Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1231 | 1232 | (Page 1233) | 1234 | 1235 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akitazama maeneo yaliyoathirika
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akipita kwenye baadhio ya maeneo yaliyoathirika na udongo kushuka na kusababisha adha kwa wasafiri.

  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akisistiza jambo kwa wananchi
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akisalimiana na wananchi

  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiwa kwenye picha na wapiga kura wake mara baada ya kukutana nao akiwa njiani kuelekea kwenye kukagua athari za mafuriko
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akitazama eneo ambalo limetoka jiwe kubwa ambalo lilishuka kwenye barabara ya Mombo- Soni na kusababisha kufungwa
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akiteta jambo na wataalamu wanaosimamia zoezi la kuondosha kifusi na mawe

  Creda likiendelea na kazi yake kama kawaida
  Baadhi ya wananchi wakipita kwenye barabara hiyo mara baada ya greda kuondoa kifusi kwenye baadhi ya maeneo yaliyokuwa wameangukiwa na vifusi
  Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto,Ramadhani Mahanyu akizungumzia suala hilo

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kadhia ambayo wamekumbana nayo watumiaji wa barabara ya Mombo-Soni kutokana na mawe na vifusi kudondoka
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na athari za barabara ya Mombo hadi Soni kuharibika .


  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akikagua athari za mafuriko kwenye barabara ya Soni hadi Mombo ambapo imefungwa kutokana na vifusi,mawe kudondoka barabarani na hivyo kusababisha adha hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akiangalia athari za barabara ya Mombo hadi Soni ambayo imefungwa kutokana na kushuka kwa mawe makubwa na vifusi
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amewaomba Vijana wa Temeke kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Vijana inayotolewa na Halmashauri hiyo.

  Kumbilamoto ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizindua Tamasha la Miaka tisa ya mbio za pole (Jogging) kwa vijana wa Dovya.

  "Nawashukuru sana vijana wa Dovya Jogging ya Temeke leo kwa kunialika katika tamasha hili kubwa la kutimiza miaka 9 ya jogging yenu pia kwa upekee nimshukuru Mbunge wa Temeke mh Mtolea kwa kunikaribisha katika jimbo lake nishiriki michezo kwani Muchezo ni ajira hivyo nawaomba mtumie fursa hii kuwaambia mchangamkie fursa za mikopo ya halmashauri ya Temeke inayotolewa kwa Vijana"amesema Kumbilamoto.

  Amesema kuwa mikopo hiyo ambayo inatokana na 10% ya mapato ya Halmashauri itawasaidia kujikwamua kiuchumi kama watabuni miradi na kujikusanya katika vikundi .

  Amesisitiza hakuna mtu wakuwafata vijana na kuwajaza mapesa mfukoni bila ya wao kujishughulisha katika ujasiliamali na kujiajiri kupitia fursa zinazo patikana .
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akiongoza Mazoezi ya pamoja katika Tamasha la Michezo la Dovya Joging Wilayani Temeke
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto  akizungumza na Vijana Yombo Dovya wakati wa Tamasha la Michezo la Jonging ya Dovya

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa na Mbunge wa Temeke Abdalah Mtolea wakati wa sherehe za klabu ya Mbio za pole ya Dovya Jogging

  0 0

  MKAZI wa Bunju jijini Dar es Salaam, James Peter amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo ya tano ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10 baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

  Droo hiyo ya tano ya wiki imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Emmanuel Ndaki.

  Akizungumza katika droo hiyo ya tano, Kajala Masanja alisema mshindi wa Milioni 10 wa wiki hii alibahatika kutangazwa mshindi baada ya kupigiwa simu mara tatu, huku mara mbili akishindwa kupokea simu kwa haraka.
  Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiagana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki baada ya kumaliza kuchezesha droo ya tano ya Sh Milioni 10 ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter kutangazwa mshindi wa droo hiyo ambapo amejishindia jumla ya Sh Milioni 10.
  Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter amejinyakulia jumla ya Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki.

  Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ya bwana James Peter


  Alisema hata hivyo baadaye alipokea simu hali inayoonyesha kwamba alikuwa na bahati kubwa kwa kunyakua fedha hizo zinazotolewa kwa mshindi mmoja kila mwisho wa wiki, huku washindi wengine zaidi ya 20,000 wa zawadi za papo kwa hapo wakijishindia zawadi kem kem.

  “Tumefanikiwa kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 ambaye anatokea jijini Dar es Salaam, akiongeza idadi ya washindi wanne kutokea jijini hapa, huku mmoja pekee akitokea jijini Mwanza,” alisema Kajala.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven aliwataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kucheza biko ili waibuke washindi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo katika kipengele cha lipa bili wataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya kumbukumbu 2456.

  “Kucheza biko ni rahisi kwa saabubu baada ya kuweka kiasi kuanzia Sh 1000 ambayo inatoa ushindi wa papo kwa hapo pia humpa fursa mtu kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku zawadi za papo kwa hapo zinatolewa na Biko ikianzia sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku hadi sasa washindi zaidi ya 20,000 wakiwa wamenyakua zawadi mbalimbali za fedha kutoka kwetu Biko,” Alisema.

  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki alisema taratibu za uchezaji wa bahati nasibu ya Biko ni mzuri kwasababu unafuata sharia zote kutoka kwenye Bodi yao, huku akiwaondoa hofu Watanzania juu ya bahati nasibu ya Biko.

  “Kila wiki ya droo ya Biko lazima tuwepo katika kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, hivyo nampongeza mshindi wa wiki hii na kuwatakia kheri wale wengine ambao wanafikiria kuingia katika tasnia ya michezo ya kubahatisha kwa sababu ni hatua nzuri kwa wachezaji wote,” Alisema Ndaki.

  Baada ya kutangazwa mshindi, Biko inatarajia kukabidhi zawadi hiyo ya fedha nono kwa mshindi wao ambaye ni Peter mapema wiki ijayo kama walivyowapatia washindi wengine waliowahi kunyakua fedha hizo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania hususan kwa mshindi wa Sh Milioni 10.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake leo Jijini Dar es Salaam.
  : Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Majaribio ya Dawa na Ufuatiliaji kutoka Mamlaka hiyo Bi. Kissa Mwamwitwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandishi wahabari( hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFDA, Emmanuel Alphonce na Meneja Majaribio ya Dawa na Ufuatiliaji kutoka Mamlaka hiyo Bi. Kissa Mwamwitwa.Picha zote na: Frank Mvungi – MAELEZO  Frank Mvungi-Maelezo

  Serikali imewahakikishia wananchi kuwa dawa zilizopo katika soko zina ubora kwa asilimia 98 na itahakiksha zinaendelea kukidhi vigezo vya ubora kama zilivyokuwa wakati zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni,miongozo na taratibu za udhibiti.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza mikakati ya Mamlaka hiyo katika kudhibiti ubora na usalama wa chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya za wananchi.

  “Katika maabara ya TFDA inayokidhi ithibati ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kati ya sampuli za dawa 199 za Binadamu zilizochunguzwa,sampuli 184 sawa na asilimia 92.5 zilikidhi vigezo vya ubora na sampuli za dawa 10 aina ya Ergometrine ya sindano ambayo ni sampuli 5 sawa na asilimia 2.5 hazikufikia ubora kwa kuwa na kiasi cha kiambata hai chini ya kiwango kinachokubalika.”Alisisitiza Sillo

  Akifafanua Sillo amesema kabla ya dawa kusajiliwa na TFDA na hatimaye kuruhusiwa kuingia katika Soko,zinafanyiwa tathmini ya Ubora,Usalama na ufanisi sanjari na ukaguzi wa mifumo ya utengenezaji bora Kiwandani na hizo ni hatua za awali za mifumo ya udhibiti wa dawa duniani.

  Pia Sillo aliongeza kuwa dawa zinapokuwa katika soko zinafuatiliwa na TFDA kuona kama zinaendelea kukidhi vigezo vya ubora hadi tarehe ya mwisho ya matumizi (expiry date) ambapo utaratibu huu hujulikana kama Post- Marketing Surveillance au Market Control kwa mujibu wa mwongozo wa shirika la Afya Duniani (WHO) na ulianza kuwekwa na TFDA tangu mwaka 2007.

  Katika utaratibu huo kila mwaka sampuli za dawa za aina tofauti zinachukuliwa na wakaguzi kutoka katika soko Zahanati,Vituo vya Afya, Hospitali,maduka ya dawa na maghala ya kuhifadhia dawa ya umma na binafsi na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara.

  Vigezo vinavyotumika kuchagua dawa zinazofanyiwa ufuatiliaji ni pamoja na dawa zenye matumizi makubwa,dawa za kutibu magonjwa ya makundi maalum kama watoto na akina mama wajawazito,dawa zenye historia ya kushindwa kustahili mazingira mbalimbali ya usafirishaji na utunzaji (unstable products)

  Kwa kipindi cha mwaka 2012/2015 Sillo alibainisha kuwa dawa zilizofanyiwa ufuatiliaji ili kuona ubora wake ni pamoja na dawa za kutibu malaria,dawa aina ya vijiua sumu (Antibiotics) Dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi,dawa za kupunguza maumivu,dawa za kutibu kisukari,dawa za kutibu magonjwa ya moyo,dawa za kuzuia kutoka damu nyingi wakati wa kujifungua aina ya misoprostol.

  Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi machi 2017, TFDA ilifuatilia katika soko,ubora wa dawa za binadamu aina ya Albendazole vidonge,mchnaganyiko wa dawa ya vidonge aina ya Diclofenac na paracetamol,dawa ya macho yenye mchanganyiko wa Dexamethazone na Neomycin,dawa za mifugo aina ya Oxytetracycline 10% na 20 ambazo uchunguzi wake uko katika hatua za mwisho na matokeo yatatolewa mara yatakapokuwa tayari.

  Aidha Sillo amesema kuwa mfumo wa kufuatilia usalama wa dawa katika soko unafanya kazi vizuri hapa nchini tangu mwaka 1989 na umeendelea kuboreshwa ambapo oktoba 2016 tulianzisha mfumo wa utoaji taarifa za madhara ya dawa kielekroniki kwa kutumia simu ya kiganjani.

  Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA) kwa mujibu wa Sheria ya Chakula,Dawa na Vipodozi,sura ya 219 ina jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa chakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda Afya za wananchi

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Ali Twahir leo wakati alipotembelea Bonde la Kibonde Mzungu kutoka na Mafuriko yalitokea hivi karibuni kutoka na mvua kubwa za Masika zinazoendelea kunyesha,[Picha na Ikulu.]14/05/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) alipokuwa akiangalia maji ya Mvua yaliyofurika katika bonde la Mwanakwerekwe nyumba mbili leo kutokana na ujenzi holela wa Nyumba za Wananchi zilizojengwa na kupelekea kutopitisha maji katika njia inayoelekea Ziwa Maboga, kutokana na mvua kubwa za Masika zinazoendelea kunyesha.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akiangalia maji yanayopita katika barabara ya Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( kushotio) alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bumbwisudi leo wakati alipofika kuwariji na kuwapa pole kutokana na Nyumba zo kuingiliwa na maji ya mvua wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Pichani ni maji ya Mvua yakiwa yamefurika na kupelekea kufunga njia ambapo wananchi na magari hupita kwa taabu kubwa katika barabara ya Bonde la Kibonde Mzungu,wakati leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) alitembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake katika ziara maalum,[Picha na Ikulu.]14/05/2017.
  Pichani ni Nyumba zinazojengwa eneo la Nyumba mbili Mwanakwerekwe ambapo hali hii hupelekea kuzipa kwa mtaro wa maji ya Mvua yanayoelekea ziwamaboga na kusababisha kuziba kwa barabara ya Mwanakwerekwe-Fuoni hatua mabyo kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) leo alitembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake katika ziara maalum.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( wa pili kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu ya Idara ya Mipango Miji,Kazi na Ujenzi katika Baraza la Manispaa ya Zanzibar Nd,Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea Mtaro wa kaji machafu katika shehia ya Chumbuni alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (kulia) alipotembelea barabara ya Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akiangalia ramani inayoonesha utaratibu wa Ujenzi wa Mitaro kutoka kwa Mkuu ya Idara ya Mipango Miji,Kazi na Ujenzi katika Baraza la Manispaa ya Zanzibar Nd,Mzee Khamis Juma (kulia) wakati alipotembelea Bonde la Maji mwanakwerekwe leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Mohamed Aboud Mohammed,[Picha na Ikulu.]14/05/2017.

  0 0

  Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusufu Singo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio ya Km 21 ya Dasani Marathon 2017 baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo la Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. Mshindi wa kwanza, Augustine Sule (aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche (wa pili kushoto) na mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka Hettierachchi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza iliyodhamini mashindano hayo kupitia kinywaji cha maji ya Dasani. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  Na Richard Mwaikenda

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameyafagilia mashindano ya mbio ya Dasani Marathon 2017 yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Kauli hiyo imetolewa kupitia kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yenye umbali wa Km 10 na 21.

  Pia aliipongeza Klabu ya Dar Running Club kwa maandalizi mazuri yaliyofanikisha mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza kupitia maji ya Dasani. Kampuni hiyo imeingia mkataba wa kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka mitano.

  "Nawapongeza nyote kwa kuchukua jukumu kubwa la kufanikisha maandalizi ya mbio hizi ambayo siyo tu ni nzito bali muhimu katika mchakato mzima wa kujenga utamaduni wa kuzijali afya zetu na ustawi wa familia zetu, uelewano uliothabiti katika kutekeleza majukumu yetu ya kifamilia na kitaifa". Alisema Mwakyembe.

  Awali akizungumza Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka Hettierachchi alisema wanataka mashindano hayo yawe makubwa ambapo hivi sasa wana mipango ya kuyapeleka pia katika mikoa mingine nchini.

  Mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya watu 1000 kutoka maeneo mbalimbali nchini, yalianzia na kuishia Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay na kupita barabara mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Ali Hassan Mwinyi.Aliyeibuka kidedea katika mbio za wanaume za umbali wa Km 21 ni Augustine Sule, wa pili akiwa Stephano Huche na Said Makula aliyeshika nafasi ya tatu.

  Kwa upande wa Wanawake aliyeibuka mshindi ni Jacquline Sakilu, wa pili akiwa Noela Remmy na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Antery John.Kwa mbio za umbali wa Km 10, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Sylvester Seleman, wa pili akiwa Daniel Sinda na Paul Pascal alishika nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza kwa wanawake alikuwa May Naari, wa pili akiwa Sara Hitis na Asia Seleman aliyetwaa nafasi ya tatu.

  Kwa upande wa walemavu aliyeshinda ni Shukuru Khalfan, wa pili alikuwa Mathias John na Jonis Stephano alishika nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21 kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja alikabidhiwa sh. mil 1, wa pili sh. 750,000 na wa tatu sh. 600,000.
  Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio zao katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
  Washiriki wakivishwa medali baada ya kumaliza kukimbia katika mashindano hayo
  Elizabeth wa NMB Bank akivishwa medali baada ya kumaliza mbio hizo
  ni mbio kwa kwenda mbele
  Mshiriki akiangalia muda alioutumia kukimbia. Kushoto ni Mwanariadha nguli wa zamani Juma Ikangaa
  Juma Ikangaa akiwavisha medali washiriki wa mbio hizo
  Mtoto akiwa miongoni mwa wakimbiaji
  Wakimalizia kukimbia
  Timu ya NMB Bank iliyoshiriki katika mashindano hayo
  Wakifurahia kumaliza mbio
  Wakiendelea na mazoezi baada ya mashindano
  Juma Ikangaa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za wanawake umbali wa Km 10, Mary Naari
  Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 10 wanaume, Sylvester Simon akikabidhiwa zawadi na Juma Ikangaa
  Dorothy Kipeja wa Dar Running Club waandaji wa mashindano hayo, akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Km 21
  Mshindi wa kwanza wa mbio za umbali wa Km 21, Augustine Sule akipongezwa na Juma Ikangaa alipokabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo (wa pili kulia)
  Mshindi wa kwanza kwa upande wa walemavu Shukuru Khalfan (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka.
  Nahodha wa timu ya riadha ya Radio EFM, Maulidi Kitenge akiwapongeza waandaji wa mashindano hayo baada ya timu hiyo kushiriki ipasavyo.
  Mtoto aliyeshiriki na kumaliza vizuri mbio hizo, akizawadiwa soda

  0 0

  Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, Sista Theodora Faustine akimkabidhi zawadi na cheti, Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita, ili ampatie mhitimu. Mahafali hayo yalifanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire)
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita ya Shule ya St. Joseph Cathedral, akizungumza na wahitimu (hawapo pichani). Mahafali hayo yalifanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire)
    
  Viranja wa darasa la PCM, Martin na Nsobya Musona wakipokea zawadi ya keki kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita ya Shule ya St. Joseph Cathedral, yaliyofanyika Jumamosi, Mei 13,2017) shuleni hapo. 
  Baadhi ya wazazi, walezi na ndugu walioshiriki mahafali ya sita ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya St. Joseph Cathedral yaliyofanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo.

  (Picha na Irene Bwire)
  Mwenyekiti wa Bodi ya shule, Bibi Margreth Ikongo akitoa shukkrani mgeni rasmi, Prof. Rwekaza Mukandala pamoja na wazazi na walezi walioshiriki mahafali ya sita ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya St. Joseph Cathedral yaliyofanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire)
  ………………………………………………………………………..


  *Asema utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha

  MAKAMU MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala amewataka vijana wanaohitimu kidato cha sita nchini wawe makini na wasikubali kusombwa na mawimbi ya dunia.

  Ametoa wito huo jana (Jumamosi, Mei 14, 2017) wakati akizungumza na wahitimu 237 wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya St. Joseph Cathedral kwenye mahafali ya sita ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam.

  Prof. Mukandala alisema: “Kwa hatua mliyofikia kila mmoja anapaswa atafakari kwa kina wito wake kimaisha. Kuweni makini, msisukumwe na mawimbi ya dunia na kujikuta mmepoteza ndoto zenu,” alisisitiza.

  “Kuhitimu kidato cha sita si jambo dogo. Ni hatua ya kuwaongiza kujiandaa na utu uzima ikiwemo kujiunga na elimu ya vyuo vya juu na kuingia kwenye ndoa. Ni muda wa kutathmini yale uliyopitia na kutafakari maisha yako ya baadaye. Ni fursa ya kutoa shukrani kwa Mungu, kwa wazazi na walimu ambao walifanya kazi kwa umakini na kujitoa ili mfikie hatua nzuri mliyopo sasa,” alisema.

  Alisema kuanzia sasa kila mmoja wao anapaswa kujiamini, kujituma zaidi na kujiona kuwa ana wajibu wa kujiletea maendeleo binafsi. “Mnapaswa kuepuka mwenendo wa kujiona mnyonge, au mtu asiyeweza kutimiza ndoto zake. Jenga tabia ya kuwa makini na maisha yako, jali mazingira yako na maendeleo yako,” alisisitiza.

  Aliwataka wahakikishe wanakuchukua hatua mahsusi na kupata taarifa sahihi kuhusu taaluma wanazozitaka. Aliwataka wawe waadilifu na wenye heshima kwa watu wote lakini pia akawaasa juu ya maisha ya kutaka kupata fedha kwa haraka na kujilimbikizia mali.

  “Epukeni rushwa na ufisadi. Mnatakiwa kujua kuwa utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha ingawa nayo ni muhimu katika maisha. Msitegemee kuishi kwa kuzingatia mambo makubwa yanayopimika kwa fedha,” alisema.

  Akitoa mfano, Prof. Mukandala alisema: “Msikimbilie kuwa na magari mengi bila kujua nani atayatumia, au kujenga nyumba kubwa bila kujua nani atahitaji nafasi hiyo kubwa. Unanunua simu mbili au tatu bila kufikia athari zake kwa afya na mahusiano yako. Kabla hujachukua hatua ni lazima ujiulize, je unakihitaji kitu hicho? Kuweni makini na matumizi ya fedha badala kujilimbikiza vitu vya anasa,” alisema.

  Aliwataka wazazi waendelee kuwalea vema vijana hao kwa sababu bado wanahitaji usimamizi wa wazazi kwa kila hatua wanayosonga mbele. “Tuendelee kuwaunga mkono watoto wetu kwa sababu jukumu letu kama wazazi bado liko palepale,” alisema.

  Mapema, akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na hadhira iliyokuwepo, Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, Sista Theodora Faustine alisema St. wanafunzi waliohitimu jana ni 237 ambao kati yao wavulana ni 140 na wasichana ni 97 waliokuwa wakichukua michepuo ya ECA, EGM, CBG, HGE, HGL, PCM, PCB na PGM.

  Alisema anaamini kwamba wahitimu wote watakuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu mwaka huu kwa sababu shule hiyo imekuwa ni ya kwanza yenye wingi wa ufaulu kuliko shule yoyote mkoani Dar es Salaam. “Tumekuwa tukipata wanafunzi bora kitaifa mara kwa mara na mwaka jana tulipata wanafunzi bora kutoka michepuo ya PCB na ECA,” alisema.

  Sista Theodora alisema wamekuwa wakifaulisha wanafunzi zaidi ya 250 kwa mwaka na kwa maana hiyo, wameweza kuandaa vijana 250 kuingia kwenye vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi. Akifafanua kuhusu malengo ya shule, Mkuu huyo wa shule alisema lengo lao ni kutoa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania na kuwandaa kuwa wawajibikaji kwa Mungu na kwa Taifa lao.

  Kwa upande wake, mwakilishi wa wazazi wenye watoto waliohitimu kwenye mahafali hayo, bw. Eric Shigongo alisema kila mhitimu anayo ndoto yake ambayo anapaswa kufanya kila awezalo kuhakikisha ndoto yake inatimia.

  “Unao uwezo wa kuchagua (power of choice) kilicho chema kwa ajili ya maisha yako ya baadaye. Nasisitiza kwa sababu najua kila mmoja wenu ana ndoto yake ya kufika mahali fulani. Hakikisha unatimiza ndoto hiyo, haijalishi utapitia mazingira gani,” alisema.

  Alisema kwake yeye anawaona vijana waliohitimu kwamba ni washindi (champions) na aliwaeleza hivyo wiki tatu kabla ya kuanza mitihani yao. Hata hivyo, aliwaasa kwamba wawe tayari kukosa mambo mengine kama kweli wanataka kufanikiwa maishani mwao.

  “kama unataka kufanikiwa maishani, huna budi kujinyima mambo mengi ili uweze kupata kile unachokitaka. Najua mmemaliza kidato cha sita lakini safari yenu ya maisha ndiyo kwanza imeanza. Ninaamini wako watu hapa watakaotusaidia kutatua changamoto za nchi hii, wako madaktari hapa, wako wahandisi, wako wafanyabiashara na yuko Rais ajaye wa Tanzania, tena Rais mwanamke kutoka katika kundi hili,” alisema.

  Katika mahafali hayo, mwanafunzi Kauthar Said aliibuka mwanafunzi bora na kupewa zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) na wanafunzi wa mchepuo wa PCM, walipewa zawadi ya keki na Mkuu wa Shule kwa kuwa ni darasa ambalo halijawahi kuwa na kesi yoyote ya utovu wa nidhamu katika kipindi cha miaka miwili waliyoakaa shuleni hapo.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewatembelea wananchi wa Kijiji Tambani ambao hawana mawasiliano ya kuvuka kwenda kutokana na daraja kuchukuliwa na maji.

  Akizungumza na wananchi cha Tambani, Ulega amesema kuwa mvua hizo zimeleta athari hivyo unahitajika ufumbuzi wa haraka.

  Amesema usafiri wa mitumbwi si salama katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa kijiji cha tambani na maeneo mengine. Kutokana na wananchi hao kukosa mawasiliano Mbunge huyo ametoa sh.milioni moja pamoja na mifuko ya saruji 100 ili kuweza kutengeneza daraja hilo.

  Wananchi wa kijiji hicho kwa kila kaya wamekubalina kutoa sh.10,000 ambazo zitafanya kazi katika ujenzi wa daraja hilo pamoja na nguvu zao zitatumika. Diwani wa Tambani, Ally Mtamilwa amsema kuwa ujio wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga ameeta matumaini kwa wananchi na kuahidi nae kutoa mifuko 20 ya saruji.
  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa mawasiliano leo.

  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa mawasiliano leo.
  Wananchi wakiwa katika kivuko ambacho si salama kwa safari baada daraja la kijiji hicho kusombwa na maji leo kufuatia mvua iliokuwa ikinyesha maeneo mbalimbali nchini.
  Wananchi wakisubiri kivuko ambacho si salama na kuwagharimu kulipa sh.500 kwa kila safari wanayoifanya kwenda katika vijiji vingine kupata mahitaji .(picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii )

  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akizungumza na wananchiwa wa kijiji cha Tambani ambao wamekosa mawasiliano kutokana na daraja kuchukuliwa na maji leo.
  Diwani wa Tambani , Ally Mtamilwa akizungumza na wananchi wake wakati wa ziara ya mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akikabidhi msaada wa sh.milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa daraja lilichukuwa na maji katika kijiji cha Tambani.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akifurahia jambo na mmoja wa marubani wa kampuni ya Samaritan's Purse kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya wanafunzi watatu hawajaelekea Marekani kwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea wilayani Karatu wiki iliyopita.

  Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu akizungumza jambo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.

  Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo wamjulia hali Doreen Elibarick

  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akimsalimia Doreen Elibarick kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani kwa matibabu.

  Utaratibu wa kuwaingiza kwenye gari kisha kwenye ndege ukiendelea na maafisa wa uwanja wa ndege wa KIA.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akifurahia Kadi zilizoandaliwa na wanafunzi wa shule ya ISM kwa ajili ya wanafunzi wenzao.
  Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulghafar Idrissa akifanya kazi ya kukandika udongo katika nyumba ya mwananchi Bi. Asha Abdalla wa Shehia ya Fuoni Migombani aliyebomokewa nyumba yake kutokana na maafa ya mvua zilizonyesha juzi Unguja.
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akitoa shukrani zake kwa wananchi mbali mbali walioshiriki katika ujenzi huo na kuhakikisha Bi.Asha Abdalla anapata makaazi ya kuishi. Picha na Afisi Kuu CCM Zanzibar.

  ………………………………………………………

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  WANANCHI visiwani vya Zanzibar wameshauriwa kuendeleza kwa vitendo Utamaduni wa uzalendo wa kusaidiana wakati wa maafa mbali mbali yanayotokea nchini bila kujadili tofauti za kisiasa na kidini.

  Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” mara baada ya ujenzi wa nyumba ya Balozi wa Nyumba kumi Bi. Asha Abdalla Baruti iliyobomoka kutokana na maafa ya mvua zinazonyesha nchini, huko Fuoni Migombani.

  Dkt. Mabodi alisema maafa yanapotokea hayachagui sehemu ya kuathiri bali yanawakumba wananchi wote hivyo ni muhimu wanajamii kushirikiana kwa mambo ya kijamii na kimaendeleo na kuacha siasa za utengano na chuki.

  Ujenzi huo umefanyika kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu huyo alipowataka uongozi wa CCM na UVCCM Wilaya ya Dimani Unguja, kumjengea makaazi ya muda mwananchi huyo ambaye hakuwa na sehemu ya kuishi kutokana na nyumba yake kuharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

  Alisema hatua ya Chama hicho kutoa msaada na kushiriki katika masuala ya shughuli za kijamii kwa wananchi itakuwa ni utamaduni endelevu kwa Unguja na Pemba.

  Alieleza kwamba lengo la CCM kutoa msaada wa kujenga makaazi ya dharura kwa wananchi wakati wa kipindi hichi cha maafa ni kuendeleza kwa vitendo siasa za waasisi wa vyama vya ASP na TANU ambao walishiriki katika masuala mbali mbali ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kuwa karibu na wananchi waliowapa ridhaa ya uongozi.

  Pia alisema wakati wa Kampeni za Uchaguzi CCM ilikuwa ikienda kwa wananchi katika maeneo mbali mbali kuomba kura za kuiweka madarakani hivyo hata kwa kipindi cha maafa na changamoto zinazoikabili jamii ni lazima kirudi kwa wananchi kuwaunga mkono na kuwafariji kwa vitendo.

  Naibu Katibu Mkuu huyo alisema CCM ya sasa Viongozi wa ngazi mbali mbali ndani ya Chama na Serikali kurudi kwa wananchi kujua changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi kwa wakati ni jambo la lazima na sio la hiari.

  “ Nasaha zangu kwa wananchi ni kwamba pindi yakitokea maafa hasa magfuriko tusaidiane kwanza kupitia umoja wetu katika mitaa mbali mbali tunayoishi kwa kuwahifadhi katika maeneo salama wenzetu wanaopata maafa huku tukisubiri serikali zetu zichukue hatua za kutoa misaada.”, alisema Dkt. Mabodi.  Pamoja na hayo aliwataka vijana nchini kuwa mstari wa mbele kwa kujitokeza muda wowote kusaidia masuala ya ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na maafa ili nchi iweze kujivunia uwepo wa kundi hilo ambalo ndio nguvu kazi ya taifa.

  Pia aliwataka viongozi wa kisiasa nchini kuondokana na mazoea ya kulalamika na kulaumu serikali hasa katika kipindi hichi cha maafa na badala yake wawe sehemu ya kuwahamasisha wafuasi wao wajitolee kuwasaidia watu waliofikwa na maafa huku serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutatua tatizo hilo.

  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni, Mh. Yussuf Hassan Iddi amesema jimbo hilo litaendelea kusaidia awamu kwa awamu wananchi mbali mbali waliopata maafa ili waweze kurudi katika hali yao ya kawaida.

  Alisema uongozi wa jimbo hilo baadae utahakikisha unajenga nyumba ya kudumu kwa mwananchi huyo ili aweze kupata uhakika wa makaazi yake.

  Kwa upande wake Mbunge Mteule wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM , Dkt.Abdulla Hasnuu Makame alisifu hatua zilizochukuliwa na CCM kwa kuendeleza utaratibu wa kuwafariji wananchi wakati wa matatizo mbali mbali ya kitaifa .

  Aliahidi kuiwakilisha vyema CCM katika Bunge hilo ili fursa mbali mbali zinazopatikana ziweze kusaidia katika kuimarisha miradi ya kijamii hasa kuongeza miundombinu ya barabara, Elimu, Afya na ajira kwa vijana.

  Mapema Bi. Asha Abdalla ameishukru CCM na wananchi wote walioshiriki katika zoezi la kumjengea nyumba yake na kuongeza kwamba hatua hiyo imemfariji na kumpa nguvu za kuendelea kufanya kazi za kujipatia kipato kwa ufanisi zaidi.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, ametembelea na kukagua kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza na kujionea utendaji kazi wa kivuko hicho pamoja na changamoto zake.

  Akiongea na watumishi wa kivuko hicho baada ya kujionea changamoto ya uendeshaji wa kivuko hicho, Dkt. Mgwatu alisema “tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia matengezo ya kinga kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo.”

  Aidha Dkt. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko cha MV. Nyerere kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, pamoja na kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.

  Katika hatua nyingine, Dkt. Mgwatu alitembelea kivuko cha MV. Mara katika Mkoa wa Mara pamoja na kivuko cha MV. Ruvuvu katika mkoa wa Kagera na kujionea utendaji kazi wa vivuko hivyo pamoja na changamoto zake.
  Kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
  Fundi wa kivuko cha MV. Nyerere akionyesha utendaji wa injini mojawapo ya kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Nyuma yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa pili kushoto) akiangalia utendaji kazi wa moja ya injini ya kivuko cha MV. Nyerere katika chumba cha mifumo ya kuendeshea kivuko hicho. Kivuko cha MV. Nyerere kinatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
  Kivuko cha MV. Mara kinachotoa huduma kati ya Iramba na Majita mkoani Mara.
  Kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika eneo la Rusumo Mkoani Kagera. Picha na Theresia Mwami.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Meneja Masoko Msaidizi wa Coca-Cola,Pamela Lugenge,akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA Copa Coca-Cola wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla pamoja na maofisa wa kampuni ya Coca-Cola wakipasha mwili kwa mazoezi kabla ya uzinduzi wa mashindano hayo.  Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua baadhi ya timu za wanafunzi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mwishoni wa wiki
  Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari wakifanya mazoezi kwa kushirikiana na wachezaji wa Mbeya City wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Wanafunzi wakionyesha umahiri wa kusakata kabumbu wakati wa uzinduzi wa mashindano katika uwanja wa Sokoine mwishoni mwa wiki.


   Michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari-UMISSETA Copa Coca- Cola kwa Mkoa wa Mbeya imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sokoine na uzinduzi huo ulionogeshwa na wachezaji wa timu ya soka ya Mbeya City ambao walishiriki kufanya mazoezi na timu za wanafunzi na kutoa ushuhuda wa michezo hiyo ilivyoibua vipaji vyao.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla,ambaye alikuwa mgeni rasmi anataka kuwaona vijana wengi wakishiriki mazoezi na michezo mbalimbali kwa kuwa michezo kama ilivyo hii ya UMISSETA Inaibua na kukuza vipaji pia sekta ya michezo bado inazo fursa nyingi za kujiajiri. 

  Alisema kampuni ya Coca- Cola imeonyesha njia kwa kudhamini michezo hii na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini michezo ya vijana kwa kuwa ndio tanuru la kuwaandaa wachezaji na kuibua vipaji. ‘’Leo hii tunaona hawa vijana wa Mbeya City wapo hapa kutoa ushuhuda wao, wanapokea mpunga (mshahara) wa maana lakini chimbuko lao wametokea kwenye michezo hii ya Copa Coca- Cola. 

  Naamini kupitia michezo hii Mbeya tutapata wachezaji wengi zaidi’.Alisema. Ofisa Msaidizi Masoko wa Coca- Cola Pamela Lugenge, alisema lengo la kampuni ya Coca Cola kuuungana na Serikali kupitia UMISSETA ni kuona wanaibua vipaji vingi vya vijana walioko shule za sekondari ambako wanaamini ndiko chimbuko la kupata timu ya taifa na klabu mbalimbali nchini.

   “Tumeamua kuanzia kwenye mizizi ngazi ya chini kabisa, tunaamini huku ndiko vipaji viliko lala, tunataka kuibuwa akina Mbwana Samata wengi zaidi kuanzia huku, ndio maana tumejikita zaidi, na tunagawa vifaa vya michezo kwa shule zote, tumeanza na shule hizi 39 za jiji la Mbeya na baada ya uzinduzi huu sasa tunakwenda kwa wilaya zote kutoa vifaa hivi,” alisema Lugenge. 

  Mchezaji wa Mbeya City, Medson Mwakatundu,akiongea kwa niaba ya wachezaji wenzake walioibuliwa na UMISSETA alisema michezo hii ni muhimu sana iwapo Tanzania tunataka kuwa na wanamichezo wazuri kwa kuwa inaibua na kukuza vipaji na alitoa wito kwa vijana kushiriki michezo kwa kuwa inazo fursa nyingi za ajira na kutangaza taifa.

  0 0
  0 0

  Teddy na Talkia Tumbi ambao ni mtu na dada yake wamefanya uzinduzi wa studio ya nywele na kuuza shanga na vito (jewelry) iliyopo kwenye mji wa Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hiyo ambayo ilizinduliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 ilihudhuriwa na Watanzania mbalimbali waliofika kuwaunga mkono.
  Teddy Tumbi akimwandalia mteja (hayupo pichani)shanga alizonunua kwenye studio yao iliyofunguliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hii ya kutengeneza nywele na kuuza shanga na vito (Jewelry) na anuani kamili ni 2575 Old Glory Road, Clemmons, NC 27012 simu 336 343 8170.
  Image may contain: 1 person
  Talkia Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.
  Mmoja ya wateja akitengeneza nywele zake.
  Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Glory Alex akipata matunda ya ufunguzi wa studio hiyo kwa kutengeneza nywele zake alipokwenda kuwaunga mkono Teddy na Talkia Tumbi mtu na dada yake walipofungua studio ya nywele na kuuza shanga na vito.
  Mmoja ya wateja akitengeneza urembo wa nywele studioni hapo.
  Ulimbwende wa kucha ukiendelea
  wasusi wakipata picha kwenye studio ya nywele na kuuza shanga na vito iliyofunguliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.
   
  Muonekano wa studio
  Mwenyekiti Glory Alex akiwa katika picha ya pamoja na Teddy Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani. 
  Mwenyekiti Glory Alex akiwa katika picha ya pamoja na Talkia Tumbi mmoja ya wamiliki wa studio hiyo siku ya uzinduzi wake uliofanyika siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakila kiapo cha uuguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwakaribisha wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiandamana na kuonyesha ujumbe mbalimbali mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya Ummy Mwakimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Waziri wa Afya Ummy Mwakimu akisaini zawadi ya mafuta ya alizeti aliyopewa na wenyeji wake halmashauri ya Itigi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuajiri watumishi wa idara ya afya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi ambao wameondolewa katika utumishi wa umma kwa kukosa sifa ya kuwa na vyeti halisi baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti nchini.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati wa maadhimsho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa imefanyika katika hospitali ya St. Gasper, Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

  Waziri Ummy amesema serikali inatambua mzigo mkubwa wa majukumu kutokana na uhaba wa wauguzi ambao umesababishwa na baadhi yao kuondolewa katika utumishi kwa kukosa vyeti halisi na hivyo imetenga bajeti ya kuajiri wauguzi wa kutosha nchini huku akiahidi kutoa kipaumbele kwa mkoa wa Singida.

  “Kuna baadhi ya Zahanati na vituo vya afya vimefungwa kwa kutokana na sakata la vyeti feki, lakini pia tunatambua kuwa wauguzi hamtoshi na hivyo kupelekea muuguzi mmoja kutoa huduma kwa wagonjwa wengi, hali hii inapunguza ufanisi wenu na kuwanyima haki ya kupumzika”, ameongeza Waziri Ummy.

  Aidha ameagiza waajiri wa utumishi wa umma na hasa halmashauri zote nchini kupeleka maombi ya watumishi wa kada za afya ili wizara iweze kutangaza nafasi hizo zijazwe na watanzania wenye sifa huku akisisitiza kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

  “Serikali imegawa vitanda 25 vya wagonjwa, magoro 25 na mashuka kwa kila halmashauri nchini huku bajeti ya wizara ya afya ikipanda kutoa trilioni 1.9 mwaka jana hadi trilioni 2.2 kwa mwaka wa fedha 2017/18, bajeti hii itasaidia kupambana na changamoto za sekta ya afya nchini nah ii ni ishara kuwa serikali imedhamiria kuimarisha afya za watanzania” amefafanua Waziri Ummy.

  Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Pulo Magesa amewataka wauguzi kuto muangusha waziri wao wa Afya kwa kuwa amekua mstari wa mbele kuhakikisha wauguzi na watumishi wote wa Sekta ya Afya Nchini wanafanya kazi katika mazingira yanayoridhisha.

  Magesa amesema serikali inaweka mazingira mazuri kwa kutenga bajeti ya kutosha ila ufanisi wake utaonekana endapo watumsihi wa sekta ya afya hasa wauguzi ambao ndio muhimili wa vituo vya huduma za afya mfano hospitali, zahanati na vituo vya afya watazingatia misingi ya uadilifu, upendo na weledi.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema wauguzi wanaweza kupunguziwa mzigo wa kupata wagonjwa wengi hasa kwa magonjwa yanayozuilika endapo kutaanzishwa mfumo wa utoaji wa huduma za uuguzi kwa ngazi za kaya ambapo kila mwanafamilia atapewa elimu ya kuzuia baadhi ya magonjwa.

  Dkt. Nchimbi amesema mfumo huo wa uuguzi kaya uendeshwe mpaka kwenye taasisi za elimu hasa shule za msingi na sekondari ili jamii iweze kuzuia kwa kiwango magonjwa yote yanayozuilika na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa .

  Aidha amemshukuru Waziri Ummy kwa kuunga mkono wazo hilo na kukubali kuanza kulifanyia kazi huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa kuwa mkoa wa Singida utatumika na sehemu ya utafiti wa mfumo huo ili kufahamu ufanisi wake

  Maadhimisho Siku ya Wauguzi Duniani ni kukumbuka ya muasisi wa taaluma ya uuguzi Bi.Florence Nightngale aliyezaliwa Mei 12 mwaka 1820. Wakati wa sherehe hizi huwa mishumaa inawashwa kama ishara ya upendo na utumishi bora moyoni mwa muuguzi. Muasisi huyu ndiye aliyefungua chuo cha kwanza cha uuguzi nchini Uingereza.

  Bi Florence alianza kutoa huduma ya afya mwaka 1844 na mwaka mmoja baadaye kulitokea vita na yeye akawa anahudumia majeruhi kwa kutumia mishumaa nyakati za usiku kwa vile hapakuwepo na nishati yoyote wakati huo. Bi Florence kwa huduma yake hiyo ya kutibu majeruhi wa vita aliweze kupunza vifo kutoa asilimia 42 hadi asilimia mbili (2).

  Wauguzi waliokuwepo kwenye maadhimisho hayo kutoka mikoa mbalimbali nchini walirudia kiapo chao cha uuguzi ambacho sehemu mojawapo inasema “Naapa mbele ya Mungu na mbele ya mhadhara huu, kuendesha maisha yangu na kutekeleza wajibu wangu wa kazi kwa uaminifu. Sitafanya vitendo vyo vyote vile vilivyo viovu na sitochukua au kutoa dawa ye yote ile ninayoifahamu kuwa ina madhara”.

  Awali wauguzi, viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini pamoja na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka na kuwaombea wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa shule ya Lucy city ya Mjini Arusha waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea hivi karibuni.

  0 0

  Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC tayari kutembelea kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
  Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa wa Saratani katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
  Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza na mabalozi wa kundi la Saratani Info lilipotmbelea kitengo hicho.
  Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza na mabalozi wa kundi la Saratani Info lilipotmbelea kitengo hicho,kulia kwake ni Kiongozi wa Mabalozi hao kanda ya Kaskazini,Veri Njau na kushot ni Mratibu katika kitengo hicho  Everlyn Ndosi.
  Kiongozi wa Kundi la Mabalozi wa Saratani la Saratani Info kanda ya Kaskazini,Veri Njau akizungumza na baadhi ya wagonjwa pamoja na mabalozi hao baada ya kuwatembelea katika kituo cha Saratani ,KCMC.
  Baadhi ya wagonjwa wa Saratani wanaopatiwa matibabu katika kitengo cha Saratani ,Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambao kundi la Mabalozi wa ugonjwaa huo liliwatembelea na kutoa msaada wa gharama za Bima ya Afya kwa watoto nane (8).
  Mabalozi wa Ugonjwa wa Saratani wakitembelea katika maeneo mbalimbali ya kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
  Mmoja wa Mabalozi wa Ugonjwa wa Saratani wa kundi la mtandao wa WhatsApp la Saratani Info ,Respicius Baitwa akizungumza kabla ya kukabidhi fedha kwa ajili ya Bima za Afya kwa wagonjwa wa Saratani nane wanaopata matibabu katika kituo hicho.
  Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akitoa neno la shukurani baada ya Mabalozi wa Kundi la WhatsApp la Saratani Info kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya Bima za Afya kwa watoto nane wanaopata matibabu katika kitengo hicho.
  Baadhi ya Mabalozi wa Saratani waliotembelea kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuwaona wagonjwa wa Saratani wanaopata matibabu katika Hospitai hiyo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.  0 0

  Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
  Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi cheti kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
  Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo.
  Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo.

  Mwanamitindo, muigizaji  na Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu nchini kusaidia kuondoa changamoto katika sekta mbalimbali ili kupunguza mzigo kwa serikali. Jokate alisema hayo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walihitimu katika shule hiyo.

  Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali husasani elimu na afya.

  Alisema kuwa kwa hali ilivyosasa, ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba  wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika jamii.

  Alifafanua kuwa shule ya wasichana ya Jangwani ni kongwe  kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyandhifa na wanashindwa kuchangia.

  “Mimi sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.

  Mrembo huyo pia amewaomba viongozi wa serikali na wafanyabiashara  waliosoma katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.

  Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo, shule yao haina madarasa na mabweni ya kutosha, haina  ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali kama sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina hata gari moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na matibabu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

  Mgongolwa amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu mitatu ili kwenda  kwenye shughuli mbalimbali za kimamoso nje ya shule.


  0 0


   Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika  leo jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa habari  wakimsikilliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel  Massaka,Globu ya Jamii.
  SERIKALI yaja na mpango mkakati wa kudumisha matibabu ya uzazi pingamizi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini Tanzania.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati waa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika jijini Dar es salaam.

  “Huwezi kutoa huduma bora na salama ya uzazi pingamizi bila kuwa na wataalamu wa ganzi ili kufanywa upasuaji usio na maumivu hivyo katika mkutano huu tunapanga kuwa na wataalamu wengi wa huduma hiyo ili kutoa huduma bora nchini.

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa licha ya kudumisha matbabu ya uzazi pingamizi pia Serikali imejidhatiti kujenga vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

  Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoka na malengo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa mahututi pamoja na kutoa huduma ya ganzi kwa wanaohitaji kupasuliwa. Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wataalam Wa Ganzi nchini (SATA) umeudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Sweden,Cameroon, Marekani , Tanzania ili kuweza kujua mchango wa kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na huduma ya ganzi.

  0 0

  Kiongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Weusi Basketball Club ya jijini Dar es Salaam, Mntambo Mngeja (kulia) akipata maelekezo ya juu ya kujiandikisha kutoka kwa mratibu ya michuano ya Sprite Bball Kings, Basilisa Biseko wakati wa zoezi la uandikishaji wa timu mbalimbali kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo. 

  Uandikishaji ulifanyika Tegeta Complex jijini Dar es Salaam huku timu zaidi ya 20 zikijitokeza kujiandikisha. Michuani ya Sprite Bball Kings inaendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa udhamini wakampuni ya Coca-Cola. 


  Ikiwa ni siku ya kwanza kwa timu mbali mbali za michuani ya kikapu ya Bball Kings, zaidi ya timu 20 zimejitokeza kujiandikisha mwishoni mwa wiki hii wakati wa zoezi la uandikishaji linaloendelea jijini Dar es Salaam. 

   Michuani ya mchezo wa kikapu ya Bball Kings inayoendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite siku ya jumamosi imeshuhudia wawakilishi wa timu mbalimbali wakijitokeza na kujaza fomu za ushiriki, huku wawakilishi wa timu hizo wakijigamba kujidhatiti kikamilifu kuchukua ubingwa wa mwaka huu. 

  Kati ya timu zilizojitokeza ni pamoja na Cavarious, Lycans, Tegeta Camp, Lord Baden, K-Warriors, DMI, St Joseph na MJ Junior. Nyingine ni Oilers, TMT, Mchenga, Bahari Beach, Street Boys, Street Warriors, Chanika Legends, God With Us, Weusi Basketball Club, Junior Basketball Club na Celestial Basketball Team. 

   Akizungumza wakati wa uandikishaji wa timu shiriki, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa wa EATV, Roy Mbowe alisema mwitikio wa timu mbalimbali umejaa hamasa kubwa na wa kuridhisha, huku kila timu iliyojitokeza ikiwa na wachezaji wasiozidi 10.

   “Mashindano hayo yanahusu vijana wenye umri wa kuanzia miaka 16 na watapaswa kuunda timu ya wachezaji 10 ambao watachuana na timu nyingine zitakazokuwa zimejiandikisha, huku tukitoa fursa katika wachezaji hao 10, timu inaweza kuwa na wachezaji wasiozidi watatu kutoka katika timu kubwa za Ligi Darasa la Kwanza za za kikapu za hapa nchini,’’alisema Mbowe. 

  Michuano ya Sprite Bball Kings itaendeshwa kwa njia ya mtoano katika hatua ya kwanza ili kupata timu 16 zitakazoingia hatua ya pili na kutaja zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa itakuwa ni Sh.milioni 10 wakati mshindi wa pili atapata Sh.milioni tatu huku pia kukiwa na zawadi ya Sh milioni mbili kwa mchezaji bora (MVP). Mashindano hayo yatakayoshirikisha wachezaji kutoka mikoa yote nchini, yanatarajiwa kuanza mwezi huu na kumalizika Julai mwanzoni.

  0 0


older | 1 | .... | 1231 | 1232 | (Page 1233) | 1234 | 1235 | .... | 1897 | newer