Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1189 | 1190 | (Page 1191) | 1192 | 1193 | .... | 1898 | newer

  0 0  Na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Tanzania inategemea kupata Megawati 400 za umeme kutoka Ethiopia ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyofikiwa baada ya ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Haile Mariam Desalegn. 

  Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya makubaliano na mikataba ambayo nchi za Tanzania na Ethiopia wametiliana saini leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  “Tukitaka kujenga uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na umeme wa kutosha,wenzetu Ethiopia wametuonyesha njia na mimi nimemuomba Mhe.Waziri atusaidie wataalamu kutoka nchini kwake ili  waje  tuwaonyeshe maeneo mbalimbali watusaidie katika kupata umeme wa uhakika kwa kujenga mabwawa ya umeme ambayo yamesaidia sana katika kupatikana kwa umeme wa kutosha nchini kwao.”Aliongeza Rais Magufuli.

  Aidha amesema kuwa kupatikana kwa umeme huo kutasaidia kuleta changamoto kwa shirika la umeme nchini katika kuwapatia wananchi bei ya chini na hivyo kuleta ushindani katika upatikanaji wa umeme nchini.

  Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Haile Mariam Desalegn amesema kuwa wana mengi ya kujifunza kutoka Tanzania kwani nchi hizi mbili zina historia inayofanana na kuongeza kuwa hakuna haja ya wao kwenda nje ya Afrika kupata uzoefu katika masuala mbalimbali.

  Ameongeza kuwa lengo kuu la kuja nchini ni kwa sababu anahamini nchi hizi mbili zinaweza kuunganisha nguvu zake na kuwa nguzo kuu katika maendeleo katika eneo la ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

  “Tanzania na Ethiopia ni nchi ambazo zina ushirikiano mzuri sana,sisi sio washindani bali tunasaidiana katika masuala mbalimbali kwani tumekuwa katika hatua mbalimbali za kuwaondoa wananchi wetu katika umaskini katika hatua zinazofanana,na huu ni wakati muafaka katika kuimarisha ushirikiano wetu kwa faida ya watu wetu kwa ujumla”Alisisitiza Mhe.Desalegn.

  Aidha amesema  kuwa  mabadiliko  ya  kilimo  katika  nchi  zetu ndio  msingi  wa  maendeleo  pamoja  na  utumiaji  wa  teknolojia  bora utasaidia katika maendeleo ya viwanda vidogo vidogo.

  Viongozi hawa wamekubaliana kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu juu ya namna sekta mbalimbali zitakavyoleta manufaa ya kiuchumi zikiwemo huduma za benki, madini na gesi, elimu na  mawasiliano.

  Ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Haile Mariam Dessalegn imekuwa ya manufaa makubwa kwa Tanzania na amesisitiza kuwa wakati umefika wa kukuza biashara kati ya nchi hizi ambazo kwa sasa thamani ya biashara kati yake ni Dola za Marekani milioni 2.24 tu.

  0 0  0 0

  Wananchi wa mtaa wa Nyantorontoro “A”Kata ya Nyankumbu wakikwa kwenye shughuli ya kujitolea ya utengenezaji wa Barabara.

  Shule ya Msingi ambayo wananchi wamejitolea kutengeneza Barabara ya kufika shuleni Hapo.
  Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorontoro Gerevas Kayelelo kulia akifokeana na moja kati ya wananchi ambaye hakutaka eneo lake kuondolewa mihogo ambayo alikuwa amepanda.


  Elias Totoe mkazi wa nyantorotoro akizungumza namna ambavyo wameweza kufikia uwamuzi wa kutoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya mitaa.

  Lecta Maningu mkazi nyantorotoro akieleza juu ya tatizo la maji ambavyo limekuwa ni changamoto katika kata hiyo.

  Wananchi wakionesha vitendea kazi

  Gerevas Kayelelo m/kiti mtaa wa Nyantorotoro A,akifafanua juu ya uwamuzi wa wananchi kujitokeza kwenye shughuli ya utengenezaji wa barabara.

  Barabara ni moja Kati ya huduma muhimu za kijamii zinazohitajika ili kurahisha na kuchochea kasi ya maendeleo lakini maeneo yaliyo mengi hapa nchini yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya miundombinu hiyo ambayo inarahisisha kasi ya maaendeleo. Kutokana na hali hiyo wananchi wa mtaa wa nyantorotoro “A” kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wamejitokeza kutengeneza barabara ya kiwango cha molamu yenye kilomita zipatazo mbili kuelekea kwenye taasisi ya shule mpya ya mtaa huo.

  Baadhi ya wananchi wamezungumza na mtandao wa Maduka Online na kwamba wamejitolea kutengeneza Barabara kwa ushirikiano ni kutokana na muda mrefu kutokuwepo kwa barabara na shule kwenye mtaa huo.

  “Kiukweli watoto wetu wamepata shida kwa muda mrefu na kusoma umbali wa kilomita nyingi kutokana na shule kukamilika tumeonelea basi sisi pamoja na mwenyekiti wetu wa mtaa kuweka jitihada za kutengeneza barabara ambayo itaelekea shuleni na itawasaidia watoto wetu kutembea kwa ukaribu kufuata elimu”alisema Lecta Maningu. 

  “Pamoja na kwamba sisi kama wananchi tumejitolea kujenga barabara ambayo inaelekea shuleni lakini tunaiomba serikali yetu kupitia kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kuona umuhimu wa kuweka maji
  shuleni hapo ili kupunguza adha kwa wanafunzi shuleni hapo kwani hakuna maji”aliomba Bi, Cesilia Clement

  Lakini pamoja na baadhi ya wananchi kutoa maeneo yao kwa hiyari ili kupitisha barabara, wapo wengine wanakwamisha juhudi za wengi kufikia malengo hayo, kama mzee aliyetambulika kwa jina la Mayenga ambaye ameonekana mgumu wa kutoa eneo lake lililolimwa mihogo jambo ambalolimesababisha malumbano makali baina yake na wananchi.

  Mwenyekiti wa Mtaa huo Gerevas Kayelelo, alisema kuwa wananchi wake wametoa ardhi yao kwa ajili ya barabara bila kuomba hata fidia ya aina yoyote.  Maduka online hadi inaondoka katika mtaa huo imeacha wananchi wakiendele na ujenzi wa barabara kwenye Shamba la Mzee Mayenga
  lenye ukubwa wa mita 150.  IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

  0 0
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Elizabeth Titus Munthali, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Honest Amedeus Matem, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Annastacia Mbunda, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Salim Ngailo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Lauden Cheyo, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Charles Peter Moshi, wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Jengo la Kibiashara la Haidary Plaza jijini Dar es Salaam, leo. 
  Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia Hotuba ya mgeni rasmi.
  Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.akizungumza wakati wa maafali hayo.
  Meza Kuu.
  Rais wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, akisoma hotuba yake wakati wa maafali hayo.
  Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba.akitoa neno la shukrani katika maafali hayo.
  Sehemu ya ndugu na marafiki wa Wahitimu wakiwa katika maafali hayo.
  Mtoa mada katika maafali hayo, Gabriel Mwero, akitoa mada.
  Baadhi ya Wahitimu waliopokea vyeti katika mahafali hiyo,wakimsikiliza mgeni rasmi.
  Mkaguzi Msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi, akitoa mada katika mahafali hiyo.
  Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, (kulia) akiteta jambo na Rais wa Taasisi hiyo ya Usimamizi wa Vihatarishi, Pius Maneno, wakati wa hafla hiyo ya maafali katika ukumbi wa Hydary Plaza.
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wahitimu wa Taasisi hiyo.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini  Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Justinian Rwezaura Ikungula Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Joseph Buchweishaija Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali  hapa nchini mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiagana na Waziri Mkuu wa Shirikisho la Kidemokrasia la Jamhuri ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini. Wakati wa ziara hiyo pamoja na mambo mengine alimaliza kwa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na Mhe. Dessalegn ameahidi kuitumia Bandari hiyo kupitisha mizigo ya nchi yake pamoja na kufanya biashara na nchi za Afrika Mashariki.Ziara hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili, 2017.
  Mhe. Dessalegn akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akiagana na Mhe. Dessalegn.
  Waziri Mkuu, Mhe. Dessalegn akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini
  Waziri Mkuu, Mhe. Dessalegn akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Innocent Shiyo mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini
  Waziri Mkuu Dessalegn akiagana na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Zulekha Tambwe.
   Mhe. Dessalegn akimpungia mkono wa kwaheri Rais Magufuli, viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi (hawapo pichani) waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuaga  mara baada ya kumaliza rasmi ziara yake nchini.
  Rais John Pombe Magufuli (wa kwanza kulia), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa pamoja wakimpungia mkono wa kwaheri kumuaga Mhe. Dessalegn,

  0 0

  Kocha Msaidizi wa timu ya Maji Maji (Wanalizombe) , Habibu Kondo amewahakikishia wanachama wa Club ya Maji Maji na wadau wa soka mkoani Ruvuma kuwa timu hiyo haitashuka daraja , hivyo wawe na amani katika michezo hii iliyobakia lazima Maji Maji itashinda na kubaki ligi kuu Tanzania bara.

  0 0


   Kufuatia uteuzi wa Bibi Blandina S.J. Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25/02/2017.  Mhe. William V. Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, amewateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa.
  Aidha, uteuzi huu ni wa kipindi cha miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 23 Machi, 2017.
   Majina ya wajumbe hao ni kama ifuatavyo:
  1. Prof. John M. Lupala
  2. Bwn. Gabriel Malata
  3. Bi. Mary Mlay
  4. Bi. Subira Mchumo
  5. Bwn. Ally Hussein Laay
  6. Bwn. Pius Maneno
  7. Bwn. Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita
  Imetolewa na:
  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipanda mti wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Upandaji Miti, kilichofanywa na Wilaya ya Ilala katika shule ya Msingi, Yangeyange, Kata ya Msongola wilayani humo mkoani Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ya Ilala Edward Mpogolo na Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando

  Msongola, Dar es Salaam
  MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa kuhakikisha wanazuia shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi na kilimo katika maeneo oevu ili kulinda mazingira.

  Amewasisitizia wananchi umuhimu wa kupanda miti mingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuzuia magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababishwa na hali ya hewa.Mjema amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti duniani, ambayo wilaya ya Ilala iliyafanya shule ya msingi Yangeyange katika Kata ya Msongola wilayani humo.

  Alisema mbali na kutunza mazingira na kuleta mvua, miti imekuwa ikitumika kama dawa na jambo la muhimu ni kuwa miti hiyo inafyonza mionzi inayotoka katika jua. “Miti hii inafyonza mionzi mikali inayotoka kwenye jua, ile mionzi badala ya kuja kutugonga moja kwa moja kwenye ngozi zetu inapita kwanza kwenye miti, miti hii inatukinga na maradhi hasa ya kansa. Lakini sasa mkiangalia maradhi ya kansa yanazidi hasa ya ngozi, miti tunakata sana, tupande na tutunze miti,” alisema mjema.

  Akizungumzia kuhusu wananchi wanaojenga katika maeneo oevu na mabondeni, aliwataka watendaji na wenyeviti wa maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo kuhakikisha wanazuia mapema ujenzi huo badala ya kusubiri mtu anamaliza ujenzi na ndipo waende kumhoji.

  Alitaka maeneo ya mabonde yote kupandwa kwa miti mbalimbali na kuwekewa mipaka hatua ambayo itasaidia kuhifadhi vyanzo vya maji, kuepusha mafuriko kwa wananchi lakini pia uvamii wa maeneo na kuingiza serikali katika migogoro.“Tusingoje mpaka mtu ameshafikisha nyumba yake juu, ndio unaenda kumuuliza nani kakwambia ujenge, ulikuwa wapi mtu anaanza kuchimba msingi hadi anamaliza, hilo ni agizo,” alisema.

  Alisema wapo baadhi ya watu wamkuwa na tabia ya kupanda miti ya nje ya nchi ambayo imekuwa ikihatarisha miti ya asili kama mpingo, mivule na mining ambayo kama ikipandwa itasaidia kutunza kurudisha uoto wa asili na kutunza kumbukumbuku kwa kizazi kijacho.

  Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa wilaya amezikumbusha Halmashauri zote za Dar es Salaam, kuhakikisha zinapanda upya miti iliyokufa ambayo ilipandwa katika barabara kuu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Mti wangu”.Maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yana kauli mbiu ya “Panda miti, tunza misitu, upate nishati”.

  Mjema alisema kwa kupanda miti tuafikisha malengo tuliyojiwekea ya kupanda miti milioni nne ifikapo 2019.Kwa mujibu wa takwimu, takribani hekta 372, 8721 hupotea kila mwaka kwa ajili ya nishati na pia hubadilishwa kwa shughuli za kilimo cha kuhahama na ujenzi.

  Aidha, matumizi ya nishati na mbao kwa mwaka inakadiriwa mita za ujazo milioni 72, wakati uwezo wa misitu ya hapa nchini ni mita za ujazo milioni 43 ambazo ni chini ya kiwango kinachohitajika. Kwa kuzingatia uvunaji endelevu nchi yetu ina upungufu wa mita za ujazo milioni 19 .

  “Twakwimu zinaonesha Mkoa wetu tunatumia nusu ya matumizi ya nchi nzima, kiwango hiki ni kikubwa hivyo hatuna budi tupande miti ili tukabiliane na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Mjema

  0 0


  Mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula akizungumza katika hafla ya kupongeza shule za msingi kumi bora kwa mtihani wa taifa wa mwaka 2016
  Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sosthenes Mbwilo akitambulisha walimu na waratibu elimu kata katika hafla hiyo.
  Mgeni rasmi, Sigisbert Rwezaula akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wakuu wa shule zilizofanya vizuri. Wengine pichani kulia ni Afisa Ugavi Wilaya, George Ngwesa.
  Walimu wakifurahia cheti walichopewa kwa kutambua kufanya vizuri kwa shule yao.
  Wageni waalikwa wakiserebuka muziki ikiwa ni moja ya shamrashara za kupongezana kwa kazi nzuri.
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na walimu wakuu wa shule kumi bora pamoja na maofisa elimu mbalimbali.
  Mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula akizungumza katika hafla ya kupongeza shule za msingi kumi bora kwa mtihani wa taifa wa mwaka 2016. . Wengine pichani kuanzia kushoto ni Afisa Ugavi Wilaya, George Ngwesa, Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sosthenes Mbwilo na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paul Sheka.

  Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepongezwa kazi nzuri na kupata matokeo mazuri ya shule zao za msingi katika mtihani wa taifa wa mwaka jana.

  Pongezi hizo zilitolewa jana na mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Sigisbert Rwezaula wakati wakati wa hafla ya kupongeza shule kumi zilizofanya vizuri katika mitihani ya mwaka jana.

  Katika hafla hiyo iliyofanyika Mwadui wilayani Kishapu ikiambatana na utoaji vyeti kwa walimu wakuu, Rwezaula ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema hakuna muujiza wa kufanya vizuri bali ni walimu kujituma.

  Aliwataka walimu wakuu wa shule ambazo hazikufanya vizuri kuhakikisha wanaweka mikakati ili ziweze kuibuka vinara kama walivyo wenzao na kuwataka kuendelea kujituma.

  ”Najua kuna changamoto nyingi kwa walimu kama upungufu au ukosefu wa fedha lakini nawaomba tuvumilie na tukabiliane nazo, jambo kubwa ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu na hatimaye wafanye vizuri,” alisisitiza.

  Aidha Rwezaula aliongeza kwa kutoa rai kwa walimu wa shule hizo za msingi zilizopo katika halmashauri hiyo kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kimasomo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  Alisema hivi sasa dunia ipo katika utandawazi ambapo kunashuhudiwa ugunduzi mkubwa wa kiteknolojia ambao unahitaji maarifa makubwa ili kuendesha masuala mbalimbali ya kitaaluma.

  ”Ni vizuri walimu mkajiendeleza kielimu msiishe hapo mlipo, msikubali kuwa nyuma ya wakati kwani hivi sasa elimu ni muhimu sana na mnashuhudia dunia ni kama kijiji mnaweza kupata habari kwa mitandao,” alisema.

  Rwezaula aliwataka kuwa na utaratibu wa kufidia vipindi vilivyopotea wakati mwalimu kapata dharura au ruhusa na kushindwa kuingia darasani na kuwafundisha wanafunzi.

  Alisema kwa kuwa na utaratibu huo kutawawezesha wanafunzi kupata wasaa wa kujifunza na kuelewa masomo yao kwa wakati na hivyo kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao.

  Awali wanataaluma hao walifanya kikao kazi cha kutathmini mambo yaliyojiri kitaaluma katika Idara ya Elimu Msingi halmashauri ya wilaya hiyo kipindi cha mwaka 2016.

  Kikao hicho kilichofanyika Mwadui kilihusisha maofisa elimu msingi, waratibu elimu kata, walimu wakuu na badhi ya walimu wa shule mbalimbali za msingi zilizopo Wilaya ya Kishapu

  0 0


  Mwenyekiti wa KILIFM Sports Center akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu KILIFM International Marathon yanayolenga kuzuia mauaji ya Albino, utunzaji wa mazingira na uoto wa asili pia kuzuia mauaji ya Tembo nchini,leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mjumbe wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Bw. Peter Mwita.
  D 1
  Mratibu wa Mashindano ya mbio za KILIFM akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu mashindano ya KILIFM International Marathon yanayotarajiwa kufanyika Augusti 13, Mwaka huu Mkoani Kilimanjaro.

  Picha na: Beatrice Lyimo – MAELEZO.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud mara alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

  Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika wengine alipowasili katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

  Baadhi ya Wahariri wa Habari na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

  Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Waandishi wa habari wakiwa katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

  Washauri wa Rais wa Zanzibar ni mongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

  Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

  Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 01/04/2017.

  0 0  Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (katikati) akifurahia zawadi ya picha ya Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (kulia). Kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA mara baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn hivi karibuni.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA mara baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn hivi karibuni.


  Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn amesema Shirika la Meli la Ethiopia (Ethiopian Shipping Line) lipo tayari kuanza kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutoa huduma nzuri.

  “Shirika letu la Meli ambalo ni la kihistoria na lililobaki pekee katika ukanda wa Afrika likiwa linamilikiwa na Serikali ya Ethiopia sasa lipo tayari kufanyakazi na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania,”amebainisha Mhe. Desalegn.

  Ameongeza kuwa mbali na shirika hilo la meli kuwa tayari kuanza kuleta meli zake Bandari ya Dar es Salaam pia Shirika Kongwe la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airline) lenye mafanikio makubwa nalo litaanza kusafirisha mizigo inayopitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

  Kwa upande mwingine Mhe.Desalegn amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Menejimenti ya TPA katika kuboresha huduma zake ambapo amesema jitihada hizo sio tu zitanufaisha Serikali zote mbili bali pia ustawi wa maisha ya watu wa Tanzania na Ethiopia nao utaimarika.

  Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amemshukuru Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kuja nchini ambapo amemuahidi kwamba mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili yatadumishwa kwa maslahi mapana ya mataifa yote.

  Awali akimkaribisha Waziri Mkuu wa Tanzania,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema TPA itaendelea na mipango iliyopo ya kuhakikisha inaboresha Bandari zake ili ziweze kuhudumia vyema wateja wote kwa wakati.

  “Tutaendelea kuboresha huduma zetu za Bandari na za sekta ya uchukuzi kwa ujumla ilituweze kufikia malengo yenu na wateja wetu ya kuhakikisha kwamba tunawahudumia vizuri na kwa ufanisi,” amesema Mhe. Mbarawa.

  Mapema akitoa taarifa ya utendaji wa Mamlaka, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimweleza Waziri Mkuu wa Ethiopia kwamba kwa sasa TPA inaendelea na mpango wake wakujenga uwezo wa kuhudumia wateja wake kwa kuzingatia kwamba sekta ya uchukuzi inakuwa kwa kasi.

  “Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi nchini na Duniani kwa ujumla, TPA inaimarisha uwezo wake wa kuhudumia mizigo na meli kubwa ilikujenga uwezo kabla ya mahitaji makubwa kujitokeza”, amesisitiza Mhandisi Kakoko.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Duniani Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Duniani Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Kiongozi huyo Mkuu Duniani wa  Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi huyo Mkuu Duniani kutoka Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba

  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba imepoteza mchezo wake wa pili tena wa kirafiki baada ya kukubali kuchapwa bao 2-0 na Timu ya Serengeti Boys ya jijini Dar es salaam inayojiandaa na safari ya Gabon. Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki walinyukwa bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys katika uwanja huo huo wa Kaitaba. 

  Katika mchezo wa leo bao la kwanza lilifungwa na Issa Abdu Makamba dakika ya 36 kipindi cha kwanza jezi namba 6 mgongoni aliyelifunga kwa mpira wa adhabu (frii kiki) na kuzama moja kwa moja. Bao la pili lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 89 na Ibrahim Abdallah na mtanange kumalizika kwa bao 2-0 ikiwa ni jumla ya bao 5-0 ikiwa ni jumla ya mchezo wa kwanza na wa pili. 
   
  Serengeti sasa baada ya kuvuna ushindi huo mkubwa wanapanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na Timu ya U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

  Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakimpongeza mfungaji wao wa bao la pili Ibrahim AbdallahShangwe kwa Vijana maarufu kwa Jina Serengeti Boys baada ya kuibuka Kidedea kwa bao 2-0 kwa kuitandika Burundi (U17) kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo.
  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI2
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kongamano la Vijana kuelelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI3
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akizungumza na Vijana na watendaji wa Mkoa wa Katavi (hawapo katika picha) juu ya matumizi ya Tovuti ya Mkoa kabla ya kuzindua Tovuti hiyo leo Mkoani Katavi.
  JENI4
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Tovuti ya Mkoa wakati wa kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI5
  Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Katavi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kongamano la vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


  Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi

  Vijana Mkoani Katavi wametakiwa kujitambua, kuchukua fursa na kuchangia maendeleo ya mkoa na taifa kwa kutumia malighafi zinazopatikana mkoani humo kuwekeza na kuacha kusubiria wawekezaji kutoka mikoa mingine ama nchi za nje kufaidika na malighafi za mkoa huo.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokua akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi na kuwataka vijana hao kuacha uvivu kwani maendeleo huletwa na jitihada za mtu binafsi.

  Mhe. Jenista amesema kuwa vijana wanaweza wakajiwekeza katika sekta isiyo rasmi kwani sekta hiyo huajiri asilimia kubwa na kuwagusa vijana wengi katika kutengeneza ajira na kuwafanya vijana wasiwe tegemezi ndani ya jamii.

  “Vijana wa Mkoa wa katavi mnayo kila sababu kujitafiti na kujua ni namna gani mtatumia sekta isiyo rasmi kutengeneza ajira ambazo zitawasaidia kuonyesha mchango wenu wa asilimia 55 kama vijana katika nchi ya tanzania ukaweza kutumika   kuleta maendeleo ya Mkoa na taifa kwani mnaweza, sababu mnayo, nguvu mnayo na uwezo mnao” amesema Mhe. Jenista

  Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico amewataka vijana wa Mkoa wa Katavi kutumia Tovuti ya Mkoa iliyozinduliwa wakati wa kongamano hilo kupata taarifa kwa wakati ili waweze kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema kuwa Tovuti ya Mkoa yenye kikoa/domeini ya www.katavi.go.tz itakua na taarifa za uhakika na za wakati hivyo kuwawezesha wananchi wa Mkoa wa Katavi wakiwemo vijana kujua taarifa za maendeleo za mkoa pamoja na masuala mengine muhimu kama vile kuelimisha vijana masuala muhimu ya kilimo bora, ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa, afya ya jamii, taaluma za kibenki na ujuzi wa aina mbalimbali za kiteknolojia utakaowawezesha vijana kujaribu.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (pichani kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.


  *Waziri Mkuu amtaka amalize migogoro ya wakulima, wafugaji 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo apige kambi katika kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka wafugaji wanaopiga wakulima. 

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo ambao walisimamisha msafara wake wakati akienda kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. 

  Akitoa kero za eneo hilo, Diwani wa Kata ya Miono, Bw. Juma Mpwimbwi alisema kata hiyo inakabiliwa na tatizo la wakulima kupigwa na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi hawachukuliwi hatua yoyote. 

  “Wafugaji wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki polisi, hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo. 

  Pia alisema mbali ya kero sugu ya maji, waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita lakini hadi sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo. 

  Naye Bw. Shabani Mkwimbi ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, alisema kata hiyo ina kituo cha polisi na mahakama lakini utendaji kazi wa viongozi waliopo hapo unatia shaka. 

  “Waziri Mkuu tunataka ukimaliza kuongea na sisi, uondoke na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Miono, Bw. Maro na msaidizi wake Bw. Rashidi pamoja na Hakimu wa hapa, kwa sababu hawa watu habari yao ni nyingine. Mkulima akienda polisi au mahakamani hashindi kesi hata siku moja, lakini mfugaji akienda anashinda,” alisema huku akishangiliwa. 

  “Hawa watu wanadai wana hela na wanafanya chochote wanachotaka, na ndiyo maana hawalali polisi hata kama wameua mtu,” aliongeza. 

  Akijibu kero zao, Waziri Mkuu aliwahakikshia wakazi hao kwamba Serikali iliyopo madarakani ni yao na hakuna hata mtu mmoja ambaye yuko juu ya sheria. 

  Alisema suala la polisi wa kituo cha Miono litashughulikiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ambaye alikuwepo katika msafara wake. “Tena Mkuu wa Mkoa yuko hapa na yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huu, atasimamia hilo.” 

  Akifafanua kuhusu suala la wafugaji kuwapiga wakulima, Waziri Mkuu alisema msimamo wa Serikali ni kuwaona wakulima wanafanya kazi zao kwa uhuru na wafugaji nao wanafanya kazi zao kwa uhuru. “Hakuna mfugaji anayeruhusiwa kupeleka ng’ombe wake kwenye mashamba yenye chakula. Hili haliruhusiwa hata kidogo,” alisisitiza. 

  “Mkuu wa Mkoa hili ni agizo. Njoo upige kambi hapa na watu wako, na usake  wahusika hadi wabainike. Ni lazima tuwajue ni akina nani wamehusika na hili,” alisema. 

  Aliwataka maafisa mifugo wa mkoa huo waende kwa wafugaji na kutambua mifugo waliyonayo na kama kuna maeneo wahakikishe wanapatiwa maeneo rasmi ili waweze kupatiwa matibabu kwa ajili ya mifugo yao. 

  Aliwataka wafugaji wanaokata mabomba ya maji ya mradi wa maji wa Chalinze (CHALIWASA) ili kupata maji ya kunywesha mifugo yao, waache tabia hiyo mara moja na akaonya kuwa watakaokamatwa, wachukuliwe hatua za kisheria mara moja. Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikuwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa pwani, Eng. Evarist Ndikilo, viongozi wa wilaya ya Bagamoyo na Mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete.

  0 0

  baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida vilivyoezuliwa paa kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha kwa takribani nusu saa na hivyo kuwakosesha zaidi ya wanafunzi 150 vyumba vya kusomea.
  Ni baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu na nne katika shule hiyo waliokuwa wakijisomea nje ya vyumba vya madarasa wakisubiri kuingia kwa zamu darasani kufanya mitihani yao
  Ni baadhi ya bati za majengo ya shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo wilayani Iramba,Mkoani Singida yaliyoezuliwa katika vyumba vya madarasa,ofisi ya mkuu wa shule pamoja na ofisi za walimu wa shule hiyo.

  baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida wakifanya mitihani yao kwenye majengo ya vyumba vya maabara baada ya vyumba vya madarasa yao kuezuliwa na upepo mkali.(Picha zote Na Jumbe Ismailly) .
  baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida vilivyoezuliwa paa kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha kwa takribani nusu saa na hivyo kuwakosesha zaidi ya wanafunzi 150 vyumba vya kusomea.  Na Jumbe Ismailly,Iramba Apr,02,2017 Maafa 

  MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa takribani nusu saa imeezua mapaa ya majengo ya shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo wilayani Iramba,Mkoani Singida imesababisha zaidi ya wanafunzi 150 kukosa vyumba vya kusomea na hivyo kulazimika kutumia majengo mawili ya vyumba vya maabara viliyopo katika shule hiyo.

  Mkuu wa shule hiyo,Lameck Ayeiko alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi,24,mwaka huu saa kumi jioni ambapo mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha kwa muda wa takribani nusu saa na hivyo kusababisha pia ofisi ya Mkuu wa shule na ofisi za walimu kuezuliwa paa na kujaa maji kwenye vyumba hivyo na kwamba zaidi ya shilingi milioni 20 zinahitajika kurudisha majengo hayo katika hali ya kawaida.

  “Ili kurudisha yale majengo katika hali yake ilivyokuwa zilikuwa zinahitajika jumla ya shilingi milioni 13,648,lakini kuboresha yale madarasa ili yakae vizuri sasa, kulikuwa kunatakiwa kuwe na ongezeko la kama shilingi milioni 6,511,000/= karibu milioni ishirini”alisisitiza mwalimu huyo.

  Kufuatia tukio hilo Mkuu wa shule huyo alisema walilazimika kufanya mkutano wa hadhara kwa kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na kufikia makaubaliano kwa kila mzazi kuchangia shilingi 10,000/=ambapo papo kwa papo zilipatikana zaidi ya shilingi laki tano kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo.

  Alipotakiwa kuzungumzia maafa hayo,Mkuu wa wilaya ya Iramba,ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maafa wa wilaya hiyo,Emmanuel Luhahula alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba baada ya kufanyika kwa tathimini ya uharibifu huo walibaini zaidi ya shilingi milioni 20 zinahitajika kurejesha majengo hayo katika hali yake ya kawaida.

  Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,Mariether Kasongo aliweka wazi kuwa kati ya shilingi milioni 30 hadi 35 zinahitajika kukarabati majengo yaliyoathirika kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa nusu saa.

  Shule ya sekondari New Kiomboi iliyoezuliwa mapaa ya baadhi ya majengo yake kwa zaidi ya wiki moja sasa,lakini hakuna kiasi chochote cha fedha kilichotengwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya kurejesha hali ya majengo ya shsule hiyo.

  Shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo Tarafa ya Kisiriri,wilayani Iramba,Mkoani Singida ipo katika Programu ya SEDP na fedha kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za kuboresha majengo ya shule hiyo yanatekelezwa kupitia mpango huo zinapatikana.

  0 0


  Spika wa Bunge  Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mhe. Elly Macha, uliotokea juzi katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu, katika tukio lililofanyika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma

  Naibu Spika wa  Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mhe. Elly Macha, uliotokea juzi katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu, katika tukio lililofanyika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 1189 | 1190 | (Page 1191) | 1192 | 1193 | .... | 1898 | newer