Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUITAKIA KILA LAKHERI TIMU YA TAIFA 'SERENGETI BOYS' KATIKA MASHINDANO YA AFCON NCHINI GABON


Yara yatoa huduma ya upimaji udongo bure

$
0
0
Wakulima wa maembe na mbogamboga Mkuranga, wakipewa elimu jinsi ya kuchukua udongo. 
 
Yara Tanzania Ltd, imewekeza katika maabara ya kupima udongo ili kuweza kutambua virutubisho vilivyopo na vinavyokosekana kwenye udogo. Mara baada ya matokeo ya udongo kampuni hiyo kupitia wataalamu wake walio bobea kwenye sekta hiyo, hutoa ushauri kwa wakulima nini cha kufanya kulingana na zao lililolimwa au linalotarajiwa kulimwa. 

Afisa ugani wa kampuni hiyo Bw. Maulid Mkima, alisema "lengo kuu la kampuni ya Yara Tanzania kuweka maabara ya udongo,ni kuweza kuwapa wateja wao huduma nzuri na mpangilio sahihi wa lishe bora na linganifu ya mimea"

TANZANIA HAIJAFIKIWA NA UGONJWA WA EBOLA-DKT MPOKI.

$
0
0
NA ALLY DAUD-WAMJW.

TANZANIA bado haijafikiwa na ugonjwa wa ebola kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kutokana na utafiti uliofanyika na wataalamu wa afya hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu tishio la uwepo wa ugonjwa huo katika nchi za jirani .

“Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari zaa kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa watanzania  hususani wanaoishi mikoa ya karibu na nchi yaa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo ikiwemo Mwanza,Kagera,Kigoma,Rukwa, Katavi na Songwe wanatkiwa kuwa makini kwani ugonjwa wa ebola  upo nchini humo.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa ugonjwa wa ebola unasababishwa na kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa mwenye ebola na mizoga  na dalili za ugonjwa huo  zinatokea`baada siku mbili pindi mgonjwa anapopata maambukizi y ugonjwa huu zikiwemo kutokwa na damu sehemu za puani,masikioni na homa kali.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa  Wizara imechukua hatua za kutoa mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya ,kuandaa  kituo cha kuhifadhi  wagonjwa na`kutibu ugonjwa wa ebola kilichopo wilaya ya temeke kwa wagonjwa wanaotokea mkoa wa  Dar es salaam na kutoa vipimo vya joto la mwili kwa wasafiri ili kutambua ugonjwa huo.

Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa Wizara itashirikiana na sekta mbalimbali za afya ili kupata mbinu za kudhibiti ugonjwa huo na Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola kupitia namba 117 bilaa y malipo kwa mitaandao yote.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya Wananchi kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa ebola kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchin leo jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Afya,waandi wa habari  wakimsikiluliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel  Massaka, Globu ya Jamii.

TADB YATEMBELEA VYAMA VYA USHIRIKA VYA MSINGI MANYARA

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Manyara
Katika kufanikisha azma yake ya kuwa benki kiongozi  katika kuleta maendeleo ya kilimo nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imevitembelea vya ushirika vya msingi mkoani Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.

Akizungumza wakati wa ziara zake katika vijiji vya Masakta, Gallapo na Gendi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Hivyo TADB ina wajibu wa kuwasaidia wakulima nchini ili kuwafikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Bw. Assenga aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwanyanyua wakulima katika uongezaji tija wa kilimo nchini kwa kutoa mikopo na kusaidia shughuli mbali mbali za uongezaji tija katika kilimo.

“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima TADB kwa kushirikisha wadau wa Kilimo, utafiti na huduma za ugani tumejipanga kuwapatia wakulima mafunzo ya kilimo cha kisasa cha ili waweze kutumia mbinu bora za kilimo,” alisema.

Akizungumza katika kikao chao na ugeni wa TADB, Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni alisema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa kuwa itachagiza juhudi za kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.

“Kwa kweli tunapongeza kwa kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi mikopo mingi kutoka taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,” alisema.

Naye Bw. Petro Dali, ambaye ni Mwenyekiti wa Gendi AMCOS alipongeza uanzishwaji wa TADB kwa kuwa licha ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo hasa kwa wakulima wadogo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kuu ikiwa ni ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.

“Benki imekuja wakati muafaka kwa kuwa tunaamini itatusaidia katika kupata mikopo nafuu ya ununuzi wa pembejeo za kilimo na gharama na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Gallapo AMCOS, Bw. Orondi Doita alitoa wito kwa Benki ya Kilimo kuanza kuwakopesha ili waweze kujipanga mapema katika ununuzi wa mazao ili waweze kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha chakula kinabaki nchini ili kuongeza usalam wa chakula.

Kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kunaleta suluhisho la changamoto nyingi zilizokuwa zinaikabili sekta kilimo nchini kwani inalenga kuboresha upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.
 Katibu wa Homari AMCOS, Bw. Abdul Msangi (kulia) akiwakaribisha wageni Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania walipotembea AMCOS hiyo.
 Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni (kushoto) akizungumza na wageni kutoka TADB walipotembea AMCOS hiyo. Wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa RIVACO, Bw. Lohay Langai (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
 Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akitaja fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya Kilimo wakati wa kikao cha pamoja kati ya TADB na Bodi ya Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni (kushoto) wakikagua mahindi katika moja ya mashamba waliyoyatembelea.
 Sehemu ya mahindi yaliyokwisha vunwa yakiwa yamehifadhiwa Kijijini Masakta.
 Mwenyekiti wa Gendi AMCOS, Bw. Petro Dali (aliyesimama) akizungumza wakati wa mazungumzo na TADB (hawapo pichani). Bw. Dali alizungumzia umuhimu wa Sekta ya Kilimo na mchango wa TADB katika sekta hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Gendi AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Gallapo AMCOS, Bw. Orondi Doita (aliyesimama) akizungumza wakati wa mazungumzo na Benki ya Kilimo (hawapo pichani). Bw. Doita alitoa wito kwa Benki ya Kilimo kuanza kuwakopesha ili waweze kujipanga mapema katika ununuzi wa mazao kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Gallapo AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.

TAASISI YA KARIMJEE JIVANJE YAMKABIDHI KITABU CHA HISTORIA KWA JAJI MKUU NA RAIS WA MAHAKAMA KUU YA KENYA, DAVID MARAGA MJINI NAIROBI

$
0
0
Meneja Mkuu taasisi ya Karimjee Jivanje, Bi. Devotha Rubama akiwasilisha kitabu cha Historia cha Taasisi ya Karimjee Jivanje kwa Mhe. Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama kuu ya Kenya, David Maraga EGH katika Taasisi ya Asia na Maonyesho ya Stawisha Maisha mjini Nairobi Mei 12-14. Nyuma ni Mwenyekiti wa Chandaria Foundation na mmiliki wa Aluminium Africa, Bw. Manu Chandaria.

UJAZO WA LITA 6494 ZA DAWA HATARI ZAKUTWA KWENYE GHALA MWENGE

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini inamshikilia mmiliki wa kampuni ya Techno Net Scientific kwa kuingiza kemikali bashirifu nchini zenye ujazo wa lita 6494 kwa kukiuka sheria na taratibu.

 Imeelezwa kuwa, mmiliki huyo amekiuka sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya 2015 na ile usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani, sheria ambayo inasimamiwa na Mkemia mkuu wa Serikali..

Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga amesema kuwa, Kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni hiyo, yenye makazi yake eneo la mwenge kunatokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema mwezi uliopita waliowataarifu kuwa kampuni hiyo inaagiza kemikali bashirifu, ambazo ni hatari kwa matumizi na zisiporatibiwa zinaweza kutumika vibaya na kuleta madhara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, baada ya ziara fupi ya kutembelea maghala mawili ya kampuni  hiyo yanayotumika kuhifhadhia kemikali hizo, Sianga amesema, uchunguzi wao umeonyesha kuwa, kampuni hiyo inaagiza kemikali bila kibali.

“Tulichogundua ni kwamba kampuni hii ya Tecno Net Scientific yenye makazi yake eneo la mwenge, imeagiza kemikali nyingi ambazo ni bashirifu, kemikali bashirifu ni kemikali muhimu kwa utengenezaji wa kawaida wa dawa za binadamu lakini pia zikichepushwa  zikiwa diverted zinaweza kutengeneza dawa za kulevya za Heroine, Cocaine na nyinginezo ambazo huzalisha kemikali taka zenye sumu ambazo zinaweza kuhatarisha afya za watu na kuchafua mazingira.

Ameongeza kuwa,wamegundua kuwa kampuni hiyo pia iliagiza kemikali nchini ufaransa kwa kibali cha kughusi na imekua ikiendesha shughukli zake za biashara ya kuuza kemikali bila kibali, licha ya vibali vyake kuisha muda wake tokea mwaka jana.

 Ameongeza kuwa, mmiliki huyo anaendesha biashara ya kemikali bila ya kuwa na wataalamu kwani yeye binafsi ana elimu cheti cha huku mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anaelimu ya darasa la saba na baadae akajiendeleza Veta na kuwa fundi magari wakati kisheria ili uweze kuendesha biashara hiyo unatakiwa uwe na kuanzia diploma ya kemia na kuendelea.

“Pamoja na Kemikali hizi bashirifu kuwa na matumizi halali kama viwandani na hospitali lakini zimewekewa utaratibu wa udhibiti kitaifa kitaifa na kimataifa kuanzia ununuaji, usafirishaji, jinsi ua uhifadhi na utumiaji wake kwakuwa kemikali hizo zikiachwa bila udhibiti watu wenye dhamira mbaya wanaweza kuzitumia kutengeneza dawa za kelevya”, amesema Sianga.

Ameongeza kuwa mamlaka inachunguza tuhuma dhidi ya kampuni hiyo zikiwezo za kumiliki kemikali ambazo hazijasajiiwa na mamlaka husika kinyume na sheria baada ya usajili wake katika biashara kukoma, kutokuwa na taarifa za mwenendo mzina wa kemikali wanazoingiza  nchini na kuzisambaza kwa wateja, na nyinginezo nyongo.

Amesema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea na utakapokamilika hatua za kesheria zitachukuliwa na atafikishwa mahakamani.
 Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge 
  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge 
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akitoa ufafanuzi  juu ya  kemikali bashirifu zinavyoweza kuchepushwa kwa matumizi mengine
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha baadhi ya Maghala kwa ndani sehemu ya ghala ya kuhifadhi Dawa.
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha ghala la pili la kuhifadhi Dawa ambapo wamebaini kuwapo kwa dawa zilizomaliza muda wake.
Sehemu ya  nje ya jengo la kampuni ya  Tecno Net Scientific  ambalo lilitumika katika kutengenezea na kuhifadhi madawa hayo

WALIMU WA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) NA VYUO BINAFSI VYA AFYA WAANDALIWA MAFUNZO YA MAADILI

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ameiagiza Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kufanya tafiti kujua chanzo cha mmongonyoko wa maadili kwa wafanyakazi wa afya wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.

Alishauri baada ya kupata majibu ya tafiti hizo kuishauri serikali hatua ya kuchukuliwa ili kuinusuru hadhi ya taaluma ya afya ambayo inajengeka katika misingi ya ukarimu na kutoa huduma bila upendeleo.

Naibu Waziri ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku nne juu ya Maadili na Utafiti kwa wakufunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na viongozi wa wauguzi wa Hospitali binafsi na Serikali katika skuli hiyo iliopo Mbweni.

Alisema watendaji wa Hospitali na vituo vya afya na hasa vya Serikali baadhi yao wanakiuka maadili ya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha mbaya

Alisema tatizo la unyanyasaji wagonjwa limekuwa kubwa zaidi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo ni tegemeo kubwa la wananchi wa Zanaizbar.

Aliongeza kuwa jambo la kusikitisha ni kuwa wafanyakazi wa hospitali za serikali ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa kukiuka maadili wanapokuwa katika vituo binafsi wanakuwa ni mfano wa kuigwa kwa tabia njema.

Hata hivyo Bi. Harusi aliwataka walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba kuwa mfano bora wa maadili na kuimarisha somo hilo kwa wanafunzi wao ili kurudisha hadhi ya taaluma ya afya na wananchi waendelee kuwaamini.

Kaimu mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Dkt. Salum Seif alisema somo la maadli ni moja kati ya masomo yanayopewa kipaumbele katika skuli hiyo lakini kupata elimu ni jamabo moja na kuitumia elimu uliyonayo ni jambo jengine. 

Alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa watakuwa waangalifu na kuongeza udadisi katika sulala la maadili kwa wanafunzi wanaomba kujiunga na Skuli hiyo na atakaeonekana hawezi kukidhi kigenzo watamuacha.

Alisema tatizo kubwa linalochangia ukosefu wa maadili Zanzibar ni watu kuoneana muhali kutokana na kujuana sana na kupelekea kuzifumbia macho sheria zilizopo.
Kaimu Naibu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Bi. Amina Abdulkadir akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kufungua warsha ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli hiyo na viongozi wa wauguzi wa Hospitali za Serikali na Binafsi huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisisitiza maadili kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya wakati akifungua warsha ya siku nne ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi katika skuli hiyo iliopo Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya maadili na utafiti wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo inayofanyika Skuli ya afya na Sayansi za tiba Mbweni.
Mkuu wa Idara ya Uuguzi Mwanaisha Juma Fakih akisoma malengo makuu ya warsha hiyo inayowashirikisha walimu wa Skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi wa hospitali za serikali na hospitali binafasi Mbweni.
Kaimu Mkuu wa Skuli ya afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Salum Seif akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo katika skuli hiyo iliyopo Mbweni.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya (wa kati kati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya maadili na utafiti inayofanyika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

WAETHIOPIA ZAIDI YA NANE WAKUTWA WAMEFARIKI PORINI KATIKA KIJIJI CHA AMANI MAKOLO MKOANI RUVUMA

$
0
0
Ditha nyoni - RUVUMA

Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.

Habari kutoka jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kupitia kaimu kamanda wa polisi ACP DISAMASI KISUSI zinasema raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi ya AFRIKA KUSINI kupitia Upande wa MALAWI mwa ziwa NYASA.

Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori wakitokea NAMANGA, ARUSHWA hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao zilianza kubadilika na kupelekea kufariki.huku miili ya marehemu hao ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya MBINGA
Jeshi la polis mkoa wa ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA ALBINO KITAIFA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gabriel Aluga na kushoto ni Afisa Mawasiliano na Habari wa chama hicho Bw. Josephat Torner.
Afisa Mawasiliano na Habari wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Josephat Torner (katikati) akifafanua jambokwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. Nemes Temba na kushoto Mwekahazina wa chama hicho Bw. Abdulah Omar.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (mwenye koto jeusi) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa


Na Husna Said & Nuru Juma- MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya ualbino yatakayofanyika Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania Nemes Colman Temba alipokutana na waandishi wa habari. 

Temba alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuibua mijadala na tafakuri kwa wadau juu ya ukusanyaji endelevu wa takwimu,uchambuzi na upatikanaji wa watu wenye Ualbino kwa wakati ili Serikali iweze kuwasajili, kuwahudumia na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanakuwa salama.

“Bila ya utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Takwimu Serikali haitaweza kupanga vyema juu ya ustawi wa watu wenye ualbino, hivyo maadhimisho ya mwaka huu yataibua mjadala wa umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu kwaajili ya kusaidia katika mipango ya maendeleo ya watu wenye ualbino”,alisema Temba.

Aidha alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyojumuisha takwimu za watu wenye ualbino ilisaidia kubaini idadi ya watu hao ambapo walikuwa 16,376 wakiwemo Wanaume 7,620 na Wanawake 8,756.

Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Mh.Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusikiliza na kutekeleza ombi la masuala ya watu wenye ulemavu kuhamishiwa ofisi ya Waziri Mkuu kwani lilikuwa ombi la muda mrefu kwaajili ya ustawi wa watu wenye ualbino na wenye ulemavu kwa ujumla. 

Kwa upande wake afisa habari na uhusiano wa wa chama hicho, Josephat Torner alisema kuwa, mauaji dhidi ya watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi kikbwa kulingana na hapo awali na mapambano dhidi ya vitendo hivyo bado yanaendelea licha ya ukimya uliokuwepo kwa sasa.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu Takwimu na Tafiti kwa Ustawi wa Watu Wenye Ualbino yatahudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wadau toka Sweden, Uholanzi, Marekani, Canada, Uingereza, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Mataifa mengine.

Siku hiyo ya kimataifa ya uelewa juu ya Ualbino itatanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo hamasa kupitia vyombo vya habari,uendeshaji wa kliniki za ngozi kwa maalbino pamoja na utoaji wa msaada wa kisheria,midahalo na makongamano na ukusanyaji wa takwimu za watu wenye ualbino.

MUWEMBE WASITISHA SAFARI DAKIKA 45 PEMBA

$
0
0
Wananchi wa kisiwa cha Makoongwe wilaya ya Mkoani Pemba, wakiwa safarini ndani ya mashua yenye mashine, wakitokea Mkoani mjini kwenda kijijini kwao, ambapo hayo ndio maisha yao ya kila siku, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Ipo haja kwa wazazi na walezi, kuwa makini na maeneo wanayocheza watoto wao, ambapo mtoto ambae hakupatikana jina lake, akikata tawi, alilolikalia karibu na skuli ya Makoongwe wilaya ya Mkoani
Mwandishi wa Shirika la Magazeti ya Serikali ofisi ya Pemba Haji Nassor, akizungumza na Mwenyekiti Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukimwi na Mazingira JSEUMA, Juma Ali Mati juu ya hatua waliofikia, ndani ya jumuia yao, kuhusu kuwaelimisha wananchi kupanda miti na kuhifadhi mazingira
Mwananchi wa shehia ya Mkanyageni wilaya ya Mkoani Pemba alietambulika kwa jina Seif, akichangia jambo kwenye mkutano wa uhamasishaji wa upandaji miti uliondaliwa na Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukiwmi na , Mazingira JSEUMA ya Kisiwani panza, wilaya ya Mkoani Pemba
Wandishi wa habari kisiwani Pemba, wakisikiliza mada kwenye mmoja ya mikutano iliofanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Gombani Chakechake Pemba, ambao uliandaliwa na kitengo cha malaria Pemba.


NA HAJI NASSOR, PEMBA

ABIRIA waliokuwa wakitokea Unguja, wafanyakazi wa serikali na taasisi binafsi pamoja na wananchi wengine, juzi walilazimika kusubiri kwa dakika 45, kwenye eneo la mpakani baina ya wilaya za Mkoani na Chakechake, kufuatia mti aina ya Muwembe kukatika na kuziba barabara.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, abiria na wananchi hao walisema, baada ya kuteremka meli bandari ya Mkoani, walipanda gari za abiria ili kuelekea kwenye mkaazi yao, ingawa walipofika mpakani walikwama.

Walisema walikaa hapo tokea majira ya saa 10:30 hadi saa 11:15 ndipo walipofanikiwa kupita baada ya taasisi kadhaa wakiwemo idara ya misitu kukakata Muwembe.Walisema kama sio taasisi za serikali zikiwemo KZU, Idara ya misitu na wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo la Vuleni kushirikiana wengeutumia hadi saa 1:30.

Mmoja kati ya abiria aliekuwa akitokea Unguja, Juma Mshihiri Hassan mkaazi wa Konde, alisema baada ya kufika hapo walishuhudia foleni ya gari zaidi ya 30 na waliarifiwa kwamba barabara imefungika, kutokana na kuanguka Muwembe katikati.

Nae Asha Msabaha Himid wa Chasasa alisema, alitarajia akapeleke mzigo kwao, kisha arudi bandarini kwa vile siku ya pili alikuwa anasafiri, ingawa kutokana na kuchelewa kuondoka hapo itakuwa vigumu.“Sisi tupo hapa zaidi ya dakika 45, maana tunakaribia tu na Muwembe huo unanguka, na kuziba njia yote, maana upande mwengine kuna bonde, hapana pakukimbilia, ingawa baadae walikuja watu kuukata na kuondoka’’,alisema.

Hata hivyo dereva wa gari ya Chakechake –Mkoani aliejitambulisha kwa jina moja la ‘Kipara’ alisema katika kipindi hichi cha mvua, lazima wawe makini maana miti huunguka kutokana na ardhi kushiba maji.

Kwa upande wake dereva aliefanikiwa kupenya kwenye eneo hilo la Vuleni na kisha Muwembe kuanguka, Ali Haji Juma, alisema aliouna umeshainama, ingawa baada ya nusu saa aliamua kupita salama.“Mimi baada ya kupita dakika 10 tu, napata taarifa kuwa, umeshanguka na gari zimekwama, ingawa na juzi nilikwama Ngwachani baada ya Muwembe kuanguka na kuziba barabara’’,alifafanua.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mkoani ambae nae juzi ni miongoni mwa wananchi waliokwama, Hemed Suleiman Abdalla, aliwashukuru watendaji wa taasisi mbali mbali, kwa umoja na mshikamano wao.

Tokea kuanza kwa mvua hizi za masika, tayari miti zaidi ya sita imeshaanguka na kuziba barabara ikiwemo eneo la Ngwachani, Ngezi, Vuleni na Mtambile.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA ATEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO ARUSHA

$
0
0
Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akila chakula cha mchana na watoto katika kijiji cha watoto kilicho chini ya Shirika la SOS Children Villages alipofanya ziara katika shirika hilo leo Ngaramtoni Mkoani Arusha.
Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akitoa boksi la sabuni kwa mlezi wa moja ya familia inayoongoza na vijana Leo Mkoani Arusha.
Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na vijana wawili wanaoongoza familia ambapo aliwapongeza kwa hatua wanazozifanya katika kuisimamia familia.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha Wageni alipofika katika kijiji cha Watoto kinachosimamiwa na Shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu (SOS Children Villages) lililopo Ngaramtoni Mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu-SOS Children Villages Tanzania Bw.Anatory Rugaimukamu akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga wakati wa ziara ya kuangalia namna shirika hilo linavyofanya kazi.
Mkurugenzi wa Shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu-SOS Children Villages Tanzania Mkoa wa Arusha Bw.Francis Msollo (kulia) akimueleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga namna shirika hilo lilivyofanikisha kutimiza ndoto za vijana wengi waliolelewa kituoni hapo Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Bw.Anatory Rugaimukamu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga (kushoto) akiongea na viongozi wa Shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu-SOS Children Villages Tanzania na kuwapongeza kwa jitihada wanazozifanya katika kuhakikisha wanakuza watoto na kutimiza ndoto zao,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Bw.Anatory Rugaimukamu na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika Mkoa wa Arusha Bw.Francis Msollo.
Baadhi ya watoto wakiwa katika shule iliyo ndani ya Kijiji cha Watoto chini ya shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu-SOS Children Villages Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga(wa Pili kutoka kushoto) Mkurugenzi Maendeleo ya watoto Margaret Mussai(wa Pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Shirika linalohudumia watoto wenye uhitaji katika malezi na elimu-SOS Children Villages Tanzania Bw.Anatory Rugaimukamu (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Shirika SOS Children Villages Tanzania Mkoa wa Arusha Bw.Francis Msollo (kulia) wakienda kuangalia makazi katika kijiji cha watoto.
Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na watoto katika kijiji cha watoto kilicho chini ya Shirika la SOS Children Villages alipofanya ziara katika shirika hilo leo Ngaramtoni Mkoani Arusha
Mama Mlezi katika kijiji cha watoto kilicho chini ya Shirika la SOS Children Villages Bi. Cylichelia Byabato akimuonesha Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya malazi ya watoto katika Kijiji hicho leo Ngaramtoni Mkoani Arusha.
Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)Bi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na watoto katika kijiji cha watoto kilicho chini ya Shirika la SOS Children Villages alipofanya ziara katika shirika hilo leo Ngaramtoni Mkoani Arusha
 

DED MEATU: MBEGU BORA, KILIMO CHA MKATABA MKOMBOZI KWA WAKULIMA WA PAMBA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza(Mwenye kofia ya njano akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba ya Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma, Singida na Tabora walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kwa wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Meja Jenerali Ezekiel Kyunga akiwasalimia wananchi wa Kata ya Mwabusalu wakati wa ziara ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) ya katika kata hiyo wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salum Kijuu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Meatu  wakati wa ziara ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) ya katika kata ya Mwabusalu  wilayani Meatu.
Bw.Charles Thobias Mkulima kutoka kata ya Mwabusalu ambaye ametumia mbegu bora ya pamba ya (UKM08) akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba ambayo ni  Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma, Singida na Tabora walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata hiyo wilayani Meatu.

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amesema Matumizi ya Mbegu bora na Kilimo cha Mkataba ni suluhu ya wakulima wa pamba inayoweza kuwasaidia kuongeza uzalishaji.

Manoza ameyasema wakati akitoa taarifa ya Wilaya ya Meatu kuhusu kilimo cha Pamba kwa Wakuu wa Mikoa nane ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba waliotembelea eneo hilo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma, Singida na Tabora katika ziara yao kuona mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.

Amesema kupitia kilimo cha mkataba wananchi watakuwa na uhakika wa kupata pembejeo bora za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na viuadudu kutoka kwa watu au makampuni yatakayoweka mikataba nao.

“Tunatarajia kuongeza uzalishaji ili kupata kata nyingi zaidi, tumewasisitiza wananchi kuwa kilimo hiki cha mbegu bora lazima kiendane na kilimo cha mikataba, wale wanaohitaji kununua pamba lazima waingie mikataba na wakulima ili wapate faida walizokuwa hawazipati; baadhi yao wamekuwa wakihangaika hawana uwezo wa kununua mbegu, viuadudu na kuhudumia mashamba, lakini wakiingia mikataba hao watakaonunua pamba watatoa huduma zote hizo kwa wakulima” alisema.

Ameongeza kuwa pamoja na kilimo cha mkataba na matumizi ya mbegu bora ili kuboresha uzalishaji wa pamba Wataalam wa Kilimo wanapaswa kuwapa wakulima huduma zote muhimu za ugani ili wazingatie taratibu

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ameitaka Bodi ya Pamba nchini kuboresha utaratibu wa kilimo cha mkataba ili kiweze kuwanufaisha wakulima badala ya kuwakatisha tamaa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri amesema ni vema Bodi ya Pamba ikaweka  utaratibu utakaowawezesha wakulima kupata mbolea na zana bora za kilimo kwa mkopo ambao watarejesha baada ya mavuno.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga amesema wakulima wa pamba kwa miaka ya nyuma wamekuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo  ukosefu wa mbegu bora na kutopanda kwa kuzingatia mistari, hivyo katika msimu wa mwaka 2017 jumla ya tani 8000 za mbegu bora zitazalishwa kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima na jitihada zinaendelea kufanywa kupitia kilimo cha mkataba kuhamasisisha wakulima kulima kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Aidha, Mtunga amesema ili kuongeza uzalishaji wa pamba wakulima wahamasishwe kulima kilimo cha mkataba na ili kilimo cha mkataba kiwe na tija kwao Bodi hiyo inaendelea kutimiza wajibu wake kusimamia masharti yaliyowekwa katika utekelezaji wa mikataba hiyo kati ya wachambuzi  na wakulima wa pamba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi amesisitiza kuwepo kwa mikakati ya kilimo cha umwagiliaji katika zao la pamba ikiwepo uchimbaji wa mabwawa makubwa yatakayowasaidia wakulima wakati wote badala ya kutegemea mvua tu.

Naye  Bw.Charles Thobias Mkulima wa kata ya Mwabusalu ambaye ametumia mbegu bora ya pamba ya (UKM08) amesema mbegu hiyo imekuwa mkombozi kwa wakulima kwa kuwa kulingana na mazao yalivyo sasa shambani, mavuno yataongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na msimu uliopita.

Utekelezaji wa Mpango wa uzalishaji wa Mbegu bora katika kata ya Mwabusalu Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu umehusisha jumla ya wakulima 1,709 katika vijiji vinne ambao kwa pamoja wameweza kulima jumla ya ekari 6,506 na unafadhiliwa na Programu ya Kuendeleza Kilimo cha Pamba chini ya usimamizi wa Bodi ya Pamba.

Rais wa Zanzibar afanya ziara Kisiwani Pemba

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiangalia jengo la ZSTC Mkoani Pemba lililoanguka ukuta kutokana na kuangukiwa na mti baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha uharibifu mkubwa alipofanya ziara maalum leo (kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipofika kijiji cha Gando kumfariji na kumpa pole Mzee Juma Mjaka Khamis (kulia) akiwa na Familia yake aliyepata maafa ya nyumba yake kuangukiwa na mti na kupelekea kukosa sehemu ya kuishi baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni kisiwani humo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Mhe,Hemed Suleiman alitembelea Kijiji cha Makombeni Wilaya hiyo kuangalia  nyumba mbali mbali za Wananchi zilizopatwa na athari  zilizotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani humo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) alipofika katika daraja la Chamanangwe leo kisiwani Pemba lililokatika kutokana na maji ya Mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha usumbufu kwa wanaotumia daraja hilo kutoka upande mmoja kuelekea sehemu nyengine   wakati alipofanya ziara maalum ya siku moja  ya kikazi (Picha na Ikulu).

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ALHAJI MUSSA MBARUKU ATEMBELEA KUONA ATHARI ZA MAFURIKO ENEO LA NEEMA DARAJANI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akiteta jambo na mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga eneo la Neema mara baada ya kukutana njiani wakati mbunge huyo alipokwenda kukagua kujionea athari zilizotokana na mvua kubwa iliyonyesha kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias Haule
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akisisitiza jambo wakati alipotembelea eneo la Neema kujionea athari za uharibifu wa barabara ya Tanga hadi Pangani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kusababisha barabara hiyo kutokupitika
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku wa kwanza kulia akiangalia athari za miundombinu ya barabara ya Tanga hadi Pangani katika eneo la Neema ambako alikwenda kuangalia namna ilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitazama
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akisalimiana na wananchi wa Tangasisi
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akipata maelekezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Bacc Technicla co.Ltd ya Mkoani Dodoma , Husein Bakeme kuhusu namna wanayofanya kuondoa adha hiyo
 Creda likiendelea kufanya kazi ya kurekebisha barabara ya Tanga -Pangani eneo la Neema ambalo lilikuwa halipitiki kutokana na kuharibika vibaya na kusababisha magari kushindwa kupita
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea eneo la Neema
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Masiwani kushoto wakati walipotembelea eneo la Neema kujionea athari za barabara kutokana na mvua zilizonyesha
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akiwa na diwani wa Kata ya Masiwani Said Alei wakati akitembelea eneo la Neema ambalo limeathirika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Tanga
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisalimiana na wananchi wa Jimbo lake
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akiteta jambo na wapiga kura wake mara baada ya kutembelea eneo la Neema ambalo limeathirika kwa miundombinu ya barabara kuharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Tanga .Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA KUTATUA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA MADAWATI

$
0
0

Na Silvia Hyera.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)  Mhe. George  Simbachawene  amewataka  Wakuu wa Mikoa  nchini   kufanya  tathmini  ya madawati  katika Mikoa yao  ili kupata taarifa  kamili  ya  madawati  yaliyopungua, kuhakikisha wanatawanya madawati yaliyokwisha tengenezwa pamoja na kutengeneza  madawati yaliopungua. 

Mhe. Waziri ametoa agizo hilo  leo alipozungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake  Mjini Dodoma katika mkutano na vyombo vya habari  ambapo aliwataka Wakuu wa Mikoa kusimamia  zoezi hili kikamilifu  na kuhakikisha  madawati yaliyotengenezwa yameingizwa kwenye vyumba vya madarasa  na sio kutoa taarifa ya kuwapo kwa madawati hayo kwa mafundi. 

 “ Wakuu wa Mikoa wanatakiwa kuja na taarifa sahihi ya idadi ya madawati iliyopo ukilinganisha na mahitaji  vinginevyo tutadanganyana kwamba madawati yapo mengi lakini kumbe baadhi ya watoto wanakaa chini” alisisitiza Mhe. Simbachawene

Alisema  kuwa kuna baadhi ya Mikoa wana madawati mengi  lakini hayajafika kwenye shule zenye upungufu hivyo ni jukumu la wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa madawati hayo yanafika mashuleni kwa wakati.
Mhe. Waziri alisema  kuanzia Disemba 2015 Serikali ilianza kutekeleza sera ya Elimu Msingi  bila malipo na kutokana na utekelezaji huo,mwitikio wa wananchi kupeleka watoto shuleni umekuwa mkubwa na  kuleta changamoto ya upungufu wa miundombinu muhimu kama vile vyumba vya wadarasa na matundu ya vyoo.

 Aidha,  Mhe. Simbachawene  ametoa   rai  kwa wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kutochoka kuendelea  kushirikiana na Serikali  katika kuboresha miundombinu hiyo muhimu kwenye shule kama walivyotoa ushirikiano wa dhati kukabiliana na upungufu wa madarasa.

Mnamo tarehe 16 Machi, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Mgaufuli aliagiza kuwa kusiwepo na mtoto anayekaa chini kwa kukosa dawati. Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu nchini wametekeleza agizo hilo kwa kiwango kikubwa. 

 Kabla ya agizo hilo mahitaji ya madawati kwa shule za Msingi yalikuwa  3,252,313 na katika shule za Sekondari 1,495,610.  Hadi sasa madawati yaliyopo ni 3,319,355 kwa shule ya Msingi  na kufanya kuwa na ziada ya madawati 66,042 na kwa upande wa Sekondari madawati yaliyopo ni 1,540,625 na kufanya  kuwa na ziada ya madawati 45,015.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Mjini Dodoma katika mkutano na vyombo vya habari na kutoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kutatua changamoto ya upungufu wa madawati kikamilifu kwa kuhakikisha madawati yaliyotengenezwa yameingizwa kwenye vyumba vya madarasa na kutengeneza madawati yaliyopungua.

RAIS DKT. MAGUFULI AIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU CDA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilikiza viongozi mbalimbali waliokuwa wakichangia mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
m.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi kuhusu uamuzi wake wa kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakifatilia kwa makini Hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutia saini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDADodoma ,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria akisoma Rasimu ya Amri ya Rais (Presidential Order) kabla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuisaini ili kuifuta, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi wakifatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza mara baada ya kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika kikao hicho.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kikao hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma Adam Kimbisa mara baada ya kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Eng. Paskasi Muragili mara baada ya kuifuta mamlaka hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 PICHA NA IKULU




VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY 16,2017

MPOGOLO AANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Manzese, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo leo amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mapandikizi ya upinzani na masalia ya wasaliti hawatapenya kwenye uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama kwa kuwa njama zao zimeshabainika. Kimesema kina taarifa kwamba waliotimuliwa CCM nao wanapanga safu za viongozi kwenye uchaguzi, lakini Chama kimejipanga vizuri katika kuchuja wagombea hivyo wenye nia hiyo hawatafanikiwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika ukumbi wa CCM kata ya Manzese wilayani Ubungo,Dar es Salaam.

Alisema kuna mapandikizi kutoka upinzani wanajipanga kugombea uongozi CCM jambo ambalo linafahamika hivyo hakuna atakayepenya na hatutaruhusu 'virusi' kwa namna yoyote ile. Mpogolo pia aliwaonya viongozi wa CCM wanaondekeza ugomvi ndani ya Chama na kuwataka wakatafute vyama vingine ambavyo ni maarufu kwa kugombana hadi kutwangana ngumi.

Alisema katika mageuzi yanayofanyika sasa Chama hakitaruhusu viongozi wa aina hiyo kuendelea kuvuruga a mani, kuwachafua na kuwakandamiza wanachama wenzao. Mpogolo alisema viongozi wenye hulka ya ugomvi, kukandamiza wanachama ndio chanzo cha kupunguza kura za

CCM katika uchaguzi, hivyo Chama hakipo tayari kuwavumilia. ''Viongozi hawa wanajulikana, kama hawawezi kubadilika, waende wakajiunge na vyama vingine ambavyo ni maarufu kwa kupigana. CCM tunahitaji kujenga umoja na upendo baina yetu maana ndio silaha ya ushindi, "alisema.

Mpogolo alisema viongozi hao wameumiza wana CCM hadi wengine wakaenda upinzani jambo ambalo kwenye CCM mpya na Tanzania, hawana fursa ya kuendelea kutesa wenzao. katika hatua nyingine Mpogolo aliwataka wana CCM ambao wanamuwaza aliyekuwa Waziri Mkuu, na mgombea urais wa

Ukawa Edward Lowassa, wasipoteze muda wao kwa kuwa huu ni wakati Rais Dk. John Magufuli. "Naona kuna watu bado wanawaza Ukawa, wengine bado wanafikiria mtu fulani. Ndugu zangu hii ni CCM mpya, hakuna Lowassa wala Ukawa. Nimepita mikoa 26,Watanzania wanasema hawataki upinzani, "alisema.

Mpogolo alipiga marufuku uendeshaji wa vikao vya kushughulika na badala yake wafanye vikao vya kujenga Chama, na katika kipindi hiki cha uchaguzi wa CCM, wajielekeze kuchagua viongozi bora wasiotokana na rushwa. Alisema CCM inatakiwa kuwa mfano katika kudhibiti rushwa na kujenga nidhamu kwa viongozi na wanachama, ili iendelee kuwa kimbilio la wanyonge na Watanzania kwa ujumla.

Mpogolo alisema Chama kina kazi ya kukomboa majimbo ya Dar es Salaam yaliyokwenda upinzani, hivyo uchaguzi ndani ya hama unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kupata safu za viongozi wa CCM watakaofanya kazi ya kumaliza upinzani.

Kabla ya kuzungumza na viongozi hao Mpogolo, alikutana na viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kukutana na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kinondoni na Ubungo ambako alipatiwa taarifa ya Chama ikiwemo maendeleo ya uchaguzi katika ngazi za mashina.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akisalimiana na Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu UDSM, wakati alipowasili Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini leo jioni akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo jana amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wakifurahia maneno yaliyokuwa yakiongewa na Mpoglo.

Mpogolo akipunga mikono kuwaaga wanachama

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama

Mpogolo akizungumza na wanachama.

Wanachama wa Msasani

Mpogolo akiagana na wanachama baada ya kumaliza kuhutubia.

JAFO ATOA WIKI MBILI KWA HALMASHAURI YA CHAMWINO KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MANZASE

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISeMI akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali, Madaktari Bingwa, Viongozi wa Dini na Siasa katika Hospitali ya Mvumi.

……………………………………………………………………………………….

Na Shanni Amanzi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)Selemani Jafo amemtaka Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino Athuman Masasi kuhakikisha kuwa Mradi wa maji wa kijiji cha Manzase unamalizika ifikapo mwishoni mwa mwezi mei, mwaka huu.

Jafo ameyasema hayo alipokuwa anafanya ziara yake katika hospitali ya Mvumi ambapo amezindua huduma ya Hospitali Kimbizi inayohudumiwa na Madaktari Bingwa ambao watatoa huduma ya kitabibu ndani ya siku tano kuanzia leo, tarehe 15 hadi Mei 19, 2017.

Madaktari hao bingwa watatibu magonjwa ya ndani kwa watu wote, watoto, mifupa, masikio, pua na koo, meno, upasuaji na magonjwa ya uzazi kwa upande wa akinamama.

Alisema katika sehemu mbalimbali alizopita kumekuwa na changamoto ya kukosa huduma bora katika vituo vya Afya kutokana na urasimu walionao Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufanya Wananchi wengi wasio na uwezo wa kupata huduma hizo katika kipindi cha nyuma na kwa kipindi hiki Serikali imeshatoa ufumbuzi ambao Viongozi mnapaswa kuzitumia vyema pesa za Miradi ya Afya kama Busket Fund katika kuboresha huduma za Afya kwa Wananchi wote.

Aidha Jafo amewataka Wananchi kushiriki kikamilifu katika kupata huduma hizo kutoka kwa Madaktari bingwa waliotoka katika hospitali mbalimbali nchini kwani huduma hizo zinapatikana kwa bei nafuu na kutoka kwa Madaktari bingwa wenye uzoefu mkubwa na wa muda mrefu .

Amepongeza ushirikiano uliopo wa Mganga Mkuu wa Dodoma Dk.James Kiologwe Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, wadau mbalimbali pamoja na Kanisa la Anglikana kwa kuweza kuendesha zoezi hilo la huduma.

Akihitimisha hotuba yake iliyojaa maelekezo ya Serikali, Jafo amesema baada ya zoezi hili kukamilika ingependeza madaktari bingwa wote walioshiriki zoezi hili katika Wilaya zote za Dodoma waje kujipongeza mjini Dodoma na kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuwa zoezi hili ni zoezi la kwanza kufanyika nchini na likiwa limefanyika mkoani Dodoma.

EFM REDIO YAMTUNZA MAMA

$
0
0
Katika kuazimisha siku ya mama duniani Efm redio kupitia kipindi chake cha uhondo wametoa zawadi kwa  wakina mama wa wasikilizaji wao katika tafrija fupi iliopewa jina la “Begi la mama”

Tafrija hiyo ilifanyika katika ofisi za efm redio siku ya jana kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 Alasiri.  Begi la mama lilitolewa kwa wakina mama 15 ambao stori zao ziliandikwa na watoto wao na kuonekana kugusa mioyo ya wasikilizaji wengi kwa yale magumu waliopitia.
  Mtayarishaji wa kipindi cha uhondo Asha manga akipeleka begi la mama likiwa limejaa zawadi kem kem
 Timu nzima ya kipindi cha Uhondo ikiongozwa na Dina Marios wakimtunza mama nguo kutoka katika begi.
 Muda wa chakula ukafika.
 Mtangazaji wa kipindi cha uhondo akimuhoji mshindi ambae alikuja na mama yake kwaajili ya kuzawadiwa begi hilo.
 Mama akiwa kashikilia zawadi alizotunzwa na Efm redio.
 Timu nzima ya kipindi cha uhondo ikiongozwa na Dina Marios mstari wa pili (wakwanza kushoto) akifatiwa na Sofia Amani, Leah Chambo, Rdj Con wengine ni Bi, Hindu, Swebe Santana, Asha manga, na wengineo.

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images