Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1222 | 1223 | (Page 1224) | 1225 | 1226 | .... | 1898 | newer

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Serikali na Wazee wa CCM uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu .(Picha na Ikulu)
  JIBO2
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.(Picha na Ikulu)
  JIBO3
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kabla ya kuaza safari yake Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.(Picha na Ikulu) 

  0 0


  Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V unapenda kuwaalika watanzania wote wanaoishi Ujerumani (TANZANIA DIASPORA) kwenye mkutano mkuu wa umoja wetu 2017. Mkutano wetu mkuu utafanyika Siku ya Jumamosi, terehe 13.05.17 saa 13:00 Mchana  katika Address ifuatayo:
  Bob's Cafe,
  Altendorfer Straße 375
  45143 Essen
  Ili kufanikisha mkutano wetu tunawaomba Watanzania kufika kwa wingi mno, mkutano huu ni muhimu sana kwani  kuhudhuria kwenu ndio mafanikio ya umoja wetu na mafanikio yako wewe mtanzania unayeishi hapa ujerumani . Umoja wa Tanzania Ujerumani ( UTUe.V) ‘’Ndio mwavuli  na Sauti ya Watanzania Ujerumani’’

  0 0


  Daktari bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China Dk. Gao, akimpima kifua mtoto Salma Mohammed mkaazi wa Kilmahewa, katika siku ya Afya ya Kijiji iliyofanyika Skuli ya Kwamtipura Wilaya ya Mjini Unguja.
  CHO2
  Daktari bingwa wa pua na masikio kutoka China Dk. Fei Jie, akimfanyia uchunguzi wa pua Bi. Amina Himid katika siku ya Afya ya kijiji iliyofanyika Skuli ya Kwamtipura.
  CHO3
  Afisa Afya akimpatia dawa mmoja wa wagojwa waliofika kupata huduma katika siku ya afya ya kijiji huko Skuli ya Kwamtipura Wilaya ya Mjini.
  CHO4
  Vijana wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi.
  CHO5
  Wananchi waliojitikeza kupatiwa huduma katika siku ya Afya ya Kijiji huko Skuli ya Kwamtipura.
  CHO6
  Watoto wakinywa Uji mara baada ya kupatiwa huduma za afya.
  Picha na Makame Mshenga.
  …………………………………………………………………………………..
  Na Mwashungi Tahir-MAELEZO ZANZIBAR
  Mkurugenzi wa Kinga na elimu ya afya Dk. Fadhil Mohammed Abdalla, amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kupima afya zao.
  Amesema hatua hiyo ni muhimu kwani humuwezesha mtu kubaini mapema iwapo amepata maradhi na hivyo kutibiwa kabla athari haijwa kubwa.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kutolewa huduma za afya katika shehia ya Kilimahewa Bondeni kutoka kwa madaktari bingwa wa China, amesema kuwa ni vyema kunapotokea fursa ya huduma bila malipo, wananchi wazichangamkie ipasavyo.
  Dk. Fadhil alisema serikali imekuwa ikichukua juhudi kubwa kuwafikishia wananchi huduma za afya karibu na maeneo yao wanakoishi.
  “Huduma hii adhimu na ni muhimu kwa kujua afya yako na baada ya kupata vipimo unapata matibabu na wengine hushauriwa wafike hospitali ya Mnazi mmoja kwa kupata matibabu zaidi.” Alisema mkurugenzi huyo.
  Dk. Fadhil amesema lengo la huduma hizo ni kuwashajiisha wananchi waweze kuelewa maradhi waliyonayo na kuwezesha kupatiwa matibabu.
  Aidha alieleza kuwa, madaktari hao hutoa elimu ya afya kuhisiana na maradhi ya kuambukiza hasa katika kipindi hichi cha mvua.  
  Nae daktari dhamana wa wilaya ya mjini Ramadhani Mikidadi Suleiman, amesema zoezi la kupima afya ni muhimu na wataalamu wa kutosha wapo hivyo wananchi wasipuuze kujitokeza.
  Katika uchunguzi uliofanya kweny zoezi hilo, Dk. Mikidadi alisema wananchi wengi wamegundulika na matatizo ya macho, meno, koo, kisukari na shinikizo la damu na kupatiwa matibabu.
  Amewahimiza wananchi kutodharau zoezi hilo litakalokuwa linafanyika kila baada ya miezi mitatu.
  Naye sheha wa shehia ya Kwamtipura Hassan Hashir Hassan, ameeleza kufurahika kwake kutokana na wananchi wengi kuitikia wito na kujitokeza katika zoezi hilo lililofanyika bila ya malipo.
  Maradhi mengine yaliyogunduliwa kutokana na uchunguzi ni tezi dume, maradhi ya mama na mtoto pamoja na kuchukuliwa vipimo vya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
  Wananchi mbalimbali wameipongeza serikali kwa kuwafikishia huduma hizo katika maeneo  yao, wakisema imesaidia kuwapunguzia usumbufu na gharama za kwenda mbali.

  0 0

  NA Ally Daud –WAMJW Dodoma.

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewasihi wanamichezo wa Tanzania wapate chanjo ya homa ya manjano kabla ya kusafiri ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano wanapokwenda nchi ambazo zina maambukizi ya ugonjwa huo.

  Akizungumza hayo mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo ili wasipate ugonjwa pindi wanapotembelea nchi zenye ugonjwa huo.

  “Nawaomba wanamichezo na watanzania kwa ujumla wapate chanjo hii ili kusudi wajilinde kutokupata ugonjwa huu kwani tumezungukwa na nchi wanachama ambao wana ugonjwa wa homa ya manjano” alisema Dkt. Mwakyembe.

  Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo kwani huwa wanasafiri mara kwa mara kuwakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

  Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas Amesema kuwa ugonjwa wa homa ya manjano una madhara hivyo ni vyema kwa wafanyakazi,wafanyabiashara pamoja na wanafunzi wanaosafiri nje ya nchi hususani nchi zenye ugonjwa huo ni vyema wakajitokeza kupata chanjo.  
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kulia akipata maelekezo juu ya nchi zenye ugonjwa wa homa ya manjano barani Afrika na Duniani kutoka kwa Afisa Habari Msaidizi Wa Wizara ya Afya Bw. Ally Daud kushoto mara baada ya kupata chanjo ya homa ya manjano katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Msemaji Mkuu wa Serikali na ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Habari Dkt Hassan Abbas wa kwanza kulia akipokea cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Afya Mazingira Dkt. Khalid Massa wa kwanza kulia mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwnja vya Bunge mjini Dodoma katikati ni Afisa Afya Remidius Kakulu.

  0 0


  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brig Generali Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,(Picha na Ikulu) 6 Mei 2017.
  ol1
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, akisalimiana wafanyakazi wa Ofisi  ya Ubalozi wa Ethiopia mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini Humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(Picha na Ikulu) 6 Mei 2017.
  ol2
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brig Generali Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,(Picha na Ikulu) 6 Mei 2017.
  ol3
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brig Generali Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,(Picha na Ikulu) 6 Mei 2017.


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akitunuku cheti kwa mmoja wa madiwani waliohitimu mafunzo ya jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
  ZA
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
  ZA 1
  Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Singida wakifuatilia kikao cha baraza hilo.
  ZA 2
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida Rashid Mandoa (katikati) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia kwake) na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Eliya Digha.

  ………………..
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida Rashid Mandoa ameagizwa kuhakikisha ofisi za halmashauri hiyo zinahamia ndani ya eneo la halmashauri hiyo na kutoka walipo sasa katika manispaa ya Singida.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo jana wakati akikabithi vyeti kwa madiwani wa halmashauri ya Singida walipohitimu mafunzo kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

  Dkt. Nchimbi amesema endapo mkurugenzi atahamishia ofisi na watendaji katika halmashauri yake watapata ubunifu wa kutatua shida na kero za wananchi na hivyo kuiendeleza halmashauri.

  “Ukikaa kwenye nyumba inayovuja ndipo utapata akili na ubunifu wa kutatua changamoto hiyo, ukiangaia wanufaika wa Tasaf wameweza kufanya mambo mazuri kwa pesa kidog waliyonayo, mkurugenzi uige mfano huo, mhamie katika halmasahuri yenu, wananchi hawafurahii kuwaona ninyi na watendaji wengine mkiishi manispaa” amesisitiza Dkt. Nchimbi.

  Ameongeza kuwa kusitasita kwao kutohamia katika halmashauri yao kutasababisha halmasahuri hiyo ikavunjwa na hivyo kukosa ajira kwa watumishi huku akiwaeleza madiwani kuwa wataponzwa wa kukosa kura katika uchaguzi ujao kwani wananchi wangependa kupata huduma kwa ukaribu.

  Dkt. Nchimbi amesema kuhusu makao makuu ya halmashauri hiyo baraza la madiwani litachagua makao makuu yao huku akishauri wazingatie eneo ambalo litafaa kwakuwa Halmashauri hiyo inapitiwa na miradi mbali mbali ya kitafa ikiwemo mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga na ujenzi wa kituo cha jeshi.

  Akizungumzia mafunzo waliyopea amesema ana imani kuwa sasa mafunzo hayo yataleta matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri ya kuwasiliana na wananchi na kujisogea pamoja na wananchi, huku akiwaasa wasitumie kauli za kuwakatisha tama wananchi.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema mafunzo yatawasaidia madiwani kusimamia miradi ikamilike na iwe na ubora unao takiwa huku akitarajia kuona wananchi wakiibua na kukamilisha miradi ya maendeleo.

  Tarimo ameongeza kuwa madiwani wanapaswa kuhakikisha simu huu wa mavuno wananchi wanavuna na kuhifadhi mazao yao vizuri pamoja na kuwaelimisha wayatumie vizuri ili wapate fedha za kujiendeleza.

  Kwa upande wao madiwani hao wamesema mafunzo hayo yamekuwa msaada kwao kwa kuwaelimisha majukumu yao na mipaka yao ili waweze kitekeleza kwa ufanisi uwakilishi wao wa wananchi.

  Wamesema wengi walikuwa hawafahamu mipaka yao na hivyo kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu huku wakieleza kuwa mafunzo yameimarisha ushirikiano baina yao na watendaji tofauti na hapo awali.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

  Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

  Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.

  Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.
   Makamu w a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo  Mhe. Makamu wa Rais ataongoza  wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kuaga miili ya wanafunzi,na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   

  0 0


  Kundi la waandishi kumi wa habari kutoka nchini Israel wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Gombe hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). Kwa sasa soko la utalii la mashariki ya kati limeanza kufunguka kwa kasi ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel Ehud Barak ametembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti.


  HAMZA TEMBA - WMU

  .......................................................................

  Kundi la wanahabari kumi akiwemo muigizaji mmoja na maofisa wa kampuni ya utalii ya Safari kutoka nchini Israel limetembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma na kufurahia vivutio lukuki vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kuahidi kuvitangaza watakaporudi nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA na Bodi ya Utalii kutangaza vivutio hivyo nchini humo.


  Akizungumza hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili, Kiongozi wa kundi hilo, Ronit Hershkovitz alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wamefurahia kuona vivutio vya kipekee katika hifadhi hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa vivutio hivyo nchini Israel. 


  “Ni furaha kubwa kuwa hapa Gombe, tumeona makundi ya Sokwe na fukwe nzuri za Ziwa Tanganyika, tuko hapa kwa ajili ya kwenda kueleza kivutio hiki na vivutio vingine vya Tanzania nchini Israel, Waisrael wanaipenda Tanzania na wanapenda kutembelea Tanzania, tumeona ongezeko kubwa la watalii katika miaka ya hivi karibuni kutoka Israel baada ya kazi ngumu ya muda mrefu, sasa tuna furaha kuona watalii wengi wanaongezeka na tungependa kuona pia Watanzania wengi wakitembelea Israel,” Alisema Ronit.


  Aliongeza kuwa, “Tunaenda kueleza taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii, magazeti, televisheni na popote tutakapoweza, lakini kubwa zaidi ni kuwaeleza marafiki zetu ana kwa ana uzuri wa Tanzania kwasababu tunaipenda Tanzania, nakupenda sana”.


  Walfson Noa, ambaye ni Mwandishi wa Mitandao ya Kijamii na Meneja Masoko wa Kampuni ya Utalii ya Safari ya Israel alisema, “Tulifanya matembezi kuwaona Sokwe wanaovutia sana huku wakiishi katika mazingira yao ya asili, hili ziwa ni la maajabu sana (Ziwa Tanganyika), hata nyani nao walikuwa wakijaribu kuingia kwenye mahema yetu ni jambo la kuvutia, katika mtizamo wa kimasoko hili ni eneo ambalo nitawashauri wateja wangu watembelee, ni kitu ambacho watu wanatakiwa kukifahamu, kugundua siri ya uzuri wa hifadhi ya Taifa ya Gombe” 


  Kwa upande wake Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo akishirikiana na Meneja Mawasiliano TTB, Geofrey Tengeneza, Meneja Mawasiliano wa TFS, Glory Mziray na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili, Hamza Temba alisema ujio wa wanahabari hao utaleta chachu ya kuongezeka kwa watalii wengi kutoka Israel pamoja na kupanua soko la utalii kwa hifadhi za mikoa ya magharibi mwa Tanzania ikiwemo hifadhi ya Gombe.


  “Tumekuja na kundi hili la wanahabari ambao wameamua kama mlivowasikia kwa dhati kabisa kwamba watakaporudi nyumbani watatumia mitandao ya kijamii, radio mbalimbali, Televisheni lakini kubwa zaidi magazeti, wataandaa makala na vipindi mbalimbali hivyo tunaamini kwa dhati kabisa watakaporudi nyumbani na kuzifanyia kazi taarifa zote walizozipata katika hifadhi ya Taifa ya Gombe ama kwa hakika tutashuhudia ongezeko kubwa la watalii kutoka nchini Israel katika siku chache zijazo,”Alisema Shelutete.


  Aliongeza kuwa, “Ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha rasilimali hizi za hifadhi zinazopatikana katika hifadhi za taifa zinaendelea kutunzwa kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo, watalii hawaji kuangalia ng’ombe kwenye hifadhi zetu, nasisitiza kuwa mifugo haikubaliki kwenye hifadhi zetu”.


  Msafara huo ulikuwa na wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel 2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari ya nchini humo.


  Hifadhi ya Taifa ya Gombe ilianzishwa mwaka 1968 kwa ajili ya tafiti za kisayansi, hususani katika kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori adimu wa jamii ya Sokwe Mtu (chimpanzees) ambao wapo hatarini kutoweka. Hifadhi hii inaelezwa kuwa na Sokwe wasiopungua mia moja ambao huishi kwa makundi na kuwa kivutio kikubwa na adimu katika hifadhi hiyo ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 52.
  Timu maalum ya wanahabari kutoka nchini Israel ikiwa na wajumbe kumi ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa ajili ya ziara ya kitalii ya siku mbili katika hifadhi ya Taifa ya Gombe. Ziaza hiyo iliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirika ya Hifadhi za Taifa Tanzani (TANAPA) kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Israel ikiwa ni mkakati maamlum wa kukamata soko la Mashariki ya Kati. Kutoka kulia wanaongoza msafara huo ni Meneja Mawasiliano TANAPA, Paschal Shelutete na Meneja Mahusiano wa TTB, Geofrey Tengeneza.
  Wanahabari kutoka Israel wakipanda kwenye boti kwa ajili kunza safari kuelekea hifadhi ya Taifa ya Gombe. Msafara huo ulikuwa na wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel 2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari  ya nchini humo.
  Msafara wa Wanahabari wa Israel wakiwa kwenye boti tayari kwa safari ya kuelekea hifadhi ya Taifa ya Gombe ambapo kutoka Kigoma mjini hadi kwenye hifadhi hiyo ni mwendo wa saa moja na nusu hadi masaa mawili.
  Mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe, Elihuruma Wilson (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa wanahabari kutoka nchini Israel kuhusu hifadhi hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea vivutio vilivyopo. Alieleza kuwa hifadhi hiyo ina vivutio vingi wakiwemo  Sokwe zaidi 100, Nyani, Kima, maporomoko ya maji, ndege aina mbalimbali na fukwe nzuri za kuogelea za ziwa Tanganyika. 
  Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (kulia), Meneja Mahusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania (Geofrey Tengeneza) na Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Glory Mziray) wakiongoza msafara wa wanahabari wa Israel kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Timu ya wanahabari wa Israel wakianza safari ya kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya kuona makundi mbalimbali ya Sokwe. Lengo kuu la ziara hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na TANAPA ni kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Israel.
  Wanahabari kutoka Israel wakipata maelezo kutoka kwa mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe kuhusu utarartibu wa kuzingatia wawapo ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo kutokupiga kelele na kuepuka matumizi ya mwanga wa kamera (Flash Lights).
  Mmoja ya wanahabari wa Israel, Gerald Eddie wa Jarida la National Geographic akiwa katika harakati za kupata taswira mwanana ya picha za Sokwe ndani hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Wanahabari wa Israel wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Sokwe akirukia matawi ya miti akiwa na mtoto wake ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara ya wanahabari wa Israel kwenye hifadhi hiyo.
  Taswira mwanana ya Sokwe Mtu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara hiyo.
  Mtoto wa Sokwe akila matunda yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara ya wanahabari wa Israel katika hifadhi hiyo. Lengo kuu la ziara hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na TANAPA ni kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania nchini Israel.
  Sokwe akiwa kapumzika kwenye maeneo yake ya kujidai ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa zaira ya wanahabari wa Israel katika hifadhi hiyo. Wanahabari hao walifurahia kuwaona sokwe hao wanaoelezewa na wanasayansi kuwa wanakaribiana na binaadamu kwa takribani asilimia 80.
  Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (wa pili kulia) akionesha kifaa maalum cha kupigia picha za angani (drone) kilichorushwa na mmoja wa mwanahabari ambaye ni mpigapicha kutoka Israel katika fukwe za Ziwa Tanganyika pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa zaiara ya wanahabari hao hifadhini hapo.   
  Kifaa hicho maalum cha kupiga picha za angani kijulikancho kama 'drone' kikiwa angani kupata taswira pana ya hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Wanahabari hao wakipiga picha za mwanahabari mwenzao na nyani wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe katika fukwe za Ziwa Tanganyika.
  Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot  Acharonot (kushoto) akiigiliza mkao wa nyani katika hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara hiyo. Matukio hayo yataonekana katika jarida hilo nchini Israel kwa ajili kutangaza vivutio vya Tanzania. Anayepiga picha ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Paschal Shelutete.
  Mpiga picha wa Jarida la National Geographic la nchini Israel, Gerald Eddie akipiga picha nyani wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe ambao pia ni kivutio cha utalii katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza katika jarida hilo.
  Nyani akiwa kambeba mtoto wake katika  hifadhi ya Taifa ya Gombe tukio ambalo pia sehemu ya vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
  Wanahabari hao hawakutaka kupitwa na tukio lolote katika ziara yao hiyo, hapo wakipiga picha boti ambayo hufanya safari za kawaida kwa wananchi wa vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika na Manispaa ya Kigoma.
  Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot  Acharonot (wa pili kushoto) na Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini humo, Ran Sarig wakiigiliza mkao wa nyani dume na jike katika fukwe za ziwa Tanganyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot  Acharonot (wa pili kushoto) na Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini humo, Ran Sarig wakifurahia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakifanywa na nyani wa hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Wanahabari hao pia walipata fursa ya kuogolea katika fukwe za kitalii za ziwa Tanganyika pembezoni mwa Hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe, Fukwe hiyo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Gombe. 
  Wanahabari hao wakiwa wanaogelea katika fukwe za kuvutia za ziwa Tanganyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe huku wakipiga picha za tukio hilo kwa ajili kutangaza kivutio hicho nchini Israel.
  Wanahabari hao pia walipata fursa kutembelea jamii ya kijiji cha Mwamgongo ambacho kinapakana na hifadhi ya Taifa ya Gombe, hapo wakimpiga picha mtoto aliyekuwa na mpira wa makaratasi ambao ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
  Mwandishi wa habari kutoka Israel ambaye ni mpiga picha wa kituo cha Televisheni cha Chanel 2, Roni Dahabari Kuban akiwapiga picha watoto katika kijiji cha Mwamgongo jirani na hifadhi ya Taifa ya Gombe.
  Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini Israel, Ran Sarig akifungwa shuka aliyoinunua na wananchi wa Kigoma katika ziara hiyo. Shuka hizo zinazofumwa kwa mikono ni maarufu Mkoani Kigoma na sehemu ya utalii wa Kiutamaduni unaopatikana katika Mkoa huo. 
  Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini Israel, Ran Sarig akipiga picha ya "Selfie" na baadhi ya watoto wa kijiji cha Mwamgongo kilichopo jirani na hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara hiyo.
  Wanahabari hao walipotembelea kijiji cha Mwamgongo kilichopo jirani na hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe walipata kujionea na kushiriki katika ngoma za asili ambazo pia ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
  Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot  Acharonot  akijaribu kuwasiliana na wanakikundi cha ngoma za asili wa kijiji cha Mwamgongo kinachopakana na hifadhi ya Taifa ya Gombe na kushudia kazi zao za mikono na ngoma ambazo ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
  Mwandishi wa habari wa mitandao ya kijamii nchini Israel, Walfson Noa akifurahia michezo na jamii ya watoto wa kijiji cha Mwamgongo wakati wa ziara hiyo.
  Watalii wa ndani nao pia walikuwemo kufurahia vivutio vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kutoa wito kwa watanzania wengi zaidi kuvitembelea. Meneja wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Paschal Shelutete (wa pili kushoto waliosimama) akiongoza mahojiano na watalii hao wa ndani.
  Picha ya pamoja ya wanahabari wa Israel, wahifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe na waongoza msafara huo ambao ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Paschal Shelutete (wa pili kulia), Meneja Mahusiano wa TTB, Geofrey Tengeneza (katikati waliosimama), Meneja Mawasiliano TFS, Glory Mziray (wa tatu kulia) na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Hamza Temba (wa nne kulia).
  Baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe msafara wa wanahabari hao ulipanda boti kwa ajili ya safari ya kurudi Kigoma Mjini.

  0 0

  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Bi.Susan Barnabas jana wakati walipofunga ndoa takatifu na kuwa mwili mmoja kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam wakisindikizwa na wasimamizi wao Benedict Mwakasindile na Bi. Leticia Mwakaila , Ndoa hiyo ilifungwa na Padri Padri Haule wa Kanisa hilo Timu nzima ya Fullshangwe inawatakiwa maisha marefu na yenye furaha katika ndoa yenu huku mkijaaliwa kuiongeza dunia.
  MUS2
  Bibi harusi Susan Barnabas na msimamizi wake Leticia Mwakaila wakiwa kwenye gari kabla ya kuingia kanisani tayari kwa tukio la kufungwa kwa ndoa hiyo jana.
  MUS3
  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akimvisha pete Mkewe Susan Barnabas wakati walipofunga ndo katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jana jijini Dar es salaa.
  MUS4
  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Susan Barnabas wakishiriki sala wakati wa ibada ya kufungwa kwa ndoa yao jana.
  MUS5
  Padri Haule wa kanisa la Mtakatifu Petro akiziombe pete za maharusi huku maharusi hao wakiwa wamezishikilia.
  MUS6
  Bibi Harusi Susan Barnabas akipozi kwa picha kwenye gari.
  MUS7
  ibi Harusi Susan Barnabas akimvisha pete mumewe Bw. Raymond Mushumbusi wakati walipofunga ndo kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Osterbay jijini Dar es salaa huku Padri Haule akishuhudia tukio hilo kulia ni Bw. Benedict Mwakasindile msimamizi wa maharusi hao.
  MUS8
  Maharusi wakisaini vyeti vya ndao mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo.
  MUS9
  Maharusi wakiwa kanisani mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo.
  MUS10
  Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam jana.

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad Jumamosi Mei 6,2017 amekabidhi Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12.6 katika vituo vya afya vinne vya afya ambavyo ni Nhobola,Songwa,Ng’wang’haranga na Dulisi vilivyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga .
  Vifaa tiba hivyo ni Vitanda sita vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama wajawazito,vitanda sita kwa ajili ya kulalia wagonjwa,shuka 12 na viti sita kwa ajili ya wagonjwa.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema vimetolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania na vitasaidia katika kupunguza adha wanayopata akina mama wajawazito wanapofika kupata huduma katika vituo vya afya.
   

  “Akina mama ndiyo wanapata adha kubwa wanapohitaji huduma za afya,baada ya kuona jinsi akina mama hawa wanavyoteseka,niliamua kuanza kutafuta watu wa kutusaidia,nashukuru ubalozi wa China nchini ulikubali kunipatia vifaa hivi kwa ajili ya wananchi wa Shinyanga”,alieleza Hamad.

  “Vifaa hivi vitasaidia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto,naomba mvitunze”,aliongeza Hamad.Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya kuozesha watoto wadogo kwa tamaa ya mali ‘ng’ombe’ kwani takwimu zinaonesha kuwa watoto wanapopata ujauzito inasababisha wengi wao kupoteza maisha wakati wa kujifungua.

  “Mkoa wa Shinyanga tunaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni,naomba tupeleke watoto shule,waacheni watoto wa kike wasome,wakifeli darasa la saba watafutieni shughuli ya kufanya siyo kuwaozesha,ni hatari kwa maisha yao”,aliongeza Hamad.

  Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kuzitaja baadhi ya changamoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali wilayani kuwa ni upungufu wa watumishi,magari ya wagonjwa na miundo mbinu. 

  Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio wakati mbunge Azza Hilal Hamad akiwa wilayani Kishapu kukabidhi vifaa tiba pamoja na kuzungumza na wananchi

  Hapa ni ndani ya kituo cha afya Nhobola wilayani Kishapu-Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola kilichopo kata ya Talaga,Bhujiku Mganga Nyanda
  Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola Bhujiku Mganga Nyanda akieleza jinsi akina mama wajawazito walivyokuwa wanapata changamoto wakati wa kupata matibabu
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika wodi ya wazazi amebeba mtoto wa mkazi wa Kata ya Talaga baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Nhobola
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia kubeba mtoto mwingine aliyezaliwa katika kituo cha afya NhobolaMwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) akimkaribisha Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) katika mkutano wa kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Nhobola
  Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akizungumza katika kituo cha afya Nhobola kabla mbunge Azza Hamad kuendesha zoezi la kukabidhi vifaa tiba 
  Kaimu katibu Umoja wa Akina mama wa CCM mkoa wa Shinyanga Rhoda John akizungumza katika kituo cha afya Nhobola
  Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akielezea changamoto zilizopo katika vituo vya afya,zahanati na hospitali wilayani Kishapu
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) akifungua mkutano wa mbunge Azza Hilal Hamad katika kituo cha afya Nhobola
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF) 
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea kuhusu msaada wa vitanda vya kujifungulia,kulalia na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Nhobola
  Vitanda vitatu vya kulalia wagonjwa,kitanda kimoja cha kujifungulia na viti vya wagonjwa vilivyotolewa katika kituo cha afya Nhobola
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kisasa cha kujifungulia
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kulalia wagonjwa
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shuka zitakazotumika katika vitanda alivyopeleka katika kituo cha afya Nhobola
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa viongozi wa kijiji,kata na wilaya ya Kishapu
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa kata ya Talaga
  Diwani wa kata ya Talaga Richard Kazangu Dominiko( CCM) akitoa neno la shukrani baada ya mbunge Azza Hilal Hamad kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Nhobola
  Mkazi wa kijiji cha Nhobola aliyejulikana kwa jina la Ng'wani Sali akimshukuru mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kupeleka vitanda katika kituo cha afya Nhobola 
  Hapa ni katika kata ya Songwa-Pichani wakazi wa kata ya Songwa wilayani Kishapu wakijiandaa kumpokea Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)  alipowasili katika kata ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda,shuka na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
  Wananchi waliobeba matawi ya miti wakiwa wamemzingira Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) alipowasili katika kata ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda,shuka na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amefungwa nguo huku akiandamana na wananchi kuelekea eneo la mkutano wa hadhara katika kata ya Songwa
  Wananchi waliobeba matawi ya miti wakiandamana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
  Maandamano kuelekea eneo la mkutano yakiendelea
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia na wananchi waliompokea
  Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza baada ya mgeni rasmi mheshimiwa Azza Hilal Hamad kufika eneo la mkutano kabla ya kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Songwa 
  Wacheza ngoma wakisalimiana na Mbunge Azza Hilal Hamad (CCM)
  Wacheza ngoma ya asili 'Wanunguli' wakitoa burudani
  Mcheza ngoma ya Ununguli akimshika nyoka
  Mcheza ngoma ya Ununguli akiwa amemkamata nyoka
  Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akiwasalimia wananchi wa kata ya Songwa
  Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akiteta jambo la mheshimiwa Azza Hilal Hamad
  Kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza wakati kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani ambao ulimfurahisha na kuwaahidi kuwadhamini ili waurekodi wimbo huo
  Akina mama wakiimba shairi
  Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akizungumza wakati wa mkutano wa mbunge Azza Hilal
  Suzana Yohana akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa kata ya Songwa 
  Mzee Hamis Bulege akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad,zawadi iliyotolewa na wazee wa Songwa ikiwa ni ishara ya kuwa wanamkubali kama kiongozi mzuri anayejali wananchi wake
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akipokea zawadi ya mbuzi
  Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akizungumza
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa kata ya Songwa
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizunguza
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akisitiza jambo
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vitanda vya kulalia na kitanda cha kujifungulia pamoja na viti vya wagonjwa
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akionesha shuka zilizotolewa katika kituo cha afya Songwa
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza baada ya kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Songwa.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  images

  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 36 ambao ni wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa gari la shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea jana tarehe 6 Mei 2017 katika ajali ya gari katika eneo la Rhotia Marera Wilayani Karatu, Arusha.

  Katibu Mkuu wa UWT Ndg Amina Makilagi ametoa salamu za pole na rambi rambi kwa familia, wazazi, ndugu na walezi waliopoteza wapendwa wao hasa watoto wadogo waliokuwa wakilelewa kuwa raia wema na nguvu kazi bora ya Taifa letu hapo baadae. 

  Katika salamu zake Ndg Makilagi amesema UWT inaungana na wanawake, wazazi na waombolezaji wote nchini kuwaombea majeruhi kupona haraka na kumuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi. Amina Imetolewa na:- AMINA MAKILAGI KATIBU MKUU WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA 07/05/2017.

  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

  Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.

  Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

  “Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

  “Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

  Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

  “Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

  Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  0 0  0 0
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017

  ……………………………………………………………………….

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Djibouti Ismail Omar Guelleh ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuanzisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo hasa katika sekta za maendeleo na uchumi.

  Viongozi walifanya mazungumzo katika ukumbi wa Ikulu ya Djibouti ambapo Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na shukurani kwa Rais Guelleh kwa mwaliko wake huo nchini mwake.

  Katika mazungumzo hayo viongozi hao kwa kauli moja walieleza haja ya kuanzisha uhusiano na ushirikiano katika sekta mbali mbali za maendeleo na uchumi kwa manufaa ya pande mbili hizo.

  Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh kwa upande wake alimuhakikishia Dk. Shein kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta za mawasiliano, utalii, uwekezaji pamoja na usafiri na usafirishaji sambamba na utayari wa kujifunza mambo mbali mbali kutoka Zanzibar ikiwemo sekta ya utalii.

  Rais Guelleh, alieleza kuwa nchi yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ambao una historia nzuri na kueleza kuwa Djibout iko tayari kujifunza mbinu zilizotumika na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii.

  Ambapo pia, kiongozi huyo alieleza utayari wa kushirikiana na Zanzibar kutokana na mafanikio waliyoyapata na njia sambamba na mikakati waliyoitumia katika kufikia mafanikio waliyoyapata na mikakati waliyoitumia kufikia mafanikio waliyonayo hasa katika suala zima la uimarishaji wa bandari, mawasiliano na vitega uchumi.

  Kiongozi huyo wa Djibouti alimkaribisha Dk. Shein pamoja na ujumbe wake nchini humo huku akisisitiza kuwa Tanzania na Djibouti zina ukaribu mkubwa na zimekuwa zikishirikiana katika kupambana na uharamia wa baharini kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Mamlaka ya Serikali ya Kimaendeleo (IGAD).

  Aidha, Rais Guelleh alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Shein mafanikio yaliyopatikana nchini mwake hasa kutokana na uimarishaji wa bandari, mawasiliano na kueleza azma ya nchi yake hivi sasa kujikita katika sekta ya utalii kutokana na baadhi ya vivutio vilivyopo ikiwemo Ziwa Assal ambalo chimbuko lake ni Bonde la Ufa pamoja na mambo mengineyo.

  Hivyo kiongozi huyo alimueleza Dk Shein kuwa pande hizo mbili zina mengi ya kujifunza kwa pamoja kwani kila upande umeweza kupata mafanikio yake.

  Kwa upande wake Rais Dk. Shein, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na shukurani kwa Rais Guelleh kwa mualiko wake huo aliompa pamoja na mapokezi makubwa aliyoyapata yeye na ujumbe aliofuatana nao na kueleza kuwa ziara hiyo itakuwa ndio kichocheo kikubwa cha mashirikiano kati ya Zanzibar na Djibouti.

  Dk. Shein alimueleza Rais Guelleh kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Djibouti hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo wa kiuchumi inategemea sekta ambazo Zanzibar nayo imeamua kwa makusudi kuziimarisha ili ziweze kuimarisha uchumi na kuleta tija.

  Alizitaja miongoni mwa sekta hizo ambazo Djibouti imepata mafanikio ni uendeshaji wa Bandari,mawasiliano na Maeneo Huru ya Kiuchumi ambayo yamekuwa ndio kichocheo kikubwa cha uchumi wa nchi hiyo.

  Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa ziara hiyo ni kielelezo cha urafiki, heshima na udugu baina ya Serikali zote mbili pamoja na wananchi wake ambapo itasaidia sana kuimarisha uhusiano na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano.

  Katika maelezo yake, Dk. Shein alimueleza Rais Guelleh kuwa Zanzibar katika ziara hiyo ina hamu kubwa ya kufahamu maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Djibouti tokea mwaka 1977 ilipopata uhuru wake kutoka kwa Koloni la Kifaransa.

  Dk. Shein alieleza kuwa ana hamu kubwa kuona maendeleo yaliofikiwa na nchi hiyo katika sekta muhimu za kiuchumi na kijamii ikiwemo sekta ya bandari, kuendeleza maeneo Huru, mawasiliano, uvuvi, viwanda, usafiri na usafirishaji, afya, elimu na sekta zote muhimu za utoaji wa huduma kwa wananchi wa nchi hiyo.

  Alipongeza juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Guelleh ambazo zimepelekea Djibouti kuwa ni mfano mzuri kwa nchi za Afrika ambazo zinatafuta maendeleo ya haraka, demokrasia pamoja na kuimarisha hali ya utulivu na usalama wa nchi.

  Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumueleza Rais wa Djibouti mafanikio yaliopatikana kwa upande wa kisiasa na kimaendeleo na kupelekea kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni Muungano wa mfano kwa bara la Afrika na kutoa salamu za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kiongozi huyo.

  Aidha, Dk. Shein alimuhakikishia Rais huyo utayari wa Zanzibar kushirikiana na Djibouti na kutoa uweledi wake katika sekta ya utalii kwa nchi hiyo kutokana na Zanzibar kupata mafanikio makubwa katika sekta ya Utalii.

  Pamoja na hayo, Dk. Sheuin alimuelkeza Rais huyi wa Djibout hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari mpya ya Mpiga Duri, mradi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uingizaji wa mizigo na makontena na kuipunguzia mzigo Bandari ya Malindi.

  Aidha, alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuifanya Zanzibar kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020, huku akitumia fursa hiyo kumualika kiongozi uyo wa Djibouti kutembelea Zanzibar kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbili hizo.

  Dk. Shein yupo nchini Djibouti kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Ismail Omar Guelleh.

  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

  0 0


  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (Kushoto)akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge, Mheshimiwa Sixtus Mapunda mara baada ya mechi kuisha na timu ya Bunge kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa bila dhidi ya NMB,  mechi hiyo ilifanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
  bu2
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (Kulia) ambae pia ni mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Bunge kabla ya kuanza mechi ya mpira wa pete kati ya Timu ya Bunge na Timu ya NMB iliyofanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
  bu3
  Wachezaji wa timu ya Mpira wa pete wa Bunge na NMB wakipiga picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi yao ambayo ilifanyika jana katika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0  0 0

  Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumza jambo wakati wa Kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito ya Arusha.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati), Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria Abubakar Bwari (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abbas Mohamed (wa kwanza kulia) , Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Arusha Peter Pereira ( wa kwanza kushoto ) na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania Sam Mollel (wa pili kushoto) wakifuatilia kutangazwa kwa washindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.  Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) akikata kamba maalum katika masunduku yaliyowekwa bahasha za walioomba kununua madini ya Tanzanite kupitia mnada. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa, (STAMICO) Mhandisi Hamis Komba na kushoto ni Mwakilishi kutoka Kampuni ya TanzaniteOne, Husein Gonga.  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) akiangalia zawadi kabla ya kumkabidhi Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari (kushoto).  Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari (katikati) akiangalia ubora wa Madini ya Tanzanite katika banda la kampuni ya Hadjarat Mining and Gemstone Company Limited. ALiyeshika kifaa cha kupima ubora ni Mkurugrenzi wa Kampuni hiyo.  Baadhi wa washiriki wa Maonesho ya 6 ya Madini ya Vito Arusha wakiwemo wanunuzi na wauzaji wakifuatilia hatua za kumpata mshindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SDK Limited, Susie Kennedy akimwonesha Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari bidhaa za madini zinazotengenezwa na kampuni hiyo.

  …………………………………………………………………………………

  Na Asteria Muhozya, Arusha

  Wadau wa Madini nchini wametakiwa kujikita katika shughuli za ukataji na usanifu wa madini badala ya kusanifiwa nje ya nchi ili kuwezesha adhma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kupitia Sekta ya Madini.

  Hayo yalisemwa na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamini Mchwampaka wakati wa kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3-5 Mei,2017.

  Aliongeza kuwa, uwepo wa shughuli za ukataji na unga’rishaji wa madini hayo nchini kutawezesha kuyaongezea thamani ikiwemo kupanua wigo wa ajira kupitia sekta ya madini.

  ” Tanzania ya sasa ni ya Viwanda. Na sisi sekta ya madini tuwe na viwanda vyetu vya kusanifu madini yetu hapa hapa nchini. Kwanza tutayaongezea thamani madini yetu lakini pia tutazalisha ajira kwa wingi,” alisema Mchampaka.

  Aidha, Kamishna Mchwampaka aliongeza kuwa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imewasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ya Madini nchini ili kuondoa kero ambazo ni kikwazo katika biashara hiyo kwa watanzania.

  “Tunataka kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa madini wa Tanzania lakini pia tunapenda wafanyabiashara wetu washiriki kwa wingi katika maonesho haya. Ni fursa kubwa ya kibiashara kwao,” alisisitiza Mchwampaka.

  Akizungumzia Mnada wa Madini ya Tanzanite uliofanyika tarehe 5 , Mei, alisema kuwa, minada hiyo itaendelea kufanywa mara kwa mara kutokana na mchango wake katika sekta husika kwa kuwa pia inasaidia kupata bei halisi ya madini hayo.

  Katika mnada wa Madini ya Tanzanite jumla ya kampuni 48 zilishiriki mnada huo ambapo madini ghafi ya Tanzanite kutoka Kampuni ya TanzaniteOne yenye jumla ya gramu 691,060.33 ziliuzwa katika mnada huo kwa dola za Marekani 3,161,860, sawa na asilimia 100 ya madini yote yaliyowasilishwa kwa mauzo.

  Pia, alizungumzia ujumbe wa Serikali ya Nigeria iliyoshiriki Maonesho hayo na kueleza kuwa, ujumbe huo ulifika kwa lengo la kujifunza namna Tanzania inavyoongeza thamani madini yake ikiwemo pia kubadilisha uzoefu na kuongeza kuwa, lengo ni kuifanya Afrika inufaike na rasilimali zake za madini.

  Ujumbe wa Serikali ya Nigeria uliongozwa na Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda, Abubakar Bwari aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abbas Mohamed pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara wa Madini kutoka nchini humo.

  0 0


   Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akizungumza wakati akitoa semina kuhusu Ukimwi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya TEMESA jijini Dar Es Salaam.
  TEM2
  Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir  (hayupo pichani) wakati akitoa semina kuhusu maambukizi mapya ya Ukimwi iliyofanyika ofisini hapo.
  TEM3
  Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akisisitiza jambo wakati alipokua akitoa semina ya Ukimwi kwa wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar Es Salaam.
  TEM4
  Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akisisitiza jambo wakati akitoa takwimu kuhusu viwango vya maambukizi ya Ukimwi kimkoa kwa wafanyakazi wa TEMESA katika semina iliyofanyika makao makuu ya wakala huo jijini Dar Es Salaam.
  TEM5
  Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akisisitiza jambo wakati akitoa takwimu kuhusu viwango vya maambukizi ya Ukimwi kimkoa kwa wafanyakazi wa TEMESA katika semina iliyofanyika makao makuu ya wakala huo jijini Dar Es Salaam.

older | 1 | .... | 1222 | 1223 | (Page 1224) | 1225 | 1226 | .... | 1898 | newer