Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1175 | 1176 | (Page 1177) | 1178 | 1179 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Trekta ambalo linafanya kazi ya kukarabari barabara ya Simu 2000
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua barabara ya simu 2000 ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielekeza jambo kuhusu ukarabati wa barabara hiyo, Wengine ni Meneja wa stendi ya Simu 2000 Bakari Shehoza na Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga
  MD Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo
  Barabara inayofanyiwa maerekebisho

  Moja ya Mzee ambaye ni mlemavu wa miguu akitoka Msalani katika eneo la Stendi ya mabasi Simu 2000 ambapo Uongozi wa eneo hilo umeagizwa kutowatoza fedha walemavu

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo (Machi 19, 2017) amezuru na kufanya ukaguzi wa barabara ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura.

  Barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya wananchi waendao Sinza, Mpaka Mwenge na Posta hadi Kariakoo sawia na Tegeta hadi Bagamoyo Pwani na Wengine kuelekea Ubungo hadi Morogoro ijulikanayo kama simu 2000 iliyopo katika Kata ya Sinza Manispaa ya Ubungo imeanza kutengamaa kwa gari kupita pasina wasiwasi zaidi ya ilivyokuwa awali.

  Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mkururugenzi huyo amesema kuwa Matengenezo hayo yanahusisha kuchonga barabara hiyo, kumwaga kifusi, kumwaga maji na kushindilia ili hata mvua zikinyesha isiathirike na kushindwa kupitika.

  "Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imetuamini na kutupa dhamana ya kumsaidia katika majukumu mbalimbali kwahiyo lazima tufanye kazi kwa bidii kwa kufatilia kwa karibu kazi zote tunazoziagiza kwa wakuu wa idara na watumishi wote katika Manispaa ili kuongeza na kukuza ufanisi katika maendeleo ya wananchi" Alisema Kayombo

  Kayombo aliongeza kuwa wapo baadhi ya watumishi ambao wanafanya kazi kwa mazoea lakini kwa Manispaa ya Ubungo kumekuwa na utumishi uliotukuka ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumpongeza msimamizi Mkuu wa Barabara hiyo sambamba barabara za Manispaa nzima Injinia Goodluck Mbanga kwa ufanisi wa utendaji kazi.

  Awali akitoa maelezo ya ukarabati wa barabara hiyo Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga alisema kuwa sasa barabara hiyo ipo katika hatua za mwisho za kukamilika ambapo amesema barabara hiyo inaanzia katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma na kuishia makutano ya barabaraba ya Shekilango.

  Injinia Mbanga amebainisha kuwa Matengenezo hayo ya kiwango cha kawaida ni kwa ajili ya muda mfupi huku Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa katika mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa muda mrefu (DMDP) kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake utaanza haraka Mara baada ya mkandarasi kupatikana.

  Sambamba na hayo pia MD Kayombo amemuagiza Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Mabasi cha simu 2000 kutowatoza malipo yoyote wananchi ambao ni walemavu wanaozuru kwenye maliwato iliyopo kituoni hapo.

  Naye Msimamizi mkuu wa Kituo cha Siku 2000 Ndg Bakari Shehoza amepongeza agizo hilo na kuahidi kulitekeleza kwa asilimia mia moja kwani limezingatia utu na uzalendo kwa wananchi wote ambao ni walemavu.

  0 0

    Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Mazungumzo hayo yalihusu zaidi kuhusu juhudi za kuongeza ushirikiano baina na CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhusiano wa kidundugu uliopo kwa siku nyingi baina ya vyama hivyo na uchumi. (Picha na Bashir Nkoromo).
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Mazungumzo hayo yalihusu zaidi kuhusu juhudi za kuongeza ushirikiano baina na CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhusiano wa kidundugu uliopo kwa siku nyingi baina ya vyama hivyo na uchumi. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
   Baadhi ya viongozi aliofuatana nao, Naibu Katibu Mkuu wa CCM wakifuatilia mazungumzo hayo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga 
   Balozi huyo wa China hapa nchini akimfafanulia jambo Mpogolo wakati wa mazungumzo hayo
    Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwa na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, baada ya mazungumzo yao jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
    Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, baada ya mazungumzo yao, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

  0 0


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akipeana Mkono na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akimuongoza  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim (kulia) kwenda katika eneo aliloandaliwa ili kufanya mazungumzo mafupi  baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt.Jim Yong Kim (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), na maafisa wengine wa Serikali walipo wasili katika moja ya Hotel jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


  Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, tarehe 19 hadi 21 Machi 2017.

  Dkt. Kim, akiwa mwenye furaha na bashasha, aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa tano kasorobo usiku na kulakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. DKT. Philip Mpango (Mb), pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo.

  Taarifa zilizipo zinaonesha kuwa akiwa hapa nchini, Dkt. Kim atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, tarehe 20 Machi 2017 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia utekelezaji wa miradi mikubwa inayo fadhiliwa na Benki hiyo pamoja na kushiriki uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara za Juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange).

  Baadae, Rais Magufuli na mgeni wake watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba mitatu: (i) Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa DART pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Ubungo (Dar es Salaam Urban Transport Project (DUTP); (ii) Awamu ya pili ya mradi wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya maji taka (Water and Sanitation Project) na (iii) Uboreshaji wa Miundombinu na Huduma za msingi katika baadhi ya miji (Tanzania Strategic Cities Project).

  Miongoni mwa miradi itakayo tembelewa na kiongozi huyo wa juu kabisa wa Benki ya Dunia Dkt. Kim, ni shule ya Msingi Zanaki ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi unaogharamiwa na Benki ya Dunia.

  Ziara ya Dkt. Kim imekuja majuma kadhaa baada ya Makamu wake wa Rais anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop alipofanya ziara yake mwezi Januari 2017 ambapo alishiriki uzinduzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi (BRT) uliofanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi hayo kilichopo Kariakoo jijini Dar Es Salaam.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Fedha na Mipango
  Dar es Salaam, 19 Machi, 2017.

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia nchi 21 Kanda ya Afrika Bw. Wilson Toninga Banda, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akipeana Mkono na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bi. Bella Bird, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi Bw. Andrew Bvumbe (katikati) wakifurahia jambo wakati  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim akisubiriwa kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  0 0

  Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa
  Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi waliohudhulia mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.


  Na Fredy Mgunda,Mufindi 

  Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya nyingime.

  “Ukienda mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara

  Aidha wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na nguzo.

  Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.

  "Tunawaomba TRA mkatoe elimu kwa mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa chini akuulizie nguzo 5 alafu awe na lisiti ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima hawa Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio kampuni" alisema Kenyatta

  Akijibu hoja hiyo meneja msaidizi WA TRA mkoa WA iringa Mustapha Mkilamwenye alisema Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka WA uelimishaji.

  Pia Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara hao kupata kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo check point.

  "Ombi lenu tumelipokea hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka TRA mkoa au wilayani kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia tutatoa elimu ya matumizi ya mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti yako kwa wafanyabiashara" alisema

  Kwa upande wake Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua kuwakutanisha wafanyabiashara na TRA kupata ufafanuzi WA kuombwa ushuru check point kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara hao Kuwa magari yako wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku tatu wakiombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.

  "Mkutano huku ni mahususi kwa wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini mnakamatwa check point na mkiobwa ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio adui kwa sababu mufindi ndio chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA mbao" alisema Chumi

  Meneja wa TRA wilayani ya Mufindi Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli tuhuma hizo na lawama tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za wafanyabiashara na kutatua matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge amekututanisha na tumewapa uelewa na sisi kama TRA tumewaambia mini cha kufanya kuondoa huo usumbufu"

  0 0


  0 0  Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanahabari kuzinduwa huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.[/caption] NMB imezindua rasmi huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS), kutoka katika akaunti za benki hiyo, kwenda kwenye akaunti za benki nyingine, sambamba na kufanya manunuzi na malipo. 

  NMB Mobile TISS, ni huduma ya kwanza kutolewa na benki nchini Tanzania, ambayo imetajwa kuwa ni njia rahisi, salama na ya haraka katika mchakato wa kutuma ama kuhamisha fedha kutoka NMB kwenda benki nyingine.

   Akizungumza katika hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa wanahabari, Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili alisema NMB Mobile TISS ni mwarobaini wa wateja wao kutumia muda mrefu kwenye foleni za kuhamisha ama kutembea na fedha mkononi. “Huduma hii inakuja kumaliza tatizo la wateja kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, tumekuja na huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo. Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili (mwenye suti ya bluu mbele) akizungumza na wanahabari kuzinduwa huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.

  Aliongeza ya kwamba, NMB Mobile TISS haiishii tu katika kuhamisha fedha kutoka akaunti ya NMB kwenda benki nyingine, bali inaenda mbali na kupokea ama kutuma miamala ya mitandao ya simu za mkononi. Huduma hiyo inayoweza kutumiwa na wateja wa NMB Mobile, inapatika na kwa mteja kubonyeza alama nyota, kishanamba 150, alama ya nyota, kisha namba 66 na mwisho alama ya reli na kufuata maelekezo (*150*66#).

  Naye Geofrey Mwijage, ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, lisema benki yake imejidhatiti vya kutosha katika kutanua huduma miongoni mwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla. Alisema NMB Mobile TISS inaenda kuwa mshirika sahihi wa Watanzania, katika kuharakisha maendeleo yao na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kuelekea Tanzania ya Viwanda.

  0 0


  0 0

   Mtaalamu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Ramadhani Nyambuka akisistiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma kwa mteja wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Machi 22 mwaka huu
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo
   Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga( Tanga Uwasa) Ruluani Luambo akisistiza jambo wakati wa semina hiyo
    Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo
   Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Joachim Kapembe akiuliza swali kwenye semina hiyo kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo

   Waandishi wa Habari Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbali mbali
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wiki ya kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 hadi Machi 22 mwaka huu kulia kwake ni Meneja Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka hiyo,Haika Ndalama
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linataraji kuwazawadia wanafunzi Saba waliofanya vizuri katika sanaa za maonyesho na uchoraji katika shule tano za sekondari nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa amesema kuwa wameamua kutoa zaidi tuzo ili kuongeza hamasa katika masomo ya Sanaa katika shule za Sekondari.

  “Tuzo hizi zitakuwa nyenzo kwa ajili ya kujenga hamasa, ari, ubunifu na juhudi katika kuleta maendeleo kupitia masomo ya sanaa. Katika program hii wanafunzi kutoka shule 5 za sekondari zitakazohusika katika kupewa tuzo hizo, shule hizi ni Loyola, Azania za Dar es Salaam, Bukoba ya Mkoa wa Kagera, Darajani toka Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha Sekondari toka mkoa wa Arusha.Amesema Shaluwa.

  Amesema ni matarajio ya BASATA kuwa utoaji wa tuzo hizi utachochea wanafunzi wengi kusoma masomo ya sanaa, kuongeza ubunifu katika kazi za Sanaa na kuwasaidia katika kuongeza ufaulu wao darasani hasa ikizingatiwa Sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.

  Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa Akizungumza na Waandishi wa Habri mapema leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari mkuu , Agnes Kimwanga.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya WFP na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. 
  FUKU 1
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford, wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Shirika lake na Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. 
  FUKU 2
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford, wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya WFP na Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Swaziland , Barnabas Sibusiso Dlamini katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye hoteli ya Westin mjini Port Louis, Mauritius, Machi 20, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  SWAZ2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa nchi za Afrika walioshiriki katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye Hoteli ya Westin mjini Port Louis nchini Mauritius Machi 20, 2017.(Picha na 0fisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala alipofika Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kujitambulisha leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao [Picha na Ikulu.] 20/03/2017.

  0 0


  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akinukuu hoja za wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko Mkoani Kagera kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkoa Machi 18, 2017 kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua.
  FV1
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kujadili na kupokea taarifa hiyo mkoani Kagera.
  FV 2
  Mkuu wa Wilaya ya Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo akichangia hoja wakati wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji ya Kukabili na Kurejesha hali baada ya athari za tetemeko mkoani Kagera.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
  ……………………….
  Na. Mwandishi Wetu

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kagera kwa hatua iliyofikiwa katika kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba10 mwaka 2016 katika Mkoa wa Kagera linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter.

  Mhe. Mhagama alionesha kuridhishwa kwake baada ya kufanya ziara  Mkoani hapo mapema wiki hii kwa lengo la kutathimini utekelezaji unaoendelea katika kurejesha miundombinu ili wananchi waendelee kutumia huduma hizo kama kawaida.

  Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama alitembelea Shule ya Sekondari Nyakato, Ihumo na Omumwani, Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi na Kituo cha Kulelea Wazee cha Kiilima na kubaini kuwa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kabyaile-Ishozi ambacho kimefikia asilimi 80 ambapo kimetumia kiasi cha shilingi 381, 506, 079.00.

  “Nikiri kwamba ukiacha baadhi ya mapungufu kwa watendaji wachache, wengi mmetupa ushirikiano mzuri kwa kulinganisha hali ilivyokuwa kwa kuangalia tukio lilivyotokea na hadi hatua za kukabili hatimaye kurejesha hali.”Alisema Waziri

  Aliendelea kushukuru ushirikiano mzuri uliopo katika kutekeleza majukumu hatimaye kufikia lengo “Kama sio ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkoa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania huwenda tusingefika hapa hivyo tuna kila sababu ya kupongeza juhudi hizi kwa niaba ya Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu tumefarijika kwa ushirikiano wenu”

  Pamoja na pongezi hizo, Waziri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Kamishna Diwani Athuman kuendelea kuzingatia taratibu za manunuzi na kila eneo linalofanyiwa kazi kufuata taratibu, kanunuzi zilizopo kwani kwa atakaye kiuka sheria na taratibu hakutakuwa na msamaha.”Hakutakuwa na msamaha kwa yeyote atakayefanya uzembe lazima sheria zichukue mkondo wake hakuna kuoneana aibu” Alisisitiza waziri.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Deogratius Kinawilo alipongeza kwa kukiri kuwa kazi inayoendelea ya kurejesha hali imefanyika kwa umakini mkubwa. “Tumefanya kazi kwa umakini mkubwa na kila mmoja alikaa kwenye nafasi yake hivyo niendelee kuwaomba watendaji wote kufuata sheria na kutekeleza yote yanayotupasa ili kuokoa mazingira ya wanakagera kwa ujumla”

  Waziri mhagama alieleza pia pamoja na jitihada zote ifike mahali kile kilichokusudiwa kitimie na miradi yote ifikapo mwezi Mei mwaka huu imekamilika” Tuendelee kutekeleza majukumu yetu katika zoezi la kurejesha hali ili ifikapo mwezi Mei angalau asilimia 80 iwe imekamiliza” Alisema waziri

  Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Januari mwaka huu na kuiagiza  Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya tathimini za shughuli zote wakati wa kukabili na urejesha hali baada ya kutokea kwa Tetemeko hilo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuzindua mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa makutano ya barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwapungia wananchi mkono wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi  wa ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiwa ndani ya moja ya basi la DART wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiagana na wananchi wa Kivukoni hawapo pichani kabla ya kupanda Basi la Mwendokasi (DART) kuelekea Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mradi wa Makutano ya barabara za juu za Ubungo jijini Dar es Salaam. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-Maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ndani ya basi la Mwendokasi wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya Wananchi wakifatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam-PICHA NA IKULU

  0 0  0 0  Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akizungumza katika uzinduzi wa programu ya kuboresha miundombinu ya usalama wa Barabarani kwa shule za msingi iliyoanzishwa na  Shirika la Amend kwa kushirikiana naTaasisi za Puma Energy na Fia. Mpango huo uliozinduliwa katika shule ya msingi Mpakani, Manzese Tip Top  umeanzishwa kwa lengo la kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi kupata ajali za barabarani. 
   Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program ya ujenzi na uboreshaji wa mindombinu ya usalama wa barabarani kwa shule za msingi. Corsaletti alianisha kuwa usalama barabarani ni ajenda namba moja kwa kampuni yao na mpaka sasa wamekwisha toa  mafunzo ya aina hayo kwa wanafunzi 39,000 kutoka shule 33 mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Geita.
   Mkurugenzi wa Mpango hu wa Shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana akizungumza katika hafla hiyo.
   Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akikata utepe kuzindua mpango wa kuwalinda wanafunzi wa shule za msingi kupatwa na ajali za Barabarani ulionzishwa na Shirika la Amend kwa msaada wa taasisi ya Puma Energy na Taasisi ya Fia kwenye shule ya msingi Mpakani ya Manzese Tip Top. Wengine katika picha ni Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (wa tano kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Amend, Ayikai Poswayo (wa kwanza kulia) na Diwani Kassim Lema ( wa kwanza kushoto).
   Washiriki katika uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye eneo ambalo limetengenezwa rasmi kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mpakani kuvuka wakati wa kwenda na kutoka shuleni.
   Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi, Thabitha  Makaranga akizungumza katika hafla hiyo. Makaranga aliwamwakilisha Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpiga.
  Wakufunzi wa masuala ya usalama barabarani kutoka shirika la Amend na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpakani iliyopo Manzese Tip Top  wakionyesha kwa mfano njia sahihi ya kuvuka barabara.  Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zitakazofaidika na mpango wa kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi kupata ajali za barabarani ulioanzishwa na shirika la kimataifa la Amend kwa msaada mkubwa wa taasisi ya FIA Foundation na Puma Energy Foundation. 

  Mpango huo ulizinduliwa juzi kwenye shule ya msingi mpakani iliyopo Manzese Tip Top ambao lengo kubwa ni kujenga miundombinu itakyosaidia wanafunzi kuepuka ajali za barabarani waendapo, wakati wa kuvuka na kurejea kutoka shuleni.

  Nchi nyingine ni Benin, Botswana, Ivory Coaste, Ghana, Malawi, Mozambique, Namibia, Senegal na Zambia.

  Mkurugenzi wa mpango huo kutoka shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana alisema kuwa takwimu si nzuri kwa Tanzania kuhusiana na ajali za barabarani ambapo inakadiliwa kuwa jumla ya watu 16,000 upoteza maisha kutokana na ajali hizo kila mwaka.

  Poswayo alisema kuwa kutokana na taasisi yao kujishughulisha na masuala ya usalama wa barabarani katika bara la Afrika, waliamua kuzindua mpango huo hapa nchini kwa lengo la kuwalinda wanafunzi na watu wengine wanaotumia barabara wakati wa shughuli zao za kila siku.

  Alifafanua kuwa mpango huo utahusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambayo itatumiwa na watembea kwa miguu, waendesha pikipiki, baiskeli na magari kuepuka ajali hizo ambazo nyingi zimeleta madhara kwa watu na wenginekubakia na ulemavu kama si kupoteza maisha.

  “Huu ni mradi wa miaka miwili ambao malengo yake makubwa ni kuwakinga wanafunzi kwenye ajali za barabarani, takwimu siyo nzuri kwa Tanzania, hivyo tumeamua kuanzia hapa na baadaye unzinduzi kama huu kufanyika nchi nyingine, tutajenga miundombinu amayo itawafanya madereva wa vyombo vya moto kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa wastani, mradi huu utafanyika kwenye shule zote zilizopo karibu na barabara,” alisema Poswayo.

  Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti alisema kuwa wanawajibika katika mpango huo kwani ni sehemu ya shughuli zao za kijamii.

  Corsaletti alisema kuwa usalama barabarani ni ajenda namba moja kwao na mpaka sasa wameweza kutoa mafunzo ya aina hayo kwa wanafunzi 39,000 kutoka shule 33 mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Geita.

  Corsaletti alisema kuwa wanafunzi wengi wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha au kupata ulemavu kutokana na ajali ambazo zinatokana na uendeshaji mbaya wa madereva au kukosekana kwa miundombinu ambayo sahihi kuwawezesha wanafunzi kuona kabla ya kuvuka barabara.

  Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo aliipongeza Shirika la Amend, Puma Energy na Taasisi ya Fia kwa kuanzisha mpango huo ili kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi.

  Injinia Chambo alisema kuwa takwimu za mwaka 2015 za ajali ya barabarani zinaonyesha kuwa zinaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 78 walipoteza maisha kwa mkoa wa Dar es Salaam kutokana na ajali za barabarani. Pia jumla ya watu wanafunzi 182 walijeruhiwa.

  “Hali si nzuri, napongeza juhudi za wadau zinazolenga kupunguza ajali za barabarani, kuna makampuni mengi ambayo hayajihuishi na shughuli kama hizi, naziomba ziunge mkono sasa ili kuboresha miundombinu na kuepusha maisha ya wanafunzi,” alisema Chambo.

  Alisema kuwa serikali inaiunga mkono juhudi za Puma Energy, taasisi ya Fia na Amend na ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuondoa tatizo hili.

  Mwisho…

  0 0


older | 1 | .... | 1175 | 1176 | (Page 1177) | 1178 | 1179 | .... | 1896 | newer