Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1190 | 1191 | (Page 1192) | 1193 | 1194 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na kuhamia CCM

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kutokana na chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.

  Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko.

  Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.

  Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini zinazotekelezeka .

  Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.

  “Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia.... sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.

  “Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema na nitajiunga na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John Magufuli sababu Chadema wameacha sera na makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.

  Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari wa mbele kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa nchini.

  Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho. 
   
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara maalum.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara maalum.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara maalum.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo kwa ziara maalum akiwa na ujumbe aliofuatana nao,(Picha na Ikulu) 02/04/2017.

  0 0

  : Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Watumbuizaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi.


  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga (kulia) akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017.
  Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye miwani) akiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo ya mwenge wa uhuru 2017 kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi

  Watoto wa alaiki wakitengeneza umbo la mlima Kilimanjaro na kuweka alama ya mwenge wa uhuru kuashiria kupandisha kwa mwenge huo katika mlima Kilimanjaro wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukabidhiwa mwenge huo kuukimbiza kwa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akimpa mkono wa baraka kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour kabla ya kumkabidhi mwenge huo kuukimbiza katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi 

  Wananchi Mkoa wa Katavi wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kujenga uchumi wa viwanda nchini. 

  Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi na kusema kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni ule utakaolifanya taifa kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za viwanda vya mataifa mengine. 

  “Tanzania tumeazimia kutoka katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao utahusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta binafsi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan katika uwekezaji mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na upatikanaji wa rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi Iddi. 

  Aidha Mhe. Balozi Iddi amesema kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika kujenga na kuendeleza viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda unaanza kwa jitihada za wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa wanazozalisha kila siku katika maeneo yanayowazunguka. 


  Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Katavi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mbio za mwenge wa uhuru zimekua zikihamasisha amani, mshikamano, kujenga uzalendo na umoja wa kitaifa kwa kuhamasisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ipo sambamba na malengo ya serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda kwa kufufua viwanda vilivyopo kuanzisha viwanda vidogo vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa. 

  Mwaka huu, ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unahusu Mkakati wa kukuza Viwanda nchini, chini ya Kauli Mbiu isemayo:- “Shiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu”. Ujumbe huu utaambatana na msisitizo wa Serikali kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa. 


  Mwenge wa Uhuru uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Hatua hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa ndoto yake iliyotafsiriwa kwa maneno aliyoyatamka mwaka 1958 kwa wajumbe wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria na kuyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa wakati huo akidai Serikali ya madaraka kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika kwa kusema “Sisi watu wa Tanganyika, tungependa kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipo jaa dharau”.Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ujumbe mkubwa kwa Waingereza kwamba, watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. 

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akisoma taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara katika mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi, Maliasili na Utalii - Dodoma. 
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii; Mhe. Atashasta Ndetiye akiongoza majadiliano wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati yake na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake - Dodoma.
  Mbunge wa Korogwe mjini, Mhe. Mary Chatanda akishiriki mjadala wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake – Dodoma. 

  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-
  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.


  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.

  Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.

  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.

  0 0
  Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, kesho Jumatatu itapambana na Black Starlets ya Ghana kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


  Katika mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni, Serengeti Boys itautumia kama ni ishara ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.

  Lakini kabla ya kutua Gabon, Serengeti Boys itakwenda Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, mwaka huu. Ikiwa huko angalau itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri. Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka hu ambako timu itasafiri hadi Cameroon.

  Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

  Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon na Guinea.

  Kila la kheri Serengeti Boys katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Afrika kadhalika kucheza fainali za Kombe la Dunia hapo Novemba, mwaka huu zitakazofanyika India. Serengeti Boys inaweza na Mtanzania tunakuomba kuichangia timu hii kwa namna ya 223344 kupitia mitandao yote ya simu.

  0 0

  Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake aliyefariki mwaka 2011.

  Akizungumza na kuonyesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba 2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki.

  Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika.

  Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha zitakazopatikana ziwasomeshee watoto ambao mmoja yupo kidato cha tano sasa hivi na mwingine cha kwanza.

  Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki wa Royal Village Hotel iliyopo Temeke na ameuziwa na kaka wa marehemu lakini katika hati ya mauzo ikiandikwa Alfred Athanas Kyoma akishirikiana na mtoto wa Marehemu.

  Majirani wa nyumba hiyo Wamesema kuwa siku chache zilizopita waliona watu wakivunja nyumba na kuingia ndani na kutoa vitu ndani vya mpangaji anayekaa hapo ambaye alikuwa amesafiri.

  Kwa sasa nyumba hiyo imewekwa mlinzi ambaye jitihada za kumwambia afungue zilishindana baada ya kugoma kuruhusu watu kuingia ndani na imeuzwa kwa kiasi cha shiliingi milion sitini (60

  0 0  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana ikawa ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo wa leo Simba wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni wakiwa na pointi 56 baada ya michezo 25.
  katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph Huku bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili.
  Kwa matokoe hayo yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.Zacharia Hans Poppe akiwa hana hamu baada ya kushuhudia Timu ya Simba ikinyukwa bao 2-1 na Timu ya Wanankurukumbi Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kagera Sugar leo hii jumapili.  Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime akisalimiana na Mayanja wa Simba leo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.


  Mashabiki waliingia kwa wingi kwenye Mtanange huo ulikuwa na hamsha hamsha ya kila aina yake.  Kikosi cha Simba kilichoanza

  Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wakiwa jukwaa kuu kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar kuanza.  Kikosi cha Kagera Sugar kikiomba kabla ya mtanange kuanza

  Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi Simba ya Jijini Dar es salaam.

  Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusuph  Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haamini kilichotokea baada ya timu yake kufungwa bao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa uwnaja wa Kaitaba mjini Bukoba.

  Mbaraka akipongezwa kwa bao

  Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog

  Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haaminiTimu yake ikiwa nyuma ya bao 2-0

  Hadi mapumziko Simba walikuwa nyuma ya bao 1-0
  Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .  Kichuya Akiambaa na Mpira

  Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea.Kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla akiachia Shuti kali ambalo lilipanguliwa na Kipa Juma KasejaKiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

  Meza kuu

  Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar akiwa amebebwa na Wachezaji wa Kagera mara baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.  Simba walipata bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 61 na mtanange kuwa 2-1  Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa pamoja na Mlinda mlango wao Juma Kaseja.

  Mtanange ulipomalizika Kipa Kaseja alipewa zawadi na Mashabiki wa Kagera Sugar pamoja na Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

  0 0


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16,2017 kwenye Uwanja wa Uhuru.

   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amesema kuwa wakati uzinduzi wa tamasha la pasaka April 16,2017 katika Uwanja wa Uhuru, mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Mchemba atakayemwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mgeni rasmi katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma atakuwa ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavumde.

  Msama alisema baada ya Tamasha hilo kutikisa vilivyo katika Uwanja wa Jamhuri mbele ya Naibu Waziri Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, tamasha hilo litahamia katika jiji la Mwanza, Simiyu na Iringa.

  Alisema kamati yake imeamua kuufikia mji wa Dodoma kutokana na watu wake kulipenda Tamasha hilo, pia heshima ya Dodoma kama mji mkuu wa nchi na makao makuu ya serikali.

  "Pamoja na mambo mengine yanayokwenda na tukio hilo, malengo ya msingi ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu, pia kutumia sehemu ya mapato kufariji watoto yatima, walemavu na wajane".alisema Msama

  Wakati huo huo,Msama alisema kuwa katika tamasha hilo Albamu mpya ya ‘Jitenge na Ruth’ ya malkia wa muziki wa injili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, itazinduliwa rasmi.

  Msama amesema kuwa,Rose Muhando mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini ambaye amekuwa akishiriki mara kwa mara katika tamasha hilo,kwa mara nyingine atalitumia jukwaa hilo la tamasha la Pasaka kuzindua albamu yake.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam ,Alex Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo,alisema albamu hiyo yenye nyimbo kibao, itazinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru.

  Msama alisema tukio la uzinduzi wa albamu hiyo na ile ya ‘Ngome Zimeanguka’ ya Kinondoni Revival, anaamini Tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti.

  Alisema uwepo wa Rose, Kinondoni Revial Choir, Kwa ‘Viumbe Vyote’ ya Tabora na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na wengine mahiri, ni faraja kubwa kwa wadau wa Tamasha hilo.

  Msama alisema, baada ya uzinduzi wa nguvu katika Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akifafanua kwa kina uzinduzi wa albamu mbili,katika tamasha la pasaka  litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.

  0 0

  Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika kongamano hilo lililo andaliwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama Mh. Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wote waliohudhuria katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo kikuu cha Dar es salaam.
    Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na Kumkaribisha Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo
  Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano hilo
   Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi ya mwanamke katika uongozi.
  Meneja wa Benki ya NMB PLC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salalaam Bi. Rehema Mwibura akielezea safari yake ya uongozi mpaka hapa alipofikia sasa na kuwaatha vijana wakike wasikate tamaa kwa kuwa wanaweza.
   Mwanachama wa zamani wa USRC Bi. Yunge Kanuda akiwasihi vijana wanawake kuwa wanayo nafasi ya kugombea ngazi mbalimbali za uongozi hivyo wanatakiwa wathubutu ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali.
  Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali inayoendelea
  Aliyekuwa Spika wa Bunge la USRC kwa mwaka 2014/2015 Protus Petro akielezea juu ya uongozi 
  Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Irene Ishengoma na aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus 2016 akielezea mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake na kuwasihi kuto bweteka kwa kuwa wanaweza.
   Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiuliza maswali na kuchangia mawazo katika Kongamano hilo.
   Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Consolata Chikoti akifuatilia kwa makini mijadala ikiendelea.
   Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wazungumzaji wakati wa Kongamano hilo.
    Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wanawake na Uongozi
    Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam.
   Picha ya pamoja ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni Asasi,vyuo na shule shule mbalimbali
  Washiriki wakiwa katika Kongamano hilo.
  Picha zote na Fredy Njeje

  Na Dickson Mulashani

  Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama, aliandaa kongamano kubwa lililohusisha watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule za Sekondari,wanavyuo,taasisi na asasi za kijamii kwa lengo la kuzungimzia masuala mbalimbali yanayowahusu vijana hasa vijana wa kike na dhana ya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwanamke katika uthubutu wa kuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

  Akizungumza katika kongamano hilo mgeni Rasmi katika ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yake katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali bila wasiwasi.

  Mh. Sophia aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke tamaa hizo.

  Kadhalika aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa wao wanaona mambo mengi zaidi katika jami.

  Mwisho alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneo la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu, alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi zaidi.     

  Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa " GPF ni ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla."

  Mathalan Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndio mfano kwao "Role Model" watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya chini mpaka uongozi wa juu.

  Nae Mkurugenzi wa  wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo pamoja na kutoa ufafanuzi wa historia za viongozi wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania alisema kuwa nia ya wanawake katika uthubutu wa katika kutafuta nafasi mbalimbali bado hauridhishi kwani safari ya kupambana na mfumo dume hata kwa wanawake wasomi bado ni ndefu


  0 0


  Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) chini ya udhamini wa Kampuni ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (Kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) na kupata udhamini kutoka kwa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuadhimisha hafla hiyo. Katikati ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu(wa pili kulia) akifafanua kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo. Kulia ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwaongoza wanafunzi na baadhi ya wakufunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kucheza nyimbo ya “Strength of a woman” ya Mwanamuziki Shaggy ambayo ina maudhui ya kuwainua wanawake wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
  Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya jinsia wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr. Eugenia Kafanabo akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
  Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Zanaki wakifuatilia hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kiwani na vitongoji vyake katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Mgagadu -Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba uliofanyika jana,akiwa katika ziara maalum ya kikazi Kisiwani humo,(kutoka kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (GAVU) akifuata Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano Miundombinu Mhe,Ali Abeid Karume .
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla alipokuwa akiwasalimia Wananchi wa Kiwani na vitongoji vyake katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Mgagadu -Kiwani Mkoa wa Kusini Pembailiyozinduliwa na jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara maalum ya kikazi Kisiwani humo,[Picha na Ikulu.] 
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Mgagadu -Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba iliyozinduliwa na jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara maalum ya kikazi Kisiwani humo.
  Wananchi wa Kiwani na Vijiji jirani katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao jana katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Mgagadu -Kiwani,akiwa katika ziara maalum ya kikazi Kisiwani humo

  0 0


  0 0


  Serikali imewaagiza waajiri wote na watumishi wa umma kwa ujumla wao, kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha fani na taaluma zilizopo katika sehemu za kazi. 

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 26 ya TPSC Mkoani Tabora, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, akisema Chuo hicho kikitumiwa ipasavyo, ufanisi sehemu za kazi utaongezeka. 

  “Kwa nafasi yangu kama waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, tunaahidi kukijengea chuo uwezo na kukiongezea ufanisi katika utoaji huduma ya taaluma bora na ujuzi katika maeneo yetu ya kazi,”alisema. 

  Alisema serikali siku zote imejitahidi kuhakikisha kwamba TPSC inatoa kozi ambazo zinatambulika katika mfumo wa elimu ili wahitimu waweze kukubalika katika soko la ajira badala serikali peke yake. 
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki akizungumza wakati ma mahafali ya 26 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania(TPSC) mjini Tabora hivi karibuni.
  Meza kuu, akiwamo Mtendaji Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo (Wa tatu kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki wakati wa mahafali ya 26 ya TPSC yaliyofanyika TPSC tawi la Tabora mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora, Hussein Simon Lufunyo, akimweleza jambo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki wakati Waziri huyo alipotembelea jingo la chuo hicho linalojengwa kwa ajili ya madarasa na ofisi,wa pili kushoto Dk.Charles Msonde Mwenyekiti wa Bodi ya Taaluma ya chuo hicho, Wa nne kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo
  Mtendaji Muu wa TPSC Dk.Henry Mambo akifuatilia kwa makini moja ya matukio wakati wa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, alipotembelea jengo la ghorofa tawini hapo, jengo hilo litatumika kwa madarasa na ofisi 
  Serikali imewaagiza waajiri wote na watumishi wa umma kwa ujumla wao, kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha fani na taaluma zilizopo katika sehemu za kazi.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 26 ya TPSC Mkoani Tabora, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, akisema Chuo hicho kikitumiwa ipasavyo, ufanisi sehemu za kazi utaongezeka.

  “Kwa nafasi yangu kama waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, tunaahidi kukijengea chuo uwezo na kukiongezea ufanisi katika utoaji huduma ya taaluma bora na ujuzi katika maeneo yetu ya kazi,”alisema.

  Alisema serikali siku zote imejitahidi kuhakikisha kwamba TPSC inatoa kozi ambazo zinatambulika katika mfumo wa elimu ili wahitimu waweze kukubalika katika soko la ajira badala serikali peke yake.

  0 0

  "Ni simanzi kubwa, baba yetu mdogo, Profesa Lloyd Manamba Binagi, amefariki dunia hii leo Jijini Dar es salaam.

  Taratibu za kuusafirisha mwili kwenda nyumbani Tarime zinafanyika. Pumzika kwa amani baba, ulikuwa nguzo muhimu kwetu, daima tutakukumbuka, Amina". George Binagi.


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai kabla ya kuanza kwa mkutano wa wabunge wa kupeana taarifa (briefing) kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma Aprili 3, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai kabla ya kuanza kwa mkutano wa wabunge wa kupeana taarifa (briefing) kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma Aprili 3, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha (Kushoto) na Mkuu wa Matawi na za Huduma za kibenki, Bw. Kitumari Massawe (Kulia) wakishilia Bango wakati wa mkutano na waandishi wa habari kama ishara ya kuanzisha huduma ya kutoza gharama moja kwa miamala ya kibenki kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya Hundi. (Picha: Mpiga Picha Wetu)
  Mkuu wa Matawi na Huduma za Kibenki, Bw. Kitumari Massawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya faida ya akaunti ya Gold ya Hundi ambapo wateja watalipa shillingi elfu kumi na sita kwa mwezi ambayo ni gharama moja na kuondoa adha na utaratibu wa kulipa huduma kwa muamala mmoja mmoja.( Kushoto) ni Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki hiyo, Bw. Francois Botha na Meneja Masoko wa First National Bank, Bi. Blandina Mwachang’a (Kulia).
  Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha ( Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kutangaza benki hiyo kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wanatumia akaunti ya Gold ya Hundi. ( Kushoto ) ni Mkuu wa Matawi na Huduma za kibenki wa First National Bank, Kitumari Massawe.

  First National Bank Tanzania imetangaza kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya hundi ikiwa ni mojawapo ya jitihada za benki hiyo kuwapa unafuu watumiaji wa huduma za kibenki. Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha amesema jijini Dar es salaam leo kwamba benki hiyo itawapatia wateja wake fursa ya kufanya miamala mbalimbali ya huduma za kibenki mara nyingi wawezavyo kwa gharama moja iliojumuishwa na bila kulipa gharama za ziada. 

  “Wateja watalipa shilingi elfu kumi na sita tu kwa mwezi ambayo ni gharama moja, hii itaondoa adha na utaratibu wa kulipia huduma kwa muamala mmoja mmoja. Mpango huu unatarajiwa kuwanufaisha wateja wetu kwa kuwapunguzia gharama za miamala huku wakitumia fedha hizo kujiongezea akiba zaidi kwenye akaunti zao. Hatua hii ni ya faida kubwa kwa wateja wetu wa akaunti ya Gold ya hundi na wateja wengine kwa ujumla”.

  Mpango wa gharama moja kwa miamala utajumuisha utoaji wa fedha kwenye ATM yoyote, miamala ya TigoPesa, malipo ya bidhaa kama DSTV, LUKU na muda wa maongezi, kuweka maelezo ya kuhamisha fedha toka kwenye akaunti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia kadi katika vituo vya mauzo popote duniani, pamoja na kuweka fedha taslimu na hundi kwenye akaunti ikiwemo kwenye mpango huu.

  0 0


  Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga ,akizungumza jambo na waandishi wa habari. (picha na Mwamvua Mwinyi)

  ……………….
  Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji

  WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

  Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.

  Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.

  Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi. “Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “

  “Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga. Alieleza,askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.

  “Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “

  “Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.

  Aidha alibainisha baada ya hapo watu hao waliruka kwenye pikipiki na kuanza kukimbilia msituni na ndipo askari walipowapiga risasi za miguu na kiunoni na kufanikiwa kuwakamata.

  “Majeruhi hao walijulikana ni wanaume hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika na walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 272 BLW aina ya Boxer yenye rangi nyeusi”

  “Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu kwa mwonekano wao walijaribu kuwawahisha hospitali ya Misheni ya Mchukwi,” alisema Lyanga. Lyanga alisema walipofikishwa hospitali daktari alithibitisha kuwa watu hao wamefariki dunia .

  Hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika huku pikipiki nyingine mbili zilitoroka na kuelekea mkoa wa Lindi na taarifa zimetolewa polisi ili wawakamate.

  Aliwataka wananchi kuwa watulivu pale wanaposimamishwa na askari polisi badala ya kujaribu kutoroka na kwa sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika kukabiliana na uhalifu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya msingi Mrusha Anna Nathan kwa niaba ya wanafunzi wenzake pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwa ajili ya kununua sukari ya kuweka katika uje wa wanafunzi. (Picha habari na Ruvuma TV ). Wanafunzi wa shule ya msingi Mrusha wilaya ya Tunduru mkoani Tuvuma wapo hatari kudondokewa na kuta za madarasa wanayoseomea kutona na madarasa hayo kuwa na nyufa za muda mrefu, Habari kamili hii hapa video yake.

  0 0


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
   
  Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu (Sumatra) pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji wamekubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliotakiwa kuanza kesho.
   
  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitisha huko kunatokana na kikao na waziri mwenye dhamana, Profesa Makame Mbarawa juu ya kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki.
   
  Amesema kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea usafirishaji.
   
  Ngewe amesema kuwa baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kupeleka bungeni.
  Nae Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Abdallah Mohamed amesema wamekubaliana na Sumatra mambo ambayo hayakuwa sawa warekebishe katika kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
   
  Amesema wasipokubaliana baada ya siku 14 watarudi katika mkutano mwingine kwa kila mmoja namna gani ya kuweza kutengeneza sheria ambazo haziathiri upande mmoja.Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala , Kasmat Jaffer amesema suala ambalo limekuwa mwiba ni kosa la kufungwa pamoja na faini hali ambayo wameona ni bora kuachana na biashara hiyo.
   
  Picha ya Maktaba Yetu,

older | 1 | .... | 1190 | 1191 | (Page 1192) | 1193 | 1194 | .... | 1897 | newer