Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Akabidhi Vifaa Kwa Kituo Cha Afya Bogowa Wilaya ya Mkoani Kijiji cha Mganyageni Pemba.

$
0
0

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia presha wazazi katika kituo hicho kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi pempasi kwa ajili ya watoto wanaozaliwa katika kituo hicho akipkea Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, akitowa shukrani kwa msaada huo kwa kituo hicho. kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Viongozi wa meza kuu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya katika kituo cha afya bogowa mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wac Wilaya ya Mkoani Mhe Hemed Suleiman alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kwa ajili ya kukabidhi Vifaa kwa ajili ya Chuma cha Wazazi katikac Kituo hicho cha Afya katika Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kukabidhi vifaa vya afya katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka, akitowa maelezo wakati wakitembelea Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka akitowa maelezo wakati wa ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar kutembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa vya Afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Siad Suleiman wakati wa hafla hiyo, wakiwa katika viwanja vya Kituo hicho Bogowa Mkanyageni Pemba.
Mfanyakazi wa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Mwanahawa Mohammed Abdallah akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi na wananchi wa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr Mbwana Shoka akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya chumba cha wazazi kwa Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba. 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pembe Mhe. Omar Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. wakati wa kukabidgi vifaa vya Afya kwa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Wilaya ya Mkoani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis wakati wa hafla hiyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakifuatilia hafla hio ya kukabidhi vifaa vya afya kwa ajili ya chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman akizungumza kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni wakati wa kukabidhi Vifaa vya Afya kwa ajili ya Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Afya katika Kituo cha Bogowa Mkanyageni kwa ajili ya Wazazi wanaofika katika Kituo hicho kuja kujifungua.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na wananchi hao na kutowa nasaha zake kabla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa chumba cha wazazi katika kituo cha Afya Bogowa Mkanygeni Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashuka kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia Sukari katika Kituo hicho kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Imetayarishwa na Othman Maulid 

Zanzinews.Blog .com

KAMISHNA MSTAAFU WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA (TIRA)BW. ISRAEL KAMUZORA

$
0
0

Kamishina Mstaafu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizungumza katika hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana jioni mara baada ya kustaafu utumuishi wa Umma, Hafla hiyo iliandaliwa na mashirika mbalibali ya bima hapa nchini ambayo iikuwa na lengo la kumuaga Kamishna Mstaafu huyo na Kumkaribisha Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Bw.George Sakware.
Kamishina Mstaafu wa Bima Bw. Israel Kamuzora aksisitiza jambo wakati akizungumza katika hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana jioni mara baada ya kustaafu utumuishi wa Umma kushoto anayemsikiliza ni Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Bw.George Sakware.
Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware akizungumza katika hafla hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa Bw. Sam Kamanga na kulia ni Kamishna Mstaafu Bw. Israel Kamuzora.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Bw. Sam Kamanga akizungumza katika hafla hiyo huku Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware katikati akimsikiliza kushoto ni Kamishna Mstaafu Bw. Israel Kamuzora.
Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware kushoto akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati akizungumza naye jambo.
Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati wa hafla ya kumuaga Kamishna Mstaafu Bw. Israel Kamuzora.
Kamishina Mstaafu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Serena katikati ni Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la MGen Insurance Bw. Charles Sumbwe akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa neno la shukurani kwa Kamishna Mstaafu Bw. Israel Kamuzora.
Mmoja wa wakuu wa mashirika ya bima akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa shukurani zake.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la MGen Insurance Bw. Charles Sumbwe katikatin akiwa pamoja na baadhi ya wakuu wa mashirika ya bima katika hafla hiyo.
Baadhi ya wakuu wa mashirika ya bima wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la MGen Insurance Bw. Charles Sumbwe akijitambulisha katika hafla hiyo.
Mmoja wa wakuu wa mashirika hayo akijitambulisha.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOWAANDALIA CHAKULA CHA JIONI VIJANA WA SERENGETI BOYS NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY-DSM.

MISA-TAN YAWANOA WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI JUU YA SHERIA MPYA YA HUDUMA ZA HABARI.

$
0
0
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Ltd,Jesse Kwayu akiwaongoza washiriki wa warsha inayotolewa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) juu ya changamoto zilizopo katika sheria mpya ya Huduma za Habari.
Baadhi ya Wanahabari kutoka mikoa ya Tanga,Arusha ,Manyara na Kilimanjaro wakishiriki katika warsha hiyo inayofanyika katika Hoteli ya Impala jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Luninga cha ITV mkoa wa Manyara,Charles Masanyika akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoa wa Manyara ,Joseph Lyimo akichangia jambo katika warha hiyo.
Wakili Msomi na Mwanahabari mwandamizi James Marenga akiwapitisha washiriki wa warsha hiyo katika vifungu mbalimbali vya sheria ya Huduma ya Habari.
Baadhi ya Washiriki.
Afisa Habari na Utafiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) Sengiyumva Gasirigwa
Baadhi ya wanahabari wanaoshiriki warsha hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI NA KAMISHNA WA TRA IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisiani hati ya kiapo cha Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Profesa Kitila Alexander Mkumb0 kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ave Maria Semakafu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Dkt. Ave Maria Semakafu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Ave Maria Semakafu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisiani hati ya kiapo cha Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Sylvester Ambokile Mwakinyuke kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisiani hati ya kiapo cha Bw. Sylvester Ambokile Mwakinyuke kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Bw. Sylvester Ambokile Mwakinyuke kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Baraka Luvanda kuwa Balozi wa Tanzania nchini India Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017 -Rais akimkabidhi nyezo za kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Bw. Baraka Luvanda kuwa Balozi wa Tanzania nchini India Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017 -Rais akimkabidhi nyezo za kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Waapishwa wakila kiapo cha maadili ya viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na waapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017. PICHA NA IKULU.

HALMASHAURI YA HANDENI YAZIPONGEZA SHULE KUMI ZA MSINGI NA SEKONDARI KWA KUFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE 2016

$
0
0
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akikabidhi zawadi kwa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tewe iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na ya sita kimkoa
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wakisomewa namba na wanafunzi wa shule ya awali kabuku nje
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wakisikiliza mwanafunzi alipokuwa akielezea tense za somo la kiingereza
 wanafunzi wa shule ya sekondari kabuku akielezea mifumo ya kibaiolojia Kwa viongozi
 Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza wakati wa Hafla hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe wakatikati na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wa mwisho kulia na kaimu afisa Elimu Msingi Bw Fikeni senzige wakikagua gwaride la wanafunzi wa kabuku.
Mwalimu na wanafunzi wkisherehesha Hafla hiyo.


Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na    moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa  la saba na kidato cha nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku nje.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni   ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

“elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni  watoto kutumia fursa ya Elimu bure inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.

Aidha ameeleza kuwa atahakikisha fedha zinazohusu madai ya walimu  zinapofika  Halmashauri zinawafikia walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.

Wakati huohuo amepiga marufuku watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuacha kuchunga mifugo hasa kwa siku za shule baada ya kubainika watoto wengi wa jamii ya wafugaji wanatumiwa kuchunga mifugo badala ya kwenda shule. 

Amewaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao wanakwamisha watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume. Amewaeleza pia wazazi ambao wanawatoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe ,amesema kuwa  kukosekana kwa chakula cha kutosha shuleni,utoro uliokithiri kwa baadhi ya wanafunzi,kutokuwajibika kwa baadhi ya walimu na wazazi pamoja na upungufu wa walimu kunasababisha kwa kiwango kikubwa kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.

Ameagiza shule ambazo mpaka sasa ambazo hazina chakula kuhakikisha wanawapa wanafunzi  chakula. Aliwataka pia kusimamia mazao ya mihogo waliyopanda ili mazao hayo yaweze kusaidia upatikanaji wa chakula shuleni  na kuongeza kiwango cha uelewa kwa wanafunzi.

Ametoa mwezi mmoja hadi kufikia 4/5/2016 kwa Maafisa watendaji Kata, Vijiji, walimu wakuu, wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kuhakikisha kuwa watoto wanapata chakula cha mchana shuleni.

Shule za Msingi zilizopata zawadi na pongezi ni Tewe iliyokuwa ya sita kimkoa na kuzawadiwa Tsh. 200,000/=., Chang’ombe Tsh. 150,000/=, Mkumba Tsh 100,000/=, Mzundu Tsh. 82,000/=, Kwaragulu , Mbwewe, Kwamdani, Kwedikwazu Magharibi, Kwedikwazu Mashariki na chogo ambazo zote zilipata Tsh 78,000/=. Mazingara sekondari imepata zawadi Tsh.100000/=.

Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni.

SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA MAJI CHALINZE

$
0
0
Serikali kwa kushirikiana na  Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirka wa Maendeleo (DPS), na Serikali ya India  kwa pamoja wametoa jumla ya Shillingi Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Chalinze kwa awamu tatu.

Akijibu Swali Mbunge wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete lililouliza kuwa Wakazi wa Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze?

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge ameeleza kuwa Serikali ipo katika utekelezaji wa mradi huo na gharama za utekelzaji wake ni Shillingi Billioni 23.4 kwa awamu ya kwanza na Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili ya mradi na kwa awamu ya tatu itagharimu Shillingi Billioni 86.9.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji umekamilika na kwa awamu ya pili ya mradi huo jumla ya vijiji 88 vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi wote waishio katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.

“Mradi upo katika hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ipo katika utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya maji” alisisitiza Mhe. Lwenge.

Pia ameleza kuwa katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi, Lulenge, tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa majaribio ya bomba kuu.

Vijiji vitatu vya Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata maji mara baada ya mkandarasi kufanya maboresho ya pampu ambazo zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa  na mkandarasi huyo ameagizwa kuhakikisha pampu  hizo zinafanya kazi kabla ya Juni 2017.

Aidha kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huu kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115), Ujenzi wa mfumo wa manomba ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki makubwa 19 na ujenzi wa vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya kuchotea maji vinatekelzwa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

CHEKELENI NI MLEMAVU WA MIKONO, ANANDOTO ZA KUWA NESI,SAIDIA KUTIMIZA NDOTO YAKE

$
0
0

BIASHARA YA NDIZI KATIKATI YA JIJI

$
0
0
 Mmoja wa Wachuuzi wa ndizi akiuza ndiz kwa mteja wake kama alivyokutwa na kamera yetu ya Mtaa kwa Mtaa katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam
Dereva wa Guta akiwa na Msaidizi wake wakisukuma Guta lilisheheni ndizi kama walivyokutwa kandokando mwa barabara ya Morogoro

KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 1

$
0
0

Tanga, KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.

Akizungumza mara baada ya Wahariri (Jukwaa la Wahariri TEF) kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema moja ya faida huipeleka kwa wananchi.

Alisema wamekuwa wakisaidia madawati, mifuko ya saruji na majengo pamoja na vyoo kwa shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada. Akikabidhi shilingi milioni 14 kwa Jukwaa hilo, Swart alisema pesa hizo zinaweza kuwasaidia katika majukumu yao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao utafanyika kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudas Balile, alisema amefurahishwa na uzalishaji wa Saruji pamoja na mipango kabambe kiwandani hapo.

Akizungumzia msaada huo, Balile alisema utasaidia katika masuala mbalimbali ya Jukwaa hilo ikiwa na pamoja na mkutano mkuu wa Moshi kesho na kutoa shukurani na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano kama huo.


Makamo Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri wa Habari (TEF), Deudatus Balile (kulia) , akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Saruji cha Tanga Simba Cement, Renhardt Swart, kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.




Afisa Mawasiliano na Masoko kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga , Hellen Maleko, (kulia) akiwakabidhi hundi yenye mfano wa shilingi milioni 14 Wahariri wa Jukwaa la vyombo vya habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo ikiwa ni msaada katika mambo yao mbalimbali ukiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.





Wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiangalia eneo uchumbani wa Matirial Kware kilometa 2 kutoka ndani ya eneo la kiwanda.
Eneo la Kware ambalo kiwanda hicho toka kianze uzalishaji wame wamekuwa wakichimba Matirialhadi hii leo ambapo Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema amewaambia Wahariri hao kuwa kuna kiwango kikifika watasimamisha uchimbaji na kuanzisha mradi wa Ufugaji Mamba.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali ya Habari wakipiga picha eneo la Kware ndani ya Kiwanda cha Saruji Simba Cement inapochimba Matirial ya kiwanda hicho.blog ya kijamii ya tangakumekuchablo 0655 902929

WAZIRI MUHONGO AZINDUA JUKWA LA NISHATI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini , Prof Sospiter Muhongo akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa Nishati nchini
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa .Sospiter Muhongo  akifungua kitamba kuashiria uzinduzi wa Jukwaa la Mazingira.
 Washiriki wa ufunguzi wa jukwaa hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini
 Baadhi ya mabalozi wakifuatilia hotuba ya waziri Muhongo.
 Mtaalam wa Madini , Ariph Kimari  akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau  waliofika katika maonesho yaliyopo katika mkutano huo
 Meneja Majanga  wa TPDC , Amour Marine akitoa maelekezo kwa watu waliofika kutembelea banda hilo.
Dk Isack  Legonda  kutoka cho kikuu cha Dar es Salaam akitoa maelezo kwa wadau walifika katika banda hilo

MWILI WA PROFESA BINAGI WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA MKOANI MARA.

$
0
0
Ndugu, jamaa na marafiki hii leo jumatano April 05,2017 wameuaga mwili wa marehemu Profesa Lloyd Manamba Binagi aliyefariki ghafla juzi jumatatu April 03,2017 Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Mwili huo utapokelewa kesho asubuhi katika uwanja wa ndege Jijini Mwanza, na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Bomani wilayani Tarime.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika malalo ya Binagi yaliyopo Kenyamanyori wilayani Tarime siku ya jumapili, April 09,2017 baada ya familia ya marehemu kuwa imewasili kutoka nchini Marekani.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!
Picha na Msubi BMG Soma zaidi hapa

Wabunge, wasomi waja juu Chadema kutoenzi demokrasia uchaguzi EALA

$
0
0
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wasomi mbalimbali nchini wameeleza kushangazwa na chama cha upinzani nchini, Chadema, kushindwa kuenzi demokrasia na misingi ya haki kufuatia chama hicho kuwasilisha majina ya wagombea wawili tu katika nafasi zao mbili za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Dodoma na wabunge hao na wasomi wengine mbalimbali wakati wa Mahojiano Maalum na Mwandishi wa habari hizi kuhusu uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika jana Mjini Dodoma.

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi huo Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Mollel alisema Bunge la Tanzania kama yalivyo Mabunge mengine duniani yameendelea kuzingatia suala la usawa wa kijinsia, na hivyo hatua ya Wabunge wa CHADEMA waliokuwa wawili tu katika nafasi mbili kukataliwa ilikuwa ni sawa.

Katika majina ya Chadema, hakukuwa na uwakilishi wa kijisia wala pande mbili za Muungano, ambapo badala yake, wagombea wote wa chama hicho walikuwa wa jinsia moja na kutoka mkoa na wilaya moja.

Mbunge Mollel ameongeza kitendo kilichofanywa na CHADEMA ni kukiuka kanuni za Bunge hilo na la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo yote kwa pamoja yamesisitiza suala la usawa wa kijinsia katika nafasi za uteuzi wa Chombo hicho cha kutunga Sheria.

“Serikali ya awamu ya nne ilijitahidi sana katika kusimamia suala la usawa wa kijinsia kwa kuwa hata katika maazimio ya Mkutano wa Wanawake uliofanyika Jijini Beijing China mwaka 1995 ulizitaka nchi zote ulimwenguni kuheshimu haki na usawa wa wanawake” alisema Mhe. Mollel.

Aliongeza kuwa pamoja na idadi kubwa ya wagombea waliofikia 400, CCM ilipata majina ya wagombea 12 kuwania nafasi sita hatua iliyodhirisha kuwa Chama hicho kimekomaa kisiasa tofauti na vyama vingine vya upinzani vilivyopo nchini.

Naye Mbunge waSingida Mjini (CCM) Musa Sima aliwapongeza Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki  na kusifu ukomavu wa kisiasa ulionyeshwa na Wabunge wa Bunge la Tanzania wakati wa mchakato wa uteuzi wa Wabunge.

Mmoja wa wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za nyuma wa Chadema Bi Esther Wassira amekaririwa na mitandao ya kijamii akilaumu mfumo wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kutozingatia misingi ya demokrasia.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeomba jina lake lisiwekwe hadharani akiwa na ngazi ya cheo cha Profesa ametabiri kuzidi kutokea kwa hatima ya Chadema katika siasa za kitaifa.

“Ni chama ambacho kinadidimia. Kila siku ukitazama misingi ya kuanzishwa kwake, sera zilizowafanya kuwepo walipo na sababu za kufika walipo zote wameanza kuzisigina,” alisema msomi huyo aliyebobea katika sayansi za siasa.

Benki ya EXIM yapata faida ya bilioni 83.6

$
0
0
 BENKI ya Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida itokanayo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.

Mapato yatakanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa na ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.

Aidha katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za kibenki yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

Faida hiyo imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki kuweza kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.

Katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa kasi, Benki ya Exim ametelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia. “Nina furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7 imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki itaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.

Utekelezaji wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa yake ya fedha jumla ya gharama ya uendeshaji ilipanda  kwa asilimia 24 hadi kufikia Tsh bilioni 99.

Benki ya Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na kuongezeka kwa mtaji.

Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda, Bw. Ponda alisema kuwa Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma bora. 

Na benki tanzu mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu baada ya kuteleza mikakati mipya baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.  
Chief Financial Officer of Exim Bank Tanzania, Mr Selemani Ponda as he shares with journalists that Exim Bank Group has achieved a pre-tax profit of TZS 83.6 Billion for the year 2016. The Group recorded a 25% growth in net interest income, fueled by asset book growth, better yields and reduction in cost of funds. Seated beside him are Senior Finance Manager, Joseph Mrawa [Left] and Deputy Finance Officer, Issa Hamisi [Right].

RAIS MAGUFULI AAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI NA KAMISHNA WA TRA


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA MAWAKALA WA PEMBEJEO ZA KILIMO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mawakala wa pembejeo za kilimo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na wapili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvu Tete Ole-Nasha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkuu wa Mkoa wa Arusha afanya mkutano watendaji wa Kata na Mitaa

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na watendaji wa Kata na Mitaa(hawapo pichani) wakati wa Kikao kazi cha Ukusanyaji wa Kodi ya Majengo.
  Wajumbe wa Kikao wakifuatilia kikao kazi walichofanya na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mtendaji wa Mtaa wa Panga, Kata ya Kati Bi. Maria M. Singo(Aliyesimama) akichangia hoja kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuhamasisha ukusanyaji wa Kodi ya Mapato.

Dkt. Kalemani amtaka Mkandarasi REA kuajiri wazalendo

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Negezi, Wilaya ya Kishapu (hawako pichani), wakati wa uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga. Uzinduzi huo ulifanyika hivi karibuni.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia), akifunua kitambaa kilichofunika Jiwe la Msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Mbunge wa Kishapu, Seleman Nchambi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akiwatunza na kujumuika kucheza ngoma pamoja na moja ya vikundi vya burudani kutoka Shinyanga, kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.

Na Veronica Simba – Shinyanga
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amemtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya M/s OK Electronics and Electric Limited, atakayetekeleza kazi ya kusambaza umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Shinyanga, kuhakikisha anaajiri wananchi wenye sifa kutoka maeneo hayo badala ya kuleta wafanyakazi kutoka mbali.
Alitoa maagizo hayo hivi karibuni katika Kijiji cha Negezi, wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa huo.
“Tumia wataalam/vibarua vijana kutoka maeneo haya. Hatutapenda uajiri watu kutoka mbali wakati wafanyakazi wenye sifa wako hapahapa,” alisema Naibu Waziri.
Aidha, Dkt. Kalemani, alimwagiza Mkandarasi huyo kuhakikisha anawalipa vibarua mara moja kila wanapokamilisha kazi husika. “Hakuna kulaza malipo kwa sababu sisi tunakulipa vizuri.”
Sambamba na maagizo hayo, Dkt Kalemani, aliutaka uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo, kujipanga na kumsimamia Mkandarasi husika ili kuhakikisha anafanya kazi masaa 24 kwa siku.
Alisisitiza kuwa, Ofisa yeyote atakayelegalega kumsimamia Mkandarasi husika kadri inavyotakiwa. Atawajibishwa kwa kuondolewa katika nafasi yake.
Naibu Waziri pia, aliwaelekeza TANESCO kuhakikisha wanawafuata wateja na kuwapatia huduma mahala walipo badala ya kusubiri wateja wawafuate katika Ofisi zao, ambazo ni chache na ziko mbali na makazi ya wananchi wengi hususan walioko vijijini.
Kufuatia maelekezo hayo; aliuomba uongozi wa Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Shinyanga, kuanzisha vituo maalum ambavyo vitatumiwa na Maofisa wa TANESCO kuwahudumia wateja walioko katika maeneo yao.
“Hatuwezi kusubiri kujenga Ofisi, shughuli ambayo itachukua muda mrefu, wakati wananchi wanahitaji umeme,” alisisitiza.
Kuhusu suala la wakandarasi binafsi, ambao hufanya kazi ya kutandaza nyaya za umeme katika nyumba za wananchi mbalimbali na kuwatoza kiasi kikubwa cha fedha; Naibu Waziri alitaka tabia hiyo ikome mara moja.
Alitoa maelekezo kuwa ni marufuku kwa Mkandarasi binafsi, kufunga nyaya kwenye nyumba ya mteja yeyote bila kwanza kupata idhini kutoka TANESCO.
Naibu Waziri, aliagiza majina ya wakandarasi binafsi ambao wataidhinishwa na TANESCO kufanya kazi ya kufunga nyaya za umeme kwa wateja, yabandikwe katika Ofisi husika ili wananchi waweze kuwatambua na pia iwe rahisi kuratibu gharama za kazi hiyo, hivyo kuwaepusha wananchi na utapeli kwa kulipishwa gharama kubwa isivyostahili.
Aidha, aliwashauri viongozi wa Halmashauri na Serikali za Vijiji, kutenga hela katika bajeti zao, kwa ajili ya kuunganisha umeme kwenye Taasisi mbalimbali muhimu zikiwemo Shule na Vituo vya Afya. Alikumbusha kwamba, kazi ya kuweka umeme kwenye nyumba na taasisi mbalimbali ni ya wahusika wenyewe, siyo Serikali.
Vilevile, Dkt Kalemani aliwataka wananchi kuwa na ufahamu wa gharama za kuunganishiwa umeme kupitia Mradi wa REA, ambazo alizitaja kuwa ni shilingi 27,000 tu. “Ole wake atakayepandisha gharama hizo kwa maslahi binafsi, atakiona cha moto.”
Aliwahimiza wananchi ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za kufungiwa nyaya za umeme, kuomba kufungiwa kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji kutandaza nyaya katika nyumba yote na ambacho kinaweza kufungwa katika nyumba isiyozidi vyumba vinne.
Uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Shinyanga; kama ilivyokuwa katika Mikoa mingine ambayo Mradi huo umekwishazinduliwa; ulienda sambamba na kumtambulisha kwa viongozi na wananchi, Mkandarasi atakayetekeleza kazi hiyo.

TAFITI YA HAKI ELIMU YABAINI ELIMU BURE IMEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Rais John Pombe Magufuli alipongia madarakani alitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.

Taasisi ya Haki Elimu ni moja ya taasisi ambayo imefanya utafiti katika swala la elimu na kuja na majibu ambayo yameonesha kuwepo kwa mafanikio makubwa katika swala hili la elimu bure.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage ametaja kuwa tafiti hiyo imebaini kuwa Sera ya elimu bila malipo imesababisha ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza hasa kwa shule za msingi.

“kulikuwa na ongezeko la asilimia 43 na asilimia 10 kwa shule za Sekondari ,hali iliyosababisha msongamano madarasani na pia kuongezeka kwa uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi kwa darasa la kwanza hadi kufikia mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 164 kwa wastani badala ya wanafunzi 45 wanaotakiwa” amesema Kalage.

Amesema kuwa utafiti huo ambao ulifanyika Wilaya za Njombe ,Mpwapwa , Sumbawanga ,Kilosa , Korogwe ,Tabora Mjini na Muleba kwa kuhusisha shule 28 na Msingi na 28 za Sekondari.

Amesema kuwa utafiti umebaini kuwa shule zenye wanafunzi wachache kati ya wanafunzi 200-300 zinapatiwa wastani wa Tsh 100,000-150,000 kwa mwezi ambayo hutatua matatizo ya msingi kama ukarabati hasa kuzingatia fedha za ruzuku zinatumwa shuleni kila mwezi.

Kalage amesema tafiti hiyo imetoa mapendekezo kwa serikali,ifanye jitihada za makusudi kuhakikisha kwamba wadau wote wanao elewa vizuri sera ya elimu bila malipo ili kurahisisha utekelezaji wake .

Amesema kuwa wadau wote wanapaswa kuzielewa nyaraka zote na miongozo kuhusiana na sera hii ili kila mdau atambue wajibu wake na jinsi anavyopaswa kushiriki katika utekelezaji wa elimu bure .

Amesema kutokana na elimu kuongeza kwa uandikishaji wa darasa la kwanza serikali ichukue hatua za makusudi kushughulikia changamoto zitakazotokana na elimu bila malipo kama vile ongezeko la wanafunzi , uhaba wa madarasa , walimu , Vitabu na Vinginevyo.

Ametaja kuwa zoezi la kupeleka fedha za ruzuku liende sambamba za serikali kutoa fedha za maendeleo kwa ajili yakuboresha miundombinu ya shule kwani shule nyingi zinachangamoto ya miundombinu na hivyo ni muda muafaka kwa serikali kuanza sasa kusaidia shule kwa kuzipa fedha za maendeleo kama amabvyo ilifanya wakati wa utekelezaji wa MMEM na MMES.
Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini , John Kalage akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa tafiti juu ya mpango wa elimu bure nchini.
Aliyekuwa Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya elimu bure iliyofanyiwa utafiti na tasisi ya Haki eleimu nchini
Baadhi ya washiriki wakisikiliza ripoti hiyo kwa makini
Dr. Richard Shukia kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Elimu na Saikolojia akitoa maelezo juu ya tafiti hiyo
Wadau wakifatilia kwa makini maelezo kutoka kwa mtafiti

SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA ANGA

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano (BASA), katika usafiri wa anga utakaowezesha nchi hizo kutoa huduma bora za anga na kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi wake.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo utaruhusu ndege za nchi hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote katika nchi hizo.

"Naamini ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa Anga na hivyo kuongeza viwango vya usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na hivyo kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.

Ushirikiano wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii, kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akibadilishana hati za makubaliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), kuhusu ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakionesha hati zao za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo, jijini Arusha leo. Mkataba huo utaimarisha huduma za usafiri na usalama wa anga.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images