0 |
|
0 |
|
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh. Bil.3.2 zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania
Ahadi hiyo imetole Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deo Ngalawa (CCM), aliyehoji Serikali ilikuwa na mpango gani wa kuwalipa Wastaafu hao yenyewe moja kwa moja bila ya kutumia fedha za mfuko wa Shirika hilo.
‘’Shirika linasuasua kujiendesha, fedha ambazo zilikuwa zitumike kwenye operation ndizo hizo zimekuwa zikitumika kuwalipa Wastaafu wa Afrika Mashariki ili kulinusuru Shirika hilo serikali haioni umuhimu wa kulipa deni hilo”.alihoji Mhe. Ngalawa.
Mhe, Ngalawa alitaka kujua kwanini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwaka 2016 ilifungia akaunti za Shirika la Posta Nchini, kutokana na kuliidai Shirika hilo kiasi cha Sh. Mil.600, ikiwa Shirika hilo linaidai Serikali kiasi cha Sh. Bil.5.
Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa na Serikali yenyewe na sio Shirika.
Aliongeza kuwa watumishi wote wa Shirika hilo wamekwisha jiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii, na wanachangia katika mifuko mbalimbali hivyo wakistaafu mifuko hiyo itakuwa ikiwalipa mafao yao na si Serikali tena.
Naibu waziri huyo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni hayo kadri fedha zitakapopatikana, watahakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu fedha zote zinazodaiwa na Shirika hilo zitakuwa zimelipwa.
Katika swali la msingi, Mhe. Ngalawa , alitaka kujua mpango wa Serikali wa kulirejeshea Shirika fedha ambazo lilitumia kuwalipa Wastaafu waliokuwa Shirika la Posta na simu la Afrika Mashariki, kunusuru Shirika hilo.
Akijibu hoja hiyo Dkt. Kijaji alikiri kuwa Shirika limekuwa likitumia fedha zake kuwalipa Wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki na kuwasilisha madai Serikalini ili lipate kurejeshewa fedha zake.
Aliongeza kuwa hadi sasa Shirika limelipa Sh. Bil. 5.9 na Serikali imesharejesha kiasi cha Sh. Bil. 2.7, alisema malipo hayo yamekuwa yakilipwa kwa awamu ambapo kwa mwezi Novemba 2016 kiasi cha Sh. 700,000,000, Desemba 2016 Sh. 1,000,000,000 na Januari 2017 Sh. 1,000,000,000.
Dkt. Kijaji amesema pia kuwa Serikali itaendelea kurejesha kiasi kilichobaki cha Sh. 3,200,000,000 kadri fedha zitakavyopatikana.
‘Serikali kupitia Msajili wa Hazina inaendelea na jukumu la kuwalipa Pensheni ya kila mwezi Wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki wapatao 292’. Aliongeza Dkt. Kijaji.
Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
0 |
|
0 |
|
fisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akimtembeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo katika baadhi ya ofisi za kampuni hiyo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto)akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akieleza kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, mipango na mikakati ya kampuni hiyo katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama katika jiji la Dar es Salaam wakati Katibu Mkuu alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO)pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipowatembelea mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Archad Mutalemwa (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) wakati Katibu Mkuu alipokutana na watedaji wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA), katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akizungumza na watendaji wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) wakati alipowatembelea mapema hii leo katika Ofisi za DAWASCO jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
…………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) zatakiwa kuongeza kasi ya usambazaji kwa wananchi ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwa kuwapa huduma za msingi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wakati akiongea na Menejimenti ya Mamlaka hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Profesa Kitila amesema kuwa licha ya ongezeko la upatikanaji wa maji, ipo vhangamoto ya idadi kubwa ya wananchi kutofikiwa na huduma hivyo hivyo ni lazima sasa Mamlaka husika kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa.
“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi, kwakufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi,” alisema Profesa Kitila.
Aidha Profesa Kitila ametoa rai kwa wateja wote wa Dawasco na Dawasa zikiwemo taasisi za umma kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazopatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa katika kuhakikisha uzalishaji wa maji umeongezeka kwa kutoka lita za ujazo wa mita 160 Milioni kwa siku hadi kufikia lita za ujazo mita 271Milioni kwa siku ambazo ni sawa na asilimia 100.37% ya lengo la upatikanaji wa maji ambalo ni lita 270 Milioni kwa siku.
Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa jumla ya Vizimba 560 (Gati za kuuzia maji) vimeunganishwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ikiwa ni muendelezo wa kuongeza kasi ya usambazaji na upatikanaji wa huduma ya maji miongoni mwa jamii.
Katika hatua nyingine Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema kuwa katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha wanakina mama wanatua ndoo za maji kichwani Dawasco inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa kuongeza usambazaji wa huduma ya maji katika eneo la takribani 1,427Km unaohusisha maeneo ya Tegeta, Mpiji hadi Bagamoyo ifikapo mwezi Julai mwaka huu ambapo tayari fedha Tsh. 117Bilioni kwa ajili ya mradi huo zimepatikana kupitia Benki ya Dunia.Mradi huo utakapokamilika unakadiriwa kuongeza idadi ya watumiaji wa maji takribani laki moja.
Katika kuhakikisha inafikia azma ya kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi Dawasco inaendesha Kampeni ijulikanayo “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani Ndani ya Siku 90” ikiwa na lengo la kuwaunganisha na huduma ya maji wateja takribani 151,000 wataunganishwa na huduma hiyo katika eneo linalopakana na Barabara ya Morogoro. Kampeni hiyo imeanza kuanzia tarehe 1 Aprili hadi 30 Juni, 2017.
0 |
|
0 |
|
D: MTU WA MISIMAMO
Baada ya kumaliza darasa la nane Tabora, alipata nafasi ya kusoma chuo kikuu cha Makerere Uganda. Alisomea ualimu na alihitimu diploma mwaka 1947. Aliporudi Tanganyika, alipata nafasi ya kazi kutoka misheni na serikalini. Serikalini kulikuwa na mshahara mkubwa na marupurupu mengi kuliko misheni lakini alikataa kufanya kazi serikalini akipinga mfumo wa tofauti kubwa ya malipo.
Misimamo yake ya kupinga sera za kikoloni ilimgharimu kwani serikali ya kikoloni ilikataa kumpa nafasi ya masomo nje ya nchi. Ni kwa utetezi tu wa rafiki yake mkubwa, Father Walsh, ndipo alipokubaliwa kwenda kusoma chuo kikuu cha Edinburgh cha Scotland Uingereza, aliposomea historia, uchumi na falsafa.
E: MTU WA KUJISHUSHA
Chuoni Edinburgh alihitimu na kupata Masters na kuwa mtanganyika mweusi wa kwanza kupata mafanikio hayo. Hata hivyo, hakupata kiburi na aliporudi, akaenda kijijini kwao Butiama ambapo alijenga kwa mikono yake mwenyewe nyumba yake ili afungie ndoa na mchumba wake Maria Magige. Alichanganya saruji na mchanga yeye mwenyewe na kufyatua matofali. Wanakijiji walimshangaa msomi kama yeye kushika tope...wasomi wa wakati huo, wengi wao darasa la nne tu lakiji walikuwa daraja la juu sana.
F: MSHAWISHI
Alijiunga na harakati za siasa chini ya TAA. TAA hakikuwa chama cha siasa moja kwa moja bali kikundi cha kudai baadhi ya haki ambazo zilikuwa za wazungu pekee. Akawashawishi wazee aliowakuta wabadili malengo na kuanzisha chama rasmi cha siasa kitakachodai uhuru kamili badala ya haki fulani pekee. Wazee wakakubali na kuanzisha TANU, Julai 7, 1954 na yeye akawa mwenyekiti. TANU ikafanikiwa kuleta uhuru, 1961.
Lakini ushawishi mkubwa kabisa katika historia yake na ya nchi ni ule wa mwaka 1958 aliposhawishi wajumbe wa TANU kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa baraza la kutunga (LEGCO). Vyama mbalimbali vilitakiwa kushiriki na chama kitakachopata wajumbe(wabunge) wengi ndicho kitakachounda serikali.
Huu ndiyo uchaguzi wa kwanza kabisa nchini na mkoloni aliweka masharti magumu kwa waafrika kupiga ili kukandamiza haki zao. Masharti hayo ni kuwepo kwa viti vitatu vitakavyoshindaniwa kwa matabaka(wazungu, waasia na waafrika) huku waafrika wakitakiwa kupiga kura zote tatu. Lengo la mkoloni lilikuwa kuhakikisha baraza la kutunga sheria linakuwa na wajumbe sawa, yaani waafrika, wazungu na wahindi. Kutokana na sharti hili, uchaguzi huu uliitwa UCHAGUZI WA KURA TATU.
Masharti mengine ya kumuwezesha mwafrika kupiga kura ni kuwa na kipato cha pauni mia nne za Uingereza kwa mwaka, pia awe na kiwango cha elimu ya darasa la 12(form four) na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.
Masharti haya yaliwakera wazee na wanachama wa TANU. Viongozi wa makao makuu na majimboni wakapanga kuususia.
Nyerere peke yake alitaka TANU ishiriki uchaguzi huu kwa sababu alihisi kama ingesusa, chama cha wazungu cha United Tanganyika Party(UTP) kingepata mteremko na kuzoa viti vyote na kuingia kwenye baraza la kutunga sheria huku TANU kikibaki nje. Kupitia fursa hiyo, wazungu wangetunga sheria kali zaidi za kuchelewesha uhuru kwa kisingizio kwamba waafrika hawajawa tayari kujitawala huku mfano ukiwa kususia uchaguzi.
Nyerere aliona mbali zaidi ya wenzake ndani ya chama.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Septemba 1958, TANU ikapanga kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa 1958 mjini Tabora kuanzia Januari 21-26, 1958 kuamua hatima ya uchaguzi.
cc. Zaka Zakazi
0 |
|
0 |
|
 |
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara wa kilimo cha pamba Riyaz Haider wakati wa akitembelea maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi, baada ya mfanyabiashara huyo kupata mkopo kutoka katika benki kuu ya Tanzania kupitia benki ya NMB. ................................
Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotewa na Mfuko huo.
PPF inatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya unatoa elimu juu ya mfumo wa ' Wote scheme' kwa sekta isiyo rasmi yaani wale wanaojiajiri kama vile mama lishe, dereva boda boda, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, Wasanii, wote hawa wanathaminiwa na PPF ndio maana unato fursa za huduma za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao ya uzeeni.
Kupitia Maonesho haya PPF inasajili wanachama wapya hapo hapo viwanjani pamoja na kukabidhi vitambulisho vya uanachama wa Wote scheme.
Hivyo ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Maahujaa kupata elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu ili kufaidika na Wote scheme.
Na kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu nao
|
 |
Mkurugenzi mtendaji wa asasi inayochochea uwekezaji sekta binafsi kwenye kilimo ( PASS ) Nicomedy Bohai akimuelezea mafanikio ya asasi hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani Dodoma. |
 |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa cheti kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa udhamini wa Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio, kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama. |
 |
Mzee Seleman Saleh akiwasikiliza Linda Mshana meneja wa mikopo kushoto na Mary Kapeja mkuu wa kitengo cha masoko na biashara wa UTT Microfince PLC kulia katika maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. |
 |
Enock Humba, Afisa matekelezo wa bima ya afya na Grace Michael afisa masoko wa elimu kwa umma wakitoa maelekezo wa watu waliotembelea banda la mfuko wa bima ya afya katika viwanja ya mashujaa mkoani Dodoma. |
 |
Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian akimuelezea kazi za PPF ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko huo kama vile ' Wote scheme' mmoja wa watu waliotembelea Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. |
 |
Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matilo fursa zilizomo ndani ya mfumo wa ' Wote scheme' wakati alipotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. |
 |
Moja ya watu waliojitokeza katika maonesho ya mifuko ya uwezekezaji na uchumi toka jamii ya wafugaji akiwa katika banda la PPF ambalo wameanzisha mfumo unaotoa fursa kwa watu wote (hata wasioajiriwa) kuweza kuchangia kima cha chini Tsh 20,000 kwa mwezi ambao utamwezesha mchangiaji kupata mafao ya uzeeni na matibabu. |
 |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa na wawakilishi wa Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi mkoani Dodoma baada ya kufungua rasmi Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. |
0 |
|
0 |
|
Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kunin’ginia.
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio.
Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.
Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
ii. Na njia ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k
SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.
VYAKULA VINAVYO CHANGIA KULETA KITAMBI
Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na :
i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.
ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.
iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo ongezwa
( added sugar ), kama vile soda na keki.
iv. Vyakula vilivyo tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate mweupe nakadhalika
v. Pamoja na vinywaji vilivyo tengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na kadhalika.
Vyakula vilivyo tajwa hapo juu, vikitumiwa bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta tatizo la kitambi.
vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo
( physical exercises ) kwa muda mrefu.
JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI.
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).
Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40 kwa wanaume na >88 cm au 35 kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.
BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.
Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.
Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.
MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
Tumekwisha ona hapo juu jinsi kitambi kinavyo patikana na vyakula pamoja na sababu nyinginezo zinazo sababisha kutokea kwa kitambi, sasa tutazame mambo yatakayo kufanya uwe katika hatari ya kupatwa na kitambi.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mambo yafuatayo huwaweka watu katika hatari kubwa ya kupatwa na kitambi :
1. Ulaji mbovu wa chakula; Ulaji mbovu wa chakula ni ulaji usio zingatia kanuni za mlo kamili. Hapa mtu hufululiza kutumia chakula cha aina fulani pekee bila kuzingatia aina nyinginezo za chakula. Mfano; mtu anaweza kuwa anakula mlo ufuatao :
Asubuhi : Mchemsho ama supu ya ng’ombe , chapatti tatu na soda moja. Mchana : Ugali nyama choma anashushia kwa maji na soda.
Jioni : Mchemsho wa kuku na bia mbili nakuendelea.
Usiku : Chips mayai au chips kuku au chips mishikaki na bia.
Mtu huyu akiendelea na utaratibu huu kwa muda mrefu, ni lazima atapatwa na kitambi.
2. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye mafuta mengi
3. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye wanga mwingi .
4. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye sukari iliyo ongezwa ( added sugar ).
5. Ulaji mfululizo wa vyakula vya ngano.
6. Ulaji mfululizo wa vinywaji vyenye ngano na sukari.
7. Kutofanya mazoezi ya mwili na viungo ( physical exercises ).
Mhusika anapokuwa katika makundi yote yali yotajwa hapo juu, hali huwa mbaya zaidi.
NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa na kitambi ni lugha ya mwili ( body-language ) inayo leta ujumbe kwako kwamba “ Mwili wako haupo salama tena “
Kama una kitambi maana yake una mafuta yasiyo hitajika mwilini, mwili wako unatumika kuhifadhi mafuta usiyo yahitaji.
Hali hii kitabibu imaanisha kwamba, ogani nyinginezo zilizomo ndani ya mwili wako zinao gelea kwenye mafuta( fats ) yasihotika yaliyomo ndani ya mwili wako, jambo linalo kuweka katika hatari kubwa sana ya kushambuliwa na magonjwa hatari kama vile shinikizo kubwa la damu, kiharusi na kisukari na kwa kutaja machache.
Hivyo basi ili kuondokana na hatari hiyo, yakupasa kupambana kuondoa hayo mafuta yasiyo hitajika mwilini mwako.
NJIA ZA KUONDOA KITAMBI.
Unaweza kuondokana na kitambi kwa kufanya diet pamoja na mazoezi ya mwili na viungo.
Vilevile unaweza kuondoa kitambi na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia dawa asilia ya kuondoa kitambi na kuondoa mafuta yasiyo hitajika mwilini.
DAWA ASILIA YA KUONDOA KIAMBI NA MAFUTA MWILINI.
Hii ni njia ya uhakika kabisa ya kuondoa tatizo la kitambi pamoja na mafuta yasiyo hitajika mwilini.
Unaweza kuondoa tatizo la kitambi pamoja na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia DAWA ASILIA IITWAYO YA MKATAA KITAMBI.
Dawa hii ni ya asili kabisa
“ Pure Herbal “, ambayo haijachanganywa na kemikali yoyote, haina side effect kwa mtumiaji na inaondoa kabisa tatizo la kitambi ndani ya siku kumi na nne.
JINSI DAWA YA MKATAA KITAMBI INAVYO FANYA KAZI.
1. Huyeyusha mafuta yasiyo hitajika mwilini.
2. Husaidia kupunguza hamu ya chakula.
3. Inazuia kutengenezwa kwa seli za mafuta ( fat cells ) katika mwili wa mwanadamu. Unapokula chakula chenye mafuta mengi, dawa hii asilia hupambana kuyafanya mafuta hayo yasitengeneze seli za mafuta mwilini mwako. Hali hii huuepusha mwili wako kuhifadhi mafuta yasiyo hitajika mwilini.
4. Husaidia kupunguza uzito wa mwili kwa haraka sana endapo itatumika pamoja na diet ya kabechi.
UFANISI WA DAWA.
Ufanisi wa dawa hii ni wa asilimia mia moja. Dozi ya dawa hii hutumika kwa muda wa siki ishirini na moja.
MATOKEO YA DAWA:
Dawa hii huondoa kabisa kitambi ndani ya siku kumi na nne.
BEI YA DAWA :
Dawa hii inaoatikana kwa kiasi cha SHILINGI ELFU HAMSINI TU (Tshs. 50,000/=)
MAHALI TUNAPO PATIKANA.
Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA.
KWA WATEJA WASIO WEZA KUFIKA OFISINI KWETU.
Kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu , tunao utaratibu wa kuwafikishia dawa mahali popote walipo ndani ya jiji la Dar Es salaam.
KWA WATEJA WA NJE YA DAR ES SALAAM.
Kwa wateja waliopo nje ya Dar Es salaam, tunawatumia dawa kwa njia ya MABASI.
Kwa wateja wa ZANZIBAR tunawatumia dawa kwa njia ya boti.
KWA WATEJA WA NJE YA NCHI:
Kwa wateja wa nje ya nchi, tunatumia dawa kwa njia ya POSTA au DHL.
WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA : 0766 53 83 84
TUTEMBELEE:
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
Balozi wa Msumbiji nchini Bi Monica Patricio Clemente akizungumza na viongozi wa TCCIA walioongozana na Makamu wa Rais-Viwanda Bw. Octavian Mshiu wa kwanza kulia, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Gotfrid Muganda pamoja na viongozi wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah-Mwenyekiti na Muhidin Swalehe.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa TCCIA mwenye dhamana ya Viwanda Bw. Octavian Mshiu akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Bw. Gotfrid Muganda pamoja na viongozi wa TCCIA Mkoa wa Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ambaye ni Mwenyekiti na Bw. Muhidin Swalehe- Afisa Mtendaji.Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa TCCIA-
Viwanda Bw. Octavian Mshiu amesema mapendekezo ambayo TCCIA imewasilisha kwa Balozi wa Msumbiji nchini yanalenga kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambao utawezesha uanzishwaji wa vituo katika mkoa wa Mtwara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na misaada ya haraka kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Makamu wa Rais wa TCCIA-Viwanda Bw. Octavian Mshiu akimkabidhi Balozi Monica Clemente nyaraka maalum baada ya mkutano na Balozi huyo ofisini kwake mapema wiki iliyopita.
Balozi Bi. Monica Patricio Clemente amesema amefurahishwa na ugeni alioupata wa uongozi wa TCCIA na kwamba mapendekezo chanya yaliyoletwa na TCCIA yana nafasi sahihi na muhimu katika kuboresha ushirikiano wa wafanyabiashara wa Mtwara na Mikoa jirani ya Msumbiji kwani mahusiano ya aina hiyo yana nafasi kubwa ya kunufaisha jamii ya wafanyabiashara, kuongeza pato la nchi zote mbili na pia kukuza uchumi wa maeneo husika.
Balozi Monica ameahidi kuyafanyia kazi majadiliano na mapendekezo ya TCCIA kwa haraka ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa mikoa inayofanya biashara pamoja ambayo matokeo yake yataleta tija kwa maslahi ya Tanzania na Msumbiji kwa ujumla
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.
Katika mkutano huo wajumbe kutoka ubalozini humo wamesema moja ya changamoto kubwa inayowakumba wafanyabiashara wengi ni lugha ambapo wamependekeza pia kuwepo kwa vituo maalum ambavyo vitakuwa vikitoa elimu ya lugha kwa wafanyabiashara hao ili kuondoa changamoto hiyo.Mwenyekiti wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ameshukuru ubalozi wa Msumbiji kwa ukarimu na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya wafanyabiashara wa Cape Delgado nchini Msumbiji na Mtwara nchini Tanzania. Pia alieleza juhudi za Chemba ya Mtwara katika kukabiliana na changamoto ya lugha na kwamba mjini Mtwara tayari kuna kituo kikubwa cha lugha kinachofundisha watanzania lugha mbalimbali ikiwemo Kireno ambacho sasa kinatiliwa mkazo zaidi.
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.
0 |
|
0 |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto) hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana, ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP, Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mifuko ya Uwezeshaji ya Serikali katika maonyesho ya mifuko hiyo yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB, Kenneth Lusesa(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia amelitaka baraza hilo lifanye tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi zinazofanana iunganishwe .
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Aprili 18, 2017) wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma. Amesema uzinduzi wa maonesho hayo ni fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha huduma.
“Lengo ni kuwa na Mifuko michache, lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi. Nitafurahi kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,” amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amesema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga kuwawezesha Watanzania wengi wafanye shughuli za kujiongezea kipato bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.
Ameongeza kuwa “uwezeshaji wananchi kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.
Amesema kuwawezesha wananchi kiuchumi, sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni jitihada za makusudi za kuwashirikisha wananchi walio wengi ambao kwa sababu za kihistoria, wamejikuta wakiwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi, hivyo kubaki kwenye hali duni jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na usalama wa nchi.
Waziri Mkuu amesema jitihada za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na kuendelezwa na awamu zote zilizofuata, ambapo kwa sasa kuna mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Amesema mifuko hiyo imesaidia upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha umaskini nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa pamoja ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 1.759 kwa wajasiriamali 400,000.
Awali Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng` Issa alisema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea wananchi uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.
Amesema kati ya mifuko 19 ya uwezeshaji mifuko 13 imeweza kushiriki katika maonesho hayo ya kwanza kufanyika nchini, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Wezesha wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank PLC, Bw. Sabasaba Moshingi aliyezungumza kwa niaba ya washiriki alisema madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa mifuko ya kuwezesha wananchi kiuchumi na fursa zitolewazo na mifuko hiyo.
Pia kuhamasisha wananchi juu ya kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika miradi yenye kuleta faida pamoja na uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi na miradi ya kiuchumi ili kuunganisha wananchi na fursa za huduma ya mikopo, mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa na mifuko hiyo.
0 |
|
0 |
|
Balozi wa Kinywaji cha Kahawa , Msanii wa Bongo Flava, (G Nako) George Mdemu akizungunza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wananachi wakionja kahawa iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Kampuni tanzu ya chakula na vinywaji nchini, imezindua bidhaa yenye mchanganyiko wa kahawa, maziwa na sukari ya “Nuru coffee Chapchap” yenye hadhi ya kimataifa na ladha thabiti.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Rayton Kwembe amesema kampuni hiyo imewawezesha Watanzania hata ya hali ya chini, kuwa na uwezo wa kuonja ladha murua yenye mchanganyiko wa maziwa, sukari na kahawa kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh 500=/
“ Nuru coffee Chapchap ni bidhaa ya kipekee na ni moja kati ya bidhaa madhubuti katika kampuni yetu. Nuru ni neno la Kiswahili linamaanisha “mwangaza” ikiwa na maana ya asili, Nishati, na matumaini . Nuru huondoa giza na kuweka dhahiri vitu vilivyofichika. Nuru hung’aa popote na kurudisha tumaini kwa watu waliokata tamaa.”
Amesema uzinduzi wa kahawa ya Nuru coffee Chapchap imekuja kwa wakati muafaka na kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa za ajira zinazotolewa nchini na kampuni hii.na pia bidhaa ya nuru coffe imekuwa nuru kwa watanzania kwani imewawezesha kujipatia chai yenye mchanganyiko wa sukari maziwa na kahawa kwa gharama nafuu kabisa kwa kuzingatia hali yetu uchumi.
“Tunayofuraha kubwa kuzindua bidhaa hii ya kiwango cha juu itakayokidhi maisha ya mtumiaji, kwa kumpatia ladha nzuri ya kahawa bora kabisa na chapchap. Nuru coffee Chapchap inatokana na aina mbili kuu za kahawa nchini, Robusta na Arabika kwa asilimia 100 na kutengenezwa kwa mchanganyiko madhubuti wa maziwa na sukari, ili kuleta ladha nzuri ya kuvutia. Tumejipanga na tuna ujasiri mkubwa juu ya bidhaa yetu mpya na hivyo hatutatetereka.”
Kwembe amesema sasa Nuru coffee Chapchap inapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Dodoma na Arusha, na pia bidhaa hii inatarajiwa kupatikana mikoa mingine nchini miezi michache baadae.
Katika kusherekea uzinduzi wa Nuru Coffee Chapchap katika soko la nchini Tanzania kampuni ya DMG Tanzania imeandaa kampeni itakayohusisha supamaketi kubwa mbalimbali kama TSN Supermarkert iliyopo kibo complex, American Super Markert pugu road na Nakumatt Mlimani City. Kampeni hiyo pia itahusisha upatikanaji wa nuru Coffee katika mitaa mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 – 25 Aprili mwaka huu.
Kitu kikubwa Zaidi katika bidhaa ya Nuru coffe ni utaalamu wa usindikaji wa bidhaaa hiyo na ufungaji wa paketi zake zinazolenga kuibua hisia ya mtumiaji kabla hata hajainunua.
0 |
|
0 |
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
AJIRA YA MADAKTARI WA TANZANIA NCHINI KENYA
Mnamo tarehe 18 Machi 2017 Ujumbe wa Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt. Cleopa Mailu uliwasili nchini ambapo ulikutana na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kuomba kuajiri kwa Mkataba Madaktari wa Tanzania mia tano (500) ili kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya. Mheshimiwa Rais alikubali ombi hilo.
Tarehe 18 Machi, 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa Madaktari wa Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Maombi hayo yalipokelewa ambapo hadi tarehe 27 Machi, 2017 ambapo jumla ya maombi takribani 496 yaliwasilishwa. Baada ya kufanya uchambuzi wa maombi haya ilibainika kuwa, Madaktari 258 walikidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Baadhi ya vigezo hivyo ni pamoja na:
· Uhakiki wa vyeti vya taaluma na vyeti vya Sekondari.
· Chuo alichosoma na mwaka wa kuhitimu masomo.
· Sehemu alikofanya mafunzo ya vitendo (Intership) na mwaka wa kuhitimu mafunzo hayo.
· Uzoefu wa kazi.
· Umri wa mwombaji usizidi miaka 55.
· Usajili wa mwombaji katika Baraza la Madaktari la Tanganyika.
· Asiwe mtumishi wa Umma, Hospitali Teule za Halmashauri na Hospitali za Mashirika ya hiyari wanaolipwa mishahara na Serikali.
Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kukamilisha utaratibu wa ajira za Madaktari wake nchini Kenya ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi hizo za kazi na kufanya uchambuzi wa maombi ya kazi, kuandaa Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya kuhusu ajira hizo za Madaktari na Mkataba wa Ajira kwa Madaktari hao, wananchi (Madaktari) watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.
Kwa kuwa ratiba ya utekelezaji wa ajira hizi za Madaktari ilikubalika na pande zote mbili kuwa iwe imekamilika ifikapo tarehe 6 Aprili, 2017 na kuwa Madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 na kwa kuwa hadi tarehe ya taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za Madaktari wa Tanzania nchini Kenya, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameamua kuwa, Madaktari hao 258 ambao waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara moja. Kufuatia uamuzi huu, Majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya Wizara www.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa Afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo.
Aidha, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini Kenya.
Imetolewa na:
Ummy A. Mwalimu (Mb),
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu cha DODOMA,
S.L.P. 743,
DODOMA.
19 Aprili, 2017
0 |
|
0 |
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo (katikati) wakiwa katika mazungumzo wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha, (kushoto) Mke wa Balozi Bibi. Meylin Suarez pia Afisa Mkuu wa Mambo ya Nje, daraja la Pili (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (GAVU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo (kushoto) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais,(kulia)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (GAVU). (Picha na Ikulu)
0 |
|
0 |
|
Ofisa wa Benki ya NMB kushoto akimkabidhi kadi yake ya benki mshindi wa shindano la bahati nasibu ya Biko baada ya kushinda Sh Milioni 10 za shindano hilo nchini Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Makabidhiano hayo ya fedha na kadi ya benki kwa mshindi huyo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB kama sehemu ya kumuandaa mshindi wa Biko kuzitumia fedha zake kwa uangalifu ili zimnufaishe kiuchumi.
Mshindi wa Biko Milioni 10 apokea fedha zake na elimu NMB
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa shindano la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Christopher Mgaya, jana amepokea fedha zake sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka Benki ya NMB ambapo alifunguliwa akaunti ya kuhifadhia fedha hizo.
Mgaya alitangazwa mwishoni mwa wiki katika droo ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akisikiliza wakati Meneja Masoko wa Biko Tanzania, wachezeshaji wa bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven, wakati anafanya mazungumzo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam. Fedha hizo alikabidhiwa jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake.
Nia ya kufunguliwa akaunti katika tawi la NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam sambamba na kupatiwa elimu ya kifedha kwa mshindi huyo limetokana na kiu ya kumuandaa kijana huyo ili aweze kuzitumia ipasavyo fedha zake kwa ajili ya kumuinua kiuchumi kutokana na uwapo wa mchezo wa bahati nasibu huo unaochezwa kwa kufanya miamala ya kifedha kwenye Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money.
Ofisa wa NMB akimkabidh mshindi wa Biko kadi yake ya ATM ya benki hiyo tayari kwa matumizi yake.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akipokea fedha zake alizoshinda baada ya kutangazwa mwishoni mwa wiki na kukabidhiwa mapema jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.
Akizungumza katika ufunguzi wa akaunti ya mshindi wao huyo jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwa mshindi wao wa Sh Milioni 10 wameona wasimuache hivi hivi badala yake wakaamua kumfungulia akaunti NMB sanjari na kupatiwa elimu ya kifedha ili zimuendeleze kimaisha.
“Biko ushindi ni nje nje kwa kuwa lengo letu ni kuwafanya Watanzania wafanikiwe kimaisha kwa kuutumia vema mchezo wetu huu kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili kwenye simu zao za Mpesa, Tigo Pesa na Airtel Money kisha kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.
“Biko tunalipa kwa haraka kwa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya ushindi wa Sh Milioni 10 inayopatikana kwa kuchezeshwa droo kila mwisho wa wiki italipwa kwa njia ya hundi na kumuingizia fedha zake benki kama tulivyofanya kwa mshindi wetu Mgaya aliyeibuka na ushindi kutokea Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,” Alisema.
Naye Mgaya alisema kwamba anawashukuru Biko kwa kumpatia zawadi yake kwa haraka sambamba na kumpeleka NMB ili apatiwe elimu namna gani atazitumia fedha hizo ili zimuendeleze badala ya kuzitumia kwa matumizi yasiyokuwa ya lazima.
“Wakati nashiriki kucheza Biko sikutaraajia kama ningeshinda, lakini baada ya awali kushinda pia Sh 5000, nilihamasika na kuendelea kucheza ambapo Jumapili sikuamini baada ya kupigiwa simu na Kajala akinitaarifu kuwa nimeshinda Sh Milioni 10, ushindi ambao hakika utanitoa sehemu moja kwenda nyingine hususan kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba.
“Nawashukuru Biko huku nikiwakumbusha Watanzania wenzangu kuchangamkia fursa ya bahati nasibu ya Biko kwa sababu haiitaji kujua lolote zaidi ya kucheza kwa njia ya ujumbe wa simu na kuingiza miamala kiasi cha Sh 1000 na kuendelea, huku kila Sh 1000 tunayolipa ikitupatia nafasi mbili, zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kubwa ya wiki yakuwania Sh Milioni 10,” Alisema Mgaya.
Bahati nasibu ya Biko imeanza kwa kasi kubwa nchini Tanzania, ambapo mbali na kumpatia zawadi yake ya Sh Milioni 10 mshindi wao, pia inaendelea kulipa fedha mbalimbali walizoshinda washiriki wao kwa haraka hali inayoongeza msisimko mkubwa kwa washiriki na Watanzania kwa ujumla.
0 |
|
0 |
|
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionyesha cheti maalum baada ya kuweka saini yake cha kuthibitisha uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar (RSA) hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Bara barani Tanzania DCP Mohamed Mpinga, Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Hamdan Makame.
Balozi Seif akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bibi Narsa Mohamed kutokana mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari vya Shirika hilo wa suala la usalama bara barani.
Balozi Seif akikabidhi cheti maalum kwa Mlezi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani wa Kanda ya Pwani inayounganisha Tanga na Bagamoyo Bwana Nurdin Ali kutokana na mchango mkubwa wa Taasisi hiyo uliosaidia kupunguza ajali za vyombo vya moto Bara barani Tanzania Bara. Picha na – OMPR – ZNZ.
Matukio ya uvunjifu wa sheria za usalama Bara barani bado yanaendelea kuoteza nguvu kazi ya Taifa wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.
Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya Bara bara na vifaa vyengine.
Balozi Seif alisema ajali za bara barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii sheria na taratibu zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.
Alisema baadhi ya madereva hao wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi bila ya kujali watumiaji wengine mbali mbali kama watoto ambao nao wana haki ya matumizi ya bara bara hizo.
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na baadhi ya madereva husababisha ajali za kizembe kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama Bara barani hapa Zanzibar ni wa busara na kuwa wakati muwafaka ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali za bara barani.
Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Justafa Mussa alisema Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa yanayotokana na bara bara.
Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi (ACP ) Mkadam Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea Bara barani kutokana na vitendo visivyotii usalama bara barani.
Alisema ajali za bara barani zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya watu 147 wakati mwaka 2017 uliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 |
|
0 |
|
Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa Shirika la Nyumba nchini(NHC) limeweka mkakati wa kuhakikisha nyumba zote zilizo katika hali ya uchakavu zinafanyiwa ukarabati mkubwa na zile ambazo kiwango cha uchakavu ni kikubwa zinavunjwa na kuendeleza upya viwanja hivyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula wakati akijibu hoja mbalimblai za Wabunge leo Mjini Dodoma.
“Shirika la Nyumba la Taifa limeshafanya uhakiki wa nyumba zake zote na kubaini hali halisi ya kila nyumba na kuweka mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba hizo kwa awamu,hata hivyo nyumba ambazo zipo katika hali ya uchakavu idadi yake sio kubwa ukilinganisha na zilizopo katika hali nzuri na bora kimatengenezo”,Aliongeza Mhe.Mabula.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 shirika lilitenga takribani shiingi bilioni 11 kwa ajili ya kuzifanyia ukarabati nyumba zake ambapo hadi mwezi Machi, 2017 jumla ya nyumba 2451 zilikuwa zimekwishafanyiwa ukarabati kupitia bajeti hiyo.
Aidha amesema kuwa shirika hilo linatarajia kumaliza ukarabati wa nyumba zote katika mwaka wa fedha 2017/18 na kusisitiza kuwa matengenezo ya nyumba hizi ni kaiz endelevu kwa shirika hivyo bajeti ya matengenezo itaendelea kutengwa kila mwaka ili wapangaji wa nyumba za shirika waendelee kuishi katika nyumba na mazingira bora.
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Suleimani Jafo akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Susan Kolimba akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Mbunge wa Mwibala (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Morogoro (CCM) Mhe. Christina Ishengoma akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mhe Saverina Mwijage akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili.
Mbunge wa Chilonwa (CCM) Mhe. Joel Makanyanga akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Mbunge wa Viti Maalum Arusha (CCM) Mhe. Catherine Magige akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017
Mbunge wa Mikumi (CHADEMA) Mhe. Joseph Haule akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Mbunge wa Busokelo (CCM) Mhe. Fredy Mwakibete akiuliza swali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Naibu wake Mhe. Anastazia Wambura wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakijadiliana jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Charles Tizaba wakijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO
0 |
|
0 |
|
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akizungumza na maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA, Mkaguzi wa Uhamiaji Sokolo Kaseko akifafanua na kuelekeza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi ya kufanya Uhakiki wa Vibali Ki- elektroniki wakati wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Uhakiki wa Vibali vya Ukaazi ki-elektroniki uliofanyika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa wa vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.
Frank Mvungi-Maelezo.
Serikali imezindua mfumo wa Kielektroniki wa Uhakiki wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia mfumo huo Kamishna Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni, Taasisi, Mashirika na watu binafsi kuhakiki vibali vya watumishi wao ili kuona kama ni halali ama si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote watakaokuwa na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara inatoa siku 90 kwa watu wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana matatizo wasaidiwe kupata ufumbuzi” Alisisitiza Dkt Makakala.
Akizungumzia lengo la mfumo huo Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara hiyo.
Aidha,Idara ya Uhamiaji inawaomba wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao katika ngazi ya Wilaya, Mikoa na Makao Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.
Mfumo huo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification” unapatikana kupitia tovuti ya uhamiaji ya www.immigration.go.tz.
0 |
|
0 |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2017. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa kwenye jengo la utawala la bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 |
|
0 |
|
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga amewataka wazazi kuacha tabia ya kuiachia Serikali na mashirika binafsi kuwawezesha vijana na badala yake washiriki kuwasaidia vijana hao ili waweze kujitegemea.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya Serikali katika kusaidia maendeleo ya vijana waliomaliza mafunzo ya ufundi chini ya Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International.
Ndemanga amesema kuwa mradi huo umeleta mabadiliko makubwa kwa vijana katika eneo hilo kwani wamefundishwa sio tu mafunzo ya ufundi bali pia ujasiriamali, namna ya kuweka hisa, kujiwekea fedha kwa ajili ya matumizi ya baadaye pamoja na masuala ya kodi lakini tatizo linalojitokeza ni wazazi kuwaachia Serikali na wadau wengine kushughulikia kila kitu.
“Changamoto ni nyingi katika kusaidia vijana hasa ambao tayari walishapata mafunzo kwa sababu wazazi wakishafahamu kuwa vijana wao wako chini ya mradi basi wanawaachia mzigo wote Serikali na wadau mbali mbali hivyo nawasihi wazazi wawasaidie vijana wao katika kujitafutia ajira”.alisema Ndemanga.
Ametoa rai kwa vijana kujitokeza kwa wakati pindi miradi hiyo inapotokea kwa sababu wengi wao wamekuwa wakichelewesha kuleta maombi hayo mpaka muda wa mafunzo unafika hivyo kwa kuwa mafunzo hayo hufanyika kwa muda maalum, vijana wanatakiwa wajitokeze mapema kwa idadi kubwa.
Aidha, Ndemanga amewataka vijana waliopata mafunzo kuwafundisha wenzao na pia wanaojiajiri wakumbuke kuwaajiri vijana wengine ili kupunguza mrundikano wa vijana wanaozagaa mitaani bila kuwa na kazi za halali.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Hamida Mohamed amekabidhi cherehani mbili kwa vijana wawili waliomaliza mafunzo ya ufundi chini ya mradi huo ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha ushiriki wa wazazi katika kuwakomboa vijana hasa kwenye masuala ya kiuchumi.
“Mradi huu umetusaidia sana kuwaona vijana wenye mazingira magumu hasa walemavu na kufahamu matatizo yao hivyo kutufanya sisi viongozi wa Serikali kufahamu namna ya kuwasaidia huku tukisaidiana na wadau mbalimbali”, alisema Mhe. Hamida.
Mradi huo wa miaka mitatu 2015 hadi 2018 unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).