Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

NEW ARRIVALs @AK CLASSIC COSMETICS.

$
0
0
 
 WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA MBELE, AK CLASSIC COSMETICS SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA TOFAUTI KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, SASA LEO KUNA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.



SERIKALI YAOMBA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA ULINZI WA RASILIMALI NCHINI.

$
0
0
Na Hassan Silayo- MAELEZO.


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewaomba wananchi kusaidia katika katika ulinzi wa rasilimali nchini. Hayo yamesemwa jana na Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi. Yustina Mallya wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es salaam.

“Wizara inaomba sote tuitafakari na kuitekeleza dhana ya Jeshi la Polisi ya Ulinzi Shirikishi ni muhimu kila mwananchi mzalendo wa nchi hii ashiriki kikamilifu kudumisha amani na ulinzi wa nchi na rasilimali zake zote”Alisema Yustina.


Aidha Yustina alisema ulindaji wa rasilimali hizo hasa wanyama pori utasaidia kujenga na kuimarisha utalii wa nchi kutokana na zaidi ya asilimia 90 utalii unategemea wanyamapori na hivyo kuingizia nchi fedha za kigeni na pia kukuza uchumi.”Kwa hapa nchini zaidi ya asilimia 90 ya utalii unategemea wanyama pori hivyo, watalii wengi huja kuwaona, kuwapiga picha na kuondoka wachache huja kuwawinda kisheria na kuchukua nyara. Wanyamapori ndio wamebeba utalii katika Tanzania na kwa maana hiyo ndio, kwa kiasi kikubwa, wamebeba uchumi wa nchi hii” Alisema Yustina.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Ujangili kutoka wizara hiyo  Bw. John Muya aliwataka wananchi waliokatazwa kuishi maeneo ya njia za wanyama kutekeleza agizo hilo ili kuepuka uharibifu unaofanywa na wanyama hao kipindi cha uhamiaji.“Napenda kutoa wito kwa wananchi kuondoka kwenye yale maeneo ambayo ni mapito ya wanyama pindi wanapohama kuondoka ili kuondoa usumbufu na uharibifu wa mali” Alisema Muya.


Yustina aliwataka wananchi kuacha kuwatazama baadhi ya wanyama kama Fisi na Tembo kama kero kwa wananchi, badala yake tuwatazame wanyamapori kama benki kubwa na kama mkombozi wa nchi yetu kiuchumi.

afrikwetu Band ndani ya triniti

WAFANYAKAZI AIRTEL DAR LEO WAKO MITAANI KUTOA SOMO JINSI YA KUJIUNGA NA AIRTEL YATOSHA!

$
0
0
 Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba akijipanga na mmoja wa afisa mauzo wa Airtel wa Dar es salaam Bi, Violet Kajubili muda mfupi kabla ya wafanyakazi wote  kuelekea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar esa salaam kuonana na wateja ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo  kuwaelimisha wateja wao jinsi ya kutumia huduma ya Airtel yatosha na promosheni ya shinda nyumba 3.

Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba  LEO amesema Airtel imefanya zoezi  la kuingia mtaani jijini dar es salaam na
wafanyakazi wao wote wa ofisi kuu jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuhakikisha kuwa kila mteja anafaham jinsi ya kufaidika na huduma zao
zote ikiwemo ya Airtel Yatosha, ambapo mteja hujiunga kwa kupiga
*149*99# Kisha kuchagua kifurushi nafuu cha  SIKU WIKI AU MWEZI ili

kuongea kwa gharama nafuu kwenda mtandao wowote nchini Tanzania
 Meneja Uhusiano wa Airtel jackson mmbando akibadilishana mawazo na Maafisa mauzo wa Airtel  wa mkoa wa Dar es Salaam leo wakati wafanyakazi hao wakijipanga kuingia mtaaani kukutana na wateja wao na kuwaelekeza jinsi ya kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha SHINDA  NYUMBA 3
 Baadhi ya maofisa na viongozi wa Timu Airtel Yatosha  wakiendelea kupeana maelekezo jinsi ya kwend a kuingia sokoni kwenye kila mtaa jijini Dar es salaam ili kuwapa somo la AIRTEL YATOSHA shinda nyumba tatu.


 Usafiri maridadi umeandaliwa ili kuhakikisha kazi na mizunguko ya Airtel yatosha tour inakamilika bila zengwe
 Meneja wa Masoko na Chapa wa Airtel Bi, Upendo Nkini nae anawakilisha Timu Yatosha kwenda mtaani sasa.AIRTEL YATOSHA NA BADOOOO!


Hii inawahusu wadau wa soka zaidi kutoka morogoro live.

$
0
0
Ofisi za chama cha soka mkoani Morogoro(MRFA) zafungwa kwa kushindwa kulipia kodi ya pango la ofis ktk uwanja wa jamhuri unaomilikiwa na CcM kwa miezi mitano,,Nini hatma ya soka/vipaji vyetu kama mkoa/taifa.
Chanzo: www.facebook.com/afande.theking?hc_location=stream

//jiachie1.rssing.com/chan-7007640/article2446-live.html

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AREJEA NCHINI AKITOKEA NCHINI NIGERIA KWENYE ZIARA YA KIKAZI.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteremka kwenye ndege GF1 alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea Nchini Nigeria alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itafikia malengo ya Umoja wa Afrika iliyojiwekea katika kukabiliana na Magonjwa hayo, mkutano huo ulimalizika jana July 17-2013 mjini Abuja Nchini Nigeria (Picha na OMR)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea Nchini Nigeria alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itafikia malengo ya Umoja wa Afrika iliyojiwekea katika kukabiliana na Magonjwa hayo, mkutano huo ulimalizika jana July 17-2013 mjini Abuja Nchini Nigeria (Picha na OMR)


CHAJA YA READYSET KUTOA NJIA MBADALA YA CHANZO CHA NISHATI.

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga,akiwaonesha wakazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam jinsi yakutumia chaji hiyo inayotumia  mionzi ya jua,zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo ,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
 Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akimsikiliza Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)akimuelimisha namna ya kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua,Chaji hizo zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
 Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akionyeshwa jinsi ya kuchaji simu na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)kwa kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua, zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini.Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.


TANZANIA YAPOKEA MKOPO WA BILIONI 87 ZA UJENZI WA VITUO VYA KUHIFADHIA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea  wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam. 
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea  wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (kushoto)akimpa mkono wa shukrani Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya  kusaini  mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dickson Maimu (wa tatu kushoto ) na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import Korea  Yong Hwan Kim(wa pili kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo baada ya halfa ya kusaini Mkataba wa Mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa, leo jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (wa pili kushoto),Balozi wa Korea nchini Chung Il(wa kwanza kulia),Mwenyekiti na Raisi wa Benki ya Export and Import Korea Yong Hwan Kim(wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Saada Salum(kushoto), wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa Kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka Benki ya Export and Import Korea.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea baada ya hafla ya kusaini iliyofanyika Wizara ya Fedha leo jijini Dar Es Salaam. 
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa  akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania  kwa Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea baada ya hafla ya kusaini iliyofanyika Wizara ya Fedha leo jijini Dar Es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha(Sera), Saada Salum(wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira A.Silima wakipiga makofi ya shukrani Baada ya Waziri wa Fedha kusaini mkataba wa mkopo wa kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka  Export and Import Benki ya Korea,jijini Dar Es Salaam.

 Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha,Elizabeth Nyambibo(wa kwanza Kushoto),Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani Mbaraka Abdul(katikati) na Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum wakifuatilia hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa  uliotolewa na Benki ya Export and Import Korea ,leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).
 

Wananchi Sasa Kupata Taarifa za Huduma za RITA kwa ‘Sms’ , Tovuti na Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua jambo katika wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
======  ==========

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.

Katika huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba 15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.

Pia wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala hao, www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo itapunguza msongamano wa wananchi kujua taarifa mbali mbali za vizazi na vifo na nyinginezo zinaztotolwa na wakala hao.

Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo ni kwa nchi nzima na kuipongeza RITA kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Media Mobile kwa kutengeneza huduma hiyo yenye ubora wa hali ya juu.

“Huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu ili kupata taarifa hizo, sasa taarifa utazipata kiganjani, tena kwa kutumia simu yako ya mkononi, ni jambo la faraja na la kujivunia,” alisema Waziri Kairuki.

Alisema kuwa Wizara yao ina mpango wa kuanzisha utaratibu ambao utaongeza kasi ya usajili wa wananchi kwa wakala hao ambapo mwananchi hataweza kupata kazi mpaka awe na cheti cha kuzaliwa. Pia hata kwa watu wanaotaka kupata leseni za biashara, kujiunga na shule na shughuli nyingine mbali mbali watalazima kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Afisa Mtendaji Kuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa wameamua kujiunga digitali ili kwenda na wakati na mpango wao mkubwa ni kupanua wigo wa huduma zao kwa kaya zote.

“Tunataka kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza taarifa muhimu kwa wananchi, hii itaturahisishia hata sisi kujua ufanisi wa shughuli zetu na kukabiliana na changamoto mbali mbali,” alisema Saliboko.

Saliboko alisema kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yao na wananchi.

TAARIFA KWA UMMA:USALAMA WA DAWA AINA YA DICLOFENAC

$
0
0
 


  1. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

  1. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

a.      Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.  

b.      Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.
   
c.        Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo  ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

  1. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO). Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya nchini.
  2. Mamlaka inasha+uri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadhari za madhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.

  1. Vilevile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) – Makao Makuu
S. L. P 77150
Dar-es-Salaam
Tanzania
Simu: +255 22 2450751
+255 22 2450512
Barua pepe: info@tfda.or.tz



HUDUMA ZA MAMLAKA YA BANDARI KUBORESHWA.

$
0
0
 Kaimu Meneja Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania Janeth Ruzangi  akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za mamlaka hiyo, kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Awadh Massawe na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.

Kaimu Meneja Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania Janeth Ruzangi  akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za mamlaka hiyo, kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Awadh Massawe na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.

SERIKALI KUONDOA VIBALI VYA UPATIKANAJI WA WAKANDARASI

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Wizara ya Maji Nurdin Ndimbe akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  wa Maji Mijini  kutoka Wizara hiyo Mhandisi Karangi Bwire.

 > Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Boniface Kasiga akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji toka Wizara ya Maji akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu taratibu za wananchi kufuata wakati wa uchimbaji wa visima PICHA  ZOTE NA HASSAN SILAYO. 

========  ======  =========
SERIKALI KUONDOA VIBALI VYA UPATIKANAJI WA WAKANDARASI

Hassan Silayo-Maelezo.


Seikali kupitia wizara ya maji imepania kuondoa vibali vinavyotolewa na Wizara hiyo katika kupata Wakandarasi, Wataalam, Washauri na kupitisha taarifa za usanifu ili kutekeleza kwa haraka miradi mbalimbali ya maji nchini.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Nurdin Ndimbe kutoka Wizara ya Maji wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. “katika kuhakikisha serikali kupitia wizara yetu inatekeleza miradi mbalimbali ya maji vijijini tumeamua Kuondoa vibali vinavyotolewa na Wizara katika kupata Wakandarasi, Wataalam Washauri na kupitisha taarifa za usanifu  kulingana na waraka uliotoka tarehe  Juni 7 mwaka huu” alisema Nurdin.

Aidha Nurdin alisema ili kuboresha mfumo wa ufuatiliaji wizara imeunda chombo cha ufuatiliaji kinachoitwa Ministerial Delivery Bureau kikiwa na dhumuni la kuboresha na kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na Wizara hiyo inatekelezeka ndani ya mda uliopangwa. Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji kutoka Wizara hiyo Naumia Rupime amewataka wananchi kuacha kuchimba visima kiholela badala yake wafuate taratibu  na sheria zilizowekwa ili kuondoa kero mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

“wananchi wamekuwa wakichimba visima kiholela na kuuza maji bila kufuata taratibu ikiwa ni kwenda kwa msajili wa mabonde katika eneo husika au bila ya kupeleka sampuli ya maji yaliyochimbwa katika Maabara ili kuthibitisha usalama wa maji hayo. alisema Naumia.



Jumla ya miradi ya maji kwenye vijiji 682 ikiwa ni wastani wa vijiji 5 kwa kila Halmashauri vipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji. Ifikapo mwezi Septemba 2013 ujenzi wa miundombinu ya maji utakuwa umekamilika  ambapo jumla ya watu milion 1.7 wanatarajiwa kupata huduma ya maji.

SMZ YAOMBWA KUMALIZA KUJENGA SKULI ZILIZOANZWA KUJENGWA NA KUZIFANYIA UKARABATI.

$
0
0
Na Miza Othman-Melezo Zanzibar     

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imeombwa kuzimaliza kuzijenga skuli ambazo tayari zimeazwa kujengwa na kuzifanyia ukarabati zile zilizo kuwa  chakavu katika Mkowa wa Kaskazini  Unguja. 

Hayo yameelezwa leo huko Baraza la Wakilishi Bweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa  Nchi Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheiri  wakati alipokuwa akichangia  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  juu ya suala zima la elimu katika mkoa huo.

Amesema  kwamba katika mkoa huo kunaumuhimu mkubwa kuzimaliza skuli zilizo azwa kujengwa na kuzifanyia ukarabati zile zilizo kua chakavu ili kuleta msta kabala mwema kwa wanafunzi na walimu mkoani humo.  
Amesema hali hiyo ita wafanya wanafunzihao kufuatilia kwa umakini zaidi masomo yao kwa vile mazingira yana ruhusu kujipatia Elimu Bora.

“Serikali ishughulikie majengo yalio kuwa machakavu kwakuyakarabati na kuyamaliza yale yalioaza kujengwa,”alisema Waziri huyo.  Aidha akizungumzia suala la ajira alieleza kuwa kwa upande wa Serikali hakutokuwa na uwezekano wa kuwajiri walimu wote  waliosomeshwa na Serikali jambo ambalo haliwezekani kutokana na uhaba wa nafasi zilizopo. “ Serikali haiwezi  kumuajiri kila mtu bila ya kuzingatia sifa alizonazo muajiriwa ili kuwepusha ubinafsi katika upatikanaji wa ajira’’.aliongeza kusema Waziri.

Hata hivyo Waziri huyo  amesema kuwa katika ajira walizozitangaza kuwaajiri walimu wapya nahatimaekatika hatua za awali  kulikuwa mtu  jina lake lilitoka kuajiriwalakini baadae jina hilo likatolewa kwa bahatimbaya au ubinafsi   basi anobwa mtu huyo  apeleke malalamiko yake katika kamisheni ya utumishi ili kusawazishiwa ukweli wa jambo hilo.

Waziri huyo alisisitiza kwa kusema   kwamba ajira za walimu zinazingatia aina ya fani kwa walimu kutokana na ajira hizo zilivyo hivi sasa serikalini.

“Tuna hitaji walimu maalumu ilikuweza kukabili masomo yao watu wa sayansi waajiriwe kutokana na kiwango chao na ati huwajiriwa kutokana na kiwangochao ili kila mmoja awe na uwezo wa kusomesha masomo kulingana na fani yake,”aliendelea kusema  Omar.Aidha alisema jumla ya walimu 521 wameajiriwa mwaka huu kwa kufuata vigezo walivyo vitaka ambao walimu hao tayari wameripoti katika vituo vyao na kwa sasa wanahitaji walimu 50 tu wa masomo ya  Sayansi.

SWAHILI TV YALONGA NA MENEJA WA JUSTIN BIEBER "JUSTIN KUKAA KIFUA WAZI

$
0
0
Katika pita pita zetu mitaa ya Connecticut, Marekani, Mwandishi wetu alikutana na picha hizi za Bieber akiwa Kifua wazi alafu amejitunisha ili kuonyesha jinsi jim inavyolipa.Mwana muziki huyu mdogo lakini maarufu amekuwa na tabia ya kuvua shati siku hizi hata akiwa klabu au mitaani kwani anasema anataka kinadada waone jinsi kifua chake kilivyo.

Katika kutafuta ukweli wa mambo ilikuweza kuhakikisha je ni kweli amesema hivyo kwa watu, Mwandishi wetu wa burudani bwana DMK alimpigia simu meneja wa Justin nakumuuliza lakini alikanusha nakusema bwana mdogo huyo amekuwa akikaa kifua wazi kwasababu summer hii joto ni kali sana na mwanamuziki huyo anashindwa kuvumilia, alipomwomba kuongea na Justin mwenyewe meneja huyo alimkatia simu.Tutaendelea kufatilia zaidi ili tuweze kupata ukweli je ni kwanini Justin Bieber  siku hizi anapenda kukaa kifua wazi? ama Je ni kwasababu anaenda Jimu sana au?....endelea kusoma Swahili TV blog na kupitia website yetu www.swahilitv.info

Mbunge awaomba wapiga kura kumvumilia juu ya ahadi za maji

$
0
0
MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Seleiman Nchambi amewaomba wapiga kura wake kuwa wavumilivu juu ya ahadi ya huduma za maji safi na salama alizozitoa wakati akigombea jimbo hilo katika uchaguzi mkuu 2010.

Nchambi ametoa kauli hiyo hivi karibuni akizungumza na mwandishi wa habari hizi kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya wapigakura wake wa Kata ya Kishapu, ambao wamelalamikia kitendo cha kuendelea kutopata huduma za maji safi na salama eneo lao ilhali mbunge wao aliwaahidi kuwapatia huduma hiyo.

Mbunge huyo alikiri kutoa ahadi ya huduma ya maji jimbo zima la Kishapu na utekelezaji wa ahadi zake unaenda awamu kwa awamu kama alivyopanga. Akifafanua zaidi alisema aliingia madarakani na kukuta sehemu kubwa ya jimbo hilo halina huduma ya maji safi na salama, lakini kwa jitihada zake mpaka sasa tayari amefanikiwa baadhi ya vijiji kuvipatia maji.

"Niliahidi maji jimbo zima la Kishapu yaani jumla ya vijiji 114, wakati naingia madarakani nimekuta hali ni mbaya ya huduma za maji...lakini hadi sasa tunapozungumza zaidi ya vijiji 30 vinapata maji safi na salama huku jitihada zingine zinaendelea," alisema Nchambi akifafanua juu ya kilio cha huduma za maji akizungumza kwa njia ya simu.

"Ahadi yangu mimi ni miaka mitano, ilani ya CCM ni ya miaka mitano, ninaenda kwa awamu yaani vijijini 10 kwa kila mwaka kwa wilaya," aliongeza kusema mbunge huyo.

Awali uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa baadhi ya vijiji vya Kata ya Kishapu, mkoani Shinyanga, vikiwemo vijiji vya Lubaga, Isoso, Mwanuru pamoja na Kishapu ulibaini kuwepo na shida kubwa ya huduma ya maji safi na salama hali inayowalazimu wananchi kutembea umbali mrefu hasa kipindi cha kiangazi kutafuta maji.

Hata hivyo uchunguzi ulibaini mzigo mkubwa wa kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika familia unawaangukia wanawake na wanafunzi ambao hutumia muda mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi ya familia. Chanzo pekee cha maji ambacho hutegemewa na maeneo mengi ya vijiji ni cha Mto Tungu ambao nao hukauka kipindi cha kiangazi na wananchi kuendelea kupata maji kwa shida.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni viongozi wa vijiji vya Lubaga, Isoso, Mwanuru na Kishapu walilalamikia kitendo cha wao kuendelea kuteseka kwa huduma za maji ilhali walipewa ahadi ya kuletewa huduma hiyo na mbunge wao kipindi cha kampeni.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Lubaga, Enock Manyenye Shimba alisema mwaka 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kijiji chao kilipewa ahadi ya kuchimbiwa visima virefu vya maji na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Seleiman Nchambi lakini anashangaa ahadi hiyo haijatekelezwa hadi leo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, George Kessy alikiri hali mbaya ya huduma ya maji Wilaya nzima ya Kishapu kutokana na eneo hilo kutokuwa na chanzo cha maji cha uhakika. Hata hivyo alisema juhudu zinafanywa kuhakikisha uongozi unaondoa kero hiyo ya huduma ya maji kwa wananchi.

"Ni kweli suala la maji ni Tatizo kwa wilaya nzima ya Kishapu, tena ni kubwa sana…,” alisema Kessy.

Na Thehabari.com, Kishapu.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

President Kikwete meets Standard Chartered CEO Liz Lloyd at Dar es Salaam State House

$
0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Standard Chartered Bank Chief executive Officer(CEO) Liz Lloyd at Dar es Salaam State House yesterday afternoon. On the left is Head of Corporate Affairs Ms.Juanita Mramba.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a photograph with the Standard Chartered Bank Chief Executive Officer(CEO) Liz Lloyd(left) at State House Dar es Salaam yesterday afternoon. On the right is the bank’s Head of Corporate Affairs Ms. Juanita Mramba(photos by Freddy Maro)

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA ATETA NA SWAHILI TV JIJINI WASHINGTON DC !

$
0
0
WAZIRI MKUU MSTAAFU,AMEONGELEA MAMBO MENGI IKIWA NI PAMOJA NA MUUNGANO,KATIBA,MABOMU ARUSHA NA MIPANGO YA 2015. TEMBELEA WWW.SWAHILITV.BLOGSPOT.COM

BALOZI MULA MULA APOKELEWA KWA SHANGWE WASHINGTON DC

$
0
0
IMG_3118

Mama Balozi Liberata Mula mula akipokelewa na mama Munanka baada ya kukutana na kujitambulisha kwa rais Obama huko White house alhamisi. Balozi Mula mula alitoa shukrani za dhati kwa mabalozi wenzake waliofika kumpongeza pamoja na Mh.EL mbunge wa Monduli na watanzania wote waliokuwapo kwa kuhudhuria hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine alieleza pia kushangazwa kwake na kufurahishwa na mapokezi yasiyo na makuu yalio ya kifamilia zaidi aliyopewa huko White house na Rais Barack Obama na familia yake alipowasilisha hati zake za utambulisho siku ya alhamisi Julai 18. IMG_3168
Mama Balozi Mula mula akiwa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa bunge la Tanzania na mbunge wa Monduli Edward Lowassa. IMG_3143
Mchungaji Shideko akifungua kwa sala. IMG_3125
Mc wa shughuli hiyo Mindi Kasiga na afisa habari ubalozini akitoa utaratibu. IMG_3164
Mama Munanka akiwa na Raymond Maro. IMG_3153
Mama Munanka akiitambulisha familia yake. IMG_3145 
Balozi wa Rwanda nchini Marekani Prof.Mathilde Mukantabana akisikiliza kwa makini. IMG_3178
Shamis akiwa na balozi wa Burundi nchini Marekani.Kwa taarifa zaidi bofya www.sundayshomari.com

Umoja wa Watanzania Ujerumani kushiriki maonyesho ya Kimataifa mjini Aschaffenburg,

$
0
0
Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya
"Brüderschaft der völker " mjini      Aschaffenburg " Ujerumani.
                   Kuanzia leo Ijumaa 19 hadi 21 Julai 2013

Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayo anza  Leo ijumaa 19 hadi  jumapili 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli
za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza
Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko
huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi
ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia
nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa
Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.
Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com pia unaweza kutembelea link ya maonyesho at http://www.bruederschaft-der-voelker.de/2013/05/29/union-of-tanzanians-in-germany/
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images