Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI LEO IJUMAA APRILI 28, 2017


TAARIFA YA KUITWA KAZINI

UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisalimiana na waendesha boda boda, eneo la kwa kwamromboo waliohuduriia kwenye uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi
1Baadhi wa wananchi waliohudhuria kushuhudia uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Muriet.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
Mke wa Mfadhili Bwa.Haroun akivishwa vazi la Kimasai na wakazi wa eneo hilo kama shukrani yao kwa kujengewa Kituo cha Polisi. 
 

Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Kata ya Muriet wakati wa ziara ya Kikazi Jijini hapa yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.

Akiweka jiwe la Msingi Mhe. Gambo amesema kwa muda mrefu alikua anakerwa na uhalifu uliokithiri katika eneo hilo na hali hiyo kumsukuma yeye kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachosaidia kudhibiti masuala ya Uhalifu.

Aliongeza kuwa baada ya kumpata mfadhili huyo alimlete eneo la ujenzi ambapo pia wahalifu walimuibia Simu yake mbele ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndipo na mfadhili alipopata ari ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo. 

“Haiwezekani mtu anaiba mbele ya Kamanda wa Polisi hakika hii ilituthibitishia kwamba uhalifu katika eneo hili umekithiri na kwa sababu hakunha Kituo cha Polisi wahalifu wanapata mwanya wa kufanya kazi hii isiyo halali kwa ujasiri zaidi” Alisema Gambo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mfadhili ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Ndg. Haruni alisema amejitolea sehemu ya mali zake ili kuwasaidia Watanzania wenzake wanaoteseka na tabia za uhalifu zinazorudisha nyuma maendeleo 

Ujenzi wa Kituo hicho utakaogharimu zaidia ya Tsh Mil 200 utakamilika mnamo mwezi Juni 2017.



 

MWAKIFWAMBA AFUNGUKA KUHUSU MPASUKO MKUBWA NDANI YA TASNIA YA FILAMU

UBA YATOA VYETI KWA WADAU WALIOPATA RUZUKU ZA MRADI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akizungumza na wanufaika wa maradi wa kuandika mawazo ya biashara ambao wapo hapa nchini juu ya namna watakvyoweza kushirikiana na Benki ya UBA katika kukuza biashra zao mpaka nje ya mipaka ya Tanzania
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi cheti kwa Hurbert  Mwashiuya juu kama mnufaika wa mradi mara baada ya kupata ruzuku 
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi  cheti kwa Bi , Aika Mtei kma mmoja wa wanufaika wa ruzuku mara baada ya kuandika mradi juu ya biashara katika mtandao
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwaeleza watendaji wa Benki ya UBA juu ya umuhimu wa kuwasaidia wanufaika hao hili waweze kuwa mfano kwa wengine
Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika na baadhi ya watendaji wa beki hiyo

KATIBU WA BUNGE AONGOZA KIKAO CHA UONGOZI LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Bunge, Ndg. Chacha Nyakega (aliesimama) akifafanua jambo wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha uongozi  wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (katikati) akiongoza kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma​

ELIMU YA KUNUNUA HISA YATOLEWA KWA CHAMA CHA MUUNGANO WA VYAMA VYA USHIRIKA(SACCOS) TANZANIA

$
0
0
 Wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania,Wakimsikiliza kwa makini  mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa wa Orbit Security  ambao ni washauri wakuu wa  maswala ya uuzaji wa hisa za Vodacom Tanzania PLC,Godfrey Gabriel alipokuwa akitoa elimu juu ya ununuaji wa hisa za  kampuni hiyo jana Morogoro.
 Baadhi ya wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania,Wakisoma mkutasari wa matarajio wa hisa  za Vodacom Tanzania  PLC, Walipokuwa wakipatiwa elimu ya ununuaji hisa za kampuni hiyo na mawakala wa uwekezaji wa Orbit Security  ambao ni washauri wakuu wa maswala ya hisa za Vodacom Tanzania PLC  jana mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni ya  uwakala wa uwezeshaji  ya Orbit Security ambao ni washauri wakuu wa  maswala ya uuzaji hisa za Vodacom Tanzania PLC  Godfrey Gabriel (kushoto) akimsikiliza  mmoja wa wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania, Gebha Nyoni  aliyekuwa akiuliza swali juu ya uuzaji wa hisa za Vodacom  baada ya kupata elimu  ya ununuaji wa hisa wakati wa   semina ya Utawala bora  kwa viongozi wa SACCOS  iliyofanyika mkoani Morogoro jana.
 Mmoja wa washiriki wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania  ,wakionyeshwa kipengele kilichopo katika mkutasari wa matarajio wa hisa  za Vodacom Tanzania  PLC na  Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni ya  uwakala ya uwezeshaji  ya Orbit  Security ambao ni washauri wakuu wa  maswala ya uuzaji wa hisa za Vodacom Tanzania PLC, Godfrey Gabriel (kushoto)wakati wa kutoa elimu juu ya ununuaji wa hisa za  kampuni hiyo jana Morogoro.
 Baadhi ya wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania  ,wakisoma fomu za kununua  hisa  za  Vodacom Tanzania  PLC ,wakati walipokuwa wakipewa elimu juu ya ununuaji wa hisa za kampuni hiyo na   mawakala wa kampuni ya  uwekezaji ya Orbit  Security ambao ni washauri wakuu wa kampuni hiyo maswala ya hisa .
Mkurugenzi wa uendeshaji  wa kampuni ya uwakala ya  uwekezaji ya Orbit  Security  ambao ni washauri wakuu wa Vodacom Tanzania PLC  kuhusiana na maswala ya uuzaji hisa,Juventus Simon akiwaelekeza  wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACCOS) Tanzania  jinsi ya kujaza fomu za kununua hisa za Vodacom wakati wa semina maalum ya kununua hisa za kampuni hiyo iliyofanyika jana Morogoro.

MWAKIFWAMBA AFUNGUKA KUHUSU MPASUKO MKUBWA NDANI YA TASNIA YA FILAMU


KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA CHATOZA FAINI MASHAMBA YA MPUNGA NA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WILAYANI MBALARI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA .

$
0
0
Mashamba ya mpunga ya Mbarali Highland Estates, Kapunga Rice Project, Kapunga Small Holders farm, pamoja na skimu za umwagiliaji za Mwanavala (Nguvukazi farm), Mwashikamile pamoja na Sikimu ya Mwendamtitu zilizoko Mbarali mkoa wa Mbeya yametozwa faini ya jumla ya kiasi cha shilingi 120,290,000/= baada ya kukiuka sheria mbalimbali za Mazingira zilizo chini ya Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe 27 aprili 2017, imetozwa na Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kuokoa Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilichoko Mkoani Mbeya kupitia kwa Mwananasheria wa NEMC- Vicent Haule , baada ya kugundua makosa mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za mazingira na umwagiliaji katika Mashamba hayo wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya Mpunga na skimu tofauti za umwagiliaji wilayani humo.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko cha Kitaifa Bwana Richard Muyungi, alisema kwamba kutokana na makosa mbalimbali yaliyokutwa katika masahamba hayo ikiwemo kutokuwa na vyeti vya ukaguzi wa Mazingira, kukiuka taratibu za umwagiliaji kwa kutoa na kutumia maji bila ruhusa, kuweka mifereji mikubwa ya kumwagilia mashambani pasipo kufuata sheria na kanuni zinazotakiwa, kutorekebisha miundombinu ya Umwagiliaji kwa mifereji ya kutolea maji. 
 
Mashamaba hayo yanapigwa faini kama ifuatavyo Mbarali Estates 33,000,000, Kapunga Rice Project 33,100,000/=, Kapunga Small Holders 3,000,000/=, Madibila farm Project 33,000,000. Pamoja na mashamba hayo pia zipo skimu za Umwagiliaji zilizotozwa faini ikiwepo Skimu ya Mwendamtitu 7,995,000, Mwanavala (Nguvukazi) 7,995,000/=, Mwashikamile 2,200,000/=.

Aidha aliongeza pia mashamba ya Mwashikamile, Mwanavala(nguvu kazi) na Kapunga Small Holders, wanatakiwa kulipa faini lakini pia baada ya kuvuna wanatakiwa kuacha mara moja kulima tena katika mashamba hayo mpaka pale watapofuata taratibu za kupata vibali vya maji na cheti cha ukaguzi wa mazingira kutoka NEMC na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji ."Kutoza faini hizi siyo kukomoa Mashamba haya ila ni kuhakikisha kuwa Wamiliki wa mashamaba makubwa ya umawagiliaji wote Nchini wanafuata taratibu na Sheria za kimazingira katika kuendesha mashamba haya" alisema Muyungi

Kikosi kazi hiko kiko MKoani Mbeya kwa kukagua na kutembelea sehemu mbalimbali za mashamba , skimu za umwagiliaji na pia kusikiliza maoni ya Wananchi jinsi ikiwa ni harakati za kurudisha ikolojia ya mto Ruaha.

MISS GRAND TANZANIA 2017 YAZINDULIWA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mratibu wa Shindano la Miss Grand  Tanzania , Rasheedah  Jamaldin akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar, juu ya uzinduzi wa shindano la urembo litakalo tambulika kama Miss Grand Tanzania  2017 linalo tarajia kuanza Juni  mwaka huu,ambapo imeelezwa kuwa mchujo wake utaanzia katika ngazi ya vitongoji mpaka Taifa .
 Meneja Matukio wa Miss Garand  Tanzania 2017 ,Abraham Mahimbo akizungumza na waandishi jisni mawakala watakavyohusika katika kuwapata warembo nchi nzima
Waandishi mbalimbali waliofika katika mkutano huo wa uzinduzi wa shindano la Miss Garand 2017 jijini Dar es Salaam leo

Muhimbili Yampatia Msaada Anayefundisha akiwa kitandani

$
0
0



Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kumpatia Joyce Kanitande msaada wa baiskeli na matibabu ambayo yatamwezesha kufanya shughuli zake za kila siku. Joyce anatapatiwa matibabu katika hospitali hiyo baada ya kupta ajali na kuvunjika mgongo wakati akiwa na umri wa miaka saba.
Bi. Joyce akiwa amekaa kwenye baiskeli baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumpatia msaada huo leo.
Mkuu wa Idara ya Utengamano, Rosemary Kauzeni akiwaeleza waandishi wa habari jinsi Joyce akavyokuwa akipatiwa matibabu yakiwamo mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake.

Bi. Joyce akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako amefikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Joyce alipata ulemavu wa mgongo baada ya kupata ajali wakati akiwa na umri wa miaka 7 na hivyo kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida.


Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa msaada wa baiskeli na matibabu kwa Mwalimu Joyce Kantande ambaye alipata ulemavu kutokana na ajali aliyoipata akiwa na umri wa miaka saba.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa amesema wameguswa na tatizo la Joyce na hivyo uongozi wa hospitali umeamua kumpatia baiskeli hiyo ili kumwezesha kufanya shughuli zake akiwa amekaa .

‘’ Tuliona stori yake kwenye gazeti moja na kiukweli tumeguswa na tatizo lake kwani Joyce alikaa miaka 18 akiwa amelala baada ya kupata ajali iliyosababisha apate ulemavu kutokana na hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji Profesa Lawrence Museru ameona ni vema tukampatia msaada wa baiskeli, lakini pia kama Hospitali tutampatia msaada wa matibabu na tutakua tukimfuata na kumrudisha nyumbani kwa kipindi chote atakachokua akija hospitalini hapa kwa ajili ya matibabu,‘’ amesema Mtawa .

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Juma Mfinanga amesema kwa kushirikiana na wataalam wengine wa MNH watamfanyia vipimo mbalimbali ili kujua tiba gani anastahili .

Naye Mkuu wa Idara ya Tiba na Utengamao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Rosemary Kauzeni amesema watatumia utaalam wao kumsaidia Bi Joyce ili aweze kufanya shughuli zake akiwa amekaa badala ya kulala hususani shughuli zake za kufundisha watoto ambazo huzifanya akiwa amelala .

‘’Tutatumia utalaam wetu kwa kumpatia tiba ya mazoezi ya viungo ili aweze kukaa wakati anapofanya shughuli zake badala ya kulala na hatimaye aweze kutawala mazingira yake,” amesema.

Kwa upande wake Bi Joyce ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada alioupata na kuwaomba watu wengine kujitokeza kumsaidia kwani ana mahitaji mengi.

MAHAKAMA YA ARUSHA YAMWACHIA HURU ALIYEKUWA MWENYEKITI UVCCM ARUSHA KWA KOSA LA KUJIFANYA USALAMA WA TAIFA

$
0
0
Na Wankyo Gati,,ARUSHA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, leo imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya baada ya kuona upande wa Jamuhuri wazembe wa kushindwa kuleta mashahidi katika kesi ya kujifanya Afisa Usalama wa Taifa (TISS).

Akisoma uamuzi wake jana uliotokana na ombi la Wakili wa Serikali Grace Madikenya la kuomba Mahakama hiyo kuiondoa kesi hiyo kwa sababu ya kukosa shahidi muhimu katika kesi hiyo na kupingwa na Upande wa Utetezi kuwa wanatumia vibaya mahakama kumtesa mteja wao, Gwantwa

Mwakuga, alisema Mahakama inasikitika kuona mwendesha mashitaka wa serikali, anatumia kigezo cha kuondoa kesi na kumkamata mshitakiwa kwa maslahi yake mwenyewe.

Alisema kesi hiyo imekuja mara ya pili baada ya kufunguliwa kesi namba 376/2016 na ilipofika katika utoaji wa ushahidi wa mpelelezi wa kesi hiyo, Mwendesha mashitaka aliomba Mahakama kuiondoa kesi hiyo kwa madai hawana nia ya kuendelea nayo na na mahakama ilikubaliana naye na kumwachia huru, lakini siku hiyo hiyo Desemba 14 Mshitakiwa alikamatwa.

“Kinachosikitisha Mahakama ilishuhudia kwa macho yake baada ya kumwachia mshitakiwa alipotoka nje alikamatwa tena na kuletwa tena Mahakamani hapa, kwa hakimu Mfawidhi Augustino Rwezile na mashitaka yalikuwa yale yale hakuna kilichorekebishwa na sasa wanaomba tena kuondoa kwa kigezo shahidi muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18, hii ni utumiaji vibaya ofisi ya mwendesha mashitaka, ili kutesa watu,”alisema.

Gwantwa alisema Mahakama inatambua nguvu ya Mkurugenzi wa Mashitaka aliyonayo, lakini nguvu hiyo isitumike vibaya ni muhimu kuzingatia maslahi ya umma,haki na utedaji kazi wa Mahakama.Alisema Mahakama hiyo imejiuliza kipya kilichorekebishwa katika kesi hiyo ya pili namba 493/2016 na kuona hakuna, isipokuwa upande waJamuhuri wamefanya kwa kukidhi mataka yao wenyewe.

“Hapa upande wa jamuhuri wazembe wameshindwa kuleta mashahidi wakitakiwa kuleta wanaleta sababu wapo Kenya mara nje ya nchi, mara kuleta mashahidi ngumu, ili mradi kucheleesha kesi hii, mshitakiwa anazo haki zao za msingi za kuona kesi yake ikiendelea, lakini Jamuhuri inatesa Wadaawa kwa ajili ya maslahi yao, kitu ambacho mahakama hii haiko tayari kuona ikichezewa kwa namna hiyo,”alisema huku akinukuu kesi mbalimbali.

Alisema vema wadau wa Mahakama wakafahamu kuwa mahakama ni hekalu la kutenda haki kwa washitakiwa na walalamikaji sio vinginevyo na haki ya mshitakiwa kuona mashauri yafike mwisho na Mahakama haiwezi kuvumilia kuona mshitakiwa anakamatwa kwa kigezo cha kutumia mahakama vibaya.

Alimalizia kusema kimsingi kifungu cha 91 cha sheria ya mwendendo wa makosa ya Jinai ambacho upande wa Jamuhuri waliomba mahakama ikitumie kuondoa shauri hilo, inakikataa na kutumia kifungu cha 225 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kumwachia huru mshitakiwa huyo.

Awali kabla ya hakimu Gwantwa kuanza kusoma uamuzi huo, Wakili wa serikali, Grace Madikenya aliiambia mahakama hiyo haipo tayari kuendelea kusikiliza shauri hilo kwani tayari ameomba kuliondoa na lipo kinyume cha sheria, huku Wakili wa utetezi Charles Adiel akiomba Mahakama hiyo kusoma uamuzi wa mahakama kwa niaba ya mteja  wake na atapokea.

Sabaya mwaka jana alifikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mawili ambapo la kwanza ni kuwa Mei 18 mwaka 2016, katika Hotel ya Sky Motel, Mshitakiwa Sabaya alijifanya Afisa usalama wa Taifa (TISS) na kupata huduma ya kulala katika hotel hiyo, kwa kupata chakula navinywaji wakati sio kweli.

Shitaka la pili Sabaya anashitakiwa kughushi kitambulisho ya TISS kilichosomeka MT.86117 wakati akijuwa wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Sabaya alikuwa akitetewa na Wakili Edna Haraka na Charles Adiel

Kingdom Heritage Presents Discover Your Potential

$
0
0



Kampuni ya KINGDOM HERITAGE imeandaa event inaitwa "Discover Your Potential" ni event yenyewe wazungumzaji wahamasishaji katika mambo ya mipango,maendeleo,ndoto na maono na ujasiliamali.

Watakuwa wakizungumza mambo kadhaa yatakayotukumbusha kutambua uwezo wetu tulio nao kila mmoja wetu kwa ulivyo na mahala ulipo na namna ya kuutumia uwezo huo ili kufikia Malengo,Mipango,Ndoto na Maono kila mmoja.

Ni Jumapili wiki hii ya 30 April 2017 katika Kanisa la Living Water Centre Kawe Kuanzia saa 9:00 mchana.Usipange kukosa! ni Bureee!

RAS TABORA AWATAKA WANAWAKE WASHIRIKIANE KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara ametoa wito kwa wanawake mkoani hapa kuungana na kushirikiana pamoja katika shughili za mbalimbali za ujasiriamali ili iwe rahisi kwao kunafaika na fursa mbalimbali mikopo ikiwemo asilimia tano inapaswa kutolewa na Halmashauri zao.

Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati akizindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi la Mkoa huo.Alisema kuwa wanawake wakiendelea kufanyakazi kwa ubinafsi hawataweza kuendelea bali wataendelea kubaki nyuma.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema kuwa wanawake wakiungana na wakaunda vikiundi vinavyoaminika watapata fursa ya kukopeshwa na Taasisi za fedha zilizopo mkoani Tabora na hivyo kukuza mitaji yao ambapo hatimaye wanaweza kuwa na uwezo wa kuanzisha viwanda vyao.

Dkt. Ntara aliongeza kuwa wakiungana watapata fursa ya wao kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo kuanzia ngazi za familia hadi taifa kutokana na wao kuwa wataalam wazuri wa matumizi ya fedha kidogo wanazopata.

Alisema kuwa mwanamke licha ya baadhi yao kutokwenda shule au kutopata fursa ya kusoma lakini bado Mungu amewajalia maarifa ambayo yanasaidia jamii kama vile kufahamu kuwa mtoto wake anaumwa wakati hajasomea udaktari, kufahamu umuhimu wa kilimo cha mboga mboga kuzungumza nyumba yake licha ya kutosomea ubwana au ubibi shamba, kuwa mtunza fedha mzuri licha ya kutosomea uhasibu.

Dkt. Ntara aliwasisitiza wanawake hao kuwa ni vema wakatumia tunu hiyo waliojaliwa katika kuunda vikundi mbalimbali katika maeneo yao na kuanzisha mradi ambapo utawasaidia wao na familia zao na hivyo kuonyesha kuwa wanawake wanaweza.

Alisema kuwa wakifanikiwa kuunda vikundi katika maeneo yao na vikaonekana havina matatizo atahakikisha kuwa anawabana Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa huu kuhakikisha kuwa wanawapatia ile asilimia tano kama ilivyoagizwa.

Dkt. Ntara aliwakubusha wanawake hao kuwa ni vema wanapouungana wakakumbuka kuwa mtaji sio fedha pekee bali ni pamoja na kuwa na elimu ya mradi unataka kuunzisha , kuwa na watu ambao unawalenga katika mradi wao na watakaoshiriki katika mradi huo.

Aidha, Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwaasa wanawake hao kuunda mtandao wa mawasiliaono kwa Halmashauri zote ili iwe kwao fursa ya kubadilishana uzoefu na kuwa rahisi kupata masoko.

Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi mkoani Tabora unalenga kusaidia kuongeza uelewa wa wanawake kiuchumi, kibiashara na upatikanaji wa mitaji.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA KUZINDUA MRADI WA MAJI KATIKA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora.

Taarifa hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wialaya ya Tabora Queen Mlozi imesema kuwa sherehe za uzinduzi wa mradi huo zitaanza asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Mwezi huo.

Amesema kuwa baada ya uzinduzi wa mradi huoi , Makamu wa Rais atapata fursa ya kuwahutubia wananchi na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabama.

Aidha , Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa viongozi wa dini zote, vyama vyote vya siasa, viongozi wa serikali na wananchi wa maeneo yaliyopo karibu na mradi huo kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza hotuba ya Makamu wa Rais.

Uzinduzi wa mradi huu utasaidia kuondoa tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaondole matatizo mbambali wananchi likiwemo la upatikanaji wa maji safi na salama.

Mradi huo wa maji ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan(JICA) umewezesha umesaidia uchimbaji wa visimana ujenzi mitandao ya mabomba katika eneo hilo wilayani Uyui.

RIP MY GUARDIAN ANGEL ISABELLA

$
0
0





































I do not pretend to be older than many but the truth is that, I'm old enough to confess that life is indeed a mystery.

I've seen a Landlord becoming a tenant of his former tenant before his death. 


I know a student who became the Vice Chancellor in his former University with most of his lecturers still teaching under him.


I have seen a rejected person becoming the bread winner for a whole community. A victor becoming a victim. A driver conductor buying the bus of his master. And A borrower recruiting his erstwhile credit bank manager. 




In life, no one knows tomorrow & you can never trust life, because it is mysterious. 


Never ever forget. U may not know the full story, Don't be quick to judge. Every coin has two sides. 


Treat everyone during your life time fairly like your own & love and forgive as much as you live. 


So let us be humble, kind, love more & do not try to be smart in anything; for we do not know what tomorrow holds for us.


Five years ago, on 28th April 2012, my Guardian Angel Isabella Benita Bulengo was laid to eternal rest at Makongo Juu, Dar es Salaam at the Age of 5 years. RIP! My Guardian Angel Isabella.

Fr. James Byebazo Rugemalira Rutakwabyera.

Rais Magufuli Awataka Watumishi 9932 Waliogushi Vyeti Kuondoka Maeneo Yao ya Kaz

$
0
0
Na Nuru Juma na Beatrice Lyimo-MAELEZO .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watumishi 9932 waliogushi vyeti, kuondoka maeneo yao ya kazi haraka iwezekanavyo kabla hawajadhibiwa kwa mujibu wa sheria. 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 

“Watumishi 9932 wenye vyeti vya kugushi na feki mishahara yao ya mwezi huu ikatwe na waondoke kazini mara moja na hizo nafasi zitangwazwe ili wasomi waweze kuziomba na majina yao yawekwe kwenye magazeti ili wajulikane” amesema Rais Magufuli 

Aidha amesema kuwa hadi kufika tarehe 15 Mei, 2017 kila mkuu wa Idara mahali pake pa kazi ahakikishe watumishi hao wameondoka na watakao kaidi agizo hilo amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia.
Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza kuwa watumisi 1538 wanaotumia cheti zaidi ya mtu mmoja kutopewa mshahara hadi pale itakapojulikana nani mwenye cheti halali na kuwataka watumishi 11,769 kuwasilisha vyeti vilivyopungua. 

Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana na masuala ya siasa kwa lengo la kujenga nchi kwani watanzania wanahitaji maendeleo. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kuwa mpaka sasa vyeti vilivyohakikiwa ni 435,000 ambapo imefanyika kwa awamu tatu iliyojumuisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali pamoja na Serikali Kuu. 

“Leo tunakabidhi taarifa ya awamu mbili iliyohusisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali ambapo imejumuisha uhakiki wa vyeti vya Kidato cha Nne, Sita, vyeti vya ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada” amesema Waziri Kairuki. 

Amesema kuwa matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yapo ya aina nne ambapo watumishi 376,969 sawa na asilimia 94.23 wanavyeti halali, watumishi 9932 asilimia 2.4 wanavyeti vya kugushi, watumishi 1538 asilimia 0.3 vyeti vyao vinatumika kwa zaidi ya mtu mmoja na watumishi 11,769 asilimia 2.8 wanavyeti pungufu. 

Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema wizara yake inakumbana na changamoto ya watumishi wa umma kugushi vyeti hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwani serikali imeziba njia zote za mkato za kuajiriwa na Serikali. 

“Leo tunaandika historia ya kipekee kwani suala la uhakiki wa yveti limefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndio yenye jukumu la kuhakiki uhalali wa vyeti hivyo” amesema Prof. Ndalichako. 

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma limeendeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 likiwa na lengo la kubaini uhalali wa vyeti kwa watumishi wake.

UTUMISHI YACHAGUA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2017

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru akitoa maelekezo ya kumchagua mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.
Wawakilishi wa wafanyakazi bora wa Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru wakishuhudia kura zikihesabiwa ili kumpata mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017 uliofanyika leo katika ofisi hiyo.

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA-TADB YAKOPESHA WAKULIMA WADOGO SHILINGI BILIONI 6.5

$
0
0
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

Mikoa mitatu ya Tanga, Morogoro na Iringa, imenufaika na kiasi cha shilingi bilioni 6.5 zilizotolewa kama mkopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali na msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Felister Aloyce Bura, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa huduma kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Dodoma.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Desemba, 2016, TADB imetoa mikopo ya jumla ya shilingi 6,489,521,120 kwa ajili ya kutekeleza miradi ishirini (20) ya kilimo katika mikoa hiyo mitatu ya Iringa, Morogoro na Tanga.

“Sambama na utoaji mikopo, Benki inatoa mafunzo kwa wakulima ambapo hadi sasa vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla ya wanachama 44,400 wamepatiwa mafunzo hayo katika mikoa hiyo mitatu” aliongeza Dkt. Kijaji

Amesema kuwa Benki hiyo inatarajia kuanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima wadogowadogo wa Mkoa wa Dodoma na mikoa mingine jirani wenye sifa.

“Benki imepata nafasi kwa ajili ya kufungua ofisi katika jengo la PSPF mjini Dodoma na itakabidhiwa ofisi hiyo mwezi Julai, 2017, baada ya mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo” Alisisitiza Dkt. Kijaji

Dkt. Kijaji amesema kuwa tayari Benki hiyo imemwandikia barua Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma ili kuomba aipatie miradi mizuri ya kilimo ambayo mkoa unapendekeza Benki iifikirie katika zoezi la kutoa mikopo itakayoanza kutolewa mwishoni mwa mwaka 2017.

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI KATIKA JAMHURI YA KOREA KWA MAFANIKIO

$
0
0


Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alifanya ziara ya kikazi jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 24 Aprili 2017 kwa mwaliko kutoka kwa Mhe. Yun Byung-se, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea. Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea mwaka 1992.

Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Yun Byung-se ambapo Waziri Mahiga aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kumpatia mwaliko wa kutembelea taifa hilo hususan wakati huu inapoadhimishwa jubilee ya miaka 25. Mhe. Mahiga aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuichagua Tanzania kuwa nchi ya kimkakati  katika uwekezaji kwa kipindi cha kuanzia 2016 -2020.

Kwa kipindi cha miaka 25, Serikali ya Korea imeisaidia Tanzania kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo Ujenzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi unaojumuisha madaraja matatu yenye jumla ya urefu wa meta 275  pamoja na barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 48; Ujenzi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 600 imejengwa na kufungwa vifaa tiba vya kisasa vya digitali, vinavyotumia zaidi teknolojia ya Tehama zikiwemo mashine za X-ray, MRI, CT-Scan, mashine maalum kwa ajili ya kupimia magonjwa ya wanawake. 

Vilevile, Ujenzi wa Hospitali ya mama na mtoto Chanika yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 160 inatarajiwa kufunguliwa siku za karibuni.Aidha, Watanzania zaidi ya 1000 wamenufaika kwa kupata ufadhili wa kusoma katika vyuo mbalimbali vya Jamhuri ya Korea.

Waziri Mahiga pia alikutana na baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Korea ambapo alitumia fursa hiyo kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania mathalani ujenzi wa Reli ya Kati katika viwango vya kimataifa; uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme; ujenzi wa maeneo ya viwanda; na huduma ya kutoa ushauri katika miradi mikubwa.

Aidha, Mhe. Waziri aliwahakikishia wawakilishi wa  makampuni ya Jamhuri ya Korea kuwa, Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji na biashara pamoja na taasisi muhimu zinazotoa huduma mbalimbali katika sekta hiyo. 

Wakati huo huo, Mhe. Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kukutana na Balozi Sul Kyung-hoon Makamu wa Rais wa KOICA ambapo aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuipatia zaidi misaada Tanzania kwa uwazi na bila ya masharti yeyote. Pia aliipongeza KOICA kwa kushirikisha jamii kuanzia wakati wa ubunifu wa mradi hadi kufikia utekelezaji pamoja na usimamizi. 
KOICA wameombwa kuongeza maeneo ya misaada na kujumuisha maeneo ya ujenzi wa miundombinu ya maji na nishati ya umeme wa jua, upepo na maji kwa ajili ya kusaidia maeneo ya vijijini. Aidha, Mhe. Waziri Mahiga alishauri KOICA kuangalia uwezekeno wa kuanzisha vituo vya kilimo cha kisasa, vituo vya kufugia na vituo vya kufundisha ujasiriamali ili jamii kubwa ya Watanzania iweze kunufaika.

Katika jitihada za kutafuta washirika kwa ajili ya kusaidia kuboresha Chuo cha Diplomasia, Mhe. Waziri akiwa Seoul alitembelea Chuo cha Taifa cha Diplomasia cha Jamhuri ya Korea na kufanya mazungumzo na Balozi Paik Ji-ah, Kaimu Mkuu wa Chuo. Lengo kuu lilikuwa kujifunza uendeshaji wa Chuo, mitaala iliyoandaliwa kutoa masomo, walengwa wa masomo hayo, aina ya wakufunzi, lugha zinazotumika kufundishia, utaratibu wa kuandaa wanadiplomasia na mifumo ya chuo hicho.

Vilevile kabla ya kuhitimisha ziara yake, Mhe. Waziri alikutana na Jumuiya ya Watanzania waishio Jamhuri ya Korea ambapo aliwahimiza kuheshimu Sheria na Taratibu za nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta utaalam utakaosaidia kuiendeleza Tanzania.

Aidha, akizungumza  na Watanzania hao ambao wengi wao ni wanafunzi, Mhe. Waziri aliwasihi kuzingatia masomo ili kufikia malengo waliyojiwekea na kuleta faida kwa familia zao na taifa kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri aliwahakikishia Wanajumuiya hao kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kufungua Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul na kuwaomba kutoa ushirikiano kwa Balozi wa kwanza wa Tanzania katika nchi hiyo. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 28 Aprili, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Yun Byung-se. Mhe. Mahiga alikuwa nchini humo kwa ziara ya kikazi ikiwa pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images