Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1194 | 1195 | (Page 1196) | 1197 | 1198 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amewataka wananchi Mkoani humo, kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, ili kuwabaini watu ambao si raiya wa Tanzania na wanalengo la kujipatia vitambulisho vya uraiya kinyume cha sheria za nchi.

  Taarifa ya kitengo cha habari na Mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imetanabaisha kuwa, Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga, wakati akizindua zoezi la uandikishaji vitabulisho vya uraiya kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa, zoezi ambalo linaratibiwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA.

  Bi. Masenza, amesema, kabla ya ugawaji vitambulisho hivyo, NIDA wataendesha zoezi la kubaini watu ambao si raiya na wanania ovu ya kujipatia vitambulisho, hivyo akawataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kuonesha uzalendo kwa kuwafichuo wale wote wasio na sifa za uraiya kwa usalama wa Taifa na watu wake.

  Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa vitambulisho vya Taifa NIDA Bw. Andrew Masawe, amesema mpaka sasa jumla ya Watanzania milioni 08 laki 04 na 99 elfu wametambuliwa na kukabidhiwa vitambulisho vya uraiya na kuongeza kuwa baada ya kukamilika kwa vitambulisho vya watumishi wa umma, zoezi hilo linaamia rasmi kwa wananchi na akawataka wananchi kuona umuhimu wa kutambuliwa kupitia vitambulisho hivyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimkabidhi kitambulisho chake mmoja kati ya wakazi wa mji wa Mafinga wakati wa uzinduzi huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akihutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga.
  Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo kwenye kiwanja cha Mashujaa Mjini Mafinga.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya  kilimo.

  Ametoa kauli leo (Jumatano, Aprili 5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Mheshimiwa Yahel Vilan, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu amesema Tanzania na Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri kwa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

  Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama watalii kwa sababu kuna fursa nyingi za utalii ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na mbuga nyingi zilizosheheni wanyama.

  Kwa upande wake, Balozi Vilan  ameipongeza Serikali kwa utendaji wake, ambapo amesema viongozi wa makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja nchini mwaka huu kushiriki katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya Tanzania na Israel.

  Amesema mbali na kushiriki katika jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo watapata fursa ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

  Pia Balozi Vilan amesema Serikali ya Israel itaimarisha kitendo cha wagongwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Israel nchini, Mheshimiwa Yahel Vilan, mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya, kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 5, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na balozi wa Israel nchini, Mheshimiwa Yahel Vilan, mwenye makazi yake jijini Nairobi Kenya, Ofisini kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma Aprili5, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  akifungua mkutano   wa wadau wa nishati ulioambatana na uzinduzi wa Jukwaa la Nishati  Tanzania (TEP) kwa niaba ya Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Samia Suluhu  jijini Dar es Salaam tarehe 05 Aprili, 2017. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania.
   Sehemu ya  wadau wa nishati wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)  katika mkutano huo.  
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa tatu kutoka kulia) na Balozi wa Uholanzi  Nchini, Jaap Frederiks ( wa pili kutoka kushoto) wakifurahia  uzinduzi wa Jukwaa la Nishati  Tanzania (TEP). Kushoto kabisa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Florens Luoga (katikati) wakifurahia jambo katika mkutano huo . Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo na kulia ni Balozi wa Uholanzi  Nchini, Jaap Frederiks
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi kutoka Chuo cha Twente  kilichopo nchini  Uholanzi, Profesa Tom Veldkamp (kulia) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo. Katikati ni Balozi wa Uholanzi  Nchini, Jaap Frederiks
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha  ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mkutano  huo.

  Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema nishati ya  uhakika ya umeme itatokomeza umasikini nchini  Tanzania ifikapo mwaka 2030.
  Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Jukwaa la Nishati  Tanzania (TEP) pamoja na  mkutano wa siku mbili  kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu mapema leo jijini  Dar es Salaam.
  Mkutano huo unaolenga kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania, unakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini kama vile Statoil,  BG na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
  Wadau wengine ni pamoja na  kampuni za kuzalisha umeme kama  vile Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Songas pamoja na  mabalozi wa nchi mbalimbali,  taasisi za kifedha na viongozi wa kiserikali.
  Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana itakayopelekea Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya  Taifa inavyofafanua.
  Profesa Muhongo alisema kuwa nishati ya kutosha itapelekea uanzishwaji wa viwanda vidogo hususan katika maeneo ya vijijini na kuzalisha ajira hivyo kupunguza wimbi la vijana kuhamia mijini kutafuta maisha.
  Akielezea mikakati ya upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeandaa mpango wa matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme ambapo gesi ni asilimia 40, maji asilimia 25, makaa ya mawe asilimia 30 na nishati mbadala asilimia 5
  Aliongeza kuwa serikali inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika sekta za nishati ili kuongeza uzalishaji wa umeme nchini.
  Akielezea  maendeleo ya mipango ya Serikali, Profesa Muhongo alisema  hadi sasa  Serikali imeshakamilisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini  Dar es Salaam na kuongeza kuwa  ugunduzi wa gesi ya kutosha katika mikoa ya Mtwara na Lindi umepelekea uanzishwaji wa viwanda vya saruji na mbolea katika mikoa hiyo.
  Alisema pia serikali ipo katika  hatua ya mwisho ya majadiliano kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta  ghafi kutoka  Hoima nchini  Uganda hadi Tanga, Tanzania na kusisitiza kuwa Serikali imeanza majadiliano kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka  jijini Dar es Salaam hadi Ndola, Zambia.
  Aliendelea kusema kuwa Serikali imekuwa ikikutana na wawekezaji kutoka  kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini kila baada ya miezi mitatu  ili kufahamu maendeleo na changamoto ya shughuli zake.
  Aliendelea kutaja mipango mingine kuwa, ni pamoja na uanzishwaji wa kozi mbalimbali katika masuala ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Waziri Muhongo alisema kuwa Serikali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wataalam wake kwa ajili ya kusomea masuala ya  gesi na mafuta katika ngazi ya shahada za uzamili na uzamivu katika vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi.
  Aidha, aliongeza kuwa  serikali kupitia balozi mbalimbali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi kusomea masuala ya gesi katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.
  “Lengo letu kama Serikali, ni kuhakikisha kuwa tunazalisha wataalam wa kutosha watakaofanya kazi katika kampuni za mafuta na gesi na hivyo kuinua uchumi wa nchi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
  Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM), Florens Luoga alisema kupitia Jukwaa la Nishati  Tanzania linaloundwa na wataalam kutoka  Tanzania na Uholanzi wanaangalia namna ya kushirikiana kupitia kubadilishana uzoefu kupitia program mbalimbali.
  Mkutano huo unaoambatana na maonesho ya  kampuni mbalimbali za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na kampuni za uzalishaji  wa umeme umeandaliwa na Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na  Taasisi ya  Teknolojia na  Sayansi ya Karume Nchini Zanzibar (KIST).

  0 0

  MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini. Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro. 

  Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza. Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)

   “Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili. Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia. Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi. Aliwatakia wageni wake chakula chema.. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es Salaam. 

   Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano. “ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua. Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi 'Application' ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville.'Meet and Greet' ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwimbaji mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Meza kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde alikuwa miongoni mwa wageni waaalikwa katika hafla hiyo.

  0 0  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Kwa  mujibu  wa  sheria  ya usajili  wa  ardhi  sura ya  334   ipo  aina   ya  mikataba  ya  pango  ambayo  baada  ya  kuwa  imeingiwa  kati  ya  mpangaji  na  mwenye  nyumba/eneo  ni  lazima  isajiliwe.

    Mikataba  ya  aina  hiyo  isiposajiliwa  inakuwa   haijakidhi  vigezo  vya  kisheria  na  hivyo  kubatilika.

  Aidha  pango  huhusisha  shughuli  mbalimbali.  Yapo  mapango  kwa  ajili  ya  biashara  maduka,  bar, mahoteli n.k.  na  pia  yapo  mapango  kwa  ajili  ya  makazi. Iwe  umepanga  kwa  ajili  ya  biashara  au  makazi  madhali  aina  yako  ya  upangaji  inahitaji  kusajiliwa  kisheria  basi  huna budi  kufanya  hivyo  ili  uhalali  wa  pango lako  upatikane.

  Kabla  ya  kuona  aina  ya  mikataba  ya  pango  ambayo ni  lazima  kusajiliwa  ni  vyema  kujikumbusha  kidogo  kuhusu  haki  za  mpangaji.

  1.HAKI   ZA  MPANGAJI.
  ( a ) Haki  ya  kutoingiliwa  na  mwenye  nyumba  ili  kumpa  uhuru mpangaji   kufurahia  pango  lake.
  ( b ) Haki  ya  kumpa  taarifa(notice)  mapema  mpangaji  ikiwa mwenye nyumba  anataka  kukagua  nyumba/eneo  lake.
  ( c ) Haki  ya  kutoondolewa  au  kusitishiwa  mkataba  mpaka  baada ya  kupewa  taarifa  maalum( notice) .
  ( d ) Haki  ya  kuambiwa  ukweli  kuhusu  hali  ya  nyumba kabla  ya  kusaini  mkataba  wa  pango. Mfano  kuambiwa  ikiwa  eneo  linajaa  maji  kipindi  cha  mvua, kuambiwa  ikiwa  nyumba  inavuja n.k.
  ( e ) Haki  ya  kukataa  sharti  lolote  ambalo  linalenga kuminya  uhuru   wa  mpangaji  au  linalovunja  sheria  yoyote  ya  Tanzania.
  ( f ) Haki  ya  kupewa  taarifa  mapema(notice)  kabla  ya  kupandisha  kodi  ya  pango.
  ( g )  Haki  ya  kupewa  taarifa  mapema(notice)   kabla  ya  kubadilisha  sharti  lolote  katika  mkataba  wa  pango.
           
     KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa wakiweka saini Nyaraka yenye maelezo ya masuala yote yaliyokubaliwa katika kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda. 
  Waziri Mahiga na Mgeni wake, Mhe. Sam Kutesa wakionesha nakala za nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa wakiweka saini Mkataba utakaotoa fursa kwa Tanzania na Uganda kushirikiana katika huduma za usafiri wa anga. 
  Prof. Mbarawa na Mhe. Kutesa wakionesha nakala za mikataba mara baada ya kuisaini. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Mhe. Mhandisi Irene Muloni wakiweka saini Mkataba ambapo Tanzania na Uganda zitashirikiana kuendeleza mradi wa umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo. 
  Waziri Mahiga na Mhandisi Muloni wakibadilishana nakala za mikataba. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye alikuwa mwongozaji wa kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kwa ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Uganda akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.
   
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba ya kufunga kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda. 
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa akisoma hotuba kwa wajumbe walioshiriki kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda 
  Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na wa pili ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa. 
  Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia hotuba za Waheshimiwa Mawaziri wa Mambo ya Nje 
  Viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali ya Uganda wakisikiliza hotuba za Mawaziri. 
  Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano 
  Bw. Gerald Mbwafu (kulia) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Maji, Bw. Sylvester Matemu kutoka Wizara ya Maaji. 
  Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakionesha nyuso za furaha kuashiria furaha yao baada ya kufanikisha mkutano wa JPC. 


  TANZANIA NA UGANDA ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA

  Tanzania na Uganda zimefungua sura mpya ya ushirikiano baada ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo kusaini nyaraka inayoainisha maeneo mbalimbali ambayo nchi hizo zimekubali kushirikiana kwa pamoja ili kuinua uchumi wa mataifa yao.

  Nyaraka hiyo iliyosainiwa leo jijini Arusha imetokana na Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda kilichofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 03 Aprili 2017. 

  "Makubaliano haya yataongeza chachu ya uhusiano na ushirikiano wetu na Uganda, japokuwa tulichelewa kufanya kikao cha JPC tokea mkataba uliposainiwa mwaka 2007 nchini Uganda". Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alisema alipokuwa akisoma hotuba ya kufunga.

  Kikao cha JPC kilifanyika kwa kuzingatia makundi ya kisekta ambapo katika kila kundi, wajumbe waliainisha maeneo yenye maslahi kwa pande zote ambayo yanajumuisha pamoja na mambo mengine: uendelezaji wa miundombinu; kilimo; viwanda; biashara; uwekezaji; nishati; utalii; utunzaji wa mazingira; uvuvi; ufugaji; afya; elimu; utangazaji; madini na masuala ya kijamii.

  Kikao hicho kilitarajiwa kuhitimishwa kwa kusainiwa mikataba sita lakini kutokana na mashauriano ya ndani ya baadhi ya mikataba kutokamilika, mikataba miwili ndio iliweza kusainiwa. Mikataba hiyo ni ushirikiano katika kuendeleza mradi wa Umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo na huduma za usafiri wa anga.

  Mikataba minne iliyosalia ambayo inahusu ushirikiano katika usafiri wa reli, usafiri wa majini; utangazaji na ulinzi wa raia itasainiwa wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika hivi karibuni hapa nchini. 

  Waziri Mahiga alieleza kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo ni muhimu kwa kuwa itaimarisha zaidi misingi ya mahusiano yetu, hivyo alizihimiza pande zote kukamilisha mashauriano hayo ili mikataba hiyo iweze kusainiwa katika muda uliopangwa.

  Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Uganda kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua uchumi kwa madhumuni ya kuwaondolea umasikini wananchi. 

  Alisema mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ni moja ya miradi itakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi, hivyo alisisitiza umuhimu wa kukamilisha taratibu zote zilizosalia ili ujenzi huo uweze kuanza.

  Alihitimisha hotuba yake kwa kuzipongeza Tanzania na Uganda kwa kufanikisha uwekaji saini wa mikataba miwili ukiwemo wa kuendeleza mradi wa Umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo ambao ulikuwa katika majadiliano kwa zaidi ya miaka minane. 

  Kikao hicho cha JPC kimefanyika kufuatia maelekezo ya Marais wa nchi hizo waliyoyatoa wakati wa ziara ya Rais wa Uganda nchini mwezi Februari 2017. Viongozi hao waliagiza kikao cha JPC kifanyike kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao ulipangwa kufanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 06 Aprili 2017.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar Es Salaam, 05 Aprili, 2017

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 6, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  walipofika na Ujumbe kutoka TLS kumtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  na  ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
   Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  akimuonesha kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akipokea  kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)kutoka kwa Rais wa chama hicho Mhe.Tundu Lissu wakati viongozi wa Chama hicho walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wakiongozwa na Rais wao Mhe.Tundu Lissu  walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS. 

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE.)

  0 0


  • ATOA SIKU 10 KWA YEYOTE ANAYEJIHUSISHA NA BIASHARA YA MOVIE, KUDOWNLOAD KAZI ZA WASANII KUACHA MARA MOJA

  • BAADA YA SIKU 10, OPARESHENI KUBWA KUANZISHWA JIJI ZIMA KUWABAINI WOTE WANAOFANYA BIASHARA HIYO.

  • AFISA BIASHARA KUFANYA TADHMINI YA MADUKA HALALI YA KAZI ZA WASANII WA FILAMU JIJINI NA KUWABAINI WOTE WANAOUZA KAZI FEKI ZA WASANII WAZAWA WA FILAMU.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepiga marufuku kuanzia leo tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji na usambazaji wa CD, flash, DVD na filamu za ngono katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Hali kadhalika Mhe. Makonda ametoa siku kumi kwa wote wanaojihusisha na biashara isiyo halali ya ku-download filamu na kazi za wasanii jijini waache mara moja kwani baada ya siku hizo, ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa bado wanajihusisha na biashara hiyo isiyonufaisha wasanii na Kuzorotesha pato la Taifa.

  Mhe. Makonda pia amemuagiza Afisa Biashara wa Mkoa kufanya tathmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu kihalali jiji Dar es Salaam.

  Mhe. Makonda ametoa maagizo hayo baada ya kutembelewa ofisini kwake na wawakilishi wa wasanii na wasambazaji, watengenezaji wa Filamu jijini Dar es Salaam, ambao walifikisha kilio chao cha kutonufaika na kazi zao za uzalishaji na usambazaji wa filamu nchini kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridhaa yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato!

  Wasanii hao wakiongozwa na Jacob Steven - JB, Vicent Kigosi - Ray walimuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati tatizo lao hilo kwa maslahi ya tasnia nzima ya sanaa nchini.
   Mkuu wa Mkoa Mh,Paul Makonda akijadiliana jambo na Kamanda Sirro
   Kikao kikendelea
  RC Makonda akiwa katika picha na Msanii wa Filamu aitwae Rado.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Viettel ya Vietnam inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano vijijini ambao umefanikisha kuweka miundombinu ya mtandao wa intaneti kwenye shule 417 hapa nchini. 

  Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015-2017, umewezesha pia ofisi za Halmashauri za Wilaya 123, Hospitali za Wilaya 74, Vituo vya Polisi vya Wilaya 131 na Ofisi za Posta 68 kufikiwa na mtandao huo. 

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2016/2017 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ukiwemo Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018 

  Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2016/2017, baadhi ya kazi zilizofanyika kwenye sekta ya mawasiliano ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Mradi wa Anuani za Makazi na Postikodi; na kuanzisha huduma ya kituo cha Jamii Centre kitakachorahisisha utoaji wa huduma muhimu katika kituo kimoja. Huduma hizo ni kulipa pensheni, ankara na huduma za kibenki. 

  “Sekta ya mawasiliano inatekeleza Programu ya Miundombinu ya Kikanda ambayo inahusisha Mradi wa Shule Mtandao (e-school), Mradi wa Video Conference ambao unahusisha ununuzi, usimikaji na ufungaji wa vifaa vya TEHAMA katika mikoa 26 na taasisi za Serikali,” amesema. 

  Amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa kituo cha kuhifadhi taarifa na mifumo ya Serikali (Government Data Centre) ambacho lengo lake ni kuimarisha usalama wa mifumo na taarifa unaoenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa taarifa za Serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. 

  Akizungumzia kuhusu ujenzi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema Serikali inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kujenga uchumi wa viwanda, na kwamba inatoa kipaumbele kwenye viwanda vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa nchini na nje ya nchi. 

  “Katika kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda, Serikali inahamasisha zaidi sekta binafsi ya hapa nchini pamoja na mashirika ya umma kujenga viwanda. Jitihada hizo zimewezesha mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF, PSPF na NHIF kuanza kufufua, kuendeleza na kujenga viwanda vipya vipatavyo 27 katika maeneo mbalimbali nchini,” amesisitiza. 

  Ameyataka mashirika ya umma yahakikishe kwamba mipango yao inaendana na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ambao dhima yake ni kujenga uchumi wa viwanda. 

  Akizungumzia kuhusu juhudi za Serikali kupambana na rushwa, Waziri Mkuu amesema Serikali inapambana na rushwa kwa nguvu zake zote na haina mzaha wala uvumilivu na vitendo vya rushwa. 

  “Hatua zilizochukuliwa kupambana na rushwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani Novemba, 2015 zimetambuliwa na mashirika ya Kimataifa yanayojishughulisha na tafiti kuhusu masuala ya rushwa duniani. Taarifa ya Shirika la Transparency International kwenye utafiti wake kuhusu mtazamo wa rushwa mwaka 2016, imeonesha kuwa viwango vya rushwa vinaendelea kupungua hapa nchini,” amesema. 

  Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali iliweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 9.75 kutokana na operesheni zilizofanywa na TAKUKURU, 

  “TAKUKURU imefanya uchunguzi wa majalada 306 ya tuhuma za rushwa na kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini kuendelea na mashtaka kwa majalada 104. Katika kipindi hicho, TAKUKURU iliendesha kesi 674 zikiwemo kesi mpya 182, ambapo katika kesi 97 watuhumiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo au kulipa faini. Kesi 407 zinaendelea kusikilizwa mahakamani,” amesema. 

  Amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaendelea na mapambano dhidi ya rushwa hususan katika eneo la ukusanyaji mapato ya Serikali, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, malipo hewa, matumizi mabaya ya fedha za ushirika na kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo. 

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali imefungua balozi mpya sita katika nchi za Algeria, Israel, Korea Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki. Amesema Balozi hizo zina kazi ya kuendeleza juhudi za kuitangaza Tanzania kama nchi yenye vivutio vingi vya utalii na rasilimali zinazoweza kutumika kuvuta uwekezaji kutoka mataifa hayo ikizingatiwa utulivu na amani iliyopo nchini. 

  IMETOLEWA NA: 
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  S. L. P. 980, 
  DODOMA, ALHAMISI, APRILI 4, 2017.


  0 0

  Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia, kikatiba na kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.

  Pia unawapongeza Wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki, tunawataka kuwa wazalendo, waadilifu, wachapakazi na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.

  Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato wa uchaguzi huo ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na shirikishi iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.

  Uteuzi uliofanywa na CHADEMA hata baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango wa Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.

  Bunge na Wabunge lazima wawe mstari wa mbele katika juhudi za kuimarisha demokrasia yetu kama Taifa na ndani ya vyama vya siasa, kamwe Bunge lisiruhusu kutumika kama “rubber stamp” kama ambavyo CHADEMA walipanga kwa kuteua wagombea wawili pekee na kwa kufanya hivyo tayari waliamua nani awe mbunge na kulinyima Bunge fursa na uhuru wa kuchagua miongoni
  mwa wagombea.

  Aidha, UWT imesikitishwa sana na kauli za MATUSI, DHARAU na KEJELI alizozitoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe dhidi ya Wabunge na Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kitendo cha Mhe. Mbowe kuwatukana Wabunge sio tu kinakiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi lakini pia kinatweza UTU na HESHIMA ya wabunge na bunge mbele ya jamii.

  UWT inaungana na Maamuzi ya Mhe. Spika ya Kuwaita watovu wa nidhamu kwenye Kamati ya Maadili.Hata hivyo tunamtaka Mhe. Freeman Mbowe kuomba radhi wabunge na Umma wa Tanzania kwa lugha isiyo na staha.

  Pamoja na kuomba radhi, tunamtaka Mhe Mbowe afute kauli yake ya kuwahusisha na kuwatuhumu Viongozi wa Serikali (Rais na Waziri Mkuu) na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa wameingilia uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ndani ya Bunge.

  UWT inaendelea kuwahimiza Wabunge kujadili na kupitisha Bajeti kwa kuzingatia vipaumbele muhimu kwa Maendeleo ya Jamii na Ukuaji wa Uchumi ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu ya Maji, Afya, Elimu, Umeme Vijijini, pamoja na kuimarisha njia za Uchukuzi na Mawasiliano k.v Barabara na Reli.  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
  AMINA MAKILAGI
  KATIBU MKUU
  UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA {UWT}
  05 April, 2017.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)


  0 0


   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akifuatilia taarifa ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wakati alipokagua barabara hiyo mkoani Manyara, leo, Kushoto ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza.
   Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuunganisha mikoa ya Dodoma na Manyara. Barabara hiyo inayojengwa na  Mkandarasi M/S China Railyway Seventh Group, imebaki KM 18 kukamilika.
   Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM88.8, Eng. Kini Kuyonza, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), tabaka la juu la kokoto kabla barabara hiyo kuwekwa lami, mkoani Manyara, leo.
   Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara Eng. Bashiru Rwesingisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8  inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Manyara na Dodoma ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Afrika Great North Road, inayoanzia Capetown (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri).
   Muonekano wa Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220, linaounganisha Wilaya ya Chemba na Kondoa katika barabara kuu ya Dodoma-Babati likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.
  Muonekano wa barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami upo katika hatua za mwisho kukamilika. Barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Manyara na Dodoma ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Afrika Great North Road, inayoanzia Capetown (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri).

   Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera (kushoto), akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), mara baada ya kumkaribisha kuanza ziara ya ukaguzi wa barabara katika Mkoa huo leo.


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye urefu wa kilometa 188.15 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

  Akizungumza mkoani Manyara mara baada ya kukagua barabara hiyo, Waziri Prof. Mbarawa amewataka Makandarasi M/S China Railyway Seventh Group anayejenga barabara ya Mela-Bonga KM88.8 na M/S China Henan International Cooperation Group anayejenga barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 kuzingatia viwango vya ubora katika ujenzi wao kama ilivyo kwenye mkataba, ili idumu kwa muda mrefu na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

  "Barabara hii ni kiungo muhimu kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa na nchi za Ukanda wa Afrika, hivyo naamini kukamilika kwake kutaibua fursa nyingi za uchumi na kuchochea maendeleo ya wananchi", amesema Profesa Mbarawa.

  Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa mkoa wa Manyara na Dodoma kutumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kujiendeleza kiuchumi na kuilinda ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwani ujenzi wake una gharama kubwa.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara, Eng. Bashiru Rwesingisa na Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma, Eng. Salome Kabunda wamemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa watawasimamia Makandarasi hao ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubora na kumalizika Oktoba mwaka huu kama ilivyopangwa.

  Barabara ya Dodoma - Babati (km 188.15) inayojengwa kwa kiwango cha lami ni kiungo muhimu kwa uchumi wa Tanzania, kwani inaunganisha nchi za bara la Afrika kutokea Capetown (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri).


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


  Muhadhiri wa chuo kikuu cha Afya na Tiba Muhimbili,Profesa Projestine Muganyizi akifafanua jambo mbele ya wadau na watafiti mbalimbali wa Afya,alipokuwa akitoa mrejesho wa utafiti walioufanya mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto,jijini Dar.

  Prof.Muganyizi alisema kuwa walikwenda Mkoani Njombe na kukutana na Wafanyakazi na viongozi wa Afya mkoani humo,mwaka jana mwezi wa sita na kufanya utafiti katika suala zima la Afya ya Mama na Mtoto.

  Katika utafiti huo,anaema walibaini mambo makuu manne,kwanza 
  ilikuwa suala la usafi katika hospitali zenyewe,kwa mazinginra ya nje vituo vingi vilikuwa vikionekana ni visafi,lakini kwa ndani ilibainika kuwa na mapungufu makubwa hasa katika eneo la usafi,Pili ni Katika uelewa wa kutoa huduma ya Afya,huduma za Mama na Mtoto zilikuwa na Mapungufu,wafanyakazi wengi walikuwa hawana weredi wa kutosha,

  Anasema na kuongeza kuwa eneo la tatu ni katika suala la ufautiliaji wa hali ya Mama akiwa Mja mzito,vituo vingi havikuwa na uelewa wa kutumia hizo kadi ,akina Mama wengi walikuwa hawafuatiliwa kwa ukaribu wakiwa na uchungu, Mwisho ni suala la kuweka Kumbukumbu za Mama akiwa kwenye uchungu,ikabainika vituo vingi hazitumii zile kumbu kumbu na jambo lingine ni suala la Huduma inayotolewa kwa Mama Mzazi,Je meridhika vipi huduma aliyopewa kutoka kwa wale wahudumu wa afya,Iakabainika kuwa akina Mama wengi walikiri wazi kuwa walihudumiwa vizuri.

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto (UNICEF) lilipokea mrejesho huo,na kwa kuwa Shirika hilo lilikuwa likisaidia kuendeleza huduma ya Afya ya Mama na Mtoto,tayari limeanza kuzifanyia kazi changamoto zote zilizo ainishwa kwenye utafiti huo,ikiwemo na kuwaelemisha wahusika wote katika suala zima la Afya la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.
  Baadhi ya wadau na Watafiti wa Afya wakifuatilia mrejesho wa utafiti uliofanywa mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto.

  Mmoja wa Wakilishi kutoka UNICEF,akichangia mrejesho wa utafiti huo uliofanywa mkoani Njombe Mwaka jana, UNICEF wamekuwa wakishiriki kwa kiasi kikubwa katika kusaidia kuendeleza huduma ya Afya ya Mama na Mtoto mkoani Njombe.
  Mhadhiri wa chuo kikuu cha Afya na Tiba Muhimbili,Profesa Projestine Muganyizi akichangia jambo mbele ya wadau na watafiti mbalimbali wa Afya,mara baada ya kutoa mrejesho wa utafiti walioufanya mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto,jijini Dar.
  Mkurugenzi wa kuratibu na kutunza utafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR),Dkt Julius Massanja akitoa ufafanuzi wakati wa kusikiliza Mresho wa Utafiti uliofanyika Mkoani Njombe uliohusu Afya ya Mama na Mtoto.Dkt Massanja alisema kuwa katika utafiti huo .kazi ya mwanzo ilikuwa ni kujua na kubaini tatizo gani,hivyo Kufuatia mrejesho wa utafiti huo wa Afya ya Mama na Mtoto uliofanywa Mkoani Njombe,Shirika la UNICEF limeanza kurekebisha mambo mbalimbali yaliyobainishwa katika tafiti hiyo ikiwemo na kuwaelemisha wahusika wote katika suala zima la Afya la kupunguza vifo vya mama na Mtoto. 

  0 0

   Daktari Bingwa aliyebobea katika Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar akifanya upasuaji wa kutumia njia ya matudu madogo kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. 
   Baadhi ya madaktari kutoka katika Hospitali za umma na binafsi nchini wakifuatilia mubashara upasuaji wa njia ya matundu madogo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imendelea kuwajengea uwezo madaktari wa ndani na nje ya hospitali kwa kufanya upasuaji wa njia ya matundu madogo (laparoscopic surgery).

  Miongoni mwa madaktari walioshiriki kwenye upasuaji huo ni kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.

  Lengo ni kuwaongezea ujuzi madaktari hao ili waendelee kufanya upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo kwa wagonjwa mbalimbali.
  Upasuaji huo unafanywa na madaktari wa muhimbili kwa kushirikiana na Daktari Bingwa aliyebobea katika magonjwa ya kinamama na uzazi, Profesa Rafique Parkar ambaye amekuwa akifanya upasuaji huo nchini Afrika Kusini, Kenya na nchi mbalimbali barani Afrika.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama na Uzazi, Vicenti Tarimo wa hospitali ya Muhimbili amesema wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji na kwamba wengine watatu walikuwa wakiendelea kufanyiwa upasuaji huo leo.
  “Leo wagonjwa wenye matatizo ya uzazi na wenye uvimbe wamefanyiwa upasuaji kwa kutumia njia hii. Kesho wagonjwa wengine watano watafanyiwa upasuaji kwa kutumia njia hii,” amesema Dk Tarimo.

  Dk. Tarimo amesema lengo ni kuwawezesha madaktari wa hapa nchini kutumia njia matundu madogo kufanya upasuaji badala ya kutumia njia ya kufungua tumbo ambayo mgonjwa anatumia muda mrefu kupona.

  “Upasuaji wa njia ya matundu madogo una faida kubwa, kwanza mgonjwa anapona haraka tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo. Wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa njia hii ya kisasa wanaweza kuendelea na kazi kwani baada ya muda mfupi wanapona,” amesema Dk Tarimo.

  Hospitali ya Muhimbili imekuwa ikifanya upasuajia wa njia ya matundu madogo na sasa inaongeza uwezo kwa madaktari mbalimbali nchini wakiwamo madaktari wa Muhimbili.

  0 0  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
  Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo


  Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi


  Na Nasri Bakari, Dar es salaam

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi Msakuzi.

  Makabidhiano ya madarasa hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili (62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi Manispaa ya Ubungo.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.

  "Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.

  MD Kayombo amesema kuwa mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa alivyokabidhiwa.

  Pia ameahidi kuweka tarazo katika vyumba viwili vya madarasa ya zamani ambapo pia ameahidi kutoa mifuko Hamsini ya Saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya walimu na kuahidi kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano.

  "Fedha hizi za kununua mifuko ya Saruji nitatoa kwenye mshahara wangu hivyo namsihi Mheahimiwa Diwani wa eneo hili naye aweze kuchangia ujenzi huu" Alisema MD Kayombo

  "Tunakushukuru sana Mkurugenzi kwa jitihada ulizozionesha katika shule hii kwa kipindi kifupi kwa kutununulia eneo la shillingi Millioni 35 na kutujengea madarasa matatu mungu akubariki sana" Alisema Bi Shahiri.

  Mkurugenzi Kayombo amewasihi walimu wa shule hiyo kujitahidi kutunza mali za serikali zikiwemo madarasa, madawati na samani nyingine.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri mara alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Pemba kuzungumza na Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba leo, akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Pemba akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
    Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri mara alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kuzungumza na Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba  leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
    Baadhi ya  Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Pemba na Afisa Tawala wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na  Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
   Baadhi ya Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo(Picha na Ikulu).

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizukumza na Makatibu Wakuu wa Ofisi yake nje  ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa mkutano wa 11 Aprili 6, 2017 wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi, katikati Dkt.Hamisi Mwinyimvua (Sera na Uratibu) na Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu).
  hag2
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipitia taarifa ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa Uwasilishwaji wake katika mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti kulia ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
  hag3
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akipongezana na baadhi ya wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge wakati wa Bunge la Bajeti  kushoto kwake  ni Naibu wake  Mhe. Antony Mavunde (Kazi, Ajira na Vijana) na wa kwanza kulia ni Mhe. John Heche (Tarime).
  hag4
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa na baadhi ya wabunge nje ya Viwanja vya Bunge Dodoma Aprili 6, 2017.

  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0


  Baada ya safari ndefu, hatimaye kikosi cha Serengeti Boys kimetua salama nchini Morocco.
   
  Serengeti imetua Morocco tayari kuweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika nchini Gabon.
   
  Mwenyekiti wa Soka la Vijana wa TFF, Ayubu Nyenzi amesema wamefika salama Casablanca lakini wanalazimika kusafiri kilomita 100 zaidi.
   
  “Tunatoka Casablanca kwenda Rabat, hivyo safari inaendelea safari hii kwa gari,” alisema.
  Kikosi hicho kiliondoka jana Alasiri kwenda Morocco kupitia Dubai, safari ambayo imechukua zaidi ya saa 24 kukamilika.

older | 1 | .... | 1194 | 1195 | (Page 1196) | 1197 | 1198 | .... | 1897 | newer