Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 10 | 11 | (Page 12) | 13 | 14 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteuwa Mussa Msheba Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usafiri wa Barabarani katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano,Zanzibar.
   
  Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi ,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu ya uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 14((2)(a) cha sheria ya Usafiri wa Barabarani(THE ROAD TRANSPORT ACT)Namba 7ya mwaka 2003.
   
  Uteuzi huo umeanza tarehe 06 Januarri,2013.
   
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI  MAELEZO ZANZIOBAR.
  13/1/2013.

  0 0


  IMG-20130114-WA000
  Marehemu Mwl. RUTH MOLLEL BIDUGA

  Familia ya Bwana Hilary J.  Biduga wa Mikocheni , Dar es Salaam , inapenda kuwakumbusha ndugu, jamaa na marafiki kufika kwenye arobaini ya Marehemu Mwl. Ruth Mollel Biduga itakayofanyika siku yaJumamosi yatarehe 19 Januari, 2013 kuanzia saa tano asubuhi nyumbani kwa marehemu Tabata , Maduka manne karibu nachuo cha Ualimu cha St. Mary.

  Vilevile ,tunapenda kuwakumbushia kuwa misa ya shukrani itafanyika Tabata, kanisa la KKKT usharika wa Tabata Matumbi siku ya Juma pili ya tarehe 20 Januari, 2013 kuanzia saa 4:00 asubuhi.

  Tunawashukuru watu wote kwa ushirikiano mwema na upendo waliotuonyesha kipindi chote cha msiba wa Mama yetu mpendwa. 

  Tunaomba Mungu awabariki sana.

  Marehemu Ruth Mollel Biduga alikuwa mama mwenye upendo, ukarimu kwa kila mtu na hii itakuwa shughuli ya wapenzi wake kumtakia safari njema na mapumziko mema. Mungu ni mwenye Heri na mwenye Huruma tele.
  - Amin

  0 0
  IMG_7465.JPG

  Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA,Dkt. Wilbrod Slaa akihutubia katika Mkutano wa wazi katika jimbo la Moshi Mjini, viwanja vya Njoro leo.Dr Slaa alizungumza mambo mbalimbali huhusiana na chama chake  ikiwemo na kuwaomba wakazi wa mji huo kujiunga na chama hicho kukijenga zaidi.
  T.Daima 3.JPG  

  Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA,Dkt. Wilbrod Slaa akihutubia katika Mkutano wa wazi katika jimbo la Moshi Mjini, viwanja vya Njoro leo.Dr Slaa alizungumza mambo mbalimbali huhusiana na chama chake  ikiwemo na kuwaomba wakazi wa mji huo kujiunga na chama hicho kukijenga zaidi
  Umati wa wakazi wa Moshi, wakiwa katika Mkutano huo leo (1).JPG   
  Baadhi ya wakazi wa  Njoro leo.wakimsikiliza Dr Slaa alipokuwa akihutubia leo kuhusiana na mambo mbalimbali huhusiana na chama chake  ikiwemo na kuwaomba wakazi wa mji huo kujiunga na chama hicho kukijenga zaidi.

  0 0

  Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri Henry Matata akihutubia wananchi katika uwanja wa wazi wa Kitangiri jijini Mwanza  uliokuwa na lengo la kuwasilisha shughuli za utendaji wa kata yake sambamba na kufafanua mikakati iliyopo juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo kwenye kata hiyo.

  Meya wa Ilemela henry Matata ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri jijini Mwanza ameapa kupambana kufa na kupona kutatua suala sugu la migogoro ya ardhi ambalo limeendelea kuwa kero ndani ya wilaya yake akiwaasa pia wananchi wa wilaya ya Ilemela kufuata utaratibu wote stahili hasa linapokuja suala la ununuzi au umiliki wa ardhi.  

  Awali vijana wanaomshabikia Meya Henry Matata waliingia viwanjani hapo kwa mbwembwe wakitokea makaburini ambako walishiriki mazishi ya mmoja kati ya mwanamtaa aliyefariki dunia kwa mapenzi ya mola katani humo.   

  Suala lililovunja rekodi ndani ya mkutano huo wa hadhara ni  hatua ya Meya huyo wa Ilemela kupitia CHADEMA kuvunja mipaka ya itikadi za siasa kwa kualika viongozi na wanachama wa vyama vyote huku akiwaachia kujimwaga na sare zao na hata nyimbo zao za vyama vyao ila tu kwa masharti ya kutohusisha kauli za kubezana zinazoweza kuleta chokochoko hali inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. 

  Shabiki nambari moko....

  Wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela nao walialikwa kwenye kusanyiko hili kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa utekelezaji pindi maswali yapapo tokea.

  Kwa utulivu kivulini wananchi wa kata ya Kitangili wakisikiliza mkutano.

  Meya ameahidi kuendelea kuhamasisha wananchi wa Kata ya Kitangiri kushiriki kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa shule za sekondari hivyo kuondoa uhaba wa vyumba vya madarasa unaoziandama shule nyingi kwa sasa.

  Kabla ya kuondoka viwanjani hapo Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata alipata picha ya pamoja  na wadau mbalimbali akiwepo Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza katika zao la samaki Bw. 'Jack Fish' ambaye pia alihamasika kuhudhuria mkutano huo.


  0 0
 • 01/14/13--21:37: uhuru marathon


 • 0 0


  WADAU WA WETU WA MTANDAO WA FULLSHANGWEBLOG TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOTE AMBAO UMETOKEA BAADA YA MTANDAO WETU KUTOKUWA HEWANI KWA SIKU YA PILI SASA KUTOKANA NA MATATIZO YALIYOJITOKEZA.

   WATAALAMU WETU WANAENDELEA NA MAREKEBISHO NA WAKATI WOWOTE TUTARUDI HEWANI KUENDELEA NA MAJUKUMU YA KUPASHA HABARI TUNAWAOMBA RADHI WADAU WETU PIA AMBAO NI NMB, NBC, SERENGETI BREWERIERS, BAYPORT, TTB NA WILNA INTERNATIONAL NA WENGINE WOTE AMBAO TUMEKUWA TUKISHIRIKIANA NAO TUNAOMBA MUWE NA SUBIRA WAKATI TUNATATUA TATIZO HILO.

  0 0


  By staff Reporter

  STANDARD Chartered Bank has appointed Liz Lloyd as Chief Executive Officer for Tanzania operations replacing Jeremy Awori whose tenure ended last year.

  A statement issued by the bank in Dar es Salaam yesterday said Liz was transferred to Dar es Salaam from her previous role as Group Head of Public Affairs, based in London, and assumed her new role as of January 2013. 

   Liz Lloyd has previously held senior roles in Group Corporate Affairs and Group Regulatory Risk and, prior to joining Standard Chartered in 2008, spent over a decade working for the former British Prime Minister, Tony Blair, including as Senior Adviser on Africa and latterly as Deputy Chief of Staff.  She has worked closely over a number of years with a wide range of African governments.

   Diana Layfield, Chief Executive Officer for Africa, Standard Chartered in response to the appointment said , “In addition to exporting talent from Africa into the Group, the region is proving to be an attractive location for some of our best international staff as we increase our investment in our businesses across the continent. 

  “I am delighted to welcome Liz to our team in Africa, following her successes in her high profile role in London, shaping the global regulatory environment for international banks.  We continue to place some of our best people in Africa as we strive to make the strongest possible social and economic contribution to the countries we operate in.”  She added.

  The statement added that Tanzania remains core to the Bank’s regional and East African strategy, given the market has seen sustained, strong growth for over a decade.  The economy is a member of Standard Chartered’s ‘7% Club’ – a list of economies which have growth rates high enough to double the size of the economy in the next 10 years. 

  Richard Etemesi, CEO for Kenya and Area General Manager for East Africa added, “We look forward to Liz bringing a wealth of additional expertise to our East Africa region. “Tanzania is playing an increasingly important role in our East African strategy, given the broad-based nature of its economic growth.  Tanzania’s discovery of 15trillion cubic feet of gas reserves off its shores is also expected to drive developments in the near-term.”

  Liz Lloyd upon taking up the new role as the Chief Executive Officer for the Bank in Tanzania, , “Tanzania holds so many opportunities and I’m excited to be leading Standard Chartered Bank Tanzania in a year of growth. 
  “Standard Chartered has important expansion and investment plans in 2013 and will play its part in the growth and development of Tanzania.” She added.
  - Ends -

  0 0

    ATC kioo chenye crake
   Ndege ya ATCL ikiwa imetua uwanja wa Kigoma baada ya kioo chake kupata nyufa na kulazimika kutua,hii ni tofauti na taarifa zilioneshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ndege hiyo iliharibika vibaya sehemu yake ya mbele pamoja na mabawa yake.

  ====  ======= ====== =======


   Taarifa ya kupata nyufa kwa kioo cha ndege ya ATCL  

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na ujumbe wa wachezaji na waandishi wa habari kutoka timu ya seattle Sounders ya Canada wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB kwenye hoteli ya serena jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya ugeni huo, Bodi ya Utalii ilisaini mkataba wa kutangaza utalii wa Tanzania katika kiwanja cha timu hiyo katika ziara iliyofanywa na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki nchini humo katika msafara huo unaoongozwa na mchezaji wa mpira wa American Football Kevin Griffin ambaye pia ni Fan Development Marketing wa Sunders FC, wachezaji hao walitembelea mbuga za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mbuga ya Tarangire ambapo walipata muda wa kujionea vivutio vilivyomo katika hifadhi hizo na kupiga picha.
  Balozi Khamis Kagasheki akimsikiliza mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi ambaye ndiye mwenyeji wa wageni hao wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam jana, kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu.
  Ugeni huo ukipata chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jana usiku kutoka kulia ni Kevin Griffin mchezaji wa mpira wa American Footballn Kasey Keller mchezaji maarufu wa mpira wa miguu vilabu mbalimbali Ulaya na Marekani na mchezaji wa timu ya Taifa ya MarekaniKristen Addings kutoka Taasisi ya Washington Global Hearthna David Glass Mtaalam Video na Majarida
  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo kushoto ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dr. Aloyce Nzuki akizungumza na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo wakati wa hafla hiyo, katikati ni Mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi.
  Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Mh. Waziri Balozi Khamis Kagasheki na wageni kutoka Seatlle Sounders kwa ajili ya kujitambulisha na kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na bodi hiyo.

  Kevin Griffin ambaye ndiyo kiongozi wa msafara huo akimshukuru Mh Waziri na Uongozi wa Bodi ya Utalii TTB kwa ushirikiano waliouanzisha katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini Canada.

  Kasey Keller akizungumza katika hafla hiyo.
  Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya Saa Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

  Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya saa Ibrahim Musa Mkurugenzi wa Utalii katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Mh. Waziri Balozi Khamis Kagashiki akiongozana na Mchezaji wa Seatlle Sounders Marc Burch kuelekea katika meza ya chakula.

  Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na waandishi wa habari kutoka Seatlle Sounders nchini Canada pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndugu Agrey Mwanri akitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa katika majumuisho ya ziara yake iliyodumu kwa muda wa siku saba Mkoani Rukwa ambapo alitembelea miradi zaidi ya 22 ambayo baadhi yake aliiwekea mawe ya msingi. 

  Katika hotuba yake hiyo alitoa maagizo mbalimbali ambayo yote yalikuwa yakilenga kwenye utawala bora, matumizi bora ya fedha za Serikali katika miradi pamoja utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Katika hotuba yake iliyodumu kwa zaidi ya saa tatu alizionya halmashauri zote nchini zitakazopata hati chafu kuwa hazitapata fedha ya ruzuku ya miradi ya maendeleo (LGCDG-Local Government Capital Development Grant) ikiwa ni kutoa funzo kwa watendaji wa halmashauri pamoja na kupandisha hasira za madiwani ili waweze kuisimamia vizuru halmashauri husika. 
  Mama Grace Mwanri, mke wa Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akitoa ushuhuda kuhusu utendaji wa mumewe "Anavyoongea na kutenda mume wangu ndivyo alivyo hata nyumbani na si kwamba anafanya hivyo kupata sifa wala umaarufu kwani mara zote huwa hapendi mambo ya kipuuzipuuzi" alisema mama Mwanri.
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza kuwatambulisha wageni na washiriki katika kikao hicho cha majumuisho kwa mgeni rasmi Ndugu Agrey Mwanri kushoto. Katika hotuba yake fupi alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa maagizo yote aliyoyatoa kwenye ziara yake yatafanyiwa kazi na kwamba miradi iliyokuwa na mapungufu itarekebishwa.
  Naibu Waziri Mwanri akizungumza na washiriki wa kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini, Chama na Serikali. Taasisi za Umma, mashirika binafsi, wajasiriamali, na watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za Umma.
  Sehemu ya washiriki wa kikao hicho katika ukumbi wa RDC katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifuatilia hotuba ya majumuisho ya Ndugu Mwanri.


  Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Festo Chonya wakifuatilia kikao hicho.
  Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho wakifuatilia kwa makini, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Godfrey Shona, Kaimu Mkurugenzi manispaa ya Sumbawanga, Mbunge Mst. na muwekezaji wa ndani Ndugu Chrissant Majiyatanga Mzindakaya na kwa kwanza kulia ni muwekezaji wa ndani Ndugu Reina Lukara.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima aweze kuyafanyia kazi katika Mkoa wake.

  Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a aweze kuyafanyia kazi katika Wilaya yake.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Idd Kimanta aweze kuyafanyia kazi katika Wilaya yake.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Mathew Sedoyeka aweze kuyafanyia kazi katika Wilaya yake.
  (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa-  Rukwareview.blogspot.com)

  0 0


  Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto Bi. Zainab Omar Mohammed. 
  VIJANA WAASWA KUTOTUMIWA KUVURUGA AMANI NCHINI.
  Vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa mstari wa mbele kulinda amani, utulivu na mafanikio makubwa yaliyoachwa  na waasisi wa taifa la Tanzania  na kuepuka kutumiwa na watu au kundi lolote  kuvunja sheria za nchi na kuvuruga amani iliyopo.
  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto Bi. Zainab Omar Mohammed wakati wa mkutano wa tathmini  ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012 unaowahusisha viongozi na na waratibu wa mbio hizo kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.
  Amesema vijana kote nchini wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii na kulinda mafanikio makubwa yaliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume  waasisi wa taifa la Tanzania.
   Amewataka vijana kukumbuka juhudi kubwa zilizofanywa na waasisi wa taifa la Tanzania katika kupigania uhuru kwa njia ya amani na Mapinduzi pale amani iliposhindikana kutokana na njama za wakoloni.
  “Nawasihi vijana wote msibabaishwe na wala msiyumbishwe na mtu au kundi lolote linaloweza kuwagawa, nawaomba muwe macho,imara na thabiti katika kulinda na kutetea mafanikio yaliyopatikana” Amesema.
  Bi. Zainab amesema juhudi za wazi zilizofanywa na waasisi  zimezaa umoja wa Tanzania ambao hivi karibuni utatimiza miaka 49 ifikapo tarehe 26,       Aprili 2013 na kubainisha kuwa umoja huo umekua mfano wa kuigwa na kielezo cha amani kwa Afrika na dunia.
  Kuhusu umoja wa watanzania uliopo amesema kuwa umeondoa ubaguzi wa rangi ,kuleta maelewano mazuri baina ya nchi majirani,kukukza lugha ya Kiswahili  jambo ambalo limekuwa chachu kubwa ya amani na upendo miongoni mwa watanzania.


  Aidha kuhusu kufanyika kwa mkutano huo wa tathmni ya mbio za Mwenge kwa mwaka 2012 nchini Bi. Zainab Mohamed amesema kuwa tathmini hiyo inatoa fursa ya kuangalia mapungufu yaliyojitokeza wakati wa mbio hizo na kutafuta namna ya kuyaondoa ili yasijirudie katika shughuli zijazo.
  Katika hatua nyingine ametoa wito kwa viongozi wa mikoa na wilaya kusimamia ipasavyo na kutoa taarifa za matumizi ya fedha zinazotolewa na wananchi kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kuondoa malalamiko na manunguniko yanayoweza kujitokeza.
  “Nawashauri viongozi wa mikoa na wilaya kuhusiana na michango inayokusanywa kutoka kwa wachangiaji mbalimbali ni vizuri kuwapa taarifa jinsi michango yao ilivyotumika kwa vitendo ili kuhakikisha kuwa waliochangishwa wanashiriki moja kwa moja  katika mipango ya kuondoa kero zao”
  Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akitoa taarifa ya wizara hiyo kuhusu mbio za mwenge kwa mwaka 2012 na ushiriki wa vijana amesema kuwa vijana ambao ni rasilimali kubwa ya taifa walishiriki kikamilifu katika kufanikisha uzinduzi wa miradi  mbalimbali ya maendeleo. 
  Amesema jumla ya vikundi 104 vya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini vilipata  fursa ya kueleza shughuli mbalimbali wanazozifanya kupitia maonesho ya wiki ya vijana mkoani Shinyanga.
  Amesema vijana walipata nafasi ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2012, umuhimu wa Vijana kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, ushiriki wa Vijana katika mabadiliko ya Katiba na ushiriki wa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na mchango wao katika kuleta  maendeleo ya nchi.
  Bw. Kajugusi ameeleza kuwa mbio  hizo kwa mwaka 2012 zilihusisha pia mapambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya, Rushwa na mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ampapo  wananchi 2363 mkoani shinyanga walijitokeza kupima afya zao wanawake wakiwa 960 na wanaume 1403.
  Amesema katika zoezi hilo watu 40 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU wanaume 17 na wanawake 23 jumla ya maambukizi ikiwa asilimia 1.75%.
  Pia ameeleza kuwa katika wiki ya vijana iliyofanyika mkoani shinyanga wananchi walihamasishwa kushiriki katika zoezi la hiari la la uchangiaji wa damu ambapo kiasi cha damu lita 342 zilipatikana.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  15/1/2013, Zanzibar.

  0 0


  This year’s Sauti za Busara Music festival, held in Stone Town, Zanzibar from 14 -17 February, is making an extra effort during the 10th edition to support free speech by featuring African artists whose music is restricted or banned in their home countries. 

  Following the coup by militant Islamists in Mali, singer Khaira Arby was forbidden from singing, in spite of her music praising the prophet Mohammad (SAW).  From Zimbabwe, militant rapper and poet Comrade Fatso criticizes the Mugabe government through his music and poetry.  Banned from state radio and television, Comrade Fatso turns to unconventional channels to spread his music.  "We have our own guerrilla tactics of getting the word out into the townships. 

  We have street teams of comrades who distribute hundreds of copies of the album into the kombis - public mini-buses used by ordinary Zimbabweans. So we create an alternative "people's radio" as the album gets played in hundreds of kombis," said Comrade Fatso. If Robert Mugabe's secret police stopped turning up at his gigs, Comrade Fatso admits that he would begin to worry. "They're always there, monitoring what we do;" reports the militant rapper-poet. "Our music is a re bellious, pro-freedom riot so if we didn't attract their attention, we'd be doing something wrong;" he says defiantly. "What we sing is truth and words are our weapon’’ he says.

  During the "Movers & Shakers" portion of Sauti za Busara, a panel of artists will discuss censorship and the importance of protecting artistic freedom and freedom of expression. Rebecca Yeong Cory, managing director of Sauti za Busara, believes that providing a space for censored artists to have a voice is vital.  "Music is one of the most powerful tools we have to speak out against injustice, to celebrate life, and to express the triumphs of the human spirit.

  Freedom of expression is a human right - and it benefits us all when it is observed and respected.  That is why Sauti za Busara, which means 'sounds of wisdom' in Kiswahili, is proud to amplify the voices of artists like Khaira Arby and Comrade Fatso, who have been banned or censored in their home countries," said Corey.

  Khaira Arby from Mali is set to perform at the 10th edition of Sauti za Busara on the final day of the three day showcase beginning 14th to 17th at the Old fort in Zanzibar. Inspired by her cousin Ali Farka Toure, Khaira Arby turns to her mixed Berber and Songhai roots and draws on a sweet mixture of desert blues and recording sophistication, blending ripping electric guitar with ngoni (forefather of banjo), funky drum breaks and traditional percussions of scraper and calabash. Though very much her own woman, Arby, born in a village not far from the famed city of Timbutku, is firmly planted in the desert sand.

  Whereas Samm Farai Monro, better known as Comrade Fatso, is one of Zimbabwe's most popular and controversial poets. He performs Toyi Toyi Poetry, radical street poetry that mixes Shona with English and mbira with hip hop. He will perform alongside Tanzania’s Mlimani Park Orchestra aka Sikinde,Atongo Zimba from Ghana, N'Faly Kouyaté from Guinea, Owiny Sigoma Band from Kenya, and fellow countrymen MokoombaFrom Tanzania the hosts of the festival will see the talented Msafiri Zawose & Sauti Band, Lumumba Theatre GroupSuper Maya Baikoko, Peter Msechu and many more.

  Entrance for Tanzanian’s is only 3,000TSH with a special rate for East African residents.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo Januari 15, 2013, jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya na wa Mkoa wa Arusha, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Afya wa Rwanda, Agnes Binagwaho, baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
   Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa na waratibu wa mkutano huo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0
 • 01/15/13--05:17: kaazi kweli kweli


 • 0 0

  Idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.


  Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tzambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.

  Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.

  Idadi kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

  Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

  Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

  Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

  UCHAGUZI TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
  Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).

  Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0


  Baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, Estaratus Mtemanyenza akitoa shukrani wakati wa kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mbunge huyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angella Kairuki.
   Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika (Kulia), akiwa katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Regia Mtema.
  Katibu wa Kamati ya Maandalizi na Msemaji wa Regia Foundation, Olivia Sanare akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema. habari kwa hsiani ya  http://francisdande.blogspot.com/

  DAR ES SALAAM, Tanzania
  ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, ametimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwake, ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alihudhuria maadhimisho hayo na kusema demokrasia ya kweli haigaiwi katika sahani ya dhahabu, bali kwa kuipigania.

  Makamba alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa, wanaopaswa kupigania haki hiyo ni vijana ambao wanayo nafasi kubwa katika safari ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015.

  Makamba alitoa kauli hiyo jana usiku katika hafla ya kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Regia, aliyefariki kwa ajali ya gari Januari 14, mwaka jana - hafla iliyofanyiola katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

  Akitoa mada iliyohusu vijana na namna anavyomfahamu Regia, Makamba alisema kama vijana watatumika vizuri katika demokrasia, watakuwa chachu ya maendeleo na kwamba ujana peke yake si sifa ya kuwa kiongozi.

  Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema lazima uchaguzi wa mwaka 2015 uamuliwe na vijana kama alivyokuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa Regia.

  Naibu waziri huyo aliwataka vijana kutafakari ni kwa nini walijiandikisha kwa wingi bila ya kwenda kupiga kura katika chaguzi mbili za 2005 na 2010 na kwamba uchaguzi ujao ni lazima wabadilike na kufanya uamuzi mgumu.

  Alitoa mfano kwamba, mwaka 2015, watajiandikisha vijana wapya  milioni 5 na kutimiza zaidi ya waliojiandikisha milioni 25, uchaguzi utakuwa umetendewa haki na vijana.

  Hata hivyo alisema ili kusukuma gurudumu la maendeleo si lazima vijana wakagombea uongozi katika siasa tu bali hata katika sekta na shughuli zingine.

   “Sikugombea nafasi ya uongozi katika nchi hii kwa sababu ya kutaka ukubwa, bali nilifanya hivyo ili vijana waige kutoka kwangu na kama sasa wengine walivyoiga kwa Regia,” alisema Makamba

  Akizungumzia alivyomfahamu Regia, Makamba alisema alimfahamu siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, katika midahalo iliyokuwa ikirushwa na televisheni nchini.

  “Nikiwa naangalia mdahalo wabunge waliokwenda kugombea majimboni, nilimwona Zitto, Halima na dada mwingine ambaye sikumfahamu akiwa nao, naye akizungumza namna anavyokwenda jimboni huku akitoa maelezo mazuri,” alisema Makamba

  Makamba alisema baadae alifahamiana zaidi kwa kuonana na kushirikiana naye katika mambo mbalimbali bungeni ambapo alikiri Regia alikuwa ni mtu mwenye uwezo na upeo mkubwa wa mambo.

  0 0


  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
  BAADHI ya watu wanajidanganya kuwa rais mzuri wa Watanzania atatokana na jina lake au umaarufu wake kisiasa katika Tanzania ya leo yenye changamoto.
   
  Si kweli. Wengi wenye uelewa wa mambo ya siasa na umahiri wa kupambanua mambo, wanajua kuwa mtu huyo ambaye ndio tegemeo la nchi, atatokana na ujuzi wake wa kubuni na kuchambua changamoto kwa ajili ya maendeleo ya Taifa lake.
   
  Katika kulisema hili, nashangaa kuona baadhi ya watu wakitembea Mashariki na Magharibi kunadi majina ya watu wao wanaotajwa kugombea urais mwaka 2015.
   
  Sipingi nia ya watu hao kuwania urais katika Taifa lao, ila nitashangaa kama wanasiasa hao watapitishwa kwa umaarufu wa majina yao.
   
  Tukifanya hivyo tutaumia. Ikulu ni mahali patakatifu na kamwe hapatastahili kwenda kwa sababu tu ya umaarufu wake wa jina linalopambwa na wafuasi wake.
   
  Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kulisema hili enzi za uhai wake. Alipinga wale walioanza kuingia kwenye dhambi ya kutaja majina ya wanasiasa wao eti wanafaa kugombea urais.
   
  Sakata hili limezidi mno mara baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kushinda awamu yake ya pili, mwaka 2010, ambapo wenye malengo ya kugombea urais mwaka 2015 walianza kujipanga.
   
  Mengi yalianza kusikika au kuonekana, pale wanasiasa hao wanavyojipambanua katika kutilia mkazo hoja zao au mahitaji yao siku za usoni.  Kwa bahati mbaya, ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna hata mwanasiasa mmoja aliyetangaza nia ya kurithi mikoba ya Kikwete.
   
  Ingawa hawajatangaza hadharani, lakini  wachambuzi wa mambo ya kisiasa, wamewabaini, hasa kwa kuorodhesha kauli zao au vikao vyao vya siri. Kwa mfano, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa na nia ya kugombea urais mwaka 2015.
   
  Japo Lowassa hajasema popote lengo hilo, lakini kila analofanya kwa sasa, linaingizwa katika mlengo wake wa Uchaguzi Mkuu, ikiwamo chaguzi za ndani ambazo zilitajwa kama silaha ya kwanza ya waziri huyo aliyejiuzulu.
   
  Viongozi wengi walioshinda katika chaguzi za ndani za CCM mwaka jana, walitajwa kuwa na uhusiano mzuri na Lowassa, wakiwamo washindi kutoka Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Taifa, ambapo Sadifa Khamis Juma, alishinda nafasi ya Mwenyekiti, wakati Mboni Mhita alishinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo.
   
  Ukiacha Lowassa, bado wapo wanasiasa wengine kutoka CCM, akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, anayetajwa kuwania nafasi hiyo ya urais mwaka 2015 na wengineo.
   
  Mbali na CCM, lakini bado wapo wanasiasa kutoka vyama vingine ambavyo huko nako kuna majina makubwa na yenye kutishia katika harakati hizo za urais.
   
  Wapo watu kama vile Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willbroad Slaa, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe pamoja na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wanaotajwa kuwania urais.
   
  Vita vyao ndani ya chama watavimaliza wenyewe, kama itakavyokuwa ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), chini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Maalim Seif Sharif Hamad na wengineo kutoka NCCR-Mageuzi, TLP na vyama vingine vyenye kusimamisha wagombea wa nafasi ya urais.
   
  Kama nilivyosema hapo juu kuwa yeyote anaruhusiwa kuwania nafasi hiyo, lakini aangaliwe umahiri wake, sifa zake zinavyoweza kulikomboa Taifa letu.
   
  Mtu huyo asipewe nafasi hiyo nyeti eti kwa kuwa anapopita barabarani wapo wachache wanaolala na yeye kupita juu yao, au kutandikiwa kanga za sandukuni kama ishara ya kumlaki mwanasiasa huyo.
   
  Tanzania yenye changamoto nyingi kama vile ugumu wa maisha, magonjwa na elimu duni, haitapiga hatua kama rais wake hatakuwa makini.
   
  Tutaanguka zaidi, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuwa makini katika mchakato huo wa kupatikana mrithi wa Kikwete, ambaye hapana shaka naye anaumiza kichwa jinsi gani ya kumuachia mrithi wake.
   
  Najua wapo ambao majina na haiba zao ni kubwa, lakini suala la urais si jambo la kitoto. Hivyo tuwahoji na kuwapima kama kweli wanaweza kuvaa kiatu hicho.
   
  Na kama tunajua kuwa hawawezi basi uungwana ni kuwaambia na kuwaweka kando bila kuleta chuki na uhasama katika siasa za Tanzania zinazozalisha matatizo kwa baadhi ya wanasiasa wetu.
   
  Huu ndio ukweli. Kuusema wakati huu ambao watu wanapita na wapambe wao kusafisha njia kunataka moyo wa chuma, hasa kwa kuangalia kuwa kila mtu anataka kuweka mtandao wake kwa ajili ya kumpatia nafasi hiyo.
   
  Rais wa Tanzania ni yule atakayeinua uchumi wa Taifa lake kwa kuwasimamia vyema watendaji wake pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali za Taifa zinawanufaisha wazawa.
   
  Kwa mfano, licha ya kujengwa shule za kata kwa ajili ya kuwafanya watoto wa masikini wapate elimu ya sekondari, lakini shule hizo hazina walimu wala vifaa vya kufundishia.
   
  Ukirudi kwenye elimu ya msingi, nako kuna changamoto nyingi, wakiwapo walimu kugoma kwenda katika maeneo yao ya kazi kwa sababu ya kukwepa maisha magumu.
   
  Shule nyingi zilizokuwapo vijijini zimekumbwa na balaa hilo, hivyo tunahitaji rais mwenye mipango na ambaye atahakikisha kila mtu anafanya kazi yake kama inavyotakiwa.
   
  Naamini watu wa aina hiyo wapo, ingawa kwa bahati mbaya, wanaweza kufichwa na wale wenye nyota zao au uwezo wa kipato wa kununua watu wa kupita nyumba hadi nyumba kuwahamasisha wajumbe wawapigie kura siku ya kutafutwa nani anaweza kupitishwa kuwania urais.
   
  Ingawa Kikwete amejitahidi katika kipindi cha uongozi wake, lakini bado hatuwezi kukaa na kubweteka na badala yake tunahitaji mwingine mwenye ujasiri, mtu makini, mbunifu na mwenye kuendeleza miradi inayowanufaisha Watanzania wote.
   
  Mwenye kujua uwezo anao, basi asifikirie tu kuwa watu watamuingiza kutokana na jina lake na atayefanya hivyo, atakuwa amekosea na kuwasaliti Watanzania.
   
  Huu ndio ukweli wa mambo. Ndio maana Mgodi Unaotembea umeona ulijadili suala hilo kwa kina, maana rais bora ndiye anayeweza kuwakomboa Watanzania.
   
  Mengi yapo yanastahili kujadiliwa kwa kina, hivyo naamini kila mmoja atakaa na kujiangalia mara mbili, huku wale wanaomwaga fedha kwa ajili ya kunufaisha majina yao, nikiwashangaa kwa kitendo hicho, huku nikiamini kuwa malengo yao yana matege na wanadanganya nafsi zao.
   
  Mungu ibariki Tanzania.
   
  0712 053949
  0753 806087

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla  maalumu ya kuwakaribisha wake wa Mabalozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013, 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla  maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013, 
  Baadhi ya wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zaoTanzania wakisubiri kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya 2013 katika viwanja vya Ikulu jjijini Dar Jan 15,2013 iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani).
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akibadilishana mawazo na baadhi ya wenza wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakati wa sherehe ya hafla ya kuukaribisha mwaka 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam,jan 15,2013. 
  Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) akibadilishana mawazo na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) katika hafla maalumu ya mwaka mpya 2013 kwaajili ya wake wa Mabalozi iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(hayupo pichani) kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan,15,2013. 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akisalimiana na Mdau Fauzia Aboud katika hafla hiyo ndani ya viwanja vya Ikulu jijini Dar e Salaam Jan 15,2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Mama Sitti Mwinyi (kushoto) katika haflaya  mwaka mpya 2013 ya kuwakaribisha (SPOUSE) wake wa Mabalozi nchini  Jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akipongezana na Consulate wa  Jamhuri ya Poland Bibi  Grazyna Tairo kwenye hafla ya kuwakaribisha wenza wa Mabalozi nchini jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akipongezana na Kiongozi Wenza wa Mabalozi nchini Celine Khalfan Juma Mpango katika hafla ya kusherehekea na kukaribisha mwaka mpya 2013  kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan 15,2013. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

  0 0


older | 1 | .... | 10 | 11 | (Page 12) | 13 | 14 | .... | 1898 | newer