Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Pombe za Viroba Zenye Thamani ya Shilingi Bilioni 10.8 Zimekamatwa Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki  maarufu kama ‘viroba’ zenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8 zimekamatwa Jijini Dar es Salaam katika msako wa pombe hizo uliofanyika kuanzia Machi 01 mpaka 03, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba  leo Jijini, Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu operesheni ya utekelezaji wa maelezo ya Serikali ya kusitisha pombe hizo za viroba hapa nchini kuanzia Machi 01, mwaka huu.

“Jumla ya katoni 99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (Viroba) zimekamatwa ambapo katoni 69,045 ni zenye ujazo wa  na mililita 50, katoni 29,344 zenye ujazo wa mililita 100, katoni 782 zenye ujazo wa mililita 90 pamoja na katoni 10,625 za chupa zenye ujazo wa mililita 100. Thamani yake ni Shilingi Bilioni 10.83,” alifafanua Makamba.

Aliendelea kwa kusema kuwa, jumla ya viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali, maduka ya jumla 18, maghala 4, baa 3 na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia viroba vilikaguliwa katika opesheni hiyo.

Makamba amesema kuwa, pombe zilizokamatwa zimezuiliwa kuuzwa  au kusambazwa kutoka katika maeneo ambayo yamehifadhiwa yaani viwanda, maghala pamoja na maduka ya jumla mpaka hapo Serikali itakapotoa tamko.

Aidha wananchi wametakiwa kushiriki katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini wanaokaidi agizo la Serikali la kuzalisha, kusambaza, kuuza au kutumia pombe hizo kupitia namba ya simu 0685 333 444  kwa kutuma ujumbe mfupi wa meseji au whatsapp au kwa kupiga simu.

Vile vile amesema kuwa zawadi kati ya shilingi laki 5 hadi milioni 1 zitatolewa kwa mwananchi atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa kwa mtu yeyote mwenye ghala au aliyehifadhi shehena ya pombe za viroba kinyume cha sheria, watu au mtu anayeingiza  pombe za viroba nchini kutoka nje ya nchi kinyume na sheria na utaratibu, anayehamisha au kusafirisha pombe za viroba kinyume na sheria, mtu mwenye kiwanda/mtambo wa kuzalisha pombe za viroba ambao hautambuliki na Serikali pamoja na mtu anayetumia stempu feki za TRA .

Pombe za viroba zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa, ajali na vifo vinavyosabaishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizo, kuongezeka kwa vitendo vyauhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waamini.

Kutokana na athari hizo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alipokuwa Mkoani Manyara, Februari 16 mwaka huu alitoa tamko la kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa pombe kali za viroba kwa nchi nzima kuanzia Marchi 01, mwaka huu.


RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM KUTOKA KATIKA ZIARA YA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya kulevya nchini Bw. Rogers Sianga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.  
PICHA NA IKULU

AFISA MAENDELEO JIJI LA TANGA AFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE LA JIJIN HILO AWATAKA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI KUJIPATIA MAENDELEO

$
0
0
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akifungua kongamano la Wanawake Jijini Tanga ambalo lilikuwa na lengo kuu la kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa wanawake ikiwemo fursa za kiuchumi sambamba na kupambana na dawa za kulevya kwa jamii lililofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga leo
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi  wa pili kutoka kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa wakati wa kongamano la wanawake Jijini Tanga kuelekea siku ya wanawake dunia kushoto ni Rehema na Yahaya Seumbe ambaye ni Afisa kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii kwenye Jiji la Tanga wakifuatilia kongamano hilo.
 Baadhi ya Wakina wanawake jijini Tanga  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo
 Sehemu ya Umati wa wanawake wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo la wanawake wa Jiji la Tanga kuelekea siku ya wanawake Dunia ambapo kilele chake itakuwa ni Machi 8 mwaka huu
 Baadhi ya waandishi wa habari jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo wa kwanza kulia ni Burhan Yakub wa gazeti la Mwananchi,Bertha Mwambele wa TBC TV na Sussan Uhinga wa Clous TV
 Sehemu ya wakina wanawake Jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano la wanawake kuelekea siku ya wanawake ambapo kilele chake ni Machi 8 mwaka huu
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia Machi 8 mwaka huu mara baada ya kufungua kongamano la wanawake Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga baada ya kumalizika kwa kongamano hilo ambapo alisema kuelekea siku ya wanawake kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Ahadi za Rais Dkt. Magufuli zatekelezwa katika ziara yake mikoa ya Kusini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mara baada ya mahubiri katika Kanisa hilo Jumapili. Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Waumini  wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.
 Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200 ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo.
 Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha ambazo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya ziara mkoani humo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa.
 PICHA NA IKULU


VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 6,2017

NEW VIDEO!!! HERI MUZIKI - SWEET LOVE

Huawei Wins ‘Outstanding Contribution for LTE Evolution to 5G’ Award at MWC 2017

$
0
0
  Huawei received the ‘Outstanding Contribution for LTE Evolution to 5G’ award at Mobile World Congress (MWC) 2017. This year is the first year that GSMA has chosen to present the award for 5th generation mobile networks (5G) and receiving such an honor helps to showcase Huawei’s contribution to technology evolution.  

Huawei wins “Outstanding Contribution for LTE Evolution to 5G” at MWC 2017
“This is the first year that GSMA sets an outstanding contribution award for 5G. Huawei is honored to receive this award” saidMr. Xu Wenwei, Executive Director of the Board, Chief Strategy Marketing Officer, “The next few years will see continuous LTE development and 5G innovations. So, we need to do the preparation in all aspects, including network deployment and industry collaboration. During the 4.5G to 5G, Huawei will keep focusing on helping our customers to improve user experience, to step into all cloud era, to enable innovative services for vertical industries, and finally to build 5G with more vitality and longer lifecycle.”

68 4.5G networks were commercially deployed worldwide in 2016 and the number of networks deployed in 2017 is expected to reach 120.
Network evolution should begin with the evolution of network architecture. In 2016, Huawei launched its CloudRAN Solution, which is a technology that applies a cloudified architecture to the Radio Access Network (RAN) and can create a 4.5G and 5G oriented architecture integrating multiple radio access technologies (RATs), frequency bands, and layers. And it is also a foundation for E2E network slicing, providing operators with a way to realize the new business model of deploying diversified new services in one network.  As an anchor for joining 4.5G and 5G, CloudRAN helps maximize network collaboration efficiency and helps operators produce business success.
Huawei is still insisting on continued investment in technical innovation in order to meet the challenge of the anticipated accelerated increase of future MBB network traffic. Huawei and the world's leading operators engage in large-scale 5G NR field tests and 5G high and low frequency hybrid field tests. The results show that continuous coverage and super ultra-large capacity can be satisfied simultaneously, and a single-user peak of 25Gbps can be achieved.
Inaddition, Huawei and Deutsche Telekom have performed the millimeter-wave high-frequency test procedure and achieved a peak rate of 70 Gbps – an industry first. Huawei’s CloudAIR solution can promote the usage of the air interface resource and realize quick deployment of 5G NR and thus solve the problem about long-term coexistence with pre-existing RATs. 
Meanwhile, by adopting 5G technology on 4G networks well in advance, Huawei and operators have jointly taken the lead in finishing the deployment of Massive MIMO in 4G live networks, providing good user experience and huge promotion of network capability.
In order to construct a new business model with industry, Huawei and vertical industry partners jointly succeeded in the incubation of many NB-IoT commercial use cases. Furthermore, Huawei announced X Labs in 2016, a new research platform that will bring together operators, technology providers, and vertical industry partners to jointly explore future use cases for mobile applications, and drive innovation in business and technology.
Huawei’s “4.5G Evolution to 5G” solution, which provides high-quality coverage, ultra-large capacity and flexible network architecture, can help operators to keep ahead on the road to 5G  and help to make 5G a reality.

---
Mobile World Congress 2017 is being held in Barcelona, Spain from February 27 to March 2 this year. The Huawei exhibition area is in area 1J50 in Hall 1, area 3I30 in Hall 3, and the Innovative City exhibition area in Hall 4 in Fira Gran Via. For more details, see:  http://www.huawei.com/cn/events/mwc/2017/


-       Ends    -

About Huawei
Huawei is a leading global information and communications technology (ICT) solutions provider. Our aim is to enrich life and improve efficiency through a better connected world, acting as a responsible corporate citizen, innovative enabler for the information society, and collaborative contributor to the industry. Driven by customer-centric innovation and open partnerships, Huawei has established an end-to-end ICT solutions portfolio that gives customers competitive advantages in telecom and enterprise networks, devices and cloud computing. Huawei’s 180,000 employees worldwide are committed to creating maximum value for telecom operators, enterprises and consumers. Our innovative ICT solutions, products and services are used in more than 170 countries and regions, serving over one-third of the world’s population. Founded in 1987, Huawei is a private company fully owned by its employees.

For more information, please visit Huawei online at www.huawei.com or follow us on:

WAZIRI NAPE NNAUYE AFUNGA FAINALI ZA KOMBE LA ULEGA CUP MKURANGA MKOANI PWANI

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira ya Kisiju wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia Waamuzi wa mpira wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimpongeza Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega kwa juhudi zake za muleta maendeleo kaaika jimbo lake na udahmini wake wa kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.
Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wageni waalikwa pamoja na wakazi wa wilayani hapo kuhusu maendeleo ya jimbo lake na lingo la kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira ya Kisiju wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia Waamuzi wa mpira wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimpongeza Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega kwa juhudi zake za muleta maendeleo kaaika jimbo lake na udahmini wake wa kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.
Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wageni waalikwa pamoja na wakazi wa wilayani hapo kuhusu maendeleo ya jimbo lake na lingo la kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kisiju Wilayani Mkuranga wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tengelea Wilayani Mkuranga wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Timu za moira za Kisiju na Tengelea wakichuana kuwania kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega ambapo fainali hiyo imechezwa jana 05/03/2017 Wilayani hapo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye pamoja na wageni engine walioalikwa wakifuatilia mpambano kati ya Timu ya mpira ya Kisiju na Tengelea wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Baadhi wa Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani wakishiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo, Mhe. Abdallah Ulega.
Baadhi wa Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani walioshiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo, Mhe. Abdallah Ulega wakipokea zawadi za jezi na doti za khanga ikiwa ni sehemu za motisha.
Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega (aliyevaa tisheti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani walioshiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Africa’s Richest Man, Dangote, happy with Magufuli’s leadership style.

$
0
0
By Staff Reporter-Tanzania Information Services- MAELEZO


African’s wealthiest person, Alhaj Aliko Dangote said, on Sunday, that he was content with the leadership style of President Dr. John Pombe Magufuli and vowed to continue working with him and his government.

Welcoming the president and his delegation at Dangote cement factory in Mtwara, Alhaj Dangote said he was satisfied with every effort taken by the President and his government to strengthen investment climate in the country.

“It is a great honor and privileged to our company to have been given such an opportunity to make such a big investment in Tanzania which is worth US $650m” Alhaj Dangote told the President.

He added that his company was ready to continue supporting government measures in addressing socio economic challenges as part of the implementation of the company’s program of corporate social responsibility.

Alhaj Dangote told President Magufuli that currently the factory was producing 750,000 to 770,000 tons per year but this year production would be raised to one million tons and in 2018 the factory would reach its production capacity of three million tons per year.

On new trucks, he said that the launching of the 580 trucks has given new hope to many low income earners in the country because the trucks would distribute cement all over the country and would allow to be sold at fordable price of not more than ten thousand shillings.

Alhaj Dangote further explained that since production started, cement prices had dropped from shillings 15,000/= per 50kg bag to shillings 10,000/= and expected to drop further following new planned distribution network by the factory following the launching of the new trucks. 

Meanwhile, President John Pombe Magufuli has instructed Ministry of Energy and Minerals and Tanzania Petroleum Development Cooperation (TPDC) to allocate part of Ngaka coalmine in Mbinga District, Ruvuma region to Dangote Cement Factory so that the later can produce coal to use in cement production.

President Magufuli issued those instructions during his tour at the factory before officially launched 580 company’s trucks to be used to distribute cement to various parts of the country.

He gave the ministry and TPDC seven days to allocate the land and issue mining license to the company and repeated his previous call that Dangote should not buy natural gas through private companies apart from TPDC.

“Dangote must be granted mining license for coal and must have direct access of natural gas from TPDC” He said and added that TPDC has to construct special pipeline to supply natural gas to the factory.

He insisted that direct supply of natural gas to the factory and access to Ngaka coal mine, the company would be at liberty to choose between the two in running the factory. 

President Magufuli said that it was high time that the responsible ministry and its institutions take necessary measures to immediately make sure that no other hindrance befall the factory.

He noted that he has been informed of various setbacks facing the company and cited delaying of clearance of company’s trucks for two months and said he was surprised when he made a phone call to enquire about the issue then they were immediately cleared.

He however noted that the company’s management was to blame for some of those problems facing the company and asked Alhaj Dangote to rethink of his management.

“Mr. Dangote, you a very a good person but people who are representing you here are letting you down and it is probably that they are conspiring with your competitors to deceive you” President Magufuli said.

President Magufuli told Alhaj Dangote that it was unusual for a business company to procure a number of trucks like he had done but surprisingly they have been left unused and instead the company continued to outsource to add more expenses to the company.

He repeated his earlier call to Dangote’s management that they must directly contact the government for their service needs instead of using individuals or private companies as go between who he said were enriching themselves and raised company’s production cost.

“Alhaj Dangote kindly look carefully at your management; it uses middlemen who cause you problems. I have already instructed the ministry to not sell gas to middlemen. We want to directly supply gas to your factory that you can produce electricity at the factory” emphasized the President.

In December last year, President Magufuli met with Alhaj Aliko Dangote in Dar es salaam to clear the air when there were various negative stories published in the media about problems facing the company and it was claimed that the company was about to close its business in the country. 

During that meeting the President assured Alhaj Dangote of his commitment and that of his government to continue to create conducive environment to enable the factory to smoothly undertake its activities.

Dangote cement factory situated at Msijute Village, Mtwara region in Southern Tanzania is the biggest cement factory in the Southern African region.

President Magufuli was in fourth day of his four-day tour of Pwani, Lindi and Mtwara regions which started last Thursday.

CRDB YAANZISHA AKAUNTI YA MALKIA KATIKA WIKI YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Benki ya CRDB imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kufungua akaunti ya Malkia ambayo itakuwa ni yenye malengo yakinifu na manufaa kwa maendeleo kwa wanawake.

Akizungumza na Globu hii, Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura amesema kuwa akaunti hii ya Malkia inakuwa na malengo makuu ya kumuwezesha mwanamke ili aweze kuwa na malengo yakinifu ya kujiendeleza kiuchumi.

Mary amesema kuwa, kampeni hii imeanza machi mosi na itakuwa ni endelevu na taratibu zake za kufungua ni kwa kima cha chini cha shilingi cha elfu hamsini (50,000) na mteja atatakiwa kuweka hela kwa muda wa mwaka mmoja bila kuzitoa.

Amefafanua kuwa, ndani ya mwaka mmoja mteja anaweza kupata faida ya kutosha na kuanzisha miradi mbalimbali.
 Mkurugenzi wa tawi la CRDB Water Front Donath Shirima (kulia) akiwa pamoja katika picha na wafanyakazi wa tawi hilo kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani  Machi 08 mwaka huu.
 Wafanyakazi wa wa tawi la CRDB Water Front katika picha za pamoja kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani Machi 08 mwaka huu.
Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura akiwa anatoa maelezo ya namna  ya  kufungua akaunti ya Malkia kwa wanawake inayolenga kumnufaisha mwanamke.
Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma katika moja ya madirisha ya benki hiyo tawi la Water Front.Picha Zote na Zainab Nyamka.

WATUMISHI WA SERIKALI, WANANCHI WADAIWA KUSHIRIKIANA KULIMA BANGI NYASA ,WATANO WAKAMATWA

$
0
0
Baadhi ya watumishi wa serikali wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamekuwa wakishirikiana na wananchi katika kilimo halamu cha zao la bangi wilayani humu. Mpaka sasa wananchi watano wakiwemo watumishi wa serikali wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na kilimo cha bangi.

WASANII WETU WAONE HAJA SASA YA KUTUMIA SANAA ZETU ZA FILAMU NA MUZIKI KULIUNGANISHA BARA LA AFRIKA-WAZIRI NAPE

$
0
0
 Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michez,Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa mmoja wa Wasanii mahiri katika tasnia ya Filamu nchini Nigeria,Mike  Ezuronye nchini Tanzania,ambaye amewasili nchini kwa mradi maalumu wa kutengeneza filamu.Waziri Nape amesema kuwa ujio wa msanii huyo ni hatua kubwa katika Tasnia ta filamu nchini,kwani ujio wake utaongeza chachu ya mabadiliko kwa namna moja ama nyingine kwa wasanii wenyewe na sanaa yenyewe kwa ujumla.

"Huyu ni mmoja wa wageni waliokuja na wengine wataendelea kuja,Sisi kama Serikali kazi yetu ni kunatengeneza mazingira mazuri waje zaidi katika nchi yetu,waje washirikiane na sisi,Wakija wataleta teknolojia,wataleta ujuzi na uzoefu wao lakini pia wakishirikiana na wasanii wetu kufanya kazi zao,kazi zetu zitaingia kwenye nchi yao na za kwao zitaingia kwenye nchi yetu na sote kwa pamoja tutafaidika kama nchi na wasanii kwa ujumla,
.
Amesema kuwa imefika wakati wasanii wa Tanzania waone haja ya kutumia sanaa zetu za Filamu na muziki kuliunganisha bara letu la Afrika,amesema kuwa hilo ni jambo kubwa sana  na anatamani Watanzania na wasanii wenyewe kwa ujumla waone wajibu walionao katika kuzitumia kazi zao kulifanya bara la Afrika kujivunia kazi za wasanii wake popote pale ulimwenguni. 
Mkurugenzi wa kampuni ya  Entertaiment Project and Design (EPD) Halima Yahaya almaarufu kwa jina la kisanii Davina akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Mike  Ezuronye nchini Tanzania.

Davina amesema kuwa ujio wa msanii huyo umefanyika kwa Msaada mkubwa wa Serikali kupitia Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo.Anasema wamefanikiwa kumleta msaniii huyo kupitia kampuni yake kwa ajili ya kufanya mradi (Project) ya Filamu hapa nchini,Davina amesema kuwa msanii huyo mahiri anatarajia kukaa nchini kwa wiki mbili mpaka pale mradi huo utakapokamilika.Pichani kulia ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
  Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Mike  Ezuronye akizungumzia ujio wake hapa nchini,kwa Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Pichani kulia ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Msanii huyo wa nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria,alipokuwa akizungumzia ujio wake hapa nchini.Picha na Michuzi Jr.

Rais atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha

$
0
0
RAIS Dk. John  Magufuli ametengua  uteuzi wa   Mtendaji  Mkuu wa Shirika  Elimu Kibaha  Dkt. Crspin  Mpemba  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia tuhuma mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.

Simbachawene amesema Mnamo Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua  rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Amefafanua kuwa kumekuwepo  malalamiko dhidi ya Mtendaji  Mkuu wa  wa shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI  iliunda kikosi kazi  ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko hayo na kugundua  kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji wa Shirika hilo.

 “Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja  zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene.

Ameongeza kuwa ili uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake.

Waziri amesema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwa kuwa tuhuma  na malalamiko mengi ya awali yaliyojitokeza  dhidi yake yanajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi ambapo kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo  uchunguzi utakapokamilika.

Jafo atoa agizo hilo jana alipokuwa akikagua mradi huo ambao ujenzi wake umeanza mwaka 2013.

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua mradi wa maji wa Wilunze Wilaya ya Chamwino.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akimsikiliza Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji Wilunze Enock Masanja.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akikagua mradi wa maji Wilunze wilaya ya Chamwino.


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino na kutoa mwezi mmoja kwa Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kukamilisha kutokana na utekelezaji wake kuwa wa muda mrefu.


Akizungumza katika ukaguzi huo, Jafo alisema utekelezaji wake umesuasua hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo waendelee kupata adha ya maji na kuiagiza Halmashauri ya Chamwino kuzuia fedha ya mkandarasi huyo zilizosalia kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka ubora wa mradi huo utakapoonekana.

Hata hivyo alisema mkandarasi aitwaye M/S Kijima fedha aliyopewa hadi sasa haiendani na kazi iliyofanyika huku akitilia mashaka mabomba yaliyowekwa kwamba yapo chini ya kiwango.

“Mkandarasi umepewa Sh. Milioni 305.7, gharama ya mradi kwa ujumla ni Sh.Milioni 347.9, umebakisha fedha kidogo ambayo ni Sh.milioni 42.1 tukiangalia kazi iliyofanyika hata haiendani na fedha ulizopewa, unachokifanya hapa ni kama maigizo huu mradi haujafikia asilimia 90 na haya mabomba yanaonekana yapo chini ya kiwango maana yameanza kupasuka,”alisema Jafo

Aidha alisema Halmashauri hiyo imekuwa na uzembe katika usimamizi wa miradi ya maji hali inayosababisha wananchi kukosa huduma ya maji kwa wakati.

Jafo alimtaka Mkandarasi huyo kukamilisha mradi huo na kwamba ifikapo Aprili 3, mwaka huu atarudi kukagua na kuiagiza serikali ya wilaya hiyo kuwakamata watu watakaoharibu miundombinu ya maji.

Hata hivyo alisema katika miradi mingi ya maji aliyotembelea amekutana na changamoto ya wakandarasi kuweka mabomba ambayo yapo chini ya kiwango na kusababisha wananchi wanapokabidhiwa mradi kushindwa kuiendesha.

Naye, Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Camp A, Waziri Sengoli, alisema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakipata adha ya maji ka takriban miaka saba huku akiwaumbua viongozi wa Halmashauri hiyo kwamba wamekuwa hawatembelei kukagua mradi huo.

Kwa upande wake, Mkandarasi huyo Enock Masanja, alijitetea kuwa ameshindwa kukamilisha mradi kwa wakati kutokana na kutopata fedha kwa wakati.

KONGAMANO LA WILDAF LA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF), Dk Judith Odunga akizungumza na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika Dar es Salaam leo (Machi 6). Kusoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi, Mwenyekiti wa shirika hilo, Naomi Kaihula (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa shirika hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi akizungumza na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) na kufanyika Dar es Salaam leo (Machi 6).

Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF, Naomi Kaihula akizungumza na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na shirika hilo na kufanyika Dar es Salaam leo (Machi 6).
Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Nimujo wakiburudisha wakati wa kongamano hilo.
Wadau na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake duniani lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) Naomi Kaihura (kushoto kwake), Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Judith Odunga (kulia kwake) na wajumbe wa shirika hilo wakati wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Shirika hilo na kufanyika Dar es Salaam leo.
Washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake duniani lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) wakifuatilia matukio ya kongamano hilo Dar es Salaam leo.

YANGA TAYARI KUWAVAA KILUVYA KESHO KOMBE LA FA

$
0
0

Na Zainab Nyammka, Globu ya Jamii

Msafara wa mabingwa wa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Yanga SC , umewasili salama jijini Dar es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya 0- 0.

Msafara huo umeelekea moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.

Timu imeendelea na mazoezi jioni ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho robo fainali kombe la FA dhidi Kiluvya ya kutoka mkoani Pwani . 

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamiana amesema kuwa  licha ya ratiba ngumu kuikabili timu yake lakini amesema yupo tayari kupambana na vijana wake ili kuhakikisha klabu inapata matokeo mazuri katika michezo yote miwili. 

Wapenzi , wanachama , mashabiki na wadau wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika michezo yote miwili ili kuipa sapoti timu hiyo . 

Mbali na hilo, droo ya kombe la Shirikisho hatua ya saba au robo fainali inatarajiwa kufanyika kesho baada ya kupatikana kwa mshindi  wa mechi kati ya Yanga na Kiluvya na kuungana na timu za Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.

HATUTAKUBALI TLS KUJIINGIZA KATIKA SIASA-MWAKYEMBE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

Amesema kuwaingiza wanachama ambao wana nasaba za siasa au viongozi wa vyama vya siasa ndani ya TLS ni kuruhusu mgongano wa maslahi na yeye kama mwanasheria hawezi kulikubali jambo hilo. DKt Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) uliokuja kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao Bw. John Seka

“Kama Wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. Hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote Wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea maelezo, katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je nyinyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?, alisema Mhe Mwakyembe.

Alisema Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila ni lazima wafahamu kwamba viongozi wanaowachagua ambao ndio watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa chama kama wanataaluma hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha mgongano wa maslahi unapoweza kujitokeza.

“Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila tatizo linakuja pale mnapotaka kuchagua viongozi ambao tayari wanazo kofia mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya siasa, hao ndio watakaobeba sura na mtazamo au mwelekeo wenu hapo hatuwezi kukubali kwa kuwa watatenganishaje uongozi wao katika chama husika na uongozi wao ndani ya TLS, huo sasa ndio mgongano wa maslahi alisema Dkt. Mwakyembe na kuongeza kuwa ndio maana mwanasheria yoyote akiingia katika utumishi wa umma uwakili wa kujitegemea anauweka pembeni ili kuepuka mgongano wa maslahi.”
Alisema TLS sasa imekuwa na haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma nchi ilipopata uhuru, kwani ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa wanachama pia na kwa hiyo ni bora tuifute hii Sheria yenu na tuwape mwanya mkajisajili kama NGO ambako kiongozi yeyote wa chama cha siasa anaweza kuwa kiongozi wao.

Amewataka wafahamu kuwa dhamira ya Serikali ni njema huku ikizingatiwa kwamba Sheria kama zilizvyo taaluma nyingine nchini bado zinahitaji uangalizi hasa ukizingatia uingiaji wa nchi katika utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Sifuni Mchome alisema kila taaluma ina namna ya uangalizi wake. alisema kama wanasheria lazima kuhakikisha hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo fani nyingine nchini. Alitaka wajiulize kama kweli hawauoni mgongano wa maslahi huku wakizingatia kuwa wanapaswa kuhudumia jamii ya watanzania bila ya kuwabagua.

“Kama wanasheria lazima tuhakikishe hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo fani nyingine, jiulizeni kama kweli hamlioni jmabo hilo kama ni kikwazo huku mkizingatia kuwa tunatakiwa kuhudumia jamii bila ya kuwabagua sasa tukijiingiza katika siasa tutaihudumiaje jamii husika? TLS kutojihusisha na siasa ni miongoni mwa kanuni za kutuimarisha kama wanataaluma,”alisema Prof Mchome

Alisema Wizara ipo kuiangalia TLS, na ndicho ilichofanya, imewastua jamani mnaenda wapi? tunataka muende katika mstari sahihi, nawataka mjiulize hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano wamaslahi hapo?

“Tupo hapa kuwangaalia, na ndicho tulichofanya, tumewashtua jamani mnanenda wapi? Hatuna nia mbaya ila tunawataka muwe katika mstari, hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano wa maslahi hapo?

Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua ya kuifuta Sheria ya TLS kama chama hicho kitaendelea na msimamo wa kujihusisha na masuala ya siasa au kiuharakati chama hicho katika siasa na hawana budi zaidi ya kuangalia namna wanavyoweza kujikwamua katika hilo.

Kama hamuwezi kuendeleza misingi ya kitaaluma ya kutojihusisha na siasa au vyama vya siasa basi serikali haitakuwa na namna zaidi ya kuifuta sheria ya TLS na TLS ya sasa itabidi ikajisajili kama NGO ili iendeleze harakati zake na Serikali itaunda sheria nyingine itakayoanzisha chombo kitakachosimamia misingi ya kitaaluma.

Naye Rais wa TLS bw. John Seka akizungumza katika kikao hicho alisema ameelewa maoni ya Serikali na kwamba kuonekama kwa TLS kama inajiingiza katika siasa kunatokana na wanachama ambao ni viongozi au wanachama katika vyama vya siasa ambao kwa sasa wanataka uongozi wa chama hicho.

Ameiahidi serikali kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wakuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati na hivyo kuiomba Serikali kuifanyia marekesbisho Sheria yake ili iweze kukabili changamoto inazokabilian nazo kama ilivyotokea sasa ambapo mwanachama ni kiongozi wa chama cha siasa na hivyo kuwa na haki ya kuomba uongozi wa TLS

Amesema anaiomba wizara na watendaji wake kuendelea katika mazunguimzo na TLS ili kuweza kuhakikisha inatekeleza na kufikia malengo yote ya kuanzishwa kwake huku akiahidi kuwa siku zote TLS haitogwanyika, itasimamia na kuongoza wanachama wake ipasavyo na kuhakikisha misingi na maadili ya taaluma ya sheria inazingatiwa ili TLS iendelee kubaki kama ilivyo sasa na kutokupendelea upande wowote.

BODI MPYA VETA YAAGIZWA KUANZA KUCHUKUA HATUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire Ndazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi wa rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi.
Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Peter Maduki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) kupitia Bakwata Suleiman Lolila (kulia) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Peter Maduki (katikati).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi na Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi, Peter Maduki.Picha na: Frank Shija – MAELEZO.


Na: Frank Shija, MAELEZO.

BODI ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam.

Profesa Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.

“Inasikitisha kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema Profesa Ndalichako.

Ndalichako ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika ucheleweshaji wa kuanza kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.

“Mhe Waziri, maelekezo yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na timu yangu tutayafanyika kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana nawe wakati wowote,” alisema Mduki.

Awali akisoma maelezo mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi amebainisha changamoto kadhaa katika eneo hili la utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwa ni pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya elimu na mafunzo ya ufundi akitolea mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo wanakadiriwa kuwa laki sita kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA, VYA Serikali na binafsi ni kati ya 125,000 tu kwa mwaka.

Bodi iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi desemba 2016 alipoteuliwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe 10 kutoka maeneo ya ujuzi mbalimbali.

MAJALIWA AKUTANA NA KAMATI MAALUM YA KUPITIA MPANGO KABAMBE WA MJI MKUU WA DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe Kamati Maalum ya Kupitia Mpango Kabambe wa Mji Mkuu wa Dodoma, Ofisini kwake mjini Dodoma Machi 6, 2017.

(Picha na Ofisi ya Waziri)

DKT.MPOKI ATEMBELEA KITUO CHA KUTOLEA CHANJO YA MANJANO CHA MNAZI MMOJA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu ya Afya,Dkt.Mpoki Ulisubisya akikabidhiwa kitabu kipya cha kadi ya manjano na mmoja wa wauguzi wa Hospitali ya mnazi mmoja ya Jijini Dar es salaam.Katibu mkuu huyo mapema leo ametembelea kituo hicho kwa ajili ya kujionea wananchi wakipata chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya njano hiyo ambapo mwisho wa zoezi hili ni mwezi huu.
Dkt.Mpoki akiongea na wananchi waliofika kwenye kituo hipcho kwa ajili ya kupata chanjo ya homa ya manjano
Katibu Mkuu Dkt. Mpoki akiwaonesha kitabu kipya cha homa ya manjano ambacho inambidi mwananchi anayesafiri toka nchini Tanzania na kwenye nchi thelathini za Bara la Afrika anatakiwa awe amepata chanjo hiyo ili kumkinga na maambukizi ya homa ya manjano.Kitabu hicho(kadi) ni mbadala ya kile cha zamani ambapo kipo tofauti na ina lenga kudhibiti udanganyifu wa raia kupata kitabu bila kupata chanjo
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara kuu ya Afya, Dkt.Mpoki Ulisubisya akimsikiliza mmoja wa mwananchi aliyefika kituoni hapo kupata chanjo
Katibu Mkuu akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kituoni hapo kupata chanjo ya homa ya manjano.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)

Na.Catherine Sungura,WAMJW

Wananchi wanaosafiri nje ya nchi wametakiwa kupata chanjo ya homa ya manjano pale wanapohitaji kusafiri hususan siku kumi kabla ya kusafiri na kupatiwa vitabu vipya.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu,Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipotembelea hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa kwa ajili ya kujionea utaratibu wa kutoa chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya chanjo hiyo kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

“chanjo hii ni muhimu hasa kwa zile nchi zenye changamoto za homa hii ya manjano,kwahiyo ni vizuri kuwa na kinga kabla ya kusafiri nchi hizo ili usije pata ugonjwa huo,’nilikua nchi ya Angola hivi karibu watu karibu elfu mbili walipoteza Maisha”amesema Dkt.Mpoki

Hata hivyo kutokana na wingi wa watu kwa jiji la Dar es salaam na uhitaji wa chanjo hiyo wamekubaliana kuweka taratibu ya kupunguza watu kupoteza muda wa kufika mnazi mmoja kupata chanjo hiyo,hivyo wameamua kupeleka huduma hiyo karibu na wananchi mahali walipo

“Muda ambao upo huku shughuli nyingi zinasimama,hivyo wataalam watakaa na kuona mahali gani panafaa ili watu msipoteze muda wakuja hadi huku mfano wa Ubungo wapate huko huko hivyo tunazitawanya huduma hizi sehemu mbalimbali kwenye vituo vyetu vya huduma za afya na taratibu zitatolewa”.

Kuhusu vitabu vipya vya chanjo Dkt. Mpoki amesema wanavyo vya kutosha hivyo hamna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kama watakosa vitabu kwani hakuna siku itatokea watanzania wote wakasafiri kwa siku mmoja,na hivyo utaratibu mpya utatenganisha wale watu wa kuchanja na wakubadilisha vitabu wasikae sehemu moja

Akijibu maswali ya wananchi waliofika kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vitabu Kaimu Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Khalid Massa alisema,kwa wale watanzania watakaotaka kuchanja watapatiwa vitabu vipya kwa kulipia shilingi elfu ishirini ila kwa wale ambao watahitaji kubadilisha kadi peke yake watalipia kiasi cha shilingi elfu tano.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mnazi Moja Dkt. Sophinia Ngonyani amesema chanjo hii ya manjano ni muhimu sana kwani zinazuia maambukizi ya ugonjwa wa manjano hususan kwa Watanzania wanaosafiri kwenda nchi zenye ugonjwa huo.

Ametaja tangu zoezi hili lianze la kubadilisha vitabu vipya na chanjo ya kudumu. Hospitali yake inachanja watu wapatao 100 hadi 150 wa siku na kwa wale wanaofika kubadilisha vitabu vipya wanapokea watu wapatao 200 kwa siku na kuongeza kuwa wanavyo vitabu vya kutosha.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupita kwa Waziri wake Mhe.Ummy Mwalimu mnamo mwezi Novemba mwaka jana alizindua vitabu vipya ya homa ya manjano ikiwa na lengo la kudhibiti utolewaji holela wa kadi hizo na kwenye taarifa yake kwa Umma ya mwezi februari mwaka huu aliwahimiza wananchi wajitokeze kubadilisha vitabu hivyo ambapo mwisho wa kubadilisha itakua ni tarehe 31 machi mwaka huu,hivyo kuanzia tarehe Mosi Aprili kadi za zamani hazitatambulika tena.Zoezi la kubadilisha vitabu hivi lilianza tarehe 9 Januari ,2017.

Nchi zilizoainishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa na hatari za maambukizi ya ugonjwa wa homa ya manjano nchi 30 za Bara la Afrika ambazo ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameron, Afrika ya Kati, Chad, Congo, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Ginea Bissau, Kenya, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Sudan ya Kusini, Sudan, Togo na Uganda

Aidha,nchi 13 kutoka Bara la Amerika ya Kusini ambazo ni Argentina, Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Panama, Paraguay, Peru, Suriname, Trinidad na Venezuela
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images