Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUIVA UWANJA WA UHURU,PIA KUFANYIKA MIKOA YA MWANZA NA SIMIYU

0
0


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni,jijini Dar es salaam kuhusiana na  maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Uhuru na kutumbuizwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa mbalimbali na nchini Tanzania.

Msama amesema mwimbaji nguli kutoka nchini Afrika ya Kusini Solly Mahlangu atakuwa ni mmojawapo wa waimbaji kutoka nje ya nchi wakiwemo wengine kutoka nchini Kenya, Ameongeza kuwa tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa ya Mwanza na Simiyu, hata hivyo tamasha hilo halitafanyika katika mkoa wa Dodoma kama ilivyotangazwa awali kutokana na uwanja wa Jamhuri ambao ulikuwa utumike siku hiyo kuwa na shughuli nyingeni. 
Msama amesema kuwa katika tamasha hilo la Pasaka litakalofanyika katika Uwanja wa Uhuru,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya tamasha hilo kurindima jijini Dar litahamia Simiyu na jijini Mwanza ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula .

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Bw. Alex Msama katika mkutano huo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama alipokuwa akisisitiza jambo kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka

taarifa ya tahadhari ya mvua kubwa katika maeneo ya pwani nchini kuanzia tarehe 06-04-2017 hadi 08-04-2017.

0
0

DKT.MENGI ASISITIZA WATANZANIA KUONDOA UOGA

0
0
WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia ubia na makampuni ya nje. kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni 50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa, alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali.  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa. (Picha zote Thebeauty.co.tz)

 Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa) walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika uthubutu wao. 

 Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania kuthubutu. Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

 Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali. Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka.  

Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya hivyo hapa nchini. Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

 Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji. Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040.

 Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote. Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa.  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Blevin Claude (wa pili kushoto) akiwa na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Beatrice ALPERTE (kushoto) katika mkutano huo. Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua masomo ya biashara walioshiriki mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wadau na wafanyabiashara kutoka makampuni 50 ya nchini Ufaransa walioshiriki mkutano huo. Mkutano ukiendelea. Sales Executive wa kampuni ya CMC Formula wauzaji wa magari ya Renault, Erica George akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati akitembelea mabanda katika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akipata maelezo katika banda la kampuni ya TOTAL. Meneja Mauzo wa Kampuni ya AIRBUS HELICOPTERS, Jean-Marc Royer (kulia), akitoa maelezo ya shughulli wanazofanya kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kutoka nchini Ufarasan zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Ufaransa yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Kushoto ni Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude. Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude akitoa neno la shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati Dk. Mengi akijiandaa kuondoka katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yalipofanyika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa jijini Dar es Salaam.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 7,2017

0
0

NCHAMBI: WANANCHI MUWE KICHOCHEO CHA MAENDELEO

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi akifungua kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu.
A 1
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati hicho kikao hicho.
A 2
Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo kutoka kushoto, Grace Chamila, Mh. Regina, Salma Kalebo na Thomas Ng’ombe wakifuatilia kikao hicho.
A 5
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kishapu ambaye ni Diwani wa Kata ya Uchungani wilayani humo, Paul Makolo akitoa uzoefu wake kuhusu namna ya fedha za Mfuko wa Jimbo zinavyofanya kazi wakati wa kikao hicho.
A
Washiriki wa kikaao hicho wakiwemo madiwani, watendaji kata, vijiji, wenyeviti wa vijiji, maafisa tarafa na viongozi wakifuatilia kikao hicho.
A 3
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi (katikati) akiongoza kikao cha Mfuko wa Jimbo jana. Wengine pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu.
A 6
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.
A 7
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo.
A 8
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, Helen Chacha, Diwani wa Kata ya Uchunga, Paul Makolo na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu wakifuatilia kikao hicho.
……………………..
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi amewataka wananchi kuwa kichocheo cha miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila kujali msingi ya tofauti zao.

Nchambi alisema hayo jana wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo jumla y ash. Milioni 82 zinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Katika kikao hicho kilichohudhuria pia na madiwani, watendaji mbalimbali na viongozi wa dini alisema wananchi wanaoibua miradi ya maendeleo na Serikali kupitia Mfuko wa Jimbo inawapelekea fedha ili zitumike kufanya miradi hiyo.

Alisema viongozi wa ngazi za kata wakiwemo madiwani na watendaji wana nafasi ya kuhamasisha wanancho wao kushiriki katika shughuli za maendeleo na kutoa elimu kuhusu fedha za mfuko huo.Mbunge huyo alibainisha kuwa katika mwaka huu fedha zinazotarajiwa kutolewa katika jimbo hilo zitasaidia katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata mbalimbali.

Nchambi alizihakikishiwa taasisi na wananchi kuwa tayari kuwasaidia katika hatua za kuunganisha umeme lengo likiwa kila mmoja apate huduma hiyo bila kujali tofauti zao mbalimbali.Kwa mujibu wa mbunge huyo nishati hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na kuzidi kuimarisha uchumi kwenye jimbo na pia halmashauri ya wilaya nzima kwa ujumla wake.  

“Tumuunge mkono Rais wetu ana dhamira nzuri na anataka kila mwananchi awe ameunganishwa umeme kwani umeme utahamasisha maendeleo kwenye jimbo letu na kata zake, tunataka jimbo liwe na shapu shapu,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga aliwataka wanakamati hiyo kuwa makini katika kusimamia fedha za Mfuko wa Jimbo.Magoiga alisema fedha hizo zinapaswa kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwa zinapaswa kusimamiwa vizuri ili kuendana na kauli mbiu ya Rais ya hapa kazi tu.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji na wenyeviti wote wa vijiji kufungua akaunti benki ili kuhifadhi fedha za miradi wanazopokea badala ya kuhifadhi kwenye akaunti binafsi.   

Mkurugenzi mtendaji aliwataka kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwa Serikali itawasaidia pale ambapo watakuwa wameibua miradi ikiwemo kuanzisha majengo ya huduma za kijamii.

Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack kwa kutoa mabati 171 kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa katika shule za msingi akisema kuwa hatua hiyo itasaidia kujenga Kishapu.

Shindano la Hoja juu ya Sifa za Rais Bora wa Nchi kama Tanzania - Milioni 55 Kushindaniwa

0
0

KIWANJA KINAUZWA KIGAMBONI KIBADA

0
0
 Muonekano wa Kiwanja. Ni Kuanzia mwanzo wa Picha mpaka mwisho wa Ukuta upande wa kushoto
Mwanzo wa Picha Mpaka kwenye ukuta wa Ghorofa kule 
Kiwanja Kipo KIGAMBONI KIBADA
Ukubwa wa Kiwanja ni Mita za Mraba (Sqmeter) 1088
Kiwanja kina hati safi na hakina mgogoro
Bei ni Milioni 65Maongezi kidogo yapo na Kiwanja hiki kinauzwa Na Mwenye Nacho 
Kwa Mawasiliano 0786 821 613
Karibu mwenye Uhitaji. Biashara Maelewano Hata 

KOCHA WA MAJI MAJI ASEMA MCHEZO WA WAO NA AFRIKA LYION JUMAMOSI UTAKUWA MGUMU SANA.

0
0
Timu ya majimaji imeendelea kufanya mazoezi ya kufa mtu katika uwanja wa Majimaji kujiwinda na Afrika Lyion huku Kocha msidizi wa Majimaji Habibu Kondo asema mchezo wao wa jumamosi utakuwa mgumu sana.

DC KASESELA AWATAKA WANANCHI KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.

Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiliwili chake.

“Kwanini watu wajichukulie hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela.

Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.

“Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 

Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.

Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe 06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo

RC GAMBO:WANANCHI LIPENI KODI ZA MAJENGO ILI KUONDOA USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA

0
0

Na.Vero Ignatus .Arusha

Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi hizo

Hata hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.

Hata hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka 2015-2016.

Vilevile Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja wapo.

Nae meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza Kwa umoja ili kurahisisha zoezi hilo na kuweza kutekeleza agizo la serikali kulipa kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema  leo ofisini kwake .Picha na Vero Ignatus Blog.

 Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa  kwa waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.

MBUNGE WA BUSEGA RAPHAEL CHEGENI AFANIKISHA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA NGASAMO

0
0

Mbunge wa Jimbo la Busega, Mkoani Simiyu, Dk Raphael Chegeni ambaye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wa ndani na nje ya nchi amefanikiwa kujenga bweni moja la wasichana katika Sekondari ya Ngasamo ikiwa ni jitihada za kuwanusuru watoto wa kike na ukatishaji masomo unaotokana na mimba pamoja na vishawishi bvingine mbalimbali.
 Vitanda katika moja ya vyumba vya bweni hilo.
MBUNGE wa Busega Dr. Raphael Chegeni amefanikisha ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ngasamo.

Bweni hilo lenye uwezo wa kuhudumu wanafunzi wa kike 48 litasaidia wasichana kupata muda wa kujisomea na kujiepusha na adha ya kutembea mwendo mrefu wa kuja na kurudi shuleni.

Kitendo hicho imekuwa kikwazo  kwa baadhi kuangukia mtego wa kukatisha masomo katokana na bodaboda Au lift kuwasababishia mimba na hivyo kukatisha masomo yao.

Mbunge huyo ameweka mpango kujenga mabweni kwa shule zilizo katika mazingira hatarishi zikiwemo Malili, Mkula, Kabita na Sogesca.

Aidha amewashukru wadau wakiwemo ubalozi wa Ireland, Canada, Tanapa na Serikali kwa kuchangia jitihada hiz0.

MENEJIMENTI YA TMA YANOLEWA KATIKA KUTEKELEZA SERA NA MIKAKATI YA SERIKALI YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUZI WA UMMA

0
0
Katika jitihada za kuhakikisha TMA inashiriki kikamilifu katika kuongeza pato la Taifa, Mamlaka iliandaa mafunzo ya siku tano ambayo yalikuwa yana lengo la kutoa uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma katika kuboresha utendaji wa kazi hasa katika usimamizi na utekelezaji wa shughuli za ununuzi na usimamizi wa mikataba.

Akizungumza wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi alisema wakuu wa idara na vitengo wafanye maboresho kwenye maeneo yaliyokuwa na changamoto na kitengo cha ununuzi waboreshe utendaji wa kazi sambamba na kusimamia vizuri taratibu zote zinazohusu ununuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kama ilivyoelekezwa na washauri waelekezi kutoka PSPTB ili kuisaidia Mamlaka yetu kutekeleza sera na mikakati ya Serikali ya kupunguza gharama za ununuzi kwa lengo la kuboresha pato la Taifa.

Aidha Dkt. Kijazi aliishukuru Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kukubali kutoa wataalam katika upande wa sheria ya ununuzi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo kila inapobidi.

Kwa upande wa Bodi ya utaalam wa ununuzi na ugavi Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bwana Paul Bilabaye kwa niaba ya Mtendaji Mkuu alitoa pongezi kwa TMA kwa uamuzi wa kutoa mafunzo haya kwa Viongozi wanaohusika na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi na Ugavi.

Mafunzo haya yamejenga uwezo kwa Idara tumizi, Kamati za tathmini, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi pamoja na Bodi ya Zabuni katika kutekeleza majukumu yake.

Mafunzo hayo ya siku tano yamefanyika katika ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu, Wakuu wa idara na wakuu wa vitengo vyote pamoja na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Mamlaka ya Hali ya Hewa.


Imetolewa na

Ofisi ya Uhusiano

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

NAPE NNAUYE APOKELEWA KWA KISHINDO JIMBONI KWAKE,ASHINDWA KUJIZUIA AMWAGA CHOZI

0
0
Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akipita juu ya migongo ya baadhi ya akina Mama walioamua kulala chini ili kiongozi huyo apite juu yao,ambapo imeelezwa kuwa imefanywa vile ikiwa ni sehemu ya heshima kubwa waliompa pamoja na upendo walionao kwa Mbunge wao kwa kusimamia ukweli.Kitendo hicho kilisababisha Mh.Nape ashindwe kujizuia na kuanza kutoa machozi.
Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalala,Mtama mkoni Lindi wakimsubiri kumsikiliza Mbunge wao Mh,Nape Nnauye.
Mmoja wa akina mama akitokwa machozi mara baada ya kumuona Mh Nape 
Baadhi ya Wasanii wa Filamu haba nchini wakiongozwa na Steve Nyerere walipanda jukwani kuzungumza machache na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Mbunge wao Mh.Nape Nnauye.
Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalala,Mtama mkoani Lindi mapema leo wakimsubiri kumsikiliza Mbunge wao Mh,Nape Nnauye aliyewasili jimboni humo kuzungumza nao machache yakiwemo na mambo ya maendeleo ya jimbo lake
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mh Nape kupanda jukwaani na kuianza kuimba nyimbo kwa pamoja huku wakicheza sambamba na shangwe za hapa na pale uwanjani hapo
Wananchi wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala kila kona uwanjani hapo
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape,alipowasili jimboni humo mapema leo kwa lengo la kuwashukuru kwa Kumchagua kuwa mwakilishi wao mzuri na pia kuzungumza mipango yao mbalimbali ya kuliletea maendeleo jimbo lake
Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape Nnauye katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema loe jioni katika uwanja wa shule ya msingi Kiwalala,Mtama mkoani Lindi
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wananchi (hawapopo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema leo jioni jimboni kwake,kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwakala,mkoani Lindi.Mh Nape aliwashukuru Wananchi wake kwa kumpigia kura za kutosha na hatimae akachaguliwa kuwa mwakilishi wao Bungeni,akawashukuru kwa mapokezi makubwa waliompa na kumuonesha ni kiasi gani bado wanampena na kumuhitaji kama kiongozi wao mpambanaji katika kuwaletea maendeleo.

''Kilichonitoa machozi ni heshima kubwa mlionipa akina Mama,Mlilala chini,makataka nipite juu yenu,si ambalo nililitegemea,Nawashukuru sana,Niwaahidi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote,kuwatumikieni,usiku na mchana,nitaikumbuka heshima hii mlionipa na sitoisahau",alisema Mh Nape huku sauti yake ikiendana na hisia ya kutoa chozi mbele ya umati mkubwa uliokuwepo pale uwanjani. 

Mh,Nape alizungumza mambo mbambali yakiwemo mambo mbalimbali ya kuiletea maendeo jimbo la Mtama,ikiwemo suala la Maji,Barabara,Elimu na Afya,kwa maeneo hayo kwa sasa atavisimamia kwa spidi kubwa kwa sababu kwa sasa amepata muda wa kutosha wa kuanza kuwahudumia wananchi wa jimbo lake na kuhakikisha anatimiza yale yote aliyokwisha waahidi wakati wa kampeni.Pia amewataka Wananchi hao kuungana na kitu kimoja na kuweka itikadi za kisiaza pembeni na kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha jimbo la Mtama linapiga hatua kimaendeleo.
Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mbunge wa jimbo lao,Mh Nape Nnauye mapema jioni ya leo
Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao alipokuwa akiwahutubia
Diwani chama cha CUF kutoka kata ya Sudi,Bw.Ali Athumani Njale akimpa mkono wa pongezi na kumtia moyo Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi,katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Kiwalala,Mtama mkoani Lindi,ambapo pia alimuachia ujumbe bahasha alioishika pichani
Baada ya kumalizika mkutano wa Kuwashukuru Wananchi wa jimbo la Mtama,ilifauata dua ya pamoja kutakiana heri na kusameheana yale yote mabaya yaliyotokea na kuanza kurasa mpya,ya kuhimizana kuishi kwa upendo na amani,na kutoruhusu migingano isiyo tija kwa kila mmoja wao.
Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye ikisukumwa na Wananchi,mapema leo jioni mara baada ya kumaliza mkutano wake,uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala,Mtama,mkoani Lindi
Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye ikisukumwa na Wananchi,mapema leo jioni mara baada ya kumaliza mkutano wake,uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala,Mtama,mkoani Lindi
Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye ikisukumwa na Wananchi,mapema leo jioni mara baada ya kumaliza mkutano wake,uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala,Mtama,mkoani Lindi
Baadhi ya Wananchi wakimsubiri Mbunge wao Mh Nape Nnauye ili wamasalimie na kusikia lolote kutoka kwake

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATOA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA 2016

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya utoaji waTuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016 zilizofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mshindi wa jumla Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Devis Deogratius (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.

...............................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.

Alisema mwaka wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi.

Alisema Serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati.

Makamu wa Rais ambaye hotuba yake ilizungumzia mafanikio na changamoto zinazokumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa.
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumbua sekta ili serikali ifanye maamuzi.

Kwa sasa kuna Kamati inayoangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi chini ya Wizara ya Viwanda , Bisahara na uwekezaji na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi Serikalini.

ZAIDI YA WATU 70 WAOKOLEWA LEO KUTOKANA NA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA KUBWA

0
0

Faustine Ruta, Bukoba

 ZAIDI ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuliko yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa nyakanyasi. 


Kinawilo alisema kuwa nyumba zote zilizoko kandokando ya mto kanoni zote zimeathiliwa na maji kiasi kwamba tumetumia mitumbwi ya uvuvi kuvusha watu.

“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuhalibika kwa kulowa maji”alisema kinawilo .Aidha mkuu wawilaya alisema kuwa kuwa wananchi wachukue tahadhali pindi mvua zinapo nyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama Zaidi. 


Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake hakuna kilichobakia kikiwa kizima kwani nimetoka mimi kama nilivyo na ninamshukuru mungu familia yangu haikuwepo. “Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana nihatali kwa binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofo wanahali gani hivyo kunatakiwa kuchua hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki”alisema Bonge .


Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake hakuna alie umia Zaidi ya vitu vyote vyandani hakuna kilichotoka.

“Yani nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli nihatali”alisema Mziba







Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Mkazi wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi leo kwenye mufda wa saa nne. Picha na habari na Faustine Ruta



Prince Motel


Crane Lodge and Tours



Hii ni nyumba ya Wageni...lakini inasemekana Usiku hawakupata usingizi kabisa!
Hivi ndivyo ilivyokuwa Asubuhi ya leo
Eneo la Ziwa Victoria...Ufukweni

Ufukweni Ziwa Victora

Patashika wakazi wakiokoa Nyasi kwa ajili ya Mifugo yao

Mkazi wa Nyakanyasi akivuka huku akiwa hana matumaini Aendako


Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi



Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii




MVUA YALETA MADHARA NA KUSABABISHA KAYA 20 KUKOSA MAKAZI

0
0

 Baadhi ya Nyumba katika eneo la Chalinze Mzee zikiwa zimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiangalia madhara yaliosababishwa na mafuriko katika jimbo hilo la Chalinze.
 wakazi wa chalinze wakiangalia nyumba zao zilizobomoka kutokana na mafuriko.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye kanzu) akiwa na wananchi wa jimbo hilo wakikagua `Bwawa la Umwangiliaji la Msoga 
 Sehemu ya bwawa la umwangiliaji la Msoga liloaribiwa na mafuriko na kupasua kingo za bwawa hilo.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu katika Ofisi za kijiji cha Msoga.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ametembelea eneo la Chalinze Mzee lilokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jimbo hilo na kusababisha madhara ya nyumba kubomoka na nyumba 9 kusombwa na maji na kusababisha zaidi ya kaya 20 kukosa pakulala.

Akizungumza Ridhiwani,ametaja  maeneo yaliyokumbwa na  mafuriko ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.

Aidha,amesema kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba,nyumba za wananchi kuharibika na kusabbishwa wananchi kukosa pa kulala,na ameongeza kuwa kwasasa wananchi hao wanahitaji msaada. 

Ridhiwani ametoa pole kwa wakazi hao na kuwaomba kuwa vumilivu katika kipindi hiki. 

TUMEKUSOGEZEA GOLI NA HIGHLIGHTS ZA MCHEZO WA MAJIMAJI VS AFRIKA LYION, MAJI MAJI 1 AFRIKA LYION 1

0
0
Timu ya Maji Maji imelazimishwa sale ya 1 – 1 na Afrika Lyion katika mchezo uliochezwa uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma, Goli la Afrika Lyion limepatikana kipindi cha pili dakika ya 61 baada ya shuti kali lililopigwa na Peter Mwalyanzi , huku goli la Maji Maji limepatikana dakika ya 74 na Kelvin Sabato .

VPL: KAGERA SUGAR, JKT RUVU WATOSHANA NGUVU KAITABA LEO. SARE YA 0-0.

0
0
Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kilichoanza kupambana na Timu ya Kagera Sugar.
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya JKT Ruvu leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya 0-0.

Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea tena leo hii jumamosi na katika Uwanja wa Kaitaba tukishuhudia Timu ya Kagera Sugar ikitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Timu ya JKT Ruvu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom msimu huu. Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kinachonolewa na Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar, Ashanti United na sasa JKT Ruvu King Kibadeni' kilionekana kukosa mbinu kuifunga Timu ya Kagera Sugar kipindi cha pili baada ya kuonekana kuwa na nguvu kwa kuingiza wachezaji waliokuwa na kasi kubwa. Kagera Sugar nao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kila mara lakini hawakuweza kupata bao lolote kwenye jitihada zao zote hizo za kipindi cha kwanza na cha pili. Hadi kipindi cha pili kinalizika dakika 90 hakuna timu iliyoweza kumfunga mwenzake.
Mchezaji wa JKT Ruvu Hassan Dirunga akiwa chini ya ulinzi wa Wachezaji wa Kagera Sugar.
Hassani tena akiwapa shida wachezaji wa Kagera Sugar
Rashid Mandawa mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar akijiandaa kuingia wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom. Picha/Habari na Faustine Ruta - Bukoba
Mchezaji chipukizi Mbaraka Yusuph (kushoto wa Kagera Sugar akiambaa na mpira huku beki wa JKT Ruvu akimkimbiza) kipindi cha pili.

Mbaraka Yusuph akilindwa na Wachezaji wa JKT Ruvu
Dakika 90 zilikamilika na Timu zote zilitoka bila kufungana, Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu.
Mchezaji hatari wa JKT Ruvu Hassan akiteta Jambo na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime dakika 90 zilipokamilika.

Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar/Ashanti United/ King Kibadeni(kushoto) akiteteta jambo na Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar mtanange ulipomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Timu ya JKT Ruvu.

AYT, TYVA NA MTANDAO WA ASASI ZA VIJANA WAJADILI MASUALA YA VIJANA NA BAJETI

0
0

Meneja Miradi wa Tamasha la Vijana, Churchill Shakim akiongoza mjadala wa kuichambua agenda ya vijana kuhusu bajeti kwenye nyanja mbalimbali ili serikali kuweza kufanikisha malengo hayo kwa vijana. (Picha zote na Geofrey Adroph)
  Mkurugenzi mtendaji wa Africa Youth Trust(AYT), Nahashon Gulali akizungumza na vijana waliokutana kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu bajeti hasa kwenye vipaumbele vya vijana kwenye bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma.

  Katibu Mtendaji wa TYVA na mratibu wa mtandao wa asasi za Vijana Tanzania, Ndugu Saddam Khalfan  akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa wakati wa kujadali na kufanyia uchambuzi bajeti hasa kwa kwenye mfuko wa vijana kwa mwaka 2017/18 uliofanyika katika ukumbi wa Wanyama jijini Dar es Salaam leo.
  Msimamizi wa Mradi kutoka AYT akiwasilisha kuhusu umuhimu wa vijana katika mpango wa bajeti ili kuweza kuinuka kiuchumi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu taasisi ya AYT pamoja namradi wa Youth Action for Development effectiveness(YADE)  kwa vijana waliokutana ili kujadili vipaumbele vya vijana kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 kwenye mkutano uliofanyika katika hoteli ya Wanyama jijini Dar leo.
Baadhi ya vijana wakichangia mada wakati wa kuichambua agenda ya vijana iliyoandaliwa kuhusu mikakati ya bajeti kwa vijana kwenye mkutano uliowakutanisha vijana kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu bajeti hasa kwenye vipaumbele vya vijana 
Baadhi ya magroup ya vijana wakijadiliana kuhusu changamoto pamoja nakuja suluhisho kwenye masuala ya msingi ya vijana hasa kuwezeshwa kiuchumi kupitia bajeti ya mwaka  2017/18.

Mkutano ukiendelea

Droo ya Milioni 10 ya nguvu ya buku kuchezeshwa Jumapili hii

0
0
MCHEZO wa bahati nasibu unaoendeshwa na Biko, unaotambulika kama Ijue nguvu ya Buku unatarajiwa kuchezesha droo yake ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, Jumapili hii.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (wapili kushoto), akimkabidhi Leseni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta kwa ajili ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta mara baada ya kupeana leseni ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini unaoitwa kama Nguvu ya Buku. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biko, Charles Mgeta, alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu Mgeta, alisema droo yao itakuwa ya kwanza tangu walipoanzisha mchezo huo wenye zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10000, 20000, 50,000, 200,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya Sh Milioni 10 ikipatikana kila mwisho wa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea leseni ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kushoto. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven.
Charles Mgeta akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya kampuni yao ya Biko kuendesha michezo ya kubahatisha, ambapo Jumapili hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuipa leseni kampuni ya Biko inayondesha mchezo wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven, kulia akizungumza na waandishi juu ya mchezo wao wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku, ambapo mwishoni mwa wiki hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.

“Leo pamoja na kutangaza juu ya kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 Jumapili, bali pia tumekabidhiwa rasmi cheti cha utendaji wa kazi zetu kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ambapo tunaamini safari yetu itakuwa ya mafanikio zaidi kwa Watanzania.

“Taratibu zetu ni rahisi kwa sababu washiriki wetu wanatakiwa kufanya miamala ya simu za MPESA, TIGO PESA na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni yetu ambayo ni 505050, huku pia akipaswa kuingiza namba ya kumbukumbuku ambayo ni 2456 ambapo kila ujumbe mmoja wa simu atatozwa kwa sh 1000, huku kiasi hicho cha pesa kikiwa na nafasi mbili ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kumuingiza kwenye droo ya wiki ya kujishindia Sh Milioni 10,” Alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe, aliwapongeza BIKO kwa kuingia katika mchezo huo kama sehemu ya kuwapatia maisha bora Watanzania kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.

“Naomba kuwatangazia Watanzania kwamba BIKO wamesajiliwa rasmi katika kuchezesha michezo hii na tunawaambia kwamba wapo salama hivyo kila Mtanzania apaswa kucheza ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi wa zawadi mbalimbali,” Alisema Mbalwe.

Biko wameanza kuchezesha mchezo huo wa bahati nasibu huku wakiwa wamejiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anajiwekea fursa ya kuibuka na ushindi wa zawadi mbalimbali kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha kutoka kwenye kampuni yao.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images