Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1233 | 1234 | (Page 1235) | 1236 | 1237 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mdau akifurahi jambo wakati burudani za Castle Lite Unlock ziliporidima katika Bar ya Stanza Goba,kampeni ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.
  Mc akisherehesha katika kampeni ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.

  Mc akisoma Kuponi ya mshindi wa zawadi kutoka Castle lite Unlocks  katika Bar ya Stanza Bar _Goba .kampeni ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.
   
  MC akimvisha mteja Kofia mara baada ya kushinda zawadi ambapo burudani za Castle Lite Unlocks zilikuwa zikiendelea katika Bar ya Stanza Goba.kampeni ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.  .


  0 0

  viongozi wa shirika la LEAT pamoja na viongozi wa kijiji cha Uhambila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kujadili maswala ya utunzaji wa Maliasili na vyanzo vya maji vilivyopo eneo hill.
  Baadhi ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za kijiji hicho.

  Na Fredy Mgunda, Iringa.


  Wananchi wa kijiji cha uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho.

  Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi kutoka shirika la LEAT upande wa wilaya ya mufindi Jamali Juma alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.

  “Mkiangalia zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama zamani”alisema juma

  Ukataji miti na uharibifu wa vyanzo unasababisha madhara mengi makubwa na ndio maana tunaona sasa kumekuwa na magonjwa mengi ambayo yanaathari ya moja kwa moja kwa mwanadamu lakini pia uharibifu huo husababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.

  Juma alisema kuwa dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu.

  “Ni kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu vyanzo vya maji kutokana na sheria zetu za mwaka 1982 hivyo kukata miti au kuaribu vyanzo vya maji sio haki ya msingi ya mwananchi” alisema Juma

  Shirika lisilo la kiserikali la Mwanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo( LEAT) wametoa elimu ya Mazingira kwa miaka minne mfululizo hivyo Vijiji vyote vya mradi ambavyo vipo wilaya ya iringa na wilaya ya Mufindi na kuiomba serikali kuendelea kuboresha Mazingira ambayo yapo chini yao.

  Franklin Masika ni Afisa ughani wa shirika la LEAT aliwataka wananchi kufuata sheria ya mazingira mwaka 2004 namba 20 na sheria ya maji ya mwaka 2009 namba 11 zinaeleza wazi kuhusu kilimo cha vinyungu au kulima kandokando ya mto au kwenye vyanzo vya maji na kuna faini zimeolodhishwa hivyo sheria hizi sio ngeni ili zilikuwa hazifuatwi lakini saizi serikali imeanza kuzifuatilia kwa umakini zaidi.

  “Mkiangalia nyie hapa kijiji cha uhambila kipo katika bonde la mto rufiji hivyo wananchi mnatakiwa kuwa makini na hizi sheria kwa kuwa lengo la serikali ni kuboresha Mazingira ya kuukuza mto ruaha mkuu ambao unahati hati ya kutoweka na nyie ni walinzi namba moja wa Mazingira “alisema Masika

  Lakini Franklin Masika aliztaja baadhi ya adhabu zinazotokana na uharibifu wa Mazingira mfano kuchepusha maji,kukinga,kuchukua au kutumia maji kinyume cha sheria ni kosa la jinai na adhabu yake ni shilingi 300,000 na isiyozidi 500,000 au kifungo cha miezi miwili na kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na hizo sheria.

  Masika aliwataka wananchi wa kijiji cha uhambila kuwa kutunza vyanzo vya maji na Mazingira kwa ujumla ili kuboresha maeneo wanayoishi na kupunguza au kufuta Kabisa milipuko ya magonjwa ilanayotokea mara kwa mara katika maeneo ya Vijijini.

  Chelsoni Kikoti, Amani Nyakunga na Reginandi Chalamila ni wananchi wa kijiji cha uhambila waliiomba serikali zitafakali upya sheria hizo kwa kuwa zinawaumiza wananchi wa vijijini kutokana na Mazingira wanayoishi kutokuwa rafiki na namna ya kupata kipato hivyo wemekuwa wakitegemea sana kilimo cha mboga mboga kuendesha maisha yao.

  “Hebu angalieni Mazingira haya tunayoishi hakuna njia nyingine ya kupata kipato zaidi ya kutegemea kulima vinyunguni ambako tunalima mboga mboga tu jamani hee tuatakufa na njaa hebu muishauri serikali juu sheria hizo”walisema wananchi

  Thomas Mtelega afisana mradi wataasisi ya mufindi kwa maendeleo (MUVIMA) aliwaomba wananchi kulima Kilimo cha kisasa kutokana na Mazingira wanayoishi na kuacha tabia za kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji mfano kulima mboga mboga ni rahisi unaweza kulima hata kwa kutumia maji.

  “Kuna maji machafu ambayo tunayoyatumia majumbani kwetu ni maji ambayo tunaweza kuyatumia katika Kilimo cha mboga mboga kwa kuchukua udongo na kuuweka kwenye gunia au visarufeti ambavyo ukipanda mbegu unaweza kupata mboga nzuri na salama kwa kuwa guni au kisarufeti kinaweza kujchuja uchafu wote na kuiacha mboga ikiwa salama hivyo nawashauri wananchi kutumia njia hii ili kuondokana na ulimaji wa karibu na vyanzo vya maji na kusababisha Mazingira yanaboresha na kuwa mazuri”alisema Mtelega
  Naye Mwenyekiti wa kijiji cha uhambila Agnes Simba aliwashukuru shirika la LEAT kwa elimu waliyokuwa wanantoa kwa miaka nne ambayo imewakomboa wananchi kwa kupata vitu vingi ambavyo sasa vimeanza kutokea na vinakuwa sio vigeni hasa maswala ya sheria za Maliasili na utunzaji wa vyanzo vya maji ambavyo vinafaida kwa wananchi wa sasa na baadae.

  0 0
 • 05/15/17--22:57: WOTE MNAKARIBISHWA


 • 0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kisiwani Pemba. Semina hiyo inatolewa kwa wajasiriamali wa Pemba ili waweze kuchangamkia fursa za mtangamano. Semina hiyo inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Uwanja wa mpira wa Gombani. 
  Sehemu ya wajumbe waliohudhuria semina hiyo, wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Konde Mhe. Mbarouk Ali akiwa pamoja na washiriki wengine wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo 
  Sehemu nyingine ya wajumbe wakimsikiliza kwa makini Waziri Mahiga hayupo pichani. 
  Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Zanzibar Mhe. Khamis Juma Maalim akisoma hotuba ya ukaribisho. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi naye akielezea jambo kwenye ufunguzi wa semina hiyo ya Mtangamano wa Afrika Mashariki. 
  Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Sanday markert kutoka Pemba, Bw.Khamis Suleiman Masoud akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayupo pichani). 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akitoa ufafanuzi masuala mbali mbali kuhusiana na semina hiyo.
  Ufunguzi wa Semina ukiendelea 
  Wakiwa katika picha ya pamoja. 
  Wananchi wa Pemba wahimizwa kuchangamkia fursa za kiuchumi katika Soko la EAC

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewataka wakazi wa Pemba na Tanzania kwa ujumla kuchangamkia ipasavyo fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujiongezea kipato. 

  Mhe. Waziri alieleza kuwa katika ulimwengu wa leo hakuna nchi duniani itakayoweza kujiimarisha kiuchumi peke yake bila kushirikiana na nchi nyingine. Ndio maana hata zile nchi zilizoendekea kama Marekani na nchi za Ulaya wana umoja wao kwa madhumuni ya kuongeza nguvu na kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. 

  Waziri Mahiga aliyasema hayo alipokuwa anafungua semina kuhusu elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake kwa wananchi wa Pemba ambayo itatolewa na wataalamu wa Wizara yake kwa siku nne kuanzia leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Gombani.

  Mhe. Waziri alieleza kuwa kabla, wakati na baada ya ukoloni nchi za Afrika Mashariki zilikuwa na aina moja au nyingine ya Ushirikiano kwa madhumuni ya kuimarisha uchumi wa nchi zao, waliotutawala. Aina moja ya Ushirikiano ni ule Umoja wa Huduma ambao ulianzishwa mwaka 1961. Umoja huo ulianzisha mashirika mbalimbali kama vile bandari, ndege, hali ya hewa, posta na reli ambayo yalikuwa yanaendeshwa kwa pamoja.

  Alisema Tanzania ipo katika eneo la kimkakati ndani ya Jumuiya ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo kubwa kuliko nchi zote, idadi kubwa ya watu, ukanda mkubwa wa bahari na ardhi nzuri yenye rutuba na kihistoria Pemba ni eneo lenye rutuba nzuri kuliko maeneo yote ya Afrika Mashariki. Hivyo, kutokana na sifa hizo hakuna budi wananchi wa Pemba na Tanzania kwa ujumla kujipanga vizuri ili kuchangamkia fursa hizo badala ya kubaki kuwa watazamaji na walalamikaji.

  Waziri Mahiga aliongeza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sifa nyingine ya pekee ya kuwa Muungano wa nchi mbili na kutoa wito kwa washiriki wa semina hiyo kutumia sifa ya umoja wao kuziendea na kuzichangamkia fursa za kiuchumi zilizopo kwenye Mtangamano.

  "Nchi nyingi barani Afrika na duniani kwa ujumla zilijaribu kuungana lakini zilishindwa, kwa mfano nchi za Ghana, Mali na Guinea, nchi za Afrika zinazozungumza kifaransa, nchi za Misri na Syria, nchi za Afrika ya Kati na nchi za Pembe ya Afrika". “Ni sisi peke yetu hadi leo tumedumisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo juzi tu tuliadhimisha miaka 53 ya muungano huo”. Waziri Mahiga alisema. 

  Aliendelea kuueleza kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kudumisha Muungano huo ambapo kwa maneno yake alisema kuwa unaonewa wivu Afrika na duniani kote.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Khamisi Juma Mwalim aliwasihi washiriki wa semina hiyo kuzingatia mafunzo yanayotolewa katika semina hiyo ili waweze kunufaika katika shughuli zao ikiwemo ujasiriamali.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

  Dar es Salaam, 15 Mei, 2017

  0 0

  Jengo la Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria lililozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn tarehe 2 Julai, 2015 Kibaha, Pwani.
  Mtaalam wa Maabara ya Uandaaji Bakteria katika Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Bw. Fumbuka Pauline akiwaeleza Waandishi wa habari baadhi ya kazi wazifanyazo wakati wa kuwaandaa bakteria 15 Mei, 2017. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Samwel Mziray.
  Mmoja wa Waandishi wa Habari (kulia) akipiga picha ya bakteria wanaoonekana kwa kifaa maalum cha kuangalia bakteria (Microscope) katika Maabara ya kuaandaa bakteria 15 Mei, 2017 Kibaha, Mkoani Pwani.
  Mtaalam wa Maabara ya Uandaaji bakteria katika Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha Mkoani akiangalia bakteria kwa kutumia kifaa maalum (Microscope) kabla ya kuwapeleka sehemu inayohusika kwa ajili ya hatua nyingine, 15 Mei, 2017.
  Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria, Bw. Samwel Mziray (kulia) akiwaeleza Waandishi wa habari baadhi ya kazi zinazofanywa katika moja ya mitambo iliyopo kiwandani hapo 15 Mei, 2017.
  Baadhi ya mitambo iliyopo katika Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.
  Kaimu Meneja Masoko na Mauzo wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria, Bw. Frank Mzindakaya akiwaeleza Waandishi wa habari (hawapo pichani) namna kiwanda hicho kinavyoandaa madumu ya dawa kwa ajili ya kuyasambaza kwa wateja wake 15 Mei, 2017 Kibaha, Mkoani Pwani.
  Mtaalam wa Uthibiti wa Ubora wa Dawa wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria, Dkt. Nicholaus Banzi akiwaelezea Waandishi wa habari namna hatua za ukuaji wa mbu na namna dawa zinazotengenezwa na kiwanda hicho zinavyoweza kuua mazalia ya viluwiluwi vya mbu wa malaria.

  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

  ………………….

  Na Benedict Liwenga-WHUSM.

  Halmashauri nchini zimetakiwa kuitikia wito wa kununua dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zilizoanza kuzalishwa hapa nchini ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani, Bw. Samwel Mziray wakati alipokutana na Waandishi wa habari na kufanya nao mazungumzo juu ya shughuli zinazofanywa katika kiwanda hicho.

  Bw. Mziray amesema kuwa, dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zinapaswa kununuliwa na kila Halmashauri nchini kwa maagizo yaliyotolewa na Serikali kupitia waraka wake kwa kuwa kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kilijengwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali katika kupambana na malaria nchini. Hata hivyo amebainisha kwamba mpaka sasa mwitikio wa halmashauri umekua mdogo kwani ni halmashauri mbili tu za Geita pamoja na Mbogwe ndizo zimeshanunua dawa hizo.

  “Lengo la Serikali kuja na mpango huu ni kupunguza vifo vitokanavyo na malaria nchini na kupunguza gharama kubwa ya kununua dawa na vifaa tiba vya kupambana na malaria”, alisema Mziray.

  Amesema kwamba iwapo kama halmashauri zitanunua dawa hizo na kuzitumia, ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa nchini na hivyo serikali kuelekeza fedha zake katika shughuli za maendeleo.

  Amesema kwamba, kwa Afrika kiwanda hicho ni moja ya kiwanda kilichobahatika kujengwa Tanzania ambapo nia ya Serikali ni kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kuharibu mazalia ya mbu.

  Ameongeza kuwa, kiwanda hiki kitazalisha mbolea ya kibaiolojia (Bio fertilizer) siku za usoni, lakini kwa sasa kiwanda kinazalisha dawa za aina mbili ambazo ni Bactivec na Griselesf ambazo hutumika kwa kunyunyuzia katika mazalia ya mbu.

  Amefafanua kwamba, kwa sasa kiwanda hicho kinaweza kuzalisha kwa wingi dawa hizo ambapo ametaja moja ya nchi iliyonunua dawa hizo ni Niger ambayo tayari imenunua lita 91,000 na nchi nyingine za Serbia na Srilanka ziko katika mazungumzo ya kununua dawa hizo.

  “Niiombe Serikali iweze kutoa msukumo zaidi kwa halmashauri ambazo bado hazijanunua dawa hizi kukitumia kiwanda hiki kufikia malengo kwani jamii inapoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa malaria”, alisema Mziray.

  Amefafanua kuwa, dawa hizo zinaweza kutumika katika kipimo cha mililita moja kwa lita 50 za maji na bei ya lita moja ni shilingi 13,000/= na zina uwezo mkubwa wa kuangamiza viluwiluwi vya mbu wa malaria.

  Kuhusu agizo la Serikali la kuzitaka halmashauri nchini kununua dawa hizo amesisitiza kwamba utekelezaji wa halmashauri hizo kuja kiwandani unapaswa kuwekewa kipaumbele na Serikali na halmashauri hazinabudi kuitikia wito huo.

  “Serikali imeshatoa waraka kwa halmashauri zote nchini kuweza kutumia kiwanda hiki kununua dawa, kwahiyo sasa kilichobaki ni utekelezajina suala la bei sio kisingizio, suala kubwa ni utayari na kuona umuhimu wa kufikia malengo ya kutokomeza malaria kwa jamii”, alisema Mziray.

  Aidha, amebainisha kuwa, jukumu la kununua dawa hizo liko chini ya halmashauri husika na inatakiwa kupanga bajeti yake ya kununua dawa hizo.

  Kuhusu suala la usalama wa dawa hizo amesema kwamba, dawa hizo ni salama kwa binadamu na Kiwanda kinafanya mawasiliano na vyombo vya habari ili kutoa elimu na mkazo mkubwa wa kununua dawa hizo.

  Kwa upande wake Kaimu Meneja Masoko na Mauzo wa Kiwanda hicho, Bw. Frank Mzindakaya amesema kwamba, Serikali hainabudi kutenga bajeti ya kutosha ili kuziwezesha halmashauri kununua dawa hizo.

  Ameongeza kuwa, dawa za kiwanda hicho wanaziweka katika vipimo mbalimbali ikiwemo vya lita 20 na ujazo wa miligramu 30 na katika matumizi makubwa mteja mkubwa ni Serikali yenyewe kwakuwa ndiyo inayonunua kupitia Halmashauri na kwenda kuzinyunyuzia katika madimbwi. Kwa mwananchi wa kawaida anaweza kununua miligramu 30 ili aweze kutumia kwa matumizi ya kifamilia ya kujikinga yeye na familia yake.

  “Serikali haijamtwisha mzigo mwananchi yeyote wa kununua dawa hizi ndiyo maana tunazisisitiza kuwa halmashauri zije kununua dawa hizi ili ziende kuwasaidia wananchi kwa kuziweka katika madimbwi makubwa na hatimaye kuwalinda wananchi dhidi ya malaria”, alisema Mzindakaya.

  Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) ni Kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo (NDC) iliyopewa dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda cha kuzalisha bidhaa za kibaiolojia zikiwemo viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao malaria (Biolarvicides). Kiwanda hiki kipo eneo la TAMCO Kibaha, Mkoa wa Pwani.

  0 0

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali imetoa asilimia miamoja ya fedha za bajeti ya dawa kwa mwaka 2016/2017 kwa ajili ya manunuzi ya dawa ikiwa ni moja ya mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini.

  Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa na kituo cha televisheni cha TBC, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa Laurean Bwanakunu alisema kuwa serikali inawahakikishia wananchi kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 imetenga fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  “Ikiwa ni asilimia 81 ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika maeneo ya mjini na vijijini, ambapo Bohari Kuu ya Dawa inahudumia vituo 5642 nchi kote” alisema Bwanakunu.

  Pia, Bwanakunu alibainisha kuwa hivi sasa kumekuwepo na upatikanaji wa dawa muhimu 110 kati ya 135 katika vituo mbalimbali vinavyotoa huduma za huduma za afya.

  Katika kuboresha huduma za usambazaji wa dawa nchini , Bohari Kuu ya Dawa imefanikiwa kufungua maduka ya dawa 7 katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Geita, Mbeya na Lindi, ambapo imeanza kusafirisha dawa kwa kutumia ndege na treni ili kufikisha dawa kwa wakati katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

  Aidha, Mikoa na Halmashauri zimetakiwa kuwasilisha maombi yao ya dawa kwa wakati ili kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  0 0

   
  Na   Bashir    Yakub.

  SHERIA  ZILIZOPITIWA :
  1. Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai, Sura ya 20.
  2. Sheria  ya Huduma za Mashtaka  kwa Taifa, Na. 27/2008.
  3. Kanuni  za  Adhabu, Sura  ya  16.
  _______________

  Tundu Lissu anasema  anaamua kumshitaki Makonda kwa kosa la kughushi nk. kwa kuwa Serikali imekataa na haioneshi nia ya  kumfikisha mahakamani Makonda.

  Kama sababu ni kuwa serikali imekataa kumpeleka Makonda mahakamani  ndio maana  Tundu Lissu na wenzake wanaamua sasa kuchukua hatua basi nao hawatafanikiwa.

  Kwa sheria ilivyo hawatafanikiwa mpaka serikali  wanayosema haitaki itake.  Kwa mujibu wa kifungu cha  97 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi  za Jinai kazi ya kufungua na kuendesha mashtaka  yote ya jinai ni kazi ya serikali kupitia  ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).

  Hata hivyo  kwa mujibu wa kifungu cha 99(1)  cha sheria hiyohiyo ni kweli bila ubishi kuwa mtu binafsi  au Wakili yeyote binafsi kama alivyo Tundu Lissu naye  anaweza  kufungua na kuendesha mashtaka ya jinai dhidi ya mtu yeyote mkosaji kama ilivyo kwa DPP wa serikali.

  Pamoja na hayo kifungu cha  97 cha sheria hiyo ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinasema kuwa ikiwa mashtaka yamefunguliwa na mtu binafsi au Wakili binafsi kama alivyo Tundu Lissu basi  mwendesha mashtaka wa serikali  akiamua anaweza kuchukua kesi hiyo.

  Pia kifungu kinasema zaidi kuwa Wakili huyo binafsi katika kesi hiyo aliyofungua atalazimika  kufuata maelekezo   ya  mwendesha mashtaka  huyo wa serikali wakati wote  wa kesi.

  Maana yake ni kuwa ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kubadili jambo lolote katika kesi aliyofungua basi atalazimika kulibadilisha. Lakini kubwa kuliko yote ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kufuta kabisa kesi ya Makonda  basi atalazimika kuifuta. Hii ndio maana ya kifungu hicho.

  KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

  0 0   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa Redio AFM ya Dodoma Bw. Tatenda J. Nyawo baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kupitia redio hiyo hivi karibuni.  Hussein Makame, NEC-aliyekuwa Dodoma

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura zilizoharibika zinazopatikana kwenye chaguzi zinasababishwa na wapiga kura wengi kukosa elimu ya mpiga kura.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani wakati akijibu swali la mmoja wa watangazaji wa kituo cha Redio AFM cha mkoani Dodoma katika mfululizo wa kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio.

  Mtangazaji huyo alihoji kwa nini inajitokeza unapotokea uchaguzi kunakuwa na kura zisizo halili au kura zilizoharibika wakati Tume imekuwa ikitoa elimu ya mpiga kura katika chaguzi zilizopita.

  Bw. Kailima alijibu kuwa kinachosababisha hali hiyo ni ukosefu wa elimu ya mpiga kura kwa wananchi, na ndio maana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi iliona umuhimu wa kutoa elimu hiyo katika kipindi chote cha mwaka.

  “Mkurugenzi tusalie hapo kwenye kura halali na zilizoharibika, elimu hii umekuwa ukiitoa maeneo mbalimbali na leo tuko hapa AFM, kwa nini hadi leo tunakuwa na kura zilizoharibika na kura zisizo halali” alihoji.

  Akijibu swali hilo, Bw. Kailima alisema ukosefu wa elimu ya mpiga kura ndio unaosababisha hali hiyo na ndio maana Katiba iliona kuna umuhimu wa Tume kutoa elimu hiyo kwa muda wote bada ya kutoa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

  “Ukiendea kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimesema Tume itatoa elimu ya mpiga kura.Lakini tumekuwa na tatizo la kutotoa elimu ya mpiga kura baada ya uchaguzi na imekuwa ikitolewa wakati wa uchaguzi baada ya uteuzi na wagombea wakiteuliwa leo kesho kampeni inaanza” alisema Bw. Kailima na kuongeza:

  “Kama Tume na wadau wanaanza kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi hicho, sasa mpiga kura atazingatia kusikiliza kampeni za chama badala ya kusikiliza utaratibu mzima wa namna ya kupiga kura kama”

  Alisema kwa kuwa Tume imeanza kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi chote cha mwaka itasaidia sana ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kura zilizoharibika zitakuwa chache sana.

  Kuhusu kura kuharibika, Bw. Kailima alisema kura yoyote iliyowekwa alama ya vema kwenye eneo la mgombea itahesabika kuwa kura halali.

  “Kwa mujibu wa muongozo na maelekezo yaliyotolewa na Tume kwa wasiamamizi wa uchaguzi, alama yoyote ikiwemo ya X itakayowekwa kwenye chumba cha picha ya mgombea au jina la chama cha mgombea au kwenye chumba cha wazi itakubalika kwamba ni alama halali” alisema.

  Alifafanua kuwa karatasi ya kura itakataliwa iwapo haina muhuri wa kituo au itakuwa na kitu au alama inayomtambulisha mpiga kura na iwapo, haijawekwa alama inayotambuliwa kuwa ni halali.

  Aliongeza kuwa karatasi ya kura itakayopigwa kwa mgombea aliyejitoa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi au ikawekwa alama kwa mgombea zaidi ya mmoja na iwapo haina alama yoyote, itakataliwa.

  Hata hivyo, Bw. Kailima aliongeza kuwa uamuzi wa uhalali wa kura kituoni utaamuliwa na msimamizi wa kituo iwapo atarijiridhisha kuwa kura imeharibika na haiwezi kuhesabiwa na ataikataa na haitahesabiwa.

  Tume imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio za kijamii katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya kutoa elimu ya mpiga kura muda wote.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe.Prof Makame Mbarawa (Wa tatu kushoto waliosimama) akishuhudia Utiaji saini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania Mkataba huo umesainiwa leo mjini Beijing Jamhuri ya watu wa China kati ya Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Li Yuanping Naibu Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China Mhe.Mbarawa yupo mjini Beijing ambapo aliwakilisha serikali ya Tanzania kwenye mkutano wa One belt one Roads Forum.

  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Li Yuanping Naibu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China wakitia saini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania .
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mkono na Naibu Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao, Li Yuanping kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China mara baada ya kutiasaini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania .

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi.

  Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.

  Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
  Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alitenda kosa.

  Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

  Kombakono ameongeza kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.

  Watuhumiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wako nje kwa dhamana.mahakama imemtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini dhamana ya milioni 5. Aidha Mahakama imemtaka kila mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka ofisi yoyote inayotambulika.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.Wakili Kibatala ameieleza mahakama kuwa, tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo atawasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake.

  Amedai kuwa, katika shtaka hilo maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.


  Aidha Hakimu Mwijage ameutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka." Hii siyo kesi ya kuchukua muda mrefu kukamilisha upelelezi, wahusika wote wapo, aliyejeruhiwa na waliojeruhi, mi nilitegemea mtakuja hapa na kusema upelelezi umekamilika", amesema Hakimu Mwijage

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipowasili Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Rioba.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akioneshwa sehemu mbalimbali za studio za Redio na Televisheni za  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika moja ya studio za Televisheni za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na mtangazaji Bi. Asha Haji alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watumishi Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)  alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa maeneo mbalimbali ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe.Dkt Faustine Engelbert leo Bungeni.

  “Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani.

  Aidha kati ya pesa izo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya hapo kahukuwa na mapato hayo.

  Amesema mtambo huu umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za Kimataifa na zile za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano ya Simu za ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa huduma bora kwa wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano nchini pamoja na usimamiaji wa miamala ya fedha  inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.

  “Aidha pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za  mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza Mhe.Ngonyani.

  Aidha Serikali itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la kuchakata taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoa huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang wanne kutoka (kushoto) Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Beno Ndulu, wapili kutoka kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe wa Mkurugenzi huyo wa IMF. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Viettel Tanzania ‘Halotel’, Do Manh Hong na wenzake nane wamehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya milioni 700 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.

  Hukumu hiyo, imetolewa baada upande wa mashtaka kuomba kufanyia marekebisho hati ya mashtaka kwa kuondoa mashtaka matatu Kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili.

  Mashtaka mapya ni pamoja na kusimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutumia mitambo ambayo haijathibitishwa na kuitia hasara Serikali na TCRA ya milioni 459.

  Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Wilbard Mashauri amesema amewatia hatiani washtakiwa mwenyewe baada ya kukiri kutenda makosa yao

  Kabla ya kuwasomea hukumu, Hakimu aliwauliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote ambapo wakili, Johavenes Zacharias ameiomba mahakama kutoka adhabu stahiki kwa washtakiwa.

  Naye Wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuwapa adhabu ndogo washtakiwa kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza na wanafamilia zinazowategemea.

  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amewahukumu washtakiwa kulipa faini ya jumla ya faini ya milioni 700. 

  Akifafanua adhabu hiyo, hakimu Mashauri amesema kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya milioni tano kwa kila shtaka linalomkabili na pia walipe milioni 459 kwa TCRA kwa hasara waliyoisababisha.

  Ameongeza kuwa, ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao na kwa wafanyabiashara wengine wanaohujumu uchumi.Ameongeza kuwa, watuhumiwa wamekuja nchini kuwekeza kwenye biashara na siyo kuhujumu mitambo ya nchini.

  "Washtakiwa hawa ni wafanyabiashara na wamekuja kwa ajili ya kuwekeza, hivyo ili kuonyesha Tanzania ipo makini kwenye masuala ya uwekezaji lazima wafate sheria" amesema Mashauri.

  Mbali ya Hong, watuhumiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka na Viettel Tanzania Limited.

  Katika mashtaka yao wamedaiwa, kuwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 Dar es Salaam walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.

  Wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho waliendesha hiyo mifumo ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila ya kuwa na leseni.Pia inadaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni. Pia katika tarehe isiyofahamika Novemba 2016 walisimika vifaa hivyo ikiwamo sim box yenye namba ya siri 1152000.8.n.t.n na Laptop mbili aina ya Dell bila ya kuwa na kibali cha TCRA.

  Katika kipindi hicho, washtakiwa hao wanadaiwa kuunganisha vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.

  Kwa upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la kusajili lakini za simu 1000.

  Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA na serikali ya Tanzania ya milioni 459.

  Mpaka Michuzi blogu inaondoka katika viunga vya Mahakama, ni mkurugenzi pekee ndiye aliyelipa faini, huku watuhumiwa wengine wakiendelea kusota lupango.Mkurugenzi huyo amelipa jumla ya milioni 479 ambazo ni faini yake ya milioni 20 ambapo ni kwake yeye na kampuni na Viettel Tanzania Ltd. 
   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel, Do Manh Hong, kwenye tisheti ya kijani na wenzake ambao ni raia wa Pakistan na Sri Lanka wakirudishwa mahabusu baada ya kuhukumiwa kulipa faini zaidi ya milioni 700 baada ya kupatikana n hatia ya mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi

  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Ahmad Khalifa  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu  kwa kosa la kumtishia kumua Hawa Mshama.

  Akisomewa mashtaka hayo katika Mahakama ya mwanzo Kinondoni mbele ya Hakimu Marko Mochiwa chini ya kifungu cha 89 -16 (2) mnamo tarehe 9/5/2017  eneo la Kinondoni Msisiri mshatikiwa alitoa lugha ya matusi  kwa Bi Hawa Mshama .

  Hata hivyo mshatikiwa alikana shitaka hilo na kuambiwa kuwa dhamana iko wazi na akishindwa ataenda mahabusu mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Mei 24.

   Ahmad Khalifa   akingizwa katika mahakama ya mwanzo Kinondoni


  0 0


  George Binagi-GB Pazzo @BMG.

  Wakazi wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

  Taharuki hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.

  Zoezi la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.

  Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.

  Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na usambazaji wa taarifa za upotoshaji.
  Zoezi la kuung'oa mti likiendelea
  Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuanguka licha ya kuvutwa
  Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
  Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
  Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limezaa matunda
  Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, akizungumzia tukio hilo
  Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works akizungumzia tukio hilo
  Mkazi wa jiji la Mwanza akizungumzia tukio hilo
  Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia tukio hilo
  Wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
  Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
  Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
  Kushoto ni dereva aliyekuwa akiendesha mtambo uliong'oa mti huo

  0 0


  0 0

   Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua moja ya semina za mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.

  KILA ifikapo Mei 3 ya kila mwaka wanahabari na wadau wa vyombo vya habari ulimwenguni huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Maadhimisho ya mwaka huu (2017) kitaifa nchini Tanzania yalifanyika mkoani Mwanza na kushirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari. 

   Miongoni mwa hoja zilizoteka mijadala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2017 jijini Mwanza ni suala zima la usalama wa wanahabari wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao pamoja na uwepo wa mafunzo anuai ya mara kwa mara kwa wanahabari kuwanoa zaidi. 

  Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), ni miongoni mwa taasisi wadau waliofanikisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka 2017 kitaifa yaliofanyika mkoani Mwanza. Bi. Valerie Msoka ni Mwanachama wa TAMWA, akizungumza katika maadhimisho ya mwaka huu kuwasilisha ujumbe wa chama hicho kwa wadau wa habari.

   Anasema TAMWA imejitahidi katika kuwanoa wanahabari ili kuhakikisha wanabobea kwenye maeneo mbalimbali ya uandishi wa habari huku lengo likiwa kuwajengea uwezo zaidi. Bi. Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA hapo nyuma kabla ya uongoziwa wa Mkurugenzi wa sasa wa chama hicho, Edda Sanga anabainisha wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia weledi na ubobezi wa wanahabari hasa katika uandishi wa habari za ukatili kwa jamii. 

  Anasema tamwa katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kwa kipindi cha mwaka 2015 na 2016 imeelimisha idadi kubwa ya wanahabari kwenye ubobezi wa uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia eneo ambalo limekuwa likionekana kupwaya kiuandishi. 

   Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2350 na wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsia ya kuandika habari za ukatili wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali. 

  Anasema waandishi hao baada ya kupata mafunzo hayo wamekuwa wakitumia ujuzi huo kuandika na kuibua habari za vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo ambalo limesaidia baadhi ya maeneo mamlaka husika kuchukua hatua juu ya vitendo hivyo, hali ambayo imekuwa ikisaidia kupungua kiasi fulani kwa vitendo hivyo kwenye jamii ukilinganisha na hapo awali.   Baadhi ya wanahabari wapiga picha ambao walishiriki mafunzo ya upigaji picha za ukatili yaliyoandaliwa na TAMWA wakimsikiliza mkufunzi wa mafunzo hayo, Mwanzo L. Millinga (wa kwanza kulia) kutoka ‘Practical School of Journalism’ (PSJ). Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kulia) akizungumza katika moja ya mikutano ya mafunzo kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa TAMWA.[/caption]   Aidha Bi. Msoka anaongeza kuwa utaratibu huo wa kuwajengea uwezo wanahabari umekuwa ukifanywa mikoa mbalimbali huku ukijumuisha wanahabari kuandaliwa kimafunzo katika semina kadhaa na baadaye kufuatiliwa kwenye utendaji ili kubaini mabadiliko kimafanikio kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo waliyopata. 

  Wananchi kwa upande mmoja nao wamekuwa wakihamasika na kutumia vyombo vya habari katika kuibua matukio hayo ya kikatili, jambo ambalo limeanza kuleta mafanikio kiasi fulani. Bi. Msoka anaendelea kubainisha kuwa TAMWA katika kutekeleza mradi wake wa GEWE II kimeweza kuunda kamati za kuelimisha jamii jinsi ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya kumi za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, ambazo zinawahusisha wanahabari ili kuwezesha jamii kushirikiana na vyombo vya habari kuweza kuvitolea taarifa vitendo hivyo bila woga. Anaeleza kuwa kwa kisi kikubwa kamati hizo zimesaidia kuibua matukio hayo kwa kiasi kikubwa kwa vyombo vya habari.    
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

  Pamoja na hayo Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kinaamini kuwa kupitia maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ya mwaka huu (2017) wanahabari kwa kutumia changamoto zilizoibuka dhidi yao, katika kujitathmini, watafanya kazi zao kwa weledi na uaminifu ikiwa ni pamoja habari zenye usawa wa pande zote husika.

   Hii ni pamoja kujitahidi wanatasnia hiyo kuibua mambo yanayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo ili yafanyiwe kazi, pia kujiepusha na habari ambazo kwa sehemu zinaweza kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao wenyewe au wananchi katika taifa la Tanzania. Kama hiyo haitoshi TAMWA, imeendelea kuwanoa wanahabari katika nyanja nyingine za kimafunzo. TAMWA ilijiunga katika mapambano ya ajali za barabarani kwa kutoa mafunzo kwa wanahabari mbalimbali. 

  Katika ufafanuzi juu ya hatua hiyo inabainisha kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga anasema katika moja ya mafunzo kwa wanahbari kuwa wana kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. Anasema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia. Sehemu ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam Sehemu ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akizungumza na wawekezaji mbalimbali katika sekta ya madini, waliowasilisha maombi ya kupatiwa leseni kwa ajili ya kuwekeza katika sekta husika.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisaini leseni mbalimbali za wawekezaji katika sekta ya madini.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ iliyohamishwa kutoka kwa Salim Mohamed Salum (wa pili kutoka kushoto) kwenda kwa wawekezaji wa kampuni ya S & T Marble and Mining Limited (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akimkabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Limestone’, mwakilishi wa Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement, Richard Magoda (katikati). Kulia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka.
  Mwekezaji, Mbarouk Saleh Mbarouk (katikati), akionesha leseni yake ya uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ katika eneo la Mkuyuni Matombo wilayani Morogoro, baada ya kusainiwa na kukabidhiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto). Kulia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka.

  Na Veronica Simba – Dodoma.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa kusaini ombi la uhamishaji wa leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya Shaba Namba ML 571/2017 kutoka kwa mtanzania David Stanley Kayongoya kwenda Kampuni ya Mechanized Minerals Supreme Mining Company Limited inayomilikiwa na raia kutoka China.

  Profesa Muhongo alikataa kusaini leseni hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 0.43 katika eneo la Fufu wilayani Chwamwino mkoani Dodoma, baada ya kubaini kuwa mtanzania anayetaka kuhamishia leseni hiyo kwa Raia wa China, hatanufaika kwa kiwango kinachoridhisha.

  Akizungumza na wawekezaji mbalimbali wa sekta husika, waliofika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, kwa ajili ya kusainiwa leseni zao za uwekezaji, jana (Mei 15), Profesa Muhongo alisisitiza kuwa ni lazima wawekezaji katika sekta husika wazingatie suala la maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla, wakati wanapotekeleza kazi zao za uwekezaji.

  Waziri Muhongo alimwagiza mwekezaji huyo raia wa China kujadiliana kwa mara nyingine na mtanzania mwenye eneo husika (David), ili kuhakikisha ananufaika ipasavyo na uwekezaji huo.

  “Ili niweze kusaini leseni hii, rudini mezani, mzungumze na kukubaliana ili David aweze kunufaika. Hatuwezi kukubali kuona watanzania wakidhulumiwa namna hii,” alisisitiza Waziri.

  Awali, ilielezwa kuwa mkataba wa mauziano ya leseni husika unaonesha kuwa David amepokea kiasi cha shilingi milioni 30 za kitanzania. Waziri alipotaka kujua endapo kuna manufaa mengine ambayo David atapata, alielezwa kuwa ataajiriwa katika kampuni hiyo kama kibarua, ndipo Waziri akakataa kusaini leseni husika.

  Ili kuhakikisha suala hilo linatekelezwa ipasavyo, Profesa Muhongo alimwagiza Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, kujiridhisha kwa kupokea ahadi za maandishi kutoka kwa mwekezaji yeyote anayeomba leseni, namna ambavyo atazingatia maslahi ya nchi, kabla ya kumpatia leseni anayoomba.

  Kwa upande wake, Kamishna Mchwampaka, pamoja na kuahidi kuzingatia na kutekeleza agizo la Waziri; aliwataka wawekezaji hao kuzingatia kanuni na miongozo mbalimbali ya uwekezaji kama inavyobainishwa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010.

  Wawekezaji wengine waliokidhi vigezo na Leseni zao kusainiwa ni pamoja na ya Salim Mohamed Salum inayohusisha uhamishaji wa leseni tatu za uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ namba ML 566/2016 iliyoko Mumbwi wilaya ya Handeni, ML 567/2016 iliyoko Ulanga Morogoro na ML 568/2016 iliyoko Kwenkambala – Handeni mkoani Tanga kwenda kampuni ya S & T Marble and Mining Limited.

  Nyingine ni leseni namba ML 577/2017 ya Mbarouk Saleh Mbarouk, inayohusisha uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ kwa kipindi cha miaka 10 katika eneo la Mkuyuni Matombo wilayani Morogoro.

  Vilevile, leseni nyingine iliyosainiwa ni ya Kampuni ya Tanzania Portland Cement, namba ML 575/2017 inayohusisha uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Limestone’ kwa kipindi cha miaka 10 katika eneo la Wazo Hill Wilaya ya Kinondoni. Ilielezwa kuwa, maombi ya leseni hiyo yanatokana na leseni ya utafiti wa madini namba PL 9416/2013.

older | 1 | .... | 1233 | 1234 | (Page 1235) | 1236 | 1237 | .... | 1897 | newer