Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

0
0


HALMASHAURI ZATAKIWA KUVITAZAMA VIKUNDI VYA JOGGING

0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akizungumza wakati wa Bonanza la Klabu ya Mbio za pole za Mzimuni Joging
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Oamry Kumbilamoto akiongoza safu ya Wakimbiaji katika Bonanza la Mzimuni

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto ameviomba vikundi vya Jogging kuanza kujisajiri hili waweze kupata fursa za mikopo kutoka Halmashauri zao.

Kumbilamoto amesema hayo alipokuwa  akizungumza na Vikundi mbalimbali vya Jogging katika Bonanza lililoandaliwa na Mzimuni Joger  na kushirikisha vikundi zaidi ya kumi.

"kila Halmashauri ina mapato ambayo inatakiwa kutoa kwa vijana  ambayo ni asilimia 10 kwa vijana na vikundi vya kina mama hivyo vikundi vya Joging vinahusisha watu wote hao katika hivi vikundi vyetu" Amesema Kumbilamoto

amesema ufike wakati wa Halmashauri zote zitenge pesa za vijana na kuacha ujanja ujanja wa kukwepa kulipia fedha hizi kwani kama wanashindwa waje kujifunza Ilala hili waweze kuwakwamua vijana na kinamama
 Wana vikundi wakikimbia katika Bonanza hilo la klabu ya Mzimuni
 Klabu ya Afya na Uchumi ikiwa katika Bonanza hilo

TAARIFA KWA WATUMISHI WA UMMA

0
0

KONGAMANO LA MAADILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

0
0

Na Dotto Mwaibale

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inatarajia kufanya kongamano linalolenga maadili kwa Taifa nchini.

Kongamano hilo litafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema ni wajibu kwa kila mwanajamii kuthamini, kuenzi na kuendeleza maadili mema, mila na desturi zinazofaa.

“Serikali hususani wizara inajukumu la kutoa muelekeo na usimamizi kuhakikisha Taifa linaenzi na kuimarisha utambulisho wake na kujenga utamaduni huru na sio huria” alisemaWambura.

Aidha Wambura alisema kuna fursa ya kubaini, kuenzi na kukuza, kuhifadhi na kurithisha utamaduni na sanaa vyenye kuzingatia na kuimarisha maadili, mila na desturi kwa kuleta maendeleo.

“Wananchi wamekuwa wanaendelea kujihusisha na shughuli mbalimbali za Kifani, Sanaa na utamaduni ikiwemo ngoma za asili, filamu, muziki, jando, unyago, matambiko, Sherehe na maadhimisho mbalimbali” alisemaWambura.

Ameongeza kuwa shughuli hizo ni halali ilimradi zifanywe kwa kuzingatia sheria na kanuni na msingi wa asili yake, kwa maana kwamba kama jambo ni la faragha na usiri libaki kwenye uhalisia wake na kuhusisha rika jinsia na asili yake.


Naibu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano la maadili litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa kuanzia saa nne asubuhi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

ZIFAHAMU TIMU ZILIZOINGIA NA KUTOLEWA KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

 Timu zilizofuzu hatua ya makundi klabu bingwa Africa ni kama ifuatavyo

1)Zanaco-Zambia
2)Mamelodi sundwon-SA
3)Wydad Casablanca-Morroco
4)USM Alger-Algeria
5)Cotton Sport-Cameroon
6)Al-Merreikh-Sudan
7)Al-Ahly-Egypty
8)CAPS United-Zimbwabwe
9)Al-Ahly Tripoli-Libya
10)St George-Ethiopia
11)Zamalek-Egypty
12)As Vita-DRC
13)Al Hilal-Sudan
14)Esperence Tunis-Tunisia
15)Ferroviario Beira-Mozambique
16)Etoile du Sahel-Tunisia.                        

 Timu zilizotolewa klabu bingwa ambazo zitakwenda kucheza mchezo wa mtoano na timu 16 zilizofuzu caf confederation cup ili kupata team 16 zitakazocheza hatua ya makundi confederation cup ni zifuatazo

1)Yanga-Tanzania
2)KCCA-Uganda
3)CF Mounana-Gabon
4)CNaPS SPORT-Madagascar
5)Rail Club Kadiogo-Burkinafaso
6)Rivers united-Nigeria
7)Tp Mazembe-DRC
8)Bidvest Witts-SA
9)FUS Rabbat-Morroco
10)Leopard-Congo
11)ASPL-Mauritious
12)Enugu rangers-Nigeria
13)Gambia port-Gambia
14)Tanda-Ivory Coast
15)Horoya AC-Guinea
16)BYC-Liberia

WAZIRI NAPE AUNDA KAMATI KWA AJILI YA KUCHUNGUZA TUKIO LA UVAMIZI WA KITUO CHA HABARI CHA CLOUDS.

0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) alipofanya ziara katika Chombo cha Habari cha Clouds leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Katikati, akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) Bw. Reginald Mengi (kulia) alipofanya ziara katika chombo cha Habari leo Jijini Dar es Salaam ,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Bw.Joseph Kusaga (wa pili kushoto) alipowasili katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas (pembeni ya Waziri) na wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Clouds Bw. Simon Simalenga.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akielezwa jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) Bw. Reginald Mengi (kulia) alipotembelea Ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Bw.Joseph Kusaga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba(MB).
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jamii wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo (hayupo katika picha) Peter Serukamba (MB) walipotembelea Kituo cha Habari cha Clouds leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence WHUSM.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano itayoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas kuchunguza tukio la uvamizi lilofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika chombo cha habari cha Clouds Media.
Akiongea katika ziara aliyoifanya  leo  Jijini Dar es Salaam  katika chombo hicho Mhe.Nape amesema Kamati hiyo itafanya kazi ndani ya masaa 24 kuanzia sasa huku akiwataja wajumbe wengine  kuwa ni Bw. Frank Balile,Bibi.Johanes Neng’ida,Bw.Jessy Kwayu na Bibi. Mabel Mabisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Serikalini (TCRA).
“Kamati hii ipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda ili tuwe na taarifa iliyokamilika na kujua hatua itakayofuata” alisema Mhe.Nape
Aidha Waziri Nape ameeleza kuwa kitendo cha uvamizi kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa kipo kinyume na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwa kuwa sheria hiyo ipo kwa ajili ya kulinda wanatasnia hao.
Aliongeza na kufafanua kuwa Serikali imesikitishwa na kitendo hicho na ndio maaana akaunda kamati ya uchunguzi itakayokuja na taarifa kamili huku akiwataka wanatasnia ya habari na wananchi kuwa watulivu na kusubiri majibu ya uchunguzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Habari ya Clouds Bw.Joseph Kusaga amemshukuru Waziri Nape kwa kuonyesha ushirikiano na kuwa pamoja katika jambo hilo huku akifurahishwa na namna Serikali inavyowajali wadau wa Habari.  
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Bw.Reginald Mengi amempongeza Mhe. Waziri kwa hatua ya kuunda kamati ya uchunguzi  kwakuaanaamini itatoa matokeo chanya yatakayolinda heshima ya Tasnia ya Habari nchini.
“Uamuzi wa kuunda kamati hii ni jambo la hekima na busara linaloendana na misingi ya taaluma ya habari nasi tutakuwa radhi kuunga mkono hatua  zitachukuliwa katika kulinda uhuru wa habari nchini” alisema Bw.Mengi.
Tukio la kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Mkonda   limetokea usiku wa  Machi 17 mwaka huu.

RAIS MAGUFULI AMEWATAKA WATANZANIA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA JUU.

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro,Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam utakaogharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kabla ya kuweka jiwe la msingi la barabara za juu eneo la Ubungo.
 
“Tutasimamia pesa izi kikamilifu ili tujenge barabara izi za juu vyema,nawataka Watanzania kusimamia mradi huu ili ukamilike haraka na hivyo Wizara,Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ili ulete ukamilike na kuleta tija kwa wananchi hawa”,Aliongeza Rais Magufuli.
 
Amesema katika ujenzi wa mradi huo bilioni 1.9 inatoka Serikalini na bilioni 186 inatoka Benki ya Dunia na ivyo ni muhimu kuulinda kwani ni pesa za Watanzania walipa kodi.
 
Aidha amesisitiza kuwa nchi ya yetu imepata mkopo huu  kwa sababu tunaaminika katika kukopesheka na tunarudisha kwa wakati,amemuomba rais wa benki ya Dunia  kuendelea kuikopesha Tanzania katika miradi mingine.
 
Rais Magufuli ameeleza kuwa mkopo huu kutoka benki ya Dunia una riba ya asilimia 0.5 na unalipwa ndani ya miaka 40 ivyo ni vyema kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia.
 
Pamoja na hayo amewataka Watanzania kuendelea kulipa kodi itakayowezesha ili Serikali iendelee kutekeleza miradi mingine na kuongeza kuwa kukamilika kwa mradi huu kutatoa sura ya pekee ya jiji la Dar es Salaam na kupunguza msogamano wa magari kwa kiasi kikubwa sana.
 
Kwa Upande wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt.Jim Yong Kim ametoa shukurani kwa Serikali ya Tanzania na kusema kuwa ameshawishika kuja nchini baada ya kusikia vongozi wengi wa Dunia wakisifia jitihada za Rais Magufuli za kuunda upya Serikali yake ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi na kuwekeza katika kujenga miundombinu na elimu.
 
“Tanzania inaelekea kuwa Taifa la watu wa kipato cha kati miaka nane ijayo na kila mtu kuwa na bima ya afya,elimu bora na muono mzuri wa mbeleni,na njia pekee ya kufika huko ni kujitegemea na kutumia rasilimali za nyumbani katika mkakati bora kabisa na hivyo kupunguza kabisa misaada ya nje ambayo imeshuka hapa nchini kwenu,”Aliongeza Dkt.Jim Yong Kim
 
Aidha amesema kuwa tangu kufunguliwa kwa Mabasi ya Mwendo kasi imepunguza msongamano kwa dakika 90 kwa siku na hivyo ufunguzi wa biashara mpya pia umeenda sambamba.
 
Amesisitiza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kusimama pamoja na Tanzania katika maendeleo na kufanya kazi pamoja.

ZOEZI LA UBOMOAJI WA MAJENGO YALIYOMO KATIKA HIFADHI YA RELI KUENDELEA NCHINI KOTE

0
0
 Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyomo katika hifadhi ya reli linaloendelea nchini limezingatia  taratibu na sheria za uendeshaji wa reli na kwamba matangazo ya notisi ya kuwataarifu waanchi waliovamiwa hifadhi hizo zilizotolewa mapema ili wananchi hao waweze kuhama.

akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji RAHCO Bw. Massanja Kadagosi amesema Ubomoaji huo unaoendelea haupo kwa ajili ya kumuonea mtu bali upo kwa ajili ya kulinda miundombinu ya reli ikiwemo pia kujali usalama wa wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli. ‘’Sheria ya Reli Na.4 ya mwaka 2002,kifungu cha 57 (2) kinabainisha kuwa mtu yoyote haruhusiwi kufanya ujenzi wowote katika hifadhi ya njia ya reli pasipo kibali cha RAHCO, kwani sheria hii inatamka wazi  kuwa mtu yeyote harusiwi kufanya ujenzi wowote katika eneo lilopangwa na mamlaka husika”
Madagosi amesema kabla ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo walitoa notisi mbali mbali ikiwemo tangazo la kuwataarifu wavamizi hao kupitia kwenye vyombo vya habari vya tarehe 25/4/2016, pamoja na kutoa barua kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ya kuwajulisha wananchi hao kuanza kuhama kabla yauvunjaji kuanza.

Mbali na Barua hizo, amesema Bw. Kadagosi  tarehe 9 hadi tarehe 10 /2/2017 waliziweka nyumba alama ya X kwa wavamizi hao, analosema kuwa watu wanaosema wananchi hao wanaovunjiwa hakuwapata taarifa za kutakiwa kuvunjiwa nyumba si za kweli kwani taarifa zilitolewa. 

Bw. Kadagosi amewataka wananchi waliovamia maeneo hayo kuhama mara moja kwani kukaa kwenye maeneo hayo sio tu ni kosa la jinai bali pia linahatarisha usalama wao.
Mkurugenzi mtendaji  Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi  habari leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia  zoezi la ubomoji wa nyumba zilizopo kwenye hifadhi ya reli
Afisa Uhusiano wa RAHCO,Catherine Moshi  akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
Waandishi wa habari na watendaji wa RAHCO wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji  Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO),Masanja Kadogosa.



DC DODOMA AKUTANA NA KAMATI NDOGO YA MKOA YA URATIBU UJENZI WA UWANJA WA MICHEZO WA KIMATAIFA DODOMA

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na Kamati ndogo ya Mkoa inayoratibu Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utakojengwa katika kata ya Nala Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)   katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
  Mjumbe wa hiyo ambaye ni Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)  wakati Kamati hiyo ilipokutana na Mkuu huyo wa Wilaya. 
 Mjumbe wa hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Dodoma Bw. Hashimu Kitambuliyo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) kuhusu mipango na mikakati iliyoweka na Kamati hiyo katika kufanikisha Mradi huo.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 21,2017

0
0

Maonyesho ya biashara ya Mauritius yazinduliwa Dar

0
0
 Maonyesho ya biashara yanayohusisha makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius yamezinduliwa leo jijini Dar es Salaam yakilenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa baina ya nchi hizo mbili kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina yao.

Maonyesho hayo ya siku mbili yameratibiwa na kampuni ya Talemwa Investment Consulting Company (TICC) ya nchini Tanzania, kwa kushirikiana kampuni za Enterprise Mauritius (EM) Mauritius na apex Trade Promotion Organisation Mauritius za nchini Mauritius huku yakihusisha zaidi ya makampuni yaliyojikita kwenye sekta za kilimo, uhandisi, nguo na usafi kutoka nchini Mauritius.

Akizungumza kwenye warsha fupi ya uzinduzi wa maonyesho hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,  Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee itakayowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizo mbili ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa za kipekee zilizopo baina ya nchi hizo.

“Mauritius ni miongoni mwa nchi ambazo zinakuja juu kwa kasi kiuchumi na zinaweza  kuwavutia wawekezaji kutoka nchini Tanzania kwenda kuwekeza kule wakati huo huo tunatarajia kwamba Tanzania ikiwa kama kitovu cha biashara na maliasili mbalimbali inaweza kuwavutia pia wawekezaji kutoka Mauritius kuja kuwekeza huku,’’ alisema.

Aliongeza kuwa katika maonyesho hayo ambayo pia yatatoa fursa kwa wahusika kujifunza tamaduni tofauti na zile za mataifa yao, mada mbalimbali zitawasilishwa sambamba na mikutano kadhaa baina ya wahusika kutoka pande hizo mbili.

Akizungumzia maonyesho hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara chini, Johnson Minja alitoa wito kwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kutafuta fursa mbalimbali za kibiashara ili kujiongeze masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

“Uwepo wa maonyesho haya ni wazi utaendelea kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuweza kutambua fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo nje ya nchi. Lakini pia maonyesho haya yatafungua milango kwa wenzetu kutoka Mauritius kutuletea mawazo na mbinu mpya kibiashara. Nawasihi sana wafanyabiashara wa Kitanzania wachangamkie sana fursa hii,’’ alisisitiza.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara chini, Johnson Minja akizungumza kwenye warsha fupi  ya uzinduzi wa maonyesho biashara ya Mauritius yaliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanayohusisha makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa baina ya nchi hizo mbili kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina yao
Ofisa Biashara Mkuu wa Tantrade, Stephen Kobro akizungumza kwenye warsha fupi  ya uzinduzi wa maonyesho biashara ya Mauritius yaliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanayohusisha makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa baina ya nchi hizo mbili kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina yao.
 

WALIOJENGA NYUMBA PEMBEZONI MWA MTO MPIGI WAAMRIWA KUBOMOA NYUMBA ZAO

0
0

Na Lulu Mussa
Bagamoyo - Pwani .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameagiza kusitishwa mara moja kwa shughuli zote za kibinadamu kando kando ya Vyanzo vya maji.

Rai hii imetolewa leo na Waziri Makamba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Mkoa wa Pwani eneo la Mto Mpiji ambao umeathirika kutokana na Uchimbaji wa mchanga na mmomonyoko wa ardhi unaohatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu kuwaondoa watu wote waliojenga pembezoni mwa Mto Mpiji na kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ndani ya siku 30. " Mkurugenzi hakikisheni kuwa wakazi hao waliovamia eneo la mto huu na kujenga makazi yao ya kudumu wanaondolewa mara moja" Alisisitiza Waziri Makamba.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea Mto Wami na kusikitishwa na uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na uchimbaji haramu wa madini, upasuaji mbao na uchomaji mkaa unaopelekea mmomonyoko wa udongo na mchafuko/tope jingi na kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa maji.

Katika kukabiliana na changamoto zilizoainishwa Waziri Makamba amesema Ofisi yake itaanda kikao kazi kitakachojumuisha wadau wote muhimu ili kunusuru Mto Wami haraka iwezekanavyo. "Serikali haiwezi kuwekaza fedha nyingi kwenye mradi mkubwa kama huu na kuona uharibifu ukiendelea na kuharibu miundombinu, hali hii haikubaliki na nitachukua hatua za haraka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida kujionea hali ya mazingira na changamoto za hifadhi katika mikoa husika. 

Hii ni ziara ya pili baada ya iliyofanyika mwezi Oktoba 2016, katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini. Katika siku ya kwanza Waziri Makamba ametembelea Mto Mpigi, Mto wami na hifadhi ya msitu wa Kibindu uliovamiwa na wananchi.

Kesi ya Wakurugenzi MSD kusikilizwa Aprili 18, mwaka huu.

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Kesi ya Matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Cosmas Aron Mwaifwani na Kaimu Meneja Manunuzi MSD, Frederick Rubanga Nicolaus itaanza kusikilizwa Aprili 18, mwaka huu.

Hatua hiyo imefikiwa leo baada ya upande wa mashtaka kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa, Aneth Mavika ameiambia mahakama kuwa, kesi leo imekuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali na wako tayari kuwasomea.

Wakili Mavika amesoma melezo hayo mbale ya Hakimu Mkazi Mkuu Respicius Mwijage ambapo katika maelezo hayo, washtakiwa wamekubali maelezo yao binafsi na vyeo vyao na kasha kukana mashtaka yote yahayohusiana na kosa hilo la matumizi mabaya ya madaraka.

Hivyo kesi hiyo namba 102 ya 2017 itaanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Aprili 18, mwaka huu.7

Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Machi Mosi na 19, mwaka 2013 washtakiwa hao wakiwa Makao Makuu ya MSD yaliyopo Temeke kwa nafasi zao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa, kusaini mkatabata namba moja wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/1011/60 wa Machi Mosi, 2013.

Iliendelea kudaiwa kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kuandaa call of oder namba 2 yenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/2011/60 ya Machi 19, 2013 na kuisababishia kampuni ya H.H Hillal & Company Limited kupata manufaa ya milioni 482,266,000.

Kesi hiyo itaendelea April 18, mwaka huu kwa shahidi wa kwanza wa upande wa jamuhuri kuanza kutoa ushahidi wake.

DC DODOMA AWATAHADHARISHA WATAKAODANGANYA KATIKA ULIPAJI FIDIA ENEO LA UJENZI WA UWANJA WA MICHEZO NALA.

0
0

Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme amewatahadharisha wakazi wa Kata ya Nala watakaofanya aina yoyote ya udanganyifu katika ulipaji fidia kwao kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utaojengwa Mjini Dodoma.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.

“Wewe kama unajijua sio mkazi halali wa eneo unapopita mradi huu naomba ukafute jina lako ila tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria” alisisitiza Mhe. Christina.

Mhe. Christina Mdeme ameongeza kuwa Serikali haipo tayari kupoteza hela kwa ajili ya kulipa watu wasiostahili katika mradi huo na kwamba kila anayehusika kulipwa fidia kihalali atalipwa.

Aidha Mhe. Christina Mdeme amewahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa Serikali haitamdhulumu mtu yoyote na atahakikisha kila anayepaswa kulipwa fidia analipwa fidia anayostahili.

Pia amewatahadharisha wakazi hao kutotumiwa na viongozi au vikundi vya watu kwa manufaa ya kujipatia pesa zinazotokana na fidia za mradi huo kwa njia za udanganyifu.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando amewaomba wakazi wa Kata ya Nala kuwa watulivu na kwamba Sheria na Taratibu za ulipaji fidia zitafuatwa kikamilifu katika zoezi hilo.

Akitoa maelezo ya kwa niaba ya Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Salum Mkuya amewahikikishia wakazi wa Kata ya Nala ushirikiano kutoka kwa Kamati yake ili kufanikisha mradi huu wa kimataifa.

Akizungumza kabla ya kufunga mkutano huo Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah amewaomba wakazi wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Serikali watakaokuwa wanatathimini maeneo yao kwa ajili ya ulipaji wa fidia.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza maoni na changamoto mbalimbali zilizopo katika kuanza kutekelaza radi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa Dodoma.
Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah akiwasisitiza wakazi wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Dodoma Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
Afisa Mipango Miji Manispaa ya Dodoma Bw. Clemence Msuva akieleza taratibu za tathimini ya eneo lililopo katika Kata ya Nala utakapojengwa uwanja wa Michezo wa Kimataifa zitavyofanyika ili kuwezesha mradi huo kuanza mapema.
Mmoja wa Mkazi wa kata ya Nala Stanley Wilson akiuliza swali kwa Kamati Ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa kuhusu utekelzaji wa mradi huo na faida watakazopata wakazi wa kata ya Nala na Dodoma kwa ujumla.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akiwahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa Sheria na Taratibu zitafuatwa katika ulipaji wa fidia kwao.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Nala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) alipowatembelea na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

KITABU CHA UWIANO WA TAKWIMU ZA WANAWAKE NA WANAUME CHAZINDULIWA JIJIJINI DAR ES SALAAM

0
0

 Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku (katikati) akiwa na wadau wakionesha kitabu cha uwiano wa takwimu za  wanawake na wanaume wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango, Ofisa wa Takwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger, Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda na Mwanahabari Philip..Kitabu hicho kimeandikwa na wanafunzi watano kutoka Tanzania waliopata mafunzo ya miezi 11 nchini Sweden.
 Mada kuhusu mafunzo hayo zikitolewa kabla ya uzinduzi.

 Wafadhili wa mafunzo hayo kutoka nchini Sweden wakifuatilia mada kuhusu mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango (kushoto) na Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa karibu hafla hiyo.
 Mtakwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda akichangia jambo
 Mada zikiendelea kutolewa.
 Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki (kushoto), akizungumzia mafunzo ya takwimu waliopata nchini Sweden.
 Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Tacaids, Jacob Kayombo akichangia jambo katika mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Jerome Kamwela akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina akichangia.
 Washiriki wa  mafunzo hayo (walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa. Kutoka kulia  Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina, Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki, Ofisa wa Jinsia wa Tacaids, Judith Luande, Philbert Mrema kutoka NBS na Mariam Kitembe kutoka NBS.

Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale

WANAUME wameonekana kuwa wengi katika nafasi mbalimbali ukilinganisha na wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki, Chisker Masaki wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Uwiano wa Taarifa za Takwimu kwa Wanawake na Wanaume Tanzania.

Alisema kitabu hicho kimeandaliwa na washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za takwimu kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Hakielimu , Ofisi yaTaifa ya Takwimu (NBS) na Chuo cha Takwimu cha AfrikaMashariki, chini ya wakufunzi  wa masuala ya ukusanyaji wa taarifa kutoka nchini Sweden.  

Masaki alisema utafiti unaonesha  kuwa kuna tofauti  kubwa   za  uwiano kati ya  mwanamke na mwaume katika  nyanja za kimaendeleo na kijamii, ambapo maeneo mengi  yanaonekana kutwaliwa na wanaume kuliko wanawake.

Akitolea  mfano  upande  wa  elimu  kuanzia  shule  za  msingi  hadi  chuo  kikuu  wasichana  wanaoandikishwa  hadi  kufikia  chuo  kikuu  ni  wachache  ukilinganisha  na  wavulana,watu  wenye  nafasi  nzuri maofisini  hasa  ngazi  za  Ukurugenzi  na  mameneja  wengi ni wanaume  ukilinganisha na   wanawake,viongozi  wa  kisiasa mfano  mawaziri na wabunge wanawake ni wachache ukilinganisha na wanaume.

Alisema pamoja na uwiano huo wa wanaume kuwa kiwango kikubwa katika  masuala ya maendeleo wanawake wamekuwa wakichukua  nafasi kubwa katika kuathirika na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Mafunzo  hayo ya ukusanyaji wa taarifa yalianza tangu mwaka 2016 mwezi Mei hadi Machi  2017  ambapo mafunzo yalifanyika nchini Sweden ni ukusanyaji wa taarifa pamoja na uandaaji wake kitabu ukafanyika Tanzania.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA ALTEO NCHINI MAURITIUS

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha sukari cha Kampuni ya Alteo ya Nchini Mauritius chenye uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani 170,000 za sukari kwa mwaka.

Kampuni ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro  kwa ubia na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.

Waziri Mkuu ametembelea kiwanda hicho leo (Jumanne, Machi 21, 2017) na kujionea namna wanavyozalisha sukari kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.

“Tekonolojia wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi mahitaji,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera vinavyozalisha tani 320,000 kwa mwaka huku mahitaji ni tani 420,000.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na
uhaba wa malighafi.

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Khalid ameikaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye viwanda vya sukari. Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo ya uwekezani wa mashamba ya miwa nchini.

Pia ameomba Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro. “ Kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro,”.

Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 21, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mfumo wa kompyuta wa kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la miwa wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017.

Serikali Imefuta Usajili wa Vibali vya Uzalishaji na Uingizaji wa Pombe za Viroba.

0
0
Na: LilianLundo – MAELEZO

Serikali imefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na Uingizaji wa aina 20 ya pombe kali za viroba zilizokuwa zimesajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam kuhusu usitishaji wa uzalishaji na uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe zilizofungwa katika mifuko ya plastiki (Viroba).

“Tumefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na uingizaji kutoka nje, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika mifuko ya plastiki (viroba) chini ya ujazo wa milimita 200,” alifafanua Ummy Mwalimu.

Aliendelea kwa kusema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa tamko la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa Februari 02, 2017 la kusitisha uzalishaji, uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe hiyo kali kuanzia Machi 01, 2017.

Ummy amesema kuwa usitishaji huo unazingatia kanuni za kukataza uzalishaji, uingizaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali za mwaka 2017 (The Environmental Management (Prohibition of Manufacturing, Important and Use of Plastic Sachets for Packakging Distilled and other alcoholic beverages) Regulations 2017) imekatazwa kutumia vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali. Badala yake wazalishaji watapaswa kufungasha pombe kali hizo katika chupa zenye ujazo usiopungua mililita 200.

Aidha amesema kuwa uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya pombe za aina hiyo unatokana na athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya na kijamii. Matumizi mabaya ya pombe hizo yamesababisha ajali nyingi, vifo, ulemavu na mzigo mkubwa kwa Serikali wa kutoa huduma kwa wahanga wa pombe hizo na ongezeko la makosa ya jinai.

Ummy amesema kwamba Viroba vilivyokamatwa na kuzuiwa vinasubiri maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu namna ya kuviteketeza.

Umoja wa Ulaya wachangia bilioni 15 miradi ya umeme vijijini

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (Kushoto-waliokaa) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF), Goodlove Stephen (Kulia-waliokaa), wakitiliana saini Mkataba wa Msaada wa Euro milioni 6.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Euro milioni 1.5 kutoka Serikali ya Tanzania, kusaidia Mfuko wa uendelezaji miradi ya Umeme Vijijini. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Mipango na REA. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

Na Veronica Simba – Dodoma
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa Euro milioni 6.5 ambazo ni sawa na takriban shilingi bilioni 15.3 za Tanzania kwa ajili ya kusaidia Mfuko wa uendelezaji miradi ya umeme vijijini.  Aidha, Serikali ya Tanzania imechangia Euro milioni 1.5, sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 3.5 hivyo kuwezesha kufikia jumla ya Euro milioni 8 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 18 za Tanzania.

Mkataba wa msaada huo, ulisainiwa hivi karibuni baina ya mwakilishi wa EU na Serikali ya Tanzania, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, mjini Dodoma. Akizungumza katika hafla ya utilianaji saini mkataba huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alieleza kuwa, fedha hizo zitatumika kujenga Kituo cha kupoza umeme wa kilovolti 220/33 wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro pamoja na miundombinu ya kusambazia umeme katika Wilaya za Kilombero na Ulanga.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (Kulia) pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) (Kushoto), katika hafla ya kutiliana saini Mkataba wa jumla ya Euro milioni 8, ambazo kati yake, Euro milioni 6.5 zimetolewa na EU na Euro milioni 1.5 zimetolewa na Serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kusaidia Mfuko wa uendelezaji miradi ya Umeme Vijijini. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

Naibu Waziri alifafanua kuwa, msaada huo uliotolewa ni kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (European Development Fund – EDF) ambao unalenga kusaidia Ukanda wa Kilimo wa Kusini wa Tanzania. “Nia hasa ni kuwezesha mazingira ya mapinduzi ya kilimo endelevu kwa Ukanda huo.”
Dk Kalemani alieleza zaidi kuwa, Mradi huo utawasaidia wananchi wanaojishughulisha na kilimo hususan katika Wilaya za Ifakara, Kilombero na Ulanga kutokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo yao na hivyo kuwa kichocheo kikubwa kwa uchumi wa viwanda.
“Nawahamasisha wananchi wa maeneo hayo wajiandae kuupokea Mradi husika kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla,” alisisitiza.

Alisema kuwa, Mradi huo utakaochukua kipindi cha miezi 36 kukamilika, utaanzia maeneo yaliyotajwa lakini lengo ni kufikia maeneo mbalimbali nchini. Kwa upande wake, Mkuu wa Mahusiano kutoka EU, Jose Correia Nunes alisisitiza kuwa, upatikanaji wa umeme ni moja ya sifa muhimu za kuwawezesha wananchi kiuchumi. “Ni kwa sababu hiyo, Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, tunalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika na wa bei nafuu ili waweze kukabiliana na changamoto ya kuondoa umaskini.”
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya hafla ya kutiliana saini Mkataba wa jumla ya Euro milioni 8, ambapo Euro milioni 6.5 zimetolewa na EU na Euro milioni 1.5 zimetolewa na Serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kusaidia Mfuko wa uendelezaji miradi ya Umeme Vijijini. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati, Dkt Juliana Pallangyo na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.

Naye mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Goodlove Stephen alisisitiza kuwa, Tanzania inao mkakati wa muda mrefu wenye lengo la kutosheleza mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu inayokua kwa kasi ili kuiondoa nchi katika umaskini. “Inakadiriwa kuwa, usambazaji wa umeme unatakiwa kuongezeka na kufikia megawati 10,000 ili kuendana na ukuaji wa uchumi unaotakiwa kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Msaada huu kutoka Umoja wa Ulaya utasaidia kuharakisha mipango husika, ikiwemo lengo la kuongeza uunganishaji umeme kufikia asilimia 75 ifikapo mwaka 2025.”

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, alibainisha kuwa Mpango-Mkakati wa miaka mitano wa REA (2016/17 – 2020/21) unalenga kuwezesha azma ya Serikali kuhakikisha vijiji 7,873 nchini, ambavyo havijapata umeme, vinapatiwa huduma hiyo kufikia mwaka 2021.

EVERTON YA UINGEREZA KUTUA NCHINI HIVI KARIBUNI

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Bw. Luca Neghesti kutoka SportPesa Tanzania leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Bw. Neghesti amefuatana na wawakilishi wa timu ya Mpira wa Miguu ya Everton ya nchini Uingereza kumpa taarifa Mhe. Waziri kuhusu maandalizi ya kuileta timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini Tanzania hivi karibuni. 
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa timu ya mpira ya Everton ya nchini Uingereza. Timu hiyo ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki. Mhe. Waziri alisema ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania. Anaozungumza nao kutoka kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu hiyo, Bw. David Harrison; Mkuu wa Ulinzi na Usalama (Head of Safety and Security) wa timu, Bw. Dave Lewis na Bw. Alan Chisholm kutoka Thomas Cook. 
Waziri Mahiga akifurahia zawadi ya jezi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu ya Everton, Bw. David Harrison. Jezi hiyo ni ya Mchezaji wa Timu hiyo ambaye pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ireland, Bw. Coleman. 
Picha ya pamoja. 



TANZANIA YATILIANA SAINI NA MFUKO WA MAENDELEO KIUCHUMI WA KUWAIT

0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Philip Mpango akisaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chahua hadi Chaya  kwa mkopo wa Dola Milioni 51 za kimarekani, katika shughuli iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dar es salaam leo.
 Naibu Mkurugenzi wa mfuko wa wa Kuwait , Hamad Al-Omar  akiabadilishana mkataba na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk .Philip Mpango.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Kuwait wakishuhudia tendo hilo la utiaji Sahii
 Viongozi wa ngazi za juukutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakishuhudia kitendo hicho cha utiaji Sahini.

Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images