Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1159 | 1160 | (Page 1161) | 1162 | 1163 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta visingizio.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza kushoto ni Kiongozi wa Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi kutoka Nchini Afrika Kusini na Wakwanza kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro ambaye ni Mtanzania.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi wa Wakurugenzi hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmoja wa Wakurugenzi wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo mkoani Lindi.
  Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt,ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais).
   
   Picha ya pamoja

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Comoro hapa nchini Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Picha ya pamoja

  0 0  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga (Kulia) akikabidhi picha yenye mahudhui ya usalama barabarani iliyochorwa na mwanafunzi wa shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent (wa kwanza kushoto) kwa mwalimu wake Bi Amina Kayeke wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy .Mwanafunzi huyo aliibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni hiyo kwa mwaka jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw Philippe Corsaletti (wa pili kulia ) na Naibu Mkurugenzi wa taasisi inayoshughulikia masuala ya usalama barabarani ya Amend, Bw Tom Bishop.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy hapa nchini Bw Philippe Corsaletti (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na na mwanafunzi wa shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent alieibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni ya Usalama barabarani inayoendeshwa na kampuni hiyo.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy hapa nchini Bw Philippe Corsaletti akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mwalimu Amina Kayeke kutoka shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar akizungumza kuhusu changamoto wanazozikabili wanafunzi wake katika masuala ya usalama barabarani. Pembeni ni mwanafunzi wa shule hiyo, Veronica Innocent alieibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni ya Usalama barabarani inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy.
  Veronica Innocent alieibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni ya Usalama barabarani inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy akizungumza mbele Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga, Uongozi wa Puma Energy, maofisa wa serikali pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni hiyo. Kwa mujibu wa Kamanda tangu kuanzishwa kwake kampeni hiyo imeweza kupunguza vifo vitokananvyo na ajali barabarani kwa asilimia 50 katika shule ambazo kampeni hiyo imeweza kufika
  Makabidhiano ya picha yakiendelea.

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Puma Energy, taasisi inayoshughulikia masuala ya usalama barabarani ya Amend, maofisa wa serikali pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo.

  KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania leo wamezindua kampeni maalumu ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi, ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kueneza elimu hiyo muhimu kuanzia ngazi ya chini.

  Ikiwa ni muendelezo tu tangu ianzishwe rasmi mwaka 2013, hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga, maofisa wa serikali pamoja na walimu.

  Utolewaji wa elimu kwa wanafunzi kuhusu usalama barabarani pamoja na matumizi ya sanaa hususani mashindano ya kuchora dhana tofauti zinazohusiana na mada kuu ya usalama barabarani vilitajwa kuwa ni ni miongoni mwa agenda muhimu katika kampeni hiyo.

  “Lengo la kuhusisha wanafunzi katika kampeni hii ni kutokana na imani tuliyonayo kwamba elimu kuhusu usalama barabarani inatakiwa kujengwa miongoni mwetu tangu tukiwa katika umri mdogo kabisa. Kwa kufanya hivyo tutakua tukiwa na elimu ya kutosha kuhusu suala hili,’’ alibainisha Meneja Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw Philippe Corsaletti.

  Kwa mujibu wa Bw Corsaletti tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo mwaka 2013, jumla ya shule 33 zenye jumla ya wanafunzi 39,000 wamefundishwa mafunzo hayo hapa nchini huku ripoti ya ukaguzi kuhusu elimu hiyo ikionyesha kupungua kwa ajali maeneo ya shule hizo.

  Akiizungumzia kampeni hiyo, Naibu Mkurugenzi wa taasisi inayoshughulikia masuala ya usalama barabarani ya Amend, Bw Tom Bishop alisema kampeni ya mwaka huu itahusisha shule 10 za Dar es Salaam na 3 za mkoa wa Kilimanjaro.

  Alizitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule za msingi Diamond na Olympio zilizopo wilaya ya Ilala, Mkwawa na Kigogo zilizopo wilaya ya Kinondoni, Buza na Amani zilizopo wilaya ya Temeke, Mbezi na Amani zilizopo wilaya ya Ubungo pamoja na Kibugumo na Kibada zilizopo wilaya ya Kigamboni.

  Kupitia kampeni hiyo, kampuni ya Puma imepanga kuendesha mafunzo hayo pamoja na kuchora tena michoro ya ukutani kuhusu usalama barabarani kwa shule 12 ambazo tayari zimekwisha pitia mafunzo hayo, kuweka miundombinu ya usalama barabarani kwa shule za msingi Ungindoni, pamoja na kuchora michoro kwenye kuta za shule za msingi Oysterbay, Mburahati na Bryson ili kutoa elimu hiyo kwa madereva.

  “Kwa upande wa shule za mkoa wa Kilimanjaro tutazitambua baadae baada ya kumaliza hizi za mkoa wa Dar es Salaam.Lengo letu ni kuzifikia shule zote hapa nchini,’’ aliongeza Bw Bishop.

  Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Kamanda Mpinga alisema tangu kuanzishwa kwake imeweza kupunguza vifo vitokananvyo na ajali barabarani kwa asilimia 50 katika shule ambazo kampeni hiyo imeweza kufika.

  “ Ndio maana natoa wito kwa wadau wengi zaidi wajitokeze kuunga mkono kampeni za namna hii kwasababu inahitajika kufika nchi nzima ili haya mafanikio tunayoyaona kwenye kampeni hii yaakisi nchi nzima,’’ alisema.

  Naye, Afisa Elimu Vifaa, Takwimu Wilaya ya Kinondoni Bi Martha Kayombo alitoa wito kwa walimu nchini kuhakikisha kwamba wanasimamia suala la usalama barabarani popote watakapokuwepo hususani maeneo ya barabarani ili kuwasaidia watoto wadogo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (Wakwanza kushoto), Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa pamoja na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi kuhusu masula mbalimbali ya mkoa huo pamoja na Taifa kwa ujumla.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo. 

  PICHA NA IKULU

  0 0
 • 03/03/17--12:55: Article 11
 • Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) katika siku yake ya kwanza nchini katika kuadhimisha miaka 100 ya benki ya standard Chartered tangu kuanzishwa kwake. 

  “ni muhimu sana kwa kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huo ni wito kwa viongozi wa soka hapa Tanzania na wadau wote wa michezo kuweka nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni. ,,,,,, ni muhimu kama taifa kuwekeza kwa vijana kuwaweka mazingira na miundombinu ya kutosha kabisa ili kuweza kuinua vipaji vyao vya soka na ndio staili inayotumiwa na mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Barnes
  Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu nchini.

  Katika siku yake ya tatu (leo) nchini gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambao watapambana vikali kuwania kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool nchini Uingereza. Barnes amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na kuwa tegemeo katika nchini yao. 

  Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. 

   “Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam.

  Aliongeza kwamba takribani timu 32 zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na timu mbili kutoka Uganda na Kenya. Mramba alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana wadogo. 

   Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia. “hii ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana ni mastaa wa taifa wa baadaye,”
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa kwanza kushoto) wakionyeshana jambo kwenye viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.

  Aidha, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake. Aliongeza kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania. Gwiji hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati pia akimtambulisha gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpoool John Barnes (hayupo) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) iliyoendeshwa na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na miundombinu ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka nchini.
  Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool, John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya miaka 15.
  Pichani juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth Park, jijini Dar es Salaam.
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen wakiwatazama timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji huyo jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akibadilishana uzoefu na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen (kushoto) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akitoa mchango wa fedha kwa ajili ya upasuaji wa macho kwa mgonjwa aliyekosa fedha kiasi cha shilingi elfu thelathini kwa ajili ya huduma za kibingwa Wilayani Mkalama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata hududma za kibingwa katika hospitali ya Iambi ya Wilayani Mkalama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda Mkorosho katika shamba la Mkulima wa kijiji cha Gumanga wilayani Mkalama kama hamasa kwa wananchi wengine wapande zao hilo.
  Wananchi wa kijiji cha Nkungi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakisaidiana kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima ili kuhamasisha kilimo hicho.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi ameagiza Kliniki tembezi ya huduma za kibingwa kwa mkoa wa Singida kuwa endelevu huku akizielekeza halmashauri kuandaa mpango wa utekelezaji wa zoezi hilo kwakuwa linagusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.

  Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Iambi Wilayani Mkalama ambako zoezi la kliniki tembezi ya madaktari bingwa wa fani nane kwa Mkoa wa Singida lilikuwa linahitimishwa.

  Amesema mara baada ya kukamilika kwa halmshauri zote saba mpango wa kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa awamu ya pili uanze mara moja kwakuwa wagonjwa wengi walionufaika ni wale webnye kipato duni na walikuwa wameshakata tama ya kupata matibabu.

  Dokta Nchimbi ametembelea wodi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji na daktari bingwa wa wanawake, wodi ya akina baba waliofanyiwa upasuaji wa magonjwa ya tezi dume na matatizo ya njia ya mkopo pamoja, ametembelea chumba cha upasuaji wagonjwa wa macho na kumalizia wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji na midomo sungura.

  Amesema, “Ukisikiliza ushuhuda wa wagonjwa waliopatiwa matibabu ya kibingwa utaona umuhimu wa kliniki tembezi, wengine walikwisha kata tamaa ya kuishi na kusubiria kifo, wengine walitengwa na kusimangwa, kuna mmoja wakati analetwa hospitali kuonana na madaktari hawa majirani waliwaambia ndugu zake watarudisha maiti lakini amepona kabisa”.

  Akitoa taarifa ya kliniki tembezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki amesema wagonjwa walioonwa na madaktari bingwa kwa muda wa siku nne ni 675 na waliofanyiwa upasuaji ni 71.

  Dokta Mwombeki ameeleza kuwa kliniki tembezi imekuwa na manufaa kutokana na kuwa na gharama nafuu kuliko hospitali kubwa za rufaa ambapo wagonjwa wengi wameshindwa kufika huko.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Injinia Geofrey Sanga ameeleza kuwa halmashauri yake imetoa milioni 18 kufanikisha zoezi hilo na kuahidi kuendelea kushikiana na Mkoa katika awamu ya pili ili wananchi wote wenye uhitaji wa huduma za madaktai bingwa wazipate.

  Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani, madaktari bingwa wanawake, wototo, macho, upasuaji, mifupa na njia ya mkojo wametoa huduma za kibingwa wilayani Mkalama kuanzia Februari 27 hadi Machi 3.

  Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Singida amezindua rasmi kilimo cha korosho kwa kushiriki zoezi la upandaji wa mikorosho na mihogo na kuhamasisha wananchi kupanda mikorosho hasa katika mashamba yao waliyolima mihogo.

  Dokta Nchimbi amesema korosho ni zao linaloweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka hamsini na pia ni rafiki wa mazingira, huku akiendelea kusisitiza kilimo cha viazi lishe kwakuwa ni mkombozi wa uchumi wa wananchi wa Singida.
  Share


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza
  dhana haramu ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye
  mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao
  umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.
  Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea.
  Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye
  mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo.
  Katibu wa BMU mtandao wa kata ya Bukondo Methusela Samweli akisoma
  Risala ambayo ilikuwa inaelezea changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo
  katika utendaji kazi wao wa kila siku wa kutokomeza uvuvi haramu.
  Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini
  taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi.
  Afisa
  mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi
  kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,akitoa taarifa ya zoezi la
  oparesheni Tokomeza uvuvi haramu.

  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bi Janneth Mobe akimkaribisha Mkuu
  wa Mkoa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasalala.
  Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akizungumza
  na wananchi wa kijiji cha nyasalala juu ya wao kutoa ushirikiano kwa serikali
  katika kupambana na uvuvi haramu.
  Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa
  akizungumza.
  Afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na
  usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii
  Ramadhan Kiteri,akimwonesha mkuu wa Mkoa nyavu aina ya dududu ambazo zimekuwa
  zikitumika kuvulia samaki ambao wanakuwa bado awajafikia muda wa kuvuliwa.


  Zoezi la uchomaji wa dhana hizo za uvuvi likiendelea.
  Wito umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo Mkoani Humo.

  Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi kwenye Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.

  Aidha mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani endapo
  uvuvi haramu ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika ziwa.

  “Ndugu wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema Kyunga

  Hata hivyo katibu wa BMU mwalo wa Daladala,Methusela Samweli amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa ambayo wanapambana nazo katika zoezi la kutokomeza uvuvi haramu ni
  kukosekana kwa vitendea kazi ikiwemo kukosekana kwa Boti kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha ambao utasaidia usalama wakati wa doria.

  Karoli Makoba na Baraka Mkwazu ni wananchi ambao
  wapo kwenye mwalo huo wameiomba serikali na BMU kuweka uhusiano wa karibu kwa kushirikiano hili kutokomeza tatizo la uvuvi haramu ambalo limeendelea kushamiri kwa kasi kubwa hususani kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.

  Kwa mujibu wa maelezo ya afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,ameelezea kuwa Doria ambayo imefanyika kwa miezi miwili imefanikisha kukamata jumla ya samaki wachanga ambao Kg 7,682,Mitumbwi 19,watuhumiwa 12,gari moja Hiace na Gari ya pili aina ya Fuso Tandam,pikipiki 3,Nyavu za makila 1,261,Makokoro
  ya kuvutwa nchi kavu 23,Dududu 41na Timba 17.

  Kiteri ameongezea kuwa Katika doria hizo
  zote kiasi cha shilingi Milion,10,080,000 zimepatikana ambazo zimetokana
  na faini mbali mbali ambazo walikuwa wakilipa watuhumiwa .

  IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE BLOG

  0 0

  Wanafunzi wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
  Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni kubadilishana uzoefu.
  Mwanafunzi Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar wakati wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA Mbweni.
  Wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhayo Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
   
  Picha ya pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa na baadhi ya walimu na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.

  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mbeya kuanzia Jumatatu, tarehe 8 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mbeya. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mbeya. 
  Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mbeya wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mbeya waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumatatu tarehe 6 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mbeya.
  Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
  Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
  Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741711 au +255 712 378516  0 0
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna mstaafu Zelote Stephen amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Rukwa kwa kufanikiwa kukamata kilo mbili za madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni heroin na lori la scania lililosheheni pombe za viroba lililokuwa likitokea Mbeya na kuingia Rukwa kwa njia za panya.


  Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limemtia nguvuni Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya Linus Tenda Kamwezi (50) mfanyabiashara mkazi wa kizwite katika manispaa ya sumbawanga aliyebainika kuyaficha madawa hayo katika maua yaliyokuwa yamezunguka nyumba yake.  


  “Pamoja na kwamba mna-resource ndogo lakini kazi mnayoifanya ni kubwa sana, nawapongeza kwa kitendo hiki na mwendelee kushika kamba hiyo hiyo dhidi ya vita hii ya madawa ya kulevya ambayo si ya jeshi la polisi peke yao bali ni la wananchi wote wa nchi ya Tanzania,” Zelote Stephen alieleza.


  Sambamba na hilo Kamanda wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alifafanua kuwa watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na lori aina ya Scania lililosheheni pombe zenye vifungashio vya nailon maarufu pombe za viroba wakitokea Mkoani Mbeya kuelekea Rukwa.


  Lori hilo lilikuwa na pombe aina tatu za konyagi,valuer na zanzi cream vikiwa ni jumla ya katoon 364 ndani ya gari no. T. 402 AFC Scania likiwa ni mali ya Kanji Lanji.


  Watuhumiwa hao ni Tuntufya Nicodema, (69), Dereva, mkazi wa Mbeya, Julio Fungameza Myovera, (57) mfanyabiashara, mkazi wa chanji na Furaha Erasto  (29), mkazi wa mbeya, tandiboi.


  Taarifa za Kukamatwa kwa lori hilo zilitolewa na wasamaria wema waliloliona lori hilo likiacha njia kuu na kuingia katika njia za panya katika Kijiji cha Nambogo Kata ya Lwiche, Wilayani Sumbawanga na kuamua kuripoti polisi.


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa onyo kali kwa vijana wanaotumia pombe za viroba na kuwatahadharisha wakae navyo mbali ili kuongeza nguvu kazi ya taifa na kutoa mchango wao katika serikali ya awamu ya tano iliyolenga kukuza viwanda.


  Zelote alisema,”kuna vijana wao wakilala wanafikiria viroba, wakiamka wanafikiria viroba, sasa ole wao wale watakaokamatwa na viroba.”


  Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa alitoa onyo kwa wafanyabiashara wote kuacha kuagiza wala kuuza pombe hizo kwani zimezuiliwa na kuwakikishia wananchi kuwa hataruhusu pombe hizo aina ya viroba kuingia ndani ya mkoa wake bila kukamatwa.

  “ Mfanyabiashra yoyote asijisumbue kwa namna yeyote ile haitapenya tumetega kila mahala, na wananchi msipende kutumia pombe hii, tukikukuta hata kama una kiroba mfukoni ni sawa na kukutwa na gongo au bangi, kwahiyo jihadharini, msinunue pombe hizi ili wauzaji washinndwe kuzalisha na kuwadodea,” Kamanda George Kyando alisisitiza.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing wakiweka jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,jana jijni Dar e Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing jana jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katikahafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla yauwekaji wa jiwe msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
   
  Baadhi ya wananchi wakishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.
  Katibu Tawala Manispaa ya Temeke, Hashim Komba akizungumza machache  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari


  Bila shaka kila mmoja wetu anakumbuka ahadi ya RC Makonda aliyoitoa mwaka jana ya kujenga viwanja vitatu (3) vya mpira kwa ajili ya maendeleo ya mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo Ndondo Cup kwani mashindano haya kwa ujumla wake yanalenga kuboresha mazingira ya michezo na kuzalisha vipaji vingi zaidi ambavyo vinabeba ajira nyingi za vijana ndani yake.

  Kimsingi RC Makonda hakuishia tu kuahidi bali alikwenda mbali zaidi na kumualika balozi wa China kushuhudia hali halisi ya viwanja vinavyotumika kwa sasa kama sehemu ushahidi wa kile alichokuwa amemueleza wakati akimshawishi.

  Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa, leo tarehe 3 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo, huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,

  Huku kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu wa taifa. Kuonyesha na kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kutoa kipaumbele cha ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni mbili ambao watakuwa vijana zaidi ya 20000.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo amewataka watumishi katika halmashauri zote nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

  Katika ziara yake mkoani Arusha katika halmashauri za Meru,Longido na Monduli alisema serikali imeshatoa fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya(Basket Fund)katika halmashauri hizo hivyo kukosekana kwa madawa na vifaa tiba sio jambo linaloweza kuvumilika.

  Alisema miradi yote ambayo fedha zimeshaletwa na serikali kuu kwenye halmashauri itekelezwe mara moja ili iweze kuwahudumia wananchi.

  Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akizungumza jambo alipotembelea eneo linapojengwa soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Orendeke Kata ya Namanga mkoa wa Arusha,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kata ya Makuyuni wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya,serikali imetenga kiasi cha Sh 700 milioni kwaajili ya upanuzi wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu. 

  Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Usa River,Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Bonifas Ukio(kulia)Mh.Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo yake. 
  Mkuu wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo akizungumza wakati wa zira ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)anayesikiliza kwa makini na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halamshauri ya Longido,Juma Mhina. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha,Lootha Laizer 
  Baadhi ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo 
  Baadhi ya Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo 
  Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Usa River,Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Bonifas Ukio(kulia)Mh.Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo yake. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akiagana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Julius Kalanga baada ya kumaliza ziara yake mkoani Arusha.

  0 0
  Baadhi ya wananchi wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka KCMC  pamoja na Mounti meru Hospital, ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide Entertaiment
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa ,Ukimwi na mengineyo
  Mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani viwanja vya Sheikh Amri Abeid

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure

  zoezi hilo ambalo limeanza jana jijini hapa, katika uwanja wa sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi,kwani zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao bure katika viwanja hivyo

  Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maadhimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha,Mkurugenzi wa Phide
  Entertaiment,Phidesia Mwakitalima alisema kuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi .

  Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao hivyo ni jambo zuri mno

  Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa, kitu ambacho sio kizuri na amewataka wananchi kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara

  Zoezi hili la kupima afya limeanza jana na linatarajiwa kumalizika Machi 8,mwaka huu  na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake

  0 0

  Paul Ibrahim Mwilombwa ni Kijana anayeishi Mkoa wa Geita Wilaya ya Chato, ni mlemavu wa viungo na mwenye kujishughulisha na maswala ya upigaji picha na mambo ya 'Graphic Design'.  hapa anaelezea historia yake na kuwaomba msaada watanzania ili apate kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.


  0 0  Hapa ni ndani ya ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga ambapo usiku wa Ijumaa Machi 3,2017 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanya sherehe ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 pamoja na kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi. 

  Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na maafisa wa polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack. 

  Akizungumza wakati wa sherehe hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema Machi 3 kila mwaka huwa ni siku ya Polisi ‘Police Family Day’ ambapo pamoja na kuadhimisha siku hiyo,jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeamua kuwafanyia sherehe ya kuwaaga wastaafu 10 wa jeshi hilo sambamba na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. 

  “Tumeanza sherehe hizi kwa mkuu wa mkoa kukagua gwaride katika uwanja wa Shycom lakini pia kutoa tuzo kwa askari na wadau waliofanya kazi vyema mwaka 2016 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga”,alisema kamanda Muliro. 

  Naye Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack alitumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na sasa vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi kikubwa. 

  Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa sherehe hizo ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri ukumbini 
  Ijumaa Machi 3,2016 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga-Aliyesimama ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza wakati wa kufungua sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.Kulia ni mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.Kushoto ni mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mama Muliro 
  Kamanda Muliro akizungumza wakati wa sherehe hiyo.Wa kwanza kulia ni Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo akifuatiwa na jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela 
  Kamanda Muliro akizungumza ukumbini 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza ukumbini. 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwaomba wadau wote wa ulinzi na usalama kuungana na jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha amani ya mkoa wa Shinyanga 
  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini 
  Wastaafu wakiwa ukumbini 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza ukumbini 
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya Shinyanga, Dkt. John Nkola akiwasalimia wageni mbalimbali 
  Viongozi wa migodi na benki mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini 
  Wadau wa ulinzi na usalama wakiwa ukumbini 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Wastaafu wa jeshi la polisi wakiwa wamekaa ukumbini 
  Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akiwasalimia wadau walioshiriki sherehe hizo.Kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Annamaria Yondani 
  Askari wa jeshi la polisi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Wafungua Shampen wakijiandaa kufungua shampen 
  Zoezi la kufungua shampen likiendelea 
  Waandishi wa habari Moshi Ndugulile kutoka Radio Faraja na Frank Mshana wa ITV/Radio One wakiwa ukumbini 
  Viongozi wa dini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa sherehe 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakigonga cheers na meza kuu 
  Zoezi la kugonga cheers likiendelea 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro (wa pili kushoto) akifurahia wakati wa kugonga cheers 
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya Shinyanga, Dkt. John Nkola akigonga cheers na meza kuu 
  Zoezi la kugonga cheers 
  Wadau wakiwa katika foleni kwenda meza kuu kugonga cheeers 
  Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde akigonga cheers na mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Sherehe inaendelea 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Sherehe inaendelea 
  Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifungua keki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi.Katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kushoto ni MC Mama Sabuni 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa ameshikilia kisu kabla ya kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro na mke wake wakijiandaa kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitabasamu kabla ya kuanza kuwalisha keki wastaafu wa jeshi la polisi 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiendelea na zoezi la kuwalisha keki wastaafu wa jeshi la polisi 
  Tunafuatilia kinachoendelea...... 


  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwalisha kesi askari polisi na wadau waliofanya vizuri mwaka 2016 katika kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Shinyanga 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akimlisha keki mke wake 
  Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akila keki 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela(katikati) na Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo (kulia) wakifurahia jambo ukumbini wakati kamanda Muliro akimlisha keki mke wake 
  Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akikabishi keki kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwa ajili ya meza kuu 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Sherehe inaendelea 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wastaafu wa jeshi la polisi 
  Zoezi la kukabidhi zawadi kwa wastaafu wa jeshi la polisi linaendelea 
  Zawadi zikiendelea kutolewa 
  Mstaafu akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Sherehe inaendelea 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwapa zawadi wastaafu wa jeshi la polisi 
  Meza kuu wakiungana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuwapa zawadi wastaafu wa jeshi la polisi 
  Utoaji zawadi unaendelea 
  Wadau wakiwa ukumbini 
  Wadau wakitoa zawadi kwa wastaafu wa jeshi la polisi 
  Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakipiga picha ya pamoja na mstaafu wa jeshi la polisi Anthony Gwandu (aliyekaa kulia) 
  Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakifurahia ukumbini 
  Kamati ya maandalizi ya sherehe wakijitambulisha ukumbini 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua muziki wakati wa sherehe 
  Ufunguzi wa muziki unaendelea 
  Wadau wakicheza muziki ukumbini 
  Meza kuu na wadau wakicheza muziki ukumbini 
  Muziki unaendelea   Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0  By Staff Reporter-MAELEZO

  African Development Bank (AfDB) Board of Directors has commended President Dr. John Pombe Magufuli for his efforts in bringing economic revolution in the country.

  The AfDB board of Directors led by Madam Lekhethe Mmakgoshi met President Magufuli at Lindi state house today where they discussed various issues of mutual interest.

  Madam Lekhethe assured President Magufuli of the bank’s continued support of his efforts to revamp the economy and pledged to see to it Tanzania remains among the bank’s leading partners.

  “We will work on your request to collaborate with your government in implementing big energy projects and construction of standard gauge central railway line” Madam Lekhethe told the president.

  During the discussion, President Magufuli expressed his government’s appreciation and that of the people of United Republic of Tanzania for the support rendered by the African Development Bank which has enabled the country to implement various development projects.

  “With AfDB support, we have managed to implement various development projects including major road networks such as Iringa- Dodoma which connects with Cape Town in South Africa up to Cairo Egypt and Namtumbo-Tunduru- Masasi road” He said and added that “AfDB is Tanzania’s key partner in development”

  Dr. Magufuli praised the bank for providing affordable/soft loans enabling the government to implement many development projects but requested the later to ease access to and expediting loans delivery so that many projects can be timely executed. 

  Meanwhile, contributing to the discussion, Dr. Namajeje Weggoro, member of AfDB Board of Directors and bank’s Executive Director for East Africa revealed that Tanzania was the leading recipient of AfDB loans and reassured the President that the bank would seriously consider his requests.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo wakati alipokuwa akiondoka Nchini kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),katika safari hiyo akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Mawaziri na Viongozi mbali mbali
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka Nchini leo kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),[Picha na Ikulu.] 04/03/2017.

  0 0

   Wanenguaji na wanamuziki wa bendi ya Fm Academia wakitumbuiza katika shoo yao iliyofanyika katika Bar ya Hawa II kimara baruti jijini Dar es Salaam
   Safu ya uimbaji ya bendi ya Fma Academia Ikiongozwa na Rais wa Bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiimba katika shoo yao ndani ya Bar ya Hawa II Kimara Baruti jijini Dar es Salaam
   Rais wa Bendi ya Fm Academia , Nyoshi El Sadatakiimba wakati wa shoo hiyo
   Malu Stonch na Partcho Mwamba wakiimba katika onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Hawa II Kimara jijini Dar es Salaam
   Mpiga Besi wa bendi hiyo akiungurumisha gitaa hiyo mbele wa mashabiki wa Kimara Baruti
   Mpiga Drum akionyesha umahiri wake wa kupiga vyombo hivyo mbele ya Mashabiki wa Kimara Baruti Dar es Salaam
  Wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia wakionyesha umahiri wao wa kutawala jukwaa mbele ya Mashabiki

  0 0

   
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen Magoiga akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa.
  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakifuatilia mkutano wa hadhara kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wilayani humo
  Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Ilobi akitoa kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.
  Wananchi wa kijiji cha Ilobi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati akizungumza nao kuhusu maendeleo alipofanya ziara ya kikazi.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametoa msaada wa mabati 171 kwa shule za msingi tatu wilayani Kishapu mkoani hapa kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa pindi yatakapokamilika ujenzi wake.

  Telack alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi, kata ya Mwaweja wilayani hapa alipofanya ziara ya kikazi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao.

  Katika msaada huo jumla ya shule tatu za Nyenze iliyopo kata ya Idukilo, Mwasubi kata ya Bunambiyu na Ilobi kwenye kata ya Mwaweja zitanufaika na msaada huo wa mabati 57 kila moja.

  Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi wilayani hapa, Telack aliagiza wazazi wote kijijini hapo wawapeleke watoto wao na kuwaandikisha shuleni ambapo alisisitiza umuhimu wa elimu kwao.

  Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo kwa wazazi ambao watashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.

  Alizungumzia umuhimu wa elimu kuwa ni haki ya kila mtoto hivyo wazazi ni wajibu wao kuhakikisha wanawaandikisha shule badala ya kuwaachia mzigo wa kufanya shughuli za shambani au kuwaozesha.

  ”Watoto siyo mali wala ng’ombe bali ni wenzetu na ni wakombozi tunataka wakuu wa mikoa watoke hapa, tunataka hata rais atoke hapa kijijini hivyo naagiza kila mtoto aende shule, kamateni wazazi ambao watoto wao hawapo shule,” alisema.

  Aidha, Telack aliwahimiza wananchi kijijini hapo na wilaya kwa ujumla kutumia fursa ya kulima mazao ya biashara yakiwemo alizeti, na pamba ili wajipatie kipato na kuendesha maisha yao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen Magoiga alimshukuru mkuu wa mkoa kwa msaada huo wa mabati na kuahidi kuchangia saruji na mbao za kumalizia kuezekea vyumba vya madarasa.

  Aliwahimiza wananchi kuendelea na kuchangia shughuli za maendeleo kwa kujenga vyumba vya madarasa hadi kufikia hatua ya boma ambapo halmashauri itamalizia ujenzi huo.

  Magoiga alimuahidi mkuu wa mkoa kuwa halmashauri itakamilisha miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kupitia nguvu za wananchi ambapo alimualika kuizindua rasmi pindi itakapokamilik

older | 1 | .... | 1159 | 1160 | (Page 1161) | 1162 | 1163 | .... | 1897 | newer