Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46369 articles
Browse latest View live

Wakazi wa Mbagala wakunwa na Taifa Moja concert

$
0
0



Msanii wa Bongo Fleva Harmonize akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka.
Msanii wa Bongo Fleva Rich Mavoko akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka.
Msanii wa Hip Hop Young Killer akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka.


Wakazi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake jana jumapili walipata burundani ya aina yake iliyoongozwa na wasanii kutoka kundi la Wasafi Classic Harmonize pamoja na mwenzake Rich Mavoko. Tamasha hilo lilikuwa ni maalum kwa kutoa elimu kwa wananchi juu uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambao ni muungano wa makampuni matatu ya simu za mikononi kupitia huduma za Airtel Money, Togo Pesa na Ezypesa.

Mbali na wasanii hao kutoka Wasafi Classic, Young Killer ambaye ni msanii wa hip hop pia alikonga nyoyo za mashabiki wake pale aliponda jukwaani akiwa ni msanii wa mwisho katika tamasha hilo.

Akiwa na kibao chake cha matatizo, msanii Harmonize alikuwa akilalizimiki kurudia kila wimbo alikuwa akiimba kwa mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki ambao walikuwa wamejikoteza kwa wingi.

Akiongea kwenye tamasha hilo Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio walikuwa waratibu na waandaaji wa tamasha hilo alisema kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza, elimu ya uhuru wa kutuma pesa bila mpaka kupitia kampeini ya Taifa Moja limefanikiwa.

‘Nia ya kuandaa tamasha hili ilikuwa ni kufika Watanzania wengi. Kama mnavyoona hapa kwa siku ya leo mtakubali kuwa elimu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka imefanikiwa, alisema Milinga’.

Watanzania wengi wanapenda burundani, natoa shukrani za dhati kwa wakazi wote wa Dar es Salaam na sana sana Mbagala na viunga vyake kwa kujitokeza kwa wingi na kuja kushuhudia burundani hii licha ya kuwa na hali ya mvua, aliongeza Milinga.

Milinga aliongeza kuwa kampeini ya Taifa Moja itaendelea nchi nzima kwa matamasha mbali mbali hili kuwafikia Watanzania na kuweza kujikomboa kiuchumi kwa kutumia vyema fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka tofauti na hapo zamani ambapo kulikuwa na changamoto nyingi pale mtumiaji wa mtandao mmoja alikuwa anatuma pesa kwenda kwenye mtandao tofauti.

DORIS MOLLEL FOUNDATION, CBA BANK WAKABIDHI VIFAA TIBA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (wa tatu kulia) sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Morogoro, Dkt. Ritha Liamue, Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe na kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John.
Mkuu wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel (wa pili kulia), baada ya kupokea msaada ya vitanda vitatu vya kujifungulia wakinamama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua, Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Wengine pichani ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (kulia), Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ritha Liamue (kushoto), pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe ambao ndio waliofadhili upatikanaji wa vifaa hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel kwa pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe wakimsikiliza mmoja wa wakinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati "Njiti" katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, walipotembelea wadi hiyo kutoa zawadi za Sikukuu ya Pasaka kwa wakinamama hao, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki.

MWIMBAJI JIMMY GOSPIAN ASHINDA TUZO YA ZABURI AWARDS 2016/17 KANDA YA ZIWA.

$
0
0
Mwimbaji chipukizi wa muziki wa Injili Jijini Mwanza, Jimmy Gospian (kushoto), ameibuka mshindi kwenye Tuzo za ZABURI AWARDS 2016/17 zilizotolewa jana kwa waimbaji wa Injili Kanda ya Ziwa na Kampuni ya Famara Entertainment, Uwanja wa CCM Kirumba.

Gospian kutoka ngome ya BMG, aliibuka mshindi katika kipengere cha Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kiume ambapo washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa wingi wa kura za mashabiki.

Washindi wengine kwenye tuzo hizo ni; Kwaya Bora-Mwanza Singers, Albamu Bora-Pokea Sifa ya Rebeka Pius, Mwimbaji Bora wa Kike-Betty Lucas, Mwimbaji Bora wa Kiume-Derick Ndonge, Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kike-Julieth Busagi, Kundi Bora-Kihayile Group na Tuzo ya Heshima-AIC Chang'ombe Vijana Choir.

Mbali na utoaji wa tuzo hizo, pia kulikuwa na uzinduzi wa Albamu ya PAZIA LA HEKALU iliyoimbwa na kwaya ya AIC Chang'ombe Vijana Choir
Jimmy Gospian akipokea tuzo yake, Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kiume
Jimmy Gospian anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo wimbo uliomtambulisha vyema uitwao, Nakujua Bwana
Jimmy Gospian (kushoto) akipokea pongezi kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Famara Entertainment
Baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya AIC Chang'ombe Vijana Choir

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye utoaji wa tuzo hizo

JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN

$
0
0
Mrembo wa Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. 

Molocaho by Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba 2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa pili kategori nyingine. 
 Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi
 Bidhaa zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee ilimpatia medali ya shaba kwa upande wa samani na katika bidhaa za mwanga Sayari Lamp pia ilimpatia tuzo ya shaba. Nafasi ya pili ilipatikana katika kiti cha Flamingo. Taarifa zilizofikia thebeauty zinasema kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016 na kiti cha Ngorongoro na kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016 ilikuwa na Sayari lamp. Na Kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016.Muonekano wa kiti cha Ngorongoro Settee uliompatia tuzo Jacqueline Mengi kupitia kampuni yake ya Molocaho by Amorette. 

 A-Prime Design Shindano aliloshiriki Jacqueline Mengi akiwa na kampuni yake ya Molocaho by Amorette la A’Design hushirikisha wabunifu, wagunduzi na makampuni yanayotengeneza bidhaa mbalimbali za ubunifu wa ndani. Shindano la A' Design limeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba wabunifu wanakuja na bidhaa bora kabisa zenye ushindani mkali katika soko la kimataifa. Kwa kawaida tuzo zake hutolewa katika kusanyiko kubwa la wabunifu linalofanyika Roma, Italia kwa kuratibiwa na OMC Design Studios SRL . Jacqueline, Miss Tanzania (2000) hivi karibuni alishiriki tuzo za rais za CTI na ana mafunzo ya Interior Design kutoka Rhodec International. Kampuni ya Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inajishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani. Sayari Lamp iliyompatia tuzo katika kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016. 

 Molocaho inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa. Katika mahojiano na jarida maarufu la Forbes alishawahi kusema kwamba anawania soko la kimataifa kutokana na ukweli kuwa bidhaa anazotengeneza zimejipambanua kwa watejaMuonekano wa kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016. 

 Jacqueline Ntuyabaliwe, pamoja na kuwa na ratiba yenye changamoto sana (Yeye ni balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa. 

 Mume wake, Reginald Mengi, ni tajiri mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania ambaye ameujenga utajiri wake kwa kufanya karibu kila kitu kuanzia uzalishaji wa kinywaji cha Coca-Cola hadi uchimbaji wa madini na kumiliki vituo vya televisheni na magazeti. Kwa tuzo hizo Amorette, inajidhihirisha kuwa chata yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania na huku ikipanda kwa kasi kimataifa.

KIPINDI CHA CLOUDS 360 KILIPORISHWA MUBASHARA KUTOKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.

$
0
0
Gari Maalumu la kurusha matangazo ya moja kwa moja la kituo cha Luninga cha Clouds likiwa katika eneo la Serengeti kwa ajili ya kurusha matangao ya moja kwa moja ya kipindi cha Clouds 360.
Watangazaji wa Kipindi cha Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakifungua kipindi katika eneo ambalo ni makazi ya Viboko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Watangazaji wa Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakiongea na Meneja Mawasilino wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza jambo na watangazaji hao wakati wakifanya mahojiano.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza jambo na Mtangazaji Sam Sasali.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema akizungumzia sifa za hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa .
Mwekezaji katika Sekta ya Utalii,Wily Chamburo (wa pili toka kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Musa (aliyevaa koti) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,Wiliam Mwakilema (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA ,Pascal Shelutete.(kulia).
Watangazaji Baby Kabaye na Hassan Noma wakifanya mahojiano na Mwekezaji katika Sekta ya Utalii,Wily Chamburo wakati kipind cha Couds 360 kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Watangazaji Baby Kabaye na Hasan Ngoma wakifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa wakati kipindi cha Clouds 360 kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mtangazaji wa Sport 360 katika kipindi cha Clouds 360 ,James Tupatupa akifanya mahojiano na Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete wakati akizungumzia Utalii wa kimichezo pamoja na namna TANAPA inavyoshiriki katika kukuza Michezo mbalimbali nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitoa neno la Shukrani wakati kipindi cha Clouds 360 kilipokuwa kikihitimisha ziara yake katika Hifadhi ya Taifa za Serengeti.
Wadau waliokuwepo katika shughuli nzima ya urushwaji wa kipindi cha Clouds 360 wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Watangazaji wa Kipindi cha Clouds 360 wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau mara baada ya kuhitimisha ziara ya urushwaji wa kipindi hicho katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

DC KASESELA KUWACHUKULIA HATUA KALI WAHARIBIFU WOTE WA MLIMA ULIOPO MANISPAA YA IRINGA

$
0
0
Wananchi mjini Iringa wakiendelea kufyeka miti kuandaa maeneo ya biashara

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwachukulia hatua watu wote waliohusika na uharibifu wa mlima uliopo Kata ya kitanzini miomboni kutokana na mlima huo kuwa ni hifadhi ya taifa.

Akizungumza na blog hii Kasesela alisema kuwa amesikitishwa na wananchi walivamia mlima huo na kuanza kujenga vibanda wakati kuna maeneo mengi yapo hapa Manispaa hivyo ni lazima hatua zichukuliwe kwa sababu saizi tunahangaika kutunza uoto wa asili halafu watu wengine wanaharibu.

"Nimefika katika eneo lile kweli wananchi wamevamia bila hata mimi kiongozi wa wilaya sijui nafikiri wametumia fursa ya sikukuu hii ya pasaka kufanya uharibu huo sitakubali kuona nakiuka maagizo ya Makamu wa Rais ya kutunza uoto wetu wa asili"alisema Kasesela

Kasesela amemuagiza Mkurugenzi kulifiatilia swala hilo na kukikisha inapofika kesho saa nne Vibanda vyote viwe vimevunjwa na kuanza kupanda miti maeneo yote yaliyokatwa miti na kuhakikisha eneo liloharibiwa linarudi kwenye ubora wake.

"Kufikia kesho saa nne vibanda vitakuwa vimebomolewa hatuwezi kuaharibu eneo kama lile lazima wachukuliwe hatua kuanzia wananchi hadi viongozi waliohusika na mpango huo kwa kuwa wananchi hawawezi kuanza wenyewe bila kupata ruhusa kutoka kwa viongozi furani" alisema  Kasesela

Lakini Kasesela alisema kuwa atakikisha anawachukulia hatua viongozi wenye uelewa mdogo wa namna ile kwasababu kiongozi mwenye akili na uelewa mkubwa hawezi kuruhusu kuaharibiwa eneo hilo.

Nawaomba wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya yote ya Iringa kuwa makini wanapoambiwa kufanya biashara katika mazingira yaliyohifadhiwa kwa kuwa wanaharibu mazingira makusudi na pia wanapata hasara zisizo kuwa na maana mfano walivamia huo mlima tayari wameshapata hasara lakini wameipa hasara kubwa serikali na jamii yote.

Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa umepuuza agizo hilo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinacha

UKARABATI WA KIVUKO CHA MV PANGANI WAFIKIA HATUA ZA MWISHO

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu ametembelea na kukagua kivuko cha MV PANGANI II ambacho kinafanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza katika eneo la Pangani. Awali kivuko hicho kilikuwa kikitoa huduma kati ya Pangani na Bweni kabla ya ujio wa kivuko kipya cha MV TANGA.

Dkt. Mgwatu amejionea kazi zilizokamilika zikiwa ni pamoja na matengenezo ya milango mipya ya kupandia abiria na magari na sasa kiko katika hatua za mwisho za ukarabati wake. Aidha, Dkt. Mgwatu aliweza pia kusafiri kutoka upande wa Pangani hadi Bweni kwa kutumia boti mpya ya MV BWENI iliyojengwa hivi karibuni kwa ajili ya matumizi ya dharura katika eneo hilo.

Akiwa katika ukaguzi huo, Dkt. Mgwatu aliambatana na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga Mhandisi Margaret Gina, Mkuu wa Kivuko cha Pangani Bw. Abdulrahman Amier pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TEMESA mkoani Tanga.

Vile vile, Dkt. Mgwatu alipata wasaa wa kuzungumza na wafanyakazi wa Kivuko cha MV TANGA ambacho kinaendelea kutoa huduma katika eneo hilo na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuhakikisha wanaongeza mapato. Aliwaomba wafanyakazi hao kuitunza boti ya MV BWENI ambayo itatoa huduma za dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala pale changamoto mbalimbali zitakapojitokeza.

Nae Mhandisi Gina alimueleza Dkt. Mgwatu kero mbalimbali wanazokumbana nazo kivukoni hapo ikiwemo kukosekana kwa vyumba vya ofisi kwa ajili ya wafanyakazi na kumuomba awasaidie kupata eneo kwa ajili ya kujenga ofisi. Dkt. Mgwatu alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Tanga.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu katikati akishuka kutoka kwenye chumba cha kuongozea kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani Tanga alipokuwa akikagua maendeleo ya ukarabati wa kivuko hicho. Nyuma yake ni Mkuu wa Kivuko Bw. Abdulrahman Ameir.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu wa pili kulia akikagua Kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani Tanga kinachofanyiwa ukarabati na kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza wakati wa ziara yake mkoani Tanga.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu aliyesimama katikati akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Kivuko cha MV Tanga kinachoendelea kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 18,2017


DAWASA YAKAMILISHA KAZI YA UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU JUU: SASA WAZALISHA LITA MILIONI 196 ZA MAJI SAFI NA SALAMA

$
0
0

Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana, mitambo hii ni mipya na kwa sasa ndiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa maji toka lita milioni 82 hadi lita milioni 196 kwa siku.

Hii ni sehemu ya mtambo wa kusafirishia mai mara baada ya kusafishwa, hapa ndipo maji hukusanywa na kusafirishwa moja kwa moja kuelekea kwa wananchi.

Hii ni sehemu ya mtambo unaotumika kuwashia mitambo ya kusukuma maji katika eneo la Ruvu Juu.









Laini ya Umeme unaotoka Chalinze (Sub-Station) na kufika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu lililopo Mlandizi Mkoani Pwani.

Laini ya Umeme unaoingia kutoka Chalinze (Sub-Station) na kufika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu lililopo Mlandizi Mkoani Pwani ambapo uunganishaji wake sasa umeshakamilika na umeme umewashwa.

Moja ya Transfoma mpya zilizopo katika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu ambalo linatumika kutoa umeme unaotumika kwenye mitambo katika eneo hilo.
 
Baada ya kazi ya kuunganisha umeme wa kutosha kukamilika 15 Aprili, 2017 kazi ya kuwasha pampu kubwa mpya za majighafi na majisafi katika Mtambo wa Ruvu Juu sasa imekamilika rasmi ambapo mtambo huo sasa umeanza kuzalisha lita milioni 196 kwa siku. 
 
Taarifa ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar Es salaam (DAWASA) inaeleza.li kufikia uwezo huo wa uzalishaji kutoka lita milioni 82 zilizokuwa zikizalishwa hapo awali, kazi mbalimbali zilifanyika ikiwemo ujenzi wa kituo kipya cha kusukuma maji na ufungaji wa pampu mpya, maeneo mapya ya kusafisha maji, mitambo ya kuchuja maji, maeneo ya kuchuja tope na tenki kubwa la kuhifadhia maji safi.

Katika kuhakikisha kuwa maji hayo yanawafikia wananachi, kituo kipya cha kusukuma maji safi na salama kilijengwa sambamba na mabomba makuu ya kusafirishia maji hayo yenye jumla ya urefu wa kilomita 70 kutoka Mlandizi hadi Dar es salaam.

Aidha, tenki jipya lenye uwezo wakuhifadhi lita milioni 10 limejengwa eneo la Kibamba lenye mwinuko; na kutoka hapo maji hushuka kwa nguvu ya mtiririko hadi katika matenki ya Kimara.

Kazi iliyokuwa imebaki ilikuwa ni kuongeza nguvu ya umeme ili kuwezesha pampu hizo mpya kufanya kazi. Hivi sasa kazi hiyo imekamilika, ukaguzi umefanyika na pampu moja baada ya nyingine zimewashwa ili kuhakiksha mfumo mzima sasa unafanya kazi.

Hadi kufika jana jioni (17 Aprili) maji yalikuwa yanaingia katika matenki yote kwa kupitia mabomba mapya bila matatizo.

tambo huo wa maji wa Ruvu Juu sasa unapokea umeme wa kutosha kutoka katika transfoma kubwa iliyopo kituo kidogo cha umeme cha Chalinze (Sub-station) yenye uwezo wa 45/55 MVA ambapo inawezesha pampu zote mpya na za kisasa zilizofungwa kuwashwa kwa wakati mmoja.

Mikataba ya jumla ya dola za Marekani milioni 99 ya upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mabomba mapya kutoka Ruvu Juu mpaka Kimara, ujenzi wa tanki kubwa lenye ujazo wa lita million 10, ofisi kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa huduma na nyumba za watumishi wa mtambo ilisainiwa mwaka 2014. Fedha hizo zilikuwa ni mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Exim ya India.

Kazi inayopewa msukumo mkubwa kwa sasa ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji yaliyoongezeka ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na jitihada na uwekezaji uliofanywa na Serikali yao.

Maeneo yanayonufaika ni pamoja na miji ya Kibaha, Mlandizi na baadhi ya Vitongoji vyake katika mkoa wa Pwani pamoja na maeneo yote yaliyopo jirani na barabara ya Morogoro yaani Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Malamba mawili, Msigani, Msakuzi, Makabe, Kibangu, External, Makuburi, Tabata, Segerea, Buguruni pamoja na Vingunguti.

MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia amefanya kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.

Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Raisi John Magufuli.

“”Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi Bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji mkuu lazima nisimamie kikamilifu “” Alisema Mkurugenzi Kihamia

Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa na serikali ili kusaidia wananchi.

“” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi “”Alisema Kihamia

Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika jiji la Arusha kwa kumjengea Mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango Na maduka yote,majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo yote ya wazi. 
 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia
 

KATIBU MPYA WA CCM WILAYA YA MBEYA AFUNGUKA

BOHARI YA DAWA (MSD) YAKARABATI GHALA LA DAWA HOSPITALI YA MIREMBE MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe mjini, Dodoma leo lililokarabatiwa na MSD.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimkabidhi funguo za jengo hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla hiyo.Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Dodoma, Innocent Mugisha.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia), wakati wa hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Helman Mng'ong'o na Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe, Dkt, Erasmus Mndeme.
 Jengo la kuhifadhiwa dawa katika Hospitali ya Mirembe lililokarabatiwa na MSD.
Picha ya pamoja mbele ya jengo hilo lililokarabatiwa na MSD.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya jengo hilomjini Dodma leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na ukarabati huo,watoa ushirikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa yenye utaalamu unaohitajika.

Ameongeza kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo, ikiwa ni pamoja na kukopeshwa, kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na kuomba ushirikiano zaidi na MSD, ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.

wafanyakazi 16 wa Kampuni ya Quality Group wahukumiwa kwenda jea miaka mitatu au kulipa faini.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyakazi16 wa Kampuni ya Quality Group, kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 22.

 Washtakiwa hao wametiwa hatiani baada ya wiki iliyopita kukiri mashtaka yao mahakamani hapo.Katika Hukumu hiyo, washtakiwa kila mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu katika kila kosa au kulipa faini ya sh. Milioni 1.5 kila mmoja katika kila kosa katika makosa matatu.

Washtakiwa hao walikuwa wanatuhumiwa  kwa mashtaka matano likiwemo la kufanya kazi nchini kinyume na sheria na kuzuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Washitakiwa wote wametiwa hatiani leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Hata hivyo, washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo hicho.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Jose Kiran (40), Prakash Bhatt (35) ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kufanya kazi yao.

Wengine ni  Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

Wengine ni,  Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) wote walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu ya kukutwa na visa za kughusho na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria

Hakimu Mkeha amesema,  washitakiwa 14 kila mmoja atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 1.5 kwa makosa matatu huku washitakiwa wawili wote kwa pamoja faini ya Sh milioni moja kwa kosa moja.

Imedaiwa kuwa, Februari 20, mwaka huu washitakiwa Jose Kiran, na Prakash Bhatt waliwazuia maofisa uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa kuripoti kwa Ofisa Uhamiajiwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kujaribu kukimbia nje ya nchi kupitia mpaka wa Horohoro.

Ilidaiwa kuwa kwa washitakiwa 14 wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu maeneo ya Kampuni ya Quality Group wilayani Ilala mkoa wa Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa washitakiwa wote wakiwa ni raia wa nchini India, walikutwa na visa zilizoghushiwa kinyume na kifungu namba 31 (1) (e) na kifungu namba 2 cha sheria  ya uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 2015.

 Iliendelea kudaiwa kuwaalidai katika mashitaka ya pili kuwa washtakiwa hao walikutwa wakiishi nchini kinyume na sheria.Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa hao walikutwa wakifanya kazi nchini kinyume cha sheria.

KUMBILAMOTO AWATAKA CUF KUIMARISHA UMOJA KATIKA KATA YA VINGUNGUTI

$
0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwaongoza Wanachama wa Chama cha Wananchi Cuf Buguruni kwenda kuweka bendera katika Matawi mawili ya Sarafina na Aluta, uwekaji huo wa bendera ni sehemu ya ujenzi wa Cuf  wa kuamsha wanachama kujitambua na kujenga umoja baina yao ili wasiyumbishwe.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Kumbilamoto akipandisha bendera katika tawi la Aluta kuashiria ujenzi wa CUF Taasisi na sio mtu ili kurejesha umoja na kuinua hali ya chama
 Wananchama wa Chama cha Wananchi Cuf Vingunguti wakicheza mziki katika mkutano wa chma hicho uliofanyika katika kata ya Vingunguti
 Naibu Meya wa  Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi mfuko wa Saruji kwa Mwenyekiti wa tawi la Sarafina Zaid Mohamedi kwa ajili ya ujenzi wa kizmba cha tawi.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Wanawake wa Chama cha Wananchi Cuf ambao walifika katika mkutano huo
Naibu meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwa katika meza kuu na baadhi ya Viongozi wa Chama cha wananchi Cuf katika mkutano wa kujenga Chama katika kata ya Vingunguti

TTCL YAKUTANA NA MAWAKALA ZAIDI YA 50 WILAYA YA TEMEKE

$
0
0
 Meneja Msaidizi wa wa mkoa wa Dar es Salaam Kusini wa mtandao wa simu ya Mkononi ya TTCL, Mwanaisha Semboko  akizungumza na Mawakala wa kuuza laini za Mtandao wa TTCL na kuwaeleza namna ya kuwafikia wananchi ambao hawajapata kuwa na laini za mtandao huo ili waweze kupata kutumia .

Semboko amesema kuwa Mtandao wa TTCL ni mtandao wa bei rahisi na wakizalendo, kwani fedha ambayo watapata kuchangia watanzania ni fedha ambayo inarudi katika maisha yao ya kila siku kwa kuendelea kujenga miundombinu ya mawasiliano ya Taifa hili .
 Baadhi ya Mawakala wakimsikiliza, Semboko wakati wakitoa mada ya faida za kuwa wakala wa mtandao huo
 Mratibu wa mkutano huo kutoka Makangarawe Youth , Ismail Mnikite  akizungumza na Mawakala waliofika katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Afisa Mauzo wa mkoa wa Dar es Salaam Kusini , Amina Salum  akizungumza na mawakala hao juu ya uzwaaji wa laini za TTCL na faida zake na kutaja kuwa ni mtandao wa gharama nafuu katika data kuliko yote
 Mmoja wa mawakala walioshiriki mkutano huo , Monica Harry akiuliza swali juu ya huduma zinazotolewa na matandao wa simu za mkononi wa TTCL
 Baadhi ya mawakala wakisikiliza kwa makini namna ya kuwaunganisha watu katika mtandao wa TTCL


TAASISI YA NAMELOK KUJENGA KITUO CHA ELIMU KWA AJILI YA WAJASILIAMALI WASICHANA WILAYANI KIBAHA MKOANI PWAN

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
KATIKA kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana  na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya  utoaji wa mafunzo  mbali mbali kwa lengo la kuweza  kuwapa fursa ya  kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya Mwendapole  iliyopo  katika halmashauri ya mji wa Kibaha  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi  huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake  hao kiuchumuni  kupitia  mafunzo ya stadi za kazi pamoja na  fursa zilizopo  kutokana na elimu watakayoipata.

Janet alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na  kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali  Hilda Kisoka  amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa  wanazozizalisha hapa nchini  hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza zaidi.

Alisema kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi  wa masoko katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani amekemea vitendo vya wanawake kufayiwa vitendo vya ukataili na unyanyasaji na  kujikuta  baadhi yao wanashindwa kutimiza ndoto  zao na malengo yao waliyojiwekea katika siku za baadae.

“Jamani mimi mwenyewe nimeshuhudia baadhi ya maeneo kuna watu wanafanya vitendo vya ukatili na kuwanyanyasa wanawake yani hili suala kwa upande mimi kwa kweli silipendi kwa sababu baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza malengo yao ambayo yamejiwekea kwa hiyi katika hili sisi kama serikali ni lazima tulivalie njuga ii kuondokana na hali hii,”alisema Seneba

Pia katika hatua nyingine alitoa wito kwa wakinababa wote katika Mkoa wa Pwani kuachana na vitendo hivyo vya kuwanyanyasa wanawake na kuwapiga bila sababu zozote za msingi na badala yake wabadilike na kuhakikisha kwamba wanawasaidia kuwawezesha katika shughuli zao mbali mbali za ujasiriamali  kwa lengo la kuweza kupambana na  wimbi la umasikini.

KITUO hicho ambacho kinajegwa katika kata ya Mwendapole kinatarajiwa mpaka kukamilika kwake kugharimu kiasi cha shilingi milioni 45  na katika awamu ya kwanza  kinatarajia kuwanufaisha wanawake  wapatao 200 kutoka Wilayani Kibaha mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine ya jirani ambao watapatiwa mafunzo  mbali mbali ya ujasiriamali.

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia  Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo kata ya Mwendapole na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet Mwasuka wa  kushoto ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasicahna na wanawake wajasiriamali  waliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Happiness Seneda kulia akiwa amemshika mmoja wa watoto huku akisikiliza maelekezo kuhusina na ujezni wa kiutuo hicho maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichan na wakinamama kinachijengwa katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok Janet Mwasuka.
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Nameloc akoinyesha eneo ambalo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichana na wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwendapole  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani

KISHAPU WILAYA YENYE FURSA LUKUKI ZA UWEKEZAJI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza katika moja ya vikao. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga na Mwanasheria wa wilaya, Wilson Nyamunda.
Mmoja wa mafundi wa bidhaa za ngozi katika kiwanda kidogo cha Badimi akiwajibika. 
Sehemu ya mifugo ambayo ni muhimu kwa uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za ngozi wilayani Kishapu.

Serikali ya Awamu ya Tano iko katika mkakati wake kabambe wa kuhakikisha kuwa Sera ya Tanzania yenye viwanda inafanikiwa, lengo kubwa likiwa ni kukuza na kuinua uchumi wa nchi.

Yote hayo yanafanyika kwa kufufua viwanda mbalimbali ambavyo vilikuwa vimekufa na kusitisha uzalishaji wake kutokana na sababu mbalimbali hatua inayokwenda sanjari na kujenga vipya.

Tunashuhudia juhudi kubwa za Serikali zikizaa matunda katika maeneo kadhaa ya taifa letu ambayo tayari wawekezaji wameanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali. 

Katika kudhihirisha hilo, pia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inayoongozwa na Waziri Charles Mwijage imejikita katika kuwezesha wajasiriamali ili wainuke na kutambulika katika soko la kitaifa na kimataifa.

Hilo linafanyika kupitia maonesho mbalimbali ya viwanda na biashara ambayo hufanyika kila mwaka lengo ni kuwapa fursa wajasiriamali hao kuonesha bidhaa zao haijalishi kama ni kubwa au ndogondogo. Katika hilo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliyopo katika Mkoa wa Shinyanga magharibi mwa Tanzania haiko nyuma kwani tayari imeanza utekelezaji wa sera hiyo muhimu kwa ustawi wa nchi.

Wilaya hiyo kupitia kikundi cha Badimi inajivunia kuwa na kiwanda kidogo cha kusindika na kutengeneza bidhaa za ngozi za wanyama zikiwemo viatu, mikoba na mikanda.Tayari wakazi wa Kishapu wameanza kuona matunda ya kiwanda hicho kidogo ambacho kinatarajiwa kuwa nia mojawapo ya kujipatia maendeleo siyo tu ya kikundi bali pia kwa taifa.

 “Dhamira yetu ni kutengeneza ajira kwa wanakikundi, kuwezesha fursa za kiuchumi miongoni mwa wanakikundi na wananchi kwa ujumla waliomo ndani na nje ya Wilaya ya Kishapu,” ndivyo anavyobainisha Said Luhende ambaye ni katibu wa kikundi hicho.

Akifafanua zaidi anasema neno Badimi likiwa linamaanisha kundi la wafugaji ambao ni walinzi na wachungaji mifugo iliundwa Novemba 11, 2009 ikiwa na wanachama waanzilishi 10.

Kikundi hicho ambacho kina jumla ya wanachama 53 ambapo 27 kati yao ni wanaume na 26 ni wanawake, walianza kuuziana hisa, kusindika ngozi na kuogesha mifugo shughuli walizoendelea nazo hadi kufikia hatua ya kutengeneza bidhaa za ngozi.  

Katibu huyo wa kikundi hicho anaendelea kudokeza kuwa malengo hasa ya mradi au kiwanda hicho kidogo ni kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi ghafi ndani na nje ya wilaya hiyo.

Idara ya Mifugo na Uvuvi ambayo inaongozwa na Mkuu wake, Dk. Alphonce Bagambabyaki akishirikiana na wataalamu wake walioenea kata mbalimbali ndiyo wenye dhamana ya masuala yote ya bidhaa za ngozi za mifugo mbalimbali.

Wilaya ya Kishapu ina idadi kubwa ya mifugo kwa ujumla na ni kweli kuwa zao la ngozi litokanalo na mifugo halithaminiwi kwa kiwango kinacholingana na thamani yake.

Kupitia idara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu inahakikisha inalifanya zao hilo la bidhaa za ngozi liwe linatambulika na kuwa na thamani kubwa kwa mfugaji wa mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Kwa mujibu wa takwimu kwa wastani jumla ya ngozi za wanyama kama ng’ombe 350, za mbuzi 800 na kondoo 280 huweza kupatikana kwa kila mwezi ambazo zinaweza kusaidia utengenezaji wa bidhaa za kutosha. 

Baadhi ya ngozi ambazo zimekuwa zikitupwa kutokana na kukosa soko sasa zitakuwa zinaokolewa na wakati huo mfugaji kwa uapnde wake atakuwa anapata faida kubwa kwa kujipatia kipato kutokana na mauzo ya ngozi ghafi.

Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba kwa upande wake anatoa pongezi za dhati kwa kikundi hicho cha wajasiriamali cha Badimi na kusema kuwa Kishapu ya viwanda inawezekana.

“Mara zote mwanzo huwa ni mgumu na mara nyingi huwa tunapenda kushiriki pale ambapo tunaona matunda ya jitihada fulani yanatokea lakini hatupendi kuonesha ushirikiano tangu mwanzo, hivyo sasa tufike mahali tutiane moyo,” anasisitiza.

Anawakaribisha Watanzania wanohitaji kujenga viwanda wafike wilayani humo ili kuwekeza viwanda hatua itakayosaidia kuzidi kujenga uchumi imara na kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa ajira.Taraba anaendelea kusema kuwa yapo maeneo yaliyopimwa yakiwemo Mwigumbi kwenye kata ya Bubiki ambayo yamekaa kibiashara na kimkakati hivyo kuwa kichocheo kikubwa cha biashara.

Kwanini Mwigumbi?
Hili ni eneo ambalo kimsingi ni njia panda ya karibu zaidi ya kwenda nchi jirani ya Kenya kwa barabara ambayo huweza kurahisisha usafiri wa magari makubwa kama malori kusafirisha bidhaa.

Si hivyo tu bali pia ni njia panda ya kwenda mikoa jirani kama Simiyu, Mara, Manyara na Arusha hivyo kuwa kitovu kizuri cha biashara hali inayoweza kufanya mzunguko mkubwa wa fedha wilayani Kishapu.
Hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli alizindua mradi wa ujenzi wa barabara kuu ambayo itaunganisha Mkoa wa Shinyanga na Simiyu hatua itakayorahisha na kupunguza usafirishaji kwenda Kenya.  

Itakumbukwa pia Mwigumbi ni eneo ambalo linatarajiwa kupitiwa na reli ya kasi ya ‘standard garge’ hivyo mkuu huyo wa wilaya anawakaribisha wawekezaji kujenga bandari kavu kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya maeneo ya jirani. 

Maeneo mengine ya uwekezaji 
Mbali ya Mwigumbi, Taraba anabainisha wilaya hiyo imejaliwa maeneo mengine ya uwekezaji kama mji mdogo wa Kishapu na mengine yakiwemo Nyasamba kwenye kata ya Bubiki, Mipa kata ya Mondo, Uchunga, Ukenyenge, Bunambiyu pamoja na Igaga.  

Pamba ndilo zao kuu la biashara linalotambulika katika wilaya hiyo lakini ukweli ni kuwa yapo mazao mengine yanayofanya vizuri na kuwainua wakulima yakiwemo mkonge, alizeti na dengu.

Anaagiza kila kata kubainisha fusra zisizopungua tatu ambazo wanaona kutokana na mazingira yanayowazunguka na kutoa rasilimali watu zinaweza kuchangia uanzishwaji wa viwanda.

Anasema lengo ni kuzitambua fursa hizo na hivyo kuanza michakato mapema ya kujenga viwanda wenyewe bila kutegemea wawekezaji kutoka nje kufika Kishapu na kuvijenga. 

Mkuu wa wilaya anawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika mazao hayo kwa kujenga viwanda kwa ajili ya kukamua alizeti kupata mafuta ya kupikia, kusindika mkonge na kutengeneza bidhaa mbalimbali pamoja na sabuni.

Anasema pamoja na hayo ni dhahiri kuwa viwanda havitajengwa na watu wa nje bali vitajengwa na wananchi wazawa kwa kutumia malighafi zinazopatikana ndani katika maeneo wanayoishi.

Kwa kutumia wananchi waliomo ndani wenye ujuzi tofauti tofauti au waliosomea katika vyuo mbalimbali na kupata mafunzo au wenye kuwa na ubunifu ambao unaweza kuleta mapinduzi ya viwanda.

Hivyo Kishapu ya viwanda inawezekana jambo muhimu ni wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuendelea kujenga uchumi imara kama ilivyo kaulimbiu ya halmashauri ya wilaya hiyo.

Kumbu kumbu ya Misa ya Marehemu Mwl. Dionis Ndege

$
0
0
Umetimiza miaka 10 na siku 14 toka mwenyezi mungu alipokuchukua katika hospitali ya regency dsm tarehe 05/04/2007 siku ya alhamisi kuu. 
 
Unakumbukwa sana na mkeo mama Helena D. Ndege, wanao: Esaka D. N. Mugasa, James, Lawi, Anna, Mary, Lucy, Catherine, Tabu, Vicent, Joseph, Mwavisu, wanao wengine wote, Wajukuu, Vitukuu, ndugu, Jamaa, marafiki, wanafunzi wako, waalimu wenzio na majirani. 
 
Unakumbukwa pia kwa mchango wako mkubwa wa elimu hapa nchini toka ulipofungua shule ya msingi sirari mwaka 1954 ukiwa mwl. mkuu, na baadaye kufundisha katika shule za utegi, abainano, marasibora na wanyere. sisi tulikupenda sana lakini mungu alikupenda zaidi.
 
Jina la Bwana lihimidiwe. Amen.
 
Misa ya kumwombea marehemu imefanyika leo tarehe 18/04/2017 saa 4.00 asubuhi nyumbani kwake shinyanga mjini - mtaa wa lubaga.

uzinduzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa Afya kujadili hali ya upasuaji nchini

$
0
0

Mkurugenzi wa Global Health kutokea Taasis ya GE, Asha Varghese akizungumzia ushiriki wa Taasis hiyo katika kongamano hilo
Mganga Mkuu wa Serikali Professa Muhammed Bakari akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa Afya kujadili hali ya upasuaji nchini (medical operation)
Washiriki wa kongamano hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mganga Mkuu wa Serikali Professa Muhammed Bakari akijadiliana jambo na washiriki wa mkutano huo.
Mganga Mkuu wa Serikali Professa Muhammed Bakari akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na changamoto zitokanazo na uhaba wa wataalamu wa upasuaji nchini na mengineo kuhusiana na kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wanaoshiriki kongamano hilo wakifuatilia kwa umakini mjadala uliokuwa unaendelea.


 

The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and Safe Surgery 2020 officially launch the National Surgical, Obstetrics and Anaesthesia Plan Process.

The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MoHCDGEC) in collaboration with Safe Surgery 2020 officially launched the National Surgical, Obstetrics and Anaesthesia Plan (NSOAP) drafting process by convening Working Groups in Dar Es Salaam.

The Planning process was officially launched by the Permanent Secretary, Ministry of Health Tanzania, Dr. Mpoki Ulisubisya, and Ms Asha Verghese- Director, Developing Health Globally at the General Electric Foundation (GE Foundation) and Deputy Permanent Secretary for health at the President’s Office Regional and Local Government (PORALG), Dr. Zainab Chaula the Director of Health and Nutrition services at PORALG, Dr. Ntuli Kapologwe as well as Regional and District Medical Officers.

The need for a National Surgical, Obstetric and Anaesthesia Plan has been informed by various studies highlighting the urgent need to prioritize safe surgery in Tanzania. A study carried out using the WHO Tool for Situational Analysis to Assess Emergency and Essential Surgical Care in 2012 found that the average travel distance for patients receiving surgical care is 119 km in Tanzania.1 The Lancet Commission on global surgery recommends that by the year 2030, 80% of the population should have access to emergency surgical care within 2hrs. However, the current proportion of Tanzania’s population that cannot access surgery within two hours is unknown.

The Lancet Commission on Global Surgery estimates that at least 20-40 surgical specialists are needed per 100,000 population. Tanzania’s density of specialist surgical workforce is 0.31 physician surgeons, obstetricians and anesthesiologists per 100,000 population. Although the rural population accounts for over 70% of the population in Tanzania, many hospitals across the country have no permanent surgical or medical specialist, anesthesiologist, and/or healthcare workers with formal specialty training in emergency or critical care. 


Furthermore, the high expenses involved are known to delay seeking care and are often a major factor in the decision not to seek care at all. Lack of affordable, quality healthcare traps families into poverty where a third of households have to borrow money or sell assets to pay for health care.

Therefore, to address these challenges, the National Surgical, Obstetric and Anaesthesia Plan will bring together clinicians, practitioners, implementers, and policymakers to work on solutions to the current state of the surgical system in Tanzania, identify what developments are necessary for a functional surgical system as well as identify which of these should be prioritized for the next seven years. The plan aims to improve access to quality, timely and affordable services as well as coordinate the existing efforts to avoid overlap.

Five teams will be formed to discuss terms of reference around workforce, service delivery, infrastructure, information management and financing and governance. It is anticipated that this plan will be completed and launched for implementation by the end of 2017.


This collaboration between the Ministry of Health and Safe Surgery 2020 demonstrates both the public and private sectors’ continuing roles in bringing safe, accessible and affordable surgery to the citizens of Tanzania.

CGI Atembelea Ofisi Ya Mufti Wa Tanzania

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. AP. Makakala akieleza jambo kwa Mufti Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, alipomtembelea Mufti Ofisini kwake Kinondoni leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. A.P. Makakala akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, leo asubuhi Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Katikati ni Mshauri wa Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Khalid.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. A.P. Makakalla akiwa katika picha ya pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, pamoja na baadhi ya Masheikh na Maafisa wa Ofisi ya Mufti leo asubuhi Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam
Viewing all 46369 articles
Browse latest View live




Latest Images