Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 25,2017

0
0


WAZIRI JENISTA MHAGAMA AWAONDOA HOFU WANACHAMA WA PPF KUFUATIA UAMUZI WAKE WA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA.

0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), jijini humo Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, akizungumza kwenye mkutano huo. Yeye alisema Jeshi la Magereza limeamua kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo PPF na NSSF katika kutekeleza mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na PPF, wanafanya uwekezaji mkubwa katika kiwanda cha viatu kule gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro na kwenye kiwanda cha sukari kwenye shamba la Mbigiri mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akifuatilia kwa makini mkutano huo

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeinhia siku ya pili nay a mwisho leo Machi 27, 2017.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeinhia siku ya pili nay a mwisho leo Machi 27, 2017.

Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkulazi huko mkoani Morogoro, Bi.Radhia Tambwe akitoa mada kuhusu uwekezaji huo ambao unafanywa kwa ubia na Mifuko ya PPF na NSSF.

Mchokoza mada ya uwekezaji katika viwanda, Profesa Humphrey Moshi akizungumza.


Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian  Daqqaro, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa kipindi ndani ya mkutano huo, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bi.Amelye Nyembe

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, akifuatilia mkutano huo
 Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Msemwa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiendelea
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, akifurahia jambo
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, Bw. Meshack Bandawe, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uwekezaji na Mifuko hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo, (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw.Gabriel Fabian  Daqqaro.
 Waziri Mhe. Jenista Mhagama
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, (PAC), Mhe.Naghenjwa Kaboyoka, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa kikao, Mhe.Amelya Nyembe, akizungumza


Wafanyakazi wa PPF wakipoz kwa picha wakati. Wafanyakazi hao ni sehemu ya kamati ya maandalizi ya mkutano huo.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, akisikilzia kwa makini watoa mada
 Washiriki wakiimba wimbo wa Taifa
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada zilziokuwa zikitoelwa

MASAUNI AWATAKA WANANCHI WAISHIO MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI, ATEMBELEA KIWANDACHA KUCHAKATA GESI ASILIA MADIMBA

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), mkoani Mtwara, Mhandisi Sultan Pwaga, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi inavyozalishwa. Hata hivyo, Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda (katikati) pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama walivyoomba uongozi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kiwandani hapo pamoja na wananchi waishio jirani na kiwanda hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Masauni aliwataka wananchi hao kudumisha amani mpakani hapo pamoja na kufuata sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za Uhamiaji Msumbiji endapo watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua mpaka huo aliwataka maafisa wakekuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) akiiangalia moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza ambazo zinahitaji marekebisho katika Gereza Lilungu mkoani Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo mkoani humo, Ismail Mlawa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake wakati alipokuwa Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara.Wapili kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua nyumba za askari Magereza wa Gereza Lilungumkoani humo ambazo zinahitaji marekebisho kutokana na kuharibika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MDAU KUMBILAMOTO ATEMBELEA MICHUZI MEDIA GROUP

0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisalimiana na Msimamizi wa Chumba cha Habari , Carthbet  Kajuna wakati alipotembelea ofsi za MMG leo.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, akisalimina na Mhandishi Mwandamizi na Msimamizi wa Habari za Mahakamani Karama Kenyunko wakati alipofanya ziara katika ofisi za MMG.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto Akiwa ndani ya ofisi ya MMG
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto,Akifurahi jambo na Mwandishi Mwandamizi wa Michuzi Blog Chalila Kibuda
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, Akisalimiana na Mkurugenzi wa Michuzi TV , Karim Michuzi wakati alipofanya ziara ya kutembelea chumba cha habri cha Michuzi Media Group

MD KAYOMBO AKAGUA ENEO LITAKLOTUMIKA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE LA MANISPAA YA UBUNGO LILILOPO MKOANI MOROGORO

0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Shamba litakaloandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane lililopo Mkoani Morogoro


Na Mathias Canal, Morogoro

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amefanya ukaguzi wa eneo kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ili kujiridhisha na kutoa maelekezo ya maandalizi kwa kufyeka majani yaliyopo katika eneo la JKT Mtaa wa Nanenane ikiwa ni hatua za ufanisi kwa ajili ya kuelekea Maonesho ya Nane Nane mwanzoni kwa mwezi Agosti.

Kayombo amesema kuwa lengo kuu la kuzuru kwanza ilikuwa ni kujionea eneo hilo sambamba na kuona hali ya utendaji kazi ili kuanza ufyekaji na kuanza kulima mazao ambayo yanakusudiwa kuoneshwa na Manispaa ya Ubungo.

Amesema kuwa katika utendaji wake amekusudia kwenda mwenyewe Field ili kuona hali ya utendaji ilivyo sio kupelekewa Taarifa pekee kwani kufanya hivyo Ukurugenzi alionao utakuwa hauna maana kama ataishia ofisini.

"Rais ametupa mamlaka makubwa ya kuwatumikia wananchi sasa kama tunakaa ofisi pekee nchi haiwezi kusonga mbele badala yake ili tuweze kuwa na mafanikio katika utendaji pamoja na Kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ni wazi kwamba tunapaswa kuzuru katika maeneo yote tunayoyaongoza" Alisema Kayombo

MD Kayombo amewapa maelekezo Afisa Kilimo na Afisa Mifugo na Uvuvi kuanza haraka iwezekanavyo usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Mita za Mraba 3600 ili kulima na kupanda mazao kusudiwa kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

Maelekezo mengine ni pamoja na kununua viuatilifu kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu na magonjwa, kuandaa mabango na kuainisha aina mbalimbali za malisho iliyooteshwa na kujenga bwawa la samaki.

Kayombo alisema kuwa eneo hilo limenunuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya Maonesho ya Nane Nane ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, Wafugaji na wavuvi kwa kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia na mbinu za kuongeza uzalishaji katika eneo la Uvuvi, Kilimo na Ufugaji.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Kaimu Afisa Kilimo wa Manispaa ya hiyo Ndg Salim Msuya amesema kuwa wanataraji kuanza kutekeleza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kujenga mabanda ya mifugo na sehemu za kusindika mazao ya mifugo, kuandaa mavazi rasmi kwa ajili ya washiriki wa Maonesho.

Mengine ni kukusanya bidhaa za mazao mbalimbali ya wafugaji, wakulima na wavuvi watakaoshiriki Maonesho hayo ya Kilimo Nane Nane kwa ajili ya kuyapeleka Morogoro.

Sambamba na hayo pia Msuya amesema kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kutengeneza matuta ya kuoteshea malisho, Kununua mbolea na kuweka kwenye eneo la malisho ya mifugo, kufunga maji katika eneo la malisho yatakayotumika kwa ajili ya umwagiliaji na mifugo itakayopelekwa wakati wa Maonesho.

Msuya ameeleza kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kuandaa mashimo katika matuta ya kuotesha miche, Vipande na Mbegu za malisho pamoja na kutayarisha eneo la kwa kusafisha eneolima na kufanya Layout ya eneo la kuchimba bwawa kwa ajili ya ufugaji samaki.

DKT KEBWE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao hicho kwa makini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki

Na Mathias Canal, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Morogoro.

Kikao hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika Katika Ukumbi wa JKT Nane Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli moja kimepitisha Agenda zote sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2016 sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2017 ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe ameitaka kamati inayoratibu shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi uaminifu kwa wananchi na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza uchumi nchini kupitia Kilimo.

Dkt Kebwe alisema kuwa TASO kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya Halmashauri zingine kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina weledi uliokusudiwa.

Sambamba na hayo pia amewasihi wadaiwa sugu kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kwani kufanya hivyo itaongeza ustawi na uimara wa Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na hatimaye Kilele chake kuwa na Tija kwa jamii.

Dkt Kebwe amewapongeza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya waliohudhuria katika kikao hicho ambapo alisema kuwa wanafanya kazi nzuri na kuonyesha ushirikiano imara katika Maandalizi hayo japo amesisitiza kuongezwa kwa jitihada za Maandalizi ili Maonesho hayo yawe na weledi na tija.

Sherehe za Maonesho ya Kilimo Nane Nane hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa kuwaelimisha watazamaji na hasa wakulima, wafugaji na wavuvi kujifunza na kupata uzoefu wa teknolojia na mbinu zinazotumika kuongeza uzalishaji katika eneo la kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Katika Maonesho hayo mambo muhimu hutawala ikiwa ni pamoja na kuonyesha mazao mbalimbali sambamba na mifugo mbalimbali kwenye mabanda.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewapongeza viongozi wote kwa namna ambavyo wanashiriki kuandaa Maonesho hayo huku akisema kuwa pamoja na Halmashauri ya Ubungo kuwa mpya na inaanza kushiriki katika Maonesho hayo kwa Mara ya kwanza atahakikisha kuwa maonesho yanakuwa na tija katika mabanda yote yanayoendelea kuandaliwa na Maafisa Kilimo, Uvuvi na Mifugaji.

MD Kayombo alisema kuwa kupitia Maonesho ya Kilimo mwaka huu 2017 wananchi watapata fursa ya kujifunza mbinu za ufugaji kwa kutumia mabanda bora, Uchanganyaji wa vyakula vya mifugo na ulishaji, Teknolojia bora ya ufugaji wa samaki wengi katika eneo dogo, Utotoleshaji vifaranga kwa kutumia incubator ya kienyeji na kisasa, Uhamilishaji wa samaki na Ng'ombe na teknolojia Nyinginezo.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho alizitaja changamoto za maandilizi za Maonesho ya Kilimo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa michango kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na kuchelewa kuthibitisha mialiko kwa wageni walioalikwa kutembelea Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

MPIGA CHAPA MKUU ASISITIZA KAMPUNI KUENDELEA KUJISAJILI

0
0

Leonce Zimbandu

MPIGACHAPA Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo ameendelea kusisiti za na kuzitaka taasisi za serikali, binafsi za uchapishaji  kuendelea kujisajili katika ofisi hiyo na kuepuka usumbufu wa kubainika kwenye msako.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kutoridhishwa na kasi ya kampuni za uchapishaji zilizojitokeza tangu wito huo utolewe Februari 13, mwaka huu, kampuni 24 tayari zimejitokeza.

Chibogoyo  aliyasema hayo alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo  wakati akijibu swali kuhusu kampuni za uchapishaji zilizotii sharia kujisajili  bila shuruti.

Alisema amesikitishwa na mwitikio mdogo wa usajili wa kampuni na taasisi za uchapishaji, hivyo akiwa muungwana ameamua kutumia fursa ya  kuwakumbusha  watimize wajibu wao kisheria.

“Inawezekana katika mkutano wangu  sikueleweka vizuri lakini usajili unahusu kampuni binafsi na serikali kwa lengo la  kutambua shughuli zao na kuepuka kujificha,” alisema.

Alisema baada ya muda uliotolewa kukamilika na ofisi hiyo ikapata  taarifa kuwa ipo taasisi au kampuni inajihusisha na uchapishaji, Ofisi itachukua hatua ya kuifuatilia.

Hivyo kabla ya hali hiyo ya ufuataliaji, itakuwa busara kwa wachapishaji hao kujisajili  ndani ya siku tano zilizobaki tangu wito huo ulipotolewa. 

Aidha, alisema   ili kuondoa usumbufu kwa kampuni za uchapishaji za mikoani, zinaweza kujisajili kwa kupitia mtandao wa Ofisi ya Mpigachapa.

Alisema Wachapishaji   halali watakaojiorodhesha watakaribishwa na kupewa fursa ya kutoa mawazo ya kuiweka nchi mahali salama kupitia nyaraka.

Hatua hiyo imechukuliwa  ili kuendeleza vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka bandia kwa kuwasaka nyumba kwa nyumba, iwapo watashindwa kujitokeza na kujisajili kwa hiari.
Mpigachapa Mkuu  wa Serikali,Cassian Chibogoyo akionesha waandishi wahabari (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake  rangi sahihi  ya bendera yaTaifa, kulia ni Afisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Shija.



WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akioneshwa taarifa ya mapato na Meneja wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, Bw. Salum Mbaya, wakati alipotembelea ofisini hapo leo.
ML 1
Fundi Mitambo kutoka Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), Eng. Godfrey Mbise, akimpa maelezo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu mfumo wa utoaji huduma katika mkongo wa taifa mkoani humo.
ML 2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa uongozi wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, leo, mara baada ya kukagua mitambo na mifumo iliyopo ofisini hapo.
ML 3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akishuka katika ndege ya Kampuni ya Ndege Nchini (ATCL), katika uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.
ML 4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), mkoa wa Kagera Bi. Dorice Uhagile, wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba ambapo amekagua uwanja huo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazokabili uwanja huo.
ML 5
Meneja wa Shirika la Posta Nchini, mkoa wa Kagera Bi. Mary Nsangila, akitoa taarifa ya utendaji kazi wa shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua  maendeleo ya Shirika hilo mkoani humo.
 ML 6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia mbele) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), mkoa wa Kagera Eng. Zephrine Bahyona (wa pili kushoto mbele), wakati alipokuwa akikagua karakana yao na kuona changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………..

TTCL KUZALISHA DOLA MIL 50.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi miwili  Kampuni ya Simu Tanzania  (TTCL), kuhakikisha kuwa inapata Dola za Kimarekani milioni 50 ili kuongeza pato kwa Kampuni na Taifa kwa ujumla kupitia Mkongo wa Taifa.

Akitoa agizo hilo leo, wilayani Bukoba mkoani Kagera, Waziri Prof. Mbarawa amesema agizo hilo limetokana na Serikali kuongeza masafa kwa kampuni hiyo kutoka 10 hadi 200 (MHZ) ambayo yana uwezo wa kuunganisha wateja wengi na wakubwa zaidi.

Amesisitiza makampuni ya Simu nchini kuchangamkia fursa ili kupata masafa yenye uwezo mkubwa kupitia mkongo huo.

“Hakikisheni mnajipanga kuipata hiyo fedha ndani ya miezi miwili na kuwapatia masafa ya kutosha wateja mlionao ndani na nje ya nchi na kujitahidi kuongeza wateja wengi zaidi”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, ameitaka TTCL kusogeza  wigo wa kuwasiliana na wateja wakubwa ili kuwashawishi kununua masafa hayo  kulingana na mahitaji yao na hivyo kutanua wigo wa kibiashara  na kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa TTCL mkoa wa Kagera Bw. Salum Mbaya amemhakikishia Waziri huyo kuwa wataanza mara moja kazi ya kutembelea wateja wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwapatia taarifa za ongezeko la uwezo wa mkongo na kuwashiwishi kujiunga ili kupatiwa masafa wanayohitaji.

Bw. Mbaya ametaja kuwa mpaka kufikia sasa nchi zilizounganishwa na mkongo wa Taifa  ni Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Kenya na Malawi.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea uwanja wa ndege wa Bukoba na kuahidi kutatua changamoto zinazoukabili uwanja wa ndege wa Bukoba ikiwemo kujenga jengo la kuongezea ndege (Control Tower) ili kuongeza ufanisi na usalama katika usafiri wa anga.

 Naye, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini mkoa wa Kagera, Bi. Dorice Uhagile, licha ya kuelezea mafanikio mbalimbali kama vile ongezeko la ndege na wateja uwanjani hapo pia amefafanua changamoto mbalimbali zinazoukabili uwanja huo na kuiomba serikali iweze kuwatatulia.

Waziri Mbarawa ameanza ziara ya kikazi wilayani Bukoba, mkoani Kagera ambapo ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara yake

RC MAKALA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA MAENEO YAO

0
0
Na Fadhili Atick Globu ya Jamii Mbeya

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi mtaa wa Shewa kata ya Mwakibete mkoani Mbeya,na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Makala ambaye ametembelea Shule ya Msingi Shewa na kushuhudia msongamano wa wanafunzi,  amepongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa madarasa kupunguza msongamano wa wanafunzi, ambapo halmashauri ya jiji la Mbeya walichangia shilingi milioni 6.3 kuunga Mkono jitihada za wananchi.

Makala ameahidi kufuatilia kwa Karibu ujenzi wa madarasa mpaka yakamilike, kwani wananchi wamekuwa wakichukizwa na baadhi ya watu wachache wanaopita kushawishi wananchi wasichangie

Makala amewaonya wote wanaoshawishi wananchi kutochangia Maendeleo kuacha tabia hiyo mara moja katika  na kuamua kuonyesha mfano wa kuchangia milioni moja katika ujenzi wa choo cha Shule msingi shewa

Pia ameagiza Tanesco na Mamlaka ya Maji kushughulikia haraka matatizo ya  Umeme na Maji katika mkoa wa Mbeya hili kupunguza kero kwa Wananchi.
 Rc Makalla akizungumza na wananchi wa kata ya mwakibete jijini mbeya
Akishangazwa na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi mwakibete ambapo idadi ilionesha wanafunzi ni wengi kuliko madarasa.
Moja kati ya Wakazi WA shewa kata ya mwakibete wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Mmoja wa Wananchi akitoa duku duku lake kwa RC Makala.
Baadhi ya wakazi wa Mwakibete wakifuatilia mkutano huo.

KATI YA WATU 3447 WALIOJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO 27 WAHISIWA KUWA NA KIFUA KIKUU MUFINDI

0
0

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akipata maelezo ya kasi ya upimaji VVU leo Mufindi kwenye kilele cha siku ya kifua kikuu na UKIMWI.

mkuu wa mkoa akiwa banda la benki ya wananchi wa Mufindi .









Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkabidhi baiskeli zilizotolewa na Africare mtoa huduma majumbani Shukuru Ngelime leo







Na MatukiodaimaBlog


WAKATI Leo ni maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Dunia imeelezwa kuwa kati ya watu 3447 waliojitokeza kupima afya zao wilaya Mufimdi mkoani Iringa idadi ya watu 27 wahisiwa kuwa na maambukizi ya kifua kikuu.

Akitoa taarifa ya upimaji wa VVU na kifua kikuu leo wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mafinga wilayani Mufindi mratibu wa Kifua kikuu na Ukimwi Mkoa Tecla Orio,alisema idadi hiyo imetokana na wale waliojitokeza kupima kwa hiari afya zao.

Alisema kuwa kwa wakati wote ndani ya wiki Moja sasa wamekuwa wakizunguka kata mbali mbali kupima kifua kikuu na Ukimwi.

"Tulifanya kampeni ya huduma shirikishi ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU, uchunguzi wa wagonjwa wa shinikizo la damu pamoja na huduma ya uzazi wa mpango"

Kuwa jumla ya wanawake 2019 na wanaume 1368 ndio waliopima Ukimwi na kifua kikuu na waliokutwa na maambukizi ya Ukimwi ni 49 wanawake ni 31 na wanaume 18 wakati waliohisiwa kuwa na kifua kikuu ni wanaume 12 na wanawake 15.

mratibu huyo aliena kwa upande wa shinikizo la damu kati ya watu hao waliopima kupitia kampeni hiyo ambao ni 655 walioonekana na shinikizo la damu ni watu 191 wakiwemo wanaume 85 na wanawake 106.

Kuhusu huduma ya uzazi wa mpango waliochunguzwa 139 na wanawake 139 walipatiwa huduma ya kansa ya mlango wa uzazi.

Akiwahutubia wananchi hao mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya zote mkoani Iringa kuanzisha utaratibu wa kuanzisha mikusanyiko ya utoaji wa elimu juu ya afya.

Kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanauelewa ndogo juu ya kifua kikuu hivyo kupitia mikusanyiko hiyo wataweza kupatiwa elimu sahihi na wanapodungulika basi kuanzishiwa tiba.

Alisema katika mkoa wa Iringa taarifa zilizopo ni zaidi ya wagonjwa 1000 ambao hughundulika kila mwaka kati yao asilimia 40 wanayo maambukizi ya VVU.

Hivyo aliwataka wananchi wakihisi kuwa na dalili za kifua kikuu kukimbilia hospitali ili kuanzishiwa matibabu na moja kati ya dalili za kifua kikuu mwili kupatwa joto Kali hata wakati wa baridi kali.

mkuu huyo wa mkoa alitaja makundi ambayo yapo hatarini kupatwa na Kifua kikuu kuwa ni watu wanaoishi na VVU, watu walio katika msongamano, wazee zaidi ya miaka 65,watoto chini ya miaka mitano, watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama kisukari, saratani na mengine

Pia watu wenye lishe duni na walevi wa kupindukia hivyo kuwataka wananchi kupima afya zao

Wakati huo huo mkuu wa mkoa amekabidhi jumla ya baiskeli 125 zenye thamani ya shilingi milioni 18.7 kwa watoa huduma wa afya majumbani.

Mratibu wa shirika la Africare G. Fund Aloyce Mkangaa alisema baiskeli hizo zimetolewa kwa wahudumu wa wilaya ya Mufindi na Iringa.

Article 19

0
0

POLISI YAIPONGEZA SGA SECURITY KWA KUIMARISHA MAFUNZO KWA ASKARI

0
0
Makampuni ya ulinzi yanayofanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam yametakiwa kutoa mafunzo ya kila mara kwa askari wake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazolikumba Jiji hilo kwa sasa. Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni ya ulinzi ya SGA Security yaliyofayika katika makao makuu ya kampuni hiyo, Mbezi Beach. Mafunzo haya yaliandaliwa na Polisi Tanzania katika kuimarisha ufanisi wa askari katika makampuni binafsi. 
 
“Natoa rai kwa makampuni mengine ya ulinzi yaliyopo Mkoa wa Kinondoni yaige mfano mzuri kutoka SGA Security kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wao ili kuwaongezea maarifa yatakayowawezesha kufanya kazi kwa kujiamini na kwa uhakika,” alisema. Alisema jeshi la polisi liko tayari kutoa ushirikiano, msaada wa kitaalamu na ushauri pale itakapohitajika huku akiongeza kuwa jeshi hilo pekee haliwezi kumaliza kabisa uhalifu bila kushirikiana na wadau mablimbali yakiwemo makampuni kama SGA Security. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzan Kaganda akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na askari wa SGA Security wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni hiyo.
 
“Aidha nawaasa kuzingatia taratibu na sheria za nchi tunapokuwa tukitimiza majukumu yetu ili kazi yetu iwe na tija kwa jamii tunayoihudumia na taifa kwa ujumla,” alisema na kuwaasa askari waliopata mafunzo kuyatumia vizuri kwa manufaa yao na kampuni kwa ujumla. 
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security -Tanzania, Eric Sambu, alisema mafunzo hayo ya mara kwa mara yamekuwa na manufaa makubwa kwa kampuni kwani wameweza kuwajengea askari wao uwezo mkubwa hivi kuwafanya wananchi waongeze imani kwao. 
 
Zaidi, Mkurungenzi Mtendaji alishukuru Polisi kuanzisha mchakato huu wa kutoa mafunzo wao wenyewe moja kwa moja hii ni ishara kuwa kazi zetu katika makampuni binafsi zinatambuliwa na Polisi wanatuchukulia kama wadau wao katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini. “Tumekuwa tukiendesha mafunzo haya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwani kazi zetu zinafanana kwa kuwa tupo ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao,” alisema. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP, Suzan Kaganda akikabidhi cheti kwa mmoja wa maaskari wa SGA Security wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo.
 
Alisema katika siku tano za mafunzo askari hao waliweza kujifunza mada tofauti kama vile matumizi ya nguvu na silaha za moto, haki za binadamu, polisi jamii, uvunjifu wa haki za binadamu, huduma kwa wateja na uhusiano wa jamii, doria, eneo la tukio, usuluhishi wa migogoro na nguvu ya kukamata. “Tutaendelea kutoa mafunzo ya aina hii mara kwa mara kwa kuwa tayari tumeona matunda yake ili askari wetu kote nchini katika sehemu ambazo tunafanya kazi waendelee kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa weledi,” alisema. 
 
Kampuni ya SGA ni moja ya makampuni makubwa ya ulinzi Afrika Mashariki huku ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika ukanda huu na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 17000 huku ikiwa imewekeza vikamilifu katika rasilimali tofauti za shughuli za ulinzi na usalama Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda akipewa maelezo kuhusu chumba cha mawasiliano cha SGA Security kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo.Kulia ni Mkuu wa Ufundi wa SGA-Tanzania Prochest Peter.
 
SGA Security ni kampuni ya kwanza binafsi kusajiliwa nchini Tanzania mwaka 1984, kama Group Four Security baadae ikajulikana kama Security Group, baada ya zaidi ya miaka 32 ya shughuli na mafanikio Tanzania na 48 Afrika Mashariki, kampuni imeweza mpaka sasa kuajiri wafanyakazi takriban 5,000 nchini Tanzania na zaidi ya 18,500 katika kanda ya Afrika Mashariki, SGA Security ni moja ya waajiri kubwa katika eneo hilo. 
 
SGA Security ina uwakilishi wa kiasi kikubwa sana katika kila eneo la huduma ya usimamizi na usafirishaji wa pesa na vitu vyenye thamani na inatoa huduma hizi kwa zaidi ya Mabenki na Taasisi za Fedha 55 katika eneo la Afrika Mashariki, pia kwenye kutoa huduma za ulinzi kwa takribani mashirika 65 binafsi, kidiplomasia na NGO sekta katika eneo hilo.
 
 SGA Security imejikita zaidi pia katika ulinzi shirikishi kupitia teknolojia zaidi za kisasa kama Closed Circuit TV na Access Control, huduma za radio, Tracking ya magari na ufuatiliaji wa mizigo iwapo safarini (RFID).

PAC YATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI BUNJU B ZILIZOJENGWA NA TBA

0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma (PAC) imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumbaza watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) .

Kamati hiyo imeitaka TBA kuendelea kubuni miradi ya nyumba kwa gharama nafuu ili watumishi waweze kupata nyumba hizo kutokana na viwango vyao.

Akizungumza wa wakati wa Kutembelea miradi ya TBA Bunju B, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Joseph Kasunga, amesema kuwa mradi ni ya gharama kubwa.

Kamati hiyo imesema TBA wamefanya kazi katika kufanya utatuzi wa nyumba kwa watumishi wa serikali wanavyostaafu wanakuwa na makazi bora.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA , Arch , Elius Mwakalinga amesema kuwa wanaendelea kufanya ujenzi katika kuhakikisha kila mtumishi anaweza kupata makazi bora .

Amesema kuwa changamoto za baadhi ya viwanja walinunua na muda lakini kuna watu wanakaa ambapo wameweza kukaa nao jinsi ya kusaidiana.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na 
wajumbe wa kamati hiyo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi  wa Bunju B
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.Picha na Dotto Mwaibale

 

WAZIRI MUHONGO AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI MKOANI SINGIDA

0
0
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo akizinduzia Mradi wa umeme Vijijini Mkoa wa Singida. Uzinduzi huo umefanyika jana Machi  24/2017 na kuhudhuriwa na wafadhili kutoka WB, EU, Norway na Denmark ambao wwnafadhili mradi mkubwa wa Backbone unaoanzia Iringa- Dodoma-Singida hadi Shinyanga. Mradi huo wa REA III unatekelezwa kuziba mapengo ya maeneo vijiji ambavyo vimepitiwa na mradi mkubwa wa Backbone na vilirukwa katika Awamu ya REA II.

MAKAMANDA WA POLISI KUKUTANA DODOMA KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU

0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

MAOFISA Wakuu wa Jeshi la Polisi wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba (pichani) alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka 2017.

Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.

“Katika kikao hicho Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa, mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.

Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya Taifa”.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke na ujumbe wake, wawekezaji kutoka Denmark na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea Kilwa mkoani Lindi.
NIS2
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS3
Sehemu ya ujumbe kutoka Ujerumani na wawekezaji kutoka Denmark wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifafanua jambo katika kikao hicho.
NIS5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

UONGOZI CHALINZE WAUJIA JUU UONGOZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI MAZINGIRA KWA KUSHINDWA KUSAMBAZA MAJI

0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo .
 
Amesema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua.Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba.Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni kubwa hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua.
Ridhiwani alifafanua kwamba hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba hayajafukiwa hivyo ni ndoto za alinacha mradi huo kukamilika mwezi huu.Kwa mujibu wake, waziri wa maji anapaswa kulieleza bunge na wananchi wa Chalinze fedha za maji zilizopelekwa kwa ajili ya mradi huo na mwezi wa kuumaliza .
"Kama mradi huu utaendelea kusuasua wananchi na wawekezaji wanaokimbilia kuwekeza Chalinze watashindwa kutimiza malengo yao na kuendelea kuishi kwenye adha hii inayowapa wakati mgumu "alisema Ridhiwani.Nao madiwani walisema, kama uongozi wa mamlaka hiyo umeshindwa kazi basi wawapishe .Diwani wa Lugoba, Rehema Mwene,aliiomba serikali imsimamie mjenzi wa mabomba na matenki amalize kazi hiyo.
Nae Hassan Mwinyikondo, alieleza hatari kubwa kwa wananchi wa maeneo ya Bwilingu na Chalinze ambao wanatumia maji yasiyo safi wala salama.
Alisema mradi wa maji wa CHALIWASA hauna faida, kutokana na wananchi kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Hussein Hading'oka aliweka hofu katika kipindi kinachokuja kuwa cha mvua za masika na kuongeza kwamba mara kadhaa viongozi wa CHALIWASA wamekuwa wakisema kipindi cha mvua mitambo yao huwa inasumbuliwa na tope.hivyo kushindwa kufanyakazi za kusukuma maji.
Alimshangaa Meneja wa Mamlaka hiyo Mhandisi Christer Mchomba kushindwa kuhudhuria kikao hicho kama alivyotakiwa na Mkurugenzi Edes Lukoa .
Meneja huyo alitakiwa kwa ajili ya kuwapatia Madiwani hao maelezo ya kina kuhusiana na tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi wa Halmashauri hiyo kwa miaka mingi sasa.Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa alisema Halmashauri imetenga bajeti iwa ajili ya maeneo ambayo hayafikiwi na CHALIWASA hivyo mamlaka hiyo lazima iwe na mpango wake.
Hivi karibuni Waziri wa Mazingira Januari Makamba alipofanya ziara ndani ya Halmashauri hiyo alifika eneo la chanzo cha maji Wami na kutoa maagizo kwa wilaya na mkoa.Aliagiza Mkuu wa wilaya Alhaj Hemed Mwanga kuhakikisha na Mkoa wanakutana na wenzao wa Morogoro kuzungumzia suala la wafugaji wanaotokea Morogoro kuvamia kando ya mto WAMI na kuhakikisha wakulima wanaolima kando ya mto wondolewe mara moja.

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI 'WABESHI" WAMUOMBA RAIS MAGULI MAENEO YA KUCHIMBA WASIVAMIE MGODI WA WILLIAMSON MWADUI

0
0

Wachimbaji wa mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi ‘Wabeshi’ wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli iwatengee eneo maalum kwa ajili ya uchimbaji ili waache vitendo vya kuvamia mgodi wa almasi wa Williamson (Williamson Diamonds Ltd).

Wachimbaji hao wa madini ambao wamekuwa wakivamia mgodi na kuambulia kupigwa,kunyanyaswa na hata kuuawa na walinzi wa mgodi huo,walisema yapo maeneo ambayo hayatumiki hivyo ni vyema serikali ikawakatia maeneo ili iwe suluhu ya mgogoro kati yao na uongozi wa mgodi.

Wakizunguza na waandishi wa habari hivi karibuni kwa nyakati tofauti Wabeshi walisema wananchi wanaozunguka mgodi huo wamekuwa hawanufaiki nao kabla na baada ya uhuru hivyo wanaamini serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Magufuli itatatua kero yao ya muda mrefu.

Walisema vijana wengi wanategemea shughuli ya uchimbaji hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kumudu gharama za maisha ikiwemo kutunza familia zao.

Mmoja wa wabeshi hao Mabula Njile mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Luhumbo alisema endapo serikali itawapatia maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo hawatavamia tena mgodi wa Williamson kwenda kuchimba mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi.

“Tunashuhudia misimamo na maamuzi mazuri yanayofanywa na rais Magufuli katika kuwatetea wanyonge,sisi wabeshi tunampenda rais Magufuli tunaomba asikie kilio chetu,hatuna ajira,tunavamia kutokana na hali ngumu ya maisha,sisi shida yetu ni kupata eneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo hatutaingia tena kwenye eneo la mwekezaji”,alieleza Njile.

Juma Ng’ombeyapi mbeshi kutoka kijiji cha Ng’wang’holo alisema hajawahi kuona kiongozi yeyote wa juu wa serikali akifika katika maeneo yanayozunguka mgodi huo ili kusikiliza kero za wananchi na badala yake baadhi ya viongozi wamekuwa wakishirikiana na uongozi wa mgodi kuwagandamiza wananchi wanaozunguka mgodi huo.

“Hakuna serikali iliyokuja kutusikiliza matatizo yetu,lakini tunaona serikali ya awamu ya tano itatusaidia,tunaomba tupewe eneo la kuchimba ili tusivamie mgodi kwani sasa wananchi tunapigwa,tunateswa,tunaumizwa na wapo ndugu zetu wamepoteza maisha kutokana na kuvamia mgodi”,alieleeza Ng’ombeyapi.

“Tuna imani kubwa na rais Magufuli tunataka atusikilize,tunasubiri maamuzi ya rais kwa sababu viongozi wengine wameshindwa kutusaidia na hatuna Imani nao,tumechoka kunyanyaswa katika nchi yetu”,aliongeza mbeshi mwingine Peter Joseph kutoka kijiji cha Ng’wang’holo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Kishapu ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo Nyabaganga Talaba alionesha kushangazwa na madai ya wabeshi na kusema wachimbaji hao ‘wabeshi’ wamepewa maeneo ya kuchimba lakini hawataki kuyaendeleza kuyachimba kama wachimbaji wadogo.

“Kwa ujumla wachimbaji hawa hawana vifaa hata ule utaalamu wa kufanya kazi za madini hawana kwa hiyo hata kama wakipewa maeneo ya kuchimba hawataweza kufanya kazi”,alisema Nyabaganga.

“Wanasema wanafanya uchimbaji wa madini lakini uchimbaji wanaoufanya ni wa kuvamia mgodi,na huo wa kuvamia mgodi tumewakataza,kwa sababu ni wizi kwa wizi mwingine,kwa sababu wanaingia siyo kihalali ,wanapora,wanajeruhi hivyo tumewakataza na wala hakuna sheria inayowaruhusu kwenda huko na hilo wanalijua”,aliongeza Nyabaganga.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi wanaozunguka mgodi huo kufanya shughuli zingine badala ya kutegemea mgodi tu kwani mgodi pekee hauwezi kuwaondolea matatizo yao yote.

“Tupo wengi sana,tuna mahitaji mengi,mgodi tu hautatuondolea matatizo yetu,na mgodi tu hautatubadilisha,kuna maisha nje ya mgodi,niwashauri tu wananchi wangu tutafute kitu kingine tunachoweza kufanya badala ya mgodi”,aliongeza Nyabaganga.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Lohumbo akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho .

Mchimbaji mdogo wa madini 'Mbeshi' akionesha jeraha kichwani lililotokana na kipigo kutoka kwa walinzi wa mgodi wa Mwadui "Mgodi wa Williamson" baada ya kwenda eneo hilo kuchimba mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi .

Mchimbaji mdogo wa madini akizungumza ambapo aliiomba serikali kuwapatia eneo la kuchimba madini .

Mchimbaji mdogo wa madini akizungumza mbele ya waandishi wa habari( wengine hawapo pichani) .

Mbeshi kutoka kijiji cha Ng'wang'holo kata ya Mwadui Lohumbo akizungumza na waandishi wa habari .

Mbeshi akionesha kovu lilitokana na kipigo baada ya kuvamia mgodi wa Williamson .
Mbeshi akiomba rais Magufuli kuwapatia eneo la kuchimba ili waache kuvamia mgodi wa Williamson .
Mbeshi kutoka kijiji cha Wizunza kata ya Mwadui-Lohumbo akielezea ukatili wanaofanyiwa wachimbaji wadogo wa madini wilayani Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

TPA yakamata makontena mengine 262 yenye mchanga wa madini Bandari kavu Dsm

0
0

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutembelea bandari ya Dar es salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa. 

Mhe. Rais Magufuli alifika bandarini siku hiyo kukagua utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kutoka migodini. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema makontena hayo yaliyokuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha yamebainika leo (jana) tarehe 25 Machi, 2017 katika msako mkali unaoendeshwa na Mamlaka yake.

Mhandisi Kakoko amesema makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es salaam. 

Mhandisi Kakoko amesema jumla ya makontena 256 yalikuwa katika bandari kavu ya MOFED, wakati makontena mengine sita yalikuwa tayari yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa.

Ametoa wito kwa makampuni yote ya madini yenye shehena za mchanga yajitokeze yenyewe na kuonesha mizigo yao popote ilipo nchini kabla haijabainika katika msako kabambe unaondeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Orodha ya makontena hayo yaliyobainika inaonesha yalifika bandarini hapo katika nyakati tofauti kutoka migodi ya Buzwagi na Pange Mines.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Bw. Ramadhani Mungi amesema bandari zote nchini ziko salama na kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kuwekwa askari na vifaa vya kisasa vya ulinzi zikiwemo kamera.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akifafanua jambo kufuatia tukio la kukamatwa kwa makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akiwa ameongoza vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya kufanya ukaguzi na kubaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es

KUELEKEA UZINDUZI WA TOVUTI MAAFISA HABARI WANOLEWA

0
0
 
Washiriki kutoka mikoa ya lindi,mtwara na Ruvuma wakiwamo maafisa Tehama wakiendelea na mafunzo ya uanzishaji na uendelezaji wa tovuti katika ofisi za umma ikiwemo halmashauri na ofisi za wakuu wa mikoa



Na Abdulaziz video,Mtwara

Katika kuelekea siku ya uzinduzi huo ambao kwa kanda ya kusini utakaofanyika mkoani Mtwara Machi 27 mwaka huu, wizara ya nchi ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Nchini PS3, imeendesha mafunzo kwa maafisa habari wa ofisi za wakuu wa mikoa pamoja na halmashauri juu ya matumizi ya tovuti, ambapo miongoni mwawashiriki wameeleza kunufaika na mpango huo utakaojenga utawala bora.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya washiriki wameshukuru Mradi wa PS 3 Kwa kuwezesha sekta za umma kuwa na tovuti ambazo zitaanza kuwa hai ifikapo March 27 na kusaidia maafisa habari kuanza kuwajibika ili jamii iweze habarika na fursa mbali mbali bila gharama kubwa

Aidha walieleza kuwa Wakati serikali ikielekea katika uzinduzi wa matumizi ya Tovuti katika ofisi za umma ikiwa ni pamoja na ofisi za mikoa na halmashauri, Tayari baadhi ya wananchi mkoani Mtwara wamepongeza hatua hiyo na kudai kuwa itasaidia kuwapo kwa uwazi katika upatikanaji wa taarifa.

wananchi hao wamesema kutokana na kuwapo kwa utandawazi unaochangiwa na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano, wananchi watanufaika na huduma hizo za Tovuti katika kupata taarifa ambazo hazina ulazima wa kuzifuatilia katika makao makuu ya ofisi husika.

Mafunzo hayo ambayo yameanza Machi 20 kwa kuhusisha maafisa habari na maafisa TEHAMA kutoka katika mikoa ya Mtwara, lindi na Ruvuma yanatarajiwa kuhitimishwa Machi 27 mwaka huu ikifuatiwa na zoezi la uzinduzi wa tovuti hizo.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images