Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA GATI NAMBA 2 KATIKA BANDARI YA MTWARA PIA AFUNGUA JENGO LA KITUO CHA KIBIASHARA CHA BENKI YA NMB MTWARA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa  Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Gati namba 2 litakalojengwa katika bandari ya Mtwara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Newala George Huruma Mkuchika mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari ya Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mtkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiaria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Biashara cha Benki hiyo mkoani Mtwara
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego wakipiga makofi mara baada ya kufungua kituo hicho cha Kibiashara cha NMB mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara baada ya kukifungua kituo hicho cha kibiashara mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma mara baada ya kufungua kituo hicho cha kibiashara cha Benki ya NMB mkoani Mtwara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mnolela ambapo pia amechangia kiasi cha Shilingi milioni 15 na akamuagiza Mbunge huyo kuchangia Shilingi milioni 10 kutoka fedha za jimbo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika kijiji cha Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mbunge mteule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akifUatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimamishwa njiani na Wanakijiji wa Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU

MAMA SAMIA MGENI RASMI UKARIBISHO WA VIONGOZI DODOMA.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla maalumu ya kuwakaribisha viongozi wa Serikali itakayofanyika Machi 5 mwaka huu mkoani Dodoma.

Hafla hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma na itafanyika mkoani humo katika viwanja vya Nyerere (Nyerere Square) kuanzia saa 8 kamili mchana.

Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Jeremia Mwakyoma ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ujio wa viongozi hao katika Mkoa huo.

Mwakyoma amesema viongozi wa Serikali kuhamia katika Makao Makuu ya Nchi ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo Mkoa utawakaribisha rasmi Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara waliohamia kutoka Jijini Dar es Salaam.

“Tukio la viongozi wa Wizara kuhamia Makao Makuu Dodoma ni la kihistoria ndio maana uongozi wa Serikali ya Mkoa umeona ni vema kuweka utaratibu rasmi wa kuwakaribisha viongozi hao,”alisema Mwakyoma.

Afisa Habari Mwakyoma amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa huo pamoja na Mikoa ya jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye hafla hiyo.Mnamo Julai 25 mwaka 2016 katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yalioadhimishwa mkoani Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli alitangaza rasmi Serikali kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Nchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Dodoma, Makao Makuu ya nchi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wengine ambapo kesho atakuwa mgeni Rasmi kwenye Hafla Maalum ya kuwakaribisha Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara pamoja na watumishi wote wa umma waliohamia Makao Makuu Dodoma wakitokea Dar es Salaam kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe Rais na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mwenyeji wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana

VINGUNGUTI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu.

Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule  ya Msingi Miembeni kata ya Vingunguti .

“lazima niwambie ukweli, hili suala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti, hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka ili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto.

Kumbilamoto ametolea mfano uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu, ambako alikuwa mapumzikoni hivi karibuni ,amesema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni.

Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza .

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo huo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa mtaa miembeni katika kikao cha kamati ya shule.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya rangi kwa kamati ya shule ya msingi miembeni
Baadhi ya Wananchi na Wazazi wakiwa wamekaa kwa makini wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembeni,Idaya Ndevumbili akizungumza na wazazi wa shule hiyo

MZEE ALINANOSWE ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE WALIOPOTEZANA MIAKA KUMI ILIYOPITA

$
0
0
Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.

Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.

Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,

Namba

0713 562954 Augustino Michael
0789682901 Lister Godfrey
0789421644 Frank Michael
0718 528632 Frank Michael
0769 56 2954 Augustino Michael.

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAPITISHA KWA 100% BAJETI YA ZAIDI YA BILIONI MIA MOJA

$
0
0
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Picha zote na Nassir Bakari)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kulia kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob
Kushoto ni Muweka hazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Jenny Machicho, Afisa utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ally Juma Ally, na Mchumi wa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo Yamo Wambura wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (kushoto) ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe Ramadhan Kwangaya na (kulia) ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo 
Mstahiki Meya Boniface Jacob (kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayobo (kulia)
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Yamo Wambura akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya matumizi ya fedha kwenye kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa kauli moja limepitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kuungwa mkono na madiwani wote waliozuru katika mkutano maalumu wa baraza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kaimu Afisa habari na Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Maria Makombe imeeleza kuwa Katika mpango huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakadiria kukusanya/kupokea kiasi cha Tshs 128,611,616,805.100 ambazo zimeelekezwa katika matumizi ya mishahara, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na matumizi mengineyo.

Fedha hizo zitatokana na makusanyo ya ndani ya Halmashauri, Ruzuku kutoka serikali kuu, Michango ya wananchi na wahisani wa Maendeleo.Aidha Halmashauri inatarajia kupokea kiasi cha Tshs 4,233,546,143.00 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara (Road Fund).

Katika fedha hizo chanzo cha makusanyo ya ndani ni Tshs 24,006,600,000.00 ambayo ni Sawa na asilimia 26% ya bajeti, Michango ya wananchi ni Tshs 500,000,000 Sawa na asilimia 1% ya bajeti, Mfuko wa barabara ni Tshs 4,233,546,143.00 Sawa na asilimia 4% ya bajeti na ruzuku kutoka serikalini na wahisani wa maendeleo ni Tshs 59,892,884,406.00 Sawa na asilimia 69% ya bajeti.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisoma makisio ya bajeti ya Halmashauri ya Manispaa hiyo ameyataja maeneo yaliopata kipaumbele katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Manispaa, pamoja na Ujenzi wa ofisi za Makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.

Vipaumbele vingine ni kuboresha miundombinu ya afya,shule za msingi na sekondari, kuboresha miundombinu ya maji, mifereji, taa za barabarani na kilimo mjini, Kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka, Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogondogo.

Mhe Jacob ameeleza kuwa Manispaa hiyo ya Ubungo imejipanga kusimamia vyema uimarishaji wa mahusiano mazuri kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine, Kuendelea kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma zilizo bora na zaharaka, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na uwazi sambamba na Kujenga uwezo kwa viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za wananchi.

Katika makisio ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa 2017/2018 asilimia 72% itatumika kwa matumizi ya kawaida na asilimia 28% itatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Maombi maalumu yamewasilishwa kupitia bajeti hii ambapo ni pamoja na maombi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Makao makuu ya Halmashauri, Ujenzi wa Zahanati, Ununuzi wa magari, Malipo ya fidia kwa wananchi kwa maeneo yaliyochukuliwa na Halmashauri kwa ajili ya matumizi ya umma.

Mstahiki Meya alieleza Dira na dhima ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuwa ni kuwa na jamii inayohamasika, inayokubalika ikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenziwa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa mkutano huoamesema kuwa Bajeti hiyo ina mambo mengi ambayo ni muhimu katika ustawi wa Manispaa hiyo hivyo ushirikiano wa pamoja kati ya madiwani na watumishi wa Manispaa hiyo itaimarisha mapato na uimara wa maendeleo katika jamii kwa kuwashirikisha wananchi.

MD Kayombo amebainisha kuwa Bajeti hiyo ina vipaumbele vingi lakini vile vilivyo muhimu zaidi vitafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo kwani ni sehemu ya kuimarisha nakukamilisha mipango ya mudamfupi katika Halmashauri.

Alisema kuwa makadirio ya mwaka 2017/2018 ya Tshs 128,611,616,805.00 yana ongezeko la kiasi cha Tshs 12,565681,576.01 ambapo Bajeti hii imepanda kwa asilimia 10 ukilinganisha na makisio ya Bajeti ya mwaka 2016/2017 ambayo yalikadiriwa kuwa ni Tshs 116,045,935,228.99.

Vipaumbele vya bajeti hii ya mwaka 2017/2018 ya Manispaa ya Ubungo vimewekwa katika sekta mbalimbali, ambapo Halmashauri imelenga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma kwa kujenga ofisi za Halmashauri, Kuboresha utoaji huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wakazi, Kutoka mikopo kwa wajasiriamali, Kuboresha usafi wa mazingira na Kuboresha miundo mbinu ya barabara, Shule na Afya.

SHULE YA MSINGI YA TUMAINI AMBAYO IPO MAENEO YA KIWANJA CHA NDEGE CHA BUKOBA SASA KUJENGWA ENEO JINGINE, KUTOKANA NA USALAMA.

$
0
0
 Baadhi  ya madarasa ya shule ya msingi Tumaini iliyopo kata ya Kashai, wilaya ya Bukoba Mjini ambayo wanafunzi watahamishwa kwa kujenegwa shule nyingene katika eneo la mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai kutokana na usalama baada ya kuwa karibu na eneo la Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
 Baadhi ya majengo mapya ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Tumaini, yaliyopo mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai yakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ujenzi wake. Shule hii inamadarasa 24 ya kuanzia darasa la kwanza hadi la Saba, na madarasa matatu kati ya hayo ni ya watoto wenye mahitaji maalumu.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rwambaizi ya Karagwe wakiwa  kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba, katika ziara ya mafunzo.
 Abiria wakiwasilisha taarifa zao ikiwemo na ukaguzi wa tiketi, kabla ya kupanda ndege ya Auric  wakitokea kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba wakielekea Mwanza.
Msimamizi wa Kitengo cha Usalama, Bi. Theodora Myaka wa Kiwanja cha ndege cha Bukoba (kushoto) akimkagua abiria Bi. Jasmindee Dhaliwa, Raia wa Bulgaria huku Afisa Usalama Msaidizi, Bw. Reginald Baraka akiangalia.

ZIARA YA KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA,MHANDISI HAMAD MASAUNI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.
 Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katikaeneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.
 Katibu wa Kamati Maalumya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma(kushoto), baada ya kutembelea eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo  ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika  ambapo Katibu huyo wa NEC  ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole, akimuelezaKatibu wa Kamati Maalumya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea eneo la Mwanyanya Mikoroshini.Picha na Abubakari Akida

TAARIFA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA OFISI YA BENKI KUU (BOT) PAMOJA NA NYUMBA ZA NHC MKOANI MTWARA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kufungua rasmi Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya watoto  mkoani Mtwara waliomfata kumsalimia mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara. Wengine katika Picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma kabla ya kufungua rasmi Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara.
Sehemu ya Nyumba hizo za Gorofa za Shirika la Nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha Leo mkoani Mtwara. PICHA NA IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 5,2017

Rais Magufuli akunwa na utendaji wa Waziri Nape

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA HISA ZA KAMPUNI YA TCCIA INVESTMENT

$
0
0
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, Ndibalema John Mayanja (katikati), akizungumza hii leo Jijini Mwanza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, na kushoto ni Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro Kiheya.

BMGHabari
Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, Ndibalema Mayanja, amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za kampuni ya TCCI Investment.

Mayanja ameyasema hayo Jijini Mwanza hii leo na kubainisha kwamba hisa hizo zilianza kuuzwa tangu Februari Mosi mwaka huu kwa bei ya shilingi Mia Nne na kwamba mwisho wa uuzwaji wa hisa hizo ni Machi 14 mwaka huu.

"Njia pekee ya kijiendeleza kiuchumi hivi sasa ni kupitia hisa hivyo nunueni hisa hizi za kampuni ya uhakika ambayo kila mwaka huwapatia wanahisa wake gawiwo lao". Amesisitiza Mayanja na kuongeza kwamba hisa hizo zinauzwa katika benki ya CRDB na kwa mawakala mbalimbali walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko na Dhamana (CMSA).

Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Joseph Kahungwa, amebainisha kwamba walionunua hisa za TCCIA Investment mwaka 2005 kwa shilingi 250, hisa zao zimepanda bei hadi shilingi 5,000 hivyo pesa hiyo iligawanywa na kupatikana bei ya shilingi 400 ya kuuza hisa mwaka huu ambapo kwenye mauzo hayo kila mwanahisa atapata gawio la hisa 12.5 kwa kila hisa moja.

Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, mesema jumla ya hisa Milioni 112 zinatarajiwa kuuzwa lengo ikiwa ni kampuni ya TCCIA Investment kupanua mtaji wake na kufikia Bilioni 45 kutoka Bilioni Nane za mwaka huu 2017 ambazo zimeongezeka kutoka hisa Bilioni Moja mwaka 2005 wakati kampuni hiyo inaanzishwa.

Amedokeza kwamba hatua hiyo itasaidia TCCIA kuongeza uwekezaji wake ikiwemo ujenzi wa majengo ya kisasa na maghara ya kuhifadhia mazao katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mtwara na Tanga pamoja na kuanzisha taasisi ya mikopo.
Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, akisisitiza juu ya umuhimu wa watanzanua kununua hisa za Kampuni ya TCCIA Investment. Pia amesema TCCIA itaendelea kushirikiana na serikali katika kuondoa changamoto za kiuwekezaji zilizopo ikiwemo upimaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanda pamoja na uwanja wa maonesho ikiwemo Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki
Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro Kiheya akitoa neno la shukurani kabla ya mkutano huo kuahilishwa. Kulia ni Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja.
Meneja Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoani Mwanza, Lutufyo Mtafywa (kulia), akizungumza kwa niaba ya meneja wa TRA mkoani Mwanza katika mkutano huo. 

Ameelezea umuhimu wa kila mfanyabiashara kuwa namba ya utambulisho wa biashara (TIN Number) na kuwasihi kutoa ushirikiano kwenye zoezi la uhakiki wa namba hizo ambapo amesema baada ya kufanyika Jijini Dar es salaam, litaendeleo Jijini Mwanza na maeneo mengine pia.
Mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo akiwasilisha maoni na ushauri wake
Baadhi ya wafanyabiashara na wadau wa biashara na uwekezaji wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya wafanyabiashara na wadau wa biashara na uwekezaji wakifuatilia mkutano huo
Picha ya pamoja.

ZIARA YA IGP MANGU NCHINI RWANDA

$
0
0
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (Kushoto), akiwasili nchini Rwanda, na kupokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini humo, (IGP) Emmanuel K. Gasana (Kulia) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda 
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (mbele kushoto) akitoa neno mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, pamoja na ujumbe alioongozana nao nchini humo jana, katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akimsikiliza mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, akitoaneno mbele ya  wajumbe kutoka Tanzania (hawapo pichani) IGP Mangu, yupo nchini Rwanda, kwa ziara ya siku moja  yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akimsikiliza mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, akitoa neno mbele ya  wajumbe kutoka Tanzania (hawapo pichani) IGP Mangu, yupo nchini Rwanda, kwa ziara ya siku moja  yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto),  na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakibadilishana hati ya makubaliano yenye mkakati wa kuhakikisha nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda, zinakuwa salama hususan maeneo ya mipakani na hata kwenye barabara zote zinazotumiwa na wafanyabiashara, IGP Mangu, pamoja na ujumbe wake amefanya ziara ya kikazi nchini humo jana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, mara baada ya kuitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda (Picha zote na Demetrius Njimbwi- Jeshi la Polisi Tanzania)

WANAMTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA WABUNIFU WA KILA NJIA ZA KUSAMBAZA –KAMISHINA SIANGA

$
0
0
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakizungumza katika hafla ya timu ya Serengeti Boys chini ya miaka 17 kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani jana.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani juu ya viongozi wa dini walivyo mstari wa mbele katika kupambana na dawa za kulevya.
Rais wa TFF, Jamal Malizi akizungumza katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliaodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Sober House, Al-Karim Banji akizungumza katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. (Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akipeana mkono wa shukrani na Rais wa TFF, Jamal Malizi katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakisalimina na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum katika hafla ya Timu ya Serengeti Boys chini ya miaka 17 kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakimkabidhi cheti , Rais wa TFF, Jamal Malizi katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga akimkabidhi cheti , Mwakilishi Michuzi Media Group,Emmanuel Massaka katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga akiwa katika picha ya pamoja wachezaji wa Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) baada timu hiyo kutembelea kituo cha Sober House leo (Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).
.Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen (kushoto)akimkabidhi mipira na jezi Mkurugenzi wa Sober House, Al-Karim Banji katika katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Wadau mbalimbali



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga amesema kuwa vita ya kupambana na dawa za kulevya ni kubwa kutokana na kila siku watu wanabuni njia mpya.

Vita ya dawa za kulevya sio lelema kutokana na kuwa watu ambao wana mbinu nyingi za kufanya hivyo, lakini watakamatwa wote na hatuingii kichwa kichwa katika kufanya kazi hiyo.

Akizungumza leo katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

“Watu watano tumewakamta na mmojawapo aliyekuwa anasambaza dawa za kulevya Tanzania Bara na Zanzibar na jumla zaidi watu 11000 wamekamatwa ’’amesema Sianga.

Sianga amesema mtandao wote unaofanya biashara ya dawa za kulevya wameukamata, na wanaendelea kupokea taarifa mbalimbali za kuweza kutokomeza mtandao wa kuingiza dawa hizo.

Amesema wanatumia njia tatu katika kupata taarifa za watu wanaofanya biashara hiyo moja ni taarifa za watu za moja kwa moja ya pili utafiti pamoja wananchi.

Aidha amesema kuwa watashirikiana na watu wa sober house katika mihadhara ya kuelimisha juu madhara ya dawa za kulevya kwa wale waliotumia na wamepona kwa sasa.

Sianga amesema anaona furaha kuona viongozi wa dini wako mstari wa mbele na kufanya atembee kifua mbele.

Kamishina huyo ametoa msaada wa Ngamizi Moja ‘Komputa’kuajili kuendeshea kazi katika kituo hicho, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Mkoa wa Pwani Hassan Hassanoo ametoa Ekari moja pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malizi ametoa fedha taslimu Sh.Milioni 1.2 sambamba na mipira na jezi.

Mkurugezi wa Sober House , Al-Karim Banji amesema kuwa changamoto iliyokuwa mbele yake katika kituo hicho ni kukosa eneo ambalo linaweza kukidhi mahitaji kwa wanaume na wanawake.

Amesema kituo kinapokea wanaume tu wakati wapo wanawake walioathirika na hawajaweza kupata msaada huo.

RAIS DK. SHEIN AWASILI NCHINI INDONESIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa na Mhe, Airlangga Hartarto miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia pamoja na Viongozi wa wengine wa Nchi hiyo pia akiwepo na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed (kulia)alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Nchi Indonesia,Rais Shein anamuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini Indonesia, [Picha na Ikulu.] 05/3/2017.

MAKAMBA ATOA TAARIFA YA OPERESHENI MAALUM YA UTEKELEZAJI WA KUSITISHA, UZALISHAJI, USAMBAZAJI, UUZAJI NA MATUMIZI YA POMBE KALI KATIKA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI (VIROBA)

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba). Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi

Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alipozungumza nao na kutoa matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba).
 ……………………………………………………………………………
Kama mnavyofahamu unywaji wa pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, ajali na vifo zivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizi, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. Madhara haya ndiyo yaliyopelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kutoa tamko tarehe 16 Februari, 2017 akiwa Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha uzalishaji, usambazaji,  uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) kuanzia tarehe 1 Machi 2017; Baadaye tarehe 20/2/2017 na tarehe 28/2/2017 nilitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu ufuatiliaji wa agizo hilo.
Ili kutekeleza kwa ufanisi agizo hili serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuratibu Operesheni Maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya serikali na kuchukua hatua stahiki.
Kikosi Kazi hicho kiko chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, na kinajumuisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango,  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.
Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote  kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na  Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya.  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).
Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu operesheni maalum  katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii ilitokana na kuwepo  kwa viwanda vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets)  ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.
Kikosi Kazi maalum katika Operesheni hii  tulikielekeza kufanya yafuatayo:-
  1. Kukagua na kuzuia (seize) pombe kali zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye viwanda na kuorodhesha idadi ya pombe za viroba zilizopo, vifungashio (packaging materials), mitambo mahususi kwa ajili ya kufungashia pombe za viroba na mitambo ya kutengeneza vifungashio;
  1. Kukagua na kuzuia pombe kali zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye maghala (warehouse /store), na maduka ya jumla (whole sale) na kuorodhesha idadi ya pombe kali zilizofungashwa katika viroba na vifungashio (packaging materials) tupu vilivyopo;
  • Kubaini iwapo kuna mapungufu yoyote kwenye ufungashaji pombe kali;
  1. Kukagua viwanda vya kutengeneza vifungashio vya sachets kubaini kama kuna ukiukwaji wa Sheria;
  1. Kukagua uhalali wa vibali na nyaraka za uzalishaji / uendeshaji wa kiwanda / msambazaji husika (mfano vibali na vyeti vya TFDA na TBS, EIA, stempu za kodi za TRA, leseni za biashara, leseni za vileo);
  1. Kukagua nyaraka zinazoonesha kumbukumbu za uzalishaji na nyaraka za usambazaji (sehemu bidhaa zilipouzwa kwa jumla) ili kujua kama uzalishaji na usambazaji unafanyika;
  • Kufanya tathmini ya Operesheni, kuboresha mapungufu na kuandaa ripoti ya Operesheni; na
  • Kuchukua hatua yeyote inayolenga kuboresha Operesheni na hali inayojitokeza
  1. UKAGUZI ULIVYOFANYIKA
Jumla ya  wakaguzi 58 walishiriki katika zoezi hili na kugawanywa katika  timu tatu (3) kulingana na mikoa ya kikodi ya TRA Dar es Salaam, ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Aidha, timu hizo pia zilijumuisha askari polisi na wanahabari.Katika operesheni hii, TFDA na TBS waliainisha viwanda vinavyozalisha pombe kali, na Manispaa ziliainisha  maduka, maghala  na baa zinazofanya biashara ya pombe kali kinyume na sheria.
Sheria mbalimbali za udhibiti ikiwa ni pamoja na Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura, 219; Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009, Sheria ya Vileo ya mwaka 1968 (ilirejewa mwaka 2012), Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura, 191 na Kanuni ya Kukataza Uzalishaji, Uingizaji na Matumizi ya Vifungashio vya Plastiki kufungia Pombe Kali, iliyochapishwa katika Gazette Serikali Namba 76 ya mwaka 2017 zilitumiwa katika kutekeleza Operesheni hii.
  1. MATOKEO YA UKAGUZI
Jumla ya viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali, maduka ya jumla 18, maghala manne, baa tatu na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe kali (viroba) vilikaguliwa ambapo matokeo ya ukaguzi ni kama ifuatavyo:-
  • Jumla ya carton 99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zimekamatwa  Kati yake vyenye ujazo wa mililita 50 ni carton 69,045 na milita 100 ni carton 29,344 za milliita 90 ni 782  Aidha,  chupa zenye ujazo wa mililita 100 ni 10,625.  Thamani yake  ni Tshs bilioni 10.83
  • Chapa mbalimbali za pombe kali za virobakama vile Red Wine, Banjuka, Officer’s Cane Spirit, Flash Ginna Dragon zilikuwa hazikidhi viwango na zilikuwa hazijasajiliwa na TFDA hapa nchini
  • Makampuni yote yaliyokamatwa hayana Vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA). Makampuni mengine yalikuwa hayajalipa kodi TRA na hayakuwa na cheti cha TFDA na wala   cheti cha TBS.
  • Makampuni mawili yalikutwa yanazalisha na kusafirisha mizigo usiku
  • Viroba vyenye thamani ya jumla ya Tshs 235 millioni vimekutwa vimefichwa kwenye maghala ya duka la jumla chini ya jengo la ghorofa (handaki) Kariakoo.
  • Baadhi yapombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika viroba na chupahazikuwa na namba ya matoleo (batch numbers) na tarehe za uzalishaji kwenye lebo (label);
  • Baadhi ya pombe kali zilizoonekana wakati wa ukaguzi wa viwanda, maghala, baa na maduka ya pombe kali hazikuwa na stickers sahihi za TRA na nyingine zilikuwa na stickers ambazo zilihisiwa na TRA kuwa bandia, na hivyo kuhitaji uhakiki zaidi;
  • Viwanda saba (7) vilikutwa vinafanya marekebisho kutokana na kusimamishwa awali  na TFDA kwa kosa la kutoweka kabisa namba za matoleo na tarehe ya kuzalishwa kwa bidhaa au kuweka taarifa husika katika bidhaa chache walizozalisha hadi hapo watakapokidhi masharti ya TFDA;
  • Baadhi ya pombe kali kwenye baadhi ya viwanda, maghala, maduka na baa zilikuwa zimefungashwa kwenye chupa zenye ujazo wa chini ya mililita 200 ambavyo ni rahisi kubebeka kama viroba.
  1. HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:-
  • Bidhaa za pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zenye ujazo mdogo zenye thamani ya takriban Tshs 10.8 billionizimekamatwa na kuzuiliwa (seized) katika store za viwanda, maduka ya jumla, baa na maghala ya wasambazaji;
  • Idara ya Uhamiaji imeagizwa kushughulikia raia wa kigeni wasio na vibali vya kuishi nchini ambao walikutwa kwenye baadhi ya viwanda wakati wa ukaguzi;
  • Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeelekezwa kuvifuatilia na kuvichukulia hatua viwanda vyote vilivyokaguliwa na kugundulika kufanya kazi bila kuwa na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment) au Cheti cha Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Auditing);
  • Mamlaka ya Mapato Tanzania imelekezwa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa viwanda na maghala yote yaliyoonekana kuwa na bidhaa zenye stickers za TRA zinazosadikika kuwa bandia.
  • TFDA na TBS wameelekezwa kufuatilia kwa karibu usitishaji wa ufungashaji wa pombe kali katika mifuko ya plastiki (viroba) na na chupa za ujazo mdogo chini ya 200mls; na
  • Bidhaa zote zilizokamatwa zitabaki hivyo hadi Serikali itakapoelekeza hatua ya baadae.
  1. HATUA ZINAZOFUATA
  • Kuendelea na na Operesheni hii nchi nzima kwa kasi zaidi. Aidha, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa, Wilaya hadi ngazi ya Vijiji zihakikishe agizo hili linatekelezwa nchini kote. Wenye viti wa Mitaa na vijiji wahusike pia kwa kushirikiana na kamati hizi. Aidha, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni Ofisi ya Makamu wa Rais kila mara kwa kufuata maelekezo yatakayotolewa.
  • Kufungua kesi mahakamani dhidi ya wafanyabiashara waliokiuka katazo hili ili adhabu kali kutolewa
  • Viroba vyote vilivyokamatwa pamoja na mizigo mingine itabaki chini ya ulinzi kwa sheria zilizotumika na mtu yeyote haruhusiwi kufanya chochote hadi maelekezo zaidi yatakapotolewa na serikali.
  • Kwa walioomba muda wa nyongeza kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, maombi hayo yatashughulikiwa baada ya Operesheni ya kuondoa pombe kali ambazo zimezalishwa na zinauzwa kinyume cha Sheria.
  1. WITO
Operesheni ya utekelezaji wa kuzuia uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya  pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki nchini ni endelevu na ina lengo la kuimarisha afya ya jamii, kudhibiti ukusanyaji wa mapato na hifadhi ya mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Katika kutimiza azma ya operesheni natoa wito ufuatao: –
  • Kila mwananchi ashiriki katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini wanaokaidi agizo la Serikali la kuzuia uzalishaji, usambazaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki na katika ujazo mdogo. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa ya wanaohusika na tutahakikisha usiri wa hali ya juu;
  1. Kwa atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu anayezalisha, anayeuza au kutumia stempu feki za TRA, atapata zawadi ya shilingi milioni moja;
  1. Mtu atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote mwenye kiwanda/mtambo wa kuzalisha pombe za viroba ambao hautambuliki na Serikali au mwenye mtambo wa kutengeneza viroba au kuchapisha chapa za viroba kinyume na sheria, atapata zawadi ya shilingi milioni moja.
  1. Mtu yoyote atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote mwenye ghala au aliyehifadhi shehena ya pombe za viroba kinyume cha Sheria atapata zawadi ya shilingi laki 5.
  1. Mtu yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa kwa mtu au watu wanaoingiza nchini pombe za viroba kutoka nje ya Tanzania kinyume na Sheria na utaratibu atapata zawadi ya shilingi laki 5.
  1. Mtu yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote anayehamisha au kusafirisha pombe za viroba kinyume na Sheria na maelekezo ya Serikali atapata zawadi ya shilingi laki 5.
Taarifa hizi zitolewe kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) au Whatsapp au kwa kupiga simu kwenye simu nambari 0685 333 444 au kwa Afisa yoyote kwenye Operesheni hii.
  • Wafanyabiasharana wananchi waliokuwa wanajihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na uingizaji wa pombe kali zinazofungashwa katika viroba wanatakiwa kutii maelekezo haya ya Serikali mara moja;
  • Taasisi za TFDA, NEMC na TBS zinaelekezwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ili kufikia malengo yanayotarajiwa; na
  • Serikali za Mitaa kupitia Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji / Mtaa na Kata washiriki katika kuwatambua na kutoa taarifa ya watu au kikundi cha watu wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizifungashwa katika viroba; n
  • Kuhakikisha wafanyabiashara wote waliokamatwa na watakaokutwa wameshindwa kulipa kodi wanalipa kodi stahiki mara moja.
January Makamba (Mb)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
5 Machi 2017

MABASI YA ABOOD NA HAPPY NATION YAPATA AJALI NA KUJERUHI 12 MLIMA KITONGA YALIKUWA YAKITOKEA MBEYA KUELEKEA DAR

$
0
0




Globu ya Jamii inatoa taarifa kwa Wenye ndugu waliosafiri kwenye Basi la Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam,yamepata ajali mlima Kitonga hivi punde,ambapo taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa katika ajali hiyo wamejeruhiwa abiria 12.

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigongana na basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni .
Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa  taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.
 
Moja ya Lori lililogongwa na kumbukia korongoni

NECTA YAENDELEA KUOMBA USHIRIKIANO WA KUBAINI VYETI FEKI.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.

Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.

Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.

Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.

RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE,AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI,AHUTUBIA WANANCHI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mtwara katika siku ya mwisho wa ziara yake katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mtwara katika siku ya mwisho wa ziara yake katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Mtwara wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mtwara mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara-PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mtwara mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara-PICHA NA IKULU 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kuwasili kiwandani hapo kwa ajili ya kuzindua magari 580 ya kusafirisha saruji nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumkabidhi barua ya malalamiko kutoka kwa madereva wanaolalamikia utoaji wa ajira hizo kiwandani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja hivyo vya kiwanda cha Dangote kabla kuzindua magari 580 ya kiwanda hicho yatakayosafirisha saruji nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kukagua kiwanda chake cha Saruji mkoani Mtwara.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani Mtwara.
Rais Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki huyo wa Kiwanda akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari hayo 580.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara kilichopo mkoani Mtwara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara kilichopo mkoani Mtwara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha kupooza umeme
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya jumapili ya kwanza ya kwaresma katika kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya jumapili ya kwanza ya kwaresma katika kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwatakia heri waumini wa kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya jumapili ya kwanza ya kwaresma katika kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini hao wa kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanafunzi wa Shule za Sekondari mara baada ya kusali katika kanisa la Katoliki la Watakatifu Wote jimbo la Mtwara. PICHA NA IKULU

Viroba vilivyokutwa na operesheni viwekwe kuzuizini-Makamba

$
0
0
Na chalila Kibuda,Globu ya jamii

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba amesema shehena za viroba vilivyopatikana katika viwanda,Maghala, Maduka ya Usambazaji pamoja na sehemu za starehe zikae kizuizini mpaka serikali itakapotoa tamko kwa watu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitoa taarifa ya operesheni, Makamba amesema viroba vilivyokamatwa vina thamani ya sh. bilioni 10.83 na operesheni inaendelea kwa kuwahusisha wenyeviti wa serikali za mitaa.

Amesema kuwa operesheni hiyo imebaini kuwepo viroba vyenye Stika za Mamlaka Mapato Nchini (TRA) zikiwa zimegushiwa na wanaofanya biashara hiyo.Makamba amesema watu waliofanya ukiukaji wa Sheria wa biashara hiyo wanajiandaa kuwafungulia mashitaka.

Waziri Makamba amesema na viroba vilivyopatikana baadhi watavipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali juu ya madhara kwa matumizi ya binadamu.
Aidha amesema kuna baadhi wafanyabiashara walikwenda kufungua kesi ya kuzuia operesheni waligonga mwamba kutokana sheria ya kufanya kazi hiyo.

Aliongeza kuwa kuna baadhi raia wa kigeni wanafanya kazi bila kibari na kutaka Idara ya Uhamiaji kufatilia raia hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba akizungumza na waandishi habari juu matokeo ya operesheni viroba leo.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images