Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

MKAZI WA KIJIJI CHA ISENGULE MKOANI KATAVI FATUMA ISSA (22) AJIFUNGUA WATOTO WANNE

$
0
0

Watoto wanne walizaliwa  na  mwanamke   aitwaye  Fatuma  Issa  22   Mkazi wa   Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema   mwambao  mwa  Ziwa   Tanganyika  Wilaya  ya  Tanganyika  Mkoa wa  Katavi wakiwa katika   chumba  maalumu  katika   Hospitali ya  Manispaa ya  Mpanda.
Huyu  ndiye  mwanamke   aitwaye   Fatuma  Issa  22  Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule   Tarafa ya  Karema   Wilaya  ya   Tanganyika    Mkoa wa  Katavi   akiwa   katika  chumba  maalumu  katika  Hospitali ya  Manispaa ya   Mpanda     baada ya kujifungua  watoto wanne kwa wakati mmoja  ambapo alijifungua  watoto hao  hapo machi 12  katika   Hospitali  hiyo  kati ya watoto hao mmoja ni wakike na watatu ni wakiume.

Mkuu  wa  Wilaya ya   Mpanda  Lilian  Matinga  akiwa  katika wodi ya  wazazi    katika   Hositali ya  Manispaa ya  Mpanda   aliwajulia  hali watoto wanne   mapacha  waliozaliwa hapo  Machi  12  mwaka huu kwa  wakati mmoja  na  mwanamke  aitwaye   Fatuma  issa  22   Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema  Wilaya ya  Tanganyika   Mkoa wa   Katavi
Picha  Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog


  Na  Walter  Mguluchuma .
    Katavi yetu Blog

MKAZI wa kijiji cha Isengule , mwambao mwa Ziwa Tanganyika  katikawilaya ya Tanganyika  mkoani Katavi , Fatuma Issa (22) amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya  Manispaa ya Mpanda mwishoni mwa wiki.

 
Muuguzi  Mkuu wa Hospitali hiyo , Alexanda Kasagula alisema mama huyo alijifungua watoto hao wanne mwishoni mwa wiki  kwa  njia ya kawaida ambapo mama na watoto wake hao  wote wakiwa na afya njema.

 
“Mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike alizaliwa akiwa  na uzito wa kilo moja na gramu 800 ,mtoto wa  pili alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 500 , watatu alizaliwa akiwa na uzito wa  kilo moja na gramu 800 huku wanne alizaliwa akiwa na kilo  moja na gramu 700.

 
Kati ya watoto hao watatu ni wakiume  hali ya mzazi na watoto wake wote  wanaendelea vizuri  bado wamelazwa  katika  wodi ya wazazi hospitalini hapa “ alieleza .
Kwa upande wake , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jafar Kitambwa alieeleza kuwa  mama huyo na watoto wake wataendelea  kuwa chini ya ungalizi hospitalini hapo  hadi hapo watakaporuhusiwa rasmi kwenda nyumbani
 
Mama huyo alieleza kuwa yeye na mume aitwae Agustino Andrew (25) kama wanando huo utakuwa uzao wao wa tatu ambapo wana idadi ya watoto watano .
 
“ Mie na mume wangu  sasa tuna idadi ya watoto  watano  uzazi wangu wa kwanza  nilizaa mtoto  mmoja ambaye yuko hai.Hii itakuwa mara yangu ya pili  kujifungua  watoto zaidi ya mmoja  katika uzao wangu wa pili   nilijifungua mapacha  lakini mmoja wao alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa na pacha mwenzake  alikufa  miezi mitatu  baada ya
kuzaliwa.

 
Nimejifungua watoto  wanne  lakini tangu nijifungue sijapata tatizo lolote la  kiafya  naendelea vizuri mie na watoto  wangu wote nawashukuru  wauguzi ambao wamenisaidia  hadi nimejiufungua salama bila ya matatizo yeyote yale “ alieleza
Alieleza kuwa  mama yake mzazi ndie anayemwangalia hospitalini hapo huku akimsadia kuwalea watoto hao .




MKURUGENZI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI INAYOFADHILIWA NA UMOJA HUO MKOANI KAGERA

$
0
0
 Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu mara baada ya kuwasili ofisini kwake.
Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na  utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii.
Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) aliwasili Mkoani Kagera Machi 13, 2017 na ujumbe wake ili kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Miradi aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa,  mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani (318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.
Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.
“Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada mkubwa. Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule  za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez.
Pai Bw. Rodriguez alisema kuwa mara baada ya kujionea hali halisi ya shule hiyo ataendelea kushawishi wafadhili mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo yenye mahitaji maalum inapewa kipaumbele katika ufadhili. Vilevile aliiomba jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu kwani ulemavu hauna ukabila, utaifa wala rangi ambapo alisema kuwa hata yeye watoto wake ni walemavu jambo ambalo alisema ulemavu hauna mzungu wala mweusi.
Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
Ukaguzi wa  Miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa
Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
Aidha, Umoja wa mataifa kupitia Shirika lake la (UNICEF) ulitoa ufadhili wa kujenga majiko sanifu katika jamii kwaajili ya kutunza mazingira kwa wananchi wa hali ya chini kwa kutumia nishati ya kuni kidogo. Pia kupitia shirika la (IOM) wananchi na kaya masikini waliokumbwa na Tetemeko  la Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama  ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba na Missenyi.
Katika Hatua nyingine Bw. Rodriguez alikagua mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa wa kufunga umeme wa jua katika Zahanati ya Bushasha Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Shule ya St. Mary Rubya Seminari Wilayani Muleba. Katika Shule ya Rubya Seminari ufungaji wa umeme wa jua uligharimu Dola za Kimarekani (50,000 USD) hadi kukamilika.

Baadhi ya watoto wa Shule ya Mugeza Mseto ilioyopo Bukoba Mkoani Kagera.
Akitoa maelezo ya Mradi huo Padre Malianus Rutagwerela ambaye ndiye Mkuu wa Seminari hiyo alisema kuwa mradi huo umeongeza nguvu ya mwanga katika shule hiyo na kuwa na umeme wa uhakika ikiwa ni pamoja na umeme wa TANESCO. Aidha aliushukuru umoja wa Mataifa kwa niaba ya uongozi wa Jimbo Katoliki la Bukoba kuwa mradi huo utaboresha zaidi elimu katika Seminari hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkazi Bw. Rodriguez alifurahishwa sana na mradi huo ambao alishuhudia ukifanya kazi vizuri. “ Nimefurahishwa na mradi huu pia sisi kama Umoja wa Mataifa tutaendelea kuona jinsi ya kusaidia shule kama hizi ili Mapadre na Viongozi wa dini waendelee kuzalishwa katika shule kama hizi ili wasaidie kueneza neno la Mungu kuhusu upendo na kuondoa chuki kati ya Wanadamu. 

Alieleza Bw. RodriguezMwisho, Bw. Rodriguez alisema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ambayo ipo chini ya Mashirika ya Umoja wa Maifa ambayo imetolewa ufadhili wa fedha na Umoja huo na kutekelezwa au inaendelea kutekelezwa Mkoani Kagera. Aidha,  alihaidi kuendelea kuushawishi Umoja huo na wafahili mbalimbali ili waendelee kuuangalia na kuufadhili Mkoa wa Kagera katika miradi mbalimbali ya maendeleao na Kijamii.
 Pichani kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu .
StoriNa: Sylvester Raphael
Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na  utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii.
Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) aliwasili Mkoani Kagera Machi 13, 2017 na ujumbe wake ili kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Miradi aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa,  mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani (318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.
Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.
“Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada mkubwa. Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule  za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez
Pai Bw. Rodriguez alisema kuwa mara baada ya kujionea hali halisi ya shule hiyo ataendelea kushawishi wafadhili mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo yenye mahitaji maalum inapewa kipaumbele katika ufadhili. Vilevile aliiomba jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu kwani ulemavu hauna ukabila, utaifa wala rangi ambapo alisema kuwa hata yeye watoto wake ni walemavu jambo ambalo alisema ulemavu hauna mzungu wala mweusi.
Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
Aidha, Umoja wa mataifa kupitia Shirika lake la (UNICEF) ulitoa ufadhili wa kujenga majiko sanifu katika jamii kwaajili ya kutunza mazingira kwa wananchi wa hali ya chini kwa kutumia nishati ya kuni kidogo. Pia kupitia shirika la (IOM) wananchi na kaya masikini waliokumbwa na Tetemeko  la Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama  ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba na Missenyi.
Katika Hatua nyingine Bw. Rodriguez alikagua mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa wa kufunga umeme wa jua katika Zahanati ya Bushasha Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Shule ya St. Mary Rubya Seminari Wilayani Muleba. Katika Shule ya Rubya Seminari ufungaji wa umeme wa jua uligharimu Dola za Kimarekani (50,000 USD) hadi kukamilika.
Akitoa maelezo ya Mradi huo Padre Malianus Rutagwerela ambaye ndiye Mkuu wa Seminari hiyo alisema kuwa mradi huo umeongeza nguvu ya mwanga katika shule hiyo na kuwa na umeme wa uhakika ikiwa ni pamoja na umeme wa TANESCO. Aidha aliushukuru umoja wa Mataifa kwa niaba ya uongozi wa Jimbo Katoliki la Bukoba kuwa mradi huo utaboresha zaidi elimu katika Seminari hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkazi Bw. Rodriguez alifurahishwa sana na mradi huo ambao alishuhudia ukifanya kazi vizuri. “ Nimefurahishwa na mradi huu pia sisi kama Umoja wa Mataifa tutaendelea kuona jinsi ya kusaidia shule kama hizi ili Mapadre na Viongozi wa dini waendelee kuzalishwa katika shule kama hizi ili wasaidie kueneza neno la Mungu kuhusu upendo na kuondoa chuki kati ya Wanadamu. 

Alieleza Bw. Rodriguez Mwisho, Bw. Rodriguez alisema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ambayo ipo chini ya Mashirika ya Umoja wa Maifa ambayo imetolewa ufadhili wa fedha na Umoja huo na kutekelezwa au inaendelea kutekelezwa Mkoani Kagera. Aidha,  alihaidi kuendelea kuushawishi Umoja huo na wafahili mbalimbali ili waendelee kuuangalia na kuufadhili Mkoa wa Kagera katika miradi mbalimbali ya maendeleao na Kijamii.
Credit ;Bukobawadaumedi

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mjane wa Marehemu Sir George Kahma, Mama Janeth Kahama akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akiweka udongo katika kaburi
Marais Wastaafu na wake zao pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika makaburi ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Sir George Kahama katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya ndugu wa familia Marehemu Sir George Kahama wakiwa mazishini katika makaburi ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya ndugu wa familia Marehemu Sir George Kahama wakiwa katika makaburi ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya Marehemu Sir George Kahama wakiwa katika makaburi ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi na wake zake Mama Sitti Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Sir Georeg Kahama
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua kaburini
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe mama Evelyne Warioba wakiweka shada la maua kaburini
Mawaziri Nape Nnaue ya Mwigulu Nchemba wakiweka shada la maua kaburini
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua katika kaburi
Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman akiweka shada ya maua kaburini
Waziri wa Mambo ya Nje Mstafu Mhe. Bernad Membe akiweka shada la maua kaburini
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Mstaafu Rashid Othman akiweka shada la maua kaburini
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiweka shada la maua kaburini

Mhe. Andrew Chenge na mkwewe wakiweka shada la maua kaburini
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga akiweka shada la maua kaburini
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa mazishini katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuele Massaka wa Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU AVUNJA BODI YA WETCU NA TTB,AAGIZA VIONGOZI WA WETCU WAKAMATWE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.

Baadhi ya wadau wa zao la tumbaku wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara (katikati) na Makamu wake, Msafiri Ngassa wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamis Issah (kulia) kuelekea kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto) wakiwa kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama hicho utakapokamilika.

Pia Waziri Mkuu amevunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania – TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo jioni (Alhamisi Machi 16, 2017) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.

Viongozi wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

“Kuanzia sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.

Amesema “Hatuwezi kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,”.

“Wakati wanachama ambao ni wakulima wakiendelea kutesema WETCU walinunua gari la sh. milioni 269 kinyume na na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau ambao ulipitisha zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.

Amesema WETCU kimekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano suala la ukarabati wa ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa ikarabatiwe kwa sh. milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za Tabora na Urambo zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na hazikukarabatiwa.

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wkatiikiwa inazalishwa hap nchini. Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya kwa dola katika sekta ya tumbaku na badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho kimekuwa kiwanyonya wakulima.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, wakuu wa wilaya zote za mkoa huo pamoja na Maofisa Kilimo na Ushirika kuhakikisha wanasimamia vizuri zao hili ili liweze kuwa na tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo waende vijijini na kuwatambua wakulima wa tumbaku katika kila kijiji na kuwasajili. “ Kuanzia leo Maofisa Ushirika wabadilishe mienendo ya kazi nataka wasimamie zao la tumbaku kwa umakini zaidi.”

MAPITIO YA MKATABA KATI YA TBC NA STRATIMES KUMALIZIKA MWEZI APRIL:WAZIRI NAPE.

$
0
0

 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(aliyesimama) akizungumza na Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii pamoja na Uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mhe. Peter Serukamaba (Mb) ilipotembelea Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba(Mb) (aliyesimama)akitoa maelezo mafupi kuhusu dhumuni la ziara ya kamati hiyo katika Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) katika kikao kazi wakati kamati hiyo ilipotembelea TBC leo Jijini Dar es Salaam .Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
Mkurugenzi wa Shirika la la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Ryioba(aliyesimama) akieleza utendaji kazi wa Shirika kwa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii wakati kamati hiyo ilipotembelea TBC leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu.

MAREHEMU SIR. GEORGE KAHAMA AAGWA NA KUZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa salamu za pole katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu wa Rais mstaafu katika Serikali ya awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mjane wa Marehemu Sir. George Clement Kahama Mama Janet Kahamawa (pili kushoto) akiwa na familia yake wakati wa Tukio la kumuaga mume wake ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu za pole kutoka Serikalini katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdurahaman Kinana akitoa salamu za rambirambi za Chama wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Serikali imesema itaendelea kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania maendeleo na ustawi wa jamii uliofanywa na marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa Taifa na Waziri msataafu marehemu Sir Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na aliyetekeleza majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa viongozi walioanzisha harakati za Serikali za uendelezaji wa mji wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha makao makuu ya nchi.

“Marehemu Sir George Kahama tutamuenzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya katika kuijenga nchi yetu hasa katika ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa nchi”.Alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdurahaman Kinana amumueleza Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa hali ya juu na alikuwa mchapakazi.

“Sir George Kahama alikuwa mtumishi na kiongozi aliyetukuka ametuachia hamasa kubwa ya kuwa viongozi bora zaidi na wenye mapenzi na Taifa letu katika kuleta maendeleo.”Alisema Ndugu Kinana.

Marehemu Sir George Kahama amekuwa Waziri na Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa leo Jijini Dar es Salaam na ameacha Mjane na Watoto.

MAAFISA HABARI WATOA MISAADA YENYE THAMANI YA SHILINDI MILIONI 12 SHULE YA WASIOONA BUIGIRI

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 17,2017


KIKOSI 841KJ MAFINGA KIMESHEREKEA MIAKA 50 TOKA KUANZISHWA KWAKE KWA KUJENGA KIWANDA CHA NAFAKA

$
0
0
Mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa Uhodari. 
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj
Baadhi ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
Hili ndio jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga nafaka za kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga.



Na Fredy Mgunda,Mafinga

Kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.

Akizungumza kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.

Nkya alisema kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili kukuza ajira na pato la taifa.

“Hapa kikosini tunalima na kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango kinachotakiwa kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja ya kuanzishwa kwa kikosi hicho”.alisema Nkya

Captain Nkya alisema Sasa hivi Jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa kikosi cha Kisasa nachenye wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu vingi vyenye faida ya kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii.

“Tumefungua kiwanda ni lazima sasa kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja kuipunguzia serikali gharama za kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga ukiangalia tunaeneo kubwa na tunanguvu kazi hivyo ni lazima tulime na kufuga kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli anataka jeshi la kujenga taifa lirudi kujitegemea”.alisema Nkya

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 kwa kuwa kudumu huko kwa kikosi hicho ni hatua kubwa sana katika ujenzi wa taifa.

Chale alikitaka kikosi cha 841kj kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea kuzalisha chakula kwa wingi kama zamani kwa saizi kikosi hicho kin alima eneo dogo sana kitu kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa kikihudumia kikosi hicho.

“Nimetembea eneo kubwa sana leo lakini nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana hivyo mnahitaji kuongeza uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha chakula kwa wingi nyie mna nguvu kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia ipasavyo”.alisema Chale

Aidha Chale alikipongeza kikosi hicho cha 841kj mafinga kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa kiwanda ambacho kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa za chakula na kukuza uchumi wa nchi kutokana na uzalishaji wake.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga kiwanda hapo ndio mnakuwa mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga kwa kukuza uzalishaji kwa kutumia raslimali watu ambao mnao katika kiosi kuzalisha na sio kila siku mnakuwa mnategemea msaada kutoka serikalini”alisma Chale

Chale alikitaka kikosi kuendelea kutunza nidhamu waliyonayo na kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na viwanda.

Naye Bwana shamba wakikosi (farm manager) luteni Francis Breek wa kikosi cha 841kj alisema kuwa wamejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuwa wana eneo kubwa na wana wataalamu wengi wanaoweza kukidhi mahitaji ya kukuza uzalishaji.

“Ukiangalia mwaka huu tumelima eneo kubwa na tumeongeza idadi ya mifugo hivyo tunatarajia kuongeza tena idadi ya mifugo na kupanua eneo la kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa tumejenga kiwanda na kiwanda kinahitaji uzalishaji mkubwa wa nafaka pamoja na ufugaji mkubwa na wenye tija”alisema Breek

Lakini pia kikosi hicho cha 841kj Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari ambalo linaonesha kila kitu kinachofanywa na kilichofanywa na kikosi hichotoka kuanzishwa kwake.

“Hongera kikosi cha 841kj kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”

GRACA MACHEL AZINDUA MPANGO WA KUWAINUA WANAWAKE AFRIKA

$
0
0
Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel amesema mapinduzi yanayotakiwa kufanyika hapa nchini kwa sasa ni ya kuwainua wanawake kiuchumi, kiafya na kijamii.
Mama Machel, ambaye ni mke wa Hayati Nelson Mandela amesema hayo leo Ijumaa wakati wa mkutano na wanahabari alipozindua mpango wa kuwainua wanawake Afrika."Mapinduzi ya kwanza yalifanikiwa wakati ule tunatafuta uhuru lakini,"amesema.
Mama Machel amesema wanawake hawana budi kushika usukani katika kuhakikisha wanafanikiwa kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo.
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Tanzania Women Chambers, Anjelina Maleko amesema kama wanawake wamebarikiwa kwa jambo moja hawana budi kuwa baraka kwa wenzao.
Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu changamoto wanazozipata wanawake kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwainua wanawake Afrika uliofanyika katika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri akiongea akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini mama Graca Machel alivyomsaidia kufikia malengo hasa kwenye suala la elimu.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Jacqueline Mneney Maleko akizungumzia mafanikio yake pamoja na njia wanazoweza kuzitumia wanawake ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa  mpango wa kuwainua wanawake Afrika na Tanzania ikiwa nchi ya kwanza.
Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri(kushoto) 
Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na mmoja waadishi wa habari mara baada ya kufanyika uzinduzi wa uzinduzi wa  mpango wa kuwainua wanawake Afrika.

RAIS AAGIZA WAFUGAJI WALIOWASHAMBULIA WANANCHI KWA VIBOKO WAKAMATWE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.

Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.
Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.

Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.

“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi...Wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Machi, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akielezea changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Maggid Mwanga baada ya kuongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiongea nao katika kijiji cha  Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017. PICHA NA IKULU

RIDHIWANI:NASHUKURU KWA KUHOJIWA NA MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA JAMII SASA IMEJUA UKWELI WA JAMBO HILO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya nchini.
Mbunge huyo amezungumza hayo  jijini Dar es salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.
"nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya roho yangu imesuuzika "alisema Ridhiwani
Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.
Msikilize hapa:

ANAISHI KWA KULA MAFUTA YA KULA LITA MOJA, SUKARI ROBO TATU NA MAZIWA LITA MBILI KWA SIKU.

$
0
0
SHUKURU KISONGA ni mtoto wa 5 kuzaliwa katika familia ya marehemu KISONGA yenye watoto 5, ni wanafunzi wa kidato chapili shule ya Sekondari MGOMBA iliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Amezaliwa mwaka 2001 , akiwa na mwaka mmoja tangu azaliwe shukuru anakubwa na ugonjwa ambao hadi sasa haujafahamika ni aina gani ya ugonjwa unaomsumbua , Tangu akubwe na ugonjwa huo mwaka 2002 hadi leo hii amekuwa akila vyakula ambavyo vinawashangaza watu.

Kwa undani wa habari hii bonyeza play. Na kwa yule atakayeguswa na tatizo hili la motto huyu anaweza kuwasiliana na mama yake mazazi kwa namba ya simu 0742 322 408 ili aweze kupata matibabu.

MAFUNZO YA UJASILIAMALI YAFUNGWA RASMI MKOA WA MBEYA

$
0
0
Mhandisi Cosmas Kinasa akizungumza machache wakati akifunga rasmi semina ya ujasiriamali ya "Manjano Dream-Makers" kwa wanawake wa mkoa wa Mbeya akimwakilisha meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya. Mafunzo ya ujasiriamali hayo yametokewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali, vipodozi na urembo kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya  wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana naMhandisi Cosmas Kisana Akizungumza Machache Wakati akifunga Rasmi Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Mbeya Kwa Niaba ya Meneja wa Sido Mkoa wa Mbeya.Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 30 kutoka Mkoa wa Mbeya  Yamemalizika. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya  ni Miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara Kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya  wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo kama hayo yatafanyika pia kwenye mikoa ya Mtwara,Tabora na Kigoma mwaka huu wa 2017.
Washiriki walionufaika kwenye mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mhandisi Cosmas Kinasa. 
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru Mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

KWA CCM NI CHUKI NA VISASI… LAKINI WAPINZANI WAKITIMUANA “WANAFUKUZA WAASI, WASALITI!”

$
0
0

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini
JUMAMOSI ya Machi 11, 2017 Chama cha Mapinduzi (CCM) ‘kiliondoa woga’ na kufanya jambo ambalo halikutarajiwa na wengi nchini baada ya kuwatimua baadhi ya wanachama na kuwavua uongozi wengini huku baadhi yao wakisimamishwa na wengine wakionywa, MaendeleoVijijiniinaripoti.
Waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba ambaye amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti Maalum na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa.
Wenyeviti wa mikoa waliofukuzwa ni Ramadhan Rashid Madabida (Dar es Salaam), Christopher Sanya (Mara), Erasto Izengo Kwirasa (Shinyanga), na Jesca Msambatavangu (Iringa).
Wenyeviti wa CCM Wilaya waliofukuzwa ni Salum Kondo Madenge (Kinondoni), Assa Harun Simba (Ilala), Makoi S Laizer (Longido), Wilfred Saileli Ole Mollel (Arusha Mjini), Omary Awadh (Gairo), (Muleba), Ally S. Msuya (Babati Mjini), na Mwenyekiti wa Wilaya ya Bunda.
Wajumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM waliofukuzwa ni Ali Khera Sumaye (NEC Arumeru), na Mathias Erasto Manga (Arumeru).
Mjumbe wa NEC, Adam Kimbisa, kutoka Dodoma Mjini amesamehewa wakati Dk. Emmanuel Nchimbi amepewa onyo kali, ambapo hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.
Wengine waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye pia ameondolewa madarakani, Hamis J. Nguli (Mwenyeviti wa Wilaya ya Singida Mjini) ambaye ameachishwa uongozi, Hassan Mzala (M-NEC Singida), Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma, Josephine Genzabuke, Ali Mchumo (M-NEC Kilwa), Chief Ally Kalolo (M-NEC Tunduru) ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali, Muhaji Bishako (Mwenyeviti wa Wilaya ya Muleba) amepewa onyo kali, na Valerian Alemreta (M-NEC- Kibaha Vijini) ambaye ameachishwa uongozi.
Katika hatua ya kushangaza sana, wapinzani wa CCM wameiona hatua hiyo ya kukisafisha Chama kama ni namna ya kukomoana, visasi na chuki na wengi ndio wamekuwa wasemaji wa wanaCCM huku wakigeuka kuwa watabiri wa ‘kifo cha CCM’.
Wapinzani siyo tu kwamba wanafurahia kwa CCM ‘kujimaliza yenyewe’, lakini tayari wamekwishawafungulia milango wanachama hao waende kujiunga na vyama vyao.
Vyombo mbalimbali vya habari – magazeti, runinga na radio – vimekuwa vikiendesha mijadala mbalimbali kuzungumzia hatua hiyo ya CCM na karibu waandishi na wachambuzi wengi wanasema CCM imefanya makosa.
Mitandao ya kijamii hiyo ndiyo usiseme, kwani imejaa ‘waandishi na wachambuzi’ wengi wanaoendelea kuikosoa CCM kana kwamba jambo lililofanyika ni geni.
Ajabu ni kwamba, wapinzani hao wanaolalamikia mambo yasiyowahusu wanashindwa kuelewa kwamba hata wao wenyewe wamekuwa wakifukuza, tena wengine bila hata kufuata vikao halali wala katiba zao, lakini katu hawasemi.
Wapinzania wanasema uamuzi wa CCM kuwatimua na kuwaadhibu wanachama ambao wamekwenda kinyume na Katiba ya Chama ni wa chuki na visasi, lakini kumbe wao wakifukuzana “wanasafisha vyama vyao kwa kuwaondoa wasaliti”.
Tatizo la wapinzani wa Tanzania ni moja: wanapenda sana kutumia fursa (Opportunists) hata mahali pasipostahili. Tena ni wasahaulifu na hawataki kukumbushwa.
Potelea mbali, mimi nitawakumbusha, na nitawakumbusha kwa mifano ili hata hao wafuasi wao waweze kuelewa, hata kama hawataamini. Potelea mbali!

Migogoro CUF
Mpaka sasa Chama cha Wananchi (CUF) kinaendelea na migogoro na agenda kuu inayozunguka ni ‘kutimuana’. Wapinzani hawalioni hilo bali wanaliona la CCM.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Haruna Ibrahim Nguyulu Lipumba, ametangaza hivi karibuni kuwatimua wakurugenzi mbalimbali, wengine wamevuliwa madaraka yao.
Hivi sasa mkakati wao ni kumtimua Katibu Mkuu, ‘kisiki’ Maalim Seif Sharrif Hamad, na inaelezwa kwamba wako tayari kutumia hata nguvu ya polisi kumng’oa.
Lakini haya yanafanyika baada tu ya Profesa Lipumba kurejea madarakani kwa nguvu ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya kiongozi huyo kutimuliwa tangu mwaka 2016 alipotaka kurejea kwenye uongozi baada ya kuwa amejiuzulu mwenyewe mwaka 2015. Hakuna anayesema kuhusu timua timua hiyo ya CUF, bali wanaiona ya CCM tu.
Ni CUF hao hao ambao mwaka 2012 waliwatimua akina Hamad Rashid Mohammed na wenzake, kutokana na mgogoro uliokuwepo kabla ya mbunge huyo wa zamani wa Wawi, Pemba hajaenda kuanzisha chama chake.
Lakini naukumbuka mkutano wa mwaka 1994 kule Raskazone, Tanga, ambapo CUF walimtimua mmoja wa waasisi wake, mzee wangu James Mapalala, katika mkakati uliokuwa umewekwa na baadhi ya viongozi wa juu kuhakikisha ‘Mkristo hawi mwenyekiti’.
Ndiyo maana mwaka 1995 wakaamua kumchukua msomi Profesa Lipumba, ambaye awali alikuwa ‘amedakwa’ na Chama cha NRA, lakini akakitosa. CUF wakampa nafasi ya kugombea urais.
Leo hii hakuna anayethubutu kukumbuka hayo ya CUF isipokuwa wanaishambulia CCM kwamba inafanya kwa chuki na visasi!

NCCR-Mageuzi na TLP
Hakuna asiyefahamu kwamba NCCR-Mageuzi ndicho kilichokuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania Bara tangu mwaka 1995. Nguvu kubwa ambayo chama hicho kiliipata ni baada ya ‘kumsajili’ Augustine Lyatonga Mrema muda mfupi baada ya kuondoka CCM Februari 1995.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wa wakti ule, Mabere Nyaucho Marando, aliamua kumkaribisha na akampisha hadi kwenye kiti chake kabla ya kumpatia nafasi ya kuwa mgombea urais.
Kutokana na mvuto mkubwa aliokuwa nao Mrema wakati huo, aliweza kuleta ushindani mkubwa kwenye uchaguzi huo mkuu wa kwanza wa vyama vingi na akashika nafasi ya pili nyuma ya Benjamin Mkapa wa CCM.
Lakini mgogoro ukaanza mwaka 1996, tena baada ya Mrema kupata ubunge wa Temeke katika uchaguzi mdogo kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Ramadhan Kihiyo wa CCM, kuvuliwa na mahakama.
Mgogoro huo ukashika kasi hadi walipokwenda Tanga mwaka 1997, ambapo mkutano wao uliingia dosari baada ya taa kuzimwa usiku na ‘waasi’ wa NCCR-Mageuzi wakaanza kurusha viti kumshambulia Mrema ambaye alikuwa anataka kukifanya chama mali yake, kwa mujibu wa taarifa zao.
Mrema amshukuru sana kaka yangu Kagenzi, aliyekuwa mlinzi wake, ambaye mara taa zilipozimwa, akitumia mbinu za hali ya juu, aliweza kumwingiza Mrema chini ya meza halafu yeye akaanza kupangua viti ambavyo vilikuwa vikirushwa kuelekea meza kuu kwa lengo la ‘kumpopoa Mrema’. Baadaye aliweza kumtoa nje na hivyo kumnusuru na zahama hiyo.
Tangu wakati huo Mrema akaapa kuwatimua waasi. 

Na kweli aliwatimua wote, akiwemo Marando ambaye ndiye aliyemkaribisha, pamoja na wanachama wengine kama Dk. Masumbuko Lamwai na wengineo.
Mgogoro ulivyozidi kupamba moto wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, Mrema akaondoka – kwa ‘kutimuliwa na wanachama’ – pamoja na akina Msafiri Mtemelwa.
Leo Herman Lwekamwa, aliyekuwa mwenyekiti na mwanzilishi wa Chama cha Labour (TLP), akamkaribisha Mrema na wenzake, akiwemo Thomas Ngawaiya.
Lwekamwa akamkabidhi uenyekiti, yeye akawa mwanachama wa kawaida. Mrema akashika nafasi ya tatu mwaka huo nyuma ya Ben Mkapa na Profesa Lipumba. Ngawaiya akawapata TLP ofisi pale kwenye mjengo wake Manzese-Argentina.
Lakini ghafla mambo yakabadilika. Mgogoro ukatokea, na Mrema akaamua kuwatimua wanachama wengi ‘wakorofi’ akiwemo Leo Lwekamwa aliyemkaribisha.
Tangu wakati huo hajabanduka madarakani na hana dalili za kuondoka leo, kesho au mtondogoo. 
David Kafulila, mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa wa kujenga ushawishi naye wakati akiwa kiongozi na mbunge ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi alikutana na dhoruba hiyo baada ya kufukuzwa kabla ya kusamehewa na kurejeshewa uanachama wake. Hivi sasa ameelekea tena Chadema ambako awali walimletea figisu!
Hakuna anayesema isipokuwa tu CCM ni watu wa chuki na visasi!

Chadema
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambacho kwa sasa ndicho kikuu cha upinzani nchini, ndicho kinachoongoza kejeli hizi za CCM kuwatimua wanachama wake.
Wafuasi wa Chadema, ambao wanashinda na kukesha kwenye mitandao, wengi wakiwa ni vijana ‘wasiojitambua wala kuelewa siasa ni nini isipokuwa tu kuongozwa na mihemko’, wanaendelea kujaza kurasa za mitandao kwa hoja muflisi kwamba CCM imejimbia kaburi kwa kuwatimua wanachama wake.
Hakuna hata mmoja miongoni mwao anayekumbuka namna Chadema ilivyowatimua akina David Kafulila na wenzake mwaka 2009 kwa madai kwamba walikuwa wafuasi wa Zitto Kabwe ambaye wakati huo alikuwa ameanzisha kampeni ya kutaka kuwania nafasi ya uenyekiti.
Hakuna hata mmoja ambaye anakumbuka kwamba mwaka 2008 Chadema walimsimamisha u-makamu mwenyekiti Chacha Zakayo Wangwe (R.I.P.), aliyekuwa mbunge wa Tarime, kwa sababu tu alihoji kuhusu masuala nyeti yaliyomgusa moja kwa moja Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, yakiwemo ya upendeleo, ukabila, ukanda pamoja na mapato ya chama na madeni ambayo Mbowe alidai alikuwa anakidai chama.
Hata wakati mauti yanampata Wangwe alikuwa safarini kutoka Dodoma kuja kujitetea kwenye Kamati Kuu. Hakuna ajuaye nini ambacho kingetokea kama ajali ile isingetokea.
Wafuasi wa Chadema, ambao siku hizi wamebatizwa jina la ‘nyumbu’, hawataki kuzungumzia lolote kuhusiana na kutimuliwa kwa akina Mtera Mwampamba na Juliana Shonza na wenzao, ambao waliwatuhumu kwamba walikuwa wakiunda Kundi la PM7 – Pindua Mbowe lililokuwa likiundwa na vijana ama wanachama 7.
Kilichowaponza pia ni ‘ukaribu’ wao na Zitto Kabwe, ambaye aliendelea kuonekana kama mwiba mkali kwa Chadema na walikuwa wakimtafutia nafasi kama mchezo wa ‘kuotea’ (Offside-Trick).
Na hatimaye walimpata Zitto na school-mate wangu Profesa Kitila Mkumbo mwaka 2013 baada ya kusema waliudaka waraka uliokuwa umelenga kufanya mapinduzi ndani ya chama.
Zitto na Profesa Kitila wakatimuliwa pamoja na ‘wafuasi’ wao na Chadema hao hao wakasema ‘wanasafisha chama kwa kuondoa waasi’.
Sasa iweje leo hii CCM, ambayo wapinzani hao hao wamekuwa wakisema inawaleta wanachama ‘waovu’, inapoamua kujisafisha hawa wapinzani waseme ni ‘chuki na visasi’? Ina maana ni wao tu wapinzani wanaoweza kujisafisha?

Wengi waliondoka CCM
Waliotimuliwa hivi karibuni si wa  kwanza kuondoka ndani ya CCM. Utamaduni huo umekuwepo kitambo tangu enzi za uenyekiti wa Mwalimu Julius Kambarage Burito Nyerere.
Tena ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kuwafukuza, kuwasimamisha, kuwavua madaraka wanachama ama viongozi wake, si hapa Tanzania pekee, bali hata katika mataifa mengine.
Miaka ya nyuma kabisa enzi za Tanganyika African National Union (Tanu), walifukuzwa akina Fortunatus Masha, Balozi Christopher Kasanga Tumbo, Oscar Saratiel Kambona, James Mapalala na wengine wengi, baada ya kupishana na Mwalimu Nyerere kutokana na kwenda kinyume na misingi ya chama.
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1985, akina Maalim Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid Mohamed, Juma Duni Haji walifukuzwa ndani ya CCM baada ya kudaiwa kuufitini uchaguzi wa mwaka huo.
Walikuwa wakipinga ama hawakuridhika na uamuzi wa CCM kumpitisha Idris Abdul Wakil Nombe kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Matokeo yake, kwa kuwa ilikuwa enzi ya chama kimoja, wakafungiwa kujihusisha na siasa. Wangekwenda wapi kufanya siasa wakati CCM pekee ndiyo ilikuwa imeshika hatamu?
Ujio wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 ndio uliowatoa kifungoni na moja kwa moja wakaingia upinzani kwa kuanzisha vyama vyao.
Kama ilivyo kwa wapinzani ambao daima huangalia kasoro za serikali ama kuanzisha choko choko, vivyo hivyo wapo baadhi ya wanachama wakorofi, wasiojua itifaki, wasiojua falsafa na itikadi za vyama, ambao kazi yao ni vurugu, kutukana na hawaheshimu hata viongozi wao.
Wapo watu ndani ya vyama, kwao busara na maslahi ya chama si kitu, jambo litafanyika kwenye vikao vya ndani, yeye kazi yake ni kusambaza nje hata taarifa za vikao vya ndani, hawa huwadhihaki viongozi wao mpaka mitandaoni bila kujali athari inayoweza kukikuta chama.
Niwafananishe na nani wapinzani jamani? Nitawafananisha na watoto wadogo, ambao walisema: “Tuliwapigia ngoma, hamkucheza. Tuliwaimbia nyimbo, hamkuitikia!”
Kwa nini kila baya ni la CCM? Kwa nini hata pale inapojikosoa na kijisafisha bado mnaiona kwamba ni mbaya? Propaganda hizi inabidi zifike mwisho! Mwenye masikio na asikie, na mwenye macho na aone!


TAASISI YA MKAPA YAKABIDHI VIFAA MBALIMBALI KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII MKOANI KATAVI VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA SH. MIL 33

$
0
0
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa (BMF) jana imekabidhi vitendea kazi (baiskeli 158, mabegi 150, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) vyenye thamani ya Shs 33,985,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga kwa lengo la kuwasaidia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na urahisi zaidi. 

Taasisi ya Mkapa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma pamoja na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi inatekeleza mradi wa Ukimwi na Kifua Kikuu chini ya Shirika la Save the Children kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria. 

Mradi huu unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma unalenga kuisaidia Serikali kupunguza maambukizi ya Kifua kikuu kwa 25% na kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa 50% mpaka kufikia 2020. Pamoja na hayo mradi unalenga kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, Kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi, kutokomeza unyanyapaaji na kuongeza upatikanaji wa urahisi wa huduma za Ukimwi hasa upimaji wa VVU. 

Katika kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa Taasisi ya Mkapa imetoa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya jamii ikiwemo mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 183 juu ya ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu ndani ya jamii. Pamoja na hayo jana imekabidhi baiskeli 158, mabegi 150, mabuti 25, na makoti ya mvua 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi zitakazotumiwa na wahudumu hao katika utekelezwaji wa majukumu hayo ya ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu na ukimwi kwenye jamii husika.

Afisa mradi kutoka Taasisi ya Mkapa Bw. David Magiri akikabidhi nyaraka za vifaa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, kulia kwake ni Katibu Tawala Katavi, Ndg. Paul Chagonja
Bi. Flora Cosmas, Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, baada ya kupokea baiskeli iliyotolewa na Taasisi ya Mkapa.

TAARIFA YA MATENGENEZO YA MFUMO WA LUKU

MAKONDA AZINDUA MRADI WA MAJI YA DAWASCO KATA YA BOKO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na wanachi wa Kata ya Boko NHC wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja  akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Boko NHC ,Dk. Alexander Kyaruzi akizungumza wakati wa kukabidhiwa mradi wa maji ya Dawasco  Boko  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Dawasco  Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO,  Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akisaini makubaliano na mwenyekiti wa kamati ya Maji Boko NHC, Dk. Alexander Kyaruzi leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Dawasco  Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA JENGO JIPYA LA WIZARA YAKE MKOANI DODOMA.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama wakati alipokagua maendeleo ya Jengo jipya la Ofisi za Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.
Meneja Kanda ya Kati kutoka Wakala wa Majengo Nchini (TBA-Brigade) Mkadiriaji Majenzi Herman Tanguye akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya mgawanyo wa vyumba vya ofisi yaliyofikiwa Katika Jengo jipya la Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama wakati alipokagua maendeleo yaliyofikiwa ya mgawanyo wa ofisi katika Jengo jipya la Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua zilizofikiwa katika Jengo jipya la Ofisi za Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi, mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (Sekta ya Ujenzi) Dkt. William Nshama (katikati), wakati alipokagua na kuona mgawanyo wa Ofisi kwa Sekta zake katika Jengo jipya la Wizara hiyo lililoko Mtaa wa Moshi mkoani Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven Ndyamukama.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(wa pili kulia) kabla ya ufunguzi wa Mkutano huo. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kufungua rasmi Mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akiwasilisha hotuba yake kwenye Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani).
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Simon Mwanguku akiwasilisha mada katika Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza. Mkutano huo umefanyika leo Machi 17, 2017 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Brass Band ya Jeshi la Magereza kikitumbuiza kwenye ufunguzi wa huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Jeshi la Magereza Wastaafu(waliosimama mstari wa nyuma).Wa pili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga na wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza (Picha zote na ASP Deodatus Kazinja).

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) akiwasili leo Machi 17, 2017 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akisaini katika kitabu cha wageni kama inavyoonekana katika picha.
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live


Latest Images