Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1236 | 1237 | (Page 1238) | 1239 | 1240 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdrahamani Kinana yuko nchini Angola akiongoza ujumbe wa CCM katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya ukombozi wa kusini mwa Afrika( Front Line State parties).
   
  Pia Ndugu Katibu Mkuu ameongoza Majadiliano na vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .
  Ujumbe wa CCM umejumuisha katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi( Ndg.Humphrey Polepole) Katibu wa Siasa na Uhusiano wa kimataifa(Ndg.Ngemela Lubinga) na watendaji wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Vyama Rafiki Vimepongeza CCM MPYA NA MWENENDO WAKE.
   Pichani kushoto Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimkaribisha Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota kutoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Kisiwani Pemba. Ushiriki na mwitikio katika semina hiyo umekuwa mkubwa kwa washiriki ambapo wameonekana kuvutiwa sana na semina hii pia wamekuwa wadadisi wazuri wa kutaka kujua zaidi fursa zinazo patikana kwenye mtangamano huo. 
  Bw. Chodota akitoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Pemba. 
  Sehemu ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Chodota (hayupo pichani). 
  Bw. Chodota akiendelea kutoa mada yake. 
  Mmoja wa washiriki Bi. Kauthari akiuliza swali mara baada ya mada kumalizika kutolewa na Bw. Chodota hayupo pichani. 
  Sehemu nyingine ya washiriki wakimsikiliza kwa makini. 
  Bw. Chodota akijibu swali lililokuwa limeulizwa na Bi Kauthari (hayupo pichani). 
  Bw. Suleimani Haji kutoka ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar naye akitoa mada kuhusu nafasi ya Zanzibar kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
  Sehemu ya washiriki wakimsikiliza kwa makini Bw. Suleimani (hayupo pichani). 
  Washiriki wakisikiliza kwa makini mada na maswali yaliyo kuwa yakiulizwa na washiriki wengine. 
  Mhe. Mbarouk Salim Ali Mbunge wa Jimbo la Wete akiuliza swali kwenye semina. Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Konga, Mhe. Mbarouk Ali akisikiliza kwa makini. 
  Meneja wa TRA kwa upande wa Kisiwani Pemba Bw. Habibu Saleh naye akiuliza swali kwa mtoa mada, Bw. Suleimani (hayupo pichani). 
  Bw. Salehe akijibu maswali hayo na kutolea ufafanuzi kwa baadhi ya mambo. 
  Serikali ya Zanzibar inashiriki moja kwa moja bila ukomo katika masuala yote ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hivyo Wazanzibari wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo na kuondokana na dhana kuwa eti, Serikali yao inabaguliwa.

  Akiwasilisha mada leo kuhusu ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye semina ya masuala ya mtangamano wa EAC inayofanyika Pemba, Afisa wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Bw. Suleima Haji alitoa ufafanuzi wa kina kuonesha namna Zanzibar inavyoshiriki katika EAC.

  Bw. Haji alieleza kuwa licha ya Zanzibar kuwa sehemu ya muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ushiriki wake umedhihirika katika mgawanyo wa miradi ya maendeleo ya EAC, hususan miradi ya Miundombinu. Alisema Zanzibar iliwasilisha mapendekezo ya miradi 10 kwenye Sekretarieti ya EAC na kutokana na vipaumbe vilivyowekwa miradi 3 imekubaliwa na mchakato wa kuitekeleza unaendelea. Miradi hiyo ni ujenzi wa Bandari ya Marhubi kisiwani Pemba, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ununuzi wa meli kubwa zitakazosafirisha abiria na mizigo kwenye nchi wanachama wa EAC.


  Aidha, kwenye miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar haijasahaulika. Zanzibar inanufaika na miradi inayofadhiliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya kukuza biashara na kupunguza umasikini katika nchi za EAC inayoitwa "East Africa Trademark" (TMEA). TMEA ambayo ni mdau mkubwa wa EAC inafadhili mradi ambao unawawezesha Wazanzibari kufanya maombi kwa njia ya mtandao ili kupata cheti cha uasili wa bidhaa. Cheti hicho ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani kinatambulisha bidhaa yako ilipotengenezwa na kupata msamaha wa kodi ya forodha inapoingia nchi nyingine za EAC. 

  Mradi mwingine unaofadhiliwa na TMEA huko Zanzibar ni ule wa kuwasilisha malamiko kwa njia ya mtandao au ujumbe mfupi wa simu pale inapotokea mfanyabiashara amekumbana na vikwazo visivyo vya forodha katika kusafirisha bidhaa zake ndani ya Jumuiya. Ujumbe huo utakapopokelewa, kikwazo kilicholalamikiwa kitafanyiwa kazi na taasisi husika mara moja.

  Benki ya dunia pia inaendesha mradi wa kutathmini utekelezaji wa Soko la Pamoja kwa upande wa Zanzibar. Kama inavyotambulika soko la pamoja lina vipengele vingi vikiwemo; usafirishaji huru wa bidhaa, huduma, mtaji na watu. Hivyo kuna umuhimu wa kupima namna nchi wanachama zinavyotekeleza vipengele hivyo.

  Ushiriki wa Zanzibar unapatikana pia kwenye uenyeji wa taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar imebahatika kuwa mwenyeji wa Kamisheni ya  Kiswahili ya EAC. Kuwa mwenyeji wa taasisi kuna faida kubwa zikiwemo kujitangaza na ajira. Kwa upande wa ajira, Bw. Haji alisema sio tu Wazanzibari wanafaidikia na ajira za Kamisheni ya Kiswahili, bali wanapata ajira hata katika Sekretarieti ya EAC na kutolea mfano kuwa Mhasibu Mkuu wa kwanza wa Sekretarieti hiyo alikuwa Mzanzibari.

  Vile vile, Zanzibar imekuwa mwenyeji wa vikao mbalimbali vya taasisi za Jumuiya. Mwaka 2010 Mahakama ya Afrika Mashariki ilifanya kikao chake Zanzibar, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) lilifanya kikao chake Zanzibar mwaka 2016 na mwezi Agosti mwaka huu utafanyika mkutano mkubwa wa masuala ya Kiswahili mjini Zanzibar. Aliendelea kusema kuwa katika Bunge la EALA la kipindi hiki, Zanzibar ina wabunge watatu, wawili wakitokea CCM na mmoja CUF. 

  Alihitimisha mada yake kwa kuwasihi Wazanzibari waache fikra potofu za kujihisi kubaguliwa badala yake waunganishe nguvu kuchangamkia fursa lukuki za kibiashara zilizopo kwenye mtangamano wa EAC. Alisema Serikali ya Zanzibar inashiriki katika kila jambo ikiwemo kushiriki mikutano ya Marais. Mawaziri na Wataalamu ili kutetea maslahi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

  Dar es Salaam, 18 Mei, 2017

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
  Baadhi ya Wanachama wa CCM Jimbo la Ilala wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Ilala kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa CCM Ilala baada ya kuzungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

  0 0


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.
  Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari,mapema leo jijini Dar kuhusiana na kampeni yao wanayotarajia kuianza hivi karibuni.

  Waandishi wa habari wakisikiliza maeleoza mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi kuhusiana na namna kampeni hivyo itakavyofanyika.

  Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo na namna wanavyoweza kutoa huduma ya ushauri mbalimbali kwa wateja wao,Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi.

  Bw. Manongi, (kushoto), akiwa na Bw.Luteganya.
   

  MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

  Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.

  Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.

  Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4) na kujishindia zawadi mbalimbali.

  Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.

  Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.

  “Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema. 

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya mkononi Halotel wamekiri makosa yalitokea na wameahidi kufuata sheria za nchi katika utoaji wa Huduma kwa wananchi.

  Kampuni hiyo imesema, itahakikisha inashirikiana na serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano kwa watanzania wote, vijijini hadi mjini.

  Mkurugenzi mtendaji wa Halotel Le Van Dai, amesema hayo leo ofisini kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inaikabili kampuni hiyo na aliyekuwa mkurugenzi wao Do Manh Hong.

  Amesema, katika kesi hiyo kulikuwa na mashtaka saba, lakini wao walihusishwa katika vipengele viwili tu ambavyo ni kushindwa kutoa taarifa za usajiri wa kampuni ya Unex ambayo ilisajili laini 1000 walizouza na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa kuiuzia kampuni hiyo laini za simu wakati ikiwa haijasajiliwa na kutokuwa na kibali cha TCRA.Kwa kutumia mwanya huo Unex walisimika mitambo ambayo ilisababisha hasara ya milioni 459 kwa serikali.

  Amesema, Halotel pamoja na kwamba walikuwa wakishtakiwa pamoja na raia saba wa Pakistani walilipa faini iliyokuwa ikiwahusu wao na hasara hiyo kwa kuwa hawan uhusiano wowote na hao waliobaki.

  "Mitambo iliyotumika kuiba mawasiliano ya simu haikuwa yetu, hatukufahamu kama Wateja wetu Unex, walitumia mitambo hiyo kuiba mawasiliano lakini hatuna uhusiano wowote na washtakiwa wengine ambao tumehusishwa nao na hata mitambo iliyotumika siyo ya kwetu" amesema Leo Van Dai.

  Ameongeza kuwa Halotel haihusiki kwa vyovyote vile na mashtaka yanayowakabili raia hao wa Pakistani kama vile kusimika mitambo ya mawasiliano kwani wao wanafanya kazi zao kwa kufuata taratibu na sheria za nchini.

  Aidha mkurugenzi huyo ametanabaisha kuwa, Halotel imeazimia kufanikisha jitihada za serikali katika kutoa huduma bora za mawasiliano na kuwa wanatarajia kuunganisha vijiji zaidi ya 1500 katika mwaka huu wa fedha kuongeza ufanisi wa huduma za mawasiliano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel ,Le Van Dai akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa kesi iliyokuwa inawakabili katika mahakama ya Kisutu iliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Wakili wa Halotel, Fatuma Seif na Kulia ni Wakili Christopher Masai

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah (aliyesimama) akiwakaribisha ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB).
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah (aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ulipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Ugeni huo upo visiwani Zanzibar kuangalia maeneo ya uwekezaji visiwani humo. 
  Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (wapili kushoto) na Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia).
  Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
  Mkuu wa Msafara wa TADB, Bibi Rehema Twalib (katikati) ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi wa Benki hiyo akihimiza jambo wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa TADB, Bw. Hussein Mbululo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah (kulia).
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akieleza dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini Tanzania.
  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kushoto) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati walipotembelea viongozi na wajumbe wa Bodi ya TADB walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Sera na Utafiti, Bw. Sheha Idrissa Hamdan (aliyesimama kushoto) akizungumza wakati Ugeni wa Benki ya Kilimo ulipotembelea wizarani hapo.
  Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.


  Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imeanza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo visiwani Zanzibar kwa kuanza mchakato wa kutoa mikopo kwa wakulima na wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha katika uchakataji wa mazao ya kilimo visiwani humo.

  Akizungumza wakati wa walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, visiwani humo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

  “Uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.

  Bw. Assenga amesema Zanzibar ina utajiri mkubwa kwenye uzalishaji wa viungo ‘spices’ ambayo ni mojawapo wa minyororo ya thamani ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali na Benki ya Kilimo.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah ameishukuru Benki hiyo kwa kuiangalia Zanzibar kuwa sehemu ya kimkakati na kutaka kuanza mikopo visiwani humo.

  0 0

   It is with deep sorrow that the family of Dr Honesmo Balilonda Kaganda of The Kairuki Hospital in Dar Es Salaam, announce the death of their beloved wife, mother, sister, friend and colleague, DR SUBILAGA KASISELA KAGANDA. Dr Subi passed away in India while on treatment on the 17th May 2017. Her funeral will be held in Dar-es-Salaam on Saturday, May 20th 2017 at Msasani Lutheran Church at 12 midday followed by her burial at Kinondoni Cemetery. May her Soul Rest In Peace. Hebrews 13:14-16

  0 0


  Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Yohana Mabena akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo wao kwa wadhamini wakuu, kampuni ya Mabibo Beer. Kulia ni msemaji wa kampuni ya Mabibo Beer, Andrea Missama na kushoto kwa Mabena ni Waziri wa Michezo wa Ustawi, Ashura Jingu. Nyuma ni warembo wa miss Ustawi 2017.
  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul akizungumza akizungumza wakati wa kutambulishwa kuwa msanii wa kutumbuiza katika mashindano Miss Ustawi 2017 yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, jijini.

  Miss Ustawi anayemaliza muda wake Evelyn Andrew akizungumza wakati wa utambulisho wa warembo hao kwa wadhamini wakuu. Evelyn anavua taji hilo, Ijumaa (Mei 19) wakati wa mashindano ya kumsaka mrembo wa chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga.


  Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na Miss Ustawi anayemaliza muda wake, Evelyn Andrew. Warembo hao watapambana Ijumaa (Mei 19) wakati wa mashindano ya kumsaka mrembo wa chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga.

  …………………………..

  Na Mwandishi wetu

  Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya nchini, Ben Paul atatumbuiza katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (Miss Ustawi) yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini.

  Mratibu wa mashindano hayo, Catherine Boniface alisema kuwa Paul ambaye anatamba na wimbo wa Moyo Machine, Phone na nyinginezo nyingi, pia atatambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki nyota nchini, Darasa.

  Mashindano hayo yamedhaminiwa na kinywaji cha Windhoek, yatashirikisha jumla ya warembo 12 ambao walikaa kambini kwa muda wa wiki mbili wakijifua chini ya mwalimu wao, Clara Michael na matron, Catherine Boniface.

  Warembo ambao wamepitishwa na kamati ya mashindano hayo ni Fatma Kivea, Elice Mwakajila, Melody Thomas, Diana Mwaibula, Hapifania Shedoekulu, Careen Kileo. Wengine ni Angelina Michael, Ruth Deogratius, Consolator Samwel, Loyce Jeck na Elizabeth Julius.

  Washindi watatu wa mashindano hayo watapata nafasi ya kushindana katika shindano la warembo wa elimu ya juu (Miss Higher Learning Institution) ambapo warembo watatu wa kwanza watafuzu katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.

  Mratibu wa mashindano hayo, Catherine Boniface alisema kuwa warembo watapanda jukwaani wakiwa wanashindania vazi la ubunifu, ufukweni na usiku na warembo watano watakaopita katika mchujo wa kwanza watajibu maswali.

  “Morali ya warembo ipo juu, kila mmoja ni mshindi, lengo letu ni kushinda taji la vyuo vya elimu ya juu na kutwaa taji la Miss Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya urembo nchini,” alisema Catherine.

  Msemaji wa kampuni ya Mabibo Beer inayodhamini shindano hilo, Andrea Missama amesema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo kama sehemu ya kampuni yao kukuza vipaji na kazi za jamii.

  Missama amesema kuwa warembo wengi wamejitokeza kushindania taji hilo ambalo mshindi wake atakiwakilisha chuo hicho katika mashindano ya urembo ya vyuo vya elimu ya juu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya ns viongozi wa halmashauri baada ya kumaliza kikao nao. 
  Mjumbe mwakilishi wa madhehebu ya dini sheikh Salum Ngaa akichangia hoja wakati wa kikao kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu pichani wakiwa na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 
  Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akichangia hoja wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akitoa maelekezo wakati alipokutana na kamati ya mfuko wa elimu ya wilaya. 

  …………………………….. 

  MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amekutana na kamati ya mfuko wa elimu wilaya na kuwaomba kuwa wazalendo katika kutafuta njia za kutatua changamoto za elimu wilayani humo. 

  Mfuko huo umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni. 

  Akizungumza katika kikao cha kuwapatia majukumu yao Mtaturu amesema mfuko huo utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari. 

  “nawapongezeni kwa heshima mliyopewa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hii,naimani kuwa mtafanya kazi kwa uzalendo mkubwa ili matunda ya uwepo wenu yaonekane kwa kuitoa elimu yetu hapa ilipo na kuipeleka mbali zaidi,”alisema Mtaturu. 

  Alisema wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia walipokutana wadau wa elimu. 

  Akitoa taarifa kwenye kikao hicho katibu wa mfuko huo Salum Athuman alisema ili kutatua changamoto za elimu zilizopo katika wilaya hiyo zinahitajika jumla ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,maabara,matundu ya vyoo na mabweni. 

  Aidha mwenyekiti wa kamati hiyo Hamis Maulid kwa niaba ya wajumbe alisema wamepokea kazi hiyo na wataifanya kwa uadilifu mkubwa ili malengo yaliyokusudiwa yatimie. 

  Disemba mwaka jana mkuu wa wilaya huyo alikutana na wadau wa elimu ili kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambapo waliweka maazimio yapatayo 37 yenyek ulenga kuboresha elimu wilayani humo na moja ya mkakati waliouweka ndio umezaa wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wenye wajumbe 15 ambao wameanza kazi rasmi ili kutafuta njia ya kutatua changamoto za elimu wilayani humo. 

  Wilaya hiyo ina jumla ya shule za sekondari 30 ikiwemo za kidato cha sita 3 na shule za msingi 108.

  0 0

  Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana.
  Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake.
  RTO Mkoa wa Singida Mrakibu wa polisi Peter Raphael Majira akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani.

  MAELEZO YA PICHA.

  …………………..

  Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.

  Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

  Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.

  Amesema pia wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani. 

  Aidha RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

  Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si kuchangia kiti.

  “Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.

  Kwa upande wao madereva hao wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Singida kwa kuendesha ukaguzi huo na kuwakumbusha juu ya sheria za usalama barabarani.

  Mmoja wa madereva wa mabasi ya wanafunzi Mkoani Singida Pyuza Gyumi amesema kwenye mafunzo hayo ya muda mfupi wameagizwa kwamba ni marufuku wanafunzi kuchangia kiti kimoja kwa madai ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani.

  “Tumekumbushwa kwamba wakati tukiwa barabarani tuwe makini wakati wote wa kuendesha na tuwe na utulivu wa hali ya juu. Pia tumekumbushwa kuwa makini wakati tunavusha kwa miguu wanafunzi ng’ambo yingine ya barabara. Kwa ujumla binadamu anatakiwa mara kwa mara akumbushwe wajibu wake hii itasaidia kufanya kazi zetu kwa ufanisi”, amesema.

  Aidha amesema jeshi la polisi kuwakutanisha na waajiri wao itasaidia kupunguza kero mbalimbali zinazowakabili kati yao na waajiri wao.

  “Kuna wakati tunashindwa kuelewana na matajiri wetu wakati wanapotulazimisha kutenda mambo ambayo ni nje ya sheria za usalama barabarani. Baada ya mafunzo haya ya muda mfupi waajiri wenye tabia hizo watabadilika na kutuunga mkono uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani”, amesema Gyumi.

  0 0

  Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.

  Mkutano huo utatanguliwa na mikutano ya kamati tendaji za SARPCCO kabla ya kufunguliwa rasmi Mei 24, 2017 na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.

  Vilevile, mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo.

  Aidha suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.

  SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.  Imetolewa na:-
  Advera Bulimba-ACP

  Msemaji wa Jeshi la Polisi.
  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0   Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  8950-Mhagama na Makamba
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba   katika kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  8987-Mhe.Kijaji
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  8994-Mhe.Makamba
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  9004-Naibu Waziri wa Habari
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  9090-Mhe.Manyanya
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng.Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  9046-Mhe.Mwakyembe
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  9110-Waziri Mwakyembe na Naibu Waziri
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na Naibu wake Mhe.Anastazia Wambura  katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
  9234-Mhe.Kigwangala
   Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.

  Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 amefanya mazungumzo na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
  Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifatilia  kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017
  Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg john Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kika na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda akisisitiza jambo

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Imebainika kuwa zipo kauli zisizo rafiki zinazotolewa Na watumishi wa Umma dhidi ya wananchi katika Jiji la Dar es salaam wanaozuru katika Ofisi mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali kutokana Na mambo yanayowakabili.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda amebainisha hayo Leo Mei 18, 2017 Wakati akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

  Mhe Makonda amesema kuwa mtumishi wa serikali ambaye atabainika kutumia lugha ambazo sio rafiki kwa wananchi atachukuliwa hatua za kinidhamu Mara baada ya kubainika kwani kufanya hivyo ni kufifisha uaminifu wa wananchi dhidi ya serikali.

  Sambamba Na hayo pia RC Makonda amesema kuwa Kazi ya watendaji serikalini ni kutatua kero za wananchi japo wapo watendaji ambao wamegeuka Na kuanza kuongeza migogoro badala ya kutatua.

  Alisema kuwa baadhi ya watumishi wa Sekta ya ardhi wanamiliki kampuni zinazojihusisha Na mambo ya Ardhi Jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likipunguza ufanisi katika utendaji kwani wanatumia muda mwingi kufikiri kuhusu kampuni zao kuliko kuwatumikia wananchi serikalini.

  Ametoa wiki moja kwa watumishi wote wanaomiliki kampuni hizi kuamua moja ama kubali wakifanya Kazi serikalini Na kuachana Na kampuni binafsi ama kubakia katika kampuni zao Na kuacha kazi serikalini.

  "Watumishi hawa hutumia vifaa vya serikali kwenye miradi yao Jambo ambalo hupelekea uchakavu Na uharibifu wa haraka wa vifaa vya serikali hivyo zuio langu hili linajikita kuwataka watumishi wa Umma katika Mkoa wangu kujikita katika utendaji wa shughuli za serikali" Alisema Mhe Makonda.

  Alisema Ardhi Na Ujenzi ni moja Kati ya Idara zenye matatizo mengi katika Mkoa wa Dar es salaam hivyo ametoa msisitizo vibali vya Ujenzi kutolewa haraka ndani ya mwaka mmoja kwani kuchelewesha kunapelekea wananchi wengi kujenga bila utaratibu.

  Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia kwa watendaji wa Sekta hiyo ya Ardhi Na Ujenzi ambayo ni pamoja Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu, Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017 huku Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kukitarajiwa kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.

  Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari, kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo, kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama vile Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na kutoa Mikakati wa Upimaji.

  Maelekezo mengine ni pamoja Na Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi, Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka Na Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.

  Pia Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamana aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki, Watumishi wote kusimamia Na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano, Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema ilani hiyo.

  Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na kwenda likizo, Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika, Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi Na Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

  RC Makonda pia ameelekeza wakuu wa Idara Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea, Wakuu wa Idara kila.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira (Katikati) akiongoza Kikao kazi cha Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji (hawapo pichani). Wa pili kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(wa pili toka kulia) ni Kamishna wa Uhamiaji – Zanzibar, Johari M. Sururu(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA, Kamishna Maurice David Kitinusa(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Edward P. Chogero.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akitoa hotuba fupi kwenye Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kilichofanyika hivi karibuni Mjini Moshi.
  Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(hayupo pichani)kwenye Kikao kazi hicho kama inavyooneka katika picha.
  Kamishna wa Pasipoti na Uraia, Gerald Kihinga akitoa ufafanuzi katika Kikao kazi cha Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji mbele ya Katibu Mkuu Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Moshi.
  Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Samuel R. Magweiga akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) katika kikao hicho.  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira kukagua moja ya majengo mbalimbali ya Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Idara ya Uhamiaji(waliosimama). Wa pili toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(wa pili toka kulia ni Kamishna wa Uhamiaji – Zanzibar, Johari M. Sururu(wa kwanza kulia)ni Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA, Kamishna Maurice Kitinusa(Picha zote na:- Kitengo cha Uhusiano Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA Moshi, Kilimanjaro)

  0 0

  Baadhi ya wananchi katika Kata ya Ifwagi wakiwa kwenye foleni kusajiliwa zoezi la Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Wilayani Mufindi.
  Maafisa wa NIDA wakiendelea na zoezi la uchukuaji alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki wakati wa zeozi la Usajili likiendelea kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi.
  Afisa Usajili mkoa wa Iringa bwana George Mushi akizungumza jambo na wananchi wa Kata ya Ikongosi wakati wakisubiri kupata huduma ya usajili vitambulisho vya Taifa (NIDA)  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi akizungumza jambo na Afisa Usajili Mkoa wa Iringa bwana George Mushi kabla ya kuanza zoezi la usajili wa Wananchi katika Kata za Ifwagi, Ikongosi na Ihalimba.
  Maafisa wa JKT na NIDA wakipokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Mhe. Jamhuri William kabla ya kuanza utekelezaji wa zoezi la Usajili
  Wananchi wakipokea maelekezo ya namna ya kushiriki zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani Mufindi.
  ………………………….

  Wananchi wa Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kusajili Vitambulisho vya Taifa kufuatia maelekezo ya Mkuu wa mkoa huo Mhe. Amina Masenza ambaye amejizatiti kuweka historia ya kuwa mkoa wa kwanza kwa wananchi wake kuwa na Vitambulisho vya Taifa; baada ya kufanikisha kwa asilimia kubwa zoezi la kuwasajili Watumishi wa Umma lililofanyika nchi nzima.

  Kwa kuanza; zoezi la Usajili kwa mkoa wa Iringa limeanza katika Wilaya ya Mufindi ambapo zaidi ya wananchi 70,000 wameshajiliwa katika Kata 20 kati ya Kata 36 zilizopo Wilaya humo, huku wananchi 50,000 wakiwa tayari na Vitambulisho vya Taifa.

  Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa zoezi hilo; Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ambako zoezi hilo linaendelea kwa sasa Mhe. Mhe. Jamhuri William amesema “kama Wilaya wamejipanga kuhakikisha zoezi la kuwasajili wananchi linafanyika katika muda mfupi iwezekanavyo na kwamba uhamasishaji umefanyika kwa njia mbali mbali kuhakikisha wananchi wanatumia vema fursa Iliyopo”

  Amesisitiza mbali na kuwasajili wananchi; Wilaya ya Mufundi pia inaendelea na zoezi la kuwasajili Wageni na Wakimbizi wanaoishi kihalali Wilayani humo, lengo likiwa ni kupata taarifa sahihi za watu na kuimarisha upatikanaji wa huduma kiurahisi kwa wananchi.

  Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amina Masenza alizindua kuanza kwa zoezi la usajili mkoa wa Iringa na kuelekeza kwa kushirikiana na NIDA kila Wilaya kuhakikisha ndani ya siku 60 kuwa wamekamilisha zoezi la kuwasajili wananchi Vitambulisho vya Taifa; na kuwahakikishia wananchi Ofisi yake itahakikisha wananchi wote wakaosajiliwa wanapata Vitambulisho vyao kwa wakati ili matumizi kuanza mara moja.

  Tayari Mamlaka imeanza mipango ya kuunganisha watoa huduma mbalimbali kwenye mfumo, ili Vitambulisho vya Taifa kuanza kutumika katika huduma mbalimbali pamoja na kuimarisha ulinzi na Usalama katika Mkoa wa Iringa.

  Katika mkoa wa Iringa zoezi la kuwasajili wananchi limekuwa likifanywa kwa ushirikiano na kikosi cha JKT ambao wamepata mafunzo ya namna ya kuendesha zoezi la Upigaji picha na uchukuaii alama za kibaiolojia.

  Ndg George Mushi Afisa Usajili mkoa wa Iringa; amesema kwa sasa zoezi linaloendelea lihahusu Kata za Ifwagi, ikongosi pamoja na Ihalimba.

  “Wananchi wanaosajiliwa ni wale wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ikihusisha ujazaji fomu, uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya Kielektroniki na uhakiki wa taarifa kwa kila mwombaji. NIDA imejipanga kuhakikisha katika kila hatua vitambulisho vinatolewa mapema iwezekavyo ili kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho hivyo katika huduma mbalimbali” alisisitiza.

  Nyaraka muhimu zinazohitajika katika kuthibitisha uraia, umri na makazi ya mwombaji ni pamoja na Cheti cha Kuzaliwa, Vyeti vya Shule ya Msingi na Sekondari, Elimu ya Juu, Leseni ya Udereva, Kadi ya Mpiga kura, Kitambulisho vya Bima ya Afya, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, pamoja na pasi ya kusafiria (Passport).

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

  Serikali imeeleza kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijawahi kumuhusisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukaguzi wa Balozi au ukaguzi wowote ule kama Umoja wa Mataifa kwa sababu hakuna ulazima wa kufanya hivyo Kikatiba na Kisheria.

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kiwengwa Khamisi Mtwana Ally (CCM), aliyetaka kujua ni mara ngapi Ofisi hiyo ya Bara imeishirikisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Zanzibar.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Ofisi hizo kila moja ina mipaka yake ya kufanya ukaguzi na kwamba jukumu la ukaguzi wa Taasisi za Muungano lipo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba majukumu ya Ofisi hiyo yameainishwa katika ibara ya 143(2) ya katiba hiyo”. Alisema Dkt. Kijaji

  Dkt Kijaji aliongeza kuwa, eneo hilo linamtaka Mdhibiti na Makguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi angalau mara moja kila mwaka na kutoa taarifa kuhusu ukaguzi wa Hesabu za Serikali, Bunge na Mahakama.

  Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa majukumu hayo yameainishwa katika kifungu cha 10 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 na kanuni zake za mwaka 2009.

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa, ukaguzi wa Balozi unafanyika chini ya fungu 34, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwa Ofisi zote za Ubalozi ni sehemu ya fungu 34.

  “Hivyo basi, ukaguzi wa Balozi kama ilivyo kwa Taasisi nyingine za Muungano unafanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .”alisema Dkt. Kijaji

  Aliongeza kuwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Zanzibar, majukumu yake yameainishwa kwenye ibara ya 112 ya Katiba (3) ya katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1984.

  Akiongeza majibu ya swali hilo, Waziri wa Mazingira na Muungano, Januari Makamba alisema kuwa wakaguzi wa pande zote kutoka Tanzania Bara na Visiwani hufanya kazi kwa kushirikiana katika mambo ya ukaguzi wa hesabu za serikali.

  Katika swali la nyongeza Mbunge wa Mkwajuni, Ally Zubeir Ngwali (CUF), alihoji ni kwanini fedha za mfuko wa Jimbo hazijawahi kukaguliwa na zitakaguliwa kwa utaratibu upi.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo alisema upo utaratibu maalum wa kushughulikia mambo hayo. 
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji

  0 0

  Na Tiganya Vincent-Kaliua
  18.5.2017

  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiako wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Celestine Mushi ametoa wito kwa 
  Mashirika Kimataifa na Umoja wa Ulaya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwasaidia atanzania wapya (waliokuwa wakimbizi wa Burundi) kuhakikishwa anaunganishwa na jamii ya Watanzania mara baada ya kupata uraia.

  Balozi Mushi ametoa kauli hiyo jana katika eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua wakati alipokuwa na Ujumbe wa Mabalozi kutoka Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo Uingereza.

  Alisema kuwa baada ya Serikali kuwapatia waliokuwa baadhi ya wakimbizi wa Burundi Uraia ni vema nchi hizo na Mashirika ya Kimataifa yakasaidia kuongeza raslimali mbalimbali ambazo zitaisaidia Serikali iweze kuwaunganisha vizuri raia hao wapya na raia wengine hapa nchini.

  Balozi Mushi aliongeza fedha za Serikali pekee hazitoshi kukamilisha zoezi la kuwaunganisha raia hao kwasababu yapo mahitaji ya wananchi mengine hapo nchini yanayotegemeza hizo fedha kidogo inazokusanya kutokana na vyanzo vyake mbalimbali vya mapato na hivyo ni vema nao wakasaidia kwa upande wao.

  Alisema kuwa kimsingi raia hao wapya wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, uhaba wa vifaa tiba, zahanati , kutokuwa na miundombinu ya kutosha ya elimu na kukosa elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango.

  Alisema kuwa kukosekana kwa elimu ya kutosha kumewafanya wakazi hao wawe na familia kubwa ambazo hawawezi wakati mwingine kuziwezesha katika huduma za jamii.

  Balozi Mushi alisisitiza kuwa kutozingatiwa kwa elimu ya uzazi wa mpango kumelifanya eneo hilo kuwa na wananchi wanaozaliana kwa wingi kuliko maeneo mengine ya Mkoa wa Tabora jambo linalofanya huduma za jamii kuwa kidogo ukilinganisha na idadi ya watu wa hapo.

  Alisema kuwa ni vema wadau wakaona ni wapi wanaweza kushirikiana na Tanzania katika kuwasaidia raia hao wapya katika kuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Dkt. John Pima alisema kuwa wastani wa raia kuzaana katika eneo la Ulyankulu ni asilimia 5.4 na hivyo kufanya kuwepo na idadi ya watu wengi katika eneo moja ambao hawawiani na huduma za jamii zilizopo.

  Alisema kuwa hatua inasabaisha kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa ,hatua iliyoilazimu Halmashauri hiyo kujaribu kuwahamishia katika maeneo mengine watoto hao ili wapate elimu.
  Dkt. Pima aliongeza kuwa kuhusu elimu ya uzazi wa mpango wamekuwa wakijitadi kuitoa lakini bado kasi ya uzalianaji ni kubwa na hivyo juhudi zaidi zinahitajika.

  Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Huduma ya Wakimbizi Suleman Mziray ujumbe wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya umekwenda Ulyankulu ili kujionea hali halisi na kuangalia jinsi gani wanaweza kuisadia Serikali ya Tanzania katika kutengamanisha waliokuwa Wakimbikizi ambao wapata uraia na Watanzania wengine.

  Alisema kuwa mabalozi hao wamekuwa na Umoja wao unajulikana kama Solutions Alliance ambao lengo lake ni kutafuta suluhusho la kuduma kwa wakimbizi.
  Mziray aliongeza kuwa ziara ya Mabalozi hao ilikuwa muhimu ili waweze kuona wapi wanaweza kusaidia katika kuboresha kundi hilo.

  Aidha , alitoa wito kwa Watanzania hao wapya kuanza kuangalia uwezekano wa kuhamia katika maeneo mengine ya kuishi ili kuepuka tatizo la ukosefu wa huduma za jamii kama maji na elimu.
  Serikali ya Tanzania imetoa uraia kwa wakimbizi wa Burundi 162,000 walioishi nchini 1972 na kuwa Watanzania.

  Ujumbe huo wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya nchini umesema utakwenda kukaa na baadaye ndio utatoa majibu iwapo wanaweza kusaidia na ni eneo gani.

  0 0


  0 0


  Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam umefikia tamati. Mkutano huu uliofanyika katika Hoteli ya Serena umehudhuriwa na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama, watendaji mbalimbali kutoka Wizara, mashirika ya umma, Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na taasisi mbalimbali za Serikali ndani ya Jumuiya. 

  Pamoja na mambo mengine Mkutano huu ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuandaa agenda zinazo hitaji maamuzi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Agenda hizo zinatokana na taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya wa mwaka 2015/2016, iliyo andaliwa na Mkutano wa ngazi ya wataalamu. 

  Baadhi ya mambo yaliyopo kwenye taarifa hiyo ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2015/2016 ambayo imekabidhiwa kwa Baraza la Mawaziri yanajumuisha mambo yafuatayo;

  · Taarifa ya namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya

  · Taarifa ya mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi juu ya kuzuia/kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika na; 
  · Taarifa ya namna endelevu ya Uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

  Aidha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari punde baada ya mkutano amesema Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri umekuwa na mafanikio makubwa kwanza, kutokana na idadi kubwa na yakuridhisha ya wajumbe walioshiriki Mkutano kutoka nchi wanachama ,na pili ni kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatika katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa Jumuiya hadi sasa inapokabidhi kwa nchi ya Jamhuri ya Uganda. 

  Mfanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uwenyekiti; 

  Waziri Mahiga ameyataja mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya kuwa ni; kuongezeka kwa nchi ya Sudan Kusini katika Jumuiya, kuboreka kwa mfumo wa elimu kwa ngazi ya elimu ya juu katika Jumuiya na kupungua kwa vikwazo vya biashara vinavyotokana na vikwazo visivyokuwa vya kiforodha ndani ya Jumuiya vilivyopelekea kurahisisha na kuhamasisha baishara katika Jumuiya. 

  Mkutano huu wa Baraza la Mawaziri utafuatiwa na Mkutano wa 18 wa Kaiwada wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uanaotarajiwa kufanyika tarehe 20 Mei, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

  Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Wakuu wa nchi unatarajiwa kupokea ripoti ya usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa. 

  Tanzania ilikabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya mwishoni mwa mwaka 2014 katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Nairobi, Kenya; na ikapewa tena nafasi ya kuendelea kushikilia kiti hicho mwaka 2015, ambapo mpaka sasa Tanzania wakati inaelekea kukabidhi nafasi hii ya uwenyekiti kwa nchi ya Uganda, Tanzania imekuwa mwenyekiti wa Jumuiya kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo. 
  Waheshimiwa Mawaziri wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Afrika Mashariki unapigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wamasuala ya Afrika Mashariki wa Uganda Mhe.Dkt.A.M Kirunda Kivejinja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (wakwanza kushoto) akifuatilia Mkutano. 
  Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Pindi Chana (wakwanza kushoto) akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki 

  0 0


older | 1 | .... | 1236 | 1237 | (Page 1238) | 1239 | 1240 | .... | 1898 | newer