Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1237 | 1238 | (Page 1239) | 1240 | 1241 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika mkutano huo. Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu na Utafiti wa Trust Care Tanzania Foundation, Fadhila Nyoni akifafanua jambo juu ya semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika mkutano na wanahabari leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akifuatilia mazungumzo hayo.

  SHIRIKA la Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wameandaa semina ya kuwajengea uwezo wa kifikra wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwabadili wanafunzi kwa ujumla kuwa na mawazo chanya yatakayowawezesha kutumia fursa anuai zinazowazunguka katika jamii mara baada ya masomo yao.

  Akizungumzia semina hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo.

  Alizitaja mada ambazo wanafunzi wanatarajia kufundishwa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo. “Semina inawaandaa vijana waliopo na ambao wanatarajia kumaliza elimu yao ya juu hivi karibuni kupata elimu na ujuzi utakaowasaidia wakiwa shule na baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kwenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa…” alisema Bw. Mbwafu.

  Akifafanua zaidi Mkurugenzi, Zambert Mbwafu, alivitaja vyuo vitakavyoshiriki katika semina hiyo; ni pamoja IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM, MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI.

  Kwa upande wa wadhamini wakuu wa semina hiyo Kampuni ya TTCL, Injinia Enocent Msasi Mkurugenzi wa Biashara TTCL alisema kampuni hiyo inaunga mkono kampuni ya Trust Care Tanzania kwa dhumuni lake la kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta za kiafya, kielimu na kijamii. Aliongeza kuwa lengo hilo linashabihiana na lengo la TTCL kuhakikisha inakuwa na jamii bora zaidi kiteknolojia, kielimu, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla.

  “TTCL imedhamini semina hii kwasababu inatoa mchango mkubwa katika kujenga taifa lenye vijana wachapakazi, vijana wenye mtizamo chanya, vijana wenye uwezo wa uthubutu, na kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha, ” alisema Msasi na kuongeza kuwa TTCL kupitia huduma zake bora za intaneti, sauti na SMS inawaunga mkono vijana mara zote na itakuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

  “TTCL kwa miaka mingi tumekuwa tukipokea vijana wanaokuja kufanya mafunzo kwa vitendo kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za elimu zinazotoa elimu katika fani tofauti tofauti. Lakini safari hii tumekuja kivingine zaidi, kwa kuja na programu ambayo itasaidia vijana kupata uzoefu baada ya kumaliza masomo yao. Hii itasaidia kuondoa changamoto ya vijana wetu waliomaliza elimu ya juu ambao mara nyingi hupoteza fursa mbalimbali za ajira kwa kukosa sifa ya uzoefu.”

  Vijana watakao pata fursa ya kufanya kazi na TTCL watajifunza mengi kawa vitendo huku wakiongozwa kwa wataalamu wabobezi katika fani mbalimbali. Tunaamini watakapomaliza programu hiyo vijana hao watapata fursa kupata ajira kwenye taasisi na makampuni mbalimbali, au kujiajiri wenyewe,” alisisitiza Enocent Msasi akizungumza na wanahabari leo. Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akiwa katika mkutano huo. Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem kwa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri.
  Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia) Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni ya Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akisalimiana na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus mara baada ya uzinduzi rasmi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam, ambapo wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki bure kupitia application ya Mdundo.com
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii yenye lengo la kuwanufaisha hasa vijana. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.
  Mtaalamu wa masuala ya Biashara Zantel, Rehene Cathbert Tarimu (kulia) akionyesha Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure mara baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Mtaalamu wa huduma za simu Emmilina Albert Vokolawene pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Teknolojia Zantel Salim Awadh.

  …………………………………………….

  Kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

  Akizindua rasmi huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema wateja wa Zantel wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi watapata nafasi ya kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya kusikiliza muziki bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.

  Aliongeza kwa kusema “Tunajisikia fahari kubwa sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zetu za kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya intaneti ya kasi zaidi ya 4G Tanzania nzima.

  Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza Zuberi alisema, “Kwa wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na mwezi ambavyo ni ;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa 2.5G watapata nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa wateja wenye simu au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa wateja wetu wanaotumia simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia simu au vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.

  Aliongeza kuwa baada ya kufanya utafiti wa kina kwenye soko la mitandao ya simu waligundua kuwa vijana wengi wanapenda muziki ambapo mpaka sasa hakuna kampuni yoyote ya simu inayotoa huduma hiyo bure, na hivyo kuwafanya Zantel kuileta huduma hiyo sokoni kwa kupitia ‘Mdundo Music Application.’

  ‘Mdundo Music Application’ ni moja ya programu kubwa kabisa za muziki barani Afrika inayowawezesha watu kuweza kusikiliza aina zote za muziki kwa kutumia intaneti. Programu hiyo ina zaidi ya nyimbo 200,000 kutoka kwa wanamuziki zaidi ya 40,000. Zantel inaamini ofa hii itawafaa zaidi vijana kwakuwa wengi wao wamekuwa kwenye utamaduni wa kisasa unaopenda ziaidi muziki na hivyo huduma hii ya bure itawavutia zaidi.

  Aliongeza kuwa huduma hiyo mpya inapatikana karibu kwenye mifumo yote ya simu za mkononi kama vile Android, iOS kwa ajili ya iPhone, Blackberry na Nokia Symbian.

  Martin Nielsen, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mdundo.com alisema, “Wateja wa Zantel wanaweza kupata orodha yote ya nyimbo kupitia Mdundo ikiwa ni pamoja na nyimbo mchanganyiko zilizoandaliwa na Ma DJ maarufu, muziki wa Afrika Magharibi na pia Mashariki. Tanzania ni soko letu ambalo linakuwa kwa kasi sana na tunatarajia kuwa mpango huu utasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uharamia kwenye soko la muziki nchini na kuwapa wateja sababu ya kufurahia muziki zaidi ya hapo awali”.

  Huduma hii mpya kutoka Zantel imekuwa miongoni mwa huduma nyingine za kibunifu na kidijitali ambazo zimeanzishwa na Kampuni hiyo hivi karibuni. Huduma hizo ni pamoja na uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G LTE upande wa Bara na Visiwani, ‘Zantel Madrasa’ huduma inayowawezsha waumini wa dini ya Kiislamu kupata mafundisho, Quran, Habari za BAKWATA na mawaidha mbalimbali ya kiislamu kwa njia ya simu, ikiwemo pia kwa njia ya SMS na ‘ Zantel Madrasa App’.

  Akizungumzia uwekezaji wa Zantel, Janin alisema wamewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 katika uboreshaji wa mtandao ambapo mpaka sasa zoezi la maboresho hayo katia maeneo ya Stone Town Zanzibar na Mkoa wa Mjini Magharibi yameshakamilika. Zoezi hilo linaloendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba linaarajiwa kufikia kikomo mwisho wa mwezi huu.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Gavu akisoma hotuba ya kufunga semina kuhusu elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake. Semina hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifanyika Pemba kuanzia tarehe 15 - 18 Mei 2017. Wengine katika picha, kushoto ni katibu wa Wizara hiyo, Bw. Salum Salum na Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Eliabi Chodota. 
  Kulia ni Mbunge wa Wete, Mhe. Ali Mbarouk akifuatilia kwa makini semina ya mtangamano. 
  Washiriki wa semina hiyo ambao wengi wao walikuwa wajasiriamali wakisikiliza hotuba ya kufunga semina. 
  Washiriki wengine wakifuatilia hotuba ya Mhe. waziri wa Nchi. 
  Mhe. Waziri wa Nchi akiendelea kuwahutubia wana semina na watu wengine waliohudhuria sherehe za ufungaji. 
  Picha ya pamoja kati ya Mhe. Gavu na washiriki wa semina. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga akiwasilisha mada kuhusu Diplomasia ya Umma kwa wana semina hiyo. 
  Wajumbe wa semina wakisikiliza mada kuhusu Diplomasia ya Umma. 
  Bi. Mindi akiendelea kuwasilisha mada. 
  Prof. Ammon Mbelle kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Mambo ya Nje kwenye semina hiyo. 
  Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Elly Chuma akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika Diplomasia yaUchumi. 
  Wajumbe wa Semina wakifuatilia mada. 
  Mjumbe wa Semina akichangia mada. 
  Watoa mada wakipongezwa na wajumbe wa semina. 

  Serikali ya Zanzibar imeahidi kuwa itaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za kiuchumi kwa madhumuni ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ili wananchi waweze kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Gavu alipokuwa anafunga semina ya siku nne kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake iliyofanyika Pemba kuanzia tarehe 15 hadi 18 Mei 2017.

  Mhe. Gavu alitoa wito kwa wanasemina hao ambao wengi wao walikuwa ni wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia ya ulimwengu wa sasa ili ziwe na uwezo wa kushindana na bidhaa nyingine katika soko la EAC.

  Aidha, Mhe. Gavu aliahidi kuwa Serikali itasaidia wajasiriamali washiriki makongamano, semina, maonesho na warsha mbalimbaili zinazofanyika nchini na nje ya nchi ili iwe fursa kwao kujifunza mambo mapya yanayoendana na ulimwengu wa sasa kwa lengo la kuboresha biashara zao.

  Mhe. Gavu aliwasihi wote waliopata na watakaopata fursa za mafunzo kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili kwa pamoja watumie mbinu, ujuzi na uzoefu wanaoupata kukabili changamoto za ushindani wa soko kulingana na mahitaji ya sasa.

  Alisisitiza umuhimu wa nchi zote wanachama wa EAC kuwahudumia raia wa nchi zote kwa usawa bila ubaguzi. Alisema endapo nchi moja ikiwa na tabia ya kunyanyasa raia wa nchi nyingine inaweza kusababisha dhana ya kulipiza kisasi hatimaye vurugu na kuleta mkanganyiko katika Jumuiya. 

  Vile vile, Waziri wa Nchi alitoa wito kwa nchi zote wanachama kushirikiana kwa pamoja kudhibiti biashara ya magendo. "Sio sahihi kwa nchi moja kufumbia macho biashara ya magendo kwa kutochukua hatua dhidi ya wanaoingiza na kununua bidhaa za magendo". Mhe Gavu alisema. Zanzibar inakabiliwa na biashara ya magendo ya zao la karafuu ambayo inasafirishwa kwa njia za panya kwenda nchi za jirani.

  Kwa upande wao wajasiriamali wameahidi kuwa watatumia mafunzo waliyopata kulikabili Soko la EAC bila khofu yeyote kama ilivyokuwa hapo awali.

  Semina hiyo ya siku nne ilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na ilitolewa na wataalamu wa Wizara kwa kushirikiana na Prof. Ammon Mbelle kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

  Dar es Salaam, 18 Mei, 2017

  0 0


  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
  Wanachana wa CCM Jimbo la Segerea wakiinua mikono kufurahia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo,jana.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
  Wanachama wa CCM Jimbo la Ukonga wamsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo,wakati 
  akiwahutubia kwenye Ukumbi wa Check Point jana.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwatambulisha Madiwani wa Jimbo la Segera na kuwapa majukumu wakati wa mkutano huo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akizungumza jamabo na mmoja wa wanachama wa CCM Kata ya Pugu wakati akiondoka baada ya kymaliza mkutano wake katika Jimbo la Ukonga jana.


  ***********************************************


  Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

  UBABE na unafiki wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) inaelezwa kuwa ndio chanzo cha kupoteza jimbo la Ukonga na mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana wakati alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika majimbo ya Ukonga na Segerea.

  Alisema viongozi hao waliendekeza mizengwe na umimi, ambapo matokeo yake waliwavuruga wanachama na jimbo likachukuliwa na upinzani,sasa wanajuta.

  "Tumewasababishia wanachama kubaki kama wakiwa, hawana mbunge,na sehemu zingine hawana madiwani. Yote ni kutokana na ubinafsi na makundi yaliyokiumiza Chama,"alisema.

  Mpogolo alisema CCM haiwezi kukubali viongozi wachache wenye roho za chuki waendelee kuwanyanyasa wanachama wenzao kwa sababu ya maslahi ya makundi yao."Naomba kila mwanachana afanye mabadiliko ndani ya nafsi yake. Hatuna namna nyingine zaidi ya 

  kubadilika na kujenga taswira nzuri ya Chama chetu. Mtu anayeona hawezi kubadilika aende vyama 
  vingine," alisema.Aliwataka viongozi na wanachama kuvua makoti ya zamani yaliyojaa chuki,roho mbaya na ubinafsi na badala yake wavae makoti mapya ya upendo ,umoja na mshikamano na kuingia kwenye timu ya ushindi ya CCM mpya na Tanzania mpya.

  Akiwa katika jimbo la Segerea, Mpogolo aliwapongeza kwa kushinda jimbo hilo na aliwapa pole kwa kupoteza kata zote za jimbo hilo,lakini aliwataka wajitathmini maana wanajua nani aliyepoteza.Mpogolo alisema chanzo cha kupoteza kata zote 13 ni wana CCM walioamua kuuza kata zote na kuwafanya wananchi wakose 'connection' Mwenyekiti wa Chama Rais Dk. John Magufuli.

  "Tumeweka madiwani hawana hata mawasiliano na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama chetu. Hata kuwaletea maendeleo itakuwa ndoto kwa kuwa hawana 'connection'na baba,"alisema.Aliwataka wanachama kuanza kujiandaa mapema kutafuta wafuasi kwa kujenga uhusiano mwema na kuwa kishawishi kwa wananchi wengine ili kuongeza jeshi la CCM.

  "Ili ushinde unahitaji wafuasi wengi na uwe kivutio.Sasa kwa tabia zetu za figisu figisu, hasira makundi, kushughulikiana tutawezaje kuvuta wafuasi.Ndio maana nawataka mbadilike ndani ya nafsi zenu,"alisema.

  Akizungumza kwa mifano Mpogolo alisema baadhi ya viongozi wamekuwa vikwazo na kuwakera wanachama mpaka wengine wanakimbia CCM jambo ambalo halina nafasi katika awamu hii."Kama tumejaa chuki, kufukuzana, kuchafuana ,kupakana matope,hatutaweza kuwavutia wanachama wapya. Wanaofitini wenzao na kufukuzana bila sababu za msingi hawana nafasi CCM,"alisema.

  Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe,alisema jimbo la Segerea ndio eneo pekee ambalo Chama kilipoteza kata zote na hailezeki ilikuwaje maana mbunge aliyeshinda ni wa CCM Bona Kaluwa.Alimuomba Mpogolo, awafunde wanachama wa CCM waondokane na mapepo yaliyosababisha wauze kata zote za jimbo hilo.

  Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joyce Kaugala ,alisema ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama ,itasaidia kuwajenga wanachama ili uchaguzi ujao waweze kukomboa kata zote.

  0 0

  Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Sylvester M. Mabumba (kulia) akiwasili katika Ikulu ya Komoro kwaajili ya hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, kushoto ni Mnikulu wa Ikulu ya Komoro Bw.Hashim Mohamed. Hafla ya kukabidhi Hati hizo ilifanyika mapema wiki hii katika Ikulu hiyo.

  Mhe. Balozi Mabumba akijitambulisha sambamba na kutoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho.
  Mhe. Balozi Mabumba akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Ikulu ya Komoro. Pembeni yake ni Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo Mambo ya Nje ya Komoro.

  ==================================================

  Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba mapema wiki hii alikabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Azali Assoumani. Hafla ya kukabidhi hati hizo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama Beit.

  Wakati akihutubia, Mhe. Mabumba alijitambulisha kwa Mhe. Rais na kueleza furaha yake ya kuteuliwa kuwa Balozi wa pili kutoka Tanzania kuja kutumikia nchini Komoro. Aidha, alieleza furaha yake kwa mapokezi mazuri aliyoyapata tangu kuwasili kwake Visiwani humo na kwamba yamemfanya ajisikie yupo nyumbani. 

  Alieleza kuwa anatambua kazi kubwa iliyopo mbele yake na kuahidi kuwa katika kipindi chake wakati akiwa Balozi nchini humo atajitahidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Komoro. Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alieleza dhamira yake ya kutaka kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yanakuwa na manufaa kwa pande zote halikadhalika kukua kwa uhusiano wa kindugu kwani mahusiano baina ya Tanzania na Komoro ni ya kihistoria.

  Pia Mhe. Rais Assoumani katika hotuba yake naye alianza kwa kuonyesha furaha yake ya kuwasili kwa Balozi pamoja na kukiri kupokea barua ya kurejea Balozi aliyepita na ya kuwasili kwa Balozi wa sasa. Vilevile alieleza kuwa kila Mkomoro hujisikia nyumbani pindi anapo tembelea Tanzania kutokana na ukarimu wanao onyeshwa wanapokuwa huko. Aidha Mhe. Rais alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa atarajie kupata ushirikiano wake pamoja na wa Serikali yake katika kipindi chote atakapo kuwa nchini humo.
  Mhe. Balozi Mabumba alitumia fursa hiyo pia kumuomba Mhe. Rais Assoumani kufanye ziara ya kikazi nchini Tanzania ili kuweza kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya wataalam kutoka Kampuni ya esri- inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), walipokutana leo Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini. Kulia ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirila la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA Tanzania) Dkt. Hashina Begum.
  Mtalaam kutoka kampuni ya esri – inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), Bi. Linda Peters akielezea jambo wakati wa kikao baina ya wataalam kutoka Kampuni hiyo na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni wataalam kutoka Kampuni hiyo Bw. Patrick Kipchumba na Mhandisi Anthony Gakobo.
  Baadhi ya wataalam kutoka Kampuni ya esri – inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) walipokutana leo Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
  Mtalaam wa Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) Anthony Gakobo akionyesha moja ya kifaa kinachotumika katika kuhakiki uhalisia wa taarifa za kijiografia mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni watalaam wa mfumo huo Bw. Patrick Kipchumba na Bi. Linda Peters.
  Mshauri wa Masuala ya Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia – Tanzania, Bi. Elizabeth Talbert akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya wataalam kutoka Kampuni ya esri- inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka UNFPA, Benki ya Dunia – Tanzani , watalaam kutoka Kampuni ya esri inayojishugulisha na kutoa huduma za Mfumo ya Taarifa za Kijiografia (GIS) pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumaliza kikao kujadili namna mfumo wa GIS unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.

  (Picha zote na Frank Shija – MAELEZO)

  0 0  Mratibu wa kampeni ya mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari Juliana Kitila akimuonyesha kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro Peter Nkaya ( wakanaza upande wa kushoto) hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mambo sita ya ya usafi wa mazingira kwenye halmashauri yake ikiwa ni kampeni ya kuendeleza muitikio wa usafi mkoani Morogoro.
  Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro ‘akiapa’ kuwa yuko tayari kuungana na serikali katika kutekeleza swala la usafi sambamba na halmashauri yake.
  Mratibu wa kampeni ya ya mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari Juliana Kitila akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama juu ya kampeni ya hiyo mjini Morogoro jana.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama akishilia bango la Nipo Tayari kama ishara ya kuwa yuko tayari kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari wakati wa semina mjini Morogoro jana.

  0 0

  Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo, katikati akipokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Biko katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia uingizaji wa fedha hizo katika akaunti ya Kapondo.

  MSHINDI wa Droo ya Bahati Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku iliyochezeshwa juzi Jumatano, Stanley Kapondo, amekabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa pesa hizo zimekuja wakati muafaka ili kuondoa changamoto zinazomkabili katika maisha yake.

  akabidhiano hayo yamefanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam kwa kusimamiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ikiwa ni siku moja baada ya kumpata mshindi wao wa droo ya Jumatano.
  Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo kushoto akifurahia fedha zake za ushindi wa droo ya Biko alizoshinda katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kapondo alisema alikuwa na uhitaji mkubwa wa pesa, hivyo aliamua kucheza Biko kama sehemu ya kutafuta suluhu ya matatizo yake.

  Alisema pamoja na kuamua kucheza Biko, hakuamini kwamba angeshinda Sh Milioni 10, badala yake alikuwa anawazia ushindi wa Sh Milioni moja aliyoona ni rahisi.

  “Niliamua kuchezaa biko kwa kufanya miamala kwenye simu yangu kwa kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kwenye namba ya kumbukumbu niliweka 2456 kama wanavyohitaji ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio sababu ya kutangazwa mshindi.

  Pesa nilizopokea kutoka Biko si za kwanza maana nimekuwa nikishinda zawadi za papo kwa hapo hadi Sh 50,000, hivyo binafsi nikajikuta nawaamini zaidi Biko ukizingatia kuwa licha ya kuwahi kucheza bahati nasibu nyingi, lakini kwa umri wangu wa miaka 52 sijawahi kubahatika,” Alisema Kapondo ambaye pia ni mtumishi wa Shirika na Umeme Tanzania TANESCO, Ubungo.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kucheza kwa wingi huku akisema zawadi za Sh Milioni 10 zitawaniwa katika droo ya Jumatano na Jumapili huku zile za papo kwa hapo zikiendelea kulipwa kwa kupitia simu za wachezaji wao.

  “Biko imezidi kukolea, hivyo ni wakati wa kucheza mara nyingi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi maana zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatolewa kila siku saa na kila siku, hivyo unachotakiwa ni kufanya miamala kwnye simu zenu za Tigo, Vodacom na Airtel, huku tiketi ikipatikana kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Heaven.

  Kwa mujibu wa Heaven, tiketi moja ya Sh 1000 itakuwa na nafasi mbili ikiwa ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, watu wakishauriwa kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya ushindi wa Biko.

  0 0

  --
   Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Jaji Thomas Mihayo akizungumza katika mkutano mfupi uliofanyika katika Stesheni ya Tazara jijini Dar es Salaam
   Baadhi ya Wasanii hao Nyota wakiwasili katika  Stesheni ya TAZARA Jijini Dar es Salaam
   aziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza  wakati wa kuwakaribisha wasanii hao nyota kutoka nchini China
   Muongoazaji wa filamu ya siri za familia akitoa Salamu za Wasanii hapa nchini
   Wasanii hao Nyota wakiwa wameketi kwa pamoja  wakati wa mkutano
   Wasanii hao  ikawakiwa katika kurekodi sehemu ya vipindi vitakavyorushwa katika cheneli za nchini China
   Baadhi ya watali hao wakiwa wamekaa katika Vibalaza vya Stesheni ya Tazara
   Wasani wa filamu nchini wakibadilishana mawasiliano na muongozaji wa kundi la wapiga picha na waandishi kutoka nchini China
   Muwakilishi wa kabila la Wadzabe akionyesha namna ya kutumia upinde kwa wasani nyota kutoka nchini China
   Sehemu ya wapiga picha waliongozana na Wasanii hao nyota kutoka nchini China
   Mmoja wa wapiga picha kutoka nchini China akirekodi wakati treni lilipo fanya ruti fupi mpaka Yombo na kurudi
   Sehemu ya Wasanii nyota wakiwa ndani ya treni
   Kundi la Wasaniihao na wapiga picha wakiwa ndani ya Treni ya Tazara wakirekodi kipindi na kufanya majadiliano  0 0


  0 0

  Tamasha la muziki wa injili lenye ubora wa kimataifa linatarajia kufanyika Jumapili,Mei 21 katika ukumbi wa Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University

  Tamasha hili linalojulikana Ni Salama moyoni, ambapo mwanamuziki Mchungaji PAUL SAFARI ndiye atakayekuwa muhusika mkuu ambapo atarekodi nyimbo zake kwa njia ya moja kwa moja (yaani live).

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Mchungaji SAFARI amesema tamasha hilo limeandiliwa kwa katika viwango vya ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa.

  “Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. amesema mchungaji Safari.

  Wanamuziki mbali mbali kama a John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ nao watatumbuiza katika tamasha hilo linalotarajiwa kuvuta watu wengi.

  Mchungaji Safari Paul ni mmoja wa wachungaji katika kanisa la DPC na pia mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili. Amekuwa sehemu ya watu waliokuza muziki wa injili Tanzania na amelea na kukuza waimbaji wengi, na ameshiriki kurekodi nyimbo akishirikiana na vikundi mbali mbali ndani na nje ya nchi.

  Albamu yake ya kwanza inayoitwa Furaha ya Bwana mwaka 2006. Na sasa baada ya miaka kumi na moja, Pastor Safari ameandaa Ni Salama Mubashara au Live DVD recording ya Ni Salama.

  Tamasha hili la aina yake, limeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa. “Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. asema Pastor Safari. Tamasha hili la Ni Salama yaani Ni Salama Live DVD recording, litafanyika tarehe 21/05/2017 katika Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University). Pia Pastor Safari atasindikizwa na John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ.

  Lengo ni kupeleka ujumbe wa neno la Mungu duniani kote kwa njia ya muziki na uimbaji na kuleta madariko katika maisha ya watu. “Watanzania tunasifika sana kwa uimbaji na tumejaliwa na Mungu katika eneo hili, lakini miziki yetu haifiki mbali kwa sababu tunakosa ufanisi na ubora katika kazi zetu. Naami Tamasha la Ni Salama litakuwa ni chachu kwa wanamuziki na waimbaji wote. Narudia tamasha hili litaweka historia. Hivyo usikose” asema Pastor Safari Paul.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akipeana Mikono na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya mara baada ya uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
  Baadhi ya watumishi wa kampuni ya StarTimes Tanzania ambao wamehudhuria sherehe hiyo
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akizungumza mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya ukopaji wa Televisheni za Star Times.
  Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya akizungumzia namna ya kuapata mkopo kutoka benki hiyo
  Sehemu ya Watumishi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Duka la Star Times Bamaga
  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Kampuni ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.

  akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mpnago huo Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal, amesema kuwa ubia huo unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB.

  "wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo" amesema Zuhra.

  Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi amesema ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes.

  Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.

  “Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia”

  Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. 

  Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.

  Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
  Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi akizungumza na namna ya kutumia Luninga hiyo iliyo na king'amuzi ndani
  Meneja Masoko wa Benki ya TPB,Amos Kisanga Akizungumza juu ya watu kufungua akaunti benki ya Posta na kuweza kukopa Luninga.

  0 0


  Na Karama Kenyuko, Globu ya Jamii

  Wafanyabiashara wa kemikali Bashirifu wameaswa kufuata sheria za nchi Katika kudhibiti matumizi yasiyokuwa salama ya kemikali hizo.

  Hayo yamesemwa Leo na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampuni ya Tecno Net Scientific kukutwa na Kemikali Bashirifu bila ya kuwa na kibali wala usajili.

  Profesa Manyele amesema, mwaka 2014 waliipatia kampuni hiyo usajili wa miaka miwili, lakini baada ya kibali chao kuisha wamekiuka sheria na kuendelea kuagiza Kemikali bashirifu kwa kutumia vibali bandia.

  Ameongeza kuwa, kufuatia kugundua hayo, vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa shughuli za kampuni hiyo na pindi taratibu za uchunguzi utakapokamilika kampuni hiyo itafikishwa mahakamani.

  Aidha ameongeza kuwa, ili kuhakikisha kemikali hizo zinatumika katika hali iliyosalama, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na Kemikali, kudhibiti matumizi matumizi yasiyofaa na kuzuia kutumia kwa kutengeneza mabomu, milipiko dawa za kulevya au kutumia kama silaha kama ilivyokuwa kwenye suala la watu kumwagiwa tindikali.

  Aidha Prof. Manyele amesema, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya Kemikali bashirifu kuhakikisha wanaenda Kutoa taarifa mwenyewe pindi vibali vyao vikiisha ili wapatiwe usajili mpya.Amesema, Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa kemikali wasiokuwa waaminifu na wanaovunja matakwa ya sheria katika uingizaji na usafirishaji wa Kemikali bashirifu.

  Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akizungumza na waandishi habari juu uingizaji Kemikali bashirifu ambazo zinafuata sheria iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

  0 0

   Mhusika mkuu katika Mchezo wa Jukwaani wa 'UNTOLD SORY ' Amani Kipimo akiwa jukwaani katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini dar es Salaam.
   Sehemu ya Waigizaji  wa mchezo wa kuigiza wa Untoldy Story wakiwa jukwaani  wakati wa utambulishwaji wa mchezo huo
   Msanii mkongwe wa Luninga na Jukwaani Susan Lewis akiwa na Mhusika mkuu wa mchezo wa Untold Story Amani Kipimo 'Ngasu'
   sehemu ya watu waliofika kushuhudia mchezo huo wa Untold Story ambao ulibua hisia na kuwa gumzo kwa watu wengi sana
   Baadhi ya waigizaji wa mchezo huo wa jukwaani wakionyesha uwezo wao wa kucheza na jukwa
   Rais wa Shirikisho la Filamu nchini Simon Mwakifamba akisiamama kwa heshima mara baada ya kuona mchezo huo ambao ulivuta hisa za wengi
   Moja ya sehemu za mchezo huo wa kuigiza ukiwa jukwaani
   Mwanamuziki wa maharufu wa Injili Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki David Robert aliyevaa T Shirt Nyekundu akishuhudia igizo hilo la UntoldStory
  Sehemu ya waigizaji wa igizo hilo
  --

  0 0

  Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Salum Maulid Salum, akizungumza kwenye ufungaji wa semina kwa wajasiriamali, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba,  na kutayarishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ akizungumza kwenye ufungaji wa semina ya siku nne, kwa wajasiriamali kisiwani Pemba, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.
  Mshiriki wa semina Othman Bakar Shehe akitoa shukuran kwa niaba ya wajasiriamali wenzake, baada ya kumaliza semina ya siku nne, ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani na kuandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Mjasiriamali Kauthar Is-haka akimkabidhi Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe Issa Haji Ussi “Gavu’ zawadi ya mikoba ya kisasa inayotengenezwa na wajasiriamali, hafla hiyo ilifanyika uwanja wa Gombani, baada ya kumaliza semina ya mtangamano wa Afrika Mashariki, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  WA kwanza kulia, ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ akifuatiwa na Katibu Mkuu wake, Salum Maulid Salum samba na Mwenyekiti wa wajasiriamali kisiwani Pemba, Khamis Suleiman wakisikiliza shukura za wanasemina, iliofanyika uwanja wa michezo Gombani juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki.
  Wajasiriamali, wafanyabiashara na baadhi ya wakuu wa taasisi za serikali kisiwani Pemba, wakisikiliza hutuba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ wakati akifunga semina juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa TEA.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela akizungumzia faida zinazotokana na mradi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akimkabidhi mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Miliki NHC Bw. Hassan Mohamed, ukarabati huo unafanywa na Shirika la Nyumba la Taifa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akiwaongoza wadau walioshiriki hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukagua baadhi ya majengo na miundo mbinu ya shule hiyo itakayofanyiwa ukarabati.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi akishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kuamua kukarabati miundo mbinu ya Shule hiyo ili kukuza kiwango cha elimu. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela
  Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Pugu yatakayofanyiwa ukarabati na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na yatagharimu zaidi ya milioni mia tisa. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

  Na Fatma Salum- MAELEZO
  Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa kukarabati Shule ya Sekondari Pugu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mkataba wa ujenzi kwa Mkandarasi wa mradi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 984 zitatumika katika awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hiyo.

  “Awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hii itaanza tarehe 1 Juni, 2017 na itafanyika kwa muda wa miezi minne. Ukarabati katika awamu hii utahusisha madarasa, vyoo kwa ajili ya wanafunzi walemavu, mabweni, jengo la utawala, mifumo ya TEHAMA, mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na mifumo ya umeme”alifafanua Bibi. Shirima.

  Alieleza kuwa zoezi hilo la ukarabati lilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa kubaini hali halisi ya mahitaji ya ukarabati na kazi hiyo ilifanywa na Mtaalamu Elekezi (Consultant).

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela alipongeza jitihada za TEA za kukarabati miundombinu ya elimu hasa kwa shule kongwe za Sekondari nchini kote mradi ambao utasaidia kuboresha elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

  “Manispaa ya Ilala inaahidi kushirikiana na TEA na uongozi wa Sekondari ya Pugu kutekeleza zoezi hili na kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu.” alisema Palela.

  Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi alieleza kuwa shule hiyo ina historia kubwa katika nchi yetu na kuishukuru Serikali kupitia TEA kwa ukarabati huo utakaosaidia kurudisha shule hiyo katika hali yake ya awali. 

  Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeazimia kukarabati jumla ya shule kongwe za Sekondari 17 ikiwemo shule ya Sekondari Pugu na zoezi hilo limeshaanza kwa shule za Sekondari Nganza, Same na Ilboru.

  0 0

  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba mtandao.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. 

  Warsha hiyo ilikuwa inakokotoa tiba mtandao ili kuwezesha mradi wa majaribio wa Tiba mtandao unaohusisha wadau mbalimbali kutekelezwa. Kitovu cha mradi huo ni kijiji cha Ololosokwan kilichopo Waso wilayani Ngorongoro. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)

  Katibu huyo alisema kutumia kikamilifu kwa kijiji hicho hakumaanishi kuwa na majengo bali kutumia kufunza wataalamu mbalimbali kutokana na ukweli kuwa kijiji hicho sasa kitakuwa mfano wa utendaji katika kusaidia wananchi wa Tanzania. 
  “Uwapo wa kijiji hiki ni tukio kubwa kwetu kwani ni kijiji cha kujifunzia, namna ya kutibu, namna ya kukusanya takwimu namna ya kubaini mahitaji na … ni mfano wa namna gani teknolojia inaweza kufanya mambo makubwa” alisema Ulisubisya . 

  Alisema yeye anaamini kwamba si lazima wataalamu watiba wafundishwe eneo moja, kama ilivyo sasa, lakini wanaweza kufundishwa katika eneo kama Ololosokwan na hivyo kuwajenga pia kisaikolojia kwamba wanaweza kufanyakazi pembezoni bila ya tatizo. 
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) akichangia jambo wakati wa kuhitimisha warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Wa pili kushoto ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya (wa pili kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia).

  Alisema mafanikio ya dhana ya tiba mtandao yatasaidia sana kuboresha hali ya watanzania kwa kuwa mahitaji yao yatajulikana mapema na kutokana na ukweli kuwa mradi wenyewe unahusisha pia ukusanyaji wa data wa uhakika kwa kuzingatia mahudhurio ya watu na magonjwa yao. 

  Pia alisema kwa utekelezaji thabiti utaonesha namna ambavyo Watanzania tuko mbele na kusema kwamba mradi huo wa tiba mtandao anauelewa na ameupigania sana nje ya nchi ambako amekwenda kuzungumza. 

  “Mwaka jana mwezi Desemba nilienda kwenye mkutano Washington unaohusu Tiba mtandao na tumeuza sana hili wazo la tiba mtandao kwa wenzetu, kwa hiyo watakuja kujifunza tunafanyaje” alisema Dk. Ulisubisya na kuongeza kwamba Wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuona dhana hiyo inatekelezeka tena kwa ufanisi. 
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) akitoa maoni wakati wa kufunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo.

  Kwa mujibu wa mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu na kutanuka kwa jinsi inavyowezekana kwa kuangalia ufanisi wa kijiji. 

  “Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira 

  Tiba mtandao katika kijiji hicho itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na watendaji waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa. 
  Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Tehama wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Felix Sukums akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao kwa mgeni rasmi (hayupo pichani), Kushoto ni Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen.

  Aidha akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo Zulmira alitaka kuwapo kwa matumizi ya maabara ya kisasa iliyopo hapo ili iweze kusaidia taifa. 

  Hata hivyo mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba Daktari wa wilaya ambako kijiji cha Ololosokwan kipo anahitaji kiasi cha dola elfu 70 kukamilisha baadhi ya mambo ili kuwa na uhakika pamoja na kuleta madaktari wa Afrika mabingwa kuja kufanya kazi kwa muda. 

  Akizungumzia suala hilo, Dk Ulisubisya alisema kwamba anajua shida iliyopo, lakini akamwagiza DMO kukaa na DAS (Katibu Tawala Ngorongoro) kuona namna ya kufanikisha haja ya sasa ya nyumba za makazi kwa gharama nafuu na kusema anaamini wanaofaidika wako tayari kusaidia kidogo. 

  Alisema bajeti hiyo naamini inaweza kupungua kwa kutumia mali ghafi rahisi yenye kudumu zaidi. 
  Majadiliano yakiendelea katika kuboresha mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao wa kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika MUHAS.
  Pia aliwashukuru UNESCO kwa kuwezesha Ololosokwan kuwa sehemu ya kujifunza na kutanua mradi wa tiba mtandao ambao amesema kwa kuzingatia teknolojia iliyopo sasa Watanzania na dunia kwa ujumla wanapata nafasi ya tiba bila kuwa karibu na bingwa. 

  Katika utekelezaji wa mradi huo hatua ya pili mifumo yote (maunganisho ya kisetelaiti) inatarajiwa kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuanza matibabu ifikapo Oktoba mwaka huu au mapema zaidi. 
  Mradi huo unoanza kwa majaribio unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwani na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao. 
  Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akifafanua jambo kwa mgeni rasmi wakati wa kuhitimisha warsha hiyo.

  Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mwezi Novemba mwaka 2016. 
  Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo. 

  Warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha , Manyara , Kilimanjaro na Dar es salaam ilichambua dhana ya tiba mtandao na kuidadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na na namna ya kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini. 

  Mmoja wa washiriki akiwalisha maoni kwenye warsha ya siku 1 ya kujadili mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyomalizika MUHAS jijini Dar es Salaam.
  Picha juu na chini wataalamu kutoka KCMC, MUHAS, UNESCO, wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akimshukuru mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya mara baada ya kufunga warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) baada ya kuhitimisha warsha ya siku 2 ya mradi wa tiba mtandao iliyofanyika jijini Dar es Salaa., MUHAS.
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akimpongeza Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen mara baada ya kufunga warsha ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari (katikati) akiongoza kikao cha pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
   Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari.
   Wajumbe wa kutokana TADB wakifuatilia kwa makini mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kulia) akieleza dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
   Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati walipotembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar (hawapo pichani). Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kushoto).
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari akihiimiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
  Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.

  Na Mwandishi wetu,           
  Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar imesema itakuwa ya mwanzo kuanza kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ili kuchagiza uwekezaji katika sekta ya uchakataji wa mazao na masoko ili kuongeza tija kwa maendeleo visiwani Zanzibar.

  Mkakati huo umewekwa bayana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bakari H. Bakari wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake.

  Bw. Bakari amesema kuwa ujio wa Benki hiyo unatoa fursa kubwa sana kwa sekta zilizo chini ya wizara yake ikiwamo biashara, viwanda na masoko.

  “Tuna imani kubwa ujio wa TADB utatusaidia kutatua changamoto zinazozikabili sekta hizi ambazo zinakabili na changamoto ikiwemo ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo,” alisema.

  Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

  Bw. Assenga alisema visiwa vya Zanzibar vitaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo visiwani humo kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.

older | 1 | .... | 1237 | 1238 | (Page 1239) | 1240 | 1241 | .... | 1897 | newer