuli za uongezaji thamani madini kwa kubadilishana uzoefu na wakataji wa madini ya vito mahiri duniani. 

"Kwa wale wafanyabiashara wa madini ya vito, mlioajiri wataalam wa kigen, natoa rai muendelee kuwahimiza watoe mafunzo kwa watanzania wanaofanya nao kazi, ili kuhawilisha utaalam huu adimu," alisisitiza. 

Vilevile, Naibu Katibu Mkuu, aliwaasa wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa Kituo kinachotoa mafunzo hayo ya TGC, kwa kuendelea kufanya shughuli za uongezaji thamani madini popote watakapokwenda. 

Alitoa rai kwa uongozi wa TGC kujenga utamaduni wa kuwaalika wahitimu wote wa Kituo hicho hususan waliojiajiri, kushiriki katika sherehe za Mahafali, ili waoneshe bidhaa zao.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, akitoa historia ya TGC, alisema kuwa, Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuwekeza katika Kituo hicho kwa malengo ya kutoa mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito kwa wachimbaji wadogo na wajasiriamali wa madini hayo. 

Aliongeza kuwa, malengo mengine ni pamoja na kukuza na kufanikisha shughuli za uongezaji thamani katika madini ya vito nchini, kukuza na kuendeleza ujuzi na ufahamu wa kutambua madini ya vito na kuongeza kipato na ajira kwa watanzania. 

Alisema kuwa, katika kujenga uwezo wa ndani na kupata wakufunzi wenye sifa za kimataifa; Wizara ilipeleka watumishi watatu nje ya nchi kujifunza masomo ya vito na usonara kwa lengo la kuwa wakufunzi katika Kituo hicho. "Watumishi hao walikwishahitimu mafunzo yao na tayari wamesharipoti kituoni."

Mhandisi Mchwampaka alisema kuwa, Wizara inakusudia kupeleka watumishi wengine watano nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo husika ili kukijengea uwezo Kituo kwa kuwa na walimu wa kutosha. 

Akizungumzia mafunzo mengine yanayotarajiwa kutolewa na Kituo hicho baadaye, alisema kuwa ni pamoja na Jemolojia, Utengenezaji wa bidhaa za mapambo pamoja na uchongaji wa vinyago vya mawe. 

"Aidha, Kituo kitaanzisha maabara ya utambuzi na uthibitishaji wa madini ya vito na bidhaa za urembo. 

Akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi, kwa niaba ya wahitimu wenzake, Theresia Mollel, alisema kuwa mafunzo hayo yamewapa uwezo kama wanawake wa kufanya kazi katika sekta ambayo wengi hudhani wanawake hawaiwezi. 

"Kupitia mafunzo haya, tunaihakikishia jamii kuwa wanawake tunaweza kufanya mabadiliko katika tasnia ya madini ya vito na kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla."

Kituo cha Tanzania Gemological Centre (TGC) kilianzishwa mwaka 2003.

Mafunzo haya hutolewa kwa muda wa miezi saba ambapo miezi sita ni nadharia (darasani) na mwezi mmoja ni mafunzo kwa vitendo.

Wanafunzi hawa wanafadhiliwa na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Maonesho ya Madini ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair) chini ya Mfuko wa Kuwaendeleza Wanawake.

 Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito, zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito, zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.

Wahitimu wa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakiwa darasani.

Wahitimu wa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakiwa darasani.

Wahitimu wa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
 Wahitimu wa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
 Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua), akijumuika pamoja na wahitimu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kucheza muziki.
 Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, akisoma historia ya Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani).

Mgeni Rasmi katika sherehe za mahafali ya Nne ya Mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito nchini, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua – walioketi) na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu.
Mwanafunzi bora, Happiness Ernest, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi.

MAHAFALI YA 29 YA KIDATO CHA SITA YA SHULE YA SEKONDARI YA AL HARAMAIN JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wahitimu wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakiingia kwenye ukumbi wa mahafali wakati wa mahafali yao ya 29, jijini Dar es Salaam jana.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shue ya Sekondari ya Al Haramain, Hairat Hashim akisoma Qur'an katika mahafali hayo.
Mwanafunzi Mohammed Fauz wa shule hiyo, akitoa mawaidha wakati wa mahafali hayo.
Mwalimu wa Nidhamu katika shule hiyo, Mwalimu Omar Hamad, akiwaongoza wanafunzi wa kidato cha tatu kughani kaswida wakati wa mahafali hayo ya 29, jijini Dar es Saaam jana.
Wanafunzi wa kidato cha tatu wakipiga dufu na kughani kaswida wakati wa mahafali hayo ya 29, jijini Dar es Saaam jana.
Rais mstaafu wa Serikali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, mhitimu wa kidato cha sita, Hassan Hamisi akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Rais mpya wa Serikali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, mwanafunzi wa kidato cha tano, Salim Mruta, akitoa shukrani zake kwa wahitimu, wakati wa mahafali hayo.
Imam wa Msikiti wa Al Haramain, Sheikh Issa Kalunga, akitoa dua wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kike wa kidato cha sita wa shule hiyo, wakiwa kwenye ukumbi wa mahafali yao hayo jana. 
Mwanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Omar Rajab, akisoma Qur'an katika mahafali hayo.
Mwanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Ally Athumani akitoa tafsiri ya Qur'an iliyosomwa katika mahafali hayo.
Baadhi ya wazazi na walezi wa wahitimu wa kidato cha sita, wakiwa kwenye ukumbi wa mahafali hayo, wakifuatilia matukio mbaimbali yaliyokuwa yakifanyika ukumbini humo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuh Jabir (wa pili kushoto), akiwa na baadhi ya walimu viongozi katika meza kuu katika mahafali hayo. Kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu Rashid Kassim.
Hali ya ukumbi ulivyokuwa wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa kidato cha tano wa shule hiyo, Mwajuma Ahmad (kushoto) na Husna Khalid wakighani utenzi mbele ya mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka (katikati, mwenye simu), akiwa meza kuu pamoja na Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa.
Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir, akimkaribisha Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka (kushoto kwake) pamoja na kutambulisha walimu viongozi kwenye meza kuu. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa na kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu Rashid Kassim.
Mhitimu wa kidato cha sita, Hassan Hamis (kushoto), akisoma risala ya wahitimu. Kulia anayemsaidia ni Waziri Hassan.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa, akizungumza wakati wa mahafali ya 29 ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain. Kushoto ni Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka.
Wahitimu wa kidato cha sita, Yusra Said (kushoto) na Raiyan Hassan wakighani utenzi mbele ya mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka.
Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir, akisoma taarifa ya shule kwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 29 ya kidato cha Sita, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka (kulia), wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu Rashid Kassim.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akizungumza na wahitimu hao, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha Kiongozi Bora, mhitimu Khadija Mashaka, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti Mwanafunzi Bora katika somo la Geography, mhitimu Mussa Baruti, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Hawa Gulamu, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Raiyani Hassan, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Sada Said, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Yusra Said, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Zaudia Ibrahim, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Bakari Gogoro, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Hassan Hamisi, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Israfil Ramadhani, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha sita mhitimu Kibeku Ramadhani, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AONGOZA HAFLA YA UCHANGIAJI VIFAA VYA MICHEZO SKULI ZA SERIKALI (1)

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe  Mama Mwanamwema Shein (kushoto) pamoja na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi pia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangiaji Vifaa vya Michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar Mhe.Mohamed Ramia wakiangalia picha ya zamani wakati Dk.Shein alivyokuwa akishiriki mchezo wa Riadha katika Skuli ya Lumumba picha hiyo iliyofikishwa katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
haf3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiwa na Viongozi mbali mbali katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi Mmoja Mjini Unguja akiwepo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia),[Picha na Ikulu.] 20/05/2017. 
haf8
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akitangaza mchango wake wa Milioni moja kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
haf9
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akitangaza mchango wa Millioni nane kwa niaba ya familia yake kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
haf10
Picha  ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipiga mpira wakati wa Uzinduzi wa Mashindano ya Vyuo Vikuu ikinadisha wakati wa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

haf4
Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja wakiwa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]  20/05/2017. 
haf5
Baadhi ya wawakilishi wa Makampuni ya kibiashara wakiwa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]  20/05/2017. 
haf6
Mfanyabishara wa Zanzibar Said Bophar alipokuwa akitangaza mchango wake mbele ya uuma uliokusanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja wakati wa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]  20/05/2017. 
haf7
Mwakilishi wa Mamlaka ya Maji safi na Salama ZAWA  Nd,Kazija Mussa Msheba akitangaza mchango wao wa Millioni tano wakati wa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana,katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja  ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]  20/05/2017. 

haf1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipowasili katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja jana katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
haf2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakifuatana  na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) walipokuwa wakiingia   katika  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi   Mnazi Mmoja Mjini Unguja jana katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

Sospeter Muchunguzi naye azoa mkwanja wa Biko

$
0
0
DROO ya saba ya mchezo wa Kubahatisha wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Sospeter Muchunguzi akifanikiwa kuibuka kidedea na kuzoa Sh Milioni 10.

Mkazi huyo wa jiji alifanikiwa kujinyakulia zawadi hiyo ya juu ya Sh Milioni 10 kutoka Biko, katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa ushirikiano na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo ya saba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Watanzania wameendelea kupata hamasa kubwa na kujitokeza kwa wingi kuwania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya saba ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo bwana Sospeter Muchunguzi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam alitangazwa mshindi.
Kajala Masanja akionyesha namba ya mshindi.

“Ni furaha kwetu kuona idadi kubwa ya Watanzania inajitokeza kwa wingi kucheza Biko na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwetu kwa kucheza bahati nasibu yetu kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 ambapo kwenye namba ya kampuni wataingiza 505050 na namba ya kumbukumbu ni 2456.

“Biko bado inaendelea kuchanja mbuga ambapo sasa tutakuwa tunachezesha droo kwa siku ya Jumatano na Jumapili kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na ushindi wa Biko na kuzoa mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.

Naye Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe, aliwataka Watanzania kuendelea kuchangakia zawadi za Biko kwa kucheza kwa wingi kutokana na utaratibu mzuri na urahisi wa mchezo wa Biko.

“Bodi yetu ipo makini kufuatilia kwa kina uchezaji wa bahati nasibu, hivyo tunawaomba watu wacheze kwa sababuBiko ni mchezo salama na unafuata kanuni, sheria na taratibu zote,” Alisema Chiku ambaye pia aliwaasa akina mama kujitokeza kwa wingi ili nao washinde mamilioni ya Biko.

Akizungumza kwa simu, mshindi huyo wa droo ya saba ya Biko, Sospeter Muchunguzi, alishukuru kwa kuibuka na ushindi huo, akisema ni mchezaji mzuri wa bahati nasibu hiyo ambapo mbali na kushinda Sh Milioni 10, pia amewahi kushinda zawadi za papo hapo mara kadhaa.

Baada ya kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 10, Biko watamkabidhi mshindi huyo fedha zake mapema wiki hii kama walivyokabidhiwa wengine ili waziweke katika mipango yao ya kimaisha.

Hatua za kufuata baada ya kuachwa na ndege

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Ni jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.

Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travelingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.

Wasiliana na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.

Kuwa makini na sheria na masharti ya tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege linakuwa na taratibu za uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo zinawasafirisha na ndege nyingine wateja wao waliochelewa, zingine siku inayofuata kama hamna kwa siku hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo au soma kwenye tiketi yako kama zipo.

Usihamaki/usiwe na hofu. Wewe sio wa kwanza kuachwa na ndege hali hiyo ishawakuta watu wengi hivyo vuta pumzi na tuliza akili yako ili ujue nini cha kufanya. Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya tatizo haraka sana kama vile kuulizia cha kufanya, kuahirisha au kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu ili usafiri na kuwahi shughuli zako kama ulivyopanga. Kwani kama kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha kufanya kutokana na hali hiyo.

Ulizia kwa wafanyakazi wa kampuni husika ya ndege machaguo uliyonayo. Kama umeshindwa kupata mawasiliano au haujui taratibu za shirika la ndege ulilokatia tiketi ya kusafiri basi ni vema ukauliza. Mashirika mengi yanakuwa na ofisi kwenye viwanja vya ndege au kama hawana basi ulizia wafanyakazi wa pale naamini wao wana uzoefu mkubwa wanaoweza kukupatia.

Lipia gharama za ziada baada ya kukosa ndege kama ulishafika tayari. Kama unaona kwamba utachelewa shughuli zako huko uendako basi huna budi kuongeza pesa kidogo ili uweze kusafiri na ndege inayofuata. Hii itakuwa nafuu zaidi kuliko kukata tiketi upya au kuahirisha safari. Kwa hiyo ni vema pia kuwa na fedha au chanzo za ziada pindi unapokuwa unasafiri kwani chochote kinaweza kutokea.

Tazama kama kuna ndege zingine zinazoelekea mahali uendapo. Kwa kawaida kwenye viwanja vya ndege vingi kunakuwa na ubao unaoonyesha ndege za mashirika tofauti zinazokwenda sehemu mbalimbali kwa siku hiyo. Hivyo inaweza kuwa fursa kwako kwa kufanya maamuzi ya kukata tiketi ili kuwahi shughuli zako.

Tumia muda huo kufanya mambo mengine. Kuchelewa safari haimaanisha kwamba ndiyo mwisho wa maisha. Kwa mfano upo Arusha na umechelewa ndege ya kukurudisha Dar es Salaam kwa siku hiyo, unaweza kuamua kutembelea vivutio kadhaa vilivyopo karibu na eneo hilo kama vile hifadhi ya Serengeti au Ngorongoro au hata Mlima Kilimanjaro.

Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema. Mara nyingine huwa tunafikia kwenye hoteli kwa mahali tunapoelekea labda uwe unarudi nyumbani. Kwa hiyo nina uhakika utakuwa umelipia hoteli wakuhifadhie chumba au kuomba usafiri wa kuja kukuchukua uwanja wa ndege. Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema kwamba utachelewa au utafika siku inayuofuata ili kuondoa usumbufu kwao na kulipishwa gharama za ziada.

Jifunze kutokana na makosa yako. Kufanya makosa ni sehemu ya kujifunza mambo mengi maisha yetu. Hivyo basi hakikisha kwamba baada ya kuchelewa safari hii utakuwa makini zaidi wakati mwingine. Kama ulichelewa kwa sababu ya usafiri basi hakikisha unatoka mapema zaidi, kama ni ulikosea kuangalia muda basi muombe mtu wa karibu yako akukumbushe.

Sababu ni nyingi ni zingine haziwezei kuzuilika kwa upande wa abiria na hata kwa shirika la ndege. Kuna wakati mwingine unaweza kuchelewa ndege kutokana na sababu za kiufundi za shirika lenyewe. Mara nyingi kwa sababu kama hizo abiria huwa wanafidiwa na mashirika ya ndege. Lakini kama ni sababu zako binafsi, Jumia Travel inakuasa kwamba uwe makini kwani utaishia kupoteza muda, kuvuruga mipango yako na kuingia gharama za ziada usizozitarajia.

Tips to consider when you miss your flight

$
0
0


By Jumia Travel Tanzania

It's not surprising to miss a bus, boat, train or flight regardless of how well you could be prepared. Some of the reasons which could lead someone to miss a flight include traffic jam, accident, flat tire or confusion on the reporting time.

To miss a flight is very stressful especially if it’s for the first time and you don’t have any alternative. There are a couple of steps to follow which Jumia Travelwould like you to know and consider once you face the situation.

Contact your local travel airline. The first thing to do once you discover that you will be late or miss the flight is to contact the airline company. Check your flight ticket or website for a phone number to call and know if there is any assistance you could get.  

Check terms and conditions on ticket you have booked. Every airline company has got its policy on how it operates. Some of them board their passengers to the next flights on the same or next day while others charge extra money for no-show. So it's better to be aware of those policies.

Don’t panic. You are not the first human being to be left behind by a flight so stay calm and think of what to do next. You will be able to make better decisions on whether to look for another flight so as to catch your itinerary as planned or postpone it. Since what is done is done you cannot do anything about it.

Ask staffs for other alternatives available. If you have no clue on what to do next or contacts of your airline company, please ask the staffs at the airport to help you. Not all the companies have offices at the airport so ask people around with a greater experience.

Pay extra money to cover the loss. If you think that you have important stuff to take care of where you are going, then you have to add some extra amount of money for no-show. This will be much easier and helpful to you rather than to cancel or postpone a flight at all. So in such situations it's advisable to have extra cash or credit card to issue emergence payments.

Check out on other flights heading to your destination. Usually almost all airports have departure boards, so check out on another flight heading to your destination. That could provide you an opportunity to book for another flight if you need to be where you want to go.

Use that time to explore other things. To miss a flight doesn’t mean that other things should stop. For example, if you miss a flight from Arusha to Dar es Salaam, try to look and visit the tourist attractions around such as Serengeti National Park and Ngorongoro Conservation Area or a trip to Mount Kilimanjaro just a few kilometers away.

Inform your hotel early. If you had booked a hotel or arranged a pick-up at airport upon arrival to your destination, inform the hotel that you will be late or arrive on the next day. This will help avoid negative implications or incurring extra costs.  

Learn from your mistakes. Making mistakes is part of learning in our lives. Hence, make sure that you do not miss your flight next time. If you were late because of traffic jam then make sure you leave earlier than before; and if you had mixed up the time of your departure, it's better to set a reminder.   

In general, there are a lot of reasons which might lead to a missed flight to both passengers and airline companies. Sometimes you could miss a flight because of technical problems from the company which in such cases travelers are compensated. But if you miss a flight on your own personal reasons, take responsibility and rectify the mistake to avoid a repeat of the same.

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo. 
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini. 

Wagonjwa wakitumia mashuka na vitanda vilivyotolewa na PPF.
Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. 

Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. 

Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. 

Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. 

Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari ‘WOTE SCHEME’ ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.

USHIRIKA WA WAUZA MADAGAA WA TUSIYUMBISHANE WAOMBA ‘JEKI’ YA TADB

$
0
0

Wajumbe wa Kikao cha Pamoja kati ya Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kikao kilijadilia changamoto zinazozikabili Ushirika huo na namna TADB inavyoweza kuwasaidia katika kuendeleza ushirika huo.

Mtaalamu wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Khamis Mkanga (katikati) akiendesha Kikao cha Pamoja kati ya Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia).


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akizungumza na Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane wakati alipofanya kikao na umoja huo. Kikao hicho kilifanyika eneo la Maruhubi mjini Unguja. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Ushirika huo Bw. Haji Omar Haji na Mtaalamu wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Khamis Mkanga (wapili kushoto).
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (wakwanza kushoto) akizungumza na Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB.
Mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane, Bibi Bahati Shabani (kulia) akitoa maelezo kuhusu shughuli za uchakataji wa dagaa. Bibi Bahati alimuelezea Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli hiyo.
Bw. Salim Kassim (wapili kulia) Mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane akifafanua jambo kwa ugeni kutoka TADB.
Ugeni kutoka TADB wakkaua dagaa walio tayari kuuzwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akmuunga mkono kwa kununua dagaa zungumza mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akishauri namna bora ya ufungishaji wa dagaa walio tayari kwenda sokoni.

……………………………………

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja kimeiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza ushirika wao kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine ili kuboresha huduma zao.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika eneo la ushirika huo mjini Unguja, Mwenyekiti wa Tusiyumbishane, Bw. Haji Omar Haji amesema licha ya fursa kubwa iliyopo kwenye eneo la ukaushaji wa madagaa, ushirika wao unakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya kuboresha huduma zao.

Bw. Haji ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa ni changamoto kubwa inayochangia kurudisha nyuma ukuaji wa biashara hiyo hivyo kuwa kikwazo katika kupambana na umaskini wa kipato miongoni mwa washirika wa umoja huo hivyo akaiomba benki hiyo kuwawezesha ili kuongeza tija ya shughuli zao.

“Uduni wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabenki na taasisis nyingine za kifedha kushindwa kutuwezesha sie wajasiriamali wa hali ya chini kwa kukosa sifa wazitakazo, hivyo tunaiomba TADB kutuwezesha ili tuongeze tija katika shughuli zetu,” Bw. Haji aliongeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki yake imesikia kilio cha umoja huo, na watatimiza ndoto zao ili kuweza kutimiza ndoto za Serikali za kuanzisha TADB ili kusaidia wakulima na wavuvi wadogo kukabiliana na mapungufu ya upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na uvuvi kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya uvuvi hasa ufugaji wa samaki ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa mazao yatokanayo na samaki nchini.

Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa eneo la uvuvi na ufugaji wa samaki ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wa samaki wadogo nchini.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya masoko kwa ajiili ya kuboresha kilimo na uvuvi hasa ufugaji wa samaki nchini,” alisema Bw. Assenga.

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WASAINI TAMKO LA PAMOJA LA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA LA HOIMA-TANGA

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakizungumza kabla ya zoezi la kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21,PICHA NA IKULU
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni na wajumbe zao katika mazungumzo ya mwisho  kabla ya kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni na wajumbe zao katika mazungumzo ya mwisho  kabla ya kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017. 
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017. 
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017. 
Wanasheria wakuu wa Uganda na Tanzania wakiweka ushuhuda wa tamko hilo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiongea baada ya yeye na Rais Dkt John Pombe Magufuli  wa Tanzania kukamuilisha   zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiongea baada ya yeye na Rais Dkt John Pombe Magufuli  wa Tanzania kukamuilisha   zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya yeye na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kukamilisha zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya yeye na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kukamilisha zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya yeye na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kukamilisha zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya yeye na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kukamilisha zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya yeye na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kukamilisha zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakipongezana  baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakiwa na Mawaziri na  maafisa waandamizi wa pande zote mbili baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakiwa na watendaji wa pande zote mbili baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU MKAPA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea  Rais huyo Mstaafu nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea Rais huyo Mstaafu  nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live


Latest Images