Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKA KITAMBI NA UZITO ULIOKITHIRI.

$
0
0


Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba akielezea jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige
Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA).
Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akionyesha Jarida linaloandaliwa na Shirika la Afya Duniani wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba.

Picha na: Frank Shija - MAELEZO


Na: Nuru Juma-MAELEZO.

Daktari Mshauri kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Dkt. Ali Mzige amewataka watanzania kuepuka uzito mkubwa na kitambi ili kufanya miili yao kukaa mbali na magonjwa yanayosababishwa na vitu hivyo.

Dkt. Mzige amezungumza hayo leo katika ukumbi wa maelezo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa watu wengi wanachukulia kawaida na wengine wanapenda kuwa na kitambi na uzito mkubwa lakini ni vitu vyenye madhara makubwa na husababisha magonjwa ambayo ni magumu kutibika.

“Unene uliokithiri huleta shida kwenye moyo, shinikizo kubwa la damu,kisukari, saratani za aina mbalimbali, kushindwa kupumua vizuri na magonjwa mengine mengi hivyo watu wanatakiwa kuepuka ili kujinusuru na magonjwa hayo,” alisema Dr Mzige.

Aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha asilimia kubwa wanawake wanavitambi na uzito uliokithiri kuliko wanaume hali inayotokana na wanawake wengi kupendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi.

Aidha aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kula vyakula vya asili,kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ili kujua mapema kama ana tatizo lolote la kiafya na kujiepusha na maradhi yanayoweza kuepukika.

Aliongeza kuwa uzito wa mtu unatakiwa kulingana na umri na urefu kwani mtoto wa mika 5 anapaswa kuwa na kilo 18, kijana mwenye miaka 14 mvulana kilo 48 na msichana kilo 49 huku mtu mzima mwanaume mwenye urefu wa futi 5 na inchi 8 anapaswa kuwa na kilo 68.

Tiba nzuri na iliyosahihi ya kuepuka maradhi mengi ni kutokaa masaa 4 bila kufanya kazi,kuzuia kitambi kisijitokeze kwa kula kiasi cha chakula kinacholingana na mahitaji yako, kupunguza ulaji wa sukari na mafuta na kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.

Muhimbili: Upungufu wa Wauguzi Kushughulikiwa, Maslahi Kuboreshwa

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na wauguzi leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.
A
 Baadhi ya Wauguzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru katika maadhimisho hayo.
A 1
 Baadhi ya Wauguzi wakirudia kiapo kwamba wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uadilifu.
A 2
Muuguzi wa Muhimbili, Furaha Tada akitoa mada kwenye maadhimisho hayo leo.
A 3
Wauguzi wakifuatilia mada iliyowasilishwa na mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo.
A 5
Philonem Kaongo ambaye ni Muuguzi Mkunga akitoa mada kwenye maadhimisho.
A 6
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru akipokea risala kutoka kwa Debora Bukuku baada ya kuisoma kwenye maadhimisho hayo.
 A 7
Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Sebastian Luziga akizungumza kwenye maadhimisho hayo leo.
…………………….
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umesema utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo na kushughulikia tatizo la upungufu wa wauguzi.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, Tawi la Muhimbili ambayo huadhimishwa Mei 12 kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu “ Wauguzi Mbiu ya Kufikia Malengo Endelevu ya Milenia.”
 
Profesa Museru amesema Serikali ipo bega kwa bega na hospitali hiyo katika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. “Serikali imeahidi kutatua tatizo la upungufu wa wauguzi katika siku chache zijazo,” amesema Profesa Museru.
 
Amesema uongozi wa hospitali unashughulikia posho za wauguzi na pia 
kuboresha mazingira ya kazi ili wauguzi watoe huduma bora kwa wagonjwa.
“Pia uongozi wa muhimbili utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ili wafanye kazi wa ufanisi,” amesema Profesa Museru.
 
Awali mwakilishi wa wauguzi, Debora Bukuku alisoma risala ikielezea changamoto mbalimbali zikiwamo mazingira magumu na hatarishi ya kazi na pia kupitia risala hiyo waliomba wapatiwe posho za sare pamoja na kuboreshewa maslahi mengine.
 
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi amewataka madaktari na wauguzi kuendelea kuandika machapisho ambayo yanaeleza mafanikio na changamoto za utoaji huduma zilizopo katika hospitali hiyo.
 
“Bila kuandika machapisho, hakuna atakayeona mafanikio yetu. Hii ni hospitali ya Taifa ambayo inategemewa na hospitali nyingine kujifunza mambo mbalimbali. Hivyo nawapongeza wauguzi kwa kuandaa mada mbambali na kuziwasilisha kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani,” amesema Profesa Museru.
 
Katika kongamano hilo wauguzi na wataalamu wengine waliwasilisha mada mbalimbali kuhusu wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa na jinsi ya kuboresha huduma kwa wagonjwa wa kansa, figo na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa magonjwa ya dharura na ajali.
 
 Muuguzi Mkunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Philomen Kaongo katika kongamano hilo alizungumzia jinsi ya kuzuia na kutibu ugonjwa wa kansa.

ZIFF KUBORESHA SOKO LA FILAMU

$
0
0

Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mtaalam wa Habari na Masoko wa ZIFF, Bi. Lara Presdon na Meneja wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Daniel Nyalusi.
Mtaalam wa Habari na Masoko wa ZIFF, Bi. Lara Presdon akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Emerson’s Zanzibar Foundation, Said ELG akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo ya Filamu itakayotolewa na taasisi yake katika Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
Baadhi ya waamdishi wa habari wakifuatilia mkutano wa waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) leo jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija – MAELEZO

TAARIFA KUTOKA WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MAKATIBU MAHUSUSI MJINI DODOMA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa 5  wa Chama cha Makatibu Mahususi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Sehemu ya wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki leo kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Makatibu Mahsusi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na waache tabia ya kutoa siri za ofisi zao kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mji Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia pekee ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya kazi.

Makamu wa Rais pia amewahimiza makatibu mahsusi kufanya tathmini ya utendaji wao wa kazi na wawe tayari katika kujifunza mbinu mpya za utendaji zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.

“Sote tunafahamu kuwa dunia imekuwa ni kijiji kutokana na utandawazi unaoletwa na mifumo ya teknolojia hivyo kutokana na mabadiliko haya hamna budi nanyi kubadilika na kwenda na wakati ili msiangaliwe kwa mtazamo hasi wa kuwa wapiga cha tu”

Kuhusu uanzishwaji wa Shahada ya Uhazili, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia makatibu mahsusi kuwa Serikali imekubali kuanzisha shahada hiyo ambapo masomo yake yataanza mwezi wa Tisa mwaka huu kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam na Tabora.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza makatibu mahsusi kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu kwa kuzingatia kuwa elimu haina mwisho.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema Serikali inafanyia kazi baadhi ya kero zinazowakabili makatibu mahsusi ikiwemo kuboresha maslahi ya kada ya uhazili nchini.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kada hiyo pamoja na watumishi wengine wanapata maslahi bora ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi kazi.

TANZANIA MISS SUPER MODEL 2017 AKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA

$
0
0
Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akimkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Katikati ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa Miss Word Super Model, Asha Ally Mabula anayetarajia kushiriki mashindano hayo Macau nchini China.
Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza wakati wa tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarjia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo.
Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Word Super Model 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Kutoka kulia ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi na Meneja Mkuu wa Tanzania Miss Super Model Ibrahim Thabit.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

Mkutano Mkuu wa Vijana Kimataifa Kufanyika Arusha kwa Siku 7

$
0
0

Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.

AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi.

Bw. Tajiel Urioh alisema kuwa, Mkutano huo unaojulikana kama kongamano kubwa kabisa la vijana nchini linalowaleta pamoja vijana wadogo kutoka nchi mbalimbali tangu mwaka 1997. Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa utafanyika mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi wa Mei mwaka 2017, ambapo vijana takribani 200 kutoka katika nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kujadili masuala yanayohusiana na Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, Demokrasia na Amani katika nchi zinazoendelea, Kuhama kuelekea kwenye Nishati safi na ya teknolojia mbadala na Elimu kwa Maendeleo Endelevu.

Aliongeza kuwa majadiliano ya mwaka huu yatajikita katika mada kuu: “Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi”. Mada hii inalenga kuwezesha ushiriki wa vijana na kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Diplomasia na Uongozi kwa kuwapa mafunzo ya vitendo katika mada ngumu ambazo zitawaongezea ujuzi wa majadiliano na kufikia muafaka wa masuala mtambuka yanayogusa maslahi ya mataifa.

“Tunaishi katika ulimwengu ambao diplomasia yenye ujasiri na uongozi vinahitajika sana hivyo basi kuwakuza vijana katika uwanja huu itachangia kukua kwa mataifa yenye watu wenye uwezo wa kuamua mambo yao. Katika mkutano wa mwaka huu wajumbe watakuja na maazimio mbalimbali ambayo kwa namna moja hama nyingine yatakuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku na watu wanaowazunguka katika jamii zao,” alisema Bw. Urioh.
Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa katika mkutano huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.

“Ni matarajio yangu makubwa kwamba mtakuwa tayari kujifunza kuendana na mada kuu ya ‛ Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi′ lakini pia kubadilishana mawazo na wajumbe wengine na kutengeneza mtandao wa vijana wenye fikra mnazoendana nazo,” aliongeza Tajiel Urioh, Mratibu wa Kitaifa wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017.

Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo alisema kongamano kama hilo la vijana lina umuhimu mkubwa kwa vijana kwani huwajenga vijana kupitia Club za UN. Aliwataja miongoni mwa vijana ambao ni matunda ya Club za UN ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Benedict Kikove, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John John Mnyika na wengine wengi.

MAONESHO YA MPIRA WA MIGUU WA FREE STYLE KUANZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania ‘Free Style Football’ , Morison Jumanne (wakwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya maonesho ya kimataifa ya uchezaji wa mpira wa miguu  unaonza leo  katika maeneo mbalimbali ya wazi na mitaa jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania, Pascal Changa na kushoto ni Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda
 Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yake nchini Tanzania  ni kwa ajili ya maonesho ya wazi ya mchezo huo  Mkoa wa Dar es Salaam.
Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan, Kotaro Tokuda akionyesha umahiri wa mchezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


BENKI YA CRDB YAWAPA SEMINA WANAHISA WAKE, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha. Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
Meja kuu ikifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa wanahisa.
Muwasilisha Mada ya iliyohusu Mambo yananoathiri Thamani na Bei za Hisa katika Soko, Laurian Malauri kutoka Orbit Securities akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.












































Kampuni ya bia SBL, yazindua bia mpya ya Serengeti Premium Lite ya sh. 1500

$
0
0
Kampuni ya bia ya Serengeti Brewaries Ltd (SBL), imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari, wakati wa uzinduzi wa bia hiyo, mkurugenzi wa fedha na bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, amesema bia hiyo itakayokwenda kwa jina la Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa kutumia utaalamu wa kisasa.

Aidha bia hiyo ina ladha kamili ambayo burudani yake ni zaidi ya bia zote za aina ya Lite ambazo kwa sasa zipo sokoni.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa sh.1500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuiya ya wanywaji wake ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta  bia halisi ya kitanzania.

Ameongeza kuwa, Bia hiyo mpya haina sukari kwa hiyo itakuwa ni chaguo zuri kwa wale wote wasiotumia sukari."Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa muda mrefu"

"Tunaamini kuwa bia hii Ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremaster), wa kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapokuwa wakifurahia urithi wetu wa amina hii ya bia", amesema Mehta.

Ameongeza kuwa, bia hiyo ya Premium Lite ina ubora wa kimataifa sawa na bia mam ya Serengeti Premium Lager ambayo nimepokea zaidi ya medalist 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.
 Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL ,Kalpesh Mehta akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uzinduzi wa bia mpya ya Serengeti ya sh.1500 katika ukumbi wa Serena Leo jijini Dar es salaam,kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka kulia ni Anitha Lwehumbiza
Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka akizungumza na waandishi wa Habari juu ubora wa bia iliyozinduliwa ya Serengeti ya sh.1500 Leo jijini Dar es Salaam.

HAMMER Q KUSHTAKIWA ZANZIBAR

$
0
0
Na Salum Vuai, MAELEZO

WASANII Hammer Q na Mossi Suleiman, wameingia matatani baada ya kutajwa kwa wizi wa wimbo wa kikundi cha taarab Culture Musical Club cha Zanzibar.

Hali hiyo imejitokeza kufuatia wasanii hao kuimba na kurekodi wimbo uitwao ‘Ukewenza’ ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wakongwe Bi. Mwapombe Hiyari Mtoro na marehemu Bwana Sami Haji Dau tangu Culture ikiitwa Mila na Utamaduni.

Katibu wa Culture Musical Club Taimour Rukun Taha amesema uongozi wa klabu hiyo unakusudia kuwachukulia hatua za kisheria wasanii hao kwa kitendo chao cha kuimba na kurekodi wimbo huo ambao ni mali ya klabu yake bila ya idhini.

Akizungumza makao makuu ya klabu hiyo Vuga mjini Zanzibar, Rukun alisema, kitendo kilichofanywa na wasanii hao kinakwenda kinyume na sheria ya hakimiliki Zanzibar, Tanzania na ile ya kimataifa.

Aidha alisema, kwa mujibu wa katiba ya klabu yao, ni marufuku kwa mtu au kikundi chochote kutumia kibiashara wimbo uliotungwa, kutiwa muziki  na kuimbwa klabuni humo bila ya makubaliano kati ya pande hizo.

“Tumesikia na kushuhudia rekodi ya wimbo wetu wa ‘Ukewenza’ ambao asili yake uliimbwa kwa pamoja  na Bi. Mwapombe na marehemu Sami Haji Dau miaka mingi nyuma, ukiimbwa na Hammer Q na Mossi Suleiman. Ni wapi walikopata idhini kwani sisi wamiliki hawakuja kutuomba wala hakuna kati yetu aliyewaruhusu,” alifafanua Rukun.

Kimsingi, Katibu huyo alisema uongozi na wanachama wa klabu hiyo wanasikitishwa na kulaani kitendo chochote cha kurekodi na kuuza nyimbo za wasanii au vikundi vyengine mbali  na Culture, kufanywa na watu wengine bila ya makubaliano.

Alieleza kuwa mbali na kurekodiwa, pia wanakerwa na mtindo wa kuzibadilisha nyimbo hizo na kuongezewa vionjo ambavyo awali havikuwemo, ikiwemo vibwagizo vilivyopewa jina la ngoma chini jambo alilosema klabu yake haifanyi.

Alisema wapo baadhi ya wasanii ambao wanaendeleza mtindo  wa kuzipiga nyimbo za Culture katika shughuli mbalimbali na pia kuthubutu kuzirekodi na kuuza wakinufaika binafsi.

“Hii ni dhuluma kwani nyimbo hizo ni mali yetu na sisi ndio wenye hakimiliki na kama mtu anataka kuzitumia lazima afuate taratibu za kisheria,” alisisitiza.

Kwa hivyo, amewatumia salamu watu wote na vikundi vinavyojinufaisha kwa nyimbo za klabu hiyo, kujiandaa kukabiliana na mkono wa sheria, akisema wakati wa kuwafumbia macho umekwisha, kwani hata wanachama wanaumizwa na vitendo hivyo ambao kimsingi ndio wenye mali.

Katika siku za hivi karibuni, Hammer Q na Mossi Suleiman wamekuwa wakisikika na kuonekana kwenye mitandao ya kijamii wakiimba wimbo wa ‘Ukewenza’ ambao wengine huuita ‘Mke wa awali, wakitumia vyombo vya kisasa badala ya vile vya asili kama ulivyorekodiwa katika uasili wake.   

POLISI YAUA WANAODAIWA KUWA NI MAJAMBAZI JIJINI MWANZA.

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limepambana na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi ambapo katika mapambano hayo, wapo waliouawa.
Tazama video hapo chini

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MAY 20, 2017

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA JIMBO LA UBUNGO NA KIBAMBA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, katika Ukumbi wa CCM Manzese, wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama kwa kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo hilo la Ubungo jijini Dar esSalaam , jana. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akizungumza kutoa tathmini ya usalama wa kisiasa katika Wilaya yake mbele ya mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick  Mpogolo, aliyekuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, jana. 
 Msanii ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Makurumla, Shukuru Mbundi, akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara wakati wa mkutano wa kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo jana. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Mabalozi na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwatambulisha Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Mabalozi wa Kata ya Manzese na kuwapa majukumu baada ya kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi (kushoto) akisebeneka na baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Manzese wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara , Rodrick Mpogolo, jana. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Kibamba, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Hoja Kata ya Salanga, jijini Dar es Salaam, jana.
 Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Salanga Jimbo la Kibamba, wakiwa bize kutunza kumbukumbu ya elimu iliyokuwa ikitolewa kwao na Naibu Katibu Mkuu jana.
 Baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Salanga wakisimama na kuimba kumpongeza Naibu Katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Salanga, Euzedius Chilipwei, wakati akiwa katika ziarayake ya kuimarisha Chama Jimbo la KIbamba jana.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akijumuika na viongozi na wanachama wa CCM kufurahi kwa pamoja kucheza muziki baada ya kumaliza kuwahutubia katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwenye Jimbo la Kibamba Kata ya Salanga jana.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akijumuika na viongozi na wanachama wa CCM kufurahi kwa pamoja kucheza muziki baada ya kumaliza kuwahutubia katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwenye Jimbo la Kibamba Kata ya Salanga jana.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu  Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana.

Naibu Katibu akiondoka ukumbini
 Akiagana na baadhi ya viongozi

SBL YAZINDUA BIA MPYA IITWAYO SERENGETI PREMIUM LITE

$
0
0
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bia mpya aina ya Lite akitosti glasi na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kushoto) na mjumbe wa bodi ya SBL, Chris Gachuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ceaser Mloka,akizungumza katika uzinduzi huo.
 Maofisa kutoka SBL wakijadiliana jambo.
 Wakati wa utambulisho. Kushoto ni mbunifu wa bia hiyo.
 Wasanii wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

Mjumbe wa Bodi Chris Gachuma akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduz huo.
 Ni furaha tupu katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza.
 Muonekano ya bia hiyo katika chupa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha (wa pili kushoto), akitosti glasi na wanahabari katika uzinduzi huo.

 Crew nzima ya Kampuni ya PR ya Concept ikiwa katika uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa  ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa miaka 20 iliyopita. 

“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wakisasa. 

Ina ladha kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa rejareja sokoni”, alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko  na jumuia ya wanywaji wake ambaokwakipindikirefuwamekuwawakitafuta  biahalisiyakitanzania.

“Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa bia ya Serengeti Premium Lite, nisemekuwani bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi. 
Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa mudamrefu.

Tunaami ni kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishajibia (bremasters) wakitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapokuwa wakifurahia urithi wetu waaina hii ya bia  ”, alisema Mehta.

Aliongeza kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite inaubora uleule wa kimataifa sawa na biamama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10 za ubora wakitaifa na kimataifa.”

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe, aliisifia kampuniya SBL  kwa kuwa inaongoza kwa ubunifu katika sekta ya uzalishaji  wapombe nchini, na vilevile akaahidi kuwa serikali itaendelea kutoa msaada kwa sekta ya biashara hapa nchini.

Dk.Mwakyembe ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi, alisema SBL  imekuwa ikishiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania akitaja mafanikio mbalimbali za program zake za kuisaidijamii.

“Programu za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na     ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi, watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili ya kuuza mazao yao ambapo SBL  hununua mazao yao kama malighafi inayotumika kuzalishiabia”, alisema Makamba.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bia mpya aina ya Lite akitosti glasi na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kushoto) na mjumbe wa bodi ya SBL, Chris Gachuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.

YANGA WAKABIDHIWA KOMBE LAO MWANZA, MBAO YANUSURIKA KUSHUKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Ligi Kuu Tanzania Bara imemalizika leo kwa timu ya Yanga kutawazwa ubingwa wa msimu wa 2016/17 ikiwa ni  mara 27 toka ligi kuanzishwa.

Yanga waliokuwa ugenini dhidi ya Mbao iliweza kupoteza mechi hiyo ya mwisho lakini walitawazwa ubingwa kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Simba.

Katika mechi hiyo iliyoanza sa  10 Mbao waliandika goli lao la kwanza na la ushindi katika kipindi cha kwanza  ambapo liliweza kudumu mpaka dakika 90 kumalizika.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Ludovic Charles kutoka Tabora ilikuwa ya kukamiana kwa kila upande huku akionekana kushindwa kuuhimili mchezo huo.

Baada ya kumalizika kwa mechi nane za Ligi zilizochezwa kwa mda mmoja timu ya Toto Afrika ya Mwanza na African Lyon zimeshuka daraja zikiungana na JKT Ruvu iliyokuwa tayari imeshajikatia tiketi ya kurudi daraja la kwanza.
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Wakiwa wanashangilia baada ya kutawazwa mabingwa leo Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya tatu mfululilzo.
 wachezaji nwa Yanga wakipokea medali zao za ubingwa baada ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya 27 na mara ya tatu mfululizo.
Kikosi cha Mbao kilichocheza dhidi ya Yanga leo katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
            Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mbaoleo katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mwali kabla ya kukabidhiwa.

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA KAMPENI YA MIMI NA WEWE MJINI UNGUJA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Unguja – Zanzibar akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua ya kampeni maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.

Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu wasiojiweza katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.

Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa Vyama vya siasa.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Mjini Magharibi,Borafya Silima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. #Picha na Adam H. Mzee/ VPO

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF.  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.  Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF.  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini.
Wagonjwa wakitumia mashuka na vitanda vilivyotolewa na PPF. --- Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. 

Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. 

Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. 

Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. 

Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.

Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wafikia tamati

$
0
0
Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ulikuwa na ujumbe na uwakilishi kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. . 

Rais Mhe. Dkt. Magufuli akizungumza katika Mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya. 

Aidha mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mhe. Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kunakila sababu ya kulinda na kudumisha Mtangamano kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama. 

Pia Mkutano huu wa 18 wa Wakuu wa nchi umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Eng. Steven Mrote kutoka Tanzania. Katika Kutano huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi rasmi uwenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni. 
Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia hadhira iliyohudhuria Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini moja ya nyaraka ya makabidhiano ya uwenyekiti wakati wa Mkutano wa 18 wa Kaiwa wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wakwanza kulia) akifuatilia Mkutano. Wengine ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (katika) na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Aziz P. Mlima (kulia) akifuatilia Mkutano 
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Charles Oyo Nyawezo kutoka Sudan Kusini kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Eng.Steven Mrote kutoka Tanzania kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa kitado cha nne aliyejishindia nafasi ya nne katika mashindano ya uandishi wa insha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Tanzania Bw.Joseph Mbogo 
Waziri Mhe. Mahiga akifuatilia Mkutano 
Picha ya pamoja

Rais Dkt. Magufuli akabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais Museveni wa Uganda

$
0
0


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kukalia kiti cha Uenyekiti alipomkabidhi wadhifa huo leo wakati wa Mkutano wa 18 wa Kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017(Picha na IKULU)
mem1
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpongeza Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Dkt.Augustine Mahiga pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe Ali Siwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem2
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufulna  Naibu Rais wa kenya Mhe. William Ruto wakiongea na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem3
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpongeza Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Dkt.Augustine Mahiga pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe Ali Siwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem4
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Naibu Rais wa kenya Mhe. William Ruto wakisalimiana  na wanafunzi wa shule za sekondari za nchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya Insha baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem5
Meza kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari za nchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya Insha baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem6
Meza kuu katika picha ya pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem7
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Naibu Rais wa kenya Mhe. William Ruto na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem8
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe baada ya kumalizika kwa mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem9
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe baada ya kumalizika kwa mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2017
mem10
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu Mstaafu Mzee Edwin Mtei aliyekuwa mmoja wa wageni mashuhuri walioalikwa kushuhudia akimmkabidhi Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 18 wa kawaida wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leoMei 20, 2017
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>