Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 26,2017


TANESCO YATOA TAARIFA YA KATIZO LA UMEME SEHEMU KUBWA YA JIJI MACHI 26

$
0
0




SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala jijini Dar es Salaam, kitakuwa kwenye maboresho makubwa Machi 26, 2017 na hivyo itapelekea eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi. Leila Muhaji imesema umeme utakosekana kuanzia saa 3 asubuhi na kurejea saa 10 jioni ambapo ametaja maeneo yatakayoathirika kufuatia kazi ya kuboresha kituo hicho ni pamoja na eneo la katikati ya jiji, Upanga, Kariakoo, Buguruni, Ilala, Mbagala na Chang’ombe.

Aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Kurasini, Kiwanda cha saruji Maweni, Wizara ya Maliasili na Utalii, (Mpingo House),Tusiime Mission na Tanzania Oxygen. Mengine yaliyotajwa ni pamoja na Ofisi ya Manispaa ya Temeke, Unilever, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jarmana Printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate, na maeneo jirani.

Bi. Leila aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Goldstar, Quaim, Robbarac, Simba Plastic, Veta, Duce, JKT Mgulani Barracks, Keko, Mkuranga,Chuo cha Diplomasia, 21st Century, Oilcom, Engen na eneo la Mtoni Mtongani.

Aidha kufuatia katizo hilo la umeme, TANESCO imetoa tahadhari kwa wananchikutoshika nyaya za umeme zilizokatika na kwuataka watoe taarifa kwenye namba za dharura za TANESCO.

Leila alisema, uongozi wa TANESCO unaomba radhi kutokana na usumbufu utakaojitokeza kutokana na kazi hiyo.

MWANAHABARI GEORGE BINAGI NA MISS PENDO KISAKA KUUAGA UKAPELA HII LEO.

$
0
0
Mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa mtandao wa Binagi Media Group, George Binagi (kulia) pamoja na Miss Pendo Kisaka (kushoto), wanatarajiwa kufunga pingu za maisha masaa machache yajao.

Wapendanao hao wanafunga ndoa hii leo March 26,2017 majira ya saa nane mchana katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, na baadae kufuatiwa na hafla itakayofanyika Ukumbi wa Sun City Hotel uliopo Ghana Green View Jijini Mwanza kuanzia majira ya saa moja jioni.

Zifuatazo ni picha za hafla ya kumuaga bibi harusi mtarajiwa (Sendoff) iliyofanyika ijumaa iliyopita March 17,2017 Jijini Dar es salaam.
Sifa na Utukufu ni kwa Mwenyezi Mungu, Amina!

JINSI KERO MAJI INAVYOWATESA WANAWAKE KISHAPU- SHINYANGA

$
0
0

Wakati nchi ya Tanzania ikiadhimisha wiki ya maji,imeelezwa kuwa wanawake wengi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji hivyo kushindwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kikamilifu.
Wanawake hao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji katika mto Tungu unaotenganisha wilaya ya Kishapu na Maswa mkoa wa Simiyu kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika mpaka sasa hali inayowafanya kuendelea kuwa tegemezi kwa wanaume.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea wilayani humo wananchi wa vijiji vya Nyenze na Ng’wang’holo kata ya Mwadui Lohumbo wilayani humo walisema maji ni changamoto kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwani wanatumia muda mwingi kutafuta maji.
Walisema licha ya kuishi karibu na mgodi wa almasi wa Williamson wanalazimika kutembea umbali takribani kilomita tano kufuata maji katika mto Tungu unaotenganisha wilaya ya Kishapu na wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Akielezea changamoto hiyo,mkazi wa kijiji cha Nyenze Agnes Daudi alisema akina mama ndiyo waathirika wakubwa kwani wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji na mara nyingi huamka kila siku majira ya saa 11 alfajiri kwenda katika mto huo na kurudi nyumbani saa 4 asubuhi.
“Licha ya kutumia muda mwingi kufuata maji,hayo maji yenyewe ya mto Tungu siyo salama kwani yanatumiwa pia na wanyama kama fisi na watu wengi kijijini huwa hawachemshi maji wanakunywa hivyo hivyo”,alieleza Daudi.
Aliongeza kuwa kutokana na changamoto hiyo,wanawake wapo hatarini kushambuliwa na wanyama aina ya fisi ambao wamekuwa wakikutana nao mara kwa usiku wanapofuata maji mtoni.
Naye Anastazia Lutamla walisema maji yamesababisha migogoro katika ndoa kwani wanaume wamekuwa wakiwatuhumu wake zao kuwa wanachelewa kurudi nyumbani kwa kisingizio cha maji.“Wanawake wanakumbana na changamoto nyingi njiani ikiwemo kubakwa,wasukuma ni waoga wengi wamekuwa hawasemi vitendo wanavyofanyiwa wakiamini kuwa ni fedheha mbele ya jamii”,aliongeza Lutamla.
Grace Maige mkazi wa kijiji cha Ng’wang’holo aliiomba serikali na mgodi wa almasi wa Williason,Karspian na El-Hilal vilivyo karibu na vijiji hivyo kuimarisha ujirani mwema kwa kuwapatia huduma ya maji wananchi kwani wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu sasa.
Naye Tungu Magega ambaye jina lake linatokana na mto Tungu ambapo alizaliwa wakati mama yake akichota maji katika mto huo mwaka 1949 alisema vijiji vinavyozunguka mgodi wa Williamson vilipaswa hudumiwa na mgodi huo hata kwa kuwachimbia visima tu.
“Nilizaliwa mwaka 1949,nipo katika kijiji hiki cha Nyenze tatizo la maji ni changamoto kabla na baada ya uhuru,tunaomba serikali itusaidie kuondoa tatizo hili,kama mgodi umeshindwa kutuhudumia,basi tunaomba hata maji kutoka ziwa Victoria yaje kijijini kwetu”,alieleza Magega.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwadui Lohumbo James Limbe alisema ni kweli kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya maji na kwamba jitihada wanazofanya sasa ni kuboresha visima vilivyopo katika baadhi ya vitongoji vilivyoharibika wakati wakisubiri maji kutoka ziwa Victoria kufika katika kijiji hicho.
Limbe alisema wanawake katika kata hiyo wanapoteza muda mwingi kwa badala ya kufanya shughuli zingine za maendeleo kwa kufuata maji katika mto Tungu ambayo hata hivyo siyo salama kwa maisha ya binadamu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba alisema suala la ukosefu wa maji lipo kwa wilaya hiyo ni kame lakini serikali inafanya jitihada za kuwapatia maji wananchi ambapo tayari bomba la maji kutoka Ziwa Victoria yameshafika katika mji wa Mhunze wilayani humo.
“Siyo kweli kuwa wananchi wote wanatumia maji ya mto Tungu,wengine wana visima,mabwawa,hivi sasa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria unaendelea Kishapu,ukikamilika tutapata maji, tatizo ni upatikanaji wa pesa”,alieleza Nyabaganga.
“Kadri tutakavyopata pesa tutapeleka maji vijijini,tumeanza na mji wa Mhunze,kila kijiji palipopita bomba tumeweka toleo la maji,tenki letu lipo mbioni kukamilika,bomba tayari limeshatandazwa”,aliongeza Talaba.
Mkazi wa kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu akichota maji ya kunywa baada ya kufukua mchanga pembezoni mwa mto Tungu unaotenganisha wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu na Kishapu mkoa wa Shinyanga,mto huo ni tegemeo kubwa la wananchi wa wilaya ya Kishapu kutokana na uhaba wa maji.
Mkazi wa kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu akichota maji ya kunywa baada ya kufukua mchanga pembezoni mwa mto Tungu
Watoto wa kike wakipeleka mifugo yao kunywa maji katika mto Tungu huku mwananchi akiendelea kufua nguo 
Mkazi wa kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu akitoka mto Tungu kuchota maji ya kunywa
Haya ni mashimo yaliyofukuliwa pembezoni mwa mto Tungu ambapo maji hujichuja kutoka kwenye mto na kuingia kwenye mashimo hayo na wananchi kuchota maji hayo kwa ajili ya kunywa
Shimo lililofukuliwa pembezoni mwa mto Tungu
Mchungaji wa mbuzi,ng'ombe akipeleka mifugo yake mto Tungu
Wananchi wakifua nguo katika mto Tungu
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

MAAFISA HABARI NA TEHAMA KUZITANGAZA HALMSHAURI NA MIKOA MBELE YA USO WA DUNIA

$
0
0

Na Afisa habari Mufindi

Jumla ya Maafisa habari na temaha 110 kutoka kwenye halmshauri na Mikoa, leo wanaendelea na mafunzo ya siku saba yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuendesha na kusimamia tovuti za taasisi zao jambo amabalo linafungua ukurasa mpya wa kupasha habari za serikali kwa umma kote duniani.

Mafunzo hayo yanayotekelezwa makao makuu ya nchi mjini Dodoma kuanzia tarehe 20 mpaka tarehe 27 mwezi huu, yanafanyika kupitia mradi wa kuimalisha mifumo ya sekta za umma (PS3) kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani maarufu kama (USAID)

Mafunzo yanatolewa kwa kuzijumuisha sekta hizo pacha za tehama na habari yatawaimarisha Maafisa habari juu ya namna bora ya kuweka na kupasha habari kimkakati na kwa ubora wa kimataifa huku Maafisa Tehama wakiimarishwa kwenye masuala ya kifundi ili kuhakikisha tovuti hizo zinakuwa kwenye hali nzuri ili zitumike muda wote. 
Aidha, Mafunzo hayo yanatolewa katika ngazi ya kanda sita ambapo kanda ya Dodoma ikiwa na Maafisa 110 inqjumuisha Mikoa ya Iringa yenye Halmashauri 05, Dodoma Halmshauri 08, Manyara halmshauri 07 Singinda halmshauri 06, Pwani halmashauri 09 Geita, halms.
Picha ni maafisa habari na tehama wakiwa kwenye mafunzo

Balozi Philip Sanka Marmo aagwa na Baba Mtakatifu Papa Francis baada ya kumaliza muda wake

$
0
0
Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo ameagwa
rasmi jana na viongozi wa Vatican, balozi huyo aliyekuwa na makazi
yake jijini Berlin, alikuwa anahudumu nchi 10 na nafasi yake hivi sasa
itashikiliwa na balozi Abdalah Possi ambaye aliapishwa jana na Rais Dk
John Magufuli.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake, mheshimiwa
Philip Sanka Marmo ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican,
akiagana na Baba Mtakatifu Papa Francis jana baada ya kustaafu
utumishi wake, (kulia) ni mke wake mama Nuruana Marmo.

Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akimpa zawadi
mama Nuruana Marmo, mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, balozi.Philip Marmo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican, mama Nuruana Marmo, wakati walipofika jana kwa ajili ya kumuaga Papa.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake Philip Marmo
akiagana jana na Mkuu wa Utawala, Vatican (Secretary of State),
Mhadhama Kardinali Pietro Parolin, balozi Marmo alikuwa anatumikia
nchi 10 ikiwemo Vatican.

Balozi Philip Marmo akiagana na Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na
Mataifa (Secretary for Foreign Relations with States), Askofu Mkuu
Paul Callagher, alipofika jana kuagana na viongozi wa Vatican, balozi
Marmo ambaye alikuwa na makazi yake jijini Berlin nchini Ujerumani
alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake, mheshimiwa
Philip Sanka Marmo ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican,
akiagana na Baba Mtakatifu Papa Francis jana baada ya kustaafu
utumishi wake, (kulia) ni mke wake mama Nuruana Marmo.
Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akimpa zawadi mama Nuruana Marmo, mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, balozi Philip Marmo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican, mama Nuruana Marmo, wakati walipofika jana kwa ajili ya kumuaga Papa.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake Philip Marmo
akiagana jana na Mkuu wa Utawala, Vatican (Secretary of State),
Mhadhama Kardinali Pietro Parolin, balozi Marmo alikuwa anatumikia
nchi 10 ikiwemo Vatican.
Balozi Philip Marmo akiagana na Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mataifa (Secretary for Foreign Relations with States), Askofu Mkuu Paul Callagher, alipofika jana kuagana na viongozi wa Vatican, balozi Marmo ambaye alikuwa na makazi yake jijini Berlin nchini Ujerumani alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican.

MAKABURI 22 YA WATU WENYE UALBINO YAFUKULIWA TANZANIA...TAS YAMUOMBA JPM KUFANYA KAMA DAWA ZA KULEVYA NA VIROBA

$
0
0

Inaelezwa kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana. 

Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. 

Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao 

Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao. “Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner. 

Aidha alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa kaburi la Nelson Msogole (50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya kufariki tarehe 28/3/2011 na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe 20/3/2017na watu wasiojulikana. “Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na kumepiga hatua?”,alihoji Torner. 

Alisema Tangu kuanze kuibuka mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 makaburi 22 nchini yamekwisha fukuliwa katika mikoa ya Mbeya ,Tabora,Mwanza,Mara ,Kagera,Rukwa, na Shinyanga. 

Aliiomba serikali ya awamu ya tano iweke mikakati ya uelewa kwenye jamii kwani huenda hawana uelewa na watuhumiwa wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. “Hiki ni kipimo cha serikali ya awamu ya tano kwa sauti ya wanyonge kwani kuna baadhi ya watu wanaishi kwenye nchi yao kwa hofu na unyonge na kuondolewa utu wao hivyo tuna imani serikali itaweka nguvu kubwa kuliko kipindi cha nyuma”,aliongeza Torner. 

Naye Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza Alfredy Kapole alisema mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya vifo vya albino zaidi ya 17 vimetokea tangu mwaka 2007 hivyo aliiomba serikali kuweka ulinzi mkubwa kwa watu hao kwani wanakiuka katiba ya nchi kwani kila mtu anastahili kuishi. 

Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mara Joseph Sinda alisema kitendo cha kufukua kinawafanya waishi kwa hofu kubwa na kuitaka serikali ijaribu kuchunguza chanzo chake ni nini na kuthibiti kama kwenye madawa ya kulevya na pombe aina ya viroba walivyofanya ili waweze kuishi kwa amani. 

Mwanaharakati kutoka mkoani wa Shinyanga Eunice Zabroni aliiomba serikali wawaimarishie ulinzi na elimu itolewe kwani wanaishi kwa hofu kwa kukosekana ulinzi imara kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji kata na wilaya hadi mkoa. 
Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimelaani vikali vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini hali inayowafanya waishi kwa hofu kubwa katika nchi yao. 
Katikati ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza wakati wa kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho ambapo walilaani vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS mkoa wa MwanzaAlfred Kapole -Picha zote na Suzy Butondo-Malunde1 blog
Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner ambapo alisema chama hicho kinaiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ualbino 
Baadhi ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa katika kikao hicho. Picha na Suzy Butondo-Malunde1 blog

SERIKALI YAONYA WAVAMIZI WA MIUNDOMBINU

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiruka mtaro wa maji uliopo pembezoni mwa barabara ya Kyaka-Bugene KM 59.1 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kyaka-Bugene KM 59.1 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera. Barabara hiyo inajengwa na mkadarasi kutoka Kampuni ya CHICO na imegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 64.96.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Jumanne Werema (wa kwanza kulia), kuhusu kukamilisha ujenzi kwa wakati wa Shule ya Msingi Tumaini iliyopo eneo la Mafumbo, wilayani Bukoba, mkoa wa Kagera.
Mhandisi Jumanne Werema kutoka Kampuni ya ujenzi wa CMG akimpa taarifa ya mradi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Shule ya Msingi Tumaini iliyopo eneo la Mafumbo, wakati alipokagua, wilayani Bukoba, mkoa wa Kagera.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akiongozana na Mhandisi Salum Chanzi (kushoto), kutoka Wakala wa Majengo nchini (TBA), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bw. Deodatus Kinawiro (kulia), kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ihungo mkoani Kagera iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi takriban miezi sita iliyopita.
Moja ya Jengo la Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ihungo linalojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), baada ya Shule hiyo kuathiriwa na tetemeko la ardhi takriban miezi sita iliyopita, mkoani Kagera.
Mhandisi Mshauri wa Kitengo maalum cha Wahandisi Washauri Wazawa kutoka Wakala wa Barabara Nchini (TECU), Eng. Mushubira Kamuhabwa (kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene KM 59.1 kwa kiwango cha lami, wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

………………..



Serikali imesema haitavumilia wala kusita kumchukulia hatua yeyote anayevamia na kujenga katika hifadhi za miundombinu ya barabara na reli kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Karagwe, mkoani Kagera mara baada ya kukagua barabara ya Kyaka hadi Bugene yenye urefu wa kilometa 59.1, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi kuacha dhana ya kuingilia miundombinu hiyo kwa imani ya kulipwa fidia na Serikali.

“Najua bado kuna watu wanaendelea kuvamia miundombinu ya usafirishaji, sasa nasema kuwa Serikali itaendelea kubomoa pasipo kulipa fidia kwa yeyote anayevunja sheria”, amesema Profesa Mbarawa.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, Waziri Profesa Mbarawa amekipongeza Kitengo maalum cha Wahandisi Washauri Wazawa (TECU), kinachosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kwa kusimamia ujenzi wa barabara hiyo kwa kuzingatia viwango na kuwataka kuendelea kuimarisha kitengo hicho ili kiweze kufikia hatua ya kujenga barabara nchini.

Aidha, amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuwahamasisha wananchi wake kuilinda na kuitunza barabara hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Mushubira Kamuhabwa, amesema kuwa kazi inaendelea vizuri kwani mpaka sasa mradi huo umefika asilimia 98 ambapo kazi iliyobaki ni uwekaji wa alama za barabarani.

Eng. Kamuhabwa ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kutokana na barabara hiyo kuwa kiungo kati ya Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka hadi Bugene umejengwa na kampuni ya CHICO kutoka nchini China na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 64.96.

Katika hatua nyengine Waziri Mbarawa ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya wavulana ya Ihungo mkoani Kagera iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi takriban miezi sita iliyopita.

Akiwa katika shule hiyo Profesa Mbarawa ameridhishwa na kasi ya mkandarasi anayejenga shule hiyo na kusema nia ya Serikali ni kuijenga shule hiyo kwa ubora wa hali ya juu ili kukabiliana na majanga mbalimbali.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bw. Deodatus Kinawiro pamoja na mambo mengine ameishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wake na kuijenga shule hiyo kwa ubora wa hali ya juu.

Ni takribani miezi sita tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kuharibu miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, madaraja, hospitali, shule pamoja na makazi ya watu.

Kutokana na uharibifu huo Serikali pamoja na wadau mbalimbali ilianza juhudi za ukarabati na ujenzi wa miundombinu hiyo.

SERIKALI KUJENGA MELI YA KISASA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Meneja wa Mamlaka ya Bandari Kanda ya Ziwa, Bw. Abel Moyo, alipokagua gati ya Bandari ya Bukoba, mkoani humo jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa mmoja wa Afisa Fedha kutoka Mamlaka ya Bandari (TPA), katika Bandari ya Bukoba alipokagua utendaji wa bandari hiyo na kubaini utaratibu mbovu wa ukusanyaji mapato.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na mafundi wanaofanya ukarabati katika bandari ya Bukoba, alipokagua utendaji wa bandari hiyo Mkoani Kagera.
Baadhi ya Watumishi wanaofanya kazi katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoani Kagera, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipooongea nao mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoani Kagera, mara baada ya kuongea nao na kuwaeleza mikakati mbalimbali ya WIzara hiyo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

………………

Serikali imewatoa wasiwasi wakazi na wafanyabishara wa Kanda ya Ziwa Victoria kuwa iko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ujenzi wa meli mpya kubwa na ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua mizigo tani 300, magari 25 na madaraja matatu kwa ajili ya sehemu ya kukaa abiria. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua bandari ya Bukoba, mkoani Kagera, Waziri Profesa Mbarawa amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo umechelewa kutokana na kukosa sifa kwa Makandarasi wawili waliojitokeza mwanzoni kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi.

“Nataka kujenga meli ya kisasa ili kuweza kufupisha safari kutoka masaa 10 hadi matano kutoka Bukoba hadi Mwanza na hivyo kufanya usafiri wa majini kuwa wa kuaminika na salama”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa kutokana na utendaji mbovu wa bandari hiyo anatarajia kuleta wafanyakazi makini kwa ajili ya kupitia taaria za kifedha za utoaji na usafirishwaji wa mizigo bandarini hapo.

Naye, Meneja wa Mamlaka ya Bandari Kanda ya Ziwa, Bw. Abel Moyo ameiomba Serikali kufanya ukarabati wa Meli nchini hasa zilizopo Kanda ya Ziwa ili kuweza kuondoa adha wanazozipata wakazi wa mikoa hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua Shirika la Posta mkoani humo na kuahidi kupeleka wakaguzi wa ndani kwa ajili ya kukagua na kujiridhisha juu ya mapato na matumizi ili kubaini ubadhilifu unaofanywa na watendaji wa Posta.

“Tunataka Posta iwe safi na kupunguza changamoto zinazoikabili kwani ni Shirika kubwa na lenye Rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kuinua mapato ya Shirika hilo”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Akiwa katika ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani humo, Waziri Prof. Mbarawa ameuagiza Wakala huo kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa katika utengenezaji wa magari yanayokuja kupata huduma katika karakana yao.

Kwa upande wake, Meneja wa TEMESA, Eng, Zephrine Bahyona amemuomba Waziri kusaidia kusisitiza Taasisi za Serikali kupeleka magari yao kwenye karakana zao na kulipa madeni kwa wakati ili kupunguzia Wakala huo mzigo wa madeni kutoka katika taasisi hizo.

Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi wilayani Bukoba, mkoani Kagera ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

AICC yashauriwa kuwekeza Dodoma

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeushauri uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuelekeza nguvu ya uwekezji katika mji wa Dodoma ili kuziba kukidhi ongezeko la huduma za kumbi za kufanyia muikutano linalosababishwa na serikali kuhamia katika mji huo.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati ya PIC kutembelea AICC mwishoni mwa wiki na kukagua miradi miwili, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Albert Obama ameshauri AICC kuupa kipaumbele mkoa wa Dodoma katika mkakati wa kujenga kituo kingine cha kisasa cha Mikutano.

“Tunahitaji kuiona taasisi hii ikipanuka na kujenga vituo vingine vya mikutano huko mikoani na moja ya mikoa ambayo tungependa muipe kipaumbele ni Dodoma maana huko ndio serikali inahamia na mahitaji ya huduma ya kumbi za mikutano yanakwenda kuongezeka”, alisisitiza Obama.

Nae Mjumbe wa Kamati hiyo, Amina Mollel alieleza kufurahishwa na juhudi za uongozi wa AICC kumilisha ujenzi wa mradi wa nyumba za kisasa (apartment) 48 ambapo azote zina wapangaji na kuwa sehemu muhimu ya kuongeza mapato ya shirika.

Aidha ameushauri uongozi wa AICC kuzingati uwekaji wa miundombinu ya walemavu katika miradi mingine inayotekelezwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa kwa ajili ya maonesho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya aliieleza Kamati ya PIC kuwa Kituo kina mipango ya baadae ya kujenga Kituo kingine cha Kisasa cha Mikutano kitakachojulikana kama Mount Kilimanjaro International Convention Centre (MKICC) ili kukabiliana na ushindani wa biashara ya mikutano kutoka nchi za jirani kama Rwanda ambayo tayari ina Kituo cha kisasa cha Kigali na Kenya ambayo tayari inatarajia kujenga Kituo cha kisasa cha Mikutano huko Mombasa.

Kaaya ameeleza kuwa AICC imefanikiwa kununua ekari 23 katika mji wa Mtwara na pia inatafuta ardhi katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Iringa kwa ajili ya kujenga Vituo vingine vya Mikutano. Aidha alieleza Kamati kuwa mbali na kujenga Vituo vya Mikutano, AICC inatarajia kujenga miundombinu kwa ajili ya Wanajuiya ya Kidiplomasia eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetenga eneo kubwa kwa ajili ya taasisi mbalimbali za kimataifa kujenga ofisi. 

Mbali na biashara ya mikutano, AICC inajishughulisha pia na upangishaji wa ofisi na nyumba na pia inatoa huduma za afya kupitia hospitali yake. Pia AICC inamiliki Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa katika mradi wa nyumba za kisasa za kupangisha za AICC ambapo mradi huu umekamilika na tayari nyumba hizo zimeisha pata wapangaji. 
Mkurugenzi wa Miliki na Miradi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Victor Kamagenge (kushoto) akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, juu ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa maonesho. Kamati hiyo ilitembelea AICC mwishoni mwa wiki kukagua miradi miwili ya ujenzi wa ukumbi wa maonesho ambapo ujenzi wa unaendelea na mradi mwingine wa nyumba za kisasa 48 ambao tayari umekamilika.

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YARIDHISHWA NA MIRADI YA TASAF, TAMISEMI , MKURABITA NA MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA MKOANI NJOMBE.

$
0
0
Kamati ya kudumu ya bunge Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea mkoani Njombe na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,TAMISEMI, Mfuko wa Rais wa Kujitegemea na MKURABITA na kuridhishwa na mchango wa taasisi hizo katika kupiga vita umasikini kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Wakiwa mkoani humo,wajumbe wa Kamati hiyo walikutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ambapo licha ya kuvutiwa na hatua ya kujiongezea kipato kutokana na ruzuku kwa kuanzisha miradi midogo midogo, lakini pia walipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za elimu, afya na lishe katika kaya za walengwa hao.

Aidha wajumbe wa kamati hiyo ambao waliongozana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki pia wamepongeza hatua ya TASAF ya kupunguza tatizo la makazi ya walimu kwa kujenga nyumba katika kijiji cha Uwemba nje kidogo ya mji wa Njombe.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe.Kairuki amesema serikali itaendelea kuweka mkazo katika miradi inayolenga kuwapunguzia wananchi adha ya umasikini hivyo akataka wananchi kuitumia fursa hiyo vizuri ili waweze kuboresha maisha yao.Waziri huyo alionyesha kuridhika na baadhi ya wananchi mkoani Njombe kwa kutumia fursa zilizowekwa na serikali kuendesha shughuli za kiuchumi kikiwemo kilimo,ufugaji ,biashara na uanzishaji wa vikundi vya kuweka akiba.

Kwa Upande wa MKURABITA,Wajumbe wa Kamati hiyo walipata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao wamepata mikopo kwa kutumia hati za ardhi iliyopimwa chini ya Mpango huo ambao baadhi yao wameweza kupanua biashara zao baada ya kukopa fedha kwa wastani wa shilingi milioni 80 na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati 

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyeongoza wajumbe hao,Mhe. Venance Mwamoto alitoa wito kwa wataalamu walioko kwenye maeneo ya wananchi kutumia muda wao mwingi kuwapatia elimu na mafunzo yatakayowawezesha kuboresha miradi wanayoianzisha ili iwe endelevu na yenye kuleta tija.

Hata hivyo wanufaika wa mikopo kutoka taasisi za fedha walionyesha kilio chao kutokana na riba kubwa wanayotozwa jambo ambalo wamedai kuwa linaathiri maendeleo ya biashara zao na kufifisha nia ya kuendelea kukopa .Zifuatazo ni picha za ziara hiyo ya kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mkoani Njombe.
 Wajumbe wa kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakikagua ujenzi wa nyumba ya Walimu inayojengwa na TASAF katika kijiji cha Ulembwe nje kidogo ya mji wa Njombe. 
 Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali Mitaa wakipata maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya Walimu katika kijiji cha Ulembwe inayojengwa TASAF ikiwa ni jitihada za serikali za kutatua tatizo la makazi kwa walimu.

 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa , wakisalimiana na walengwa ya TASAF katika kijiji cha Ulembwe mkoani Njombe katika ziara ya kamati hiyo kukagua miradi ya TASAF,MKURABITA,TAMISEMI na Mfuko wa Rais wa Kujitegemea.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe ,Christopher ole Sendeka (watatu  kulia), baadhi ya wabunge na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyevaa Kaunda suti nyeusi ) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Uwemba mkoani Njombe.

 Baadhi ya walengwa wa TASAF katika wa kijiji cha Ulembwe ,nje kidogo ya mji wa Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge waliofanya ziara kijijini hapo .Wakiwa kijijini hapo ule usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone ulidhihirika baada ya Waziri Kairuki kuahidi kumsomesha mmoja wa watoto kutoka kaya ya mlengwa hadi kidato cha nne. 
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wananchi walionufaika na fedha kutoka mfuko wa Rais wa kujitegemea katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambaye anaendesha kilimo cha viazi mviringo.
 Waziri Kairuki na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala bora na Serikali za Mitaa wakiangalia bidhaa za ususi zinazofanywa na baadi ya wanawake kupitia kikundi chao kilichowezeshwa na Mfuko wa Rais wa Kujitegemea mjini Njombe.
 Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Rais wa kujitegemea mkoani Njombe aliyetumia fedha alizokopeshwa na mfuko huo kuanzisha mradi wa kufuga n’gombe.

 Waziri Kairuki wa kwanza kushoto akifuatiwa na mhe. Mwamoto,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Njombe akiwemo mkuu wa mkoa huo Christopher Ole Sendeka ,nyuma yao ni baadhi ya wanufaika wa MKURABITA. 
 Waziri Kairuki aliyevaa gauni lenye rangi nyekundu na Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya utawala na serikali za mitaa mhe. Venance Mwamoto wakitoa nasaha kwa baadhi ya wanufaika wa MKURABITA mkoani Njombe.
 ‘’Karibuni tena Mkoani Njombe’’ndivyo wanavyoelekea kusema wenyeji kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea mkoa huo kukagua miradi ya TASAF,TAMISEMI ,MKURABITA na Mfuko wa Rais wa Kujitegemea.
Waziri Angellah Kairuki watatu kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na Mhe.Magreth Sitta na Mhe.Ruth Mollel ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge wa utawala na serikali za mitaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ulembwe nje kidogo ya mji wa Njombe.

Article 17

Harmorapa ni nani?

$
0
0
Hamorapa ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anapendwa kwa mambo mengi, vingi ikiwemo vioja na vichekesho.Na kwa siku za karibuni amekuwa hakosekani kwemye matukio makubwa makubwa ungeweza kudhani yeye ni Mwanahabari,lakini siyo kweli.

Juzi juzi alionekana akikimbia kwa kuogopa bastola kwenye tukio la Nape pale St Peters.Ungemuuliza yeye kuwa alifikaje pale kwenye tukio na kukaa mbele vile wala asingeweza kukupa majibu.

Lakini pia alionekana akiwa katikati ya wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii kule Clouds TV pale walipoenda kutoa pole baada ya ule unaodaiwa uvamizi wa Makonda.

Hapo napo ungeweza kumuuliza Harmorapa alifuata kitu gani katikati ya Waheshimiwa wabunge,asingeweza kukupa jibu la kieleweka.

Huyo ndiye Harmorapa ambaye jana amepewa mkataba wa kuwa Balozi wa Kinywaji cha Swala,ili kijitangaze kupitia kwake.

Asili yake ni mikoa ya kusini mwa Tanzania.Lakini pia kuibuka kwake kwa kasi kubwa kumetokana na yeye kuwa anahangaika kumuiga mwanamuzuki mwenzake aliywmtangulia kwenye fani aitwaye Harmonise,ambaye pia kwao ni kusini.

Wana ugomvi mkubwa na msanii huyo Harmonise, ambaye ni member Bendi ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Huyo Harmonise anaishi kinyumba na Wolper (mchumba,wabongo kwa uchumba usioisha😂) Mwanafilamu maarufu Wolper.Ameshampeleka mpaka ukweni Mtwara.Kwahiyo utaona kuwa ugomvi ule unawaunganisha wanamuziki kwa upande mmoja pamoja na wasanii wa filamu kwa upande mwingine.
Hamorapa pia anaye mpenzi wake ambaye humuita 'Wolper'.Jambo hilo linazidi kumkoroga mwenzake Harmonise.

Aghalabu wawili hao wanatukanana sana Hamorapa na Harmonise. Hamorapa anadaiwa pia kuchukua kipande cha jina na Harmonise yaani "Harmo".

Harmonise anaamini mwenzake huyo ameiba kipisi cha jina hilo kwa manufaa yake ya kimuziki ili limpaishe.

Harmorapa anaenda mbali na kudai kuwa yeye sura yake imefanana na ya Harmonise. Mwenzake anapinga sana hilo.Kuna wakati Harmonise alidai kuwa yeye hawezi kufafanana na Harmorapa kwa sura kwakuwa Harmorapa kafanana zaidi na Kima.

Hata pale ambapo Diamond alionesha nia ya kumchukua Harmorapa ajiunge na WCB,alikataa akiogopa kuwa ugomvi wake na Harmonise ungezidi kuwa mkubwa.Hivyo anajitegemea kimuziki akiwa chini ya meneja wake.

Juzi Ijumaa EATV waliwaalika wote ili waingie studio na kuzungumzia ugomvi huo.Harmorapa alitangulia kufika.Baadaye alipowasili Harmonise na kulikuta gari la Meneja wa Harmorapa pale kwenye parking akageuza na kuondoka huku akionesha alama ya tusi kwa kutumia kidole.Hayo aliyasema Hamorapa akiwa studio usiku huo.

Hayo ndiyo mambo ya Wasanii na wanamuziki. Ugomvi huwaletea umaarufu pia.Umri na kabila tuviweke kapuni.

Ni mimi

Kasenyenda

JWTZ kuanza kulipa Deni wanalodaiwa na TANESCO

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania,  Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na wanahabari kuhusu Jeshi hilo kuanza kulipa deni wanalodaiwa na Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanzia siku ya kesho. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Ngome jijini Dar es Salaam.

NEWZ ALERT:Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa


SPIKA JOB NDUGAI NA WAJUMBE WA KAMATI ZA BUNGE ZA BAJETI NA NISHATI NA MADINI WATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa muhtasari Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye ameongoza wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti bandari ya Dar es salaam kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini iliyokuwa imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
Sehemu ya  makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo imezuiwa  kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali 
  Sehemu ya wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti wakitembelea bandari ya Dar es salaam kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo  imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa maelezo  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti bandari ya Dar es salaam juu ya makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini iliyokuwa imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa na wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti akiongea na wanahabari katika bandari ya Dar es salaam baada ya kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO CHATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KANISA KUU LA KKKT SHINYANGA

$
0
0

Kushoto ni Mkurugenzi wa wanawake,Watoto na Diakonia katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ernest Ambarang'u akiwatambulisha viongozi kutoka TAS.Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu kutoka TAS Severin Edward ,akifuatiwa Happiness Ngaweje na afisa mahusiano na habari (TAS)Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS,Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakimsikiliza Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akiendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino huku akiitaka jamii kutoa ushirikiano wa dhati katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakipa somo kuhusu masuala ya ualbino
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria akieleza namna kanisa hilo linashiriki katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Mchungaji Jackson Maganga akizungumza kanisani

Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza jambo kanisani
Wachungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Viongozi wa TAS wakiwa kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakiwa nje ya kanisa baada ya ibada kumalizika
Viongozi wa TAS wakiondoka katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

Kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria











Chama cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.



Viongozi hao wakiongozwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS ,Josephat Torner wametoa elimu kuhusu mambo ya ualbino kanisani hapo wakati wa ibada ya Jumapili leo Machi 26,2017.



Akizungumza kanisani hapo Torner alisema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino kwa viongozi wa dini na waumini wao na wanaendelea pia kutoa elimu hiyo kwa makundi mengine ya watu katika jamii wakiwemo waganga wa kienyeji.



“Tumeona vita hii tunayopambana nayo bila kumjua hasa adui ni nani,ni vyema elimu iwafikie watu wengi zaidi na tunaamini kupitia nyumba za ibada jamii itakuwa na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya ualbino ili kukabiliana na tatizo la mauaji ya watu wenye ualbino na hata vitendo vya kufukua makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini”,alieleza Torner.



Alisema bado watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu masuala ya ualbino hali inayosababisha kuongezeka kwa unyanyapaa ambapo sasa hata wamiliki wa nyumba za kupanga wanawanyima vyumba watu wenye ualbino wakihofia kupata matatizo.



“Nyumba za ibada zina watu wengi,tutapita kwenye makanisa na misikiti kutoa elimu hii ili viongozi na waumini waelewe hasa maana ya ualbino ili tuungane pamoja kutokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino”,aliongeza Torner.





“Kutokana na imani potofu katika jamii watu wenye ualbino wanaishi kwenye vituo maalum,wanaishi kwa hofu kubwa ya kuuawa na sasa kuna baadhi ya watu wameanza kufukua makaburi ya watu wenye ualbino hivyo kunahitajika jitihada zaidi katika kupambana na ukatili huu”,alisema Torner.



Alisema mbali na jitihada zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili huo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili.



Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kanisa hilo,Mchungaji Jackson Maganga alisema kanisa hilo lina programu nyingi za kutoa elimu kwa waumini wake juu ya vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino na kwamba kanisa hilo liko tayari kushirikiana na chama hicho katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino.





Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa hilo,ametusogezea picha 23 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini





Mchungaji Geofrey Kaijunga akitoa mahubiri katika ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.





Mchungaji Geofrey Kaijunga aliwataka waumini wa kanisa hilo kumtegemea mungu kwa kila jambo huku akisisitiza kuwa thamani ya mtu hupanda pale anapookoka





Ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea





Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, akiwakaribisha kanisani viongozi wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania



Afisa Programu kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward akiteta jambo na Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI MKOA WA SHINYANGA YAFANYIKA KWENYE MACHIMBO YA NYANGARATA

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Simon Berege akimwongoza Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani mkoa wa Shinyanga kwenda kukagua mabanda yaliyokuwa yanatoa huduma za kupima VVU,uchunguzi wa kifua kikuu,tohara na huduma zingine za afya sambamba na zoezi la kuandikisha watoto ili wapate vyeti vya kuzaliwa
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye suti nyeusi) na Meneja wa AGPAHI kanda ya ziwa Dkt. Nkingwa Mabelele(kulia) wakisikiliza maelezo ya wataalamu wa afya katika banda la kupimia VVU
Ndani ya banda la uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu-Wataalamu wa afya wakitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu 
Zoezi la tohara kwa wanaume linaendelea-Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiwa katika banda la kutolea huduma ya tohara kwa wanaume bure. Kwa Taarifa kamili BOFYA HAPA

CCM YATANGAZA MAGEUZI YA KUIMARISHA CHAMA KIUTENDAJI NA UTAWALA

$
0
0

 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akzungumza na Waandshi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
 

Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa...

1 Arusha - Elias Mpanda
2 Dar - Saad Kusilawe
3 Dodoma - Jamila Yusuf
4 Geita - Adam Ngalawa
5 Iringa - Christopher Magala
6. Kagera- Rahel Degeleke
7. Katavi- Kajoro Vyahoroka
8. Kigoma- Naomi Kapambala
9. Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
10. Lindi-Mwanamasoud Pazi
11. Manyara -Paza Mwamlima
12. Mara -Innocent Nanzabar
13. Mbeya -Wilson Nkhambaku
14. Morogoro- Kulwa Milonge
15. Mtwara -Zacharia Mwansasu
16. Mwanza- Raymond Mwangala
17. Njombe- Hossea Mpagike
18. Pwani- Anastanzia Amasi
19. Rukwa- Loth Ole Nesere
20. Ruvuma- Amina Imbo
21. Shinyanga -Haula Kachambwa
22. Simiyu- Donald Etamya
23. Singida- Jimson Mhagama
24. Tabora- Janeth Kayanda
25. Tanga- Allan Kingazi.

"Makatibu wengi tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra...

'Kuhusu suala la Mkuu mkoa mkoa wa DSM, kwanza napenda kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria'...

CCM inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza'..

'Mkuu wa mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu'..

"  Humphrey Polepole
Katibu wa CCM itikadi na Uenezi -Taifa
26.3.2016

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TASWE YAANZA KWA KISHINDO UKUMBI WA CARDINAL RUGAMBWA OYSTERBAY - DAR

$
0
0
Maonyesho ya Kimataifa ya Ushirika wa akinamama wajasiliamali wa Tanzania (TASWE) yameanza kwa kishindo leo katika ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay.

 Akizungumza kwa juu ya maonyesho hayo, mwenyekiti na mwanzilishi wa Taswe Saccos, Bi Anna Matinde alisema "Maonyesho haya yamekuwa na hamasa kubwa wafanyabiashara na bidhaa kutoka Comorro, Afrika Mashariki na mikoa mbalimbali nchi zinapatikana hapa kwa wingi na kwa bei nafuu.

 "Tunawakaribisha wote mje mkutane na wafanyabiashara hawa pamoja na wadau wetu na kujionea bidhaa mbalimbali. Maonyesho yanaaza saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku", . Aliongeza Anna Matinde.
Mfanyabiashara kutoka Comorro, Siti Marahaba akiuza baadhi ya bidhaa zake katika maonyesho ya kimataifa ya Taswe
 Bi Sarah Abiudi akionyesha bidhaa za kiafrika zinazopatika katika maonyesho ya Taswe.
 Bi. Arafa Awadhi Mfanyabiasha mwanachama wa Taswe (kulia) akitoa maelezo juu ya bidhaa zake na mmoja ya mteja aliyetembelea maonyesho hayo
 Wafanyabiashara kutoka zanzibar wakionyesha bidhaa mbalimbali za kiasili zinazopatikana katika maonyesho ya kimataifa ya TASWE
 Mjasiliamali kutoka Nairobi Kenya, Bi Jesca Alphonce akionyesha namna ya ktumia moja kati ya bidhaa za urembo kwa wateja waliojitokeza kwenye maonyesho hayo
 Mfanyabiasha na mwanachama wa Taswe bi. Elizabeth akionyesha bidhaaa kwa wateja waliotembelea maonyesho
 Maonyesho haya ya akina mama wanachama wa Taswe yanaendelea ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay ambapo yalifunguliwa jana Machi 25, 2017 na kilele chake kitakuwa 31.03.2017.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images