Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1198 | 1199 | (Page 1200) | 1201 | 1202 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Afisa wa Uhasibu Mwandamizi wa NSSF Tabora Bw. Mussa Ndelemiko, akitoa utambulisho na dhumuni la ziara ya viongozi wa NSSF katika Kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora.
  Afisa Mtendaji Kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora Bi. Rehema  Midelo (kulia), akitoa utambulisho wa viongozi wa Kata.
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora.
  Diwani ya Kata ya Mtendeni Mh. Yahya Mhamali akizungumza katika hafla hiyo. 
   Baadhi ya viongozi wa Kata ya Mtendeni.
   Mifuko ya Saruji ikishushwa tayari kwa ajili ya makabidhiano.
   Saruji ikishushwa.
   Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo.
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz (kulia), akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Mtendeni wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mh. Yahaya Mhamali katika hafla iliyofanyika mkoani Tabaro.
  Diwani wa Kata ya Mtendeni Mh. Yahya Mhamali akitoa neno la shukrani NSSF.
  Mkazi wa Mtendeni Bw. Idd Mkwama, akitoa shukrani kwa msaada uliotolewa na NSSF na kutoa rai kwa taasisi zingine kuiga mfano wa NSSF katika kuboresha ustawi wa jamii.
  Diwani wa Kata ya Mtendeni Mh. Yahya Mhamali akishukuru msaada uliotolewa na NSSF.
   Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz, akizungumza baada ya kukabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Mtendeni mkoani Tabora.
   Diwani ya Kata ya Mtendeni Mh. Yahya Mhamali, akitoa shukrani zake kwa uongozi wa NSSF baada ya kupokea mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mtendeni. 
  Mkazi wa Mtendeni Bw. Idd Mkwama, akitoa shukrani kwa msaada uliotolewa na NSSF na kutoa rai kwa taasisi zingine kuiga mfano wa NSSF katika kuboresha ustawi wa jamii.
  Mkazi wa Mtendeni Bi. Fatma Said Makalla, akitoa shukrani kwa msaada uliotolewa na NSSF.
   Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz, akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Mtendeni mkoani Tabora.
   Diwani wa Kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora, Mh. Yahya Mhamali akimuonyesha Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz, akiangalia eneo litakalojengwa Zahanati hiyo.
   Kukagua eneo la ujenzi wa Zahanati.
  Picha ya pamoja katika eneo la ujenzi wa Zahanati hiyo.
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Bi. Nour Aziz akiwa kwenye picha ya pamoja na Mh. Diwani wa Kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora Mh. Yahya Mhamali (mwenye koti), Afisa Mtendaji wa Kata Bi Rehema Abubakar Midelo pamoja na wafanyazi wa NSSF Tabora.

  0 0


  Na Mwandishi Wetu, Mwanza

  BOHARI ya Dawa (MSD) imeshiriki Jukwaa la Biashara, lililoandaliwa na Kampuni ya magazeti ya TSN,jijini Mwanza.

  Katika Jukwaa hilo,MSD pia imeshiriki maonesho ya vifaa tiba.


  Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo jijini Mwanza jana Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (pichani kulia) amewahakikishia wadau wa Mwanza fursa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha dawa nchini,endapo watakidhi ubora unaohitajika.

  Amesema,hatua hii inafuatia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi na taasisi za Umma katika uwekezaji.

  Bwanakunu amefafanua kuwa uanzishwaji wa viwanda nchini utapunguza gharama za uagizaji dawa na vifaa tiba toka nje ya nchi, kuokoa fedha za kununua nje,kusafirisha,kugomboa na kupata dawa kwa muda mfupi.

  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wadau wa Utalii nchini kutoa maoni na michango yenye tija itakayopelekea upatikanaji wa Sera bora itakayoleta ufanisi katika uendeshaji wa huduma zinazotolewa katika sekta ya Utalii.

  Hatua hiyo inakuja ikiwa, Sera ya Taifa ya Utalii iliyopo ilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka 17 iliyopita.

  Katika kutambua hilo, Wizara imeanza kupitia upya Sera hiyo ili kuhakikisha Sekta ya Utalii inakwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani yakiwamo ya teknolojia, kijamii, kiuchumi, kisiasa na mazingira

  Akizungumza katika mkutano unaofanyika kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha kwa mikoa ya kanda ya Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki alisema Sera inafanyiwa marekebisho kwa kuwa imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika sekta hiyo.

  Aidha, alisema kwa kutambua mchango wa utalii kiuchumi , ni wazi kuwa sera wezeshi ya utalii yenye kutoa mwongozo wa utaratibu bora na sahihi wa usimamizi, uendelezaji na utendaji katika sekta hiyo unahitajika.

  ’’ Tunataka kuibadilisha sera hiyo ili iweze kujibu changamoto za aina ya utalii wa sasa ambao kipindi cha nyuma haukuwepo, akitolea mfano utalii mikutano pamoja na utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukikua kwa kasi hapa nchini.

  Kutokana na hali hiyo, Dkt. Nzuki amesema marekebisho ya Sera hiyo yanahitaji mchango mkubwa kutoka kwa wadau kwa kuwa inaendeshwa kwa kiasi kikubwa na Sekta Binafsi katika kutoa huduma na kufanya biashara za utalii hapa nchini.

  Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga alisema uhuishwaji wa Sera hiyo utazingatia namna ambavyo wazawa wataweza kuwa wanufaika namba moja kwa kuwaandalia mazingira rafiki ya kuendesha biashara ya utalii tofauti na sasa ambapo makampuni mengi ya utalii ni ya watu kutoka nje.

  Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Lugimbana alisema sera iliyopo sio mbaya ila tatizo lililopo Serikali imeshindwa kuitekeleza licha ya kuwa kuna baadhi ya vitu muhimu ambavyo havimo kwenye sera hiyo ikiwemo changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.

  Aliongeza kuwa mara baada ya kuhuisha sera hiyo itaweza kusaidia kuonesha jinsi gani wadau wa utalii wanayokumbana na changamoto mbalimbali katika kuwahudumia watalii.

  Kwa upandwe wa Mwenyekiti wa TATO, Wilbert Chambulo alisema suala la kuifanyia marekebisho ya sera hiyo ni jambo jema ila sasa serikali iangalie namna ya kuboresha mashirikiano katika utoaji wa maamuzi kwa wafanyabiashara wa utalii nchini badala ya kuamua yenyewe pekee yake

  Mkutano huo wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau umeanza kufanyika mkoani Arusha kwa kuwashirikisha wadau kutoka mikoa minne ya Kanda ya Kaskazini na badaaye utafanyika katika kanda zingine kwa muda wa siku mbili mbili kwa ushirikiano kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirikisho la Vyama Vya Utalii Tanzania (TCT) pamoja na Benki ya Dunia chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


   
  Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa TPSF Dkt. Reginald Mengi pamoja na makamu mwenyekiti TPSF Mr. Salum Shamte.
  A 2
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, (mwenye suti nyeusi), kushoto ni Mhe. Dkt), Philip Mpango Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Reginald Mengi Mwenyekiti TPSF, pamoja na Ndugu Salum Shamte Makamu mwenyekiti TPSF
  A 1
  Baadhi ya washiriki wa Kikao cha majadiliano baina ya serikali na sekta binafsi.

  0 0  0 0

   Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

   
  Na Daudi Manongi-MAELEZO DODOMA.

  Serikali imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku  kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.

  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.

  “Serikali ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani wapo wataalamu wanaoendeleza utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole Nasha.

  Aidha amesisitiza kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.

  Amezitaja pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.

  Ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia masuala hayo.

  “Tuna timu tayari iko mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao,hivyo pamoja na WETCU kuvunjwa kazi za chama hicho zinaendelea kama kawaida”Alisema Mhe.Ole Nasha.

  0 0


  Meneja uhusiano na matukio wa kituo cha redio cha Efm Neema Mukurasi (kulia) akizungumza na washindi wa pikipiki Rehema Nassoro (katikati) na Alphonse Daudi wakati wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ inayoendeshwa na kituo hicho na kudhaminiwa na kampuni ya Zantel iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washindi hao kila mmoja alikabidhiwa pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.
  Rehema Nassoro akisaini fomu ya baada ya kuibuka mshindi wa pikipiki kwa upande wa wanawake wakati wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ inayoendeshwa na kituo cha redio cha Efm na udhaminiwa na kampuni ya Zantel iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Katika mwendelezo wa kampeni hiyo, washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.
  Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel Said Mkumba (kulia) akimwonyesha kadi ya njano mmoja ya washiriki katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni baada ya kuibuka washindi. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.
  Washiriki wa shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel wakichuana katika mwendelezo wa kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Tsh1.9 milioni baada ya kuibuka na ushindi. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.   Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel, Said Mkumba (kushoto) akiwakagua washiriki waliokuwa wakichuana katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni baada ya kuibuka washindi. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.
  Alphonse Daudi, mkazi wa Gongo la Mboto akifurahi baada ya kukabidhiwa pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 millioni aliyoshindi kwa upande wa wanaume wakati wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ inayoendeshwa na kituo cha redio cha Efm na udhaminiwa na kampuni ya Zantel iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni meneja uhusiano na matukio kutoka Efm Neema Mukurasi. Katika mwendelezo wa kampeni hiyo, washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.
  Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel, Said Mkumba (kulia), akimwonyesha kadi ya nyekundu mmoja ya washiriki katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni baada ya kuibuka washindi. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo na kuingia katika hatua ya fainali ambapo watachuana na washiriki wengine kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam.

  0 0  Kutoka STESHENI YA PUGU - Dar es Salaam ambako leo tarehe 12 Aprili 2017 kuanzia saa Nne asubuhi, Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge railway) wa awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.

  Fuatilia moja kwa moja kupitia tovuti rasmi ya Rais, Bofya Link hapa chini. 


  0 0

  Na Nuru Juma na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Shirika la usafiri wa Anga Tanzania (ATCL) limetoa fursa kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kuzungumza na mashirika ya ndege ya nchi wanazoishi ili kuunganisha watanzania kufanya kazi na nchi hizo.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi alipokuwa akizungumza na wajasiriamali na wananchi katika mdahalo wa Diaspora uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

  Mhandisi Matindi alisema kuwa Diaspora wanatakiwa kuanza kutumia fursa zinazopatikana katika usafiri wa anga ili kusaidia watanzania kufaidika na shirika hilo kwani ni sekta inayotoa ajira kwa Watanzania wengi.

  “Shirika la ndege linahitaji wauza tiketi, wauza chakula, wasafirishaji na wapokeaji wa mizigo pamoja na wauzaji wa spea za ndege, hivyo Watanzania walioko nchini pamoja na DIASPORA wanatakiwa kushirikiana ili kupata watu wenye taaluma mbalimbali watakaofanya kazi na shirika hilo,” alisema Matindi.

  Mhandisi Matindi ameongeza kuwa ATCL ipo tayari kushirikiana na Diaspora katika kujenga uchumi wa nchi kwa kuangalia fursa ambazo wengi hawafahamu kama zipo nchini Tanzania.

  Aidha, Mtendaji Mkuu huyo aliwataka Watanzania wanaomaliza masomo ya masuala ya ndege nje ya nchi kurudi nyumbani ili waweze kuajiriwa na shirika hilo kwa ajili ya kuongeza wataalamu nchini na kukuza uchumi wa Nchi.

  Vile vile amewataka watanzania kuelewa kuwa ununuzi wa ndege ni kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi na si ufujaji wa fedha kama Watanzania wengi wanavyodhani pia ametoa rai kwa Watanzania kutumia usafiri wa shirika hilo kwani unatoa huduma sawa na mashirika mengine tena kwa gharama zinazokidhi mahitaji ya Mtanzania.

  Mnamo mwaka 2016, Serikali ilianza kuwekeza katika kufufua Shirika la Usafiri wa Anga Tanzania kwa kuanza kununua ndege mbili mpya. Aidha Serikali ina mpango wa kuongeza ndege mbili za saizi ya kati zenye uwezo wa kubeba abiria 132 na moja kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 264 ifikapo mwaka 2018.

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika  kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam. A
  Kaimu Mkurugenzi Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akielezea kuhusu mapato na matumizi ya Taasisi hiyo katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam. A 1
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi cha TUGHE tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Tamba  akiongelea kuhusu maslahi ya wafanyakazi katika kikao cha  wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam. A 2
  Kulindwa Kasubi akichangia mada kwenye kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam.
   A 3
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya  Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo  Waane akiongelea umuhimu  wa watumishi wa umma kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu za kazi katika kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam.
   A 4
  Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akichangia mada kwenye kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam.
   A 5
  Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard  Karau akichangia mada kwenye kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam.
   A 6
  Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi uliopo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Anna Nkinda – JKCI

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema inaendelea na mchakato wa ndani wa kufanyia marekebisho ya kuhuisha na kuimarisha maeneo yaliyo mazuri ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuwasilishwa Bungeni ili kuendana na wakati.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma. “Serikali inaendelea na mchakato huu wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hii Bungeni ili iweze kuendana na wakati kwa kuondoa upungufu uliopo kwa maslahi mapana ya nchi yetu”,Aliongeza Mhe.Kabudi.

  Amesema kuwa baada ya miaka 20 kupita tangu sharia hiyo ya ndoa itungwe,Serikali kupitia tume ya kurekebisha Sheria iliifanyia mapitio ya sheria hiyo na kubaini maeneo kadhaa yenye udhaifu na hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho.

  Amebainisha kuwa Kutokana na maoni hayo ya tume,mwaka 2008 Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria iliandaa waraka wa baraza la Mawaziri uliokuwa na mapendekezo ya marekebisho ya sharia ya ndoa ya mwaka 1971,hata hivyo desemba 2010 kabla waraka huo kujadiliwa na kuridhiwa na baraza la Mawaziri mchakato wa mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya muungano ukaanza na kulilazimu Baraza kusitisha kwa muda mchakato huo.

  “Serikali ilikuwa na matarajio kuwa wakati tume ya mabadiliko ya katiba inakusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba,wananchi wangetoa maoni kuhusu Sheria ya ndoa pamoja na sheria nyingine zinazofanana na hiyo na hivyo maoni yaliyotolewa wakati wa Sheria ya Ndoa yalikuwa machache sana”Alifafanua Mhe.Kabudi.

  Sheria ya ndoa mwaka 1971 ni matokeo ya mjadala mpana na shirikishi kupitia waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 1969.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na familia ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii nchini. Waziri Mkuu huyo wa 10 wa Israel aliliongoza taifa hilo mwaka 1999 - 2001.
  Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (wa pili kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe muda mfupi baada ya kuwasili na ndege ya shirika na ndege la Israel (Israel Air) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimuongoza mgeni wake, Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (kushoto kwake) kuelekea kwenye maandalizi ya ziara yake ya kitalii nchini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Wizara ya Maliasili na Utalii imesitisha utoaji wa vibali vya kusafirisha mkaa kutoka Wilaya moja hadi nyingine kuanzia terehe 01 Julai mwaka huu.

  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na kuungwa mkono na Baraza la wafanyakazi la Wizara wa Maliasili na Utalii kwa lengo kupunguza uharibifu mkubwa wa mazingira hususan ukataji wa miti hovyo.

  Baraza hilo lililofanyika mjini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2017 pia lilijadili umuhimu wa kutumia mkaa mbadala kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya ambapo mpango mahususi wa kutumia mkaa mbadala utakaozalishwa na kiwanda cha Mufindi – Iringa utawasilishwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

  Baraza la Wafanyakazi wa Maliasili na Utalii pia limepitisha kwa kauli moja kuongeza jitihada katika kukabiliana na ujangili hasa katika Pori la Akiba la Selous, Pori Tengefu la Loliondo, Rungwa na Yaeda Chini. Nguvu zaidi ya kukabiliana na changamoto ya uingizaji wa mifugo katika maeneo ya hifadhi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ujangili pia ilijadiliwa.

  Aidha, Baraza liliazimia mali za majangili pamoja na mifugo itakayokamatwa katika maeneo ya hifadhi yataifishwe kwa mujibu wa sheria.

  Katika kukabiliana na changamoto ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi, Baraza liliazimia kuwa usafirishaji wa magogo ufanyike kwa kutumia nyaraka halisi (Original Documents) badala ya vivuli vya nyaraka (Photocopy).

  Baraza hilo la Wafanyakazi pia liliazimia kuwa watumishi wote wa wizara wazingatie sheria na kanuni za utumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi pamoja na utoaji wa huduma kwa Umma.

  Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi hufanyika mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka uliopita na kutoa maoni yao kwa bajeti ya Wizara inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuweka mkakati wa kukabiliana nazo. Wajumbe wa Baraza hilo ni wawakilishi wa watumishi kutoka katika Idara, Vitengo, Taasisi na Vituo vya Wizara.

  Imetolewa na;

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Maliasili na Utalii,
  11 Aprili, 2017
  Dodoma.

  0 0

  Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
  Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akimuangalia Mkuu wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati) wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (Kushoto) akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia).
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Katikati) akizungumza na Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kulia). Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto).

  ……………..

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia azma ya serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda kwa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda nchini kwa kutoa mikopo nafuu kwa wakulima nchini.

  Azma hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

  Bibi Kurwijila amesema kwamba TADB itakeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo, mifugo, samaki na misitu ili kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini.

  “Benki imepitia upya mpango mkakati wake katika kutoa mikopo ili kuwezesha kufikia wakopaji wengi zaidi ili kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo hasa katika kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini,” alisema Bibi Kurwijila.

  Bibi Kurwijila ameongeza kuwa katika kuchagiza malengo hayo, TADB imejpanga katika Kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya upembuzi wa miradi ya Maendeleo ya Kilimo na Umwagiliaji nchi nzima ili kubaini mahitaji halisi ya fedha na pia kusaidi kupanga maeneo ya vipaumbele ili kuanza kutoa mikopo hasa kwa utaratibu mahsusi.

  Ametaja malengo mengine ya kimkakati ya TADB ni pamoja na kuboresha huduma kwa kuanzisha mazao maalum ya huduma za kibenki kwa wakulima wadogowadogo kulingana na mnyororo husika wa thamani na pia kuanza huduma za Zaidi kupitia taasisi za fedha zilizopo (wholesale lending and Refinancing) ili kufikia wakulima wengi zaidi.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa mpaka sasa Benki imefanikiwa kukopesha jumla ya shilling bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.

  Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga.

  “Kupitia mafunzo hayo TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka,” ameongeza.

  Kwa mujibu wa Bw. Assenga, TADB imeweza kuinua idadi ya wakulima watumiao mabenki na vyombo vya fedha wapatao 2,359 ambao kati yao wanawake ni 863 sawa na asilimia 36.6 ya wanufaika.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano alisema taasisi za umma zina wajibu wa kuisaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini.

  0 0

   Baadhi ya mawaziri na wabunge wakiwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhudhulia kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A
   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A 1
  Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luaga Mpina akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A 2
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A 3
  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A 4
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba  akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  A 5
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy MWalimu  akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 1
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama  akijibu hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 2
   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Ufundi Mhe. Stella Manyanya  wakifuatilia  hoja mbalimbali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 3
  Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Mbunge wa Mhe katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 4
  Mbunge wa Vitimaalum (CCM) Mhe. Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 5
  Mbunge wa Vitimaalum (CCM) Mhe. Fatma Toufiq  akiuliza swali katika katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Z 6
  Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Mhe. Joseph Mbilinyi  akiuliza swali katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  X
  Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Waitara akiuliza swali katika katika kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  X 1
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge wakifuatilia  kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  X 2
  Baadhi ya wabunge wakifuatilia kikao cha sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Leo.
  Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

  0 0

   Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ukisindikizwa na wanataaluma jana April 11, 2017 ambapo mwili unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni leo April 12, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (kulia) akiangalia mwili wa Marehemu Profesa Maselle ukishushwa toka katika gari maalumu lililokuwa limebeba mwili huo jana, wapili kulia ni Profesa Ayubu Magimba
   Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ambapo taratibu za kutowa heshima za mwisho zilifanyika jana April 11, 2017 na leo April 12, 2017 mwili huo unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
   Wanataaluma mbalimbali wakiwa wanaushusha mwili wa mpendwa wao marehemu Profesa, Samuel Maselle kwa maandalizi ya kutowa heshima za mwisho jana
   Baadhi ya viongozi katika meza Kuu akiwemo Profesa, Ephata Kaaya (wa tatu kushoto) wapilikushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Lawrence Museru na wa kwanza kushoto ni Profesa Ayub Magimba
   Baadhi ya wanafamilia na wana Taaluma wa Muhas

   Kaimu Mkuu wa Skuli ya Tiba, (MUHAS) Dokt, Erasto Mbugi akisoma wasifu wa Marehemu

    Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akisoma wasifu kwa niaba ya Hospitali ya Taifa na kutowa Rambirambi kwa niaba  ya wafanyakazi wa hospitali hiyo
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete akisoma wasifu wa Marehemu Maselle kwa niaba ya Taasisi hiyo
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akisoma wasifu kwa niaba ya Taasisi hiyo na kutowa Rambirambi kwa niaba  ya wafanyakazi wake
   Ndugu wa Marehemu akishukuru kwa wote waliyojitolea kwa hali na mali kushirikiana na familia bega kwa bega kusaidia kuokoa maisha ya ndugu yao na hata mlipo sikia ndugu yetu katutoka hamkutuacha peke yetu na mmekuwa mstari wa mbele kufanikisha shughuli nzima za maandalizi ya kumsindikiza mpendwa wetu Profesa Maselle kuelelea katika nyumba yake ya milele na mmekuwa nasi mwanzo hadi kufikia tulipo fikia. nawashukuruni sana na mungu awabariki
   Sehemu ya wanataaluma mbalimbali
   Baadhi ya wana taaluma wakifatilia kwa umakini yaliyokuwa yakiendelea Chuoni hapo   Aliyewahi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Marina Njelekela akitowa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Samuel Maselle katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas 
   Waombolezaji wakitowa heshima za mwisho
   Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (aliyeshika mwamvuli) akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitaliya Taifa Muhimbili

   Wanataaluma wakiubeba mwili wa marehemu Maselle kuuweka katika gari maalumu tayari kwa kuelekea nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach
  Mwili wa Marehemu Maselle ukiingizwa jana katika Gari

  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango akisisitiza jambo mbele ya wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano maalum wa Sekta hiyo na Serikali iliokuwa na malengo ya kuweka mazingira bora ya uhusiano na ushirikiano mwema katika kukuza uchumi wa nchi na kuiwezesha Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
  Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mdau wa Sekta Binafsi, Bw. David Mwaibula kabla ya kupokea kitabu cha utafiti wa masuala ya Sekta hiyo, katika mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza na wadau kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ambapo ameiomba Serikali iwaamini wawekezaji wazawa kwa maendeleo ya Taifa na kuongeza kuwa Taifa lolote haliwezi kujengwa na wageni.


  Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia kwa makini maelezo ya wadau wa Sekta Binafsi wakati wa mkutano maalum wa Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango akihutubia Jumuiya ya wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano maalum wa Sekta hiyo na Serikali iliokuwa na malengo ya kuweka mazingira bora ya uhusiano na ushirikiano mwema katika kukuza uchumi wa nchi na kuiwezesha Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifuatilia kwa makini mijadala namna ya kuboresha uhusiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, mkutano uliofanyika ukumbi wa Serengeti, Hazina, Mjini Dodoma.

  Kamishna wa Bajeti, Bi. Mary Maganga na Kamishna wa Sera Bw. Adolf Ndunguru, wote kutoka Wizara ya Fedha na mipango, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi katika kukuza maendeleo ya nchi, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Serikali ili kupata maoni ya Sekta Binafsi katika masuala mbalimbali.

  Wadau kutoka Sekta Binafsi, Mohamed Bajwa (kulia) na Richard Ngalewa, wakiwa katika mkutano uliotishwa na Serikali ili kujadili namna Sekta Binafsi na Serikali vinavyoweza kushirikiana kukuza maendeleo ya nchi kupitia uwekezaji.
  Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Kabwe Zuberi Zitto, akisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa kuhusu umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi nchini wakati wa mkutano kati ya Serikali na Sekta hiyo, uliofanyika Mjini Dodoma, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda akihitimisha mkutano wa Serikali na Sekta Binafsi kuhusu masuala ya uwekezaji nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-(WFM).
   
   

  Na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na Taaasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara nchini na kukuza uchumi ili kuiwezesha Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda.

  Mkutano huo uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (MB), Mh. Charles Mwijage ulifanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

  Katika mkutano huo Serikali ilipata nafasi ya kusikiliza baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili Sekta hiyo na kuahidi kuandaa namna bora ya kuzitatua kwa manufaa ya Taifa.Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Mpango alisema kuwa mkutano huo umelenga zaidi katika kuboresha mahusiano na uaminifu kati ya Sekta Binafsi nchini na Serikali.

  “Sekta Binafsi na Sekta za Umma inabidi zifanyekazi kwa pamoja kwa maendeleo ya Taifa, niwaombe wafanyabiashara mtoe taarifa za watumishi wa Umma wasio waadilifu ili kuondoa hali ya kutoaminiana”, alisema.Dkt. Mpango aliongeza kuwa Serikali inaahidi kutatua kero mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo hususani suala la utitiri wa kodi na marejesho ya kodi ili kupunguza maumivu kwa wafanyabiashara na kukuza uchumi wa nchini.

  Alisema kuwa Serikali inafarijika kufanya mazungumzo na Sekta Binafsi na inatambua ushiriki wake katika maendeleo ya nchi, hivyo itajenga utaratibu wa kufanya mazungumzo ya namna hiyo angalau kila robo mwaka.Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dkt. Reginald Mengi aliwaomba viongozi wa Serikali kuwaamini wawekezaji wazawa kwa maendeleo ya Taifa na kuongeza kuwa Taifa lolote haliwezi kujengwa na wageni.

  Alisema kuwa mkutano huo uwe mwanzo mpya wa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta hiyo kwani hivi karibuni kulikuwa na hali ya kutoaminiana kati yao kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wachache kukosa uaminifu.“Huu ni mwanzo mpya wa kuachana na zile habari za kutoaminiana, habari za kuona wadau wa Sekta Binafsi ni wakwepa kodi na wala rushwa, Serikali inabidi ianze kuizungumzia vizuri hii Sekta kwa maendeleo ya nchi”, alisisitiza.

  Aidha, Mwenyekiti huyo alizungumzia namna ambavyo Sekta hiyo imekuwa ikiridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano licha ya kuwapo na changamoto mbalimbali.Mkutano huo ulitoa nafasi kwa baadhi ya wajumbe ambao ni wadau wa Sekta binafsi na viongozi wa Serikali kutoa maoni yao ya namna ya kuboresha biashara na kukuza uchumi wa nchi.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango.
  12/04/2017.

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusadia timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens, ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchini. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkomwa na Nahodha, Sophia Mwasikili.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queen kwa lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwa na vifaa bora vitakavyowawezesha kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi

  Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na viatu vya mpira pair 20 na socks pair 40 vitawawezesha wachezaji hao kuondoka na changamoto ya vifaa vya michezo hususani viatu bora vya kuchezea mpira ambavyo ni nyenzo muhimi katika mchezo wa soka.

  Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya timu ya Kilimanjaro Queens, Mwenyekiti wa soka la wnawake Amina Karuma alisema “ Tunajisikia furaha kupokea vifaa hivi na nawapongeza sana Airtel kwa kutimiza ahadi yao yakutupatia vifaa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kukuza soka la wanawake nchini. Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea kukua kwa soka la wanawake kwa kushirikisha timu za wasichana katika michuano ya Airtel Rising Stars kila mwaka na kwa kupitia michuano hii tumeweza kupata vipaji tunavyoviona leo katika timu zetu za wanawake.

  “Tunawahakikishia vifaa hivi vitatusaidia saana kwani viatu vya mpira ni nyenzo muhimu sana lakini pia ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wachezaji wetu. Tunayo mipango mingi na michuano mbalimbali iliyopo mbele yetu na tumejipanga kufanya vizuri lakini pia kujiandaa vyema kwa michuano ya AFCON inayotegemea kuanza Februari Mwakani. “Aliongeza Karuma

  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ katika kuhakikisha tunaendeleza kukuza soka la wanawake nchini tumeona ni vyema kuwapatia wachezaji wa timu ya taifa ya Kilimanjaro Queen vifaa hivi ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia kutekeleza adhima yetu ya kukuza mpira wa wanawake nchi. Tunapenda kuwapongeza sana Kili Queen kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo michuano ya CECAFA ambapo timu hii iliibuka kuwa washindi na hivyo Airtel kuahidi kuwapatia vifaa ili kuendelea kuboresha kiwango chao cha mpira”

  Tunajisikia furaha kutimiza ahadi hii na ni matumaini yetu vifaa hivi vitatumika vyema kwenye michuano mingi ijayo katika mwaka huu pia. Aliongeza Matinde

  Kikosi cha Kilimanjaro Queens kinajengwa na wachezaji 8 walioibuliwa kutoka katika michuano yakukuza vipaji vya mpira kwa vijana ya Airtel Rising Stars yanayodhaminiwa na kuendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kila Mwaka

  0 0


   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia akiwakumbusha watumishi wa kwenye Kata (hawapo Pichani) kutekeleza yale yote yaliyoainishwa kwenye Ila ni ya Chama cha Mapinduzi katika utendaji kazi wao wa Kila siku.
  A 2
  Baadhi ya Watumishi wa Kwenye Kata za Muriet naTerrati wa kifuatilia Kikao
  A 3
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia(Kulia) akiwa na Afisa Tawala wa Jiji Ndg. Frank Sanga kwenye Kikao na Watendaji wa Kata
  A 4
  Mtendaji wa Kata ya Muriet Joachim Kisarika (Pilikushoto) akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Jiji na Ujumbe wake kuhusu Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata yaMuriet.
  A 5
  Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet umefika hatua ya mtamba wa panya, Kituo hiki kinajengwa na mdau wa maendeleo.
  …………..
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Juma Kihamia amewaagiza watendaji wa Kata kukamilisha miradi yote viporo iliyopo kwenye  Kata kabla ya kuanza kutekeleza miradi mipya iliyopitishwa katika kata husika.
  Kihamia ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Serikali katika Kata ya Muriet na Terati wakati wa ziara ya keyakutembelea Kata zote 25 zaJiji la Arusha na ambapo ziara hiyo imekamilika katika kata ya Muriet.

  Amesema kuwa lengo hasa la kutembelea Kata zote na kuonana na watumishi hao ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao na kufanya kazi kwa kuzingatia Miiko na Maadili ya Serikali huku na kuhakikisha kwamba shughuli zote za kwenye Kata zinafanyika kwa kuzingatia Sheria, kanun, taratibu na miongozo iliyopo. 

   “Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya Serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwekaribu zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji Mkuu lazima nisimamie kikamilifu“Alisema Mkurugenzi Kihamia.

  Kupitia  Kikao  hicho amewataka watendaji wote Kuhakikisha kwamba Miradi viporo iliyopo kwenye Kata na Mitaa inakamilika kabla ya mwezi Juni ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi na sikuanza kutekeleza miradi mipya nakuacha Fedha na nguvu zikipotea katika miradi ya miaka ya nyuma ambayo haikukamilika.

  Alisema kuna miradi ya mwaka 2015/2016 ambayo Fedha zimeshakutumika lakini haikukamilika sasa endapo tutaiacha tena mwaka huu miradi hiyo itaanza kuharibika na kukosa thamani kabisa hivyo tukapoteza Fedha za Serikali ambazo zilishaingizwa kwenye miradi hiyo ni vyema tukaikamilisha ndipo tuanze miradi mipya.

  Vile vile alisema kuwa watendaji wa Serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka  viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalamike wakati kuna kiongozi katika maeneo hayo ambao wanalipwa na Serikali ilikusaidia wananchi.

   ” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya kwenda kulalamikia masuala madogo  madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi” Alisema Kihamia.
  Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika Jiji la Arusha kwa kumjengea Mtumishi uwezo wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwajasili wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

  Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa Serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama Utoaji wa Mikopo kwa vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha biashara zilizopo kwenye maeneo yao ya Utawala ikiwemo idadi ya mabango na maduka yote, majengo na maeneo ya wazi pamoja na miradi viporo

  0 0


older | 1 | .... | 1198 | 1199 | (Page 1200) | 1201 | 1202 | .... | 1897 | newer