Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46328 articles
Browse latest View live

MD KAYOMBO AWAONYA MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUTOPOKEA RUSHWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa
Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
MD Kayombo akisisitiza jambo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Maafisa Watendaji wa Kata 14, Watendaji wa Mitaa 91 pamoja na Wahasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameonywa kutopokea Rushwa wala hongo ya aina yoyote kutoka kwa wamiliki wa biashara mbalimbali katika Manispaa hiyo kwani kufanya hivyo watadhoofisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kama ilivyokusudiwa.

Kauli ya onyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato na kutoa maelekezo ya majukumu ya kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo Jumamosi Machi 18, 2017 katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa hiyo ilipo Mtaa wa Kibamba CCM.

Kayombo ameeleza kuwa kwa mtumishi yoyote wa Manispaa kwa ngazi yoyote atakayebainika kujihusisha na ubadhilifu kwa kuchukua Rushwa kwa walipa kodi atachukuliwa hatua Kali za kisheria kwa kuiibia serikali kwani kuihujumu serikali kwa kuiibia mapato au kuzuia ukusanyaji wa mapato ni kosa kwa mujibu wa taratibu na sheria.

“Nina amini kwamba mnaishi vizuri na wananchi wenu kwahiyo mnawafahamu vizuri wafanyabiashara wanaokwepa kulipa Kodi lakini hata walipaji wazuri hivyo jambo la ukusanyaji mapato litakuwa jepesi sana kwenu kutokana na uzoefu mlionao” Aliongeza Kayombo

Mkurugenzi huyo amewasisitiza Watendaji hao kusimamia vyanzo vyote vya mapato ikiwemo Hotel Levy, Service Levy, Mabango makubwa na madogo (Bill Board), Leseni za biashara na Vileo, Upimaji afya kwa ngazi za Mitaa hususani katika Migahawa.

Hata hivyo amewataka Watendaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano, Uaminifu, na Weledi mkubwa kwani kufanya hivyo kutasababisha ukusanyaji mkubwa wa Mapato kwa mwaka 2016/2017.

Kayombo Amewataka Watendaji wote kukagua Maduka yote katika maeneo yao ya kazi ili kubaini Maduka yasiyokuwa na leseni na Yale yenye leseni kuwa na Leseni za Manispaa ya Ubungo kwani wafanyabiashara wa Maduka mengi wamekuwa na kisingizio cha kukata leseni na Kodi mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni na kutaka kulazimisha kuitumia leseni hiyo kama halali kwa Manispaa ya Ubungo.

Sambamba na hayo pia MD Kayombo amewataka Maafisa biashara kutochelewesha leseni za wafanyabishara waliokamilisha taratibu zote za kumiliki leseni kwani kufanya hivyo ni kuchelewesha huduma kwa wananchi na kuongeza makwazo kwa wafanyabishara kwa sababu tu ya kuchelewa kusaini leseni.

Alisema kuwa litakuwa ni jambo la aibu na lisilovumiliwa kwa kuruhusu sheria zitungwe kwa umakini mkubwa lakini utekelezaji wake uwe hafifu.

MD Kayombo aliongeza kwa kusema kuwa hakuna Haki bila wajibu hivyo Watendaji hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea lakini pia kutofanya kazi kwa kuongozwa na tamaa.

MD Kayombo amesema kuwa Oparesheni hiyo ya itakayodumu kwa miezi mitatu ya ukusanyaji wa mapato itaanza jumatatu Machi 20, 2017 kwa ushirikiano baina ya watendaji kutoka Makao makuu ya Wilaya, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mitaa na wenyeviti wa serikali za Mitaa.

Waziri Ummy atoa rai kwa madaktari kuomba nafasi za kazi Nchini Kenya

$
0
0

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto imebainisha kuwa inatarajia kuwapeleka Madaktari wake waliopo nchini Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya kufuatia kuombwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenyatta.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo, Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa, ujumbe maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta kupitia kwa Wiziri wake wa Afya uliokutana na Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na kuomba ombi lao hilo la kutaka madaktari 500, ambao wataajiliwa kwa mikataba maalum ya kuanzia miaka 2 kwa kufanya kazi nchini Kenya.

“Natoa rai kwa madaktari wazawa waliopo nchini kuomba nafasi za ajira ya Udaktari nchini Kenya kwa mkataba maalum. Zoezi hilo limeanza rasmi leo Machi 18 mpaka Machi 27, mwaka huu wawe wameomba.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa waombaji ni wale watakaokidhi vigezo maalum ikiwemo asiwe katika utumishi wa Umma, Asiwe amejiliwa na mashirika ya umma ama mashirika teule ambayo yanalipiwa na Serikali.

Kwa Mujibu wa Waziri Ummy ameeleza kuwa muombaji lazima awe amehitimu mafunzo ya “internalship” na mwisho awe amesajiliwa na baraza la Madaktari nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameweka wazi kuwa, ajira hiyo itakuwa ni ya miaka miwili ambapo watapata mishahara na malupulupu mbalimbali katika ajira zao hizo huku akibainisha kuwa, jambo hilo ni jema na linaiingizia Taifa sifa kwa kupeleka wataalamu wake nje ya nchi kupata ajira.

Kwa upande Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa, moja ya vigezo ambavyo vinahitajika kwa madaktari hao ni pamoja na kuwa na digrii ya kwanza na Internal ship huku akiongeza kuwa, kwa upande wao Wizara imejipanga kuimalisha madaktari wa ndani ikiwemo kiwaajili.

Naye Katibu Mkuu Utumishi, Mh. Laulian Ndumbalo amewatoa hofu watanzania licha ya kuwapeleka Madaktari hao nje kupatiwa ajira, nchini bado ina Madaktari wengi wanaofikia zaidi ya 1000, huku kila mwaka wakiajili Madaktari 400 hadi 450.

Imeelezwa kuwa Madaktari hao watakaojitokeza watapata faida kubwa kwani watakuza mahusiano mema ya nchi za Afrika Mashariki kupitia kada hiyo huku pia wakitarajia kuipatia maendeleo nchi ya Tanzania. Jambo ili ndio la kwanza linafanyika huku ikielezwa kuwa idadi hiyo ya madaktari kutoka Tanzania kwenda kupatiwa ajira nje ya mipaka yake ni kubwa, licha ya madaktari wengi kuwepo nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Botswana na mataifa mengine.

Madaktari hao wenye kutaka kujiunga wanaweza kutembelea tovuti ya wizara ya Afya na kupata maelezo mbalimbali.

WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Matiku Makori kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuzitafutia utatuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  jijini Dar es Salaam jana walisema utaratibu anaoufanya mkuu huyo wa wilaya unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwani unakwenda na kasi ya kazi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu.

"Binafsi nampongeza mkuu wetu wa wilaya kwa kazi hiyo anayoifanya ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake na kuzitafutia utatuzi ni jambo zuri na hasa anapokuwa na wasaidizi wake, wanasheria na Katibu Tawala " alisema Fabiola Sumary mkazi wa Mbezi kwa Yusuph.

Sumary alisema anapowashirikisha wenzake hasa wataalamu wake wakati wa kusikiliza kero hizo inasaidia kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja bila ya kupoteza muda mwingi.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la mama Mshindo alisema mpango huo umesaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza msongamano ofisi ya mkuu wa mkoa ambako wananchi wengi walikuwa wakikimbilia kupeleka malalamiko yao.

Mkazi mwingine Francis Malota alisema mkuu huyo wa wilaya bila ya kujali jua, mvua  na kula amekuwa akiwasikiliza wananchi wake zaidi ya 70 kila siku jambo linaloonyesha jinsi anavyowajali.

"Tangu asubuhi hadi saa moja usiku amekuwa akisikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake tunamuombea kwa mungu amzidishie hekima hiyo" alisema Caroline Mwangoka mkazi wa Mbezi kwa Mangi.

Mkuu huyo wa wilaya kila wiki amejiwekea utaratibu wa kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake ikiwemo migogoro ya ardhi, jamii na ndoa.

DIAMOND AULA UBALOZI WA BIDHAA ZA GSM

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul (Diamond Platnum) amekuwa Balozi wa Bidhaa za GSM na kuwataka watanzania wanunue bidhaa hizo kuacha kutumia gharama kwa kufuata nje ya nchi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Diamond amesema kuwa licha ya kuwa balozi katika bidhaa za GSM ameweza yeye kununua kutokana vitu mbalimbali katika maduka hayo.

Amesema kuwa GSM walikuwa na uwezo wa kutafuta wasanii wa nje ya nchi lakini wakaona kuna umuhimu wa kuwatumia wasaani wa ndania kama mabalozi katika bidhaa zao. 
 
"Hivyo katika hilo na kuchangia maendeleo kwa wasanii wetu wa hapa nyumbani,wanaojituma na kuonesha mafanikio yao makubwa kwa kile wanachokifanya,sisi kama GSM tumeamua kutimia msanii Diamond Plutnum kuwa Balozi wa bidhaa zetu" alisema

Aidha amesema kuwa ubalozi huo utafanya kutangaza muziki wake kwa mashabiki wa ndani na wan je ya nch. Diamond amesema kuwa balozi hakuadhiri ubalozi mwingine kutokana kuwa kinachotangazwa ni bidhaa ambazo haziingiliani. 

 Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum) akizungumza na waandishi habari baada ya kukabidhiwa ubalozi wa bidhaa za GSM leo jiiini Dar es Salaam.
 Afisa Masoko wa GSM, Lauma Mohammed  akizungumza na waandishi wa habari juu ya Diamond kuwa Balozi wa Bidhaa za GSM leo jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari wakimsikilizwa Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum)  hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam. 

UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MAJESHI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya SMZ katika Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 1i kwa mwaka 2017 (BAMATA) yaliyofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo.
Maaskari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Maaskari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakiangalia ratiba Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 (BAMATA) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo (kushoto) katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo (kulia) Waziri wa Ulinzi Majeshi ya Kujenga Taifa Mhe,Dkt.Hussein Mwinyi. 
Kikosi cha Maaskari Kanda ya JKT wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na kutoa heshima wakati ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo. 
Maaskari wakiimba wimbo maalum wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo.
Kikosi cha Maaskari Jeshi la Wananchi JWTZ Kanda ya Ngome wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na kutoa heshima wakati ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,Mkoa wa Mjini Magharibi, [Picha na Ikulu] 18 /03/2017.

DKT SHEIN AFANYA UTEUZI.

$
0
0
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 17 cha sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia namba 6 ya mwaka 2016, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Bwana Omar Zubeir Ismail kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Omar Zubeir Ismail alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar.

Uteuzi huo uliosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, umeanza leo tarehe 18 Machi 2017.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO-ZANZINAR

18 Machi 2017

WANAWAKE WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma kupitia chama tawala CCM JACKLINE MSONGOZI, amewataka wanawake mkoani humo kuwa mstari wa mbele katika kupambana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi ili kulinda mazingira.

Meya wa jiji achangia Mabati, mifuko ya cement 100 ujenzi wa darasa shule ya Maweni.

$
0
0
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema). Meya wa Jiji la Dar,Isaya Mwita akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika shule ya msingi ya Maweni iliyopo Kata ya Mji Mwema wilayani Kigamboni.Anayeshuhudia kuli ni Mkuu wa Shule hiyo,Zuhura Mwaliko na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo,Kabega Ally. Uongozi wa Shule ya Msingi Maweni ukimtembeza mgeni rasmi kuangalia maeneo ya shule hiyo na changamoto zake. Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akimuongoza Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita kuzungukia majengo ya shule hiyo kujionea changamoto zake akishirikiana na Mkuu wa shule hiyo,Zuhura Mwaliko.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam akiangalia dampo linalotumiwa na shule hiyo kutupia na kuchomea moto uchafu jinsi lilivyo.
Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akimuonyesha Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (katikati) eneo ambalo limewekwa kwa ajili ya kujengwa madarasa endapo fedha zitapatikana
Mkuu wa Shule ya Maweni,Zuhura Mwaliko akieleza jambo kwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita. Mojawapo la darasa ambalo halijakamilika katika shule hiyo Wakinamama waliojitokeza katika mkutano huo wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa madarasa ya shule ya maweni.

Wakinababa waliojitokeza katika mkutano huo wa harambee
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maweni wakiimba wimbo wa shule hiyo kabla ya mkutano kuanza.

Wanafunzi walioshiriki katika mkutano huo. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko akizungumza katika mkutano huo. Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo,Kabega Ally akizungumza katika mkutano huo..

 
Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akizungumza katika mkutano huo wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa shule hiyo. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maweni,Denis Edifonce akisoma risala iliyobeba ujumbe wa changamoto iliyonayo shule hiyo mbele ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Zuhura Mwaliko. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche akizungumza katika mkutano huo. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche akimtunza mwanafunzi aliyekuwa akicheza nyimbo za asili katika mkutano huo. Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche. Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akimpatia hela kijana Denis Edifonce aliyesoma risala iliyoandaliwa na shule hiyo ambayo ilikuwa na ujumbe mzito uliomgusa meya huyo. Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche. Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwitaakisisitiza jambo kwa viongozi walioko meza kuu kuhusu maendeleo ya kata ya Mji Mwema. Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mkutano huo. Walimu na wazazi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mkutano huo.
Mkazi wa Mtaa wa Maweni,Rehema Kitunda akizungumza kwa niaba ya wakinana mama wenzake na kuchangia ujenzi huo.
Mkazi wa Mtaa wa Maweni,Daudi Mwasambile akizungumza kwa niaba ya wakinana mama wenzake na kuchangia ujenzi huo.
Burudani za ngoma za asili zikiendelea katika mkutano huo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwapongeza vijana wa ngoma za asili walionesha uwezo wao na kuwapa moyo wa kuzidi kujituma kutokana na vipaji walivyoonesha na kuwapa nafasi ya kufika ofisini kwake ili azungumze nao aone jinsi gani anaweza kuwasaidia ili wafike katika malengo yao waliyoyakusudia katika tasnia ya sanaa ya muziki.
 

NA CHRISTINA MWAGALA, Dar

MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Simenti pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni.

Shule hiyo ambayo inaupungufu mkubwa wa madarasa pamoja na uzio wa shule , inajumla ya wanafunzi 1300 ikiwemo na wale wenye ulemavu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya chagizo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Meya Isaya alisema kwamba hatua hiyo ni kwa jili ya kuzisaidia shule ambazo zinaupugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.

Alisema kwamba wakati alipokuwa akiwania nafasi ya Udiwani Kwenye kata yake ya Vijibweni , na kisha kupata nafasi ya kuwa Meya wa jiji, moja ya vipaumbele vyake ilikuwa ni kuzisaidia shule ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa.

“ Niseme tu kwamba jiji hili ambalo linarasilimali nyingi halafu wanafunzi wanakaa chini, sio jambo zuri, lazima watu ambao tumechaguliwa na wananchi ambao ndio wenye watoto wanasoma hapa, tutimize majukumu yetu” alisema Meya Isaya.

“ Kama kwenye Kata yako unaona kabisa wanafunzi wanakaa chini na wewe diwani upo, basi ujue huna sifa ya kuwa diwani na wananchi watakuwa na haki ya kukuondoa madarakani kwenye uchaguzi ujao.

Alifafanua kwamba” jambo la uchagiaji wa kusaidia wanafunzi wasikae chini sio la kisiasa bali ni katika sehemu ya kuwasaidia wananchi hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana ya kisiasa.

“ Hapa leo hii tukijenga madarasa kila motto anasoma akiwa amekaa kwenye madarasa mazuri, madawati ya kutosha, lakini watoto hao sio wa chadema, sio wa CCM wala CUF bali ni wananchi wote, nawaombeni sana kwenye suala la elimu tusilihusihwe na mambo ya siasa” alisema Meya Isaya.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Celestine Maufi pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo.

Hata hivyo Diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 ,madawati 60 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa .

Hata hivyo awali akisoma lisara kwa mgeni rasmi iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo, Mwalimu Selemani alisema kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.

Alifafanua kwamba kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wananfunzi wenye ulemavu wamelazimika kusomea kwenye chumba cha darasa kimoja jambo ambalo linawapa shida walimu kwenye ufundishaji.

MV KAZI YASHUSHWA MAJINI

$
0
0
 Kivuko cha MV KAZI kikielea majini baada ya kushushwa kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi. Kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
 Muonekano wa kivuko kipya cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
 Kivuko cha MV KAZI kikisubiri kushushwa kwa mara ya kwanza majini kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
 Kivuko cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
Mkurugenzi wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mwenye kofia akiwa kwenye kivuko cha MV KAZI mara baada ya kukishusha majini kwa mara ya kwanza tayari kwa ukaguzi wa mwisho. Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni.
PICHA ZOTE NA LAFRED MGWENO (TEMESA)

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.



VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 19,2017

USIKU WA MISS PENDO KISAKA NA MWANAHABARI GEORGE BINAGI WAFANA.

$
0
0
Jana ijumaa March 17,2017 kuamkia leo jumamosi, ilikuwa ni siku muhimu kwa Malikia wa nguvu, Pendo Kisaka, ambapo ndugu, jamaa na marafiki zake walijumuika naye kwenye Sendoff yake kuelekea kwenye ndoa anayotarajiwa kufunga na mwanahabari/ mwanablogu, George Binagi, March 26,2017 Jijini Mwanza.

Shughuli ilifanyika katika ukumbi wa Heinken, Mbagala Kijichi Jijini Dar es salaam. Ni mwendeleo wa kuelekea kwenye ndoa takatifu ya wawili hao iliyotangazwa March 12,2017 kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
BMG
Bibi harusi mtarajiwa akimvisha saa mmewe mtarajiwa
Bibi harusi mtarajiwa (kulia) na best lady wake (kushoto)
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake na kusema ahsante kwa malezi yenu bora
Bibi harusi mtarajiwa, Pendo Kisaka (katikati), akimtambulisha mmewe mtarajiwa, George Binagi (kushoto)

TANZANITE ONE WATOA MILIONI 20 KWA SACCOS YA MADALALI WANAWAKE WA MADINI ARUSHA

$
0
0

Madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo la mererani pekee duniani yakiwa tayari yamekatwa na kusanifiwa sasa yatauzwa kimataifa katika kituo kitakachonjengwa Arusha
Mtaalamu wa kukata madini Adam Idd Lacha akiwa anakata na kusanifu madini ya Tanzanite ya kampuni ya Tanzanite one ambayo ndio inatoa mafunzo hayo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa anapewa maelezo juu ya madini ya Tanzanite , na wakurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Juma na Hussein Gonga. Alipokuwa katika kituo cha kuuza madini cha kampuni hiyo.
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sky Associate Group, Faisal Juma Shahbhai akizungumza na madali wanawake wa madini
Muonekano wa Mgodi wa kisasa wa uchimbaji madini wa tanzanite One Mererani kwa nje .PICHA ZOTE NA MUSSA JUMA



ANDREA NGOBOLE, PMT


Kampuni ya Tanzanite One, imetoa msaada wa Sh 20 milioni kwa chama cha Madalali wanawake,wanaouza madini ya Tanzanite mkoani Arusha .

Wakurugenzi wa kampuni hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO), Faisal Shabhai na Hussein Gonga walitangaza uamuzi huo wakati wakizungumza na madalali , katika ukumbi wa polisi jijini hapa.

Faisal alisema kampuni yao ambayo inachimba Tanzanite, imetoa msaada wa sh 20 milioni,ili kuendelea kutekeleza mahusiano mema na wadau wa Tanzanite na jamii ya wanawake ambao wanajihusisha na biashara ya kuuza madini hayo.

Alisema msaada huo, umetokana na maombi ya wanawake hao, kusaidiwa waliyotoa katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na viongozi wa Tanzanite One.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetenga kiasi cha sh 200 milioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya kisasa Mererani.

Gonga alisema kwa sasa tayari wametoa matofali 65,000 ambayo yapo eneo ambalo itajengwa hospitali hiyo ili kuondoa matatizo ya ukosefu huduma za afya katika mji wa Mererani.

Awali Mwenyekiti wa chama hicho, Eugen Augustine alisema madalali wa madini wanawake mkoani Arusha, wanakabiliwa na tatizo la mtaji mdogo na hivyo kushindwa kunufaika na biashara yao.

Alisema kutokana na tatizo hilo, ndio sababu waliomba msaada kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha na Tanzanite One ili wasaidiwe.

Katika hatua nyingine, Kampuni hiyo, imetoa msaada wa mahindi magunia 250 kwa wananchi wakazi wa kata ya Naisinyai ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo kwa jamii inayozunguka migodi yake.

Faisal alisema msaada huo, utasaidia makundi maalum katika jamii na ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kushauri kampuni hiyo, iongeze misaada kwa jamii inayowazunguka.

Kampuni ya Tanzanite One inamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO).

LIVE: GWAJIMA AKITOA MAJIBU YA MWANAMKE ALIYEDAI KUZAA NAYE

MAKADA WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA UBUNGE, BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, Dkt. Egina Makwabe, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Leonce Nicholaus Mulenda, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Zainab Kawawa, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, jana. Katikati ni dada zake Mariam Kawawa na Zamaradi Kawawa.  Picha na Mafoto Blog
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, anayetetea nafasi yake, Charles Makongoro Nyerere, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Dkt. Evance Mujuni Rweikiza, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Shedrack Mana Mashauri, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Aliyewahi kuwa Miss Tanzania wa mwaka 1998, Kada wa CCM, Basila Kalabha Mwanukuzi akiongozana na mtoto wake, Patrick Nubi, wakitoka Ofisi ndogo za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam, kuchukua Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Bunge la Afrika Mashariki. Baadhi ya Makada wa CCM jana walijitokeza katika Ofisi hizo kuchukua Fomu baada ya kutangazwa kuanza kutolewa fomu hizo. 
 Wagombea wakipishana kuingia kuchukua fomu kwenye Ofisi hizo Lumumba jijini Dar leo.
 Baadhi ya Vijana waliojitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo wakiwa katika foleni ya kuiingia kuchukua fomu.
 Badhi ya Makada wakiwa katika foleni kusubiri kuingia kuchukua fomu.
Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM,Moses Bahati Ole-Neselle.
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM,Grace Emmanuel Sameji.
Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM,Nicholaus George Ngassa.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MAURITIUS KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiogozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo wakati alipopokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).

 Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo. Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.

 Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017. 

 Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo. Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.

Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Mhe Philip Marmo Amvisha Cheo Kanali wa JWTZ jijini Berlin

$
0
0
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo na  Acting Colonel Joseph Bakari wakisikiliza maelezo kabla ya hatua ya kumvua cheo cha zamani na kumvika kipya
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha kofia ya cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akipikea zawadi maalumu ya  Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM)  toka kwa Kanali Joseph Bakari wakati wa hafla hiyo
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akiwa na  Kanali Joseph Bakari na mkewe 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kushoto)  Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri (wa pili kulia) Colonel Joseph Bakari na mkewe 
 Tukio hilo la kuvisha Cheo  lilihitimishwa na kuimbwa wimbo wa Taifa wa Tanzania.
 Picha ya pamoja na ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine ilifanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani. Source: Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Berlin Ujerumani



Katika hali ambayo haijazoeleka na iliyoonekana kuwa ngeni, Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo alimvisha Cheo Kanali Joseph Bakari aliyepandishwa Cheo hivi karibuni kutoka Luteni kanali.
Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na  ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine ilifanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu tukio hilo  Mhe. Balozi alitanabaisha kuwa kwake ni tukio la kwanza na la la aina yake kupewa dhamana hiyo  na kwamba amepokea maelekezo husika kutoka Makao Makuu ya Jeshi kupitia Wizarani. 
Akisoma sehemu ya maelekezo hayo alisema “ kwa kawaida Afisa anapopanda cheo akiwa nje ya nchi iwapo hataweza kwenda Tanzania kuvalishwa cheo hicho na viongozi husika wa JWTZ, cheo hicho kipya huvishwa na Afisa Mkuu au Balozi wa Tanzania katika Nchi aliyepo”. 
Hivyo, kwa mujibu wa sheria na mamlaka aliyekuwa nayo anatakiwa kumvisha Cheo kipya cha ukanali mhusika kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Kwa mujibu wa maelekezo hayo Kanali Bakari alipandishwa cheo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kuanzia tarehe 31 Januari 2017.
Akitoa nasaha fupi na salam za pongezi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, wageni waliohudhuria hafla hiyo na Watanzania wote kwa ujumla kwa  Kanali Bakari aliyefuatana na Mkewe Bi Lucy Mlingi, Mhe. Balozi alimkumbusha Kanali Bakari kuwa ni dhahiri kuwa kupandishwa kwake cheo kumetokana na imani ya Mkuu wa Majeshi na viongozi wengine wakuu katika utendaji wake,uadilifu, bidii katika kazi na utii. Hivyo ni vizuri ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa weledi,  bidii zaidi na moyo wa kujituma ili kuleta tija na ufanisi zaidi kwa manufaa ya JWTZ, Tanzania na Dunia kwa ujumla. Mwisho aliipongeza familia yake hususani  Mkewe kwa mafanikio hayo na kuwatakia   heri, Baraka na afya njema.
Kanali Joseph Bakari ni mwakilishi wa JWTZ katika Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM) kama Mshauri na msaidizi wa Mkurugenzi wa Michezo katika Baraza hilo.
Baraza hilo liliundwa tarehe 18 Februari 1948 mara baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Dhima kuu ikiwa ni kutumia shughuli za michezo na utimamu wa mwili kama njia ya kueneza amani duniani badala ya vita. Baraza hilo lina jumla ya nchi wanachama 134 Tanzania ikiwemo. Miongoni mwa shughuli  za Baraza hilo ni kuandaa mashindano ya michezo ya majeshi ya Dunia.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 kwa mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 kwa mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein bwakiagana baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 PICHA NA IKULU.

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI JIMBONI KWAKE,AKABIDHI BAISKELI KWA MLEMAVU

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akiendeseha baiskeli hiyo kabla ya kumkabidhi mkazi wa Makorora Mbwana Hamisi leo kwa ajili ya matumizi yake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa Makorora Jijini Tanga leo wakati wa Hafla ya Makabidhiano hayoMbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa miguu Mbwana Hamisi Mkazi wa Makorora Jijini Tanga ili iweza kumsaidia kutembea kwenye shughuli zake ambapo baiskeli hiyo ina thamani ya zaidi ya milioni moja.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande aliyevaa kanzu akimshukuru Mbunge huyo aliyesimama kulia akisalimia na mama mzazi wa Mlemavu huyo Mariam John
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akisalimiana na Mama Mzazi wa Mlemavu wa Miguu Mariam John mara baada ya kumkabidhi mwanae baiskeli ya kutembelea

Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Makorora Kata ya Makorora Jijini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku wa pili kushoto akimsikiliza mkazi wa Makorora Jijini Tanga mara baada ya kumalziika zoezi la kukabidhi Baiskeli

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MAULID YA KUMSALIA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) YAFANA SEGEREA MWISHO, DAR ES SALAAM

$
0
0
Siku ya jumamosi ya 11 Machi 2017 katika viwanja vya Madrasat Rahman iliyopo Segerea Mwisho jijini Dar-es-salaam palikuwa hapatoshi kwa mkusanyiko wa waumini wa dini ya Kiislam waliokusanyika katika shughuli ya kisomo cha Maulid ya kumsalia mtume Muhammad (S.A.W). Shughuli hiyo ya Maulid ilifana sana kwa kuhudhuriwa na wingi wa waumini , wanazuoni na viongozi mbali mbali wa dini hiyo.
Unaweza kujumuika nao katika at Rahman Madrasa Segerea





Viewing all 46328 articles
Browse latest View live




Latest Images