Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1179 | 1180 | (Page 1181) | 1182 | 1183 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni wa kumtafuta diwani wa kata ya Igombavanu wilayani mufindi akikitumikia chama.  Na Fredy Mgunda, Mufindi 

  KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama ametangaza nia ya kugombea nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la afrika mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.

  Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili inatumika barani afrika kama lugha mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba zaidi barani afrika.

  “Nimetembea nchi nyingi hapa afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati baba wa taifa mwalimu Julias Kabarage Nyerere”.alisema Mhagama

  Mhagama alisema kuwa atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wengi ni wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.

  “Tanzania tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata mali ghafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa nchi”.alisema Mhagama.

  Aidha Mhagama amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapaulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania ya viwanda.

  “Angalia sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili nzuri ya kuukalibia uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki nitandelea kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda vyao”.alisema Mhagama

  Mhagama aliwaomba watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wa mataifa ya Afrika wamekubaliana kufungua fursa za kiuchumi baina ya nchi hizo pamoja na kuweka utaratibu wa kutumia hati moja ya kusafiria.

  Alitoa kauli hiyo jana (Jumatano, Machi 22, 2017) wakati akingumzia makubaliano yaliyofikiwa katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP) uliofanyika nchini Mauritius Machi 20 hadi 21, 2017. Waziri Mkuu alimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli.

  Waziri Mkuu alisema viongozi hao wamekubaliana kwamba mataifa ya Afrika yawe na hati moja ya kusafiria, ambayo itawawezesha wananchi kuingia nchi yoyote ndani ya bara hilo bila ya vikwazo kwa lengo la kurahisisha muingiliano wa watu na bidhaa.

  Alisema jambo jingine walilokubaliana ni kuimarisha Jumuiya zao ikiwemo ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kuzishawishi nchi nyingine ambazo hazijajiunga kujiunga jumuia hizo.

  Alisema viongozi hao walijadili namna watakavyoweza kuinua uchumi na kuweka mikakati ya kuimarisha viwanda, ambapo Tanzania ipo katika nafasi nzuri kwa kuwa tayari inatekeleza mpango wa kukuza uchumi wake kwa kupitia sekta ya viwanda.

  Viwanda ndiyo mkombozi wa changamoto mbalimbali barani Afrika ikiwemo ya ajira, hivyo Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake,” alisema.

  Jukwaa hilo lilizinduliwa Machi 20, 2017 na Waziri Mkuu wa Swazland Bw. Barnabas Sibusiso Dlamini kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Chad, Idriss Deby. Pia Bw. Dlamini alimuwakilisha Mfalme Muwsati wa III.

  Bw. Dlamini alisema nchi za Afrika zinatakiwa kuboresha mitaa yake na kujikita katika kutoa elimu ya masuala ya sayansi na viwanda ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa masuala hayo angu wakiwa na umri mdogo.

  Alisema iwapo wanafunzi wataanza kujifunza masuala ya viwanda kuanzia shule watakuwa na uelewa wa kutosha wa masuala hayo jambo ambalo litawarahisishia kupata ajira katika viwanda mbalimbali, hivyo kuondokana na tatizo la ajira linalozibakili nchi nyingi za Afrika.

  Uzinduzi wa jukwaa hilo ulikuwa na ajenda nne ambazo zilihusu sekta ya viwanda, kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika, kukuza ujuzi katika taaluma mbalimbali na kurahisisha muingiliano wa watu na bidhaa baina ya mataifa hayo.

  Jukwaa hilo lilifanyika kwa siku mbili lilihudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 23, 22017.

  0 0

   Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha kuengeneza nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee kilichopo nje kidogo ya mji wa Port  Louis nchini Mauritious. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo zilizoshonwa  kwa vitambaa vilivyotengenezwa na kwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee cha Mauritius wakati alipotembelea kiwanda hicho, nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini Mauritius, Machi 22, 2017.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza viongozi wa kiwanda cha  nguo cha Mauritius cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis Machi 22, 2017.


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.

  Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini Tanzania na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi pamoja na nguo kwa kuwa kuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.

  Waziri Mkuu alitembelea kiwanda hicho kilichoko katika mji wa Latour Koenig jana (Jumatano, Machi 22, 2017) na kujionea namna wanavyotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuamua kuwakaribisha waje kuwekeza nchini.

  “Tumefarijika na uwekezaji wenu na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nvingi na yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema madhumuni  ya kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika  viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na kuwawezesha wakulima kupata tija.

  “Tunalima pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi ”  alisema.

  Alisema viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato.

  Mbali na kuwakaribisha wawekezaji hao, pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya kuiuza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho Bw. David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.

  Bw. David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200. “Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka makubwa barani Ulaya,”

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 23, 2017.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeanza kuandikisha wanachama kutoka sekta na serikalini za binafsi na ongezeko hilo imetokana na wanachama kutumia fursa ya kuchagua mfuko ulio sahihi wenye ubora .

  Akizungumza leo na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge amesema pamoja na kuwepo kwa huduma hiyo mfuko umeboresha huduma za ulipaji wa mafao kwa wakati.

  ‘’ Mwanachama wa LAPF anaekaribia kustaafu hutaarifiwa mapema ili kujiandaa kwa kuwa na nyaraka zote zinazohitajika na hulipwa siku moja kabla ya kustaafu’’.

  Mkeyenge ameongeza kuwa kwa mwaka 2015\2016 mfuko wa Pensheni umeweza kulipa kiasi cha bilioni 107 kwa wanachama wake huku kipindi cha mwaka 2011\2012 mfuko ulifanikiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni 38.1 kwa wanachama hii ilitokana na ongezeko la wanachama.

  ‘’Mwaka 2015\2016 wanachama 316 wamepewa mikopo kiasi cha bilioni 10.5 ambapo hadi kufikia sasa LAPF ina wanachama zaidi ya 165,000’’.aliongeza Mkeyenge.

  Mfuko wa Pensheni umekuwa ukiwahudumia wanachama wake kwa takribani zaidi ya miaka 70 na mafao ambayo yanatolewa ni pamoja na pensheni ya uzee,warithi,ulemavu,mikopo ya elimu pamoja na pensheni ya kujitoa.
  Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya LAPF inavyofanya kazi kwa wanachama leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Afisa Matekelezo Mwandamizi LAPF, Katiti Katiti.picha na Emmanuel Mssaka,Globu ya jamii.
  Afisa Matekelezo Mwandamizi LAPF, Katiti Katiti akizungumza na waandishi wa habari juu ya LAPF inavyofanya kazi kwa wanachama wake, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge
  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe S. Kebwe ametoa rai kwa vijana kujiweka katika vikundi ili wapate fursa za kupata mikopo kutoka Serikalini na kwa wadau mbalimbali. 

  Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo leo mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii juu ya maendeleo ya vijana wenye ulemavu waliopo chini ya Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na shirika la Plan International.

  Mhe. Kebwe amesema suala la vijana na wanawake kuunda vikundi ni la muhimu kwani Serikali kupitia Halmashauri zote nchini ina utaratibu wa kutenga asilimia kumi kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri husika kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na vijana ili waweze kujikwamua hasa katika nyanja ya kiuchumi.

  “Serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu hivyo kupata mradi kama huu wa kuwasaidia vijana kiuchumi kutoka Umoja wa Ulaya ni fursa nzuri kwa vijana kujikomboa na njia rahisi ya kuoneka mna uhitaji ni dhahiri kuwa mnatakiwa muwe katika vikundi,”alisema Mhe. Kebwe.

  Mhe. Kebwe ameongeza, uundwaji wa vikundi unasaidia kufahamu ukubwa wa kikundi, kiasi cha msaada, eneo kikundi kilipo na aina ya shughuli inayofanywa na kikundi husika.

  Amefafanua kuwa kwa hali halisi fedha za mradi haziwezi kutolewa kwa mtu mmoja mmoja bali ni kwa njia ya vikundi ili kurahisisha ufatiliaji na kupunguza gharama za uendeshaji hivyo vijana wasitarajie kupata mkopo au kusaidiwa na shirika wakiwa wamekaa vijiweni.

  Aidha,amewasisitiza vijana hasa walemavu kujitokeza kwa wingi katika awamu ya mwisho ya mradi huo kwani mradi huo upo kwa ajili ya vijana wote.

  Mradi huo wa miaka mitatu (2015/2018) unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

  0 0

  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa
  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akipanda mti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (katikati) akiongozwa na Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (wa pili kushoto) kutembelea bwawa la maji na kupanda miti katika kilele cha Wiki ya Maji. Wengine pichani kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Steven Cleophace (kulia).
  Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese na viongozi kuhusu mradi wa maji ya bwawa la Sekeididi.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
  Wananchi wa kijiji cha Sekeididi Kata ya Sekebugoro wakifuatilia maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa yaliyofanyika kijijini hapo.
  Baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la upandaji miti.  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameagiza wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa na Maji kuhakikisha hakuna mtu anayefanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.

  Telack alitoa agizo hilo juzi wilayani hapa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati wa kilele cha maadhimisho Wiki ya Maji yaliyofanyika kijiji cha Sekeididi.

  Aliagiza wakurugenzi hao kuhakikisha vyanzo hivyo vinapandwa miti ili kutunza uoto wa asili ambao mara nyingi huathiriwa na ukame kutokana na kukosekana kwa miti.Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao wasimamie utekelezaji wa sheria ya utunzaji wa mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji, kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji.

  “Utunzaji wa vyazo vya maji ni jambo muhimu katika upatikanaji wa maji na hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti eneo linalozunguka vyanzo.“Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu cha 57, kifungu kidogo cha 1 kinakataza mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji,” alisema.

  Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti kwenye bwawa la Sekeididi ambalo litakuwa likitoa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.Telack aliwataka wananachi kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao.

  Alisema miradi hiyo imeibuliwa na wananchi wenyewe kupitia vikao vyao na hivyo wanapaswa kuendeleza jitihada zao ili kunufaika nayo kwa kuwa wasimamizi wake.Awali akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la maji kijijini hapo, Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya, Bernad Bwire alisema kuwa lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 119.8 za maji.

  Alisema bwawa hilo linalojengwa kwa gharama ya sh. milioni 662.4 linatarajiwa kuhudumia wananchi 16,627 wa vijiji vinne vya Bugoro, Ngwashinong’ela na Mwagalankulu katika kata ya Sekebugoro.

  Mhandishi Bwire alisema ili kulifanya bwawa lidumu wananchi wamejipanga kuhifadhi mazingira yanayolizunguka kwa kuzuia mifugo kuingia katika eneo la bwawa.Aliongeza kuwa katika kipindi cha Wiki ya Maji jumla ya miti 230 imeshapandwa na kuwa wanatarajia kupanda mingine 800 zaidi katika eneo la kuzunguka bwawa hilo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati Bw. Sunil Kaushal pamoja na ujumbe wake uliomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati Bw. Sunil Kaushal ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  0 0


  Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt Gideon Kaunda akizungumza na Wananchi wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika katika kijiji cha Image wilayani Kilolo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
  Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kulia), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia), Mbunge wa Kilolo, Mhe.Venance Mwamoto (wa tatu kulia) wakisoma maombi ya wananchi ya kuunganishiwa umeme katika Mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu, wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika katika kijiji cha Image wilayani Kilolo.
  Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana wa Jamii ya Kimasai wilayani Kilolo wakitumbuiza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika katika kijiji cha Image wilayani Kilolo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kuli mstari wa nyuma) pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuzindua mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa. Wa nne kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt Gideon Kaunda. Waliosimama mbele ni Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana wa Jamii ya Kimasai wilayani Kilolo.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na hadhira (haipo katika  picha) katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi vya Luninga  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy akizungumza na hadhira (haipo katika picha) akitoa maelezo mafupi kuhusu Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali ya China  katika  hafla ya  Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa nchini China, Bi. Ma Li akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wakifuatilia kinachoendelea kwenye uzinduzi wa tamthiliya
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG wakipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika
  Tamthiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” ikioneshwa mara baada ya kufanyika uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Kikundi cha Burudani kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kikiendelea kutoa burudani
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu  wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG (katikati waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji na washiriki wa  Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo

  Na Shamimu Nyaki.

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba Wataalamu wa lugha ya Kichina hapa nchini kutafsiri Filamu za Kiswahili kwa lugha ya kichina ili zipate soko nchini China.
  Prof. Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina  inayoitwa “Mfalme Kima” iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo amesema kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa watanzania katika filamu za kichina ni kutumia lugha ya Kiswahili.
  “Njia rahisi ya kufikisha ujumbe  kwa watu wote ni kutumia lugha mtambuka katika tamthiliya  zetu hii itasaidia sana kukuza uhusiano wetu na Jamhuri ya Watu wa China”,Alisema Prof.Ole Gabriel.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy ameelza kuwa ushirikiano wa shirika hilo na Kampuni ya Star Times ambayo ndio waandaji wa Tamthiliya hiyo umeleta mafanikio makubwa ikiwemo  kuongezeka kwa watazamaji wanaopenda tamthiliya za kichina zenye tafsiri ya lugha ya Kiswahili zinazooneshwa katika luninga hiyo.
  “Ushirikiano wetu unazidi kuimarika na tunaamini utaleta mafanikio makubwa zaidi kwetu sote katika kutoa elimu na Burudani kupitia Tamthiliya na vipindi vingine  vinavyopatikana katika visimbuzi vya Star Times”,Alisema Bibi Suzan.

  Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya Kichina “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili imezinduliwa leo Jijini Dar es Salaam ambapo maudhui yake yanatoa elimu pamoja na Burudani.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakati wakiwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha polisi, Oysterbay, leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika eneo la mradi unaoendelea wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Oysterbay,leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba.
  Mtaalamu wa Majengo kutoka kampuni inayojenga Kituo cha Polisi Oysterbay, Mhandisi Fanuel Malekela, akitoa maelezo ya mchoro wa ujenzi wa kituo hicho kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wapili kushoto),wakati kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa mradi huo.Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(watatu kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Polisi, Albert Nyamhanga, akitoa maelezo ya mradi wa Ujenzi wa kituo cha Polisi,Oysterbay kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu(watatu kulia), wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(kulia), akiwaongoza kutoka ndani ya jengo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa kituo cha polisi,Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.Huku sehemu kubwa ya mradi huo ikiwa imekamilika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na mbunge wa Mtama Nape Mosses Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la kusitishwa kwake uteuzi wa cheo hicho baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape.

  Akizungumza na waandishi nje ya Hoteli ya Protea leo, Nape amesema wanatakiwa kukubaliana na hali halisi kwani uteuzi uliofanywa huwezi kuukosoa na anashikuru kwa kuweza kupata muda wa kufanya kazi na Rais Magufuli.

  “Wanachi mnatakiwa kukubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Rais wetu kwani tukumbuke kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Nape na maamuzi yaliyofanywa yana tija kubwa sana kwa tasnia ya habari, michezo na wasanii na hampaswi kuanzisha matatizo, Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania,"

  Nape amesema kuwa anawashauri watanzania wote kuwa watulivu na zaidi amefurahi kufanya kazi kama Waziri wa habari na amewaomba wana tasnia ya habari ya habari kushirikiana na Waziri Mteule Harrison Mwakyembe kwani ni mwanahabari na pia ni mwanasheria mzuri.

  “Nina amini nilitumia akili zangu zote na kwa akili nawashukuru wasanii, waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu. Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana ila ninawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe na kuendelea kumwamini Rais wetu John Pombe Magufuli kwani ndiye tuliyepewa na mungu, ndiye rais tuliyemchagua,” amesema Nape.
  Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo
   
   Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akifafanua jambo kwa msisito alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(CPC) Bw. Guo Jinlong alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na mgeni wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(CPC) Bw. Guo Jinlong alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na  mgeni wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(CPC) Bw. Guo Jinlong alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  mgeni wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(CPC) Bw.Guo Jinlong (wa tatu kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (Picha na Ikulu).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye Mkutano wa mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana, katika Ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.


  Judith Ferdinand, BMG

  Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi, nchini, imehimizwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchi jirani katika kutoa mafunzo kwa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ili kuendane na teknolojia ya kisasa.

  Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika mafunzo endelevu ya 27 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Rocky City Mall Jijini Mwanza.

  Profesa Mbarawa amesema,kwa kutumia wataalamu kutoka nje ya nchi, itasaidia na kuwawezesha wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi, kubadilishana uzoefu pamoja na kuendana na soko la ushindani.

  Pia amewaomba wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,wanapopata fursa katika miradi ya ujenzi watumie elimu walionayo, kwa ajili ya maslahi ya taifa sambamba na uadilifu.

  “mchina na mturiki hawawezi kujua historia ya Tanzania lakini ninyi mnaijua nchi yenu, hivyo zitumieni fursa zinapojitokeza katika kubuni michoro ambayo itadumu zaidi ya miaka mia, kulingana na historia ya nchi,katika miradi ya ujenzi,” amesema Profesa Mbarawa.

  Hata hivyo ameiomba, bodi hiyo kuhakikisha inasimamia na kufuata sheria namba 4 ya mwaka 2010 katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi hasa kwa wakaguzi wa majengo.
  Kaimu Msajili wa Bodi, Albert Munuo, akizungumza kwenye mkutano huo.

  Kaimu Msajili wa Bodi hiyo, Albert Munuo, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha wataalamu na wadau wa sekta ya ujenzi kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kukabiliana na changamoto za utandawazi, ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi, ambapo mpaka sasa yamewanufaisha wataalamu 5,556.
  Mwenyekiti wa Bodi Dkt.Ambwene Mwakyusa, akizungumza kwenye mkutano huo.

  Mwenyekiti wa Bodi, Mbunifu Majengo, Dkt.Ambwene Mwakyusa, amesema, sekta hiyo inathamini jamii inayoitumikia hivyo wametoa vifaa vya maabara za sayansi, vyenye thamani ya milioni 3, ili kuhamasisha vijana wanaosoma masomo ya sayansi, kuja kusomea ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.
  Mwenyekiti wa Bodi Dr Ambwene Mwakyusa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) vifaa vya maabara.

  Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema vifaa hivyo atavipeleka katika shule moja ya wasichana ya sayansi, sambamba ameishukuru bodi hiyo kupitia wataalamu wa ujenzi kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitakua chachu kwa wanafunzi kusoma masuala ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.
  Wajumbe waliohudhuria mkutano huo.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
  . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote. 
  Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam. 
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma)  yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda  nje ya nchi ambapo ameagiza  Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa. 
  Moja ya kontena likiwa lina gari ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake anakuwa ameficha magari ya kifahari.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU
   
   


   

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetoa kadi za bima kwa wachezaji wote 23 wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti boys' kwa ajili ya masuala ya matibabu.

  Kaimu Mkurugenzi na Masoko Mfuko huo Angela Mziray alisema wamekuwa washirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuwa sehemu ya udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

  Angela alisema kwa sababu ugonjwa unakuja bila taarifa na wachezaji wapo kwenye hatari ya kuumia na kuugua pia kwahiyo imekuwa vizuri kwa TFF kuliona hilo nakuwapatia kadi za bima ya afya.

  "Namshukuru Rais Jamal Malinzi kwa kusimamia suala hili mpaka leo tumefikia hatua hii na ninaahidi kwa niada ya NHIF tutaendelea kushirikiana na TFF katika masuala mbalimbali," alisema Mziray.

  Kwa upande wake Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema bima hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa wachezaji hao kwakua wataweza kutibiwa mahali popote nchini hata wasipokuwa kambini.

  NHIF imefika asilimia 90 nchi nzima wakiwa na zaidi ya vituo 6000 kwa ajili ya kutoa huduma ya afya.

  Serengeti ambayo inaendelea na kambi jijini Dar es Salaam inataondoka wiki ijayo kuelekea mkoani Kagera kwa kambi ya wiki moja kabla ya kuelekea nchini Morocco kwa kambi ya mwezi mzima.
  Kaimu Mkurugenzi na Masoko Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray akizungumza na vijana wa Serengeti Boys pamoja na waandishi wakati wa makabidhiano ya kadi za Afya za Bima kwa ajili ya matibabu leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya soka la Vijana Ayubu Nyenzi na Meneja wa Uanachama wa NHIF Eletruda Mbogoro.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akizungumza na vijana wa Serengeti Boys pamoja na waandishi wakati wa makabidhiano ya kadi za Afya za Bima kwa ajili ya matibabu leo Jijini Dar es salaam. 
  Kaimu Mkurugenzi na Masoko Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray akikabidhi kadi za Bima kwa ajili ya matibabu kwa vijna wa Serengeti Boys leo Jijini Dar es salaam.
  Vijana wa Serengeti Boys wakiwa katika chumba cha Mazoezi (Gym) ambapo Mwenyekiti wa Michezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Msifu Chenjela kuwa wana ruksa ya kuutumia pale watakapohitaji .
  Viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na vijana wa Serengeti Boys mara baada ya kukabidhiwa kadi za Bima ya Afya leo Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili NIDA kutembelea na kukagua maendelea ya mradi wa Vitambulisho vya Taifa.
  Nje, Ulinzi na Usalama Mh. Adad Rajab (Mb), akiongea jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya NIDA baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Andrew W. Massawe. Kulia ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Kanali Mstaafu Ramadhani Issa Abdallah(Mb).Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew W. Massawe, akisoma ripoti ya Utekelezaji Mradi wa Vitambulisho vya Taifa kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge. Kushoto ni Mh Sophia H. Mwakagenda(Mb) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi Mh. Balozi Simba Yahya.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakisikiliza jambo wakati walipotembelea kituo cha uchakataji taarifa cha NIDA (NIDA DATA CENTER). Katikati ni Mh. Adad Rajab(Mb) mwenyekiti wa kamati na kulia ni Mh. Sophia H. Mwakagenda(Mb) Mjumbe wa kamatiAfisa uzalishaji Vitambulisho vya Taifa Bw. Jeremiah Kivelege akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama hatua za uzalishaji Vitambulisho vya Taifa walipotembelea kituo kikuu cha Uhifadhi na uchakataji wa Taarifa (Data centre)Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew W. Massawe akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu ubora wa Kitambulisho.


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akimpokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba(Mb) mara baada ya kuwasili katika ofisi za NIDA makao makuu.
  wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Adad Rajab (Mb) wakiwasili katika makao makuu ya ofisi za NIDA.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba (MB) akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge Mh. Adad Rajab (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo katika ofisi za NIDA.
  ……………..  Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama leo imefanya ziara ya kukagua mradi wa Vitambulisho vya Taifa; ambapo mbali na kupokea taarifa ya utekelezaji pia walitembelea na kukagua kituo kikuu cha Kuhifadhi, kuchakata na kuzalisha Vitambulisho vya Taifa -Data Centre.

  Akizungumza wakati wa kukaribisha Kamati hiyo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa NIDA imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa pamoja na changamoto kubwa ya fedha iliyopo.

  Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo; Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Adad Rajab (Mb) amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na NIDA na kwamba Kamati imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na NIDA na kwamba Kamati yake itaendelea kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya fedha kwa NIDA ili kuwezesha kukamilisha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa, kwani manufaa ya kuwa na mradi huu kwa Taifa ni makubwa katika Nyanja zote.

  Wakitoa maoni yao wajumbe wa Kamati hiyo wameitaka Wizara kuiwezesha NIDA na kuharakisha matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki kwani tayari idadi kubwa ya wananchi wameshatambuliwa na taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo.

  “Kutokana na manufaa makubwa ya mradi huu kwa Taifa, Serikali ihakikishe inatumia kila mbinu kuhakikisha matumizi yaliyokusudiwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa”

  Akisoma taarifa yake kwa Kamati hiyo; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Andrew W. Massawe ameieleza Kamati hiyo mpaka sasa NIDA imekamilisha Usajili wa Watumishi wa Umma nchi nzima ambapo watumishi 500,605 wamesajiliwa, NIDA imeanza kuwasajili wageni wanaoishi kihalali nchini, kufungua ofisi katika Wilaya zote nchini pamoja na kuanza zoezi la kuwasajiliwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini akiitaja baadhi; Lindi, Iringa, Geita, Singida, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Manyara n.k.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akitoa taarifa fupi ya utendaji kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.ambayo imeitembelea hospitali hiyo leo. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangallah na Mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba.
  Baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia ripoti ya utendaji iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangallah (kushoto), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba na Mkurugemzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru wakisiliza maoni ya wajumbe wa kamati hiyo leo.
  Mjumbe wa Kamati hiyo, Dk Faustin Ndugulile akitoa maoni yake baada ya mkurugenzi wa hospitali hiyo kuwasilisha taarifa ya utendaji ya hospitali hiyo kwa wajumbe.
  Baadhi ya wakurugenzi, wakuu wa idara wa hospitali hiyo wakifuatilia taarifa ya utendaji ya MNH iliyotolewa leo kwa wajumbe wa kamati hiyo.
  Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua jengo ambalo litatumika kutoa tiba kwa wagonjwa wa figo.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga akiieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jinsi huduma ya telemedicine inavyofanya kazi baada ya kuunganishwa na hospitali nyingine za mikoa. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba, Mjumbe Joseph Mbilinyi (katikati), Mjumbe Mussa Hassan Zungu na Zitto Kabwe.


  ………………
  Na John Stephen, MNH

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutokana na ubunifu wa kufanya mageuzi makubwa ya kuboresha huduma za afya.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Lucia Mlowe wakati akichangia taarifa ya utendaji iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.

  “Napenda kuwapongeza viongozi na wafanyakazi wa MNH kutokana na ubunifu wenu mkubwa mnaofanya katika kuleta maendeleo ambayo yamelenga kutoa huduma bora. Kutokana na juhudi hizi Serikali inapaswa kutoa fedha ilizoziahidi kwa MNH.

  “Nchi nzima inaitegemea MNH, Serikali ione huruma kwa MNH iwapelekee fedha, isiwaache pekee yao,” amesema Mlowe.

  Mjumbe wa kamati hiyo msheshimiwa Faustin Mdugulile ameipongeza MNH kutokana na mageuzi makubwa ya kuboresha huduma za afya na ameahidi kuisema MNH bungeni ili serikali kushughulikia changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

  Naye Mwekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba ameitaka MNH kuwashirikisha wadau wa afya katika kutoa huduma za afya ili kupunguza gharama za uendeshaji.

  “Naishauri serikali iwaachie wadau wa afya kusimamia vifaa tiba zikiwamo mashine za CT-Scan, MRI na vikiwamo vifaa vingine ili kupunguza gharama za uendeshaji. Nchi nyingine za ulaya wanatumia njia hii kuendesha hospitali na lengo ni kupunguza gharama,” amesema Serukamba.

  Awali kabla ya wajumbe wa kamati hiyo kuzungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Museru amesema MHN imeanza ukarabati wa majengo ya kutolea huduma za upasuaji kwa kina mama.

  Amesema kutokana na ukarabati huo, vyumba vya upasuaji vimeongezeka kutoka vyumba viwili hadi wanne, kwenye jengo la upasuaji vyumba vimeongezeka kutoka saba hadi vinane na jengo la watoto vyumba viwili hadi hadi vinne.

  Profesa Museru amesema katika mwaka wa fedha 2016/17, hospitali inaendelea na mkakati wa kuongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka vitanda 17 hadi kufikia vitanda 77.

  Amesema kwamba katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2016, hospitali imetumia Sh. 59.650 bilioni na kwamba Sh. 24.512 bilioni zilitumika kwa matumizi ya kawaida wakati Sh.29.888 bilioni 29.888 zilitumika kulipa mishahara ya wafanyakazi.

  “Sh. 5.250 bilioni zilitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikilinganishwa na sh. 51.017 bilioni ambazo zilizotumika katika kipindi cha Julai mpaka Disemba 2015 ambapo sh. 19.222 bilioni zilitumika katika matumizi ya kawaida, sh. 30.703 bilioni zilitumika kulipa mishahara ya wafanyakazi na sh. 1.092 bilioni zilitumika katika shughuli za miradi ya maendeleo,” amesema Profesa Museru.

  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  0 0


  0 0


  Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akikabidhi Bendera kwa manahodha wa timu ya taifa ya riadha kwa upande wa wanaume,Fabian Joseph (kushoto) na Magdalena Shauri (kulia)Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru (mwenye miwani) ,Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na kushoto ni Meneja wa timu ya taifa ya riadha Meta Petro.
  Raisi wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akizungumza na wanariadha 28 wanaoelekea nchini Uganda kwa ajili ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru akitoa neno kwa wanariadha hao,Shirika la Hifadhi za Taifa ndilo limedhamini wanariadha hao ambao idadi yao katika ushiriki wa mbio hizo imevunja rekodi ya tangu mwaka 1991.
  Baadhi ya wanariadha watakao iwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika jumapili hii.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Whilleam Gidabuday akizungumza wakati wa hafala hiyo.
  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanariadha wa timu ya taifa iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha.

  Kikosi cha wanariadha 28 na viongozi 12 kitakachopeperusha Bendera ya Taifa nchini Uganda katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika yatakayofanyika Jumapili hii katika mji wa Entebe.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mabalozi walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuiwakilisha Tanzania katika nchi  mbalimbali duniani wameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa wamejizatiti kikamilifu kwenda kusaidia juhudi kubwa za Bodi hiyo katika kuitangaza Tanzania kama eneo bora la Utalii duniani katika nchi wanazokwenda kufanyakazi sambamba na kuhamasisha wafanyabiashara kutoka mataifa hayo kuwekeza nchini katika sekta ya utalii ikiwa ni utekelezaji wa jukumu lao kubwa la kukuza diplomasia ya uchumi.

  Wamepongeza juhudi zinazofanywa na TTB katika kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii lakini wakaomba iangalie namna gani inaweza kusaidia katika kuboresha huduma zitolewazo na wadau wa utalii kwa watalii wanaotembelea Tanzania kama vile mahotelini kwani bado hatufanyi vema katika suala la huduma bora na nzuri kwa watalii. 

  Aidha wameiomba TTB kushauri mamlaka na watoa huduma wengine katika sekta ya utalii kupunguza gharama wanazotoza kwani ni kubwa sana kiasi cha kuifanya Tanzania kulalamikiwa na wageni wengi kuwa ni eneo la utalii ghali sana ukilinganisha na nchi nyingine ambazo ni washindani wetu katika sekta ya Utalii.

  Hayo yamesemwa leo  na mabalozi hao wakiongozwa na Balozi Omari Yusuph Mzee walipotembelea makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania kwa lengo la kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi na kupanga mikakati ya namna balozi hizo zinavyoweza kushirikiana na TTB katika kuitangaza Tanzania na kuhamashisha wawekezaji kutoka nchi wanazokwenda kufanyakazi kuja nchini kuwekeza katika sekta ya utalii.

  Mapema  Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi aliwaelezea waheshimiwa mabalozi mikakati mbalimbali ambayo Bodi yake imekuwa ikitekeleza katika kuitangaza Tanzania nje ya nchi kwa lengo kuvutia watalii wengi zaidi na kukuza utalii kwa ujumla. Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweka matangazo katika maeneo na vyombo mbalimbali vya habari nje ya nchi, kualika na kuleta nchini watu maarufu ili kuja kutembelea vivutio vyetu vya utalii, kuteua mabalozi wa hiari wa utalii na kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii.

  Mkurugenzi Mwendeshaji Bibi Devota Mdachi aliwakabishi mabalozi hao vielelezo mbalimbali vya utalii wa Tanzania na kuahidi kuwa bodi yake itakuwa ikiwatumia vielelezo mbalimbali vya utalii vitakavyo wasaidia katika kutekeleza jukumu la kusaidia utangazaji utalii katika nchi walizopangiwa. Mabalozi hao watano na nchi wanazo kwenda ni Omari Yusuph Mzee (Algeria), Matilda Masuka (Korea Kusini), Dkt. Pindi Chana (Kenya), Grace Mgovano (Uganda), Fatma Rajab (Qatar) na Balozi Abdallah Kilima (Oman).  
   Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi devota Mdachi akizungumza na Mabalozi waliomtembelea ofisini kwake jana.Kushoto ni Balozi Omari Yusuph Mzee na kulia ni Balozi Abdallah Kilima.
   Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana akisisitiza jambao wakati wa mazungumzo baina yao na Mkurugenzi Mwendshaji wa TTB walipomtembelea ofisini kwake Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mwendshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Balozi Abdallah Kilima moja ya majarida ya TTB yanayozungumzia utalii wa Tanzania wakati timu ya mabalozi sita walioteuliwa hivi karibuni walipomtembela Mkurugenzi huyo ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
  Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika baadhi ya nchi duniani wakiwai katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa TTB Bi Devota Mdachi (wa nne kushoto) na baadhi ya Maafisa waandamizi wa TTB . Kutoka kushoto ni Bw. Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB, Mh. Balozi dkt Pindi Chana , Mh. Balozi Omari Yusuph Mzee, Mh. Balozi Fatma Rajab  (wa tano), Mh. Balozi Grace Mgovano (wa sita), Mh. Balozi Matilda Masuka (wa saba) na Bw. Philip Chitaunga Meneja Huduma kwa watalii wa TTB.

older | 1 | .... | 1179 | 1180 | (Page 1181) | 1182 | 1183 | .... | 1897 | newer