Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI

$
0
0
Jitihada za Wizara ya Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.

Serikali imetunukiwa Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno. Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).
Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali (kushoto) akipokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Sera ya Mtandao wa Kimataifa wa Nishati Mbadala (REN21) yenye makao makuu yake nchini Ufaransa, Profesa Arthouros Zervos.

Akikabidhi Tuzo hiyo Jijini Dar es Salaam, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo; Magali alisema Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania wa kufikisha huduma ya umeme maeneo ya vijijini pamoja na uwezeshaji wa mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wanaosambaza umeme katika maeneo ya vijijini.

“Kwa mwaka huu, Serikali yetu imetambuliwa kwa kufikisha umeme vijijini na juhudi zake za kuhakikisha kunakuwa na mzingira rafiki kwa watoaji na wasambazaji wa huduma ya umeme vijijini,” alisema Magali.
Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali wakionesha Tuzo walizopokea kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno.

Kwa upande wake Dkt.Mhandisi Pallangyo aliipongeza kampuni ya Ensol kwa kupokea tuzo kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuendeleza ushirikiano na kampuni zote zinazojihusisha na usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini.

Alisema Serikali itaendelea kuandaa mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kutimiza azma ya kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya Nishati ya Umeme.
Aidha, Dkt. Mhandisi Pallangyo alizitaka kampuni nyingine zinazoshughulika na uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini kujiunga na Taasisi za Kimataifa ikiwemo ya Alliance for Rural Electrification ili kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Taasisi hizo.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi zake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali.


Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu

$
0
0
Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
 
 Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz).
 
 Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni kwa pamoja wakizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo. Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim (wa pili kulia) Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Makumbusho wakisoma vitabu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Dr. Ntuyabaliwe Foundation Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo (katikati) akionyesha waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) muonekano wa awali kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation. Kushoto ni Mama Mengi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Shule, Haji Shabani Kibwana Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.
 
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho kabla ya uzinduzi huo. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la uzinduzi wa maktaba hiyo
 

NKAMIA AKIMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAZI NZURI

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAPOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA OMAN

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land Cruiser  kutoka kwa  Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. 

Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia Dodoma. 
Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo. 
Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
Balozi Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii.  

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAPOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA OMAN

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dokta Binilith Mahenge akisoma taarifa ya mkoa pamoja na miradi ambayo mwenge wa Uhuru 2017 utafanya kazi ya kufungua, miradi itakayozinduliwa, itakayowekwa mawe ya msingi na itakayo kaguliwa TAARIFA KAMILI HII HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Afungua semina Elekezi kwa Viongozi wa Mkoa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka  Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.           

Na Imma Msumba, Arusha
Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.
 
Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.
 
Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji  wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.
 
Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.
 
Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.
 
Nae katibu tawala wa mkoa  Richard  Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.
 
Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.
Mkuu  wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.
Kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Mh: Calist Lazaro pamoja na viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha.

SAFARI ZA ATCL MKOANI TABORA ZAZINDULIWA RASMI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakikata keki kama ishara ya kuzindua rasmi safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo.
Baadhi ya viongozi na wabunge wakiingia kwenye ndege aina ya Bombardier Dash 8 Q400 ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), iliyotua kwa mara ya kwanza mkoani Tabora katika uzinduzi wa safari za ndege mkoani humo. 






Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, wakiwa ndani ya ndege kuelekea katika uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akihutubia wananchi wa Tabora (hawapo pichani), waliohudhuria uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakati wa uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo. 

Baadhi ya wabunge wakirejea mkoani Dodoma mara baada ya uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora. Uzinduzi huo ulifanywa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.

………………………………………………………………………………

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imeanzisha safari zake kutoka Tabora kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika mikoa hiyo na mikoa jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za kampuni hiyo mkoani Tabora, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa kuanzishwa kwa safari hizo katika mikoa hiyo kutatanua wigo wa kibiashara na kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo za utalii na kilimo.

“Naamini wananchi wa mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani, sasa mtanufaika kwa ujio wa ndege hii, matumaini yangu kwamba mtatumia usafiri huu ambao hautumii muda mrefu katika kurahisisha shughuli zenu za kibiashara na kijamii”, amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kutumia fursa ya ujio wa ndege hiyo kama chachu ya kuleta maendeleo katika mkoa huo.

Sambamba na hilo Eng. Ngonyani, amesema kuwa katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika nchini Serikali itaongeza ndege nyingine tatu katika mwaka wa fedha 2017/18 ambapo hadi kufikia mwezi Julai mwakani ndege hizo zitakuwa zimewasili.

Naibu Waziri Ngonyani amefafanua kuwa ndege mbili kati ya hizo zitakuwa za masafa ya kati aina ya CS 300 ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja na ndege moja ya masafa marefu aina ya Boeing 787 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

Katika hatua nyingine, Eng. Ngonyani amewaagiza wafanyakazi wa ATCL kufanya kazi kwa juhudi, uadilifu na weledi kwa lengo la kuijengea sifa kampuni hiyo na kuvutia wateja ili kujiimarisha katika soko la ushindani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya kupata usafiri wenye gharama nafuu na wa muda mfupi.

Naye, Mkuu wa Mkoa huo Bw. Aggrey Mwanri, amewataka wananchi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya usafiri huo ambao walikuwa wakiusubiri muda mrefu.

Uzinduzi wa safari za ndege mkoani humo ni moja ya hatua za kuboresha usafiri wa anga nchini ambapo Serikali kupitia ATCL ina mpango wa kuanzisha safari katika mikoa mingine na nchi jirani ili kurahisisha huduma za kijamii na kibiashara.

SINGIDA INAZALISHA NUSU YA ASALI YOTE INAYOZALISHWA NCHINI; WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AELEZA.

$
0
0
 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha wazalishaji nyuki cha Kisaki katika manispaa ya Singida.

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali inayozalishwa na kikundi cha wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kikundi hicho Philemon Kiemi. 

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward Mashimba kwa kuhitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya kumtunuku cheti cha mafunzo hayo.
Eneo la kikundi cha wafugaji nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya kutosha katika kijiji cha Kisaki, Manispaa ya Singida. Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha uzalishaji nyuki Philemon Kiemi.

……………………………………………………………………………….

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda Mkoa wa Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.

Amesema Singida imekuwa ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi nzima ukiwa ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.

Mheshimiwa Pinda amesema asali ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana pia dawa huku akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta kuzalisha mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata soko la ndani.

Ameongeza kuwa kuwa wananchi watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta milioni 35 kufuga nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku ikiwafaidisha kwa kuvuna asali na mazao yake.

Mheshimiwa Pinda amewaasa vijana waliohitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kuhakikisha wanaisambaza elimu waliyoipata kwa wenzao pamoja na wao kuwa wagujai nyuki wa mfano katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singda Elias Tarimo amesema Manispaa ya Singida ina vikundi 16 vya uufugaji nyuki na wafugaji nyuki wengi wakiwa katika kata za Uhamaka, Mungumaji, Mtamaa, Mwankonko na Kisaki.

Tarimo amesema wataendelea kuhamasisha vijana na wakazi wengi kufuga nyuki kisasa na kusisitiza ufugaji nyuki kibiashara ndio wenye tija na manufaa kwa mfugaji.

Mmoja wa wahitimu Jacob Edward Mashimba amesema mafunzo ni mazuri na yatawasaidia katika kutunza mazingira kutokana na jamii imekuwa ikikata miti kwa wingi.

Mashimba amesema katika jamii anayotoka ya kihadzabe ambayo bado inategemea asali kama chakula kikuu elimu ya ufugaji nyuki kibiashara itasaidia licha ya upungufu wa baadhi ya vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki.

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM SHAKA HAMDU SHAKA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHE; ZELOTE STEPHEN ZELOTE

$
0
0
Mhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Zelote Stephen Zelote wa kwanza kushoto akimpokea kaimu katibu mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipowasili ofisi za Mkoa kuzungumza Mambo mbali mbali ya kimaendelea pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2015.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akizungumza Mambo mbali mbali ya kimaendelea pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2015 pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen Zelote wa kwanza kulia.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe:Zelote Stephen Zelote wa kwanza kushoto akielezea jinsi ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyo tekelezwa katika mkoa wake kwa Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipowasili Mkoani hapo wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoan Rukwa.

Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe:Zelote Stephen Zelotemara baada ya kumaliza

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa NNE Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen Zelote wa nne kushoto pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Rukwa.

(Picha na FAHADI SIRAJI)

UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI WA MWAKA 2016/17 KUFANYIKA DAR ES SALAAM MWISHONI MWA MWEZI MEI, 2017

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema akizungumza hivi karibuni na Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/17. Kwa Dar es Salaam, utafiti huu unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Mei, 2017.

Na: Veronica Kazimoto.

Wito umetolewa kwa Wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam ambao kaya zao zimechaguliwa kitaalam kwa ajili ya  Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 kutoa ushirikiano kwa wadadisi wataokusanya taarifa za utafiti huo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu.

Akizungumza hivi karibuni katika  Mkutano wa Wadau wa Utafiti huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema amesema Utafiti huu ni muhimu sana kwani husaidia kujua hali halisi ya ugonjwa wa UKIMWI na hivyo kuongeza nguvu zaidi ya kuondokana na ugonjwa huo.

"Mimi niwaeleze tu kwamba, utafiti huu ni muhimu sana katika mkoa wetu wa Dar es Salaam kwa kuwa utatusaidia kujua hali halisi ya maambukizi ya VVU na hatimaye kupata nguvu zaidi za kuondokana na ugonjwa huu, hivyo nawaagiza kusimamia zoezi hili na kuwahimiza Wananchi wote ambao kaya zao zimechaguliwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaofanya taarifa za utafiti huu", amesema Mjema.
Mkurugenzi Msahauri, Dkt. Cecilia Makafu kutoka Shirika la ICAP Tanzania akiwasilisha mada kuhusu Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 kwa wadau wa Utafiti huo wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mjema amefafanua kuwa, utafiti huu ni wa kwanza kukusanya taarifa zinazohusiana na maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU na wastani wa maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote pamoja na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count).

Aidha,  utafiti huu utapima uwepo wa viashiria vya usugu wa dawa, kiwango cha maambukizi ya kaswende pamoja na homa ya ini (Hepatitis B).

Akizungumzia kiwango cha maambukizi ya VVU katika tafiti zilizopita, Mkuu wa Wilaya huyo ameeleza kuwa, maambukizi yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011 na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizi ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo nchi nyingi za ukanda huo zina kiwango cha zaidi ya aslimia 10.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/17 uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe amesema kuwa, kwa mkoa wa Dar es Salaam, utafiti huu utahusisha kaya zisizozidi 1,000  na Wananchi watakuwa na hiari ya kukubali kupima ambapo kwa wale watakaogundulika kuwa na maambukizi, watapata rufaa ya kwenda kupatiwa matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI hauhusishi watu wote bali ni kaya chache tu ambazo zimechaguliwa kitaalam ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine na kwa hapa Dar es Salaam kaya zilizochaguliwa hazizidi 1000", amesema Dkt. Magembe.

Utafiti wa aina hii ni wa mara ya nne (4) kufanyika nchini Tanzania ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili mwaka 2007 na wa tatu mwaka 2011.

Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 /17 unafanyika nchini, chini ya usimamizi wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)  na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

TEMESA Yaunda Kikosi Kazi Kufuatilia Deni La Tsh Bilioni 10 Kutoka Taasisi Za Umma

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar Es Salama.

WAKALA wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imeunda kikosi kazi maalumu kitakachohusika na zoezi la ukusanyaji wa madeni ya kiasi cha Tsh Bilioni 10 inazodai TEMESA katika taasisi za Serikali.

Hadi kufikia mwezi machi mwaka huu TEMESA imekusanya kiasi cha Tsh milioni 157 inazodai kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari- MAELEZO na kurushwa hewani na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC).

Dkt Mgwatu alisema kuwa TEMESA ina jukumu la kutoa huduma za kiuhandisi kwa Taasisi za Umma na watu binafsi ikiwemo uzalishaji na utengenezaji magari pamoja na uboreshaji mitambo na huduma za vivuko na huduma za ushauri na uendeshaji.

“TEMESA imekuwa ikiongeza vivuko kulingana na mahitaji ya huduma hivyo ina mpango wa kuongeza kivuko kimoja katika eneo la Kigamboni na kufanya vivuko kuwa vitatu vitakavyofanyakazi saa 24 kwa lengo la kurahisisha huduma ya usafishaji” alifafanua Dkt. Mgwatu.

Aidha alisema kuwa katika mwaka wa Fedha 2017/2018 TEMESA imepanga kuboresha zaidi matumizi ya TEHAMA kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi ndani ya TEMESA na kuboresha huduma ili kuwavutia taasisi na watu binafsi kupata huduma za taasisi hiyo.

Vilevile Dkt. Mgwatu aliongeza kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka 2017 TEMESA imepanga kupunguza gharama za tozo za utengenezaji wa magari kwa taasisi za umma na watu binafsi.

Mbali na hayo Wakala wa Ufundi na Umeme nchini kwa mwaka 2016/2017 imeweza kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa iliyokamilika ndani ya muda uliopangwa ambapo imeshiriki pia katika ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA 10 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira, na Walemavu Jenista Mhagama.
 Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC), Balozi John Kijazi akitoa utambulisho wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwenyekiti Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Dkt. Reginald Mengi wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa.
 Rais wa Taasisi ya Wakuu wa Makampuni CEO Round Table Ally Mfuruki akisalimiana na Mwenyetiki wa Taasisi za Kibenki ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Benno Ndulu wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) Mhandisi Raymond Mbilinyi (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandisi, Mussa Iyombe akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospether Muhongo (katikati), Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (kushoto).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo
Mei 6, 2017 tayari kwa kuendesha mkutano wa 10 wa Baraza hilo. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na kushoto kwa Rais ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma muhtasari wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam 
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi akisoma hotuba yake wakati wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es
salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
akifafanua masuala kadhaa ya wizara yake wakati wa mkutano wa 10 wa Baraza hilo ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akufuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.
Jenista Mhagama 
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto kwake ni Waziri  
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Rais Dkt John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, 
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika mkutano wa 10 wa Baraza hilo ukumbi wa mikutano wa Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akufuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika mkutano wa 10 wa Baraza hilo ukumbi wa mikutano wa Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akufuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika mkutano wa 10 wa Baraza hilo ukumbi wa mikutano wa Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akufuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama akiongea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika mkutano wa 10 wa Baraza hilo ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akufuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama

NEC YATOA UFAFANUZI UTARATIBU WA KUMPATA MBUNGE NA DIWANI VITI MAALUM.

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika  Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.

Amesema  kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura ambazo chama husika kimepata. 

Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya wanachama wanaopendekezwa kuwa wagombea wa Viti Maalum ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Amesema kuwa  Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015,  ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa  liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na sifa zilizoainishwa kwa mujibu wa Sheria.

ZIARA YA BULEMBO KUKAGUA MCHAKATO WA UCHAGUZI CCM MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, katika Ofisi ya CCM mkoa huo, mwanzoni mwa ziara yake, kukagua uhai wa chama na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa CCM. Waliokaa kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa  huo, Lugano Mwafongo
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaji Abdallah Bulembo akiwasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Jumuia hiyo leo. Anayemkaribusha ni Mjumbe wa NEC, Ramesh Patel.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akisalimia baadhi ya wanachama wa CCM nje ya Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala baada ya kuwasili kweye ofisi hiyo, leo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akipokea saluti ya Kijana wa CCM alipowasili ofisi ya CCM wilaya ya Ilala jana akiwa katika ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa skafu na kijana wa CCM alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala kufanya ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia  ya Wazazi alhaj Abdallah Bulembo akisalimia wana CCM
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Buulembo akimsalimia Mbunge wa zamani wa Ukonga, Paul Rupia nje ya Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala alipowasili kwenye ofisi hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM wilaya ya Ilala, baada ya kuwasili kuanza ziara hiyo. Kulia ni Mjumbe wa NEC Ramesh Patel
Baadhi ya viongozi wa CCM kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi waliofuatana na Bulembo kwenye ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj abdallah Bulembo akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye ukumbi kilikofanyika kikao cha viongozi wa Jumuia hiyo, Tabata jana.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini, Tabata
Ukumbi ukilipuka kwa nyimbo za mapokezi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo alipingia ukumbini
Mwenyekiti wa Jumuiaya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili meza kuu tayari kuendesha kikao. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mjumbe wa NEC, Ramesh Patel ambaye anajiita Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Daes Salaam, Lugano Mwafongo (kushoto)  akiwa na viongozi wengine kwenye kikao hicho cha Tabata
Wanachama wa CCM ambao ni kutoka Jumuia ya Wazazi wakishangilia wakati wa kikao hicho
Baadhi ya viongozi kutoka makao makuu ya jumuia ya Wazazi wakiwa ukumbini
Katibu wa Jumuia ya wazazi Wilaya ya Ilala Sophia Hamad akisalimia
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Ilala, Anastazia Mongi akisalimia
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiteta jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe ukumbini
Katibu wa CCM wilaya ya Ilala akikabidhi taarifa ya mchakato wa uchaguzi katika maeneombalimbali wilayani humo kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akizungumza maneno ya utangulizi kwenye kikao hicho
Wanachama wakiwa ukumbini
Ofisa wa CCM kutoka MakaoMakuu ya Jumuia ya Wazazi Ndugu Kalolo akisalimia
Mjumbe wa NEC Ndugu Ramesh Patel akizungumza kumkaribisha Bulembo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mAlhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa Jumuia ya Wazazi kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mAlhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa Jumuia ya Wazazi kwenye kikao hicho
Katibu wa UVCCM Kata ya Liwili, Ilala Mariam Issa na Katibu wa UVCCM jimbo la  Segerea wakifurahi ukumbini wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akimtambulisha mbunge wa Segerea Bona Kalua kwenye mkutano huo
Mwenyekii wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akisoma taratibu za uchaguzi ndani ya CCM wakati wa kikao hicho PICHA ZOTE NA CCM BLOG

WANAFUNZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KARATU LEO

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii  inaeleza kuwa leo saa tatu asubuhi imetokea ajali katika eneo la Rhotia Wilaya ya  Karatu Mkoani Arusha, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza mwelekeo na kupindukia korongoni wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani ya ujiranimwema na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya mjini Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha,  Afande Charles Mkumbo, wanafunzi 32 , walimu 2 na dereva wa gari hilo wamepoteza maisha huku wanafunzi  wengine 4 na mtu mzima mmoja  wakiwa wamejeruhiwa.

Chanzo cha ajali hiyo mbaya kutokea mkoani humo bado haijajulikana na uchunguzi unaendelea. Globu ya Jamii inatoa rambirambi kwa wafiwa na kuwatakia majeruhi nafuu ya haraka. 
Zoezi la uokoaji likiendelea.

 Umati wananchi ukiwa katika nje ya chumba cha maiti cha hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kutambua miili ya wanafunzi na wanafunzi waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
 Umati wananchi ukiwa katika nje ya chumba cha maiti cha hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kutambua miili ya wanafunzi na wanafunzi waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

YANGA YAJIKITA KILELENI, YAJIPIGIA TANZANIA PRISONS 2-0

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mashiuya (kulia), akichuana na beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail. (Picha na Francis Dande). 

 Kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, akipata huduma ya kwanza baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. 


Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mashiuya (kulia), akichuana na beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. 
Beki wa Yanga, Vincent Bossou akimtoka kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Obrey Chirwa.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya wananfunzi, Walimu na Dereva Arusha

ATCL KUPATA NDEGE MPYA JULAI MWAKA HUU-NGONYANI

$
0
0
Na Tiganya Vincent,RAS-Tabora.

Serikali imesema kuwa mwezi Julai mwaka huu (2017)itanunua ndege nyingine mpya aina ya Dash 8-Q 400 kwa ajili kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania ili  liliweze kutoa kutoa huduma za usafiri wa anga katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo itaiweza ATCL kufikisha ndege nne (4) ambapo itaiwezesha kuongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na  miji ya nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi , Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Safiri za Ndege za Shirika la ATCL mkoani Tabora.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia Julai mwakani (2018)Shirika la Ndege hapa nchini linakuwa na uwezo wa kumiliki Ndege sita zenye uwezo wa kubeba abira kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri mikoa mingi hapa nchi na nje ya Tanzania.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa hadi hivi sasa , serikali imeshanunua ndege mbili  aina ya Bombardier Dash 8-Q400  zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.

Alisema kuwa hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya  Bombardier Dash 8-Q400  ambayo itakuwa na uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132 kila moja na Boeing 787 (Dreanliner ) itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 262.
Aidha ,Mhe. Ngonyani alisema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha inaimarisha viwanja vya ndege kwa kukarabati miundombinu na kuboresha mifumo mbalimbali ya huduma za usafiri wa anga.
Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sanjari uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa  nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa.
Mhe. Ngonyani alisema kuwa Serikali kupitia Shirika lake imekusudia kuhakikisha kuwa mikoa yote hapa nchini inaunganisha na usafiri wa anga.

Alitoa wito kwa kwa wananchi kutumia usafiri wa anga hasa wa Shirika hilo kama huduma ya kawaida na ya kuongeza fursa ya kibiashara kwa ajili kuimarisha kipato kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

Mhe. Ngonyani aliwaomba wakazi wa Tabora na maeneo mengine hapa nchini kutumia huduma za usafiri wa anga katika kutanua wigo wa biashara zao na kuhamasisha utalii na kuimarisa sekta ya kilimo cha kisasa hapa nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho alisema kuwa Shirika la Ndege hapa nchini linatoa huduma nafuu ukilinganisha na mashirika mengine yanayotoa huduma hiyo hapa nchini.

Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia usafiri huo na kutokuwa wa watu wachache kama yalivyo mashirika mengine hapa nchini.

Dkt. Chamuriho alisema kuwa Shirika hilo linatoza gharama nafuu ukilinganisha na Kampuni nyingine zinazotoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.

Alisema kuwa hivi sasa kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 330,000/- na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 250,000/-.

Dkt. Chamuriho aliongeza kuwa safari ya kwenda na kurudi kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 499,000/- na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 380,000/-

Nao wabunge wa Mkoa wa Tabora na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemshuru Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahidi yake kwa vitendo kwa kuanza kiliimarisha upya Sherika la Ndege hapa nchini.

Waliomba Serikali kupitia Shirika la ATCL kuendelea kupunza nauli za usafiri wa ndege ili wananchi wengi waweze kutumia usafiri wa anga hasa kupitia Shirika lao.
Wamesema kuwa haitakuwa na maana kama nauli zitakuwa juu na wananchi kuona usafiri wa anga ni watu matajiri tu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wawekeza popote ndani na nje ya nchi kwenda mkoani humo kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo kufuatia kuimarika kwa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, barabara na mawasiliano ya simu.

Alisema kuwa Tabora inayoa ardhi nzuri inayokubali ufugaji na ukilima wa mazao mbalimbali kama vile tumbaku, mahindi, alizeti mbunga, karanga miazi, mihogo na mengine mengine hatu inayowezo kuwawezesha kufunga viwanda vidogo na vikubwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya safari za ndege za Shirika hilo mkoani Tabora zitakuwa Jumatau, Jumatano Ijumaa na Jumapili.

JPM AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUJITATHMINI

$
0
0
   Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujitathmini, kurekebisha makosa yao pamoja na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali badala ya kuilalamikia kuwa haiwasaidii.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo wakati akiongea na wafanyabiashara wa sekta binafsi katika mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema kuwa tenda mbalimbali za ujenzi wa miundombinu zimekuwa zikitolewa na Serikali mara kwa mara lakini wakandarasi nchini wamekuwa hawazitumii fursa hizo na matokeo yake zinatolewa kwa wakandarasi kutoka nchi zingine.

“Serikali inatangaza tenda nyingi za ujenzi wa miundombinu na kwa kiasi kikubwa huwa inawalenga wakandarasi wa ndani kuliko wanaotoka nje lakini wakandarasi wetu wamekuwa hawazitumii fursa hizo, Serikali itachoka kuwabeba hivyo wakae wajitathmini,” alisema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa wakandarasi wanatakiwa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kupata tenda zinazotolewa na Serikali kwa urahisi pia amewataka wawe wazalendo katika upangaji wa bei za kazi zao.

Akitoa mfano wa kukosa uzalendo, Rais Magufuli amesema kuwa wakandarasi wa hapa nchini walipoombwa kutoa bei za ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walitaja kiasi cha shilingi kati ya bilioni 150 na 200 wakati Wakala wa Majengo (TBA) waliyajenga kwa bilioni kumi tu.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wafanyabiashara wa sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda na kuwahakikishia kuwa Serikali iko pamoja nao katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa taasisi zinazohusika na huduma za bandari zikiwemo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuanza kutoa huduma zao kwa saa 24.

“Tumeamua kufanya hivyo ili kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara kwani wamekua wakipata shida kwa kutumia muda mrefu kupata huduma katika bandari yetu, nafikiri njia hiyo itachochea wafanyabiashara kuwekeza zaidi”, alisema Mhe. Majaliwa

Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo kwani maendeleo ya ujenzi wa viwanda unategemea malighafi zinazotokana na kilimo.

Aidha Majaliwa alisema Serikali imekusudia kupanua wigo katika sekta ya kilimo kwa kuleta zana bora za kilimo, kuendelea kupunguza kodi katika mazao pamoja kuiwezesha Benki ya Kilimo kuendelea kutoa mikopo kwa wingi.

Nae, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Dkt. Reginald Mengi ameipongeza Serikali kwa kutekeleza ahadi mbalimbali walizojiwekea zikiwezo za elimu bure, ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa ndege pamoja na kukaa na wananchi na wadau mbalimbali kusikiliza na kutatua changamoto zao.

“Ushiriki wa wadau kwenye kikao hiki ni muendelezo chanya wa mahusiano mazuri kati ya Serikali na sekta binafsi, ninaamini majadiliano haya yatatatua changamoto za wafanyabiashara wa sekta binafsi”,alisema Dkt. Mengi.

BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA

$
0
0
Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo
Mjane wa marehemu na mtoto wao (katikati), akisaidiwa na dada yake aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia kuingia katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili huo.


Jeneza likiingizwa kanisani.


Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili huo.
Wanahabari wa Sahara Media alikokuwa akifanya kazi marehemu katika Kituo cha Televisheni cha Star TV na ndugu jamaa wa marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo. 
Wanahabari wakiandika wasifu wa marehemu Revocatus Bulizya.
Wanahabari Kibwana Dachi (kulia) na Ben Mwanantala 
wakiwa kwenye ibada hiyo.
Katekista wa Parokia ya Muhimbili akiongoza ibada hiyo.
Ni huzuni katika ibada hiyo.

Na Dotto Mwaibale

VILIO na majonzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari Revocatus Bulizya wa Kituo cha Televisheni cha Star TV wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam leo asubuhi.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali akiwepo aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia ambaye ni ndugu ya mke wa Bulizya.

Akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo Katekista wa Paroko ya Kanisa Katoliki MNH, alisema ni wakati wa kila mmoja wetu kutafakari juu ya maisha yake ya kimungu.

Alisema hakuna njia ya kukutana na mungu bila ya kifo na ndio maana wakati wote tunatakiwa kujiandaa kwa sababu hatui ni lina tutatoweka duniani kama alivyotuacha ndugu yetu Revocatus Bulizya.

Recocatus Bulizya alzaliwa tarehe 29-10-1979 na kufariki dunia tarehe 2-5-2017 kwa kugongwa na pikipiki 'bodaboda' maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam wakati akirejea nyumbani kwake akiwa ameongoza na mke wake.

Mazishi ya marehemu yamefanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa nje kidogo ya jijini Dar es Salaam na mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.


Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images