Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

INOCENT MELECK AJITOKEZA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo, Inocent Meleck amechukua fomu ya kugombea Ubunge Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi .

Meleck amechukua fomu hiyo akiongeza Idadi ya Vijana wengi ambao wamejitokeza kuchukua fomu hiyo katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam .

Meleck amesema kuwa yeye amechukua fomu hili aweze kupata nafasi ya kuwa mbunge wa Afrika Mashariki kama wanavyofanya vijana wengine wa CCM hili waweze kuwakilisha nchi.

Aidha alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti Wa CCM kwa kuweka mfumo ambao umemuwezesha kila mtu kupata fursa ya kugombea hasa kwa vijana .

Aidha alitoa Rai kwa wana CCM ambao wana lengo na nia nzuri ya kupata nafasi ya kujitokeza kuchukua fomu kwa kufika Lumumba au Zanzibar kuchukua fomu kwani nafasi hiyo inatoa fursa hiyo kwa vijana.

Inocent Meleck akisalimia na mpiga picha Mwandamizi wa CCM , Bashir Nkoromo

TANAPA YAWAPA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI NA UPIGAJI PICHA WAHIFADHI UJIRANI MWEMA NCHINI

$
0
0
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha kuwa linaboresha mawasiliano yake baina ya wananchi wanaoishi maeneo jirani na hifadhi wameamua kuwapa mafunzo maalum ya wiki moja yanayolenga kuwajengea uwezo Wahifadhi Ujirani Mwema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku hususan utoaji wa Elimu ya Uhifadhi kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi nchini.Miongoni mwa mammbo ambayo wameweza kujifunza ni utoaji taarifa kwa njia ya habari. Ilikufanikisha hilo TANAPA imewapa mafunzo ya kitaalam maofisa wake hao katika mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma. Pichani juu ni Mhariri wa Habari Mwandamizi wa Machapisho ya Mwisho wa wiki ya Gazeti la Habarileo, kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Oscar Mbuza akitoa mafunzo ya uandishi bora wa habari za kijamii kwa maofisa hao.
 Maofisa Uhifadhi Ujirani mwema kutoka hifadhi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo ya uandishi wa habari.
 Maranyingi habari huendana na picha, ili somo hilo la Habari liwezuri na liende sawa maofisa hao pia walipewa mafunzo ya namna ya upigaji picha bora za Habari na namna ya kutumia Kamera. Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Mroki Mroki alitoa mafunzo hayo kikamilifu.
 Muda wa majadiliano ulikuwepo baada ya kutoa mada, ambapo pia maswali yaliulizwa na kujibiwa.
 Washiriki wakifuatilia kwa umakini somo la upigaji picha.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi nae alishiriki mafunzo hayo kama mwenyekiti wa mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo. Source: TSN Digital

RAIS WA BENKI YA DUNIA AONDOKA NCHINI BAADA YA ZIARA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, ameondoka nchini baada ya ziara ya kikazi ya siku tatu na kuagwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake ya Siku tatu Dkt. Jim Yong Kim, pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli, alishiriki tukio la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya juu (Ubungo Interchange) katika makutano ya barabara Ubungo itakayogharimu Sh.188.7 Bilioni kati ya hizo Benki ya Dunia itatoa Sh186.8 kwa ajili ya ujenzi na usanifu na Sh1.9 Bilioni zitatolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa fidia.

Aidha umma umeshuhudia utiwaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo itakayo fadhiliwa na Benki ya Dunia hapa nchini, yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.74.

Miradi hiyo ni ile ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa mabasi yaendayo haraka-DART, Mradi wa kusambaza maji safi, mazingira na ukusanyaji wa maji taka, na mradi wa uendelezaji wa miji ya Arusha, Dodoma, Tanga, Kigoma, Mwanza, Mbeya, na Mtwara.

Pia katika ziara hiyo, Dkt. Kim alipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Manispaa ya Ilala, ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi. 
Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim (wa pili) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakitoka katika eneo la kupumnzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Waziri Mpango amemuaga Rais huyo baada ya kuwepo nchini kwa takribani siku tatu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (wa pili kushoto) baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi hapa nchini, ambapo alishiriki uwekaji wa jiwe la Msingi katika ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (aliyevaa tai) akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa kumuaga Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim aliyekuwepo nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kumuaga Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, muda mfupi kabla ndege iliyombeba Rais huyo kuondoka.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na afisa mwingine wa Serikali wakishuhudia wakati Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bi. Bella Bird wakibadilishana mawazo baada ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuondoka nchini. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Mohammed Dewji ashinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bora Afrika 2017

$
0
0
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa mwaka 2017 inayotolewa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Afrika (Africa CEO Forum). Dewji ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda Abdulsamad Rabiu (CEO wa BUA Group), Issad Rebrab (CEO wa Cevital), Naguib Sawiris ( CEO wa OTMT Investments), Said Salim Awadh Bakhresa (CEO wa Bakhresa Group) na Strive Masiyiwa (CEO wa Econet). Akizungumza kuhusu ushindi huo, Dewji ameishukuru Africa CEO Forum kwa kutambua mchango wake kwa kumchagua kuwa mshindi tuzo hiyo lakini pia kuwashukuru Watanzania na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya kudhibiti na kubana matumizi mabaya ya pesa ya umma. 

“Ninashukuru sana Africa CEO Forum kwa heshima hii ambayo mmenipa, napenda kutoa tuzo hii kwa nchi yangu Tanzania, bila wao nisingekuwa hapa na MeTL Group isingekuwa katika nafasi iliyonayo sasa, nawashukuru sana kwa kuniruhusu mimi na familia nzima ya MeTL kukua na kufika hapa,“Pia napenda kutoa heshima kwa Rais wangu John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri na wote tunajua Afrika inavyokabiliwa na vitendo vya rushwa lakini yeye ni mmoja wa watu ambao wanapambana na rushwa, kubana matumizi mabaya na wenye mwono katika kazi yake.” alisema Dewji. 

Aidha Dewji alisema kwa sasa bara la Afrika uchumi wake unakua kwa kasi huku akitolea mfano wa ripoti yam waka 2015 ambayo ilionyesha uchumi wa Afrika unakua kwa asilima 4 kwa mwaka kulinganisha na Ulaya inayokua kwa asilimia 1.5 hivyo kuwashauri wanachama wa Afrika CEO Forum kutumia vyema fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi. Washindi wengine wa tuzo zilizotolewa na Africa CEO Forum ni; CEO of the Year
  • Abdulsamad Rabiu, CEO, BUA Group
  • Issad Rebrab, Chairman, Cevital
  • Mohammed Dewji, CEO, MeTL - WINNER
  • Naguib Sawiris, Chairman, OTMT Investments
  • Said Salim Awadh Bakhresa, CEO, Bakhresa Group
  • Strive Masiyiwa, CEO, Econet
Young CEO of the Year
  • Anta Babacar Ngom Bathily, DG, Sedima - WINNER
  • Basil El-Baz, PDG, Carbon Holdings
  • Darshan Chandaria, PDG, Chandaria Industries
  • James Mworia, PDG, Centum Investments
  • Mohamed Ben Ouda, DG, SNTL
  • Lamia Tazi, DG, Sothema
African Company of the Year
  • CIEL Group
  • ECONET
  • Elsewedy Electric - WINNER
  • Label’Vie
  • MTN
  • OCP Group
African Bank of the Year
  • Attijariwafa Bank - WINNER
  • Banque Centrale Populaire
  • Ecobank
  • Mauritius Commercial Bank
  • Standard Bank Group
  • . United Bank For Africa
Private Equity Investor of the Year
  • Actis
  • Afrinvest - WINNER
  • Development Partners International LLP
  • Helios Investment Partners
  • Leapfrog Investments
  • The Abraaj Group
International Corporation of the Year
  • Allianz - WINNER
  • Coca-Cola
  • Mota-Engil
  • Orange
  • Siemens
  • Vitol
Tuzo za Africa CEO Forum zimetolewa Geneva, Switzerland ambapo wanachama wa jukwaa hilo wapo katika mkutano wa siku mbili wakijadili mambo mbalimbali ambayo yanawahusu wao kama Watendaji Wakuu na jinsi gani wanaweza kulisaidia bara la Afrika.

UJUMBE MZITO KUTOKA CHINA WAWASILI DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, alipowasili na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga. (Picha na Bashir Nkoromo).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, baadaya kumookea na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

ILALA YAZINDUA MRADI WA MAJI WA MAMILIONI PUGU

$
0
0
"Nikizindua kisima  tu nawashukuru wananchi kwa sapoti yao tunamshukuru mbunge wa ukonga Mh Waitara aliechangia Milioni tatu  katika fedha za mfuko wa jimbo,niliwasisitiza wananchi watunze mradi huo wa maji kwani ni ukombozi kwa kata yao ya pugu",alisema Kumbilamoto.
 Naibu Meya akizindua mradi mkubwa wa kisima cha maji katika jimbo la ukonga kata ya pugu mtaa wa bombani na kigogo B ,Mradi huo wa maji umegharimu kiashi cha fedha Milioni  67.610.000 kama sehemu za juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na mfuko wa Jimbo
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akifungua  bomba la Maji kuashiria kuwa Maji yanaanza kutumika katika eneo la Pugu Kajiungeni
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akimtwisha ndoo ya Maji mmoja wa wakazi wa Pugu mara baada ya Maji ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na wakazi wa Jimbo la ukonga kata ya Pugu mtaa wa bombani Kigogo B.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto  akishuka bondeni kuangalia chanzo cha maji katika eneo la Pugu

Airtel yazindua HATUPIMI bando, Ongea bila kikomo

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
 Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) ,  Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto)  na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja  wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.

 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.

“Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.

“HATUPIMI Bando” itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo

Airtel tunaamini “HATUPIMI” ni ofa ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru wakuonge watakavyo bila kikomo. Aliongeza Nchunda

Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza Nchunda.

Airtel imekuja na ofa yake ya HATUPIMI ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya Airtel Money, Vile vile airtel wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja wake wote huduma zao popote walipo.

WIZARA YA HABARI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKEMEA VITENDO VYA MMOMONYOKO WA MAADILI NCHINI.

$
0
0
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Kulia) akizungumza na wadau wa Sekta ya Utamaduni (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha Wadau tuzungumze kujadili namna ya kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lily Beleko
KEME 1
 Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lily Beleko akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini leo Jijini Dar es Salaam
KEME 2
Mkurugenzi wa Mawasiliano Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Bw. Bernard James akichangia mada wakati wa kikao na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini leo Jijini Dar es Salaam
KEME 3
 Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akijibu hoja za wadau wakati wa kikao na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini leo Jijini Dar es Salaam
KEME 4
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya utamaduni walioshikiki kikao cha wadau kujadili namna ya kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
……………
NA: Shamimu Nyaki – WHUSM.
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imewataka wadau wa Sekta ya Utamaduni na jamii kwa ujumla kusaidiana katika kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili ambao umekuwa kikwazo katika kuulinda Utamaduni wa mtanzania.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa anazungumza na Wadau wa Sekta ya Utamaduni katika muendelezo wa kikao cha “WADAU TUZUNGUMZE” ambapo amesema kuwa suala la mmomonyoko wa Maadili linaanzia ngazi ya familia hivyo linapaswa kukemea kwa nguvu zote.
“Suala la mmomonyoko wa maadili ni mtambuka na huanzia ndani ya familia na huendelea kujigawa kulingana na umri, rika, na hatimaye jamii kwa ujumla hivyo ni budi watu wote kulikemea ili tuwe na jamii yenye maadili mazuri”, Alisema Mhe. Anastazia.
Aidha Mhe. Anastazia ameeleza kuwa Wizara yake itaendelea kuchukua hatua zinazostahili ikiwemo kutoa elimu kwa kuwatumia maafisa Utamaduni wa kila Mkoa  ili kuhakikisha suala la mmomonyoko wa maadili linashughulikiwa kwa kina kwa kuwa Wizara ndio yenye dhamana ya kuratibu na kusimamia maadili ya jamii.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Lily Beleko amesema kuwa Idara yake inafanya juhudi kubwa za uhamasishaji wa jamii nzima kwa kushughulikia mipango madhubuti ya kuanzisha mifumo ya kudhibiti mmomonyoko wa maadili hapa nchini.
“Suala hili la maadili linahusu jamii nzima hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuhusisha na kushirikisha jamii yote kuchangia katika mjadala wa kupata njia sahihi za kupambana na mmomonyoko wa maadili ya jamii yetu.”Alisema Bibi Lily.
Naye Mkurugenzi wa mawasiliano Baraza la Maaskofu Tanzania Bw. Bernad James ameishauri Serikali kuendelea kukemea vitendo vyote vinavyosababisha maadili kumomonyoka hasa udhibiti wa maudhui katika sehemu tofauti ikiwemo  Muziki na Filamu ambayo ndio maeneo yanayohusisha watanzania wengi.
Kikao cha “WADAU TUZUNGUMZE” kilichoanzishwa na Mhe. Waziri wa Habari Utamaduni  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwa lengo la kukutana na wadau na kujadili changamoto zilizopo katika Wizara yake na namna ya kuzitatua  leo kimeshirikisha Wadau wa Sekta ya Utamaduni ambapo  mada ya leo ilikuwa “Je Maadili rasmi ya Mtanzania yapo au hayapo”.



WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex alipofanya ziara kwa ajili ya kusikiliza changamoto zao leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika soko hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) alipotembelea katika soko hilo leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Simbachawene amefanya ziara katika Soko hilo hili kusikiliza changamoto kutoka kwa wafanyabiashara hao na kukagua utekelezaji wa agizo alilolitao wakati wa ziara yake ya kwanza sokoni hapo mapema mwaka jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (wapili kutoka kushoto) akitembelea baadhi ya vizimba vya wafanyabiasha katika soko la wafanyabiashara wadogowadogo la Machinga Complex leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Meneja wa Soko hilo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.

Na: Mpiga Picha Wetu.

………………

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA ndogondogo katika Soko la Machinga Complex Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kubadilika na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria badala ya kufanya biashara zao kimazoea.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipofanyaa ziara ya kikazi katika Soko hilo ili kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa soko hilo.

“Nawapa pole sana ndugu zangu wafanyabiashara wa Machinga Complex mnaendesha biashara zenu bila kuzingatia sheria jambo linalo wagharimu hivi sasa katika biashara zenu leo nimekuja kuwarejesha kwenye mstari,” alisema Simbachawene.

Aidha Waziri Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Machinga Complex kwa kile kinachodaiwa utendaji wao mbovu na kujaza nadfasi zote zilizo wazi,

Wakati huohuo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuteua Wajumbe wa Bodi ya Machinga Complex ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Soko hilo.

Pia Waziri Simbachawene ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kulipa kodi zao kwa wakati huku hakitishia kuwaondoa katika vizimba (eneo la mraba la mauzo) wale wote watakao kaidi amri hiyo halali ya kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na mikataba yao.

Awali akimkaribisha Waziri Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa ujio wa Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa imekuja wakati muafaka kwani ni takribani kipindi cha karibu mwaka mmoja tangu alipompa maagizo ya kushughulikia changamoto zinazokabili jengo la Machinga Complex kazi ambayo waliikamilisha na kukabidhi taarifa katika ofisi ya Waziri Simbachawene.

“Nidhahiri kuwa ziara yako Mhe. Waziri itatoa majawabu yatakayopelekea kutatua changamoto kadhaa zinazolikabili soko hili la Machinga Complex na ni imani yangu kwamba utatoa maagizo na kufanya maamuzi nasi hatuna budi ya kuyapokea na kutekeleza” alisisitiza Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bibi. Sipora Liana amesema kuwa changamoto kubwa inayokabili Soko hilo ni pamoja na deni linalokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi bilioni 38 zianzodaiwa na Shirika la hifsdhi za Jamii (NSSF) ambao ndiyo waliojengwa majengo ya soko hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine inayokabili Soko hilo ni kutokuwapo kwa chombo cha maamuzi (Bodi) ambayo kazi yake kubwa ingekuwa kushughulikia changamoto zote za mradi huo.

Soko la Machinga Complex limejengwa kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosekanaji wa soko la uhakika kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo ujenzi wake ulifanyika chini ya udhamini wa NSSF na kumilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam likiwa na uwezo wa kuchukua takribani wafanyabiashara 4206.

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA LAZIDI KUNOGA,KWAYA YA ULYANKULU,JOHN LISSU,GOSBERT WATANGAZA KUSHIRIKI

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam , wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

WAIMBAJI wa muziki wa injili wamezidi kumiminika kuthibitisha ushiriki wao katika Tamsha la Pasaka litakalozinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jiji Dar es Salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine mitano kuutangaza ufalme wa Mungu na malengo yake mengine ya uwepo wake.

Akizungumza jijini jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo linalofanyika mara ya 17, Alex Msama, alisema ni faraja kwao kuona waimbaji mahiri wakizidi kuthibitisha tukio hilo litakalowaleta na nyota wa ndani na nje ya nchi.

Msama amewataja waimbaji wengine wapya ni Goodluck Gosbert anayetamba na kibao cha Ubarikiwe, John Lissu, Kwaya ya Ulyankulu, moja ya kwaya kongwe na maarufu iliyowahi kutamba na vyimbo nyingi zenye ujumbe kamili wa neno la Mungu ukiwemo ‘Kwa viumbe Vyote’ unaotikisa hadi sasa.

‘Tunashukuru sana kwani waimbaji wamezidi kuthibitisha kuashiria kuwa maandalizi ndiyo yameshika kasi na wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili, wakae mkao wa kupokea Baraka za Mungu kupitia ujumbe wa nyimbo,’ alisema Msama.

Alisema katika uzinduzi wa tamasha hilo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, utakwenda sambamba na uzinduzi wa albamu ya Kinondoni Revival Kwaya pamoja na kazi albamu mpya ya malkia wa nyimbo za injili nchini na Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando.

“Uzinduzi wa Tamasha la Pasaka April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, utakuwa wa aina yake kwa sababu kutakuwa na uzinduzi wa albamu mpya mbili; moja ya Kinondoni Revival Kwaya na nyingine Ruthu ya Rose Muhando,” alisema Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukuza muziki wa injili kupitia matamasha.

Kuhusu mikoa ambayo Tamasha hilo litapita, Msama alisema baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam, mashambulizi yatahamia mjini Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na kumaliza kazi hiyo mkoani Iringa kwa mwaka huu na kuwataka wadau wa muziki wa injili kuwa tayari kupokea Baraka.

Pikniki Adui wa Mazingira Ukanda wa Utalii

$
0
0



Pikiniki zinazofanywa na watu mbalimbali katika fukwe zilizoko kwenye ukanda wa utalii visiwani Zanzibar, zinachangia uharibifu mkubwa wa mazingira unaotishia kuwakimbiza watalii.

Shughuli ya kusafisha mazingira iliyofanywa juzi katika eneo dogo kwenye ufukwe wa Muyuni ulioko Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja, ilikusanya karibu tani moja ya takataka zikiwemo chupa za plastiki.

Operesheni hiyo iliyochukua saa moja, ilijumuisha wafanyakazi wa Amber Resort na Best of Zanzibar, na kusafisha eneo linaoandaliwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa kitalii utakaofanywa na kampuni ya Pennyroyal.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja Mradi wa Amber Resort Murtaza Hassanali, alisema vijana wanaotembeza watalii (mapapasi) pamoja na wageni wanaofika hapo, huondoka wakiacha vitu vingi visivyofaa ambavyo hugeuka kuwa taka na sumu kwa viumbe wa baharini.

Aidha alieleza kuwa, pikiniki zinazofanywa na watu kutoka mjini na maeneo mengine hasa vijana, ni chanzo kikuu cha uharibifu wa fukwe hizo.

"Angalia ufukwe wote umejaa chupa za plastiki, karatasi za foili, mifuko na viatu visivyofaa na hakuna mtu anayejali kusafisha. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa mazingira ya baharini," alisema.

Hata hivyo, alisema kampuni yake inakusudia kuubadilisha ufukwe huo kwa kusambaza vifaa vya kuwekea taka na kutoa elimu kwa wakaazi wa kijiji hicho juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira.

Aidha alisema kwa kushirikiana na serikali ya wilaya kupitia ofisi ya halmashauri, wataandaa mabango ya matangazo yanayohimiza wananchi kuhifadhi fukwe na maeneo yote ya kijiji hicho na kuyaweka katika sehemu tafauti.

Kwa upande wake, Nahya Khamis Nassor, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) anayesomea elimu ya afya na mazingira, alisema inasikitisha kuona fukwe zinazotegemewa kuwa kivutio kwa watalii, zimekithiri uchafu bila uangalizi.

Alifahamisha kuwa, Kamisheni ya Utalii Zanzibar inafanya kazi kubwa ya kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini kwa kusambaza vipeperushi vinavyoonesha uzuri wa mandhari pamoja na taarifa mbalimbali ili kuwashawishi watalii kuendelea kuja visiwani humu.

Hata hivyo, alisema pale watakapokuja na kukuta hali ni tafauti, watalii hao watahisi wamedanganywa na huenda wakafikiria mara mbili kabla hawajaamua kuja tena au hata kuvitangaza visiwa hivi kwa wananchi wenzao.

"Uchafu huu unaozagaa ufukweni unaishia baharini kwa kusombwa na maji yanapojaa. Plastiki haziozi na samaki wanaweza kuzila bila kukusudia na hii ni hatari kwa rasilimali za baharini kutoweka," alieleza Nahya.

Pamoja na kuwaomba wakaazi wa kijiji hicho kuzilinda na kuzihifadhi fukwe zao, aliishauri serikali ya wilaya kuunda kanuni maalumu zitakazosaidia kudhibiti uchafu unaotishia kuwakimbiza watalii.

Alisema itakuwa vyema, kanuni hizo ziweke adhabu ikiwemo faini kwa mtu yeyote atakaepatikana akichafua mazingira kwa makusudi kama inavyofanyika katika nchi na miji mingine.

Ofisa mratibu wa kampuni ya Amber Resort Mohammed Issa Khatib, alisema mpango huo utakuwa endelevu ili kuhakikisha elimu ya usafi wa mazingira inawafikia wananchi wote kijijini hapo na watu wengine wanaokitembelea ambao alisema ndio wanaoacha athari kubwa ya uchafu.

Aliwaomba wavuvi na vijana wanaofanya biashara za kitalii ufukweni waache kutupa taka ovyo, kwani kufanya hivyo kunachafua mandhari na taswira ya Zanzibar nzima mbele ya macho ya watalii.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA POLISI MURIET

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia ,ametembelea kata ya Muriet na kujionea maendeleo ya kata hiyo hususani kwenye swala la ujenzi wa Kituo cha Afya cha Muriet,Ofisi ya Kata ya Muriet sambamba na Kituo cha Polisi cha Muriet .
 
Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Kata wa Muriet akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wakikakua ujenzi wa Kituo cha Polisi.picha na Imma msumba
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia Akiwa ameongozana na Wakuu wa Idara mbali mbali kutoka Ofisi ya Jiji wakikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Muriet Ulipofikia kwa sasa.picha na Imma msumba
Muonekano wa juu wa  Kituo hicho cha Afya kinavyoonekana ambapo ujenzi unaendelea kwa sasa.picha na Imma msumba
Wakuu wa Idara mbalimbali wa Jiji la Arusha wakiwa wameongozana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha walipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Muriet.picha na Imma msumba
  Muonekano wa nje wa  Kituo cha Polisi cha Muriet kinachoendelea kujengwa  ulipofikia kwa sasa.picha na Imma msumba
 
 
 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 22,2017

UBALOZI WA MAREKANI WATOA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI KWA WANAMITANDAO

$
0
0
USA8
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizotolewa.
USA9
Maofisa wa Ubalozi wa Marekani pamoja na Mkufunzi huyo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo .
USA10
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Ricci Shryock akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
USA6
Mwanablog Vero kutoka mkoani Arusha akipokea cheti chake.
USA11
Baadhi ya washiriki wakifurahia jambo kutoka kwa mkufunzo huyo wakati wa mafunzo hayo.
USA01
Mkurugenzi wa Mtandao wa www.fullshangweblog.com Bw. John Bukuku akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari (Multmedia Journalisim) kutoka kwa Mkufunzi Ricci Shriyock kutoka nchini Senegal mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo yaliyoandaliwa , kufadhiliwa na Kufanyika kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam nchini Tanzania washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari wa Mitandao ya kijamii wamekabidhiwa vyeti hivyo leo Ubalozini hapo.
(PICHA KWA HISANI YA UBALOZI WA MAREKANI)
USA2
Mwanablog Shamim Mwasha wa 8020fashion akipokea cheti chake.
USA4
Mwanablog Freddy Njeje wa Blog za Mikoani akipokea cheti chake.
USA5
Mwanablog Josephat Lukaza wa Lukazablog akipokea cheti chake.
USA7
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabloga Tanzania Bloggers Network Krantz Mwantepele ambaye pia alikuwa mratibu wa mafunzo hayo akipokea cheti chake.
USA12
Miss Populler akipokea cheti chake mara baada ya mafunzo hayo.

SHERIA IMERUHUSU KUDAI ZAWADI ULIZOTOA UCHUMBA UNAPOVUNJIKA.

$
0
0
Na Bashir Yakub.

Una mahusiano na mwanaume au mwanamke ambaye kimsingi mpo katika uchumba. Unampa zawadi nyingi naye anakupa zawadi. Mnayo ahadi ya kufunga ndoa na kuishi kama mme na mke . Na kwasababu hiyo unajitoa sana kimatumizi kwa mtu huyo. 

Lakini katika mazingira usiyoyaelewa unaona sasa mambo hayaendi vizuri. Hayaendi vizuri katika kiwango ambacho sasa mahusiano yamevunjika kabisa. Hakuna tena mahusiano. Au bado yapo lakini kwa mambo unayofanyiwa unaona kabisa hutakiwi tena.

Kumbuka huko nyuma umegharamia sana. Umegharamia kwa fedha na mali. Swali ni je vitu hivi haviwezi kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?. Na je sheria imeongelea kuhusu jambo hili ?. 

Majibu ya maswali haya yote ni ndiyo. Ni ndiyo, na gharama pamoja nazo zawadi zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa kuona sheria imeongelea hata mambo ya uchumba lakini ndio ukweli. 

Wengi tunaijua sheria katika kuongelea wizi, dhamana, mikataba, mirathi, ndoa, na mengine. Lakini ni vyema tukajua kuwa sheria ni pana na imeongelea mambo mengi mno. Hili la uchumba nalo ni sehemu ya yaliyoongelewa.





BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA WARSHA YA BIASHARA CLUB KWA WATEJA WAKE AMBAO NI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI

$
0
0
Benki ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki na huduma endelevu za kimaendeleo kwa wateja wake. 

Zaidi ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza fedha, jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu , jinsi gani taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za mtu binafsi zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi zinapatikana kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha. 

Kwa kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na kilimo Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa bidhaa zinazo zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya tafiti mbalimbali nchi nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo maalumu kwa wajasiriamali wadogo na wakati, 

kuzisaidia taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa misitu kwa pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na kuwaunganisha wanachama na fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa kimataifa. Akiongea kwenye warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam, 

Mkurugenzi Mkuu wa KCB Bwana Godfrey Ndalahwa alisema kwamba, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi. “ Dhumuni letu sio kutoa suluhisho yakinifu kwa masuala ya kibenki tu bali pia ni kuwapa ujuzi na nyenzo zinazohitajika katika kufanikisha biashara zao” Wanachama wa KCB Biashara club watapatiwa ujuzi wa kutosha kupitia warsha mbalimbali ambapo ushauri wa kibiashara utatolewa kutoka kwa wataalam waliothibitishwa. 

Warsha hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kuwa kwenye mtandao na kuwasiliana wao kwa wao na kushirikishina ujuzi bora wa kibiashara. Katika kuongezea hili, pia wanachama watapata fursa ya kusaidiwa na mameneja uhusiano wanaowasikiliza kwenye mahitaji yao ya kifedha. Wanachama wa KCB Biashara club pia watanufaika na fursa zilizopo nje ya nchi ambapo matawi ya benki za KCB yapo. 

“ Ikiwa ni moja ya maidhinisho yanayotolewa na club hii, tumeweza kupata maelezo kutoka kwa mtendaji wa KCB Biashara club Bwana Moses Odipo ambaye ametushirikisha safari za kibiashara za mwaka 2017. Hii itawawezesha wanachama wetu kushiriki kwenye safari za mkoa mpaka safari za kimataifa katika kuwezesha biashara zao.Wanachama watahudhuria maonesho ya kibiashara ya Kimataifa ili kujifunza jinsi wajasiriamali wengine wa kiwango chao wanavyo jiendesha kwa dhumuni la kuboresha biashara zao . 

Wakati akitoa mchanganuo wa KCB Biashara Club, Bwana Masika Mukule, mkuu wa kitengo cha wateja masuala ya kibenki, alisema kwamba, Biashara club imedhamiria kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwapa nyenzo na kuhakikisha wana ujuzi sahihi wa kuendesha biashara zao na kutoa dondoo juu ya taarifa za kifedha zinazohitajika na taasisi za kifedha pindi wanapo omba mkopo. 

“Mwaka huu warsha yetu ina maudhui mazuri sana yaliyoandaliwa kwa kufuata maoni yaliyotolewa kwenye warsha yetu ya mwaka jana na tunaamini mwakani tutakuwa tumewawezesha baadhi ya wajasiriamali wadogo na wakati kufikia kiwango cha wateja wa kiwango cha juu.Bwana Mukule aliendelea kusema kwamba KCB wanazo bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la wajasiriamali wadogo na wakati ikiwa ni pamoja na Masharti ya mkopo, overdaft facilities, Overdraft facilities, Bank Guarantees, Invoice Discounting, Documentary letters of Credit, Asset Based Finance na Bills Discounting. 

Mbali na hizi kitengo hiki kinatoa mikopo ya nyumba kwa wanao nunua, matengenezo au kumalizia ujenzi, Advantage Banking na bidhaa za kibenki kwa wateja wetu waliopo nje na ndani ya nchi .Wanachama wetu wana mengi ya kupokea kutoka kwetu,” Alimalizia Bwana Mukule
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KBC, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Edgar Masatu akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.



Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.


Wafanyabiashara wakifuatilia.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SAMAKI CHA MAURITIUS

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa samaki katika kiwanda cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitazama makasha yenye minofu ya samaki wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha samaki cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

BOMOA BOMOA KANDO YA RELI YALIKUMBA ENEO LA KURASINI DAR

$
0
0
 Katapila likibomoa majengo ya Baa ya Pentagon  katika oparesheni ya bomoa bomoa nyumba zote zilizojengwa katika hifadhi ya Reli ya Kati eneo la Mivinjeni, Kurasini Dar es Salaam.
 Makontena ya biashara yakiwa yamefumuliwa na katapila
 Baa ya Pentagoni ikiwa imebomolewa 
 Katapila likiendelea na kazi ya bomoa bomoa

 Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa na vibanda vya biashara pamoja na wananchi wakishuhudia ubomoaji huyo
 Askari wakilinda doria wakati wa ubomoaji
Wataalamu wakipima mita 20 kutka kwenye reli ili nyumba na mabanda yaliyo ndani ya hifadhi ya reli zibomlewe kupisha ujenzi wa reli ya kisasa.

PICH ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0754264203

WAZIRI NAPE APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOTOKEA CLOUDS MEDIA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Hassan Abbass.
Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.


Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.

Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.

Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.“Nimeipokea ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.

Kamati aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas .

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA KATBU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) NDUGU GUO JINLONG

$
0
0


Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam kwa mazungumzo leo Jumatano Machi 22, 2017 .
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa ujumbe aliofuatana nao Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong akisalimiana na viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong wakishuhudia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt.Lu Youqing wakitia saini mkataba moja ya mikata mitatu.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong wakishuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Aziz Mlima na Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt.Lu Youqing wakitia saini mkataba moja ya mikataba mitatu
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong wakishuhudia na Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Fred Kibuta na Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt.Lu Youqing wakitia saini Mkataba moja kati ya mikataba mitatu.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images