Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1191 | 1192 | (Page 1193) | 1194 | 1195 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Mkurugenzi waKampuni ya Jamii Media limited, Mike Mushi akiteta jambo na Wakili wake, baada ya kusomewa maelezo ya awali dhidi ya kesi yao ya mtandao inayomkabili pamoja na mkurugenzi mwenzake, Maxence Melo.
   Wakurugenzi wa Jamii Media Limited, Maxence Melo kulia na mwenzake Mike Mushi, wakiwa wakiwa nje ya mahakama ya Hakimu Kisutu baada ya kesi yao kupangiwa tarehe ya kuanza kisikilizwa.

  Wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuendesha shughuli za mtandao wa kijamii bila kusajiliwa na kuzuia polisi kufanya uchunguzi.

  Kesi iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba itasikilizwa Aprili 2 wakati kesi nyingine iliyopo mbele ya hakimu Victoria Nongwa itaanza kusikiliza Aprili 3, mwaka huu. Upande wa mashtaka umesema katika kesi hiyo utawasilisha mashahidi saba⁠⁠⁠⁠


  0 0

  Mratibu wa Jukwaa la Nishati Tanzania ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hudson Nkotago akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Jukwaa hilo utakafanyika tarehe 6 April 2017.Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.Kulia ni Mratibu wa Nishati wa Kanda ya Afrika kutoka Ubalozi wa Falme ya Uholanzi Rogier Verstraeten.
  Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi cha Hanze,nchini Uholanzi Dk. Linda Maat akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Jukwaa hilo utakafanyika tarehe 6 April 2017.Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.Kutoka kulia ni Mratibu wa Nishati wa Kanda ya Afrika kutoka Ubalozi wa Falme ya Uholanzi Rogier Verstraeten na Mratibu wa Jukwaa la Nishati Tanzania ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hudson Nkotago (katikati).
  Afisa Sera, Utawala na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi, Neema Matafu akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Jukwaa hilo utakafanyika tarehe 6 April 2017.Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.Kulia ni Mratibu wa Nishati wa Kanda ya Afrika kutoka Ubalozi wa Falme ya Uholanzi Rogier Verstraeten.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Ubalozi wa Uholanzi nchini leo Jijini Dar es Salaam.

  Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe akisalimiana na waalimu na viongozi wa Chuo cha Waalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kikazi na kushiriki mahafali ya Chuo hicho na kutoa vyeti kwa wahitimu.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt Harrison George Mwakyembe akizungumza katika mahafali ya Chuo cha waalimu Michezo Malya Jijini Mwanza.
  Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw. Yusufu Omary Singo akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi fupi ya uwalimu wa michezo yaliyofanyika Chuo cha Mwaalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza.
  Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa kozi fupi ya uwaalimu wa michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe alipokuwa akizungumza nao katika mahafali ya Chuo hicho Jijini Mwanza.

  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM

  …………………………………………………………………………………….

  Na Mwandishi Wetu -Mwanza

  Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na hata nje ya nchi.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo.

  Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe.

  Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma.

  Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali, umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu.

  Mbali na jukumu la kuongeza aina ya kozi zitakazo tolewa na chuo hicho kwa ngazi ya Stashahada (Diploma) mkuu huyo amemweleza waziri changamoto zinazo kikabili chuo hicho ambazo nipamoja na uhaba wa maji, Gym ya mazoezi, hali inayosababisha timu mbali mbali za mpira wa miguu zinazo tamani kwenda kuweka kambi katika eneo hilo kushindwa kutokana na ukosefu wa Gym, “Mh. Waziri ilikuja timu ya Mbao FC, kilio chao kikubwa ilikuwa ni eneo la Mazoezi ya viungo (Gym Fitness centre)” alisema mkuu huyo wa chuo.

  Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Michezo nchini Dkt. Yusuph Singo Omary, kutoka Wizara ya habari, amesema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kutenga shule 55 ikiwa ni hatua itakayo saidia katika kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini kuanzia vijana wanapokuwa wadogo.

  Awali akimkaribisha Waziri wa habarikuzungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi Msafiri, alimuomba waziri, Wizara ya habari kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kuona Umuhimu wakukisaidia chuo hicho katika kukiendeleza, “Tunaomba Mhe. Waziri ili chuo hiki kiweze kwenda mbele basi vema kila Halmashauri ikaagizwa kugharamia angalau Walimu wawili kila mwaka”, alisema Msafiri na kuongeza kuwa endapo Halmashauri zote nchini 189, zikileta walimu wawili tu basi tutakuwa na wanafunzi 378, hii itakisaidia chuo chetu kukua zaidi, lakini pia kupata walimu wenye weledi.

  Kwa upande wao wahitimu hao wamemuomba waziri kupewa kipaumbele katika Michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA, Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Catherine Laurent, amesema wao wamejifunza Sheria na kanuni za Michezo mbali mbali kwa kipindi chote walichokuwepo chuoni hapo hivyo wanaomba kupewa kipaumbele katika kufundisha michezo pindi warejeapo kwenye vituo vyao vya kazi kwani sasa wanatambua sheria, kanuni na taratibu zinazo ongoza michezo waliyo jifunza.

  Chuo cha michezo Malya kilianzishwa mwaka 1979, kikiwa na lengo la kufundisha na uendeleza walimu wa michezo katika ngazi ya Astashahada na badae mwaka 1995, ndipo kilianza kuzalisha walimu wanafunzi wa ngazi ya Stashahada (Diploma). Lakini pia kimekuwa kikiendesha kozi fupi za wiki mbili ambazo huwajengea uwezo wahusika kabla yakuendelea na ngazi ya Diploma.

  0 0

   Mwalimu wa mazoezi ya Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, Dulla Salum, akiongoza mazoezi ya wanamichezo mbali mbali waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri na kudhaminiwa na bia ya Windhock  na Coca Cola. 
  Baadhi ya wanamichezo kutoka sehemu mbailmbali wakifanya mazoezi katika Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam jana waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri na kudhaminiwa na bia ya Windhock na Coca Cola.
     Mwalimu wa mazoezi ya Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, Dulla Salum, akiongoza mazoezi ya wanamichezo mbali mbali waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri na kudhaminiwa na bia ya Windhock na Coca Cola. 
   Baadhi ya wanamichezo kutoka sehemu mbailmbali wakifanya mazoezi katika Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam jana waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri na kudhaminiwa na bia ya Windhock na Coca Cola. 
  Mwalimu wa Home  Gym ya Mwenge jijini Dar es Salaam, Andrew Mango, akiongoza mazoezi ya wanamichezo mbali mbali waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa 'Afya ni Utajiri' na kufanyika katika kituo cha mazoezi cha Infinity Fitness kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Mwalimu wa mazoezi ya Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, Dulla Salum, akiongoza mazoezi ya wanamichezo mbali mbali waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri. 
  Mazoezi yakiendelea.
  Wanamichezo mbalimbali wakiwa katika mazoezi.
  Mazoezi yakiendelea.
  Wanamichezo wakiendelea na mazoezi.
  Mwalimu wa mazoezi ya Infinity Fitness iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, Dulla Salum, akiongoza mazoezi ya wanamichezo mbali mbali waliojumuika kwenye Jumamosi ya Mazoezi iliyoitwa Afya ni Utajiri na kudhaminiwa na bia ya Windhock na Coca Cola. 
  Walimu wa mazoezi

  0 0

  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa pili aliyevaa suti nyeusi akitoa salama zake za mwisho kwa mchungaji Leornad Lukala jana katika kanisa la KKKT usharika wa Ukonga jijini hapa.

  Waumini mbalimbali wa kanisa hilo akiwemo Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wakiongozwa na mchungaji wa kanisa hilo wakitoa salamu za mwisho.

  Meya wa jiji la Dar es Isaya Mwita akiwa kwenye ibada ya kumuaga mchungaji Leornad Lukala jana katika kanisa la KKKT usharika wa Ukonga jiji hapa.
  ……………


  NA CHRISTINA MWAGALA, (OMJ) Dar

  MEYA wa jiji la Dar es Saalaam Isaya Mwita ameonya tabia kwa baadhi ya watu kuwa nyanyasa wajane na kusisitiza kuwa wasitengwe badala yake familia zichukue jukumu la kuwasaidia kikamilifu.

  Meya wa jiji ametoa kauli hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki wakati wa misa ya kumuaga mchungaji Leornad Lukala wa kanisa la KKKT usharika wa Ukonga , mtaa wa Mongolandege mwishoni mwa wiki.

  Alisema kwamba katika familia nyingi kumekuwa na dhana potofu ya kuwanyanyasa wajane huku ndugu wa familia wakidiriki kuwadhurumu mali jambo ambalo hufanya watu hao kuishi kwenye mazingira magumu.

  Aliongeza kwamba jambo hilo katika jami ya kitanzania halikubaliki na wala kuvumilika na hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari juu ya watu hao.

  “ Kumekuwa na tabia ya watu kunyanyasa wajane , hawa watu wakishaondokewa na wenziwao , basi familia utakuta ndio zina sauti badala ya mfiwa, wanazurumu mali, ndio mana kumekuwa na kesi kadha wa kadha kwenye Mahaka zinazo shugulikia mambo ya mirasi” alisema Meya Isaya.

  “ Naomba niwaombe sana, wajane wasitengwe, wapewe huduma zao kama ilivyokuwa awali, msifanye watu hawa wakajutia kubaki duniani, msitumie nafasi zenu kuwa zalilisha, wapeni huduma kama wengine” aliongeza.

  Lakini sitaki kuingia mambo ya Mahakama, ila ninachotaka kueleza hapa ni kwamba , hawa watu wasitengwe, wapewe haki zao, na familia zisiwatelekeze, zichukue nafasi ya kuzihudumia, hii itakua ni kinga ya kupunguza kesi za mirasi” alifafanua.

  Alisema kuendelea kuwazurumu na kuwatenga wajane, ndio chanzo cha kwenda Mahakamani kushtaki , mabaya zaidi jambo hili halitesi familia ambayo imeshtakiwa ila yule ambaye ameshtaki.

  Katika hatua nyingine Meya Isaya alisema kwamba , viongozi waliopewa nafasi za kuhuumia wananchi wanapaswa kuacha alama pindi wanapomaliza muda wao.

  “ Naomba sana viongoziambao tumepata nafasi za kuwatumikia wananchi, iwe ni kwenye sekta ya dini, kisiasa, serikalini, na sehemu nyingine, tujitahii sana kuacha alama kwenye maeneo yetu, ambazo zitafanya leo hii mtu akifa zinaonekana na kukumbukwa” alisema Meya Isaya.

  Mchungaji Lukala alifariki dunia Machi 30 mwaka huu njiai akipelekwa kwenye kitiuo cha afya cha Mongolandege ambapo atazikwa leo kijijini kwao Mwanalumango Kisarawe mkoani Pwani.

  Awali Meya Isaya alitembelea ofisi ya Kata ya Ukonga na kufanya mazungumzo mbalimbali na Diwani wa kata hiyo Juma Mwipopo,ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuziwezesha kata ili kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili

  0 0

  Baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza 'Njoo Baadae' mwishoni mwa mwaka jana, COYO kutoka Rock City anatukutanisha na video yake mpya 'ZIWAFIKIE', iliyosimamiwa na director kutoka Arusha, Nisher.

  "Naweza kusema hii ndio video yangu ya kwanza ramsi, japo nimewahi kufanya video zingine hapo kabla ambazo nahesabu kama ilikuwa ni safari ya kujifunza" Amesema Coyo.

  "Sababu za kumchagua Nisher, kwanza kiukweli nazikubali kazi zake, nalikubali jicho lake na kwa kuzingatia hii ndio video yangu rasmi ya kwanza, nilihitaji kufanya na mtu makini kama yeye" aliongeza Coyo.

  Audio ya 'ZIWAFIKIE' ambayo inatarajiwa kuanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio baadae wiki hii au wiki ijayo, imetayarishwa na maproducer wawili, Daydream na Kid Bway.

  Tafadhali share kadri uwezavyo!


  MITANDAO YA KIJAMII YA COYO:

   

  0 0
  Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumza jambo kwenye mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi
  Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Prof. Simon Msanjila akiwaasa wazazi kwenye mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi

  Robert Shetkintong, Naibu Balozi wa India nchini akifuatilia mijadala katika kikao cha wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchiBaadhi ya wazazi walioshiriki mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi mwishoni mwa wiki.

  Wazazi wametakiwa kuwa waangalifu wa watoto wao wanaosoma nje ili kuhakikisha wanasoma na kuhitimu vizuri kama inavyotakiwa.

  Akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasoma nje, Mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema hilo likifanyika taifa litanufaika zaidi.

  “Tuendelee kushirikiana kwa pamoja ili kuona watoto wetu walioko nje kwa masomo wanamaliza masomo yao na kutimiza ndogo zao inavyotakiwa. Sisi wazazi tuna mchango mkubwa sana katika hili,” alisema Mollel mwishoni mwa wiki.

  Alifafanua kwamba kuna watoto wamekuwa wakipewa fedha nyingi na wazazi wao kiasi kwamba nao wanapofika nje huwa bize kufanya matanuzi badala ya kusoma kama ambavyo tunatarajia.

  “Unakuta mtoto anapewa fedha nyingi hadi anashindwa kujua azitumie kwa matumizi gani, ndipo hapo wengine unakuta wanajiingiza kwenye ulevi na mambo mengine kama hayo. Ni lazima tunapowapa fedha tujiridhishe je ni kwa ajili ya nini na wanazitumiaje,” alisema Mollel.

  Kwa mujibu wa Mollel ni jambo zuri mzazi au mlezi kuhakikisha mwanae anapata matunzo bora ikiwamo kumpatia kile ambacho anaamini kwamba kitamsaidia kusoma vizuri, lakini kwenye suala la kuwapa fedha nyingi watoto huwachanganya kimaisha na kusababisha baadhi yao kujikuta wakifanya ambavyo hawamkutarajia.

  Mollel ambaye alikuwa akiongea katika kikao cha wazazi ambao wanasoma nje baada ya kuunganishwa na GEL, alishauri kuundwa kwa umoja wa wazazi ambao watotyo wao wanasoma nje kupitia GEL (GELPA), ushauri ambao uliungwa mkono na wazazi.

  Wazazi waliokuwepo kwenye mkutano huo waliunga mkono kuanzishwa kwa GELPA, huku wengine wakitaka jambo hilo lifanywe mara moja iwezekanavyo wakisema kuwa lina umuhimu mkubwa.

  Naye Robert Shetkintong, Naibu Balozi wa India nchini ambaye alikuwa kati ya wazungumzaji katika mkutano huo amewahakikishia Watanzania kwamba nchi yake ni sehemu salama kwa wageni kusoma.

  “India ni nchi nzuri, haina ubaguzi wa aina yoyote, unaweza kuona hata mimi naona kama mwafrika, naonekana kama mchina kwa kiasi fulani, lakini ndio naibu balozi wa taifa la India hapa Tanzania,” alisema.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Prof. Simon Msanjila alisema “Hata mimi nimewahi kusoma nje, ninazijua changamoto za kusoma nje, lakini ninachoweza kushauri ni kwa wazazi kushirikiana na kulea jamii yetu iliyoko huko nje. Kwenda kusoma nje kuna faida kadhaa ikiwamo kuchukua mawazo mapya kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

  Profesa Msanjila aliwashauri pia watu na makampuni yanayofanya kazi ya uwakala wa vyuo vya nje kuhakikisha wanafuatilia vyuo wanavyoviwakilisha vinatambulika.

  “Mzazi unawajibika kufuatilia vyuo ambavyo mtoto wako anatarajia kwenda kusoma. Unaweza kulazimisha ili mradi aende nje kwa sababu tu unapenda aende nje, lakini nawashauri kwamba ni suala la msingi sana kuhakikisha mtoto anasoma katika chuo ambacho kweli kinatambulika.

  Akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa, Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalik Mollel alisema “Nikuondoe hofu kuhusiana na vyuo tunavyowakilisha, kwani utaratibu ambao tunautumia ni kwamba kabla ya kuanza kupeleka wanafunzi katika chuo, huwa tunakifuatilia na kukipeleka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili kuhakikiwa,” alisema.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. 
   ============================================= 


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amelipongeza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa kuridhia na kupitisha azimio namba 2348 (2017) la kuongeza muda kwa Misheni ya Ulinzi wa Amani chini ya MONUSCO iliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi tarehe 31 Machi, 2018.

  Mhe. Mahiga ametoa pongezi hizo wakati akihutubia Baraza hilo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani hivi karibuni.

  Mhe. Mahiga ambaye aliwakilisha nchi 15 za SADC alisema kuwa anaupongeza Umoja wa Mataifa kwa ujumla chini ya uongozi wa Katibu Mkuu, Bw. Antonio Guterres kwa kufikia uamuzi wa kuongeza muda kwa MONUSCO na jitihada nyingine nyingi za kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili DRC kwa muda mrefu ikiwemo ukosefu wa amani na usalama.

  Mhe. Mahiga alisema kuwa, kupitishwa kwa azimio hilo kunatoa matumaini mapya kwa wananchi wa DRC na dunia kwa ujumla kwamba Umoja wa Mataifa una nia ya dhati kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo.

  Aidha, Mhe. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo kuuomba Umoja wa Mataifa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Kikosi Maalum cha Force Brigade Intervention-FIB kilichoundwa na SADC ambacho kinashirikiana na MONUSCO katika ulinzi wa amani nchini DRC. 

  Alieleza kuwa katika kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwa FIB kimeonesha uwezo mkubwa kwa kufanya operesheni ngumu za kukabiliana na vikundi vya waasi na kuvidhibiti, hali iliyopelekea MONUSCO kuaminika zaidi. FIB ina mchango wa vikosi vya ulinzi wa amani kutoka nchi tatu za SADC ambazo ni Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.

  “Kuanzishwa kwa FIB miaka minne iliyopita ulikuwa ni uamuzi wa pekee kwa Baraza la Usalama na SADC katika masuala ya ulinzi wa amani hususan kwenye maeneo yenye changamoto kubwa za usalama na amani. Hivyo naamini pamoja na kwamba FIB ni Chombo cha muda bado kinahitaji kutambuliwa na kupongezwa” alisema Waziri Mahiga.

  Kuhusu changamoto mbalimbali ambazo MONUSCO inakabiliana nazo ikiwemo matishio mapya ya usalama katika maeneo ya Kivu, mbinu mpya za mashambulizi za waasi, ukatili kwa raia na ukiukwaji wa haki za binadamu Waziri Mahiga alisema masuala haya yanailazimu pia MONUSCO kubadilisha mbinu za operesheni ikiwemo kuongezewa vifaa na bajeti ili kuweza kukabiliana kikamilifu na changamoto hizo. 

  Pia aliliomba Baraza la Usalama, SADC, Umoja wa Afrika, ICGLR na Nchi zinazoongea Kifaransa kushirikiana katika kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto zinazoikabili DRC kwa sasa.

  Vile vile, Mhe. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo kwa niaba ya SADC kuiomba na kuialika Jumuiya za Kimataifa kuisaidia Tume ya Uchaguzi ya DRC ili iweze kuandikisha wapiga kura na kuandaa uchaguzi nchi nzima. Pia aliwaomba wanasiasa wa nchini DRC kukabiliana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo kwa sasa na kukwamisha utekelezaji wa Mkataba uliofikiwa mwezi Desemba 2016 chini ya Baraza la Maaskofu (SENCO) la DRC.

  Mhe. Mahiga aliongeza kusema kuwa SADC itatuma Misheni Maalum ya Mawaziri nchini DRC katika kipindi cha majuma mawili kuanzia sasa kwa ajili ya kwenda kuzungumza na kushauriana na wadau mbalimbali wa masuala ya siasa nchini DRC ili kutafuta suluhu.”Sisi , nchi wanachama wa SADC hatupo tayari kuona Mkataba wa Desemba unakwama” alisisitiza Waziri Mahiga.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 03 Aprili, 2017.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Joy Sawe akifungua semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kwa Wahariri wa Habari na baadhi ya wamiliki wa Blogs iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Meneja wa Idara ya Takwimu za Kodi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Fred Matola akiwasilisha mada juu ya Takwimu Rasmi wakati wa semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kwa Wahariri wa Habari na baadhi ya wamiliki wa Blogs iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mkoani Dodoma Aprili 3, 2017.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakifuatilia taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Baraza hilo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Aprili 3, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakifuatilia taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Baraza hilo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Aprili 3, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Dodoma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akiwasilisha hotuba yake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyazi Ofisi hiyo uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 3, 2017.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyazi uliofanyika Aprili 3, 2017 Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mara baada ya kufungua mkutano huo katika Ukumbi wa mikutano Ofisi hiyo Dodoma.

  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dr. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko makubwa ya Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwateua Wakuu Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa iliyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.


  Katika Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Faustine Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa  mkoa wa  Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu Kamishna  wa Uhamiaji Selemani  Bandiho  Kameya amehamishiwa Mkoa wa Tabora.

  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio  Paulus Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Manyara  Naibu Kamishna  Peter Jerome Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya  Kamishna Msaidizi  Ali Mohamed ambaye amehamishiwa   kuwa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa  Arusha. 

  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Mkemi Mhina Seif  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Mjini Magharibi na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja.

  Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa wamebaki katika Vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Laurent  Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Alexander Ihano  na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara  Naibu Kamishna  Fredrick Eustace  Kiondo.

   Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Abdallah  Ramadhani Towo  mkoa wa Kagera na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Anastazia  Gasper Ngatunga mkoa wa Shinyanga.

  Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Makakala pia amewateua  Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa wapya katika baadhi ya mikoa hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mary Francis Palmer   kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Plasid  Mazengo,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji  James Andrew Mwanjotile, Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa  Mtwara,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Hope Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Iringa,  na  Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji  Hosea Alphonce Kagimbo  Mkoa wa Njombe.

  Wengine ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Rashid Salum Magetta  Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Songwe,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Carlos John Haule,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Julieth Deodatus Sagamiko Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Manyara,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Albert Joseph Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Kilimanjaro na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Paul Laurent Eranga,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Mwanza.

  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Tanga,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Shaban Omar Hatibu  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Katavi,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji   Remigius Ibrahimu Pesambili Mkuu  wa Uhamiaji  Mkoa wa Kigoma na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.

  Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume [AAKIA] na Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Uhamiaji Fulgence Andrew Mutarasha  kuwa  Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere[JNIA].

  Imetolewa na
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini
  Dr. A. P. Makakala

  3 Machi 2017

  0 0

  Askofu  wa  kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akifaya maombi
  Baadhi ya  waumini  wa kanisa hilo
  mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa
  Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalimaakiwaombea  waumini wake na Taifa
  Wachungaji wakiwa katika maombi
  Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe
  Waumini  wakiwa katika maombi maalum
  Na MatukiodaimaBlog 
  ASKOFU  mkuu  wa kanisa la Pentecote  Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima  amewataka  viongozi wa  dini  nchini  kutumia nyumba  za ibada  kumwombea Rais Dkt John Magufuli na  kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba  hizo kusema kuumbua viongozi  wa  serikali .

  Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika  nchi  hii si  ya kubenzwa makanisani na wachunguzaji ama viongozi wengine wa  dini bali ni kazi ambayo inapaswa  kuombewa  zaidi  ili  Taifa  lizidi kubarikiwa .

  Askofu  huyo ametoa kauli hiyo jana  wakati wa  uzinduzi wa kanisa hilo  Mtwivila  mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul Mtakwimwa   ,kuwa hivi  sasa  heshima ya  nyumba  za ibada  imeanza kupoteza uwepo  wa Mungu kutokana na baadhi ya  watu  kutumia  nyumba   za  ibada kama  sehemu ya masengenyo na utapeli jambo  ambalo  si  sahihi .

  Alisema  kitendo  cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya  watu  kuishambulia serikali ama  kufanya utapeli  wa fedha  za  waumini wao kwa kuwatoza fedha  kama malipo ya huduma  wanayoitoa si  sahihi na si kazi ya  nyumba  za ibada hasa makanisa .

  Pasipo  kutaja majina ya makanisa   yaliyogeuzwa majukwaa ya wanasiasa na baadhi ya  watu  waovu ama yanayofanya utapeli  wa  pesa  kwa  waumini  wake ,alisema  kuwa yamezuka makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa  kuitwa makanisa  ili yalipaswa kuwa ni vyama  vya siasa ama nyumba  za  waganga  wa  kienyeji kwa maana ya  wapiga ramli .

  “ Baadhi ya makanisa  yamepoteza sifa ya  kuitwa ni makanisa maana  wanafanya  vituko vya ajabu sana  ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo  wanaotumiwa na wanasiasa  kueneza siasa makanisani na  kila  siku  wao ni kuwa ni wachonganishi  dhidi ya  serikali na  watu wake na wengine wamegeuka  watabiri wa  uongo na watenda miujuzi hatarishi kwa jamii “

  Alisema  kuwa kazi ya viongozi wa  dini  ni  kuhubiri  neon ili  watu  wote  waweze kumjua Mungu na  sio kuhubiri siasa ama  kuifundisha kazi serikali ya  kufanywa wakati si  jukumu la kanisa kuwa  iwapo watu  wote  watamjua  Mungu  watafanya kazi ya kuhudumia  jamii  kwa  kutanguliza  hofu ya  Mungu hivyo  hakutakuwa na ufisadi , wizi ama watumishi  hewa hivyo kazi ya kanisa ni kuwafanya watu waijue kweli na kweli  iwe ndani ya  mioyo yao.

  Askofu Dkt   Ndalima  alisema kuwa kanisa   lake  limeenea  nchi nzima na katika mkoa  wa Iringa  wameanzisha makanisa mawili  katika  mji  wa Iringa na Nyololo  wilaya ya  Mufindi ila lengo lao ni  kuhubiri neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa  kanisa la ujanja ujanja  kama  wanavyofanywa baadhi ya  watu  wanaojiita manabii  ila kazi wanayoifanya  ni  sawa na manabii  wa uongo .
  Akielezea  kuhusu utendaji kazi wa Rais  Dkt  Magufuli askofu  huyo  alisema kanisa lake  linampongeza kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna  tena maandamano ya  vurugu na  kuwa kila wakati makanisa  yake yatatenga mudu  wa  kumuombea Rais na  watendaji  wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada  zake na  sio  kutumia  matukio na kashfa  za  viongozi  kuhubiri kanisani .
  MWISHO


  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James akibadilishana mkataba wa kibajeti na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer mara baada ya kusaini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer akizungumza jambo na waandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi bilioni 486.9 uliotolewa na umoja huo kwa Serikali ya Tanzania ili kusaidia Bajeti.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James akitoa ufafanuzi kwa wahandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi bilioni 486.9 ambao Serikali imeupata kutoka umoja wa ulaya (EU) kwa ajili ya kusaidia Bajeti.Kushoto kwake ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Na Daudi Manongi - MAELEZO

  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa 2017/18.

  Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

  “Nadhani mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo”,Aliongeza Katibu Mkuu huyo.

  Pamoja na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na kuweka mkazo katika viwanda na kilimo.

  Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na nishati.

  “Mkataba ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.

  Amesema kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi ya sera yanahitajika.

  0 0

  Na Lydia Churi-MAHAKAMA, ARUSHA

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amewataka Majaji wa Mahakama Kuu nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia Maadili, kuwa waaaminifu na kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kesi zimalizike kwa haraka katika Mahakama mbalimbali.

  Akifungua Mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tazania kuhusu Uongozi katika shughuli za Mahakama  leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi amesema lengo la Mafunzo hayo ni kujadiliana kwa kina nini kifanyike ili kesi zimalizike mapema kwenye mahakama mbalimbali nchini.

  Jaji  Wambali alisema katika mkutano huo, Majaji watapata nafasi ya kujifunza Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania wenye nguzo tatu ambazo ni pamoja na masuala ya Utawala, Upatikanaji wa haki kwa wakati na imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za Mahakama.

  Katika Mafunzo hayo pia Majaji watajadiliana ni nini kilifanyika mwaka jana katika umalizwaji wa mashauri, changamoto zilizojitokeza na nini kifanyike ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

  Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo  alisema  yamegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni la Majaji wa Mahakama ya Rufani, kundi la pili ni la Majaji  Wafawidhi  wa Kanda 14 za Mahakama Kuu ya Tanzania na  kundi la Tatu ni la Majaji wengine wote.

  Alisema Majai wa Mahakama ya Rufani watapatiwa Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama katika usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, ambapo Majaji Wafawidhi watapewa mafunzo kuhusu Usimamizi wa uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine watapatiwa mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa kuleta mabadiliko.

  Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Benki ya Dunia ni Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania na yanalenga katika kuboresha utendaji kazi na kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama.

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma (wa pili kushoto) akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha kuhudhuria Mafunzo ya Majaji yaliyoanza  jijini humo.Kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali. Kushoto kwa Jaji Wambali ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama Bibi Wanyenda Kutta.

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akifungua Mafunzo ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa AICC leo jijini Arusha. Mahakama inaendesha Mafunzo kwa Majaji wote wa Tanzania ambapo Majaji wa Mahakama ya Rufani wanahudhuria Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama katika usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, Majaji Wafawidhi kuhusu Usimamizi wa uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine wanapatiwa mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa kuleta mabadiliko.

  Waheshimuiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo yao yaliyoanza  jijini Arusha.


  0 0

  AOMBA WANANCHI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAMUUNGE MKONO KUFANIKISHA AZMA YAKE

  Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera ameazisha ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya, lengo la kuanzisha kituo hiki ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya Tunduru huzidiwa na wagonjwa kushindwa kupata matibabu kwa wakati.

  Kata ya Nakayaya ipo umbali wa kilomita tano toka Tunduru mjini, kituo hiki kinatarajiwa kuhudumia kata ya Nakayaya, Masonya, Mlingoti na Nandembo/ Tarafa ya Mlingoti na Nampungu pamoja na maeneo ya jirani.

  DC Homera alianzisha mchakato huo kwa kutafuta eneo la kujenga kituo na mara baada ya kupata eneo alimtafuta mchora ramani wa kituo cha afya na mara baada ya kupata ramani alitafuta vijana wa kusafisha eneo na hivi sasa mchanga wa kuanzia ujenzi upo eneo la ujenzi.

  Jumla ya mifuko mia tatu ya saruji imepatikana, fedha bado zinakusanywa toka kwa wananchi, wafanyabiashara, makundi ya Vijana mbalimbali wa wilaya ya Tunduru,hivyo anawaomba wadau wengine wamuunge mkono.

  Jumla ya matofali elfu thelathini zina hitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha afya na zoezi la ufyetuaji utaanza hivi karibuni, vikundi mbalimbali vya vijana vinatarajia kuweka kambi ili kufanikisha zoezi hili.

  Aidha, Dc Homera amewaomba wananchi wote waungane kufanikishe ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya na hivi karibuni atatoa utaratibu wa kujitolea.

  "Tunduru Mpya itajengwa na wenye moyo, wananchi wenzangu wa Tunduru nawaomba tuungane kujenga kituo hiki cha afya na hivi karibuni nitatoa utaratibu wa kujitolea kila mmoja Wetu, tumtangulize Mungu mbele tutafanikiwa kwa ushauri namna ya kufanikisha namba zangu ni +255759814088. Tumuuge mkono Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania nasi kwa upande Wa wana Tunduru tuna wajibika"
  Mchoro wa kituo hicho kitakavyoonekana mara baada ya kukamilika.


  Muonekano kwa nje itakavyokuwa.

  Sehemu mbalimbali ndani ya kituo hicho kitakavyoonekana  0 0  0 0

   Speaker of the Senate of Kenya, Rt Hon Ekwe Ethuro addresses the Assembly where he called for urgent international action to save millions of people from famine and drought 
   The EALA Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega consults with Hon Dora Byamukama at the 136th Inter-Parliamentary Union Assembly in Dhaka, Bangladesh 
    Rt Hon Daniel F. Kidega, Speaker of EALA addresses the IPU Assembly. 
   A section of the delegates in attendance at the global Parliamentarians meet.

  …tells Parliamentarians to take “bull by the horns” in redressing inequalities

  East African Legislative Assembly, Dhaka, Bangladesh: 3rd April 2017: EALA Speaker, Rt Hon Daniel Fred Kidega is calling on global Parliamentarians to pay more attention in ensuring promotion of economic stimulus programmes that address social challenges and support local value chains in a bid to narrow the widening poverty gaps and redress inequalities. 

  At the same time, Rt Hon Kidega says Parliaments should appropriate more resources in the States’ budgets to check on rising inequalities and hold Executive accountable on the same. 

  The Speaker was addressing the 136th Inter-Parliamentary Union Assembly (IPU) taking place in Dhaka, Bangladesh.    The annual event which is themed: Redressing inequalities: Delivering on dignity and well-being for all” brings together over 50 Speakers and 1400 legislators from the globe.

  In his remarks, Rt Hon Kidega maintained that despite the emergence of BRIC countries and other economies as well as attempts to generate wealth, much more was needed to reduce the inequality and to raise the standards of living.

  He said the East African Community region had similarly been gravely affected by inequalities. “The State of East Africa Report 2016 depicts not all citizens have seen or felt the benefits of increasing national GDP figures at the individual/family front. If anything, life continues to be harsher and harder. The economic boom has not generated the jobs as was expected, while levels of poverty and malnutrition remain high”, the Speaker said, while remaining optimistic the trend could be reversed.

  The Speaker cited issues contributing to inequality as disparity in income levels throughout the world, uncertain political environments, the gender norms and stereotypes and the imbalance of economic power.

  In many countries, Rt Hon Kidega said, fruits of economic development increasingly failed to reach those who deserve the same – instead benefitting companies, financial services and vested interests. He said the rate of unemployment in the globe was similarly high.

  “Statistics in East Africa reveals that 7 out of the 10 persons you see walking in the streets are jobless, while another 6 out of 10 live in informal settlements. Yet, the largest population, the youth, constitute about 8 out of 10 persons and their age range is below 30 years”, Such is replicable in many parts of the globe”, he noted.

  The Speaker called on Parliaments to enact relevant legislation to make greater impact.   He informed the convention that EALA had legislated a number of pieces that protect society and address inequalities including; the EAC Persons with Disabilities Bill, 2016, the EAC Gender, Equity and Equality Bill, 2016, the EAC Conflict Management Bill, 2011 and the EAC Human and Peoples Rights Act 2011.

  “He further called for dialogue to resolve political issues saying politically instigated inequalities more often than not arise from disputed elections and uncertainties which result into conflicts and sometimes wars.    The ramifications are sometimes too much to bear leading to refugee crises and instabilities in the nations”, Rt Hon Kidega said.

  Analysts contend that Poverty reduction is often compromised by income inequality. The International Monetary Fund (IMF) urges poor and resource rich nations to simultaneously explore reduction of inequality and bolster long-term economic growth.  However, inequality correlates to shorter spells of economic expansion and volatility to crises.  

  The 136th IPU was opened by the Prime Minister of the Republic of Bangladesh, Hon Sheikh Hasina at the Parliament of Bangladesh yesterday. The Prime minister thanked delegates for electing Bangladesh as the chair of both Inter Parliamentary Union (IPU) and Commonwealth Parliamentary Association (CPA). The Prime minister mentioned her government’s short, medium and long-term initiatives for the development of the country and said the government is making stride to build the country in a planned way.

  “The 100 Million young people are prepared to make the world a better place. Let us not make them frustrated. They are the face of change and let us globalise human compassion”, he said.

  The Emergency items include a call for urgent international action to save millions of people from famine and drought in parts of Africa and the Yemen jointly presented by the Republic of Kenya together with Belgium and the United Kingdom. Speaker of the Senate of Kenya, Rt Hon Ekwe Ethuro, presented the merged proposal to the Assembly yesterday.

  “We need to request for international organisations to come to the aid of the affected nations.  Without global action, people will simply starve to death”, the Speaker remarked.The Speaker of the Parliament of Uganda, Rt Hon Rebecca Kadaga and the Speaker of the Burundi National Assembly, Rt Hon Pascal Nyabenda also addressed the Assembly.

  In attendance also are a delegation of the Parliament of Rwanda led by the Deputy Speaker and legislators from the Transitional Assembly of the Republic of South Sudan.

  The Inter-Parliamentary Union (IPU) is the global organization of national Parliaments. It works to safeguard peace and drives positive democratic change through political dialogue and concrete action. To that end, IPU fosters contacts, co-ordination, and the exchange of experience among Parliaments and Parliamentarians of all countries. IPU also contributes to the defence and promotion of human rights - an essential factor of Parliamentary democracy and development.  EALA is an Associate Member of the IPU.  0 0  0 0

  MFUKO wa uwekezaji wa pamoja wa UMANDE UNIT TRUST (UUT) leo umezindua rasmi mpango-mkakati wake wa kifedha utakaowawezesha wawekezaji wadogo na wale wenye kipato cha chini na cha kati waweze kununua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kupitia njia ya vipande.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CORE Capital Limited ambayo ndio iliyobuni mfuko huo, Bw George Fumbuka  alisema kiwango cha chini cha ununuzi wa hisa za Vodacom ni 85,000/= (hisa 100 kwa 850/= kila hisa), kwa mkupuo kinaweza kuwa kiasi kikubwa kwa wawekezaji wadogo wadogo, wa kipato cha chini.

  “Mantiki ya mkakati huu ni kuwakusanya pamoja wale wote wenye mitaji midogo ili waweze kwa pamoja kufikia viwango vinavyohitajika katika ununuzi wa hisa za VODACOM. Kima cha chini ni shilingi 13,500 tu, yaani vipande 100 vya shilingi 135/= kila kimoja. Dhana hii si mpya kwa Watanzania; mara nyingi tu hutumika kwenye shughuli za pamoja, huitwa “UMOJA NI NGUVU”.’’ Alisema

  Alisema mpango huo pia utatoa fursa kwa wawekezaji wa kigeni wakiwemo watanzania wanaoishi nje ya nchi (diaspora) kuweza kunufaika na hatua hiyo ya serikali kwa kuwa uuzwaji wa hisa hizo kupitia soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) hautoi fursa kwa wawekezaji wa kigeni.

  “Kwa kuwa mauzo ya hisa hizo hapa nchini hayahusishi wawekezaji wa kigeni wakiwemo watanzania wanaoishi nje yaani Diaspora, milango ipo wazi kwao kupitia mfuko wa uwekezaji mtaji wa Umande (Umande’s capitalisation fund),utakaowawesha kununua vipande badala ya wao kwenda moja kwa moja kwenye soko la hisa,’’ alisema.

  Zaidi Bw Fumbuka aliwahakikishia walengwa wa mpango huo kuhusiana na uhakika wa wao kujipatia gawio na faida zitokanazo na mtaji (dividends and capital gains) kama kawaida kwa kuwa thamani ya vipande itakwenda sambamba na thamani ya hisa za kampuni hiyo ya huduma za simu za mkononi.

  “Mpango mkakati huu una baraka zote za Kampuni ya Vodacom na za Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA) chini ya Kanuni za Mifuko ya Uwekezaji ya mwaka 1997.” Alibainisha.

  Hata hivyo alifafanua kwamba watakaopitia mkakati huo, wawe ni wawekezaji wadogo wadogo au wale wa nje, hawataweza kumiliki hisa za VODACOM moja kwa moja; badala yake watamiliki vipande vya Mfuko utakaopatikana kwa michango yao.

  “Kwa maana hiyo Mfuko wa UUT ndiyo utanunua hisa za VODACOM kwa niaba yao na watafaidi matunda ya uwekezaji kwa njia hiyo. ‘’ alisema huku akiongeza kuwa Vipande vitanunuliwa kwa njia ya simu tu: *150*36#, huku kima cha chini kikiwa ni Tsh 13,500/=.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CORE Capital Limited ambayo ndio iliyobuni mfuko huo, Bw George Fumbuka (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo mpango-mkakati unaoendeshwa na kampuni hiyo kupitia Mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa UMANDE UNIT TRUST (UUT) utakaowawezesha wawekezaji wadogo na wale wenye kipato cha chini na cha kati waweze kununua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kupitia njia ya vipande. Wengine ni Meneja wa Mfuko huo Bi Sandra Felician na Naibu wake Bi Nkunde Shoo  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Tanzania ni Moja ya nchi salama kwa ajili ya uwekezaji barani Afrika kwa sababu haina matatizo ya migogoro ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa mali ya wawekezaji ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonyesho ya Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.

  Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Ufaransa kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa katika kilimo, nishati, utalii,usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

  Makamu wa Rais amesema maonyesho hayo ya kibiashara ambayo yataambatana na kongamano kubwa la Kibiashara kati ya nchi hizo Mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kukutana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kibiashara na uwekezaji.

  Ameeleza kuwa katika kuelekea katika uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa ambayo yamekuwa na teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwemo taifa la Ufaransa.

  Makamu wa Rais amewahakikishia wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza nchini kuwa serikali itafanya kila linalowekezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji.

  Amesema katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha kazi ya usafiri na usafirishaji nchini.

  Kwa upande wake, Balozi Ufaransa hapa nchini Malika BERAK amesema kuwa ufunguzi wa Kongamano hilo kubwa la Kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo Mbili.

  Balozi huyo amesema kuwa kongamano hilo litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.
  Kongamano hilo la siku Nne la Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania litawakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Ikulu- Dar es Salaam.
  4-April-2017


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
  Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bibi. Melika Berak akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bibi. Melika Berak wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dkt. Reginald Mengi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo alipotembelea banda la Kampuni ya Supperdoll (wasambazaji wa Matairi aina Michellin) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Kutoka kulia kwake ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini Melika Berak na Mkurugenzi Mtendaji wa Supperdoll Seif Seif(kushoto).

older | 1 | .... | 1191 | 1192 | (Page 1193) | 1194 | 1195 | .... | 1896 | newer