Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1210 | 1211 | (Page 1212) | 1213 | 1214 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani katika mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu, leo mkoani Pwani
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi kanda ya kusini ARI-NALIENDELE Dr Shamte Shomari akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.

  wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.picha zote na Emmanuel Massa,Globu ya Jamii.

  SERIKALI kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imejipanga kuhakikisha pembejeo za korosho kwa`msimu ujao wa`mwaka 2017/18 kwa wakulima wa zao la korosho zinawafikia wakuima kwa`wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za Salfa ya unga na lita 30,000 za viatilifu vya maji zimeshawasili katika Bandari ya Dar es Slalaam.

  Akifungua mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na wapuliziaji dawa wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi ya kuwafunza wawakilishi wa wakulima na wadau wa zao la korosho namna ya kuhudumia zao hilo.

  Alisema katika msimu uliopita wa mwaka 2016/17 upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho ulikuwa wa kuridhisha kutokana na kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kulikowezesha uagizaji wa pembejeo nao ufanyike kwa wakati.

  “Kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kuliwezesha uagizaji wa pembejeo ufanyike kwa wakati hivyo kumfikia mkulima kabla ya muda wa kupuliza dawa kwenye mikorosho haujafika,”amesema Sanga.

  Aliongeza kuwa, kiasi cha pembejeo kilichoagizwa kilikuwa cha kuridhisha mpaka sasa bado vipo viuatilifu vilivyobaki katika maghala ya Mwendapole Kibaha na Naliendele Mtwara pamoja na Mtwara mjini.

  Alisema katika msimu wa`mwaka 2017/18 serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania inejipanga vizuri kuhakikisha kuwa pembejeo za korosho zinawafikia wakulima kwa wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za salfa yaunga na lita 30,000 za viuatilifu vya maji zimeishawasili katika bandari ya Dar es Salaam na ziko katika hatua ya kusafirishwa katika vituo vilivyotengwa katika Halmashauri zote.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania ambaye ni Mwenyekiti tawi la Dar es Salaam Mangile Malegesi ambao ndiyo waandaaji wa mafunzo hayo amesema mbegu zilizowasili zinatarajiwa kuanza kutolewa mwezi ujao.

  Hata hivyo alisema mafunzo haya yamelenga kuifikia mikoa inayojishughuisha na zao hilo ambayo ni mkoa wa Pwani,Tanga ambapo awamu ya pili itakuwa ni mikoa ya Mtwara, Lindi,na Ruvuma.

  0 0


  0 0

  Na Husna Saidi-MAELEZO

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu chuoni hapo.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Chuo hicho Lila Mandu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu lengo la kongamano hilo.

  Mandu alisema lengo kuu la kongamano hilo ni kuchunguza kwa kina masuala mbalimbali ya kijinsia pamoja na kubaini mbinu bora za kuondoa ukosefu wa usawa wa jinsia katika muktadha wa Taasisi za Elimu ya Juu.

  “Tutatathmini sababu na changamoto zinazosababisha ukosefu wa usawa wa kijinsia katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa kutumia mifano mizuri kutoka Taasisi zingine ambazo zinajitahidi kuhamasisha usawa na haki za wanawake na wanaume pia,” alisema Mandu.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kongamano hilo litabainisha fursa za kimkakati katika kuwahusisha wadau wa masuala ya jinsia katika kuhamasisha usawa na haki za watu wote ambapo litakuwa na washiriki 140.

  Aliwataja washiriki hao kuwa ni wasomi kutoka DUCE, Taasisi na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi, wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu katika masuala ya jinsia, wawakilishi wa mashirika ya haki za binadamu, watunga sera pamoja na wasomi wanaotambulika Kimataifa katika masuala ya jinsia.

  Kwa upande wake, Mratibu Kitengo cha Jinsia DUCE Fatma Hamad alisema licha ya maovu wanayotendewa wanawake kuendelea kujitokeza hapa nchini, kongamano hilo litasaidia kutoa elimu ya jinsia na usawa ili kusaidia Serikali na wananchi kwa ujumla kuondokana na hadha hiyo.

  Chuo cha DUCE pamoja na waandaaji wa kongamano hilo wamealika wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia, wasomi, waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kongamano hilo.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na mgeni wake Mwenyekiti wa Kampuni ya “Engineering Consultants Groups”-ECG Bw.Amr Hassan Allouba yaliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya “Engineering Consultants Groups”-ECG Bw.Amr Hassan Allouba (katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohamed Haji Hamza. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na mgeni wake Mwenyekiti wa Kampuni ya “Engineering Consultants Groups”-ECG Bw.Amr Hassan Allouba alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo na ujumbe wake . 

  Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulyahaya Mzee (kushoto) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali kuhusu Ripoti ya mkaguzi na Mdhibiti wa fedha za Serikali iliyozungumzia upotevu wa fedha katika Mawizara mbali mbali ambazo zimekuwa zikilipwa kwa makosa,katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]24/04/2017.

  0 0  0 0


    Prof.Raphael Tihelwa Chibunda  0 0  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini kutumia nafasi zao kuhimiza wazazi na walezi kuishi maisha yenye nidhamu, kuthamini kazi yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu na kusimamia malezi ya watoto na kuzingatia maadili ya Taifa kwa ujumla.

  “Tabia na mwenendo mzuri ni lazima uanzie katika ngazi ya familia, mtaani na hatimaye katika jamii. Tukirudia utamaduni wetu wa zamani wa kusimamia maadili kwa pamoja, jamii yetu itanusurika kwa kiwango kikubwa,” amesema.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 24,2017) wakati akifungua kongamano kuhusu mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, lililofanyika mjini Dar es Salaam.

  Amesema kila mzazi au mlezi aone aibu, uchungu na ajutie anapoona mtoto yoyote akienda kinyume na utaratibu wa kawaida wa maisha na ni vema wakatumia nafasi yao kwa kuwahimiza vijana hao waishi maisha ya nidhamu na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.

  Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga jamii yenye  kuzingatia maadili nchini na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli amekuwa akiwasisitizia Watanzania wote kuzingatia maadili katika jamii kwa kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vyote vya rushwa na ubadhirifu.

  Amesema maadili katika Taifa ni moja ya tunu muhimu kwa kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha maendeleo, ujenzi wa umoja, amani, upendo, uvumilivu na mshikamano kwa jamii.

  Amesema maadili ni nyenzo muhimu sana katika ujenzi wa Taifa na huliepusha kuingia katika mifarakano na migogoro. “Hivyo hatuna budi nasi kuyalinda maadili hayo kwa uwezo wetu wote, ili tuyarithishe kwa vizazi vijavyo, kama vile sisi tulivyoyarithi kutoka kwa waasisi wa Taifa letu,”.

  “Hata hivyo, ninyi ni mashahidi kuwa katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia vitendo vya mmomonyoko wa maadili na matokeo yake yanaonekana dhahiri kama kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, kuiga tamaduni za nchi za kigeni ambazo sio njema na hazina tija kwa jamii, na Taifa kwa ujumla”.

  “Ni ukweli usiopingika kuwa mmomonyoko wa maadili ni miongoni mwa vichocheo vinavyopelekea matumizi ya dawa haramu za kulevya. Hivyo ni matarajio yangu kuwa mtaliangalia kwa kina tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo kwa kiasi kikubwa linatuathiri kama Taifa katika mipango ya Serikali na maendeleo ya Taifa letu,” amesema.

  Hivyo Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa BAKWATA kwa kuwa na wazo la kufanya kongamano hilo lenye kulenga kujadili namna ya kurejesha maadili katika jamii. Tukumbuke kuwa Watanzania tutaendelea kuishi kwa upendo, amani na utulivu iwapo tutazingatia maadili.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini inafanikiwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa waathirika wote wa matumizi ya dawa hizo wakiwemo vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanakombolewa dhidi ya janga hilo.

  Amesema Serikali itahakikisha inashughulikia mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na dawa za kulevya bila ajizi, ambapo vyombo vyote vya kisheria vimeelekezwa kushirikiana katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa ya kulevya kwa kusimamia sheria ipasavyo.

  Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Bw. Rogers Siyanga amewaomba viongozi wa dini kuiunga mkono mamlaka hiyo kwa sababu inafanya kazi kubwa ambayo inahitaji msaada wa watu wote.

  Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi amesema viongozi wa dini nchini wana jukumu la kukataza maovu na kuiamrisha jamii kufanya mambo mema badala ya kuiachia Serikali pekee kufanya kazi hiyo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, APRILI 24, 2017.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kushiriki tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliofanyika Vinna Hotel Mabibo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

  Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari jijini hapa. Amesema kuwa. Aprili 22 mwaka huu majira ya mchana, walipokea taarifa ya kuwa watu wasiofahamika wakiwa na silaha walivamia mkutano huo na kujeruhi baadhi ya watu. 

  Kamanda Sirro ameongeza kuwa, mpaka sasa watuhumiwa watatu waliokamatwa wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitafuatwa juu yao na amewasihi watu kutii sheria bila shuruti kwani hakuna mtu au kikundi chochote cha watu wanaoweza kuwa na mamlaka ya kushambulia wengine. 

  "Kama unamalalamiko pitia polisi, au mahakamani siyo kuvamia kundi la watu wengine kama wako juu ya sheria, tunafuatilia wale wote waliohusika katika kufanya shambulio hilo na mtu mmoja aliyejeruhiwa sana anataja watu walioshambulia" amesema Sirro. 

  Kamanda Sirro, amesema jeshi la polisi linaamini kuwa watu waliofanya uvamizi huo walifanya kwa utashi wao wenyewe na kwamba pindi upelelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani. 

  Aidha amewaonya baadhi ya viongozi wa CUF waliotangaza kuwafuata watu fulani na kuwawajibisha ni vema wakumbuke kuwa hakuna mtu aliyeko juu ya sheria kwani hakuna mtu aliyeko juu ya mamlaka. 

  Mapema wiki iliyopita, watu wasiojulikana wakiwa na bastola walivamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo. 

  Mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF , ulivurugika baada ya vurugu kubwa zinazodaiwa kufanywa na wanachama wa CUf ambao wanamuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. 

  katika vurugu hizo, Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.
  Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliotokea mwishoni mwa wiki hii. 

  0 0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
  Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga baada ya Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi baada ya Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Pembeni yake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo siku ya Jumatatu April 24, 2017 wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Swahiba Mdeme,Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania na Canada Col. Adolph Mutta, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, Mhe. Josephat S. Kandege, Afisa wa Ubalozi Bwn. Dismas Assenga na Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin. Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania walikuja Washington, DC kuhudhuria mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF
  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, na Mhe. Josephat S. Kandege

  0 0


  0 0  Dar Es Salaam – Usiku wa tarehe 20 Aprili katika Club ya Next Door ndani ya Masaki, Dar es Salaam, Castle Lite ilizindua promosheni ya 'Castle Lite Unlocks kwa mara ya kwanza Tanzania, na hivyo kuiweka nchi katika msisimko wa aina yake. Chumba kilikuwa kimejaa hamasa wakati Castle Lite ikimzindua Mfalme wa Muziki Kimataifa-FUTURE.

  Uzinduzi huo ulishereheshwa na malkia mpya wa muziki wa pop na mtangazaji maarufu wa televisheni, Mini Mars, tangazo hilo lilibainisha kwamba Rapa ambaye ni mshindi wa tuzo ya “Turn On The Lights” atakuwa nyota katika onesho la Julai 22, 2017 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambapo upatikanaji wa tiketi utatangazwa katika hatua nyingine zitakayofuata.

  Castle Lite pia imetangaza kwamba mwanamuziki Diamond Platnumz atakuwa mshiriki mwenza katika tamasha hilo la Extra Cold Unlocks. Diamond Platnumz ni msanii wa kwanza Afrika Mashariki kusaini mkataba na kampuni ya kurekodi muziki ya Universal Music na hivyo kuwa mwanamuziki rasmi wa kimataifa.

  “Ninawaahidi Watanzania burudani ya kipekee”, alisema Diamond Platinumz alipokuwa akizungumza kuhusu tamasha hilo.

  Likiwa linawashirikisha wasanii wengine maarufu wa Kitanzania ambao watatangazwa katika hatua zitazofuata kuelekea katika tamasha hilo,

  “Kampeni ya 'Castle Lite Unlocks' imekuwa kwenye harakati za maandalizi kwa miaka michache sasa, ambapo Castle Lite imebadili mfumo wa kawaida uliozoeleka kwa kuwaletea wasanii wa ngazi ya juu kimataifa ili kuburudisha nchini mbalimbali Afrika na kwa mara ya kwanza burudani inaletwa katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki jijini Dar es salaam alisema Mkurugenzi wa Masoko wa Afrika Mashariki, Thomas Kamphius.

  "Tunaelewa kwamba wateja wetu sio kila mara wanapata fursa ya kuona baadhi ya matukio haya makubwa, hivyo tunataka kuwaletea fursa hii na kuendelea kuwaletea burudani za namna hii kwa miaka ijayo.Kamphius aliongeza.

  Fuatilia matangazo mbalimbali katika vyombo mbalimbali vya habari , ikiwepo Radio, TV, mitandao ya kijamii na Magazeti ili kupata muendelezo wa matukio kutoka sasa hadi siku ya tamasha lenyewe Julai 22. Kwa hivi sasa chukua Castle Lite yako soma maelekezo jinsi ya kushiriki ili kupata fursa ya kushinda nafasi ya kuwa sehemu ya sehemu ya Burudani ya'Castle Lite Extra Cold Unlocks' ndani ya Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Ofisi ya kupambana na rushwa mkoa wa Ruvuma TAKUKURU kwa kipindi cha miezi tisa toka julai 2016 hadi marchi mwaka huu imeokoa fedha kiasi cha shilingi 91,811,768.91 zilizokuwa zimetolewa katika miradi mbalimbali,iliyokuwa inaviashiria vya ubadhirifu habari kamili hiyo hapa chini

  0 0

  Shirika la Anga la Etihad limetangaza uteuzi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara yake tanzu ya Airline Equity partners, Bwana Robin Kamark ambaye atashughulikia kuongoza na kuendeleza mikakati ya uwekezaji inayojumuisha wabia wa Shirika hilo kama vile; Airberlin, Alitalia, Jet Airways, Air Serbia, Air Seychelles, Etihad Regional na Virgin Australia.

  Mtendaji huyo mkuu atakuwa chini ya Rais wa Shirika hilo na Mkurugenzi Mkuu. Kamark anachukua nafasi ya Bruno Matheu ambaye alishika wadhifa huo tangu Mei 2016 ambaye imeelezwa kwamba anaachia ngazi kutokana na sababu zake binafsi.

  Kamark amefanya kazi katika sekta ya anga kwa takriban miaka 17, huku akifanikiwa kufikia malengo ya mikakati yake ya kibiashara na masuala ya utawala katika Shirika la SAS ambako pia alikuwa akitekeleza majukumu yake kama Ofisa Mkuu wa Biashara.

  Kwa miaka mitano yake ya mwishoni amefanya kazi kama Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Biashara katika kitengo cha bidhaa za ASA zinazoongoza kwa huduma za kifedha na biashara.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, Mhe. Mohamed Mubarak Fadhel Al Mazrouei amesema kwamba “Shirika hili linaendelea kuwekeza duniani katika kiwango chenye ubora wa juu, ikiwamo kujenga timu nzuri itakayoongoza biashara na kuipelekea katika hatua kubwa zaidi za maendeleo.”

  Alisema, “Robin ni kiongozi anayeheshimika katika sekta ya anga duniani pia ana uzoefu mkubwa kutoka Shirika la SAS. Amefanya kazi kubwa ya kuboresha shirika hilo la ndege. Hivi karibuni amepanua wigo wa taaluma yake katika masuala ya huduma za kifedha.”

  Aliongeza kuwa, “Ushirikiano na kampuni yetu utaendelea kuwa alama muhimu katika biashara na Robin ataongoza mipango hiyo kwa kuweka mikakati na kuendeleza dhamira yetu.”

  “Tunapenda kumshukuru Bruno kwa juhudi zake kubwa alizoonyesha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kutokana na kufanikiwa kujenga na kuhimarisha ushirikiano wetu katika kitengo cha Airline Equity partners,” alisema kiongozi huyo.

  Kamark ataongoza mikakati ya maendeleo kwa kuongeza ufanisi katika biashara, mapato na kuboresha bei baina ya Shirika la Ndege la Etihad na wabia wake ulimwenguni. Pia atasimamia mikakati ya kiutawala kwa wabia wa mashirika ya ndege ambayo Shirika la Etihad linashirikiana nayo.

  Kamark amepata elimu ya shahada ya kwanza na uzamili katika masula ya uongozi wa biashara, huku akifuzu kwenye Shule ya Utawala ya Norwegian.Alianza kazi ya uhasibu katika sekta ya viwanda vya uzalishaji bidhaa, pia alitumikia jeshi kabla ya kujiunga na SAS mwaka 1995.Kamark ataanza majukumu yake rasmi Oktoba mwaka huu.

  Akishukuru uteuzi huo Kamark alisema, “Ninaishukuru Bodi ya Shirika la Anga la Etihad kwa ujasiri wao wa kuniteua. Haya ni majukumu makubwa, kunipa nafasi hii muhimu kuendeleza na kuboresha mikakati muhimu ya Shirika.”


  Ofisa Mikakati na Mipango wa Shirika hilo, Kevin Knight ataungana na Bruno Mathew katika kuendeleza Idara ya Airline Equity Partners.

  Kamark anakuwa miongoni mwa watendaji wa juu katika Shirika la Anga la Etihad akiungana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad (Peter Baungartner), Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege Etihad (Jeff Wilkinson), Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Uwanja wa Ndege (Chris Youlten).

  Uongozi wa Shirika la Hala linalohusika na masula ya Masoko na Huduma za Hadhi ya juu, watatangaza mkurugenzi wake wa kudumu mwishoni mwa mwaka huu.

  Bodi ya Shirika la EAG kwa sasa linaendelea na mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wake mpya ambaye atachukua nafasi ya Rais na Mkurugenzi wa sasa, James Hogan ambaye awali ilitangazwa ataachia ngazi baadaye mwaka huu.

  0 0


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

  Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.

  “Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama

  Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.

  “Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana

  Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

  Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.

  Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.

   Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri  leo Mjini Dodoma.
   Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.
   Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

   Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

   Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
   Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
   Makomandoo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa mapambano.
   Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.

  Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.


  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akizungumza katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, Wabunge hao walikuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia)akimkabidhi kitabu chenye Sheria Mbali mbali za Bunge Mhe. Douglas Syakalima (wa pili kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu na Kiongozi wa Msafara wa kutoka Bunge hilo, Wabunge hao wamekuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kaunda suti nyeusi katikati)akipiga picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mhe. Douglas Syakalima, ambae ni Mwenyekiti wa Kamati na Kiongozi wa Msafara/Ujumbe huo katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigala King akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE).

  0 0

  Mwuonekano wa jengo la Mahakama ya Watoto iliyopo katika Jiji la Mbeya.

  Na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania


  Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuhusu habari za vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa watoto.

  Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa matamko ambayo yanaitaka jamii kufahamu haki za mtoto ikiwa ni hatua ya kuwaepusha watoto wasiathiriwe na tabia hatarishi.

  Miongoni mwa viongozi hayo ni Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Waziri wa Afya,Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Ummy Mwalimu akiwemo Naibu wake. Dkt. Hamis Kingwallah na baadhi ya viongozi wengine mbalimbali.

  Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa asasi za kiraia na dini mbalimbali wameungana ili kuhakikisha watoto hao, wanakua katika maadili mema na kuweza kutimiza ndoto zao.

  Mbali na hilo, kuhakikisha kwamba watu wanaowarubuni watoto wanachukuliwa hatua za kisheria.

  Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wa Miaka Mitano yaani 2015/16 hadi 2019/20, imejenga Mahakama nyingine ya watoto ambayo iko katika Jiji la Mbeya.

  Kupitia mpango huo, hivi sasa Tanzania ina mahakama mbili za watoto ambazo moja iko katika jiji la Dares Salaam na nyingine jiji la Mbeya.

  Mahakama hizi mbili ziko katika maeneo ya katikati ya jiji, ikiwa dhamira ya Mahakama ya Tanzania, kuhakikisha kwamba inaboresha huduma za utoaji haki na kusongeza huduma zake karibu na wananchi.

  Mahakama ya Watoto ni Mahakama ambayo imeanzishwa kisheria kwa lengo la kushughulikia kesi maalum zinazohusu watoto.

  Umri ambao Mahakama hiyo mtoto ni mtu aliye na umri wa chini ya 18 kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyosema sura ya kwanza, kifungu cha 5.-(1) na ilivyo katika Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 pamoja na kanuni zake, marekebisho ya mwaka 2006.

  Mahakama hii inashughulikia makosa mbalimbali ambayo yanaweza kufanywa na watoto kama shuleni, mitaani na sehemu nyinginezo.

  Kuna mambo mbalimbali ambayo pia Mahakama hii inayashughulikia mfano vile taratibu za kuasili watoto na mambo ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na mchakato mzima wa kufanya hivyo, ikiwemo kupokea mashauri ya madai.

  Usikilizaji wa mashauri katika Mahakama hii, hufanyika faragha. Lengo la usikilizaji wa mashauri haya kusikilizwa kwa siri ni kulinda maslahi ya mtoto.

  Hivyo jamii inapaswa kuzifahamu haki za mtoto kama vile haki ya kuishi, kupata huduma bora za afya, mahali pa kuishi.kupata elimu, haki ya kutambuliwa, haki ya kurithi mali, haki ya kutonyanyaswa, ikiwemo kutofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Ukeketaji,iliyofanyika Desemba 5, mwaka jana, Sihaba Nkinga, alisema hali bado ni mbaya.

  Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba taarifa zinaonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watatu wa kike na mtoto mmoja wa kati ya saba wa kiume walifanyiwa ukatili wa kingono.

  Kupitia maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Bi Zainabu Issa ametaka jamii ipige vita vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, ili kuwawezesha kufikia ndoto zao ikiwa ni hatua ya kuwawezesha ustawi wa maisha yao na hatimaye kulijenga taifa la kesho.

  “Ninasema kesi dhidi ya ukatili wa watoto sasa zisizidi miezi sita au mwaka, kesi zisikae, muda mrefu Mahakamani.Ninasema sasa mtu akipatikana na hatia ya kuumpa ujauzito mwanafunzi au kubaka afungwe miaka 30 jela,” alisema Mkuu huyo wa wilaya wakati siku ya maadhimisho hayo yaliyofanyika Mkoani Tanga, wilaya ya Pangani.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Appi akizungumza maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, alipiga marufuku vitendo vya baadhi ya walimu kuwafungia mageti wanafunzi wanapochelewa kufika mashuleni kwa kuwa vinaweza kuwasababishia watoto kujiunga na makundi yenye tabia hatarishi.

  Alisema ili kuweza kuwaepusha watoto kutoathiriwa na tabia hatarishi, Mkuu huyo alipendekeza walimu watumie adhabu mbadala pale baadhi ya wanafunzi wanapofanya makosa wakiwa mashuleni.

  Alisema adhabu mbadala zinaweza kutolewa na walimu, wakati wa kipindi cha mapunziko.

  Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mwanzo Mjini Mbeya, Mhe. Onesmo Zunda akizungumzia kuhusu uzoefu wa usikilizaji kesi za watoto zinazohusiana na madai alisema amekuwa akisikiliza kesi za ndoa na talaka nyingi kutoka vijijini kuliko mjini.

  “Kuna changamoto katika kusikiliza kesi hizi. Miongoni mwa changamoto tunazokabiliana hizo ni mgawanyo wa mali hasa pale inapotoa mtu anapokuwa amefariki dunia au wazazi kutengana mmojawapo akiwa ana fedha au mali au kaoa mke mwingine. Nyingi hivyo mgawanyo wa mali huwa unaleta malalamiko katika baadhi ya familia,” alisema Mhe. Zunda.

  Alifafanua kwamba katika kesi hizo ni Baba anapotaka kubaki na watoto halafu mama hataki. Hata hivyo anasema Mara nyingi mama huwa anataka kubakia na watoto, lakini baba hataki kutokana na tabia ya mama.

  “Hivyo tunatumia sheria pale ndoa inapotaka kuvunjika tunachoangalia zaidi ni maslahi ya mtoto hata kama mtoto ana umri wa zaidi ya miaka 7,” anasititiza Mhe. Zunda.

  Akitolea mfano wa kesi mojawapo, ambapo alisema alitoa maamuzi kwamba mtoto abaki kwa baba kwa sababu mama alikuwa na tabia ya ulevi. Alisema uamuzi huo kwa mujibu wa shuhuda za watoto.

  Ingawa kulingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ni jukumu la baba kuwapa watoto matunzo japo jukumu la kuwalea watoto ni la wazazi wote. Hatahivyo, mwanamke anatakiwa achangie katika kuhudumia watoto. Iwapo wazazi wametengana amri ya matunzo hutolewa na Mahakama ili baba asiyeishi na mtoto.

  Matunzo hayo huwa ni pamoja na kutoa nguo, chakula, kugharamia masomo shuleni na matunzo yataendelea hadi kufikia umri wa miaka 18.

  “Licha ya changamoto tunazozipitia tunajitahidi kuzitatua kwa kutumia sheria ,hakuna rufaa zinazofunguliwa,”alisema Mhe. Zunda.

  Mhe. Zunda alizitaja takwimu za kesi za ndoa na talaka walizozipokea kwa kipindi cha mwaka huu yaani Januari hadi Machi 23,mwaka huu, kuwa 26 na hivyo kati ya hizo 11 bado zinaendelea kushughulikiwa na nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi.

  Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mwanjelwa, Mhe. Happiness Chuwa, alisema ili kukabiliana na tatizo la kesi zinazo husiana na watoto ni vema jamii ikiwa ina tabia ya kuwatambulisha watoto na kuandika wosia.

  Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto, iliyopo eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Devotha Kissoka, akizungumza wakati wa Wiki ya Sheria iliyofanyika mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, alisema mtoto akikosa anaweza kupelekwa katika makao ya watoto.

  Ikiwa kuna tatizo, ambalo limeleta mabishano kuhusu mtoto baba yake au wazazi wake ni wakina nani? Mahakama hiyo inatoa amri Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya vipimo vya utambuzi (DNA testing).

  Alizitaja takwimu zinazohusu kesi za madai katika Mahakama hiyo za kipindi cha mwaka 2016 ni 154 na katika kipindi cha mwaka 2015 zilikuwa kesi 19.

  Hakimu huyo alifafanua kwamba sababu ya kuongezeka kwa kesi hizo ni hali ya uchumi, hivyo hali hiyo imetokea kwa watoto walio nje ya ndoa.

  Alisema Mahakama hiyo, pia huwa inasikiliza kesi za jinai mfano wizi wa kutumia silaha, kujeruhi na kuua.

  Mhe. Kissoka aliongeza kwamba ieleweke kwa mujibu wa Sheria, mtoto aliyechini ya umri wa miaka kumi hawezi kutenda kosa la jinai.

  Desemba 5, mwaka huu Tanzania iliazimisha Maadhimsho ya Kupiga Vitendo vya Ukatili dhidi ya Watoto, mfano kufanyishwa kazi ngumu, kubaka na kuolewa chini ya umri mdogo, au kutopewa fursa ya kupata elimu bora kwa ajili ya maisha yao ya baadae.

  Mtoto ana haki ya kupata dhamana katika mashitaka yote isipokuwa yale, ambayo sheria imemtaka hayana dhamana.

  Mhe. Kisoka alizitaja adhabu ambazo hutolewa kwa mtoto, miongoni mwa adhabu hizo ni kuachiwa kwa masharti kwa kipindi fulani, lakini kisizidi miaka mitatu, adhabu ya kulipa faini, adhabu ya kuripoti kwa Afisa Ustawi wa Jamii, adhabu ya kupelekwa katika shule maalum.

  Pamoja na adhabu hizo mahakama ina uwezo wa kutoa amri mbalimbali kama vile kulipa faini, kuachiwa bila masharti yoyote.

  Kutokana na maoni ya watu mbalimbali mfumo mmoja wa kisheria na nguvu za pamoja zitasaidia kupunguza au kutokomeza vitendo vya kikatili na unyanyasaji dhidi ya watoto. Hii inatokana na sababu bado umri wa mtoto bado ni tatizo kwa kuwa mtoto ana weza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 au kuoa wakati huohuo mtu anaitwa mtoto akiwa na umri chini ya miaka 18.

  0 0


  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage
   
  Na David Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu za uwekeza kwenye vifaa tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu(Infusion Fluids).

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.

  “Gharama za miradi hii inakadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 36.5 na kutoa ajira za moja kwa moja 1600 na zisizo za moja kwa moja 5000”, Alisema Mhe.Mwijage.

  Amesema mradi huu unakadiriwa kutumia pamba tani elfu 50 kwa mwaka na Serikali ya Mkoa wa Simiyu inaendelea na jitihada za kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kuwalenga wajasiriamali wadogo,wa kati mpaka wakubwa bila kujali kama ni wa kutoka ndani au nje ya nchi.

  Aidha amesema kuwa azma ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imeainishwa vyema katika mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/17-2020/21 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.

  Pamoja na hayo ameainisha kuwa ili kufikia azma hiyo ushiriki wa mchango wa mtu mmoja mmoja,makundi ya watu,taasisi za umma na taasisi binafsi unahitajika.

  Amebainisha mikakati minne ambayo imeanza kufanyiwa utekelezaji ni ya ngozi,mafuta ya kula,nguo na mazao jamii ya kunde uku wakati huohuo mpango wa wilaya moja,zao moja na uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda chini ya SIDO unaendelea nchini kote.


older | 1 | .... | 1210 | 1211 | (Page 1212) | 1213 | 1214 | .... | 1904 | newer