Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1216 | 1217 | (Page 1218) | 1219 | 1220 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
   Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017
   Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017
  Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017

  0 0

  Kamati za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamoja kutofanya kazi na kuwanufausha wananchi huku ikiwa imegharimu fedha nyingi za serikali na wahisani hasa benki ya dunia.

  Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki hii mara baada ya kukagua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo imekamilika licha ya kutofanya kazi.

  Dkt. Nchimbi amesema sababu kubwa ya kutofanya kazi miradi hiyo ni udhaifu wa kamati za maji na wanasiasa katika maeneo ya miradi kutojali shida ya wananchi ya kukosa maji na hivyo kuitelekeza miradi hiyo badala ya kuisimamia.

  Amesema lengo la miradi hiyo ni wananchi wapate maji safi na salama kwa umbali usiozidi kilometa nne kama ilivyoagizwa na serikali.

  “Katika ukaguzi wangu nimebaini mifumo katika miradi hii ya maji ipo vizuri sana. Baadhi inaendeshwa kwa umeme na mingine kwa mafuta ya dizel. Makubaliano yalikuwa baada ya kukamilika miradi hii iendeshwe na kamati za maji kwa asilimia mia moja”, amesema.

  Dkt. Nchimbi amesema wajibu wa kamati hizo ni pamoja na kukusanya fedha zinazotokana na kuuza maji kwa wateja pamoja na matengenezo ya miundombinu ya visima hivyo ili miradi hiyo iwe endelevu.

  “Fedha zinazopatikana ndizo zitakazoendesha mradi husika ikiwemo kugharamia matengenezo ya mashine, pampu, miundombinu, kununulia dizel, umeme na kumlipa mhudumu wa mradi. Makubaliano ni miradi ikikamilika inabaki mikononi mwa wananchi kupitia kamati zao za maji. Serikali na wafadhili hawatahusika tena”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.

  Dkt. Nchimbi amesema serikali na benki ya dunia imegharamia fedha nyingi kwenye miradi hiyo hivyo haiwezi kuendelea kuona miradi inabaki kuwa mapambo badala ya kuwaondolea wananchi kero ya maji.

  “Naagiza wananchi wajipange upya chini ya kamati zao wachague jumuiya za watumiaji maji. Kwenye jumuiya hizo za maji wanaweza kuwepo pia wale waliokuwa kwenye kamati za awali za maji. Jumuiya hizi ziwajibike kikamilifu zihakikishe zinapata fedha kutokana na mauzo ya maji ili waendeleze miradi hiyo kwa ufanisi”, amesema Dkt. Nchimbi.

  Akiijengea nguvu hoja yake hiyo amesema kuanzia mei mwaka huu anataka kuona kila wananchi wa manispaa ya Singida,anapata maji safi na salama kwa umbali mfupi.

  “Rasilimali maji ni msingi kwa maisha ya viumbe hai wakiwemo binadamu. Maji yakiwepo tena kwa umbali mfupi mambo yote yatakwenda vizuri. Maji yanasaidia kuweka mazingira safi na afya za wananchi zinaboreka. Maji yana mchango mkubwa kwa jamii inayoelekea kwenye Tanzania ya viwanda”, amesema.

  Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wanatarajia baadhi ya miradi na hasa ile ya umeme kuibinafisha kwenye mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA) kwa ajili ya kuiendesha. Mingi itaendelea kumilikiwa na wananchi wenyewe.

  Awali mhandisi wa maji manispaa ya Singida Max Hassan Kaaya amesema wanaendelea kuelimisha jamii kuwa miradi hiyo ya maji ni mali yao hivyo jukumu la kuiendesha ni lao. Pia wanapaswa kuilinda na kuitunza vizuri.

  Naye mkazi wa kijiji cha Mtamaa Hongoa Bunka amesema elimu zaidi itolewe ili kubadilisha fikiri potofu ya baadhi ya wananchi kuwa jukumu la kuendesha miradi ya maji ni la serikali. Wabadilike na kutambua kuwa ni mali yao na wao ndio watakaoiendesha.

  0 0

  Warembo wa castle lite wakiwa tayari kuwapokea wateja katika Bar ya La Chaz Sinza Mori ambapo burudani mbali mbali ziliendelea. ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.
  Mc akifurahi jambo na mteja aliyefika La Chaz Bar mara baada ya kujipatia Castle lite
  Mc akisoma Kuponi ya zawadi ya mteja aliyoshinda katika Bar ya La Chaz Sinza Mori  katika kampeni ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.
  Burudani ya Muziki ukiendelea katika Bar ya La Chaz Sinza Mori mapema wiki hii  katika kampeni ya Castle Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.

  0 0

  Wafanyakazi wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakigawa wine kwa viongozi ambao wamehudhuria uzinduzi wa usafiri wa anga Dar es Salaam – Songea, kupitia shirika hilo katika uwanja wa ndenge wa songea mkoani Ruvuma.Kwa undani wa habari hii tiazama video yake hapo chini.

  0 0
  0 0


  0 0

  Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (kushoto), akizungumza katika Mkutano wa Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto Mkoani Tanga, wakati alipokuwa akiwahamasisha wanafunzi hao kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo amewataka kutumia maarifa yao yote kuhakikisha ushirikiano huo unakuwa wa kudumu.
   Naibu Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) anayesimamia Elimu, Utafiti na Ushauri, Fahamu Mtulya akizungumza jambo katika warsha hiyo.
  Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto Mkoani Tanga wakimsikiliza Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao juu ya umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Ukafika muda wa maswali.
  Picha ya pamoja.

  0 0


  MKAZI wa Mwanza, Pildas Emmanuel ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano la ‘Ijue Nguvu ya Buku’ katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

  Droo ya bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi katika simu za mikononi kupitia huduma za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa ambapo pia ilichezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema kwamba droo hiyo imeshirikisha washiriki zaidi ya 10,000 Tanzania nzima na kufanikiwa Emmanuel kutoka Mwanza kunyakua fedha hizo na kuingia katika historia ya mshindi wa kwanza kutoka mkoani.

  Alisema Biko wamefurahia kuona mshindi wa droo ya tatu ametoka mkoani, baada ya droo mbili za awali ambazo zote washindi wake walitoka jijini Dar es Salaam kwa Christopher Mgaya na Nichoulas Mlasu kuibuka na Milioni 10.

  “Tunawapongeza washiriki wote wanaogombania gurudumu la mchezo wetu wa Biko ambao umeshika kasi, huku nikimpongeza pia mshindi wetu wa mkoani Mwanza, Emmanuel kuibuka na ushindi huu ambao kwa hakika unaweza kubadilisha maisha yake.
  “Bado kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 10 kwa droo ya wiki pamoja na zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 500,000 na Milioni moja kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za mikononi huku namba yetu ya kampuni ikiwa ni 505050 na namba ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

  Naye Emmanuel alisema bado haamini ametangazwa kushinda zawadi hiyo inayoweza kumfanya atimiz ndoto zake za kimaisha kwa kuhakikisha kwamba fedha hizo anazitumia vizuri endapo atakabidhiwa kutoka Biko, huku akikiri kuwa ametokea kuupenda mchezo wa Biko.

  “Nimekuwa nikicheza Biko kwa sababu ni mchezo mzuri maana hauna mlolongo mrefu, hivyo wakati nasubiria zawadi yangu kutoka Biko, nawashauri Watanzania wote kugombania gurudumu la Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda donge nono,” Alisema.

  Baada ya kutangazwa kunyakua Sh Milioni 10, mshindi huyo anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake mapema wiki hii kwa utaratibu wa kufunguliwa akaunti katika benki ya NMB sambamba na kupewa elimu ya kifedha kama walivyopatiwa washindi wenzake wa jijini Dar es Salaam.
  Msanii nyota wa filamu Tanzania, ambaye pia ni balozi wa Biko, Kajala Masanja, akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 10 aliyoshinda mkazi wa Mwanza, Pildas Emmanuel katika mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na Kampuni ya Biko Tanzania. Droo hiyo ilichezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.

  0 0

  Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machema (kushoto), akishiriki zoezi la usafi pamoja na Wananzengo wengine wa Kata hiyo katika Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
  BMGHabari
  Wananzengo wa Kata ya Buzuruga wakiwa pamoja na diwani wao, Richard Machema (mwenye kofia), katika zoezi la usafi kwenye Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
  Zoezi la usafi la kuondoa vichaka na taka katika mazingira ya Kituo cha Afya Buzuruga limeelezwa kusaidia kuteketeza maficho ya masalia ya mbu pamoja na baadhi ya vijana wasio na maadili mema waliokuwa na desturi ya kujificha kwenye vichaka hivyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa bangi.
  Uteketezaji wa taka hatarishi ikiwemo chupa umelalamikiwa na wakazi wa Kata ya Buzuruga na kuomba suala hilo kufanyiwa kazi ili kuwa na uteketezaji taka usio hatarishi katika jamii
  Usafi ukiendelea
  Usafi ukiendelea

       Mwananzengo wakiongea na Lake Fm kuhusiana na usafi huo

  0 0

  Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao unaelekea kuisha. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi. 

  Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/2018 Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi. “ESRF imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti mbalimbali, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo mbalimbali.

   “Kama jinsi mnavyojua nchi yetu imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo kwa nchi.” alisema Dkt. Kida.

   Kwa upande wa mtoa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018. Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. Joviter Katabaro akitoa taarifa kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. 

   “Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule nchini kitoke, kuna upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,” alisema Dk. Katabaro. Kwa upande wake, Prof. Haidari Amani (Mtafiti Mshirki mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto ambazo zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri kuanzia wakulima wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho wanakifanya. Mtafiti Mwenza wa ESRF, John Shilinde akitoa taarifa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mtafiti Mwenza Kiongozi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akijibu maswali ya baadhi ya washiriki waliohudhuria. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo wakati wa kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo. Picha juu na chini ni baadhi ya washiriki wakitoa maoni na kuuliza maswali kuhusu bajeti zilizotolewa taarifa. Baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo nchini walioshiriki kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo.

  0 0


  Na Koleta Njelekela-STAMICO

  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza uchimbaji wa makaa ya mawe katika mlima wa Kabulo uliopo Kiwira katika wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe.

  Mratibu wa Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kiwira, Mjiolojia Alex Rutagwelela ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO amesema kazi ya uchimbaji iliyoanza tarehe 30/04/2017 inaendelea vizuri na tayari tani 100 zimechimbwa katika siku ya kwanza. Lengo la mradi ni kuchimba tani 200-300 kwa siku.

  “Tumeanza uchimbaji na tani hizo, kama njia mojawapo ya kujaribu mitambo ya uchimbaji, kabla ya uzinduzi rasmi ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni, baada ya Shirika na wadau wake, kukamilisha maandalizi ya uzinduzi.” Alifafanua Mjiolojia Rutagwelela. 

  Aidha Rutagwelela amesema matarajio ya STAMICO ni kuchimba kati ya tani 6000 hadi tani 9000 za makaa ya mawe kwa mwezi kwa kuanzia, kiwango ambacho kinatarajiwa kuongezeka kadiri kazi ya uchimbaji inavyoendelea.

  Mratibu huyo amesema awamu ya kwanza ya Mradi wa uchimbaji makaa ya mawe inatekelezwa kupitia leseni zake mbili za uchimbaji mdogo wa madini Primary Mining Licences (PMLs) zilizopo ndani ya leseni ya utafiti ya Kabulo zenye ukubwa wa Hecta 16.52. 

  Leseni hizo mbili za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo zina tani zipatazo 241,865 za mashapo ya makaa ya mawe yaliyoko karibu na uso wa ardhi ambayo yataruhusu Uchimbaji wa Mgodi wa Wazi (Open pit mining) kufanyika. 

  “Uchimbaji huu, ambao umeanzia kwenye mlima wa Kabulo na baadae mlima wa Ivogo, utaiwezesha STAMICO kuzalisha makaa ya mawe na hivyo kupunguza uhaba wa madini hayo nchini ambayo ni moja ya vyanzo vya nishati ya umeme. Makaa ya mawe hutumika kama moja ya vyanzo vya Nishati katika shughuli za uzalishaji viwandani vikiwemo viwanda vya Saruji nchini” alifafanua Rutagwelela.
   Wataalam wa STAMICO wakiendelea na kazi ya uchimbaji makaa ya mawe katika Mlima wa Kabulo uliopo Kiwira wilayani Ileje mkoa wa Songwe.
   Shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe zinazofanywa na STAMICO, zikiendelea katika Mlima Kabulo-Kiwira.


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Serikali ya Mkoa wa Tabora imewaagiza kwa wakazi wa Mkoa huo kuanza kulima kwa wingi mazao wengine kama vile alizeti , pamba, mpunga na miembe ya kisasa ili waweze kuwa na fursa pana ya kujiongezea kipato badala ya kutegemea tumbakuli pekee kama zao kuu la uchumi katika maeneo mengi.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati anawahutubia wakazi na Wafanyakazi kwenye sherehe za kilele cha Mei Mosi kilichofanyika katika Maspiaa ya Tabora.

  Alisema kuwa Mkoa huo umebahatika kuwa na ardhi ambayo mazao mbalimbali kama vile mpunga , pamba, alizeti na hata matunda kama vile maembeo yanastawi , lakani bado wananchi hawayapa kipaumbele.

  Bw. Alisema kuwa wananchi wakiyapa kipaumbele na kwa kuzingatia ukulima wa kisasa yatasaidia kufungua fursa ya uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo kuelelekea viwanda vikubwa kwa kuwa malighafi itakuwepo ya kutosha viwanda vitakavyoanzishwa.

  Aliseme kuwa endapo kila familia itakuwa walau na hekari moja ya shamba la alizeti Mkoa wa Tabora utakuwa ndio mzalishaji mkubwa na mafuta hayo na wawekezaji wengi watajitokeza kuanzisha viwanda wa usindikaji wa zao hilo na hivyo kutoa ajira kwa wakazi wengi na wakinamama kupata fursa ya kuuza vyakula.

  Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa Tabora inayofursa kubwa ya kuwa na viwanda vikubwa vya kusaga na kukoboa nafaka endapo wakulima watalima mpunga na mahindi kwa wingi na kwa kuzingatia utaalam.

  Kuhusu suala la kilimo cha miembe, mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wakazi wa kuanza kuwa na mashamba makubwa ya miembe ya kisasa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa matunda hayo kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani.

  Alisema kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora imeshaanza taratibu mbalimbali za kuhakikisha kuwa viwanda vya zamani vinafufuliwa na vipya kama vile vya kusindika tumbaku vinajengwa ili kuongeza ajira kwa wakazi wa Tabora.

  Aidha alitoa kwa wafanyakazi wote Mkoani humo kuonyesha mfano kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kilimo kwa kuwa na mashamba ya kisasa kama sehemu ya kuhamasisha wananchi juu ya kilimo cha kisasa ambacho kinafaida zaidi.

  Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.

  0 0

  Rais mstaafu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi(TUCTA) Bi.Magreth Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kwa sasa watumishi wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya waajiri kutovitambua vyama hivyo.

  Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo kwa upande wa kitaifa maadhimisho hayo yamefanyikia mkoani Kilimanjaro.

  Bi. Magreth Sitta amesema kuwa, itakuwa ni jambo jema zaidi iwapo kama waajiri watakaa na wafanyakazi wao na kuziangalia changamoto zilizopo ili hata Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizipata aweze kulifikisha suala hilo kwa Spika wa bunge liweze kutizamwa kwa makini ili kupunguza changamoto husika.

  Aliendelea kusema, serikali na makampuni binafsi hulipa kwa mwezi mishahara duni ambapo ni ujira mdogo sana kwa siku ikilinganishwa kupanda kwa gharama za maisha.

  Amesema kwa sasa ukubwa wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE) kodi ya mapato inayotozwa na serikali inawalazimisha watumishi wa serikali na sekta binafsi kulipa kodi mara tatu kwa na zaidi.

  Miongoni mwa ulipaji wa kodi hizo ni pamoja na ulipaji kupitia mishahara yao ya kila mwezi, kulipa kodi kila wanunuapo bidhaa mbalimbali na ulipaji wa kodi wakati wa kustaafu.

  Aliendelea kusema kuwa, tatizo lingine kubwa ni baadhi ya taasisi za umma na za binafsi ambazo zimekuwa zikikwepa kutekeleza sheria za kazi ikiwemo sheria ya ajira na mahusiano kazini sheria Na. 6 ya mwaka 2004.

  Amesema sheria hiyo inalenga kuwashirikisha wafanyakazi kupitia mabaraza ya wafanyakazi kupitisha bajeti za taasisi za umma zilizopokelewa Bungeni bila kuzingatia sheria hiyo hali ambayo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwenye makampuni ya tasisi binafsi na kuiomba serikali iwe mfano mzuri katika kulipa michango ya wafanyakazi katika mifuko iliyopo.
  Rais Mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi ambaye pia ni mgeni rasmi B. Magreth Sitta akizungumza na wafanyakazi wa umma na taasisi binafsi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
  Wanachi wakimsikiliza Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta leo katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
   Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Meneja Rasilimali watu wa  Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA),Pius Matagi kwa nimbi ya Mkurugenzi Mkuu leo katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
   Watumishi wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) wakishangilia baada ya mtumishi mwenzao kukabidhiwa cheti cha ushiriki kwa niamba ya Mkurungenzi Mkuu wa shirika hilo kutoka kwa Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta.
   Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbalimbali leo jijini leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wasamalia wema wakiwapatia  huduma ya kwanza  majeruhi marabaada ya kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
   Baadhi ya wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD marabaada ya kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini  Dar es Salaam.
   Majeruhi akiwa  kwenye gari la MSD  akiendelea kupewa hudum ya kwanza

  0 0


  0 0

   Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa  akisalimiana na  Makamu  wa Rais Mama Samia  Suluhu walipokuwa  katika  Sherehe za  Mei  Mosi  zilizofanyika kitaifa mkoani  Kilimanjaro leo 01/5/ 2017  Katika viwanja  vya  Chuo  cha Ushirika  Mkoani  Kilimanjaro.
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti  Mtendaji  wa  IPP.  Dr  Reginali Mengi  walipokuwa  katika  Sherehe za  Mei  Mosi  zilizofanyika  Kitaifa Mkoani  Kilimanjaro leo 01/5/ 2017 katika viwanja  vya Chuo cha Ushirika  mkoani Kilimanjaro.
    Baadhi ya  Wabunge wakiwa  pamoja na watumishi  wa Serikali  katika Sherehe za Mei  Mosi  zilizofanyika  kitaifa mkoani  Kilimanjaro  leo katika viwanja vya Chuo  cha Ushirika  Mkoani  Kilimanjaro
  Wafanyakazi wa Kiwanda Chakutengenza  Sukari  (TPC)  Wakipita Kwa maandamo mbele ya mgeni Rasimi Rais Dr John Magufuli  ikiwa ni ishara ya  kusheherekea  Maadhimisho ya Sikukuu ya wafanyakazi  Duniani  ambapo Tanzania Kitaifa  yamefanyika  mkoani  Kilimanjaro   
  PICHA  NA  PMO

  0 0

  Na Nuru Juma, Husna Saidi - MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aahidi nyongeza ya kawaida kwa mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi wanaostahili.

  Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.

  Dkt. Magufuli alisema Serikali ilisitisha upandishaji wa vyeo na mishahara kutokana na kuwepo na watumishi hewa na walioghushi vyeti lakini baada ya kuondolewa Serikali itahakikisha inashughulikia maslahi ya wafanyakazi.

  “Watumishi 9932 walikuwa na vyeti feki,watumishi hewa walikuwa 19706 hivyo kama Serikali ingeongeza mishahara inamaana watumishi hawa pia wangefaidika na pesa ambazo hawakustahili kuzipata”, alisema Dkt. Magufuli.

  Aidha aliwataka waajiri kuheshimu na kutoa mikataba ya kazi na kutowanyanyasa wafanya kazi wao na wafanyakazi kuomba kazi kulingana na elimu zao na waache tabia ya kughushi vyeti.

  Aliongeza kuwa Serikali itashughulikia mfumuko wa bei za bidhaa na kuhakikisha viwanda vingi vitajengwa sehemu mbalimbali nchini ili kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TUCTA Dkt. Yahya Msigwa ameipongeza Serikali kwa kutekeleza ahadi zake na kuopngeza kuwa hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali inayodhamira ya dhati ya kuwajali wananchi wake wakiwemo wafanyakazi.

  Ameongeza kuwa wanayo imani kubwa kwa Serikali kuwa itatekeleza ahadi yake ya kufanyia maboresho ya maslahi ya umma kama ambavyo umeonyesha nia njema ya kutekeleza ahadi zake.

  Alizitaja baadhi ya ahadi zilizotekelezwa kuwa ni pamoja, kupiga vita rushwa na ufisadi, kuondoa watumishi hewa, Serikali kuhamia Dodoma, ujenzi wa miundombinu ya reli, vita dhidi ya dawa za kulevya pamoja na ununuzi wa ndege.“Ni imani yetu kuwa ahadi hii ya kuboresha maslahi kwa Watumishi wa Umma itatekelezwa kwa wakati kwani tayari umekwisha ondoa mambo yaliyokuwa yanakwamisha zoezi hilo,” alisema Dkt. Msigwa.

  Wakati huohuo Katibu Mkuu huyo ameiomba Serikali kuharakisha kubuni namna ambavyo wafanyakazi watanufaika na Mifuko ya Jamii na wanaodai mapato yao kusikilizwa kesi zao kwa wakati.

  Maadhimisho hayo yameuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,Naibu Spika Tulia Ackson, Mawaziri Jenister Mhagama na Angella Kairuki, Profesa Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na baadhi ya Wabunge. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Uchumi wa Viwanda Vizingatie Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi”.

  0 0
  NA K-VSI BLOG/Khalfan Said
  WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wameungana na wenzao jijini Dar es salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi.

  Kitaifa sherehe hizo zinaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mjini Moshi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi.”

  Aidha jijini Dar es Salaam, Wafanyakazi wa PPF na wengine kutoka sekta ya Umma na Binafsi, walifanya matembezi kutoka eneo la Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru huku wakiongiozwa na brass band ya Jeshi la Magereza.

  Kwa upande wao wafanyakazi wa PPF  walianza kwa kukusanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo barabara ya Samora/Morogoro ambapo walipewa maelekezo ya umuhimu wa ushiriki wao katika maetembezi hayo na kujiunga na wenzao eneo la kuanzia matembezi pale Mnazi moja.
  Mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Bw. Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi na magari kadhaa kutoka taasisi za umma na binafsi yakionyesha huduma zitolewazo na taasisi hizo.
  Huduma zitolewazo na PPF ni pamoja na kulipa Mafao ya Uzeeni, Mafao ya Wategemezi,Mafao ya Elimu, Mafao ya Kiinya Mgongo, Mafao ya Kifo, Mafao ya Ugonjwa na Mafao ya Uzazi. Lakini pia kazi nyingine za Mfuko huo ni kusajili wanachama kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama “Wote Scheme”

  Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, wakiwa kwenye matembezi ya kuadhimisha Mei Mosi jijini Dar es Salaam Leo.

  Kiongozi wa kundi la wafanyakazi WA PPF, wwlioshiriki matembezi ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, Mohammed Siaga, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza matembezi hayo.

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu ujio mpya wa Posta ya Kidijitali ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio mpya wa Posta ya Kidijitali ofisini kwake jana Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtenda Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania aliyemaliza muda wake akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa waandishi hao na mrithi wake Deo Kwiyukwa (hayupo pichani) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha na Uhasibu Cyprian Mugemuzi.Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.   Meneja wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Nashon Mudala (aliyesimama kulia) akifafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa wafanyakazi wa Zantel ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi wanapokuwa kazini wakati wa ziara fupi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma. Ziara hiyo ilifanywa na wafanyakazi hao mara baada ya kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya, Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid (Kushoto) na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
  Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kulia ni Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
  Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
  Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Waliokaa Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur
  Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
  Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akiwaonyesha wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel picha iliyotumwa na wadau wa usalama barabarani inayoonyesha matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wazembe. Wafanyakazi hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.

  0 0

  Mei Mosi 2017, umefanyika uzinduzi wa kampeni ya "Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksu" inayoratibiwa na 102.5 Lake Fm Mwanza @lakefmmwanza #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo.

  Kampeni inalenga kuhamasisha jamii kuweka mazingira katika hali ya usafi muda wote huku Wananzengo wa minadani wakipata fursa ya kipekee. Endelea kuitegea sikio 102.5 #LakeFm Mwanza kwa burudani na habari zaidi.

  @bmghabari @gbpazzo ©Ng'arishaNzengoUchafuNuksi√√√√

older | 1 | .... | 1216 | 1217 | (Page 1218) | 1219 | 1220 | .... | 1897 | newer