Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

RC NCHIMBI ABAINISHA KUSHINDWA KUMPATIA CHANJO MTOTO NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akitoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akifurahi mara baada ya kutoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.

………………………………………………………………………

Wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki za binadamu hasa haki ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za serikali za kupambana na maradhi, umaskini na ujinga.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida.

Dkt. Nchimbi amesema watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kupata chanjo zote ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini, surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, na pepopunda ambayo yanazuilika kwa chanjo na motto akiugua kupona ni nadra

“Mtoto akiumwa magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona anaweza kupata ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie kukamilisha chanjo zote” amesisita

Ameongeza kuwa serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote zinapatikana na hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha motto anapata chanjo pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale wasiowapeleka watoto kupata chanjo.

Akisoma taarifa ya hali ya chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Salum Manyatta amesema Mkoa wa Singida kwa sasa una chanjo zote zinazohitaji na zinatolewa katika vituo 197 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Dkt. Manyatta amesema kwa mkoa wa Singida wananchi wana uelewa wa chanjo ambapo kila mwaka zaidi ya asilimia 95 hufikiwa na chanjo karibia zote huku changamoto ikiwa ni katika kukamilisha chanjo ambazo huhitaji dozi zaaidi ya moja.

Ameongeza kuwa baadhi ya wazazi hujifungulia nje ya vituo vya kutolea huduma za afya mfano majumbani na hivyo kupelekea watoto kukosa chanjo za awali.

Dkt. Manyatta amesema katika kukabiliana na changamoto za baadhi ya watoto kukosa chanjo, jitihada zilizowekwa ni pamoja na kupitia kadi ya mtoto kuona endapo amekamilisha chanjo kabla hajapewa huduma nyingine za afya.

Jitihada nyingine ni viongozi wa serikali ngazi za vijiji kuandaa orodha ya watoto ambao hawajakamilisha chanjo na kuwafatilia wazazi au walezi wakamilishe chanjo hizo, kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa chanjo na kutoa huduma ya mkoba na kliniki tembezi ili kuwafikia watoto wanaoishi maeneo ya vijijini sana.

Kauli mbiu ya wiki ya chanjo mwaka huu ni “Chanjo Humkinga Kila Mtu, Pata Chanjo”.

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANZANIA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Gari maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri.
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.Picha na Ikulu.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MUUNGANO MJINI DODOMA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na mabalozi kutoka mataifa tofauti wanaowakilisha nchi zao.(PICHA NA OMR)
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mh. Ali Hassan Mwinyi kulia ni Kaimu Jaji Mkuu Mh. Profesa Ibrahim Hamisi Juma
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mh. Ali Hassan Mwinyi aliyeketi katikati na kulia ni Kaimu Jaji Mkuu Mh. Profesa Ibrahim Hamisi Juma
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Gadi ya “Komando” la vijana likiwajibika kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kwaya ya Makongoro kutoka mkoani Mwanza ikitumbuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kikosi cha Komandoo wa JWTZ kikitoa heshima kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO MJINI DODOMA

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Raisn Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na walioshiriki katika zoezi la kuchanganya udongo kuasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Gadi ya “Komando” la vijana likiwajibika kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Onesho la ndege vita kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Onesho la mbwa wa polisi kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Onesho la Komandoo wawili kuvuta lori la tani 7 kwa mikono kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kikosi cha Komandoo wa JWTZ kikitoa heshima kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma


PICHA NA IKULU

RAS –TABORA AWATAKA WACHIMBAJI MADINI WA KITUNDA KUJIKINGA NA VVU

0
0
Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora(RAS) Dkt. Thea Ntara amewataka Wachimbaji Wadogo wadogo waliopo eneo la Kitunda wilayani Sikonge kuzingatia matumizi mipira ya kufanyia mapenzi(condom) wanapoamua kufanya hivyo ili kujikinga na maambukizi yanayowekusababishia kupata Virusi vya UKIMWI.

Hatua hiyo itasaidia waweze kuendelea kuwa na afya nzuri itakayowasaidia kuishi maisha mengi na kukatiza ndogo zao.
Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana wilayani Sikonge wakati akitoa pole kuifuatia Maafa ya wachimbaji Saba wa madini katika eneo la Kitunda ambapo sita walikufa kwa kufukiwa na kifusi na mmoja alikufa kwa kukosa hewa.

Alisema kuwa umati wa wachimbaji ulipo katika eneoi hilo ni zaidi ya elfu kumi, hivyo ni vema wakatumia mipira kujikinga na UKIMWI wakati wakifanya mapenzi ili uwepo dhahabu hapo usije ukasababisha tatizo lingine katika jamii hiyo na ile inayowazunguka.

Dkt. Ntara alisema kuwa wachimbaji wengi katika eneo hilo bado wanaumri mdogo hivyo ni vema wakalinda afya zaidi ili wasiweze kutumbukia katika matatizo yatakayokazi maisha yao na kupoteza nguvu kazi ya Taifa ambayo bado inahitajika sana kwa maendeleo ya nchi hii.

Alisema kuwa ni vema wakatumia fursa hiyo ya uwepo wa dhahabu katika eneo hilo kwa kulinda na kuimarisha afya zao na sio kutumia fursa hiyo kutafuta matatizo ambayo wanaweza kujikinga nayo au kuyaepuka.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka baadhi vijana wenye tabia za kubaki kuachana na tabia hiyo bali wafuate taratibu za maridhiano zaidi ili kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI.

Alisema kuwa mtu anayetumia nguvu mara nyingi akumbuki kujikinga jambo ambalo linaweza kumsababishia yeye au mwenzake matatizo.

Katika hatua nyingine RAS huyo ameaagiza Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge Daktari Mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha wanapeleka kwa wingi mipira ya kiume ya kufanyia mapenzi katika eneo hilo la wachimbaji madini wadogo ili kuwakinga na maambukizi mapya ya VVU.

Alisema kuwa eneo lina wanchi wengi , hivyo ni vema wakapelekewa vifaa vya kujilinda ili waendelee kuwa na afya bora ambazo zitawasaidia wao kujitafutia kipato halali na kuchangia katika ujenzi wa nchi kwa njia mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi.

Dkt. Ntara aliwaagiza pia viongozi hao kupeleka huduma mbalimbali kama vile za kufungua Zahanati, Mtaalamu wa Afya, kufungua Shule ya Awali kwa ajili kukabiliana na wingi wa watu katika eneo hilo ili nao kama walivyo wananchi wapate fursa za huduma za jamii kwa karibu.

Alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa juu ya kujilinda na magonjwa ya mlipuko kama vile kipundupindu , na pia kuwapa matibabu pindi wanapokuwa na magonjwa mbalimbali kama vile malaria.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka wachimbaji madini hao kuzingatia usafi ili wasije wakapata maambukizi ya kipindupindu.Alisema kuwa eneo hilo linawananchi wengine endapo usafi usipozingatiwa upo uwekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora amewataka vijana wote walipo katika eneo ambao hawajafanya tohara kufanya hivyo ili kuimarisha afya zao na kujikinga na magonjwa ambayo yanasababisha na wanaume kutofanya hivyo.

Alisema kuwa huduma hizo zinatolewa katika Hospitali nyingi ni vema wakachangamkia fursa hiyo.

MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA KAZINI 2017 MKOANI KILIMANJARO

0
0


Maonesho ya wiki ya usalama na afya kazini yameanza leo siku ya Jumatano tarehe 26/04/2017 katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimepata fursa ya kuonyesha namna zinavyozingatia masuala ya usalama na afya kazini kwa wafanyakazi wao. 

Miongoni mwa taasisi zilizopata fursa ya kushiriki maonyesho hayo kwa mwaka huu ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini za Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara ambazo zinamilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.

Ambapo katika maonesho hayo migodi hiyo ya imekuwa ikionesha vifaa mbalimbali vya uokozi pamoja pamoja na mbinu zitumikazo kuhakikisha mazingira ya usalama kwa wafanyakazi wao wawapo kazini.

Maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi yameandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakiwa na kauli mbiu ya “ Ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za usalama na afya” .Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele chake Aprili 28,2017.

Zifuatazo ni picha mbalimbali wakati wa maonesho hayo siku ya kwanza Aprili 26,2017
Banda la mgodi wa Bulyanhulu-Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiandaa kupokea wageni mbalimbali 
Maandalizi yanaendelea
Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu 
Msaidizi wa Meneja Mkuu wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Margaret Mandia akimkaribisha Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato akifurahia jambo baada ya kufika katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akimwelezea Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato namna mgodi huo unavyotunza mazingira na kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo yao ya kazi
Afisa Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akitoa ufafanuzi kwa mwananchi aliyefika katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa uhakiki wa usalama kutoka mgodi wa Bulyanhulu Amina Mohamed akimwelezea kuhusu masuala ya usalama mgodini kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda hilo
Afisa Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akitoa maelezo kwa maafisa kutoka shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) waliotembelea banda hilo
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu 
Afisa rasilimali watu mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akiwaelezea watalii kuhusu DVD ya Bulyanhulu inayohusu usalama mgodini na mahusiano ya jamii 
Afisa viwango vya usalama mgodi wa Bulyanhulu Setieli Kimaro akitoa elimu kuhusu mambo ya usalama mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la la mgodi wa Bulyanhulu
Mdau kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds Limited Gamba Isack akiangalia bango kubwa lililopo katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu 
Afisa afya mgodi wa Bulyanhulu Tumaini Sylvanus akielezea kuhusu masuala ya afya mgodini
Afisa Mahusiano mgodi wa Bulyanhulu William Chungu akifurahia jambo na mwananchi aliyembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu
Mhandisi wa uchimbaji mgodi wa Bulyanhulu Fikiri Thomas akiwaonesha wananchi namna wanavyochimba madini
Banda la mgodi wa Buzwagi- Maafisa kutoka mgodi wa Buzwagi wakijiandaa kwa ajili ya maonesho
Nje ya banda la mgodi wa Buzwagi
Mkufunzi Idara ya Uokozi mgodi wa Buzwagi Azaeli Kitange akitoa elimu kuhusu usalama mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Maandalizi yanaendelea
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akiwaelezea wananchi kuhusu namna mgodi huo unavyojitahidi kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa salama mgodini
Mwananchi akiuliza swali kwa maafisa kutoka mgodi wa Buzwagi
Mkufunzi Idara ya Uokozi mgodi wa Buzwagi Azaeli Kitange akimwonesha mwananchi aliyetembelea banda la mgodi huo vifaa vinavyotumika katika uokoaji mgodini
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa somo kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akimwelezea mwananchi namna mgodi huo unavyojitahidi kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa salama kazini

Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akiendelea kutoa elimu kwa wananchi
Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akieleza jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akitoa elimu ya usalama kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi huo
Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akielezea masuala ya afya kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi 
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Buzwagi 
Banda la Mgodi wa North Mara- Maafisa kutoka mgodi wa North Mara wakijiandaa kuanza kufanya maonesho 
Afisa usalama mgodi wa North Mara Samwel Nyansika akimwelezea masuala ya usalama mgodini mwananchi aliyetembelea banda hilo 
Kulia ni Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akiwaeleza wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya mgodini 
Kiongozi wa awali Idara ya Mahusiano mgodi wa North Mara Annamaria Baisi akitoa somo kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi huo 
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akimwonesha mwananchi kifaa kinachotumika kubaini ulevi kwa wafanyakazi wanaoweza kufika kazini huku wamelewa 
Afisa usalama na afya mgodi wa North Mara Athanas Fredrick akiwaelezea masuala ya usalama mgodini wanafunzi waliotembelea banda la mgodi huo 
Mwananchi akitembelea banda na mgodi wa North Mara 
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi waliotembelea katika banda hilo 
Afisa Mazingira mgodi wa North Mara Sara Cyprian akimwelezea mwanannchi namna mgodi huo unavyotunza mazingira 

Afisa usalama na afya mgodi wa North Mara Alfred Mwema akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo 
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akimpima kilevi mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo wakati akiwaelezea namna wanavyopima wafanyakazi mgodini 
Kiongozi Idara ya Mahusiano Jamii mgodi wa North Mara Fatuma Mssumi akielezea masuala mbalimbali kuhusu mgodi huo katika kuimarisha afya na usalama kazini. 


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO , SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO

0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo Jijini Arusha,Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqarro.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Meru wakiimba wimbo wa Taifa kama picha hapo juu inavyoonekana wakiongozwa na mwalimu Neema Lema ,na hii inayofuata hapa chini wakiongozwa na mtafsiri na mwalimu Viola Wilson .Picha na Vero Ignatus Blog
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia kwa makini kile ambacho mtoto mwenye ulemavu Amina kutoka shule ya msingi Meru akitumia kompyuta katika kuhariri video aliyoichagua,aliyeshika kipazasauti ni mtaalam wa masomo ya Tehama katika kitengo cha walemavu bi.Betha Denis.Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amtembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu  katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa. 

Akiwa katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68 miongoni mwao wasichana wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo. 

Akisoma risala mbele ya Mkuu huyo wa mkoa  mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,384 wavulana wakiwa ni 709 na wasichana wakiwa ni 675

Amesema shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya  Finland walioshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili wakichangia zaidi ya sh, milioni 180  huku fedha hiyo ikisaidia kujenga jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop) 184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya Laminationi na printa 4.

Pia vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo

Gambo alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi 

Awali Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veola Wilson na Neema Lema 

Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua kero zao
 Gambo amewaagiza watumishi wa  jiji la Arusha wakiwemo wataalam wa vitengo mbalimbali  kuhakikisha wanatatua kero za wananchi haraka iwezekanavyo ili kuondokana na kero zinazowakabili.
 Miradi iliyokaguliwa ni pamoja   na  Visima viwili  vya maji vilivyoko magereza vilivyogharimu milioni 372, madarasa 6 Shule ya msingi Olasity,madarasa 4 ya Shule ya msingi Burka Estate ambayo yamegaharimu jumla ya  shilingi 218 milioni .

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 27,2017

0
0

MAGUFULI:MTANZANIA ALINDE NA KUIMARISHA MUUNGANO

0
0

Kila mtanzania ametakiwa kuhakikisha anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa miaka 53 iliyopita.

Akizungumza leo wakati akihutubia wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa ni muhimu watanzania wakalinda Muungano kwa vile una manufaa kwa nchi zote mbili.

“Kila mtanzania ahakikishe anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wetu, kwa vile Muungano na amani iliyopo nchini ndio chachu ya maendeleo yetu” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa “Muungano ndio silaha yetu, ni nguvu yetu, mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa nguvu zote na yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” alisema Rais Magufuli

Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika miaka 53 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni pamoja na kuunganisha mataifa mawili na kuunda taifa moja lenye nguvu.

Rais Magufuli alitaja mafanikio mengine ni pamoja na kuwa ni kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini, nchi kavu na reli, kukabiliana na matatizo ya umaskini, ukosefu wa ajira na kukua kwa uhusiano wa diplomasia kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali ambapo yamepelekea mafanikio katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, na jamii.

Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa sherehe za Maadhimisho ya Muungano kufanyika mkoani Dodoma ambapo, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kujenga miundombinu ili kufikia azma yake ya kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma ifikapo mwaka 2020.

“Niwahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi nyuma tena,ambapo awamu ya kwanza ya watumishi wa Serikali takribani 3,000 kwa ngazi za Mawaziri,Naibu Waziri,Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wameshahamia Dodoma, kama tulivyoahidi kufikia mwaka 2020, Serikali yote itakuwa imehamia hapa”, alisisitiza Rais Magufuli.

Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano zenye kauli mbiu isemayo “Miaka 53 ya Muungano, tuulinde na kuimarisha, tupige vita dawa za kulevya na kufanyakazi kwa bidii”, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano ambapo ni Mama Maria Nyerere na Mama Shadya Karume.

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU IKOLOJIA YA MTO RUAHA CHATEMBELEA BONDE LA IHEFU

0
0
 Wajumbe wa Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha (kikundi namba 2) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisubiri kupanda boti ya upepo ili kutembelea eneo la bonde la Ihefu lililoko Mbalari- Mkoani Mbeya kugagua ikolojia ya Bonde hilo.
 Wajumbe wa Kikosi kazi wakiwa ndani ya boti katikakti ya bonde la Ihefu wakiakagua ikolojia ya bonde hilo. Kuanzia kulia ni Mkurugenzi Tume ya Umwagiliaji Injinia Seth Lusweme, Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi na Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji Idris Msuya.
 Afisa Mkuu toka TANAPA Kanda ya Arusha Vitalis Uruki akiongea na Wanahabari mara baada ya ziara ya kikosi kazi katika bonde la Ihefu katika Wilaya ya Mbalari Mkoani Mbeya.
Picha ikionyesha hali ya ikolojia katika bonde la Ihefu inavyoonekana kwa sasa

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI

0
0

Mohammad Al Bulooki, Makamu wa Rais Mtendaji wa Kitengo cha biashara cha Shirika la ndege la Etihad; Mhe. Saif Saeed Ghobash, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Utalii na Utamaduni (TCA) Abu Dhabi, Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege la Etihad wakisheherekea uzinduzi wa ndege shindano la masaa 48 la kuitangaza Abu Dhabi katika Soko la usafiri la Uarabuni.

Msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson akiruka matuta ya jangwa la Abudhabi wakati aliposhiriki shindano lililozinduliwa na Etihad la masaa 48 ili kuitangaza Abudhabi kwa wasafiri wake.



Wakazi wa Nchi ya Falme za Kiarabu na wasafiri wa kimataifa watajionea maeneo mbalimbali ya vivutio vinavyopatikana Abu Dhabi kwa siku mbili tu.

vShirika la Ndege limezindua shindano hilo kwenye Instagram na zawadi zaidi ya 500 zitashindaniwa.

Shirika la Ndege la Etihad limeamua kuwazawadia mamilioni ya wageni wanaosafiri kupitia makao makuu pamoja na wakazi wa nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuleta shindano linalofanyika angalau mara moja kwa mwaka na kuwahusisha watu wote kwa siku mbili.

Kampeni hiyo ya 48 Hour Challenge ni sehemu ya shughuli za Etihad katika kupanua wigo wa kuitangaza Abu Dhabi kama sehemu nzuri ya mapumziko kwa wasafiri na watu wanaopenda kuishi katika nchi ya Falme za Kiarabu hasa wanaopenda kutembelea wakati wa likizo fupi. Wakiwa kwenye jiji hilo watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yameandaliwa kupitia programu hiyo.

Kampeni hiyo ya Shirika la Ndege la Etihad itazinduliwa na msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson ambaye atatangaza jinsi watu wanavyoweza kunufaika na ofa hiyo ya saa 48 wakiwa Abu Dhabi.

Baadhi ya video zake zitaonyesha ofa katika maeneo ya vivutio vya Abu Dhabi. Pia, video za kampeni hiyo zitaonekana kupitia mtandao ambapo wateja watashare na wenzao katika mitandao ya kijamii. Pia wataweza kuona kupitia chaneli za kwenye ndege wanaposafiri.

Wilson alisema, “Kwangu mimi nilijua hii inaamanisha kukaa uwanja wa ndege, au kusafiri bure lakini sivyo kampeni hiyo inavyomaanisha.”

“Mtu atapata fursa ya kusafiri katika ukanda wa jangwa ikiwa ni pamoja na kutembela maeneo ya kuvutia ya kiutamaduni. Abu Dhabi imenifunza kuwa kutembelea maeneo mbalimbali nikiwa safarini ni sehemu mojawapo ya kuburudika. Hii inaweza kuwa ni miongoni mwa njia nzuri za kupumzika na kujiweka katika hali ya kujisikia vyema. Vilevile nimepata muda wa kujionea mambo mengi kwenye nchi hii. Niwapo safarini sitarudia tena kukaa tu uwanjani na kusubiri ndege tu.”

“Abu Dhabi ni sehemu nzuri, yenye joto kiasi na watu wake wenye ukaribu wa hali ya juu. Mji huu una kila kitu kinachohusiana na mapumziko. Kuna sehemu tulivu na maeneo mazuri ya kutembelea. Ni mji unaovutia na kupendeza ambao una vitu vya kipekee unavyoweza kujionea kwa muda mfupi na kwa wakati.”

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Kuzinduliwa kwa programu hii ya Shirika la Ndege la Etihad kutawawezesha watu kutembelea maeneo mbalimbali wakati wakisubiri kusafiri.
Pia itahamasisha watu kujua zaidi kuhusu jiji hili tunaloishi na kufahamu mambo mengi yanayohusu Abu Dhabi pamoja na kuona fursa zilizopo hususan kwa wageni katika masuala ya utamaduni na maeneo ya kupumzika katika fukwe.”

Alisema, “Ni heshima kwa shirika letu la kitaifa la Falme za Nchi ya Kiarabu ambalo makao makuu yake yapo hapa Abu Dhabi, kutokana na kuwapo kwa miundombinu mizuri, ukarimu kwa watu wake na mazingira mazuri ya kuvutia. Hii ni sehemu nzuri ya kutembelea kwa wote wanaosafiri kupitia Abu Dhabi na pia tumewapa fursa hata wale wanaoishi hapa.”
Shirika hilo limetumia fursa ya kujitangaza kutokakana na kuwepo uzinduzi wa Soko la Usafirishaji Uarabuni. Etihad imebuni mashindano hayo maalumu kwa lengo la kujitangaza.

Kwa mwaka huu mzima wa 2017, Shirika la Ndege la Etihad litatoa jumla ya zawadi 500 na wale ambao watashiriki kampeni ya 48 Hour Challenge watatuma hashtag ya #EtihadChallenge kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Shirika la ndege la Etihad limechagua hoteli mbili Abu Dhabi pamoja na maeneo ya shughuli mbalimbali. Wateja watajishindia kulala usiku mara mbili kutoka kwenye hoteli 60 Abu Dhabi na wengine watajishindia kulala usiku mmoja bure.
Wateja wa daraja la kwanza watapata nafsi kulala bure wakati wateja wa daraja la juu watapata nafasi ya kulala siku mbuli bure.

Wateja wanaotumia ndege ya Airbus A380s watazawadiwa kulala mara mbili usiku katika hoteli ya kisasa ya Emirates Palace.

Abu Dhabi ambayo ndiyo kitovu cha maeneo mazuri ya kupumzika na eneo lenye vivutio vingi vya kibiashara ulimwenguni, kuna eneo kubwa lenye mchanga wa ufukweni, maeneo ya utalii kama vile Yas Waterworld na Ferrari World ikiwa na pamoja na jangwa lenye historia ya kipekee. Pia taasisi ya utamaduni kama vile Manarat Al Saadiyat na hivi karibuni makumbusho ya Louvre yatafunguliwa
Kuna maeneo ya kihostoria, migawaha ya kimataifa, maeneo ya michezo ya gofu, mbio za magari maarufu Fomula 1 Etihad Airways Abu Dhabo Grand Prix na mashindano mengine ya magari ya Yas Marina Circuit.


Abu Dhabi pia inatoa fursa kwa wageni kufanya manunuzi katika maduka makubwa na maarufu. Pia, utapata nafasi ya kuchagua bidhaa kwenye maduka makubwa kama vile Yas Mall, Abu Dhabi MALL, Marina Mall na The Galleria ambayo ni miongoni mwa eneo kubwa ulimwenguni kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa.

Rick Wilson amefanikiwa kumaliza kufanya shughuli zifuatazo kwenye kampeni hii ya Abu Dhabi 48 hours Challenge;-
·        Ametembelea maeneo muhimu ya slingshot
·        Ameshiriki mashindano ya magari
·        Amejionea mashindano ya Formula 1 track
·        Amejionea maporomoko ya maji ya Yas Waterworld
·        Amenunua bidhaa kwenye maduka makubwa
·        Amefurahia kupata kifungua kinywa katika jengo la Etihad Towers
·        Amejionea mchanga wa jangwani
·        Amekula vyakula vya kiasili
·        Amepanda ngamia
·        Amejifunza namna ya kucheza
·        Ametembelea jangwa
·        Amelala kwenye hoteli ya nyota tano
·        Amefika kwenye ufukwe wa Saadiyat Golf Club
·        Ameendesha gari kwenye mashindano ya Formula Rossa, Ferrari World Abu Dhabi
·        Amekula kwenye migahawa ya kiutamaduni
·        Ametembelea Msikiti wa Sheikh Zayed Grand
·        Ametembelea Iris Yas Island
·        Amefika Yas Viceroy

Video ya Ricky Wilson’s 48 Hour Challenge unaweza kuitazama: https://www.youtube.com/watch?v=lhZgRWOQQrw

Unaweza kupata picha za matukio hapa https://we.tl/xXrIF1vBf4 

Kwa maelezo zaidi kuhusu shindano hilo la Etihad Airways’ stopover tembelea:www.etihad.com/abudhabi

WAKAZI WA TABORA WANAOKWENDA KITETE WAONDOKA NA ADHA YA SEHEMU YA KUKAA

0
0
 Tiganya Vincent, RS-Tabora

 Wananchi wa Mkoa wa Tabora wanakwenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya kunyeshewa mvua na kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la Mahali pa Kungonjea kuona wagonjwa.
 
Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.
 
Uzinduzi huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi wakati wa sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo Kitete.
 
Alisema kuwa kukamilika  kwa jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha muda mrefu cha viongozi na wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu kupumuzika wakati wakisubiri muda wa kuona wagonjwa wao wanapata matibabu katika Hosptali hiyo.

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na gharama nafuu.
 
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia miradi.
 
Alisema kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo zilizosaidia kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi hao na hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando ya barabara.
 
 

Sekta binafsi yajipanga kukutana na Rais kwenye Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara- TNBC

0
0
WADAU wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu. 

Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini - TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu, ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Akiwakaribisha wadau wa Sekta Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi hawakomoani, ndio maana TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili kulifikisha taifa kwenye uchumi wa viwanda.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano wa ndani ulioambatana na chakula cha jioni kilichoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi.

Dk Mengi pia alisema serikali na sekta binafsi wana malengo yanayofanana ya kutokomeza umaskini na kutengeneza ajira kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kutekelezeka kwa urahisi iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu baina ya serikali na Sekta Binafsi. Katibu Mtendaji wa TNBC Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utakuwa ni fursa nzuri kwa serikali na sekta binafsi kubadilishana mawazo kuhusu wajibu wa kila upande katika kuboresha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini ili kukuza uchumi wa nchi. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akijitambulisha katika mkutano huo. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano ulioambatana na hafla ya chakula cha jioni uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi.. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiendelea na mazungumzo na wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano huo ulioambatana na chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi akifafanua jambo katika mkutano wa ndani ambao ni sehemu ya kujiandaa kukutana na serikali chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) linalotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Mei jijini Dar es Salaam.. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakati mkutano huo ukiendelea.. Mkutano ukiendelea.

KAWAIDA WADAU wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu. Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini - TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu, ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. 

 Akiwakaribisha wadau wa Sekta Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi hawakomoani, ndio maana TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili kulifikisha taifa kwenye uchumi wa viwanda.

TGGA YAZINDUA UPANDAJI MITI 600 KILA MKOA TANZANIA

0
0
 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. PICHA NA JOHN BANDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


John Banda, Dodoma

CHAMA cha Tanzania Girl Guides (TGGA) kimezindua mradi wa upandaji miti kitaifa katika Shule ya Msingi ya Mtumba Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides nchini, Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshaanza upandaji wa miti hiyo katika mikoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza

Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.

Naye Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa, Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Guides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika hilo zinafaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye rutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali   


 Wanachama wa Tanzania Girl Guides wakichimba moja ya mashimo ya kupanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba Manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti katika shule mbalimbali nchini.
 Wanafunzi wanachama wa TGGA
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya kabila la Wagogo wakati wa uzinduzi wa upandaji miti shuleni hapo
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika kitaifa shuleni hapo juzi.


 Mwenyekiti wa TGGA, Marha Qorro akimwagilia mti baada ya kuupanda


 Viongozi na wanachama wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja
 Viongozi wa TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma
 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa TGGA
Wanafunzi wanachama wa TGGA wakiwa na miche ili waendelee na zoezi la kupanda miti shuleni hapo

RAIS DKT MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMSHO YA SIKU YA UHURU WA HABARI

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamio.

Rais wa Jamuhuri y Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari Mei mwaka huu.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu, yatafanyikia jijini Mwanza kwa Siku mbili mfululizo kuanzia Mei 2 na 3 mwaka huu yakiwa na maudhui yanayosema fikra yakinifu kwa wakati muhimu'.

Akizungumzia madhimisho hayo, Mwenyekiti wa Misa Tanzania Salome Kitomary amesema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha wadau wa Habari kuweka msukomo wa mataifa kutunga sheria za vyombo vya habari ambazo zinahakikisha Uhuru wa habari katika nchi husika.

Amesema lengo lingine ni kufikia makubaliano ya kitaifa juu ya kuanzisha utaratibu wa usalama na ulinzi wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mtandao na nje ya mtandao.

Aidha Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutetea Sera na mfumo wa mageuzi ya kisheria kwa ajili ya vyombo vya Habari na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake makamu wa rais kutoka umoja wa clabu za waandishi Tanzania, UTPC, Janne Mihanji amewataka waandishi wawe ndio wapangaji wa ajenda za taifa badala ya kutumiwa na wanasiasa.

Aidha amewaasa waandishi wakiwa katika maeneo yao kazi, kuchukua tahadhari wakiangalia usalama wao zaidi kwani hakuna habari bora kuliko uhai wa mtu mwenyewe.

LINK-JARIDA LA NCHI YETU-MUUNGANO EDITION

0
0

Airtel yatumia Teknolojia ya mawasiliano kuboresha elimu ya sekondari

0
0
Tabora Aprili 26, 2017, KATIKA kutimiza dhamira ya kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kuendeleza jamii, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani imeanzisha mpango utakaowawezesha wanafunzi wa sekondari kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao wao wa intaneti

Mafunzo hayo kwa kupitia mtandao yanayojulikana kama“Studi Academy” yanapatikana kupitia mtandao wa Airtel wa 3G. ambapo katika kijiji cha Mbola Mkoani Tabora Airtel kwa kushirikiana na Erickson wameboresha zaidi mawasiliano ya intaneti ya kasi ya 3G ili kuhakikisha kuwa shule na vituo vya huduma za afya zinafaidika na mpango huu kabambe kwa kuinua upatikanaji wa huduma za masomo kupitia mtandao na kuanza kuwafaidisha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu.

Akiongelea ujio na mafanikio ya mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya Lolangulu , Cleophas Bugomba alisema” Shule yetu imekuwa na changamoto ya walimu wa kutosha kwa masomo ya sayansi hivyo kuwepo kwa masomo haya kupitia mtandao kumesaidia kupunguza changamoto hii kwa kiasi kikubwa. Mafanikio haya tumeyaona kupitia matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili ambapo ufaulu wa wanafunzi hususani katika masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na fizikia umekuwa wa kiwango kikubwa pamoja nakuwepo kwa changamoto hizi za walimu wa kutosha wa masomo hayo”.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kitado cha tatu mwaka 2017 Irene Tamson ambayo pia ni mwanafunzi bora wa kike aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa mkoa wa Tabora alisema” mpango huu wa “Studi Academy” unaowezeshwa na intaneti ya Airtel umenisaidia sana kufanya maswali mbalimbali na kupata majibu sahihi hapo hapo, kujifunza vitu vipya na kupata nyezo muhimu pindi nikijisomea binafsi au kwa makundi. Tunafurahi kuweza kunganishwa na mtandao na kujifunza kutoka kwa wengine kutoka nchi za ulaya lakini pia kupata nyenzo muhimu za kujifunzia kwanjia ya technologia ya kisasa.”

Nae Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema, “tunajisikia fahari kuwa na mtandao bora unaotuwezesha kutoa huduma kwa jamii ikiwemo mpango huu wa Studi Academy, lengo letu Airtel ni kutoa suluhisho kupitia teknolojia ya mtandao ili kuwafikia watanzania wengi zaidi ili wapate mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kwa maeneo ya pembezoni”.

Mipango na dhamira yetu Airtel ni kuendelea kushirikiana na wadau wetu kama Ericsson na Health kutumia fursa ya mawasiliano kuiwezesha jamii kwa kurahisisha baadhi ya changamoto za elimu na afya,”. Alieleza Bi Bayumi

Airtel Tanzania pia kupitia mpango wake wa kuendelea kutoa mawasiliano bora kwa kuzingatia ubunifu mwaka jana ( 2016) walishirikiana na VETA na kuzindua Applikesheni kabambe ya VSOMO ili kuwawezesha watanzania nchini kote kujisomea kozi za ufundi stadi kutoka kwenye vyuo vya Ufundi VETA kupitia simu za mkononi ili kutoa fursa kwa watanzania nchini kujiendeleza kielimu bila kujali changamoto zinazosababishwa na mazingira au ukosefu wa vifaa vyakujisomea karibu nao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu iliyopo kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakisoma kwa kupitia njia ya mtandao baada ya Airtel kwa kushirikiana na Erickson pamoja na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani  kuwawezesha wanafunzi hao kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao kwa kupitia mpango ujulikanao kama “Studi Academy”.

TAMASHA LA BODABODA KUFANYIKA MEI 13

0
0
Nuru Juma na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
MAKAMPUNI ya JP Decaux pamoja na International Republican Institute (IRI) yameandaa Tamasha la waendesha pikipiki linalotarajia kufanyika Mei 13 mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Parkers Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JP Decaux, Shaban Makugaya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
“Lengo la tamasha hili ni kuweka uamsho, msisitizo na kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa dhumuni la kuzingatia sheria za usalama kwa matumizi ya barabara pamoja na kudumisha umoja, ushirikiano na mshikamano katika jamii”. Alisema Makugaya.bodaBodaAidha, Makugaya amesema kuwa, tamasha hilo ni la kwanza kufanyika nchini na Kampuni hiyo imejipanga kulifanya kila mwaka nchi nzima ambapo jina la maonesho litabadilika kulingana na mji au mkoa ambao tamasha litafanyika.
Aliongeza kuwa usafiri wa pikipiki umekua njia rahisi za kumuwezesha msafiri kufika haraka hivyo mashirika hayo yameamua kuwakutanisha madereva hao na kuwapa elimu ya usalama barabarani ili waweze kuepuka ajali za barabarani zinazosababisha vifo vya watanzania wengi.
Akifafanua zaidi, Mkurugenzi huyo amesema kuwa waendesha bodaboda watakaoshiriki katika tamasha hilo ni lazima wawe na leseni na watoke katika vikundi vyao vilivyosajiliwa na kutambulika kisheria.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya JP Decaux, Elia Moshi amesema tamasha hilo litahusisha michezo mbalimbali ikiwemo ya soka kati ya timu ya trafiki na waendesha pikipiki, burudani ya mziki wa kizazi kipya, taarabu na singeli pia zitakuwepo ili kuboresha tamasha hilo.
“Tamasha hili litafayika mkoani Dar es Saaam pekee na linatarajia ushiriki wa watu kati ya 5000 na kuendelea ambapo mshindi wa kwanza atajipatia pikipiki pamoja na fedha taslimu na kutakua na zawadi zingine kwa ajili ya washindi wengine pamoja na washiriki,” alisema Moshi.
Bodaboda Superstar ni onesho linalojumuisha burudani na elimu ambalo limelenga kuwaleta pamoja waendesha pikipiki na wananchi ambapo Kauli mbiu ya tamasha hilo ni ‘Sote ni Ndugu’.

WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE.

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.


Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu  Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.


“Makampuni haya yana wajibu mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi,kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa kazi.”Aliongeza Mhe.Mavunde.


Aidha amesema Ofisi yake imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Sheria kwa kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia matakwa ya Sheria,elimu ya Sheria za kazi inatolewa kwa waajiri,wafanyakazi na vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza Sheria.


Kuhusu ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini amesema  Serikali iliunda kikosi ambacho kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,NSSF,SSRA,OSHA ,Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.


Amesema kikosi kazi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa na kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa Sheria za kazi,afya na usalama mahali pa kazi,masuala ya hifadhi ya jamii,fedha na kodi.


Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali inatambua umhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za ajira kwa watanzania na kuchangia kukua uchumi kwa ujumla.


“Serikali itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwekeza na kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini”Alisisitiza Mhe.Mavunde.

TANZANIA NI TAJIRI YA MAUDHUI YA FILAMU,WASANII TUWE WABUNIFU-RAIS WA TAFF

0
0
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images