Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumz na Mbunge wa Kavuu, Dkt. Pudenciana Kikwembe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WADAU WA ELIMU TANZANIA WAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE - HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII KUWASILISHA MAPENDEKEZO YA ELIMU

$
0
0
Picha ya pamoja ya wadau wa elimu Tanzania na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge, huduma na Maendeleo ya Jamii baada ya kikao cha kuwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka wa fedha 2017/2018 uliofanyika katika ukumbi mdogo wa bunge mjini Dodoma.

Baada ya Kikao hicho wanakamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii waliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa elimu ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii, Mhe. Azzan Zungu akifungua kikao na kuwakaribisha wadau wa elimu waliofika katika mkutano huo ili kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18.
Kiongozi wa wadau wa elimu Tanzania(Head of Deligation) , Ndugu Saddam Khalfan akielezea madhumini ya kikao hicho kilichokuwa kinahusiha kuwasilisha mapendekezo na maoniya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18 kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Ndugu Karoli Kadeghe kutoka ACTIONAID Tanzania akiwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu kuhusu serikali kuongeza uwekezaji wa fedha za ugharamiaji elimu kupitia rasilimali za ndani ili kuepukana na utegemezi wa fedha za wahisani kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.

Pia aligusia umuhimu wa uwekezaji wa miundombinu ya shule na kuboresha maslahi ya walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Katibu mtendaji wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania, Ndugu Alphonce Lusako akihimiza na kuishauri kamati ya bunge kuisimamia serikali kutoa bajeti ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wote wenye sifa wanaodahiliwa vyuo vikuu nchini bila ubaguzi wowote. Bajeti husika ijikite katika maboresho ya mafunzo kwa vitendo kazi (Internship), mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Pia aliiomba kamati hiyo kutoa pendekezo kwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kuweka utaratibu thabiti na endelevu wa Kukusanya fedha za mikopo kwa wanufaika waliokwisha nufaika na mikopo hiyo ilikuongeza Wigo wa kuwapa mikopo wanafunzi wapya wa vyuo vikuu nchini. 

Pia tunaiomba serekali Ilitazame upya suala la ukusanyaji wa madeni ya walionufaika na mikopo, kubadilisha ghafla Makusanyo toka asilimia nane (8%) hadi asilimia kumi na tano(15%) ni kuvunja mkataba wa mkopaji na mkopeshaji, jambo hili linavunja sharia. Kama ni lazima kufanya hivyo basi makusanyo hayo ya asilimia kumi na tano (15%) yaanzie kwa hawa wanaokopeshwa sasa ili wakope wakiwa wanalijua hilo.
Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa elimu Tanzania(Ten Met) wakichangia mada kuhusu bajeti ya elimu katika masuala kama kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurudi mashuleni, upungufu wa madarasa pamoja na vitendea kazi vya elimu.
Wajumbe wakiangalia video ya hali halisi ya baadhi ya shule nchini pamoja na makazi ya walimu iliyoandaliwa na ActionAid Tanzania na Ten Met.

YANGA YAMWAGIWA MABILIONI YA UDHAMINI NA SPORTPESA LEO

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Mkamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga ukiwa ni mkataba wa miaka kitano wenye thamani ya zaidi bilioni 5, uwekaji huo wa saini na makabidhiano yamefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas na kushoto ni Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Charles Mkwasa.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya mkataba wa udhamini baina ya Klabu ya Yanga na Kampuni ya Michezo ya kubahatisha ya SportPesa ya nchini Kenya, uwekaji huo umefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya Nchini Kenya SportPesa imeimgia mkataba na klabu ya Yanga wa udhamini wa miaka mitano ukiwa na thamani ya takribani bilioni 5.

Uwekaji huo wa saini umefanyika leo katika makao makuu ya Klabu ya Yanga ukishuhudiwa na wanachama mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Makamu Mwenyekiti Clement Sanga.

Akizungumza baada ya kutia saini hati ya makubaliano ya mkataba huo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Sanga amesema kuwa mkataba huu utakuwa na faida kubwa sana kwa klabu kwani wameweza kuongelea mambo mbalimbali ya kimaendeleo yakiwemo soka la Vijana.

Sanga amesema ni mara ya kwanza katika mikataba waliyowahi kuingia akiwa kama kiongozi umekuwa na viyi vingi sana vya kimaendeleo ukiachilia fedha wanazozipata za udhamini.

"katika mikataba tuliyowahi kuingia nikiwa kiongozi wa Yanga huu ni moja ya mkataba tuliozungumzia maendeleo ya klabu mbali na fedha tunazozipata ila tumeangalia katika Uwanja wetu wa Kaunda na hata soka la Vijana na mambo mengine mengi,"amesema Sanga.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas amesema Yanga watapata zaidi ya bilion 5 kwa miaka mitano na kwa mwaka wa kwanza wataanza kwa kupata milion 950 na itaongezeka kwa asilimia 5 kila mwaka na hii inakuwa klabu ya pili kuweza kuingia nao mkataba baada ya Simba kusaini wiki iliyopita.

Tarimba amesema makubaliano yao na Yanga yapo ambayo hayajawekwa wazi ni ya ndani ya klabu na si vizuri kuyasema ila kuhusu bonus zitakuwa sawa ambapo timu ikichukua ubingwa wa ligi au kagame au michuano yoyote ya kimataifa kutakuwa na fedha watakazopatiwa nje ya fedha ya udhamini.

Klabu Yanga inatarajiwa kufaidika na udhamini hasa kwa makubaliano waliyoingia ya kukarabatiwa uwanja wa mazoezi, kukuza vipaji vya soka la vijana pamoja na kupatiwa gari la wachezaji.





MHAGAMA KUFUNGUA MKUTANO WA BODI ZA MIFUKO YA HIFADHI JUU YA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, anatarajiwa kufungua mkutano wa Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania.

Mkutano huo unaoratibiwa na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) utafanyika Arusha Mei 19 na 20 mwaka huu,utahusu hatua iliyofikiwa mwaka huu na mada kuu, itakuwa uchumi wa viwana kama fursa ya uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Pia utaangalia hatua iliyofikiwa ya ushiriki wa mifuko hiyo kwenye uwekezaji wa viwanda na uchumi wa viwanda wenye tija.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Katibu Mkuu wa TSSA Meshack Bandawe alisema mkutano huo utakaofunguliwa na Waziri Mhagama, utashirikisha bodi nane za mifuko pamoja na wakuu wa mifuko hiyo ya hifadhi.

Alisema kwenye mkutano huo Bodi, Wakuu wa mifuko hiyo pamoja na wadau watapata fursa ya kujadili mafanikio , hatua na maendeleo yaliyofikiwa kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda nchini.

“ Kwenye mkutano huo tutaangalia mafanikio na hatua iliyofikiwa katika uwekezaji wa viwanda kama fursa muhimu hapa nchini ili uwekezaji wetu uwe na tija ambao utasaidia kukuza uchumi wa nchi na mifuko yenyewe ,”alisema Bandawe.

Katibu Mkuu huyo wa TSSA alisema kuwa mifuko hiyo imeanza utekelezaji kwwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya viwanda na baadhi iko kwenye upembuzi yakinifu.

Alidai kuwa miradi hiyo ikikamilika itatengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania ambao watakuwa wananchama wa mifuko yenyewe na hivyo kuwa na tija katika taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Bandawe nia ya mkutano huo ni kufikia lengo la uwekezaji wa viwanda na utahudhuriwa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Benki Kuu (BOT),Wizara ya Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango, Msajili wa Hazina na wadau wengine.

Bandawe alieleza kuwa TSSA inaundwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni NSSF, PPF,LAPF,PSPF, GEPF,NHIF,WCF na ZSSF.

KUNDI LA WASANII 7 MAARUFU KUTOKA CHINA NA WAPIGA PICHA 100 WAWASILI NCHINI KWA SHUGHULI ZA UTALII

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo akiwakaribisha Wasnaii hao katika Hotel ya Ramada Incore jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo  akikabidhi zwadi ya Tisheti kwa wageni hao ambao wamekuja kutalii nchini
Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo akiwa katika picha ya pamoja na wasnii kutoka nchini china

--
 Wasanii Maharu saba kutoka nchini China ,Lu Yi, Du Haitao,Yao Di,Tian Liang,Yin Zheng,Mai Dina na Hao Shaowen, wakishuka kwenye gari ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa Jijini Dar es Salaam wakitokea nchini  China  kwa ajili ya kutembelea mbuga za Wanyama hapa nchini na Vivutio vya kitalii.
 Msani kutoka nchini China,Yao Di akitoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya ziara maalum katika vivutio mbalimbali nchini
 Msani kutoka china  akicheza ngoma za Asili na kundi la Sanaa la Wanne Star
 Mmoja wa Wasanii kutoka nchini China akifurahi na kundi hilo la Wasaniiwa Wanne Star
 Wasanii Maharu saba kutoka nchini China ,Lu Yi, Du Haitao,Yao Di,Tian Liang,Yin Zheng,Mai Dina na Hao Shaowen wakicheza ngoma kwa pamoja na kikundi cha Sanaa za utamaduni hapa nchini cha Wanne Star
 Msani kutoka nchini China,Yao Di akicheza ngoma za asili na kikundi cha Wanne Star
 Wasanii hao wakipiga picha na nyoka
  Wasanii hao wakipiga picha na nyoka

  Wasanii hao wakipiga picha na nyoka

AZANIA TEAM YAKABIDHIWA BENDERA, VIZA, TIKETI NA VIFAA VYA MICHEZO TAYARI KWENDA ANFIELD, LIVAPOOL KUMENYANA NA MABINGWA WENGINE WA KINYAN'GANYIRO CHA STANDARD CHARTERED WAY TO ANFIELD NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Viongozi wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad (kushoto), Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Mohammed Bashrahili (katikati), wakiwa na Kocha wa timu hiyo, Saleh Afifi wakati wa hafla ya kukabidhi timu hiyo, bendera, Viza, Tiketi pamoja na vifaa vya michezo tayari kuelekea Jijini Liverpool, nchini Uingereza kwa ajili ya kinyan'ganyiro hicho na mabingwa wengine duniani pia kuona mchezo wa mwisho wa Ligi ya Uingereza kati ya timu ya Liverpool na Midlesbrough katika katika Uwanja wa Anfield jijini humo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, wakiwa katika hafla hiyo, Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad (wa tatu kulia), Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Mohammed Bashrahili (wa pili kulia) na Kocha wa timu hiyo, Saleh Afifi wakiwa pamoja na wachezaji wa timu hiyo, wa hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Standard Chartered, nchini Tanzania, Juanita Mramba, akizungumza katika hafla hiyo, kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, nchini, Balozi Ami Mpungwe (katikati), wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, nchini Tanzania, wadhamini wa timu hiyo, Balozi Ami Mpungwe akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, nchini Tanzania, wadhamini wa timu hiyo, Balozi Ami Mpungwe akizungumza wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Balozi wa Uingereza nchini. Bi. Sarah Cooke.
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Mmoja wa wakilishi wa benki hiyo, akitoa maelezo machache kuhusu safari hiyo, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, wakiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad (kulia), wamiliki wa timu hiyo, wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Deoniz Malinzi, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo, ya kukabidhi bendera, viza, tiketi na vifaa vya michezo kwa timu hiyo. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Balozi Ami Mpungwe.
Wachezaji wa Azania Team, wakiwa na baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa BMT, Deoniz Malinzi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Balozi Ami Mpungwe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke.
Nahodha wa timu hiyo, Khalid Said akielezea matumaini yake na jinsi walivyojianda kwa fainali hiyo, mashindano yatakayofanyika Uwanja wa Anfield jijini Liverpool, nchini Uingereza.
Mchezaji wa timu hiyo, Ahmed Afif, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Thomas Bishanga, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Rajb Ally, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Abdallah Khalid, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Bryan Donald, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Shabaka Khamis, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa nne kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke (wa tano), Balozi Ami Mpungwe (wa tatu) wa Benki ya Standard Chartered pamoja na Mwenyekiti wa BMT, Deoniz Malinzi (wa pili kushoto) na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini.



Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia anayefurahi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia anayefurahi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said (wa pili kushoto), akiwa ameishikilia Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mara baada ya kukabidhiwa. Wa pili kulia anayefurahi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo, akipongezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya mashindano ya fainali hizo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Nahodha  wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya mashindano ya fainali hizo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, Awadh Fuad.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo, Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke, Balozi Ami Mpungwe wa Benki ya Standard Chartered pamoja na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo, akiagana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, mara baada ya kumalizika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo, akiwa na baadhi ya wachezaji, wakipata vitafunwa na vinywaji.

Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

$
0
0
Na Nuru Juma-MAELEZO

Serikali inamkakati wa kuhakikisha inajenga Magereza katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa kilimo ambayo pia yana ukubwa wa kutosha ili kazi ya kuwarekebisha wafungwa iwe rahisi kufanyika huku shughuli za uzalishaji zikiwa zinaendelea.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mhe Devotha Minja Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro. 

“Magereza hayo yatajengwa katika maeneo yenye Kilimo na yatakuwa ni kwa ajili ya watu waliokwisha hukumiwa huku yale Magereza ya mijini yawe kwa ajili ya mahabusu tu ili wawe karibu na Mahakama,”alisema Mwigulu. 

Aliongeza kuwa mkakati huo wa Serikali ni wa muda mrefu na wanahitaji kufanya hivyo ili kurahisisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wafungwa na pia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Magereza.

Hili pia linatokana na tamko la Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilowahi kulitoa hivi karibuni kuwa wafungwa wako katika kutumikia adhabu hivyo wanatakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ili kwanza kujipatia chakula na sio kukaa tu bure na kusubiri kila kitu wafanyiwe na serikali.

Aliongeza kuwa Serikali ina mkakati wa kutumia bajeti inayotengwa na nguvu kazi wanayoipata kutoka kwa wataaalam walionao kwa upande wa askari Magereza na wafungwa ili kukarabati Magereza chakavu na kujenga nyumba za askari.

Aidha alibainisha kuwa suala la kukatwa kwa umeme katika Magereza, nyumba za askari,pamoja na maeneo na maeneo mengine ya kambi za Jeshi la Polisi na Magereza limeshafanyiwa kazi na serikali kwa kupitia hazina imekwishatoa fedha kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

Mheshimiwa Waziri aliliambia Bunge kuwa sheria zimeainisha baadhi ya haki za mfungwa zikiwemo huduma za afya kwa wakati,kupewa chakula, uhuru wa kutembelewa na ndugu zake na kupata mawasiliano kwa kusoma magazeti,kusikiliza taarifa za habari na kuandikiwa barua na ndugu zao,haki ya kukata rufaa ikiwa hakuridhika na hukumu yake, malazi safi na yakutosha pamoja na kushiriki michezo mabalimbali.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 27, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 17, 2017

$
0
0
 Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri  wa Nishati na Madini Mhe.Prof  Sospeter Muhongo akizungumza jambo na Naibu Waziri wake Mhe.Dk. Medard kalemani  katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Zaynab Vullu akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.Abdallah Bulembo  akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki leo katika viwanja vya Bunge  Mjini Dodoma.
 Waziri wa Mambo  ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimskiliza  Mbunge wa Mwibara Mhe.Kangi Lugora katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.Wengine Pichani ni Mbunge wa Mtama Mhe.Nnape Nnauye
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba  akizungumza jambo na Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe.Dk Hussein Mwinyi,Waziri wa Ardhi,Nyumba  na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Magembe katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mhe.Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017
 Mbunge wa Sikonge(CCM) Mhe.Joseph Kakunda akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akisoma Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 leo katika  kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

Jumia Travel yajizatiti kufanya mapinduzi ya usafiri barani Afrika

$
0
0


Na Jumia Travel Tanzania

Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ndani na nje ya bara la Afrika, Jumia Travel imedhamiria kukomboa jitihada za masuala ya usafiri kupitia kampeni yake mpya itakayojulikana kwa ‘DemocratizeTravel.’

Akizungumzia juu ya kampeni hiyo Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amebainisha kuwa lengo kubwa ni kuondoa ile dhana potofu kwamba kusafiri ni gharama kubwa na ni jambo gumu ambalo mtu wa kawaida hawezi kulifanya.

“Dhumuni letu kubwa ni kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni mwetu haswa linapokuja suala la mchakato mzima kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hii inamaanisha kupunguza gharama hususani za malazi, upatikanaji wa taarifa pamoja huduma bora kwa kila mtu. Pia kupitia kampeni hii tunataka kuwaonyesha wateja wetu uzuri uliofichika kuhusu bara la Afrika kwa kuwapatia suluhu ya mahitaji yao yote pindi wanapotaka kusafiri kama vile; hatua au mambo ya kuzingatia,malazi, chakula na shughuli za kufanya mahali waendapo,” alisema Bi. Dharsee.

“Hatutoishia hapo bali tunataka pia kuondoa mitazamo tofauti ya kwamba sehemu za kutembelea zilizopo nchi za Magharibi kama vile Ulaya na Marekani au Dubai ni bora zaidi ya Afrika. Mbali na kuwarahisishia waafrika kusafiri kwenye maeneo waliyopo lakini pia tunawawezesha kuvuka mipaka kwenda sehemu zingine duniani. Hapa msafiri ataweza kulipia gharama za kusafiri, kwa mfano kwenda jijini London nchini Uingereza, kwa fedha ya nchi yake anayotokea. Hayo yote yanawezekana na yamerahishwa kwani kupitia mtandao wetu mteja ataweza kukata tiketi ya ndege na kufanya huduma ya malazi kwa sehemu anayokwenda kwa wakati mmoja,” aliongezea Meneja Mkaazi wa Jumia
Travel nchini.

Kampuni hiyo imesema mbali na kuelekeza kampeni hiyo kwa wateja wake lakini pia itawashirikisha hoteli washirika katika kuhakikisha wanawafikia wateja na kukua kwa haraka zaidi. Hayo wanayahakikisha kupitia kuwatangaza mtandaoni ili kukuza muonekana na biashara zao, kuwapatia mifumo ya teknolojia inayoendana na soko la Afrika ili kuwarahishia uendeshaji wa biashara zao kama vileExtranet, SMS au barua pepe pamoja na kuchochea utoaji na uboreshaji wa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi zaidi.

“Uzinduzi wa kampeni hii utakwenda sambamba na uwasilishaji wa ripoti yetu ya masuala ya ukarimu na utalii barani Afrika ambayo tutaitoa siku chache zijazo. Kwenye ripoti hii tumezungumzia masuala yote tuliyoyaona kuhusiana na mustakabali mzima wa sekta hii kwa ujumla. Lakini pia kutakuwa na shughuli zingine zinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kama vile kwa wateja wetu kuwashirikisha wenzao picha au video fupi za sehemu walizotembelea, walijisikiaje na walivutiwa zaidi na vitu gani,” alihitimisha Bi. Dharsee.

LAKE CEMENT YACHANGIA DAMU KATIKA KUOKOA MAISHA WAHITAJI DAMU

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Uchangiaji wa damu salama unahitajika kutokana na kuwa na wahitaji wengi ambao wanatakiwa kuwekewa katika kuokoa maisha yao.
Hayo ameyasema Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki , Fatuma Mjungu wakati uchangiaji wa damu katika kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kimbiji Manispaa Kigamboni jijini Dar es Salaam , amesema kuwa kwa mwaka jana walikusanya damu chupa 160,000 lakini malengo yake ni ukusanyaji wa chupa 300,000.
Fatuma amesema kutokana na mikakati waliojiwekea kwa mwaka huu watafikia lengo la kukusanya damu chupa 300,000 kwa kuhamasisha wananchi kuchangia damu.

Amesema Lake Cement wamekuwa wakijitoa katika katika suala la uchangiaji damu na kutaka viwanda vingine kujitokeza katika kufanya uchangiaji damu popote pale watawafikia.

Afisa Rasilimali wa Watu wa Lake Cement, Ahmed Nyang’anyi amesema kuwa wanatambua umuhimu wa damu katika kuokoa maisha kwa watu wanaohitaji kwa akina mama wakati wa uzazi na makundi mbalimbali .
Nyang’anyi amesema kuwa wataendelea kuchangia damu kila mwaka kutokana na mahitaji yake kwa wahitaji ni wengi ikilinganishwa na damu iinayokusanywa.

Meneja wa Afya, Mazingira Mahala Pakazi, Happy Mboma amesema hakuna kiwanda kinachozalisha damu hivyo kila mtu anawajibu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha wahitaji wa damu.Amesema kuwa wanaochangia damu nao ni wahitaji damu hiyo kwa sababu hakuna mtu ambaye anajua atapata uhitaji damu wakati gani.
Makamu wa Rais wa Kiwanda Lake Cement, Afroz Ansari akizungumza na waandishi wa habari wakati uchangiaji damu katika kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Kiwanda Lake Cement, Afroz Ansari akiwa katika uchangiaji damu.
Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki , Fatuma Mjungu akizungumza wakati uchangiaji damu wa kiwanda cha Lake Cement juu ya uhitaji damu katika kuokoa maisha.
Afisa Rasilimali wa Watu wa Lake Cement, Ahmed Nyang’anyi akizungumza wakati wa uchangiaji damu wa kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.

WADAU WAIPONGEZA SERIKALI KWA UAMUZI WA KUIVUNJA MAMLAKA YA USTAWISHAJI WA MAKAO MAKUU, DODOMA (CDA)

$
0
0


Na: Frank Shija – MAELEZO

WADAU mbalimbali wameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuivunja Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) iliyofikiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Wakitoa maoni yao juu ya umauzi huo wa Serikali, wameeleza kuwa kuvunjwa kwa Mamlaka hiyo kumekuja wakati muafaka kwani kutapunguza kero na migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiendelea katika Manispaa ya Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana,iliyokuwa inashughulikia changamoto za wananchi dhidi ya CDA, Bw. Aron Kinunda alisema kuwa uamuzi huo huko sahihi kwani umekuja wakati muafaka kwa kuzingatia malengo halisi ya uanzishaji wa mamlaka hiyo kuwa yamekamilika kwa asilimia kubwa ukizingatia na mahitaji halisi ya wakati huu.

“Ni hatua nzuri katika mustakabari wa maendeleo ya Dodoma, kwani sasa migogoro mingi ya ardhi iliyokuwa inatokana na mgongano wa kisheria haitarajiw kujitokeza tena na badala yake Manispaa itajikita katika kuweka mazingira rafiki ya umiliki wa ardhi ikiwemo kuongeza muda wa hati ya umiliki kutoka miaka 33 hadi 99 kama ambavyo maeneo mengine ya nchi yanavyofanya.” Alisema Kinunda.

Aliongeza kuwa wananchi watakuwa wamefarijika sana kwani walikuwa wanaiona CDA kama adui yao mkubwa ambapo imesababisha malalamiko mengi ya kuchukuliwa ardhi zao bila ya kulipwa fidia na urasimu katika upimaji na utoaji wa hati za viwanja.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuwa CDA hakuna usimamizi mzuri wa ardhi jambo linalosababisha kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi itokanayo na mgongano wa kisheria uliopo kati ya Mamlaka hiyo na Manispaa ya Dodoma.

“Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999 inatambua umiliki wa ardhi upo chini ya Serikali za Mitaa, kitu ambacho kwa Dodoma ni tofauti kwa kuwa ardhi yote iliyopimwa iko chini ya CDA kitu ambacho hata Manispaa imekuwa mpangaji,” aliongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma, Mzee Chidawali amesema kuwa uamuzi wa uamuzi huo umepokelea kwa nderemo na vifijo na ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa Dodoma wanaona ni kama ukombozi kwao.

“ Rais Magufuli anapaswa kupongezwa sana kwa uamuzi aliouchukua wa kuivunja CDA hakika amefanya jambo jema sana, sasa wananchi watapata ahueni katika kushughulikia masuala yao ya umiliki wa ardhi,” alisema Chidawali.

Aidha aliongeza kuwa katika upande wa taaluma ya uandishi wa habari uamuzi huo umewasaidia kurejesha uhusiano mwema baina yao na wananchi kwani wamekuwa wakiacha kuripoti habari za maendeleo badala yake wamekuwa wakijikuta wanaandika habari kuhusu migogoro ya ardhi zaidi iliyokuwa inasababishwa na CDA.

Chidawali alisema kuwa baada ya kupata taarifa juu ya uamuzi huo amepata fursa ya kusikia maoni ya wadau mbalimbali ambapo kwa nyakati tofauti wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua jambo linalotoa tafsiri chanya juu ya dhamira njema ya Serikali yake ya kuwajali wanyonge.

“Binafsi nje ya taaluma ya habari mimi ni mzawa wa Dodoma tumekuwa na malalamiko ya muda mrefu hasa kuhusu uhalali wa kumiliki ardhi, tunaitwa wavamizi katika maeneo ambayo tumekuwa tukiyamiliki enzi na enzi,” alifafanua Chidawali.

Naye Mwenyekiti wa Soko la Chadulu Jakton K. Matoto amesema kuwa Jumuiya yao imepokea kwa mikono miwili uamuzi huo na kuongeza kuwa ni imani yao kuwa baada ya Manispaaa kuchukua majukumu ya CDA itakwenda kufanya mapitio na kutatua migogoro yote iliyokuwa ikiendelea kutokana na uwepo wa mamlaka hiyo.

Mwenyekiti huyo ameonyesha matumaini ya mji wa Dodoma kukua kutokana na kile anachodai kuwa CDA ndiyo cahnzo cha Dodoma kubaki nyuma kimaendeleo kwani wawekezaji wengi wamekuwa wakishindwa kuwekeza kutokana na muda mfupi wa hati ya umiliki wa ardhi ambapo mmiliki anapewa miaka 33 wakati maeneo mengine ya nchi muda ni miaka 99.

Wakati huohuo Matoto ametoa rai kwa Manispaa ya Dodoma kujipanga ili kuendana na hali ya mahitaji ya sasa ikiwa ni mapoja na upimaji wa viwanja kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma ilianzishwa mwaka 1973 kwa malengo ya kutengeneza master plan na kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo zaidi ya ekari 260,000 za ardhi zimepimwa na na kupatiwa hati zinazomilikiwa na CDA, kufuatia kuvunjwa kwake na maelekezo ya Rais kuwa rasirimali zote ziwe chini ya Manispaa ya Dodoma ambayo itaendeleza shughuli zilizokuwa zikifanya na mamlaka hiyo kwa mujibu mtaratibu na sheria za nchi.

SERIKALI: AWAMU YA 3 YA REA KUVIFIKIA VIJIJI, VITONGOJI NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA NCHI.

$
0
0
Na Nuru Juma,MAELEZO,DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia mradi wa awamu ya 3 ya usambazaji wa umeme vijijini (REA) imekusudia kusambaza umeme katika vijiji, vitongoji vyote, taasisi za umma na maeneo ya pembezoni mwa nchi ikiwemo visiwa.

Hayo yamesemwa leo bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokua akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA) Wilfred Rwakatale.

Dkt. Kalemani amesema kupitia mradi wa REA, Serikali inatarajia kukamilisha usambazaji umeme vijijini mwaka 2020 hadi 2021, na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) inaendelea kusambaza umeme maeneo yote ya mjini ambayo hayajapata nishati ya umeme.

“Baadhi ya vijiji ambavyo vipo ndani ya mamlaka za miji vinapelekewa umeme na shirika la Tanesco na bei ya Tanesco na REA ni tofauti kwani kwa mteja wa awali wa Tanesco hulipia 177,000 na REA hulipia 27,000””, alisema Mhe.kalemani.

Kwa mujibu wa Kalemani amesema Serikali bado inaendelea kujiridhisha na kuangalia ni vijiji gani vinastahili kupelekewa umeme kwa mradi wa REA ili kuhakikisha kuwa malengo ya mradi yanaweza kufikiwa katika muda uliopngwa.

Dkt. Kalemani ameongeza kuwa wakati wa uzinduzi mradi huo ulianza na mikoa 10 na walibakisha mikoa 15 kwa Tanzania bara na hadi sasa wamemaliza utaratibu wa kuwapata wakandarasi watakaojenga miundombinu ya mradi huo katika mikoa yote nchini.

Aidha Dkt. Kalemani amesema wakati wowote kuanzia sasa Serikali inatarajia kuwapangia vituo vya kazi na wakandarasi hao.

Aliwataka makandarasi hao kufanya kazi kwa bidii katika mikoa yao ili kuhakikisha wanamaliza kazi zao kwa wakati na umeme unapatikana katika vijiji vyote bila kubagua nyumba.

Katika swali lake la msingi, Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kusambaza umeme katika baadhi ya vijiji vilivyopo katika baadhi Wilaya za Mkoa wa Kagera.

Utekelezaji wa mradi wa Rea wa wamu ya 3 umeanza tangu Machi 2017 na unatarajia kukamilika mwaka 2021.

MTAMBO WA KUHAKIKI HUDUMA ZA MAWASILIANO WAPELEKEA SERIKALI KUKUSANYA MABILIONI

$
0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni.
“Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote,”aliongeza Ngonyani
“Kuanzia Oktoba 2013 hadi Februari 2017, kiasi cha shilingi 63,015,450,230 zilipatika na katika hizo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya mfumo huu mapato hayo hayakuwepo.”
“Aidha pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea,” aliongeza Naibu waziri Ngonyani.

ROCKSTAR TV LAUNCH IN SOUTH AFRICA ON MTN

$
0
0

ROCKSTAR TELEVISION SWITCHES ON ITS AFRICAN-BORN-AND-ROOTED BOUQUET OF CHANNELS AND CONTENT IN SOUTH AFRICA WITH LEADING MOBILE TELECOMMUNICATIONS GIANT MTN PROVIDING CUTTING EDGE PAN AFRICAN AND INTERNATIONAL CELEBRITY-DRIVEN-CONTENT FROM THE WORLDS OF MUSIC, ENTERTAINMENT, FASHION, SOCIALITES, SPORTS, COMEDY, FOOD, LIFESTYLE, HEALTH & FITNESS, MEDIA, BUSINESS AND OTHERS TO OVER 30 MILLION MTN SOUTH AFRICAN SUBSCRIBERS.

#RockstarTV has launched its first phase of main channel and channels bouquet of artists, celebrities and all-access-exclusive and never-before-seen content and personal perspectives direct from the artist and celebrities themselves straight to the handset or device of the MTN South African subscriber to view and consume wherever they are, whatever time, however they want on demand. Rockstar TV is available to all MTN South Africa subscribers via the network’s ‘MTN Shortz’ and ‘MTN Play’ platforms.

“We are thrilled with revealing this 1stpiece of the puzzle as we bring the next-generation of world class cutting edge premium content to fans, audiences and subscribers across South Africa via the MTN Network.” says Jandre Louw, the Founder & CEO of Rockstar Television. “Rockstar TV is revolutionary and a world first, proudly born and rooted in and from the African continent, this is only the first part of the big extensive multi-piece jigsaw and more will be revealed and announced in the days and weeks ahead,” he added.

#RockstarTV is the new All-Access-Pass. The ‘Rockstar-Pass’ gets fans and audiences closer to the artist, celebrity and the worlds they live and roam in day-to-day unfiltered and filtered, on-stage, off-stage, in front of the camera and behind the camera, wherever the celebrity roams, than any All-Access-Pass can possibly dream about. Uncompromised, real and verified. Full stop.

#RockstarTV programming consist of bespoke premium artist and celebrity channels, main channels and packaged content formats including ‘SHOOOOSH!’, ‘KINGS & QUEENS’, ‘Hall of Fame Africa’, ‘Rockstar Diaries’, ‘HOT5!’, ‘ROCKSTAR LIVE!’, ‘Raw & Uncut’, ‘The Studio’, ‘SuperFan!’, ‘Rockstars Unplugged’, ‘Moguls’, ‘Say What?!’, ‘Rockstar Sessions’, ‘Fashionably Rockstar’, ‘Kebangabong!’, ‘Rockstar Academy’ and ‘I AM ROCKSTAR’ to name a few.

“Rockstar TV opens an unprecedented new world for the first time for African artists, celebrities and stars with a myriad of platforms and opportunities to expose and commercialize their content across audiences in countries and regions they’ve never bridged into before,” says Seven Director of Music and Talent at Rockstar Television.

#RockstarTV on MTN includes ‘SHOOOOSH!’ the worlds premiere Pan African music entertainment news channel, a proudly born and rooted African network based across the continent with its branches spread wide across the globe providing cutting edge current African perspectives locally from across the continent and the rest of the word, in world class formats with unrivaled access.

Check out, follow, tune in to and subscribe to #RockstarTV on TELEVISION via Cable and Satellite TV services, channels and platforms or on MOBILE on mobile networks in your country or ONLINE on partner platforms.

MRADI WA MATREKTA YA URSUS MKOMBOZI WA WAKULIMA TANZANIA.


MKURUGENZI MTENDAJI WA IMF ASISITIZA UMUHIMU WA KILIMO NA NISHATI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa pili kulia) akieleza kuwa Tanzania inakua kwa kasi kiuchumi jambo ambalo linawavutia viongozi wengi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake, alipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiongoza Mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (mbele kulia) ambapo alisema mahitaji makubwa wa nchi ni maendeleo ya kilimo na upatikanaji wa nishati ya umeme ili viweze kuchochea uchumi wa viwanda. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba ( kulia) wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao uliohusu suala la Uchumi katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (watatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu hali ya uchumi katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (hayupo pichani) wakimuaga baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

IMF YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUPAMBANA NA RUSHWA NA UKWEPAJI KODI

$
0
0

Na. Said Ameir – Maelezo

Shirika la Fedha Duniani (IMF) linaziunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kupambana na vitendo vya rushwa na ukwepaji wa kodi kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kielelezo cha dhamira ya kweli ya Serikali yake ya kuleta maendeleo kwa faida ya wananchi wote.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dk. Tao Zhang amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zinazofanya vizuri katika kukuza uchumi wake pamoja na kupata mafanikio katika sekta ya huduma za jamii ambayo ni matokeo ya kazi nzuri na sera madhubuti za uchumi.

“Ukuaji wa uchumi wenu umekuwa kwa kiwango cha wastani wa asilimia 7 katika miaka ya hivi karibuni na viashiria vya maendeleo katika sekta ya jamii ni vizuri kwa mfano kupungua kwa vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 60 na uandikishaji wa watoto elimu ya msingi umeongezeka kwa asilimia 36” Dk. Zhang alieleza.

Dk. Zhang aliongeza kuwa kutokana na mwenendo wa sasa wa ukuaji wa uchumi wake, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kupata mafanikio zaidi ikiwemo lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati kama ilivyoelezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2020.

“Kuna mambo mengi ambayo yanatoa fursa kwenu ikiwemo uanachama wenu katika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, raslimali ambazo zimo mbioni kupatikana katika miaka ya karibuni na rasilimali watu kubwa na iliyoelimika“, Dk. Zhang alieleza.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF, aliwaambia washiriki wa mhadhara huo kuwa kitu muhimu sasa kwa Tanzania ni kuendelea na usimamizi mzuri wa uchumi na kusimama katika kuchukua hatua kufungua fursa zake za maendeleo.

Dk. Zhang ameongeza kuwa, kama zilivyoweza kufanya nchi nyingine, anaamini Tanzania inaweza kufikia hatua hiyo, hivyo ameainisha maeneo matatu muhimu ambayo Tanzania ikiyafanyia kazi ipasavyo yataleta mabadiliko makubwa na kuipaisha nchi katika ngazi nyingine ya juu ya maendeleo.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kuongeza uwekezaji kwa kushughulikia vikwazo vinavyozorotesha uwekezaji na kuongeza nafasi za ajira, kuchukua hatua madhubuti kuimarisha nafasi ya sekta binafsi katika uchumi na kuongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuhakikisha kuwa mafanikio yanayopatikana yanamfaidisha kila mwananchi kwa kupata fursa za elimu, afya na huduma za kifedha.

Dk Zhang, ambaye alikuwa akitoa mada kuhusu “Kufikia Mafanikio: Tanzania Kufikia Lengo la kuwa Nchi ya Kipato cha Kati” katika mhadhara uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu, mtaa wa Mirambo, amesema IFM iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inafikia malengo yake ya maendeleo ikiwemo la kufikia nchi ya uchumi wa kiwango cha kati.

“Nchi yenu imepata mafanikio makubwa katika miaka ya karibuni na sisi (IMF) tuko pamoja nanyi kuhakikisha mnafikia malengo yetu ya maendeleo. Tumejiandaa kushirikiana nanyi kwa kusaidia ushauri wa kisera na kwa kuwajengea uwezo” Dk. Zhang alieleza.

Akizungumzia utenganamo wa kikanda, Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo wa IMF alieleza kuwa ametiwa moyo na kasi ya utengemano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuielezea kuwa moja kati ya ushirikiano wa kikanda unaokua haraka sana.

Mhadhara huo ulihudhuriwa na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo makatibu wakuu, Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa zilizopo nchini, wataalamu wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakiwemo wahadhiri na watafiti kutoka vyuo vya elimu ya juu na taasisi za utafiti pamoja na vyombo vya habari.

Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini

$
0
0


Mratibu wa mradi wa usafi wa mazingira uitwao Nipo Tayari Juliana Kitira akimuonyesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Kigoma, Elinatha Elisha takwimu za hali ya usafi wa mazingira katika halmashauri yake kwenye simina inayofanyika Morogoro. Mradi huo pia unahamasisha uwepo wa vyoo bora na kunawa mikono na maji safi baada ya kutoka chooni.
Mkurugenzi wa wilaya ya Bagamoyo Fatuma Latu akiangalia msimamo wa wilaya yake katika usafi wa mazingira kupitia mradi wa Nipo Tayari chini ya Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Watoto, Walemavu na Wazee kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara Yefred Myenzi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Sabas Damian Chambasi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro.

=====  ====== ========

Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kuchangamkia fursa ya fedha za kitanzania bilioni 250 zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji safi na salama vijijini (2016-2020).

Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba aliwaambia wakurugenzi wa wilaya katika semina inayofanyika mjini Morogoro jana kuwa ni halmashauri chache tu ndio zimeanza kupata fedha hizi mara baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa na wafadhili.

"Kuna fedha za kutosha katika mradi huu ukilinganisha na mwamko wa halmashauri katika kuchangamkia fursa hii ya kuongeza mtandao wa maji katika maeneo yao," alisema na kuongeza kuwa fedha hizi zinaweza kuzisaidia halmashauri kuanzisha miradi mipya na kukarabati ile ya zamani ili iweze kutoa maji kwa wakati wote wa mwaka.

Alisema moja ya sharti la upatikanaji wa fedha hizi ni ufanisi katika utekelezaji wa miradi iliyopita na ubora wa ripoti za kila mwezi kama ambavyo programu hii inavyozitaka halmashauri. Kigezo hiki ni muhimu sana katika kuvuka hatua moja hadi nyingine na kupata fungu kubwa zaidi la fedha ambalo litawezesha kutekeleza miradi mikubwa zaidi katik halmashauri husika.

Kwa mfano halmashauri zinaweza kupokea aina mbili za malipo kama vile paundi za kiingereza 50 kwa ajili ya kuendeleza kituo cha maji na fungu hili linaweza kuongezeka hadi paundi 1,500 kulingana na ufanisi wa utekelezaji katika hatua ya mwanzo.

"Ukipata paundi zaidi ya 1,500 kwa mara moja kwa miradi ya vijijini ni nyingi sana katika kuiboresha na kuifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wakati wote. Na pia fedha hizi zinaweza kutumika kuanzisha vituo vipya vya kusambazia maji hivyo kufanya mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi katika eneo husika," alisema.

Alisema ni halmashauri 57 tu ambazo ziliweza kuvuka vigezo viwili vya mwanzo kwa mwaka jana na kuweza kupata fungu kubwa zaidi la kiasi cha paundi za uingereza 5,000, fedha ambazo kwa miradi ya maji vijijini zinaweza kusaidia sana katika upatikanaji wa maji wakati wote wa mwaka.

Aliwahimiza wakurugenzi wa wilaya kuchangamkia fursa hii ya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mingi ya maji na kuifufua ile ambayo imekufa ianze kufanya kazi tena na kuongeza mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi ili kufikia adhma ya serikali ya asilimia 95 wa watu wanaopata maji katika miaka michache ijayo.

Injinia Mutazamba aliongeza kusema lengo la kuwakutanisha wakurugenzi wote nchini katika semina hiyo ni kuweza kuwaeleza kwa kina kuhusu fursa hii ya fedha za wafadhili ambazo bado zipo nyingi na zinaweza kusaidia kupunguza na hata kumaliza kabisa tatizo la maji hasa sehemu za vijijini.

Alisema programu hii ya kuongeza mtandao wa maji vijijini unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya shirika la kimataia la DFID la uingereza na serikali ya Tanzania.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MAY 18,2017

NAIBU MKURUGENZI WA IMF AKUNWA NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, AAHIDI KUFUNGUA DIRISHA LA MIKOPO KWA TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
BEN2
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akielezea kuhusu ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) ambapo alisema itasaidia kuchochea maendeleo si tu kwa Tanzania bali na nchi jirani, wakati wa Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.
BEN3
Naibu Mkurugenzi  wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu nia ya Shirika hilo kufungua fursa zaidi za mikopo kwa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
BEN4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne kushoto) na Naibu Mkurugenzi  wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
BEN5
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.
BEN6
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang ameahidi kufungua madirisha ya mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukuza uchumi.

Bw. Zhang aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Shirika la Fedha la Kimataifa limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na ipo juu ya wastani wa ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.
Ameishauri Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi  katika ukuaji wa Uchumi ili uchumi huo uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na mfumo shirikishi wa kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema kuwa juhudi za Tanzania  kwa sasa ni  kuchochea ukuaji wa Kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija.

“Umasikini haujatatuliwa kwa kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa mpaka sasa watu walio katika  umasikini na ukosefu wa huduma za lazima ni takribani asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango
Kama nchi imeamua kwenda kwenye uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa mkazo ni upatikanaji wa umeme wa kutosha na wenye bei nafuu .

Amesema kuwa Serikali imefanya juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini bado kazi hiyo haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya usafirishaji ni changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa nchi ambao ni wazamani na umeharibika.

“Serikali imeamua kujenga Reli yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge)  ambayo ni ya gharama, na kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola Bilioni 7.6, lakini umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango.

“Tayari tumeanza ujenzi wa reli hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa 200 kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri fedha zinavyo patikana” alifafanua Waziri Mpango .
Amesema kuwa, kumekuwa na tatizo la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati jambo linalofanya baadhi ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni  vema Serikali ikaendelea kuangalia vipaumbele  katika ujenzi wa miundombinu ili iweze kuchochea uchumi.

“Suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa kuwa Sekta Binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi nyingi Duniani” Alishauri Bw. Mkwezalamba.

Ameishauri Tanzania kuendelea kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa ni moja ya eneo ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo chanya na ya haraka katika ukuaji wa Uchumi.

Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo, Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kunakuwa na viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata ajira. Aidha tayari Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kupata elimu.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>