Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1192 | 1193 | (Page 1194) | 1195 | 1196 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona. Aliyeketi ni Kaimu Naibu Mrajisi Udhibiti na Usimamizi, Collins Nyakunga.
  Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona.

  Kaimu Mrajisi wa Vyama vya ushirika nchini, Tito Haule amevitaka vyama vyote vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha, ambayo inavighalimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo halisi wa vyama husika na kuwaingiza wanachama wao katika matatizo kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo huku akiwashauri kuangalia huduma ambazo zinawalenga wananchi moja kwa moja.

  Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati wa kusaini makubaliano na Benki ya Wanawake ya Covenant ambayo yataiwezesha benki hiyo kuweza kutoa huduma mbalimbali za bima pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini, Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma Mrajisi ameitaka benki hiyo kuhakikisha inatimiza adhma ya kutoa huduma ambazo zitawanufaisha wanachama moja kwa moja na sio viongozi wachache.

  “Vyama vingi vimekuwa na mazoea ya kujiingiza katika mikopo mikubwa na wakati mwingine hata kuzidi uwezo halisi wa vyama husika, lakini pia viongozi wanaokuwepo wanakuwa sio waaminifu na kujikuta wanashindwa kusimami matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu na kujikuta wanaviingiza vyama katika matatizo makubwa,” alisema Haule na kuongeza kuwa, “Ninawsaihi viongozi waache utaratibu huu ambao umeendelea kuvifanya vyama vya ushirika kushindwa kuwa sehemu ya ukombozi wa wanachama wake bali sehemu ya kuwakandamiza,”

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo utakao iwezesha benki hiyo kufika maeneo mbalimbali nchini kutoa huduma kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini amesema atahakikisha benki yake inafanya kazi waliyokubaliana na msimamizi huyo wa vyama vya ushirika kwa uaminifu na weledi ili kuweza kuwainua wanachama wa vyama vya Ushirika.

  “Tumefanya utafiti kwa muda mrefu sasa, kuangalia namna ambavyo tunaweza kuwasaidia wajasiriamaliwadogo miongoni mwao wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wafanya biashara, tumegundua wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa huduma za Bima ya matibabu pamoja na ajali, hivyo tumeanzisha huduma hizo ili kuwaondolea mzigo ambao wanaupata kila siku wanapopata fedha wanashindwa kuweka akiba,”

  Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kumshukuru mrajisi kuwapatia ruhusa ya kuhudumia vyama vya Ushirika nchini na kusisitiza kuwa watatoa ushirikiano kwa ofisi hiyo ili kuhakikisha mamilioni ya wanachama wa vyama vya ushirika wananufaika moja kwa moja na huduma zitakazo tolewa na benki hiyo.

  0 0

  Kwa sasa, juhudi za Rais Dkt. Magufuli kufufua huduma bora na za uhakika katika Mashirika na Makampuni ya Umma zinazidi kuleta *Matokeo chanyA+* Kampuni Simu ya TANZANIA -TTCL ndiyo kampuni pekee inaongoza kwa sasa kwa kutoa huduma za intanet bora na za uhakika. Rais wangu... *mzalendo na mchapakazi..* Nchi yangu... *Matokeo chanyA+*

  0 0

  Jovina Bujulu –MAELEZO

  Ubora na thamani ya lugha ya Kiswahili duniani unadhihirika kwa kukubalika kwake,  hali hii inayopelekea lugha adhimu ya Kiswahili kuendelea kukua na kutumika katika nchi mbalimbali duniani kijamii, kiuchumi na hasa kibiashara na ushirikiano wa kimataifa.

  Mchango wa lugha hii inaipa hadhi kubwa nchi yetu ambayo ni kitovu cha lugha hii inayotumika kama lugha rasmi ya mawasiliano katika nyanja mbalimbali na pia ndiyo lugha unganishi inayotumiwa na watu wengi nchini.

  Kihistoria, lugha ya Kiswahili imekuwa na mchango mkubwa kutokana na kutumika katika harakati za ukombozi  na pia kuwaunganisha Watanzania na kuwafanya wawe wamoja.

  Mara baada ya Uhuru Tanzania ilianzisha Baraza la Kiswahili (BAKITA) na kupewa jukumu la kuimarisha na kueneza lugha hii , pia kuhakikisha inatumika kwa ufasaha pamoja na kukuza msamiati wake ili iweze kukidhi matumizi yake.

  Mwaka 1968, lugha hii ilianza kutumika  kufundishia katika shule za msingi hapa nchini. Hatua hii ilimaanisha kila mwanafunzi wa shule ya msingi kuifahamu vizuri kwa kuiandika, kuisoma na kuielewa.

  Aidha, historia ya kuikuza na kuieneza lugha hii imeanzia mbali, mwaka 1962 hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliitumia kuhutubia Bunge la Tanganyika, baada ya utawala wake, Rais aliyemfuatia, Ali Hassan Mwinyi aliendeleza matumizi ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za mawasiliano.

  Naye Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe.Benjamin Mkapa na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete walifanikisha maendeleo ya lugha hii kwa kuhimiza matumizi fasaha katika nyanja za elimu, shughuli zote za Serikali, katika shughuli au mikusanyiko rasmi pamoja na matumizi mengine ya mawasiliano.

  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakikuwa nyuma katika kuhakikisha kinakuza, kinaeneza na kinakifanya Kiswahili kitambulike zaidi duniani.Miongoni mwa jitihada hizi ni pamoja na kuanza kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo ili kuipa msukumo kwa wananchi wa mataifa mengine yanayohitaji kujifunza lugha hii.

  Katika kutambua juhudi hizi za Chuo, Balozi wa kwanza wa Kiswahili Barani Afrika, Mama Salma Kikwete, hivi karibuni alimkabidhi tuzo ya Kiswahili  Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mkandara, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake  kwa kurasimisha lugha hiyo  kutumika katika shughuli zote za Chuo na kitaaluma ikiwemo mikutano ya Baraza la chuo.

  Aidha, Mama Salma alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwekeza katika kuendeleza lugha Kiswahili ili kuieneza kibiashara ndani na nje ya Bara la Afrika.

  Kutokana na umuhimu wake katika mawasiliano hivi karibuni Bunge la Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeidhinisha lugha Kiswahili itumike katika mikutano yake ya Bunge.

  Bunge hilo linajumuisha Wabunge kutoka katika nchi sita za jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini zimepitisha lugha hiyo kutumika katika nchi zao. Hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa kukipaisha Kiswahili kimataifa.

  Ni kutokana na muktadha huo, baadhi ya wataalamu wa lugha wameishauri Serikali kuanzisha kozi ya ukalimani katika vyuo vyake ili kuongeza idadi ya wakalimani hapa nchini hatua ambayo itawaongezea ajira wahitimu wa kozi hiyo.

  Hadi sasa inakadiriwa kuwa idadi ya wakalimani nchini haizidi 20 mbao ndio wanaotoa huduma katika mikutano mbalimbali ya kimataifa.

  Akizungumza jijini Dar es Saaam hivi karibuni Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Selemani Sewangi alisema kuwa huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuanzisha kozi hiyo ili kupata wakalimani wa kutosha na wenye weledi, uwezo na maarifa katika kukalimani lugha ya Kiswahili kwenda lugha nyingine mbalimbali duniani.

  Aliendelea kusema kuwa Tanzania haina kozi hiyo nyuoni, hivyo uwepo wa wataalamu hao hasa kipindi hiki ambacho nchi inapokuwa kiuchumi kwa kasi, kazi hiyo itoe mchngo wake ikizingatiwa sekta ya utalii inaendelea kuimarika na kuwa na ongezeko la wageni mbalimbali wakiwemo watalii, wawekezaji na wengine hatua ambayo itakuwa fursa ya kutangaza utajiri na maliasili zilizoko nchini mwetu.

   “Kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatafsiri lugha ya Kiswahili wakidhani wanafanya taaluma ya ukalimani, jambo ambalo si sahihi kitaaluma, watu hawa hawawezi kupata ajira kutokana na kukosa vigezo vya elimu rasmi ya ukalimani” alisema Dkt. Sewangi.

  Akifafanua juu ya maana hasa ya ukalimani Dkt. Sewangi alisema kuna mkanganyiko  kati ya kutafsiri na kukalimani, ambapo alisema kuwa kutafsiri kunaweza kufanywa na mtu yoyote, lakini kukalimani ni lazima mtu asomee kozi maalumu  ili aweze kutambulika kimataifa.

  Katika kuonyesha msisistizo wa kuhakikisha kuwa Kiswahili kinapaa kimataifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa Kiswahili ni lugha ya Waafrika na inazungumzwa katika nchi nyingi na imekubalika kutumika katika mikutano ya Umoja wa Afrika, hivyo aliwashauri Watanzania kuipenda lugha hiyo.

  Hivi karibuni Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Haile Mariam Dessalegn ambapo alisema kuwa nchi yake imekubali kuchagua Chuo Kikuu kimoja ili lugha ya Kiswahili ifundishwe nchini mwake kwa kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Aidha, Rais Dkt. Magufuli aliahidi kupeleka wataalamu wa lugha ya Kiswahili ili wafundishe katika chuo kitakachoteuliwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia kufundisha lugha hiyo.

  Kwa kuzingatia umuhimu wa lugha ya Kiswahili huu ni wakati muafaka kwa watunga Sera, Mamlaka husika na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuanzisha kozi ya ukalimani katika vyuo vyetu ili wahitimu wapate fursa za ajira katika nchi mbalimbali  na hivyo kuzidi kuipa hadhi  na kuieneza lugha ya Kiswahili ambayo inakisiwa kuwa ni lugha ya 10 miongoni mwa lugha 600 zinazozungumzwa duniani.

  0 0

  Spika wa bunge, Job Ndugai akimwapisha Mama Salma Kikwete kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
  Mama Salma Kikwete akiapa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa kwa mkewe mama Salma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Wajumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania  (KICoT Corporation) leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo  na Wajumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania  (KICoT Corporation) leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiimba wimbo wa Taifa pamoja na Mshauri Mkuu wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania  (KICoT Corporation), Mhe. Balozi Mstaafu wa Korea Kusini hapa nchini Kim, Young-Hoon ambaye alimwambia Mhe. Makamu wa Rais kuwa bado anaukumbuka wimbo wa Taifa la Tanzania.

                                    . 


           Watanzania waliosoma Nchi Korea Kusini wameunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuleta wawekezaji ambao wanataka kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya nguo, vifaa tiba, uzalishaji wa nishati ya umeme wa jua, kilimo na katika sekta ya Sanaa,utamaduni na michezo.

  Mwenyekiti wa Baraza la Uwekezaji kutoka Korea Kusini hapa nchini Kakono David ametoa kauli hiyo wakati anaongoza Ujumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea Kusini ambao wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa viwanda hivyo utatoa fursa kubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania na amesisitiza kuwa kwa kuanzia wawekezaji hao wataanza kuwekeza katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mazungumzo na ujumbe huo wa Baraza la Uwekezaji Kutoka Korea Kusini amesema amefurahishwa na ujio wa wawekezaji hao na amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya Tano inaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji ili kazi ya ujenzi wa viwanda nchini iweze kwenda kwa kasi inayotakiwa.

  Makamu wa Rais amesema ujenzi wa viwanda unaoendelea kufanywa na wawekezaji nchini utasaidia kuongeza pato la taifa na kutoa ajira kwa Watanzania.Amesema Tanzania ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji Tanzania Bara na Zanzibar hivyo ni wakati muafaka kwa watendaji wa sekta husika kwa ushirikiano na serikali kujiimarisha katika kuondoa ukiritimba ili kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

   Makamu wa Raia pia amefurahishwa na mpango wa wawekezaji hao kutoka Korea Kusini ambao wanataka kusaidia uimarishaji wa haki za wanawake hapa nchini na amekaribisha Jumuiya ya Wanawake kutoka Korea Kusini kuja Kufanya ziara ya kikazi hapa nchini.
   

  0 0   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge  Dr Elly Marko Macha , katika Viwanja  Bunge Mjini  Dodoma  3 March 2017 Mbunge huyo  amefariki hivi karibuni  alipo kuwa katika matibabu Nchini Uingereza.Picha na PMO

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Savants Initiative Bw. Peter Thadeo (kulia) akifafanua  jambo  kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya Jiongeze Kijana mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Mawasiliano toka kituo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo na kushoto ni Afisa Habari toka Iadara ya Habari (MAELEZO) Bw. Benjamin Sawe.
  Afisa Mawasiliano toka Kituo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo (kushoto) akisisitiza jambo  kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya Jiongeze Kijana mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Savants Initiative Bw. Peter Thadeo na kulia ni Mwanzilishi na afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Inspassion group Bw. Fortunatus Ekklesiah
  Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

  0 0

  Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. 

  Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kw mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu.

  Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

  ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya 'Taifa Kwanza, Leo na Kesho', hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya. 

  Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza kulimaliza. Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.

  Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.

  Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
  Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
  Aprili 4, 2017
  Dodoma

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  Serikali imewasahuri wananchi wote wanaofaidika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) nchini kuzitumia vizuri ruzuku wanazozipata kwa kuendelea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi katika maeneo yao.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mtabwe Mhe. Khalifa Mohamed Issa lililouliza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) upo katika Awamu ya Tatu ya Utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini nini kimefanyika ili ruzuku ziweze kumudu mahitaji ya chakula, Elimu, Afya na lishe Bora kwa watoto.

  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema kuwa Serikali inaendelea kutoa ruzuku wa Kaya Maskini ila inasahuri pia wananchi waendelee kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato na isitegemee ruzuku pekee.

  “Niwaombe wananchi wanaopata ruzuku kutoka mpango wa TASAF wajishughulishe pia na shughuli nyingine za kiuchumi na kutotegemea ruzuku pekee” Alisistiza Mhe. Angella.

  Ameongeza kuwa ruzuku zinazotolewa ni kichocheo cha kuifanya kaya iweze kujikimu hasa katika kupata mahitaji muhimu huku ikiendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka akiba na kutekeleza miradi ya ujasiriamali ili iweze kusimama yenyewe na kujitegemea baada ya kutoka katika umaskini uliokithiri.

  Mhe. Angella Kairuki ameeleza kuwa vigezo vya kupata kaya maskini ni wa uwazi na huanishwa na Jamii katika mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka Halmashauri za Wilaya na kusimamiwa na Viongozi wa Vijiji, Mitaa na Shehia.

  Aidha uzoefu uliopatikana umeonesha kwamba kwa kiwango cha ruzuku kinachotolewa kwa wananchi wanaofaidika na Mpango huo kimewawezesha kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ufugaji,ujasiriamali na  ujenzi wa nyumba bora, hivyo viwango hivyo sio vidogo kama wengi wanavyodhani.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

  0 0


  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

  Serikali imeendelea kuchukua hatua kwa kuendelea kutoa elimu katika Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Miji 72 ili kuondokana na tatizo la ndoa za utotoni zinazobababisha watoto kukosa haki ya msingi ya kupata elimu.

  Akijibu swali la Mhe. Anna Kilango Malecela Mbunge wa Viti Maalum (CCM) lililouliza Je, Serikali ina Mkakati gani wa kutokomeza ndoa za utotoni? Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa msisitizo utazidi kuwekwa katika utoaji wa elimu kwa familia, wazee wa mila na jamii kwa ujumla.

  “Tutajikita kutoa elimu zaidi ili jamii iachane na mila na tamaduni zilizopitwa na wakati za kuoza watoto wa kike” alisisitiza Mhe. Dkt. Kigwangalla.

  Ameongeza kuwa Serikali inatambua athari kubwa zinazosababishwa na ndoa za utotoni katika jamii ya watanzania na itaongeza nguvu katika kutoa elimu na kupambana na wale wote watakaojihusisha kwa namna moja au nyingine kuwanyima watoto wa kike haki yao ya kupata elimu.

  Aidha kulingana na takwimu za Afya na Idadi ya Watu nchini za mwaka 2016 ndoa za utotoni zimeshamiri katika mikoa ya Shinyanga kwa asilimia 59, Tabora kwa asilimia 58, Mara kwa asilimia 55 na Dodoma kwa asilimia 51 hivyo Serikali itaendelea kupambana kutokomeza ndoa za utotoni nchini.

  Kwa upande wa muundo wa kisera na kisheria, Serikali imezifanyia maboresho Sera na Sheria ili kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa na mimba za utotoni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Elimu Sura 353 ambayo inatoa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 30 kwa mtu yoyote atakayempa mimba mwananfunzi wa shule ya Msingi au Sekondari.

  Katika kutokomeza ndoa na mimba za utotoni Serikali itaanza utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto mwezi June 2017 unaojumuisha Sekta zote zinazohusu wanawake na watoto kwa lengo la kutokomeza aina zote za ukatili na kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 47 hadi 10 ifikapo mwaka 2020.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo ya kiufundi kutoka kwa Mkurugenzi wa kinga na Elimu ya Afya Dk.Fadhil Mohamed Abdalla wakati alipotembelea ujenzi wa kituo kipya cha Afya Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba leo, akiwa katika ziara maalum ya kikazi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Kituo kipya cha ZSTC cha kununulia Karafuu katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,uzinduzi huo umefanyika leo katika ziara maalum ya kikazi katika Mkoa huo,(Picha na Ikulu) 04/04/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Dkt.Said Seif Mzee (katikati)mara baada ya kukizindua kituo cha shirika la ZSTC cha ununuzi wa Karafuu katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba leo, akiwa katika ziara maalum ya kikazi,(Picha na Ikulu)

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Dkt.Said Seif Mzee (katikati)mara baada ya kukizindua kituo cha shirika la ZSTC cha ununuzi wa Karafuu katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba leo, akiwa katika ziara maalum ya kikazi,(Picha na Ikulu)

  Maafisa mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za Uzinduzi wa Kituo kipya cha Shirika la ZSTC cha kununulia karafuu katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,uzinduzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hatupo pichani),(Picha na Ikulu) 04/04/2017.

  0 0

   Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu yake. 
   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt Jayaka Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge.

   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt Jayaka Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge.
   Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa na wabunge wanawake kwenda kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini Dodoma.
   Mhe. Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni Mjini Dodoma.
   Mhe. Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
   Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu hoja mbalimbaliz za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
   Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika leo Bungeni Mjini Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mama Devotha Gabriel.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa awamu ya pili  saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni. 
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt Jayaka Mrisho Kikwete akifuatilia shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikaza nati katika daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 wakati alipokagua barabara hiyo, mkoani Arusha leo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akikagua moja ya daraja lililopo katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 inayojengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil Jiangsu J/V wakati alipokagua barabara hiyo, mkoani Arusha leo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa eneo la Sakina mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa uongozi wa Kampuni ya ujenzi ya Chicco, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa KM 26, mkoani Arusha, leo.

  0 0

   Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
   Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akimsikiliza Mhasibu Mkuu kutoka Mfuko wa Rais wa kujitegemea Bw.Ahazi Kibona juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
  Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumz ana waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.

   
  Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa atafungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017. 

  Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi.Beng’i Issa amesema Maonyesho hayo yameandaliwa na Baraza hilo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. 

  “Tumeamua kufanya maonesho haya kwa mara ya kwanza kwa sababu changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa mifuko hii haifahamiki sana na wananchi, wengi walikuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata fursa ya kupata mitaji na kusaidiwa na mifuko hii ambayo imeanzishwa na Serikali kwa ajili yao”,Aliongeza Bi.Beng’i. 

  Amesema maonyesho hayo yatawapa wananchi fursa ya kuonana na watu ambao wamefanikiwa katika kipindi kilichopita na hasa kujua jinsi gani watafaidika na mikopo ambayo inapatikana kupitia mifuko hii. 

  Ameitaja mifuko ambayo itashiriki ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wananchi, Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo , Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati na Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya Nchi. 

  Mifuko mingine ni Mfuko wa kuwasaidia makandarasi,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,Mfuko wa Misitu Tanzania,SELF Microfinance Fund na PASS Trust Fund. 

  Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni “WEZESHA WANANCHI KIUCHUMI ILI KUJENGA UCHUMI WA KATI NA TANZANIA YA VIWANDA” 


  0 0  0 0

  0 0


  Aliyekuwa Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile ambaye sasa ameteuliwa kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Lindi Mjini, akizungumza maneno ya Utangulizi, baada ya kupokewa na Mwangalizi Msaidizi wa Kituo cha Kulea Wazee wasiojiweza kilichopo Msimbazi Centre, Dar es Salaam, Sista Angelina (kushoto), wakati viongozi mbalimbali wa Jumuia hiyo walipofika kwenye kituo hicho ili kusalimia wazee hao na pia kuwazawadia vitu mbalimbali ikiwemo nguo, ikiwa ni sehemu za kuanza maadhimisho ya Siku ya Jumuia ya Wazazi ambayo kilele chake kitakuwa Machi 8, 2017 mjini Bukoba. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Lugano Mwafongo
  Wakiendelea kufanya utambulisho
  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akisalimiana na Mkandawile alipowasili ili kkabidhiwa misaada
  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akisalimiana na Katibu wa Jumuia ya Wazazi Ilala Lugano Mwafongo,
  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akiendelea kusalimia.

  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akiendelea kusalimia
  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akiendelea kusalimia
  Msimamizi wa Kituo cha Kutunza Wazee wasiojiweza cha Msimbazi Centre, Sista Wilibroda Mangwangi akiendelea kusalimia
  Masista hao wakapiga picha ya kumbukumbi na baadhi ya viongozi hao
  Picha ya pamoja msafara mzima na masista hao
  Mwafongo akizungumza tayari kuanza kukabidhi misaada kwa Sista huyo
  Viongozi waakanza kumkbidhi zawadi.Wapili kushoto ni Mkandawile na furushi la nguo
  Akakabidhi  Kukabidhi kukaendela  Kukabidhi kukaendelea  Mkandawile akimsalimia mmoja wa Wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho  Naam wakimsalimia kwa bashasha  CCM Oiyeee, Wakamwambia  Wakimsalimia Mzee mwingine mwenye umri unaokadiriwa kuwa tisini ambaye analelewa na kituo hicho  Wakampa zawadi


  Byeee, Mkandawile akimuaga Mzee huyo

  Karibuni jena jamami. Mzee kwenye kituo hicho akisema
  Kila mmoja akijitahidi kuwaliwaza wazee hao. mwishoni Viongozi hao wameagidi kujikusanya na kutoa msaada wa dawa kwa ajili ya wazee kwenye kituo hicho. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizindua rasmi vifaa vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi za picha za kuchora toka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA) pamoja na watendaji wengine wa Wizara mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA), Watendaji waWizara pamoja na wageni toka nje ya nchi mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) Dkt. Herbet Makoye pamoja na viongozi wengine na watendaji wa TaSUBA wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye pamoja na watendaji mbalimbali wa Wizara na wa taasisi hiyo kuelekea kuangalia maeneo mbalimbali ya taasisi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi maji ya bahari yalivyoharibu kingo za taasisi hiyo wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akionyeshwa baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya Studio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipiga nyimbo kwa kutumia kinanda ndani ya moja ya Studio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)


  Na Lorietha Laurence.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilling 100 kwa ajili ya  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) vitavyowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo namna ya kutengeneza picha jongefu.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Wilayani Bagamoyo, Dkt.Mwakyembe amesema kuwa vifaa hivyo ni muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wa Taasisi hiyo katika kuwaongezea ujuzi katika vitendo na baadaye kuwa watendaji bora na makini.

  “Vifaa hivi ni tija katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa vitendo na hivyo kuzalisha watu wenye taaluma zenye tija na zenya kuleta matokeo chanya kwa ajili ya maendeleo nchi”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

  Aliongeza kwa kuhaidi kuwa atahakikisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Mabalozi wanapata fursa ya kuitembelea TaSUBa ili wajionee kwa macho hazina kubwa waliyonayo katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni.

  Aidha aliupongeza viongozi na walimu wa TaSUBa kwa jitihada wanazozifanya za kutoa elimu kwa vijana jambo ambalo linawajengea uwezo wa kujiajiri kupitia taaluma ya sanaa hivyo kuondoa utegemezi na kukuza uchumi wa nchi.

  Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bibi Erica Yegela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) ipo kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote na hivyo wanakaribishwa kujiunga na kujifunza sanaa,utamaduni na uandaaji wa vipindi. 

  Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za maendeleo kiasi cha shilling millioni 100 amabazo zimefanikisha kununua vifaa vya kufundishia kwa vitendo.

  “Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia kiasi hiki cha fedha ambapo kwa kiasi kikubwa kimefanikisha manunuzi ya vifaa hivi vya kufundishia na huu ni mwanzo mzuri nasi tunaahidi kutumia ipasavyo katika kuzalisha wanataaluma hodari” alisema Dkt. Makoye.

  Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kufanikiwa katika kununua vifaa kumekuwapo na changamoto mbalimbali zinazoikabili- Taasisi hiyo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi huku wengi wao wakiwa wamestaafu,uhaba wa ofisi za waalimu na wafanyakazi pamoja na miundo mbinu chakavu.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakati wa hafla fupi ya chakula cha usiku ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa timu ya Serengeti Boys,jana usiku tarehe 04, Aprili 2017, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.
  Nahodha wa timu ya Serengeti Boys akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mbele Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuwatakia heri Serengeti Boys ambao wanajiandaa na fainali ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika Nchini Gabon

  Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa timu ya Taifa ya Serengeti Boys iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi akitoa neno la shukrani kwa timu ya Serengeti Boys ambao walialikwa kwenye hafla maalum ya chakula cha jioni na Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oyster Bay, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihudumu chakula kwa nahodha wa Serengeti Boys Issa Abdi Makamba wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na wachezaji wa Serengeti Boys mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.

  0 0


  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano kushoto pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba wakisaini makubaliano baina ya kampuni hizo mbili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Timiza Vikoba, jana jijini Dar es Salaam.

  Maendeleo Bank kwa kushirikiana na Airtel Tanzania jana wamezindua huduma mpya ijulikanayo kama Timiza Vikoba yenye lengo la kuviwezesha vikundi vya vikoba nchini kutumia njia ya kisasa na salama itakayorahisisha ukusanyaji wa michango, kutoa mikopo na marejesho ya mikopo ya mikopo kwa urahisi kabisa.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini makubaliano baina ya kampuni hizo mbili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Timiza Vikoba.

  Huduma hii ya Timiza Vikoba inawawezesha wateja wa Airtel na Maendeleo Bank walio katika vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50 kupata huduma za kifedha masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu kwa kupiga *150*60# na kisha kuingia kwenye menu ya Airtel Money na kusajili kikundi na kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo kwakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi.
  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema “Maendeleo Bank ni benki inayokua kwa kasi nchini kwa kutoa huduma mbalimbali zenye gharama nafuu, zenye urahisi wa kutumia ikiwemo ile ya akaunti za kuweka akiba, kutoa mikopo na huduma nyingine nyingi”.

  Maendeleo Bank leo tunajisikia fahari kushirikiana na Airtel katika kuleta huduma ya Timiza Vikoba, huduma hii itasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kuweza kuweka akiba kupitia simu zao za mikononi ili kufungua fursa mpya katika huduma za kifedha nchini.

  “Dhamira yetu ni kuenedeleza tabia ya kujiwekea akiba katika jamii na pia kuwapa wateja uwezo wa kukopa na kupokea mikopo kupitia simu zao za mikononi kwa kuwa tunaamini ni ni njia bora na rahisi Zaidi kuliko ile iliyozoeleka. Mteja ukitumia huduma hii ya mikopo ya Timiza Vikoba unajitengenezea historia yako ya mkopo kidogo kidogo na baadae kujipatia mkopo mkubwa kwa masharti rahisi Zaidi” 

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya alisema “huduma ya Airtel Money imekuwa ikiongoza kwa huduma za kibunifu na kisasa Zaidi na leo hii tunazindua ushirikiano wa kipekee na Maendeleo Bank kupitia huduma ya Timiza Vikoba ili kuwawezesha wafanyabiashara katika vikundi vya Vikoba nchi nzima kufanya miamala yao ya kifedha kwa njia salama, uhakika na urahisi zaidi.

  Huduma hii italeta uwazi na kuviwezesha vikundi vya Vikoba kuhakiki taarifa zao kwa kwa kupata taarifa za miamala mbalimbali kwa wakati kupitia simu zao za mikononi. Tunaamini huduma hii itachochea wafanyabiashara bila kujali maeneo walioko kujiunga na kutengeneza vikundi vya Vikoba ili kunufaika na kukuza biashara zao.

older | 1 | .... | 1192 | 1193 | (Page 1194) | 1195 | 1196 | .... | 1897 | newer