Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1180 | 1181 | (Page 1182) | 1183 | 1184 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkutano Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, (AICC), leo Machi 23, 2017. Kauli mbiu ya mwaka huu ya mkutano huo ni, "“Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii” 
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (pichani juu), ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda..
  Waziri ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2017 wakati akifungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa KItuo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
  “Nimeelezwa kuwa nyinyi PPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Jeshi la Magereza mmeingia kwenye makubaliano ya pamoja ya kuanzisha viwanda vikubwa na vya kisasa vya kuzalisha sukari katika eneo la Mkulazi na Mbigiri Morogoro.” Alisema Waziri Dkt. Mpango
  Akifafanua zaidi kuhusu mpango wa PPF kwa ushirikiano na NSSF na Jeshi la Magereza kwenye uwekezaji mkubwa wa viwanda, Dkt. Mpango alisema, “Mimi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama ni mashuhuda wa hilo kwani tuliweza kujionea eneo la mradi la Mkulazi na ujenzi wa miundombinu tulipolitmbelea katika eneo hilo mwezi Desemba mwaka jana.” Alisema.
  Akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw.Ramadhan Khijjah, (pichani juu), alisema, kauli mbiu ya mkutano huu wa 26 wa Wanachama na Wdau wa PPF ni “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Hifadhi ya Jamii”.
  “PPF imedhamiria kwa dhati kabisa kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ya kjuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda kama inavyoelezwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/2017 hadi 2010/21.
   Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio alisema Mkutano wa mwaka huu ni wa siku mbili na umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 800 na lengo la kuchagua kauli mbiyo iliyoelezwa hapo juu ya “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii” ili kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
  Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Rmmanuel Martin, akitoa taarifa ya fedha ya Mfuko
   Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi.Irine Isaka, (mbele kushoto), ni miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria mkutano huo
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizunhumza na Meneja wa PPF, Mkoani Arusha, Bw. Sule
   Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw.Adam Mayingu (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Bw. Daudi Msangi
   Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akitoa hotuba ya ukaribisho
   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PPF
   Baadhi ya wageni waalikwa kutoka WCF
   Wajumbe wakiwa mkutanoni
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba yake ya ufunguzi
   Bi.Stephanie Nandi, akiwa na mwanaye mchanga akitoa ushuhuda baada ya kufaidika na Fao la Uzazi
   Mfugaji Bw.Mrida Mshoto Marocho, akitoa ushuhuda kuhusu faida aliyopata ya bima ya Afya, baada ya kujiunga na mpango wa Wote Scheme
   Bw.Kulwa Mohammed, mmoja wa watu waliotoa ushuhuda wa jinsi alivyofaidika na Fao la Elimu. Kulwa ni Mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM)
   Mjumbe akipitia jarida la PPF lenye maelezo ya kina kuhusu shughuli mbalimbali za Mfuko
   Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo
  Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred akitoa maelezo ya uwekezaji ya Mfuko huo.
  Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi tuzo, Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu wa TANESCO, Nathan K. Daimon, baada ya Shirika hilo la Umeme nchini kuwa mshindi wa jumla kwa Mashirika ya Umma yanayowasilisha michango yao kwa wakati na mingi inayofikia Bilioni 2 kwa mwaka.
   Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, (kushoto), akipeana mikono na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, wakati akimkabidhi vifaa vya hospitali kwa niapa ya PPF pembezoni mwa mkutano huo. PPF imetoa msaada wa vifaa hivyo vyenye thamani inayokaribia Milioni 100. Vifaa hivyo kwa mujibu wa Waziri Ummy, vitapelekwa kwenye vituo vya afya 11 kote nchini
  Waziri Ummy akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo
  Mgeni rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kushoto), akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi.Irine Isaka, wakati akiondoka ukumbi wa Simba baada ya kufungua mkutano huo

  0 0

   Waziri  wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania  Gerson Lwenge ameishukuru Kuwait kwa kusaidia miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa hapa nchi na kueleza kuna anatarajia ushirikiano zaidi hasa katika miradi ya umwagiliaji. 

  Kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa  na Mfuko Wa Kuwait Wa Maendeleo ya Kiuchumi kwa miradi mikubwa ya umwagiliaji. 

  Waziri Lwenge alitolea mfano wa mradi wa hivi karibuni katika mikoa ya Same na Mwanga, Kaskazini  mwa Tanzania, mradi ambao una thamani ya dola za marekani milioni 34.

  Waziri pia aligusia miradi mingine miwili  ya umwagiliaji katika  bonde la Muhongo na Luichi kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambayo ina thamani ya dola za marekani milioni 15. 

  Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait unatarajia kutuma wataalamu wake Tanzania kwa  lengo la kutathmini miradi hii  miwili katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018. 

   Waziri pia alitoa Pongezi na shukrani zake za dhati kwa ujumbe wa Kuwait Red Crescent Society uliofanya ziara nchini Tanzania hivi karibuni na kufungua visima 16 katika shule mbalimbali  za serikali ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Kisima kwa Kila Shule.

  Ikumbukwe kuwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassim Al Najema ameanzisha  mpango huo wa Kisima kwa Kila Shule kuunga mkono wito wa Rais John Magufuli wa kusaidia sekta ya elimu nchini na kukabiliana na ukame na uhaba wa maji safi ya kunywa.

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli inautashi wa dhati wa kuboresha mazingira ya uwekezani na biashara nchini kwa kuondoa rushwa na urasimu katika sekta ya umma, hivyo amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Mauritius kuja nchini.

  Amesema Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kubadili mifumo yake ya kisheria, kitaasisi na kifedha ili kuhakikisha wawekezaji wanahudumiwa ipasavyo na kupewa umuhimu wanaostahili kwani ni wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

  Waziri Mkuu amesema hayo jana (Alhamisi, Machi 23,2017) wakati akifungua kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius lilifanyika katika Hotel ya Labourdonnaise mjini Port Louisnchini Mauritius. Kongamano hilo liliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

  Alisema Tanzania ina uchumi imara unaofuata misingi ya soko huria, ambapo mwekezaji ana uhuru wa kufanya biashara bila ya kuingiliwa na Serikali, hivyo sekta binafsi imepewa kipaumbele katika shughuli za kiuchumi na kibiashara nchini.

  “Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli nawakaribisha kwa mikono miwili kuja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda na utalii na kutembelea vivutio vya utalii na kupata burudani ya aina yake na kwa wafanyabiashara Tanzania ni mahali pazuri kwa kuwekeza,” alisema

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind Kumar Jugnauth katika mkutano wa Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na Mauritius kabla ya kufungua mkutano huo mjini Port Louis, Machi 23, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
    Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind  Kumar Jugnauth akizungumza katika mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius mjini Port Louis Machi 23, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji  kati ya Tanzania na Mauritius wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua  mkutano huo mjini Port  Louis  Machi 23, 2017
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius mjini Port Louis nchini Mauritius , Machi 23, 2017.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji  kati ya Tanzania na Mauritius wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua  mkutano huo mjini Port  Louis  Machi 23, 2017
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind Kumar Jugnauth baada ya kufungua mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius mjini Port Louis Machi 23, 2017  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak  ambaye aliongozana na Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte, Ikulu jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimsikiliza Balozi wa  Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak  alipokuwa akifanya mazungumzo nae mapema leo , Ikulu jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza  Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte, Ikulu jijini Dar es salaam. alipokuwa akifanua jambo mapema leo , Ikulu jijini Dar es salaam.
   Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK (katikati) akimtambulisha Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi huo Bi. Beatrice Alperte (kushoto) kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK (kushoto) na Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte (kulia), Ikulu jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  0 0

  Benjamin Sawe-Maelezo

  Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema mpaka kufikia mwaka 2020 litawawezesha watanzania kutumia gesi majumbani mwao hivyo kupelekea upungufu wa uharibifu wa mazingira nchini.

  Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Eng. Kapuulya Musomba amesema muda mrefu kumekuwa na uharibifu wa mazingira hivyo kupatikana kwa nishati ya mafuta na gesi kutaiwezesha Tanzania kuwa mahali salama kimazingira ikiwa ni pamoja na ukuaji wa sekta ya uchumi.

  Alisema katika robo ya pili ya mwaka 2017 shirika limekamilisha usambazaji wa mabomba ya gesi kwa matumizi ya majumbani jijini Dar es Salaam na zaidi ya viwanda 300 vimeunganishwa na nishati ya gesi hapa nchini hivyo kupelekea upatikanaji wa umeme wa uhakika.

  Kuhusu upangaji wa Bei kwa matumizi ya gesi itakayosambazwa majumbani Eng. Musomba amesema Taasisi yake itashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.

  Hivi sasa zaidi ya asilimia 50 ya umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia hivyo mipango ya Serikali ni kulifanya Shirika hilo kuchangia zaidi mapato Serikalini yanayotokana na rasilimali hiyo.Alisema Eng. Musomba

  Alisema TPDC imejipanga kuwekeza kwenye shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi ili Taifa linufaike na rasilimali hiyo.

  Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Eng. Musomba alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.

  Alisema kukamilika kwa mradi wa (Liqufied Naturla Gas- LNG)utakuwa ni fursa kwa watanzania kupata ajira katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kuchangia pato la mwananchi,wawekezaji na Taifa kwa ujumla.

  Alisema uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana hivyo amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuilinda miundombinu inayopita maeneo yao.

  TPDC inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hiyo ya gesi na mafuta.

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishusha miti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya vyanz vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba mti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisaidia katika zoezi la ubebabji miti kwa ajili ya kuotesha.
  Wafanyakazi wa MUWSA wakiwa wamebeba mit kwa ajili ya kuotesha katika chanzo cha maji cha Shiri.
  Kaimu Mkurugenzi wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji cha Shiri.

  Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiotesha miti katika chanzo hicho.
  Hii ni sehemu ya mitiiliyooteshwa Mwaka jana katika eneo hilo zoezi lililooongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Saidi Mecky Sadicki.
  Huu ndio mti uliooteshwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Mecky Sadicki katika eneo hilo.
  Chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai kinachoimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi.(MUWSA.)
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuotesha miti katika chanzo hicho.


  Chanzo kipya cha maji cha Mkashilingi kilichopo jirani na chanzo cha chemichei cha Shiri.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Kufatia kuzinduliwa kwa ofa Kabambe ya Airtel ijulikanayo kama “Hatupimi Bando” ofa inayowapa wateja wake uhuru wa kuongea bila kikomo, wafanyakazi wa Airtel wamejipanga kuingia sokoni na kukutana na wateja kwa lengo la kutoa elimu zaidi juu ya huduma na bidhaa za Airtel

  Mpango huu unategemea kufanyaka leo ijumaa ambapo wafanyakazi wa Airtel nchi nzima watakutana na kuzungumza na wateja wao ana kwa ana katika maeneo mbalimbali na kuitambulisha ofa hii ya “Hatupimi Bando” pamoja na kuwaunga wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel ili nao pia waweze kufurahia bidhaa na huduma mbalimbali na kujiunga na ofa hii kabambe ya “Hatupimi Bando”

  “Tunapenda wateja wetu waelewe vyema ofa hii ya “Hatupimi Bando” itakayowasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha gharama katika matumizi yao ya simu kwani ofa hii inawapatia gharama nafuu zaidi za mawasiliano sokoni.

  wateja wetu wanaweza kujinga “Hatupimi Bando” Kwa kiasi cha shilingi 1000/= ,shilingi 5000 kwa wiki, na vilevile unaweza kujiunga na kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= na kufurahia huduma yakutopimiwa dakika na kuongea bila kikomo”. Alisema Jackson Mmbando, Meneja Uhusiano wa Airtel

  Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza Mmbando

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mwaine Ismail Nchemba (Viti Maalum ) Tabora akifafanua jambo wakati kamati yake ilipozuru tawi la Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Tanga leo asubuhi.
  Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dk.Henry Mambo akifurahia jambo wakati wakiwasilisha taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea Chuo hicho tawi la Tanga leo asubuhi
  Wanakwaya wa Chuo wakiimba wimbo maalum mbele ya wajumbe wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, leo asubuhi chuoni hapo.
  Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Tanga , Hassanal Issaya, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mwaine Ismail Nchemba (Viti Maalum ) Tabora baada ya ujumbe wa Kamati hiyo kuwasili tawini hapo eneo la Nkange Jijini Tanga. wa pili kushoto ni kushoto kwa Mkurugenzi huyo ni Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo.

  0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.

  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, leo (jana) amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bi. Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.

  Ameeleza kwamba pamoja na mambo mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama hicho, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa kipindi cha mwaka 2017 - 2022.

  “ Kutokana na Chama chetu kuwa Kinara wa Demokrasia wanachama wengi wamejitokeza kuwania nafasi hizo ili waweze kuiwakilisha vyema CCM na serikali inazoziongoza katika Bunge hilo muhimu.

  Pia Wana CCM na wananchi kwa ujumla tukumbuke kuwa fursa hizi zisingeweza kujitokeza kama nchi yetu ingekuwa katika mashaka na migogoro, hivyo wito wangu tuendelee kuwa wamoja ili wenzetu waweze kutuwakilisha vyema.”, alisema Bi. Waride.

  Kikao hicho kimefanyika kwa kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la 2012, ambayo inatoa Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya CCM Zanzibar, kupokea na kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.

  Bi. Waride amesema jumla ya wana CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba waruhusiwe na CCM kugombea nafasi hizo.

  Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inapaswa kuwakilishwa na Wabunge tisa (9).

  Aidha kikao hicho kilimtambulisha Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake aliyopewa na Chama ipasavyo.

  Hata hivyo Kikao pia kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hizo muhimu za Uongozi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama hicho.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mberwa Kairuki akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping wakati wa hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho iliyofanyika Ikulu kwenye Ukumbi wa Great hall of the people siku ya Ijumaa tarehe 17 Machi 2017.

  Balozi Kairuki (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping   Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Mbelwa Kairuki amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping tarehe 17 Machi 2017.  

  Hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya China (Great Hall of the People) ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi na maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China. 

  Katika mazungumzo mafupi baada ya kuwasilisha hati, China na Tanzania zimekubaliana kukuza zaidi mahusiano ya kiuchumi kupitia mpango maalum wa China wa kuhamishia viwanda vyake nje ya China (Production Capacity Cooperation Programme) pamoja na programu ya kukuza ushirikiano wa biashara na ujenzi wa miundombinu ijulikanayo kama Maritime Silk Road initiative. 

  Aidha, Tanzania imeihakikishia China kuendelea kuunga mkono sera yake ya ONE CHINA POLICY sambamba na kuunga mkono mtazamo wa China kuhusu mgogoro wa Bahari ya Kusini mwa China.

  0 0

  Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Wanachama Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Africa Region ) Bw. Demetrius Mgalami akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 72 wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika kusini Mhe Lindiwe Maseko ( wa pili kushoto) na Katibu wa Chama cha  CPA Afrika ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania   Dkt Thomas Kashililah.
   Wajumbe wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika  wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano huo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji CPA Afrika  wakati wa Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Viongozi wa Kamati hiyo.
  Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Lindiwe Maseko akizungumza wakati wa Mkutano huo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia waliokaa mbele) ambaye pia ni Mwenyejiti wa Bodi ya Chama cha CPA Afrika akiongoza kikao cha Bodi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Mhe. Lindiwe Maseko. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo.(Picha na Ofisi ya Bunge).                                              

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe akisalimiana na Naibu wake Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili katika ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.

  0 0

  Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuanzia Jumatatu, tarehe 27 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mtwara. 
  Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mtwara. 

  Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mtwara wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mtwara.

  Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

  Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.

  Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 784 661 080 au +255 714 646 322..

  0 0

  Wafanyakazi wa Coca-Cola wakiwagawia wanafunzia wa Shule ya Sekondari ya Olorieni Vinywaji vya Coca-Cola katika eneo la shule hiyo. 
  Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni akionyesha kipaji cha kucheza na Baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali. 
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza na baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali. 
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
  Wanafunzi wa wawili wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza muziki kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola katika shule mbalimbali. 
  Mwongozaji wa Promosheni (Supervisor) Onesmo Swila Akimkabidhi zawadi ya mipira ya miguu mwalimu wa michezo wa shule ya Sekondari ya Olorieni katika promosheni yao ya Onja msisimko na Coca-ola inayoendeshwa katika shule mbalimbali jijjini Arusha. 
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kuimba kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali. 
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha. 
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakigongeana sheazi mara baada ya kugawiwa vinywaji kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha. (Picha na Ferdinand Shayo). 

  Kampuni ya Bonite Bottlers Kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola imezidi kuhamsisha wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao kupitia Promotioni ya Onja Msisimko na Coca-Cola wanayoiendesha katika shule mbalimbali jijini Arusha. 
   
  Cocacola imefanya hayo katika shule Sekondari ya Olorieni jijini Arusha ambapo baadhi ya wanafunzi walipata Fursa ya kuonyesha vipaji vyao ikiwemo kucheza na baiskeli katika jukwaa, kucheza muziki pamoja na kuimba. Msimamizi wa promosheni hiyo Onesmo Swila amewataka wanafunzi katika shule hizo wanazotembelea ikiwemo Sekondari ya Olorieni ambayo wameitembelea, kuendeleza vipaji vyao kwa kila fursa wanayopata kwa kuwa kipaji ni hazina.

   “wanafunzi acheni kuficha vipaji vyenu, vionyesheni, ili mpate fursa ya kuvikuza, sisi Coca-Cola tumeamua kuwahamasisha kwa lengo kuwatia moyo ili mfikie malengo yenu.” Alisema Onesmo Aidha licha ya kuwashukuru walimu wa shule hiyo kwa kuwakubalia kutembelea shule hiyo na kuwagawia wanafunzi zawadi ikiwemo ya kinywaji cha Coca-Cola, amesema ziara hiyo wataendelea nayo katika shule mbalimbali jiji Arusha ili kuwaonjesha wanafunzi Msisimko wa Coca-Cola. 

  Mwalimu wa Michezo katika Shule ya Sekondari ya Olorieni, Haroon Maluli akipokea zawadi ya Mipira kutoka Coca-Cola, Ameshukuru kwa zawadi hiyo huku akiwasihi wanafunzi kutoficha vipaji vyao, bali wavionyeshe kwa kila fursa inayopatikana ili kuvikuza zaidi. “Tunashukuru kwa zawadi ya mipira, ila nawasihi wanafunzi kutumia fursa kama hii iliyoletwa na Coca-Cola kuonyesha vipawa vyenu, kwani hata sisi tulivyokuwa tunasoma hatukuvificha ndio maana tupo hapa” alisema Mwalimu Haroon.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Serikali ya Korea kupitia mradi wa ''Thank you Small Ribray program'' leo imekabidhi Vifaa na kuzindua maktaba ndogo ya kisasa katika ofisi za makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo balozi wa Korea nchini Song Geum Young amesema kuwa serikali yake licha ya kusaidia serikali katika miradi mingi lakini kwa sasa wameamua kusaidia katika kuwawezesha watoto kupata elimu inayoendana na wakati.

  "sisi kama korea tunaamini kuwa ukimpa mtoto elimu umeweza kumpa maisha ya kesho, hivyo vifaa hivi vitaweza kuwasaidia katika kukuza taaluma yao " amesema Balozi.Balozi ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto waweze kutumia maktaba hiyo kwa kutumia sehemu hiyo kwa ajili kukuza taaluma yao .
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakikata utepekuashiria uzinduzihuo.

  Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young akizungumza kabla ya uzinduzi wa wa Maktaba ya kisasa ambayo imetolewa na Serikali ya korea.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo, akikabidhi vitabu kwa Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah
  Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika Makumbusho ya Taifa.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika ukumbi wa Makumbusho ya taiafa kwa msaada wa Serikali ya watu wa Korea.
  Baadhi ya wadau walioshiriki tukio hilo
  Viongozi mbalimbali akiwemo na balozi mteule wa korea wakifatia hotuba ya balozi
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakishuhudia tukio hilo
  Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah akizungumza na waandishi wa habari 

  Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa

  Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young wakipata maelekezo jinsi ya namna vifaa vya kielektronic vinavyofanya kazi katikakutoa elimu kwa watoto ndani ya maktaba hiyo ambayo imefadhiliwa na serikali ya Korea

  Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah wageni waalikwa wengine waliohudhuria katika hafla hiyo

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017.
  Profesa Palamagamba kabudi akila kiapo mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ,kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
    Waapishw wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe  Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache  baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017

  0 0


  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO mala baada ya kutoka kula kiapo leo Jijini Dar es Salaam.
  PLO 1
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bi. Flora Mwnyenyembegu wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura(wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
  PLO 2
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Khalfan Milao wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
  PLO 3
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bibi. Zamaradi Kawawa wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
  PLO 4
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo  Yusuph Omary wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
  PLO 5
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa OElisante Ole Gabriel akimtambulisha Kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
  PLO 6
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake mapokezi yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura.
  Picha zote na Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.

  FORUMCC imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa hapa nchini Tanzania. 

  Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili.

  Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la bajeti ya mwaka 2017/18.

  Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi amesema serikali kupitia TAMISEMI iko karibu na wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza majanga mbalimbali hapa nchini, na wao TAMISEMI wana jukumu la kubwa kwenye asasi za kiraia kuingia kwenye miradi inayohusu mabadiliko ya Tabianchi.

  Pia Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona aliwaomba wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo kushirikiana na FORUMCC ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwenye suala la mabadiliko ya Tabianchi linalotishia maendeleo ya jamii za mbalimbali na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

  Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara mbalimbali, watafiti na waandishi wa habari. 
  Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akitoa mada kuhusu kazi za TAMISEMI pamoja na ushirikiano wake kwenye masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali pamoja na kutoa maoni kwa maofisa wa wizara kuangalia namna ya kushirikiana ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
  Mkutano ukiendelea uliowakutanisha wadau mbalimbali uliowakutanisha ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
  Mtaalamu wa Masuala ya Nishati, Erneus Kaijage akiwasilisha mada kuhusu uwekezaji wa fedha katika sekta ya nishati kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi leo jijini Dar es Salaam


  Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wadau mbalimbali wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliowakutanisha wadau hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Sayansi jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali waliokutana ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
  Mwezeshaji wa Mkutano wa FORUMCC, Abdallah Henku akizungumza jambo kwenye mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi.  Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara, watafiti na waandishi wa habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) mkutano ulipofanyika leo ulioandaliwa na FORUMCC.

  Picha ya Pamoja

older | 1 | .... | 1180 | 1181 | (Page 1182) | 1183 | 1184 | .... | 1898 | newer