Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1205 | 1206 | (Page 1207) | 1208 | 1209 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujuliza (Kulia) akisisitiza jambo wakati mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara, kushoto ni Bw. Albert Msangi.
  Sehemu ya washiriki  wa mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara.
  Mmoja wa washiriki akichangia wakati wa mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Hakuna kitu kinachoudhi kama kuwa sehemu na marafiki, familia au ndugu lakini unakuta kila mtu ameinamia skirini ya simu yake! Kwa kiasi kikubwa kuja kwa mtandao wa intaneti kumewafanya watu kujikita zaidi na simu zao badala ya watu au kufaidi mazingira yanayowazunguka.

  Kuna tafiti nyingi zimekwishafanyika na kuthibitisha kuwa muda mwingi unaotumika kwenye intaneti una madhara kama vile ya kimwili na kiakili. Mbali na kuwepo kwa faida lukuki za mtandao huo, Jumia Travel ingependa kukujulisha kuwa yafuatayo yanaweza kukumba endapo utautumia vibaya:

  Intaneti husababisha hali ya kujisikia vibaya, kukosa furaha na wivu. Mtu anaweza kushangaa na kujiuliza hii inaweza kutokeaje. Jibu ni rahisi sana. Mambo tunayoyaona kwenye mitandao ya kijamii yanayowekwa na watu maarufu, ndugu, jamaa au marafiki wa karibu huweza kukukosesha furaha kwa namna moja ama nyingine. Hebu jaribu kufikiria unamuona rafiki yako wa karibu ameweka picha zake akiwa amesafiri sehemu ambayo wewe hujawahi kufika au chakula usichowahi kukila utajisikiaje? Ingawa sio wote wanaoweza kujisikia vibaya lakini kwa asilimia kubwa wengi wao hupatwa na wivu au kusononeka nafsi kuona kwamba inawezakana wao wasije kuwa na maisha kama yale.


  Intaneti husababisha watu wengi kujihisi kuwa wanapitwa na wakati. Tangu enzi za kale kila nyakati zimekuwa na mitindo tofauti ya maisha hapa duniani. Kwa bahati mbaya sio watu wote ambao wanao uwezo wa kuendana na mitindo au fasheni zilizopo. Hali hii imewafanya wengi kujihisi kupitwa na wakati endapo wasipoishi kama wanavyoona kwenye mitandao. Kupitia mitandao ya kijamii kama vile Instagram watu wanaweza kuwashirikisha wenzao picha na video za namna wanavyoishi kuendana na wakati. Ambapo mara nyingi yale yanakuwa sio uhalisia wa maisha yao.    

  Intaneti imekuwa ni chanzo kikubwa kwa watu wengi kutokuwa na utulivu wa akili. Nadhani hii hali inawakuta watu wengi katika maisha yao ya kila siku katika ulimwengu wa sasa wa intaneti. Kuna wakati unajaribu kujikita kwenye suala fulani lakini shughuli zinazoendelea mtandaoni kupitia simu yako ni kikwazo kikubwa. Kwa mfano, unataka kukamilisha kazi uliyopewa na bosi wako, mara ujumbe wa Whatsapp umeingia, hujatulia Facebook, Twitter na Instagram nazo zote zinakujulisha kuwa unapitwa huku. Kwa hali hii sidhani kama kuna jambo ambalo mtu anaweza kulikamilisha kwa ufanisi na usahihi unaohitajika.

  Intaneti inawanyima watu fursa ya kufurahia maisha halisi yanayowazunguka. Kwa sasa ni jambo la kawaida kabisa sasa kuona familia imekwenda hotelini kupata chakula pamoja na kubadilisha mazingira ya nyumbani lakini ukakuta kuanzia watoto mpaka wazazi wote wameinamisha nyuso zao kwenye skirini za simu zao. Hakuna tena ile hali ya zamani kwamba muda wa chakula ndipo familia hukutana kwa pamoja, kuzungumza, kucheka na kubadilishana mawazo juu ya yale waliyoyapitia siku nzima. Kwa hali ilivyo sasa hivi huwezi kusikia tena vicheko au gumzo kwenye familia nyingi kwani vyote hivyo vimeamia kwenye simu. Usishangae ukamuona mtu anacheka mwenyewe ukadhahania ni punguani, hapana, ni mambo ya intaneti hayo.

  Intaneti imekuwa ni chanzo kikubwa cha watu kutokuwa wabunifu katika masuala mbalimbali. Hebu jaribu kufikiria ingekuwaje kama hizo video unazozitazama kupitia YouTube, habari unazoziona Facebook au Twitter, au picha unazoziona kupitia Instagram; vyote hivyo ungevipataje kama waliogundua nao wangekuwa wanatumia muda wao kwenye intaneti kupitia kazi za wenzao. Hii inamaanisha kwamba hatupaswi kutumia muda mwingi kuwa watumiaji wa vitu vya kwenye intaneti badala yake nasi tuwe wazalishaji ili kuwanufaisha na wengine zaidi. Unaweza kukuta mtu tangu siku inaanza mpaka inaisha yeye anaimaliza kwenye mitandao ya kijamii akipitia, kutazama na kusoma habari za watu wengine.

  Yaliyozungumzwa katika makala haya ndio maisha ya wengi kwa sasa jinsi yalivyoathiriwa na kuja kwa intaneti. Lakini zipo mbinu kadhaa za kuweza kujiepusha na madhila hayo yote. Jumia Travel inashauri kwamba jukumu la mtu kuepukana na uraibu wa matumizi ya intaneti ni la kwake mwenyewe. Kwa mfano, kujiwekea au kutenga muda maalumu wa kuingia mtandaoni, kuzima ishara zitokanazo na mitandao ya kijamii au kuzima kabisa intaneti kwenye simu yako mpaka muda fulani inaweza kusaidia pia.

  0 0


  0 0

  Na: Lilian Lundo - MAELEZO.

  Maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui hasa kulinda amani ya nchi yetu kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrasha zitakazopamba maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma Aprili 26 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pia yatapambwa na burudani nyingine kutoka vikundi mbalimbali.

  Taarifa ya Waziri Mhagama ametaja shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama (JWTZ,JKT, Polisi na Magereza) na onesho la mbwa na farasi waliofunzwa.

  Aidha, Waziri Mhagama aliongeza kuwa mambo mengine yatakayofanyika ni gwaride la uzalendo la wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, vikundi vya muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi Maturumbeta.

  “Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuumarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,” alifafanua Waziri Jenista Mhagama.

  Ametoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri siku hiyo ya Jumatano tarehe 26 Aprili 2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,” alisema Jenista Mhagama.

  Maadhimisho ya Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iabnze kutumiza azma ya kuhamia katika makao makuu hayo mapya. 

  0 0

  Na Ripotawetu Globu ya Jamii.

  Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbalimbali ya kihalifu pamoja na Madawa ya kulevya, Unyang'anyi wa kutumia Silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro amesema operation hii ni endelevu na jumla ya kete 366 za dawa za kulevya zimekatwa pamoja  puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.

  Aidha Sirro amesema kuwa Operatini kali ya kuwasaka wahalifu wa makosa hayo mbalimbali ikiwemo kosa la kupatikana na madawa ya kulevya  bado inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waalifu.

  " Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao na pindi  upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.

  Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa mnamo tarehe 15 mwezi huu 2017 majira ya saa moja usiku maeneo ya Kiwalani kwa Ally Mboa, Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.

  " Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika maeneo hayo ambapo yaliskia harufu ya bhangi na kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea. Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.
   Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na watuhumiwa waliokamatwa kwa Makosa mbalimbali ya kiharifu katika jiji la Dar es Salaam.
  Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu mbalimbali walivyo vikamata leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

  Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa mafao waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo.

  Mhe. Magige aliliambia Bunge kuwa waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambao waliachishwa kazi mwaka 2000, hawajalipwa mafao yao hadi sasa.

  Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa katika zoezi la ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi hao Serikali ililipa Sh. 217,366,296 mwezi Januari, 2000 ambapo baadae walipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao kuwa wamepunjwa.

  “Serikali baada ya kupokea malalamiko hayo, ilihakiki na baada ya kujiridhisha mwezi Agosti, 2000, ilitoa idhini ya kulipa tena kiasi cha Sh. 273, 816, 703 kwa ajili ya mapunjo ya mishahara na mafao ya wafanyakazi hao” aliongeza.

  Hata hivyo, Mhe. Magige hakuridhishwa na majibu ya Dkt. Kijaji na alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisema kuwa Serikali imewalipa wafanyakazi hao awamu ya kwanza tu na hawakupewa nyongeza yoyote licha ya kuwasilisha malalamiko hayo.

  Mhe. Magige aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ilishawahi kwenda kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu, na Serikali iliipa jukumu la kusimamia malipo hayo Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo mpaka sasa bado haijalipa.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (MB), Mhe. Ramo Makani aliliomba Bunge limpe muda wa kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili aweze kutoa majibu sahihi.

  0 0


  0 0

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimpima Mama Mjamzito moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 kati ya hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.Picha na Anna Nkinda – JKCI.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ametembelea Tenki la Maji la terminal lilipo karibu na chuo kikuu cha ardhi ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu na chini.

  Pia ametembelea tenki kubwa jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na ametembelea Ofisi za Dawasco Mkoa wa Kibaha na kumalizia ziara yake kwa kutembelea mtambo wa kuzalishia Maji wa Ruvu juu ambapo umeanza kuzalisha maji mapya leo.
   Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa ameambatana na Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco,mhandisi, Cyprian Luhemeja katika ziara ya kutembelea   Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
   Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa DAWASA, mhandisi Romanus Mwangingo, akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhusu tenki jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mtambo huo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
   Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco, mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
   Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji leo jijini Dar es Salaam.
   Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakimsilikiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
    Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana.
  Sehemu ya mtambo wa kusafirishia maji.
  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu ambaye pia Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiongea na Watendaji wa Wilaya ya Mufindi (haapo pichani) katika Mkoa wa Iringa wakati wa mkutano kati ya Wajumbe wa Kikosi Kazi na Watendaji wa Wilaya hiyo.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wialaya ya Mufindi wakisikiliza maoni mbalimbalimbali ya Wajumbe wa kikosi kazi cha kuimarisha ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilchoteuliwa na Mkamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania (hawapo pichani) .
  Katibu Tawala wa Mkoa wa mbeya Bibi Mariam Mtunguja akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikosi kazi hiko kilipotembelea Wilaya ya Mufindi.

  ………………

  Halimashauri ya Wilaya ya Mufindi imepewa mwezi mmoja kuhakikisha vyanzo vote vya maji vinaainishwa, kutambuliwa na kuhakikisha shughuli zote zinazosababisha kukauka kwa vyanzo hivi zinaachwa mara moja.

  Aidha Halmashauri imeangizwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kutenga maeneo ya mashamba ya kulima chakula na maeneo ya kupanda miti ili wananchi wawe na ardhi ya kujitosheleza na endelevu ya kilimo cha mazao ya chakula. Kwa sasa miti inapandwa kila sehemu na vijiji vingi sasa havina maeneo ya mashamba ya kilimo cha vyakula ya kutosha na hivyo kusababisha wananchi kuendelea kuvamia mabonde kwa ajili ya kilimo cha Vinyungu.

  Maagizo haya yametolewa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Taifa cha kunusuru na kuweka mikakakti endelevu ya kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea wakati wa mkutano wa Kikosi kazi pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 
   
  Aidha ameangiza mpango kazi wa utoaji wa elimu kwa wananchi katika hali endelevu kwa vijiji vyote 121 ambao utawaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya Mto Ruaha mkuu na vyanzo vote vya maji uwasillishwe katika sekretariat ya kikosi kazi ndani ya siku nne ili kujua ni jinsi gani wilaya itahahakikisha suala la elimu kwa umma linakuwa endelevu.

  Wakichangia katika kikao hiko, Wajumbe mbalimbali wa kikosi kazi hiko wamesisitiza juu ya Watendaji wa Wilaya hiyo kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria za ardhi na Mazingira ili kuwezesha ikolojia ya mto Ruaha mkuu inatunzwa vizuri.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariama Mtunguja, alisisistiza haja ya kila mtendaji kujituma na kuacha kutoa visingizio vya ukosefu wa fedha kwa kila kazi ambazo hazijafanyika hata zile ambazo ni wazi hazihitaji fedha yoyote. Alihoji kwa nini hata kazi ya kuweka mipaka ya vyanzo via maji vinavyojulikana kwa kupanda miti ya asili katika mipaka hiyo kunasubiri fedha ya serikali kuu.

  Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William alishukuru kikosi kazi hiko kwa kufika katika Wilaya yake na ameahidi kusimamia na kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na kikosi kazi hiki. Aidha Viongozi mbali mbali wakiwemo Madiwani na Wevyeviti wa Halmashauri wamekubaliana na maelelezo ya kikosi kazi kuhusu hatua kali kwa watakaokaidi maagizo ya serikali kuhusu kunusuru mto Ruaha mkuu ili kunusuru mazingira na kuwepo kwa uhakika wa maji kwa watumiaji wote.

  Kikosi kazi hicho kimeundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni jitahada za kuweza kuokoa ikolojia ya mto Ruaha mkuu ambao unazidi kuharibika siku hadi siku kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli mbali mbali za ki binadamu katika vyanzo vya maji ya mto huu.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (Kushoto) akionyeshwa na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG toka nchini India maeneo ambayo maji yanapita kuelekea kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika eneo la tanki la maji safi lililopo Kibamba 19 Aprili, 2017.

  Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (DAWASA), Bw. Romanus Mwangingo (aliyevaa tai) akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (Kushoto) kuhusu maendeleo waliyofanya katika kusambaza maji kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika eneo la tanki lililopo Kibamba 19 Aprili, 2017.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG, Watendaji toka DAWASA na DAWASCO wakati wa ziara yake ya kikazi leo 19 Aprili, 2017.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akimsikiliza Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo wakati akieleza taarifa ya maendeleo ya usambazaji maji kwa wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo leo 19 Aprili, 2017.

  Baadhi ya Maofisa Waandamizi wa DAWASA na DAWASCO wakifuatilia taarifa ikiyosomwa na Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo (hayupo pichani) mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo leo 19 Aprili, 2017.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo(wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali na Watendaji wa DAWASA na DAWASCO pamoja na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakielekea katika sehemu ya mtambo wa kusukuma maji (IN TAKE) ambao unasukuma maji kwenda mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakati alipofika eneo la Mto Ruvu kujionea namna maji yanavyokusanywa na kusukumwa kwenda mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakiwa katika mazungumzo katika eneo la mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017.  Na Mwandishi Wetu.


  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiaji Prof. Kitila Mkumbo leo ametembelea Mtambo wa Ruvu Juu uliopo eneo la Mlandizi Mkoani Pwani na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kupitia Wizara anayoiongoza.
      

  Akiwa mtamboni hapo alipata fursa ya kushuhudia mtambo huo ukifanya kazi kama ilivyotarajiwa baada ya upanuzi wake kukamilika, ambapo hivi sasa mtambo una uwezo wa kuzalisha maji safi na salama kiasi cha lita milioni 196 kwa siku.  


  Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani hapo, Prof. Kitila amesema kwamba ziara hiyo ni muhimu kwake kwa kuwa amejifunza mambo mengi kuhusu namna maji yanavyopatikana ambapo ametoa pongezi kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika eneo hilo.


  “Uwekezaji huu ni mkubwa sana uliofanyika katika eneo hili, uwekezaji huu unahitaji kutunzawa ili kudhibti upotevu wa maji”, alisema Prof. Mkumbo.


  Amewataka Mameneja wa Miradi ya Maji kuhakikisha kuwa wanajiwekea malengo katika kuwahudumia wananchi na ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba wanayatunza maji wayapatayo kwakuwa upatikanaji wake ni mrefu na Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuyapata maji hayo.


  Aidha, Serikali imetekeleza mradi huo kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) ambapo katika ziara yake hiyo ameweza kupita na kujionea maeneo mbalimbali yanayozalisha maji na kuyahifadhi ikiwemo Matenki ya maji yaliyopo eneo la Chuo Kikuu cha Ardhi yenye ujazo wa lita milioni 45, tenki la maji safi la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10, Ruvu Darajani (In-take), Mtambo mpya wa Ruvu Juu.


  Sambamba na ziara hiyo, Prof. Kitila alipata wasaa wa kutembelea Ofisi ya Dawasco iliyopo Kibaha na kuktana na watendaji wa ofisi hiyo akiwemo Meneja wa DAWASCO Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo ambaye alitoa taarifa yake kuhusu maendeleo yaliyofikiwa katika kuhakikisha kuwa maji yanawafikia wananchi jambo ambalo lilimfurahisha Prof. Kitila.


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Bw. Romanus Mwangingo ameeleza kuwa, kwa sasa tayari maji toka Mtambo wa Ruvu Juu yameanza kuzalishwa baada ya shughuli za upanuzi katika mtambo huo kakamilika.


  Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na kuhudhuriwa na Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, DAWASA, DAWASCO, Wakandarasi pamoja na Mshauri wa mradi wa mfumo wa maji wa Ruvu Juu.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akijibu swali la Mhe. Raisa Adallah Musa Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu mapema leo asubuhi, amesema kuwa Wizara kwa kutumia bajeti ya maendeleo ya Serikali na vyanzo vingine vya mapato inaendelea kutekeleza mkakati wa kurekebisha na kuboresha miundombinu ya Ofisi za Balozi na makazi ya watumishi wa ubalozini katika maeneo mbalimbali yenye uwakilishi Duniani. 

  Mkakati huu unahusisha ukarabati wa majengo yaliyopo, ujenzi wa majengo mapya, sambamba na ununuzi wa majengo mapya. Mkakati huu unaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha ujao 2017/2018. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akijibu maswali kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge katika Kikao cha Bunge kwenye kipindi cha maswali na majibu

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

  Makamu wa Rais M


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.
  Makamu wa Rais amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara mbili jambo ambalo amesema halifai hata kidogo.

  Makamu wa Rais amemtaka Kamishna wa TRA kukomesha mara Moja tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara bali watumie lugha nzuri ili kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.

  Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

  Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA nchini Charles Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Kamishna Kichere amesisitiza kuwa kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi ataendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kurejesha nidhamu katika utendaji wa kazi na ukusanyaji wa mapato.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Bw. Charles Kichere (kushoto) aliyemtembelea leo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere (kushoto)ambaye aliongozana na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi TRA Bw. Richard Kayombo (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA)Tanzania Bi. Mariamu Mwayela mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Kichere.
  he Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

  Makamu wa Rais amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara Mbili jambo ambalo amesema halifai hata kidogo.

  Makamu wa Rais amemtaka Kamishna wa TRA kukomesha mara Moja tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara bali watumie lugha nzuri ili kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.

  Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

  Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA nchini Charles Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Kamishna Kichere amesisitiza kuwa kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi ataendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kurejesha nidhamu katika utendaji wa kazi na ukusanyaji wa mapato.


  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere,alipokutana nae leo Ikulu jijini Dar, kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere,alipokutana nae leo Ikulu jijini Dar, kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  0 0

  Tumekusogezea kwa kina mpambano wa masumbwi ulio wakutanisha Benson Mwakyembe na Mada Maugo , Dullah Mbabe na Mwaipopo siku ya jumatatu ya pasaka mkoani Ruvuma

  Kama ulikosa mahojiano ya wali ya mpambano basi haya hapa chini bonyeza play.

  0 0


  Na Grace Michael, Dodoma.

  Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wamepongeza mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaojulikana kama Toto Afya Kadi kwa kuwa ni msaada mkubwa kwa watoto chini ya umri wa miaka 18.

  Mbali na mpango huo, wamesema kuwa hatua kubwa ya uboreshaji wa huduma za matibabu uliofikiwa na Mfuko huo kwa sasa unatoa hamasa kwa Watanzania kujiunga na huduma zake na kunufaika nazo.

  Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti mjini hapa wakati wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji ambayo yalizinduliwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambayo yatahitimishwa Aprili 22, mwaka huu.

  “Kwa kweli NHIF kwa sasa tunawapongeza sana hasa kwa kuwa na madirisha mengi ambayo yanamwezesha kila mwananchi kujiunga na kutumia huduma za Mfuko huu…awali Mfuko ulihudumia watumishi wa Umma tu lakini kwa sasa tunashukuru na tunawapongeza kwa hili,” alisema Bw. Sebastian Kingu.

  Akizungumzia huduma za matibabu mmoja wa wanachama waliotembelea banda la Mfuko, Bi. Prisca Peter alisema kuwa Mfuko umekuwa mkombozi mkubwa wa afya za wananchi wengi na imesaidia kwa kiasi kikubwa hasa wanachama wake wanapopatwa na maradhi yanayohitaji fedha nyingi.

  “Mimi binafsi niushukuru sana Mfuko huu maana mpaka sasa katika familia yangu tumepata huduma ya upasuaji tena mkubwa ambao bila Mfuko ingeleta shida kubwa ndani ya familia lakini kwa kuwa tunahudumiwa na Mfuko tulipata matibabu vizuri kabisa bila kutoa hata shilingi moja,” alisema Bi. Prisca.

  Alipotembelea banda hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na utaratibu huu wa kupata huduma kupitia Bima za Afya hivyo akautaka Mfuko kuongeza kasi ya utoaji elimu na uhamasishaji kwa wananchi.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa ukishiriki shughuli mbalimbali zinazofanyika kwa wananchi kwa lengo la kuwafikia Watanzania wengi na kutoa huduma bora ya matibabu.

  Katika maonesho hayo, Mfuko unatoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko kupitia makundi yaliyowekwa ili wanufaike na huduma za matibabu.

  Akizungumzia hilo, Meneja wa NHIF, Mkoa wa Dodoma Bi. Salome Manyama alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unatoa huduma nzuri na bora zaidi kwa wanachama wake lakini pia kuhakikisha unahamasisha wananchi kujiunga ili wanufaike na huduma zinazotolewa.
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Dodoma, Salome Manyama akipokea cheti cha ushiriki wa Maonesho ya Mifuko ya Uwezashaji kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde akimsikiliza Meneja wa NHIF, Mkoa wa Dodoma Salome Manyama alipotembelea banda la Mfuko katika Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde akisaini kitabu cha wageni katika banda la NHIF.
   Ofisa wa NHIF, Enock Humba akitoa elimu kwa wananchi waliofika bandani hapo.
  Maofisa wa NHIF, Grace Michael na Enock Humba wakihudumia wananchi waliofika bandani hapo kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu huduma za Mfuko.

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akimuapisha Mhe. Dkt Getrude Rwakatare kuwa Mbunge.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akimkabidhi Mhe. Dkt Getrude Rwakatare vifaa vya kazi mara baada ya kumuapisha kuwa Mbunge leo Aprili 20, 2017 Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. 
   Naibu Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
   Mbunge wa Kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali  katika kikao cha tisa  cha Mkutano wa kumi wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Suzan Kolimba akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
   Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Mhe Cosata David Chumi  akiuliza swali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
   Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Stella Manyanya akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwele akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Igunga Mhe. Dalali Kafumo wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. 
  Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO

  0 0  NA: Abuu Kimario – BODI YA FILAMU

  Waingizaji na Wasambazaji wa Filamu za nje watakiwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya filamu nchi.

  Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati akizungumza na wadau wa Sekta ya filamu nchini mara baada ya kupokea maandamano ya Amani ya waigizaji wa Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) katika makutano ya mtaa wa Magira na Lukoma, Kariakoo Jijini Dar es Salaam leo.

  Makonda amesema kuwa lengo la Serikali siyo kuwazuia wafanyabiashara hao, bali inawataka wafuate sheria na taratibu zinazosimamia sekta hiyo muhimu katika maendeleo ya taifa letu.

  “Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam haitawaonea haya wafanyabiashara wote wanaouza kazi za wasanii wa muziki na filamu ambao hawazingatii sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hizo kwani kufanya hivyo kunalikosesha taifa mapato yatokanayo na Kodi na kusababisha kukosekana kwa uwiano kwenye ushindani wa kibishara kati ya filamu za ndani na filamu kutoka nje ya nchi,” alisema Makonda.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao akiwasilisha salamu za Waziri wa Wizara hiyo alisema kuwa, Waziri Mwakyembe anasikitishwa na uharamia unaofanywa na wafanyabishara wasiokuwa waaminifu na kusababisha kudumaza kazi za wasanii wazawa.

  Aliongeza kuwa Serikali haitaishia kufanya operesheni za kushtukiza pekee, badala yake Serikali imeendelea kufanya maboresho ya Sera na Sheria zinazosimamia kazi za wasanii nchini ili ziendane na wakati.

  Awali akitoa ufafanuzi kuhusu sheria Na.4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya kuigiza nchini alisema kuwa waingizaji na wasambazaji wa filamu za kutoka nje nchi wanao wajibu kisheria kuwasilisha kazi zao katika ofisi zake kwa ajili ya ukaguzi ili kujiridhisha kama kazi hizo zinakidhi vigezo vya kisheria ikiwemo maudhui na maadili, kisha zinapangiwa madaraja kulingana na maudhui yake.

  Fissoo alisema kuwa sheria pamoja na kanuni zake hazihishii tu kwa watengenezaji na wasambazaji wa filamu za ndani, hivyo ni vyema wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo wakazingatia sheria hiyo na kanuni zake, kinyume chake ni uvunjifu wa sheria kwa makusudi.

  “Niseme tu kuwa lengo la Serikali sio kuwazuia kufanya biashara yenu ya uingizaji na usambazaji wa filamu za nje, kinachofanyika ni kuhakikisha mnafuata sheria na taratibu kama wafanyabiashara wengine ili kuleta usawa kwenye ushindani wa kibiashara”, alisema Fissoo.

  Kwa muda sasa Serikali imekuwa ikihamasisha wafanyabiashara wa kazi za Muziki na Filamu kuzingatia sheria ili kulinda maslahi ya pande zote. Kikao cha leo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wa Wizara na taasisi zinazosimamia kazi za wasanii nchini ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha inatekeleza ahadi yake ya kuinua hadhi na maslahi ya wasanii.

  0 0


  Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali yao na kuvipa muda vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha matatizo na wahusika.

  Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo vya kihalifu au viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu iliyotawala nchini kuhusu vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.

  Waziri mkuu amesema “tukitoa taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini chanzo chake alisisitiza,”.

  Kadhalika Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.

  Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane lililotokea miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa Taifa lina mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana nayo katika mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi kuainisha namna wanavyoshirikiana.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo vyetu vina weledi,vifaa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi juu mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la mtu kutoweka au kufariki na haina kikomo cha uchunguzi, mara zote uchunguzi unategemeana na aina ya tukio lenyewe au mazingira lilipo tokea

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama vyote vya Ushirika nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na mwenendo mbaya hali inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha tamaa wakulima.

  Amesema hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika wilayani Bagamoyo Bodi ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 30 ambapo Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini upotevu wa sh. bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.

  Hata hivyo amesema kwamba hasara hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vya ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata na wilaya, ambavyo vyote vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa.

  Amesema matatizo hayo yako katika vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya Tumbaku, Kahawa,Pamba, Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali imeanza kupitia taarifa za ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na sasa wanaendelea na uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.

  Waziri Mkuu amesema wakimaliza kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha tumbaku watachunguza vyama vingine vya pamba, kahawa na chai lengo likiwa ni kuwalinda wakulima na kuhakikisha wanapata tija. “Naomba kusisitiza hatua zinaendelea kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na ushirika,”.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma Kikwete aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ubadhirifu wa sh. bilioni 30 uliofanywa na Bodi ya Korosho nchini.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S.L.P 980, DODOMA
  ALHAMISI, APRILI 20, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,  (kulia) bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017.

older | 1 | .... | 1205 | 1206 | (Page 1207) | 1208 | 1209 | .... | 1897 | newer