Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE IMEITAKA SERIKALI KUHAKIKISHA INATOA FEDHA ZA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA NAMBA TATU

0
0
KAMATI ya Kudumu ya Bunge imeitaka serikali kuhakikisha inatoa fedha za mradi wa ujenzi wa jengo la abiria namba tatu (terminal III) kwa wakati ili mradi huo uweze kukamilika kama ilivyopangwa. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla aliyasema hayo wakati wa kufanya majumuisho baada ya kutembelea mradi huo leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 

Alisema kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati uliopangwa utawapa heshima Watanzania lakini pia kupunguza msongamano katika jengo la sasa la Terminal II. 

“Nchi inapoenda kwa sasa ni kuzuri, lakini ili kukamilika ujenzi huu kwa wakati tunaomba serikali itoe fedha ili kufanikisha hilo, baada ya kukamilika kila ndege itatua hapa nchini na hivyo kuongeza pato la Taifa,” alisema Profesa Sigalla. 

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Salim Msangi alisema, miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mradi huo ni serikali kutotoa fedha kwa wakati pamoja na sheria ya Mamlaka ya Mapato (TRA) ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ilipitishwa mwaka 2015. 

Alisema kabla ya sheria hiyo wakati inapitishwa vifaa vya ujenzi wa uwanja huo vilikuwa na msamaha wa kodi lakini baada ya kupitishwa msamahaka huo uliondolewa hali iliyosababisha baadhi ya vifaa kukwama bandarini na wakati mwingine kukaa muda mrefu. 

Aliongeza kuwa mradi huo ulikuwa unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka jana lakini ulichelewa kutokana na kuchelewa kuwasilishwa kwa fedha zaidi ya Sh bilioni 290 kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya mradi huo. 

“Tunaiomba serikali iwezeshe kupatikana kwa fedha za mradi kwa wakati pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza ili kutochelewesha mradi na kuepuka gharama zinazoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kukamilika kwake,” alisema. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuliho alitoa ufafanuzi kuhusu notisi iliyotolewa na Mhandisi Mshauri ya kusitisha huduma kuanzia jana hadi atakapoliwa deni lake. 

Alisema tayari serikali inafanyia kazi deni hilo na kwamba ipo katika hatua nzuri ya kuhakiki vocha za malipo kabla ya kufanya malipo ya mhandisi huyo. 
01.Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla akizungumza na wana kamati wakati wa ziara ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
02.Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akizungumza wana kamati wakati wa ziara ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
03.Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Shanif Mansoor akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam.
Wana kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla
.Wana kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge wakitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
Ujenzi ukiendelea wa jengo la abiria namba tatu (Terminal. )Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MRADI WA UJENZI -OFISI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wakwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

RC MAKONDA AZINDUA VISIMA VITATU VYA MAJI MBAGALA MAJI MATITU

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amezindua visima vitatu vya Maji vilivyopo Mbagala Maji matitu shuleni, amesema kuwa uzinduzi wa miradi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 22 ya mwezi wa tatu.

Amesema kuwa rasilimali hiyo ni adhimu na ni miongoni mwa rasilimali zinazoathirika sana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

"Naomba nitoe rai kwa kila mmoja wetu kwa nafasi na majukumu aliyonayo katika sekta ya maji, kuanzia watendaji wa Mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma mpaka mtumiaji mmoja mmoja ahakikishe analinda na kutunza vyanzo vya maji,"amesema Makonda.

Aidha, kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Maji na Majitaka; punguza uchafu yatumike kwa uangalifu" Makonda amewaomba wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinafamu kwenye vyanzo vya Maji kama kando kando kwa mto Kizinga uliopo Temeke.

Hata hivyo, Makonda ameipongeza Serikali kupitia DAWASA na wadau wa maendeleo wanaosaidia ujenzi wa miradi hiyo, kwani mbali na kuboresha mazingira ya kiafya, itapunguza matumizi ya maji safi kwa shughuli zisizo za lazima.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na na baadhi ya akina Mama wa Mbagala Maji matitu mara baada ya kuzindua visima hivyo,katika maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimtwisha mama ndoo ya maji marabadaa ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasili katika uzinduzi wa visima vya maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam

DC DODOMA AWATAHADHARISHA WATAKAODANGANYA KATIKA ULIPAJI FIDIA ENEO LA UJENZI WA UWANJA WA MICHEZO NALA.

0
0

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MASUALA YA UTAMADUNI

0
0

Na Dotto Mwaibale


SERIKALI ya Tanzania na China zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020.

Nchi hizo zimetiliana saini za mkataba huo kupitia kwa Mawaziri wa wizara husika katika masuala ya utamaduni ambapo kwa China Naibu Waziri wa Utamaduni, Gong Wei alihusika katika tukio hilo.

Kwa Upande wa Tanzania Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alishiriki kutia saini.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, Gong Wei alisema kwa muda mrefu nchi ya China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika mambo mengi ikiwepo sanaa na utamaduni hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee kudumu.

Alisema katika kudumisha ushirikiano huo Serikali ya China itatoa kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa ajili ya kununua samani kwa Wizara hiyo ambazo zitatumika katika maofisi ambapo alimuomba Waziri Nape kueleza ni samani gani zitakazo hitajika ili ziletwe.

Waziri Nape aliishukuru China kwa msaada huo na kusema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali.

Katika hafla hiyo mawaziri hao waliweza kupeana zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakiangalia zawadi.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakisaini mkataba huo.
 

UONGOZI WA AZAM WALAANI VIKALI VURUGU WALIZOFANYIWA, YAKUBALI MATOKEO YA KUFUNGWA

0
0
 Ofisa habari wa Azama Jaffar Iddy 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Klabu ya soka ya Azam fc, iliyokuwa  imelaani vikali  vitendo vya vurugu zilifanywa na timu ya Mbabane swallows katika mchezo ulifanyika nchini Swazland mchezo ambao walikubali kipigo cha goli 3-0, na kusema wao wanaliachilia mbali suala hilo wakijua CAF ndio wenye maamuzi ya mwisho.

 Azam ilikuwa ikishiriki kwenye ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF iliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kushindwa kulinda ushindi wao wa nyumbani wa goli 1-0  na kutolewa kwa jumla ya goli 3-1 mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumzia tuhuma zilizokuwa juu yao kuwa waliwafanyia fujo Mbabane kwenye mechi ya awali iliyochezwa  jijini Dar es saalm, katika uwanja wa Chamazi complex, Ofisa habari wa Azama Jaffar Iddy amesema kuwa hizo taarifa hazina ukweli.

Iddy amesema sababu ambazo zimesambaa kuwa waliwafanyia fujo Mbabane  sio za kweli bali waliamua tu kutengeneza sababu kwao kuhakikisha wanatimiza azma yao,ambayo  anaamini ndiyo iliyopelekea klabu hiyo kupata matokeo hasi.

Amesema kwa matokeo waliyoyapata ya kufungwa mabao 3-0, kimpira wameyakubali lakini walicheza katika mazingra magumu sana kwa kuwa waliwachezesha wachezaji ambao walikuwa na majeraha kama Salum abubakari( sure boy) ,akisumbuliwa na dole gumba, Himid mao bega na Frank Domayo akisumbuliwa na Malaria..

Amesema katika mchezo wa mpira, yote huwa yanatokea katika uhalisia wa matokeo ya mpira ambayo yapo matatu, kufungwa, kushindwa na kutoka sare, hivyo basi wamekubali wamashindwa lakini wao kama Azam fc, jukumu la nini? Kifanyike! baada ya wao kufanyiwa vurugu zile ni jukumu la mechi kamishna maana ndiye alikuwa msimazi wa mchezo hule.

Pia amesema ingawa wameingia kambini na wachezaji wachache waliopo huku nane(8) wakiitwa kikosi cha timu ya Taifa, (Taifa stars), tayari kwa mchezo wao  na Yanga, unaotarajia kufanyika April mosi mwaka huu, na FA CUP, wanasumbuliwa na baadhi ya wachezaji ambao anaamini wanaweza kukosa michezo kaza inayowakabili, kama Kingu na John bocco, ambaye walimuacha Afrika kusini kwa matibabu Zaidi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAURITIUS

0
0
 Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watanzania wanaosoma na wale wanaoishi nchini  Mauritius kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji wa Port Louis, .
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watanzania wanaosoma na wale wanaoishi nchini  Mauritius kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi  22, 2017.  Kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed na kushoto ni Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Mauritius, Merday Venkatasamy.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma jambo katika kipeperushi wakati akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.

MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA

0
0
Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika Jijini Mwanza.

Judith Ferdinand, BMG
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.

Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo  pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.

Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.

Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442  lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza  kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.

Kwa upande wake  Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye  mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.

Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina  wataalamu wake.

"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.

Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo  cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.

Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
Displaying Pix.JPG

WATANZANIA WAISHIO NJE WAASWA KUTOJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wanaoishi nje ya nchi wazingatie sheria za Taifa husika na kamwe wasijihusishe na biashara haramu ya dawa za kulevya.

“Vita ya dawa za kulevya ni kubwa, hata hivyo Serikali tunaendelea kupambana nayo. Nchi ilikuwa inapoteza vijana ambao walikuwa wamejiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya. Nawaomba msithubutu kuingia huko mtafungwa,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Machi 22, 2017) wakati akizungumza na Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Mauritius katika mkutano alioutisha kwenye hoteli ya Meridien mjini Port Louis.

Amesema katika kudhibiti biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya Serikali iliamua kuunda Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na inafanya kazi vizuri. “Na tutakamata kila mtu anayejihusisha na biashara hiyo bila kujali cheo, uwezo na mamlaka aliyonayo,”.

Amesema mamlaka hiyo inafanyakazi ya kutafuta wazalishaji, watumiaji na wafanyabiashara, lengo likiwa ni kuokoa vijana ambao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na madhara waliyoyapata baada ya kutumia dawa za kulevya.

Katika hatua nyinngine, Waziri Mkuu amewataka Watanzania hao walioko nchini Mauritius kujenga mshikamano wa pamoja na wawe na uzalendo na nchi yao. Pia wawe mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya Taifa.

 Amesema ni vema wakatumia fursa walizonazo katika kutafuta wawekezaji na kuwashawishi waje nchini na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, uvuvi, nishati na utalii.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amewaomba Watanzania hao wazidishe mshikamano miongoni mwao kwa kuwa umoja wao ndiyo nguzo yao.

“Mko hapa kwa ajili ya kutafuta elimu na wengine mnafanya kazi, shughuli ambazo  zitawasaidia kuboresha maendeleo yenu na Taifa kwa ujumla, hivyo nawaomba mzingatie kilichowaleta,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Mauritius, Bw. Donald Kongwa ambaye ni Ofisa wa benki ya Standard Chaetered nchini Mauritius amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kipato wanachokipata watakitumia kwa kuwekeza Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, amesema wanaunga mkono na kupongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika  kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, ujenzi wa miundombinu ya kisasa, ununuzi wa ndege pamoja na kuimarisha uwajibikaji na nidhamu kwa watumishi wa umma.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, MACHI 22, 2017.

WAZIRI MKUU AHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA NCHINI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika samaki aina ya jodari na kuwakaribisha viongozi wa kiwanda hicho kuja nchini kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya samaki.

Amesema Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji na pia ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya samaki, ambayo ni bahari, mito na maziwa ambayo aina mbalimbali za samaki.

Waziri Mkuu amesema hayo jana jioni (Jumanne, Machi 21,2017) wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha Mer des Mascareignes kilichoko  jijini Port Louis nchini Mauritius.

“Tanzania kuna fursa nyingi za uwekezaji hasa kutokana na mazingira yake. Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda ili kuongeza tija kwa Taifa na kwa wananchi kiujumla hivyo wanahitaji wawekezaji waliotayari kuja kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed alisema Tanzania inahitaji wawekezaji watakaowekeza kwenye uvuvi wa kina kirefu na ujenzi wa viwanda vya samaki.

Dkt. Khalid alisema lengo la uwekezaji huo ni kukuza uchumi wa Taifa pamoja kupanua soko la ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake.

Naye Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Patrick Hill alisema wamefurahi na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa na uwekezaji na kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali.

Alisema kampuni yao inajishughulisha na usindikaji wa samaki aina moja tu ya jodari na wananunua kutoka kwa makampuni makubwa ya uvuvi huku wateja wao wakubwa wakiwa ni bara la Ulaya.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda kingine cha  Chantier Naval Del`Ocean Indien Limited (CNOI) ambacho kinatengeneza na kukarabati meli , boti na pantoni na kujionea uwezo mkubwa walionao, ambapo Watanzania wanaweza kuja kujifunza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, MACHI 22, 2017.

MKUU WA MKOA WA TANGA, MARTIN SHIGELLA AWAPIGA MSASA MAKATIBU TAWALA

0
0

Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi kwa kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
 
Amesema Utafiti huo utaangazia pia kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.
 
Amesema Tafiti tatu zilizotangulia zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti na utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa  kipekee ambapo kwa mara ya kwanza wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa watahusihwa.
 
Kwa upande wake, Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga, Tonny Mwanjoto, aliwataka Makatibu Tawala kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi shuleni kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
 
Alisema kufanya hivyo itasaidia  juhudi za Serikali kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ikiwa na pamoja na kuyatokomeza moja kwa moja.



Wajumbe wa mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi 2016 /2017 wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Makatibu Tawala kutoka Wilaya za Tanga na Wawakilishi wa TACAIDS pamoja na Wadau wa Maendeleo uliofanyika leo  ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.



Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga, Tonny Mwanjoto akizungumza na waandishi wa habari wa Tanga mara baada ya kuisha kwa mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashria na Matokeo ya Ukimwi 2016/ 2017.
blog ya kijamii ya tangakumekuchablog, 0655 902929

Tanzania "BIG ISHU AWARDS"

0
0
Kwa mara ya kwanza Candy and candy group of companies wanakuletea Tuzo ya heshima Tanzania "BIG ISHU AWARDS" 

Tuzo hiyo itatolewa kwenye taasisi mbalimbali,kutokana na ubunifu na namna walivyofanikiwa kubadilisha maisha ya wengi nchini Tanzania.

Tuzo hizo zitalenga makampuni na mashirika mbalimbali kutokana na namna ambavyo zinatoa fursa za kimaendeleo kwa watanzania.

Tuzo hizi pia zinatoa fursa ya kukutanisha wamiliki wa makampuni na mashirika mbalimbali kuweza kusheherekea na kubadilishana mawazo siku hiyo.
Orodha na vipengele vitakavyoshindaniwa katika tuzo hizo ni:-
-CORPORATE COMPANIES
-AGENCIES
-NGO'S
-SOCIAL NETWORKS
-GOVERNMENT MINISTRIES
-MEDIA
-EDUCATION INSTITUTION
-SPORTS
TOURISM AND HOSPITALITY
-ENTERTAINMENT
Big ishu watazindua kampeni ya media kutangaza washiriki wote na miradi yao waliyoanzisha ya kuwasaidia wananchi kubadilisha maisha yao.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi:-
                              
                        Simu namba:- +255652052263
                              
                        Barua Pepe:- joe@afwab.com

camera za usalama zaanza kuwekwa bara barani Zanzibar

0
0
Mafundi wakiweka Security Camera katika sehemu mbali mbali za Mji wa Unguja,Camera hizo zitaweza kufanikisha kuonekana kwa matukio mbali mbali ya Barabarani ikiwemo ajali pamoja na matukio us Uhalifu.

Mahojiano na Dj D-Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A

0
0

Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.
Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.
Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2
Karibu usikilize

MASAUNI AVIAGIZA VYOMBO VYAKE KUONGEZA KASI ZAIDIKUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU, WAUZA DAWA ZA KULEVYA MKOANI LINDI, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini Kilwa mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu zaidi katika ukamataji wa wahamiajiharamu pamoja na wauza dawa za kulevya. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi, Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache kutokana na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga nyumba mpya katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni eneola Mitwero mkoani humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo hilo makazi mapya yatakapojengwa. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Masauni aliongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia ramani ya ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia) akimkaribishaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ofisini kwake kwa ajili ya kupewa taarifa ya mkoa huo, wakati Naibu Waziri Masauni alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC akabidhiwa gari

0
0
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Beni ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akikabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 kwa Aldo Nsuha  mshindi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya benki hiyo iliyodumu kawa muda wa miezi mitatu. Kulia ni mke wa mshindi huyo, Zenobia Tarimo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wateja wawili wa benki hiyo walishinda zawadi ya gari kila mmoja.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Beni ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akikabidhi nyaraka za bima za gari aina ya Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 kwa Aldo Nsuha  mshindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyodumu kawa muda wa miezi mitatu. Kulia ni mke wa mshindi huyo, Zenobia Tarimo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Beni ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akikabidhi vibao vya namba za gari aina ya Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 kwa Aldo Nsuha  mshindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyodumu kawa muda wa miezi mitatu. Kulia ni mke wa mshindi huyo, Zenobia Tarimo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya Benki ya NBC, Aldo Nsuha mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam akijaribu kuwasha gari lake aina ya Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam leo. Anayemuangalia ni mke wake, Zenobia Tarimo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 23, 2017

0
0

BREAKING NEWZZ:Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri

0
0

Qatar Yaadhimisha Miaka Kumi (10) Huduma ya Usafiri wa Anga.

0
0

Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania,Basel Haydar, akizungumza alipokutana na waandishi wa habari katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam.
Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania Basel Haydar, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini, katika sherehe za Kutimiza miaka kumi (10) ya kutoa huduma nchini Tanzania.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa tasnia ya usafiri wa anga nchini Tanzania wakimsikiliza kwa makini meneja mahusiano ya umma (PR Manager) wa Qatar Airways Bi.Gayathri Pradeep alipokua akielezea jinsi Qatar Airways wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wateja wao.
 Wageni mbalimbali wakibadilishana mawazo walipokutana kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya miaka kumi (10) ya kutoa huduma ya usafiri wa anga wa shirika la Qatar Airways zilizofanyika Serena hoteli Dar es salaam
Wageni (waandishi wa habari) na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga wa Qatar Airways Tanzania katika picha ya pamoja katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam. 


SHIRIKA la ndege la Qatar (Qatar Airways) limeadhimisha miaka kumi ya kutoa huduma ya usafiri wa anga kati ya miji ya Dar es Salaam na Doha huko Mashariki ya Kati jijini jana.

Sherehe hizo zilizofanyika zilihudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini.

Shirika hilo lilianza kutoa huduma ya usafiri huo wa anga kati ya Dar es Salaam na Doha mwaka 2007 likitumia ndege aina ya Airbus 320.

Huduma hii ilipanuka zaidi miaka mitano badaye kwa shirika hilo kuanza kurusha ndege zake moja kwa moja kutoka kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro na badaye Zanzibar mwaka 2015 ili kukidhi mahitaji ya soko lililokuwa likikua kwa kasi.

Leo hii Qatar inatoa huduma za ndege zake zinazoruka kila siku moja kwa moja kutoka Dar es Salaam, Kilimanjaro and Zanzibar kupitia Doha na kupanuka kwenye miji zaidi ya 150 huko Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Pacific na miji muhimu kama vile London, Paris, Dubai, Shanghai na Beijing.

Mtendaji Mkuu wa shirika hili Ehab Amin, alisema: Qatar Airways ina furaha kuadhimisha miaka kumi ya huduma zake hapa nchini ambazo zinalipa shirika uwezo wa kutimiza haja ya kusafirisha watalii na wafanyabiashara katika eneo hili la Afrika ambalo lina vivutio vizuri na biashara kedekede.

“Qatar Airways inajivunia ufanisi mkubwa wa huduma zake nchini Tanzania, na tunachukua nafasi hii kuwapongeza wateja wetu wanaotufanya tujivunie mafanikio haya.

Tuna heshima kubwa ya kuendelea kutoa huduma Tanzania, kujenga uhusiano na wafanya biashara kwa mtazamo wa muda mrefu na kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu kwa miaka dahali ijayo,” alisama.

Shrika limekuwa kiungo kikubwa cha watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa takriban miaka kumi yote wakitembelea vivutio vya utalii kama vile Serengeti, Selous, Ngorongoro, Zanzibar na kwingineko nchini Tanzania.

Wakati huo huo, shirika limekuwa mstari wa mbele kusaidia kukua kwa biashara katika eneo zima la Afrika Mashariki likihudumia wafanyabiashara kujitanua katika zaidi ya miji 150 duniani kote.

Ndege husafirisha abiria kila siku kutoka Uwanja wa Julius Neyrere Dar es Salaam kwenda Doha moja kwa moja kwa masaa sita. Safari huanza saa 11 na nusu jioni na kuwasili Doha saa tano na dakika 25 usiku katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamad siku hiyo hiyo. Ndege ya kurudi kutka Doha huanza saa tatu asubuhi na kuwasili Dar es Salaam saa tisa mchana.

Safari nne kati ya saba za wiki kutoka Kilimanjaro kwenda Doha hupitia Zanzibar na zilizobaki tatu kutoka Zanzibar kwenda Doha hupitia Kilimanjaro. Abiria wa Qatar Airways hujivunia huduma, takrima na ukarimu kutoka kwa wafanyakazi wake wenye bashasha na mvuto wa upendo wakitoa vyakula vitamu vilivyopikwa kwa ustadi na wapishi maridhawa na mahiri.

Abiria pia wanajivunia huduma bora ya usafiri kutoa uwanjani baada ya kushuka kwenye ndegekatika uwanja wa Hamad wenye hoteli, bwawa la kuogelea, gym, uwanja wa squash na spa.

Shirika hili linaloendelea kukua kwa kasi na huduma bora duniani linapanua huduma zake kwa kusafirisha abiria wake kwenye mjji mipya kama vile Adelaide, Auckland, Atlanta, Birmingham, Boston, Helsinki, Los Angeles na Sydney.

NINAYO YASHIRIKIANA NA HEIFER INTERNATIONAL KUWANUFAISHA WAKULIMA

0
0
 
Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisilo na kiserikali la Heifer utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao wa www.NINAYO.com .Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya.
Meneja uendeshaji wa kampuni ya NINAYO Bovan Mwakyambiki akiungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisolo na kiserikali la Heifer International Tanzania utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.


Kampuni ya Ninayo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Heifer International Tanzania ambalo limejikita katika kuondoa umasikini na matatizo ya njaa leo wameshirikiana katika kuwasaidia wakulima wa Tanzania kupata taarifa zote zinazohusu mauzo au manunuzi ya mazao mbalimbali kupitia mtandao wa Ninayo.com.

Ninayo ni jukwaa la mtandao wa kibiashara unaowawezesha wakulima kuuza, kununua au kuangalia bei elekezi za mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo pia kuwapa uwanja mpana wa kulifikia soko la bidhaa hizo kwa urahisi.

Njia hii ya mtandao imejikita katika kutatua mambo makubwa matatu ikiwemo tatizo la kushindwa kwa mkulima katika usambazaji ambapo wanunuaji/wateja hawafahamu ni mazao ya aina gani wakulima wanauza, Mahitaji yasiyofahamika ambapo wakulima hawafahamu ni kiasi gani wanunuaji wapo tayari kununua mazao yao na kukosekana kwa utaratibu wa kuwaunganisha wanapohitaji kufanya biashara za mazao yao.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ninayo Jack Langworthy alisema matumizi ya intaneti yanazidi kukua kwa kasi sana nchini Tananzia, na hivi sasa intaneti imesambaa hadi vijiji maskini.

“Tunashukuru kwa kukua kwa kasi ya mitandao hasa kupitia simu za mkononi, ni uvumbuzi ambao umeleta mapinduzi katika kila sekta duniani, kuanzia kwenye bishara ya teksi, hoteli na zaidi sasa inaweza kupatikana kwa wakulima katika masoko ya Tanzania kukabiliana na mahitaji mahitaji mbalimbali ya chakula kwa bei elekezi kwa watu wote na hivyo kupunguza upotevu wa mazao mbalimbali”.

Ninayo itasaidia kuwaunganisha wakulima kwa pamoja katika soko rasmi, na itaweka bei elekezi kwenye biashara ya mahindi, maharage, ndizi, maembe, matikiti maji pamoja na bidhaa nyingine nyingi za kilimo katika kuleta uwazi na ukweli wa bei ya soko na hivyo kuwawezesha wakulima kujivunia mazao yao.

Aliongeza kuwa Ninayo mpaka sasa imefanikiwa kuwaunganisha wakulima wa mikoa kama Iringa, Mbeya, Morogoro na Njombe pamoja na wanunuaji wa bidhaa zao, jambo lilisaidia kuongeza kipato chao.

Aliendelea kusema kuwa Ninayo inaunganisha hadi wakulima wasio na uwezo wa kupata intaneti kwa kupitia njia ya ujumbe mfupi wa maneno.kwa upande wake Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya alipongeza juhudi zinazofanywa kupitia mtandao huo akisema itasaidia kuwaunganisha wakulima na wateja wao nchini na Afrika mashariki yote.

Ushirikiano kati ya Ninayo na Heifer International ni katika kuelimisha wakulima jinsi ambavyo wanaweza kunufaika kwa kuuza mazao yao kwa kupitia mtandao huo. Heifer ambao wanafanya kazi na mamia ya wakulima nchini itawasaidia wakulima wake kutumia mtandao wa Ninayo ili waweze kujipatia faida kwa kuhakikisha wanauza bidhaa zao kwa bei za kujiridhisha.

“Kama shirika linalohusika na kutokomeza njaa na umaskini, huwa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kulingana na bei zilizo za kibiashara na kwa manufaa kwao pia kupata wanunuzi sahihi na hivyo kupitia mtandao huu utasaidia kusulisha changamoto hiii” alisema.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images