Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

ENG. NGONYANI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UYOVU- BWANGA.

$
0
0


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akipokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, kuhusu ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokagua barabara hiyo jana, mkoani Geita
A
Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, akitoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.
A 1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mhadisi Mkazi Eng. Juma Msonge, baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita.
A 2
Sehemu ya barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Synohdro, mkoani Geita. Hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 60.
A 3
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Geita, Eng. Harun Senkuku, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ambae alikuwa mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara yake.
…………….
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa Km 45 inayojengwa na Mkandarasi M/S Sinohydro Corporation.

Akizungumza mkoani Geita jana, mara baada ya kukagua  barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amemtaka mkandarasi huyo kahakikisha wanamaliza sehemu iliyobakia kwa muda uliopangwa.
“Nimeridhishwa na kasi yenu, hakika mmepiga hatua sana kwani awali nilipopita kukagua barabara hii haikuwa hivi”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.

Aidha,  Eng. Ngonyani, amewapongeza wasimamizi wa barabara ya Biharamulo – Bwanga kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU),  kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation  kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyomo kwenye mkataba.

Kwa upande wake, Mhandisi mkazi wa barabara hiyo Eng. Juma Msonge, amemhakikishia Waziri huyo kumaliza barabara hiyo kwa wakati.
Eng. Msonge ameongeza kuwa kwa sasa mradi huo umefika asilimia 60 ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya kuweka matabaka ya lami ambapo ameshaweka km 30 kati ya 45 zilizopo kwenye barabara hiyo.

Naibu waziri  Ngonyani, amemaliza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

PICHA ZA WANAFUNZI 32,WALIMU 2 NA DEREVA 1 WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI HUKO KARATU MKOANI ARUSHA

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY 8,2017

WAZIRI MWIGULU NA WATENDAJI WAKE WAKUU WAJADILI BAJETI YAKE IKIWA NI MAANDALIZI YA MWISHO KABLA YA KUIWASILISHA KWENYE BUNGE LA BAJETI MJINI DODOMA JUMANNE

$
0
0
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba  wa pili kushoto akitoa Maelekezo kwa  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha cha maandalizi ya mwisho cha kupitia Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kuiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni na wa kwanza kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara mjini Dodoma. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyenyanyua mkono akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bajeti  ya Jeshi la Polisi nchini mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya  jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara hiyo mjini Dodoma. 
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akipokea taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake,  kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara mjini Dodoma. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  nchini, Dkt. Juma Malewa wa pili kulia akitoa ufafanuzi mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye wa tatu kulia  akitoa ufafanuzi kuhusu Jeshi lake mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kusomwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 

PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa huzuni na masikitiko  makubwa taarifa ya vifo vya watoto 32, walimu 2 na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha, vilivyosababishwa na ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu - Arusha. 

Tunasikitika sana kwa kuwa ajali hii imetokea wakati wazazi, walezi na walimu wakitekeleza wajibu wao wa msingi wa kumpatia mtoto haki ya kuendelezwa Kielimu.

Kufuatia msiba huu mkubwa, kwa niaba ya Wizara na kwa niaba yangu mwenyewe ninatoa pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa wanaandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali. Tunamuomba .
 
Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira  katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla. 

Tunaziombea roho za watoto wetu wapendwa zipumzishwe mahali pema peponi, Amiin. Ni maombi yetu pia kuwa Majeruhi waliopo hospitalini watapata nafuu ili waweze kuendelea na masomo.

Ummy Mwalimu, Mb
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/05/2017

WACHIMBAJI WADOGO WAIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU YA UCHIMBAJI BORA

$
0
0
Mchimbaji mdogo wa Madini ya Almas ambaye pia ni Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems Gregory Kibusi, akiangalia ubora wa Madini ya Alams.
Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems Gregory Kibusi, (kulia), akionesha madini ya Almas . Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza Kishan Bhatti.
Madini ya Almas ambayo bado hayajasanifiwa.
Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini ya Almas (TANSORT) kutoka Wizara ya Nishati na Madini Archard Kalugendo (kulia) akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kushoto) namna ya kupima ubora wa Madini ya Tanzanite.
Mjiolojia kutoka Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Jumanne Shimba, akiangalia madini kwa kutumia kifaa maalum cha kinachotumiwa na kituo hicho katika mafunzo.
Mnunuzi wa Madini ya Tanzanite (kushoto) akiangalia ubora wa Madini ya Tanzanite katika Banda la Kampuni ya TanzaniteOne. Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya TanzaniteOne.
Watumishi kutoka Kituo Cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakimsikiliza mgeni aliyembelea banda la kituo hicho ili kujua shughuli za mafunzo ya usanifu na unga’rishaji wa madini zinavyofanyika. Mikufu inayoonekana katika picha pamoja na mapambo mengine imetengenezwa kituo hapo. Kituo hicho kiko chini ya Wizara ya Nishati na Madini.


Ujenzi wa kisima cha maji kilichojengwa na Kampuni ya SANA Gems Ltd ikiwa ni sehemu ya kuwezesha jamii inayozunguka mgodi wa kampuni hiyo kunufaika na uwepo wa mgodi husika.

………………………..


Na Asteria Muhozya, Arusha

Wachimbaji wadogo wa Madini walioshiriki Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito, Arusha wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji bora na uhifadhi wa mazingira kwa wachimbaji nchini.

Ombi hilo lilitolewa na Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya SANA Gems, ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini ya Almas, Gregory Kibusi.

Kampuni ya SANA Gems inayofanya shughuli zake za uchimbaji mkoani Shinyanga ndiyo kampuni pekee ya wachimbaji wadogo iliyokuwa ikionesha madini ya Almas katika Maonesho hayo.

Kibusi aliongeza kuwa, ushiriki wa wachimbaji katika maonesho hayo ni fursa kwao ya kukutana na wanunuzi na kujenga mtandao wa kibiashara hivyo kuiomba serikali kuendelea kuwahamisha wachimbaji wadogo nchini kushiriki katika maonesho hayo kwa kuwa, yanawezesha uhakika wa masoko ya madini yao.

“Nikiwa pia kama Katibu Mkuu wa wachimbaji wadogo Shinyanga, natoa wito kwa wachimbaji nchini kutumia vyama vyao washiriki maonesho haya ya Arusha kwa kuleta madini yao. Soko la uhakika lipo,” alisema Kibusi.

Aidha, Kibusi alitumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji nchini kuachana na matumizi ya zebaki na kuwataka kutumia njia bora zinazoelekezwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh, alisema kuwa, kampuni hiyo imeshiriki Maonesho hayo ili kuweza kujenga mtandao wa kibiashara ikiwemo pia kutoa fursa kwa Watanzania kujifunza namna Madini ya Almas yanavyochimbwa na mahali yanapopatikana.

Aidha, ameitaka Serikali ifikishe umeme katika eneo hilo na maeneo mengine mbapo shughuli za uchimbaji mdogo zipofanyika ili kuwezesha kuharakisha maendeleo ikiwemo kuwezesha shughuli za kiuchumi na kupanua wigo wa ajira.

Akizungumzia namna kampuni hiyo inavyosaidia eneo linalozunguka mgodi wake alisema kuwa, kampuni hiyo imetengeneza kisima cha maji kwa ajili ya kijiji cha Hukiro pamoja na kuboresha baadhi ya miundombinu katika zahanati iliyo jirani na mgodi wa kampuni hiyo

Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yalifunguliwa rasmi tarehe 3 Mei na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

$
0
0

Na Beatrice Lyimo na Fatma Salum-MAELEZO



MAKAMUwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaongoza maelfu ya Watanzania kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vicent waliofariki kwa ajali ya gari Mei 6 mwaka huu Mkoani Arusha.


Katika tukio hilo lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa, Wazazi na wote walioguswa na msiba huu.


“Shukrani kwa Rais wa Kenya na Wakenya wote kwa ujumla kwa kujumuika na Watanzania katika kuomboleza msiba huu ulioukumba taifa, ambapo Rais Uhuru Kenyata amemtuma Waziri wa Elimu wa nchi hiyo kuwakilisha Wakenya katika kuomboleza msiba huu” anasema Makamu wa Rais.


Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Elimu, Jeshi la Polisi na wazazi kulinda Sheria za Usalama barabarani ili kulinda maisha na ndoto za watoto.


“Msiba huu umegusa kila Mtanzania, hivyo tuzidi kuwaombea Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hivyo tujipe moyo na nguvu kwamba hili limetokea na kwa Mwenyezi Mungu tujirudishe” ameongeza Makamu wa Rais.


Hata hivyo Makamu wa Rais ametoa wito kwa madereva wa magari mbalimbali kuwa makini na waangalifu katika vyombo vya moto wanavyovitumia.


Aidha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ametoa pole kwa wazazi wote waliondokewa na watoto na ndugu zao, wafiwa na watanzania wote walioguswa na msiba huo.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewapa pole wazazi na wanajumuia wote na kusema kuwa kama kuna kitu kinatuunganisha sote ni kifo kwani kila binadamu ana mwisho wake.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa Mwenyezi Mungu ametoa nafasi ya kutafakari umoja wetu na ushirikiano wetu kama taifa kupitia msiba huo.


Vilevile Waziri wa Elimu kutoka nchini Kenya Dkt. Fred Matiang’I amesema kuwa Kenya itaendelea kuwa pamoja na Watanzania kwenye kipindi hiki kizito cha msiba huo mzito ulioukumba taifa.


Mbali na hayo Rais Dkt. John Magufuli kwenye ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa amepatwa na uchungu na majonzi makubwa alipoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha.


“Tumepoteza mashujaa wetu katika elimu, tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Rais Magufuli.


Wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent walipata ajali ya basi Mei 6, mwaka huu Mkoani Arusha walipokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema.

UZINDUZI WA UMISSETA COPA COCA-COLA 2017 MKOANI MWANZA WAFANA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya Copa Coca-cola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Meneja Mkuu wa Masoko Nyanza Bottling Co. Ltd Mwanza, Deus Kadico akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jiji ni Mwishoni mwa wiki.
Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni ya Coca Cola nchini, Pamela Lugenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikabidhi vifaa vya michezo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bugogwa baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma na wa pili kushoto ni Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo nchini, Pamela Lugenge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikabidhi vifaa vya michezo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bugogwa baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma na wa pili kushoto ni Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo nchini, Pamela Lugenge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikagua timu ya ya mpira wa miguu ya Nyamagana baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo nchini, Pamela Lugenge akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akipiga mpira golini ishara ya uzinduzi wa michuano ya Copa Coca-cola iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Makamu wa Rais Mama Samia aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga miili ya ndugu zao leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye 
uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent.
Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Jeshi la Wananchi(JWTZ) wakiingiza miili ndani ya uwanja kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.


Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa 
 katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent waliofariki kwenye ajali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8-May-2017 ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.

Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.

Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.

Katika kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Fred Matiang’i.

Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.

BENK YA WANAWAKE TAWI LA MKWEPU WAUNGANA NA TAIFA KUOMBOLEZA VIFO VYA WANAFUNZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya Wanawake Tawi la Mkwepu wameungana na Taifa kuombolea vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja  vilivyotokana na ajali iliyotokea Karatu mkoani Arusha tarehe 6 May,  mwaka huu.

Kwa niaba Benki ya Wanawake wametuma salamu za pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa waliokuwa wanandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali.

Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira  katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla. 

SERIKALI KUFUTA USHURU NA TOZO MBALIMBALI KWA WAKULIMA

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini Mhe. Jacob Zuma, ambaye atawasili nchini kwa ziara ya siku 3. Pamoja na mambo mengine, Rais Zuma pia atatembelea Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha tiba ya ugonjwa wa moyo (Jakaya Kikwete Cardiac Institute), na pia kufungua rasmi Ubalozi wao hapa nchini. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Suleiman Salehe, akimsikiliza Waziri Mahiga (Hayupo pichani) katika mkutano na waandishi wa Habari 
Sehemu ya waandishi wa habari wakinukuu maeneo mbalimbali yaliyotajwa na Waziri Mahiga kwenye mkutano na waandishi wa habari. 
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea. 


Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini

1. UTANGULIZI

(i) Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Gedleyihlekisa Zuma anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitaifa ya siku tatu hapa nchini, kuanzia tarehe 10 hadi12 Mei 2017, kwa mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(ii) Ziara hii inafanyika baada ya Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Zuma kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

(iii) Mheshimiwa Rais Zuma anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 10 Mei 2017, jioni na kupokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Magufuli. 

(iv) Ziara hii itatoa fursa kwa Viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara. Ujio wa Mheshimiwa Rais Zuma ni fursa nzuri sana ya kuendelea kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano mazuri naya kihistoria kati ya nchi zetu mbili. 

(v) Mheshimiwa Rais Zuma anafuatana pia na wafanyabiashara takribani 80. Hii ni fursa muhimu sana katika kukuza mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Hivyo, tarehe 11 Mei 2017, kutakuwepo na Kongamano la Wafanyabiashara katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JINCC).

(vi) Ziara ya Mheshimiwa Rais Zuma inaenda sambamba na vikao vya Tume ya Pamoja ya Marais (Bi-National Commission - BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Mkutano wa Marais umepangwa kufanyika tarehe 11 Mei, 2017. Mkutano huo utatanguliwa na Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 10 Mei, 2017 na kikao cha Makatibu Wakuu kitafanyika tarehe 8 na 9 Mei, 2017.


2.0. RATIBA



(i) Wakati wa ziara hiyo, tarehe 11 Mei 2017, Mheshimiwa Rais Zuma atakutana na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Magufuli kwa mazungumzo ya faragha kabla ya kushiriki mazungumzo rasmi yatakayowahusisha wajumbe wa pande mbili.

(ii) Aidha, Viongozi hao watashuhudia uwekwaji saini wa Mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali ya ushirikiano. 

(iii) Siku hiyo hiyo, Mheshimiwa Rais Zuma atashiriki chakula cha mchana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini katika Hoteli ya Hyatt Regency. Pia, Mheshimiwa Rais Zuma na Mheshimiwa Rais Magufuli watashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini litakalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

(iv) Aidha, jioni ya siku hiyo, Mheshimiwa Rais Zumana ujumbe wake watashiriki Dhifa ya Kitaifa ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima yake na Mheshimiwa Rais Magufuli.

(v) Tarehe 12 Mei 2017, Mheshimiwa Rais Zuma anarajiwa kufungua rasmi Jengo jipya la Ubalozi wa Afrika Kusini nchini pamoja na kutembelea Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

(vi) Mheshimiwa Rais Zuma na ujumbe wake wataondoka siku hiyohiyo kurejea Afrika Kusini.


3.0. MAHUSIANO BAINA YA TANZANIA‎ NA AFRIKA KUSINI

(i) Mahusiano ya Tanzania na Afrika Kusini ni mazuri na ni ya muda mrefu tangu wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini zilizoongozwa na Chama kikongwe cha African National Congress (ANC). Nchi hizi mbili zimeendelea kushirikiana kwa karibu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kikanda na hasa ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika. Kwa sasa, Afrika Kusini ni Mwenyekiti wa SADC na Tanzania ni Mweyekiti wa SADC Organ, hatua inayotoa nafasi ya kushirikiana zaidi. 

(ii) Aidha, ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini umekuwa ukiimarika kila mara kwa Viongozi wakuu kutembeleana na viongozi wa ngazi za juu Serikalini kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi zetu mbili. Kama mtakumbuka Julai 2011, Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alifanya Ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini ambayo ndiyo iliyozaa Mkataba wa Ushirikiano wa Tume ya Marais ambayo ndiyo iliyotuwezesha kukutana leo.

(iii) Uhusiano wa Vyama vya Siasa vya CCM na ANC

Vyama vya ANC na CCM vina mahusiano mazuri na Viongozi wa vyama hivyo wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa ajili ya kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati yao.

(iv) Mikataba ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hadi sasa, Tanzania na Afrika Kusini tayari zimetia saini Mikataba ya Ushirikiano (MoU) kumi na tano (15), ambayo inagusa sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, sayansi na teknolojia, uwekezaji, utamaduni na kilimo.

(v) Ushirikiani katika Utatuzi wa Migogoro katika Kanda

Tanzania na Afrika Kusini zimeendelea kufanya kazi pamoja katika juhudi za utatuzi wa migogoro na kuhakikisha kwamba Afrika inakuwa sehemu salama. Nchi hizi mbili zimeshiriki katika kutatua migogoro nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Sudan Kusini. Tanzania na Afrika Kusini zote zimechangia Askari katika Brigedi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Amani na Usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (United Nation Force Intervention Brigade-FIB) kwa lengo la kutuliza uvunjifu wa amani Mashariki mwa Kongo. Vile vile, nchi hizi mbili kwa pamoja zimekua zikishirikiana katika kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Sudan Kusini.

(vi) Uhusiano katika Nyanja za Uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Ø Uhusiano ya uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huo mzuri umezidi kuchochea na kurutubisha ushirikiano wetu wa muda mrefu na wa kihistoria. 

Ø Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zinazochangia idadi kubwa ya wawekezaji wa kigeni nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre-TIC) kimesajili jumla ya miradi 226 kati ya mwaka 1990 hadi 2016. Miradi hiyo ina thamani ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 803.15 na imetoa ajira zipatazo 20,916.

(vii) Uhusiano katika Sekta ya Biashara

Ø Kiwango cha biashara (volume of trade) imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Mwaka 2007 ilikuwa Tsh Milioni 976,331 na mwaka 2016 ni Tsh 2,402,211.20. Hili ni ongezeko kubwa na linaleta matumaini ya ushirikiano zaidi.

Ø Bidhaa ambazo Tanzania inauza nchini Afrika Kusini ni pamoja na maua, kahawa, wanyama hai, chai, nguo, pamba, vito vya thamani, tumbaku na mafuta ya kupikia. Bidhaa zinazoagizwa kutoka Afrika Kusini ni pamoja na maziwa na mazao yote ya maziwa, matunda aina ya apple, mbegu za mahindi, mafuta ya soya, sukari kwa matumizi ya viwanda, juisi za matunda, mafuta ya kulainisha mitambo, bidhaa za vileo, Acrylic polymers, lami, magari, pampu za maji, bidhaa za chuma, vitabu, mashine, na trela.

(vii) Mchango wa Madawati wa Afrika Kusini kwa Serikali ya Tanzania

Ø Katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kwa kupitia Ubalozi wake hapa nchini, Serikali ya Afrika Kusini iliweza kuchangia jumla ya madawati 1100 kwa shule za Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Madawati hayo yalikabidhiwa kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Ø Pamoja na hayo, Serikali ya Afrika Kusini inatarajia kuanzisha programu mahsusi ya kubadilishana walimu na uzoefu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuinua sekta ya elimu. 

4.0. TAARIFA FUPI KUHUSU TUME YA USHIRIKIANO YA MARAIS (BI-NATIONAL COMMISSION) KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI

Sasa naomba niwape taarifa fupi kuhusu Mkutano wa Tume ya Ushirikiano ya Marais

(i) Tanzania na Afrika Kusini zilisaini Mkataba wa kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano ya Marais (Bi-National Commission-BNC) tarehe 19 Julai 2011 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi. Tume ya Ushirikiano ya Marais imechukua nafasi ya Tume ya Uchumi ya Pamoja ya Marais (Presidential Economic Commission-PEC) iliyoanzishwa mwaka 2005. Kama nilivyosema awali, Mkataba huu ulisainiwa wakati wa ziara ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano, Mhshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

(ii) Mkataba wa kuanzisha BNC umeainisha maeneo kumi (10) ya ushirikiano ambayo ni Biashara na Uwekezaji (Trade and Investment), Maendeleo ya Miundombinu (Infrastructure Development), Kilimo (Agriculture), Elimu, Sayansi na Teknolojia (Education, Science and Technology), Ulinzi na Usalama (Defence and Security), Habari, Utamaduni na Michezo (Infrastructire, Culture and Sports), Afya (Health), Nishati na Madini (Energy and Minerals) na Maliasili na Utalii (Natural Resources and Tourism).

(iii) Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Mashirikiano ya Marais (BNC) unatarajiwa kufanyika kuanzia leo, tarehe 8 hadi 11 Mei, 2017. Mkutano wa Marais utatanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu tarehe 8 na 9 Mei, 2017 ukifuatiwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 10 Mei, 2017. Mkutano wa Marais utafanyika tarehe 11 Mei, 2017 ambapo Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Zuma watakuwa Wenyeviti Wenza wa Mkutano huo. 

(iv) Wakati wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Marais, Mikataba ifuatayo inatarajiwa kutiwa saini:-

(a) Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Masuala ya Bio Anuwai na Uhifadhi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini (Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Government of the Republic of South Africa on Cooperation in the Field of Biodiversity Conservation and Management);

(b)Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Maji kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini; na

(c) Hati ya Makubaliano katika Sekta ya Uchukuzi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini;

(v) Pia kuna Mikataba mingine inaendelewa kufanyiwa kazi na mara itakapokamilika, Mawaziri wa sekta husika watasaini. Mikataba hiyo ni pamoja na wa Sekta ya Utalii, Sekta ya habari, Sekta ya kilimo, sekta ya afya, niitaje hiyo tu kwa sasa.

(vi) Tofauti na Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC), Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) inashirikisha Marais wa Nchi mbili ambapo katika JPC inaishia katika ngazi ya Mawaziri. Ushiriki wa Marais katika Tume ya Pamoja ya Ushirikiano unatoa uzito wa pekee katika utekelezaji wa maeneo ya mashirikiano yaliyoafikiwa.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 08 Mei, 2017

Tanzania na Afrika Kusini za dhamiria kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Marais ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya Makatibu Wakuu nao wakifuatilia kwa makini Hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Mlima.
Dkt. Mlima akiendelea kuzungumza 
Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, Bw. Edward XolisaMakaya naye akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo. 
Dkt. Mlima pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Innocent Shiyo (wa kwanza kulia), wakimsikiliza kwa makini Bw. Makaya (hayupo pichani). 
Sehemu nyingine ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano huo. 
Sehemu ya washiriki kutoka Tanzania na Afrika Kusini walioshiriki katika ufunguzi huo wakiendelea kuwasikiliza viongozi (hawapo pichani)walikuwa wakitoa hotuba zao wakati wa ufunguzi huo. 
Wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumaliza ufunguzi. 
Dkt. Mlima akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ufunguzi. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akielezea jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo kukamilika. 





Wataalamu wa Tanzania na Afrika Kusini wapo katika mkutano wa siku nne wa kuandaa mpango bora wa kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi hizo.

Mkutano huo unaojulikana kama Tume ya Ushirikiano ya Marais (Bi-National Commission-BNC) umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima jijini Dar Es Salaam leo.

“Mkutano huu ni muhimu sana kwa kuwa licha ya nchi zetu kuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri tokea enzi za ubaguzi wa rangi, lakini bado utakuwa chachu ya kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo tutakayokubaliana na wenzetu” Balozi Mlima alisema. 

Balozi Mlima alieleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zilikubaliana kuanzisha Tume ya Marais ya Uchumi (Presidential Economic Commission-PEC) mwaka 2005 na mwaka 2011 nchi hizo zilisaini BNC ambayo ilichukuwa nafasi ya PEC. Tokea uwekaji saini wa makubaliano hayo, chombo hicho hakikuweza kukutana licha ya kuwa, makubaliano hayo ndiyo yatakuwa mwongozo katika majadiliano yatakayoendelea hadi tarehe 11 Mei 2017.

Kwa mujibu wa Balozi Mlima, uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaendelea kuimarika kadri siku zinavyokwenda. Kwa takwimu zilizopo takribani makampuni 226 ya Afrika Kusini yamewekeza nchini mtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 803.15 na kuajiri zaidi ya watu 20,917. Alisema idadi ya makampuni inaweza kuongezeka kwani kuna makampuni mengi mapya kutoka Afrika Kusini yameshaonesha dhamira ya kuwekeza nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, Bw. Edward Makaya alieleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini hazijafanya vya kutosha kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kijamii. Alisema hadi wakati huu nchi hizo zimesaini makubaliano na mikataba takribani 14 ambayo ni michache ukilinganisha na urafiki na udugu uliopo baina ya nchi hizo. 

Hivyo, alisistiza umuhimu wa kikao hicho kufanya majadiliano yatakayowezesha uwekaji saini wa mikataba mingi zaidi. Alisisitiza umuhimu wa mikataba hiyo kuzingatia maslahi ya pande zote. 


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 08 Mei, 2017

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU AKANASHE MAKERE

$
0
0

ILIKUWA NI SEKUNDE, DAKIKA, SAA, WIKI, MWEZI  MWAKA NA SASA NI MIAKA MITANO UMETIMIZA TANGU BIBI YETU KIPENZI AKANASHE SHEDRACK MAKERE UTUTOKE GHAFLA TAREHE 08/05/2012 SAA 10 JIONI BILA YA KUTUAGA KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIKUSUMBUA.

UNAKUMBUKWA SANA KWA UCHESHI, UPENDO NA KUWAJALI KILA KIUMBE CHA HAPA DUNIANI. HALIDHALIKA UNAKUMBUKWA SANA NA WANAO, WAJUKUU, VITUKUU, KILEMBWE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO. UMETUACHIA HUZUNI NA PENGO KUBWA KATIKA UKOO.

MWENYEZI MUNGU, MUUMBA WA MBINGU NA NCHI AENDELEE KUKUPA MWANGA NA RAHA YA MILELE HUKO ULIPO KWANI YEYE NDIYE ALIYETOA NA YEYE NDIYE ALIYETWAA. JINA LA BWANA DAIMA LIHIMIDIWE. AMEN!

BALOZI ASHA-ROSE MIGIRO AWATEMBELEA WANADIASPORA READING

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro alifanya ziara ya kuwatembelea watanzania waishio Reading na Bekshire tarehe 6/5/2017. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Balozi Migiro alipata fursa ya kufanya mkutano na kuwatembelea baadhi ya watanzania hao kwenye maeneo yao ya kazi.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro akiwa pamoja na baadhi ya wana diaspora waishio Reading na Bekshire waliohudhuria mkutano.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Bw. Daniel Samwenda mmoja wa wamiliki wa kampuni ya McDaan Finance inayojishughulisha na shughuli mbali mbali za kifedha kama kutoa mikopo ya muda mfupi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro akipata maelezo kutoka kwa Bw. Hassan Abdula Mkurugenzi wa Kampuni ya Hill View Family Co. Ltd inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI PAMOJA NA UJUMBE WA MWENYEKITI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mtungi (kulia) aliemtembelea leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akisisitiza  jambo mbele ya ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto) na kulia ni Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mtungi katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto), pale ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa ulipomtembelea leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto), Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mtungi (kulia) pale walipomtembelea na ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akimsikiliza Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mtungi (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma. 
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akizungumza jambo pale ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe.John Shibuda ulipomtembela leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akisaini Cheti cha homa ya Manjano alichokabidhiwa leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akionyesha Cheti cha homa ya Manjano alichokabidhiwa leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.


(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI APRILI HAUJAONGEZEKA UMEBAKI ASILIMIA 6.4

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa za watu na Takwimu  Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Aprili. Kulia ni Mtakwimu, Hashim Njowele.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji  ilivyokuwa mwaka ulioisha.

Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017  kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,"alisema

Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi.

Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Ma
chi.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo alisema  uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.

KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, DKT LEONARD CHAMURIHO AKEMEA UDOKOZI NA WIZI KATIKA USAFIRI WA ANGA.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Masuala ya Kiuchumi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Dan Malanga (wa kwanza Kushoto) akimsikiliza Meneja wa uwanja wa ndege wa Dodoma, Julius K. Mlungwana,(wa Pili Kushoto) wakati kamati ya kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ilipotembelea kiwanja cha ndege Dodoma May, 8 2017.
Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Masuala ya Kiuchumi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Dan Malanga (Amesisima) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha 42 cha wajumbe wa kamati ya kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga kilichofanyika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma May, 8 2017.
Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Rogatus Hussein Mativila akifungua kikao cha 42 cha wajumbe wa kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga Kilichofanyika Ukumbi wa Hazina mijini Dodoma May, 8 2017.
Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga katika picha ya pamoja wakati wa kikao cha 42 kilichofanyika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma May, 8 2017.
Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga Wakitembelea Vifaa vya Kutolea Huduma za Usafiri wa Anga kama sehemu ya mkutano wao wa 42 uliofanyika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma May, 8 2017.
Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga Wakikagua Njia ya Ndege ya Uwanja wa Ndege wa Dodoma Kama Sehemu ya Mkutano wao wa 42 uliofanyika Ukumbi wa Hazina Dodoma May, 8 2017.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana ateta jambo na Wazir pamoja na Pole pole jijini Arusha

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Katibu wa Makamu wa Rais Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalamiana na Katibu wa Makamu wa Rais Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo Katibu wa Makamu wa Rais Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TISA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 8, 2017.

$
0
0
Spika  wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA)  Mhe.Catherine Nyakao Ruge  akila kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Mariam Kisangi(CCM) akiuliza swali katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Angelina Malembeka (CCM) akiuliza swali katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe.Eng Ramo Makani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA)  Mhe.Catherine Nyakao Ruge  akichangia mchango wake wa kwanza katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Naibu  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani   akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof Palamagamba Kabudi akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge  katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akiwa na Naibu wake wakifuatilia hoja mbalimbali za wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Mikumi(CHADEMA) Mhe.Joseph Haule akichangia hoja katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.


Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images