Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

RE THE QUEENS BATON COMING TO TANZANIA

0
0
By Ayoub  Mzee-London
Today i was present at Buckingham Palace , where H.M The Queen launched the Queen's Baton.The Queen’s Baton Relay has officially been launched by Queen Elizabeth II as the countdown to the Commonwealth Games on the Gold Coast in 2018, finally begins.
The relay began with a ceremony and concert in front of Buckingham Palace before the torch heads off on a 388-day, 230,000km journey to the Gold Coast carrying a special message from the Queen.

The Queen, her husband Prince Philip the Duke of Edinburgh, and their son Prince Edward, the Earl of Wessex, sent the torch on its way for a grand tour of all 52 Commonwealth nations and territories in Africa, the Americas, the Caribbean, Oceania, Asia and Europe before it arrives to spend the final 100 days touring Australia.

Over  the  years ,the  buton  relay  has  evolved  into  a powerful symbol of  unity and  diversity of  the  Commonwealth of  nations.

The  Buton  will  be  in  Tanzania  on  the 8/4/2017.Kenya on  the 5/4/2017,Uganda on  the 25/3/2017 and  Rwanda  on  the 22/5/2017






JE MWISHO WA KUTOA MATUNZO YA MTOTO NI MIAKA MINGAPI ?.

0
0

Na  Bashir  Yakub.


Matunzo  ya  mtoto  hasa  kwa  wazazi  waliotengana  ni  pamoja na  chakula,  makazi,  mavazi,  elimu,  pamoja  na  malezi  bora. Wazazi  wote  kwa  pamoja  yaani  baba  na  mama  wanao wajibu   kila  mmoja  kwa  nafasi  yake kuchangia  katika   matunzo  ya  mtoto.

Aidha  makala  haya  kupitia Sheria  ya  Mtoto ,Na. 21  ya  2009   yatajibu  ikiwa  suala  kutoa  matunzo  ya  mtoto  ni  la  milele  au  linao  muda  maalum.  Lakini  kabla ya  hayo  tutizame  nani  ana  mamlaka  ya kufungua  shauri  kudai  matunzo  ya  mtoto.

1. NANI  ANAWEZA  KUFUNGUA  SHAURI  LA  MATUNZO.

Wengi  wetu  twajua  kuwa  ni mama  wa  mtoto  pekee  ndiye  anayeweza kufungua  shauri  la  mtoto  kupatiwa  matunzo.  Dhana  hii  si  kweli.
Kifungu  cha  42( 1 )   cha  Sheria  ya  Mtoto  kinawataja  wafuatao  kuwa  na  mamlaka  ya  kuomba  mtoto apatiwe  matunzo :

( a ) Mzazi  wa mtoto.  Kifungu  hakikutaja  mama  wa mtoto  bali  mzazi  wa  mtoto. Kwahiyo  hata  baba  anaweza  kufungua  shauri  akimtaka  mama  kutoa  matunzo  ya  mtoto.  Mama  kumtelekeza  mwanae   nako ni kumnyima  mtoto  matunzo  .
Wako    mama  wanakimbia  nyumba  zao  na  kuwaacha  watoto. Unaweza  kutumia  kifungu  hiki  kumtaka  mama amchukue  mwanae  na  akae  nae  ikiwa  ni  sehemu  ya  matunzo.

( b ) Mlezi  wa  mtoto  naye  amepewa  mamlaka  ya  kufungua  shauri  kuomba  matunzo  ya  mtoto.  Wako  watu  wako  mjini  lakini  wamewaacha  watoto  vijijni  wakilelewa  na   ndugu au  rafiki.

Lakini  pia  yapo  mazingira  ambapo  kwa  amri  ya  mahakama    imeamriwa  mtoto  asikae  na  wazazi  bali  akae  na  mlezi  kutokana  na sababu  mbalimbali. Au  kwasababu  nyingine  yoyote mtoto  anakaa  na  mlezi .

Basi  ni  katika  hali  hiyo  mlezi  huyo  anayo  mamlaka  ya  kuomba  au  kufungua  shauri  akishinikiza  mzazi/wazazi  kutoa  matunzo  ya  mtoto.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.

WAFANYABIASHARA WADOGO DODOMA KUNUFAIKA NA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan , amewataka viongozi wa mkoa wa Dodoma wahakikishe wanatenga haraka maeneo maaluma kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ili nao waweza kunufaika na mpango wa Serikali kuhamia mkoani Dodoma , Kwa undani wa habari hii bonyeza play.

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA HUDUMA KWA WATEJA SHINYANGA

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua Duka la Huduma ya wateja mjini Shinyanga kwa lengo la kurahisha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.


Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa duka hilo la huduma kwa wateja lililopo karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.

Awali akizungumza wakati wa kuzindua duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel nchini Sunil Colaso alisema wamezindua duka hilo ili kuongeza wigo wa soko mkoani Shinyanga na kuwasogezea huduma wananchi.

“Tunafuraha kubwa kufungua duka hili leo ambalo ni miongoni mwa maduka sita ambayo yanafunguliwa mkoani Shinyanga,hili ni duka la pili Mjini Shinyanga na tunatarajia kufungua maduka mengine ndani ya mwezi huu”,alieleza Colaso.

Aidha Colaso alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Shinyanga kufika katika duka hilo la huduma kwa wateja ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kurudisha namba zilizopotea,kuuza laini,simu,kurekebisha namba za siri za Airtel Money na huduma nyinginezo.

Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema uwepo wa duka hilo utaongeza ajira kwa vijana na pia itarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za simu kwa wananchi ikiwemo huduma za pesa.

“Yanapofunguliwa maduka mengi inasaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma,nawaomba wananchi kila mtu asajili simu yake kwa majina yake halisi ili kupunguza vitendo vya uhalifu",alisema Matiro.

“Nawaomba wananchi mtumie maduka haya kupata huduma mnazohitaji badala ya kutumia watu wa kati ambao baadhi yao siyo waaminifu,kumbukeni mawasiliano ni maendeleo,bila mawasiliano maendeleo yanakuwa ni shida,na sisi tunapoangalia vipaumbele vya maendeleo huwa tunaangalia pia kuna mawasiliano gani”,aliongeza Matiro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro katika duka la huduma kwa wateja wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo katika mtaa wa Buzuka karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 14,2017.
Meneja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma kwa wateja.Katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro na Afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga wakimsikiliza mkurugenzi huyo wa Airtel.Picha zote na Kadama Malunde

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NA MILA KUWAEPUSHA WANANCHI NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA KUFUFUA WATU

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dini, wa mitaa na wa mila katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini mbeya
 Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu kutoka shoto pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika wa kwanza kushoto katika picha ya Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala  ameitisha kikao na viongozi Dini na mila kwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo.Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi wa Dini Mila na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.

" matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua  hayapaswi kuachwa yaendelee , bibilia na Quruan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba  mnisaidie   kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Aamesema Makala.

 Makala awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.

Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo

KAMPUNI YA BIN SLUM YAKABIDHI MSAADA WA MATAIRI 12 KWA HUDSON KAMOGA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBULU MKOANI MANYARA

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga kulia akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa kampuni ya Bin Slum kwa mchango wake katika maendeleo ya wilaya ya Mbulu baada ya kampuni hiyo kupitia kwa meneja Mauzo wake Bw. Salum Aljabiry kumkabidhi moja ya matairi 12 ya magari madogo kutoka kwa Kampuni ya hiyo jijini Dar es salaam .Kampuni ya Bin Slum imetoa msaada huo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli.
2
Mkurugenzi wa Harmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga kulia akipokea moja ya matairi 12 ya magari madogo kutoka kwa Salim Aljabiry Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bin Slum .Kampuni hiyo imetoa msaada huo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli.
345
Baadhi ya matairi yanayouzwa na kampuni ya Bin Slum Chang'ombe jijini Dar es salaam.

MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI,ATOA TAHADHARI

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mt Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivuka moja ya sehemu ambazo zina maji katika bonde la mto Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha Dar es Salaam na kuleta madhara kwa wakazi hao
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza katika maeneo ya bonde la Mto Msimbazi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuza maembe.
 




Na Ripota wa globu ya jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo hayo.

"la kwanza katika ngazi ya mkoa kulingana na utabiri wa hali ya mvua, zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50 maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili usema kinga ni bora kuliko tiba "Aamesema Makonda

amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia ili waweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi kupunguza Madhara.

amesema hayo yanayo onekana leo ni tabia mbaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunavyoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi la pili tunaambiwa tuhakikishe kuwa atuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga

ametaja kuwa maji hayo mengi hutokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa pwani hasa katika eneo la kisarawe na kuhitaji kupita katika mto huu hivyo ukijengwa ndipo madhara haya  huonekana .

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA UAMUZI WA KUHAMIA DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). ZXCCC

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ATEMBELEA UJENZI WA MFEREJI WA MAGAONI UNAOJENGWA KUKABILIANA NA ADHA YA MAFURIKO

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku aliyevaa shati jeupe wa kwanza kulia akiangalia namna uchimbaji wa mfereji wa kupitishia maji wakati wa mvua unavyochimbwa wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku aliyevaa shati jeupe wa kwanza kulia akiangalia namna uchimbaji wa mfereji wa kupitishia maji wakati wa mvua unavyochimbwa wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo.
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wa kwanza kulia akisisitiza jambo kwa mafundi wanaoendelea na ujenzi wa mfereji wa magaoni kwa ajili ya kupitishia maji ya mvua ikiwa ni mpango madhubuti wa kukabiliana na adha ya mafuriko nyakati za mvua.
 Kazi  zikiendelea kama inayoonekana kwenye eneo hilo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wa tatu kutoka kushoto akisisitiza jambo kwa msimamizi wa mradi huo Ephahim Lucas wakati alipotembelea ujenzi wa mfereji huo ili kuona kasi yake ya utendaji kama inakidhi viwango.
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitazama namna mafundi wakiendelea na uchimbaji wa mfereji mkubwa kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua ikiwa ni mpango mkakati wa kuondokana na adha ya mafuriko nyakati za mvua
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitazama ujenzi wa mfereji huo kulia ni msimamizi wa mradi huo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiingia kwenye mfereji huo kwa ajili ya kuukagua wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mapema leo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitoka kwenye mfereji huo mara baada ya kuukagua mapema leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akitoka kwenye mfereji huo mara baada ya kuukagua mapema leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiwa na msimamizi wa mradi huo akikagua baadhi ya maeneo ili kuona namna unavyojengwa
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbarukuakiwa na msimamizi wa mradi huo wakitembelea kwenye mfereji ambao utatumika kupitisha maji yatakayojaa kwenye makazi ya wananchi wakati wa mvua
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiingia kwenye moja ya chemba zilizopo kwenye ujenzi wa mfereji huo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi huo mara baada ya kuutembelea leo kuona namna ujenzi wake unavyoendelea. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Prof. Muhongo azindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoa wa Pwani

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.

Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.

Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg International Services.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga alieleza kuwa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu unahusisha vipengele Mradi vitatu vya utekelezaji.

Alisema kuwa kipengele cha kwanza cha utekelezaji kitahusisha kufikisha umeme kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme wa gridi na kipengele cha Pili kitahusika na kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme.

“Kipengele cha Tatu katika Mradi huu kitahusika na usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi, ambayo ni vigumu kufikiwa na umeme wa gridi yakiwemo maeneo ya Visiwa”, aliongeza Mhandisi Nyamo-hanga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Alisema kuwa Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Pwani utahusisha vipengele vyote vitatu na utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 204 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.2 ambapo utekelezaji wa sehemu ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika Machi 2019.

Mhandisi Nyamo-hanga alitoa wito kwa wananchi watakaounganishiwa umeme kukamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao mapema ili wakati mkandarasi atakapofika katika maeneo yao, wawe tayari kulipia na kuunganishiwa umeme.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo, alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini imefanyika kwa ufanisi kwani katika mwaka 2007 ni asilimia 2.5 tu ya watanzania waishio vijijini walikuwa na umeme lakini mpaka mwisho wa mwaka 2016, upatikanji wa umeme vijijini ulifikia asilimia 49.5.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.

Alisema kuwa, Watanzania wana haki ya kujivunia miradi hiyo inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na TANESCO, kwani ni ya kipekee duniani kutokana faida zake kwa wananchi wa vijijini ambapo gharama mbalimbali zinabebwa na Serikali huku mwananchi akitakiwa kulipia shilingi elfu 27,000 ili aunganishiwe umeme.

Alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wa miradi hiyo, bajeti iliyotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17 ili kusambaza umeme vijijini ni zaidi ya shilingi Trilioni moja.

Kuhusu hali ya Umeme katika mkoa wa Pwani, aliwaagiza watendaji wa TANESCO na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, kujadiliana ili kufahamu mahitaji halisi ya umeme, hasa ikizingatiwa kuwa kuna viwanda vinavyoendelea kujengwa na vilivyopo ambavyo vinahitaji si chini ya megawati 60.
Watendaji kutoka kampuni ya Steg International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutodai fidia katika miradi ya Umeme, kutokana na umuhimu wake katika huduma za kijamii kama vituo vya Afya, Shule, majumbani na shughuli za kiuchumi ili kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi hao.

Wabunge pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani, walipongeza juhudi za usambazaji umeme nchini zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Profesa Muhongo na kutumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zinazopaswa kushughulikiwa na Serikali ili wananchi pamoja na viwanda viweze kupata umeme wa uhakika.

VIJANA WA KAZI MOUNTI MERU RICKERNEST BAND WAHIDI MAKUBWA NDANI YA JIJI LA ARUSHA NA MIKOA YOTE YA TANZANIA

0
0

waimbaji wakiwa wanaendelea kupata burudani na mashabiki

wanenguaji hatari kutoka bendi ya Rickinest Band wakionyesha uwezo wao wa kukata mauno jukwaani 
 
vijana wa kazi kaskazini Arusha wakitoa burudani ya nguvu ndani ya Triple A sport bar bendi town ijulikanayo kama Mounti Meru Rickernest


waimbaji wa bandi ya Rickinest wakiwa wanaserebuka pamoja na wadau wa muziki wa bandi mkoani Arusha



Apa mzuka ulikuwa umepanda hatari waliamua kuonyesha makeke ya kila aina 
 


washabiki wa bandi ya Rickinest wakiwa wana show love kwa pamoja mara baada ya burudani kukolea


wanadada wa A-Town waliouthuria katika show hiyo ya Mounti Meru Rickinest Band wakiwa katika pozi


Wa kwanza kushoto ni shabiki mkuu wa band ya Rickinest music band Omary Matelephone akiwa anabadilishana mawazo na shabiki mwenzake ambalo jina lake alikuweza kufahamika mara moja


mmoja wa wakurunzi wa band hiyo wa kwanza kulia akiwa anaserebuka sebene la nguvu wakati wanamuziki wakifanya yao (picha zote na Woinde Shizza,Arusha)


Bendi hii ya Mounti Meru Rickernest bandi inafanya onyesho lake kila siku ya ijumaa ,jumamosi na jumapili katika ukumbi wa Triple A sport bar

Bendi hii ni mpya na imeaidi kutoa burudani ya nguvu kwa mikoa yote ya hapa nchini

MJENGONI BENDI KUFANYA UZINDUZI RASMI MARCH 3 KATIKA UKUMBI WA TRIPLE A SPORT BAR

0
0
Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni classic band inatarajia kufanya utambulisho wao rasmi kwa mara ya kwanza mapema march 3 katika ukumbi wa Triple A spot bar uliopo ndani ya jiji la Arusha

Akiongea na waandishi wa habari Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa pamoja kuwa bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi katika siku hiyo ya alyamisi.

Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na wanamuziki wa bandi ya mjengoni

Kwa upande wake mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdeme alisema kuwa bendi yake imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.

Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya jirani kuhuthuria onyesho hilo kwani bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.

Alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa mbili usiku adi majogoo ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha

wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu

Rais wa bendi ya mjengono Robert Mukongya (Digital) akiwa anaimba ndani ya jukwaa .Habari picha na Woinde Shizza,Arusha 

SEMINA ELEKEZI KUHUSU MAGEUZI NDANI YA CHAMA KWA WENYEKITI NA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA WILAYA YAENDELEA LEO MJINI DODOMA

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili ukumbini na viongozi wengine wa meza kuu tayari kuendelea na siku ya pili ya semina elekezi kwa Wenyekiti na Makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya nchini, kuhusu mageuzi na mabadiliko ndani ya Chama, leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. 
 Washiriki wa semina hiyo wakiwa wamesimama kumlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wa meza kuu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai, baada ya kuwasili ukumbini. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo na kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Lela Ame Silima
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akifungua kuendelea kwa siku ya pili kwa semina hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendelea kuongoza semina hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga, Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dk. Abdallah Juma Abdallah, na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Lela Ame Silima, Katibu wa NEC Oganaizesheni mstaafu Mohammed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo.
 Semina ikiendelea
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendelea kuongoza semina hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Dk. Abdallah Juma Abdallah, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Lela Ame Silima, Katibu wa NEC Oganaizesheni mstaafu Mohammed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo.
 Sekretarieti ya semina hiyo wakiwa kazini
 Sekretarieti ya semina hiyo wakiwa kazini
 Wajumbe kwenye semina hiyo
 Maofisa waandamizi wa CCM wakifuatilia hali ya mambo kwenye semina hiyo  
 Mshiriki akipata habari motomoto na za uhakika kwenye gazeti la uhuru wakati akiwa kwenye semina hiyo
 Mshiriki akipitia Kitabu cha Mabadiliko ya Katiba ya CCM na kanuni zake, wakati akiwa kwenye semina hiyo
 Katibu wa seretarieti ya CCM, Anamringi Macha akimsalimia Ofisa Mwandamizi wa Chama, ukumbini
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo ndugu Vyohoroka, akisalimia washiriki wenzake ukumbini. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Daniel Zenda. KWA PICHA NYINGINE KEM KEM ZA SEMINA HIYO MUHIMU TAFADAHLI/>GONGA HAPA

RC MTWARA ATAJA SABABU ZA MKOA WAKE KUFANYA VIBAYA KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MWAKA 2016 NA MATOKEO YA DARASA LA SABA .

0
0
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego ataja sababu zilizopelekea mkaoa huo kushuka kwa elimu mwaka 2016-17, katika matokeo ya kidato cha pili .ambapo shule 10 zilizofanya vibaya shule 9 zimetoka mkoani humo na matokeo ya darasa la saba ambapo mkoa huo ulikuwa wa pili kutoka mwisho.Hii hapa video yake.

BancABC YAZINDUA AKAUNTI MAALUM NA YA KIPEKEE

0
0
 Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya JIONGEZE MARADUFU uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo. Kulia ni Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC.
 Bi. Joyce Malai Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akionyesha bango lililoandikwa Jiongeze Maradufu katika uzinduzi wa akaunti hiyo maalum ya kipekee katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es salaam.
 Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC akizungumza jambo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya Jiongeze maradufu. Uzinduzi huo ulifanyika katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es salaam.

 Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati,  na  Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC wakionyesha (bidhaa) Akaunti mpya na ya kipekee JIONGEZE MARADUFU iliyozinduliwa na BancABC.
Joyce Malai akitoa ufafanuzi kuhusu akaunti maalum ya Jiongeze Maradufu iliyozinduliwa na BancABC.



JIONGEZE MARADUFU. Pata riba hadi asilimia kumi na sita (16%)kwa mwaka katika amana hii na kujipatia fursa ya kukopa dhidi ya amana yako.

 BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba maalum utakayojiwekea.

Katika hali ya kawaida kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa mabenki. Kwa kuanzia amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.

Faida nyingine ni  uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.

BancABC imechukuwa hatua kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila ubabaishaji.

Akiongea jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii iliyopo sasa.

 “Tunathamini mchango mzuri wa wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya kipekee kama zawadi maalum”.

Hii haina tofauti ya kupata faida ya biashara hata kabla hujaianza!  Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati muafaka, katika muda inayohitajika haswa.  Tuna hakika bidhaa hii mpya ya kibenki itawavutia wateja wengi  hasa wale walio makini”, alisema Joyce.

“Riba ya  asilimia16% inayolipwa kabla hujamaliza muda wa kuweka akiba, ni kivutio kikubwa, ambacho kitamfanya mteja ajivue majukumu makubwa ikiwa pamoja na kulipa ada za shule, kodi ya nyumba, usafiri au kuitumia kama mtaji kwenye biashara zingine azipendazo kwa kuchukua mkopo ambao dhamana ni amana yako katika benki hapo kwa hapo.

 “Vile vile nawasihi wale wote ambao hawana akiba na  BancABC kutumia nafasi hii na kufaidika kwa kufungua akaunti na kupata maelezo zaidi juu ya faida ya huduma hii ya kipekee.  BancABC iko makini kukutana na wateja wake ili kujenga misingi ya mafanikio ya pamoja“, alimalizia.
BancABC ipo tayari kutoa huduma hii kwa wateja wake na wasio wateja kuanzia leo   kwa miezi miwil.
 

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA OPEN HEART YA NCHINI AUSTRALIA YAFANYA UPASUAJI WA MOYO

0
0
Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiana na madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati akielezea jinsi kambi hiyo ya upasuaji inavyoendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa.

Dkt. Nyangasa alisema, “Kwa kushirikiana na washirika wetu wa OHI tulianza kambi maalum ya upasuaji kuanzia tarehe 10/03/2017 hadi leo  tarehe 17/3/2017 tumefanya  upasuaji kwa wagonjwa 11 ambao wanaendelea vizuri,  kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima ni wawili”,.  

Dkt. Nyangasa alisema  katika kambi hiyo  ambayo inamalizika tarehe 17/3/2017 walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 25 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni 10.

Kuhusu uhitaji  wa damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa Moyo Dkt. Nyangasa alisema wagonjwa hao wanahitaji damu nyingi hivyo basi aliwaomba wananchi wajitokeze kuchangia  damu ambayo itatumika kwa wagonjwa.

“Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu na  uchangiaji huu wa damu  usifanyike mara moja bali  uwe endelevu  kwani Taasisi inatoa huduma kwa wagonjwa wakati wote siyo wakati wa kambi maalum za matibabu ya moyo pekee yake”, alisisitiza Dkt. Nyangasa.

Tangu kuanza kwa mwaka huu  wa 2017 JKCI kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake wa nje ya nchi ambao ni  Madaktari  Afrika wa  Marekani, Hospitali za  Apolo Bangalore na BLK zote za nchini  India na Open Heart International ya Australia wamefanya  matibabu ya moyo ya kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuziba matundu ya moyo kwa mgonjwa wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo. Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu mguuni kwa mgonjwa wa moyo na kuupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba kwa jina la kitaalamu Coronary Artery Bypass Graft (CABG). Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili. Habari/Picha na Anna Nkinda – JKCI.

WAZIRI NAPE AWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI KUTENDEA HAKI SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI NA SHERIA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA

0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.

Na: Lorietha Laurence – WHUSM, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuzisoma, kuzielewa na kuzifanyia kazi sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na ile ya Haki ya kupata Taarifa ya mwaka 2016 ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuuhabarisha umma.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ambapo licha ya kuwataka kuzijua sheria hizo pia amewataka kuwa wabunifu kuendana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia katika utendaji kazi wa kila siku.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.

Aidha aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hizo mbili kutatengeneza daraja litakalounganisha na kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa wananchi. “Ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano kuzijua na kuzitendea kazi sheria hizi ili kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano baina ya serikalini na umma hivyo kuondoa ugumu uliokuwepo hususani katika kupatikana kwa taarifa muhimu kwa wananchi” alisema Waziri Nape.

Aliongeza kwa kufafanua kuwa endapo utekelezaji wa sheria hizi mbili muhimu utasimamiwa na kuzingatiwa basi kutakuwepo na matokeo chanya ya kiutendaji na hivyo kuleta mafanikio makubwa yanayotarajiwa na umma.

Waziri Nape pia aliwataka Maafisa Mawasiliano hao kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuendana na maendeleo ya teknolojia ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma na kutoa taarifa kwa wakati.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Nuru Milao akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kufungua rasmi Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma tarehe 14 Machi 2017.

“Zama hizi sio zile za maafisa mawasiliano kujisifia kwa kuwa na safari nyingi badala yake kuwa watekelezaji wa kazi zao kwa wakati na matokeo yanayoonekana kwa umma ila kwa atakayeshindwa kutekeleza hayo basi tutaomba atupishe” alisema Waziri Nape.

Aidha alieleza kuwa anafahamu kuwa kuna changamoto nyingi ambazo maafisa mawasiliano wanakumbana nazo katika utendaji wao wa kazi ikiwemo ukosefu wa vifaa ingawa si kigezo cha wao kutokutekeleza wajibu wao.

Katika kuhakikisha kuwa changamoto ya ukosefu wa vifaa inatatuliwa Waziri Nape alitoa Wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka kipaumbele katika bajeti hii mpya kwa kutenga kiasi cha fedha ambacho kitasaidia kununua vifaa kwa ajili ya Maafisa Mawasiliano wa Wizara, Taasisi, Mikoa, Wilaya na Halmashauri .
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao alisema kuwa umuhimu wa mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji pamoja na kutathmini utendaji kazi wao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Elizabeth Simon Kitundu ameishukuru Wizara kuandaa mafunzo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini na kuyafanyia Mkoani Dodoma kwani kwa kufanya hivyo itarahishisha mfumo wa kimawasiliano na kutangaza fursa zilizopo Mkoani Dodoma hivyo kuwafanya watumishi wa umma kuwa na amani katika kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma.

Mkutano wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini umefanyika kwa mara ya 12 huku lengo ikiwa ni kuwakutanisha kwa pamoja maafisa hao kutoka katika ngazi mbalimbali za kiutendaji serikalini ikiwemo Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa, Wilaya na Halmashauri ili kuweza kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt Hassan Abbas akichangia jambo wakati wa kikao cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali kutoka Wizara,Taasisi ,Halmashauri,Wakala na Mashirika ya Umma,Tamisemi na Idara zinazojitegemea wakimskiliza kwa makini Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(hayupo Pichani) wakati akifungua Kikao kazi cha 12 cha Maafisa hao kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) akichangia jambo wakati wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Mawasiliano kutoka Idara ya Habari-MAELEZO wakati wa kikao cha 12 cha Maafisa hao wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AFUNGA SEMINA YA WATENDAJI, WENYEVITI NA MAKATIBU WA WILAYA NA MIKOA MJINI DODOMA LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa wakati wa kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli  wakati akifunga kufunga semina ya watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa  katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa baada ya kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.

PICHA NA IKULU

WAZIRI NAPE AZIFAGILIA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU NA IDARA YA HABARI MAELEZO KWA UBUNIFU NA WELEDI

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye (pichani) amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano ya Rais, Ikulu, 
 na Idara ya Habari MAELEZO kwa ubunifu na weledi wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.

Waziri Nape alisema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili Maafisa Mawasiliano wa Serikali wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali ,amewataka kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano hasa mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nafuu na rahisi.  
“Nawapongeza sana wakurugenzi vijana Dkt. Hassan Abbasi wa MAELEZO na Greyson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu  wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa”alisema Waziri Nape.
Waziri Nape aliongeza kuwa pamoja na ubunifu wao katika mitandao ya kijamii, utayarishaji wa makala za Serikali na kujibu hoja kwa haraka kupitia taarifa kwa umma,  wameweza pia kubuni vipindi vya TUNATEKELEZA na SAFARI YA DODOMA ikiwa ni mkakati wa kusukuma mbele ajenda za Serikali.
Aidha, Waziri Nape amewataka Maafisa Mawasiliano kutumia fursa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari binafsi  kupitia vipindi vya bure kwenye Televisheni, redio na magazeti  kuhakikisha mambo mazuri yanayotekelezwa na Serikali yanatangazwa na kuweza kusikika kwa Wananchi.
“Nimezungumzia hoja na haja ya mabadiliko kiutendaji, lakini nikiwa kiongozi ambaye pia katika maisha yangu nimefanya kazi ya kuongoza kitengo cha habari na uenezi nafahamu changamoto zinazoikabili kada hii,lakini unaweza ukageuza changamoto kuwa fursa,kwahiyo tujiongeze ndugu zangu ” alisema Waziri Nape. 
 Waziri Nape alitoa wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi pamoja na watendaji wakuu katika ofisi za umma kuhakikisha wanatenga fedha katika bajeti kwaajili ya kununua vifaa vya kutendea kazi ili kuviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi katika kuisemea Serikali.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images