Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1217 | 1218 | (Page 1219) | 1220 | 1221 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Shamba la Wananchi lililoko katika wilaya ya Mbarali katika kata ya Kapunga ambalo limekuwa liktumia maji kwa muda wote bila ya kuyalipia chochote Serikalini lijulikanalo kama Mwashikamile lenye ukubwa wa ekari 800 limepewa ruhusa ya kufungua mfereji wa maji uliokuwa umefungwa baada ya Shamba hilo kulipa madeni yote ya maji na kulipa faini waliyopigwa na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha.

  Akiongea na Wananchi wa eneo hilo la mwashikamile Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko Bwana Richard Muyungi amewahimiza viongozi wa shamba hilo kuhakikisha hawaenedelei kuchepush mifereji ya maji bila kuyalipia na kutekeleza maagizo ya serikali ya kupata vibali vote halal vya matumizi ya maji na kilimo cha umwagilaji. Kikosi kazi kimewaruhusu Wananchi kuendelea na umwagiliaji wa maji katika mashamba yao ya Mpunga mpaka pale watakapovuna. 

  Bwana Muyungi alisisitiza kuwa hakuna wananchi wote wameruhusiwa kuendelea kutumia maji hadi kuhakikisha kuwa mazao yote mashambani yanavunwa la msingi ni kuea maji hayo wayalipie. Alsema wananchi katika mashamba memgi tayari wamekwishatoa michango ya kulipia maji lakini viongozi hawataki kulipia maji jambo ambalo haliwezi kuvumilika. 

  Aidha akiongea, Mwenyekiti wa eneo hilo la Mwashikamile Bwana Leonard Mwashikamile ameshukuru sana Kikosi kazi kwa kuwaruhusu tena kufungua mfereji wa maji na pia aliahidi kwa niaba ya Wananchi wa kijiji hicho kutunza maji yote yanayotumika kwa umwagiliaji na kuwa atahakikisha Wananchi hawachepushi maji ya wizi tena. 

  Shamba la Mwashikamile lilikuwa ni moja kati ya mashamba pamoja na skimu za umwagiliaji zilizopigwa faini na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha katokana na kuchepusha maji bila kuyalipia na bila kibali chochote..

  Pichani Wananchi wa Kijiji cha Mwasikamile ambao ni Wakulima wa mashamba ya mpunga ya Mwashikamile wakishirikiana kwa pamoja kufungua mfereji wa kupitishia maji ili kumwagilia mashamba yao baada ya kulipa faini waliyotozwa na Kikosi kazi cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha. 
  Mwenyekiti wa Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Bwna Richard Muyungi akiongea na Wakulima wa mashammba ya Mpunga ya Mwashikamile mara baada ya kuzuru shambani hapo.

  0 0


  Mkurugenzi wa 102.5 Lake FM, Doreen Estazia Noni akiiunua mfuko wa takataka na mtangazaji wa a kituo hicho Tatu Rajab wakati wa zoezi la kusafisha jiji la Mwanza lijulikanalo kwa jina la Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksi. Zoezi hilo litakuwa linafanyika mara kwa mara.
  Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. 
  Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
  Katibu wa wenyeviti wa mitaa jiji la Mwanza, Hamza Shido akishiriki katika kampeni hiyo ya 'Ng'arisha Nzengo' iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102​.
  Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
  Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishangilia mara baada ya kuhitimisha kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza ijulikanayo kwa jina la 'Ng'arisha Nzengo'.
   
   Kituo cha Redio cha 102.5 Lake FM kimezindua kampeni ya kufanya usafi kwa jijini la Mwanza ijulikanayo kwa jina la  Ng’arisha Nzengo, Uchafu Nuksi yenye lengo la kuufanya mji huo kuwa msafi zaidi.

  Mkurugenzi wa kituo hicho Doreen Estazia Noni amesema kuwa wameamua kuanzisha kampeni hiyo ya usafi ili kuupendezesha zaidi mji huo ambao ni minongoni mwa miji mikubwa hapa nchini.Doreen amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Lake Fm nikuhakikisha inatoa mianya ya kuiwezesha jamii kufikia kusudi la maendeleo binafsi na jamii nzima kwa ujumla.

  “Neno ni la kabila ya Wasukuma lenye maana ya nyumbani, tumeamua kutumia neon hili ili kufikisha ujumbe haraka kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kampeni hii ni  endelevu kituo chetu cha redio kitaendelea kuhamasisha mpaka kufikia lengo letu,” 

  “Kituo chetu cha redio kimeamua kupanua wigo wake kwa kujihusisha katika masuala mbalimabli ya kijamii na kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mtazamo chanya na si kuhabarisha na kuburudisha tu,   naomba ushirikiano mkubwa kwa wadau,  serikali na watu  binafsi katika kufanikisha kampeni hii,” alisema Doreen.

  Mbali ya 102.5 Lake FM, kampeni hiyo pia imewashirikisha wadau wengine kama Baamedas tv, Genic Studios , viongozi wa Jumuiya ya biashara ndogondogo, minada na masoko , mwenyekiti Justin Sagala, mwenyekiti wa Afya Minadani, Gosbert Lucas, katibu wa afya, Mariam Magembe, kiongozi wa wa madereva  wa daladala  Dede Petro, serikali na Asasi binafsi.

  Mkuu wa maudhui na vipindi  wa redio hiyo,  Yusuph Magupa ambaye pia ni mwenyekiti wa kampeni hiyo amesema kuwa  afya ni ghali na wakazi wa Mwanza wanapaswa kuishi katika mazingira salama ili kulinda afya yako.

  Kupitia uzinduzi wa kampeni hii iliyozinduliwa rasmi siku ya jumatatu ya Mei Mosi, katika kipindi cha asubuhi cha Kokoliko, Magupa amebainisha mpango mkakati wa kampeni hiyo kuwa nikuhakikisha elimu ya usafi kwa afya bora inaeleweka na kuzingatiwa katika jamii.

  Katibu wa kampeni hii, Iman Hezroni ambaye ni pia ni mtangazaji  wa redio hiyo amesema kuwa mbali ya wao, kampeni pia imewashirikisha wakazi wa Mwanza kwa asilimia kubwa ili kuzidi kujenga mahusihano mazuri baina ya kituo na wananchi.

  Hezron amesema 102.5 Lake Fm itahakikisha inatoa fursa kwa wanajamii kusikika na kueleza matakwa yao ili kutafuta mikakati ya matakwa yao kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa kituo redio hiyo ipo kwa ajili wananchi.

  Alisema kuwa  Mkurugenzi wa kampuni ya 102.5 Lake Fm  kwa sasa anafanya mazungumzo na  Jumuiya ya biashara ndogo ndogo, minada na masoko ambapo maazimio yaliyofikiwa ni kuijenga ziara maalum ya kuitembelea minada  yote ndani ya jiji la Mwanza, iliyopewa jina la Gulio la mtaa.

  Alifafanua kuwa dhamira ya ziara hiyo nikusogeza elimu ya usafi katika maeneo hayo,uboreshaji wa huduma ya vyoo minadani pamoja na maboresho ya kimiundombinu katika minada kupitia Gulio la mtaa lakini pia litatimiza zana ya kupeleka radio kwa wananzengo, kwa kuhakikisha inawaburudisha na muziki wa kisasa pamoja na ule wa asilia.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na Taasisi mbalimbali waliomsindikiza katika katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo. PICHA NA IKULU.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik wakati akielekea kupanda ndege katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.


  0 0

  Serikali ya Tanzania imejipanga kulinunulia Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ndege mpya sita aina ya BOMBARDIER na moja aina ya BOEING 787-8 DREAMLINERNER Ili kupanua wigo wa utoaji huduma kwa mikoa yote ya Tanzania pamoja nan chi jirani na Tanzania.

  0 0

  George Binagi-GB Pazzo
  Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.

  Akizungumza jana wakati wa zoezi hilo, Machemba alisema uamuzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani na kwamba hatua hiyo pia itasaidia kuondoa hatari za kimazingira ikiwemo magonjwa kituoni hapo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Kituo cha Afya Buzuruga, Daniel Buluya, alisema awali mazingira ya Kituo hicho hayakuwa salama hatua ambayo ilikuwa inahatarisha usalama wa wagonjwa na watumishi wa afya kituoni hapo.

  Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei Mosi ili kutoa mwanya wkwa wafanyakazi pamoja na viongozi mbalimbali kutafakari changamaoto zinazowakabiri wafanyakazi na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Moshi mkoani Kilimanjaro huku kauli mbiu ikiwa ni "Katiba na Utawala, Vizingatie Haki na Maslahi ya Wafanyakazi".
  Tazama Video hapo chini.

  0 0

  Na Dkt Hassan Abbasi

  Mei 3, 2017 Wanahabari hapa nchini wanaungana na wanahabari wenzao kote duniani kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Nikiwa mwanataaluma hii, kwanza nawapongeza wanatasnia wenzangu kwa kuadhimisha siku hii mujarabu.

  Pili, ni matarajio yangu kuwa wanahabari hasa wa nchini, pamoja na kupiga kelele kuhusu maslahi na haki zao kama ilivyo kawaida, safari hii watatitumia siku hii kujitazama upya namna wanavyotekeleza wajibu wao kwa jamii.

  Hata kauli mbiu ya waasisi wa siku hii inadhihirisha hoja na haja hii ya kujitazama upya. Kaulimbiu ya mwaka huu iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inasomeka: “Critical Minds for Critical Times: Media’s role in advancing peaceful, just and inclusive societies.” 
  Kauli mbiu hii, kwa mtazamo wangu, na hata uchambuzi wa wanahabari wengi nguli duniani, kwa kifupi inalenga sana kusisitizia umuhimu wa kuwa na wanahabari wenye akili (critical minds).

  Lakini si wenye akili tu kwa kuwa na uwezo wa kuchambua habari na kufuata misingi ya taaluma yao, sehemu ya pili ya kauli mbiu inachagiza hoja ya wajibu wa wanahabari kwa jamii hasa katika mawanda ya amani na maendeleo ya jamii (Media’s role in advancing peaceful, just and inclusive societies).”

  Nawapongeza UNESCO kwa kuja na mada hii aushi kabisa inayosadifu kile ambacho wengi tumekuwa tukijiuliza: Je, licha ya kulalamikia uhuru na haki zao, vyombo vya habari vya leo vinatimiza wajibu wao kwa umma? 

  Je, vimekuwa sehemu ya kuchagiza maendeleo au kuendekeza siasa za kuzuia maendeleo ya watu? Vinafanya nini kuchangia jamii yenye maendeleo endelevu?

  Ni mtazamo wangu, wa wanahabari wengi nguli duniani na hata wananchi wa kawaida kuwa tukijaribu kutafuta majawabu ya maswali haya tutapata majibu yenye kupishana sana. Yapo maeneo lazima tuwapongeze wanahabari, wameitumia na kuitumikia vyema tasnia lakini pia yapo maeneo tumetetereka sana. 

  Ndio maana, akiichambua kaulimbiu ya mwaka huu, mwandishi nguli wa gazeti la New York Times, Jim Rutenberg, anabaisha kuwa moja ya changamoto inayowahitaji wanahabari kujitafakari  mwaka huu ni kuibuka kwa habari zisizofuata maadili wala kujali ukweli, akirejea dhana mpya katika taaluma ijulikanayo kama “fake news.”

  Anasema ni wakati sasa wanahabari kujitathmini na kurejea katika uandishi wa kweli na mahiri wa habari akisisitizia: “Na wakifanya hivyo, watakuwa wamefanya uandishi wa habari wa kweli na utakaoiokoa taaluma ya habari (good journalism that saves journalism.”

  Niseme tu nikiwa nimepata fursa ya kuwa mwanahabari kwa muongo mmoja hivi na sasa nikielekea katika muongo mwingine wa kuwa katika upande wa pili wa habari-mtoa habari na msimamizi wa sekta ya habari, nimeshuhudia mengi yanayojuzu wanahabari tujikosoe na kujisahihisha.

  Kwa kuwa leo tunajikosoa ili kujisahihisha yale mazuri mengi tunayoyafanya tuyaweke pembeni. Tuangalie wapi tunapaswa kuboresha. Tujikite katika changamoto zetu na tunatokaje hadi kurejea kuwa “critical minds.”

  Katika makala haya na siku hii ningeweza kuanisha jinsi uandishi wetu unavyokiuka misingi ya uandishi wa habari, jinsi leo tulivyo na waandishi wasiohoji wala wasioenzi misingi adhimu ya taaluma. Lakini nimeona kubwa zaidi, walau kwa uzoefu wangu mpaka sasa, ni moja.

  Nalo ni ugonjwa unaoenea kwa wanahabari wengi kutoelewa vyema au kuamua kufumbia macho misingi ya nadharia kuu za kifikra zinazoongoza taaluma yenyewe, nadharia mbili ambazo ni ile ya uhuru wa kujieleza (freedom of expression) na uhuru wa wanahabari (press freedom theory).

  Tatizo kubwa na matatizo mengi yua kimaadili katika sekta ya habari na dhana ya “fake news” vinaanzia hapo. Kumeibuka aina ya waandishi wanaoamini kuwa wanaweza kuandika chochote, wakati wowote na juu ya yeyote na kwa namna yoyote ile bila kujali haki na staha za wengine.

  Ni kwa sababu ya mitazamo kama hii basi unakutana na waandishi kama Nyamnjoh (2005) katika tasnifu yake “Africa’s Media, Democracy and the Politics of Belonging,” wakilalamikia kushamiri kwa uandishi wa kuchochea ukabila, udini, itikadi za kisiasa au kutetea waovu kwa sababu za kinasaba. 

  Ni kwa sababu pia ya uandishi wa habari kuonekana ni fani ya mtu anayeitamani tu basi kuingia na kuanza kuandika chochote na atakavyo ndio maana waandishi kama Lawrence Kilimwiko katika andishi lake “Media Power and Politics in Tanzania: Critical Analysis of Media Trends and Practice” analalamikia uandishi wa kuzusha tu habari na kupaka matope watu.

  Huu ulevi unaochangiwa pia na wanaharakati na waandishi wenyewe wasioelewa kwa kina haki na wajibu wa kazi na taaluma yao na kuona kwamba uhuru wao haupaswi kuhojiwa wala kudhibitiwa (vinginevyo ni kuingilia uhuru wa habari).

  Dhana hii haina mantiki na naomba leo, tukiwa tunatafakari “critical minds” katika taaluma hii, tukumbushane ukweli kwamba iwe ni fani au taaluma kamili, uandishi wa habari haujawahi kuwa jambo huru la mtu kuandika anachotaka bila kujali misingi iliyowekwa. 

  Kutoka wanafalsafa wa kale kama Plato, wanamageuzi na watetezi wa uhuru wa kujieleza kama John Stuart Mill hadi wanasiasa watetezi wa uhuru wa habari kama Thomas Jefferson na Mahatima Gandhi, wote hawa wanasema uandishi wa habari wa “fake news” haufai. Tusikilize nasaha zao. 

                               Wanafalsafa na Uhuru wa Kujieleza 

  Inafahamika kuwa wanafalsafa wa kale ni miongoni mwa waasisi wa haki mbalimbali za kiraia, kisiasa na kijamii na kwamba wanakubalika kuwa waasisi pia wa uhuru wa kujieleza. 

  Katika kujenga hoja yangu kwamba uhuru wa habari una ukomo, nitawatumia wanafasalafa wawili; mmoja wa zama za kale zaidi (ancient philosopher) na mmoja wa zama za hivi karibuni za kimageuzi (enlightenment philosopher).  

  Tuanze na mwanafalsafa wa kale, Plato, ambaye anajulikana sana katika ulimwengu wa kujenga hoja. Ingawa baadhi ya wasomi wanasema Plato hakuchukua sana muda wake kuainisha masuala ya uhuru wa mawazo lakini yapo matukio au maeneo ambapo Plato aligusia hili.

  Katika kitabu chake maarufu kiitwacho “Republica,” ambapo amesisitiza hoja na haja ya kusema ukweli lakini pia kutoeneza uongo na chuki kwa kiwango cha kuiharibu jamii, Plato anaandika bayana kuwa wanaoeneza uongo (of liar poets and storytellers) lazima wazuiwe kufanya hivyo. 

  Kutoka zama za kale tunaweza pia kujifunza kitu katika zama za mageuzi ya kifikra katika karne ya 19 (enlightenment period). Hapa tunakutana na mwanafalsafa anayekubalika duniani kuwa “Baba wa Uhuru wa Habari/Kujieleza” Mwingereza John Stuart Mill.

  Mill (1806-1873) atakumbukwa kwa kueleza nadharia mbalimbali za kusisitizia uhuru wa mawazo na wa vyombo vya habari kuwa lazima uwepo ili kusaidia katika kukuza demokrasia na moja ya nukuu yake mashuhuri ya kutetea haki hizi inasema:

  “If all mankind minus one were of one opinion, and only one person was of the contrary opinion, mankind would be no more justified in silencing that one person, than he, if he had the power, would be justified in silencing mankind.”

  Akimaanisha kuwa hata kama wanadamu wote wangekuwa na mtazamo kuhusu jambo fulani lakini mmoja wao akawa na mawazo tofauti, dunia nzima haipaswi kumnyamazisha huyo mmoja, na kama ingewezekana, basi ni huyo mtu mmoja ndiye angepaswa kuinyamazisha dunia! 

  Lakini pamoja na kupigania kwake huko haki na uhuru wa habari na mawazo, Mill kwa upande wake amepata kukiri kuwa uhuru huo una mipaka na kwamba mtu hawezi tu kukurupuka na kuongea/kuandika hata yanayowadhuru wengine. 

  Akiandika katika fasihi yake mashuhuri duniani “On Liberty” anasema: “The only freedom which deserves the name is that of pursuing our own good in our own way, so long as we do not attempt to deprive others of theirs, or impede their efforts to obtain it.” 

  Kwamba uhuru kamili wa kujieleza utakuwa hivyo iwapo tu haudhuru haki za watu wengine na wala hautawazuia watu wengine kufurahia haki zao. Huu ni msisitizo kuwa uhuru wa habari una ukomo. 

                                Wanafalsafa wa Kisiasa

  Nimeona pia katika muktadha huu tuangalie jinsi wanasiasa mashuhuri duniani ambao pia wanakubalika kuwa sawa na wanafalsafa nao walivyoainisha kuhusu uhuru wa habari na mipaka yake. 

  Nianze na mmoja wa waasisi wa Taifa la Marekani, Thomas Jefferson.Kwa wasiomfahamu kiongozi huyu, basi mintaarafu tu, ndiye kiongozi wa kisiasa, kwa mapenzi yake katika uhuru wa watu na wa habari, alipata kunukiliwa akisema angetamani vyombo vya habari viwepo lakini serikali isiwepo.

  Jefferson aliyaeleza mapenzi yake hayo makubwa namna hiyo juu ya uhuru wa kujieleza na habari katika barua yake ya Januari 16, 1789 kwenda kwa rafiki yake kipenzi Kanali Edward Carrington, akiandika:

  "The basis of our government being the opinion of the people, the very first object should be to keep that right; and where it left to me to decide whether we should have government without newspapers, or newspapers without a government, I should not hesitate a moment to prefer the latter."

  Hata hivyo, naye pamoja na mapenzi yake hayo yasiyomithilika, kama wanafalsafa wengine, aliamini kuwa uhuru huo una mipaka. 

  Katika barua yake kwenda kwa rafiki yake mwingine mkubwa, James Madison, wakati wa mjadala nchini Marekani kuhusu haki za kiraia, Jefferson alitaja mambo yanayoweza kuwa kizuizi cha uhuru wa habari kuwa ni pamoja na: 

  “Matendo yanayoweza kusababisha madhara kwa uhai wa mtu, uhuru wao kwa ujumla, mali zao au kushambulia heshima ya mtu au kuharibu amani na utulivu na ushirikiano wetu wa mataifa.”

  Mbali ya Jefferson, Mahatma Gandhi anafahamika kuwa mpigania uhuru wa aina yake na Baba wa Taifa la India. Anakumbukwa kwa namna alivyotoka kuwa mwanahabari hodari, mwanasheria hodari na kisha kuwa mpigania uhuru hodari akitumia falsafa yake ya kutotumia nguvu. 

  Pamoja na ukweli huo Gandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza na kwamba taaluma ya habari ikiwa fani adhimu lazima watu wake wajue kuwa kalamu isiyotumika kwa umakini haijengi bali hubomoa. Aliandika: 

  “Freedom of the press is a precious privilege that no country can forego….The sole aim of journalism should be service…even so an uncontrolled pen serves but to destroy.”

  Ningeweza kuendelea kuwataja wanamageuzi ya kisiasa na wengineo walioweka misingi mizuri kuhusu wajibu wa wanahabari lakini yatosha tu kwa leo kuhitimisha kwa kutaja mtazamo wa kimataifa kuhusu dhana hii.

  Jumuiya ya kimataifa nayo katika kupambana na “fake news” hasa baada ya matukio ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia iliweka misingi ya kisheria katika kupambana na tatizo hili. 

  Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Kiraia (1966) inashadidisha uhuru wa habari lakini pia inataja masuala makubwa manne ambayo ni ukomo wa haki ya kujieleza/habari.

  Masuala yanahusu kukiuka misingi ya amani, usalama wa nchi, afya ya umma, haki ya faragha na haki ya mtu kutovunjiwa heshima yake yameainishwa. 

  Ndio maana katika mataifa yote, hata tunayoyaona kuwa yamestaarabika zaidi, watu wamepata kufikishwa mahakamani kwa kukiuka haki hizi na wapo wanaosakwa mpaka sasa na mifano ya akina Julian Paul Assange wa WikiLeaks na Edward Joseph Snowden inatosha katika hili.  

  Ni kwa hoja hizi basi nihitimishe kwamba taaluma ya habari ni adhimu na adimu sana lakini tuitendee haki kwa kutimiza wajibu wetu huku tukienzi misingi ya ukomo unaolenga kulinda haki za wengine.

  Kwa Tanzania tutimize wajibu wetu kama “critical minds” na pia tutimize wajibu wetu katika kuifanya kalamu yetu kuchangia katika maendeleo ya Taifa hususani wakati huu Serikali yetu ya Tanzania ambapo imetunga sheria muhimu sana; Sheria ya Huduma za Habari Na. 12, 2016 inayosisitizia kwa kina haya niliyoyaeleza.

  Nawatakia maadhimisho mema na tafakuri njema. 

  *Mwandishi wa makala haya ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO. Anapatikana kwa baruapepe: mih@habari.go.tz.

  0 0

  Na Husna Saidi & Nuru Juma- MAELEZO

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kushughulikia suala la huduma za afya bure kwa watu wenye ulemavu.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla kwa niaba ya Waziri Ummy Mwalimu.

  Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa Alex aliyetaka kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, Dkt. Kigwangalla alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kutoa huduma za afya bure kwa makundi maalum likiwemo watu wenye ulemavu.

  “Dhumuni la Sera ya Afya ya mwaka 2007 ni kuwezesha watu wenye ulemavu wazingatiwe katika makundi maalum ya watu wanaostahili msamaha utolewao kwa kuzingatia endapo mlemavu huyo hana uwezo wa kulipia huduma hiyo au awe katika makundi maalum ili kupata huduma bora za afya kama ilivyo kwa watu wengine,” alisisitiza Dkt.Kigwangalla.

   Sera hiyo imeainisha makundi maalum yanayostahili kupata msamaha wa huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma kuwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 60, watoto chini ya miaka mitano,watoto waishio katika mazingira hatarishi, wajawazito na watu wasiojiweza kiuchumi.

   Aliongeza kuwa watu wengine ambao wapo kwenye makundi maalumu ni  wenye magonjwa sugu kama  Kifua kikuu, Ukimwi, Kisukari, Magonjwa ya Moyo, Pumu, Sikoseli, Ukoma, Saratani na Magonjwa ya Akili.

  Aidha alisema kuwa katika kuweka uwiano sawa kwa Watanzania wote bila ubaguzi  Serikali ya awamu ya tano ina pendekezo la kutoa bima ya afya ya lazima kwa watu wote ambapo utasaidia pia kwa watu wenye msamaha kupata huduma bora.

  Kama Serikali itapitisha pendekezo la kutoa bima ya afya ya lazima kwa Watanzania wote litasaidia upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

  0 0

  Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akiwasilisha mada kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3. Mkurugenzi wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini 'TMF', Ernest Sungura akiwasilisha mada kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai akichangia mada katika mkutano huo. Mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group, Antony Diallo akichangia hoja kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3 linashirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Mh.Rashidi Shangazi mbunge wa jimbo la Mlalo Wilaya ya Rushoto mkoani Tanga katikati ni Rauph Mohamedi mtangazaji wa Ruvuma TV na wa mwisho aliyeshika mic yenye nembo ya Ruvuma Tv ni Mh.Joseph Mhagama mbunge wa jimbo la Madaba mkoani Ruvuma.

   Mbunge wa Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma Mhe.Joseph Mhagama azungumzia mambo manne ambayo anapambana nayo kwa sasa katika jimbo lake katika kuhakikisha anawalete maendeleo wananchi wa jimbo hilo, Kwa undani wa habari hii, hii hapa video yake.

  0 0
 • 05/02/17--05:35: TAHADHARI YA UTAPELI

 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiswasili Uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam  baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam  na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.


  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni , Stephen Katemba amesema kiwanda cha Lake Cement kinafuata sheria za utunzaji wa mazingira kwa wananchi wa Kimbiji. 

  Katemba amesema hayo wakati alipokwenda kusherekea siku ya wafanyakazi na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanywa na Lake Cement, amesema kuwa kiwanda kwa kufuata sheria ya mazingira na sheria za wafanyakazi kamwe migogoro haiwezi kutokea. 

  Amesema kuwa wafanyakazi lazima wafanye kazi kwa kujituma ili kiwanda kiweze kujiendesha katika kuweza kufikia malengo ya kutimiza kwa wafanyakazi wake. 

  Katemba amesema wakati kitendo cha Kiwanda kudhamini mashindano mbalimbali katika eneo la kimbiji ni kuonyesha kiwanda kinajua wajibu wake. 

  Makamu wa Rais wa Lake Cement , Afroz Ansary amesema wanawajibu wa kuwa karibu na jamii ya Kimbiji katika shughuli za kijamii . Mafanikio ya kiwanda yanatokana na jamii inayozunguka kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii. 

  Nae Afisa Utumishi wa Kiwanda hicho, Ahmed Mstapha amesema kuwa kiwanda cha Nyati Cement kinatekeleza majukumu yake kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho. 

  Amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na wananchi katika shughuli mbalimbali ambazo zinajitokeza katika eneo la Kimbiji.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akizungumza na wafanyakazi mara baada kutembelea kiwanda hicho katika siku ya wafanyakazi na kushiriki shughuli mbalimbali ikwemo ya upandaji jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utumishi wa Manispaa ya Kigamboni, Cosmas Hinju akizungumza wakati wa shughuli ya upandaji miti katika kiwanda cha Lake Cement jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Lake Cement, Afroz Ansary akizungumza juu ya udhamini wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.
  Meneja Rasilimali Watu wa Lake Cement, Julieth Domel akizungumza juu jinsi wanavyoshugulika na wafanyakazi wa kiwanda kwa kufuata sheria za Kazi. 
  Wananchi wakiangalia fainali ya Kata ya Kimbiji iliyodhaminiwa na Lake Cement jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA,  kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho Mhe. Dr. Elly Marko Macha aliyefariki tarehe 31 Machi 2017.

  Akitoa taarifa ya nafasi hiyo kuwa wazi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameijulisha Tume juu ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge huyo.

  Amesema taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, akizungumza hii leo kwenye Kongamano la Wanataaluma na Wadau wa Habari kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

  Kilele cha Maadhimisho hayo ni kesho Mei 03,2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
  Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura, akiwasilisha mada hii leo kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
   Mtaalamu wa masuala ya teknolojia nchini, Innocent Mungy, akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
  Mwanasheria na Mwanataaluma ya Habari, James Marenga, akichangia mada kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Sahara Media Group, Dkt.Antonny Diallo, akichangia mada kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini (Tanzania Bloggers Network TBN), Joachim Mushi, akichangia mada kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
  Mwanataaluma ya habari nchini, Flora Magabe, akichangia mada kwenye Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, linalofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
  Mmoja wa wanataaluma ya habari nchini, akichangia mada kwenye kongamano hilo
  Mwenyekiti wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari, akifuatilia kwa umakini kongamano hilo.
  Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akiwa kwenye kongamano hilo
  Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya Sahara Media Group, Dkt.Antonny Diallo (kulia), kwenye kongamano hilo.

  Wanataaluma na wadau wa habari wakiwa kwenye kongamano hilo
  Wanataaluma na wadau wa habari wakiwa kwenye kongamano hilo, ambapo kulia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Simon Berege.
  Afisa kutoka Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Hilda Kileo akiwa kwenye kongamano hilo.
  Wanataaluma na wadau wa habari wakiwa kwenye kongamano hilo.

  0 0

  Na Karama Kinyunko.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili umekamilika.

   Wakili wa Serikali, Onolina Moshi aliyaeleza hayo leo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

  Mheshimiwa, kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika naomba ahirisho kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH). Amesema Moshi.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo   hadi Juni Mosi,2017 kwa PH.

  Wema amewakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.

  Mbali na Wema washtakiwa  wengine ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima.Watuhumiwa hao wawili wanatetewa na wakili Peter Kibatala na Hekima Mwesigwa.

   Wema ambaye ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 alifikishwa mahakamani hapo na kupandishwa kizimbani baada ya kusota mahabusu katika kituo kikuu cha Polisi (Police Central ) Dar es Salaam kwa muda wa siku Sita.

  Awali ilidaiwa kuwa, Februari 4 mwaka huu, huko Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili.

  Hata hivyo washtakiwa hao wote walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana.

  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BAADA ya kusimama kwa kipindi cha takribani wiki tatu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.

  Kwa mujibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.

  Afisa habari wa Shiriukisho la Mpira wa Miguu Alfred Luacs amesema kuwa michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

  Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utaanza saa 1.00 usiku.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaarifiwa kuwa, amri ya kukamatwa kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya jamii Forums, ilitolewa na afisa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SSP Ramadhan Kindai.

  Kauli hiyo imetolewa na yeye mwenyewe SSP Kindai wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu Thomas Simba dhidi ya mkurugenzi mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo na Mwanahisa wa Kampuni hiyo, Mike William.

  Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai, alitoa amri hiyo baada ya washtakiwa kushindwa kutoa taarifa sahihi iliyochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums..

  Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum, Kindai amedai kuwa waliomba taarifa kutoka kwenye kampuni ya jamii Forums kutokana na kesi iliyofunguliwa na Afisa Msimamizi wa mauzo ya rejareja wa Oil Com, Usama Mohammed.

  Ameongeza kuwa Usama alifika kwenye ofisi yao na kulalamika kuwa Februari 13,2016 kuna habari ilichapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kwamba kampuni ya Oil Com wanakwepa kodi bandari ya Dar es Salaam na kwamba wanaiibia serikali.

  Amedai kuwa katika kufuatilia kupata ukweli, ASP Fatuma Kigondo aliingia kwenye mtandao huo kutafuta aliyechapisha taarifa hizo ambapo waligundua kuwa ni Fahara JF Expert member ndiye aliyechapisha taarifa hiyo.

  Kufuatia hayo, Februari 23, mwaka Jana Kigondo aliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Jamii forums ili awapatie taaarifa za mtu huyo ambapo walipokea barua toka Jamii Forums ikidai kuwa wanahaki ya kulinda faragha za wateja wao.

  Pia barua hiyo ilikuwa ikitaka kujua tunaomba taarifa hizo kwa kifungu kipi cha sheria na kwamba Majibu hayo hayakuwa chanya kwa kile walichokiomba.

  Aliongeza kuwa, waliandika tena barua Aprili Mosi, 2016 kuwakumbusha Jamii Forums kutoa taarifa walizoziomba sababu kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) Cha Sheria ya Mashauri ya Jinai (CPA) kinawapa mamlaka ya kuomba nyaraka kutoka katika ofisi yoyote na lakini hawakujibu.

  Amedai kuwa kutokana na hayo waliona wanakosa haki ya kuendelea na upelelezi, na kuwa wanawadhoofisha katika upelelezi wo ndipo wakaona wawakamate.

  Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho. 

  Melo na Mike wanadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka jana, huko Mikocheni wakiwa wakurugenzi wa Mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao unaendesha tovuti ya jamii forums wakijua jeshi la Polisi Tanzania linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yake kwa njia ya kuuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa taarifa alizonazo.

  0 0


  Fuatilia yaliyojiri kwenye Kongamano la Wanataaluma na Wadau wa Habari kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, lililofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

  Kilele cha Maadhimisho hayo ni kesho Mei 03,2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
  #BMGhabari

  Tazama hapa picha

  0 0

    Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Naibu Waziri  wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt,Ashatu Kijaji  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
    Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.Dkt Khamis Kigwangala akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Waziri  wa Nishati na Madini Mhe.Prof.Sospeter Muhongo  akitolea ufafanuzi  hatua  zilizochukuliwa na Serikali juu ya Tetemeko la ardhi lilitokea Mkoani Kagera ivi Karibuni katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Salma Kikwete na Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) Mhe. Hawa Ghasia  wakijadili jambo  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Waziri wa Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Upendo Peneza akiuliza swali katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
   Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM) Mhe.Peter Serukamba akizungumza jambo na Mbunge wa Nzega Mjini Mhe.Hussein Bashe katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
  Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Haki,Maadili na madaraka ya Bunge  Mhe.Almas Maige akisoma hoja za kamati hiyo kuhusu Shauri la kudharau Mamlaka ya Spika linalowahusu Mhe.Freeman Mbowe,Mhe Halima Mdee  na Mhe.Ester Bulaya na Shauri la kuingilia Uhuru  na Haki za Bunge linalowahusu Bw.Paul Makonda na Pastory Mnyeti katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.

  Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO,DODOMA

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi afisa wa usalama kutoka shirika la TANESCO Mkoa wa Singida Juma Mauba zawadi ya cheti na  TV flat screen baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora mwaka 2017.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa ameshikama na Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Singida Aaran Jumbe (kulia kwake) na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (kushoto kwake) wakiimba wimbo maalumu wa wafanyakazi wa Mshikamano daima pamoja na wimbo wa taifa.
   Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa Mkoa wa Singida.

   Watumishi wa Kutoka Halmashauri ya Ikungi wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na kuonyeshwa mazao ambayo huzalishwa kwa wingi wilayani humo ambayo ni viazi vitamu na alizeti katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa Mkoa kwa Mkoa wa Singida.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akitoa zawadi ya mpira kwa viongozi wa wafanyakazi wanawake kwa halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida ili waweze kuunda timu za wanawake katika halmashauri zao.

  Waajiri wote Mkoani Singida hususani wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wenye watumishi wengi wameelekezwa kujenga mahusiano mazuri baina yao ili kuboresha utumishi wao.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa maelekezo hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani hapa yaliyofanyika katika uwanja wa Peolpe’s mjini Singida.

  Dkt. Nchimbi amesema mwajiri na mtumishi sio maadui bali wanapaswa kujenga mahusiani mazuri hasa kwa mwajiri kujenga mazoea ya kufahamu sifa za watumishi wake, shida na matatizo yao.

  Ameongeza kuwa waajiri wamekuwa wakisubiria watumishi wakosee ndio wawape adhabu lakini haipaswi kuwa hivyo kwani mwajiri anatakiwa ahakikishe anaweka mazingira mazuri na kumuelimisha mtumishi asifanye makosa.

  “Ukiona mtumishi anafanya mambo yanayokinzana na sheria, kanuni na utaratibu, usimkaripie wala kumtega, mtafutie afisa ustawi wa jamii. Kwa vyo vyote afisa ustawi wa jamii atamrejesha kwenye mstari stahiki na mambo yatakwenda vizuri”.

  Aidha Dkt Nchimbi amewataka wakurugenzi kutofanya ziara nyingi nje ya halmashauri zao bali wajikite katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi na watumishi wao ambazo watazibaini endapo watafanya ziara za kutosha katika halmashauri zao.

  Amesema ili kuboresha maslahi ya watumishi, waajiri wanapaswa kuandaa mafunzo kwa watumishi juu ya matumizi bora ya fedha ili waweze kutunza fedha zao, kila halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya watumishi kupewa viwanja vya makazi pamoja na kila halmashauri kuwa na afisa ustawi wa jamii atayehusika na watumishi kwa ajila ya masuala ya ushauri.

  Pia Dkt. Nchimbi amekemea tabia mbaya ya baadhi ya wakuu wa idara/vitengo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wafanyakazi wa kike walio chini yao.

  “Wakuu hawa wa idara/vitengo wanakiuka sheria kanuni na taratibu kwa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi humo humo kazini. Wakati mwingine wanafanya mapenzi na wake za watu. Tabia hii haikubaliki na haivumiliki hata kidogo. Viongozi au wakuu wa idara/vitengo wenye tabia ya aina hii, waiache mara moja”, amesema Dk.Nchimbi.

  Kwa upande wao wananchi na watumishi Mkoani Singida wamempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua zake utumishi wa umma ambapo kwa sasa amerejesha nidhamu na uadilifu kwa kiwango cha kuridhisha.

  Wananchi hao wamesema chini ya serikali ya awamu ya tano watumishi wa umma wamebadilika sana na sasa wanatoa huduma kwa ukarimu mkubwa, wepesi na uharaka zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.

  “Huko nyuma watumishi wa umma wengi walikuwa wana urasimu wa hali ya juu. Walikuwa wakitoa huduma huku macho na akili zao zikiwa kwenye ‘whatsapp’. Mbaya zaidi mwananchi ukipeleka kero zako, wanakuona ni msumbufu. Hivi sasa mambo ni tofauti kero za wananchi zinatafutiwa majibu na majawabu kwa wakati,” ameongeza Dkt. Nchimbi akiunga mkono maoni ya wananchi.

  Mmoja wa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo Sombi Hangida amekiri kwamba ni kweli watumishi wa umma wamebadilika mno na sasa wanatoa huduma bila kuomba rushwa na wamekuwa na lugha rafiki kwa wananchi.

  Awali mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoani Singida Aaran Jumbe amehimiza kuhusu mabaraza ya wafanyakazi kufanyika katika maeneo ya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na hasa kuwashirikisha vyama vya wafanyakazi.

  Jumbe ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikitoa ushirikiano kwa vyama vya wafanyakazi na kuomba ushirikiano huo uendelee huku akisisitiza zawadi za mfanyakazi hodari zinazo ahidiwa na taasisi na halmashauri zitolewe kwa wakati.

older | 1 | .... | 1217 | 1218 | (Page 1219) | 1220 | 1221 | .... | 1897 | newer