Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1211 | 1212 | (Page 1213) | 1214 | 1215 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Nuru Juma na Husna Saidi-MAELEZO

  Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Nafaka umeanzisha Kampeni ya Kijana Inuka na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwa lengo la kuepukana na kilimo cha mvua na vijana waweze kujiajiri wenyewe.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Wilaya ya Temeke Joseph Kunguru alipokutana na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

  Kunguru alisema kuwa kilimo hicho ni kilimo biashara na kinahitaji maji na miundombinu ya uhakika ili kuwafanya wananchi kulima kilimo chenye tija badala ya kulima kwa kutegemea mvua.

  “Kilimo hiki kinaonekana ni kilimo ghari sana kwani ujenzi wa Green House unaonekana ni kilimo cha watu wenye pesa lakini ukweli ni kwamba wananchi wakiungana pamoja katika kilimo hiki wanaweza kufanikiwa badala ya kulima kwa kutegemea mvua,” alisema Kunguru.

  Aidha alisema kuwa vijana wengi mtaani hawana ajira hivyo viongozi kupitia kampeni hii watumie fursa hiyo kuwaelimisha kuhusiana na kilimo hiki cha umwagiliaji ili waweze kujiajiri wenyewe.

  Umoja huo wa kilimo cha Mbogamboga na Matunda na Nafaka umesajiliwa kisheria na ulianza na wanachama 17 mpaka sasa wapo 100 ila wanachama hai wapo 74 hivyo wanawasihi wananchi waendelee kujitokeza kujiunga.

  Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hicho Sifa Karuka alisema alihamasika kujiunga na kikundi hicho baada ya kupata taarifa kuhusu kilimo hicho cha kisasa licha ya kuwa na shughuli zake binafsi hivyo anawasihi wakinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

  Nae Diwani wa Kata ya Buza James Raphael Mkude aliwahamasisha madiwani wenzie kuweza kuunda vikundi kama hivyo katika kata zao ili wananchi wao hasa vijana wasiokuwa na ajira waweze kujikwamua kiuchumi.

  Kikundi hicho kimeiomba Serikali kupitia Maofisa Ugani kutoa mafunzo kwa vijana ambao hawana ajira kuhusiana nakilimo hicho ili kupunguza ukosefu wa ajira kwa kujitegemea wao wenyewe. 
  Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga Wilaya ya Temeke, Joseph Kunguru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya kuwahamasisha Vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Buza, Manispaa ya Temeke, James Raphael Mkude na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Waziri Pembe Waziri.
  Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Raphael Mkude akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana Kampeni ya kuwahamasisha vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa umakini mkutano baina yao na viongozi wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Husna Saidi – MAELEZO. 

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt BILINITH MAHENGE ameamua kutema cheche kwa Maafisa kilimo wazembe ambao hawajui majukumu yao habari kamili hii hapa chini

  0 0

  Na Husna Saidi na Nuru Juma- MAELEZO

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

  Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Edward Kichere wakati wa mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku za Jumatatu saa moja kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.

  Kichere alisema, mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.

  Aliendelea kwa kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

  Alisema kuwa TRA ina waajiriwa wapya ambao wamepewa mafuzo ya miezi sita katika chuo cha kodi juu ya mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa moja na mamlaka hiyo kwaajili ya kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.

  “Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbasli kama vile Tigo Pesa , Airtel Money na MPesa ili kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” alisema Kichere.

  Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.

  Aidha Kichere alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria bila kutumia nguvu au uonevu wowote.

  Hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi ili kuleat maendeleo nchini.

  0 0  0 0

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt, Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kuzungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akizunguza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Farouk Karim akiuliza swali katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari katika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
  Meneja Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Issa Khamis akijibu maswali ya waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya malaria yaliyoadhimishwa kwa mkutano wa waandishi wa habari Wizara ya Afya Zanzibar .Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

  Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema pamoja na mafanikio makubwa katika kupambana na Malari Zanzibar, bado shehia tano zinaendelea kutoa wagonjwa wa maradhi hayo zaidi ya asilimia tano.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja, amezitaja shehia hizo kuwa ni Tumbatu Jongowe, Miwani, Micheweni, Chukwani na Kiwengwa.

  Hata hivyo amesema maambukizi ya malaria katika maeneo hayo yanasababishwa na wasafiri wanaoingia na kutoaka nje ya Zanzibar mara kwa mara ambapo mwaka jana asilimia 55 ya wagonjwa waliogundulika walikuwa na tabia hiyo.

  Amesema takwimu za Malaria Zanzibar zinaonyesha mafanikio mazuri ambapo mtu mmoja kati ya watu mia moja hupata ugonjwa huo katika jamii isipokuwa shehia hizo tano.

  Naibu Waziri wa Afya amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na Malaria ikiwemo kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa na kusafisha mazingira kwa lengo la kuondosha mazalio ya mbu wanaoeneza maradhi hayo.

  Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake mwaka jana iligawa vyandarua 705,000 bila malipo na kufanya zoezi la kupiga dawa nyumba za wananchi ya kukinga malaria bila ya kuangalia vyeo vya wamiliki wa nyumba hizo licha ya kukabiliana na changamo nyingi katika kazi hiyo.

  Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikataa kupigiwa dawa nyumba zao kwa madai kwamba zinawaletea athari za afya jambo ambalo halina ukweli kwani dawa hiyo ni salama kwa afya.

  Amekubusha kuwa Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira ya mwaka 2012 pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya udhibiti wa mbu na mazingira hivyo wananchi watakaokataa kupigiwa dawa sheria itawabana.

  “Watu wanaokataa nyumba zao kupigiwa dawa ya kukinga maluaria bila sababu za msingi zinazokubalika, sheria hii itawabana na hatua muafaka zitachukuliwa dhidi yao, ” alisisitiza Naibu Waziri.

  Meneaja Kitengo cha kumaliza malaria Mwinyi Khamis alisema Zanzibar imeweka mikakati ya kumaliza kabisa malaria ifikapo mwaka 2023 hivyo juhudi za jamii na Wizara ya Afya ni muhimu.

  Amesema mwaka jana watu watano walibainika kufa kwa malaria Zanzibar wakiwemo watoto wawili wenye umri chini ya miaka mitano.

  Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohd amewashauri wananchi wasikubali kula dawa ya malaraia bila kupimwa na kuthibitishwa kuwa wanayo malaria.

  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema Malaria bado ipo Zanzibar, chukua tahadhari.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hotuba yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Aprili 25, 2017 Dodoma.
  Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wakimsikiliza Naibu wake Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi hiyo ikiwa ni maandalizi ya ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Mjini Dodoma.
  Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi. Khadija Mwenda akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa Mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisalimiana na Mwakilishi wa TUCTA Bw.Ramadhani Mwenda mara baada ya mkutano wa waandishi wa habari Aprili, 25, 2017 Dodoma
  Naibu wake Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari Aprili 25, 2017 Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  ………….

  Na. Mwandishi Wetu- Dodoma


  Serikali imewataka waajiri wote na wadau kwa ujumla kuhakikisha kuwa sehemu za kazi, mitambo na vifaa vya kufanyia kazi vinafanyiwa ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa havileti madhara kwa wafanyakazi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

  “Kwa upande wa Serikali jukumu letu kubwa ni kuweka na kusimamia sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kutunga na kusimamia Sheria za Usalama na Afya Mahali pa Kazi, na kuweka viwango mbalimbali vya usalama na afya sehemu za kazi” alisisitiza Mavunde.

  Mavunde alisema kuwa kwa sasa kanuni ya kuripoti ajali na magonjwa imekamilika na kuanza kutumika tangu mwezi Septemba, mwaka 2016.

  Ambapo ameshauri wafanyakazi kuwasaidia waajiri wao kusimamia mifumo iliyopo, kujilinda wao binafsi ili wasiumie ama wasipate magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kutumia ipasavyo vifaa vyote vya kujikinga wawapo kazini.

  Mavunde alisema kuwa serikali inaendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu za ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, hivyo bado kuna changamoto ya kupata taarifa kuhusu ajali na magonjwa yatokanayo na kazi hii inatokana na waajiri wengi kutoripoti taarifa hizo kama sheria inavyoelekeza.

  kwa mantiki hiyo Serikali inaandaa mfumo ambao utaongea na mifumo mingine ili kupata taarifa za ajali na magonjwa.

  Aliongeza kuwa “Serikali kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imejipanga kuhakikisha kuwa Usalama na afya za wafanyakazi hao zinalindwa kwa kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia taratibu zote za Usalama na Afya kwa mujibu wa sheria na 5 ya Mwaka 2003, ili kulinda nguvu kazi ya taifa hili”.

  Aidha, tarehe 28 Aprili ya kila mwaka, Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ili kuwakumbuka wahanga wa majanga yanayotokea sehemu za kazi.

  Madhumuni makubwa ya kuadhimisha siku hii ni kuendesha kampeni ya Kimataifa ya kuboresha usalama na afya kazini na kuhamasisha utengenezaji ajira zenye staha. Kwa kuhamasisha waajiri na wafanyakazi na umma kwa ujumla kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha kuwa suala la ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yanapungua au kutotokea kabisa sehemu za kazi.

  Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajia kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kujumuisha shughuli hizo kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 ambapo yatatanguliwa na kongamano la wadau wa Usalama na Afya.

  0 0


  0 0  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Mhe.Anastazia Wambura,Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba,baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Miss Tanzania Supermodel Bi.Asha Mabula katika viwanja vya Bunge mara baada ya mrembo uyo kutembelea Bungeni hapo  Mjini Dodoma. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  0 0  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya Malaria Duniani kwa  waandishi wa Habari Mjini Dodoma na kusisitiza kuwa vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni bure kwa vituo vyote vya Afya vya Umma nchini.
  WA 1
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
  WA 2
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
  Picha zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.
  …………….
  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haitosita kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya Umma nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo vya malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.

  Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.

  “Huduma ya kupima Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka kutekeleza agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.

  Aidha amwewaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa karibu ili kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.

  Mhe Ummy Mwalimu amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.

  Siku ya Malaria Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni “ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.

  0 0

  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwasiliana na baadhi ya jamaa zake kabla ya kuondoka uwanjani hapo.


  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiaga wakati akielekea ndani ya uwanja tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran.  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa katika utaratibu wa kuingia ndani ili aweze kukaguliwa kama abiria wengine wa kawaida tayari kwa safari kuelekea nchini Iran.


  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akipunga mkono kuaga wananchi wake wa jiji lake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi (10),akiwa nchini humo atakutana na Rais wa Iran, Hassan Rouhani,Mwenyeji wake,Meya wa Jiji la Teheran, Muhammed Bakir Galbaf na kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea nchini humo.

  NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ

  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa mualiko wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili utakaofanyika katika mji wa Bashar.

  Aidha Meya atapata nafasi ya kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar utakao husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.

  Katika mkutano huo ambao utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada ya mkutano huo ataelekea mjini Teherani kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo Muhammed Bakir Galbaf ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara katika majiji hayo mawilI.

  Aidha katika mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye majiji na namna ambavyo wanaweza kuyatatua.

  “ Iran na Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi wamekuwa wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji haya mawili kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi na wao wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.

  Aliongeza kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni mmoja wapo.

  “ Kushudia kwangu kampeni sio kwamba nataka kugombea nafasi ya uras hapa nchini , hapana ila ni moja ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao” alifafanua.

  Hata hivyo Meya aliwasi wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na mafuriko.

  0 0

  Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

  Wafungwa wote ambao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wawe wametumikia nusu (½) ya vifungo vyao vilivyobaki, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi).

  Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

  Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi. Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

  Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

  Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability). Ulemavu huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

  Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-

  Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.
  Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

  Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangik.

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji na upokeaji au utoaji rushwa.

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (fire arms, ammunitions and explosives).

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti au kujaribu kutenda makosa hayo.

  Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

  Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki, uharibifu wa miundombinu au kujaribu kutenda makosa hayo.

  Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).

  Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.

  Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mhe. Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.

  Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.

  Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).

  Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.

  Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za Serikali na ujangili (poachers).

  Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.


  Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.

  Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 16/03/2017.

  Wafungwa warejeaji wa makosa/wafungwa waliowahi kufungwa gerezani (Recidivists).

  Wafungwa 2,219 watafaidika na msamaha huu na wataachiliwa huru. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.


  Meja Jenerali Projest Rwegasira

  KATIBU MKUU
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  26/04/2017

  0 0

  Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo amesimamisha kwa muda uchimbaji wa madini aina ya dhahabu katika machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge ili kuepusha maafa zaidi yasije yakatokea.

  Hatua hiyo inafuatia maafa yaliyokea hivi karibuni ambapo wachimbaji wadogo wadogo sita walifariki baada ya kufukiwa na kifusi na mmoja kufariki kwa kukosa hewa wakati wa uchimbaji wa dhahabu katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge.

  Uamuzi huo umetolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabaora Bw, Mwanri baada ya yeye na kwa kushirikiana na Kamati na Ulinzi na Usalama mkoani humo kutembelea machimbo yalisababisha maafa hayo kwa ajili ya kujionea na kasha kuwapa pole wafiwa.

  Alisema kuwa yeye na Kamati yake wameona ni vema wasimamishe kwa muda ili taratibu zote za kuhakikisha usalama na zile Baraza la Taifa la Mazingira za mpango wa ulinzi wa mazingira(Environmental Protection Plan) zinafuatwa kabla ya kendelea na shughuli za uchimbaji.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa lengo ni kutaka Wachimbaji hao waendele kuchimba katika hali ya usalama bila kuharatisha maisha yao na nguvu kazi ya Taifa.

  Kufuatia hatua hiyo , Bw. Mwanri aliwaagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati na Magharibi Salim Salim na Afisa Madini Mkazi wa Tabora Laurent Mayala kuhakisha kuwa umbali kutoka shimo moja la uchimbaji hadi jingine unazingati matakwa ya Sheria na Kanuni kuliko ilivyo sasa ambapo kutoka shimo hadi shimo ni mita 3 hali ambayo ni hatari.

  Aliongeza kuwa ni vema Ofisi hizo zikahakikisha kuwa wanawapanga wachimbaji wadogo wadogo hao kulingana na matakwa ya kisheria na sio kuwaacha wachimbo ovyo ovyo ambapo hivi sasa mashimo yako karibu karibu sana na hivyo kuhatarisha maisha yao .

  “Mimi siko tayari kuona watu wengine zaidi wanafariki kwa sababu ya uchimbaji usiozingatia matakwa ya kisheria na ambao hauna baraka za NEMC. Hivyo kaeni chini na wamiliki wa mgodi muwapange vizuri kwa kuzingatia sheria na bila upendeleo” aliagiza Mkuu huyo wa Mkoa.

  “Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ilishaahidi kuwa itawashika mkono wachimbaji wadogo wadogo , lakini ni vema tukahakikisha kuwa Mpango wa Ulinzi wa Kimazingira umezingatiwa na kuwepo na wakaguzi watakao hakikisha kuwa taratibu za umbalimbali toka shimo hadi shimo umezingatiwa ili kulinda usalama wao kwanza ” anasititiza Mkuu wa Mko huyo

  Alisema kuwa kuwepo kwa madini ya dhahabu katika eneo la Kitunda ni neema , lakini neema hiyo neema hiyo ni vema utafutaji wa neema hiyo ukazingatia taratibu bila kusababisha maafa mengine kama yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watano walifia mgodini , mmoja alifia hospitalini na mwingine alikufa kwa kosa hewa katika mgodi mwingine.

  Aidha ,Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Maafisa Madini kuharikisha katika ufuatiliaji wa Kibali cha NEMC na kuandaa Mpango Kazi wa Uchimbaji Mzuri na salama ili vijana wanaojihusisha na uchimbaji wa madini katika eneo la Kitunda wasikae muda mrefu bila kuendelea na kazi yao ya uchimbaji madini.

  Alisema kuwa vijana hao hawana kazi nyingine wanayotegemea kujiingizia kipato zaidi ya uchimbaji wa madini katika eneo hilo , hivyo ni vema watendaji hao kwa kushirikiana na wamiliki wa mgodi huo kuhakikisha mambo yafanyika haraka iwezekanavyo.

  Aidha alitoa kwa wachimbaji madini hao kukikisha kuwa sehemu ya mapato yao wayatumie katika kuboresha maisha yao na familia zao kwa kujenga nyumba nzuri, kuvaa vizuri kula vizuri na kulipa kodi zinatakiwa ili neema hiyo iwe na tija kwao.

  Bw. Mwanri alisema kuwa haitakuwa na maana ya kuwepo kwa neema hiyo kama watapata fedha na kuendelea kuishi maisha duni .

  Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora Wilbroad Mtafungwa ametoa onyo kwa baadhi ya vijana wanaendesha vitendo viovu katika eneo hilo kama vile uvutaji bangi, uporoaji na ubakaji kwa kisingizio cha uwepo wa madini ya dhahabu kuacha mara mmoja la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

  Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani huo ili kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wachimbaji hao wanaendesha shughuli zao katika mazingira rafiki, limeamua kufungua Kituo Kidogo katika eneo hilo.

  Hatua hiyo inalenga kuwepo na ulinzi saa 24 siku zote kwa ajili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na uvunjivu na amani na sheria ambao unaweza kujitokeza..

  Aidha ,RPC huyo pia aliwaonya wachimbaji wadogo hao kutoenda katika machimbo wakati wote wa zuio hadi hapo watakaporuhusiwa la sivyo watakabiliana na Askari watakaokuwa wakilinda machimbo hayo

  Katika hatu nyingine , Kamanda huyo ameowanya Polisi wote watakaokuwa wakilinda eneo hilo kutojihusisha na uchimbaji madini kwani kufanya hivyo kutawasababisha migogoro na wao wakuwa wamekiuka kiapo chao.

  Eneo la mchimbo ya Kitunda linawachimbaji zaidi ya 10,000 ambao wanaendesha shughuli hizo .

  0 0

  Ofisa wa benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam kushoto, akimkabidhi moja ya karatasi muhimu baada ya kufanikiwa kumfungulia akaunti mshindi wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku, Nicholaus Mlasu aliyeibuka na ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko mwishoni mwa wiki. Makabidhiano ya fedha za ushindi huo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Picha zote na Mpiga picha Wetu.

  Milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’ zamfikia Nicholaus Mlasu

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  ZAWADI ya juu ya Sh Milioni 10 inayotolewa na Bahati Nasibu ya Biko, Ijue Nguvu ya Buku imetolewa jana na kukabidhiwa mshindi Nicholaus Mlasu, mkazi wa Ukonga Mombasa, Manispaa ya Ilala, huku akipokea fedha zake Makao Makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.

  Fedha za mshindi huyo ziliingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yake iliyofunguliwa kwenye benki hiyo kwa ajili ya kijana huyo kujipanga vizuri kabla ya kuanza kuzitumia fedha hizo kwa maendeleo yake.
  Meneja Masoko wa Biko Tanzania waendeshaji wa Bahati Nasibu kwa njia ya ujumbe wa maneno kwenye simu za mikononi, Goodhope Heaven kulia akizungumza jambo wakati wa kumfungulia akaunti mshindi wao wa Sh Milioni 10 na kumkabidhi fedha hizo jana Makao Makuu ya benki ya NMB, jijini Dar es Salaam. Katikati ni mshindi huyo Nicholaus Mlasu akifuatiwa na Ofisa wa NMB Makao Makuu.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kwamba mbali na kutoa fedha hizo kila mwisho wa wiki, pia wanaendelea kutoa pesa za papo kwa hapo ambapo ongezeko la washiriki ni kubwa.

  Alisema wale wanaoshinda papo hapo fedha kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja hupokea kwenye simu zao wanazotumia ambazo ni Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ikiwa ni baada ya kuingia kwenye kipengele cha lipa bili, kuingiza namba ya kampuni 505050 na kuingiza namba ya kumbukumbu 2456.
  Meneja Masoko wa Mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko, Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 10 mshindi wao wa wiki Nicholaus Mlasu, Jijini Dar es Salaam jana. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB ambapo pia benki hiyo ilimfungulia akaunti ya kuhifadhi fedha zake alizokabidhiwa na Biko.
  Mshindi wa Sh Milioni wa Bahati Nasibu ya Biko kutoka Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam, Nicholaus Mlasu, akifurahia burungutu lake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.
  Nicholaus Mlasu akifurahia pesa zake Sh Milioni 10.
  “Kwa wiki mbili tumeshalipa Zaidi ya Sh Milioni 50 kwa Watanzania wanaoishiriki bahati nasibu yetu ya Ijue Nguvu ya Buku ambapo wiki iliyopita pia tulimkabidhi mshindi wetu wa Sh Milioni 10, Christopher Mgaya na leo tumemkabidhi bwana Mlasu fedha zake.

  “Biko tunasema kila mtu anaweza kushinda kwa kuhakikisha kwamba anacheza mara nyingi Zaidi ili ashinde zawadi za papo kwa hapo pamoja na kujiwekea nafasi nzuri ya kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo kubwa ya wiki inayochezeshwa kila mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa ushauri wa kitaalam wale wanaoshinda fedha hizi ili wazitumie vizuri na kuboresha uchumi wao kwa kutumia vyema fedha za ushindi wa Biko,” Alisema.

  Naye Mlasu alisema kwamba licha ya kushiriki bahati nasibu za kila aina, lakini mchezo wa Biko umemkosha Zaidi kwa sababu hauna mlolongo mrefu na zawadi zake zikiwa ni za haraka, jambo linaloweza kuwanufaisha washiriki wake, hivyo ni wakati wa kila Mtanzania kucheza Biko.

  “Nimefurahishwa zaidi jinsi Biko inavyochezeshwa na ndio maana nilipo pokea simu ya Kajala Masanja anayechezesha droo kubwa ya wiki nilianza kuhisi huenda bahati imeniangukia ukizingatia kwamba kwa jinsi nilivyokuwa nacheza Biko niliamini kuna siku nitapata ushindi,” Alisema Mlasu.

  Bahati Nasibu ya Biko inaendeshwa kwa mtindo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu za mikononi kwa kufanya miamala ya kifedha kuanzia Sh 1000, huku kila Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo sambamba na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kutafutwa mtu mmoja wa kushinda Sh Milioni 10 ambapo tayari Mgaya na Mlasu wamekabidhiwa fedha zao kwa ajili ya kuzitumia kwa manufaa yao.


  0 0

  Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kutilia mkazo suala la kuwapeleka watoto kupata chanjo mara zinapotangazwa ili kuendana na msemo wa kinga ni bora kuliko tiba.

  Rai hiyo ilitolewa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo ya polio wenye kauli mbiu ya “jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya” uliofanyika katika Zahanati ya Mumbwi iliyopo Katika Kijiji cha Mumbwi kata ya Komkonga.

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe mbaye pia alikuwa mgeni rasmi alieleza kuwa Serikali inajitahidi kutoa chanjo bure hivyo wananchi pia wanao wajibu wa kuhakikisha wanapeleka watoto wao kupata chanjo hizo kwaajili ya ustawi wa afya za watoto.

  “Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inazo chanjo za kutosha, chanjo mkoba na chanjo tembezi zitafika kwenye maeneo ambayo bado hayana zahanati ili kuhakikisha watoto wote Wilayani Handeni wanachanjwa” alisema Mh. Gondwe.

  Aidha , aliwataka Maafisa Tarafa, Watendaji Kata na Vijiji kuweka agenda ya usafi na mazingira, afya na bima kuwa ndelevu katika viko vyao vya Vijiji.Akizungumzia suala la malaria kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani Mh. Gondwe alisema kila mwanachi anawajibu wa kutunza mazingira na kutokomeza mazalia ya mbu ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.

  “Chanjo zinatolewa bure,vipimo vya malaria vinatolewa bure na baadhi ya dawa za malaria bure lakini ni vyema kila mwananchi kuwa na bima ya afya ili kuepuka gharama za matibabu na kuhakikisha kuwa suala la afya haliwi tatizo kwenye Wilaya ya Handeni”alisema Mh.Gondwe.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Simon Mdaki alieleza kuwa chanjo zingharamiwa hivyo ni vyema wananchi kutambua umuhimu wa kupeleka watoto kupata chanjo.mtoto akiuguwa wasikimbilie kuhisi motto kalogwa badala yake wamuwahishe hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa unaomsumbua. Polio sio ugonjwa wa kulogwa ni chanjo ndio inapaswa kupatiwa motto angaliakiwa mdogo.

  Aidha aliwataka wananchi wote kuzingatia kinga na kutunza mazingira kutokomeza madimbwi na mazalia ya mbu huku wakizingatia matumizi bora ya vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa malaria.

  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ilikuwa na lengo la kutoa chanjo kwa watoto 2883 badala yake wamechanja watoto 3435 sawa na asilimia 119 (kwa kipimo cha penta) mbali na changamoto mbalimbali zinazokabili Idara ya Afya.

  Uzinduzi huo ulipambwa na kikundi cha ngoma za asili cha chanika kofi na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Chama CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Handeni, Wataalamu wa Afya na watendaji wa Halmashauri.

  Alda Sadango.
  Afisa Habari. 
  Halmashauri ya Wilaya Handeni.

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizindua zoezi la utoaji chanjo Kwa watoto kwa kumpatia mtoto matone ya chanjo ya polio.

  Mh Godwin Gondwe akiwa kwenye picha ya pamoja na walezi wahakikishe watoto aliowapatia chanjo huku akiwa amembeba mtoto ikramu mbarouk Mara baada ya kutoa chanjo Kwa watoto wao.
  Viongozi mbalalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakiongozwa na mkuu wa Wilaya Mh Godwin Gondwe wakiwa wamebeba watoto waliopatiwa chanjo
  Baadhi ya wazazi waliojitokeza kuleta watoto wao kupatiwa chanjo.

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wakati kijiji cha Kitumbi.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw Ramadhani Diliwa akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo.
  Kaimu Mkurugenzi Bw Simon Mdaki akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitumbi
  0 0
  Wakazi wa Gongolamboto wakipita katika daraja ambalo kingo zake zimesombwa na mafuriko barabara ya kuelekea Machinjio ya Pugu Kajiungeni Dar es Salaam leo.Jitihada za makusudi zisipochukuliwa daraja hilo litasombwa na maji.
  Mwonekano wa eneo hilo baada ya kusombwa na mafuriko.

  Daladala likipita kwenye daraja hilo.


  Na Dotto Mwaibale


  MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kuinusuru daraja linaloungani eneo la Gongola mboto na Machinjio ya Pugu ambalo lipokatika hatari ya kusombwa na maji.

  Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na wakazi wa Pugu Machinjioni ambao wamesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mawasiliano kati ya wananchi wa eneo

  hilo na Gongolamboto yatatoweka hivyo kuwa adha kwao kwa kufika makwao kwa kupitia Pugu Kajiungeni badala ya barabara ya Gongo lamboto Pugu Machinjioni kupitia kiwanda cha kutengeneza nguo cha Namera.

  "Tunaomba manispaa yetu ilifanyie ukarabati daraja hili ambapo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha " alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.

  Mkazi mwingine wa eneo hilo Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo linasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi kwani watalazimika kutumia njia ndefu kufika mashuleni kwao kutokana kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.

  Jithada za kumpata diwani wa eneo hilo ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kupiga simu yake ambayo haikupatikana.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akionesha masuke ya zao la mtama wakati akikagua mojawapo ya mashamba ya wakulima wa Kata ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
  Mkulima wa mtama, Mariam Nkinga (kulia) akiwaonesha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese mtama uliochanua katika shamba lake.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akiangalia mtama katika shamba lililopo kata ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (kulia) na Ofisa Kilimo halmashauri ya wilaya hiyo, Sarai Pura wakiangalia mtama uliostawi katika shamba.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na mkulima, Sendama Luhende, Ofisa Kilimo, Sarai Pura na mkulima Mariam Nkinga wakati wakikagua shamba.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu akiendelea kukagua shamba la mtama katika Kata ya Mwaweja.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga akikagua shamba darasa lililolimwa na Ofisa ugani Kata ya Uchunga, Aristidia Tasingwa.

  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amewaagiza maofisa ugani wa kata zote kuhakikisha wanawafikia wakulima na kuwafundisha mbinu bora za kilimo chenye tija.

  Ameagiza pia wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame hususan mtama na uwele badala ya kuwa na kasumba ya kung’ang’ania kilimo cha mahindi ambacho katika sehemu kubwa ya wilaya hakifanyi vizuri.

  Taraba alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake kwenye mashamba ya mtama katika kata za Uchunga, Mwaweja na Ukenyenge kujionea na kufanya tathmini ya kilimo wilayani humo.

  Aliwataka maofisa hao kujiwekea utamaduni wa kutembelea mashamba ili kuwafundisha namna ya matumizi ya mbegu bora kwani wengi wao hupanda bila utaalamu.

  Aliwataka kusimamia Sheria ndogo ya mwaka 2008 ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu inasisitiza kuwa kila kaya wilayani humo iweze kulima ekari mbili za mazao yanayostahili ukame ambayo ni mtama.

  Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa hata hivyo wakulima wengi wilayani humo wameweza kutekeleza sheria ndogo hiyo lakini wamepata changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa maarifa ya matumizi ya aina sahihi za mbegu.

  “Ziara hii imetufundisha mambo mengi kwa mfano shambani hapa tumeshuhudia wakulima hawa wametumia mbegu za aina tano tofauti katika shamba moja sasa kama wangepata elimu wangetumia mbegu za aina moja zisizoshambuliwa na ndege.

  ”Hivyo naagiza wataalamu wa kilimo wahamie mashambani kufundisha wakulima na wawe na mashamba darasa yawe mfano wa kujifunzia wananchi nao waige na kusonga mbele,” alisisitiza Taraba.

  Aidha, alipiga marufuku wakulima kuuza wa mazao kwa ajili ya matumizi mengine pasipo kujiwekea akiba na kuonya atakayefanya hivyo atachuliwa hatua kali ikiwemo kupigwa faini.

  Taraba ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya alionya kuwa wapo baadhi ya wakulima wana tabia ya kufanya biashara ya mtama kwa ajili ya kutengeneza pombe huku wao wakibaki bila ya chakula.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake mkulima wa mtama katika Kata ya Mwaweja, Mariam Nkinga kwa niaba ya wenzake aliomba Serikali iwapelekee mbegu fupi zinazokua kwa haraka.

  Alisema wanapata changamoto ya mtama wao kuliwa na ndege aina ya kwelea pamoja na wadudu ukiwa shambani kutokana na mbegu wanazotumia kuchelewa kukomaa na hivyo kukaa muda mrefu shambani.

  Nkinga alioimba wataalamu wawe wanapita mara kwa mara kunyunyizia dawa mazalia ya wadudu na ndege waharibifu wa mazao ili wasiweze kuzaliana na kufika mashambani.

  Aliwashauri wananchi kulima zao la mtama kwa wingi na kuacha kasumba ya kuchagua chakula na kulima mahindi ambayo matokeo yake hawastawi yanakufa kutokana na ukame.

  0 0

  Ubalozi wa Kuwait unaendelea kuiunga mkono Shule ya Sekondari ya Tolido iliyopo Tanga kwa kuipatia idara ya shule hiyo mashine ya kutoa kopi(photocopy machine) iliyopokelewa na msimamizi wa Shule Bi, Basilisa Soka.

  Mashine hiyo inatarajiwa kuisaidia Shule na kurahisisha kazi za idara kwa ajili ya kuinua kiwango cha elimu.

  Itakumbukwa kuwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Al-Najem alizindua kisima cha maji katika shule hiyo mwishoni mwa mwaka jana 2016 ambapo mradi wa ujenzi wake ulifadhiliwa na Msamaria mwema raia wa Kuwait na kutekelezwa na Asasi ya Direct Aid-ofisi ya Tanga, kisima hicho ndio cha kwanza kuzinduliwa tangu ubalozi wa Kuwait kuzindua mpango wake wa 'Kisima cha maji kwa kila Shule'.

  Idadi ya visima ambavyo tayari vimezinduliwa ndani ya mpango huo vimefikia visima 27 katika shule mbalimbali katika kipindi cha miezi minne tu.

  Ubalozi wa Kuwait utaendela kuisaidia Shule ya Tolido ya Sekondari mjini Tanga na shule nyingine Tanzania ili kuunga mkono mchakato wa elimu nchini.

  0 0


  Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha kilichoundwa na Makamu wa Rais wa Tanzania kilichoko Mkoani Mbeya, kimeeendelea na ziara yake kwa kutembelea skimu ya Mwendamtitu iliyopo wilayani Mbarali. Katika ziara hiyo Kikosi kazi kiligundua jinsi ambavyo miundombinu ya skimu hiyo inavyopoteza maji ambayo yalitakiwa kuingia Mto Ruaha. 

  Aidha pia kimegundua kuwa skimu hiyo imeanzishwa pasipo kufuata sheria za umwagiliaji kwani haina kibali cha umwagiliaji wala kibali cha matumizi ya maji yanayoingia katika mfereji wa skimu hiyo.

  Wakiongea katika ziara hiyo Wajumbe wamesikitishwa an kitendo cha skimu hiyo cha kutumia maji mengi pasipo kuwa na kibali chochote wala pasipo kuwa na miundombinu ya mifereji inayowezesha maji kurudi mto Ruaha mKuu.” Katika skimu hii Maji yanatitririka bure na kwa aina hii ya umwagiliaji kamwe mto Ruaha Mkuu hautapata maji, ila tutachukua hatua stahiki” aliongea Mjumbe Injinia Seth Luswema.

  Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo wameiomba Serikali iwasaidie kuwapatia elimu jinsi ya kuendesha skimu hiyo na pia kuelekezwa jinsi ya kuweka miundombinu rafiki kwa ajili ya kuokoa kiasi cha maji kinachopotea. Wamesema wao hawana elimu yoyote na hawajui kama wanakosea kwa jinsi wanavyoendesha skimu hiyo.

  Kikosi hiko bado kipo Mkoani Mbeaya katika wilaya ya Mbalari kwa ajili y akuzungukia na kukagua maeneo mbalimbali amabayo yanachangia maji kutokwenda Mto Ruaha Mkuu.
  Mjumbe wa Kikosi kazi Injinia Seth Luswema (wa kwanza kushoto), akiwa meza kuu pamoja na Viongozi wa Chama kwa wilaya ya Mbalari, Kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi, uchumi na maliasili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Katibu wa CCM wilaya na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mbalari.
  Wajumbe wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha, wakipata maelekezo toka kwa Katibu wa skimu ya umwagiliaji ya Mwendomtitu akielekeza juu ya wanavyotumia maji ya umwagiliaji ya Mto Ruaha kumwagilizia mashamba ya mpunga.
  shamba la vitunguu lililoko karibu na kianziao cha maji cha askimu cha mwendamtitu wilayani Mbalari likionekana kushamiri kwa sabau ya maji ya kusukuma na pampu wanayotoa mto Ruaha.
  Wajumbe wa Kikosi kazi wakisikiliza maoni ya Wananchi wa kata ya Mwendamtitu walipotembelea skimu yao ya umwagiliaji.

  …………..

older | 1 | .... | 1211 | 1212 | (Page 1213) | 1214 | 1215 | .... | 1897 | newer