Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI MACHI 2017 UMEONGEZEKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 6.4

$
0
0
Ofisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Veronica Kazimoto (kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwapatia taarifa hiyo.

 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dar es Salaam leo kupata taarifa ya mfumuko huo wa bei kwa mwezi Machi.
Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongeza hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari 2017.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi wa Februari 2017.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi Machi 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi 2016.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari 2017.

Taarifa hiyo imeonesha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi 2017 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2016.

Benki ya NMB yadhamini mkutano wa mwaka wa TEF

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB –Richard Makungwa (kulia) akimpongeza mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF- Teophil Makungwa mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini kutoka benki ya NMB. NMB imetoa kiasi cha fedha hiyo kama sehemu ya ufadhili wa mkutano wa mwaka wa jukwaa la wahariri ambao umefanyika mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo

 BENKI ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika kwa siku moja ya Aprili 4, 2017 mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali nchini ambao ni wanachama wa TEF. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano huo, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema NMB inathamini mchango wa waandishi wa habari nchini na imekuwa ikishikiana nao kwa muda mrefu hivyo kudhamini mkutano huo ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano ulipo baina ya NMB na waandishi wa habari.

 “Kwa niaba ya uongozi wa Benki ya NMB, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kwa kutambua kuwa NMB ni benki iliyo karibu na jamii yote ya Watanzania na kugusa mahitaji ya kila jamii ya watanzania wa kila kada. “Waandishi wa habari kwa NMB ni wadau muhimu sana kwani mafanikio ya NMB mpaka kufikia hapa kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na vyombo vya habari. Hivyo tunafarijika na sisi kushikiriana nanyi kwenye shughuli zinazowagusa ninyi moja kwa moja,” alisema Makungwa na kuongeza. 

“Kwa NMB, huu ni mkutano muhimu sana na maazimio mtakayoyafikia, yatakuwa yenye tija huku mkiweka mbele uzalendo wan chi yetu. Mkiwa mnaendelea na mkutano huu, tambueni kuwa tunawathamini sana na kazi zenu tunazithamini sana.” Udhamini wa NMB kwa mkutano mkuu wa mwaka wa TEF una thamani ya milioni 20 na hiyo siyo mara ya kwanza kwani hata mwaka jana ilidhamini mkutano wa TEF, mkutano mkuu wa mwaka wa TBN, mkutano wa TAJATI na pia NMB kuwezesha kutolewa kwa tuzo za uandishi mahiri kwa kushirikiana na MCT.

DC KASESELA MAZOEZI LAZIMA IRINGA ILI KUJENGA UCHUMI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye mazoezi na wananchi wa kijiji cha Tosamaganga pamoja na mwanachama wa club ya Tosamaganga sports club.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akicheza Mpira wa kikapu kuashiria kuwa anapenda Mpira wa kikapu

Na Fredy Mgunda,Iringa


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwaomba wananchi kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimalisha afya zao pamoja kuujenga uchumi wa nchi hii.

Tukiendelea kufanya mazoezi tutapunguza sana kupata magonjwa mbalimbali kwa kuwa tuna kuwa tunaimalisha afya na kujenga miili yetu lakini hii itasababisa wananchi kujituma kufanya kazi kwa nguvu na morali mpya kila mwanzo mwa wiki kwa kuwa wanakuwa na nguv,stamina na akili Mpya kutokana mazoezi ya mwisho mwa Juma.

"Kwa mfano mimi saizi nipo sawa kiakili kutokana na haya mazoezi maana bila haya mazoezi nisinge kuwa vizuri kiaafya,saizi naweza kufanya kazi kwa masaa mengi kutokana na hili zoezi la Leo sasa nawaomba wananchi na viongozi mbalimbali kufanya mazoezi ili kuongeza ufanisi kazini"alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashukuru wananchi wa Tosamaganga sports club kwa kuanziasha club ya Tosamaganga ambayo inamichezo mingi kama mpira wa miguu,mpira wa pete,riadha,na mpira wa kikapu hivyo naomba wananchi wengine waanzishe vitu kama hivi ili Wilaya nzima iwe inafanya mazoezi kwa kuimalisha Afya.

Kasesela amewataka viongozi wa kata,kijiji,mtaa,na tarafa kuanzisha mazoezi huku waliko ili kupanua wigo wa eneo kubwa la watu kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao na kupunguza kunyemelewa na magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yanapunguza nguvu kazi za taifa katika kujenga uchumi wa taifa.

"Hii ni moja ya club ambayo nimeizindua ambayo itatuongezea wigo wa sehemu za kufanyia mazoezi ya kuimalisha afya zetu na kuipa moyo serikali kupanua wigo wa maeneo ya kuafanyia mazoezi" alisema Kasesela

Nao baadhi ya viongozi wa club ya Tosamaganga sports club walimushukuru mkuu wa Wilaya kwa kukuza Michezo katika Wilaya ya Iringa na kuongeza ufanisi wa kazi hasa makazini kwa kuwa ndio jadi ya kukuza uchumi katika mkoa wa Iringa.

SAMIA SULUHU KUNUSURU BONDE LA MTO RUAHA MKUU

$
0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

Amesema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

Aidha, Makamba amewataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.

Vile vile, ameongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

"Hali hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,"amesema Makamba.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.​

TALISS,DAR SWIM CLUB ZANG’ARA KLABU BINGWA YA MCHEZO WA KUOGELEA

$
0
0
Sonia Tumiotto wa Dar Swim Club akionyesha ufundi wake katika staili ya Breaststroke.A 1
Mwakilishi wa benki ya CRDB akimpongeza muogeleaji nyota wa Tanzania anayesoma Uingereza kwenye shule ya St Felix baada ya kushinda medali ya dhahabu.A 2
 Muogeleaji wa Tanzania anayesoma shule ya St Felix,Collins Saliboko ‘ akipambana’ katika mashindano ya Taifa.A 3
 Waogeleaji wakionyesha staili ya kuchupa ‘diving’.A 4
Hilal Hilal akichapa maji kwenye mashindano hayoA 5
Peter Itatiro akionyesha staili ya backstroke katika mashindano hayoA 6
 Kocha wa Dar Swim Club, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya kupasha viungo moto kwa Waogeleaji wake.A 7
 Adil Bharmal wa Taliss akipambana katka staili ya Breastsroke  A 8
Reuben Monyo wa Dar Swim Club akionyesha uwezo wake katika mashindano hayoA 9
Romeo mihaly wa Champion Rise akipozi na Tan Liu wa Taliss na Saffiro Kweka wa DSC baada ya kushinda medali.A 10
 Collins Saliboko akipozi na wenzake baada ya kushinda medali.

Na Mwanishi wetu
Klabu kongwe ya mchezo wa kuogelea Tanzania, Taliss imeshinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya kuogelea ya klabu bingwa yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye bwawa la kuogelea la Hopac, Kunduchi jijini.

Klabu hiyo imejikusanyia pointi 3,587  katika mashindano magumu na ya kusisimua yaliyoandliwa na Chama Cha Kuogelea nchini (TSA) na kudhaminiwa na Davis & Shirtliff, CRDB Bank, Mediterraneo Hotel & Restaurant, Coca Cola, Aggrey & Clifford na  The Terrace.
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka amesema kuwa Taliss iliweza kujikusanyia pointi 1,681 kwa upande wa waogeleaji wa kike wakati kwa upande wa waogeleaji wa kiume, klabu hiyo ilipata pointi 1,886.

Namkoveka alisema kuwa nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu nyota  ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) kwa kupata pointi  2,587 . klabu hiyo ilipata pointi 1,564  kwa upande wa wanawake na pointi 663 kwa upande wa wanaume.

Nyota kadhaa wa mchezo huo nchini chini ya muogeleaji namba moja nchini kwa upande wa wanawake, Sonia Tumiotto na wenzake,  Smriti Gorkarn, Celina Itatiro, Anjan Taylor na Maia Tumiotto  waliweza ‘kufunika’ katika mashindano hayo kwa kuwa na ‘kasi ya ajabu.

Klabu ya Morogoro  maarufu kwa jina la Mis Piranha ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 1,434. MIS ilipata pointi 606 kwa upande wa wanawake na jumla ya pointi 828 kwa upande wa wanaume.

Waogeaji wa klabu ya Mwanza (MSC) walishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 1,122 huku klabu ya Zanzibar, Wahoo ikimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi 497. Nafasi ya tano ilichukuliwa na klabu ya Bluefins kwa kupata pointi 442 wakati Champion Rise ikiibuka ya sita kwa kupata pointi 221.

Klabu za Moshi iliopata pointi, KMKM, Kennedy House School, Zanzibar Dolphins, , Heaven of Peace academy  na JKT zilimaliza katika nfasi ya saba mpaka ya 13.Namkoveka alisema kuwa mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na maandalizi mazuri na sapoti kutoka kwa wadhamini.

 “Tunashukuru kumaliza salama mashindano haya, kwa kweli yalikuwa magumu na kwa mara ya kwanza, jumla ya waogeleaji 172 walishiriki, hii ni ishara kuwa mchezo wetu unakuwa na tunatarajia kupata mafanikio zaidi katika timu zetu za taifa,” alisema  Namkoveka.

IN LOVING MEMORY

“BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU NA WADAU WA MICHEZO KUFANYIKA MEI 20 MWAKA HUU MJINI KOROGWE”

$
0
0


NA MWANDISHI WETU, KOROGWE.


BONANZA la Michezo la siku sita litakalohusisha walimu wa michezo na wadau mbalimbali linatarajiwa kufanyika Mei 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Halmashauri ya Korogwe .

Bonanza hilo limefadhiliwa na asasi ya Inuka wenye lengo la kupiga vita madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo na nidhamu kwa jamii

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kaimu Mratibu wa Inuka Kanda ya Ziwa,Gaudance Msuya alisema lengo kubwa litakuwa kuiamsha jamii na kupenda kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya zao.

Alisema katika bonanza hilo michezo itakayokuwepo ni mpira wa miguu,riadhaa ,mpira wa pete,kuvuta kamba na kukimbiza kuku na kutembea na magunia.

Aidha alisema washindi kwenye michezo hiyo wata zawadiwa zawadi mbalimbali ambapo zaidi ya milioni mbili zimetengwa kwa ajili ya zawadi kwa washiriki watakofanya vizuri.

“Ndugu zangu watu wa Korogwe hii ni fursa ya kipekee hivyo ninawaomba mjitokeze kwa wingi kushiriki kwenye bonanza hili ambalo litakuwa na faida kubwa licha ya kuwepo kwa zawadi hizo”Alisema.

Hata hivyo alisema kwa washiriki ambao wangependa kushiriki wawasiliane na Ofisa Michezo wilaya ya Korogwe ili kuweza kuthibitisha ushiriki wao.

Mratibu huyo aliyataka mashirika mbalimbali ikiwemo mabenki kuona namna ya kuunga mkono jambo hilo kwa kuona namna ya kufadhili ambapo wanaweza kuwasiliana na mratibu huyo kwa simu namna 0683122320/0683122340.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSAIDIZI WA PEMBEJEO

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Shenal Nyoni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kwa kuongeza gharama za pembejeo kwa kushirikiana na baadhi ya mawakala wa pembejeo za kilimo.

Amesema Serikali italipa madeni yote ya mawakala wa pembejeo za kilimo mara baada ya kukamilisha uhakiki na kujiridhisha juu ya uhalali wake, sababu bado inawahitaji mawakala ili kushirikiana nao katika kuhudumia wakulima kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Aprili 10, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kati yake na mawakala wa pembejeo za kilimo pamona na Maofisa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Gharama ya madeni ni kubwa kuliko pembejeo zilizosambazwa. Hii inatokana na udanganyifu mkubwa unaofanywa na mawakala kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali wanaohusika na masuala ya pembejeo,”

Amesema kuwa kwenye eneo la pembejeo kuna matatizo makubwa kutokana na baadhi ya Maofisa kuzungumza na mawakala na kuongeza gharama za pembejeo kwa lengo la kuibia Serikali na kisha kugawana fedha. “Sasa Serikali haiwezi kulipa madeni ya kutengenezwa bali tutawalipa stahili zenu baada ya uhakiki kukamilika kama nilivyosema awali,”.

Waziri Mkuu ameongeza mawakala wa pembejeo waliwasilisha Serikali deni la sh. bilioni 65.4 kwa huduma waliyoitoa katika mikoa 25 ambapo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekamilisha uhakiki wa madeni hayo kwa mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha ambayo madeni yake ni asilimia 70 ya madeni yote.

Amesema ripoti ya uhakiki wa mikoa nane kati ya 10 imetoka (imebaki Katavi na Kigoma) na kubainisha kuwa mikoa hiyo inadai sh. bilioni 36 kati ya hizo sh. bilioni 11 bado zinaendelea kuhakikiwa, sh. bilioni 14 zimekataliwa hivyo siyo madeni halali, sh. bilioni 8.2 ndiyo deni halali na sh. bilioni 2.3 zinachungizwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Waziri Mkuu amesema uhakiki wa madeni kwa mikoa 15 iliyobakia ambayo madeni yake ni asilimia 30 unaendelea ambapo amewasihi mawakala hao kuwa wavumilivu katika kipindi ambacho Serikali inafanya uhakiki kwa kuwa inataka itende haki kwa kila mtu kulipwa deni lake kwa kiwango kinachostahili na watakaobainika kufanya udanganyifu watachukuliwa hatua za kisheria.

(MWISHO)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P 980, DODOMA
JUMATATU, APRILI 10, 2017.

KAMPUNI YA TATA YAWAFADHILI WATANZANIA KWENDA NCHINI INDIA KWA MAFUNZO YA KUTENGENEZA MAGARI

$
0
0
 Viongozi wa kampuni hiyo ukitoa zawadi ya ua kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi.
 Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi (kulia), akikabidhiwa zawadi ya picha ya tembo na viongozi wa kampuni hiyo. Kutoka kushoto ni Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
 Mama wa msichana pekee anayekwenda kupata mafunzo hayo, Fatma Mussa Ngulangwa (kushoto), akimkabidhi binti yake, Mariam Shamte maua ikiwa ni ishara ya kumuaga.
 Fr.Lucas Wakuganda akimkabishi maua mtoto wake anayeondoka kwenda masomoni nchini humo.
 Mhitimu wa mafunzo hayo, Osmund Kapinga (katikati), akiwa amewainua mikono vijana hao ikiwa ishara ya kuwaaga. 
 Mkufunzi wa mafunzo wa kampuni hiyo, Oscar Mwakagenda (kushoto), akitoa maelekezo ya injini za gari zinazofanya kazi mbele ya mgeni rasmi na uongozi wa kampuni hiyo.
 Ni furaha tupu katika hafla hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya karakana ya mafunzo.
 Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akizungumza Makao Makuu ya Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakati wa  hafla ya kuwaaga vijana wanne wa kitanzania ambao wanakwenda nchini India kwa mafunzo ya miezi tisa ya kutengeneza magari. Kutoka kushoto ni viongozi wa kampuni hiyo, Sarvan Keshri na Udayagiri Veeru.

  Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akisisitiza jambo.
 Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya Tata, Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Tata imetoa ufadhili kwa vijana wanne wa kitanzania kwenda nchini India kujifunza utengenezaji wa magari.

Kati ya vijana hao msichana ni mmoja ambapo wanatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea mji wa Jamshedpur nchini humo kwa mafunzo ya miezi tisa kupitia mpango wa Skill pro- International Business Commarcial Vehicles Skill Development Program.

Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi akizungumza Dar e Salaam jana aliwataka vijana hao wakiwa nchini humo kuwa mabalozi wa kutangaza sifa nzuri ya Tanzania na si vinginevyo.

"Tumieni fursa hii mliyoipata  kwenda kusoma na kuitangaza nchi yetu msiende kucheza na kututia aibu kwani katika vijana 25 kutoka nchi mbalimbali za Afrika nyie wanne ndio mnaiwakilisha nchi yetu" alisema Masingi.

Masingi aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha vijana hao na kuahadi serikali kushirikiana nayo ili kupanua soko la ajira kwa vijana nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania Prashant Shukla alisema hii ni awamu ya tatu kwa kampuni hiyo kupeleka vijana nchini India kujifunza kutengeneza magari ambapo kwa awamu ya kwanza hakuna kijana wa kitanzania aliyehudhuria mafunzo hayo.

Alisema kwa awamu ya pili alipelekwa mtanzania Osmund Kapinga ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi bora na katika awamu hii ya tatu wanakwenda hao wanne.

Alisema lengo la kuwapeleka vijana hao nchini India ni kujifunza kazi hiyo ili nao wakirudi waweze kuwa walimu wa wenzao hivyo kuisaidia serikali kukuza ajira nchini hasa kwa vijana.

Alisema kampuni hiyo kwa Tanzania inafanya kazi  mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza lakini wanatarajia kwenda mkoani Mbeya kufungua tawi na baadae itafuatia  mikoa mingine ambapo vijana wanaopata mafunzo kupitia mpango huo wataenda kuwafundisha wenzao.

Mhitimu wa mafunzo hayo nchini humo Osmund Kapinga alisema kampuni hiyo ni kubwa na mbali ya kutengeneza magari ya aina zote inavitu vingi inavyo tengeneza hivyo aliwasihi wenzake wanaoondoka kuchangamkia fursa hiyo hadimu ili wakirudi waweze kuwasaidia watanzania wenzao.

Vijana waliopata fursa ya kwenda kupata mafunzo hayo ni Mariam Hemed Shamte, Anord Peter Nditu, Elias Jones Tette na Adam Abdallah Pwimu.

HABARI DEVELOPMENT ASSOCIATION KUZINDUA KLABU ZA KUPINGA UJANGILI TANZANIA

$
0
0

Na theNkoromo Blog
Taasisi ya Waandishi wa Habari ambao ni wanaharakati wa kupinga ujangili ya Habari Development Developmnet Association (HDA) itafanya uzinduzi rasmi wa  klabu za kupinga ujangili Tanzania kwa kufanya matukio mbalimbali kwa siku tatu mjini Morogoro.

Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, Katibu Mkuu wa Habari Taasisi hiyo Daniel Sarungi, aliyataja matukio yatakayoambana na uzinduzi huo utakaofanyika kuanzia Aprili 20 hadi 22, 2017, kuwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu tabia za Tembo na Faru ambapo Mbuga za Wanyama na Hifadhi watatoa mabanda maalum kwa ajili ya kutoa elimu hiyo na kisha washiriki kupewa fursa ya kuuliza maswali yatakayojibiwa na watalaam.

Sarugi alisema, siku itakayofuata itatumika kwa michezo miongoni mwa mabalozi wa wanyama na baadaye Wizara ya Maliasili na Utalii itatoa takwimu kuhusu ujangili ya idadi ya tembo na faru waliouawa na idadi ya kesi za ujangili zilizotolewa hukumu na zinazoendelea kusikilizwa.

Alisema, siku ya tatu ndipo utafanyika uzinduzi rasmi wa klabu za kupinga ujangili, uzinduzi ambao utafuatiwa na matembezi maalum kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu hadi Uwanja wa Michezo wa Jamhuri mjini Morogoro.

Sarungi amwakaribisha wadau na wananchi kwa jumla  kufika kushiriki matembezi hayo na kwamba hakutakuwa na gharama ya ushiriki isipokuwa atakayesukumwa kushiriki atatakiwa kuwahi mapema ili kuandaliwa vifaa vya matembezi ikiwemo fulana.

Amesema, tukio hilo limeungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utali, PAMS Foundatuion, TBL kupitia vinywaji vyake vya Ndovu na Bavaria, Leopard Tour, Hakuna Matata Foundation na Better Dayz Co Ltd.

Ameziomba kampuni na taasisi nyingine kujitokeza kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli katika vita dhidi ya ujangili kupitia majukumu yao ya kijamii na kwamba nafasi ya udhamini wa tukio hilo bado ipo wazi.

Sarungi amesema, hatua ya kufanya harakati hizo, ni kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kukuza utalii nchini, hasa ikiwemo hatua  yake ya kununua ndege hatua ambayo itaongeza idadi ya watalii kuja nchini.

"Baada ya kuona juhudi hizi za Rais na sisi kama Wazalendo tunaona ni lazima tuhimize utokomezaji wa ujangili kwa kuwa itakuwa haina maana kama watalii wataongezeka huku wanyama kama tembo na faru akiwa wametoweka", alisema Sarungi.

Alisema kufuatia ongezeko la matukio ya Ujangili imesababisha Tanzania kuwa nchi ya tatu katika makosa ya jinai barani Afrika, hivyo klabu za kupinga ujangili vimejitolea kushiriki kikamilifu katika mapambano ya kupinga ujangili ili kuhakikisha wanayama wanalindwa hasa kwa kutolewa elimu kwa jamii.
 Katibu wa Habari Development Association (HDA), Daniel Sarungi akizungumza na Waandishi wa Habari, jana, Dar es Salaam. Wapili ni Mratibu wa Uzinduzi wa Klabu za kupambana na Ujangili Tanzania, Christopher Kajituel na kulia pia ni mratibu wa Uzinduzi huo,  Chaano Samson.
 Mweka hazina wa Habari Development Association Kaimu Mzinja (aliyesimama) akijadili jambo, wakati uongozi wa Tasisi hiyo ukitangaza uzinduzi huo wa Klabu za kupinga ujangili, leo.
 Sarungi na Kaimu wakijadili jambo
Viongozi wa Associan hiyo wakiwa katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali kuhusu uzinduzi wa Klabu hizo za kupinga ujangili Tanzania. Picha zote na theNkoromo Blog

wanafunzi wa kidato cha tatu walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini watembelea ofisi za Airtel

$
0
0

Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.
Wanafunzi hao wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakitumia komputa kubwa iliwekwa kwaajili ya wateja katika duka la Airtel Makao Makuu kuangalia bidhaa na huduma mbalimbali wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji wa Mitambo wa Airtel , Frank Munale akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano. Akishuhudia ni Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
Afisa Huduma kwa wateja wa Airtel, Stephen Makongoro akiwaonyesha baadhi ya wanafunzi jinsi ya kupata huduma mbalimbali kupitia komputa kubwa iliyopo katika duka la kisasa la Airtel wakati wanafunzi hao wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ATETA JAMBO NA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa nyumbani kwake mjini Dodoma akiwa njiani kuelekea mkoani Iringa kuzindua kikosi kazi cha Taifa cha bonde la mto Ruaha Mkuu.

Mbunge wa Mtama Mh Nape akutana na wazee maarufu wa jimbo lake kuzungumzia maendeleo yao kwa pamoja

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao ,kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche .
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A ,katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa kaniasa la Katoliki,Mtama Lindi Vijijini.Mh Nape alizungumza mambo mengi ikiwemo na kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali,amewaomba kuziweka kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafirie namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.

"Ndugu zangu,Wazee Wangu siasa kwa sasa zimekwisha,niwaombe tu,itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando,tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo,na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo,basi ntahakikisha yale yote niliyo yaahidi wakati wa kampeni,ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyakupunguza kwa kiasi kikubwa",alisema Nape.Picha na MichuziJr.
 Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama na kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mh. Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo. 
 Baadhi ya akina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao
 Mmoja wa Wananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo,ambalo amemuomba Mh Nape alifanyie kazi
Mh.Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja


MSANII ROMA MKATOLIKI AZUNGUMZIA SAKATA LA KUTEKWA KWAKE NA WASANII WENZAKE, AONGOZANA NA WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0

.Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kwakuwa inaonesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe
Roma Mkatoliki akifafanua zaidi kwa waandishi wa Habari

Roma akiwaonesha wana habari namna alivyojeruhiwa aliokuwa akiteswa na hao watekaji ambao mpaka sasa hawajajulikana ni akina nani,kufuatia Uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujula kwakuwa inaoyesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Mkewa wa Msanii huyo Bi Nancy.

Baadhi ya Wana Habari wakimsubiri msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Roma Mkatoliki kuja kuzungumza nao na kuwaeleza kilichowatokea

Baadhi ya Wana habari wakifuatilia tukio hilo
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam


Mke wa Roma Mkatoliki pamoja na baadhi ya wasanii wakisubiri kuanza kwa mkutano huo wakati Msanii huyo akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kutekwa kwake kulia ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe.
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akiongozana na wasanii Roma Mkatoliki na wenzake ili kuzungumzia sakata la Roma Mkatoliki lililotokea hivi karibuni.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE ,APRILI 11, 2017


DKT. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA TBC

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe picha za Viongozi mbalimbali waliowahi kuongoza TBC wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akionyeshwa mikanda ya santuri zenye hotuba za Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akionyeshwa baadhi ya machapisho yaliyohifadhiwa ndani ya studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia picha mbalimbali za wasanii na watu maarufu katika ubao wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza mtangazaji wa Redio France International (RFI) wakati wa ziara yake katika studio za redio hiyo Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwa ndani ya studio ya Redio France International (RFI) wakati wa ziara yake katika studio za redio hiyo Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia mtambo wa redio uliokuwa ukitumika zamani enzi za ukombozi wa Bara la Afrika ambapo matangazo yake yalirushwa na mtambo huo wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) kipindi hiko.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia moja ya mitambo ya redio inayotumika sasa kurusha matangazo ya moja kwa moja ndani ya studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Makao Makuu-Barabara ya Nyerere.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia meza iliyokuwa ikitumika na Mwalimu Nyerere wakati alipokuwa akitembelea Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) enzi za uhai wake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayub Rioba mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Taasisi hiyo 10 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na watendaji wengine toka Wizarani mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Makao Makuu ya Taasisi hiyo 10 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

PROF. MAGHEMBE - NI MARUFUKU KUSAFIRISHA MKAA KUTOKA WILAYA MOJA KWENDA NYINGINE KUANZIA MWEZI JULAI. ASHAURI MAJANGILI WACHUKUE MATREKTA WAKALIME LAA SIVYO WAJIANDAE NA KIFUNGO CHA MIAKA 25 JELA

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 24 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo terehe 10 Aprili, 2017 katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Esther Malima. 
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati waliokaa) na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kufungua mkutano huo leo terehe 10 Aprili, 2017 katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 24 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo terehe 10 Aprili, 2017 katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akiimba wimbo wa Umoja wa Wafanyakazi (Solidarity Forever) muda mfupi kabla ya kufunga mkutano huo leo terehe 10 Aprili, 2017 pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Baraza hilo, Esther Malima (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Mrimia Mchomvu.

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kshoto) akizungumza katika mkutano huo leo terehe 10 Aprili, 2017.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa baraza hilo kutoka kwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe (hayuko pichani) katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma leo. 
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
 Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo.
 Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti.
 Baadhi ya wajumbe Sekretarieti wakiteta jambo nje ya ukumbi.


NA HAMZA TEMBA - WMU
...................................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametangaza mabadiliko makubwa katika biashara ya mkaa nchini na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mkaa wowote utakaosafirishwa kutoka wilaya moja kwenda nyingine ili kunusuru misitu inayoteketea kwa kasi hapa nchini.

Amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka kwenye Idara, Vitengo na Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo.

“Kuanzia mwezi Julai hakuna ruhusa ya kutoa vibali vya kuhamisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, mkaa utachomwa, utauzwa ndani ya wilaya kwa ajili ya matumizi ya watanzania wanaohitaji nishati ya mkaa, lakini biashara ya mkaa ya kutoa Dodoma kwenda Dar es Salaam mpaka Zanzibar marufuku.

“Wamekata misitu yetu yote, mito yetu imekauka, tunashindwa kupata maji ya umwagiliaji kwasababu watu wengi huko nje wanataka mkaa wetu, Tanzania jamani sio shamba la bibi, wale wote watakaotoa mkaa kutoka eneo moja hadi jingine kinyume na sheria hii watashuulikiwa kwa utaratibu wa uhujumu uchumi”, amesema Maghembe.

Amesema kuwa kwa upande wa miji mikubwa kama Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga vitaanzishwa viwanda maalumu vya kuzalisha mkaa ambao utauzwa kwa vibali maalumu katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Amesema mkaa huo hautakuwa na athari nyingi za kimazingira kwa sababu utazingatia taratibu za uzalishaji endelevu.

Wakati huo huo, Waziri Maghembe amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kumuhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Kikosi cha Kufuatilia na Kuzuia Uharibifu wa Misitu wa Wakala hiyo, Arjason Mloge kutoka Makao Makuu ya Taasisi hiyo kwenda chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kilichopo mkoani Kilimanjaro na badala yake atafutwe mtu mwingine muaminifu.

Amesema uamuzi huo ni kufuatia udhaifu uliojitokeza katika usafirishaji wa rasilimali za misitu ndani na nje ya nchi ikiwemo usafirishaji kwa kutumia nakala za vibali ambazo sio halisi, yaani “Photocopies”. “Agizo hili litekelezwe mara moja kabla ya saa sita mchana wa leo na niwe nimepewa nakala ya barua hiyo ya uhamisho” amesema.

Kufuatia uamuzi huo amepiga marufuku kuanzia leo usafirishaji wa mazao ya misitu ndani na nje ya nchi kwa kutumia nakala zisizo halisi (Photocopies). Ameongeza kuwa katika kuunga mkono Sera ya Uchumi wa Viwanda ya Serikali ya awamu ya tano hakuna gogo litakalosafirishwa kwenda nje ya nchi.

“Wawekezaji wanahimizwa kujenga viwanda vya kuchakata magogo hayo hapa nchini ili kutoa ajira kwa Watanzania pamoja na kutoa faida halisi inayotokana na rasilimali hizo kwenye uchumi wa taifa”, amesema.

Akizungumzia changamoto ya mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini amesema Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 sehemu ya 21 (1) hairuhusiwi kabisha kuchunga mifugo katika Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Hifadhi za Misitu. Amewataka watumishi wa Maliasili kusimamia Sheria hiyo pamoja na kutoa wito kwa wananchi kuifuata kikamilifu.

Katika hatua nyingine, Waziri Maghembe amewataka majangili wote nchini kuachana na biashara hiyo haramu ambayo hailipi kwa sasa na badala yake wachukue matrekta wakalime.

“Mtu ambaye alikuwa anaishi kwa kutegemea ujangili sasa atafute trekta akalime, kwa sababu akifanya ujangili tukamkamata tu, na tukimkamata atakaa kwenye hoteli ya mkuu wa magereza (magereza) kwa zaidi ya miaka 25”.

Aidha, Waziri Maghembe ametoa pongezi kwa watumishi wote wa Wizara ya Maliasili kwa kazi nzuri wanayofanya ya kupambana na ujangili nchini pamoja na ulinzi wa maliasili za taifa (Misitu, Wanyamapori na Mambo ya Kale) ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 20.5 kwenye pato la taifa. Amesema matokeo chanya ya kupambana na ujangili yameanza kuonekana japo ujangili bado upo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki amemueleza Waziri Maghembe kuwa maelekezo yote aliyoyatoa yamepokelewa kwa ajili ya kuyafanyiwa kazi, huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa akimueleza Waziri huyo kuwa watalinda na kusimamia Malisili za Taifa na kwamba katu hawapo tayari kuandikwa kwenye vitabu kuwa walishiriki katika kutoweka kwa maliasili hizo.

MRADI WA ECOPRC WAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI JUU YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU NA MABADILIKO YA TABIA NCHI, MJINI MOROGORO

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Elinasi Monga akifundisha somo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo aliweza kukazia suala la waandishi wa habari kujua visababishi na viashiria ambavyo ni vyema kujua na kuweza kuvifanyia kazi kwa ufasaha zaidi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.

Katika mafunzo hayo Mratibu wa Mradi huo alisema kuwa wakulima wadogo wadogo ndiyo wanaathika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa wamekuwa hawana uelewa mzuri katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Aliongeza jambo lingine linalorudisha nyuma ni serikali za mitaa kukosa mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Mwisho alisisitiza uongozi mbovu katika sekta ya misitu huchangia uharibifu wa misitu kwa kiasi kikubwa.
`
 Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Elinasi Monga akisisitiza jambo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akifundisha somo juu ya kiwango vya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, Nyenzo shirikishi pamoja na umuhimu wa misitu ya jamii ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhiria mafunzo hayo.
Kikundi cha tatu kikijadiliana.
Kikundi cha pili kikijadiliana. Kikundi cha kwanza wakijadiliana. Kuhusu Mradi wa ECOPRC Mnamo tarehe 25 Oktoba 2012, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Norway zilikubaliana kuingia katika mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wananchi kupitia Mafunzo ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM), Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa Kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) na Mabadiliko ya Tabianchi (“Empowering Communities through Training on Participatory Forest Management, REDD+ and Climate Change Initiatives – ECOPRC”). Lengo kuu la mradi huu ni kujenga uwezo wa vikundi mbalimbali vya kijamii ili viweze kusimamia misitu kwa uendelevu na kwa faida; lengo mahususi ni kuongeza tija katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu kwa namna ambayo inaleta faida kijamii, kiuchumi, kimazingira na kiutawala bora kwa jamii zinazojihusisha na shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi. Mradi huu ni wa miaka mitano, unaotekelezwa na washirika wanne ambao ni Chuo cha Misitu Olmotonyi (Mshirika Kiongozi), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA); Kituo cha Misitu na Watu (RECOFTC) cha Bangkok-Thailand na FORCONSULT, kitengo cha ushauri elekezi cha Kitivo cha Misitu na Hifadhi ya Mazingira Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine. Shughuli za Mradi zinatekelezwa katika malengo mahususi sita: 1. Programu ya kujenga uwezo wa Taifa katika USM/MKUHUMI umeandaliwa na kurasimishwa kupitia mafunzo yatokanayo na uzoefu na uwezo wa kusharadiana na mazingira halisi. 2. Ufanisi na Uwajibikaji wa Halmashauri za Wilaya na Watumishi wake Unaongezeka Kwa Kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau katika nyanja za USM, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi. 3. Kuboresha Maarifa na Uelewa wa Viongozi wa Vijiji Katika usimamizi endelevu wa shughuli za USM, MKUHUMI Mabadiliko ya Tabianchi. 4. Kutoa Fursa kwa Watendaji, Watekelezaji na Watoa Maamuzi ili Waweze Kupitia, kufanya Mageuzi na Kutambua Mazingira Wezeshi kwa Sera za USM, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi. 5. Miundombinu ya Chuo cha Misitu inaboreshwa ili kuongeza ufanisi katika kutoa Mafunzo bora 6. Usimamizi na Uendeshaji wa Mradi.
 Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Daniel Lucas akifundisha somo juu ya kuimarishwa Utawala Bora katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Meneja wa Mradi wa ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akifunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Alisema kuwa nia ya nia ya mradi wa ECOPRC ni kuziwezesha jamii ziishizo vijijini na wadau wengine kupitia mchakato mahsusi wa kuwajengea uwezo ili kuboresha Usimamizi Shirikishi wa Misitu na kuwa na uboreshaji wa njia za maisha katika jamii. lengo la mafunzo haya ni kuhamasisha serikali katika Usimamaizi Shirikishi wa Misitu ili kuwa na faida za kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa jamii zinazojihusisha na Usimamizi Shirikishi wa Misitu. Kushoto ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Mussa Twangilo (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, James Lyatuu (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Henry Mwakifuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Beatrice Philemon (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Safia Maftah (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Saada Mbarouk (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa Blogger na mwandishi wa habari, Cathbert Angelo Kajuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Josephine Mallango (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Agrey Evarist (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Kalokola Aporinary (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Prosper  Kaijage (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC) mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wao.

TWAWEZA yatoa Taarifa ya Tafiti za Uwezo Tanzania

MBUNGE BUPE MWAKANG'ATA AIPIGA TAFU SHULE YA MSINGI KIGOZILE

$
0
0
 Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji
 Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili ya kuongezea kununua mifuko ya saruji kwa ajili ya kukarabati shule ya kigonzile

Na Fredy Mgunda,Iringa
Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameipiga jeki shule ya msingi Kigonzile iliyopo kata ya Nduli mkoani iringa kwa kuipatia mifuko zaidi ya ishirini ya saruji kwa lengo la kusaidia ukarabati wa shule hiyo akiwa na lengo la kumuunga mkono mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati katika juhudi za kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mwakang'ata alisema kuwa ameamua kumuunga mkono mbunge huyo kwa kuwa ni mpenda maendeleo na mchapa kazi.

“Mimi napenda kufanya kazi za kimaendeleo hasa za kijamii ndio maana kabati aliponiambia kuwa anakuja kufanya maendeleo ya ukarabati wa shule ya msingi kigozile nilikubali haraka kwa kuwa na napenda kufanya maendeleo” alisema Mwakang'ata

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  ametutuma kufanya kazi kwa wananchi wakawaida kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi kuliko watu wa kipato cha kati na cha juu hivyo hata mimi nimeamua kufanya kazi za kwasaidia kuleta maendeleo wananchi wengi wa chini.

Aidha Mwakang'ata aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli na kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko kusubili serikali kuleta maendeleo.

“Mkiwa mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi basi nchi hii itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na wananchi kufanya kazi kwa nguvu na moyo wa kuinua uchumi” alisema  Mwakang'ata

Mwakang'ata aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati hivyo nawaomba viongozi wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa nyingi za kusaidia kukarabati miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu bora.

“Hichi nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma kwenu katika swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile ambayo ilikuwa katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake” alisema Mwakang'ata

Mwakang'ata namkaribisha pia mbunge Ritta kabati kuja Rukwa pia aje asaidie maendeleo kwa kuwa naye ni mpenda maendeleo na wananchi wa Rukwa wanapenda maendeleo na ninahakika watampokea kutokana na uchapakazi wake.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images