Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 122 | 123 | (Page 124) | 125 | 126 | .... | 1896 | newer

  0 0  0 0


  Good Morning People,

  2013 Kenya is celebrates fifty years since the first day that Kenya attained internal self-rule. Tulipata full independence from Britain on 12 December 1963.

  To me this is the most important year in our life time sabu we don't know if we will ever see another 50 Years. Morale ya Maisha niko nayo na nafurahia. Jubilee ya Kenya 50years this year with a brand new single Nonini ft Chris Adwar-Kenya produced by Musyoka of Decimal Media.


  NB: For the first time i have opened up a little bit into my private life which is totally worth it. I have my Wife and Son who are a blessing to me on the song lyrics and music video. ENJOY!!!

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini leo Julai 19, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Majaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai, 19, 2013 baada ya kuhani msiba huo wa Jaji mstaafu Buxton Chipeta.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013 kwa ajili ya kuhani na kuaga msiba huo.
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo leo.Picha na OMR

  0 0
 • 07/19/13--13:12: Article 11

 •  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akitoa zawadi ya Mashine moja ya kutolea kopi, Kompyuta Mpakato (Laptop) moja, jezi na mipira 22 jana kwa Wanakikundi cha Mambo Safi  jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.


   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akisoma Kitabu cha Kikundi cha Mambo Safi jana jijini Dar es Salaam kinachoelezea kazi mbalimbali zifanyazwo na Kikundi, kulia ni Katibu Msimamizi wa Kikundi hicho Bi. Anna Ludovick.

  Wanamichezo wa Kikundi cha Mambo Safi katika Kata ya Kimara jijini Dar es Saalam wakicheza ngoma ya kitamaduni jana mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Said Bakari  Jecha  kuwa Mwenyeki wa Baraza la  Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

  Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 9(1)cha Sheria ya chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Namba 8 ya mwaka 1999.

   Aidha Dkt Shein amemteua Abdulrahman Rashid kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)
  Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu  wa  uwezo  alipewa chini ya kifungu  Namba  8 (a) (1) cha  sheria  ya  Bodi  ya  Mapato  Zaznzibar (ZRB)  Namba 7 ya mwaka 1996 kama  ilivyorekebishwa  na Sheria Namba 8 ya 2009.

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Dkt.Abdulhamid  Yahya Mzee ,Uteuzi wa Said Bakar Jecha unaanzaa  Julai 20,na uteuzi wa Abdulrahman Rashid  unaaza Julai 18 mwaka huu.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 19/07/2013


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya mapema leo tarehe 19 Julai 2013, baada ya mwenge huo kumaliza ziara yake Mkoani Katavi na kuanza ziara ya siku nne Mkoani Rukwa.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Challa B leo tarehe 19 Julai 2013. Mwenge wa Uhuru umeanza ziara yake ya siku nne Mkoani Rukwa kwa kuanzia na Wilaya ya Nkasi na kuendelea Kalambo na Sumbawanga. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na viongozi wengine pamoja na watumishi wa serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru uliowasili Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani Katavi. Ujumbe wa mwenge mwaka huu ni "Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali".
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na viongozi wengine pamoja na watumishi wa serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru uliowasili Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani Katavi.
   
  Baadhi ya watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0
 • 07/19/13--13:37: CALL FOR INTERVIEW.
 • THE UNITED REPUBLIC OF TANANIA

  MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE


  CALL FOR INTERVIEW.


  Ministry of Health and Social Welfare is hereby announcing the names of applicants who have been selected to appear for an interview for the post of laboratory technologist. The interview will be conducted at National Blood Transfusion Services (NTBS) head office at Ilala-Mchikichini opposite Msimbazi Centre on 27thJuly, 2013 starting from 9.00 am.


  The interviewees should appear with all Academic and professional credentials (original certificates). The cost regarding to travel, accommodation and meals should be incurred by the candidates themselves.
  S/NO

  NAME

  SEX

  TELEPHONE NUMBER

  1

  MAYALLA WILLIAM

  M

  TEL 0712 063564/ 0786 015066

  2

  MATHAYO MBUYA

  M

  TEL 0768 229280/ 0656 264844

  3

  HASSAN O. MBEGA

  M

  TEL 0756 877175/ 0787 877175

  4

  DAVID ENOCK

  M

  TEL 0762 742232

  5

  TOGOLANI G. MAYA

  F

  TEL 0714 640074

  6

  SUZANA D. MBOTO

  F

  TEL 0787 576771

  7

  SHABANI R. MZIRAY

  M

  TEL 0754 942946/ 0713 992143

  8

  HUSSEIN ATHUMAN

  M

  TEL 0655 866606


  ACTING PERMANENT SECRETARY

  MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE

  P.O.BOX 9083


  DAR ES SALAAM


  0 0

    Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wekiwemo Maofisa vijana waliohudhuria Semina. Katikati ni nWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, anayemfuatia  Kulia kwake ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Seth Kamuhanda na Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Profesa Ole Sante Gabriel, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo na Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili ya kuwajengea Maofisa Vijana uwezo zaidi wa kumudu shughuli za kimaendeleo iliyoanza jana 18/7/2013 na inatarajiwa kumalizika leo 19/7/2013 jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Seth Kamuhanda akitoa maelezo machache ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe,  Dkt. Fenella Mukangara kwa ajili ya kufungua rasmi Semina hiyo ya siku mbili jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya washiriki wa Semina ya Maofisa Habari iliyozinduliwa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe,  Dkt. Fenella Mukangara wakisikiliza hotuba ya Waziri jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar 

   Zaidi ya watoto 1,553 wamegundulika wakiishi katika mazingira magumu kati ya hao watoto 398 walikuwa tayari wameshajiingiza katika ajira za watoto.

  Hayo yamesemwa  leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Mbweni na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman wakati alipokuwa akisoma  Hotuba  ya Bajeti ya  Wizara hiyo huko katika  Baraza la Wawakilishi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

  Amesema watoto hao walibainika wakiishi katika mazingira magumu na kujiingiza katika ajira zisizo rasmi baada ya wizara hiyo kufanya uchunguzi kupitia serikali za mitaa.
    
  Amesema watoto hao wanaume walikuwa 1,014 na 539 ni wanawake ambao kati ya hao watoto 381 wamefanikiwa kurejeshwa skuli na kupatiwa vifaa vya kujisomea.

  Aidha alisema kuwa katika hali hiyo pia walifanikiwa kuwawezesha  wazee walio kuwa katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kuanzisha shughuli za kiuchumi, zikiwemo biashara na ufugaji.

  “Hii ni awamu ya kwanza ya Mradi kuwasaidia watoto na wazee wenye mazingira magumu ambao umegharamiwa na Jumuiya ya Ulaya kupitia save the children  na utekelezaji wa mradi huu unahusisha Wizara zinazoshughulikia masuala ya Kazi,  Elimu, Ustawi wa Jamii pamoja na Taasisi za Kiraiya”alisema Haroun.

  Waziri alifahamisha kuwa katika awamu ya pili ya mradi huo umelenga kushughulikia tatizo la ajira za watoto katika shehia mbali mbali za Unguja na Pemba. Sambamba na hayo waziri huyo alieleza malengo yake kwa wizara hiyo mwaka ujao ni kuongeza upatikanaji wa fursa za ajira kwa wanawake na wanaume hususani vijana.

  Mengine ni kuengeza kutanua mipango ya uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na kuimarisha utekelezaji wa sheria za kazi,na kuimarisha uhusiano kazini na utekelezaji wa viwango vya kazi.

  Aidha alisema wataimarisha utekelezaji wa sheria namba nane ya mwaka 2005 juu ya usalama na Afya kazini pamoja na kuratibu na kusimamia uundaji,tathmini ya utekelezaji wa Sera na Mipango ya Wizara.  

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) akifungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi wa Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


  “TAASSISI ZA UMMA ZITUMIE FURSA KULETA KASI YA MAENDELEO” KOMBANI/


  Na James Katubuka.


  Uwajibikaji katika Taasisi za Umma nchini ndiyo njia pekee itakayowezesha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano  (FYDP) 2011/12-2015/16, sanjari na Malengo ya Milenia (MDGs) . Kwa kuzingatia hiloSerikali inaendelea kuhakikisha mazingira ya kazi yanaboreshwa ili watumishi wawe na kasi zaidi kama sehemu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa kutoa huduma bora kwa Umma.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) amesema hayo hivi karibuni wakati akifungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano jijini Dar es Salaam.


  “Kutokana na kuthaminiwa kwa mchango wa watumishi wa umma katika kuleta maendeleo Serikali nyingi ikiwepo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimewekeza katika kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma ili waweze kuwajibika ipasavyo” Mh. Kombani alisema.


  Aliongeza kuwa ubora wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa umma ni suala muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yoyote, hivyo Tanzaniakwa kuwekeza katika rasilimali hiyo itapiga kasi zaidi ya kimaendeleo.


  “Mimi ni miongoni mwa wanaoamini kwamba utendaji mzuri au mbaya wa Serikali unahusishwa moja kwa moja na kiwango cha huduma zitolewazo na Serikali kwa umma kupitia taasisi zake” Mh. Kombani alitoa angalizo.


  Aidha,alisema ukiilinganisha Tanzania na nchi za Barani Asia na Amerika ya Kusini ambazo tuna historia zinazoshabihiana, inaonekana kuwa zimepiga hatua ingawa mbinu zilizotumika toka nchi hizo zinakaribiana, hivyo  kutokana na uhalisia huo Serikali imefanya jitihada  za kuboresha na kufikiri upya namna ya kufikia malengo ya maendeleo haraka husani  mchango wa Utumishi wa Umma.


  Mh. Kombani alisema kwamba uwajibikaji wa watumishi wa Umma nchini ni chachu ya kufikia malengo ya Kitaifa ya Milenia mwaka 2025, ikizingatiwa kuwa malengo hayo yamejikita katika kuleta hali bora zaidi kwa maisha ya wananchi, utawala bora, amani ,umoja na mshikamano na kujenga uchumi imara.


  Katika kuchangia hilo,  Mtendaji MkuuMsaidizi wa Tume ya Mipango nchini Bw. Florence Mwanri alisema mpango huo uliozinduliwa  na Serikali mwaka 2011 kwa lengo la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Milenia wa mwaka 2025, umetoa vipaumbele ambavyo ni kuimarisha Miundombinu, Kilimo, Uvuvi na Misitu, Kuboresha Elimu, na kuendeleza Sekta ya  Utalii, Biashara na Uchumi.


  Hata hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Dkt. Martern Lumbanga akitoa mchango wake alisema ili kutekeleza mpango huo ipasavyo ni vizuri kujifunza kutoka kwa nchi nyingine ambazo miaka thelathini iliyopita zilikuwa sawa na Tanzania kimaendeleo. Dtk. Lumbaga aliainisha nchi hizo ni kama vile Jamhuri ya watu wa China,   Korea ya Kusini, Vietnam, Cambodia, Botswana na Ghana.

  “Utawala wa Kisiasa wa nchi hizi uliweza kuziunganisha Sekta za Umma na Sekta binafsi kutumia Rasilimali muhimu katika kubuni mbinu mbalimbali za kuwavutia wawekezaji wa nje kuwekeza katika sekta nyeti za uchumi zilizoimarisha pato kwa kiwango cha juu” Dkt. Lumbaga alisema.


  Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Dkt. Lumbanga alisisitiza kwamba Sekta za Umma zinatakiwa kuwa chombo cha kubuni na kuwezesha maendeleo kwa mifumo ya kiufundi, kwa kuzingatia maadili ya kiutawala ili kujenga imani kwa umma na kuhakikisha mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP) unaratibiwa kikamilifu.


  Mkuu huyo wa Utumishi mstaafu alisisitiza kuwa sekta ya umma nchini inatakiwa kuwajengea uwezo Watumishi wake ili wawajibike ipasavyo, kuwa na mawasiliano ya kiutendaji yaliyo hai muda wote na kutambua kwamba Utumishi wa Umma upo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.


  Naye Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Bw. Phillemon Luhanjo akizungumzia kuhusu changamoto zinazoukabili Utumishi wa Umma na mtazamo wa Sekta binafsi dhidi ya Utumishi wa Umma nchini, alisema moja ya changamoto ni  dhana ya kukubali kubadili fikra na kuleta  fikra endelevu zitakazokuwa chachu ya maendeleo nchini katika nyanja za Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni.

  “Sekta binafsi zinatakiwa kushirikishwa katika kuandaa mipango yetu ya maendeleo” Bw. Luhanjo alisema.


  Alifafanua kuwa kwa upande wa sekta binafsi zinatakiwa kupewa fursa ya kuchangia mawazo endelevu ili mpango wa maendeleo uwe wenye manufaa.

  Bw. Luhanjo aliainisha kuwa Taasisi za umma zinatakiwa kufikiri juu ya mahitaji ya wananchi hususani suala la umasikini na kusisitiza Utumishi wa Umma lengo lake si kujilimbikizia mali, bali lengo kuu ni kutekeleza malengo madhubuti ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi.


  Alisema ili kukabiliana na changamoto zilizopo Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma  unaendelea kuimarika, mahusiano na Sekta binafsi yanaimarishwa zaidi, bajeti ya nchi iimarishwe ili kupunguza utegemezi wa wafadhili wa nje na Sekta ya Umma kutambua mchango wa Sekta binafsi katika kuleta kasi zaidi ya maendeleo.


  Pamoja na hayo, Katibu Mkuu mstaafu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Joseph A. Rugumyamheto akizungumzia kuhusu ushirikishwaji na wajibu wa Utumishi wa Umma  katika kuleta maendeleo nchini  alisema jukumu la Utumishi wa Umma katika kuleta maendeleo ya kitaifa limekuwepo toka kipindi cha uhuru mpaka sasa.


  Bw. Rugumyamheto alisisitiza Utumishi wa Umma ndio chombo pekee chenye jukumu kubwa la kuwezesha uratibu wa programu za maendeleo za kijamii na kiuchumi hapa nchini.


  Katibu Mkuu mstaafu alisema wachambuzi wa masuala mbalimbali wameandika kuwa Utumishi wa Umma katika kipindi cha Uhuru ulikuwa unazingatia taaluma na ulikuwa ni chombo kilichowajibika kikamilifu kutimiza matakwa ya Kisiasa na Kijamii. Hivyo, kwa sasa kasi iongezeke zaidi.


  Bw. Rugumyamheto aliainisha kuwa kwa sasa Utumishi wa Umma una wigo mkubwa wa uwepo wa wataalamu wengi wenye ujuzi katika fani mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali, pia matumizi ya teknolojia hususani maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamerahisisha uandaaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusimamia utekelezaji wake, hivyo Utumishi wa Umma uliopo una nafasi kubwa ya kuwahudumia wananchi ipasavyo na kufikia malengo kwa haraka. 


  Akizungumzia kuhusu hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Vijana nchini Nigeria Dkt. Tunji Olaopa  alisema kinachohitajika ni kuwa na mpango  utakaoiwezesha kuondokana na dhana ya utendaji wa mazoea na kutoka katika fikra ya utamaduni wa kitawala wa kirasimu na kujikita katika mfumo wa ujasiriamali ikiwamo  ubunifu katika kushughulikia masuala ya mishahara na masilahi ya watumishi ili kuwajengea morali na uwajibikaji kwa umma.


  “Utawala makini na uliojitolea kuutumikia umma ndio nguzo ya maendeleo, na ikumbukwe kwamba Utumishi wa Umma ukishindwa kuwajibika ipasavyo na masuala yote yahusuyo maendeleo yanakwama” Dkt. Olaopa alisema. Aidha, Dkt. Olaopa aliipongeza Tanzaniakuwa ni miongoni mwa nchi zenye sifa ya kuwa na utawala bora unaoheshimika Barani Afrika.

  Mtafiri Adamolekun katika tafiti yake ya mwaka 2005 aliyoitoa mwaka 2009 kuhusu masuala ya Utawala Barani Afrika imeainisha kuwa Tanzaniani moja kati ya nchi zilizofanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Umma. Utafiti huo ulihusisha nchi nyingine kama Benin, Burkina Faso, Ethiopia, Ghana, Kenya, mali na Senegal.


  Akichangia mada, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Rwekaza Mkandala alisema Rasilimaliwatu ni msingi wa maendeleo,hivyo ni lazima nchi kuwa na Watumishi wa Umma waliopewa mafunzo bora na ujuzi unaokidhi mahitaji.


  Prof.Rwekaza alisema kuwa Watumishi wa Umma wanatakiwa kuwa na uzalendo na nchi yao na wasiohitaji kusimamiwa ili kutekeleza majukumu yao.

  Alisema “ili Utumishi wa Umma ufanikiwe unahitaji kwenda sambamba na Teknolojia kulingana na mazingira halisi yaliyopo na muda husika, pia unahitaji kuwa na vitendea kazi mahimu kufanikisha hilo ikiwamo mifumo ya kompyuta itakayoiwezesha mifumo mbalimbali niliyobuniwa na Serikali kufanya kazi ipasavyo”.


  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejjimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu alisema Serikali imeainisha maeneo matano ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ambayo ni kilimo, elimu, nishati, miundombinu na rasilimali na hivi sasa kuna chombo kitakachosimamia na kutathmini mipango itakavyotekelezwa, chombo hicho kinaitwa Presidential Delivery Bureau.

  (Mwandishi WA makala hii ni Afisa Habari, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma).  0 0


  Baada ya kuwepo hewani tangia mwaka 2007, blog ya Kamerayangu kubadilika karibuni na kuitwa kamerayangu.com. Pamoja na habari mbali mbali pia itakuwa inawapatia kazi mbali mbali ambazo zinafanywa na blog hii ikiwa pamoja na kutambulishwa kwa Online TV.  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika nyakati tofauti  ikulu jijini Dar es Salaam
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao

  0 0
 • 07/20/13--03:58: FAIDA ZA GESI ASILIA.
 •  Kamishina wa Nishati na Masuala ya Petroli toka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Hosea Mbise akizungumza na waandishi wa habari kuhusu faida zitokanazo na gesi asilia, kushoto ni  Mhandisi Seleman Khatib anayehusika na Nishati na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya habari Zamaradi Kawawa akifuatiwa na Kaimu mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Wizara ya Nishati na Madini Veronica Simba PICHA NA ELIPHACE MARWA (MAELEZO).

  FAIDA ZITOKANAZO NA GESI ASILIA NCHINI

  Utafiti wa mafuta na gesi nchini ulianza tangu mwaka 1952 chini ya kampuni za BP na Shell. Hadi sasa kampuni zipatazo 19 zinaendelea na utafiti katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo maeneo ya kina kirefu cha maji baharini, mwambao wa bahari, na katika bonde la ufa.


  Kiasi cha Gesi Asilia iliyogunduliwa nchini Tanzania, inakadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni 41.7, kati ya hizo, zaidi ya futi za ujazo trilioni 33 zimegunduliwa katika kina kirefu cha maji baharini. Uhakiki wa gesi hii pamoja na utafiti unaendelea na mategemeo makubwa ni kuendelea kugundua gesi zaidi na pia hata mafuta.


  Kawaida, Gesi Asilia inaweza kutumika kama nishati (energy) na vile vile inatumika kama malighafi (feedstock) katika baadhi ya viwanda (Gesi asilia inatumika kutengeneza Mbolea, Plastics, Methanol pamoja na kemikali nyingine nyingi) na pia ya kuuzwa nje ya nchi kama bidhaa (export commodity).


  1.1.    Faida zilizopatikana kutokana na Gesi Asilia Nchini

  Faida halisi zilizopatikana kutokana na matumizi ya Gesi Asilia nchini ni ni pamoja na zifuatazo:


  Sekta ya umeme

  Sekta ya umeme ilianza kutumia Gesi Asilia tangu mwezi Julai, 2004,  hadi sasa kiasi cha megawati (MW) 418.5 huzalishwa nchini kwa kutumia nishati hiyo. Takriban Dola za Marekani Bilioni 4.4, sawa na Shilingi za Tanzania Trilioni 7, zimeokolewa kwa kutumia gesi asilia kufua umeme kuanzia Julai 2004 mpaka Machi 2013.


  Sekta ya Viwanda.


  Gesi Asilia inatumika katika viwanda 37 vilivyopo Dar es Salaam. Takwimu zinaonyesha kuwa, viwanda 37 vinavyotumia Gesi Asilia, vimepunguza gharama za nishati kwa kiasi cha zaidi ya Dola za Marekani Milioni 400, sawa na shilingi bilioni 640, ikilinganishwa na kama vingetumia mafuta katika kuendesha mitambo yao kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2004 hadi Disemba, 2012.


  Sekta ya Usafiri

  Hadi sasa, magari 40 yamewekewa mfumo wa kutumia gesi asilia. Mfumo huu unatumika sambamba na mfumo wa mafuta ya petroli uliopo kwenye magari. Kwa kipindi cha kuanzia Mei, 2011 hadi Machi, 2013 magari hayo yametumia gesi yenye thamani ya Shilingi milioni 22.88. Kwa kipindi sawa na hicho, magari hayo yangetumia mafuta ya petroli yenye thamani ya shilingi milioni 46.2. Hivyo, fedha iliyookolewa kwa magari 40 kutumia gesi asilia badala ya mafuta ya petroli kwa kipindi hicho ni shilingi milioni 23.32.


  Mapato Serikalini.


  Kuanzia Julai, 2004 hadi Machi, 2013, Serikali iliweza kukusanya jumla ya Dola za Marekani milioni 201.2, sawa na shilingi bilioni 321.9 kutokana na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na mauzo ya gesi asilia.

  Mapato kwa Halmashauri za Kilwa (Lindi) na Mtwara Vijijini (Mtwara)

  Sheria inazitaka kampuni zinazozalisha na kuuza Gesi Asilia kulipa Kodi ya Huduma (Service Levy), ambayo ni asilimia 0.3 ya mauzo ya Gesi Asilia. Fedha hizi hulipwa kila baada ya uzalishaji wa kipindi cha miezi mitatu (robo mwaka). Halmashauri zinazofaidika na mapato hayo ni Kilwa (Lindi) kutokana na mradi wa Songo Songo na Mtwara Vijijini (Mtwara) kutoka mradi wa Mnazi Bay.


  Kuanzia kipindi cha mwezi Julai, 2004 mpaka Disemba, 2012, jumla ya kiasi cha shilingi milioni 885 zimelipwa kwa Halmashauri ya Kilwa kama kodi ya huduma (service levy), kwa wastani wa takribani shilingi milioni 109 kila baada ya miezi mitatu.


  Kwa upande wa mradi wa Mnazi Bay, Halmashauri ya Mtwara Vijijini hupata wastani wa shilingi milioni 16 kila mwaka. Kiasi hiki ni kidogo sana kutokana na uzalishaji na uuzaji mdogo wa gesi ingawa visima vilivyopo Mnazi Bay vina uwezo wa kuzalisha gesi nyingi zaidi. 

  Kufuatia hazina kubwa ya gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha maji baharini, Serikali pamoja na kampuni zilizowekeza kwenye utafutaji zimeamua kuwekeza katika uzalishaji mkubwa wa Gesi Asilia ili kuleta tija zaidi kwa Taifa na watu wake.

  Aidha, miradi yote ya gesi kama nishati, viwanda, mitambo ya kufua umeme pamoja na viwanda vya petrochemicals, kwa kiasi kikubwa vinategemea kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi Bay (Mtwara) na Songo Songo (Lindi) hadi Dar es Salaam.


   IMETOLEWA NA:


  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  19 JULAI, 2013  .


  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akitoa vyeti kwa Wahitimu wa mpira wa Goal wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi kutoka Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zanaki Bi. Rehema Tunzu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo. 
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akijiandaa kupiga mpira aliopasiwa toka kwa  kocha wa mpira wa Goal (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative uliofanyika shule ya Sekondari ya Zanaki jana jijini Dar es Salaam. 
   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zanaki Bi. Rehema Tunzu akituliza mpira aliopasiwa toka kwa kocha wa mpira wa Goal Initiative (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd ufunguzi huo ulifanyika jana shule ya Sekondari Zanaki jana jijini Dar es Salaam. 
   Mkufunzi wa mchezo wa Goal Bwana Brian Suskiewile akitoa maelekezo kwa Washiriki (hawapo pichani) jinsi ya kutumia mpira wa Goal wakati wa ufunguzi wa mchezo huo jana jijini Dar es Salaam katika shule ya Sekondari ya Zanaki, kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa mafunzo ya mpango wa mchezo wa Goal Initiative. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd. Ufunguzi huo ulifanyika jana katika shule ya Sekondari ya Zanaki iliyoko jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Prof. Ibrahim Lipumba, wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Gen Mstaafu wa Jeshi, George M. Waitara (Rtd) wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Dkt. Regnald Abraham Mengi, wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.


  0 0

   
   Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jovin Kitambi akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu ziara ya tume hiyo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa za mikoa ya Pwani na Dar es Salaam pamoja na wakala 37 za Serikali, kushoto ni Katibu wa tume hiyo Bi. Claudia Mpangala na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya habari Zamaradi Kawawa. 
   Naibu Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi wa Walimu Edwin Mikongoti akijibu swali toka kwa waandishi wa habari kuhusu  ziara ya tume hiyo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa za mikoa ya Pwani na Dar es Salaam pamoja na wakala 37 za Serikali. 
  Katibu Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya tume hiyo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa za mikoa ya Pwani na Dar es Salaam pamoja na wakala 37 za Serikali.


  PICHA NA ELIPHACE MARWA (MAELEZO)-


  ===========  00000000000   ==========

  ZIARA YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA KATIKA SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZA MIKOA YA PWANI NA DAR ES SALAAM PAMOJA NA WAKALA 37 ZA SERIKALI


  Tume ya Utumishi wa Umma ni matokeo ya maboresho mbalimbali yaliyoanzishwa na Serikali kwa lengo la kuufanya Utumishi wa Umma uongeze ufanisi, utoe matokeo yenye tija na uwajibikaji wa utoaji huduma bora kwa wananchi. Kufuatia marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, Tume ya Utumishi wa Umma ni rekebu yenye jukumu la kusimamia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazohusu rasilimali watu katika Utumishi wa Umma.


  Ili kutekeleza jukumu la urekebu Tume inatoa Miongozo, inaweka viwango vya uzingatiaji, inawezesha na kuelimisha waajiri juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma, inafanya ukaguzi kwa Mamlaka zinazosimamia rasilimali watu katika Utumishi wa Umma. Pamoja na jukumu hili la urekebu, Tume ni Mamlaka ya Rufaa kwa watumishi wote wa Umma isipokuwa watumishi waliopo kwenye masharti ya kawaida (Operational Services) na wale wanaoteuliwa na Mheshimiwa Rais.


  Aidha, Idara ya Utumishi wa Walimu ya Tume ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu ya Walimu wote katika Utumishi wa Umma. Idara hii inashughulikia masuala ya Walimu ya usajili, upandishwaji vyeo, kuwathibitisha kazini na mashauri ya nidhamu.


  Ni wajibu wa Tume kuhakikisha kuwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu zinashughulikia masuala yote yanayohusu rasilimali watu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unakuwa mmoja na watumishi wote wana taratibu za usimamizi, hadhi na haki zinazofanana.


  Ili kuhakikisha kuwa Waajiri wanazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa rasilimali watu, Tume hufanya ukaguzi kuangalia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika usimamizi wa rasilimali watu katika Utumishi wa Umma na hufanya ziara kwa taasisi mbalimbali za umma kwa lengo la kujitangaza kwa wadau wake, kuelezea  majukumu ya Tume na utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na marekebisho yake yanayohusu uendeshaji na usimamizi wa Utumishi wa Umma.  Hivi karibuni, Mwenyekiti, Makamishna na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma, walifanya ziara katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mikoa ya Pwani na Dar es salaam pamoja na Wakala 37 za Serikali, katika ziara hizo kulikuwa na  fursa ya kufanya majadiliano  kati ya Tume ya Utumishi wa Umma, Menejimenti na Watumishi wa Taasisi hizo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa rasilimali watu. Aidha, katika kipindi hicho Tume ilifanya ukaguzi kwa Taasisi 42 kuangalia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika maeneo ya ajira, upandishwaji vyeo, nidhamu, OPRAS na likizo za watumishi.  

  Kufuatia ukaguzi na ziara hizo changamoto zifuatazo zilijitokeza katika usimamizi wa rasilimali watu katika Utumishi wa Umma;-

  i)      Baadhi ya Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu hazizingatii Sheria ipasavyo katika kushughulikia usimamizi wa masuala ya rasilimali watu katika maeneo yafuatayo.

  ●  Usimamizi hafifu  katika Upimaji wa Wazi wa Utendaji kazi kwa watumishi (OPRAS).

  ● Watumishi kuchelewa kupandishwa vyeo kwa wakati pamoja na kuthibitishwa kazini.

  Mashauri ya nidhamu yanaendeshwa bila kufuata taratibu zilizowekwa kwa mfano, Mamlaka za Nidhamu kutochukua hatua pale mtumishi anapothibitika kufanya makosa.

  ● Baadhi ya waajiri kutokiri kupokea na kujibu barua au hawajibu kabisa barua au kutoa mrejesho.

  ii)      Baadhi ya Mamlaka na Wakala za Serikali kukabiliwa na upungufu wa rasilimali watu na rasilimali fedha na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

  iii)     Utunzaji usioridhisha wa kumbukumbu za watumishi.

  Ili kukabiliana na changamoto ambazo zimejitokeza, Tume inawasisitiza Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu na Watumishi wa Umma kutekeleza yafuatayo;-

  i)      Watumishi wanapaswa kuelewa kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Hivyo ni lazima wabadilike, wasifanye kazi kwa mazoea, wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria.

  ii)      Mamlaka za Ajira na Nidhamu na Watumishi wanapaswa  kuhakikisha kwamba wakati wote wanatimiza wajibu wao wa kushughulikia masuala ya kiutumishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ili kuboresha utendaji wao wa kazi na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi.

  iii)     Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu wachukue hatua kwa wakati dhidi ya ukiukwaji wa Sheria mara inapobainika na kushughulikia mapema madai mbalimbali ya watumishi.

  iv)     Waajiri watekeleze Upimaji wa Wazi wa Utendaji Kazi kwa watumishi wao (OPRAS), kikamilifu kwa mujibu wa Mfumo wa upimaji utendaji kazi, kwa mfano kufanya Mapitio ya nusu mwaka na kufanya tathmini ya mwaka, ili kufikia azma ya Serikali inayotaka Utumishi wa Umma utoe matokeo yenye tija na huduma bora inayotarajiwa na wananchi.  OPRAS inasaidia watumishi wa Umma kufanya  kazi kwa malengo yaliyowekwa na yenye kupimika.


  v)     Waajiri wazingatie kukusanya na kutunza takwimu za kiutumishi ili kuwezesha kupanga mipango ya maendeleo na matumizi ya rasilimali watu.


  vi)     Waajiri wajenge tabia ya kukiri na kujibu barua kwa wakati, vile vile wajali haki za msingi za watumishi ili kuepuka malalamiko (grievances) yasiyo ya lazima mahali pa kazi. Wanapaswa pia, kuanzisha dawati la kushughulikia malalamiko ya watumishi.


  vii)    Watendaji wa Mamlaka na Wakala za Serikali wanapaswa kuelewa lengo la Serikali la kuwafanya wajitegemee ni kuwafanya waweze kujiendesha bila kuitegemea Serikali, hivyo wanatakiwa kuwa wabunifu na wafanye kazi kwa bidii na uadilifu.


  Ni matarajio ya Tume kuona Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu zinatekeleza maagizo ya Tume yanayotolewa kwa wakati na kutoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo. Aidha, wazingatie Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika kushughulikia mashauri ya nidhamu ili haki iweze kutendeka.

  Mwisho, Tume inawasisitiza Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu kwamba rasilimali watu ni lazima ipewe kipaumbele katika utendaji wa majukumu yao. Rasilimali watu ndio inayowezesha rasilimali nyingine zitumike vizuri ili kuleta maendeleo kwa kila Taifa Duniani.  Imetolewa na:  Jovin B. Kitambi

  Mwenyekiti

  Tume ya Utumishi wa Umma

  19/07/2013
  0 0

   Afisa Habari Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Germanus Kyafula(kushoto)akieleza kwa vyombo vya habari nchini kuhusu mfumo mpya wa kupokea malalamiko kwa njia ya ujumbe wa simu ya kiganjani katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es salaam, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa Wilfred Warioba. 
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini taarifa inayotolewa na maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es salaam. 

  Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa Wilfred Warioba(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa kupokea malalamiko kwa njia ya ujumbe wa simu ya kiganjani kushoto ni Afisa Habari Mkuu wa Tume hiyo Germanus Kyafula na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari.

  Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu Francis Nzuki akiwaonesha waandishi wa habari kijitabu chenye sheria namba 7 ya mwaka 2001 iliyounda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es salaam kulia ni Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Umma na Mafunzo Alexander Hassan.PICHA ZOTE NA FRANK MVUNGI.

  ========  =========  =========
  Na Georgina Misama-MAELEZO

  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeanzisha mfumo mpya wa kupokea malalamiko na taarifa kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa njia ya ujumbe wa simu ya kiganjani.


  Hayo yamesemwa na Msemaji wa Tume hiyo Germanus Kyafula wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam. “Tume imeamua kuanzisha utaratibu huu mpya, ambapo watanzania watakuwa na fursa ya kuwasilisha malalamiko yao wakati wowote bila ya kuja kwenye ofisi zetu au kutumia barua kwa njia ya posta kama ilivyokuwa awali”alisema Germanus .

  Akifafanua utaratibu huo alisema mwananchi atatakiwa kuandika ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani kwenda namba 0754 460259 ili kufungua malalamiko pale ambapo ataona haki zake za msingi zimekiukwa au misingi ya utawala bora haijafuatwa.Aidha Germanus alisema utaratibu huu mpya  ulianza tarehe 27 Juni na mpaka sasa umeongeza idadi ya malalamiko yanayowasilishwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali ambapo Tume ishapokea malalamiko 127.

  Naye Mkurugenzi wa Idara ya haki za Binadamu Francis Nzuki akitoa ufafanuzi alisema Tume itashirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za bunadamu na kutoa vipeperushi  ambavyo vina taarifa ya huduma hiyo.  Tume imesema ina mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi, lengo ni kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo hasa wananchi wa vijijini.

  Tume ya haki za binadamu na utawa bora imesema sambamba na utaraibu huu mpya, bado inaendelea kupoke malalamiko kwa utaratibu wa zamani ambapo wananchi walikuwa wakifika wenyewe kwenye ofisi za Tume na kufungua jalada la malalamiko yao.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni. Picha zote na OMR
  Na www.sufianimafoto.com.
   MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. 

  Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi.

  Mbali na Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete.

  Mara baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali ya rufaa ya Jeshi,  Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.

  Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni.
   Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
   Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur.
   Baadhi ya wananchi waliofika kupokea na kushuhudia mapokezi  hayo ya miili ya mashujaa wetu.
   Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
   Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
   Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima.
   Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
   Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
  Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo.

  0 0

  IMG_9312 

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo Ilala alipofanya ziara rasmi katika masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti bei za bidhaa kabla na kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Mstahiki Meya aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei bidhaa zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
  IMG_9295
  IMG_9315
  IMG_9286
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.

  0 0

  Dar es Salaam. Mtu asiyejulikana juzi usiku alimvamia mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad (pichani) na kumwagia maji usoni yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.
  Tukio hilo lililotokea juzi saa 1 usiku karibu na kituo cha Polisi cha Oysterbay, lilithibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ally Mlege kwa kusema kuwa bado polisi wanaendelea na uchunguzi wao ili kuwabaini waliohusika.
  “Ni kweli tukio hili limetokea ila polisi wanaendelea na uchunguzi. Tukikamilisha uchunguzi tunatarajia kutoa taarifa kamili za tukio zima,” alisema na kuongeza;
  “Hatuna haja ya kuficha ukweli wa tukio hili, uchunguzi wetu ukikamilika na watuhumiwa wakikamatwa kila mtu atajua.”
  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mtu huyo, alimkuta Saad akiwa anazungumza na mmoja wa wafanyakazi wake katika duka lake jipya lililopo karibu na Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
  “Wakati akizungumza na mfanyakazi wake, huyo mtu alikuwa kama anapita na alichomoa kitu fulani na kummwagia Saad usoni na kisha kukimbia,” zilieleza taarifa hizo na kuongeza;
  “Baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya AMI, sasa hatujui kama bado yupo hapo au ameondoka, ila sisi tulizungumza naye na alitueleza mwonekano wa mtu aliyemwagia tindikali.”
  Taarifa hizo zilifafanua kwamba polisi wanazitumia taarifa hizo walizopewa na Saad, ili kuweza kumkamata mhusika.
  Taarifa hizo zilifafanua kuwa polisi wanapanga tena siku ya kumhoji kwa mara ya pili Saad, kwamba watataka kufahamu kama mfanyabiashara huyo alikuwa akipewa vitisho au ujumbe wowote, kabla ya kukutwa na tukio hilo.
  Hata hivyo, habari nyingine zilizolifikia Mwananchi Jumapili zilieleza kuwa mtu huyo baada ya kummwagia Saad tindikali, alipanda pikipiki na kutokomea eneo hilo.
  “Walikuwa wawili, mmoja alikwenda kufanya unyama na mwingine alibakia katika pikipiki, baada tu ya kumwagia tindikali mtu yule alikimbia mpaka pale alipokuwa imesimama pikipiki, alipanda na kuondoka kwa kasi,” zilieleza habari hizo.
  Taarifa zilizopatikana jana asubuhi zilieleza kuwa ndugu na marafiki wa mfanyabiashara huyo, walikuwa katika mipango ya kumpeleka nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
  HABARI KWA HISANI YA MWANANCHI.CO.TZ

older | 1 | .... | 122 | 123 | (Page 124) | 125 | 126 | .... | 1896 | newer